Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104415 articles
Browse latest View live

Baba wa Akwilina atamani kukutana na Polisi Aliyempiga Risasi Mwanaye ili Amng'ate hata Meno Tu

0
0
Akwilini Shirima ambaye ni baba mzazi wa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline aliyepigwa risasi na polisi Februari 16, 2018 amesema siku akikutana na askari aliyemuua mwanaye atapambana naye hadi kifo.

Akizungumza leo Februari 19, 2018 nyumbani kwake Kijiji cha Olele, Shirima alisema endapo muuaji atakuwa ni kijana mwenye nguvu kumzidi, atapambana naye hata kwa kumuuma kwa meno.

"Najua ni ngumu kukutana na aliyempiga mwanangu risasi, lakini laiti ningekutana naye kama ni kijana mwenye nguvu kunizidi nitapambana naye hata kumuuma kwa meno,” amesema.

“Kama ni mzee mwenzangu nitapambana naye hadi kifo ila kwa bahati mbaya siwezi kumpata, hivyo sina namna. Kwa kweli hiki kifo kimezima ndoto ya familia ya kuondokana na umasikini.”

Shirima ameiomba Serikali kuliangalia suala hilo kwa kina na kuona namna ya kumsaidia kwa kuwa tegemeo lake limeondoka na wao kwa sasa hawana msaada wowote na wanachosubiri ni kifo.

"Jamani hii ni taa yangu imezimika na kuniacha gizani kwani toka nimepata taarifa za kifo chake sijaweza kula chochote. Nimekuwa kama nguruwe aliyetelekezwa porini bila msaada," amesema.

"Nilipopata taarifa za kifo cha mwanangu nilishtuka sana na kuhoji ni mwizi au nini kimetokea, lakini baadaye nikaambiwa ni Serikali imefanya mambo hayo. Imenitia uchungu sana na siwezi hata kula"

Shirima amesema ni afadhali mwanaye angeugua akamuuguza kuliko kifo cha ghafla alichokipata ambacho kimewaacha kwenye hali ambayo haitafutika mioyoni mwao katika maisha yao yote.

Mama wa marehemu, Costanzia Akwilini amesema mauaji ya mwanaye ni ya kinyama na bora angekuwa mbuzi angekula nyama kujifariji kuliko kwa mwanaye ambaye hakuna anayeweza kumfuta machozi.

"Mwanangu hakuwa mwanasiasa ameuawa akiwa kwenye gari akielekea kwenye shughuli zake, familia tulijinyima tukajichanga kwa kushirikiana na majirani ili asome aje atukomboe,” amesema.

“Leo nasubiria niletewe maiti kwenye jeneza. Kwa kweli imeniuma sana na kunikatisha tamaa. Naomba Serikali itende haki katika tukio hili," amesema mama wa marehemu katika mahojiano hayo.

Akwilina alifariki dunia Februari 16, 2018 baada ya kupigwa risasi kichwani akiwa kwenye daladala wakati polisi wakiwatawanya waandamanaji ambao ni wafuasi wa Chadema.

Credit: Mwananch

Black Panther yaingiza Bilioni 432 Tsh kwa siku 3 tu !

0
0
Matarajio ya filamu ya ‘Black Panther’ kufanya vizuri yameanza kuonekana katika siku tatu tangu ilipoachiwa Ijumaa iliyopita mjini Johannesburg, Afrika Kusini.

Filamu hiyo imetajwa kuingiza kiasi cha dola milioni 192 ambapo kwa fedha za kitanzania ni zaidi ya shilingi bilioni 432 kwa nchini Marekani.

Kutokana na kiasi hicho kilichoingiza filamu hiyo, kimevunja rekodi zilizowahi kuwekwa na filamu kibao kwenye box office, ikiwemo ile iliyowahi kuwekwa April mwaka jana na The Fate of the Furious, iliyoongozwa na Felix Gary Gray.

Wakati huo huo kampuni ya The Walt Disney Company yenye makao yake makuu mjini California, Marekani, inakadiria kuwa Black Panther itaingiza kiasi cha Bilioni 491 za kitanzania ndani ya siku nne kwa Marekani pekee.

Filamu hiyo pia imeingiza kiasi cha Bilioni 813 za Kitanzania kutoka sehemu zingine duniani. Pia Black Panther imekuwa filamu ya pili kutoka kwenye kampuni ya Marvel kuwa na ufunguzi mkubwa zaidi ikiongozwa na filamu ya The Avengers ya mwaka 2012.

Black Panther imewakutanisha waigizaji kama Chadwick Boseman ambaye ndio staa wa filamu hiyo, Lupita Nyong’o ambaye asili yake ni mkenya japo alizaliwa Mexico na kukua nchini Kenya, Michael B. Jordan, Danai Gurira, John Kani na Connie Chiume.

Ripoti ya Mauaji ya Akwilina Inatisha...Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya February 20

0
0

Ripoti ya Mauaji ya Akwilina Inatisha...Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya February 20

Zijue Faida 6 za Kutumia Maji ya Vuguvugu Nyakati za Usubuhi

0
0
Inawezekana unatumia kikombe cha chai  au kikombe cha  kahawa kila siku asubuhi, wengi wao hutumia maji ya kawaida ili kuanza siku vizuri. Hivi vitu vimekuwa ndio tabia ya kila siku , hata hivyo wachunguzi wanasema kunywa maji ya uvuguvugu  asubuhi wakati tumbo halina kitu unapata faida  za kiafya zaidi.

Madactari wanashauri kutumia maji ya uvuguvugu   yaliotiwa  liau au ndimu ili  kupunguza radical ndani ya mwili. Kutumia maji ya moto  inaongeza na kufungua utumbo ili kukufanya wewe upate haja kubwa kwa urahisi

Na hapa kuna faida 7  za vitu vinavyotokea katika mwili wako utakapoanza kutumia maji ya moto kila asubuhi.

1. Yanasaidia kuondoa Mikunjo.
Kunywa maji inakusaidia usizeeke mapema,hakuna mtu anaependa kuzeeka mapema.hata hivyo  sumu ndani ya mwili inaweza kukufanya uzeeke mapema. Wakati mwili wako unapotoa sumu  utapunguza magonjwa   na uzee. Maji ya  moto usaidia kuondoa sumu na yanasafisha kabisa. Zaidi sana  yanasaidia kurejesha cells za ngozi iwe inaonekana kuvutia na nyororo.

2. Huepusha maumivu.
Dawa ya nguvu  ya kutegemea kupunguza maumivu wakati wa hedhi ni maji ya moto, yanafanya misuli ya tumbo  irelax  na kupungua kwa maumivu. Maji ya moto husaidia mzunguko kapirali  na misuli katika mwili pia.

3. Yanasaidia kupunguza uzito.
Inawezekana unajaribu kupunguza uzito  na umesikia kuwa maji ya moto asubuhi yanaweza kuwa ni msaada mkubwa kwako. Hii ni kweli., maji ya moto yanaongeza joto la mwili, ambalo  linabadilisha ongezeko la  kiasi cha metabolic, kuongezeka kwa metabolic  mwili unakuwa na uwezo wa kuchoma carories siku nzima.

Kama ukianza na kunywa maji ya moto yenye limau. Utausaidia mwili wako kuvunja vunja mafuta  yalioko ndani.

4. Yanaboresha digestion.
Unapokunywa maji ya moto asubuhi unastimulate  digestion yako  na  kuusaidia mwili kuwa na digestion bora. Kunywa maji ya baridi ya ya kula chakula inaweza kusimamisha digestion yako, na mwili wako ukawa  na matatizo, maana maji yabaridi yana gandisha mafuta yalioko kwenye chakula na kufanya digestion iwe ngumu kwako. Ni bora ukatumia maji ya moto kuliko ya baridi.

5. Yanaboresha mzunguko wa damu mwilini.
Kunakuwa na mlimbikizo wa  mlolongo wa nervous na mlimbikizo wa mafuta mwilini , lakini unapotumia maji ya moto yanaenda kuondoa hio migandanizo. Hii process inaflash sumu yote  ndani ya mwili na kuufanya mzunguko wa damu kuwa mzuri na kufanya misuli kupumzika.

6. Yanakufanya Upate Usingizi Vizuri.
Unapotumia maji ya moto  wakati wa chakula cha usiku, na kabla ya kwenda kulala, utaufanya mwili wako kurelax na  kulainisha nerves zako. Hii itakufanya ulale vizuri na kuwa na utashi mzuri kwa ajili ya kuamka asubuhi.

Tumeona  faida 7 za kushangaza   ambazo zinaweza kutokea katika mwili wako utakapoanza kutumia maji ya moto kila asubuhi na jioni . Anza sasa kutumia maji ya moto kila siku ili uone faida  nzuri  tulizosoma hapo juu kwa ajili ya manufaa yako .

Mimi nimeanza  kujaribi na nimeona kuna faida, anza na wewe leo.

Majina ya Viongozi wa Chadema Waliotakiwa Kufika Kwa Mkuu wa Upelelezi Kwa Mahojiano

0
0


Majina ya Viongozi wa Chadema Waliotakiwa Kufika Kwa Mkuu wa Upelelezi Kwa Mahojiano



MSIBA WA AKWILINA: Mnyika Aeleza Barua Waliyoipokea CHADEMA kutoka Polisi

0
0
Mbunge wa Jimbo la Ubungo na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Mnyika February 19, 2018 amezungumza na AyoTV na millardayo.com akiwa nyumbani kwenye msiba wa Akwilina Maftah.

Mnyika ametoa pole kwa familia ya Akwilina kwa msiba uliotokea na kutaka watu kuacha kuzungumza mambo yasiyohusu msiba kwa sasa pia Mnyika amegusia kuhusu barua waliyoipokea kutoka Jeshi la Polisi ikitaka baadhi ya Viongozi wa Chama hicho kufika ofisi za jeshi la Polisi.

“Nimepewa taarifa kwamba Jeshi la Polisi limepeleka Barua makao makuu ya Chama likituita baadhi ya Viongozi ambao limetutaja kwa majina, wamechelewesha barua makusudi pamoja na kwamba barua imechelewa wameambiwa watutafute popopte tulipo,” -Mnyika VIDEO:

Ben Pol baada ya kuona Alikiba na Ommy Dimpozi wameweka nywele rangi kama yeye

0
0
Baada ya Alikiba kubadili rangi ya nywele zake na kuweka Nyekundu kisha Ommy Dimpozi naye kufanya hivyo huku ikiaminika kwa mashabiki kuwa wamem-copy msanii Ben Pol kwa kuwa yeye awali alibadili nywele zake na kuzifanya kuwa za kijani.

Sasa baada ya wasanii hao kufanya hivyo mashabiki walitegemea labda Ben Pol angechukulia tofauti na kuamini kuwa wamemuiga yeye lakini imekuwa tofauti baada ya Ben Pol ku-post picha ya wawili hao nakuandika kuwa… “Nimefarijika sana leo  ” – Ben Pol


Je, Morgan Tsvangiria Alipewa Sumu ya Kummaliza Taratibu?

0
0
Mengi yanaweza kuelewa, lakini kikubwa ni kwamba mpinzani wa kweli nna mwanafunzi kindakindaki wa Zimbabwe, Morgan Tsvangiria amefariki dunia.

Lakini kuna tetesi kitoka kwa watu wake wa karibu kuwa kiongozi huyo alipewa sumu ya kummaliza taratibu.

Waliofanya unyama huo ni "viroboto" wa aliyekuwa Rais wa Zimbabwe, Dk. Robert Mugabe ili kuepusha usumbufu.

Mmoja wa wadogo wa Tsvangiria alisema tuhuma hizo mwaka jana, lakini alidakwa na vyombo vya usalama na akakaa kimya. Juzi kakinukisha tena

Habari Njema..Uwanja wa Uhuru, Azam Complex kupigwa Afcon

0
0
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe ametaja viwanja vitakavyotumika katika mashindano ya vijana chini ya miaka 17 katika fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) mwakani.

Waziri Mwakyembe alisema Uwanja wa Taifa utatumika kwaajili ya ufunguzi na kufungukia mashindano hayo, huku viwanja vingine vya Uhuru na Azam Complex Chamazi vikitumika katika mechi za mashindano hayo.

"Tunataka tufanye mabadiliko katika hizi nyasi bandia za uhuru tuweke mpya, lakini uwanja wa Gymkhana utatumika kwa mazoezi, bado kuna viwanja vingine tunaendelea kuvichagua ili timu zipate sehemu ya kufanyia mazoezi kwa urahisi," alisema Mwakyembe.

Waziri Mwakyembe alisema wanajua wingi wa timu nane zinazokuja zitakuwa na viongozi, wachezaji na mashabiki hivyo wanajiandaa kuhakikisha wageni hao wanapata mahitaji yao mapema.

"Magari yanahitajika kwaajili ya kuwabeba wageni wetu hivyo inabidi yapatikane na kuandaliwa mapema, lakini pia tunajupanga juu ya suala la foleni wasiweze kukutana nalo,'' alisema.

Mwakyembe aliongeza kwamba wanaendelea na maandalizi, wapo katika hatua nzuri kwa ajili ya mashindano hayo.

 Mwananchi

Muafaka wa Mtoto Aliyerudishwa Tanzania Wapatikana

0
0
Familia mbili za wanandoa Baraka Malali na Ashura Mussa waliokamatwa nchini China Januari 19,2018 wakiwa na mtoto wao mwenye umri wa miaka miwili zimekubaliana mtoto atunzwe na babu yake Hashim Mbarouk.

Hayo yamebainishwa na Kamishna Msaidizi wa Ustawi wa Jamii, Daniel Masunzu leo wakati wakizungumza na wanahabari ambapo amesema kwamba Mbarouk ni babu upande wa mama aliyempokea mtoto huyo aliporejeshwa nchini Februari 14,2018.

Masunzu amesema baada ya majadiliano na pande hizo mbili, amesema muafaka umepatikana mtoto atakuwa chini ya familia ya Mbarouk na Zuhura Nyangasa ambaye ni bibi yake upande wa mama.

“Familia zote mbili zimekubaliana kuhusu hatua hii. Mtoto kukaa upande wa Mbarouk haina maana kwamba matunzo watayatoa wao peke yao, bali ndugu wengine wana jukumu la kuendelea kufanya mawasiliano na mtoto kwa ajili ya matunzo,” amesema Masunzu.

Wanandoa hao (Baraka na Ashura ) walikamatwa China Januari 19,2018 wakiwa na mtoto wao mwenye umri wa miaka miwili na miezi tisa wakituhumiwa kupatikana na dawa za kulevya.

Download Application ya MCHAMBUZI HURU Kwenye Simu yako Kusoma Habari za Siasa Kila Baada ya Lisaa Limoja

0
0

Maswala ya Siasa na Matamko ya kila siku ya Wanasiasa Hakikisha Umedownload App ya Mchambuzi Huru Kwenye simu yako


Kama we ni Mpenzi wa Habari za Siasa Usipitwe na Hii Application ya Mchambuzi..... 

Bonyeza HAPA Kudownload kwenye Simu yako


Kifo cha Akwilina: Baba Mzazi Atamani Kukutana na Muuaji wa Mwanaye Ili Apambane Naye

0
0

Kifo cha Akwilina: Baba Mzazi Atamani Kukutana na Muuaji wa Mwanaye
Akwilini Shirima ambaye ni baba mzazi wa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline aliyepigwa risasi na polisi Februari 16, 2018 amesema siku akikutana na askari aliyemuua mwanaye atapambana naye.

Akizungumza na MCL Digital leo Februari 19, 2018 nyumbani kwake Kijiji cha Olele, Shirima alisema endapo muuaji atakuwa ni kijana mwenye nguvu kumzidi, atapambana naye hata kwa kumuuma kwa meno.

"Najua ni ngumu kukutana na aliyempiga mwanangu risasi, lakini laiti ningekutana naye kama ni kijana mwenye nguvu kunizidi nitapambana naye hata kumuuma kwa meno,” amesema.

“Kama ni mzee mwenzangu nitapambana naye hadi kifo ila kwa bahati mbaya siwezi kumpata, hivyo sina namna. Kwa kweli hiki kifo kimezima ndoto ya familia ya kuondokana na umasikini.”

Shirima ameiomba Serikali kuliangalia suala hilo kwa kina na kuona namna ya kumsaidia kwa kuwa tegemeo lake limeondoka na wao kwa sasa hawana msaada wowote na wanachosubiri ni kifo.

"Jamani hii ni taa yangu imezimika na kuniacha gizani kwani toka nimepata taarifa za kifo chake sijaweza kula chochote. Nimekuwa kama nguruwe aliyetelekezwa porini bila msaada," amesema.

"Nilipopata taarifa za kifo cha mwanangu nilishtuka sana na kuhoji ni mwizi au nini kimetokea. Imenitia uchungu sana na siwezi hata kula"

Shirima amesema ni afadhali mwanaye angeugua akamuuguza kuliko kifo cha ghafla alichokipata ambacho kimewaacha kwenye hali ambayo haitafutika mioyoni mwao katika maisha yao yote.

Mama wa marehemu, Costanzia Akwilini amesema mauaji ya mwanaye ni ya kinyama na bora angekuwa mbuzi angekula nyama kujifariji kuliko kwa mwanaye ambaye hakuna anayeweza kumfuta machozi.

"Mwanangu hakuwa mwanasiasa ameuawa akiwa kwenye gari akielekea kwenye shughuli zake, familia tulijinyima tukajichanga kwa kushirikiana na majirani ili asome aje atukomboe,” amesema.

“Leo nasubiria niletewe maiti kwenye jeneza. Kwa kweli imeniuma sana na kunikatisha tamaa. Naomba Serikali itende haki katika tukio hili," amesema mama wa marehemu katika mahojiano hayo.

Akwilina alifariki dunia Februari 16, 2018 baada ya kupigwa risasi kichwani akiwa kwenye daladala wakati polisi wakiwatawanya waandamanaji ambao ni wafuasi wa Chadema.

Rais wa FIFA Kuwasili Nchini Februari 22

0
0
Rais wa FIFA Kuwasili Nchini Februari 22
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amethibitisha kuwa Rais wa Shirikisho la soka duniani (FIFA), Gianni Infantino anatarajiwa kuwasili nchini alfajiri ya Februari 22 kwaajili ya mkutano mkuu wa mwaka wa FIFA

Baada ya kuwa hapa nchini, Infantino ataonana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli.

Waziri Mwakyembe ameeleza kuwa Rais wa FIFA anatarajia kuwasili nchini usiku wa saa nane kuamkia Februari, 22  mwaka huu 2018 ambayo ndiyo siku ya mkutano na saa tatu asubuhi yake ataelekea Ikulu kukutana na viongozi wakuu wa nchi.

Huku Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Wilfred Kidao akisema mkutano huu wa viongozi wa FIFA na CAF umebeba ajenda mbalimbali  ikiwemo kujadili Maendeleo ya Soka la Wanawake, Maendeleo ya Soka la Vijana, Utaratibu wa kusaidia Vilabu vya soka pamoja na vipaumbele mbalimbali vya kukuza soka kwa nchi za Afrika.

Infantino anatarajiwa kuondoka nchini mara baada ya kumaliza mkutano wake na kushiriki chakula cha jioni.

Diamond Atoa Fulsa kwa Vijana... Sasa Aanza Kusaka Vipaji vya Utangazaji Mikoani

0
0
Diamond Atoa Fulsa kwa Vijana... Sasa Aanza Kusaka Vipaji vya Utangazaji Mikoani
Wakati mashabiki wa Diamond Platnumz wakisuribiria ujio wa Wasafi Radio na Tv, muimbaji ameonyesha kutaka kutoa fursa kwa vijana.
Diamond ana mpango wa kusaka vipaji vya utangazaji kwa ajili ya Wasafi Radio na TV.

“Pleae tell me, From your perspective which City has the best Radio and Tv Presenters…?,” aliandika Diamond Instagram na kuendelea, “Eti nna swali…Hivi ni Mkoa Upi Una Vipaji sana vya Watangazaji?.”.

Baada ya post hiyo watu mbali mbali walipendekeza mikoa tofauti tofauti, miongoni mwao ni DJ Nicotrack mtangazaji wa kipindi cha Dj Show cha Radio One, Dj huyo alipendekeza mikoa ya Mbeya na Arusha.

Mwili wa Akwilina Kuagwa Alhamisi Katika Viwanja vya NIT Dar

0
0
Mwili wa Akwilina Kuagwa Alhamisi Katika Viwanja vya NIT Dar
Maziko ya mwili wa aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline yatafanyika Februari 23, mkoani Kilimanjaro.

Akizungumza na MCL Digital, kaka wa marehemu, Moi Kiyeyeu amesema baada ya kikao cha familia, wamekubaliana kuwa Akwilina atazikwa mkoani humo baada ya kuagwa Februari 22, 2018 katika viwanja vya NIT, Mabibo jijini Dar es Salaam.

Akwilina aliyefariki dunia Februari 16, 2018 baada ya kupigwa risasi akiwa kwenye daladala wakati polisi wakiwatawanya waandamanaji ambao ni wafuasi wa Chadema

“Tutamuaga ndugu yetu siku ya Alhamisi katika viwanja vya chuo cha NIT pale Mabibo na siku hiyo hiyo tutaanza safari kuelekea Rombo-Mashati Olele mkoani Kilimanjaro na mazishi tutafanya Ijumaa,” amesema Kiyeyeu.

Wasichana wa Shule Waponea Kutekwa na Boko Haram

0
0
Wasichana wa Shule Waponea Kutekwa na Boko Haram

Wasichana wa shule na walimu kaskazini mashariki mwa Nigeria wamefanikiwa kukimbia shambulizi lililofanywa na wanamgambo wa Boko Haram kwenye shule yao.

Walioshuhudia walisema kuwa wanamgambo hao waliokuwa na magari waliwasili kwenye mji wa Dapchi, jimbo la Yobe siku ya Jumatatu, ambapo walianza kufyatua risasi na kulipua vilipuzi.

Mwezi Aprili mwaka 2014, Boko Haram waliwateka nyara wasichana wa shule 270 katika mji wa kaskazini mashariki wa Chibok.

Wakaazi na raia waliojihami huko Dapchi wanasema wanaamini wanamgambo hao walikuwa na mpango wa kuwateka nyara wasichana.

Wanasema kuwa vikosi vya jeshi la Nigeria vikisaidiwa na ndege za jeshi, baadaye vilizima shambulizi hilo.

Mwezi Septemba mwaka uliopita zaidi ya wasichana wa shule 100 wa shule ya Chibok waliunganishwa na familia zao kwenye sherehe katika mji mkuu wa Nigeria Abuja.

Sehemu kubwa ya wasichana hao waliokolewa mwezi Mei kufuatia mpango uliokumbwa na utata wa kubadilishana wafungwa na serikali ambapo makamanda wa Boko Haram waliachiliwa.

Lakini zaidi wa wasichana 100 bado wanashikiliwa na Boko Haram na haijulikani waliko.

Wanamgambo wa Boko Haram wamekuwa wakiendesha harakati za kutaka kuwa na taifa lao la kiislamu kaskazini mwa Nigeria. Mzozo huo unaaminiwa kusababisha vifo vya maelfu ya watu.

Chemical Afunguka Kuhusu Muziki wa Singeli

0
0
Chemical Afunguka Kuhusu Muziki wa Singeli
MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva, Claudia Lubao ‘Chemical’, amefunguka kuwa kwa upande fulani Muziki wa Singeli, ulimpunguzia heshima kutoka kwa mashabiki wake ambao walikuwa wamekwisha muamini kupitia aina ya muziki wake alioanza nao wa kuchana.

Akichonga na Full Shangwe, Chemical alisema suala la kuimba Singeli lilitoka kwa menejimenti yake aliyoachana nayo, lakini kwa upande wake anaamini muziki wao unaweza kuwa umemuongezea mashabiki kidogo kwenye upande huo, lakini kwa mashabiki wake ambao tayari walikuwa wamekwisha mpokea vizuri kwenye Hip Hop, wamemshusha thamani.

“Ukweli ni kwamba siamini sana kupitia Muziki wa Singeli, ninaamini kwamba muziki wangu niliokuwa ninaufanya ulikuwa ni mkubwa kuliko Singeli,” alisema Chemical na kuongeza kuwa kwa sasa hafikirii tena kufanya muziki huo labda baadaye sana.

Mwaka jana, Chemical aliachia wimbo uitwao Kama Ipo Ipo Tu ambao kimsingi mwenyewe ameulalamikia kuwa umemshushia heshima.

Kiongozi wa Chadema Kuagwa Leo na Kusafirishwa Iringa kwa Maziko

0
0
Kiongozi wa Chadema Kuagwa Leo na Kusafirishwa Iringa kwa Maziko
VIONGOZI mbalimbali wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wanatarajia kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa Katibu wa Chama hicho kata ya Hananasifu, Daniel John.

Daniel alikutwa amefariki dunia kwenye ufukwe wa Coco, Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam huku mwili wake ukiwa na majeraha na inadaiwa alitekwa na watu wasiojulikana akitokea katika shughuli za kampeni za uchaguzi wa marudio wa Jimbo la Kinondoni.

Taarifa kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Mawasiliano wa chama hicho, Tumaini Makene, jana ilieleza kuwa mwili wa marehemu John unatarajiwa kuzikwa kesho mkoani Iringa.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa mwili utapelekwa Kanisa Katoliki Hananasifu kwa ajili ya misa ya kumuombea marehemu itakayoanza saa 5.00 asubuhi.

“Viongozi wa chama, wakiwemo wakuu na waandamizi, wanatarajiwa kuongoza shughuli ya utoaji wa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Katibu wa Chama Kata ya Hananasifu, Jimbo la Kinondoni, Kamanda Daniely John, itakaofanyika kesho (leo), jijini Dar es Salaam,” alisema Makene.

Alisema baada ya ibada, waombolezaji watatoa heshima za mwisho na baadaye mwili kusafirishwa kwenda mkoani Iringa ambako atazikwa katika kijiji cha Chikelewatu wilayani Mafinga.

Aidha, Chadema imetoa wito kwa wanachama wa chama hicho kujitokeza kutoa heshima zao.

Juzi, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni aliweleza waandishi wa habari kuwa uchunguzi wa tukio la kuuawa kwa kada huyo wa Chadema unaendelea vizuri, na kwamba hadi sasa Jeshi la Polisi limeshamkamata shahidi mmoja ambaye anatoa ushirikiano mzuri.

Masauni alisema pindi uchunguzi utakapokamilika, taarifa itatolewa kwa wananchi ili wafahamu ukweli wa tukio hilo ambalo limeleta sintofahamu kwa jamii.

Soma Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo

0
0

Waziri Atoa Wiki Mbili Mgodi wa Nyakavanglaa Ufunguliwe

0
0
Waziri Atoa Wiki Mbili  Mgodi wa Nyakavanglaa Ufunguliwe
Leo February 20, 2018 stori nayokusogezea ni kuhusu agizo alilolitoa Naibu Waziri Wa wizara ya Madini Doto Mashaka Biteko ameagiza kufunguliwa mgodi wa Nyakavanglaa ndani ya wiki mbili uliopo katika Kata ya Malengamakali Wilaya na Mkoa Wa Iringa ili kuwarahisishia huduma wachimbaji wadogo za kujiingizia kipato chao.

Biteko ameyasema hayo February 19, 2018 wakati akizungumza na wachimbaji wadogo kwenye mkutano wa hadhara mara baada ya kuwasili mgodini hapo kukagua hatua za kiusalama zilizofikiwa tangu kufungwa kwa mgodi huo February 12, 2018 kufuatia matukio matatu ya ajali ambayo yalipelekea vifo vya wachimbaji wanne.

“Jichungeni na kujilinda wenyewe ili kila kinachopatikana serikali ijue imepata kiasi gani na wachimbaji wameingiza kiasi gani na kisemwe hadharani, ndugu zangu Rais anahangaika kuona kila eneo ambalo lina wachimbaji wadogo wana rasimishwa na hatimaye wananufaika na madini yao,”  -Biteko

“Mimi nataka niwaambieni wale wote wanaofikiri katika serikali hii inayoongozwa na Rais Magufuli wanaweza kupenya na dhahabu watafute jambo jingine la kufanya maana jambo hilo limepitwa na wakati” -Biteko
Viewing all 104415 articles
Browse latest View live




Latest Images