Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104694 articles
Browse latest View live

Marekani Yaiwekea Korea Kaskazini Vikwazo Vizito

$
0
0
Marekani Yaiwekea Korea Kaskazini Vikwazo Vizito
Waziri wa fedha nchini Marekani ameyaonya mataifa yanayoshirikiana kibiashara na Korea Kaskazini kwamba yanafanya hivyo yakijihatarisha yenyewe.

Akitangaza vikwazo vipya Steve Mnuchin amesema kuwa kampuni yoyote iliosaidia kufadhili mpango wa kinyuklia wa Pyeonyang itapoteza haki ya kufanya biashara na Marekani.

Pia aliambia maripota kwamba Marekani sasa huenda ikaanza kupanda na kuchunguza meli zinazo safirisha mizigo Korea Kaskazini.

Vikwazo hivyo vinalenga mabenki na kampuni zinazomiliki meli ambazo Marekani inasema zinafanya biashara na Korea Kaskazini.

Rais Trump alivitaa vikwazo hivyo vizito zaidi, lakini waandishi wanasema kuwa vikwazo kama hhivyo vilivyowekwa hapo awali vililenga mitandao ya kibiashara ya Korea Kaskziniu.

Vikwazo hivyo vinalenga zaidi ya meli 50, kampuni za uchukuzi nchini Korea Kaskazini lakini pia China na Taiwan.

Korea Kaskazini inakabiliwa na vikwazo vya kimataifa pamoja na vile vya Marekani kuhusu mpango wake wa Kinyuklia.

Lakini taifa hilo liliendeleza majaribio ya makombora yake mwaka uliopita ikiwemo majaribio ya silaha za kinyuklia mbali na kombora la masafa marefu linaloweza kufika Marekani.

Marekani inasema kuwa vikwazo hivyo vipya vinalenga kuifinya zaidi Korea Kaskazini ,kupitia kukata vyanzo vyake vya fedha na mafuta ili kutoendeleza mpango wake wa Kinyuklia.

Idara ya fedha nchini Marekani imeorodhesha kampuni 16 hususan za meli zilizopo nchini Korea Kaskazini , lakini tano zimesajiliwa Hong Kong, mbili nchini China mbili Taiwan moja Panama na nyengine moja Singapore.

Meli 28 zimeorodheshwa katika orodha hiyo nyingi zikitoka Korea Kaskazini lakini mbili zina bendera ya Panama moja kutoka Comoros na moja ilio na bendera ya Tanzania.

Akizungumza katika mkutano na vyombo vya habari siku ya Ijumaa, Trump alionya dhidi ya hatua kali iwapo vikwazo hivyo havitazaa matunda.

''Iwapo vikwazo hivyo havitafanya kazi tutaingia katika awamu ya pili na awamu ya pili kitakuwa kitu kibaya pengine kibaya sana kwa ulimwengu''.

''Ni taifa taifa lisiloaminika na lisilofuata kanuni, iwapo tutakubaliana itakuwa kitu kizuri na iwapo haitawezekana , kitu kitafanyika''.

Hatahivyo hakuelezewa zaidi ni hatua ghani zitakazochukuliwa katika awamu ya pili.

Marekani imekuwa ikiuwekea utawala wa taifa hilo vikwazo tangu 2008 na vikwaza hivi vipya vinaweza kufuata vikwazo vyengine vilivyowekwa mwezi Novemba vilivyolenga meli za Korea Kaskazini pamoja na kampuni za China zinazofanya biashara na Pyongyang.

Umoja wa mataifa ulifuata nyayo hizo baada ya kuwekewa vikwazo vyengine vilivyoungwa mkono na mataifa 15 wanachama wa baraza la usalama la umoja ikiwemo hatua za kukatiza uagizaji wa mafuta kuingia Korea Kaskazini kwa silimia 90.

Waziri Ataka Mgodi Kuwalipa Fidia Wananchi

$
0
0
Waziri Ataka Mgodi Kuwalipa Fidia Wananchi
Serikali imetoa siku mbili kwa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kukamilisha mchakato wa ulipaji fidia wa nyumba zaidi ya 80 za wananchi zilizopata nyufa kutokana na milipuko ya shughuli za ulipuaji miamba.

Wananchi wa Nyamalembo wanaoishi karibu na mgodi huo wamekuwa na malalamiko ya zaidi ya miaka mitano wakilalamikia nyumba zao kupata nyufa zinazosababishwa na milipuko, huku Serikali kupitia Wizara ya Madini ikiagiza mara kwa mara mgodi kulipa fidia bila utekelezaji.

Akizungumza jana Februari 23,2018 na wananchi wa Nyamalembo na Katoma wanaozunguka mgodi wa GGM ambao wamekuwa na malalamiko ya miaka mingi, Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amesema madai ya wananchi sasa yamefika mwisho.

Amesema migogoro mingi katika sekta ya madini inawezekana inasababishwa na upungufu wa sheria za madini na kusema pamoja na sheria na kanuni mpya kutungwa, bado zipo sheria zinasababisha matatizo kwa wananchi.

“Kama sheria inaonekana ni kikwazo au inasababisha matatizo kwa jamii hatutaona tabu kurudi nyuma na kuirudisha bungeni kufanyiwa marekebisho,” amesema.

“Nia yetu sio kumkandamiza mwananchi, bali ni kutaka

mwananchi aone maendeleo ya kuwa na mwekezaji katika maeneo yenu na hatuoni sababu ya mwekezaji kuwa kero kwa wananchi.”

Amesema kama zipo sheria na kanuni zinazombana mwekezaji kutoa haki kwa mwananchi, Serikali ipo tayari kuzirekebisha na kuwataka wawekezaji kutotumia udhaifu wa kisheria kumkandamiza mwananchi.

Katika hatua nyingine, Nyongo ameutaka mgodi huo kuwalipa fidia wananchi wa Mtaa wa Katoma wanaoishi ndani ya leseni za mgodi, na kama hawapo tayari kuwalipa wawaachwe waendeleze shughuli zao na kuitaka halmashauri kuwapa wananchi hati za ardhi ili waweze kupatiwa huduma ya maji na umeme.

Makamu wa Rais wa Anglo Gold Ashanti, Simon Shayo amesema masuala mengi yanayolalamikiwa yapo kisheria na kuomba yatizamwe kwa mujibu wa sheria ili haki itendeke kwa pande zote mbili.

Lipumba Amwashia Moto Maalim Seif

$
0
0
Lipumba Amwashia Moto Maalim Seif
Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba amesema chama hicho hakina nguvu kama awali kutokana na kutoshiriki uchaguzi wa marudio Zanzibar.

Akizungumza leo Februari 24, 2018 katika mkutano wa ndani na wananchama wa CUF kwenye ukumbi wa Makonyo Chake Chake Pemba, Profesa Lipumba amesema uamuzi huo wa kutoshiriki uchaguzi uliobarikiwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad ndio tatizo la CUF kutokuwa na nguvu.

Amesema chama hicho kimekosa nguvu kwa kuwa hakimo tena katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) Zanzibar.

Wakati Lipumba akieleza hayo, Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar upande unaomuunga mkono Maalim Seif, Nassor Ahmed Mazrui amesema hawatambui ziara hiyo kwa maelezo kuwa Profesa Lipumba si kiongozi wao.

“Chama kinawataka wanachama, viongozi na wapenzi wa CUF waliopo Pemba na Unguja kuwa watulivu na kuendelea na shughuli zao za maisha ya kawaida na kupuuza kabisa ujio huo wa Profesa Lipumba,” amesema Mazrui.

Katika maelezo yake Profesa Lipumba amesema  Serikali ya Umoja wa Kitaifa ilikuwa ni fursa kubwa kwa CUF katika kupiga hatua za maendeleo kwa jamii na Taifa, kwamba kutokuwemo ni sawa na kuwakosesha haki wananchi wanaokiunga mkono chama hicho.

“Wawakilishi wangapi tumekosa kwa kugomea uchaguzi hili nataka lieleweke kuwa mtu akifanya jambo lazima aangalie maslahi ya mbali badala ya kuangalia maslahi ya karibu,” amesema.

Amesema kutokana na CUF kutokuwemo katika SUK, chama tawala kinaweza kubadili hata Katiba kwa urahisi.

Januari 28, 2016 Baraza Kuu la Uongozi la CUF lilitangaza kutoshiriki uchaguzi wa marudio visiwani Zanzibar uliotangazwa na Tume ya Uchaguzi (ZEC), likitoa hoja 12 zilizosababisha kufikia uamuzi huo.

Uchaguzi huo wa marudio wa rais wa Zanzibar, wawakilishi na madiwani ulifanyika Machi 20, 2016.

Uamuzi wa CUF kutangaza kutoshiriki uchaguzi huo ulitokana na mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha kufuta matokeo ya uchaguzi wa rais, wawakilishi na madiwani uliofanyika Oktoba 25, 2015 kwa maelezo kuwa sheria na kanuni zilikiukwa na baadaye kutangaza Machi 20, 2016 kuwa siku ya kupiga kura upya.

Tanzia: Hakimu Afariki Dunia Ghafla

$
0
0
Tanzia: Hakimu Afariki Dunia Ghafla
Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Juma Hassan Kasailo amefariki dunia ghafla jana jioni Februari 23, 2018.

Taarifa za kifo cha hakimu huyo zimethibitishwa na Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Ilvin Mugeta.

"Mimi niko safarini, lakini ninazo taarifa hizo kuwa Hakimu Kasailo amefariki dunia,” amesema Mugeta leo Jumamosi Februari 24 alipozungumza na MCL Digital.

Kasailo atazikwa kesho Jumapili Februari 25, saa 7:30 mchana Segera kwa Msisi, wilayani Korogwe mkoani Tanga. Mwili wa marehemu unaagwa leo mchana nyumbani kwake, Chanika Buyuni jijini Dar es Salaam.

Mwanamke Atumia Mbegu za Kiume za Mwanawe Aliyefariki Kupata Wajukuu

$
0
0
Mwanamke Atumia Mbegu za Kiume za Mwanawe Aliyefariki Kupata Wajukuu
Miaka miwili ilioipita, Rajashree Patil alipoteza mwanawe wa miaka 27 aliyefariki kutokana na saratani ya ubongo.

Huku akipata changamoto za kuweza kuishi bila mwanawe Rajashree alitumia shahawa ya mwanawe ambaye alikuwa hajaoa yaliohifadhiwa ili kupachika mimba mwanamke mwengine aliyeikuza.

Hatua hiyo ilifanikiwa na mama aliyepaichikwa mimba hiyo akajifungua pacha. Rajshree amemtaja mmoja wa pacha hao jina la mwanawe.

Hiki ni kisa kisichokuwa cha kawaida cha mwalimu mwenye umri wa miaka 49 kutoka India ambaye alikabiliana na changamoto za kila aina ili kutomsahau mwanawe aliyefariki akiwa na umri wa miaka 27 kutokana na saratani.

Akisaidiwa na mama aliyekubali kupachikwa mimba hiyo kwa lengo la kulipwa mwanamke huyo alifanikiwa kupata watoto wawili mmoja akiwa mvulana na mwengine msichana.

Anasema kuwa ni njia mojawapo ya kuhakikisha kuwa mwanawe anaishi. Baada ya kufuzu kutoka chuo cha uhandisi cha Sinhgad mjini Pune, Mwanawe Rajshree Prathamesh alielekea mjini Ujerumani 2010 kusomea shahada.

Prathamesh alipatikana na uvimbe katika uboingo wake 2013 na kufariki miaka mitatu baadaye.
Mwaka 2013, alipatikana na uvimbe wa ubongo na kufariki 2016 lakini mbegu zake za kiume zilihifadhiwa na baadaye kutumika kumpachika mama wa mimba za biashara aliyejifungua pacha hao.

''Nimempata mwanangu Pramesh'', mamake Rajashree Patil aliambia BBC.

''Nilimpenda sana mwanangu, alikuwa mwerevu sana shuleni na alikuwa akisomea shahada katika uhandisi nchini UJerumani alipopatikana na uvimbe huo ikiwa ni awamu ya nne ya saratanii katika ubongo.

Madaktari walikuwa wamemwambia Pramesh kuhifadhi shahawa yake kabla ya kuanza matibabu ya kutumia kemikali na miale, alisema.

Prathamesh ambaye alikuwa hajaoa alikuwa amemchagua mamake na dadake Dnyanashree kutumia shahawa hiyo baada ya kifo chake.

Wakati huo bi Rajshree hakubaini kwamba hiyo itakuwa njia ya kumpata mwanawe.

Shahawa hiyo iliohifadhiwa ilichanganywa na yai ambalo halijaulikani mwenyewe na kupachikwa kwa kizazi cha mwanamke anayefanya biashara ya kukuza mimba.

Baada ya mwanawe mwenye umri wa miaka 27 kufariki kutokana na saratani ya ubongo miaka miwili iliopita, Rajshree alikataa kuomboleza na badala yake alitumia shahawa hiyo ya mwanawe kupata wajukuu hao.

Pacha hao walizaliwa februari 12 na Rajshree aliwapatia majina ya Prathamesh baada ya jia la mwanawe na Preesha (zawadi ya mungu).

Dr Supriya Puranik, ni mtaalam wa mfumo wa IVF katika hospitali ya Sahyadri
Huku akisukumwa na lengo la kumpata mwanawe Dr Supriya Puranik, ambaye ni mtaalamu wa IVF katika hopsitali ya Sahyadri alisema mbinu ya IVF ilikuwa kitu cha kawaida lakina kisa hiki kilikuwa cha kipekee kwa kuwa mama aliyekuwa na huzuni alitaka kumpata mwanawe kwa gharama yoyote ile.

Waziri Afichua Siri ya Watu Kuchacha..Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya February 25

$
0
0
 

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya February 25

VIDEO: Zari Atoboa Siri Rasmi Kuachana na Diamond, Amwanika Vibaya “Kukumbatiana na ma X Kwenye Public”

$
0
0
Kwa mara ya kwanza Zari the Bossy Lady ambaye ni mama watoto wa msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Diamond Platinumz amefunguka kuhusu sababu za kuachana na C.E.O huyo wa kundi la Wasafi Classic Baby (WCB), amesema Diamond hakutegemea alichokipost kwani siku kabla ya kuachana walikuwa wamechuniana kwa takribani muda wa wiki tatu mfululizo, huku akiwa ameifungia simu yake, ”Block”.

Zari akiwa nchini Uingereza amepata nafasi ya kuzungumza na BBC  Swahili na kufunguka kila kitu kuhusu ishu nzima mpaka kufikia maamuzi hayo ya kutangaza kwenye akaunti yake ya instagram kuachana na Diamond katika siku ya wapendanao.

‘’Kwanza I didn’t think ali expect my post he didn’t see it coming ,nimekaa sana mda mrefu nikajifikiria vitu vingi nikasema unajua ni nini I need to post this, I  need to end this..tulikuwa tuna jaribu ku move forward kuhusu hiyo skendo eti amepata mtoto, lakini leo unasikia hivi unaona vile eti kukumbatiana na ma x kwenye public ni vitu vya kunidharirisha vitu vya kunifanya niwe very disrespected na watoto wangu’’, amesema Zari.

Zari amesema saivi hata akitembea kwa miguu kwenda kumuomba msamaha hawezi kumsamehe kwa sababu Imani juu yake imekwisha, na amesema kwa sasa hahitaji kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine.

Ameongezea kuwa wale wanao dhani ni kiki hawajaachana Zari amesema ni kweli wameachana na tangu kusambaa picha za Diamoni akikumbatiana na  EX wake ambaye ni Madam  Wema Sepetu, Zari amesema alimzimia simu na hawakuweza kuongea kwa wiki tatu na kisha akaamua kuchukua uamuzi wa kuachana nae.

Zari pia amezungumzia mipango yake ya hivi sasa ambapo amesema atakuwa anafanya vitu vingi ikiwemo kuendesha biashara na kazi zake ambazo amekuwa akifanya ikiwemo kusimamia shule yake iliyopo Afrika Kusini, kufanya matangazo na hivi karibuni anakuja na kipindi chake sehemu ya pili ya show yake ijulikanayo kama reality show.

Tazama Video hapa chini:

PICHA: Msanii AY Awafunga Ndoa na Mchumba Wake wa Siku Nyingi

$
0
0

MSANII wa Bongo Fleva, Ambwene Yessayah ‘AY ‘ amefunga ndoa na mchumba wake wa siku nyingi, Remy jana katika ufukwe wa bahari ya Hindi jijini Dar es Salaam.

Ambwene Yessayah ‘AY ‘ (katikati) akiwa na mkewe (wa pili kushoto) kabla ya kufunga ndoa leo katika  ufukwe wa bahari ya Hindi.


Mtoto wa Mwigizaji Ray na Chuchu Hans Apata Ubalozi wa NMB

$
0
0
MTOTO wa Staa wa Filamu Bongo, Vicent Kigosi ‘Ray’, aitwaye Jaden Kigosi, amepata shavu kutoka kwa wazazi wake baada ya kumfungulia  akaunti ya ‘NMB Mtoto Akaunti’ kwa ajili ya akiba itakayoweza kumsaidia hapo baadaye.

Akizungumza na waandishi wa habari  wakati wa kumfungulia akaunti hiyo, Makao Makuu ya Benki ya NMB, Posta jijini Dar, Ray alisema kuwa, huo ni uamuzi aliouchukua yeye na mwenzi wake  Bi Hans baada ya kuridhishwa na huduma za Benki ya hiyo. Pia kutokana na kushawishika na umahiri wa umahususi wa akaunti hizi za mpango wa NMB Mtoto Akaunti.

 “Niwaombe tu mastaa wenzangu kuwa, suala la mtoto kumfungulia akaunti benki ni muhimu sana kwani sisi wazazi tupo leo lakini hatujui kesho yetu itakuwaje?

“Ili usimnyime haki ya maisha mazuri mwanao hapo baadaye, basi ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha anamfungulia akaunti mwanaye ila hata asipokuwepo ataweza kusoma bila shida,” alisema Ray.



Ray aliambatana na mzazi mwenzake ambaye pia ni msaniiwa Bongo Movies, Chuchu Hans katika kumfungulia mtoto wao NMB Mtoto Akaunti.

Kwa upande wake Meneja Huduma za Kibenki  NMB, Caroline Mosha, ametoa wito kwa walezi na wazazi kuwa na utamaduni wa kuwafungulia akaunti watoto na vijana wao bila kusahau kuwahimiza kuhusu elimu ya fedha#NMBWajibu. www.nmbbank.co.tz/wajibu

Musa Mateja

SOMA Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Jumapili

Miujiza ya Sharifu Seif Mohamed..JE Umeachwa na Mme/Mke au Mpenzi, Umesongwa na Mitihani ya Maisha..Piga Simu Upate Muujiza Wako

$
0
0
SHARIFU SEIF MOHAMED ANAWASHUKURU WALE WOTE WANAOENDELEA KUPIGA SIMU, WENYE MATATIZO NA WALE WANAOTOA  SHUKRANI NA SHUHUDA JINSI TIBA ZAKE ZINAVYO WASAIDIA,

(Rudisha mahusiano yako ndani ya masaa 72 tu)

SHARIFU MOHAMED Ni  mtaalam na mnajimu maarufu wa nyota na kubashiri mambo yanayo watesa binadamu duniani kote na kupata ufumbuzi, Anatumia kitabu cha QUR'AN na Nyota

Je Umeachwa na UMPENDAE awe Mme/Mke na bado unampenda? Je Umekimbiwa na Mmeo/ Mkeo n anaishi na mtu mwingine? Je Umejaribu sehemu nyingi bila mafanikio? Mpigie simu SHARIFU SEIF sasa hivi ujionee Muujiza wa Papo kwa Papo, Anauwezo wa hali ya juu wa kusambaratisha mahusiano yao na kumrejesha kwako haraka sana na Kumfanya Atimize Ahadi zote Ndani ya Muda Mfupi Endapo Utafwata Atakacho Kuelekeza

 ZINDIKO LA NYUMBA NA BIASHARA, PETE ZA BAHATI, HUMALIZA KABISA TATIZO   HUZUIA CHUMA ULETE KWENYE BIASHARA, HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA, NA KUPONYA MAGONJWA SUGU ANAO UWEZO WA KUMRUDISHA ALIE MBALI AU ALIECHUKULIWA MSUKULE, KUPANDISHA NYOTA NA KUSHINDA BAHATI NA SIBU, KASAFISHA NYOTA NA KUKUPA MVUTO WA AJABU, KUTOA NUKSI NA VIFUNGO MBALIMBALI,  MAFANIKIO YA MAISHA NA UTAJIRI BILA MASHARI, NA MENGINE MENGI YA SIRI,

JE UMAHANGAIKA KUPATA MTOTO BILA MAFANIKIO? WASILIANA NA MTAALAMU HUYU KWANI YEYE HUFAULU PALE WOTE WALIPOSHINDWA, PIA UMALIZA KAZI ZILIZO SHINDIKANA NA WATAALAM WENGINE NDANI YA MASAA 24 TU,

(NA ANATIBU KWA NJIA YA SIMU UKIWA NCHI YOYOTE AU MKOA WOWOTE ENDAPO UTAFWATA MAELEKEZO YAKE)

Kwa ushauri na mawasiliano  zaidi Piga SIMU No:

Mobile +255 654-836970
WhatsApp 0622766715

Zitto ataka Uitishwe mkutano wa Kitaifa wa maridhiano

$
0
0
Arusha. Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ametaka uitishwe mkutano wa kitaifa wa maridhiano ili kujadili hali ya kisiasa na usalama nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Jana Jumamosi, Februari 24, 2018 jijini Arusha, Zitto amesema katika mkutano huo zijadiliwe changamoto zote za kisiasa na kukubaliana kanuni za demokrasia ya vyama vingi.

"Hii ni kutokana na dhahiri kuwa mfumo wa vyama vingi nchini upo hatarini zaidi kuliko wakati wowote,” amesema.

Amesema mkutano huo unatakiwa kuwashirikisha pia viongozi wa vyama vya wafanyakazi, wafanyabiashara, wakulima na wafugaji.

Amebainisha kuwa hali ya kisiasa sasa si ya kuwaachia wanasiasa pekee kwa kuwa pia inahusu uhai wa watu na wengine ambao hata hawajihusishi na siasa.

Zitto yupo mkoani hapa kutembelea kata ambazo zina madiwani wa chama hicho na kuzungumza na wajumbe wa kamati za maendeleo za kata hizo.

Mwanza: Rais Magufuli Azuia kaya 1,900 Kuondolewa Uwanja wa ndege

$
0
0
Asema wananchi hao ni wapigakura wake, ataka wasiondolewe mpaka watakapolipwa madai yao.

Mwanza. Rais John Magufuli amezuia kuondolewa kaya zaidi 1,900 zinazoishi katika nyumba zilizopo karibu na Uwanja wa Ndege wa Mwanza hadi itakapofanyika tathmini kwa sababu wananchi hao ni wapigakura wake.

Kiongozi mkuu huyo wa nchi ametoa kauli hiyo leo Februari 24, 2018 baada ya kusikiliza changamoto zinazowakabili wafanyakazi wa uwanja

huo ambao walimweleza kuwa uwepo wa kaya hizo unakwamisha ujenzi wa uwanja huo.

Akijibu jambo hilo, Rais Magufuli amesema wasiondolewe hadi pale watakapolipwa madai yao huku pia akiwataka wananchi hao kutoendeleza makazi yao.

"Hawa watu ndio walionipa kura, pamoja na hivyo msiwaondoe hadi pale mtakapokamilisha kuwalipa madai yao," amesema Rais Magufuli.

Oktoba mwaka jana, Rais Magufuli aliagiza kusitishwa kwa ubomoaji wa nyumba za wananchi zaidi ya 2,000 wanaodaiwa kuvamia eneo la uwanja huo, kituo cha polisi na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Siku hiyo wakati akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa daraja la juu la waenda kwa miguu eneo la Furahisha jijini Mwanza, Rais Magufuli aliagiza ubomoaji huo usitishwe hadi atakapotolea uamuzi suala hilo.

Leo mjini Mwanza, Meneja wa uwanja huo, Ester Mandale alimweleza Rais Magufuli kuwa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya ukosefu wa jengo la wasafiri, uwanja kukosa uzio pamoja na ndege kuzuiwa kubeba samaki.

Amesema baada ya ndege kuzuiwa kusafirisha samaki kwenda nchi za nje, wanalazimika kusafirisha kwa kutumia magari wakati wenzao wa Kenya wanatumia ndege, hivyo kuikosesha Serikali mapato.

Akizungumzia changamoto hiyo, Rais Magufuli alimwagiza meneja huyo kufanya tathmini inayohitajika katika ujenzi wa jengo la usafiri pamoja na uzio kisha aiwasilishe kwa ajili ya kuanza ujenzi huo.

Kuhusu usafirishaji wa samaki, Rais Magufuli aliagiza kufanya uchunguzi kwa wenzao wa Kenya kujua wanasafirishia kwa gharama kiasi gani.

Rais ameondoka jijini Mwanza na anaelekea Chato kwa ajili ya mapumziko.

Chanzo: Mwananchi

Chadema Yataka Wanachama wao Wenye Majeraha Kutibiwa

$
0
0

Siku 10 baada ya wanachama wa Chadema kukamatwa na polisi eneo la Mkwajuni wilayani Kinondoni jijini hapa, chama hicho kimelalamika baadhi yao kuendelea kushikiliwa na polisi katika kituo cha Oysterbay wakiwa na majeraha ya risasi bila kupatiwa matibabu, wala kufikishwa mahakamani.

Wakati chama hicho kikuu cha upinzani nchini kikieleza hayo, Polisi Mkoa wa Kinondoni wamesema hakuna mahabusu mgonjwa anayeshikiliwa bila kutibiwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Jumanne Murilo alimweleza mwandishi wetu jana kwamba, polisi wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mahabusu wagonjwa wanatibiwa katika hospitali za Serikali bila malipo yoyote.

Akizungumza na Mwananchi, Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano, Uenezi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema alisema wanachama wao watatu walishambuliwa kwa risasi Februari 16.

Mrema alibainisha kuwa wanachama hao walishambuliwa kwa risasi wakati polisi wakiwatawanya wafuasi wa Chadema waliokuwa wakielekea ofisi ya msimamizi wa uchaguzi wa ubunge Jimbo la Kinondoni kudai barua za viapo vya mawakala wao.

Aliwataja wanachama hao kuwa ni Isaack Ngaga, Erick John na Aida Oromi. “John na Ngaga wao walikamatwa wakiwa majumbani mwao baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali. Hawa hawakukamatiwa kwenye vurugu,” alisema Mrema. “Mmoja kati yao (John) alikamatwa na watu waliojifanya watumishi wa haki za binadamu na kudai wanataka kwenda kumhoji, alipokataa ndipo walitoa vitambulisho vyao vinavyoonyesha wao ni Polisi.”

Alisema hatua iliyochukuliwa hadi sasa ni kuwaelekeza wanasheria wa Chadema kufungua kesi Mahakama Kuu kumshtaki Mwanasheria Mkuu wa Serikali na polisi, kuwataka wawafikishe mahakamani wanachama hao. “Tumemwelekeza mwanasheria wetu kufungua kesi ili wanachama wetu hao watatu wapelekwe mahakamani na kupatiwa matibabu,” alisema Mrema.

Alisema kuendelea kushikiliwa bila kupelekwa hospitali wakati wana majeraha ni hatari kwa maisha yao, kwa kuwa vidonda hivyo vitaoza.

“Wanakaa nao kinyume na sheria, mpaka sasa walipaswa wawe wameshawapeleka mahakamani,” alisema.

Kwa upande wake, Murilo alisema sheria ipo wazi inawaelekeza mahabusu wote wanapougua kutibiwa.

“Si hao mahabusu wa Chadema pekee, mahabusu yeyote anapougua hupelekwa hospitali za Serikali ambako hutibiwa bure kwa mujibu wa sheria,” alisema.

“Kama wanaolalamika wangekuwa mahabusu ningekuwa na cha kuzungumza, lakini kama wapo nje waache waendelee kusema, ninachojua hakuna mahabusu ambaye hajatibiwa.”

Mmoja wa ndugu wa Aida, Hilda Sigala alisema, “Jana (juzi) nilikwenda kumtembela ndugu yangu kituoni. Amenieleza kuwa mpaka sasa hajapelekwa hospitali na wanampaka dawa tu ya kukausha kidonda wakati ana jeraha la risasi. Yupo kituoni tangu Februari 16.”

Alisema hali hiyo si sahihi kwa sababu kidonda alichonacho Aida kinazidi kuwa kikubwa jambo ambalo ni hatari kwa afya yake.

 

Serikali Yawaonya Wanaotumia majahazi Kubeba Abiria

$
0
0
WIZARA ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar, imesema serikali haijaruhusu majahazi kubeba abiria kutokana na usalama mdogo na ukosefu wa vifaa vya uokozi vya mawasiliano.

Naibu Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na usafirishaji, Mohamed Ahmada, aliyasema hayo wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Chake Chake, Suleiman Sarhani, aliyetaka kujua tatizo la usafiri Pemba linatatuliwa vipi.

Ahmada alisema kwa mujibu wa Sheria za usafiri baharini zinazoratibiwa na Mamlaka ya Usafiri Majini (ZMO), vyombo vilivyotengenezwa kwa kutumia mbao ikiwamo majahazi ni marufuku kubeba abiria.

''Mheshimiwa Naibu Spika nataka kutoa taarifa kwamba serikali bado haijaruhusu majahazi kubeba abiria kutokana na usalama mdogo na ukosefu wa vyombo vya kisasa vya uokozi,''alisema.

Alisema majahazi mengi hadi sasa hayana vifaa vya kisasa vya mawasiliano ya redio pamoja na vifaa vya uokozi wakati yanapotokea majanga ya ajali baharini.

Alisema serikali inafahamu licha ya kupiga marufuku majahazi kuacha kubeba abiria, lakini wapo manahodha wanaokaidi agizo hilo la kisheria .

''Hivi karibuni nimeshuhudia mwenyewe huko Tanga jahazi limepata ajali na kuzama huku abiria wakipoteza maisha ikiwamo watoto,''alisema.

Alisema wizara imeanza ukaguzi wa vyombo hivyo katika maeneo ya bandari Unguja na Pemba na kuona kwamba vinatekeleza agizo la serikali la kuacha kubeba abiria

JE Umehangaika na Matatizo ya Kimapenzi Kwa Muda Mrefu? Muone Shehe Chalo Atakutatulia Matatizo yako Kirahisi

$
0
0

JE umehangaika na matatizo haya kwa muda mrefu mtalamu Challo anayo dawa ya kuvuta mpenzi Je unasumbuliwa na mpenzi umeachwa na mpenzi au Mme mke na Bado unampenda na umejaribu sehemu nyingine Bila mafanikio njoo utatuliwe haraka na kundumisha ndoa yenu..

Umekimbiwa na mmeo mkeo au mpenzi na anaishi na mtu mwingine atarundi haraka kusafisha nyota mvuto wa mwili na biashara minguu kufa ngazi kuwaka moto ngiri tumbo kuunguruma na wakina Baba wasiojiweza katika tendo la uyumba kuchelewa kufika kileleni tunatibu Busha Bila oprasheni bali kwa kutumia vitabu vya dini

Tunatoa pete ya utajiri Bila mashariti mkufu wa bahati unauza Mali ya haindi unapoteza pesa kwenye biashara yako Bila kujua unataka kupandishwa cheo

Wasiliana na mtalamu Shehe Challo 0714006521

Mjasiriamali Carol Ndosi Amuandikia Barua ya Wazi Rais Magufuli

$
0
0
Mjasiriamali maarufu nchini Tanzania, Carol Ndosi amemuandikia barua ya wazi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akifikisha kilio chake kwa kugusia mambo makubwa matatu.

Jambo la Kwanza, Bi. Ndosi amemuomba Rais Magufuli aangalie upya kuhusu suala la wanafunzi wa kike wanaopata mimba kutorudi mashuleni, kwani agizo hilo alilotoa mwaka jana (SOMA HAPA AGIZO HILO)  litapelekea watoto wa kike 8,000 kila mwaka kuacha shule.

Mambo mengine aliyoyazungumzia ni kuhusu hali ya usalama kwa wananchi na muktadha wa demokrasia nchini kuhusu matukio yanayoendelea nchini likiwemo la kupigwa risasi kwa mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji (NIT), Akwilini Akwelina. Soma barua hiyo kwa undani

BARUA YA WAZI KWA MHESHIMIWA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI

Mheshimiwa Rais wangu mpendwa Dr John Joseph Pombe Magufuli, Shikamoo. Natumai ni mzima wa afya na unaendelea kutimizia wajibu wa kazi ya taasisi yako. Nimeona ulikua kwenye kikao cha wakuu wa nchi za Afrika Mashariki nchini Uganda. Pole na Safari.

Kati ya mambo niliyofarijika kuyasikia ni pale wewe na Mhe. Uhuru Kenyatta mlipowaambia mawaziri wa wizara husika wakae chini ma kushughulikia migorogoro midogo iliyokua inajitokeza hivi karibuni na kuharibu mahusiana ya nchi zetu mbili. Hakika sisi ni jumuiya na yatupasa kufanya kila namna kulinda jumuiya hii.

Mhe. Rais wangu mpendwa Dr John Pombe Magufuli, nimeona pia ulivyorudi, umepitia Mwanza kwanza. Mwanza ni mikoa ambayo naipenda sana pia kutokana na mazingira ya kibiashara yaliyopo na hata wakazi wa huko walivyo wakarimu. Kupitia matamasha yetu ya na shughuli za The Launch Pad za uwezeshaji wa vijana na wanawake, tunatarajia kuendelea kushirikiana na wananchi wa mkoa huu kuendelea kutengeneza ajira, kutangaza mkoa na kuwawezesha vijana na ujuzi wa ujasiriamali na kutafuta ajira.

Hakika ni wakazi wenye kujituma sana kwenye nyanja mbalimbali. Hawatofautiani sana na wakazi wa Kimara, waliokua na nyumba zao, maisha na biashara kwenye maeneo waliyobomolewa kwa agizo na mpango wa serikali. Nawaza tu, tamko lako kwa wakazi wa Mwanza waliokua wabomolewe makazi yao limenipa faraja sana. Hata hivyo limenipa pia simanzi na kuwaza je kama wenzetu wa Kimara wangepata kusikia kutoka kwako rais wetu mpendwa kabla hawajapoteza mali na mustakabali wa maisha yao, hakika leo hii tusingekua tunasikia vilio na laana kutoka kwa waathirika wa ubomoaji Kimara.

Rais wangu mpendwa Dr John Pombe Magufuli, nakumbuka kukufuatilia sana uchapaji wako wa kazi ulivyokua waziri, tena tumeshakutana kwenye press conference na mikutano mbali mbali nilivyokua mwandishi wa habari ninayeingia field. Ulikua unanipa faraja sana kuona kuna viongozi ambao ‘they walk the talk’. Actually kipindi kile ilikua no talk sana kwako mengi yalikua ni vitendo. Ni historia yako hii iliyonipa faraja hata matokeo yalivyo tangazwa kuwa umeshinda uchaguzi wa urais (niseme ukweli nilimpigia kura Mama Anna Mghwira, I am an unapologetic feminist fortunately).

Ni mmoja kati ya wale walioamini kabisa katika nia na dira yako uliyoingia nayo ya kwanza kuwa mtetezi wa wanyonge, yaani nilikua nina imani sana kuwa wale wanyonge ambao kwa mtazamo wangu ndio majority ya Watanzania, ungeweza kuwafikia kwa huduma zote za msingi za kijamii. Niliamini kabisa kwa nia yako ya kuanza safari ya Tanzania ya viwanda, itatukomboa kiuchumi na kimaendeleo.

Ulipoanza na kupunguza matumizi ya Serikali na safari zisizo na tija kwa maendeleo ya nchi, mimi na wenzangu wengi tulifarijika sana. Makinikia ndio ilikua iwe homerun, bado tuna imani, Hakika hata msemo wako wa ‘Hapa Kazi Tu’ ulinipa muamsho mpya wa kujituma zaidi, binafsi hata na changamoto zote nilizokua napitia, zingine zinazohusiana na maamuzi ya viongozi wengine serikali kwa wafanyabiashara kama sisi, nilijitahidi kutokata tamaa na kuendelea na KAZI hadi pale nilipo komolewa kuliko. Mimi ni yule niliyeandika barua kwako mjasiriamali ambayo ilieleza changamoto tulizo pitia kama mtayarishaji wa tamasha na jinsi tulivyo athirika na kufungiwa kwa Uwanja wa Leaders na sheria mpya ya matamasha ambayo hata hivyo imeonekana kubagua.

Rais wangu mpendwa Dr John Pombe Magufuli, bado nina imani una nia njema kabisa na Watanzania. Naamini hili kupitia jitihada zako mbali mbali za miradi ya maendeleo haswa ya miundo mbinu. Wengi wanahoji ‘priorities’ na kama zina-akisi ‘utetezi wa wanyonge’. Hawajaona SGR na Flyover zinawasaidia vipi wanyonge kwa sasa. Huwa najibu inawezekana kabisa hatujui ‘grand vision’ yako kwa ajili ya Tanzania. Tukupe muda kidogo.

Kama Mtanzania niliyejaliwa vipaji na ujuzi katika nyanja mbali mbali, Nilichoka kulalamika, kila ninachofanya actually najaribu kuendana na mpango wa maendeleo wa taifa #FYDP, jinsi gani ninaweza kusupport jitihada za serikali kwa nafasi na platform zangu.

Na kwa heshima zote na taadhima Ndio maana ulivyo tuhakikishia mtoto wa kike mwenye kupata mimba kutoruhusiwa kurudi shuleni, na ulivyo sisitiza kuwa unajitahidi kuweka elimu bure halafu watoto wa kike wanachezea nafasi kwa kupata mimba, hadi ukasema ‘mkitaka wajengeeni shule au waende VETA’, niliyabeba haya na kusema kweli ingawa ni haki ya mtoto kupata shule, lakini Rais wetu hili hebu ngoja tutafute suluhishi hadi pale ambapo ungekaa na kutufikiria tena baba.

Nasema kutufikiria tena sababu naamini kabisa kama mtetezi wa wanyonge, hutokubali kuwaacha wasichana zaidi ya 8000 wanaoacha shule kila mwaka kutokana na mimba za utotoni. Hakika hawa ni nguvu kazi ambao tunawahitaji kusukuma gurudumu la maendeleo na hata Tanzania ya viwanda.

Nilikaa na kufikiria jinsi gani ya kukuunga mkono kwenye hili, mimi ndio yule uliyeambiwa ninaye shirikiana na watanzania kujenga shule ya waathirika wa mimba na ndoa za utotoni. Shule hii itakua ya Ujuzi na Stadi Za Kazi ili kuunga jitihada za Tanzania ya Viwanda na dhana ya kuongeza thamani kwenye uzalishaji.

Rais wangu mpendwa Dr John Pombe Magufuli, umesikia matukio ambayo kwa kweli YANATISHA mno na kubadilisha historia nzima ya nchi yetu kama jamii inayoheshimu sheria na kuendeleza amani. Naamini kabisa huyafurahii haya.

Kutoka waathirika wa matukio ya Zanzibar, hadi maaskari wa Kibiti, na sasa haya kisiasa yanayo ripotiwa kila siku. Kwa jinsi ninavyo amini ulivyo muumini wa Mungu na hata kututamkia ni Mungu ndiye anaye kuongoza, lazima itakua inakusikitisha na kukuuma mno kuona wananchi wako wanavamiwa kwa mashambulizi ya risasi, wengine hadi kupigwa risasi 30 NA! Na hata kijana mdogo kama Akwilina Akwilin Bafta kupoteza maisha kwa risasi.

Nawaza sana wakati mgumu unaopitia sasa maana naona kabisa nia uliyo kuwa nayo na sisi kama taifa inazidi kuchafuliwa. Najiuliza mimi kama Mtanzania ninaye jitahidi kufanya kila niwezalo kuchangia maendeleo ya nchi yangu na kutetea katiba na haki za wananchi nikusaidie vipi ili uweze kuendeleza nia yako.

Nikuombe pia uongee na sisi baba. Wewe ni baba yetu, tunahitaji kusikia kutoka kwako nchi inaelekea wapi na haya matukio na uminywaji wa demokrasia na kutumika vibaya kwa mamlaka kwa baadhi ya viongozi na taasisi. Naomba nikuhakikishie hamna Mtanzania anayefurahia haya yanayoendelea na wala hamna ambaye anakinzana na nia yako njema ya kuleta maendeleo na usawa katika taifa hili. Tuko na wewe, kila Mtanzania kwa nafasi, uwezo na uwepo wake.

Wengi wangependa kuwepo na mazingira yatakayo wawezesha wao kutimiza wajibu na nafasi zao kama Watanzania kuleta maendeleo nchini na kwenye maisha na jamii zao. Kila kukicha naona manung’uniko ya Watanzania kuhusu mambo mbali mbali. Nakataa kuendelea kuwa jamii inayolalama kila siku haswa kwa haya tunayo yalalamikia. It has to end.

Tunaomba na Tunakuhitaji sana utumie mamlaka yako uliyopewa na Mamilioni ya Watanzania kuhakikisha matukio haya, uminywaji wa haki za binadamu, ukiukwaji wa katiba na demokrasia, na matumizi mabaya ya viongozi na mamlaka YANAFIKA KIKOMO.

Rais wangu mpendwa Dr John Pombe Magufuli, Sijui utaona suluhishi gani linafaa kuondokana na hii hali ya sasa hivi, Katiba mpya ingekua ni kipaumbele hakika mengi yasingetokea. Sijui pia kama kuna nafasi ya kukaa chini na ya kuyajadili haya kama taifa. We are not happy baba. We are hurting. From our very cores.

Wako MNYENYEKEVU katika Ujenzi wa Taifa

Carol Ndosi

Fahamu Faida za Unywaji Maziwa kwa Binadamu

$
0
0
Maziwa ni moja ya kimiminika kinachotajwa na kuaminiwa kuwa kinamkinga binadamu na baadhi ya magonjwa pia maziwa ni dawa tosha kwa magonjwa mbalimbali.

Zifatazo ni faida za unywaji maziwa:

i.) Huimarisha meno
Maziwa ni chanzo bora cha madini ya kalisiamu, hivyo basi maziwa ndicho kitu halisi kinachohitajiwa na meno yetu. Pia maziwa huzuia kutoboka na kuoza kwa meno. Kalisiamu hufyonzwa na miili yetu kukiwa na vitamini D;

ii.)Maziwa husaidia kupunguza uzito wa mwili

Utafiti unaonesha kuwa wanawake wanaokunywa maziwa hupunguza uzito zaidi kuliko wale wasiokunywa. Inashuriwa kunywa maziwa wakati wa chakula cha jioni au unapokula matunda.

iii.)Kujenga misuli ya mwili

Hili ni kutokana na protini zinazopatikana katika maziwa. Wanariadha wengi hunywa maziwa baada ya mazoezi, hii ni kwa ajili ya kuupa mwili virutubisho vya kutosha kwa ajili ya kujijenga tena

iv.) Husaidia kupunguza maumivu ya hedhi

Wanawake wengi wanakabiliwa na maumivu wakati wa hedhi. Maziwa yamedhibitishwa kuzuia na kupunguza maumivu haya kwa kiasi kikubwa.

v.) Hupambana na maradhi mengine

Kwa miongo kadhaa tafiti zimebaini kuwa maziwa huzuia magongwa kadha wa kadha. Magonjwa hayo ni kama vile shinikizo la damu na kiharusi. Inaaminika pia maziwa hupunguza lehemu (cholesterol) mwilini na kuongeza uwezo wa macho kuona. Baadhi ya watafiti wameeleza kuwa unywaji wa maziwa huzuia ania fulani za saratani.

Chanzo na Mitandao.

Jibu la Rayvanny Kwanini Jason Derulo Hajaposti Ngoma yao

$
0
0
Msanii wa muziki Bongo kutoka label ya WCB, Rayvanny amesema Jason Derulo muda wowote ataposti ngoma ‘Tip Toe Remix’ waliofanya pamoja.

Hata hivyo muimbaji huyo amesema kuwa hata asipofanya hivyo kitendo cha kukubali kufanya naye kazi ni heshima kubwa amempatia.

“Atapost, kwa sababu ujue unavyoendesha page zako kuna ratiba unakuwa umepanga, so kuna vitu ambavyo nimeshaongea naye najua ni muda gani ataposti,” amesema Rayvanny.

Tip Toe ni ngoma ya Jason Derulo ambayo amemshirikisha French Montana, ngoma hii ilitoka December 7, 2017. Rayvanny ameshirikishwa katika remix ya ngoma hiyo

Vanessa Mdee Afunguka Kuvunjwa Moyo

$
0
0
Malkia wa Bongo Fleva anayefanya vizuri ndani na nje ya nchi, Vanessa Mdee amefunguka na kudai anamshukuru Mungu kwa kupokelewa vizuri albamu ya 'Money Monday' mpaka sasa japokuwa kuna baadhi ya watu wanataka kumvunja moyo.

Vanessa amebainisha hayo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha 'FRIDAY NIGHT LIVE' (FNL) kutoka EATV baada ya kuulizwa swali na Bill Sepenga kuhusiana na mauzo ya albamu kama yanaenda vizuri au laa.

"Mauzo yanaenda sana kusema ukweli yani nimestaajabishwa sana na mauzo ya albamu, nimefurahi kuona watu wapo teyari kupokea albamu. 'Is fun' kuona watu wengine wanataka kunivunja moyo. Mimi naenda baa nauza 'CD' mwenyewe wengine wananifukuza wananiambia albamu zimepitwa na wakati", amesema Vannessa.

Kwa upande mwingine, Vmoney amesema  anawashukuru watu wote wanaondelea kumpa ushirikiano kwa namna moja ama nyingine katika kununua albamu yake ya kwanza kwa mwaka 2018.
Viewing all 104694 articles
Browse latest View live




Latest Images