Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Yametimia! Safari ya Akwilina Yafika Mwisho Azikwa Kijijini kwa Wazazi Wake

$
0
0
Yametimia! Safari ya Akwilina Yafika Mwisho Azikwa Kijijini kwa Wazazi Wake
Mwili wa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini umezikwa nyumbani kwa wazazi wake kijiji cha Olele wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro.

Akwilina aliyeuawa Februari 16, 2018 amezikwa leo Februari 23, 2018 saa 8:45 mchana na mamia ya waombolezaji baada ya kumalizika kwa ibada ya mazishi iliyofanyika kanisa la Mtakatifu Theresia Parokia ya Olele.

Baada ya uwekaji maua katika kaburi, watu mbalimbali wakiwemo wanafamilia watatoa salamu za rambirambi.

Polisi Yafunguka Sababu za Kumkamata Zitto Kabwe

$
0
0
Polisi Yafunguka Sababu za Kumkamata Zitto Kabwe
Saa chache baada ya Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT- Wazalendo), Zitto Kabwe kuachiwa kwa dhamana, polisi imesema ilimkamata na kumuweka mahabusu kwa kuwa walifanya mkutano wa hadhara bila kuwa na kibali.

Wakati polisi ikieleza hayo, baada ya kuachiwa Zitto ameeleza aliyoyakuta mahabusu jambo lililomlazimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei kutoa ufafanuzi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Februari 23, 2018 Kamanda Matei amesema Zitto alikamatwa jana, Februari 22 saa 11 jioni katika Kijiji cha Mhale, Wilaya ya Mvomero akiwa anafanya mkutano wa hadhara.

Kamanda Matei amesema Zitto anashtakiwa kwa kifungu 74 na 75 vya kanuni ya adhabu kwa kufanya mkutano bila kibali.

Kamanda huyo amesema awali Zitto alikuwa akifanya mkutano wa ndani, lakini baadaye wananchi walijaa nje na ndipo alipotoka kuwahutubia.

Zitto ameachiwa kwa dhamana na kutakiwa kuripoti kituo kikuu cha polisi cha mkoani Morogoro, Machi 12, 2018.

Hata hivyo, Zitto akizungumza na waandishi wa habari nje ya kituo cha polisi amesema yupo katika ziara ya kutembelea kata zinazoongozwa na madiwani wa chama hicho na kufanya vikao vya ndani.

Amesema ataendelea na ziara yake hiyo kama kawaida kwa kuwa kukutana ni haki ya kikatiba na hakuna mwenye uwezo wa kuizuia.

"Tunataka kuona wananchi wanapata haki zao za msingi bila kubughudhiwa na kukutana na kuzungumza ni haki ya msingi ya raia na hakuna mwenye uwezo wa kuinyang'anya," amesema Zitto.

"Sisi viongozi lazima tushuke chini kwa wananchi wetu ili kuona changamoto zinazowakabili na kwa pamoja tuzitafutie ufumbuzi.”

Amesema lengo la ziara yao ni kuzungumza na madiwani kuhusu utekelezaji wa ahadi zao kwa wananchi na kuangalia wamefanikiwa kuzitekeleza kwa kiasi gani.

Akizungumza alichokikuta mahabusu, amesema kuna watuhumiwa waliowekwa mahabusu muda mrefu bila kupelekwa mahakamani.

" Huko mahabusu nimekuta watuhumiwa zaidi ya 20  ambao wengi wao wamekaa mahabusu bila kufunguliwa mashataka yoyote. Inawezekana  Mungu ameamua niingie huko ili nijionee mateso wanayopata,” amesema.

Hata hivyo,  Kamanda Matei amekanusha madai ya uwepo wa watuhumiwa wa muda mrefu katika kituo hicho akidai wote hufikishwa mahakamani kwa wakati.

TRA Yakamata Kilo 750 za Sukali ya Magendo

$
0
0
TRA Yakamata Kilo 750 za Sukali ya Magendo
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga, imekamata mifuko 15 ya sukari ya magendo inayokadiriwa kuwa na thamani ya Sh1 milioni.

Sukari hiyo imekamatwa leo Ijumaa Februari 23, 2018 na kuthibitishwa na kaimu mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Godwin Gondwe.

Gondwe amesema kukamatwa kwa sukari hiyo mifuko 15 sawa na kilo 750 ni mwendelezo wa operesheni walioanzisha kwa ajili ya kufuatilia na kuwadhibiti wafanyabiashara wanaokwepa  kodi na kuisababishia Serikali hasara.

Amewataka wafanyabiashara kufuate taratibu katika kufanyabiashara zao kwa kulipa kodi, waache tabia ya kufanya magendo kwani Serikali ipo macho na haiwezi kukubali hasara.

"Hili ni onyo kwa wafanyabiashara wote ambao wanafanya biashara za magendo, kamwe hatuwezi kuwaacha wala kuwasamehe kama watafanya magendo. Vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vipo na tutawakamata," amesema Gondwe.

Naye meneja wa TRA Wilaya ya Korogwe, Remigius Lwambano amesema mifuko hiyo 15 thamani yake ni Sh1.6 milioni kwa bei ya sasa ya mfuko wa kilo 50 kwa Sh110,000.

Amesema sukari hiyo inaonyesha inatoka nchini Brazil,  imeingia nchini kupitia njia za panya na kusambazwa kwa wananchi.

JE Umehangaika na Matatizo ya Kimapenzi Kwa Muda Mrefu? Muone Shehe Chalo Atakutatulia Matatizo yako Kirahisi

$
0
0

JE umehangaika na matatizo haya kwa muda mrefu mtalamu Challo anayo dawa ya kuvuta mpenzi Je unasumbuliwa na mpenzi umeachwa na mpenzi au Mme mke na Bado unampenda na umejaribu sehemu nyingine Bila mafanikio njoo utatuliwe haraka na kundumisha ndoa yenu..

Umekimbiwa na mmeo mkeo au mpenzi na anaishi na mtu mwingine atarundi haraka kusafisha nyota mvuto wa mwili na biashara minguu kufa ngazi kuwaka moto ngiri tumbo kuunguruma na wakina Baba wasiojiweza katika tendo la uyumba kuchelewa kufika kileleni tunatibu Busha Bila oprasheni bali kwa kutumia vitabu vya dini

Tunatoa pete ya utajiri Bila mashariti mkufu wa bahati unauza Mali ya haindi unapoteza pesa kwenye biashara yako Bila kujua unataka kupandishwa cheo

Wasiliana na mtalamu Shehe Challo 0714006521

Maadui wa JPM Hadharani..Habari Zilizopo Katika magazeti ya Leo Jumamosi ya February 24

$
0
0

Habari Zilizopo Katika magazeti ya Leo Jumamosi ya February 24

Madiwani Warushiana Vijembe Kwenye Mkutano

$
0
0
Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita amelazimika kuingilia kati kuwatuliza wajumbe wa baraza la madiwani la jiji hilo waliokuwa wakipigana vijembe kwa misingi ya vyama.

Wajumbe waliokuwa kwenye kikao cha kupitia utelezaji wa bajeti ya mwaka 2016/17 walitumia muda mwingi kusifia vyama vyao badala ya kujikita kwenye hoja iliyo mbele yao.

Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea aliposimama alihoji ni kwa nini chumba chao cha mikutano hakina vipaza sauti wakati bajeti iliyopita ilihusisha ukarabati.

Mkurugenzi wa Jiji, Sipora Liana alimjibu kuwa fedha zilikwisha lakini jitihada zinaendelea ili vipaza sauti vipatikane.

Aliposimama diwani wa Kibondemaji, Abdallah Mtinika alimpongeza meya Mwita ambaye ni diwani wa Chadema kwa kutekeleza ilani ya CCM.

"Nikupongeze meya, tunaona ilani ya CCM inatekelezwa kwa vitendo mambo yanakwenda sawa na ndiyo sababu leo mtu anasimama anakosa la kusema matokeo yake anaulizia vipaza sauti," alisema.

Kauli hiyo ilimuinua diwani wa Tabata, Patrick Asenga aliyekanusha kutekelezwa ilani ya CCM katika Jiji la Dar es Salaam.

"Nikupongeze meya kwa kuwa kwa mara ya kwanza Jiji la Dar es Salaam mambo yanakwenda sasa hiyo ni kutokana na uongozi imara wa Ukawa, hakuna mambo ya CCM hapa," alisema Asenga.

Meya Mwita aliingilia kati na kuwataka madiwani kujikita kwenye hoja zilizomo kwenye makabrasha.

Akizungumza na MCL Digital baada ya kikao hicho leo Februari 23,2018 Meya Mwita amesema anatambua maendeleo hayana vyama na lengo lake ni kuifanya Dar es Salaam iwe jiji lenye maendeleo zaidi.

"Ukitaka mambo yaende vizuri, wakati mwingine hutakiwi kuipa nafasi sana siasa ndiyo sababu sina ubaguzi, nataka madiwani wote wawe kitu kimoja kwa ajili ya maendeleo," amesema Mwita.

Billnass Afunguka Kuhusu Kuacha Kufanya Kazi na Petitman

$
0
0

Baada ya story kuwa nyingi mtandaoni kuhusu msanii Billnass kuacha kufanya kazi na Petitman huku zikihusishwa na story ya kuwa wameshindwana na isitoshe wana ugomvi, sasa Billnass amezungumza kuhusu hilo na kusema kuwa hawajagombana bali Petitman kaamua kujitoa mwenyewe.

Msanii Billnass amesema kuwa…
“Ameamua kufanya vitu vyake ni hatua nzuri tu na sisi tunaendelea, amejitoa sijui kama ameona amepoteza hela yake na muda wake kwangu naamini kila mtu anamaamuzi yake hatuwezi kufanya kazi milele, hatuna tatizo lolote”

Nigeria: Wazazi wa Wasichana Waliotekwa Washikwa na Hasira

$
0
0
Kumekuwa na ongezeko la hali ya hasira kwa wazazi wa wasichana wanaodaiwa kutekwa na kundi la wapiganaji wa Boko Haram ambao siku ya jumatatu wamevamia shule moja ya wasichana katika mji wa Daptch nchini humo.

Wazazi wa wanafunzi hao waliokuwa waliokuwa bweni shule Dapchi wamesema kuwa hadi sasa hawaelewi mahala walipo watoto wao.

Serikali ya Nigeria imetoa kauli ya kuomba radhi kwa taarifa zisizo sahihi zilizotolewa siku ya jumatano kwamba baadhi ya wanafunzi waliokolewa na vikosi vya serikali wakati si kweli.

Makundi ya wanaharakati nchini Nigeria yameitaka serikali kutoa orodha ya majina ya wasichana hao waliotekwa ili kuweza kujua idadi yao kamili.

Tukio kama hilo nchini Nigeria lilitokea mwaka 2014 ambapo wasichana 276 wa Chibok walitekwa na Boko Haram.

Hii ndio sababu ya Ugonjwa wa Kutokwa na Machozi ya Damu

$
0
0
Kuna magonjwa mengi duniani na mengine mapya huibuka kila siku huku mengine yakipatiwa tiba na mengine tiba zake zikiendelea kutafutwa na wataalamu wa afya. Inawezekana wewe ni moja kati ya wengi ambao hawajawahi kusikia ugonjwa wa kutokwa Machozi ya Damu.

Wataalamu wanasema kuwa kupitia uchunguzi walioufanya wamegundua kuwa ugonjwa huu unatokana na kasoro kwenye vinasaba (genes) za binadamu jambo ambalo hupelekea matatizo kwenye mishipa ya damu na hatimaye damu kuvuja maeneo ya mwili kama machoni.

Wanasayansi katika Chuo Kikuu cha London katika Taasisi ya Afya ya Watoto na Hospitali ya Great Ormond Street (GOSH), ambao walishiriki utafiti huo, wameeleza kuwa kupatikana kwa ugunduzi huo kutasaidia kupatikana tiba ya ugonjwa huo.

Haya yametokea baada ya kesi mbalimbali za watu kuwa na ugonjwa huo maeneo mbalimbali duniani.

Watoto Wanaolazimishwa Kutazama Mama zao Wakibakwa na Kuuawa

$
0
0
Kutoka nchini Sudan Kusini, ripoti ya Umoja wa Mataifa leo February 23, 2018 inaeleza kuwa watoto nchini humo wanalazimishwa kutazama jinsi mama zao wanavyotendewa vitendo vya ubakaji na wengine wakiuawa.

Ripoti ya wachunguzi wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa imeeleza kuwa maafisa 40 wanaweza kuhusishwa katika uhalifu wa vita na uhalifu wa aina nyingine unaoendelea nchini humo dhidi ya binadamu.

Inaelezwa kuwa raia wamekuwa wakiteswa na kuharibiwa na vijiji vikiharibiwa. Migogoro kati ya vikundi vya serikali imeendelea Sudan Kusini pamoja na mpango wa amani uliosainiwa mwaka 2015.

Baada ya Kifo cha AKWILINA Sheria inasemaje kwa Vifo Kama Hivyo

$
0
0

Baada ya tukio la kupigwa risasi na kufariki mwanafunzi wa chuo cha NIT Akwilina Akwilini wakati wa maandamano ya CHADEMA licha ya kwamba yeye hakuwa kwenye maandamano hayo, tumemtafuta mwanasheria Jebra Kambole ambaye ameeleza kuhusu sheria inasemaje endapo vinatokea vifo vya aina hiyo..?

Mwanasheria Jebra Kambole amesema kwamba sheria inatoa muongozo kwamba kimsingi jeshi la polisi lina mamlaka ya kufanya uchunguzi aidha linajichunguza lenyewe au linachunguza kitu kingine na wakishajua nani amefanya kosa atachukuliwa hatua za kisheria.

Msikilize hapa chini mwanasheria JEBRA KAMBOLE akieleezea vizuri kwa kubonyeza PLAY

Wazazi wa Akwilina Wafunguka Haya Baada ya Kumzika Mtoto Wao

$
0
0
Wazazi wa Akwilina Wafunguka Haya Baada ya Kumzika Mtoto Wao
Wazazi wa marehemu Akwilina Akwilini Bafta wamefunguka baada ya mazishi ya mtoto wao huyo ambayo yalifanyika jana (Ijumaa) katika eneo la nyumbani kwao, katika kijiji cha Marangu Kata ya Marangu Kitowo wilaya ya Rombo, ambapo Serikali kupitia Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira, Waziri wa Elimu, Prof. Ndalichako waliongoza maelfu ya Watanzania katika ibada maalum ya kuuaga mwili huo.

Akiongea na Bongo5, Baba mzazi wa Akwilina, ameishukuru Serikali pamoja na Watanzania waliojitokeza katika kuuaga mwili huo pamoja na ushirikiano huku akiwaomba Watanzania kwa ujumla kuzidi kumkumbuka.

Hata hivyo Mama Mzanzi wa marehemu alipohojiwa na Bongo5 ameshindwa kuongea lolote huku machozi yakizidi kumtoka kwa uchungu akisema hana neno lolote la kusema.

Hali ya usalama nyumbani kwa kina Akwilina kuliimarishwa na ulinzi wa kutosha kwasababu ya wingi wa watu waliojitokeza kumuaga binti huyo wakati vilio na simanzi vikitawala katika kijiji cha Marangu.

Kwa upande wa Serikali msafara wake uliondoka nyumbani kwa wazazi wa marehemu baada ya mazishi hayo yaliyofanyika majira ya Alasiri na kuwaacha baadhi ya wafiwa nyumbani kwao.

Pretty Kind Akubwa na Skendo ya Uchawi Kisa Hiki Hapa

$
0
0
Pretty Kind Akubwa na Skendo ya Uchawi Kisa Hiki Hapa
MSANII wa filamu Bongo, Suzan Michael ‘Pretty Kind’ amejikuta akitafunwa na skendo ya uchawi kutoka kwa watu wake wa karibu ambao alikuwa anaishi nao, New Delhi nchini India, kutokana na mambo yake kumuendea poa huku wenzake yakibuma.

Chanzo chetu kutoka nchini humo kilidai kuwa, wasichana wengi wa Kibongo waishio India wamefurahi mno kusikia msanii huyo kafungiwa na Naibu Waziri, Juliana Shonza kufanya sanaa, sababu alikuwa anawatambia mno.



“Pretty kwa Wabongo wengi kule India wanamjua kwa kutumia ‘ndumba’ ili mambo yake yamnyookee kwani alipokuwa huko alikuwa akiwazidi wasichana wote na kila alichokifanya kilikuwa kikimnyookea tofauti na wengine.



“Hali hiyo ilisababisha minong’ono sana mpaka ameondoka na hakuna aliyempenda,” kilidai chanzo hicho ambacho kiliomba kuhifadhiwa.



Badaa ya madai hayo, Risasi Jumamosi lilimsaka Pretty ambaye alifunguka kama ifuatavyo:

“Jamani mimi siyo mchawi, wananizushia sababu ya chuki zao binafsi, mimi nipo karibu na Mungu kuliko wanavyodhani, hata usiku huwa nakesha nikisali, sasa huo uchawi nafanya saa ngapi.”

Polisi Yatoa Sababu za Mauaji ya Kikatili ya Diwani wa Chadema

$
0
0
Polisi Yatoa Sababu za Mauaji ya Kikatili ya Diwani wa Chadema
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Urich Matei amefunguka na kusema kuwa kifo cha Diwani wa Kata ya Nawala tarafa ya Ifakara wilayani Kilombero, Godfrey Joackim (CHADEMA) aliyefariki kwa kupigwa mapanga huenda ni kisasi.


Matei amesema kuwa kiongozi huyo kuna wakati aliwahi kuwaambia wanakijiji kuwa mtu ambaye alikuwa anafahamika kwa jina la Kenani Haule ndiye alikuwa anawasaliti hivyo baada ya muda mtu huyo aliuliwa kwa kupingwa mapanga.

"Mwanzoni mwa mwaka 2016 watu wa Nawawala walikuwa na ugomvi kati ya wanakijiji na bodi ya sukari akiwa diwani wa eneo lile alisimamia wananchi wale kudai lile shamba, kuna kesi ambayo ipo mahakamani mpaka sasa inaendelea lakini aliwaambia mtu mmoja anaitwa Kenani Haule ndiye tatizo, kwa hiyo diwani Godfrey Joackim aliwaambia tu kuwa huyo Haule ndiye anawasaliti hivyo aliwaambia hata kama Kenani akifariki basi wao watakuwa na uwezo wa kupata shamba na kweli muda mfupi Kenani Haule aliuawa kwa kukatwa katwa mapanga tukio ambalo lilitokea kama lilivyotokea kwake, kimsingi kabisa tunaamini Godfrey Joackim atakuwa ameuawa kwa ajili ya kisasi baada ya kifo cha Kenani Haule" alisema Matei

Aidha Kamanda Matei amedai kuwa jeshi la polisi bado linaendelea na uchunguzi na msako mkali unaendelea na kudai hilo ni tukio baya kutokea Morogoro kwa sababu wamempoteza kiongozi wa wananchi wa Nawala na kuwataka wananchi yoyote ambaye anataarifa juu ya mazingira ya mauaji hayo awape taarifa jeshi la polisi ili waweze kuzifanyia kazi zaidi.

Familia Yagoma Zari na Diamond Kuachana .... Wataka Wamalizane

$
0
0
Familia Yagoma Zari na Diamond Kuachana
SIKU chache baada ya mrembo Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kutangaza kummwaga mpenzi wake, staa wa Bongo Fleva, Abdul Nasibu ‘Diamond Platnumz’, inasemekana kuwa, familia ya msanii huyo imewagomea wawili hao kuachana.

Taarifa ambazo Ijumaa lilizipata zilidai kuwa, ndugu wa Diamond hawakupendezwa na kitendo cha wawili hao kutengana kwa jinsi walivyokuwa wameshibana. “Familia imekataa kabisa.

Diamond na Zari hatua waliyokuwa wamefi kia si kwamba ni wachumba, bali ni mume na mke kwa sababu wamekaa pamoja kwa muda mrefu na ukizingatia tayari wana watoto wawili waliozaa pamoja,” Ijumaa lilitonywa.

Ijumaa lilielezwa kuwa, baadhi ya ndugu wa karibu wa Diamond wamekutana mara kadhaa na kulijadili suala hilo ili kuangalia uwezekano wa wawili hao kumaliza tofauti zao na kuishi kama zamani.

Gazeti hili lilielezwa kuwa, mbali na ndugu hao wa upande wa mama’ke Diamond, Sanura Kassim ‘Bi Sandra’, ndugu wengine wa upande wa baba yake Diamond, Abdul Jumaa nao Hawakufurahishwa na kitendo hicho.

“Ndugu wa baba Diamond nao hawakufurahia.

Baba Diamond mwenyewe licha ya kuwa ana mapenzi na mkwewe mwingine ambaye ni Hamisa Mobeto, lakini bado anataka mwanaye asimuache Zari,” Ijumaa lilielezwa katika uchunguzi wake.

Alipotafutwa baba Diamond, mzee Abdul Juma, alikiri kwamba kama familia hawakufurahishwa na jambo hilo na wanaangalia namna ya kuzungumza na mkwe wao (Zari) ili ikiwezekana wakae sawa.

“Nafanya bidiii ya kuwafi kia wenzangu kule (upande wa mama Diamond) ili ikiwezekana tuone namna ya kuwasuluhisha,” alisema baba Diamond.

Alipotafutwa mama Diamond kuhusu suala hilo, alipokea simu na kusikiliza kasha kupotea hewani na hata alipopigiwa tena, simu yake iliita bila kupokelewa.

Ijumaa pia lilimpigia simu kaka yake, Diamond, Romy Jons ili kumsikia anazungumziaje kuhusu suala hilo ambapo alipopatikana alisema: “Nipo hospitalini, naomba nikutafute baadaye.”

Hata hivyo, hadi muda unayoyoma, Romy hakurudi hewani hata alipotafutwa tena na Ijumaa, simu yake haikupatikan
Zari na Diamond (pichani) waliodumu kwenye uhusiano na kufanikiwa kuzaa watoto wawili, Tiffah na Nillan, walikuwa kwenye msuguano kwa kile kilichoelezwa kuwa ni usaliti aliokuwa akiufanya Diamond

Wakati anaandika waraka wa kummwaga Diamond, Zari alisema alifi kia uamuzi huo kutokana na Diamond kuwa na skendo nyingi za wanawake zinazoandikwa kwenye mitandao na vyombo vya habari.

Yanga Kuomba Kusogezewa Mechi Dhidi ya Kagera Sugar

$
0
0
Yanga Kuomba Kusogezewa Mechi Dhidi ya Kagera Sugar
Klabu ya soka ya Yanga kupitia kwa msemaji wake Dismas Ten, imesema imedhamiria kuiandikia barua Bodi ya ligi kuomba kusogezwa mbele kwa mchezo wake  wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar.


Ten ameweka wazi hilo huku akitaja sababu kubwa kuwa ni ugumu wa ratiba unaoikabiri timu hiyo hivyo inahitaji kupata muda wa maandalizi ya mechi ya Ligi ya mabingwa Africa dhidi ya Township Rollers ya Botswana.

''Tunatazama uwezekano wa kupeleka barua kwenye shirikisho au bodi ya ligi ili kuomba mechi yetu dhidi ya Mtibwa isogezwe mbele tuweze kujiandaa vizuri na mechi ya kimataifa, tunataka kushinda ili tufike mbali zaidi ya tulipoishia msimu uliopita'', amesema.

Yanga imeondoka jijini Dar es salaam kuelekea Songea kwenye mchezo wake wa kombe la shirikisho dhidi ya Majimaji na baada ya mchezo huo itaelekea Mtwara kucheza mchezo wa ligi na Ndanda FC Februari 28 kabla ya kurejea na kwenda Morogoro kucheza na Mtibwa Machi 3.

Yanga ambayo inashika nafasi ya pili kwenye ligi ikiwa na alama 37, inatarajia kucheza mechi yake ya klabu bingwa Africa hatua ya kwanza Machi 6 dhidi ya Township Rollers kwenye uwanja wa Taifa Dar es salaam.

Benki Zatoa Onyo kwa Mamlaka za Serikali Juu ya Akaunti Kanisa la Kakobe

$
0
0
Benki Zatoa Onyo kwa Mamlaka za Serikali Juu ya Akaunti Kanisa la Kakobe
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Benki Tanzania (TBA), Dk Charles Kimei ameonya kuwa umakini unahitajika katika mamlaka za Serikali kwa kuwa kutoa siri za mteja kutoka benki na kuziweka hadharani kunaweza kuua sekta hiyo.

Kimei, ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa CRDB alisema hayo wakati akitoa mada katika kongamano la maendeleo ya viwanda lililofanyika katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Kigamboni jijini hapa jana .

Onyo la Kimei limekuja siku tatu tangu Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), iweke hadharani taarifa ya akaunti ya Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF) iliyopo katika Benki ya NBC kuwa ina zaidi ya Sh8 bilioni.

Februari 19, TRA ilitoa taarifa ya matokeo ya uchunguzi iliyoufanya baada ya kiongozi wa kanisa hilo, Askofu Zachary Kakobe kutoa kauli katika mkesha wa Krismasi mwishoni mwa mwaka jana kwamba ana fedha nyingi kuliko Serikali.

Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere akitoa taarifa ya uchunguzi huo, alisema Askofu Kakobe hana akaunti wala fedha katika taasisi yoyote ya kifedha nchini zaidi ya kuwa mmoja kati ya wasimamizi wakuu wa akaunti ya kanisa analoliongoza.

Kichere alikwenda mbali zaidi na kusema akaunti za kanisa hilo zipo NBC zikiwa na zaidi ya Sh8 bilioni, ambazo ni fedha za sadaka, zaka na changizo zinazotolewa na waumini. Hata hivyo suala hilo halijakubalika miongoni mwa benki.

Dk Kimei alisema miongoni mwa masuala muhimu katika biashara ya benki ni usiri wa taarifa za mteja na mamlaka za Serikali katika kutekeleza majukumu yake taarifa za benki hazipaswi kuwa kitu cha kwanza bali zitolewe iwapo Mahakama itahitaji.

Jambo hilo ambalo limezua mjadala miongoni mwa wachumi na wataalamu wa sekta za fedha lilizungumzwa pia na Mkurugenzi wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Godfrey Simbeye katika kongamano hilo.

Simbeye alisema ni muhimu kwa mamlaka husika kupima matokeo ya jambo wanalotaka kulifanya kabla ya kuchukua hatua.

“Jambo la kutoa taarifa za mteja ni baya kwa jicho la kiuwekezaji, wafanyabiashara wakubwa hawatataka kuja nchini kuwekeza kwa kuhofia kutokuwa na usiri katika mambo yao ya kifedha,” alisema Simbeye.

Alisema hali kama hiyo inaongeza hatari na imani hasi ya wawekezaji juu ya mazingira ya kufanya biashara nchini.

Nayo benki ya NBC, ambako kanisa hilo ndio huweka fedha zake imetoa kauli kuhusu hatua ya TRA kuweka wazi taarifa za kifedha za Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), huku wadau wa sekta ya benki wakiendelea kulaani jambo hilo.

NBC baada ya kuulizwa na Mwananchi Jumanne wiki hii kuhusu namna ilivyotimiza jukumu lake la kulinda taarifa za mteja kama sheria na utaratibu unavyotaka, jana ilijibu kwa njia ya barua pepe ikisema mambo yote yalifuata utaratibu na matakwa ya kisheria.

“Kulinda taarifa za mteja ni miongoni mwa vipaumbele vya benki yetu na tunafanya hivyo kwa kufuata sheria, kanuni na utaratibu wa nchi, katika suala la Kakobe taratibu zote zilifuatwa kwa mujibu wa sheria na NBC haina utaratibu wa kutoa taarifa za mteja bila kumhusisha,” ilieleza taarifa ya benki hiyo.

Mwanzoni mwa wiki, Kichere aliliambia Mwananchi kuwa TRA walitoa taarifa kwa kuongozwa na busara kwa kuwa kabla ya kufanya uchunguzi waliutaarifu umma hivyo hata baada ya uchunguzi waliona ni vyema kuweka wazi matokeo ya kile walichokichunguza.

Katika kongamano la jana, wadau wa sekta ya fedha walisema ili taasisi za fedha ziweze kushiriki kikamilifu katika sekta ya viwanda nchini, Serikali imetakiwa kupunguza kukopa nchini, kutoa elimu ya benki kwa wananchi na kuanzisha chombo maalumu cha ukopeshaji wa mitaji kwaajili ya viwanda.

Akifungua mkutano huo, naibu waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stella Manyanya alisema taasisi za fedha zinapaswa kuisaidia Serikali kufikia adhima yake ya kuwa na nchi ya uchumi wa viwanda kwa kuwezesha uwekezaji katika eneo hilo.

“Kama taasisi za fedha zitaelekeza nguvu katika kuendeleza viwanda lengo la Serikali yetu litafikiwa, Watanzania wengi wanathubutu, lakini wanapata changamoto ya mitaji na elimu ya biashara,” alisema Mhandisi Manyanya.

Akichangia mada hiyo, Kimei alisema asilimia 70 ya fedha zilizopo katika mzunguko hapa nchini zipo katika benki za biashara na asilimia 30 katika taasisi za mitaji kama mifuko ya hifadhi za jamii.

“Kuna fursa ya kuwekeza na kupata faida kubwa katika sekta ya viwanda sasa, lakini benki za kibiashara hazina uwezo wa kutoa mikopo ya muda mrefu kwakuwa fedha zake nyingi ni amana za watu huku amana za mtu mrefu zikiwa asilimia 40 tu,” alisema Dk Kimei.

Alisema mifuko ya jamii ina uwezo wa kutoa mikopo ya muda mrefu lakini hilo si jukumu lake ni si salama kwao kwa sababu hawana uwezo mkubwa wa kujua taarifa za mkopaji na kukokotoa hatari na faida za mikopo yao.

Alisema wanasiasa na viongozi wa dini wanatakiwa kusaidia kuishauri jamii kuhusu umuhimu wa kuweka akiba katika benki kwa ajili ya kukuza uchumi wa nchi na kinga yao wakati wa dharura.

Simbeye alisema ni muhimu kuwa na mfuko maalumu kwaajili ya viwanda kwasababu benki za biashara zinalenga zaidi faida kuliko huduma ndiyo maana mikopo yao mingi ni kwa wafanyabiashara.

“Mwaka jana fedha ambazo zilikopeshwa kwa sekta binafsi ni trilioni 16.3, asilimia 9.8 tu ndo zimekwenda kwenye viwanda ... kujenga uchumi wa viwanda ni mradi wa kitaifa kama ilivyo SGR hivyo ni muhimu serikali ikatenga fedha mahususi kwaajili yake,” alisema Simbeye.

Nimeachana na Diamond Kabisa Sina Mpango wa Kurudiana nae Tena- Zari

$
0
0
Nimeachana na Diamond Kabisa na Sina Mpango wa Kurudiana nae Tena- Zari
Zari Hassan maarufu Zari The Boss Lady amesema hafikirii na hatarajii kurudiana na mzazi mwenzake Naseeb Abdul 'Diamond'.

Zari aliyezaa watoto wawili na Diamond ambaye ni msanii maarufu wa muziki ndani na nje ya nchi amesema hayo jana Februari 23,2018 alipohojiwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC).

"Nilikaa muda mrefu nikafikiria vitu vingi ndipo nikasema unajua nini, nahitaji kufikia mwisho wa hili," amesema Zari alipoulizwa swali na mtangazaji Mariam Omary kuhusu ujumbe aliouweka katika akaunti yake ya kijamii ya Instagram akielezea kuachana na mzazi mwenzake.

Alipoulizwa ulikaa na kutafakari ukaona ufikie hili, Zari alijibu, "Tulikuwa tunajaribu kuona tuna-move kutoka  scandal (kashfa) ya kuwa amepata mtoto na tunaweza kusonga mbele."

"Lakini vitu kama hivi leo unasikia hivi leo unaona vile sijui kukumbatiana na ma X kwenye public, vitu vya kunidhalilisha, kunifanya nisiheshimike na watoto wangu, nimeachana naye kabisa," amesema.

Alipoulizwa iwapo Diamond alimpigia simu kumuomba msamaha baada ya picha hizo kusambaa, Zari amesema hakufanya hivyo na hakuona haja ya kumpigia simu kumuuliza.

Kuhusu Diamond kama atakwenda kumwomba msamaha atakubali Zari amesema, "Si alishakuja kipindi  fulani alipozaa na huyo dada fulani (Hamisa Mabeto) sioni kama itawezekana."

Alipoulizwa iwapo Diamond atatuma watu wa kumwombea msamaha; Zari amesema hawezi kulizungumzia hilo kwa kujibu 'no comment'.

Zari alipoulizwa iwapo hilo la kuachana ni kutafuta kiki amejibu, "Yaani tumeachana kabisa, it's done. Sijui kama amekubali, tangu video zile zimetoka na X wake nimem-block wiki tatu hatuongei ndipo nika-post."

Hivi Katika Ndoa Nani Humtunza Mwenzake?

$
0
0
 Hivi Katika Ndoa Nani Humtunza Mwenzake?
BILA shaka wengi watakuwa wamejaribu kujiuliza, swali hili je ni nani hasa, ana wajibu wa kumtunza mwenzake baina ya wanandoa au kati ya mke na mume?

Ni mwanaume au ni mwanamke ama ni wote kwa pamoja, kila mmoja kwa nafasi yake?

Sheria inasemaje kuhusiana na suala au hoja, hii? Awali ya yote, suala la matunzo kwa wanandoa, lenyewe, liko kwa mujibu wa sheria.

Hivyo ni sawa na kusema kuwa matunzo siyo suala la hisani, zawadi au upendeleo fulani maalum kutoka kwa mume kwa ajili ya mke au mke kwa ajili ya mumewe.

Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 imeweka bayana habari nzima ya matunzo baina ya wanandoa.

Niseme mapema tu kuwa wapo wanaojua kuwa mume peke yake ndiye mwenye wajibu au jukumu la kutoa matunzo kwa mke.

Tena kuna baadhi ya wanawake hujiaminisha kuwa fedha zao si za kutunza familia bali ni za kujipamba na kununua kile wanachotaka kwa vile kazi ya kutunza watoto na yeye mama ni ya baba au mume.

Sivyo hivyo muda wote wakati mwingine mama.

Matunzo ni nini?

Kifungu cha 63(a) cha Sheria ya Ndoa, 1971 kinataja vitu ambavyo kisheria ndivyo vinavyotambulika kama matunzo kwa wanandoa ambao ni mume na mke.

Kifungu hiki kinabainisha bayana kuwa, makazi, mavazi na chakula, haya ndiyo mahitaji ya msingi ambayo, kila, mwanandoa mume au mke mwenye wajibu wa kuyatoa, kwa kuzingatia uwezo na nafasi yake kiuchumi, atatakiwa kuwapa au kuyatimiza kama wajibu wake kwa mwanandoa mwenzake.

Wajibu wa mke kutoa matunzo kwa mume wake.

Ni vema ikafahamika kuwa suala la matunzo linawahusu wanandoa wote yaani mke pamoja na mume.

Kila mmoja anao wajibu kwa mwenzake katika kutoa matunzo. Isipokuwa wajibu wa aina gani kwa nafasi fulani, unatofautiana baina ya hawa wahusika wawili.

Hii ni kutokana na ukweli kwamba, mke na mume wote wanao wajibu unaoambatana na mipaka katika kutoa matunzo yanayowahusu ili ndoa yao idumu.

Kifungu cha 63(b) cha Sheria ya Ndoa, 1971 kinasema kuwa mwanamke au mke ambaye ana uwezo ana wajibu wa kutoa matunzo kwa mume wake ambaye hajiwezi, ambaye ana ugonjwa wa kimwili au kiakili ambao haumuwezeshi kufanya kazi ya kumwingizia kipato.

Hivyo basi, wajibu wa mwanamke au mke kumhudumia mwanaume  ambaye ni mume ni pale tu mwanaume huyu anapokuwa amepatwa au kufikwa na ulemavu au ugonjwa wa akili au mwili.

Na kama haitoshi, ugonjwa au ulemavu husika ni lazima uwe ni kwa kiwango cha kutomwezesha mhusika au mume kufanya kazi.

Tofauti na mwongozo huu, dhahiri mlengwa atakuwa nje ya muktadha wa ulinzi au utetezi wa kifungu hicho.

Maana yake ni kuwa, ikiwa mwanaume au ume wa ndoa anajiweza siyo mgonjwa au siyo mlemavu au ni mgonjwa au mlemavu lakini ugonjwa au ulemavu huo haumzuii, kuweza, kufanya kazi ya kujiingizia kipato basi mwanamke au mke wake hatawajibika kumpa matunzo.

Wajibu wa mume kutoa matunzo kwa mke wake, huu unabainishwa katika kifungu cha 63(a) cha sheria hiyo kinachosema kuwa ni wajibu wa mume kumtunza mke wake au wake zake kwa ndoa ya mke zaidi ya mmoja kwa kuwapa makazi, mavazi na chakula kutokana na uwezo wake wa kipato uchumi.

Kwa muktadha wa kifungu hiki hapo juu, utaona tofauti kati ya wajibu wa mwanamke mke katika kutoa matunzo na ule wa mwanaume (mume). Kwa mwanaume au mume wa ndoa kutoa matunzo ni muda wote ndani ya ndoa.

Haijalishi, aidha mke husika ni mlemavu au mgonjwa, ni mzima wa afya; anao uwezo wa kufanya kazi lakini ni mama wa nyumbani, lazima mwanaume (mume) atatoa matunzo.

Jambo la msingi la kuzingatia hapa ni kuwa mwanaume au mume wa ndoa atawajibika kutoa matunzo husika kwa kuzingatia uwezo wake wa kipato au uchumi binafsi.

Haitowezekana kuishawishi mahakama, katika shauri, kuamuru mwanaume au mume kutoa matunzo zaidi kuliko uwezo wa kipato chake na hata kukubaliwa kutoa chini ya kile kiwango kinachowezekana kulingana na uwezo wake.

Nililazimisha Mapenzi kwa Mwanaume Anbaye Hakuwa na Muda Nami- Fedha Kessy

$
0
0
Nililazimisha Mapenzi kwa Mwanaume Anbaye Hakuwa na Muda Nami- Fedha Kessy
Mwanamuziki wa Bongo Flava, Feza Kessy amefunguka sababu ya kuandika ngoma yake iitwayo Kaa Kijanja ambayo amemshirikisha Nikki wa Pili.

Muimbaji huyo ambaye ni mtangazaji pia wa Choice Fm, amesema katika maisha yake ilitokea akampenda mtu ambaye hakuwa na muda naye.

“Napenda kulazimisha vitu vitokee lakini kwenye mapenzi hapana, kwa  sababu kuna mtu nilikuwa nalazimisha mapenzi lakini hakuwa upande wangu,” amesema Faza.

Ameongeza kuwa kitu hicho kilimkatisha tamaa kwani licha ya hivyo aliyempenda alikuwa akimsaliti katika mapenzi, hivyo akaamua kuondoka katika mahusiano hayo.

Fezza Kessy kwa sasa anatamba na ngoma inayokwenda kwa jina la Simple ambayo amemshirikisha Dammy Krane, mdundo ukiwa ni wa producer S2kizzy.
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images