Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104747 articles
Browse latest View live

Mo Music Afanyiwa Unyama na Mchumba Wake Aamua Kuolewa na Mwanaume Mwingine

$
0
0
Mo Music Afanyiwa Unyama na Mchumba Wake Aamua Kuolewa na Mwanaume Mwingine
MSANII anayetamba na Wimbo wa Bajaj, Moshi Katemi ‘Mo Music’ amejikuta kwenye msongo wa mawazo baada ya mwanamke aliyekuwa mbioni kumuoa aitwaye Iptisam kuolewa na mtu mwingine, kutokana na mvutano wa dini baina yao.

Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichopo karibu na msanii huyo, Mo Music alikuwa ameshatoa posa hadi mahari lakini tatizo likawa kwenye dini; yeye Mkristo binti Muislam na wote hawakuridhia kutoka kwenye dini zao, ndipo msichana huyo akachumbiwa na mtu wa dini yake na kuamua kumtosa mshkaji bila kurudisha mahari.

Kutokana na ishu hiyo paparazi wetu alimvutia waya Mo Music ambaye alikuwa na haya ya kusema; “Dah umenitonesha kidonda, ni kweli demu kaolewa wiki iliyopita, kitendo cha kubadili dini ningewakera wazazi wangu ndo’maana nikawa nasuasua, tupo kwenye mvutano waturudishie mahari yetu wanatuzungusha.”

Penzi la Wema Sepetu na Damond Lampa Kigugumizi Kadinda

$
0
0
Penzi la Wema Sepetu na Damond Lampa Kigugumizi Kadinda
MWANAMITINDO maarufu wa mavazi Bongo, Martin Kadinda, ambaye awali alikuwa meneja wa staa mkubwa wa Bongo Muvi, Wema Sepetu, amepata kigugumizi kikubwa cha kuelezea kuhusu mrembo huyo kurejesha penzi lake na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.

Akizungumza na Amani, Kadinda alipata kigugumizi hicho baada ya kuulizwa endapo mastaa hao watarudisha mapenzi atalichukuliaje suala hilo ambapo alishindwa kufafanua badala yake aliishia kuguna na kuomba kama kuna swali lingine aulizwe.

“Jamani mimi siwezi kuzungumza chochote kuhusu hilo na hata sijui nianzie wapi kuzungumza lakini kama kuna ishu nyingine yoyote nitazungumza kwa mapana yote lakini siyo hilo hata kidogo kwa kweli,” alisema Kadinda.

Wema anatajwatajwa kurudisha ‘majeshi’ kwa Diamond baada ya hivi karibuni, mzazi mwenziye Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kutangaza kummwaga Diamond.

Tanzia: Cannavaro Apata Pigo Afiwa na Mwanaye

$
0
0
Tanzia: Cannavaro Apata Pigo Afiwa na Mwanaye
WAKATI akipambana kuitumikia klabu yake iliyoko nchini Shelisheli kucheza mechi za kimataifa, nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amepatwa na msiba baada ya kufiwa na mwanaye.
Mwanaye ambaye alikuwa bado mchanga amefariki usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Cannavaro anatarajia kuwasili nchini leo akitokea Shelisheli ambako amekwenda kuitumikia Yanga katika mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya St Louis. Yanga ilipata sare ya mabao 1-1 na kusonga mbele huku Cannavaro akicheza kwa dakika 90.

Irene Uwoya Awatolea Povu Wanawake wa Bongo "Haina Haja ya Kuleana"

$
0
0
Irene Uwoya Awatolea Povu Wanawake wa Bongo "Haina Haja ya Kuleana"
Kupitia kwenye ukurasa wa instagram wa muigizaji Irene Uwoya ameamua kuyaanika ya moyoni kuhusu wanawake ambao hawatoi ushirikiano kwa wanawake wenzao na hupenda kuona wenzao wakianguka au kufeli kimaisha ambapo hufurahishwa na jambo hilo.

Kupitia ukurasa wa instagram wa Irene Uwoya ameandika


“Hivi kwanin wanawake tunakuwa hatupendani???yani najiulizaga sana badala sisi tushirikiane ndo kwanza tunarudishana nyuma…mtu akifanya kitu kizuri au biashara ndo wa kwanza kuponda na kurudishana nyuma…yani unamskia mtu kabisa anakuponda mbayaaa afu hujawah ata kugombana na nae na pengine unamsaidiaga tu sana”

“Yani unashangaaa wanaokuunga mkono ni wanaume badala ya wanawake wenzako afu ukifanya mabaya ndo anakusifia balaaah ili uwendeleee kuharibuuu…!afu Sasa yeye akifanya lake anataka umuunge mkono anasahau yeye hakuwah kufanya hivyo!!!yani kuna mijitu ina rohooo daaahhh!!!”

Mimi Sasa hiv nimeamua si support mtu yeyote asie ni support na haina haja ya kuleana kabisa mtu asiye kuwa na humuimu kwenye maisha yako haina haja ya kuwa sehemu ya maisha yako atakurudisha nyuma tu!!!”

“Achana na watu wasio na faida wala mchango wowote kwenye maisha yako badilika!!!achana na marafiki wanao kushauri stareheee tu sikuzote…kaaa fikiri katika hao rafiki zako kuna siku atamoja walikushauri kitu cha maana cha kuingiza pesa??? au bataaa tuuu??? punguza watu wasio na mashiko kwenye maisha yako punguza marafiki wasio na faida” -Uwoya



Viongozi wa Dini, Wanasiasa Wajipanga Kukutana na Rais Magufuli

$
0
0
Viongozi wa Dini, Wanasiasa Wajipanga Kukutana na Rais Magufuli
Viongozi dini na wanasiasa wamepanga kwenda kumuona Rais John Magufuli wakiwa na pendekezo la kukamilishwa kwa mchakato wa kupatikana Katiba Mpya.

Azimio hilo limefikiwa kwenye kongamano la viongozi wa siasa na wa dini lililoandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), lililofanyika jana jijini Dar es Salaam.

Mbatia alisema lengo la kongamano hilo ilikuwa kujadili hali ya nchi kutokana na hofu iliyomo miongoni mwa wananchi, huku kukiwa na malalamiko ya ukandamizwaji wa demokrasia kutoka kwa vyama vya siasa.

Akisoma mapendekezo ya mkutano huo, Mwenyekiti wa TCD ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCR -Mageuzi, James Mbatia alisema pia kuna haja ya kujenga taasisi imara za usawa na haki.

Mbatia alisema mapendekezo mengine ni kuimarishwa uhuru wa kutoka maoni na kuwataka wadau wa siasa kujiepusha na siasa za chuki.

Hata hivyo, mwakilishi wa CCM, Wilson Mukama akizungumza na Mwananchi baada ya kumalizika kongamano hilo alisema Katiba Mpya si kipaumbele cha Serikali ya sasa.

Mukama aliyewahi kuwa katibu mkuu wa chama hicho alitoa mfano wa Kenya akisema licha ya kuwa na katiba mpya imeendelea kuwa na vurugu.

Wakizungumza nje ya ukumbi kutokana na waandishi wa habari kutoruhusiwa katika kongamano hilo, Amir wa Shura ya Maimamu nchini, Alhaj Sheikh Musa Kundecha alisema Jeshi la Polisi linatumia nguvu kubwa hali inayotia hofu wananchi.

Kuhusu mfumo wa demokrasia, alisema kumekuwa na ukandamizwaji wa vyama vya upinzani wakati vipo kisheria.

Askofu Benson Bagonza wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Karagwe mkoani Kagera alisema kinachohitajika sasa ni kuwa na siasa shirikishi bila kujali jinsi na vyama vya siasa.

Viongozi wa dini Mwanza

Wakati TCD na viongozi wa dini wakiazimia hayo Dar, mkoani Mwanza viongozi wa dini wameitaka Serikali kutimiza wajibu wa kulinda usalama wa raia na mali zao kwa kudhibiti vitendo vya watu kutekwa, kupotea na kuuawa vinavyoanza kushamiri.

Wakizungumza na waandishi wa habari jana, viongozi hao wametaja kutekwa kwa baadhi ya wasanii, kupotea kwa mwandishi wa habari wa kujitegemea wa Mwananchi, Azory Gwanda na vifo vya watu wawili wakati wa mchakato wa uchaguzi mdogo Jimbo la Kinondoni kuwa miongoni mwa mambo yanayotia doa Taifa.

Akisoma tamko la asasi za kiraia kuhusu hali ya usalama wa raia, haki za binadamu, na utawala wa sheria, Sheikh Mohammed Hassan alisema ni wajibu wa Serikali kuchunguza na kuchukua hatua dhidi ya watu kupotea na vifo vyenye utata.

Askofu Stephen Genga alisema, “Pamoja na kuomba Tanzania iwe Taifa lenye jamii yenye hofu ya Mungu; ni wajibu wetu viongozi wa dini kuonya na kukemea matukio ambayo si tu yanakiuka mafundisho ya dini zote, bali pia haki ya msingi ya binadamu ya kuishi.”

Tamko asasi za kiraia

Jijini Dar es Salaam, asasi 100 za kiraia zimetoa tamko likitaka mchakato wa Katiba Mpya ufanyike mwaka huu.

Akisoma tamko hilo, mkurugenzi wa shirika la Equality For Growth (EfG), Jane Magigita alisema Serikali itazame upya suala la upatikanaji wa Katiba Mpya kwa kuwa ndiyo suluhisho la matatizo yanayotokea kwa jamii.

“Suala la katiba limekuwa ni kilio kikubwa na hitaji la Watanzania wengi ili kutibu hali inayojitokeza. Tunashauri mchakato wa Katiba Mpya ufanyike mwaka huu kwa kuwa mwaka 2019 na 2020 Taifa litakuwa katika uchaguzi,” alisema.

Kuhusu upatikanaji wa fedha za kuendeleza mchakato wa Katiba Mpya, mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Dk Hellen Kijo Bisimba alisema hilo lipo ndani ya uwezo wa Serikali kwa kuwa kuna mambo mengi imefanya ambayo hayakuwa ndani ya bajeti ya nchi na kwamba kuna haja ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kufungua ofisi zake wilayani na kuajiri wataalamu wa kusimamia uchaguzi na kuachana na mfumo wa sasa unaoonekana kuwa na mgongano wa kimasilahi.

NEC Yafunguka Juu ya Mwitikio Mdogo wa Wananchi Katika Kupiga Kura

$
0
0
NEC Yafunguka Juu ya Mwitikio Mdogo wa Wananchi Katika Kupiga Kura
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imejibu hoja mbalimbali zinazotolewa na wadau kuhusu sababu zinazochangia mwitikio mdogo wa wananchi kujitokeza kupiga kura tofauti na idadi ya watu waliojiandikisha.

Ufafanuzi huo unatokana na idadi ya wapiga kura waliojitokeza katika uchaguzi mdogo wa ubunge wa Kinondoni na Siha uliofanyika Februari 17 pamoja na chaguzi nyingine za hivi karibuni za ubunge na udiwani.

Katika Jimbo la Kinondoni kati ya wapiga kura 264,066 waliojiandikisha ni wapiga kura 45,454 tu waliofika kupiga kura, huku Siha kati ya waliojiandikisha 55,313 waliopiga kura ni 32,277.

Katika uchaguzi mdogo wa majimbo ya Kalenga na Chalinze uliofanyika Machi 16, 2014, kati ya waliojiandikisha kupiga kura 71,964 ni 29,541 tu walijitokeza kupiga kura huku Chalinze kati ya 92,000 walioandikishwa waliopiga kura walikuwa 24,422.

Pia, Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 ni wapigakura milioni nane pekee waliopiga kura kati ya milioni 21 waliojiandikisha huku mwaka 2015, kati ya wapiga kura milioni 23.2 walioandikishwa na waliojitokeza kupiga kura walikuwa milioni 15.6.

Jana, Naibu Katibu Uendeshaji Uchaguzi wa NEC, Irene Kadushi alijibu hoja mbalimbali za wadau akisema mwitikio wa wapiga kura wakati wa chaguzi ndogo hutofautiana na wakati wa uchaguzi mkuu na kitendo cha watu kuhama chama kimoja na kisha kuruhusiwa kugombea nafasi ile ile imechangia idadi ndogo ya wapigakura kwenye uchaguzi mdogo wa Februari 17. “Miaka ya nyuma tulikuwa na changamoto ya fedha katika kutoa elimu ya mpiga kura, lakini tatizo hilo limepatiwa ufumbuzi wa kutosha na sasa elimu ya mpiga kura ni endelevu. Hakuna taasisi yoyote inayoiingilia NEC katika utendaji wake ikiwemo Serikali ambayo jukumu lake huishia kwenye kuipatia tume fedha kwa ajili ya shughuli zake,” alisema.

Bosi huyo wa uchaguzi wa NEC alisema muundo wa tume hiyo unachangia wananchi kuwa na mtazamo kuwa wateule wa Serikali wanaosimamia uchaguzi kwenye ngazi za chini wanakipendelea chama tawala.

“Hii imepelekea (sababisha) sisi kuomba tupatiwe ofisi kwenye kanda mbalimbali hapa nchini jambo litakalotusaidia pia katika utunzaji wa vifaa vyetu vya kazi. Pia, tunataka tuwe na uwezo wa kuajiri wafanyakazi hasa wasimamizi wa uchaguzi hali itakayoiongezea tume kuaminika kwake,” alisema na kuongeza.

“Kikubwa ni watu waongeze uaminifu wao kwa tume ambayo imekuwa ikifanya kazi kubwa, kwani hata nchi ambazo tume zake zinaonekana ziko huru na haki bado zinalalamikiwa kwa mambo kadha wa kadha.”

Trump Ataka Walimu Wapewe Bunduki Marekani

$
0
0
Trump Ataka Walimu Wapewe Bunduki Marekani

Rais wa Marekani Donald Trump amesema kwamba kuwapatia walimu silaha kunaweza kuzuia mashambulio ya risasi katika shule kama lile lililowaua watu 17 wiki iliopita mjini Florida.

''Mwalimu mwenye bunduki anaweza kukabiliana na washambuliaji mara moja'', alisema. Bwana Trump alitoa pendekezo hilo huku manusura wa shambulio hilo la tarehe 14 mwezi Februari wakimtaka kuhakikisha kwamba shambulio kama hilo halitokei tena.

Rais huyo wa Republican pia aliunga mkono wito wa kuwakagua wanakotoka wanunuzi wa bunduki. Manusura wengine wakati huohuo waliwataka wa bunge wa Florida kuweka udhibiti wa bunduki.

''Tutakuwa thabiti iwapo kutakuwa na ukaguzi mbali hali ya kiakili ya mtu anayetaka kumiliki bunduki''. Trump aliwaambia wanafunzi kutoka shule ya upili ya Marjory Stoneman Douglas wakati wa hafla hiyo iliorushwa hewani moja kwa moja katika ikulu ya Whitehouse.

''Haitakuwa maneno kama ilivyokuwa awali'', aliongezea. Rais huyo wa Marekani pia aliunga mkono pendekezo lililoungwa mkono na muungano wa wamiliki wa bunduki NRA .

Rais Trump akishikilia baadhi ya maandishi yake wakati wa mkutano huo
Aliaahidi kuangazia kuhusu wito kwa walimu kupewa bunduki. ''Iwapo una mwalimu ambaye ana bunduki'', alisema ''anaweza kusitisha shambulizi lolote kwa haraka. Iwapo mwalimu angemiliki bunduki , ijapokuwa najua ni swala ambalo lingezua utata, wangepewa mafunzi maalum na wangesaidia pakubwa''.

''Kusingekuwa na uhuru wa kuingia katika shule na kuanza kufyatua risasi, kwa sababu washambuliaji wangekuwa waoga''.

Wanafunzi kuingia na bunduki darasani Texas, Marekani
Majimbo kadhaa ya Marekani tayari yanaruhusu bunduki ndani ya vyuo na taasisi za elimu kulingana na tovuti ya kujihami katika vyuo. Jimbo la Florida hatahivyo halifanyi hivyo.

Rais huyo wa Marekani alisikiliza malalamishi ya mabadiliko ya sheria za umiliki wa bunduki siku ya Jumatano kutoka kwa wanafunzi 40 , walimu na familia.

Baadhi ya wale waliohudhuria hafla hiyo ya saa moja waliunga mkono wazo la rais Trump kuwahami walimu.
Lakini Mark Barden ambaye mwanawe aliuawa katika shambulio la 2012 katika shule ya Sandy Hook Elementary School mjini Connecticut - anasema ''ongezeko la bunduki sio suluhu. Walimu wana majukumu zaidi kwa sasa kwa wao kuchukua jukumu jingine la kutumia nguvu ili kumuua mtu'', alisema.

Mtangazaji Ajifungua Akiwa Anatangaza Redioni

$
0
0
Mtangazaji Ajifungua Akiwa Anatangaza Redioni
Mtangaza mmoja wa redio nchini Marekani amejifungua akiwa hewani wakati wa kipindi chake cha alfajiri.

Cassiday Proctor, mtangazaji wa kipindi cha redio cha alfajiri katika kituo cha redio cha The Arch katika mji wa St Louis nchini Marekani alitangaza kujifungua kwake kupitia njia ya upasuaji siku ya Jumanne.

Bi Proctor alianza kuhisi uchungu wa kujifungua siku ya Jumatatu .Kituo chake cha habari kilishirikiana na hospitali ambayo alijifungua ili matangazo yake kwenda moja kwa moja hewani.

Aliambia BBC kwamba alipata fursa ya kwenda hewani moja kwa moja alipokuwa akijifungua mtoto huyo wiki mbili kabla ya muda uliotarajiwa.

''Ilikuwa furaha kuweza kuwa hewani na wasilikizaji wetu katika siku muhimu ya maisha yangu'' , alisema bi Proctor kuhusu kipindi hicho.

Alisema kuwa kujifungua ukiwa hewani ni mwendelezo ya kile kinachoendelea kila siku katika kipindi hicho ,''mimi huwaambia watazamaji wangu kila kitu kinachoendelea katika maisha yangu.'' .

Mtoto huyo aliyekuwa na uzani wa 7lbs 6oz amepatiwa jina Jameson baada ya wasikilizaji kupendekeza jina la mtoto huyo katika shindano mwezi Januari.

Majina 12 ya kijinga pamoja na mengine 12 yaliochaguliwa na mtangazaji huyo na mumewe yaliwekwa katika sehemu moja .

''Tulipiga kura hadi tulipopata Jameson'', alisema mkurugenzi wa vipindi Scott Roddy .

Mtangazaji mwenza wa bi Proctor Spencer Graves aliambia BBC kwamba hatua hiyo ya kujifungua hewani ilikuwa ya kipekee.


Nay wa Mitego: Naangaikia Kuupeleka Mziki Mbele Siwezi Kujibishana na Mtu

$
0
0
Nay wa Mitego: Naangaikia Kuupeleka Mziki Mbele Siwezi Kujibishana na Mtu
Rapa Nay wa Mitego anayetamba na kibao chake kipya kilichopewa jina la 'Mikono Juu' amefunguka na kudai hawezi kujibishana na mtu yeyote kwa sasa kwani yeye anachokihangaikia ni kupeleka mbele muziki wake ili watu wake waweze kuupata.

Nay ameeleza hayo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo 'PB' inayorushwa na East Africa Radio na kusema kwa sasa amejikita katika kufanya kazi zake zaidi na sio kutafuta kiki kama wanavyofanya wasanii wengine.

"Sasa hivi sitaki kujibizana na mtu kabisa kabisa, 'this time' mimi nataka kufanya kazi zaidi ili nipeleke muziki wangu kwa watu wangu. Miaka miwili mitatu nyuma nilikuwa nafanya zaidi kazi hivi vitu vingine vilikuwa vinakuja nyuma. 'This time' nikiona mtu anaiingia kwa ajili ya kutaka kuleta kelele na mimi nampisha maana huo sio muda wangu", amesema Nay.

Kwa upande mwingine, Nay wa Mitego amesema wimbo wake mpya kuchezwa kwenye bodaboda na sehemu mbalimbali ndicho alichokuwa anakitafuta kitokea na kudai hata vitu vingine vikija sio mbaya ili mradi muziki wake utangulie mbele.

TRA Yaingia Matatani Baada ya Kuweka Hadharani Taarifa za Fedha za Kanisa la Kakobe

$
0
0
TRA Yaingia Matatani Baada ya Kuweka Hadharani Taarifa za Fedha za Kanisa la  Kakobe


Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imejikuta matatani baada ya wadau, maofisa wa benki na viongozi wa dini kuhoji uhalali wa mamlaka hiyo kuweka hadharani taarifa za fedha za Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF).

Juzi, TRA ilitoa taarifa ya uchunguzi ilioufanya kuhusu kauli ya kiongozi wa kanisa hilo Askofu Zachary Kakobe aliyoitoa wakati wa ibada ya mkesha wa Krismasi mwishoni mwa mwaka jana kuwa ana fedha nyingi kuliko Serikali.

Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere alisema wangefanya uchunguzi kuhusu kauli hiyo, lakini taarifa aliyoitoa juzi ilionyesha kuwa Askofu Kakobe hana akaunti katika benki yoyote nchini bali ni mmoja wa wasimamizi wakuu wa akaunti ya kanisa analoliongoza.

Kichere alisema akaunti za kanisa hilo zipo katika benki ya NBC zikiwa na zaidi ya Sh8 bilioni na zinatokana na fedha za sadaka, zaka na changizo zinazotolewa na waumini.

Kichere alipotafutwa na Mwananchi jana kuhusu hatua ya kutangaza taarifa za kifedha za kanisa hilo alisema taarifa yake kwa vyombo vya habari inaeleweka na inajieleza hivyo hawezi kutoa maoni zaidi.

“Wakati nataka kufanya uchunguzi nilieleza wazi nia yangu, hata baada ya kumaliza uchunguzi niliona ni busara kusema yaliyobainishwa katika uchunguzi, sitaki ‘ku-comment’ (kutoa maoni) zaidi, mjadala wa masuala ya Kakobe ulishafungwa,” alisema Kichere.

Akizungumzia taarifa ya TRA, ofisa mwandamizi wa benki moja nchini ambaye hakutaka utambulisho wake uwekwe hadharani alisema kitendo cha mamlaka hiyo kutoa taarifa za fedha kwa umma ni uvunjifu wa sheria.

Alisema kwa mujibu wa sheria taarifa za kibenki zinapokuwa zinahitajika na vyombo au mamlaka za Serikali zinaweza zikatolewa mahakamani, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa au polisi lakini si kwa umma.

Alisema Askofu Kakobe ana nafasi kubwa ya kuwafungulia mashtaka uongozi wa benki na mamlaka iliyotoa taarifa zake kwa umma.

Mkurugenzi mtendaji wa benki (jina limehifadhiwa) alipoulizwa kuhusu utaratibu wa kawaida wa utunzaji wa siri za mteja alisema sheria ya huduma za benki inaelekeza vizuri kuhusu jambo hilo lakini taarifa zinaweza kutolewa kwa mujibu wa sheria kutokana na mazingira na madhumuni fulani.

Alisema hata pale ambapo taarifa zinaonekana ni muhimu kutolewa kwa mamlaka yoyote ya Serikali iliyokidhi vigezo, bado hairuhusiwi kuziweka kwa wazi bali inapaswa kuzitumia kwa kazi yake tu kwa kuwa kuzichapisha kwa namna yoyote ni kuvunja sheria.

“Suala la taarifa za mteja ni siri kubwa ndiyo maana hata ofisa wa benki hana namba ya siri ya mteja. Inapotokea taarifa za mteja zimetolewa halafu zikachapishwa na ile mamlaka iliyopewa taarifa hizo, mteja anaweza akafungua kesi ambayo ni kubwa dhidi ya benki na hiyo mamlaka,” alisema.

Suala hilo halikuwapita viongozi wa dini, kwani nao walikuwa na maoni yao.

Askofu Benson Bagonza wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Karagwe alisema hatua hiyo ni mbaya na haikubaliki kwa taasisi za dini.

“Hiyo ni mbaya sana. Kama Askofu Kakobe asingesema kile alichosema asingechunguzwa. Kwa hiyo kama hutaki kuchunguzwa usiseme kitu? Kwa hiyo maisha yetu yanakwenda mbali hadi kwenye mali za kanisa?” alihoji Askofu Bagonza.

Kauli hiyo iliungwa mkono na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Dk Alinikisa Cheyo aliyeitaka TRA kufuata maadili ya kazi.

“Nafikiri TRA wana maadili wanaposhughulika na wateja wao. Huwezi kuweka wazi madeni na mali za mteja wako. Si makanisa tu hata wateja wa kawaida, labda ni kwa sababu ya mlolongo wa yaliyotokea.” alisema Dk Cheyo.

Hapa Ndipo Ilipofikia Kesi ya Evans Aveva na Mwenzake

$
0
0
Hapa Ndipo Ilipofikia Kesi ya Evans Aveva na Mwenzake.
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa imemaliza maelekezo waliyopewa na Mkurugenzi wa Mashtaka DPP katika jalada la kesi ya utakatishaji fedha inayomkabili Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na mwenzake.

Hayo yameelezwa na Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Leonard Swai, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Victoria Nongwa wakati kesi hiyo ilipoitishwa kwa ajili ya kutajwa.

Swai alidai,  upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika ila kwa upande wao washamaliza maelekezo waliyopewa na DDP kuhusu kukamilisha upelelezi katika baadhi ya maeneo ambapo tayari wamerudisha jalada la kesi hiyo ili aweze kulipitia tena.

Pia Swai amedai kuwa mshtakiwa Aveva ameshindwa kufikia mahakamani kwa sababu anaumwa, pia amepelekwa Kliniki.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Nongwa aliahirisha kesi hiyo hadi March 1,2018 kwa ajili ya kutajwa.

Katika kesi hiyo, mshtakiwa mwingine ni Godfrey Nyange ambapo kwa pamoja wanadaiwa kula njama ya kughushi fomu ya maombi ya kuhamisha fedha ya March 15, 2016 wakionesha Klabu ya Simba inalipa mkopo wa USD 300,000 kwa Evans Aveva wakati si kweli.

Kuhusu shtaka la kutakatisha fedha, Aveva anadaiwa kuwa kati ya March 15, 2016 katika benki ya Baclays Mikocheni alijipatia USD 300,000 wakati akijua zimetokana na kughushi

Ratiba ya Kumwaga Akwilina Yabadirika Hii Hapa Ratiba Kamili

$
0
0
Ratiba ya Kumwaga Akwilina Yabadirika Hii Hapa Ratiba Kamili

Ratiba ya kuaga mwili wa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline imebadilika.

Ratiba ya awali ilieleza kuwa mwili wa mwanafunzi huyo baada ya kutolewa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), ungepelekwa nyumbani kwa dada wa marehemu eneo la Mbezi Louis na mchana kuelekea katika viwanja vya NIT, Mabibo kwa ajili ya kuagwa.

Ratiba mpya iliyotolewa leo Februari 21, 2018 na msemaji wa familia, Festo Kavishe inaeleza kuwa baada ya mwili kutolewa MNH, utapelekwa NIT kwa ajili ya kuagaw.

Kavishe ameiambia MCL Digital kuwa ndugu wataanza safari kuelekea NIT saa 5:00 asubuhi.

Soma: Mwili wa Akwilina kuagwa leo, familia yatoa mchanganuo gharama za Serikali

“Hii ni kwa sababu mazingira ya hapa nyumbani eneo ni finyu. Mpendwa wetu tutamuaga kule NIT saa tano,” amesema.

Amesema nyumbani itafanyika ibada fupi ya wanajumuiya kabla ya kuanza safari kuelekea NIT.

Kifo cha Akwilina kilitokana na kupigwa risasi na polisi Februari 16 akiwa ndani ya daladala eneo la Mkwajuni, Kinondoni jijini Dar es Salaam wakati polisi wakiwatawanya wafuasi wa Chadema waliokuwa wakiandamana kwenda ofisi za mkurugenzi wa Halmashauri ya Kinondoni kudai viapo vya mawakala wao walioshiriki uchaguzi mdogo wa ubunge Kinondoni, Februari 17.

Suluhu Linapatikana Mezani Nasio Maandamano- Gambo

$
0
0
Suluhu Linapatikana Mezani Nasio Maandamano- Gambo
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amefunguka na kuwashukuru Chama cha wafanyakazi Tanzania (TUCTA) kwa kuweza kutatua changamoto za wafanyakazi kwa kukaa nao mezani badala ya ule utaratibu wa zamani uliozoeleka wa kuandamana.

Gambo ameeleza hayo kupitia ukurasa wake maalumu wa kijamii asubuhi ya leo mara baada ya kupata taarifa ya mkoa wake kuchaguliwa kuwa wenyeji wa shughuli za Mei mosi kitaifa 2018.

"Tunawashukuru sana kwa kutupa heshima hii ya kuwa mwenyeji wa maadhimisho haya muhimu yanayohusu wafanyakazi wetu. Nimewapongeza kwa utaratibu wenu wa kutafuta suluhu ya changamoto za wafanyakazi kwa kukaa mezani na serikali badala ya utaratibu wa kizamani wa kuandamana", amesema Gambo.

Sherehe za hizo zilizopewa jina la 'Sikukuu ya wafanyakazi' huwa zinaanzimisha kila ifikapo mwezi wa Tano tarehe moja nchini Tanzania ambapo Rais wa nchi huwa anatumia jukwaa hilo kutatua shida na kero za wafanyakazi papo kwa hapo pamoja na kutangaza kushusha au kupandisha daraja za mishahara bila ya kusahau kodi ya kichwa.

IGP Sirro Awaonya Askari Wanaowabambikia Kesi Watu

$
0
0
IGP Sirro Awaonya Askari Wanaowabambikia Kesi Watu
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro amewataka askari kuzingatia maadili ya kazi na kuacha kuwabambikia watu kesi, kujiingiza katika vitendo vya rushwa.

Sirro ametoa kauli hiyo jana Februari 21, 2018 katika ziara yake ya siku moja wilaya za Handeni na Korogwe mkoani Tanga, ambako licha ya mambo mengine alikagua majalada ya kesi, vielelezo na kuzungumza na askari kuhusu nidhamu.

Amesema askari atakayebainika kupokea rushwa na kuwabambikia watu kesi atachukuliwa hatua za nidhamu.

“Ninatembelea vituo vya polisi kukagua majalada ya kesi, kuangalia sababu za kesi kuchelewa. Pia, ninaangalia kama kuna kesi ambazo wahusika wamebambikiwa ili kuyafanyia kazi mambo haya,” amesema Sirro.

Pia, amevitaka vyombo vya dola Tanga kutoa elimu dhidi ya kesi za ubakaji na wizi wa mifugo kwa kuwa  zinaonekana kukithiri na kutaka hatua stahiki zishukuliwe kwa wahusika.

“Kama kuna kubambikia watu kesi tutabaini, tukimbaini askari tutamwajibisha ndiyo maana ninapitia majalada na vielelezo kuona wanakwama wapi ili tujue kama tatizo ni ofisi ya mkemia mkuu, waseme ili tuweze kufuatilia na kumaliza hizi kesi kwa kutenda haki,” amesema.

Baada ya Kuwasili Nchini Rais wa FIFA Amtaja Samatta

$
0
0
Baada ya Kuwasili Nchini Rais wa FIFA Amtaja Samatta
RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Gianni Infantino amewasili nchini leo alfajiri Feb. 22, 2018 kwa ajili ya mkutano wa FIFA unaofanyika jijini Dar es Salaam.

Rais huyo wa FIFA akiwa uwanjani hapo baada ya kuwasili alipata fursa ya kuzungumza na waziri Mwakyembe ambapo alimtaja nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta, anayecheza soka la kulipwa KRC Genk ya Ubelgiji.

“Nilisikia mchezaji bora wa Afrika kutoka Tanzania, Mbwana Samatt, anayecheza Genk, hii ni nchi ya mpira licha ya changamoto za shirikisho siku za nyuma, lakini kwa sasa mpo kwenye mstari kutokana na uongozi mpya kwa kushirikiana na CAF  na FIFA,” alisema Infantino.

Vilio, Simanzi Vyatanda Muhimbili Wakati wa Kuchukuliwa Mwili wa Akwilina

$
0
0
Vilio, Simanzi Vyatanda Muhimbili Wakati wa Kuchukuliwa Mwili wa Akwilina
VILIO na simanzi vimetawala wakati wa kuchukua mwili wa aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini aliyeuawa kwa kupigwa risasi Feb 16, 2018.

Mwili wa Akwilina umechukuliwa leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na kupelekwa NIT k wa ajili ya kuagwa kabla ya kupelekwa nyumbani kwao Rombo kwa mazishi.

Jeneza lenye mwili wa mwanafunzi huo liko katika gari maalumu la kubebea maiti.



Baada ya kuaga mwili wa mwanafunzi huyo, saa 10 jioni safari kuelekea wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro kwa mazishi itaanza. Akwilina atazikwa kesho.










Muhubiri Maarufu Nchini Marekani Afariki Akiwa na Miaka 99

$
0
0
Muhubiri Maarufu Nchini Marekani Afariki Akiwa na Miaka 99
Mhubiri maarufu nchini Marekani na duniani, Billy Graham amefariki duniani akiwa na umri wa miaka 99.

Graham ambaye ni raia wa Marekani aliyeanza kuhubiri jijini London Uingereza mwaka 1954, alikusanya maelfu ya watu kila mahali alipofanya mikutano ya injili.

Katika eneo la Afrika Mashariki, Graham aliwahi kuhubiri Tanzania miaka 55 iliyopita, wakati ikiitwa Tanganyika ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya Afrika aliyoifanya katika miaka ya 1960.

Inaelezwa kuwa katika mkutano wake uliofanyika Februari 28,1960 watu 40,000 walihudhuria mkutano wa siku moja.

Hata hivyo, taarifa iliyopatikana katika mtandao wa shirika lake haikueleza ni sehemu ipi mkutano huo ulifanyika mbali ya kufahamisha makadirio ya watu waliohudhuria.

Mhubiri huyo ambaye alikuwa mkosoaji mkubwa wa viongozi wabaguzi wa rangi amehubiri zaidi ya watu milioni 210.

Graham, akiwa na umri wa miaka 16 baada ya kumsikiliza mhubiri mmoja alianza huduma ya mahubiri mwaka 1939.

Mhubiri huyo alifanya kazi kama ofisa wa mauzo na aliendelea na kuwa mmoja wa wahubiri wenye ushawishi mkubwa miongoni mwa watu wa dini zote huku akiwashauri marais na viongozi wengine wengi duniani juu ya imani ya Kikristo.

Mwaka 1949, alipata umaarufu wakati akihubiri kwa wiki nane kwenye hema kubwa huko Los Angeles. Graham ni mhubiri aliyeepuka kashfa mbalimbali zilizowazonga wahubiri wengi waliotumia vituo vya televisheni kusambaza injili.

Jeshi la Polisi Limekana Kumkamata Mwandishi wa Habari Emmanuel Kibiki

$
0
0
Jeshi la Polisi Limekana Kumkamata Mwandishi wa Habari Emmanuel Kibiki
Jeshi la polisi mkoa wa Njombe limekana kumkamata mwandishi wa habari Emmanuel Kibiki ambaye anadaiwa kukamatwa majira ya saa tisa usiku wa kuamkia leo Februari 22, 2018  na watu waliojitambulisha kuwa ni jeshi la polisi.


Akizungumza na www.eatv.tv Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe, John Temu amesema kuwa wao hawajamkamata mwandishi huyo na kudai huenda akawa amekamatwa na taasisi zingine ila si jeshi la polisi.

"Hakuna ukweli wowote ule kama kungekuwa na ukweli stori ingekuwa imeshafika kwetu ila inawezekana labda taasisi zingine za upelelezi zinafanya kazi zikawa zimemkamata maana taasisi za upepelezi huwa zinawakamata watu zenyewe, kwa hiyo watu wanapicha tu kuwa mtu akikamatwa basi jeshi la polisi ndilo linakuwa limemkamata.Kwa sababu kama sisi tungekuwa tumemkamata mpaka asubuhi hao polisi wangekuwa wamewasiliana na mkoa kutoa taarifa" alisema John Temu

Februari 22, 2018 zimeibuka taarifa zikidai kuwa mwandishi wa habari wa Makambako amekamatwa majira ya saa tisa usiku na watu ambao walijitambulisha kuwa ni jeshi la polisi lakini upande wa jeshi la polisi wamekataa kuhusika kumkamata mwandishi huyo wa habari.


Takukuru: Hatucheleweshi Kesi Inayomkabili Malinzi Bali Jalada Lipo kwa DPP

$
0
0
Takukuru: Hatucheleweshi Kesi  Inayomkabili Malinzi Bali Jalada Lipo kwa DPP
TAKUKURU imeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa hawaicheleweshi kwa makusudi kesi ya utakatishaji fedha inayomkabili aliyekuwa Rais wa (TFF), Jamal Malinzi na wenzake bali jalada lipo kwa DDP.

Mbali na Malinzi, washtakiwa wengine ni Katibu wa TFF, Mwesigwa Selestine na Mhasibu wa shirikisho hilo, Msiande Mwanga.

Wakili wa TAKUKURU, Leornad Swai amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na jalada lipo kwa DDP analipitia ili atoe kibali cha usikilizwaji wa kesi hiyo.

Hata hivyo, Wakili wa utetezi Abraham Senguji amedai ni miezi 8 hadi sasa wateja wao wapo gerezani, hivyo anaomba upande wa mashtaka uharakishe upelelezi.

Baada ya kueleza hayo, Swai alidai kuwa hawacheleweshi upelelezi wa kesi hiyo kwa kusudi bali jalada lipo kwa DDP analipitia hivyo anaomba kesi iahirishwe hadi tarehe nyingine.

Baada kueleza hayo, Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi March 1,2018 kwa ajili ya kutajwa.

Washtakiwa kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 28, ikiwemo ya utakatishaji fedha ambazo ni Dola za Marekani, 375,418.

Mwanamume Atolewa Uvimbe wa Kilo 1.8 Kwenye Ubongo

$
0
0
Mwanamume atolewa uvimbe wa kilo 1.8 kwenye ubongo
Madaktari nchini India wamefanya upasuaji wa kipekee na kuondoa uvumbe wa uzani wa kilo 1.8 kutoka kwa mwanamume wa umri wa miaka 31.

Wanasema huo huenda ukawa uvimbe mkubwa zaidi kuwahi kutolewa kwenye ubongo wa binadamu.

Upasuaji huo, ambao ulidumu saa saba, ulifanyika mnamo 14 Februari katika hospitali ya Nair mjini Mumbai magharibi mwa nchi hiyo.

Lakini taarifa za upasuaji huo hazikutangazwa moja kwa moja kwa sababu madaktari hawakuwa na uhakika iwapo ulifanikiwa.

"Sasa ni suala tu lake kupona, lakini maisha yake hayamo hatarini tena," Dkt Trimurti Nadkarni, mkuu wa upasuaji wa mfumo wa neva, ameambia BBC.

Santlal Pal, mwuzaji duka kutoka jimbo la Uttar Pradesh kaskazini mwa India, amekuwa akiishi na uvimbe huo kwa miaka mitatu.

Madaktari wanasema Pal alipoteza uwezo wake wa kuona kutokana na uvimbe huo.

Hata hivyo, kuna matumaini kwamba huenda akapata uwezo wa kuona tena baada ya kupona.

Mke wake ameambia gazeti moja India kwamba alikuwa ameambiwa na madaktari katika hospitali tatu tofauti Uttar Pradesh kwamba uvimbe huo hauwezo kuondolewa.

"Visa kama hivyo huwa hatari sana," Dkt Nadkarni alisema, na kuongeza kwamba Pal alihitaji painti 11 za damu wakati wa upasuaji huo.

Mwanamke aliyetajwa kuwa mwenye uzani mkubwa zaidi duniani amefariki
Aidha, alitumia mtambo wa kumsaidia kupumua kwa siku kadha baada ya upasuaji huo.
Viewing all 104747 articles
Browse latest View live




Latest Images