Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104712 articles
Browse latest View live

John Mnyika:Katiba Mpya Haipatikani Mwaka 2014 Kama Ilivyokuwa Ikitarajiwa na Wengi

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Ubungo Mh.John Mnyika amefunguka na kuweka wazi kuwa Katiba Mpya haiwezi kupatikana mwaka 2014 kama ambavyo ilikuwa ikitarajiwa,Mnyika amefunguka hayo leo akiwa katika kipengele cha Kikaangoni Live

kinachofanyika kila siku ya Jumatano kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV.
Mnyika amesema kuwa hata kama ikitokea UKAWA wakirudi bungeni suala la kupatikana kwa katiba mpya litakuwa ni kitendawili kutokana na namna mchakato ambao ni lazima kupitia ili kupata hiyo Katiba mpya.
"Ni kweli 2014 haiwezekani kupatikana kwa Katiba mpya,kwani siku 60 alizotoa Rais Kikwete hata kama UKAWA ikirudi bungeni hazitoshi kumaliza ibara zote 271 na sura 17 kama mpaka sasa zinabishaniwa sura mbili tu. Hata kama ikipatikana, itahitaji kupigiwa kura ya maoni, kwa taarifa nilizonazo toka ndani ya tume ni kwamba inawezekana ikiwa Mwezi Machi 2015.Hata ikiwa muda huo, Shirikisho la Serikali Tatu likiwa ndio muundo Katiba za Tanganyika na Zanzibar zitapaswa kuandikwa upya. Hivyo, kutahitajika Bunge Maalum na kura ya maoni ya Tanganyika, na hata tume ya maoni hata kama itatumia maoni kwa sehemu yaliyokusanywa na Warioba na rasimu ambayo wanadai wanayotayari. Hata kama ingekuwa katiba mpya ya Serikali mbili, bado Sheria muhimu zinazokinzana na katiba mpya zitapaswa kuandikwa upya. Hivyo, kwa vyovyote vile, katiba mpya haiwezi kutumika kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Mbali na hilo Mnyika ameweka wazi msimamo wa Umoja wa Katiba ya Wanchi (UKAWA) kuwa hawawezi kurudi katika Bunge Maalumu la Katiba kama hakutakuwa na maridhiano yenye kuheshimu na kutambua maoni ya wananchi na kutambua misingi ya rasimu ya Katiba uliyotokana na maoni ya wananchi

Alichokisema Anti Ezekiel baada ya kusemekana anatoka na dansa wa Diamond Platnumz.

$
0
0
Mwanzoni mwa wiki hii miongoni mwa stori ambazo zilitoka na kuenea kwenye magazeti kadhaa ni pamoja na inayomhusu Anti Ezekiel kusemekana kuwa anatoka na dansa wa Diamond Platnumz.
Taarifa ya awali ilidai kuwa mpenzi huyo wa dansa wa Diamond alienda kufanya vurugu nyumbani kwa Anti Ezekiel,Anti Ezekiel kapatikana na kaongelea mahusiano yake na Moses Iyobo ambaye ndiye dansa wa Diamond Platnumz. 

SIKILIZA HAPA CHINI:

Msichana wa Kihindi Aachana na Familia Yake Tajiri na Kuhamia Kijijini kwa Kijana Mkenya

$
0
0
Tumezoea kuona kwenye filamu au tamthilia simulizi la msichana mrembo anaotoka katika familia ya kitajiri aliyechagua kuyaacha maisha ya raha na kuishi uswahili na kijana anaempenda.

Huko Kenya, kumeripotiwa tukio halisi lililovuta hisia za wengi na kuzungumzwa zaidi kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari, ambapo msichana wa kihindi ameamua kuachana na familia yake tajiri na kuambatana na kijana wa Kenya aliyezama nae kwenye vilindi vya mahaba.

Msichana huyo wa kihidi anaifahamika kwa jina la Sarika Patel, ameolewa na kijana wa kabila la Bukusu, Timothy Khamala uamuzi ambao ni nadra kutokana na mila na desturi za kihindi na kilichoshangaza zaidi ni kuwa wawili hao wanaishi maisha duni kijijini.

 Kwa Sarika, maisha ya umasikini sio kikwazo cha kulipata penzi la kijana Timothy aliyenasa kwenye penzi lake.

Safari ya penzi la Sarika na Timothy ilianzia nyumbani kwao Sarika ambapo kijana Timothy alikuwa akifanya kazi na baadae kutimuliwa kwa kudhaniwa kuwa ana uhusiano na princess wa jengo hilo (Sirika) jambo ambalo lilikuwa kweli.

Ingawa wawili hao wamejitoa na kuendelea kuishi pamoja licha kukiri kuwa wanakabiriwa na changamoto kubwa ya kutengwa na jamii ya upande wa familia ya kwao Sarika kwa kuwa kitendo hicho sio sahihi hata kidogo kwa mujibu wa mila na desturi zao, ambapo watu wa jamii sawa ndio wanaooana.

Hata hivyo, Sarika ameelezea msimamo wake kuwa utofauti wa rangi na tamaduni au ufukara wake hauwezi kumtenga na mpenzi wake wa dhati Timothy.

Mapenzi sio pesa, mapenzi ni moyo.

Diamond Platnumz Is More Than Grateful To Be Alive

$
0
0
Many of us are used to complaining about every little thing in life whether good or bad. We will complain about not having a job and then complain even more when we get one.

An underground artist will  complain about poor publicity when he is struggling to make it, and then complain about poor pay or something else when he gets the publicity he so desired, but not Diamond Platnumz.

Tanzania sensation Diamond Platnumz is more than grateful for what he has and although there is so much more he is yet to achieve, he has chosen to at least be thankful that he is alive as there are those struggling even to breathe.

Wakati Tukipumua mda huu..sehemu flani kuna mtu ndiyo pumzi yake ya mwisho..ni vyema kuacha kulalamika na tujifunze, kuishi maisha yetu na kuridhika na tulicho nacho(siyo kuridhika kubweteka)

As we breathe right now, another person takes his last. Is better to stop complaining, and learn to live our life with what we got.”

His grateful nature for what he has could be the reason the ‘Number One’ hit maker is making it big in a world many have found impossible to survive in.

This should teach us to at least thank the most high for whatever little we have in life and maybe we will view life differently and live happily.

Baby Madaha Amwagana Kimapenzi na Manager Wake Mkenya Joe Kairuki

$
0
0
STAA wa filamu Bongo, Baby Joseph Madaha amemwagana na aliyekuwa mwandani wake ambaye pia ni meneja wake, Joe Kairuki pasipokuwa na sababu za wazi.

Chanzo chetu cha kuaminika kilichoomba hifadhi ya jina lake kimetutonya kuwa, Madaha na Joe wamebaki kuwa mtu na bosi wake ila msanii huyo sasa amejiweka kwa mwanaume mwingine.

Katika kujua ukweli wa ishu hiyo, mwandishi wetu alimpigia simu Madaha ambaye alisema: “Hee unaniuliza kuhusu Joe, mbona umechelewa kujua? Nimeachana naye, sasa nimejipatia mpenzi wangu mwingine na tunapendana kupita maelezo.”

Nisha 'Watu Bwana Eti Nina Mimba! Sijui Wanatoa Wapi Haya Maneno'

$
0
0
Stori: Gladness Mallya
MWANADADA kutoka kiwanda cha filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ amepangua madai kuwa ni mjamzito na kudai ni maneno ya ya watu licha ya kwamba ukikiangalia kwa makini kitumbo chake unaweza kuhisi kuna kitu ndani.

Akizungumzia madai hayo na kwamba ndicho kinachomfanya asijichanganye na wenzake kama kawaida, Nisha alisema kutoonekana kwake ni maamuzi tu. “Eti nina mimba! Mh…nashangaa sana, sijui watu wanatoa wapi hayo maneno, mimi sina mimba na nilikuwa sionekani kwa sababu nilisafiri, pia mwezi mtukufu huwa sitoki hovyo, nikiamua kuzaa watu wataniona tu,” alisema Nisha.

Angalia Video ya Wimbo wa Mrembo Aliyedaiwa Kuchepuka na Jay Z Akimdiss Beyonce Huku Akionesha Urembo Wake

$
0
0
Mrembo aliyeripotiwa kuwa mchepuko wa Jay tangu miaka miwili iliyopita ameamua kuachia audio na video ya wimbo wake maalum kumdiss Beyonce, wimbo alioupa jina la ‘Sorry Ms Carter’.

Katika wimbo huo, msichana huyo ameeleza kuwa alikuwa anamheshimu sana Beyonce na ndio sababu aliamua kutochepuka na mumewe, lakini anaona Bey amevuka msitari na ndio maana  ameamua kumvaa.

Mrembo huyo anamkumbusha Beyonce kuwa mumewe anapenda sana wasichana wazuri wanamitindo kama yeye.

“You know what I was gonna respect you but since you crossed over into my lane it’s time to check you“The man? He likes model chicks. He likes all naturally flawless model chicks, like me.



You actin’ nonchalant for the audience / ‘Cause I ain’t just another shorty you put the naughty on.”

Katika interview aliyofanya muda mrefu uliopita, msichana huyo alieleza kuwa alikutana na Jay Z wakati wanafanya tangazo na ndipo alipopata mshituko na kudata kwake. Alieleza kuwa baadae Jay Z alimtuma mmoja kati ya walinzi wake na alimuomba amuandikie namba ya simu kwenye karatasi ili baadae jamaa akitulia ampigie.

Kwa lugha ya kujigamba, mrembo huyo anadai alionesha utofauti na kumkatalia kwa kuwa alimheshimu Beyonce.

Jack Wolper Adaiwa Kutibua Uchumba wa Ney wa Mitego na Siwema

$
0
0
Kuna tetesi na Minogono Kitaani kuwa Mwanamuzi Ney wa Mitego anachepuka na Mbongo Movies Jackline Wolper...
Ney Ameulizwa kuhusu hilo na Kujibu kuwa hizi ni story tu zinasema ila si kweli kuwa wanatoka wote, Ney Amezidi kusema kuwa habari hizi zinafanya mpaka muda mwingine wanagombana na mpenzi wake Siwema kwani Watu wanamletea umbea usio wa Kweli ...Amesema Jack Wolper ni rafiki yake na ukaribu wao ni wa Kikazi Zaidi .

Nifuate Instagram Kujua Mengi :Bonyeza hapa: Instagram

Baada ya Kusifiana Instagram Hatimaye Agness Masogange na Mkenya Corazon Kwamboka Wakutana

$
0
0


Agness Masogange na Mwanadada Mkenya Corazon Wote wamejaliwa maombo mazuri yenye kuwafanya wanaume wa run mad, Hawa walianza kusifiana Kupitia Instagram huku wakiwa hawajakutana uso kwa uso , Agness akiweka picha basi Corazon ata comment na kuisifia vile vile Corazon akiweka picha Masogange ata comment kuisifu , Wawili Hao hatimae wameonana South Afrika na Kula Bata Pamoja.....Kwa unavyoona Who is Cute zaidi?

Nifuate Instagram Kujua Mengi :Bonyeza hapa: Instagram

Jokate Amfanyia Interview Ex Wake Diamond, Mashabiki Wadai Wanaoneana Aibu!

$
0
0
Msimu wa pili wa kipindi cha The One Show cha TV1 umeanza. Kinachofanyika kwa sasa ni kurekodiwa kwa vipindi hivyo vitakavyoanza kurushwa hivi karibuni. 
Leo, watangazaji wa kipindi hicho, Ezden Jumanne na Jokate Mwegelo walikuwa wakimhoji Diamond Platnumz. 

Diamond ameshare picha kwenye Instagram akiwa amekaa kwenye kochi na ex wake Jokate, na kuvutia comments nyingi kutoka kwa mashabiki. 

Baadhi ya mashabiki wamedai kuwa wawili hao waliowahi kuwa wapenzi kwa muda mfupi, walikuwa wakioneana aibu. Ni kweli?

Nifuate Instagram Kujua Mengi :Bonyeza hapa: Instagram

Bob Junior: Sijarudiana na Mke Wangu ila Naumia Kuwa Mbali Na Mwanangu (Audio)

$
0
0
Rais wa Masharobaro, muimbaji na mtayarishaji wa muziki, Bob Junior amekanusha tetesi zilizokuwepo kuwa amerudiana na mke wake.

Akiongea na segment ya Inbox ya kipindi cha New Chapter cha Radio Free Africa, Bob Junior amesema mazoea ya kuwa na mke na kumuona mtoto wake kila siku yanamfanya awe na huzuni kubwa kuwa mbali nao. Junior amesema aliachana na mke wake na hajarudiana naye tena na hana mpango wa kuoa hivi karibuni.

Hivi karibuni kwenye Instagram Bob Junior alipost picha ya mwanae na kuandika:

Namshukuru Mungu kukupata wewe maisha yangu yote nguvu zangu zote Nitapigana hadi kufa ni kwaajili yako my son Rummy Raheem Rummy maisha yako huta jutia kupata baba kama mimi ila amini kilicho tokea……. ukija kukuua ipo siku utajua yote naishi kwenye maumivu mengi juu yako sana na hapa naandika text hii nalia sana kwa kuwa mbali nawewe sikuoni karibu my son ila jua i love u na kama mapenzi kupenda nasema nitakupenda na hata kuja yoyote kuzidi mapenzi yangu kwako mengine sisemi ila jua mwanangu nipo kwenye wakati mgumu wa kuto kuwa karibu na wewe i love u my son ( rummy .”

Sikiliza mahojiano ya Bob Junior Hapa Chini:

Wema Sepetu Ang'aka 'Maswala ya Kuforciana Kuzaa Sipendi na Sitaki Jamani Sitaki'

$
0
0
Wema Leo Ameamua Kuwafungukia Wala wanaopenda kumforce azae, Wema aliweka Picha ya Kim Kardashian akiwa amembeba Mtoto wake na Kuandika Mbona Huyo Kazaa akiwa Miaka ya 30 sasa kwanini watu wanamforce wakati yeye bado yupo 20's Jisomee Mwenyewe hapo chini:
Nifuate Instagram Kujua Mengi :Bonyeza hapa: Instagram

Baada ya Kufanya Siri Sasa Mambo Hadharani Kati ya Petit Man na Dada wa Diamond

$
0
0
Hivi karibuni kumekua na tetesi za chini ya kapeti kuwa dada yake msanii Diamond, Esma ana mahusiano ya kimapenzi na mfanyakazi wa ENDLESS FAME, Petitman maarufu kama Mutoto ya Madame Wema au Petitman Wakuache....sasa leo hii imebainika wazi kua wawili hao ni wapenzi...

Ilianza hapa....

MENEJA wa Wema Sepetu, Martin Kadinda aliweka picha hii kwenye ukurasa wake wa instagram ana kuandika "ALERT!!! ALERT!!!"
 Akiashilia kuna kitu hapa........

Hatuja kaa vizuri Usipojipanganitakupanga wa Instagram akaibuka na hii:

Nifuate Instagram Kujua Mengi :Bonyeza hapa: Instagram

Naibu Waziri Stephen Maselle Na Mchange walipanga Kuilipua Helkopta Ya CHADEMA ili Kumuua Slaa

$
0
0
Diwani Sebastiani amewaambia wanahabari kuwa mwakajana walifanya vitendo haramu wakishirikiana na CCM na baadhi ya waliokua wanachadema wakiongozwa na Mchange. Wanasema wamekuja kuomba toba kwa viongozi wa juu wa CHADEMA na wanachama ili wasamehewe kwa usaliti huu mkuu Wanasema baada ya Zitto kuvuliwa madaraka ndani ya Chadema ,Mchange alipewa Dili na CCM la kuwarubuni madiwani na viongozi ndani ya CHADEMA ili watoe matamko na kuonyesha kuwa Chama kina mpasuko Anasema January 2014 Mchange alimpigia simu kuwa Naibu waziri wa Nishati na Madini Steven Masele ana dili la shilingi milioni 180. Na baadae Masele alimpigia simu wakakutana na kupanga njama za kufuatilia ziara ya Dr. Slaa kanda ya ziwa na kupanga kuilipua Helkopta ya Dr.Slaa iliyokua itue Shinyanga

 ANGALIA VIDEO HAPA CHINI:

Aina za Mabinti Na Tabia Zao Katika Mapenzi Kulingana na Maumbo ya Miili Yao

$
0
0
Inasemekana wadada wana tabia tofauti katika mapenzi kulingana na maumbo ya miili yao:

1. Wasichana wafupi wanaongoza kwa wivu wa mapenzi na kuwajali wapenzi wao

2. Wasichana warefu huwa hawawajali wapenzi wao na hawaogopi mahusiano kuvunjia hawajui
kubembeleza hata kdogo

3. Wasichana wenye DIMPOZ,MWANYA,M
ATEGE MBINUKO,MAHIPS NA KITEMBE,hawa huongoza kwa kutokuwa WAAMINIFU katika mapenzi

4. Wasichana WANENE huongoza kwa MAPENZI YA KWELI yaani akipenda amependa kweli

5. Wasichana WEMBAMBA hawa huwa ni WABISHI sana na hawa wanaongoza kwa kutendwa!

6. Wasichana wenye NGOZI NYEUSIwanaongoza kwa KUTOA MIMBA na kupenda wanaume warefu na weupe

7. Wasichana weupe wakiongoza kwa kuzalia nyumbani, na hawa weupe weng wao
huolewa wakiwa na watoto tayari huku wakipenda kuolewa na waarabu kulko wanaume weusi.

Je kuna kundi jingine unalolijua na tabia zao?

Ephraim Kibonde Wa Clouds Azua Mtafaruka Asubuhi ya Leo Agonga Gari na Kukimbia Traffic Wamshika Ubungo

$
0
0
Asubuhi ya leo Kibonde wa Clouds anadaiwa kusababisha ajali asubuhi hii eneo la Makumbusho, amemgonga dereva mwingine kwa nyuma. Trafiki walipofika kupima ajali, Kibonde karudi nyuma kaendesha gari lake kasepa! Trafiki katumia gari lililogongwa kumfukuzia. Walifanikiwa kumkamata eneo la Mwenge. Trafiki aliingia katika gari lake nakumwomba arudi eneo la ajali ili wakapime na kuchora mchoro wa ajali. Kibonde kagoma na kumtaka trafiki ashuke katika gari lake, trafiki naye kagoma kushuka. Mchezo ulioendelea Kibonde aliondoa gari na kuanza kupiga misele, akizunguka mitaa akiwa na trafiki huyo! Trafiki aliwasiliana na wenzake ambao walianza kuifuatilia gari hiyo ya Kibonde kila kiunga cha jiji hususani eneo la Mwenge na Ubungo. Hayawi, hayawi yakawa, Kibonde akatokea maeneo ya mataa ya Ubungo, hapo nikashuhudia senema ya Kibonde na trafiki! Trafiki wa kike aliyekua eneo hilo akaipiga mkono gari ya Kibonde iliyokuwa kasi, gari hiyo haikuonesha dalili za kupunguza mwendo. Trafiki alikomaa kusimama mkono wake ukiwa juu kuashiria kumtaka Kibonde asimame huku akipaza sauti katika radio call akisema ananigonga, afande, ananigonga! Akiwa katika hali hiyo, kuna gari ilikotokea sikujua ikakatisha kati ya trafiki na gari ya Kibonde ndiyo ikawa kigingi cha gari ya Kibonde na kutiwa mbaroni na Kupigwa Mitama kadhaa Aligoma kuendesha gari ikabidi livutwe hadi polisi Urafiki ambapo kwa sasa amepelekwa Oystabay! Kwa utafiti wangu kidogo nilioufanya nikifukuzana na muda kuwahi kanisani, ni kwamba Kibonde na watu wengine aliokuwanao ndani ya gari lake walikuwa 'TINGASI'!

Basi la Kampuni ya Five Aliance Laungua na Kuteketea Kwa Moto Likiwa Safarini

$
0
0
Hili ni basi la kampuni ya 5 Aliance ambalo linafanya safari zake kati ya Mtwara na Dar es salaam limeungua asubuhi ya August 09 likitokea Mtwara kuelekea Dar es salaam.
Taarifa ya awali inasema kuwa hakuna abiria aliyepata madhara yoyote juu ya kuungua kwa basi hili ambalo limeteketea kijiji cha Mihambwe mkoa wa Lindi.

Mwanafunzi Chuo Kikuu Alazimishwa Kurekodi Picha za Ngono Baada ya Kudanganywa Anapelekwa Ulaya

$
0
0
Kweli dunia ina mambo! Kuna watu wanajaribu kutumia kila fursa inayopatikana kujinufaisha kwa kupata fedha hata ziwe ‘chafu’, kwao kitu cha maana ni kupata utajiri kwanza.

Kundi la watu wanaofanya biashara ya kusafirisha watu, wamekuwa wakitumia fursa ya ukosefu wa ajira kama chambo cha kuwanasa vijana na kuwaingiza kwenye biashara haramu kama ukahaba.

Hivi karibu kundi hilo linalosafirisha watu lilipita katika vyuo vikuu kadhaa nchini Uganda na kuwaahidi wanafunzi kuwa lingewatafutia kazi Ulaya na Marekani, kwani lina uzoefu wa kutosha na kazi hiyo. Mmoja wa vijana ‘waliobahatika’ kupata nafasi ya kwenda Ulaya kufanya kazi ni Sunday Bekunda (25), mwanafunzi wa mwaka wa pili katika Chuo Kikuu cha Makerere, Kampala.

Kwa bahati mbaya ‘neema’ ya kwenda Ulaya iligeuka balaa baada ya kutekwa na kulazimishwa kufanya ngono na wanawake mbalimbali huku akirekodiwa kwenye kamera za video.

“Ilikuwa ni Januari 2013, nilipokutana na mwanaume mmoja anayeitwa Charles kutoka katikati ya Jiji la Kampala, ambaye aliniahidi kunipeleka Kenya kufanya kazi katika kiwanda.

“Sikujua kuwa Charles alikuwa msafirisha watu. Alikuwa anaonekana kama mzazi wa makamo aliyefanya kazi kwa miaka mingi.

“Nilifungua moyo wangu na kumweleza changamoto nyingi ninazopitia na namna nilivyo hangaika kutafuta kazi ili nipate fedha za kulipia masomo ya ziada. Kwa kifupi ni kama nilikuwa namwambia Charles kuwa sikuwa natafuta kazi bali nilikuwa nataka kazi yoyote.”

Safari ya Kenya

“Siku iliyofuata nilikuwa tayari kwa safari na nilimkuta Charles akiwa kwenye gari la binafsi aina ya Toyota Noah. Alikuwa pamoja na wasichana sita na wavulana wawili. Alituambia kuwa tutaingia Kenya kwa kupitia mpaka usio rasmi unaoitwa Chepskunya.

“Tukiwa njiani, Charles alikuwa anaongea sana na kutusisitizia kuwa ‘tusimwangushe’ tukifika huko. “Tulipofika Kenya walituchukua na kutuingiza kwenye nyumba moja nzuri ya makazi ya watu, hapo tulikutana na wenzetu 15, wavulana wawili kutoka Rwanda na Wakenya 13.”

Kutekwa

“Charles alituacha hapo tukiwa chini ya mwanamke mmoja na wanaume wanne wenye miili iliyojengeka vyema. Watu hao walianza kutupiga makofi na kutulazimisha tuvue nguo. Ndipo nilipobaini kuwa kilichoonekana kama ni safari sasa imegeuka utekaji.
“Baada ya kupigwa tuliambiwa tutoe mifukoni kila kitu tulichokuwa nacho na kuweka juu ya meza. Nilishtushwa nilipoona vyeti vya wanafunzi wa Uganda kutoka Vyuo Vikuu vya Kyambogo, KIU (Kampala International University), Nkumba na UCU (Uganda Christian University). Hata vyuo vya Kenya vilikuwapo.

“Mwanamke alitutishia kutuua kama tusingetii walichosema. Kudhihirisha alichokuwa anamaanisha, alituonyesha mkanda wa video wa mtu akiuawa na kupasuliwa tumbo.

“Halafu wakaweka video vyingine iliyotuonyesha biashara tutakayokuwa tunaifanya, ambayo ni kuigiza picha za ngono.”

Ratiba ya kufanya ngono

“Walituongoza hadi ghorofa ya juu na kutuweka katika vyumba tofauti. Katika chumba nilichokuwepo aliingia mtu na kuniambia nitoe nguo kisha akanipa chupi tatu zinazobana.

“Hicho chumba kilikuwa na mwanga mkali na kamera za CCTV katika kila kona. Baadaye wakamleta Bridget, mmoja wa wasichana niliotoka nao Uganda, kisha wakaniambia kuwa nipo huru kufanya naye ngono. Walipoondoka na kufunga mlango, Bridget alianza kulia na kupiga kelele.

“Matukio mabaya yalianza rasmi siku iliyofuata wakati yule mwanamke alipoingia kwenye chumba changu akiwa ameshika mikanda mitatu ya ngono. Baadaye waliletwa wanawake na wanaume niliokuja nao nikaambiwa nifanye nao ngono wakati watu wengine wakirekodi kwa kutumia kamera kubwa.

“Nilipoishiwa nguvu, yule mwanamke alitoka nje na kurudi halafu alinichoma sindano yenye dawa ambayo ilinifanya nipate nguvu tena na kuendelea. Nikapewa ratiba ya kulala na wanawake asubuhi, wavulana jioni (mashoga) na wanawake watu wenye umri mkubwa usiku.

“Wanawake hao walikuwa wanawalipa wale jamaa ili tufanye nao ngono. Kuna wakati nilikuwa nalazimishwa kulala na wanawake saba kwa siku huku nikipata maumivu makali.”

Mauaji

“Baada ya wiki tatu wote tuliitwa sebuleni na kupewa taarifa kuwa mmoja wetu, aliyeitwa Sam Muteesi kutoka Uganda, alikuwa amekataa kuwatii kwa hiyo alitakiwa auawe mbele yetu. Walimfunga kwenye kiti, japokuwa alikuwa akiomba sana msamaha walimfunika  usoni kwa kutumia begi hadi alipokufa.

“Kwa kipindi chote cha Januari na Februari 2013, nilikuwa nikifanya ngono za kila aina kila siku huku nikitumia dawa za kulevya na pombe.
“Mwanzoni mwa Machi, Charles alikuja kwenye chumba changu na kuniambia kuwa ninatakiwa kwenda kuoa Uingereza. Halafu akafungua kompyuta yake na kunionyesha picha ya mwanaume mzee mzungu.

“Akaniambia nipite mbele ya kompyuta hiyo nikiwa nimevaa chupi nilizopewa ili huyo mzungu anione (kupitia Skype) kama nifaa.

“Huyo mzungu alinipenda, hivyo Charles akawa amepata ‘dili’ ambayo ingenipeleka Uingereza, lakini kwa kuwa sikuwa Mkenya nilitakiwa nirudi Uganda kuchukua hati ya kusafiria.

Atoroka

“Wakati tukivuka mpaka kuingia

Uganda, nilifanikiwa kukimbia pale Mbale tulipokuwa tumesimama kunywa chai. Nilitoa taarifa yangu na kufunguliwa faili namba SD REF 65/19/03/2013. Kwa kuwa Charles alikuwa mtu mwenye nguvu (kifedha) hakufanywa chochote.

“Kutokana na mateso niliyopitia nilikuwa kama kichaa, nililazwa katika Hospitali ya Vichaa ya Butabika na nilipewa matibabu kati ya Agosti na Desemba 2013.

“Pia nilipimwa vipimo vingine na kugundulika kuwa nilikuwa na maambukizi yote makubwa ya magonjwa ya zinaa.“Nimeamua kusimulia habari yangu kama sehemu ya kampeni ya kuwaonya vijana wa vyuo vikuu kuwa makini na watu wanaowaahidi kuwatafutia kazi nje ya nchi.”

Imeandaliwa na Goodluck Eliona kwa Msaada wa Redio Netherlands Worldwide (RNW)



Wabunge CCM Wameguka Katiba Mpya...Mwigulu Nchemba Apasua Jipu

$
0
0
Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimeanza kumeguka baada ya baadhi ya wabunge wake ambao ni Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, kuunga mkono kauli ya Naibu Katibu Mkuu wake, Mwigulu Nchemba.

Nchemba ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha, Jumanne iliyopita akichangia wakati wa mjadala wa mabadiliko ya kanuni, alilitaka Bunge Maalumu la Katiba lijitathmini kama lina ulazima wa kuendelea wakati hakuna uhakika wa kupatikana kwa theluthi mbili.

Alisema kitendo cha Bunge hilo kukaa kwa siku 84 bila uhakika wa kupatikana kwa theluthi mbili kwa pande zote mbili inayohitajika kupitisha Rasimu ya Katiba Mpya, hakiwezi kueleweka kwa Watanzania.

Nchemba alisema ni vyema kujua idadi ya wanaoshiriki awamu ya pili ya Bunge hilo ili kutoa uthibitisho  kimahesabu kama uamuzi wa kuendelea kwa Bunge unaweza kuwa na maana.

Jana Mwigulu Nchemba alizidi kusisitiza kauli aliyoitoa akisema ni msimamo wake binafsi kama mtoto wa maskini. Alisema anatambua jinsi walipa kodi watakavyoumia, rasimu hiyo itakapokwama kupita kutokana na kukosekana kwa theluthi mbili ya pande zote.

Hata hivyo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye  juzi alijibu akisema kauli ya Nchemba ni mtazamo wake binafsi na hakuongea kama kiongozi wa chama hicho.

Lakini jana wabunge mbalimbali wa CCM walijitokeza hadharani wakisema wanaunga mkono kauli ya Nchemba ili hesabu ijulikane badala ya kuendelea kutafuna fedha za wananchi bila tija.


Madawa ya Kulevya Yamtesa Tena Agness Masogange...Abadili Uraia

$
0
0
Stori: Imelda Mtema
MAJANGA! Baada ya kuchomoka kwenye ule msala wa awali wa madawa ya kulevya, video queen matata Bongo, Agness Gerald ‘Masogange’ amejikuta akiteseka kwa ishu hiyo kwa mara nyingine.

Kwa mujibu wa taarifa zilizolifikia Risasi Jumamosi, Masogange alipatwa na msala huo mara baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar hivi karibuni akitokea nchini Afrika Kusini ‘Sauz’ ambapo alidakwa na polisi wa kitengo cha kudhibiti madawa ya kulevya nchini kilicho chini ya Godfrey Nzowa.

Akisimulia ishu hiyo, Masogange ambaye umaarufu wake mkubwa ulizaliwa katika video ya Wimbo wa Masogange wa Abednego Damian ‘Belle 9’, alisema alikamatwa na watu wa uhamiaji nchini baada ya kuhisiwa kuwa hati yake ya kusafiria ina matatizo.

“Walinikamata baada ya kuiona hati ilikuwa na ule msala wa awali lakini walinihoji na nikawapa majibu ambayo yaliwaridhisha, wakaniachia.


“Hii ishu inanitesa sana lakini nashukuru Mungu kwa kuwa nakamilisha taratibu za kuwa raia wa Afrika Kusini, nitaishi kule,” alisema Masogange alipobanwa na Risasi Jumamosi.

Juzi wakati gazeti hili likienda mitamboni, Masogange alikuwa kwenye Ubalozi wa Sauz nchini katika harakati za mwisho kukamilisha taratibu za kuwa na uraia wa Afrika Kusini ambako amesema ndiko atakapokuwa akiishi.

Julai 9, mwaka jana, Masogange alikamatwa na madawa ambayo yalihisiwa kuwa ni ya kulevya nchini Afrika Kusini, akashikiliwa na polisi kwa miezi kadhaa.

Septemba, mwaka jana Mahakama ya Kempton ya jijini Johannesburg, baada uchunguzi kukamilika na kubainika kuwa hayakuwa madawa ya kulevya bali ni kemikali zinazotengenezea madawa ya kulevya, Masogange alitakiwa kulipa faini ya R30,000 (Sh4.8 milioni), akawa huru.
Viewing all 104712 articles
Browse latest View live




Latest Images