Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104414 articles
Browse latest View live

Mzee Akilimali Aibeza Simba "Hakuna Dalili za Simba Kufanikiwa Waarabu ni Moto wa Kuotea Mbali"

0
0
Mzee Akilimali Aibeza Simba "Hakuna Dalili za Simba Kufanikiwa Waarabu ni Moto wa Kuotea Mbali"

KATIBU wa Baraza la Wazee wa Yanga, Mzee Ibrahim Akilimali amesema haoni dalili yoyote ya watani wao Simba kusonga mbele kwenye Kombe la Shirikisho Afrika kwani wamepewa chuma.

Kauli hiyo ya Mzee Akilimali imekuja baada ya Simba kutinga raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo sasa itacheza na Al Masry ya Misri Machi 6, mwaka huu.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Mzee Akilimali alisema haoni dalili za Simba kufanikiwa kwenda hatua kubwa kufuatia kukutana na Waarabu ambao ni moto wa kuotea mbali katika michuano hiyo.

“Safari hii naona nao wamepata chuma kwa sababu miaka ya nyuma walikuwa wanatucheka kwamba hatuwezi kucheza na Waarabu nao ndiyo walikuwa wanajifanya wanawamudu kwa kuangalia historia.

“Lakini jambo zuri wamepata bahati na wamerejea kwenye michuano ya kimataifa ila sasa wale wanaokutana nao ni chuma cha moto, Simba hawawezi kwenda popote,” alisema Mzee Akilimali.

Al Masry ni miongoni mwa timu ambazo zinatoa upinzani mkali kwa vigogo wa soka Misri ambapo ni Zamalek na Al Ahly na sasa wapo nafasi ya nne katika Ligi ya Misri wakiwa na pointi 42.

Kocha wa Al Masry ni mshambuliaji wa zamani wa Zamalek, Hossam Hassan ambaye alikuwepo kwenye kikosi cha Zamalek kilichong’olewa na Simba mwaka 2003 katika Klabu Bingwa Afrika.

Tundu Lissu Amuwashia Moto Msajili "Jaji Mutungi Usiitishe Chadema Jitafakari"

0
0
Tundu Lissu Amuwashia Moto Msajili "Jaji Mutungi Usiitishe Chadema Jitafakari"
Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu amefunguka na kumtaka Msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Mtungi kujitafakari, kwani amedai kuwa Jaji huyo amekuwa ni mpofu kwa mambo mabaya wanayofanyiwa watu wa upinzani nchini.

Lissu amesema hayo kufuatia Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi kuwaandikia barua CHADEMA ambayo anadai inatuhuma mbalimbali pamoja na vitisho mbalimbali

"Nimesoma barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, yenye tuhuma na vitisho vingi dhidi ya CHADEMA, bila kutoa ushahidi wowote na kwa kutegemea taarifa za upande mmoja tu, Msajili Mutungi ameituhumu CHADEMA kwa kufanya siasa za kibabe na vurugu na kukiuka Sheria ya Vyama vya Siasa na Kanuni za Maadili ya Vyama vya Siasa. Msajili Mutungi anastahili kujibiwa hadharani na kukumbushwa mambo kadhaa. Inaelekea amejisahau sana au anafikiria Watanzania ni wajinga wasioelewa mambo yake."

"Msajili wa Vyama vya Siasa amekosa sifa na uadilifu (moral authority) ya kunyooshea kidole CHADEMA au chama kingine chochote cha upinzani kuhusiana na jambo lolote linahusu Sheria ya Vyama vya Siasa na kanuni zake. Tangu 2015 nchi yetu imeshuhudia ukiukwaji mkubwa wa Sheria ya Vyama vya Siasa ukifanywa. Mikutano ya hadhara na maandamano ya amani, ambavyo ni haki ya vyama vya siasa kwa mujibu wa Sheria hiyo, imepigwa marufuku bila uhalali wowote. Msajili Mutungi hajawahi kukemea ukiukwaji huo wa sheria wala kutetea haki ya vyama vya siasa"

"Viongozi wa vyama vya upinzani, hasa CHADEMA, wameuawa, wametekwa nyara na kupotezwa, wamepigwa risasi katika majaribio ya kuuawa, wameteswa, wamekamatwa na kushtakiwa kwa kesi za uongo. Msajili Mutungi amekuwa bubu na kiziwi asiyesikia wala kukemea uonevu na ukandamizaji huu dhidi ya vyama anavyovisimamia. CCM na serikali yake zimetoa hongo kurubuni madiwani, wabunge na viongozi wengine wa vyama vya upinzani kujiuzulu nafasi zao. Yote ni makosa ya maadili kwa mujibu wa sheria. Msajili Mutungi hajawahi kuliona hilo.

Umoja wa Ulaya Watoa Tamko Mauaji Utekaji Nchini

0
0
Umoja wa Ulaya Watoa Tamko Mauaji Utekaji Nchini
Umoja wa Ulaya (EU) umetoa tamko kuhusu matukio ya utekaji na mauaji yanayotokea nchini, ukiitaka Serikali kufanya uchunguzi wa kina.

Taarifa ya umoja huo uliyotolewa leo Februari 23, 2018 inaeleza kuwa imetolewa na ushirikiano wa mabalozi wa nchi wanachama wa umoja huo wenye uwakilishi Tanzania na kuungwa mkono na mwakilishi na mabalozi wa Norway, Canada na Uswisi.

“Tunashuhudia kwa wasiwasi mwendelezo wa matukio ya hivi karibuni yanayotishia nidhamu ya kidemokrasia na haki za Watanzania, katika nchi iliyojizolea umaarufu mkubwa duniani kwa utulivu, amani na uhuru.”

“Tumesikitishwa na kifo cha mwanafunzi aliyepigwa risasi mwisho wa juma lililopita Akwilina Akwilini, anayeombolezwa nchi nzima. Tunakaribisha wito wa Rais John Magufuli wa uchunguzi wa haraka,” inaeleza taarifa hiyo.

Katika taarifa hiyo EU imetoa wito wa uchunguzi wa kina kwa vifo vyote vya wanaharakati wa kisiasa na haki za binadamu.

“Tunatoa pole za dhati kwa familia zao zote. Tuna wasiwasi na ongezeko la ripoti za ukatili katika miezi ya hivi karibuni, kama vile, jaribio lililohatarisha maisha ya mbunge Tundu Lissu; kupotea kwa watu kama mwandishi wa habari Azory Gwanda na mashambulio yaliyopoteza uhai wa viongozi wa Serikali,” inaeleza EU.

Umoja huo umesema pia yametokea matukio yaliyowahusisha wawakilishi wa vyombo vya usalama na wananchi Mkoa wa Pwani ndani ya miaka miwili iliyopita.

“Tunaungana na Watanzania katika kuwaomba wahusika wote, kutunza amani na usalama wa michakato ya kidemokrasia, watu wake na kuheshimu utawala wa sheria bila udhalimu.”

Akwilina alipigwa risasi Februari 16,2018 eneo la Kinondoni Mkwajuni, wakati Polisi wakiwatawanya wafuasi wa Chadema waliokuwa wakielekea ofisi za msimamizi wa uchaguzi wa ubunge Jimbo la Kinondoni kudai viapo vya mawakala wao.

Lissu ambaye ni mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) na Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), alipigwa risasi Septemba 7,2017 nje ya makazi yake mjini Dodoma. Kwa sasa yupo nchini Ubelgiji akiendelea na matibabu.

Azory ni mwandishi wa habari wa kujitegemea wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), aliyetoweka tangu Novemba 21, 2017 Leo ametimiza siku 95 tangu alipopotea.

Kumbe Wema ndo Chanzocha Kuvunja Penzi la Diamond na Zari.... Zari Athibitisha Afunguka A-Z

0
0
Kumbe Wema cha Kuvunja Penzi la Diamond na Zari.... Zari Athibitisha Afunguka A-Z
Unazikumbuka picha za Wema Sepetu na Diamond Platnumz zilizosambaa wakiwa wamekumbatiana kwa mahaba wakati wa sherehe ya kumkaribisha Maromboso au ‘Mbosso’ iliyofanyika mwezi uliopita katika hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam?

Basi tukio lile ndio limesababisha Diamond kuweza kupigwa chini na mama watoto wake, Zari The Bosslady.

Akiongea katika kipindi cha runinga cha Dira ya Dunia ya BBC Swahili, Zari amesema, “Tulikuwa tunajaribu kuona we can move from hiyo sikendo ya kupata mtoto. So we can move forward lakini vitu kama hivyo leo unasikia hivi unaona vile sijui kukumbatiana huko na maex kwenye public vitu vya kunidhalilisha, kunifanya niwe very disrespect na watoto wangu unaona tu like it’s just not right.”

Prof Jay Awatupia Lawama Jeshi la Polisi

0
0
Prof Jay Awatupia Lawama Jeshi la Polisi
Mbunge wa Jimbo la Mikumi Joseph Haule 'Prof Jay' amefunguka na kusema kuwa leo Februari 24, 2018 kuna watu watatu ambao ni majeruhi wa kupigwa risasi lakini mpaka sasa hawajapatiwa matibabu na wanashikiliwa na jeshi la polisi.


Prof Jay amesema kuwa mwanachama mmoja wa CHADEMA ambaye amemtaja kwa jina la Aida Ulomi ameamua kugoma kula ili apatiwe haki yake ya msingi kwani hakufikishwa mahakamani kama ambavyo sheria zinataka iwe.

"Leo ni siku ya 9, Tangu Kamanda mwenzetu Aida Ulomi apigwe risasi ya mguu, polisi bado wanamshikilia kituo cha Oysterbay na wengine kadhaa bado wanashikiliwa kwenye vituo mbalimbali, hajapelekwa mahakamani, hana matibabu yeyote na amegoma kula, twendeni tukamwone na kumsaidia" alisema Prof Jay

Mbali na huyo pia Mbunge wa jimbo la Tarime vijijini John Heche amewataja watu wengine ambao nao walipigwa risasi Februari 16, 2018 wakati jeshi la polisi likiwatawanya wanachama wa CHADEMA ambao walikuwa wakiandamana kwenda kwa Mkurugenzi wa uchaguzi jimbo la Kinondoni kudai barua za utambulisho wa mawakala wao.

"Mpaka sasa ni watu watatu wanashikiliwa na jeshi la Polisi katika kituo cha osterbay Polisi. Wote ni majeruhi Wa risasi wanauguza vidonda na haki yao ya kupata matibabu imevunjwa. Hapo ni Aida Olomi...Kigamboni, Issack lomanus Ngaga....Kibaha, Erick John.... Kinondoni. Jana siku nzima wako kwenye vikao na bado wanatupiana mpira, kila ngazi inasubiria maelekezo kutoka juu. Ni uvunjifu Wa Sheria za nchi na taratibu za haki za binadamu" Alisema Heche

Zahir Zorro: Serikali Pekee Itafanikisha Kukamatwa Aliyesababisha Kifo cha Akwilina

0
0
Zahir Zorro: Serikali Pekee Itafanikisha Kukamatwa Aliyesababisha Kifo cha Akwilina
Muimbaji mkongwe wa muziki nchini, Zahir Ally Zorro amesema anaamini serikali itafanishwa kukamatwa kwa aliyesababisha kifo cha Mwanafunzi Akwelina Akwilini ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi katika maandamano.

Zahir Zorro ambaye ni baba mzazi wa wanamuziki Banana na Maunda Zorro, ametumia mtandao wa twitter kuipongeza serikali kwa kugharamikia mazishi ya Akwelina na kutoa rai hiyo.

“Ahsante kwa Serikali yetu Sikivu. Kusikia kilio cha wengi na kujitoa kumrudisha Akwilina Nyumbani, vifo hutokea kwa wakati na muda uliopangwa, japo sababu hutatanisha. Tunaamini Mkono Mrefu wa Serikali utafanikisha kukamatwa Muuwaji. Ni vyema akamatwe au Atauwa tena tu!,” amesema Zahir Zorro.

Marehemu Akwelina Akwilini ambaye alikuwa mwanafunzi wa Chuo cha NIT aliuawa kwa kupigwa risasi February 16 mwaka huu katika maandamano yaliyojumuisha wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). mwali wa Akwelina ulizikwa hapo jana katika kijiji cha Kitowo kata ya Marangu, Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro.

Lipumba Kukutana na Viongozi wa CUF Zanzibar

0
0

Lipumba Kukutana na Viongozi wa CUF Zanzibar
Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba leo Februari 24, 2018 ameanza ziara Zanzibar na atakutana na kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa chama hicho.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF- Bara upande unaomuunga mkono Profesa Lipumba, Magdalena Sakaya ameieleza  MCL-Digital leo Jumamosi Februari 24, 2018 kuwa:

 “Ziara inaweza kuwa ya siku moja au mbili, akimaliza atarejea Dar es Salaam.”

“Katika ziara hii Profesa Lipumba atakutana na viongozi wa CUF wa Pemba na Unguja kwa lengo la kuimarisha chama.”

Leo saa 4 asubuhi Lipumba alitarajiwa kufanya mkutano katika ukumbi wa Makonyo uliopo Chakechake, Mkoa wa Kusini Pemba.

Wakati Sakaya akieleza hayo, Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar upande unaomuunga mkono Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad, Nassor Ahmed Mazrui amesema hawatambui ziara hiyo kwa maelezo kuwa Profesa Lipumba si kiongozi wao.

“Chama kinawataka wanachama, viongozi na wapenzi wa CUF waliopo Pemba na Unguja kuwa watulivu na kuendelea na shughuli zao za maisha ya kawaida na kupuuza kabisa ujio huo wa Profesa Lipumba,” amesema Mazrui.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba, Shekhan Mohamed Shekhan amesema ana taarifa kamili ya ujio wa kiongozi huyo.

"Ni kweli tumepokea taarifa ya ujio wake na tutatoa ulinzi kwa maana anatambuliwa na vyombo husika kama kiongozi, ukizingatia zaidi mazingira walionayo kwenye chama chao,” amesema.



Polisi Yakiri Kuwashikilia Waliojeruhiwa Kwenye Maandamano ya Chadema

0
0
Polisi Yakiri Kuwashikilia Waliojeruhiwa Kwenye Maandamano ya Chadema
JESHI la Polisi kupitia Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Muliro Jumanne limethibitisha kuwashikilia watuhumiwa watatu wenye majeraha ya risasi katika Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Muliro amesema watuhumiwa hao ni wale waliokamatwa kwenye maandamano ya CHADEMA yaliyofanyika Februari 16 mwaka huu na kusababisha kifo cha mwanafunzi Akwilina Akwilini.

Aidha, kamanda huyo amekanusha taarifa ya kwamba majeruhi hayo hawajapatiwa matibabu tangu wakamatwe, amesema wote wamepelekwa katika hospitali za serikali hivyo hakuna asiyepatiwa matibabu kama inavyoelezwa.

Awali Mbunge wa Mikumi (CHADEMA), Joseph Haule aliandika kupitia Twitter na Facebook kuwa;

“Leo ni siku ya 9, Tangu Kamanda mwenzetu AIDA ULOMI apigwe risasi ya mguu, polisi bado wanamshikilia Kituo cha Oysterbay na wengine kadhaa bado wanashikiliwa kwenye vituo mbalimbali, Hajapelekwa mahakamani, hajapata matibabu yeyote na amegoma kula, twendeni tukamwone na kumsaidia…”

Wastara Umekuwa Mshumaaa Unamulikia Wenzio Wakati Nawe Unateketea- Florah Mvungi

0
0
Wastara Umekuwa Mshumaaa Unamulikia Wenzio Wakati Nawe Unateketea- Florah Mvungi
Muigizaji wa filamu za Bongo, Florah Mvungi amemfananisha Wastara sawa na mshumaa unaoteketea ukiwaangazia watu kutokana na yale anayopitia katika maisha yake.

Hivi karibuni Wastara alielekea nchini India kwa ajili ya kupata matibabu ya mguu uliokuwa ukimsumbua kwa kipindi kirefu, hivyo Florah ni kama ameamua kumitia moyo..

“Kitu kizuri ni kwamba wewe ni wa furaha siku zote, umekuwa msaada kwa wengi tuu huku ukionyesha furaha yako kwa yote uliyowafanyia pasipo kujua kumbe nawe ulikuwa na maumivu makali, umekuwa mshumaaa unamulikia wenzio wakati nawe unateketea,” ameandika Flora Instagram na kuendelea.

“Mungu akutie nguvu na akupe uponyaji wa milele ili uishi ukiyafurahia maisha Dada yangu, msaada wako naujua mimi na siwezi kusahau, nakupenda, upone inshaallah urudi salama,” amesisitiza.

January 26 mwaka huu Rais Dkt. John Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli walimchangia Wastara Tsh. Milioni 15 kwa ajili ya matibabu na February 4 ndipo aliondoka nchini kuelekea India.

Wolper Aingizwa Mjini kwa Mara Nyingine

0
0
Wolper Aingizwa Mjini kwa Mara Nyingine
Mrembo kutoka kiwanda cha filamu Bongo, Jacqueline Wolper ametoa kilio chake kwa makampuni ya simu za mikononi nchini.

Wolper ametoa kilio hicho kwa kitendo kinachofanywa na baadhi ya watu kusajili laini kwa kutumia jina lake( na majina mengine ambayo sio yao) na kufanya utapeli kwa watu.

Mrembo huyo amebaisha hayo kupitia matandao wa kijamii wa Instagram ambao kunaonyesha mtu anayetumia jina lake alipokea muamala wa pesa kitu ambacho yeye hajakipokea.

Zitto Kabwe Afunguka Kuhusu Unyanyasaji Wanaoupata Mahabusu Kutoka kwa Polisi Wakiwa Rumande

0
0
Zitto Kabwe Afunguka Kuhusu Unyanyasaji Wanaoupata Mahabusu Kutoka kwa Polisi Wakiwa Rumande
Mbunge wa jimbo la Kigoma Mjini , Mhe. Zitto Kabwe amefunguka na kudai kuwa jeshi la polisi nchini limekuwa likikiuka utaratibu na kuvunja sheria na kusema akiwa rumande amemshuhudia kijana ambaye amevunjwa mbavu kituoni na hajapelekwa kutibiwa.

Zitto Kabwe amesema hayo leo Februari 24, 2018 akiongea na waandishi wa habari na kusema kuwa kitendo cha yeye kukamatwa na kulazwa ndani kwa siku moja kumemfanya agundue kuwa kuna Watanzania wengi wanateseka na kupata shida kwenye vituo vya polisi nchini.

"Watanzania wanateseka sana chini ya mikono ya polisi, sheria inataka ndani ya masaa 48 polisi wame wamewafikisha mahakamani watuhumiwa lakini tumekutana na watu wamekaa ndani siku 3 hata maelezo tu hawajaandika, wengine wana siku 20 wapo ndani hawajafikishwa mahakamani" alisema Zitto Kabwe

Kiongozi huyo aliendelea kudai kuwa polisi wamekuwa wakiwatesa wananchi ndani ya vituo hivyo vya polisi na kusababisha majeraha kwa baadhi ya watuhumiwa bila kuwapeleka hospitali kwa matibabu.

"Tumekuta watu ambao wanateswa, kijana mmoja mpaka mbavu zimevunjika na zaidi ya siku saba hajapelekwa hospitali kwa matibabu, mpaka jana tunaondoka hajapelekwa hospitali, tulipozungumza na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro tulimweleza hilo, kuna watu ni wagonjwa hawajapelekwa hospitali akasema atashughulikia sasa sijui kama yeye alikuwa hajui hilo" alisema Zitto Kabwe

Mbali na hilo Zitto Kabwe amesema hali kiujumla ya nchi yetu kwa sasa ni tata kwa kuwa suala la mauaji yameendelea kutokea kinyume na mazoea yaliyokuwepo kipindi cha nyuma na kudai kuwa kuna kila sababu ya uchunguzi wa mauaji hayo kuanzia yale ya Kibiti mpaka haya ambayo yanaendelea sasa kuchunguzwa na vyombo huru na si jeshi la polisi kwa kuwa jeshi hilo nalo linatuhumiwa.


Chadema Yataka Kutibiwa kwa Wanachama Wenye Majeraha Walioshikiliwa na Polisi

0
0
Chadema Yataka Kutibiwa kwa Wanachama Wenye Majeraha Walioshikiliwa na Polisi
Wakati Chadema wakilalamikia wanachama wake watatu kushikiliwa na polisi katika kituo cha Oysterbay wakiwa na majeraha ya risasi bila kupatiwa matibabu, Polisi Mkoa wa Kinondoni imesema hakuna mahabusu mgonjwa anayeshikiliwa bila kutibiwa.

Leo Februari 24, 2018 Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano, Uenezi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema ameieleza MCL Digital kuwa wanachama hao walishambuliwa kwa risasi Februari 16, 2018.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Jumanne Murilo amesema polisi wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mahabusu wagonjwa wanatibiwa katika hospitali za Serikali bila malipo yoyote.

Katika ufafanuzi wake, Mrema amebainisha kuwa wanachama hao walishambuliwa kwa risasi wakati Polisi wakiwatawanya wanachama wa chama hicho waliokuwa wakielekea ofisi ya msimamizi wa uchaguzi wa ubunge Jimbo la Kinondoni kudai barua za viapo vya mawakala wao.

Amewataja kuwa ni Isaack Ngaga, Erick John na Aida Oromi.

“John na Ngaga wao walikamatwa wakiwa majumbani mwao baada ya kuruhusiwa kutoka Hospitali. Hawa hawakukamatiwa kwenye vurugu,” amesema Mrema.

 “Mmoja kati yao (John) alikamatwa na watu waliojifanya watumishi wa haki za binadamu na kudai kuwa wanataka kwenda kumhoji, alipokataa ndipo walitoa vitambulisho vyao vinavyoonyesha wao ni Polisi.”

Amesema hatua iliyochukuliwa hadi sasa ni kuwaelekeza wanasheria wa Chadema kufungua kesi Mahakama Kuu kumshtaki Mwanasheria Mkuu wa Serikali na polisi, kuwataka wawafikishe mahakamani wanachama hao.

“Tumemwelekeza mwanasheria wetu kufungua kesi ili wanachama wetu hao watatu wapelekwe mahakamani na kupatiwa matibabu,” amesema Mrema.

Amesema kuendelea kushikiliwa bila kupelekwa hospitali wakati wana majeraha ni hatari kwa maisha yao, kwa kuwa vidonda hivyo vinaoza.

“Wanakaa nao kinyume na sheria, mpaka sasa walipaswa wawe wameshawapeleka mahakamani,” amesema.

Kwa upande wake, Murilo amesema sheria ipo wazi inawaelekeza mahabusu wote wanapougua kutibiwa.

“Siyo hao mahabusu wa Chadema pekee, mahabusu yeyote anapougua hupelekwa hospitali za Serikali ambako hutibiwa bure kwa mujibu wa sheria,” amesema.

“Kama wanaolalamika wangekuwa mahabusu ningekuwa na cha kuzungumza, lakini kama wapo nje waache waendelee kusema, ninachojua hakuna mahabusu ambaye hajatibiwa.”

Mmoja wa ndugu wa Aida, Hilda Sigala amesema, “Jana nilikwenda kumtemebela ndugu yangu kituoni. Amenieleza kuwa mpaka sasa hajapelekwa hospitali na wanampaka dawa tu ya kukausha kidonda wakati ana jeraha la risasi. Yupo kituoni tangu Februari 16.”





Taharuki Yatanda Mbozi Baada ya Mbwa Ageuka Binadamu

0
0
Taharuki Yatanda Mbozi Mbwa Ageuka Binadamu
Wananchi wa kijiji cha Mpanda Kata ya Nyimbili  wilayani Mbozi mkoani Songwe wameshikwa na taharuki baada ya mbwa aliyewasumbua kwa siku nyingi kwa matukio ya uhalifu hasa kwa kukamata kuku kijijini hapo kugeuka na kuwa binadamu na kuanza kuongea.


 Afisa Mtendaji wa kijiji hicho amethibitisha tukio hilo kutokea na kuongeza kuwa wamekumbwa natahauki kubwa kuona kitu cha ajabu binadamu kujibadilisha kuwa mbwa na kuanza kufanya uhalifu kitu ambacho kimewashitua wengi. Inadaiwa mbwa huyo kwa siku alikuwa anakamata kuku kuanzia watatu mpaka wa tano.

Mmoja wa wamashuhuda wa tukio hilo alisimulia kuwa "Kuku walianza kupotea muda mrefu kwa hiyo tulichukua jukumu la kumtaarifa Afisa Mtendaji kwamba kuna mbwa amemaliza kuku za wananchi kwenye kitongoji cha Mpanda kati kwa hiyo baada ya hapo tumeamua kuamka na kuanza kufukuzana na huyo mbwa, tulianza kufukuzana naye kuanzia saa kumi na mbili na kufika saa nne ya asubuhi wakati tunakaribia kumkamata akabadilika na kutokea binadamu" alieleza mwananchi

Afisa Mtendaji aliendelea kusimulia juu ya tukio hilo na kusema baada ya mbwa yule kubadilika na kuwa binadamu alianza kuongea akiwaomba wananchi wamuue na kukiri kuwa yeye ni mchawi na alitumwa.

"Baada ya hapo alijitambulisha anaitwa Happy Victor akaomba tusimrudishe kwao Ilemi bali tumuue na kusema kuwa mtoto wake anatuachia tumle sisi tukasema hapana hatuwezi kukuuwa ila tunakuomba utupe maelezo huku Mbozi umekujaje akasema huku nimekuja kuna mtu amenileta ila mama yangu ni mshirikina alichomewa nyumba kule Ilemi kwa hiyo mimi ni yule mbwa ambaye alipotea kule Ilemi aliyekuwa anatuhumiwa kwamba anakichaa. Sisi tukamsihi kwamba wewe basi sisi tunakuomba hizo nguo vaa akasema nikivaa hizi nguo nitabadilika kuwa mbwa yule wa kichaa" alisema Afisa Mtendaji

Kwa upande wake Afisa Tarafa ya Vwawa Haji Hamisi Ibrahamu amewataka wananchi kuachana na mambo ya kishirikina ambapo amewataka wazee wa mila na wachungaji wakemee tukio hilo na kusema kuwa mtu huyo wao watamfikisha kwenye vyombo vya sheria kwa kufanya uhalifu.

Mapacha Walioungana Kwenda Afrika Kusini Kwaajiri ya Uchunguzi

0
0
Mapacha Walioungana Kwenda Afrika Kusini Kwaajiri ya Uchunguzi
Pacha walioungana Maria na Consolata Mwakikuti wamesema wakati wowote wataenda nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi zaidi juu ya afya zao.

Pacha hao wanaosoma Chuo Kikuu cha Katoliki cha Ruaha (Rucu), wanaendelea kupatiwa matibabu ya moyo kwenye  Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).

Maria na Consolata walifikishwa JKCI wakitokea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa, walikokuwa wamelazwa tangu Desemba 28, 2017.

Katika ujumbe wao walioutuma jana jioni Februari 23, 2018, pacha hao wamesema wanahitaji maombi zaidi wakati huu wanapotarajia kufanyiwa uchunguzi nchini Afrika Kusini.

“Jamani ni sisi Maria na Consolata tunaomba sala zenu maana tunatarajia kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya uchunguzi zaidi ila kwa sasa tuko Dar es Salaam.  Tarehe tutajuzana. Tunahitaji sala zenu,” waliandika.

Maria na Consolata hutumia simu moja katika mawasiliano.

Yanga Tayari Kuvaana na Majimaji FC

0
0
Yanga Tayari Kuvaana na Majimaji FC
Kikosi cha Yanga kimeondoka asubuhi ya leo kuelekea mkoani Ruvuma, wilaya ya Songea, kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Majimaji FC.

Yanga itakuwa mgeni katika mchezo mhuo utakaopigwa majira ya saa 10 jioni katika Uwanja wa Majimaji uliopo mjini Songea.

Ikumbukwe Yanga ilifuzu kuendelea na mashindano baada ya kuifunga Ihefu kwa jumla ya matuta 4-3 baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Katika mchezo wa kesho, timu itakayoshinda itaungana na Njombe Mji FC kwenye hatua ya 8 bora, ambayo ilifuzu baada ya kuitoa Mbao FC ya jijini Mwanza.

Video: Diamond Agawa Urithi Kwa wanae Baada ya Kuachana na Zari

0
0
Video: Diamond Agawa Urithi Kwa wanae Baada ya Kuachana na Zari

Msanii wa bongo fleva Diamond platnumz baada ya kuachana na mama watoto wake zari, kutokana na kuwa na skendo mbali mbali za kimapenzi na wasanii tofauti akiwemo Hamisa mobetto amezaa nae mtoto  mmoja na hivi karibuni kuonekana katika picha ya mahaba na wema sepetu ambae alikuwa na mahuziano na e zamani, hivyo Diamond ameamua kuwapa urithi watoto wake wawili Nillan na Dully.

Tazama video hapo chini

Mtoto wa Ray Apata Dili Nono NMB Ateuliwa Kuwa Ubalozi

0
0
Mtoto wa Ray Apata Dili Nono NMB Ateuliwa Kuwa Ubalozi
MTOTO wa Staa wa Filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’, aitwaye Jarden Kigosi, amepata shavu la Ubalozi wa Benki ya NMB, ambapo amemfungulia akaunti kwa ajili ya kuhakikisha wanamwekea fedha zitakazokuja kumsaidia baadaye kwenye masomo yake na maisha ya baadaye.

Akizungumza na Global Publishers wakati wa kumfungulia akaunti hiyo, Makao Makuu ya Benki ya NMB, Posta jijini Dar, Ray alisema kuwa, amefurahishwa na hatua ya benki hiyo kumtumia mwanaye kama mmoja wa mabalozi jambo ambalo hata yeye alikuwa akilitamani sana japo hakujua wapi angeweza kumfungulia akaunti kwa ajili ya maisha yake ya badaye.

“Niwaombe tu mastaa wenzangu kuwa, suala la mtoto kumfungulia akaunti benki ni ya muhimu sana kwani sisi wazazi tupo leo lakini hatujui kesho yetu itakuwaje?

“Ili usimnyime haki ya maisha mazuri mwanao hapo baadaye, basi ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha anamfungulia akaunti mwanaye ila hata asipokuwepo ataweza kusoma bila shida,” alisema Ray.

Ray aliambatana na mzazi mwenzake ambaye pia ni msaniiwa Bongo Movies, Chuchu Hans katika utambulisho wa mtoto wao Jarden kama Balozi wa NMB.

Rais Magufuli Arejea Nchini Baada ya Kumaliza Ziara yake Uganda

0
0
Rais Magufuli Arejea Nchini Baada ya Kumaliza Ziara yake Uganda
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amerejea nchini leo, Feb 14, akitokea nchini Uganda alipokuwa amekwenda kwa ajili ya mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Miujiza ya Sharifu Seif Mohamed..JE Umeachwa na Mme/Mke au Mpenzi, Umesongwa na Mitihani ya Maisha..Piga Simu Upate Muujiza Wako

0
0

SHARIFU SEIF MOHAMED ANAWASHUKURU WALE WOTE WANAOENDELEA KUPIGA SIMU, WENYE MATATIZO NA WALE WANAOTOA  SHUKRANI NA SHUHUDA JINSI TIBA ZAKE ZINAVYO WASAIDIA,

(Rudisha mahusiano yako ndani ya masaa 72 tu)

SHARIFU MOHAMED Ni  mtaalam na mnajimu maarufu wa nyota na kubashiri mambo yanayo watesa binadamu duniani kote na kupata ufumbuzi, Anatumia kitabu cha QUR'AN na Nyota

Je Umeachwa na UMPENDAE awe Mme/Mke na bado unampenda? Je Umekimbiwa na Mmeo/ Mkeo n anaishi na mtu mwingine? Je Umejaribu sehemu nyingi bila mafanikio? Mpigie simu SHARIFU SEIF sasa hivi ujionee Muujiza wa Papo kwa Papo, Anauwezo wa hali ya juu wa kusambaratisha mahusiano yao na kumrejesha kwako haraka sana na Kumfanya Atimize Ahadi zote Ndani ya Muda Mfupi Endapo Utafwata Atakacho Kuelekeza

 ZINDIKO LA NYUMBA NA BIASHARA, PETE ZA BAHATI, HUMALIZA KABISA TATIZO   HUZUIA CHUMA ULETE KWENYE BIASHARA, HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA, NA KUPONYA MAGONJWA SUGU ANAO UWEZO WA KUMRUDISHA ALIE MBALI AU ALIECHUKULIWA MSUKULE, KUPANDISHA NYOTA NA KUSHINDA BAHATI NA SIBU, KASAFISHA NYOTA NA KUKUPA MVUTO WA AJABU, KUTOA NUKSI NA VIFUNGO MBALIMBALI,  MAFANIKIO YA MAISHA NA UTAJIRI BILA MASHARI, NA MENGINE MENGI YA SIRI,

JE UMAHANGAIKA KUPATA MTOTO BILA MAFANIKIO? WASILIANA NA MTAALAMU HUYU KWANI YEYE HUFAULU PALE WOTE WALIPOSHINDWA, PIA UMALIZA KAZI ZILIZO SHINDIKANA NA WATAALAM WENGINE NDANI YA MASAA 24 TU,

(NA ANATIBU KWA NJIA YA SIMU UKIWA NCHI YOYOTE AU MKOA WOWOTE ENDAPO UTAFWATA MAELEKEZO YAKE)

Kwa ushauri na mawasiliano  zaidi Piga SIMU No:

Mobile +255 654-836970
WhatsApp 0622766715

RPC Kinondoni azungumzia majeruhi wa risasi waliopo Oyestrebay Polisi

0
0

JESHI la Polisi kupitia Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Muliro Jumanne limethibitisha kuwashikilia watuhumiwa watatu wenye majeraha ya risasi katika Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Muliro amesema watuhumiwa hao ni wale waliokamatwa kwenye maandamano ya CHADEMA yaliyofanyika Februari 16 mwaka huu na kusababisha kifo cha mwanafunzi Akwilina Akwilini.

Aidha, kamanda huyo amekanusha taarifa ya kwamba majeruhi hayo hawajapatiwa matibabu tangu wakamatwe, amesema wote wamepelekwa katika hospitali za serikali hivyo hakuna asiyepatiwa matibabu kama inavyoelezwa.

Awali Mbunge wa Mikumi (CHADEMA), Joseph Haule aliandika kupitia Twitter na Facebook kuwa;

“Leo ni siku ya 9, Tangu Kamanda mwenzetu AIDA ULOMI apigwe risasi ya mguu, polisi bado wanamshikilia Kituo cha Oysterbay na wengine kadhaa bado wanashikiliwa kwenye vituo mbalimbali, Hajapelekwa mahakamani, hajapata matibabu yeyote na amegoma kula, twendeni tukamwone na kumsaidia…”
Viewing all 104414 articles
Browse latest View live




Latest Images