Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104756 articles
Browse latest View live

Matapeli Wamuweka Nyalandu Katika Wakati Mgumu

$
0
0
Matapeli Wamuweka Nyalandu Katika Wakati Mgumu
Aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Mhe Lazaro Nyalandu amejikuta akipata wakati mgumu kuuaminisha umma kuwa jina linalotumika mitandaoni kutangaza safari ya kwenda Israel sio lake, hii ni baada ya Watanzania wengi kuomba nafasi baada ya tangazo la kwenda kuzuru nchini huko kutangazwa mtandaoni

Mhe Nyalandu amesema kuwa akaunti hiyo ya Facebook ambayo inatumia jina lake, sio yake hivyo watu wote waliojaza fomu na kumpatia namba mtu huyo wasiendelee kufanya hivyo kwani ni tapeli wa mitandaoni.

“Fake News alert❗Habari hii ya kupeleka watu Israel sio ya kweli na Account iliyotumika kuandika sio yangu. Tafadhali ipuuzeni. So many sad people out there wanaokaa kutungia wenzao UONGO. Sad!,”ameandika kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii kuutarifu umma na kuweka tangazo hilo.
Tayari zaidi ya watu 400 wameshaomba kwenda kuzuru nchini Israeli baada ya tangazo hilo kuwekwa na mtu huyo anayejiita Lazaro Nyalandu.

Simba Yaanza Mazoezi Kujiandaa na Vita Dhidi ya Mbao FC

$
0
0
Simba Yaanza Mazoezi Kujiandaa na Vita Dhidi ya Mbao FC
Vinara wa ligi kuu soka Tanzania Bara klabu ya soka ya Simba inaanza mazoezi ya kujiandaa na mchezo wake wa kiporo raundi ya 19 ligi kuu dhidi ya Mbao FC ya Mwanza.


Baada ya kurejea nchini jana ikitokea Djibouti kwenye mchezo wake wa marudiano dhidi ya Gendarmerie, benchi la ufundi la klabu hiyo lilitoa mapumziko ya siku moja kwa wachezaji.

Kwa mujibu wa taarifa ya klabu hiyo, mazoezi yanatarajiwa kuanza leo saa 10:00 jioni katika uwanja wa Boko Veterani jijini Dar es Salaam.

Simba imefanikiwa kutinga hatua ya kwanza ya michuano ya kombe la shirikisho baada ya kuitoa Gendarmerie kwa jumla ya mabao 5-0 na inatarajiwa kukutana na Al Masry ya Misri.

Simba inaongoza msimamo wa ligi kuu soka Tanzania Bara ikiwa na alama 42, ikiwazidi wapinzani wao Yanga wenye alama 37 katika nafasi ya pili huku Azam FC ikiwa katika nafasi ya tatu na alama 35.

Familia ya Akwelina Yamuangukia Rais Magufuli "Waliofanya Unyama Huu Wapewe Adhabu Staiki"

$
0
0
Familia ya Akwelina Yamuangukia Rais Magufuli "Waliofanya Unyama Huu Wapewe Adhabu Staiki"
Familia ya binti Akwelina Akwelini aliyepigwa risasi Februari 16, 2018 na mwili wake kuagwa jana Februari 22, 2018 kwenye viwanja vya Chuo cha (NIT) Mabibo Dar es salaam wamemuomba Rais wale wataobanika kufanya mauaji hayo wapewe adhabu inayostahiki.


Familia ya binti huyo ilisema hayo kupitia kwa msemaji wa familia ambaye alikuwa akitoa historia ya marehemu Akwelina na kumuomba Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa. Joyce Ndalichako awafikishie maombi yako kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

"Familia inaendelea kukuomba utuombee kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli ili wale wote waliohusika kufanya kitendo hiki cha kinyama wapewe adhabu inayostahili ili iwe fundisho kwa wote wenye tabia ya kufanya vitendo hivyo vinavyoigharimu taifa bila kuogopa vyeo vyao wala umaarufu wao au kazi zao tukijua kwamba Tanzania ni nchi yenye amani" alisema msemaji huyo wa familia

Mwili wa binti Akwelina Akwelini unatarajiwa kuzikwa leo Februari 23, 2018 huko nyumbani kwao Rombo Kilimanjaro

Baada ya Kuachiwa kwa Dhamana Zitto Kabwe Atema Cheche "Tusirudishwe Nyuma na Vitisho"

$
0
0
Baada ya Kuachiwa kwa Dhamana Zitto Kabwe Atema Cheche "Tusirudishwe Nyuma na Vitisho"
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Mhe. Zitto Kabwe amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya kutoka Mahabusu alikokuwa anashikiliwa toka jana Alhamisi usiku alipokamatwa na Jeshi la Polisi mkoani Morogoro.

Zitto amesema kukamatwa kwake hakumfanyi asitishe ziara ya Chama cha ACT Wazalendo iliyopagwa kutembelea kata zote zilizo chini ya chama hicho kama walivyotangaza awali.

“Tusirudishwe nyuma na vitisho, usumbufu na sheria kandamizi. Harakati za kulinda Demokrasia yetu na Uhuru wa kukusanyika, kujieleza na kupashana Habari lazima ziendelee. Ni wajibu wetu kulinda Demokrasia ya Vyama vingi na kuiimarisha iwe madhubuti kwa ajili ya Maendeleo ya Watu wetu. Baada ya kulala bure jana polisi Morogoro, tunaendelea na kazi yetu ya kutembelea kata zote ambazo Wananchi walitupa dhamana kwa kuchagua madiwani wa Act Wazalendo,“ameeleza Zitto Kabwe.

Kwa upande mwingine Zitto amelaani mauaji ya Diwani wa CHADEMA huko Ifakara, Morogoro aliyekatwa mapanga na watu wasiojulikana.

“Nawapa pole Wananchi wa Ifakara kwa msiba wa Diwani wao aliyekatwa mapanga mpaka kufa jana Usiku. Nilipata Taarifa hizo nikiwa selo ya Polisi. Mauaji ya namna hii kwa Viongozi wa kisiasa yanatia doa nchi yetu na ni mwendelezo ya uvunjifu mkubwa wa haki za raia.“-amesema Zitto.

Hali ya Lissu Yazidi Kuhimarika "Kwa Sasa Naweza Kusimama Kutembea Bado"

$
0
0
Hali ya Lissu Yazidi Kuhimarika "Kwa Sasa Naweza Kusimama Kutembea Bado"
Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amezungumzia hali ya afya yake akisema kwa sasa anachoweza kukifanya ni kusimama peke yake na ili atembee anahitaji msaada wa magongo.

Lissu ambaye pia ni rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) anayeendelea na matibabu ya viungo katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Leuven nchini Ubelgiji alisema hayo jana alipozungumza na Mwananchi.

“Mie naendelea vizuri na kwa sasa ninaweza kusimama kidogo tu. Sijaanza kutembea bila magongo,” alisema.

Kuhusu hali ya mguu wa kulia ambao uliathirika zaidi na risasi alizoshambuliwa Septemba 7, 2017 mjini Dodoma, alisema: “Bado sio salama sana na unahitaji kufanyiwa kazi ya kitabibu zaidi.”

Awali, Lissu kupitia ukurasa wake wa mtandao wa jamii wa Instagram aliandika ujumbe wa kumshukuru Mbunge wa Tandahimba (CUF), Ahmad Katani aliyemtembelea Ubelgiji na picha ya wawili hao ilianza kusambaa juzi usiku mitandaoni ikiwaonyeasha wakiwa na nyuso za furaha.

Lissu alimshukuru mbunge huyo kwa kumtembelea huku akieleza kuwa ni miongoni mwa wabunge waliompeleka Nairobi nchini Kenya akitokea Hospitali ya Rufaa ya Dodoma alipopelekwa baada ya kushambuliwa.

“Katani alikuwa kwenye msafara wa wabunge walionipeleka Nairobi, Kenya mara baada ya jaribio la mauaji la Septemba 7 na alikaa Nairobi kwa siku nne. Nimefarijika sana na ugeni huu wa ndugu yangu na kaka yangu Katani,” alisema mbunge huyo.   

   

Akwilina Kuzikwa Leo Viongozi Wamiminika Kijijini Kwao Marangu

$
0
0
Akwilina Kuzikwa Leo Viongozi Wamiminika Kijijini Kwao Marangu

Viongozi mbalimbali wa Serikali wameanza kuwasili nyumbani kwa wazazi wa aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini kijiji cha Marangu, Kata ya Marangu Kitowo, Olele mkoani Kilimanjaro.

Mwili wa mwanafunzi huyo aliyeagwa jana katika viwanja vya NIT, Mabibo jijini Dar es Salaam umefika kijijini hapa leo Februari 23, 2018 saa 3:30 asubuhi.

Viongozi waliofika mpaka sasa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Leonard Akwilapo, Mkuu wa Chuo Cha NIT, Profesa Zacharia Mganilwa pamoja na viongozi wengine wa wilaya.

Ibada ya misa ya kuombea mwili wa marehemu inatarajiwa kuanza saa 6:00 mchana katika kanisa la Mtakatifu Theresia Parokia ya Olele.

Mwili huo utaondoka nyumbani saa 5 asubuhi kuelekea katika kanisa hilo.

Tido Muhando Apandishwa Tena Kizimbani kwa Tuhuma za Uhujumu Uchumi

$
0
0
Tido Muhando Apandishwa Tena Kizimbani kwa Tuhuma za Uhujumu Uchumi
Stori ya Kimahakama nayokusogezea ni kuhusu kesi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Tido Mhando ambapo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha kesi ya uhujumu uchumi ya kusababisha hasara ya Shilingi Milioni 887 inayomkabili hadi February 28,2018 kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali (Ph).

Mwendesha Mashtaka wa (TAKUKURU), Leornad Swai amemueleza Hakimu Mkazi Mfawidhi, Victoria Nongwa kuwa kesi hiyo imeitishwa kwa ajili ya kumsomea Tido maelezo ya awali.

Hata hivyo, Wakili wa Tido, Ramadhan Maleta ameieleza Mahakama kuwa amechelewa kumuandaa mteja wake kutokana na kuchelewa kupewa maelezo ya (Ph), hivyo anaomba ahirisho.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Nongwa ameahirisha kesi hiyo hadi February 28,2018 kwa ajili ya Tido kusomewa (Ph).

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka Tido anakabiliwa na makosa matano ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka.

Inadaiwa alilitenda kosa hilo June 16,2008 akiwa Dubai kama mtumishi wa TBC alitumia madaraka yake vibaya kwa kusaini mikataba ya uendeshaji wa vipindi kati ya TBC na Channel 2 Group Corporation (BVI) bila kutangaza zabuni na kuisababishia channel hiyo kunufaika.

Inadaiwa kati ya June 16 na November 16,2008 akiwa Falme za Kiarabu, kama muajiriwa wa TBC kwa cheo cha Mkurugenzi Mkuu kwa mamlaka yake alilisababishia shirika la TBC hasara ya Sh.Mil 887.

Ulinzi Mkali Wawekwa Kijiji Atakapozikwa Akwelina

$
0
0
Ulinzi Mkali Wawekwa Kijiji Atakapozikwa Akwelina
Vyombo vya ulinzi na usalama vimeimarisha usalama katika eneo atakalozikwa mwanafunzi wa chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline katika kijiji cha Olele wilayani Rombo.

Uchunguzi uliofanywa na MCL Digital saa 2:00 hadi saa 4:30 asubuhi leo Ijumaa Februari 23, 2018 umebaini uwapo wa askari wengi wakiwamo wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) na askari kanzu.

Mbali na askari kanzu, wameonekana maofisa usalama wa Taifa na polisi waliovalia kiraia, wakiwa wameegesha magari kimkakati, mita kati ya 100 hadi 150 kutoka nyumbani kwa wazazi wa marehemu.

Ofisa mnadhimu wa polisi namba moja wa Mkoa Kilimanjaro, Koka Moita, ambaye amezoeleka kuwa katika sare, leo ameonekana akitembea kwa miguu mitaani akiwa amevalia kiraia.



Moita alipoulizwa kuhusu usalama, alikiri kuna ulinzi wa kutosha japo amesema anayeweza kuzungumzia hilo ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamis Issah.



Mbali na polisi, lakini wapo mgambo ambao wameshika doria maeneo ya maegesho ya magari ya wageni mbalimbali na eneo la kanisa itakapofanyika ibada.

Askari wa usalama barabarani, nao wameonekana barabara kuu ya Olele-Useri, wakisimamia usalama wa watembea kwa miguu na watumiaji wengine wa barabara, jirani na shughuli za mazishi zitakapofanyika.

Shilole Amuwekea Ngumu Uchebe "Sikubali Mume Wangu Aoe Mke wa Pili Hata Kama Dini Inaruhusu"

$
0
0
Shilole Amuwekea Ngumu Uchebe "Sikubali Mume Wangu Aoe Mke wa Pili Hata Kama Dini Inaruhusu"
Baaada ya Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainab Abdallah, kushangaza watu wengi kwa kutoa pongezi kwa Mume wake baada ya kuoa mke wa Pili, Sasa Mwanamuziki Shilole yeye amesema kwamba katu hawezi kukubali Mumewe Uchebe aoe mke wa Pili hata kama Dini yake inaruhusu.

….>>>“Mimi mume wangu hawezi kuowa mke wa pili, anaoa mke wa pili how..? hata kama dini inaruhusu, mimi nina mapungufu gani mpaka uoe mke wa pili na mimi sina mapungufu yeyote mpaka uoe mke wa pili na mume wangu kamwe hawezi kuoa mke wa pili na sito kubali hatujawai kuzungumza na uchebe hana plan hizo” – Shilole

Mchungaji Akiponza Kituo cha Redio Chafungiwa na Kutozwa Faini ya Milioni 2

$
0
0
Mchungaji Akiponza Kituo cha Redio Chafungiwa na Kutozwa Faini ya Milioni 2
Serikali ya Rwanda kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Mawasiliano nchini humo (RURA), imekifungia kituo cha redio ya kidini cha  Amazing Grace 105.1 FM kurusha matangazo kwa kipindi cha mwezi mmoja pamoja na kulipa faini ya faranga milioni 2 sawa na Tsh milioni 6, baada ya redio hiyo kurusha matangazo yaliyowadhihaki wanawake kwa kuwataja kuwa ndiyo chanzo cha matatizo duniani.

Mamlaka hiyo imeeleza kuwa mnamo Tarehe 29 Januari 2018 Mchungaji wa Kanisa la Kisabato, Niyibikora Nicholas akitangaza injili kupitia kituo hicho cha redio alisikika hewani akisema wanawake ni moto wa kuotea mbali kwani ndo chanzo cha maovu na migogoro isiyoisha duniani.

Mchungaji huyo akiwa LIVE hewani aliendelea kusema kuwa hata Mungu hawapendi wanawake, kwani mwanamke hajawahi kuwa mtu mwema tangu enzi za bustani ya edeni ambapo alikula tunda alilokuwa ameambiwa asile na kumshawishi na mumewe kufanya dhambi.

Mamlaka hiyo ilichambua mahubiri yake yote ambapo imeeleza kuwa maudhui yote yalitoa mifano lukuki ya kwenye biblia inayowaelezea wanawake kuwa ni watu wabaya huku mchungaji huyo akiwataka wanaume wasiwaamini wanawake kwani wanawake ni watu wabaya.

Mhubiri huyo alizua mjadala mzito kwenye mitandao ya kijamii nchini Rwanda na kuwakasirisha wanawake ambapo Mwavuli wa Utetezi wa Haki za Wanawake Rwanda (Profemmes Twese Hamwe) na Jukwaa la Waandishi wa Habari wa Kike Rwanda (ARFEM) walipaza sauti zao kutaka achukuliwe hatua kwa tuhuma za uchochezi wenye misingi ya kijinsia na kulenga kusababisha mtafaruku kwenye jamii.

Tayari Ofisi ya Mwendeshaji Mkuu wa Mashtaka imeliagiza jeshi la polisi kitengo cha upelelezi wa makosa ya jinai kuanza upelelezi juu ya madai yanayomkabili Mchungaji huyo.

Chanzo:The New Times

Papa Francis Ataka Kanisa Lifunge Kuombea DRC, Sudan Kusini

$
0
0
Papa Francis Ataka Kanisa Lifunge Kuombea DRC, Sudan Kusini
Papa Francis ametangaza Ijumaa ya Februari 23 kuwa siku ya kufunga na sala kwa ajili ya kuziombea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Congo (DRC) na Sudan Kusini zinazokumbwa na migogoro ya kisiasa.

Nchi zote mbili zinakabiliwa na usalama mdogo na mgogoro wa binadamu katika miaka michache iliyopita. Baba Mtakatifu ameomba kuingilia kati kiroho akiwaomba waumini waaminifu kufunga na kuomba kwa ajili ya amani ya nchi hizo Februari 23.

Pia, mkakati huo una lengo la kutafuta amani ulimwenguni. Papa amewaalika waumini wengine waaminifu wasio Wakatoliki kushiriki katika kutafuta amani ya nchi mbili hizo na duniani kote.

Wito wake ulijibiwa na Mkuu wa Kanisa la Anglikana la Kimataifa, Justin Welby, ambaye aliwaagiza watu kufuata wito wa Papa. Pia, Welby alielezea uzoefu wa kile alichokiona katika safari za awali DRC na Sudan Kusini.

"Katika ziara yangu kwenye nchi hizo mbili miaka ya hivi karibuni, ilikuwa haiwezekani kuelezea kiwango kikubwa cha uharibifu. Migogoro hii inasababisha kupotea uhai wa watu wengi. Idadi kubwa ya watu imelazimika kukimbia nyumba zao, ambako kunasababisha familia na jamii kuvunjika.

"Kuna idadi mpya ya zaidi ya watu milioni moja waliotawanyika ndani ya nchi. Njaa inasababisha mateso makubwa na hatari. Katika Sudan Kusini, watu milioni sita wanakabiliwa na njaa. Vurugu za unyanyasaji na udhalilishaji wa kijinsia hufanywa kwa kiwango kibaya sana katika nchi zote mbili.

"Wakati wa ziara yangu ya mwisho, nilimsikiliza kiongozi wa kisiasa akiniambia kuhusu mateso na mauaji ya watu wake. Nilitembelea kambi ya wakimbizi nchini Uganda iliyojaa watoto wa Sudan Kusini ambao familia zao zilikimbia nyumba zao ili kuepuka mauti," ilisema taarifa rasmi.

Alitoa pia masuala ambayo waamini wanaweza kuomba wakati wa kufunga:

• Viongozi wa Sudan Kusini na DRC wageuze mioyo yao kutoka vita hadi amani - na kutafuta ufumbuzi wa amani kwa matatizo ya kisiasa.

• Kwa wakimbizi wote kutoka nchi hizi.

• Kwa msamaha, uponyaji na mahusiano mapya.

• Kwa makanisa ya mitaa kufanya mengi ya kuwaangalia watu ambao wanateseka, na kuleta amani.

Hali nchini DRC kwa kiasi kikubwa inakwamishwa na hatua ya kuendelea kubaki madarakani kwa Rais Joseph Kabila ambaye muhula wake ulimalizika mwishoni mwa mwaka 2016. Kushindwa kuandaa uchaguzi kulimaanisha yeye kuendelea kubaki ofisini.

Maandamano ya dhidi ya Kabila yaliyoandaliwa na vikundi vya kiraia likiwemo kanisa yamevunjwa kikatili. Uchaguzi, hata hivyo, umepangwa kufanyika baadaye mwaka huu. Kabila, walio karibu naye wanasema, hatagombea na ameahidi kuteua mrithi mwezi Julai mwaka huu.



Rais Magufuli, Kenyatta Watoa Maagizo kwa Mawaziri "Mnatakiwa Myatatue Nyinyi, Yasifike Kwetu"

$
0
0
Rais Magufuli, Kenyatta Watoa Maagizo kwa Mawaziri "Mnatakiwa Myatatue Nyinyi, Yasifike Kwetu"
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli leo Ijumaa Februari 23, 2018 amekutana na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta na kufanya naye mazungumzo ambapo kwa pamoja wametoa maagizo kwa Mawaziri wao kutatua changamoto ndogo ndogo zinazojitokeza kwenye biashara kati ya Tanzania na Kenya.

Rais Magufuli ambaye wamekutana na Uhuru Kenyatta na kufanya mazungumzo hayo katika Hoteli ya Munyonyo jijini Kampala, amesema wao marais hawana tatizo kwani vitu vidogo vidogo kama biashara ya viatu, nguo, ngano, gesi mawaziri wa nchi mbili wakae wayamalize.

“Kuna mambo madogo madogo yanakuwa yanajitokeza katika biashara kati ya Kenya na Tanzania, tunataka mawaziri wote wa upande wa Kenya na Tanzania mkae muyasolve myamalize, sisi huku juu hatuna tatizo,“amesema Rais Magufuli.



Rais Magufuli yupo nchini Uganda katika Kikao cha 19 cha Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kilichoanza jana Alhamisi jijini Kampala.

Fujo za Mashabiki Zasababisha Kifo cha Askari

$
0
0
Fujo za Mashabiki Zasababisha Kifo cha Askari
Askari Polisi mmoja nchini Hispania amefariki kwa mshituko wa Moyo baada kuanguka wakati akijaribu kutuliza ghasia za mashabiki kwenye mchezo wa EUROPA kati ya Athletic Bilbao na Spartak Moscow jana usiku.


Askari huyo wa kiume aliyetambulika kwa jina la Inocencio Arias Garcia, alikuwa na umri wa miaka 50. Baada ya Garcia kuanguka wakati wa vurugu hizo nje ya uwanja wa San Mames,  kabla ya mchezo  alikimbizwa Hospitali lakini tayari alikuwa ameshapoteza maisha.

Shirikisho la soka nchini Hispania RSFF pamoja na Rais wa La Liga Javier Tebas, wametoa pole kwa familia ya Garcia pamoja na kukemea vitendo vya vurugu michezoni huku wakitaka vyombo vya usalama kuwashughulikia mashabiki waliohusika katika tukio hilo.



Katika vurugu hizo zilizohusisha makundi ya mashabiki wa timu za FC Spartak Moscow na Athletic Bilbao imeripotiwa kuwa mashabiki watatu wa Kirusi na afisa mmoja wa polisi walipelekwa hospitali baada ya kujeruhiwa.

Katika mchezo huo wa marudiano ulimalizika kwa Bilbao iliyokuwa nyumbani kwenye uwanja wa San Mames kukubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Spartak lakini imefanikiwa kusonga mbele kwa jumla ya mabao 4-3 baada ya kushinda 3-1 kwenye mchezo wa kwanza.

Mwana FA: Hivi Hizi Nywele Mmepatwa na Nini Safari Hii nyi Kina Defao?

$
0
0
Mwana FA: Hivi Hizi Nywele Mmepatwa na Nini Safari Hii nyi Kina Defao?
Wakati style ya kubadili rangi ya nywele zao na kuweka rangi tofauti tofauti ikiendelea ku-trend, Mwana FA hajakaa kimya katika hilo.

Katika moja ya picha za Ommy Dimpoz ambazo anaonekana na akiwa amepaka rangi kichwani ambazo ameposti katika Instagram, Mwana FA ameandika; Hivi hizi nywele mmepatwa na nini safari hii nyi watoto kina Defao?smh.

Baada ya kuona comment hiyo Ommy Dimpoz alimjibu Mwana FA; mkubwa ukitaka kutisha piga pink 😂😂😂.

Siku za hivi karibuni wasanii wengi wamekuwa wakipaka rangi tofauti tofauti katika nywele zao, miongoni mwao ni Ben Pol, Alikiba, Ommy Dimpoz, Lava Lava, Vanessa Mdee. Hapo awali kulikuwa na Harmonize, Queen Darleen na Amber Lulu ambao wanaendelea hadi sasa.

Waziri Kigwangalla Ataka Ulinzi Uimarishwe

$
0
0
Waziri Kigwangalla Ataka Ulinzi Uimarishwe
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameuagiza uongozi wa wakala TFS kujenga kituo cha ulinzi wa kudumu katika eneo la chanzo cha maji ya mto Zigi kilichopo ndani ya Hifadhi ya Mazingira Asilia Amani ili kulinda chanzo hicho.


Dk. Kigwangalla ametoa agizo hilo wakati akizungumza na waandishi wa habari  baada ya kutembelea eneo la chanzo hicho na kukuta uharibifu mkubwa unaofanywa na baadhi ya wananchi wanaodaiwa kuchimba madini ya dhahabu katika eneo hilo la hifadhi ambapo ni kinyume cha sheria.

"Nimeagiza uongozi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania  (TFS) wajenge kituo cha ulinzi cha kudumu katika eneo hili, na waweke walinzi wetu wa kudumu hapa badala ya kutegemea kufanya patrol (doria) na kuondoka, kwa sababu eneo hili wananchi wanaamini lina madini ya dhahabu kwa hiyo kila siku wataendelea kuja kujaribu kuvuna dhahabu kutoka hapa", amesema Dkt. Kigwangalla.

Pamoja na hayo, Dkt. Kigwangalla ameendelea kwa kusema "kwa sababu sisi kazi yetu ni kuhifadhi maliasili ambayo tumepata kama urithi wa nchi yetu, niwahakikishie kwamba tutaimarisha ulinzi kwa kuanzisha kituo cha ulinzi hapa ili askari wawe wanabadilishana na kudhibiti kabisa uharibu ambao umekuwa ukifanyika, kwa sababu maji yanayotoka katika chanzo hiki yanakwenda kunywesha Muheza yenyewe na wilaya wa Tanga, tukiharibu hapa yatakosekana maji safi na salama".

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala huyo, Prof. Dos Santos Silayo amesema pamoja na eneo hilo kwa sasa kuwa linalindwa na askari wa Suma JKT watahakikisha ulinzi unakuwepo muda wote kwa kutekeleza agizo hilo la Waziri la kujenga kituo cha ulinzi cha kudumu ili askari wawepo katika eneo hilo muda wote.


Msajili wa Vyama vya Siasa Anasukumwa Wanataka Kuifuta Chadema- Mnyika

$
0
0
Msajili wa Vyama vya Siasa Anasukumwa Wanataka Kuifuta Chadema- Mnyika
Naibu Katibu Kuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) bara Mhe. John Mnyika amefunguka na kusema kuwa kuna kila dalili serikali kupitia kwa msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Francis Mtungi.


Mnyika akiongea na waandishi wa habari leo Februari 23, 2018 amesema kuwa kuna njama ambazo zinapangwa kuhakikisha kuwa chama hicho kinafutiwa usajili wake jambo ambalo Mnyika anasema jambo hilo hawataliweza.

"Msajili wa vyama vya siasa anasukumwa , dhamira yao ni kutafuta mwanya wa kukifuta Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jambo hili hawaliwezi na kama wanafikiri wanauwezo wa kuifuta CHADEMA wajaribu kufanya hivyo. Wafahamu kwamba wakizuia mlango wa demokrasia, watu watafanya siasa kwa njia nyingine, sisi tutakabiliana na msajili kwa njia yoyote kuhakikisha jambo hili halifanikiwi" alisema Mnyika

Aidha Mnyika amesema kuwa Msajili wa vyama vya siasa nchini amekitaka chama cha Demokrasia na Maendeleo kujieleza kutokana na matukio ya Februari 16, 2018 hivyo amedai tayari wameshamjibu msajili huyo wa vyama vya siasa.

Mbali na hilo Mnyika amewataka wanachama wa CHADEMA pamoja na viongozi wake wakiwepo madiwani pamoja na wabunge wajilinde sana katika kipindi hiki kwani amedai kwa sasa wanashambuliwa kila kona kwa njia mbalimbali.


Ibada ya Kuuaga Mwili wa Akwilina Kanisaini Inaendelea

$
0
0
Ibada ya Kuuaga Mwili wa Akwilina Kanisaini Inaendelea
Mwili wa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini umeshapelekwa  katika Kanisa la Mtakatifu Theresia Parokia ya Olele Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro ambako inafanyika ibada ya kuaga mwili wa marehemu.

Baada ya ibada hiyo ndugu, jamaa, viongozi na watu wa kada mbalimbali watatoa heshima za mwisho na kisha mwili kupelekwa nyumbani kwa ajili ya mazishi yatakayoanza saa saba mchana.

Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH issa simba Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Kutumia Vitabu vya QUR-AN

$
0
0

Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH issa simba said Mtabibu wa Nyota za Binadamu   Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..

JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Maalim Hussein Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO . Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.

Issa simba said Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
Anatibu kwa Kutumia Vitabu vya QUR-AN .Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA.

Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI.  Humaliza Kesi zilishindika ndani ya siku 14 tu..na mengi zaidi

+255 622588038au 0679119679 au +255 764318107

Mdogo wa Marehemu Akwilina Apata Neema Ndalichako Ahaidi Kumsomesha

$
0
0
Mdogo wa Marehemu Akwilina Apata Neema Ndalichako Ahaidi Kumsomesha
Waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako ameahidi kumsomesha mdogo wake Akwilina Akwilini, Angela Akwilini ambaye kwa sasa anasoma kidato cha tatu.

Akizungumza leo Februari 23, 2018 baada ya mazishi ya Akwilina aliyeuawa kwa kupigwa risasi Februari 16, 2018 eneo la Mkwajuni jijini Dar es Salaam, Profesa Ndalichako amesema atamsomesha Angela hadi Chuo Kikuu.

Nguvu ya Nafsi Yamzidi Padri Atangaza Kufunga Ndoa

$
0
0
Nguvu ya Nafsi  Yamzidi Padri Atangaza Kufunga Ndoa
Katika historia ya Kanisa Katoliki duniani ni mwiko kwa Padri kuoa, lakini hii iko tofauti kwa  Fr. Patrick Henry Edet, ambaye yeye ametangaza kufunga ndoa baada ya mwili wake kuzidiwa nguvu ya nafsi.

Padri huyo ambaye mwaka jana mwezi Novemba alitengwa kwa muda na kanisa la Roma katika jimbo kuu Katoliki la UYO nchini Nigeria, amesema kuwa kwa sasa haoni umuhimu wa kuendelea kuiumiza nafsi yake kwa kile anachoamini kuwa kuoa sio dhambi bali ni utamaduni tu wa kikatoliki ambao hauna maana kwa sasa.

Fr. Henry ambaye amehudumu kwa miaka 11, amedai kuwa huu ni muda mwafaka kwa Wakatoliki kufikiria suala hilo kwani kuna matatizo mengi yanatokea kwenye taasisi hiyo, ambayo yanatokana na sheria ya kutokuoa au kuolewa kwa watumishi.

“Kuanzia leo, naachana na masharti magumu ya Kanisa la Kikatoliki, mwili wangu umeshindwa na nguvu ya nafsi. Mtanisamehe wale wote waumini ambao nimewaudhi kwa maamuzi yangu, mimi ataka niishi kwa ajili ya Mungu hivyo ni lazima nitimize andiko lake la kuzaliana duniani. Ninataka kuwa mtu huru wa mwili na nafsi na kwa andiko hilo natangaza rasmi kuwa mwezi Machi 17 mwaka huu nafunga ndoa hivyo basi nitakuwa muumini wa kawaida,“amenukuliwa Fr. Henry na gazeti la NewsDesk la Nigeria .

Kanisa Katoliki nchini Nigeria limekuwa likikubwa na kashfa mbalimbali za kinidhamu baina ya viongozi wa dhehebu hilo nchini humo, mwaka jana Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis aliwataka mapadri wote nchini humo kumuunga mkono Askofu Mkuu wa Jimbo la Ahiara aliyemsimika baada ya tamko la mapadri nchini humo kukataa usimikwaji wake.

Mwaka 2015 wakati Kiongozi huyo mkubwa wa Kanisa Katoliki duniani alipozuru nchini Kenya, Kanisa Katoliki Nigeria walimtaka aiangazie nchi hiyo ikiwemo kufikiria namna ya kuboresha baadhi ya masharti magumu ya viongozi wa dhahebu hilo ikiwemo ya kuoa.
Viewing all 104756 articles
Browse latest View live




Latest Images