Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104414 articles
Browse latest View live

Mrisho Gambo Darasa Wanaume "Epukeni Wanawake wa Aina Hii"

0
0
Mrisho Gambo Darasa Wanaume "Epukeni Wanawake wa Aina Hii"
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amewashauri wanaume nchini waliyo kwenye mahusiano na wanawake ambao hawana mawazo ya kupambana na hali ya uchumi kwa sasa, kujiondoa mara moja kwenye mahusiano hayo kwani ni hatari kwao kwa maisha ya baadae.

Gambo amesema kama mwanaume unataka uwe na uchumi mzuri kwa kipindi hiki ni bora ukaachana na wanawake wanaopenda starehe na kuwa na mwanamke mwenye kutoa ushauri namna gani ya kujikwamua katika maisha haya ya sasa ambayo watu wengi wanalalamika kuwa ni magumu.

“Mwanaume Kama unania ya dhati kuwa na economic freedom in this tough economy basi inatakiwa uepukane na wale wanawake aina ya “Babe nina njaa, nibebee Pizza au Chips kuku asisahau kuweka mayonaise” au “Babe simu Iphone X imetoka naomba ninunulie”. Achana na huo ujuha…Badala yake pata mwanamke aina ya “Babe umekula au unataka nikupikie chakula gani leo” au “Babe ni nini future yako naona hujaweka vizuri vipaumbele vyako”. Spidi ya mwanaume kuwa na maendeleo na hatimae kushinda uhuru wa kiuchumi inategemeana sana na aina ya mwanamke uliyenae,“ameeleza Mhe. Gambo kwenye ukurasa wake wa Twitter na kumuelezea mwanamke bora wa kuoa.

“Mwanamke bora ni Uwekezaji wenye faida kubwa na mwanamke asiejua nafasi yake ni Mzigo na Liability kubwa sana. Na pale upatapo maendeleo usiwe mbahili… usisahau ku-enjoy na mwanamke aliyekua nyuma ya mafanikio yako..” that’s smart dating and how we smart people do.“ameeleza Gambo.

Sugu Awasili Mahakamani kwa Hajili ya Kusomewa Hukumu Ulinzi Wahimarishwa

0
0
Ulinzi umeimarishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya ambako itatolewa hukumu ya kesi inayomkabili mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu Sugu na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga.

Katika eneo la mahakama wapo askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wakiimarisha ulinzi nje ya jengo. Tayari washtakiwa wameshafika mahakamani.

Mahakama leo Februari 26,2018 inatoa hukumu ya kesi ambayo Sugu na Masonga wanashtakiwa kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli.

Wawili hao wanadaiwa kutenda kosa hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Desemba 30,2017 eneo la Uwanja wa Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.

Hukumu inatarajiwa kutolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Michael Mteite aliyesikiliza kesi hiyo. Upande wa mashtaka na wa utetezi ulikamilisha ushahidi Februari 9,2018.

Jamhuri iliwasilisha mashahidi watano na kielelezo kimoja cha sauti iliyodaiwa kurekodiwa na shahidi wa tano, Inspekta Joram Magova.

Upande wa utetezi uliwasilisha mashahidi sita wakiwamo Sugu na Masonga waliokana kutamka maneno wanayoshtakiwa kuyatoa.

Washtakiwa walitetewa na mawakili Sabina Yongo, Boniface Mwabukusi na Hekima Mwasipu kabla ya kujitoa, hivyo sasa wanawakilishwa na Peter Kibatala.

Kwa mara ya kwanza, Sugu na Masonga  walifikishwa mahakamani Januari 16 na kusomewa mashtaka na Wakili wa Serikali Mkuu, Joseph Pande aliyeeleza upelelezi ulikuwa umekamilika na walikuwa tayari kuendelea na usikilizaji.

Hatimaye Albamu ya Diamond Platnumz ya ‘A Boy From Tandale Kutoka Wiki Ijayo

0
0
 Hatimaye Albamu ya Diamond Platnumz ya ‘A Boy From Tandale Kutoka Wiki Ijayo
Hayawi hayawi sasa yamekuwa hatimaye albamu ya Diamond Platnumz ya ‘A Boy From Tandale’ yenye ngoma takribani 20 kutua mwezo ujao.

Albamu hiyo inatarajiwa kutua rasmi mwezi ujao tarehe 16 huku ikiwa na hit kibao kama , ‘Hallelujah’ aliyoshirikisha Morgan Heritage’,‘Waka Waka’ aliyomshirikisha Rick Ross, ‘Marry You’ aliyomshirikisha Ne-Yo , ‘African Beuty’ aliyomshirikisha Omarion pamoja na ngoma zingine alizofanya mwenyewe kama ‘ Sikomi’ pamoja na zinginezo kutoka kwa wasanii kutoka Afrika.

Kwa mujibu wa meneja wa msanii huyo Sallam SK, kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram ameweka rasmi tarehe hiyo huku akiujuza uma kuwa kwa sasa unaweza kutoa Pre-Order albamu hiyo.

Ajali Mbaya ya Daladala Yatokea Kimara

0
0
Ajali Mbaya ya Daladala  Yatokea Kimara

Basi la abiria (Daladala) linayofanya safari zake kati ya Mbezi na Makumbusho jijini Dar es Salaam limepinduka leo Jumatatu, Februari 26, 2018 asubuhi katika eneo la Kimara Korogwe.

Polisi wapo eneo la tukio kufanya jitihada za kuokoa watu waliokuwemo kwenye ajali hiyo ambapo basi limepinduka na kugeuka magurudumu yakawa juu.

Idadi ya majeruhi haijajulikana na iwapo kuna watu waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo. Tutakupa taarifa zaidi baadaye.

Alhamdulillah Nimerudi Tena- Wema Sepetu

0
0
Alhamdulillah Nimerudi Tena- Wema Sepetu
Muigizaji wa filamu mwenye nyota yake bongo na Afrika Mashariki Wema Sepetu, amefunguka na kusema amejisikia vizuri na furaha kwa yeye kurudi kwa mara nyingine katika mitandao ya kijamii.


Wema amebainisha hayo asubuhi ya leo baada ya kukabidhiwa ukurasa wake wa kijamii instagram na watu waliokuwa wanamhangaikia kuupata tokea waharifu kuuiba kwa takribani mwezi mmoja sasa.

 huu wakati ni kweli. Namshukuru sana Tizzo, daah nime-miss kweli ukurasa wangu. Najua jinsi mlivyoni-miss kwa sana. 'But it feels good to be back", amesema Wema.

Kutokana na hilo, wapenzi na mashabiki wa Wema Sepetu wamepokea ujumbe huo kwa shauku kubwa huku wengine wakimpa maneno yenye faraja kutoka na kupotea mitandaoni kwa kipindi kirefu kidogo.

Kada wa CCM, Shyrose Bhanji Aukana Ujumbe Ulioandikwa Katika Instagram yake Kuhusu JPM

0
0

Kada wa CCM, Shyrose Bhanji amuomba radhi Rais Magufuli kwa ujumbe uliosambaa ukitokea katika ukurasa wake wa Instagram. Amesema alidukuliwa

Kupitia akaunti yake ya Instagram ulisambaa ujumbe unaosema ''Sikubaliani na utawala wa Rais JPM, niko tayari kwenda jela"

Breaking News: Mahakama Yawahukumu kwenda Jela Sugu, Masonga Baada ya Kukutwa na Hatia

0
0
Breaking Newa: Mahakama Yawahukumu kwenda Jela Sugu, Masonga Baada ya Kukutwa na Hatia
MBUNGE wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga wahukumiwa kifungo cha miezi mitano jela baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais

Miujiza ya Sharifu Seif Mohamed..JE Umeachwa na Mme/Mke au Mpenzi, Umesongwa na Mitihani ya Maisha..Piga Simu Upate Muujiza Wako

0
0

SHARIFU SEIF MOHAMED ANAWASHUKURU WALE WOTE WANAOENDELEA KUPIGA SIMU, WENYE MATATIZO NA WALE WANAOTOA  SHUKRANI NA SHUHUDA JINSI TIBA ZAKE ZINAVYO WASAIDIA,

(Rudisha mahusiano yako ndani ya masaa 72 tu)

SHARIFU MOHAMED Ni  mtaalam na mnajimu maarufu wa nyota na kubashiri mambo yanayo watesa binadamu duniani kote na kupata ufumbuzi, Anatumia kitabu cha QUR'AN na Nyota

Je Umeachwa na UMPENDAE awe Mme/Mke na bado unampenda? Je Umekimbiwa na Mmeo/ Mkeo n anaishi na mtu mwingine? Je Umejaribu sehemu nyingi bila mafanikio? Mpigie simu SHARIFU SEIF sasa hivi ujionee Muujiza wa Papo kwa Papo, Anauwezo wa hali ya juu wa kusambaratisha mahusiano yao na kumrejesha kwako haraka sana na Kumfanya Atimize Ahadi zote Ndani ya Muda Mfupi Endapo Utafwata Atakacho Kuelekeza

 ZINDIKO LA NYUMBA NA BIASHARA, PETE ZA BAHATI, HUMALIZA KABISA TATIZO   HUZUIA CHUMA ULETE KWENYE BIASHARA, HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA, NA KUPONYA MAGONJWA SUGU ANAO UWEZO WA KUMRUDISHA ALIE MBALI AU ALIECHUKULIWA MSUKULE, KUPANDISHA NYOTA NA KUSHINDA BAHATI NA SIBU, KASAFISHA NYOTA NA KUKUPA MVUTO WA AJABU, KUTOA NUKSI NA VIFUNGO MBALIMBALI,  MAFANIKIO YA MAISHA NA UTAJIRI BILA MASHARI, NA MENGINE MENGI YA SIRI,

JE UMAHANGAIKA KUPATA MTOTO BILA MAFANIKIO? WASILIANA NA MTAALAMU HUYU KWANI YEYE HUFAULU PALE WOTE WALIPOSHINDWA, PIA UMALIZA KAZI ZILIZO SHINDIKANA NA WATAALAM WENGINE NDANI YA MASAA 24 TU,

(NA ANATIBU KWA NJIA YA SIMU UKIWA NCHI YOYOTE AU MKOA WOWOTE ENDAPO UTAFWATA MAELEKEZO YAKE)

Kwa ushauri na mawasiliano  zaidi Piga SIMU No:

Mobile +255 654-836970
WhatsApp 0622766715


Jaji Mkuu Atoa Maagizo Haya kwa Majaji, Mahakimu

0
0
Jaji Mkuu Atoa Maagizo Haya kwa Majaji, Mahakimu

Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma amewataka majaji na mahakimu kumpunguzia maumivu mwananchi anayefuata haki mahakamani kwa kutimiza malengo waliyojiwekea, kuwapa ushauri pamoja na kusikiliza na kumaliza mashauri haraka.

Akizungumza na watumishi walio chini ya Msajili wa Mahakama ya Wilaya ya Tabora mjini hapa juzi, jaji mkuu aliwataka watumishi wa mahakama kuwa na tabia ya kuwapa elimu wananchi kuhusiana na haki zao.

Alieleza kuwa wananchi wengi hawajui haki zao na elimu kuhusu haki zao itawasaidia. “Haki huanza kwa usuluhishi, mahakama inapaswa kuwaongoza na kuwaelimisha wananchi ili wajue kuwa ni sehemu ya kupata haki na si vinginevyo,” alisema.

Akizungumzia ujenzi wa Mahakama ya Wilaya ya Sikonge, alisema utakamilika mwaka huu na kuanza kazi mara moja. Hadi sasa Sikonge haina mahakama ya wilaya na inategemea ile ya Tabora na wananchi hutumia muda na pesa nyingi kufuata haki zao mjini humo.

Aliongeza kuwa wakati wakisubiri ujenzi wa Mahakama ya Wilaya ya Uyui yenye mahakama moja, tena ya mwanzo wanajipanga kutumia mahakama zinazotembea kuwapunguzia mzigo wananchi wa maeneo yasiyo na mahakama.

Awali, akizungumza na sekretarieti ya Mkoa wa Tabora, Profesa Juma aliyataka mabaraza ya kata yatekeleze majukumu yake kwa kuzingatia sheria ili kuwapunguzia watendaji wa Serikali malalamiko. Jaji mkuu aliongeza kuwa mabaraza hayo ambayo yalianzishwa kwa matakwa ya Katiba ya nchi kazi yake ni usuluhishi na ndiyo maana hata adhabu zake ni ndogo.

Alimuelekeza Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri kufuatilia kwa ukaribu utendaji kazi wa mabaraza hayo kwa kuwa ndiyo yamekuwa chanzo cha migogoro ya ardhi na mashauri ya mirathi.

Akizungumza katika mkutano huo, Mwanri alisema ofisi yake hupokea malalamiko yanayohusiana na ucheleweshaji wa majalada ya hukumu.

Shy-Rose Bhanji Afunguka Kuhusu Kauli Yake ya Kupinga Utawala wa Rais Magufuli

0
0
Shy-Rose Bhanji Afunguka Kuhusu Kauli Yake ya Kupinga Utawala wa Rais Magufuli
ALIYEWAHI kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shy-Rose Bhanji amekanusha taarifa ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii ikidai kuwa anapinga utawala wa Rais Dkt. John  Magufuli.


Taarifa hiyo ilionekana imeandikwa kwenye akaunti yake rasmi ya Instagram lakini  amesema ilikuwa imedukuliwa na watu wasiojulikana ambao wali-post ujumbe huo wenye nia ya kumchonganisha na Rais.

“Account yangu ya Instagram ilikuwa hacked na watu wasiojulikana ambao walipost vitu ambavyo sihusiki navyo. Naomba radhi kwa Rais wangu JPM na wote waliokerwa na jambo hilo,” ameandika ShyRose.

Mahakama YawatiaHhatiani Sugu, Masonga

0
0
Mahakama YawatiaHhatiani Sugu, Masonga
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya imewatia hatia mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu Sugu na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya, Michael Mteite aliyeanza kusoma hukumu leo Februari 26,2018 saa 03:32 asubuhi amesema washtakiwa wana hatia kwa makosa waliyoshtakiwa.

Baada ya kuwatia hatiani washtakiwa, hakimu Mteite anasubiriwa kutamka adhabu dhidi yao.

Sugu na Masonga wanashtakiwa kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli.

Wawili hao wanadaiwa kutenda kosa hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Desemba 30,2017 eneo la Uwanja wa Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.

Huu Hapa Uamuzi Mwingine wa Mahakama Juu yaMamlaka ya DPP Kuhusu Kuzuia Dhamana

0
0
Huu Hapa Uamuzi Mwingine wa Mahakama Juu yaMamlaka ya DPP Kuhusu Kuzuia Dhamana
Mahakama ya Rufaa imesema Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) anapowasilisha hati kuzuia dhamana kwa washtakiwa kwa kukidhi matakwa ya kisheria mahakama inakuwa imefungwa mikono.

Uamuzi huo umetolewa siku chache baada ya Mahakama hiyo Februari 2 kutoa hukumu iliyomwondolea DPP mamlaka ya kuzuia dhamana ya mshtakiwa bila hata kulazimika kutoa sababu, baada ya kubatilisha kifungu cha 148 (4) cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai, kinachompa mamlaka hayo.

Katika hukumu ya Februari 23 kuhusu rufaa iliyokatwa na aliyekuwa mwanasheria wa Kampuni Hodhi ya Mali za Reli (Rahco), Emmanuel Massawe, Mahakama imesema DPP anapowasilisha hati ya zuio la dhamana dhidi ya mshtakiwa, hata mahakama inakuwa imefungwa mikono isipokuwa tu, kama itathibitika kuwa DPP alichukua uamuzi huo kwa nia mbaya. Massawe alikata rufaa akipinga uamuzi wa Mahakama Kuu uliotolewa na Jaji Isaya Arufani Aprili 12, 2016.

Katika maombi hayo namba 51 ya mwaka 2016, Massawe na wenzake waliomba dhamana licha ya DPP kuizuia chini ya kifungu cha 36 (2) cha Sheria ya Uhujumu Uchumi.

Mahakama Kuu ilikataa kutoa dhamana ikieleza DPP anapowasilisha hati kuzuia dhamana chini ya kifungu cha 36 (2) cha Sheria ya Uhujumu Uchumi, mahakama inakuwa haina mamlaka ya kuitoa.

Massawe, kupitia jopo la mawakili Dk Rugemeleza Nshalla, Fulgence Massawe na Jeremiah Mtobesya, alikata rufaa Mahakama ya Rufaa akipinga uamuzi wa Mahakama Kuu wakitumia hukumu ya mahakama hiyo iliyobatilisha kifungu cha 148 (4) cha CPA.

Kifungu hicho kinampa DPP mamlaka ya kuizuia Mahakama au ofisa wa Polisi kutoa dhamana kwa mshtakiwa au mtuhumiwa baada ya kuwasilisha hati ya maandishi, kwa maelezo kuwa usalama au masilahi ya Jamhuri yataathirika.

Awali, Mahakama ya Rufaa katika hukumu ya Februari 2 ya rufaa ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya mwanaharakati wa haki za binadamu, Mtobesya alisema kifungu hicho ni kinyume cha Katiba na ni batili.

Hukumu hiyo ilitolewa na jopo la majaji watano wa Mahakama ya Rufaa waliokubaliana na ya awali iliyotolewa na Mahakama Kuu. Majaji waliosikiliza na kutoa hukumu ya rufaa hiyo ni Bernard Luanda (kiongozi wa jopo), Kipenka Mussa, Bethuel Mmila, Stellah Mugasha na Jacob Mwambegele.

Mahakama katika rufaa ya Massawe imeitupilia mbali ikikubaliana na hoja za Wakili wa Serikali Mkuu, Tumaini Kweka na uamuzi wa Mahakama Kuu wa kuwanyima dhamana washtakiwa.

Hukumu hiyo iliyoandikwa na Jaji Richard Mziray kwa niaba ya jopo la majaji watatu walioisikiliza wakiongozwa na Mbarouk Mbarouk na Rehema Mkuye ilisomwa Ijumaa iliyopita na naibu msajili wa Mahakama ya Rufaa, Amir Msumi.

Katika hukumu hiyo ambayo Mwananchi imeiona nakala yake, majaji hao wanasema ingawa mawakili katika hoja zao walijaribu kuishawishi Mahakama itoe uamuzi kwa kufuata kesi ya Mtobesya, haiwezi kutumika kwenye rufaa hiyo kwa kuwa ni mashauri mawili tofauti.

Majaji hao wamesema rufaa ya Mtobesya ilikuwa ya Kikatiba ikihoji uhalali wa kifungu kinachompa mamlaka DPP kuzuia dhamana, wakati katika rufaa ya Massawe anapinga uamuzi wa Mahakama Kuu kumnyima dhamana.

Wakati wa usikilizwaji wa rufaa hiyo, Mahakama imesema ilibaini kuwa hoja ya msingi iliyotawala mjadala wa hoja za mawakili ni iwapo hati ya DPP aliyoiwasilisha mahakamani chini ya kifungu cha 36 (2) cha Sheria ya Uhujumu Uchumi kuzuia dhamana kwa maelezo kuwa itaathiri masilahi ya Jamhuri inatosha kuwanyima dhamana.

Majaji katika hukumu hiyo wanasema Mahakama inakubaliana na wakili wa Serikali, Kweka kuwa DPP anapowasilisha hati ya zuio la dhamana dhidi ya mshtakiwa, hata Mahakama inakuwa imefungwa mikono isipokuwa tu kama itathibitika kuwa alichukua uamuzi huo kwa nia mbaya.

Wamesema Mahakama ilishaweka masharti matatu ya msingi ya hati ya DPP ya zuio la dhamana chini ya kifungu cha 36 (2) cha Sheria ya Uhujumu Uchumi, katika kesi ya DPP dhidi ya Nuru Dirie na mwenzake, katika taarifa za sheria za mwaka 2002 (TLR).

Masharti hayo yanatajwa kuwa ni; DPP lazima awasilishe hati ya maandishi; ieleze sababu kuwa usalama na masilahi ya umma yataathirika kwa kutoa dhamana kwa washtakiwa; na hati hiyo ni lazima ihusiane na kesi ya jinai ama inayosubiri kusikilizwa au inayosubiri rufaa.

Hukumu hiyo inaeleza masharti hayo yalithibitishwa na Mahakama katika kesi ya rufaa ya DPP dhidi ya Li Ling Ling ya 2015 .

Majaji hao wamesema hati ya DPP inaweza tu kuwa batili inapothibitika kwamba alifanya hivyo kwa nia mbaya au matumizi mabaya ya utaratibu wa kimahakama, jambo ambalo halikuwa hoja katika rufaa hiyo.

   

Hivi Ndivyo Zari Alivyojiliwaza Katika Sherehe ya Valentine Party

0
0
Hivi Ndivyo Zari  Alivyojiliwaza Katika Sherehe ya Valentine Party
Mrembo Zari The Bosslady wikiendi hii alikuwa mmoja wa wageni katika sherehe ya Valentine Party ambayo ilifanyika katika klabu ya usiku ya Rio Nightclub, iliyopo katika wilaya ya Wood Green, Kaskazini mwa mji wa London.

Zari alitokelezea akiwa na gauni lake fupi na viatu virefu vyote vikiwa na rangi nyekundu. Zari alikuwa ameambatana na muandaji wa sherehe hiyo, Lady Naaa huku Naj akiwa miongoni mwa wageni wengine waliohudhuria sherehe hiyo.

Katika sherehe hiyo Rayvanny na Barakah The Prince walitumbuiza.



Zuma Arudishiwa Mashtaka 18 Yaliyoondolewa

0
0
Zuma Arudishiwa Mashtaka 18 Yaliyoondolewa

Waendesha mashtaka wanaochambua tuhuma zinazomkabili rais wa zamani wa Jacob Zuma kuona uwezekano wa kuepuka kufikishwa mahakamani wamependekeza kuwa mashtaka yote dhidi yake yarudiwe.

Gazeti la City Press limefahamishwa pasi na shaka kwamba wanasheria watano waandamizi walipendekeza kwa ujumla wao Ijumaa iliyopita kwamba Zuma afikishwe mahakamani na ashtakiwe kwa mashtaka ambayo yaliondolewa awali.

Inaaminika walitiliana saini makubaliano ya awali ambayo Ijumaa alikabidhiwa Mkurugenzi wa Taifa wa Mashtaka Shaun Abrahams, wakimtaarifu kuhusu mapendekezo yao.

Kwa hali hiyo, Zuma anatarajiwa kukabiliwa na mashtaka 18 ya ufisadi, utakatishaji fedha na udanganyifu yote yakitokana na malipo yenye utata 783 aliyopokea siku za nyuma.

Huu unaweza kuwa mwanzo wa mapambano kadhaa ya kisheria dhidi ya Zuma ambaye hivi karibuni alilazimishwa na chama chake cha ANC kujiuzulu. Anatarajiwa kuwa mlengwa mkuu wa tume inayochunguza kashfa ya serikali kuwekwa mfukoni na mafisadi.

Tangu Jumatano wiki iliyopita, timu ya waendesha mashtaka imekuwa ikifanya kazi kuweka pamoja mashtaka yanayoelezea makosa ambayo Zuma na mshtakiwa mwingine watakabiliwa nayo baada ya miaka mingi ya ushindani wa kisheria.

Vyanzo kutoka ndani ya vyombo vya usalama zinasema ingawa kulikuwa na kutofautiana kwingi na mvutano juu ya nani anapaswa kubaki kuwa sehemu ya timu ambayo inaweza kumshtaki Zuma, wote walikubaliana kwamba alishindwa kutoa hoja ya kushinikiza mashtaka yake yatupwe.

"Hakuna kurudi nyuma. Zuma anapaswa kushtakiwa kortini. Siwezi kufikiri kama Abrahams anaweza kupuuza mapendekezo ya waendesha mashtaka watano aliowateua kumwongoza juu ya uamuzi huu," alisema mtoa habari.

"Kwa kweli, bosi wa mashtaka wa KwaZulu-Natal Moipone Noko alisisitiza Desemba kuwa Zuma lazima afikishwe mahakamani siku 14 baada ya korti kutoa uamuzi wa kutupilia mbali mashtaka hayo kwamba hayana maana.”

Zitto Kabwe Afunguka Haya Baada ya Kutajwa Katika Orodha ya Watu Hatari Nchini

0
0
Zitto Kabwe Afunguka Haya Baada ya Kutajwa Katika Orodha ya Watu Hatari Nchini
Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amemjibu Mkurugenzi wa kampuni ya CZI, Cyprian Musiba na kusema kuwa taarifa aliyoitoa haimtishi bali analitaka taifa kushughulika na watu wanaomfadhili ili kuharibu mahusiano ya taifa la Tanzania na nchi nyingine duniani.

Zitto Kabwe aliandika hayo katika ukurasa wake wa mtandao wa Twitter, baada ya Musiba kuitisha mkutano na vyombo vya habari ili kutangaza orodha ya watu hatari na wanaotishia usalama wa nchi, ambapo naye (Zitto) alitajwa kuwa miongoni mwa watu kwenye orodha hiyo.

Aidha alitaka watu kumpuuza na kutoshughulika naye na badala yake washughulike na Idara ya usalama ambayo aliitaja kuwa ndiyo inayomfadhili katika kufanya yote hayo.

Katika mkutano aliofanya na waandishi wa habari, Cyprian Musiba alitaja orodha ya watu ambao aliwataja kuwa ni hatari kwa usalama, na taifa linapaswa kuchukua hatua za haraka dhidi yao ili taifa lisije likaingia kwenye matatizo.

Katika orodha yake, Musiba aliwataja Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe kuwa ni mtu hatari kwa taifa na chama hicho kimepeleka vijana kupata mafunzo nchini ujerumani, ambao wana kazi ya kuratibu mipango ya kiharifu.

Musiba alimtaja pia mwanadada Mange Kimambi na kusema kuwa yeye anatumiwa na Shirika la Kijasusi la nchini Marekani (FBI), ili kuhamasisha watu wafanye uasi ndani ya serikali yao. Alieleza kuwa hii ni kutokana na serikali iliyopo madarakani kutokuendana na sera za Marekani na hivyo FBI kupitia Mange Kimambi imeamua kuingilia kati.

Aliendelea na kumtaja mjasiriamali Maria Sarungi kuwa ni hatari kwa taifa kwani yeye hutumia mitamdao ya kijamii kujadili mambo ya kuikashifu serikali iliyoko madarakani.

Vilevile alimtaja pia Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kuwa ni mtu wa kuangaliwa, kwani anahamasisha maandamano

Aliendelea kuwataja pia Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, Mbunge wa Tarime Vijijini John Heche, Musa Tesha, John Marwa  pamoja na Evarist Chahali.


Mahakama Yawahukumu Kifungo Wanawake 15 Raia wa Uturuki Waliojiunga katika Kikundi cha Islamic State

0
0
Mahakama Yawahukumu Kifungo Wanawake 15  Raia wa Uturuki Waliojiunga katika Kikundi cha IS
Mahakama nchini Iraq imewahukumu kifo wanawake 15 raia wa Uturuki, baada ya kupatwa na hatia ya kujiunga na kundi la Islamic State.

Baadhi ya ripoti zinasema kuwa wanawake 15 walipewa hukumu ya kifo, na wengine wakahukumiwa kifungo cha maisha.

Wanawake hao walikiri kuolewa na wapiganaji wa Islamic State au waliwasaidia kufanya mashambulizi ya kigaidi.

Maelfu ya raia wa kigeni wamepigana na kuuliwa wakipigana na IS nchini Iraq na Syria.

Serikali ya Iraq imatangaza kumalizika kwa vita vyake na kundi hilo mwezi Disemba. Licha ya IS kutimuliwa kutoka ngome zake kuu, kundi hilo limeendelea kufanya mashambulizi ya kujitoa mhanga na mashambulizi mengine.

Wanawake hao wanaotajwa kuwa kati ya umri wa miaka 20-50, walikuwa wamevalia nguo nyeusi wakiwa mahakamani mjini Baghdad siku ya Jumapili. Wanne walikuwa na watoto wadogo.

Mmoja alimuambua jaji kuwa alikuwa amewapiga vita wanajeshi wa Iraq akiwa na IS.

Takriban wanawake 560 na watoto 600 wamezuiliwa nchini Iraq kwa kushukiwa kuwa wapiganaji au jamaa za wapiganaji wa IS.

Mapema mwezi huu mwanamke raia wa Uturukialikuhukumiwa kifo na wengine 10 wakahukumiwa kifungo cha maisha jela.

Mbao Yaitumia Salamu za Maaangamizi Simba Katika Mechi ya Leo

0
0
Mbao Yaitumia Salamu za Mahangamizi Simba Katika Mechi ya Leo
Kikosi cha Mbao kimeamua kupeleka salamu kwa wapinzani wao Simba kuelekea mchezo wao wa leo Jumatatu utakaopigwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwa kusema kuwa wamekuja jijini Dar es Salaam kupata ushindi na si vinginevyo.

Mwenyekiti wa timu hiyo, Solly Zephania Njashi, alisema kuwa maandalizi yao ya mchezo wa leo yapo vizuri na wamejiandaa vya kutosha na wamekuja kwa ajili ya kupata ushindi.

“Sisi tumejiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo wetu wa kesho (leo) na mashabiki wafike kwa wingi kwani tuna uhakika tutaibuka na ushindi, tumejipanga kuhusu hilo.
“Sisi tumekuja kupata ushindi, siyo kupoteza, sema tatizo huwezi jua naye mpinzani wako amejipanga vipi kwenye mchezo huo, lakini sisi tupo vizuri na kikosi hakina majeruhi, bali kuna mmoja tu ambaye tulimpandisha kutoka kwenye academia, ila mwalimu atatoa ripoti kama atacheza au la,” alisema Njashi.

Soma Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Siku ya Leo

0
0

Kauli ya Zitto Kabwe Baada ya Hukumu ya Sugu

0
0
Kauli ya Zitto Kabwe Baada ya Hukumu ya Sugu
Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe baada ya Mbunge wa Mbeya mjini kuhukumiwa miezi mitano jela amesema kuwa ipo haja ya kufanya jambo ambalo dola itaamua kuwaweka jela wote na kutorudia walichofanya kwa mbunge huyo.

Zitto Kabwe amesema leo kuwa ameona mashtaka ya Mbunge huyo yaliyopelekea kuhukumiwa jela miezi mitano.

Wabunge wa Upinzani tusimame kuhesabiwa sasa,
Nimeona mashtaka ya Sugu yaliyopelekea kuhukumiwa kwenda jela miezi 5. Wabunge wote wa vyama vya Upinzani kwa namna moja ama nyengine tunasema haya kila wakati kwenye mikutano yetu. Kuna haja ya kufanya jambo ambalo dola itaamua kutusweka jela wote au kutorudia walichofanya kwa Sugu. Ninawasiliana na wenzangu tupate UNITED DEMOCRATIC FRONT,’ ameandika Zitto katika ukurasa wake wa Facebook.

Mawakili wa Sugu, Masonga Wajipanga Kukata Rufaa

0
0
Mawakili wa Sugu, Masonga Wajipanga Kukata Rufaa
Baada ya mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu Sugu na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga kuhukumiwa kifungo cha miezi mitano jela, wakili wao Peter Kibatala amesema wanakusudia kukata rufaa.

Sugu na Masonga wamehukumiwa adhabu hiyo leo Februari 26,2018 na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya, Michael Mteite.

Wawili hao wamehukumiwa kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli, kosa walilotenda kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Desemba 30,2017 eneo la Uwanja wa Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.

Akizungumza na MCL Digital, Kibatala amesema baadaye watatoa taarifa ya nini kinaendelea ila wanakusudia kukata rufaa.

Baada ya hukumu kutolewa viongozi wa Chadema waliokuwepo mahakamani waliingia kwenye magari yao na kuelekea katika ofisi za chama hicho Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.

Wakati wa usomwaji wa hukumu hiyo, nje ya jengo la mahakama ulinzi uliimarishwa kukiwa na askari waliotanda hadi maeneo ya jirani.

Sugu ni mbunge aliyeweka rekodi ya kupata kura nyingi kuwashinda wabunge wote wa majimbo katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Katika uchaguzi huo, Sugu alipata kura 108,566 akiwaacha wapinzani wake kugawana kura 57,690.

Hukumu imetolewa na hakimu Mteite aliyesikiliza shauri hilo baada ya upande wa mashtaka na wa utetezi kukamilisha ushahidi Februari 9,2018.

Jamhuri iliwasilisha mashahidi watano na kielelezo kimoja cha sauti iliyodaiwa kurekodiwa na shahidi wa tano, Inspekta Joram Magova.

Upande wa utetezi uliwasilisha mashahidi sita wakiwamo Sugu na Masonga waliokana kutamka maneno waliyoshtakiwa kuyatoa.

Washtakiwa walitetewa na mawakili Sabina Yongo, Boniface Mwabukusi na Hekima Mwasipu kabla ya kujitoa na kazi hiyo kufanywa na Kibatala.

Kwa mara ya kwanza, Sugu na Masonga  walifikishwa mahakamani Januari 16 na kusomewa mashtaka na Wakili wa Serikali Mkuu, Joseph Pande aliyeeleza upelelezi ulikuwa umekamilika na walikuwa tayari kuendelea na usikilizaji.
Viewing all 104414 articles
Browse latest View live




Latest Images