Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104427 articles
Browse latest View live

Kim Kardashian Amuonyesha Mtoto Wake wa Tatu kwa Mara ya Kwanza

0
0
Kim Kardashian Amuonyesha Mtoto Wake wa Tatu kwa Mara ya Kwanza

Leo February 27,2018 kupitia mtandao wa instagram, Staa Kim Kardashian ambaye umaarufu wake umekuja zaidi katika kipindi cha “Kardashians” huko nchini Marekani ambapo ameamua kuweka wazi uso wa mtoto wake wa tatu kwa mara ya kwanza katika mitandao ya kijamii.

Kupitia ukurasa wake wa instagram Kim Kardashian ameandika “Baby Chicago”


Mtoto wa tatu wa Kim Kardashian na rapper Kanye West ambaye ni Chicago alizaliwa mwezi uliopita kwa njia ya upandikizaji “surrogate” ambapo mwanamke huyo alilipwa hela kwaajili ya kumzalia Kim Kardashian pamoja na Kanye West mtoto wa tatu.

Wazo hilo la upandikizaji lilikuja katika familia ya West ambapo Kim Kardashian alishindwa kubeba ujauzito kutokana na sababu za kiafya ambazo zingempelekea kupoteza maisha na hii ni kutokana na report aliyoitoa daktari wa Kim Kardshian.

Waziri Majaliwa Awapa Onyo Kali Vijana "Ole Wenu Tukikukamata Tutakutupa Miaka 30 Jela"

0
0
Waziri Majaliwa Awapa Onyo Kali Vijana "Ole Wenu Tukikukamata Tutakutupa Miaka 30 Jela"
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imedhamiria kuwalinda watoto wa kike na ndiyo maana tunawataka watoe taarifa za watu wanaotaka kuwakwamisha kimasomo kwa watendaji wa vijiji kwenye maeneo yao.

Alitoa agizo hilo jana (Jumatatu, Februari 26, 2018) wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wakazi wa wilaya ya Masasi akiwa katika siku ya kwanza ya  ziara yake ya kikazi mkoani Mtwara.

Waziri Mkuu alisema watoto wa kike wanatakiwa kuheshimiwa katika jamii kwa kuachwa waendelee na masomo yao bila ya usumbufu wa aina yoyote na atakayebainika kukatisha masomo atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Alisema Serikali  itatoa adhabu kali ya kifungo cha miaka 30 jela kwa mtu atakayekatisha elimu ya mtoto wa kike iwe kwa kumuoa, kumpa ujauzo na hata ukikutwa naye nyumbani kwako, katika nyumba ya wageni.

“Tukikukuta na binti wa shule katika kona isiyoeleweka tunakukamata na kukuchukulia hatua za kisheria. Ole wenu vijana, mkibainika mmewapa mimba mabinti wanaosoma, adhabu yake ni miaka 30 jela.”

Waziri Mkuu alisema kwa wazazi au walezi watakaowaozesha watoto kike ambao bado wanafunzi na kwa upande wa wazazi watakaomsindikiza mtoto kwenda kuoa mwanafunzi wote watachukuliwa hatua za kisheria.

Pia Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwataka wanafunzi wote kusoma kwa bidii ili watimize ndoto zao na wasikubali kushawishika kwa sababu watashindwa kufikia masomo yao.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, FEBRUARI 27, 2018.

Alikiba Kufunga Ndoa Ijumaa Hii na Mrembo Toka Kenya

0
0
Alikiba Kufunga Ndoa Ijumaa Hii na Mrembo Toka Kenya

Orodha ya wasanii wanaotoka katika kundi la ukapera inazidi kupungua kila kukicha – Alikiba anadaiwa kutaka kufuata nyayo hizo.

Msanii huyo ametajwa kutaka kufunga ndoa na mrembo huyo aliyefahamika kwa jina la Amina kutoka mjini Mombasa nchini Kenya, Ijumaa ya wiki hii.

Kwa mujibu wa chazo chetu kimesema kuwa, taarifa hizo ziliaza kusambaa baada ya Abdu Kiba kutumbua jibu wiki iliyopita wakati akifanya mahojiano na gazeti moja la huko Kenya.

Hata hivyo inafahamika kuwa Alikiba amekuwa akienda mara kwa mara Mombasa kutokana na kuwa na ukaribu na Gavana wa mji huko, Joho.

Soma Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Siku ya leo

Kutana na Mtabibu Mongwa Mganga wa Waganga Sasa Anapatikana Mikoa Yote

0
0
KUTANA NA MTABIBU MONGWA MGANGA WA WAGANGA SASA WAKO MIKOANI KARIBU YOTE NCHINI...
.
HIVYO WATATOA TIBA MAENEO YOTE YA MBEYA ,DODOMA, IRINGA , MOROGORO, MWANZA,ZANZIBAR

==>KWA WALE WENYE KUHITAJI TIBA

Husafisha nyota na kutoa Pete za bahati na kwawale walio sumbuka kwaajili ya matibabu na hawakufanikiwa chochote sasa njoo ujionee miujiza hapo kwahapo bila malipo yoyote malipo baada yakazi napia humpa mtu jini la mali kwayule anaye taka kumiliki bila mashariti yoyote
Tunatibu magonjwa mbalimbali yaliyo shindikana mpenzi aliye kukimbia nakumrudisha kwa masaa 24 tu napia natoa dawa za nguvu za kiume kuurefusha uume paka pale unapotaka .
Natoa dawa za biashara na mvuto ==tunatoa dawa zauzazi kwa wale kina mama wenye matatizoya uzazi walio angaika kwa muda mrefu bila kupata mafanikio yoyote njoo umalize tatizo lako sasa
Natoa mazindiko yanyumba na mwili biashara na mvuto kazini
Kupandisha nyota ili kungaa kupandishwa cheo kazini kurudisha mali zilizo pote zilizo ibiwa kuzulumiwa
Kesi zilizo shindikana uzimaliza mara moja namengine mengi ya siri piga simu

+255 764291657
+255 764291657
+255 764291657
+255 764291657

Mbowe ' Usalama wa Taifa Wanaratibu Mikakati ya Kuwabambikizia Kesi wana CHADEMA'

0
0

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia kwa Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe kimeongea na waandishi wa habari leo katika Makao makuu yao

Mbowe amesema Usalama wa Taifa wanaratibu mikakati ya kuwabambikizia kesi wana CHADEMA na wao wamejipanga kutokana na huo mkakati. Amemwambia Rais Magufuli kuwa wapo tayari kwa lolote maana wanapigania demokrasia

Mbowe amesema Mkoa wa Morogoro unaongoza kwa kuwabambikizia kesi viongozi wao. Lakini hata kwa mauaji, Mkoa huo unaongoza maana kuna historia ya watu wa CHADEMA kuuawa.

Amemuhusisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bwana Amosi Makala kwenye kuratibu kesi ya Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi(Sugu).Amesema hukumu ilifahamika na ilipangwa Hotelini, wote walifahamu na Amosi Makala anajua hilo

Aliongeza kwa kusema “CCM kama wanataka kurudisha uhalali wao wa uongozi waseme na wananchi watawaelewa na sio kutumia bunduki kukatisha uhai wa watu. Halafu tumeshaanza kuzoea kuuwawa, hili jambo si zuri maana tunakoelekea ni kutaka kuua upinzani”

Chadema Yakimbiwa na Wadiwani Wawili na Wanachama 20 Kagera...Watimkia Chama Hichi

0
0

KYERWA, KAGERA: Madiwani wawili wa CHADEMA, TulakilaTwijuke wa Kata ya Bugomora na Sadath Jeremiah wa Kata ya Kibale wamehamia CCM
-
Pia wanachama takribani 20 kutoka vyama mbalimbali vya Upinzani Wilayani humo wamehamia CCM
-
Madiwani na Wanachama hao wamedai kuridhishwa na utendaji wa Rais John Magufuli na kwamba hawajahongwa na mtu yeyote

JE Umehangaika na Matatizo ya Kimapenzi Kwa Muda Mrefu? Muone Shehe Chalo Atakutatulia Matatizo yako Kirahisi

0
0
JE umehangaika na matatizo haya kwa muda mrefu mtalamu Challo anayo dawa ya kuvuta mpenzi Je unasumbuliwa na mpenzi umeachwa na mpenzi au Mme mke na Bado unampenda na umejaribu sehemu nyingine Bila mafanikio njoo utatuliwe haraka na kundumisha ndoa yenu..

Umekimbiwa na mmeo mkeo au mpenzi na anaishi na mtu mwingine atarundi haraka kusafisha nyota mvuto wa mwili na biashara minguu kufa ngazi kuwaka moto ngiri tumbo kuunguruma na wakina Baba wasiojiweza katika tendo la uyumba kuchelewa kufika kileleni tunatibu Busha Bila oprasheni bali kwa kutumia vitabu vya dini

Tunatoa pete ya utajiri Bila mashariti mkufu wa bahati unauza Mali ya haindi unapoteza pesa kwenye biashara yako Bila kujua unataka kupandishwa cheo

Wasiliana na mtalamu Shehe Challo 0714006521


Mkuu wa Wilaya ya Pangani Awapa Dalasa Wanawake

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Pangani Awapa Dalasa Wanawake
Mkuu wa wilaya ya Pangani Bi. Zainab Abdallah amefunguka na kudai anawaheshimu wanawake wenzake wanaojishughulisha kutafuta pesa kwa namna moja ama nyingine huku akiwataka wasiwape upenyo baadhi ya watu ambao wanataka kuwarudisha nyuma kimaendeleo.

Bi. Zainab ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake maalumu wa kijamii asubuhi ya leo baada ya kuwepo kwa imani potovu kwa baadhi ya wanaume ambao wanawakatazia wanawake zao kutojihusisha na ufanyaji kazi wa aina yeyote ile.

"Heshima ya mwanamke ni kujishughulisha na kuingiza kipato chako mwenyewe, haijalishi umeajiriwa au kujiajiri. Haijalishi unauza Mama Ntilie, unajishughulisha na kilimo au biashara yoyote ile. Kikubwa heshimu unacho kifanya na usimpe nafasi mtu kudharau kinacho kuingizia rizki. Nawapa heshima wanawake wote ambao wanajishughulisha na wanajua uchungu wa kutafuta pesa, nawapenda", amesema Mkuu wa Wilaya Zainab.

Mkuu wa wilaya ya Pangani Bi. Zainab Abdallah amesema hayo ikiwa kama ni ishara ya kuelekea siku ya wanawake duniani ambayo huwa inaadhimishwa kila ifikapo Marchi 8 ya kila mwaka na kudai ataendelea kufanya hivyo mpaka kufika tarehe hiyo.

Mbowe Amshtumu Mkuu wa Mkoa wa Mbea Kuhusika Katika Kifungo cha Sugu

0
0
Mbowe Amshtumu Mkuu wa Mkoa wa Mbea Kuhusika Katika Kifungo cha Sugu

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mhe. Freeman Mbowe amedai kuwa hukumu ya kesi ya Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘SUGU’ ilipangwa hotelini siku 4  kabla ya mahakama kutoa hukumu.

Mhe. Mbowe amesema kuwa suala hilo lilipangwa na hata Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amosi Makala alilijua hilo kuwa SUGU atafungwa huku akimtuhumu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amosi Makala kuhusika.

“Hukumu ya SUGU ilifahamika na ilipangwa hotelini, kwamba Sugu anafungwa miezi mitano tulipata taarifa hizo siku 4 kabla. Na kwamba polisi walikusanywa mkoa mzima wa Mbeya, Mkoa mzima wa Songwe, watu wa usalama wa taifa wakajazwa Mbeya kukabiliana na presha ya wananchi ni jambo liliratibiwa. Mkuu wa Mkoa wa Mbeya anauhusika na anajua jambo hili, Amosi Makala,”amesema Mhe. Mbowe leo Jumanne kwenye mkutano wake na Waandishi wa Habari uliofanyika katika Ofisi za makao makuu Jijini Dar es salaam .

Kwa upande mwingine Mhe. Mbowe amesema kuwa CHADEMA hawaingilii maamuzi ya mahakama bali wanawasema baadhi ya watendaji wa mahakama wanaotumika kisiasa.

“Tunaiheshimu sana mahakama, Muhimili wa mahakama ndio muhimili ambao unasaidia wa Kuregulate nchi, lakini mahakimu mmoja mmoja wanapotumika ndio wanaichafua mahakama na wanalichafua taifa,“amesema Mbowe.

Serikali Kutoa Chanjo ya Shingo ya Kizazi kwa Wasichana 614,734 wa Miaka 14

0
0
Serikali Kutoa Chanjo ya Shingo ya Kizazi kwa Wasichana 614,734 wa Miaka 14
Serikali inatarajia kutoa chanjo kwa wasichana 614,734 wenye umri wa miaka 14 nchini ili kuwakinga na saratani ya shingo ya kizazi.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema hayo leo Februari 27,2018 katika mkutano wa wadau wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi.

Mkutano huo umewashirikisha viongozi wa dini na wadau wa sekta ya afya.

Ummy amesema Serikali itaanza kuchanja wasichana wa umri huo ambao hawajaanza vitendo vya kujamiiana waliozaliwa kati ya mwaka 2003 na 2004.

Amesema kutokana na mazingira ya upatikanaji wa chanjo hiyo na gharama kuwa kubwa, wataitoa kwa wasichana wenye miaka 14.

Ummy alisema ilipaswa kutolewa kwa wasichana wa kati ya miaka 9 hadi 14.

“Gharama ni Sh30,000 kwa kila msichana wakati Sh5.5 milioni hutumika kumtibu mgonjwa mmoja wa saratani katika Taasisi ya Ocean Road," amesema Waziri Ummy.

Mfalme Morocco Afanyiwa Operesheni ya Moyo

0
0
Mfalme Morocco Afanyiwa Operesheni ya Moyo

Mfalme Mohammed VI wa Morocco Jumatatu amefanyiwa operesheni ya moyo katika kliniki ya Paris, Ufaransa baada ya mapigo ya moyo kutokuwa ya kawaida, timu yake ya matibabu ilitangaza.

Madaktari hao katika taarifa, wamesema mfalme huyo mwenye umri wa miaka 54 alipata dalili za kusumbuliwa na moyo Januari 20.

"Tiba ya kuondoa mapigo yasiyo ya kawaida," au mrindimo usio wa kawaida ilifanyika kwa ufanisi kurejesha mapigo ya moyo ya kawaida.

Mfalme Mohammed, ambaye anatarajiwa kurejea kwenye shughuli zake za kawaida baada ya kipindi cha kupumzika kilichoamriwa na madaktari wake, ametawala Morocco tangu Julai 1999 alipofariki baba yake Mfalme Hassan.

Aidha, Septemba mwaka jana alifanyiwa operesheni ya jicho jijini Paris.

Mbowe, Viongozi Chadema Watinga Kituo Kikubwa cha Polisi

0
0
Mbowe, Viongozi Chadema Watinga Kituo Kikubwa cha Polisi
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na viongozi wengine wa chama hicho wanakwenda kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mchana Jumatatu Februari 27, 2018 Mbowe amesema wanakwenda kuripoti kuitikia wito wa Polisi.

Amesema katibu mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji hatakwenda kwa kuwa yupo nje ya nchi na atakaporejea atakwenda kwa kuwa hawana sababu ya kugoma.

Februari 20,2018 Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam iliagiza kukamatwa viongozi saba waandamizi wa Chadema akiwamo Mbowe.

Wito huo ulikuja siku chache baada ya tukio la kuuawa kwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini.

Akwilina aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa ndani ya daladala eneo la Mkwajuni, Kinondoni jijini Dar es Salaam wakati polisi wakiwatawanya wafuasi wa Chadema waliokuwa wakienda ofisi za mkurugenzi wa Halmashauri ya Kinondoni kudai viapo vya mawakala wao.

Viongozi wengine mbali ya Mbowe na Dk Mashinji ni naibu makatibu wakuu, John Mnyika (Bara) na Salum Mwalimu (Zanzibar).

Pia, wamo mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Halima Mdee; mwenyekiti wa Kanda ya Serengeti, John Heche na Esther Matiko ambaye ni mweka hazina wa Bawacha.

Mdee, Matiko, Heche na Mnyika walisharipoti awali na walitakiwa kurejea kituoni leo. Viongozi wengine waliwakilishwa na wanasheria.

Mbowe akizungumza na waandishi wa habari amesema wana taarifa kuwa watakamatwa na kwamba kuna mpango wa kubambikiziwa kesi.

Nondo za Azamu Zarejea Mazoezini Tayari kwa Ajiri ya Kuivaa Sigida United

0
0
Nondo za Azamu Zarejea Mazoezini Tayari kwa Ajiri ya Kuivaa Sigida United
Wachezaji wawili wa Azam FC, Nahodha Himid Mao ‘Ninja’ na mshambuliaji Wazir Junior, wamerejea rasmi mazoezini jana baada ya kukosekana dimbani kwa muda mrefu wakiuguza majeraha yanayowakabili.

Himid alikuwa akisumbuliwa na maumivu chini ya goti la mguu wake wa kulia huku Junior akikabiliana na tatizo kwenye kifundo chake cha mguu wa kulia, na tayari nyota hao wameanza kupata nafuu na sasa wanamalizia programu ya mazoezi mepesi kabla ya kuruhusiwa kurejea rasmi katika ushindani.

Nyota hao wamerejea wakati kikosi cha Mabingwa hao wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA Kagame Cup) kikijiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) dhidi ya Singida United, utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex Jumamosi hii saa 1.00 usiku.

Junior anayetakiwa kufanya programu hiyo ya mazoezi mepesi kwa muda wa wiki moja, alisema anamshukuru Mungu kurejea tena dimbani huku akikiri kuwa ‘amemiss’ kucheza mpira.

Kikubwa ni kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kurudi tena na nitaendelea kujituma kama ilivyokuwa awali kutokana na majeruhi haya ndo ilikuwa hivyo lakini tutapambana kama ilivyokuwa mwanzo, nimeumiss sana mpira nimemiss sana kucheza mpira na kuonyesha vile mashabiki wanataka.

Lakini naamini kwa rehema za mwenyezi Mungu tutakaporejea tena basi mashabiki watafurahia vile walivyokuwa wakivisubiria, alisema Junior

Mchezo huo unatarajia kuwa mkali na wa aina yake kutokana na ushindani wa timu hizo uliokuwa kwa siku za hivi karibuni, tokea Singida United irejee Ligi Kuu msimu huu, ambapo katika mtanange wa mzunguko wa kwanza uliofanyika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.

Mbali na kukutana katika ligi, pia mwanzoni mwa mwaka huu zilikipiga kwenye nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi, ambalo Azam FC imelitwaa, licha ya matajiri hao wa viunga vya Azam Complex kukutana na upinzani mkali, walifanikiwa kushinda bao 1-0, lililowekwa kimiani kiufundi na Shaaban Idd.

Ushindi wa Azam FC kwenye mchezo huo utaifanya kuzifukuzia timu mbili za juu, Yanga iliyo na mchezo mmoja mkononi ikiwa nafasi ya pili kwa pointi 37 na Simba ambayo ipo kileleni kwa pointi 45, pia itaipa nafasi ya kuongeza pengo la pointi dhidi ya timu hiyo kutoka Singida, kwa sasa zikipishana pointi moja kwenye nafasi ya tatu na nne, Azam FC ikiwa nazo 35 na Singida 34.

Muhimbili Wafanya Upasuaji Maalumu wa Mgongo

0
0
Muhimbili Wafanya Upasuaji Maalumu wa Mgongo

Madaktari bingwa wa Taasisi ya Tiba Mifupa Muhimbili (Moi) kwa kushirikiana na madaktari wa Hospitali ya BLK India leo wamefanya upasuaji maalumu wa mgongo kwa kutumia matundu (minimal invasive spine surgery) kwa mgonjwa aliyedhoofika uti wa mgongo.

Upasuaji huu umefanywa kwa mafanikio na jopo la madaktari bingwa wanne ambao wameongozwa na Daktari bingwa wa upasuaji wa mgongo, Profesa Joseph Kahamba wa Moi na mtaalamu wa upasuaji wa mgongo kwa njia ya matundu, Dk Puneet Girdhan kutoka hospitali BLK India ambapo wamekamilisha upasuaji huo kwa saa nne.

Akizungumza wakati wa upasuaji huo, Profesa Kahamba amesema unamwezesha mgonjwa kupona kwa muda mfupi, kutopata jeraha kubwa la mgongo na kutoongezewa damu.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moi, Dk Respicius Boniface amesema wao na Hospitali ya BLK ya India walianzisha ushirikiano mwaka 2016 na hii ni mara ya pili kwa wataalamu kutoka hospitali hizo kufanya upasuaji kwa kushirikiana.

"Pamoja na upasuaji huu, tumeanzisha huduma za upasuaji wa magoti kwa njia ya matundu (athroscopy) ambapo tayari zaidi ya wagonjwa 300 wameshafanyiwa kwa ufanisi mkubwa na wagonjwa wengine wengi wanaendelea kunufaika zaidi," amesema.

Amesema kutokana na mabadiliko ya teknolojia ya matibabu , upasuaji wa kupanua njia za mishipa ya fahamu na kuimarisha uti wa mgongo kwa nyenzo za kisasa umeshika hatamu na Moi inafanya mabadiliko makubwa ili kuendana na teknolojia mamboleo kutoa huduma.


Jerry Muro Akoshwa na Kasi ya Okwi "Kwangu Mimi Okwi Ndiye Mchezaji Bora Chirwa Hawezi Mfikia Okwi"

0
0
Jerry Muro Akoshwa na Kasi ya Okwi "Kwangu Mimi Okwi Ndiye Mchezaji Bora Chirwa Hawezi Mfikia Okwi"
Aliyewahi kuwa Afisa Habari wa klabu ya Yanga, Jerry Muro, ameeleza mtazamo wake wa kuwa nani anaweza kuwa mfungaji bora katika msimu huu wa Ligi Kuu Bara.

Muro amesema anampa nafasi kubwa mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi, kutokana na kiwango kizuri ambacho amekuwa akikionesha akiwa na Simba.

Mbali na hilo, Muro pia amemtaja mchezaji wa Yanga, Obrey Chirwa kuwa hawezi kumfikia Okwi, kwani kiwango chake si kama cha mwenzake.

Muro amesema Chirwa amekuwa akigoma kila wakati kuichezea hata timu yake, hivyo hampi na nafasi ya kuchuana na Okwi na akaenda mbali kwa kusema hastahili kulinganishwa naye.

"Kwangu mimi Okwi ndiye mchezaji bora kwa sasa, hauwezi ukamlinganisha na Chirwa ambaye amekuwa akigoma hata kuichezea Yanga, Okwi ni ''Real Proffesional" hivyo hawezi kufikiwa na Chirwa katika mbio za ufungaji bora" alisema Muro.

Okwi mpaka sasa amefikisha mabao 16 katika mechi 19 alizocheza msimu huu, wakati Chirwa ana mabao 11.

Polisi DR Congo Ahukumiwa Kifungo Cha Maisha Jela Kwa Kuwapiga Risasi Waandamanaji

0
0
Mahakama kuu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, imemuhukumu kifungo cha maisha askari polisi aliyewafyatulia risasi waandamanaji wanaompinga rais wa nchi hiyo Joseph Kabila.

Polisi huyo ambaye aliwapiga risasi za moto waandamanaji wawili na kuwauwa papo hapo siku ya Jumapili Februari 25, 2018. aliibua hisia kali kwa raia wa Congo baada ya video yake kusambaa mitandaoni.

Waumini wa kanisa Katoliki wakiongozwa na viongozi wao waliandamana katikati ya mji wa Kinshasa wakishinikiza rais Joseph Kabila ang’atuke madarakani.

Kwa mujibu wa mtandao wa Frontline Defenders, Shirika ambalo linafanya kazi chini ya mwavuli wa Haki za Binadamu limeripoti kuwa mpaka sasa zaidi ya watu 35 wanaoandamana kushinikiza Rais Kabila kujiuzulu wameuawa na Jeshi la polisi nchini DR Congo.

Hata hivyo haki za binadamu bado wanadai hukumu hiyo haijatenda haki sawasawa kwani imewaacha wakuu wa Jeshi la polisi.

Chanzo: Frontline Defenders

Jeshi la Polisi Lawashikilia Watu Zaidi ya Kumi wa Mauaji ya Diwani wa Chadema

0
0
Jeshi la Polisi Lawashikilia Watu Zaidi ya Kumi wa Mauaji ya Diwani wa Chadema
Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linawashikiliwa watuhumiwa zaidi ya 10 wa mauaji ya aliyekuwa diwani wa Chadema, Kata ya Namwawala Wilaya ya Kilombero, Godfrey Lwena.

Akizungumza na MCL Digital leo Februari 27, 2018 Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Ulrich Matei amesema watuhumiwa hao wanashikiliwa kwa uchunguzi na upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani.

Lwena aliuawa na watu wasiojulikana kwa kukatwa na mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake akiwa nyumbani kwake Februari 22, 2018.

Matei amesema kwa sasa majina ya watuhumiwa hayo yanahifadhiwa ili kutoharibu uchunguzi, na kwamba yatawekwa wazi baada ya upepelezi kukamilika.

Awali, katika taarifa yake kwa nyombo vya habari kamanda Matei amesema mauaji hayo yanatokana na kisasi kufuatia kifo cha mkazi wa kata hiyo, Kennan Haule aliyeuawa na watu wasiojulikana mwanzoni mwa mwaka 2016.

Amesema mtu huyo ameuawa kufuatia mgogoro wa shamba uliopo kati ya wananchi na Bodi ya Sukari ambapo Lwena alinukuliwa akiwaambia wananchi kuwa Haule asipokufa hawatapata haki yao na baada ya siku kadhaa aliuawa.

Amebainisha kuwa eneo hilo lina migogoro ya muda mrefu ya mashamba na watu wengi wameuawa katika mazingira yanayofanana.

 “Tunaendelea na uchunguzi wa kina katika eneo lile la Namwawala na kata za jirani ili kubaini hao wanaoendesha haya mauaji na wote watachukuliwa hatua za kisheria,” amesema  Matei.

Hii Hapa Ratiba Mpya ya Simba na Yanga

0
0
Hii Hapa Ratiba Mpya ya Simba na Yanga
Shirikisho la soka nchini limebadili tena ratiba ya ligi kuu soka Tanzania Bara mara hii ikihusisha michezo ya timu za Simba na Yanga kusogezwa mbele na mwingine kurudisha nyuma.


Kwa upande wa mchezo wa Simba SC dhidi ya Stand United uliotakiwa kuchezwa jumapili ya Februari 4, umerudishwa nyuma kwa siku mbili hadi Ijumaa Februari 2, ukipigwa katika uwanja wa taifa Dar es salaam.

Mchezo huo umerudishwa nyuma ili kuipa nafasi klabu ya Simba kujiandaa na mchezo wake wa hatua ya kwanza kombe la Shirikisho dhidi ya Al Masry ya Misri utakaopigwa Februari 7.

Kwa upande wa Yanga mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar uliokuwa uchezwe Februari 3 kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro umepelekwa mbele na tarehe yake itatajwa hapo baadae.

Simba inaongoza ligi ikiwa na alama 45 kwenye mechi 19, huku wapinzani wao Yanga wakiwa katika nafasi ya pili na alama 37 kwenye michezo 18. Yanga kesho itakuwa ugenini kucheza na Ndanda FC kwenye mchezo wa ligi kuu.

Usain Bolt Atapata Fursa ya Kuchezea Soka Uwanja wa Manchester United

0
0
 Usain Bolt Atapata Fursa ya Kuchezea Soka Uwanja wa Manchester United
Bingwa wa Olimpiki Usain Bolt hatimaye atapata fursa ya kuchezea soka katika uwanja wa Manchester United wa Old Trafford.

Mshindi huyo wa dhahabu mara nane katika Olimpiki atakuwa nahodha wa timu ya pamoja na watu mashuhuri na wanasoka ambayo itashiriki mechi ya Soccer Aid ambayo itaandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Watoto (Unicef) mnamo 10 Juni.

"Ni ndoto yangu kufanikiwa kama mchezaji wa soka ya kulipwa. Kucheza dhidi ya baadhi ya wachezaji nyota, hilo litakuwa jambo la kufurahisha sana," raia huyo wa Jamaica amesema.

Manchester United wameandika kwenye Facebook: "Inafanyika hatimaye ... Usain Bolt ataonyesha ustadi wake katika kusakata kambumbu katika Old Trafford majira yajayo ya joto #SoccerAid!

Usain Bolt kwa chati ya sekunde 9.58
Robbie Williams atakuwa nahodha wa timu pinzani kutoka England wakati wa mechi hiyo.

Usain awali amezungumzia nia yake ya kutaka kucheza soka ya kulipwa baada yake kustaafu riadha mwaka jana.

Wikendi, aliandika ujumbe wa utani kwenye Twitter - ambao ulizua uvumi sana - akidokeza kwamba alikuwa amejiunga na klabu fulani.

"Robbie na timu yake ya England wawe macho, kwani haitakuwa rahisi kwao," amesema Usain, na kuongeza kwamba amepanga "kitu maalum cha kusherehekea" timu yake ikishinda.

Bolt, 31, ni shabiki wa Manchester United, na wakati mmoja alipiga simu kwenye runinga ya klabu hiyo, MUTV, bila kutarajiwa.

"Nimekuwa nikisemamuda mrefu kwamba ninataka sana kufanikiwa katika mchezo wa timu kwa sababu uwanjani ni bidii ya mtu binafsi," alisema wakati huo.

"Huwa najiimarisha upesi na kufahamu ninafaa kufanya nini punde ninapopata kazi. Ninapopata maagizo, huyafuatilia vyema sana," alisema.

Mechi hiyo ya Soccer Aid itawaleta pamoja watu mashuhuri na wachezaji nyota wa zamani wa soka.

Mechi hiyo, ambayo huchezwa kila miaka miwili kufikia sasa imechangia kuchangisha jumla ya £24 milioni tangu kuzinduliwa kwake 2006.

Mechi hiyo awali imewashirikisha wachezaji wa zamani kama vile Maradona, Alan Shearer na Ronaldinho wakicheza dhidi ya watu mashuhuri kama vile Mark Wright, Jack Whitehall na Olly Murs.

Will Ferrell, Gordon Ramsay, Mike Myers na Craig David pia wamewahi kucheza.

"Kutwaa tena taji hili kwa niaba ya England litakuwa jambo zuri sana Usain akiongoza Soccer Aid World XI (Timu ya Dunia)," alisema Robbie Williams, ambaye ni mwanzilishi mwenza wa Soccer Aid.
.
Viewing all 104427 articles
Browse latest View live




Latest Images