Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104689 articles
Browse latest View live

Nuhu Mziwanda ' I Love Ma Shi shi Baby, Yameisha..Ntaishije Bila yeye Kwa Mfano'

$
0
0
Haka ni Ka Movie Kengine Ka kali in the Making....Jana Nuhu Alihojiwa Kwenye Radio fulani Maarufu Bongo na Kuelezea Ugomvi Wake na Shilole na kuonyesha wamepigana chini , Lakini Masaa Machache alipost Picha akimbusu Shilole Kwenye Kurasa yake ya Instagram na Kuandikia :

"I love ma Baby.yameisha ntaishije bila yeye kwa mfano"

Akina Dada Msijidanganye la Sivyo Mtaishiwa Kufunuliwa tu Mpaka Akili ziwakae Sawa

$
0
0
Leo nimeona niwape vipande vyao hawa akina dada kuanzia umri wa miaka 30 na kuendelea ambao bado hawajaolewa, utakuta mdada mtu mzma kabisa ana umri wa miaka zaidi ya 30 anatafuta wanaume wa kumuoa kwa kuweka masharti lukuki tena magumu Kinoma

Mara nataka Mwanaume Handsome, Mcha Mungu, mwenye elimu ya degree, awe ameajiliwa au anabiashara.

Nabaki kuwashangaa sana nyiyi viumbe, unataka mwanaume mcha Mungu je wewe ni mcha mungu? Ungekuwa na tabia nzuri ungefikisha umri huo ukiwa nyumbani?

Tambua kuwa kitendo cha kufikisha miaka 30 nyumbani na huna mume wala mchumba inabidi ujiulize mara mbili ulikosea nini huko nyuma Kwasababu Kupata Mume umri huo kwa sasa ni Bahati , Wengine Kabisa wanakataa wachumba wakiwa kwenye early 20's Wakijua watastay young Forever...

Utakuta mwingne alizalia nyumban halafu anakuja naye na sifa zake eti nataka mwanaume mnyenyekevu na ambaye hajawai kuoa nyambaaafu wewe umezalia nyumban halafu leo unataka mwanaume ambaye hajawahi kuoa for what?

Mimi nawaambia msijidanganye hata kidogo, mkitaka masharti hayo mtaishia kufunuliwa tu mpaka akili ziwakae sawa.

KWAHERINI

Huddah Monroe na Vera Sidika Waendelea Kurushiana Matusi, Ni Hatari!!

$
0
0
Warembo wa Kenya waliokuwa marafiki wa karibu, Huddah Monroe na Vera Sidika wameendelea na drama yao ya kurushiana vijembe kwenye mitandao ya kijamii. 

Leo Vera amemwamkia Huddah na kuwaeleza followers wake wa Instagram kuwa mwakilishi huyo wa Kenya kwenye shindano la Big Brother hana lolote na hata madai kuwa anamiliki kampuni ya masuala ya nyumba ni uongo mtupu.

Damn right I got into some gossip. Yes. Bitch always lie about one thing it two!!! FYI; these are bbm messages and chose to keep my friend anonymous and not show dp cz I honestly don’t want to involve,” ameandika Vera.

“Well. She’s the FACE OF CAMPARI Like really??? Campari really? Damn at least lie about being face of summit beer by Keroche breweries a local company that nobody would bother to Google that shit! You own a boutique!?? Enheeee! You forgot to mention you also own a “REAL ESTATE” company that doesn’t have a website neither a physical address coz honestly I’m interested in properties!! They say you look broke cz damn Bitch claims she own all these yet even her hair looks like the perfect spot for chicken to lay eggs! While you were struggling with braids for two years straight to save up for two lace wigs that don finish. Yet still pointing fingers at the Queen of weaves. You just learnt this the other day! Sit yo ass down.

Stop claiming it’s photoshop coz woman I have am the list of names of the people u been running your mouth to and everything in detail. Don’t let me go there. Cz trust me I can. I’m like a f*cking pig. I definitely enjoy getting dirty! Cz this has to stop!!! Don’t f*cking bring my name up;

PS;The face of Campari is UMA THURMAN google that shit before you start lying to very intelligent people. You look ESTU’PIDO!!! (insert Spanish accent)
Next time they will record your conversation and I will gladly post it here. Since u don’t wanna air your issues out. And let’s see how “photoshopped” that would be!
Btw. Today I have decided to give u 1 day of fame!!! Make you little bit relevant coz I know how much u die for attention. There you go!”

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Huddah akajibu:

SO Petty Bitch Vera Getting Shady on Me on INSTAGRAM .. . Seems like Huddah BOSS chick can’t keep this hoe up off me . U too jealous of my Real Estate Biz, Sadly, I’m so business savy and u only a Hoe the only job u Do.. I’m willing for the top Forbes, headed to the top, dot, org… I’ll Personally blow up those two bags of fat on ur Chest.. .. Bitch I get money so I does what I pleases.. Broke Vee so crusty, disgust me… That Bitch talk slick, I’m a have to terminate her That little nappy headed hoe.I introduced you to Business.. You my seed, seems The Weeds Already grown.. il have to Terminate ya ‘ just like You did to the seed in ur Tummy ..

Be Blessed ya’ll.”

Beautiful Jokate In Love Again ..Tuwaache Wafanye Yao

$
0
0
Kupitia Mtandao wa Kijamii mrembo Jokate amemweka wazi mpenzi wake mpya ambae ni Mtangazaji maarufu Kenya na kuonyesha ni jinsi gani alivyo na furaha. This Is Love jamani Tuwaache wafanye yao... Beautiful Jokate In Love Again .

Kauli ya Samwel Sitta Bungeni Leo Yawatibua Wadau wa Siasa Nchini

$
0
0
Nashindwa niamini au nisiamini nabaki nikiduwaa na kushangaa kwani Nondo /jembe niiliyoitegemea imeshaingia shubiri, karubuniwa na tu hako kakiti ka uenyekiti wa bunge la katiba?


Yaani mpaka sasa macho yangu hayaamini yule aliyekuwa mkombozi mtetezi wa wanyonge kipindi kile alichokuwa SPIKA WA BUNGE alikuwa mstari wa mbele kutetea maslahi ya Tanzania na jamii kwa ujumla ndo huyu leo yu tena kwenye UENYEKITI wa KATIBA na anafanya yasiyostahili mbele ya macho ya Watanzania 


Spika wa BMK ameishauri serikali kupitia kwa waziri wa habari Mh Fenela kuwashughulikia ITV kwa kuendesha mijadala na makongamano.

Spika sitta amekereka kwa watu kutoa maoni yao kuhusu mchakato wa kuijadili rasimu ya katiba ambayo ni haki ya msingi kwa kila Mtanzania. Je akiwa Rais ataruhusu demokrasia nchini kweli?

Menina: Situmii Mkorogo Weupe asili yangu na Sina Boyfriend Kwa Sasa

$
0
0
Msanii wa muziki aina ya Afro-pop na mtangazaji wa kipindi cha Dance 100% kinachorushwa kupitia kituo cha Televisheni ya vijana EATV Menina la Diva amefunguka na kuweka wazi kuwa hatumii mkorogo bali weupe ni asili yake

Menina amefunguka hayo leo alipokuwa katika kipengele cha Kikaangoni Live kinachofanyika kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV kila siku ya Jumatano kuanzia saa sita kamili ya mchana.
Menina ameweka wazi suala hilo baada ya mashabiki kutaka kujua kama ameanza kutumia mkorogo kutokana na rangi yake kuonekana ni nyeupe ndio alipofunguka na kudai kuwa yeye ni mweupe na weupe wake ni wa asili kwani yeye ana asili ya shombe shombe

MAHUSIANO YAKE.
Kutokana na urembo wake na muonekano wake vijana wengi katika ukurasa wa Facebook wa EATV walichanganyikiwa na kila mmoja alijikuta akijaribu bahati yake ya mtende baada ya kusikia kuwa mrembo huyo kwa sasa bado yupo Single na hana mtu ambae yup[o nae katika mahusiano ndipo hapo sasa watu walipoanza kutoa namba zao za simu kama hawana akili nzuri,lakini mwisho wa siku Mwanadada Menina alisema kuwa kweli yupo Single na anapata usumbufu mkubwa kwa watu wengi lakini kwa sasa wavumilie tu maana hawawezi kuambulia kitu chochote kile labda wale kwa macho.

Hivi Unamchukuliaje Mpenzi Wako Mwenye Majibu Kama Haya Ukichat Nae

$
0
0
Eti ukiwa unachat mpenzi wako anakupa majibu kama haya unamchukuliajeee 
mfano 

1.ukimwambia kila ukimwambia bby i love you much au nakupenda sana mpenzi wangu 
yeye hujibu asante au thanks badala ya kusema i love you too mpenzi wangu 

2.ukimtumia vocha hukaa kimya ukimpigia hujibu asante nimeipataa. 

3.ukimwambia nimekumic mpenzi wangu hujibu asante au thanks au k thanks 

4.ukimwambia kuhusu sex huandika k au sawa au bila kujibu

jee unamuongeleajee mpenzi kama huyu kwa wale wataalamu saikolojia

Aibu! Aunt Ezekiel Anusurika KUPIGWA Baada ya Kufumaniwa na Mume wa Mtu

$
0
0
Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson anadaiwa kukinukisha nyumbani kwa Wema Isaac Sepetu baada ya kunusurika kufumaniwa na mume wa mtu, Moses Peter Iyobo a.k.a Moze Iyobo ambaye ni densa wa Nasibu Abdul ‘Diamond’.

Habari zisizokuwa na shaka zinadai kwamba tukio hilo lilijiri Jumapili iliyopita nyumbani kwa Wema, Kijitonyama, Dar ambapo Aunt alisababisha tafrani iliyosababishwa na mke wa mwanaume huyo aliyetajwa kwa jina la Mwengi Ally.

Kwa mujibu wa mashuhuda wetu waliokuwa wakizungumza kwa kupokezana, Mwengi alidai kwamba Aunt amekuwa akitembea na mumewe huyo hivyo timbwili lilianzia nyumbani kwa Aunt, Mwananyamala A jijini Dar.

Ilidaiwa kwamba, huku Aunt akiwa hajui hili wala lile, ghafla waliibuka wasichana saba na kumuanzishia mwigizaji huyo.Mashuhuda hao walidadavua kwamba katika kujinusuru na kipigo ambacho alihisi akiwa peke yake, angeumizwa Aunt alikimbilia  nyumbani kwa shoga yake, Wema.

Ilidaiwa kwamba wasichana hao hawakuishia hapo kwani walimkimbiza Aunt hadi wakamuona akiingia kwa Wema ambapo walipofika getini walikutana na meneja wa msanii wa Bongo Fleva, aitwaye Mirrow, Petit Man ambaye walimuomba amtoe Aunt ili wamshikishe adabu ajifunze kukaa mbali na waume za watu.

Ilisemekana kwamba katika tafrani hiyo getini, Wema alitoka na msichana wake aitwaye Careen lakini Aunt hakutoka ambapo waliwaambia wasichana hao kuwa Aunt hawezi kutoka na isitoshe wa kulaumiwa ni Moze Iyobo kwani yeye ndiye anayedaiwa kumtongoza Aunt na kuanza kuchati naye hadi mkewe akanasa meseji zao za mapenzi.

Baada ya kujazwa data hizo, Mwandishi alimtafuta Mwengi ili kupata maelezo ya kina kuhusiana na ishu hiyo ambapo alikiri kwenda kwa Aunt na Wema lakini hakufanikiwa kumpata Aunt kwani kama angemkamata, maafa yangetokea.Mwengi alisema kuwa siku ya tukio aliitwa na Aunt maeneo ya Mlimani City, Dar na akamwambia aende na mtoto akamfanyie shopping.

Alisema baada ya kuambiwa hivyo hakuwa na hiyana kwani alijua kuwa ni kama mama yake mkubwa na shoga wa mpenzi wa baba yake mkubwa ambaye ni Diamond, kumbe nyuma ya pazia kulikuwa kuna kitu kingine kimejificha.“Niliporudi nyumbani, mume wangu aliniambia nimpige picha kwa kutumia simu yake, nilipoifungua ndipo ikaingia meseji kutoka kwa Aunt.

“Nilipoisoma ile meseji nikagundua kuwa walianza kuchati muda mrefu kuhusu mapenzi yao, ndipo nikakusanya jeshi langu na kumfuata nyumbani kwake nikamshikishe adabu, amshukuru Wema kumficha maana sipati picha kwa jambo ambalo lingetokea. Ingekuwa mwisho wake wa kupora waume za watu,” alisema Mwengi.

Alipotafutwa Aunt na kuulizwa juu ya sakata hilo, alijibu kwa kifupi: “Sina muda mchafu wa kuongea halafu nimelala, kwa sasa niache nipumzike.”

Laana ya Mama Yamtisha Wema Sepetu

$
0
0
NYOTA  wa  Filamu  za  kibongo  Wema  Sepetu  amesema  kuwa  katika  maisha yake  anajitahidi  hakosani  na  mama  yake  mzazi, Mirium Sepetu  ili  kukwepa  kupata  laana  ya  kile  ambacho  anaweza  kumtamkia  na  kuharibu  mwelekeo  mzima  wa  malengo  yake  aliyojipangia  kuyatimiza  akiwa  ndani  ya  ndoa  yake……

Akizungumza  na  Mpekuzi, Wema  alisema  kuwa  ndio  maana  kipindi  ambacho  mama  yake  hakutaka  kuolewa  na  mchumba  wake  Nasibu  Abdul  ‘Diamond’  hakupenda  kutumia  nguvu  ama  uwezo  wake  wa  kifedha  kumpuuza  mzazi  wake  kwani  anaamini  angemuumiza  na  kumfanya  amtamkie  maneno  mabaya

Natambua  fika  kuwa  Mungu  ametuagiza  kuwaheshimu  wazazi  wetu  kwani  hawa  ni  miungu  wadogo, wakitamka  neno  lolote  baya  baada  ya  kuwaudhi  huwa  linaumbika  na  kuwa  shida  kwa  mhusika, ndio  maana  wakati  anaweka  mikingamo  ya  mimi  kuolewa  na  Diamond  sikulazimisha  bali  niliendelea  kumsihi  akubali.” Alisema  Wema.

Penzi  la  Wema  na  Diamond  linazidi  kupamba  moto  hasa  baada ya  hivi  karibuni  kuvishana  pete  nyingine  ya  uchumba  baada  ya  mama  Wema  kubariki  penzi  lao

Anayezuia Mijadala Amepoteza Sifa za Uongozi Kama Ana Nia ya Kugombea Urais Imekula Kwake

$
0
0
Aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Humphrey Polepole amesema makongamano na mijadala inayohusu Katiba mpya yataendelea kwa sababu ni ya lazima pia ni haki ya kikatiba.

Akizungumza kwenye Kongamano la Katiba lilioandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) jana, Polepole alisema mtu anayezuia wananchi kuendelea kuzungumzia Katiba amepoteza sifa za kuwa kiongozi wa nchi.

Huku akishangiliwa na washiriki wa kongamano hilo, Polepole alisema Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi ya kidemokrasia, inayoheshimu haki za binadamu na utawala wa kiraia. Hivyo inashangaza kusikia kuna kiongozi anajaribu kuwafunga mdomo wananchi.

“Nimesikia mtu mmoja anasema msifanye makongamano. Sijamfahamu vizuri, lakini ninachokiona ni kwamba anaendelea kupoteza sifa za kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano kama alikuwa anataka kufanya hivyo,” alisema Polepole.

Ingawa hakumtaja jina, juzi Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, Samuel Sitta na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Rehema Nchimbi hivi karibuni walikaririwa wakihoji uhalali wa mijadala inayoendelea sasa kuhusu Katiba Mpya.

Sitta, akiongoza kikao cha Bunge la Katiba juzi, alimtaka Waziri wa Habari na Utamaduni kuvichunguza vyombo vya habari vinavyorusha matangazo ya watu aliodai wanapotosha ukweli kuhusu Katiba.

Ingawa Sitta hakukitaja chombo chochote, alikuwa akielekeza maoni yake kwenye mdahalo uliorushwa Jumatatu wakati wajumbe wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, wakiongozwa na Jaji Joseph Warioba waliposhiriki na kujibu hoja mbalimbali zinazoonekana kuwa na utata kwenye Rasimu ya Katiba.

Wanaodaiwa kumuua Afisa Usalama wa Taifa waburuzwa Mahakamani

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, leo imwapindisha kizimbani watu wanne wanaodaiwa kumuua kwa kumpiga risasi Ofisa Usalama wa Taifa, Sylvanus Mzeru maeneo ya Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere, Aprili 29, mwaka huu usiku.

Watuhumiwa hao ni Mohamed Othuman, Lucy Wiston,Omary Said , Kelvin Peter ambao walisomewa shitaka lao na wakili wa Serikali, Seina Kapenge.Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 20, mwaka huu itakaposikilizwa tena katika mahakama hiyo.

Viatu Virefu Vyamuumbua Maimatha wa Jesse, Ateguka Mguu

$
0
0
Na Gladness Mallya
MTANGAZAJI maarufu Bongo, Maimartha Jesse amejikuta akiteguka mguu baada ya kudondoshwa na viatu virefu alivyokuwa amevaa

Paparazi wetu alimshuhudia Maimartha akiwa anachechemea kwenye sherehe moja ya kitchen party hivi karibuni huku akiwa bado amevaa viatu virefu na alipoulizwa kulikoni anachechemea alijibu kwamba aliteguka mguu baada ya kudondoshwa na viatu virefu.

“Nimeumia mguu baada ya kudondoshwa na hivi viatu virefu lakini sikomi kwa sababu navipenda sana na nikivaa ndiyo nakuwa mrembo zaidi,” alisema Maimartha.

Diamond Amchefua Wema Sepetu, Wema Afikiria Kuchukua Uamuzi Mzito

$
0
0
Stori:Mayasa Mariwata
KAULI ya nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kwamba hawezi kuoa kamwe, inadaiwa kumchefua mwandani wake, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’, Amani limenyetishiwa.

Aliporejea Bongo kutoka Marekani juzikati, Diamond alitoa kauli hiyo na kuandikwa kwenye ukurasa wa mbele wa gazeti dada la hili, Ijumaa, toleo la wiki iliyopita likiwa na kichwa cha habari; ‘DIAMOND: SITAOA KAMWE’ ambapo ndani yake alieleza jinsi ambavyo mastaa wengi waliooa wameanguka kisanii.

MTU WA KARIBU AYASEMA YA WEMA
Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa mastaa hao, Wema hakufurahishwa na habari hiyo kwa sababu anajua yeye ndiye mke mtarajiwa wa Diamond.

Ilidaiwa kwamba, Wema alijikuta akipoteza ile furaha ya kwamba wawili hao wangefunga ndoa mwezi huu (Agosti) kama ilivyotabiriwa na mnajimu maarufu Bongo, Maalim Hassan Yahya Hussein.

“Baada ya kauli hiyo ya Diamond na kutotimia kwa utabiri wa Maalim Hassan kwa sababu hakuna hata dalili za maandalizi ya tukio hilo muhimu kwenye maisha ya mwanadamu, Wema ameanza kukata tamaa, lakini amesema hawezi kulazimisha ndoa kwa mwanaume kwa kuwa si utamaduni wa wanawake wa Kitanzania wala Kiafrika.
“Unajua Kibongobongo au hata Kiafrika hai-sound vizuri na pengine haiwezekani kwa mwanamke kulazimisha kuolewa kama mwanaume hataki. Hicho ndicho kilichomtibua Madam (Wema) baada ya kusoma alichokisema Diamond,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:

“Wema amehisi yeye ni girl lover (mpenzi) tu kwa Diamond na si wife material (mke mwema) kwa hiyo  anawaza sana kuhusiana na ishu hiyo japo mahaba niue kati yao yanaendelea, lakini anafikiria kuchukua uamuzi mzito.”

WEMA SASA
Baada ya kuinyaka ishu hiyo, gazeti hili lilimtafuta mlimbwende huyo anayeshikilia Krauni ya Miss Tanzania 2006 ili kumsikia mwenyewe ambapo alifunguka yake ya moyoni.
Mwanadada huyo alisema kuwa kwa sasa haumizi tena kichwa kuhusu  suala la ndoa na Diamond na kwamba hana haraka nalo.

“Mimi naamini sana mambo ya utabiri, lakini siumizi kichwa na suala la kuolewa na Diamond na kamwe siwezi kumlazimisha anioe.

Aliporejea Bongo kutoka Marekani juzikati, Diamond alitoa kauli hiyo na kuandikwa kwenye ukurasa wa mbele wa gazeti dada la hili, Ijumaa, toleo la wiki iliyopita likiwa na kichwa cha habari; ‘DIAMOND: SITAOA KAMWE’ ambapo ndani yake alieleza jinsi ambavyo mastaa wengi waliooa wameanguka kisanii.

MTU WA KARIBU AYASEMA YA WEMA
Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa mastaa hao, Wema hakufurahishwa na habari hiyo kwa sababu anajua yeye ndiye mke mtarajiwa wa Diamond.

Ilidaiwa kwamba, Wema alijikuta akipoteza ile furaha ya kwamba wawili hao wangefunga ndoa mwezi huu (Agosti) kama ilivyotabiriwa na mnajimu maarufu Bongo, Maalim Hassan Yahya Hussein.

“Baada ya kauli hiyo ya Diamond na kutotimia kwa utabiri wa Maalim Hassan kwa sababu hakuna hata dalili za maandalizi ya tukio hilo muhimu kwenye maisha ya mwanadamu, Wema ameanza kukata tamaa, lakini amesema hawezi kulazimisha ndoa kwa mwanaume kwa kuwa si utamaduni wa wanawake wa Kitanzania wala Kiafrika.

“Kikubwa katika mapenzi ni upendo wa kweli ambao ananionesha bila kipimo. Wala sina papara, hata kama mtabiri kasema ndoa yetu ni lazima ifungwe mwaka unaogawanyika kwa mbili kwa maana ya mwaka 2016 kama itashindikana mwezi huu, hilo kwangu si tatizo la kunifanya nililie kuolewa na Chibu (Diamond).

“Ninachojua mimi Mungu ndiye anapanga yote na kama ndoa ipo ipo tu maana kuna watu wapo kwenye ndoa na hawana upendo wa kweli kama tulionano sisi,” alisema Wema.

MAMA WEMA ANASEMAJE?
Paparazi wetu alimtwangia simu mama yake Wema, Mariam Sepetu na kumuuliza mambo mawili, kuhusu bintiye kuvishwa pete ya ndoa na Diamond na suala la Mbongo Fleva huyo kusema hataoa kamwe!
“Mimi niseme nini? Sina la kusema kuhusu Wema. Mambo yake ni yake mwenyewe na huyo Diamond wake. Kwanza kwa nini mnipigie mimi, si mumtafute yeye mwenyewe?” alisema mama huyo kwa sauti ya utulivu.

MAMA DIAMOND AFUATA NYAYO
Katika hali ya kushangaza, mama Diamond, Sanura Kasim ‘Sandra’ ameonekana kunawa mikono kwa kauli aliyowahi kuitoa siku za nyuma kuhusu mtoto wake na masuala ya kutooa au kuoa.

Nasibu ni mtu mzima sasa, siwezi kumpangia lolote kuhusu kuoa au kutooa. Wakati ukifika, anaweza kusema lolote ambalo ataliona ni zuri katika maisha yake.”
KUHUSU PETE YA NDOA
Kuhusu Diamond kumvisha pete ya ndoa Wema, tendo ambalo lilifanyika hivi karibuni wakiwa nchini Afrika Kusini, Amani lilifanikiwa kuzungumza na shehe mmoja ambaye aliomba hifadhi ya jina lake ambapo alisema alichokifanya Diamond kwa Wema ni usanii.

“Diamond amemfanyia usanii mwenzake. Pete gani bila kufunga ndoa. Halafu katika Uislam, hakuna tendo la wanandoa kuvalishana pete, hayo mambo wanayafanya wenyewe, ” alisema shehe huyo.

WEMA AIZUNGUMZIA PETE
Wema alipopewa nafasi ya kuizungumzia pete hiyo alisema Diamond aliipenda tu akaamua kumnunulia na kumvisha lakini haihusiani na ndoa.

“Sisi (na Diamond) tulikuwa Afrika Kusini, baby wangu akaipenda pete, akainunua na kunivalisha, haina uhusiano na ndoa,” alisema Wema.
GPL



Kwa Nini sisi Wanawake/Wasichana Wanene na Wenye Makalio Mkubwa Hatupati Waume wa Kutuoa ?

$
0
0
1. Tunaongoza kwa kuwa vimada kwa waliooa, lakini sisi 

hatuolewi:  (a)Miili yetu imepitwa na wakati, (b)Labda 

wanadhani tutashindwa mechi. 

2. Tufanyaje ili nasi tupate wanaume wa kutuoa?  

(a)Tuifanyie miili yetu diet/tujikondeshe ili tuwe wembamba, 

(b)Tuanze kuwatongoza wanaume.  

NALILETA MEZANI TULIJADILI. Nimefanya uchunguzi 

yakinifu na nikajiridhisha kwa 95% kuwa sie wanawake 

wanene na wenye makalio makubwa huwa ni ngumu sana 

kuolewa, kwa nini? 

Uzuri wa Mtoto wa Kike wa Rais Kagame Wampagawisha Zamaradi Amfaninisha na Cleopatra

$
0
0

" Nimeshindwa kuvumilia... Huyu Binti wa Kagame ni a REAL definition of beauty... #natural Beauty... kuna ile story ya Cleopatra ambae ndio anasemekana alikuwa ndio mwanamke mzuri kuliko wote duniani.. Na kwa hilo kila mtu ana picha ya Cleopatra aliejijengea kichwani.. KIUKWELI kabisa Hii picha ninayoiona leo ya huyu msichana ndio PICHA YA CLEOPATRA niliyokuwa nayo kichwani miaka yote!! SHE IS EXTREMELY BEAUTIFUL!!! kwa upande wangu." by Zamaradi Mtetema VIA instagram

Ali Kiba Aamua Ku Unfollow Watu Wote Aliokuwa Anawafollow Instagram, Mashabiki Wamwambia Sio Deal

$
0
0
Baada ya Alikiba kuunfollow watu aliokuwa akiwafollow kwenye akaunti yake ya Instagram ameeleza sababu za kufanya hivyo.
Kupitia mtandao huo, Alikiba ameandika:

Thank you for taking time to jot down your opinion . It would be good if you understood my point of view as well . The social platform that keeps me in touch with my fellow artists , fans and others across the world is twitter. Instagram is limited to pictures… hence more of a preference then an interaction platform . On twitter, I will continue to interact with my fellow artists and celebrities , entertainment and political shareholders , my dear fans and all others See you on twitter and thanks again for taking the time to share your opinion . Much appreciated

Haya ni baadhi ya maoni ya watu wanaomfollow.

Haulefadhili
Inakuwaje hakuna mtu unaye mfollow bro!! Ti me it doesn’t make sense and this means hakuna mtu yyte unaye mpenda au kumkubali or wat?? Wewe kwangu ni kama brother ila kwa hili la (( 0 follow)) silielewi.

Williamkiteleki
Even mi nimekua sana disapointed coz dunia now days imehamia kwenye social netwrk bro kiba..so kwa star kama wewe ukitaka ku coup na mastaa wenzako na hata watu mbalimbali na kujifunza mengine kutoka kwako lazma uwe nao karibu kwenye mitandao ya kijamii(follow them) coz dunian huwezi jua kila kitu kuna vingne lazma utajua kupitia wengne.. dats how life is.. so it will be gud sana kama ukizingatia hili kaka.. unaweza ukaona ni kitu kidgo bt am sure utajifunza vingi kupitia hilo bro

Nay wa Mitego Adai Alikuwa KIBAKA Kabla ya Kuwa Msanii wa Bongo Flava

$
0
0
Kwa mara ya kwanza staa wa Bongo Fleva, Emanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ ameibuka na kuuelezea upande wa pili wa maisha yake kuwa kabla hajawa mwanamuziki alikuwa mwizi balaa!

Akizungumza na mwandishi wetu ana kwa ana jijini Dar es Salaam juzi, staa huyo alikiri kupitia katika majanga kibao maishani mwake likiwemo la kulala katika vituo mbalimbali vya polisi vya jijini Dar kufuatia kufanya matukio ya uhalifu.

“Kwanza kabisa nilikuwa nalala Feri na watoto machokoraa. Nilikuwa naona ndiyo maisha japokuwa nilijua kuna maisha mengine mazuri zaidi lakini ningeyapate?

“Dah! Yaani kusema kweli nilipita kwenye majanga makubwa sana jamani! Anyway, kimsingi ukweli wa maisha yangu siwezi kuuficha maana nitakuwa najiongopea bure kwani ni kweli niliishi katika maisha ya matukio sana,” alisema Nay.

Akizidi kutiririka , Nay ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wa Mr Nay aliweka bayana kwamba kwa nyakati tofauti aliwahi kuiba  vitu mbalimbali (hakupenda kuvitaja) kwa watu wa karibu yake akiwemo Prodyuza Paul Mathysse ‘P Funk’ na kwenye studio moja iliyopo maeneo ya Mwenge jijini Dar.

“Enzi zangu nilikuwa balaa, Majani mwenyewe (P. Funk) nilishawahi kumliza, nakumbuka pia kuna jamaa zangu walikuwa na studio ya muziki pale Mwenge nao niliwapiga.

“Tena hawa jamaa wa studio nakumbuka walikuja kinitaiti nikiwa kwenye msiba, wakanitia pingu na kunipeleka kituo cha polisi lakini bahati nzuri marehemu John Mjema, alikuwa mshikaji wangu sana, akaja kunitoa,” alisema Nay.

John Mjema ‘Bomba la Mvua’ alikuwa mwanamuziki wa Kizazi Kipya, alifariki dunia Februari 10, 2008 kwa kujichoma kisu cha shingo nyumbani kwake Mtoni Kijichi jijini Dar.

Nay akaongeza: “Kulala polisi nadhani ni kama mara saba hivi na mara zote aliyekuwa akinitoa ni John Mjema. Yeye wakati ule alikuwa akifanya kazi kule maeneo ya Feri.”

Pamoja na matukio hayo ambayo Nay ameyafanya, alisema alishatubu na kumwomba Mungu amsamehe kwani anaamini ujana ndiyo ulikuwa ukimsumbua.

“Yaliyopita si ndwele, kwa sasa naganga yajayo maana muziki unanilipa na naendelea na harakati zangu kama kawaida, nilishasahau hayo matukio ya ajabuajabu,” alimaliza Nay.

Miongoni mwa mafanikio makubwa aliyoyapata msanii huyo kupitia muziki wa Bongo Fleva ni kujenga nyumba Kimara-Rombo jijini Dar na gari la kutembelea aina ya Nissan Murano.

TundaMan Aeleza Alichoshauriwa na Ali Kiba Baada ya Kupokea Simu na Kuugua, 'Inawezekana ni Ushirikina'

$
0
0
Mwimbaji wa Tip Top Connection, TundaMan aliwashangaza wengi baada ya kueleza kuwa alipokea simu yenye namba nyingi asizozielewa na ghafla akapata mshtuko na kuishiwa nguvu, hali iliyomsababisha akimbizwe hospitali ambapo alipewa matibabu.

Licha ya kuwa wataalam na mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) walieleza wazi kuwa kitaalam simu haiwezi kabisa kuwa chanzo cha tatizo hilo, TundaMan alisisitiza kuwa yeye ndiye aliyepata tatizo na anajua kilichotokea.

“Wao wanasema haiwezekani kwa sababu hilo tatizo halikuwakuta…lakini kwa kuwa mimi ndiye nimekuwa affected kwa siku mbili tatu, mimi naamini kuwa tukio hilo lipo na limekuja baada ya kupokea ile simu. Wao wanaongea kitaalam siwezi kubishana nao, lakini mimi limenikuta na nimeona.” Aliiambia tovuti ya Times Fm.

Kutokana na sintofahamu hiyo, Tundaman ameeleza kuwa msanii mwenzake, Ali Kiba alimshauri kwenda katika nyumba ya ibada ili apate dua maalum.

“Yeah inawezekana (ni ushirikina) kwa sababu vitu kama hivyo huwa vinatokea sana na ndio maana ndugu yangu Ali Kiba amenishauri nikapate dua.” Amesema Tunda Man.

Ameeleza kuwa tayari amechukua uamuzi huo ingawa hali yake pia inaendelea kuimarika baada ya kupata matibabu. Kwa mujibu wake,  Dua ndilo kimbilio lake la mwisho. 

Miili ya Waliokufa Kwa Ebola Yatupwa Hovyo Mitaani, Liberia

$
0
0
Ugonjwa wa Ebola unaendelea kuwa tishio kubwa kwa watu Afrika Magharibi huku idadi kubwa ya watu ikipoteza maisha.

Kufuatia hofu ya kuambukizwa ugonjwa huo hatari kwa kugusa au kuwa karibu na wagonjwa au miili ya waliopoteza maisha kwa ugonjwa huo, ndugu wa marehemu wameripotiwa kuiburuza miili ya ndugu zao kutoka majumbani kwao na kuitupa hovyo mitaani hali inayoongeza hatari zaidi ya maambukizi.

Kwa mujibu wa Daily Mail, ugojwa huo hatari unaoweza kusababisha mtu kutokwa na damu machoni, mdomoni na masikioni umeshaua takribani watu 9,000 katika nchi za Afrika Mashariki.

Madaktari wanaohudumia wagonjwa wa Ebola wanapata changamoto kubwa ya kukwepa maambukizi huku baadhi yao wakiripotiwa kupata maambukizi na kupoteza maisha.

Hali ya hatari imesababisha abiria wanaosafiri kutoka Afrika Magharibi kufanyiwa vipimo katika viwanja vya ndege kwa hofu ya kuusambaza ugonjwa huo katika nchi wanazokwenda.

Mke Wangu Hajalikubali Jina la Mtoto Wetu; Nilitaka Tumwite UKAWA

$
0
0
Mimi nimezaliwa na kukulia uswazi wakati waifu wangu ni wa kishua. 

Jamii niliyokulia (hukoo uswazi kwetu) kuna katabia ka kuwapa watoto majina kulingana na matukio maarufu yanayotokea au majina ya watu maarufu. 

Mfano kuna watoto wanaitwa cossovo, sunami, osama, michael jackson (kipindi alivokufa), obama, samunge, neymar, baloteli nk....

Kasheshe inakuja kwamba mke wangu amejifungua kidume sasa mimi nimependekeza tumwite "UKAWA" (kwasababu ndio jina lililobamba kwa sasa Tz) lakini wife haelewi wala hasikii. 

Ubaya au uzuri jina hili limekubalika sana kwa ndugu na marafiki zangu. 

Sasa wadau hapo ndipo ninapovurugwa maana mwenyewe nilikua naomba sana mwanetu azaliwe kukiwa na tukio kubwa ili na mimi niadopt vizuri utamaduni wetu.
Viewing all 104689 articles
Browse latest View live




Latest Images