Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104747 articles
Browse latest View live

Wajawazito Ghana Watumia Vidonge vya Kuwachubua Ngozi Watoto Tumboni

$
0
0
Wajawazito Ghana Watumia Vidonge vya Kuwachubua Ngozi Watoto Tumboni
Wanawake nchini Ghana wameonywa kutotumia dawa za kujichubua ilikubadilisha ngozi ya watoto kuwa nyeupe wakati bado wako tumboni. 

Wataalam wa afya wanasema dawa hizo haramu zinapelekea madhara ya uzazi ikiwemo viungo vya ndani vya mtoto kuharibika.

Mamlaka ya Vyakula na Dawa Ghana (FDA) imesema utumiaji ya vidonge vya Glutathione ni hatari ikiongezea kuwa inataka " umma ifahamu kuwa hamna dawa zilizoruhusiwa na FDA aina ya vidonge vya kuchubua ngozi ya mtoto aliye tumboni"

Vitendo vinashamiri nchini Ghana, kwa mujibu wa FDA, mara nyingi vidonge vinaingizwa kinyemela ndani ya mizigo kwa viwango vikubwa kupitia viwanja vya ndege.

Polisi na vikosi vya usalama wanafanya kazi pamoja kuwashika na kuwashtaki makampuni na watu binfsi watakaokuwa na vidonge visivyoruhusiwa.

Korea Kaskazini 'Inaisaidia Syria na Silaha za Kemikali'

$
0
0
Korea Kaskazini 'Inaisaidia Syria na Silaha za Kemikali'
Korea Kaskazini imekuwa ikiwatumia vifaa Syria ambavyo vinaweza tumika katika kutengeneza silaha za kemikali, ripoti ya chombo cha habari Marekani imesema kikinukuu ripoti kutoka Umoja wa Mataifa.

Kwa mujibu wa ripoti ya UN ambayo haijatolewa, wataalam wa bakora Pyongyang wameonekana katika viwanda vya kutengenezea silaha nchini Syria, gazeti la New York Times imesema.

Shutuma hizo zinakuja baada ya ripoti mpya ya utumiaji wa gesi ya chlorine na vikosi vya Syria, shutuma hizo zimekanushwa na serikali.

Korea Kaskazini ipo chini ya vikwazo vya kimataifa sababu ya programu yao ya nuklia.


Vifaa hivyo vinaripotiwa kupatikana kiwizi na kutumwa Syria na Korea Kaskazini vikiwemo vigae venye uwezo wa kuzuia joto na tindi kali mwingi na vipima joto. Vigae vinasemekana kutumika katika kujenga majengo ambapo silaha za kemikali zitatengenezwa.

Inasemekana wamtumiwa makumi ya mizigo ndani ya miaka kadha.

Gazeti hilo linasema, taasisi ya utafiti ya maswala ya sayansi ya Syria inasemekana kuwalipa Korea Kaskazini kupitia makumpuni bandia.

Serikali ya Syria imeripotiwa kuiambia Umoja wa Mataifa kuwa raia wa Korea Kaskazini waliopo Syria ni makocha na wanariadha tu.

Syira iliungana na mkutano wa silaha za kemikali na kukubali kuteketeza silaha hizo mwaka 2013 baada ya shambulio lililotumia gesi ya sarin na kuwaua mamia ya watu Ghouta.

Tangu mwaka huo, imeshutumiwa kwa kutumia silaha hizo marufuku mara kwa mara katika vita hiyo ya wenyewe kwa wenyewe.

Aliyemuhukumu Sugu Achukua Likizo

$
0
0
Aliyemuhukumu Sugu Achukua Likizo
Hakimu Michael Mteite aliyemhukumu kifungo cha miezi mitano jela mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ameanza likizo jana.

Mteite, ambaye ni Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya, alitoa hukumu hiyo juzi kwa Sugu pamoja na katibu wa Chadema Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga baada ya kuwatia hatiani kwa kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli.

Sugu na Masonga walitoa kauli hiyo Desemba 30 mwaka jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.

Hakimu huyo alipopigiwa simu jana na mwandishi wa Mwananchi aliyetaka kujua kuhusu uwepo wake likizo, kabla hata ya kuelezwa hilo alimtaka kuwasiliana na Msajili wa Mahakama.

Hata alipotumiwa ujumbe wa maneno (sms) kujulishwa kwamba msajili alishalizungumzia hilo na kilichohitajika ni kauli yake, hakujibu.

Awali, akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, naibu msajili mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, George Herbert alisema Hakimu Mteite amechukua likizo kwa mujibu wa sheria na utaratibu wa utumishi kama ilivyo kwa watumishi wengine wa umma pindi muda wao unapokuwa umefika.

“Ni likizo yake ya mwaka… na amechukua likizo kama mtumishi mwingine ambaye anaweza kuchukua likizo muda wake unapokuwa umefika. Kimsingi ni kwamba amechukua likizo ya muda wa wiki tatu kuanzia leo (jana) na ni likizo huwa anachukua kila mwaka muda unapokuwa umefika.

“Hivyo suala la kusema kwamba eti amechukua likizo kwa sababu ya hukumu aliyoitoa jana (juzi) haina msingi wowote, bali ni haki yake kuchukua likizo hiyo. Inapofika Februari kila mwaka huchukua likizo yake na huwa inategemea majukumu anayokuwa amepangiwa kuyafanya,” alisema naibu msajili.

Taarifa ya kusudio la rufaa

Akizungumzia taarifa ya kusudio la mawakili wa Sugu na Masonga kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo na kuomba dhamana kwa wateja wao, Naibu Msajili Mfawidhi, Herbert alisema baada ya hukumu kutolewa juzi, mawakili hao walianza mchakato wa kukata rufaa na siku hiyohiyo walipatiwa nakala ya hukumu.

Alisema kilichokuwa kikisubiriwa hadi jana ni nakala za mwenendo wa kesi ili kukamilisha utaratibu wa kukata rufaa.

Herbert alisema kukata rufaa ni haki ya mlalamikaji anapoona hajaridhishwa na hukumu.

Alisema, “Kinachofanyika ni kuhakikisha wanapatiwa mwenendo wa shauri na hilo lipo hatua za mwisho kukamilika kwa sababu wameshapata nakala ya uamuzi ulitolewa jana ileile,” alisema.

Mke wa Sugu, Masonga walonga

Happy Msonga ambaye ni mke wa Sugu na Grace Mallya wa Masonga wakizungumza kwa nyakati tofauti walisema wanajua fika hukumu ilitolewa kwa mrengo wa kisiasa, hivyo hawakubaliani na adhabu waliyopewa waume wao.

Grace alisema, “Ukiachilia mbali ndani ya familia tu, lakini wale watu wa nje wanavyo ‘comment’ unaona kabisa hakuna haki iliyotendeka.”

Alisema anazidi kumuombea mume wake aendelee kuwa na nguvu na imara zaidi katika kipindi chote anachopitia kwa kuwa ana imani hayo ni mapito na yatakuwa na mwisho ambao huwa ni ukombozi katika harakati za kisiasa.

Happy alisema walitarajia kilichotokea kwa kuwa walishaona dalili mwanzoni baada ya hakimu kukataa kujitoa wakati washtakiwa walishamkataa.

Alisema wana imani na mawakili, Peter Kibatala na Faraji Mangula kwamba watafanikiwa kukata rufaa kwa ajili ya uamuzi mwingine. Alisema kwa sasa wanawaombea kwa Mungu, Sugu na Masonga waendelee kuwa na afya njema.

Wakati Sugu akitumikia adhabu ya kifungo, mama yake mzazi Desderia Mbilinyi imeelezwa na familia kuwa ni mgonjwa.

Wasemavyo wapigakura Mbeya

Akizungumzia hukumu iliyotolewa kwa Sugu na Masonga mkazi wa Uyole, Bahati Longopa alisema Mahakama imetenda haki kulingana na vifungu vya sheria. Hata hivyo, alisema ni vyema ingetoa hukumu ya kifungo cha nje ili mbunge huyo aweze kuwatumikia wananchi katika shughuli za maendeleo.

Mkazi wa Sabasaba, John Mbika alisema ni mapema kuzungumzia hilo hivyo ni vyema Mahakama ikaachiwa iendelee na kazi.

Mkazi wa Nonde, Rehema Mwanjonde alisema Mahakama imetenda haki kwa mujibu wa sheria lakini akaitaka Chadema ikate rufaa ili Sugu aweze kuwatumikia wananchi na kusimamia shughuli za maendeleo.

Hoja sita za Lissu

Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu akizungumzia hukumu hiyo katika waraka alioutoa juzi aliibua hoja sita.

Lissu anayeendelea na matibabu nchini Ubelgiji katika hoja ya kwanza alisema hukumu hiyo si mwisho wa mjadala mahakamani na kwamba bado kuna fursa na haki ya rufaa Mahakama Kuu na ikibidi Mahakama ya Rufaa.

Pili, alisema hukumu hiyo haina maana Sugu atakaa gerezani muda wote, kwamba kuna haki ya dhamana (pending appeal) na kubainisha kuwa hivyo ndivyo walivyofanya kwa viongozi na wanachama wengi wa Chadema.

Katika hoja ya tatu, Lissu ambaye pia ni mwanasheria mkuu wa Chadema alisema hukumu ya Sugu haina athari yoyote kwa mbunge huyo kuhusu kugombea tena au kupoteza ubunge wake kwa sababu Katiba inaweka masharti ya kifungo cha miezi sita au zaidi na kwa makosa ya utovu wa uaminifu.

“Uchochezi au kutoa lugha ya matusi sio makosa ya utovu wa uaminifu,” alisema.

“Nne, pamoja na kwamba sijaona nakala ya hukumu, adhabu ya kifungo bila faini kwa kosa la kwanza ni kinyume na ‘sentencing principles’. Hii ni mojawapo ya hoja zetu zilizoshinda katika kesi ya Peter Lijualikali (mbunge wa Kilombero) Mahakama Kuu mwaka jana,” alisema.

Tano, Lissu alisema hata kama Sugu atakaa gerezani muda wote huo (wa miezi mitano), hukumu za kesi za kisiasa kama hiyo hazijawahi kuwapunguzia heshima wapigania haki popote duniani.

Jambo la sita alisema, “Naunga mkono pendekezo la Zitto (Kabwe-mbunge wa Kigoma Mjini) kwamba wabunge wetu wote warekodi maneno aliyofungiwa nayo Sugu na kuyaweka mitandaoni ili watukamate na sisi pia, mpaka wakimbie wenyewe au watukamate na kutufunga wote.”

Kauli ya Manara Kuhusu Hali ya Bocco

$
0
0
Kauli ya Manara Kuhusu Hali ya Bocco
Mshambuliaji wa klabu ya soka ya Simba SC, John Bocco ameelezwa kupona majeraha aliyoyapata kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mwadui FC na muda wowote ataanza kucheza kama kocha atampanga.

Afisa habari wa Simba Haji Manara amethibitisha hilo wakati akijibu maswali ya mashabiki wa klabu hiyo waliokuwa wanataka kujua hali ya nahodha huyo wa Simba kupitia ukurasa wake wa Instagram.

''Niwajuze tu kuwa hali ya Bocco anaendelea vizuri na yupo tayari kucheza kama kocha atampanga'', Manara alimjibu moja ya mashabiki waliouliza.

Aidha Manara ameongeza kuwa majeruhi pekee aliyebaki kwenye kikosi cha Simba ni Haruna Niyonzima ambaye hivi karibuni alipelekwa India kwaajili ya matibabu na Manara ameongeza kuwa naye yupo mbioni kurejea.

Majeruhi wengine wa muda mrefu ndani ya kikosi cha Simba ambao tayari wameanza mazoezi mepesi ni mlinda mlango Said Nduda na mlinzi Salim Mbonde ambao wote wamesajiliwa msimu huu wakitokea Mtibwa Sugar.

Kilichosababisha Mavunde na Biteko kufanya ziara mkoani Shinyanga

$
0
0
Kilichosababisha Mavunde na Biteko kufanya ziara mkoani Shinyanga
Naibu Waziri wa wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde jana 27 Februari 2018 wametinga Mkoani Shinyanga kwa ziara ya kikazi ya siku moja ambapo pamoja na mambo mengine watatembelea mgodi wa EL-Hillal Minerals Ltd.

Mhe Biteko ametinga Mkoani Shinyanga akitokea ziarani Mkoani Tabora huku Mhe Mavunde akiwa ametokea Mkoani Mwanza ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi mwaka 2015-2020.

Wakati Mhe Mavunde akiwa kwenye ziara ya kukagua Viwango vya Kazi na Usajili wa waajiri kwa mfuko wa fidia wa wafanyakazi (WCF) ni sehemu ya kukagua Viwango vya Kazi na kufuatilia utekelezaji wa agizo la Mhe Jennister Mhagama ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira ambaye aliwataka waajiri wote nchini wawe wamejisajili kwenye mfuko wa Fidia wa Wafanyakazi kabla au ifikapo tarehe 30 Septemba 2017.

Alisisitiza waajiri kujisajili na mfuko wa fidia kwa wafanyakazi kwani kutofanya hivyo Kwa mujibu wa Kifungu cha 71(4) atashitakiwa Mahakamani na akikutwa na hatia adhabu yake ni faini isiyozidi TSh 50,000,000 au kifungo cha miaka mitano au vyote kwa pamoja.

Wakati huo huo Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko alisisitiza umuhimu wa wachimbaji wadogo nchini kulipa kodi huku akieleza kuwa wachimbaji wanapaswa kujiunga kwenye vikundi kwani serikali imetenga maeneo mengine ambayo itatoa wataalamu kuyafanyia Utafiti ili kuimarisha uchimbaji nchini kwa wachimbaji wadogo kuwa wenye tija na hatimaye kuwafanya kutoka katika uchimbaji mdogo kufikia wa kati na hatimaye kuwa wachimbaji wakubwa.

Pia ameendelea kusisitiza juu ya Wamilili wa Leseni za Madini kote nchini, kutunza takwimu za gharama za uendeshaji wa shughuli zao za uchimbaji na kila Mwezi ziwasilishwe kwa Afisa Madini kwani kutokufanya hivyo wataingia katika mikono ya sheria kwa kulipa faini ya shilingi milioni 50 mpaka milioni 150 au kifungo cha mwaka mmpja jela.

Pia, Mhe Biteko alieleza dhamira ya ziara yake kuwa anapokuwa katika maeneo mbalimbali anawakumbusha wachimbaji nchini kufuata sheria na taratibu za nchi.

Tido Mhando Asomewa Maelezo ya Awali Mahakamani

$
0
0
Tido Mhando Asomewa Maelezo ya Awali Mahakamani
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemsomea maelezo ya awali mkurugenzi mkuu wa zamani wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando anayekabiliwa na mashtaka matano likiwamo la matumizi mabaya ya madaraka.

Kabla ya kusomewa maelezo leo Februari 28,2018 mbele ya Hakimu Mfawidhi, Victoria Nongwa, Wakili wa Serikali Dismas Mganyizi, alimkumbusha mashtaka yanayomkabili Tido anayetetewa na wakili Ramadhani Maleta.

Baada ya kusomewa, Tido ambaye yuko nje kwa dhamana amekubali maelezo binafsi na kwamba alikuwa mkurugenzi mkuu wa TBC mwaka 2006 hadi 2010.

Amekubali kuwa alikuwa msimamizi wa shughuli za TBC lakini si zote.

Pia amekubali kutoa maelezo kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na kuwa alifikishwa mahakamani Januari 26,2018.

Tido amekana mashtaka yanayomkabili na upande wa mashtaka katika kesi hiyo utaanza kutoa ushahidi Machi 28,2018.

Anakabiliwa na mashtaka manne ya kutumia madaraka vibaya na moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh887.1 milioni.

Tido anadaiwa Juni 16,2008 akiwa Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), akiwa mkurugenzi mkuu wa TBC kwa makusudi alitumia madaraka yake vibaya kwa kusaini mkataba wa kuendesha na kutangaza vipindi vya televisheni kati ya TBC na Channel 2 Group Corporation (BV1) bila kupitisha zabuni kinyume cha sheria ya ununuzi, hivyo kuinufaisha BVl.

Katika shtaka la pili anadaiwa kutumia vibaya madaraka yake ikielezwa Juni 20,2008 alisaini makubaliano ya utangazaji wa digitali duniani kati ya TBC na BVl.

Tido katika shtaka la tatu anadaiwa Agosti 11,2008 na Septemba 2008 akiwa Dubai alitumia vibaya madaraka yake kusaini mkataba wa makubaliano ya ununuzi, usambazaji, kufunga vifaa vya usambazaji na mnara wa utangazaji kati ya TBC na BVI na kuifaidisha BVI.

Shtaka la nne, anadaiwa Novemba 16,2008 akiwa Dubai alitumia vibaya madaraka yake kusaini mkataba wa makubaliano ya kuendesha miundombinu ya utangazaji kati ya TBC na BVI na kuinufaisha BVI.

Tido katika shtaka la tano anadaiwa kati ya Juni 16 na Novemba 16,2008 akiwa Dubai aliisababishia TBC hasara ya Sh887.1 milioni.

Fatma Karume na Mtoto wa Chacha Wangwe Kufungua Kesi 10 Ikiwemo ya Kupinga Wakurugenzi Kusimamia Uchaguzi

$
0
0
Fatma Karume na Mtoto wa Chacha Wangwe Kufungua Kesi 10 Ikiwemo ya Kupinga Wakurugenzi Kusimamia Uchaguzi
TAASISI tatu zinazojihusisha na utetezi wa sheria na haki za binadamu, zitafungua jumla ya kesi 10 ndani ya miezi mitatu katika Mahakama Kuu ya Tanzania, kupinga zilichodai sheria kandamizi zinazominya demokrasia na uhuru wa kujieleza.

Taasisi hizo ni Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC).

Baadhi ya sheria ambazo zimeanza kupambana nazo kwa kufungua kesi ili zifanyiwe marekebisho, zimesema, ni Sheria ya Vyama vya Siasa, Sheria ya Jeshi la Polisi na Sheria ya Uchaguzi.

Wakizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, viongozi wa taasisi hizo walisema tayari wameshafungua kesi mbili katika Mahakama Kuu na kwamba kesi nane zitafunguliwa baada ya miezi miwili.

Walisema kesi hizo zimefunguliwa na wapiga kura wawili, Bob Chacha Wangwe na Allan Bhujo watakaowakilishwa na mawakili kutoka taasisi hizo tatu.

"Tayari tumeshafungua kesi mbili katika mahakama kuu, na kesi zingine nane tutazifungua miezi miwili ijayo na kufanya jumla ya kesi kuwa 10," alisema Fatma Karume kutoka TLS.

Akizungumza katika mkutano huo, Karume alisema wamejiandaa kuzipinga sheria hizo alizoziita kandamizi, kwa mustakabali wa Watanzania.

"Hatutakata tamaa kwenye hili," alisema Karume. "Tumeshuhudia vitendo vingi ndani ya nchi vinavyowanyima wananchi demokrasia na uhuru wa kujieleza.

"Hii ni kinyume na katiba na ndiyo maana tumeunganika kupinga sheria hizo kwa mustakabali wa taifa."

Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa LHRC, Anna Henga, alisema haki ya kukusanyika, kujieleza ni haki ya kila Mtanzania.

Atiwa Mbaroni kwa Tuhuma za Kumbaka Mtoto wa Miaka Minne

$
0
0
Atiwa Mbaroni kwa Tuhuma za Kumbaka Mtoto wa Miaka Minne
JESHI la Polisi mkoani Mwanza, linamshikilia Soli Mkanzabe (24), mkazi wa mtaa wa Nyegezi kwa tuhuma za kumnajisi mtoto wa miaka minne (jina limehifadhiwa) na kumsababishia majeraha na maumivu makali katika sehemu za siri.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna (DCP) Ahmed Msangi, katika taarifa aliyoitoa jana kwa vyombo vya habari, alisema mtuhumiwa alitenda kosa hilo juzi majira ya saa 10 jioni katika maeneo ya mtaa wa Password kata ya Nyegezi, Nyamagana mkoani hapa.

“Inasemekana mtuhumiwa alikuwa akiishi jirani na nyumbani kwao mtoto. Inadaiwa kuwa majira tajwa hapo juu, mtuhumiwa alifika nyumbani kwao mtoto na kumkuta akicheza na wenzake kisha alimwita waende wote chumbani kwake.

Mtoto alimfuata mtuhumiwa na kwenda naye chumbani na baadaye mtuhumiwa alifanyia mtoto ukatili wa kumbaka na kumsababishia maumivu makali katika sehemu za siri huku mtuhumiwa akimwonya mtoto kuwa asiseme kwa mtu yeyote juu ya jambo hilo,” alisema DCP Msangi katika taarifa hiyo.

Msangi alisema baada ya mtoto kufanyiwa ukatili huo, alikaa kimya bila kumwambia mtu yeyote hadi mama yake aliporejea kutoka kazini.

Kamanda Msangi alisema wakati mama yake akienda kumwogesha, ndipo alipogundua kuwa mtoto amefanyiwa unyama huo kisha alitoa taarifa kituo cha polisi.

Alisema baada ya kutoa taarifa, polisi walifanya ufuatiliaji wa haraka hadi eneo la tukio na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa.

Kutokana na kumkamata huko, DCP Msangi alisema polisi wako katika upelelezi na mahojiano namtuhumiwa na kwamba uchunguzi ukikamilika, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.

Kuhusu mtoto huyo, Msangi alisema alipelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana na kwamba hali yake inaendelea vizuri.

Treni ya Abiria Iliyokuwa Ikielekea Kigoma Yapata Ajari

$
0
0
Treni ya Abiria Iliyokuwa Ikielekea Kigoma Yapata Ajari
TRENI  ya abiria iliyokuwa ikisafiri kutoka Tabora kwenda Kigoma imeanguka mchana huu kati ya stesheni ya Malagarasi na Uvinza, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Ferdinand Mtui amethibitisha.  Hadi sasa hakuna kifo kilichothibitishwa wala idadi ya majeruhi, kamanda huyo ameahidi kutoa taarifa zaidi baadaye baada ya kufika eneo la tukio.

Kwa mujibu wa shuhuda wa Global Publishers ajali hiyo imetokea mchana huu Februari 28, 2018, baada ya mabehewa mawili ya mbele na kichwa chake kuacha njia na kuanguka.

NEC Yamjibu Mbowe Yamtaka Akasome "Hapaswi Kiongozi Kama Yeye"

$
0
0
NEC Yamjibu Mbowe Yamtaka Akasome "Hapaswi Kiongozi Kama Yeye"
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imefunguka na kudai malalamiko yaliyotolewa jana (Jumanne) na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe sio ya kweli bali yamejaa upotoshaji wa hali juu ambao haupaswi kufanywa na kiongozi kama yeye.


Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa tume hiyo, Kailima Ramadhani baada ya kupita siku moja tokea Mhe. Mbowe kuzungumza mbele ya waandishi wa habari kuwa Tume ya Uchaguzi iliwafanyia hujuma katika kutoka viapo vya Mawakala wao kwenye chaguzi ndogo za marudio Jimbo la Kinondoni na mambo mengine.

"Tume ya Taifa ya Uchaguzi haijibu malalamiko kwa matakwa ya mtu anavyotaka kujibiwa bali inajibu hoja kwa mujibu wa matakwa ya Katiba, Sheria, Kanunu na maadili ya uchaguzi na maelekezo yote ambayo yapo kwa mujibu wa sheria. Kama majibu ya tume hayakuwafurahisha CHADEMA, tume inasisitiza kuwa walijibiwa kwa matakwa ya sheria na katiba sio matakwa ya Mkurugenzi wa uchaguzi, Tume, Chadema au chama chochote cha siasa",   amesema Kailima.

Aidha, Mkurugenzi Kailima amesema Kanuni, Sheria, maelekezo na maadili ya uchaguzi yameweka utaratibu wa kushughulikia malalamiko na changamoto zinazotokea wakati wa uteuzi, kampeni ambako kuna kamati za maadili na jinsi ya kukata rufaa.

"Kwa masikitiko CHADEMA walitekeleza hatua moja tu katika vipengele hivyo wakati wa uchaguzi, kipengele walichotekeleza ni pale baadhi ya wagombea wao walipoenguliwa kugombea ndipo walifuata utaratibu kwa kuwasilisha rufaa kwa Tume ya Uchaguzi na tume ilipitia na ikawarudishia wagombea wao kwenda kugombea", amesisitiza Kailima.

Mkurugenzi Kailima ameendelea kufafanua

"CHADEMA walitaka wakati wa kampeni, Tume ifanye maamuzi kinyume cha maadili waliyoyasaini. Wakati wa kampeni kuna kamati za maadili ngazi ya jimbo ambayo mwenyekiti ni msimamizi wa uchaguzi na wajumbe ni kutokea vyama vyote vilivyosimamisha wagombea na ndio wanaofanya uamuzi. Chadema waliwasilisha malalamiko kwa tume badala ya kuwasilisha kwenye kamati hizo za maadili zinazosimamia malalamiko yote".

Kwa upande mwingine, Mkurugenzi wa Uchaguzi Kailima Ramadhani amemsihi Mbowe na chama chake wasome sheria za uchaguzi na kuzielewa na kumsisitizia kuwa tume ipo tayari kumpa elimu ya mpiga kura na kuzifahamu sheria hizo zake kwa mapana.

Lina Aitaja Idadi ya Wanaume Aliotoka Nao Kimapenzi Afunguka Walivyofaidi Penzi Lake

$
0
0
Lina Aitaja Idadi ya Wanaume Aliotoka Nao Kimapenzi Afunguka Walivyofaidi Penzi Lake
Msanii Linah Sanga ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake wa 'Same boy' akiwa ameshirikiana na msanii Recho amefunguka na kuweka wazi idadi ya wanaume ambao ametembea nao na kufaidi penzi lake.


Linah Sanga akiwa kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa live kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV amesema kuwa toka amekuwa Linah na watu kumtambua kama msanii ametoka jumla ya wanaume watano japo anadai kuwa kuna wanaume wengine ambao ametoka nao kimapenzi hawakumbuki.

"Kwa haraka haraka nishatoka kimapenzi na wanaume kama watano hivi toka watu wamenifahamu kama Linah, sina idadi kubwa sana japo siwezi kuwakumbuka wote wengine nimeshawasahau kabisa, kuna watu wana idadi kubwa ya watu wametembea nao sema tu ni kwa sababu si wasaniii" alisema Linah Sanga

Wabongo Kibongo Wamuombea Msamaha Daimond kwa Zari

$
0
0
Wabongo Kibongo Wamuombea Msamaha Daimond kwa Zari
Wakati rais wa WCB, Diamond Platnumz akiwa busy na maandalizi ya uzinduzi wa Wasafi Redio na Wasafi TV, mashabiki wa muimbaji huyo bado wanaendelea kumbembeleza aliyekuwa mama watoto wa muimbaji huyo, Zari The Bosslady arudishe moyo nyuma.

Zari na Diamond

Mfanyabiashara huyo wa kike machachari Afrika Mashariki alimuacha baba watoto wake, Diamond kwa madai amekuwa ni mwanaume ambaye amekuwa akimzalilisha na kumkosea heshima.

Katika siku ya wapendanao, Zari aliandika ujumbe mzito wakumuachana Diamond hali ambayo aliwashtuwa watanzania wengi hasahasa mashabiki wa Diamond.

Diamond mpaka sasa hajazungumza chochote juu ya hilo lililotokea, lakini mashabiki wake wameamua kumuombea msamaha muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri katika tasnia ya muziki.

Huu hapa chini ni ujumbe wa mashabiki hao kwa Zari waliouandika kupitia mtandao wa kijajii wa Instagram.

aminamoha10

Zari mrudie tu Diamond hakuwa na nia mbaya ndio maana ilikuwa hadharani sema midomo ya watu na media inatia sana chumvi ili miachane, angalia hata ile kumbatio Diamond alikuwa kama hana ushirikiano wa kutosha, mengine ni hali ya ubinadamu lazima yatokee. Wanaume wote nadhani ni sawa ila wanashangilia tu yawenzao, Hamna hata mmoja atakaesema hana mchepiko. Unakaa South yeye anakaa Dar lakini still anajiproud kwako kuwa ndio mke akupendae, usione nyumba hizi mnalaa wote kila siku but utasikia Leo hapa kesho kule ilimradi tafarani. Huwezi sema ukimwacha utakua mwenuewe si kweli, je uendako mwenzako kwa nini alikimbia? Anakuja kwako kwa nini? Zimwi likujualo halikuli likakwisha please think twice

amuru_tanzania

Please shemeji Zarinamond do not hesitate to say NO with a big NO, learn to say no in small letters, go back to your gentleman.

mrlv3462

U look so petty but mnapendeza xna ukiwa na baba watoto wako mond

sihakaadam

Acha ujinga ww, rudi kwa mwenzio muelewane mulee watoto wenu, mm naamini wanaume unawajua vizuri tu…. Cha msingi piga moyo konde rudi muelewane basi maisha yaende… Musiwape maneno wapambe nuksi…. Ujinga wala afi mtu

tiridentebe

Mamy naomba umsamehe jmn

paulinafaustin

Zari maisha ni safari ndefu sana hebu jaribu kutuliza akili yako utafakari kwa kina hata wazazi wetu walipitia mapito kama yako lakini walivumiliana mpaka hapa walipofikia kwahiyo maisha ya ndoa yanamisukosoko piga moyo konde ili muweze kulea watoto wenu kwa pamoja hakuna binadamu mkamilifu.

Majeruhi wa Risasi Maandamano ya Chadema Wapata Dhamana

$
0
0
Majeruhi wa Risasi Maandamano ya Chadema Wapata DhamanaLeo February 28, 2018 Watu watatu wanaodaiwa kuwa wafuasi Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na shtaka la kufanya mkusanyiko isivyo halali.

Hata hivyo, watu hao watatu wameunganishwa katika kesi ya wafuasi 28 wa CHADEMA ambao walifikishwa mahakamani hapo wiki iliyipita.

Washtakiwa hao watatu walisomewa kosa lao mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Godfrey Mwambapa na Wakili wa Serikali, Patrick Mwita.

Wakili Mwita aliwataja washtakiwa hao watatu kuwa ni Isack Ng’aga, Erick John na Aida Olomi.

Wakili Mwita amedai washtakiwa hao, March 8, 2018 wataunganishwa na wenzao 28, ambao walifikishwa mahakamani hapo wiki iliyopita.

Kwa pamoja wanadaiwa kuwa  February 16, 2018 huko Kinondoni katika eneo la Mkwajuni lililopo katika Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, walifanya mkusanyiko usio wa Halali kinyume cha sheria.

Inadaiwa kuwa mkusanyiko huo ulikuwa na nia ya kufanya uvunjifu wa amani na kusababisha Taharuki kwa wananchi.

Washtakiwa wote walikana shtaka hilo na wapo nje kwa dhamana kwa kila mshtakiwa kuwa na mdhamini mmoja ambaye alisaini ahadi ya Shilingi Milioni 1. 5 na wasitoke nje ya jiji la Dar es Salaam bila ya kuwa na kibali cha mahakama. Upelelezi bado haujakamilika. Kesi imeahirishwa hadi March 8,2018.

Jaji Mkuu Aitaka Serikali Kuishirikisha Mahakama

$
0
0
Jaji Mkuu Aitaka Serikali Kuishirikisha Mahakama
Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Hamis Juma ameishauri Serikali kuishirikisha Mahakama kwenye mipango yake ya uanzishaji wa maeneo mapya ya kiutawala ili kupunguza changamoto za upatikanaji wa haki kwa wananchi.


Akizungumza wakati wa ziara yake mjini Kigoma, Jaji Mkuu amesema mipango ya Serikali ya uanzishwaji wa Wilaya au Mikoa uzingatie pia uanzishwaji wa Mahakama na kwamba, Mikoa na Wilaya mpya ndizo zenye ukosefu wa Mahakama hali inayowafanya wananchi kufuata mbali huduma za Kimahakama.

Akitolea mfano wa Wilaya ya Uyui, Mkoani Tabora, Jaji Mkuu amesema, kutokana na Wilaya hiyo kuzunguka Mkoa, wananchi wake hulazimika kufuata huduma za Mahakama Kuu zilizopo umbali wa zaidi ya kilometa 377.

Amefafanua kwamba, kupitia Mpango wa Maboresho Mahakama itaanzisha Mahakama zinazotembea yaani Mobile Courts, kwenye maeneo yote yenye changamoto kama hizo kabla ya kujenga Mahakama kwa kuwa changamoto ya upatikanaji wa huduma za Kimahakama bado ni kubwa nchini.

JE Umehangaika na Matatizo ya Kimapenzi Kwa Muda Mrefu? Muone Shehe Chalo Atakutatulia Matatizo yako Kirahisi

$
0
0
JE umehangaika na matatizo haya kwa muda mrefu mtalamu Challo anayo dawa ya kuvuta mpenzi Je unasumbuliwa na mpenzi umeachwa na mpenzi au Mme mke na Bado unampenda na umejaribu sehemu nyingine Bila mafanikio njoo utatuliwe haraka na kundumisha ndoa yenu..

Umekimbiwa na mmeo mkeo au mpenzi na anaishi na mtu mwingine atarundi haraka kusafisha nyota mvuto wa mwili na biashara minguu kufa ngazi kuwaka moto ngiri tumbo kuunguruma na wakina Baba wasiojiweza katika tendo la uyumba kuchelewa kufika kileleni tunatibu Busha Bila oprasheni bali kwa kutumia vitabu vya dini

Tunatoa pete ya utajiri Bila mashariti mkufu wa bahati unauza Mali ya haindi unapoteza pesa kwenye biashara yako Bila kujua unataka kupandishwa cheo

Wasiliana na mtalamu Shehe Challo 0714006521

Hii Ndio Kazi ya Shanga Kiunoni Kwa Mwanamke Pamoja na Maana ya Rangi zake

$
0
0
Najua wengi mtakuwa mnafahamu rangi na maana zake lakini kwa wale wasiojuwa  ama wanaopenda kuvaa lakini wanajinunulia rangi yeyote huu ndo wakati mwafaka.

Wanaume wengi wanaopenda wanawake wao wavae shanga ili kusisimuana tu .Je mnafahamu zinamaanisha nini?....Karibu  tujifunze  pamoja.

Katika swala la mahaba shanga hutumika kusisimuana haswa pale utakapompata mwanaume anayejuwa kuzitumia vizuri na unaweza kuvaa hata kumi ukitaka .  Jana  niliguswa  sana na simulizi la rafiki yangu juu  ya  shanga, hivyo nikaona  boraniandike  na wengne wajue.Hii ni sehem ndgo ya simulizi  lake.

 "Nilikutana na boyfiriend wangu maeneo ya  Shycom …tukaelekea kwenye disko. Tulikuwa tunacheza madensi, halafu blues, ya Boyz to Men ikaanza kupigwa. Wenye disko walipunguza taa. Mimi na boyfriend wangu tukakumbatiana na kuanza kucheza Blues. Miili yetu iligusana na akaana kunipapasa taratibu kufuatana na beats za muziki. Nilifurahi sana. Akateremsha mikono yake kwenye kiuno changu. Alivyogusa  shanga zangu akawa kama mwili wake umekufa ganzi. Alisisimuka we! Akanishika kwa nguvu, niligundua kuwa ham yake ilikuwa juu....."


 Naamini utakuwa umejifunza kitu fulani  muhimu kutokana na simulizi hilo.Sasa turudi kwenye mada yetu.Kuna wengine wanananunua rangi kama pink, blue, gold hizi rangi hazina maana kwenye sita kwa sita ni urembo tu kupendezesha kiuno.

RANGI ZENYE MAANA PINDI UWAPO KITANDANI  NA MPENZI WAKO

Nyekundu:  ukimkuta mwanamke amevaa shanga ya rangi hii unatakiwa kuelewa kwamba mwanamke huyu yupo kwenye hedhi, kwahiyo wewe fanya mengine lakini sio kutumbukia unless yeye mwenyewe amekuruhusu na wewe uwe na uwezo wa kutumbukia hata akiwa kwenye hedhi (kitu ambacho kiafya akishauriwi).

Nyeupe:  ukimkuta mwanamke amevaa shanga nyeupe hiihumaanisha hana tatizo lolote litakalomfanya asikupe raha ya sita kwa sita, kwahiyo ukitaka tu muda wowote unapata.

Nyeusi: ukimkuta mwanamke amevaa rangi nyeusi hii humaanisha ya kwamba yupo tayari kukupa raha za sita kwa sita lakini uwanja wake haujakatwa majani, kwa hiyo chaguo ni lako kama unataka kutumia siku nzima kutafuta goli haya, ama kama utamsaidia kumkatia majani uwanjani vizuri zaidi ama kama huwezi yote basi mpe muda akate mwenyewe.

Kumlinda Mpenzi ni Sawa na Kulinda Samaki Baharini..Ukilinda Kigamboni Wenzako Wanavua Bagamoyo

$
0
0
Jamani wanawake wengine hawajielewi, hawaelewi jinsi mahusiano yalivyo complex.Ngoja niende direct tuende kwenye point. Mke wangu ana tabia ambayo hakuna mwanaume wa aina yoyote atamvumilia. Nimechoka sasa ni muda muafaka wa action najua iko siku atajuta kunifahamu.

Wote tunafanya kazi za kuajiriwa, hivyo tunatoka asubuhi tunarudi jioni, japo yeye anatangulia kurudi nyumbani. Sasa ana tabia ya kubeba kila umbea anaopata kutoka kwa mashosti zake na kuja kunisimulia mimi. Story za nani anatembea na nani, mke wa nani ana mahusiano na nani, mume wa nani anatembea na nani, nani ana tabia gani etc. Mimi huwa sina tabia ya kufuatilia maisha ya watu, nimejiwekea commitment kwa kazi yangu na familia yangu. Ya mtaani siyapi uzito, japo ni muhimu kujua ABC za kitaa.

Moja, Kuna jirani yetu ana duka, mke wangu akapata story kuwa yule mama na mumewe ni waathirika. Mwenzangu akatangaza marufuku kwenda kununua kitu chochote pale. Nikamweleza kuwa kama ukimwi ungekuwa unaambukizwa kwa style hiyo basi sijui kama kuna binadamu angebaki hapa duniani. Akaninunia.

Lingine linalofanana na hilo: Kuna siku alikuja akanisimulia habari za mama mwingine mwenye duka pale gengeni a.k.a. Mama J ambaye hana mume alivyo na tabia mbaya, Kuwa anawaingiza wanaume kwake anawabadilisha tu. Sikutaka kupoteza muda kwenye huo mjadala, kumbe yeye alitaka atoe ultimatum kuwa ni marufuku kwenda kununua bidhaa kwenye hilo duka. Siku moja akaniomba nimsindikize tukachukue maziwa mida ya jioni kwani mwenye kuuza hakuweza kuleta. Wakati huo, tulikuwa tunatafuta mayai ya kienyeji na upatikanaji wake ni wa shida.

Sasa tukiwa tunapita barabarani nikaona kwa duka la mama J ana mayai ya kienyeji tena mengi tuu. Saa ya kurudi nikashauri tuchukue mayai, akasema twende nyumbani. Nikamshawishi kwani upatikanaji wa mayai ni shida, tukapitia pale tukachukua mayai kumi. Pia nikanunua vocha ya tigo. Mama J akasema vocha iliyobaki ni ya kurusha. Nikamwambia poa nirushie, nikamtajia namba. Kumbe hapo ndo nikawa nimetibua nyongo bila kujua.
Tulipotoka pale njia nzima nikaona mtu kanuna hataki kuongea. Kufika home kaniita chumbani akaanza kunigombeza, eti mbona alishaniambia tabia za yule mama alafu bado naenda kununua vitu kwake?


Pili, nikipigiwa simu haijalishi ni muda gani na ni wapi, lazima aulize nani amekupigia na anasemaje. Ukweli hata nikimwambia hawezi kumfahamu kila mtu na siyo kila kitu naweza kumsimulia, mambo mengine ni ya kikazi. Kila wakati anapekua simu yangu kana kwamba niko polisi.

Tatu, tumebahatika kuwa na usafiri, na tunapokaa daladala ni za shida kidogo. Hivyo, kila asubuhi lazima tutoke wote, tumpitishe mtoto shule, then nimdrop yeye kazini. Sasa tukiwa njiani akimwona mtu yeyote anayemfahamu ananiamrisha tumpe lifti huyo mtu. Kumbuka mimi simwulizi kuwa huyo mtu ni nani wake. Nachukulia kawaida. Sasa ikitokea mimi nimemkuta mtu ninayemfahamu au rafiki yangu, huyo mtu akishuka kwenye gari, basi nitaulizwa maswali kama vile niko polisi nahojiwa. Na bahati mbaya ikiwa ni mwanamke, basi ananuna na wakati mwingine nikitaka kusimama anasema twende bana tunachelewa. Hii imenikera sana kuliko kawaida.

Sasa, kuna shosti zake wa karibu sana, mara nyingi nawapa lifti anapotoka kazini, basi anawasifia sana kuwa wana tabia nzuri, sometimes ananiomba tuwapeleke mpaka mjini japo sina ratiba ya kwenda huko. Sasa hao mashosti zake nimetembea nao na hajui. I just wanted to prove kuwa mambo yake ya kijinga hayanizuii kufanya nikiamua. Jamani kumlinda mpenzi ni sawa na kulinda samaki baharini, ukilinda Kigamboni wenzako wanavua bagamoyo.

Anyway, nipeni wazo mbadala nimfanyeje ili aelewe hilo somo?

TRCA Yafungia Nyimbo za Diamond, Nay wa Mitego, Roma, Young Dee na Wengine Kisaa Hichi Hapa

$
0
0
Mamlaka ya Mawasiliano(TCRA) imepokea orodha ya nyimbo 15 zisizokuwa na maadili kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kupiga marufuku nyimbo hizo kuendelea kurushwa katika vyombo vya habari huku ikisema hatua za kisheria kuchukuliwa kwa watakaokiuka.

Hashim Lundenga Akubali Yaishe..Aamua Kuachana na Shindano la Miss Tanzania

$
0
0

BURUDANI: Kampuni Waandaaji wa Shindano la Miss Tanzania(Lino International Agency) yatangaza kuachana rasmi na uandaaji wa shindano hilo

Miaka ya hivi karibuni shindano hilo liligubikwa na kasoro ikiwemo ucheleweshwaji wa zawadi kwa washindi

Je, kipi kifanyike ili kuinua tena shindano hili la urembo nchini?

Kiongozi wa wanafunzi wa Chuo Auawa Baada ya Kupigwa na Risasi na Polisi Katika Maandamano

$
0
0

KENYA: Kiongozi wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Meru, Evans Njoroge ameuawa kwa kupigwa risasi na Polisi jana Februari 27, 2018 katika maanadamano chuoni hapo
-
Wanafunzi hao waliandamana wakishinikiza Chuo hicho kupunguza ada kwa kiasi cha shilingi 8,500 za Kenya ambazo ni sawa na Tsh 188,566 na kuboreshewa miundombinu chuoni hapo
-
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa wanafunzi wa Chuo hicho baada ya vurugu walikimbia nje ya chuo na kwenda kujificha mashambani baada ya kuona gari la Polisi
-
Shuhuda mmoja alisema kuwa maaskari baada ya kuwakosa chuoni walienda uraiani kuwatafuta, alisema mtoto mmoja aliwaelekeza Polisi wanafunzi hao walipojificha
-
Shuhuda huyo alisema alisikia mlio wa bunduki na alipotoka alimkuta askari anabadilisha mavazi yake na kubakia na nguo za kiraia
-
Kwa upande wa mashuhuda wengine wamesema kuwa polisi huyo aliyemuua mwanafunzi anafahamika ni Afisa wa jeshi la polisi la kituo cha Nchiru.
Viewing all 104747 articles
Browse latest View live




Latest Images