Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104659 articles
Browse latest View live

Historia imeandikwa Mtwara na Yanga

$
0
0
Kwa mara ya kwanza katika historia, Yanga imefanikiwa kupata ushindi kwenye ardhi ya Mtwara ikicheza dhidi ya Ndanda FC baada ya kuifunga 2-1 kwenye mchezo wa VPL uliochezwa uwanja wa Nangwanda Sijaona.

Kabla ya mchezo wa leo (Februari 28, 2018) timu hizo zilikuwa zinecheza mechi tatu kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona, Yanga haikuwahi kupata ushindi.

Ushindi huo wa Yanga dhidi ya Ndanda ni wa sita mfululizo kwenye ligi tangu iliposhinda 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika mechi sita zilizopita.

Ruvu Shooting 0-1 Yanga
Azam 1-2 Yanga
Lipuli 0-2 Yanga
Yanga 4-0 Njombe Mji
Yanga 4-1 Majimaji
Ndanda 1-2 Yanga
Yanga imefikisha pointi 40 ikiwa nyumba

Akilimali: Simba hata ikichukua Ubingwa, Lakini bado ni timu ya kawaida mno

$
0
0
Mjumbe wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimali, amesema kuwa anawapa Simba nafasi ya kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara, endapo watapambana zaidi huku akisema bado ni timu ya kawaida mno.

Akilimali ameeleza kuwa, Simba imekuwa ikifanya vizuri msimu huu tofauti na miaka ya nyuma, lakini bado anaiona ya kawaida kwa kusema endapo watapoteza baadhi ya mechi zijazo, basi nafasi hiyo hawana.

Akilimali ametamba kuwa wao watapambana kwa kila liwezekanalo waweze kuzidi kuutetea ubingwa kwa tofauti ya pointi na si magoli, kutokana na watani wao kuwa na wastani mzuri wa mabao ya kufunga mpaka sasa.

Mpaka sasa Simba ndiyo timu pekee ambayo haijapoteza mchezo hata mmoja kwenye ligi, katika michezo 19 iliyocheza msimu huu.

Simba hivi sasa wako katika maandalizi ya kujiandaa na mchezo ujao wa ligi dhidi ya Stand United ya SHinyanga utakaochezwa Ijumaa ya wiki hii.

VIDEO: Mrisho Gambo awapa siku 14

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amewapa siku 14 wafanyabiashara na wawekezaji walipo mkoani humo wawe wamemeshajiandikisha katika zoezi la vitambulisho vya taifa kwa wale ambao hawana mpaka sasa hivi.

Gambo ametoa kauli hiyo akiwa ofisini kwake kwa lengo la kuwapa vipaumbele watu hao kushirikishi katika zoezi hilo ili wasike kupata shida endapo watahitaji kuenda kuchukua hati ya kusafiri ambayo kwa sasa mpaka upatiwe ni lazima uwe na kitambulisho cha Taifa.

"Serikali ya awamu ya tano ya Rais John Magufuli ni serikali ambayo inajali makundi yote ya kijamii pamoja na wafanyabiashara. Tumeona ni muhimu kutengeneza utaratibu kupitia ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha kwa ajili ya kuwatengenezea mazingira rahisi wafanyabiashara na wawekezaji na kupitia mpango huo tumeona tuweke utaratibu maalumu wa kutenga wiki mbili kuanzia Marchi 15, 2018 ili waweze kushiriki kikamilifu", amesema Gambo.

Mtazame hapa chini Mrisho Gambo anavyoongea zaidi

Serikali imeyafunga Makanisa ya Kikristo zaidi ya 700

$
0
0

KIGALI, RWANDA: Serikali imeyafunga Makanisa zaidi ya 700 kwa kukosa kutimiza masharti yaliyowekwa ya usafi na usalama

Afisa wa Serikali Justus Kangwagye amesema Kutumia uhuru wa kuabudu hakufai kuingilia haki za watu wengine

Taarifa zinasema baadhi ya Makanisa yamekuwa yakifanya kazi kwa kutumia mahema na hayana maeneo ya kutosha ya kuegesha magari ya waumini

Baadhi ya waumini wamekuwa wakiegesha magari yao pembezoni mwa barabara na kusababisha misongamano ya magari

Aidha, amesema baadhi ya Makanisa hayo yalikuwa yakifanya kazi bila kuwasilisha upya maombi ya leseni na kwamba hawataruhusu yafunguliwe

Hii Mimba Imenipa Funzo Sasa Nimekua Naacha Utoto- Gigy Money

$
0
0
Hii Mimba Imenipa Funzo Sasa Nimekua Naacha Utoto
MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’ amefunguka kuwa kwa sasa ameachana na mambo ya kitoto ili kuwa mama bora kwa mwanaye anayetarajia kumpata.



Akizungumza na Showbiz Xtra, Gigy alisema kutokana na kwamba anatarajia kupata mtoto hivi karibuni, amejikuta akiachana kabisa na mambo ya kitoto aliyokuwa nayo kabla ya ujauzito na sasa anafikiria mambo ya kiutu uzima zaidi.


“Nimekua kwa kweli, unajua huu ujauzito umenipa funzo la maisha na sasa naenda kuwa mama hivyo ili niwe mama bora lazima nibadilike kwa kila kitu siyo kuendelea na yale maisha ya kitoto ya kujiachia kihasarahasara,” alisema Gigy

Wolper Asahau Maumivu ya Kuachwa Asema “Sijawahi Kuumia Kuachana na Mwanaume"

$
0
0
Wolper Asahau Maumivu ya Kuachwa Asema “Sijawahi Kuumia Kuachana na Mwanaume"
STAA wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper amefunguka kuwa licha ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanaume tofauti na kubwagana nao, kamwe hajawahi kuumia kuachana nao.

Akichonga na Showbiz Xtra, Wolper alisema alikuwa na kawaida ya kuwaanika wanaume aliokuwa akiingia nao kwenye uhusiano ili watu wote wajue akidhani itakuwa ngumu kusalitiwa lakini ikawa kinyume chake na kuachana nao jambo ambalo hajawahi kujutia au kuumia kwa kuwa akiachana na mtu anaangalia waliopo kwenye foleni anachangua tu anayemtaka.

“Sijawahi kuumia kuachana na mwanaume ila kinachoniumiza sana ni kwa nini nilimtangaza watu wakamjua ndiyo maana kwa sasa sitaki tena kumtangaza niliyenaye, siwezi kuumizwa na kuachana kwa kuwa unakuta wengi wako kwenye foleni naangalia mwenye sifa za kuwa nami sichagui ana kazi au fedha naangalia mwenye mapenzi,” alisema Wolper.

Linah Afunguka Kuhusu Ndoa "Sipo Tayari Kufunga Ndoa"

$
0
0
Linah Afunguka Kuhusu Ndoa "Sipo Tayari Kufunga Ndoa"
Msanii wa Bongo Fleva Linah Sanga maarufu kama 'Ndege Mnana' amefunguka na kudai hayupo tayari kufunga ndoa na Shaban Mchomvu (mwanaume aliyezaa na Linah) kwa sasa kutokana na kuwepo kwa baadhi ya vitu vinavyowakwamisha kufanya hivyo.


Linah amebainisha hayo wakati akizungumza kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa mubashara kupitia ukurasa wa kijamii facebook wa EATV kila Jumatano kuanzia majira ya saa 8:00 mchana hadi 10:00 alasiri kwa saa za Afrika Mashariki na Kati.

"Suala la ndoa zito sana, sina maana nakataa kuolewa na mzazi mwenzangu ila mambo ya ndoa sio ya kukurupuka japo natamani kuolewa kwa kuwa mimi ni mtoto wa kike, lakini sidhani kama nipo tayari kwa sasa hivi kuolewa. Mungu atusamehe tu tunazaa nje ya ndoa. Suala la ndoa ni la kujipanga sana", amesema Linah.

Pamoja na hayo, Linah amedai hata mzazi mwezake anafahamu fika kitu ambacho kinawakwamisha kutimiza jambo hilo la ndoa kwa wawili hao.

Tanzania Yazikataa Meli za Korea Kaskazini

$
0
0
WWaziri wa Mambo ya Nje, Dk. Augustine Mahiga amewafahamisha  mabalozi wa nchi tano ambazo ni wajumbe wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwamba meli mbili zilizoonekana zikielekea Korea ya Kaskazini zikipeperusha bendera ya Tanzania;


Inadaiwa kuwa Meli hizo zilizokuwa zikipeperusha bendera ya Tanzania zilionekana kwa njia ya satelaiti, moja ikielekea Korea ya Kaskani moja kwa moja na nyingine ilinaswa ikihamisha mizigo ambayo haikutambulika kwenye meli nyingine ambayo baada ya zoezi hilo la uhamishaji ilielekea Korea ya Kaskazini baada ya kupakia mizigo hiyo.

Balozi Mahiga amewaomba Mabalozi hao kutoka Marekani, Uingereza, Ufaransa Urusi na China kuisadia Tanzania kuweza kuzibaini meli zinazopeperusha bendera ya Tanzania na kwenda kinyume na utaratibu wa kimataifa wa usafirishaji baharini.

Januari mwaka huu Tanzania ilizifutia usajili meli zote 450 zilizokuwa zinapeperusha bendera ya Tanzania kwenye maji ya kimataifa baada ya kupatikana kwa meli iliyokuwa imebeba shehena ya silaha na dawa za kulevya huku ikipeperusha bendera ya Tanzania.

Wiki moja iliyopita Rais wa Marekani Donald Trump alitishia kuyawekea vikwazo vya Kiuchumi Kidplomasia Kisiasa na kibiashara mataifa yote yatakayokiuka vikwazo vilivyowekwa na Umoja wa Mataifa na Marekani dhidi ya Korea ya Kaskazini.

TCRA Yawazipiga Marufuku Nyimbo za Diamond, Nay, Gigy na Roma

$
0
0
Mamlaka ya MTCRA Yawapiga Pini Diamond, Nay, Gigy na Romaawasiliano(TCRA) imepokea orodha ya nyimbo 15 zisizokuwa na maadili kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kupiga marufuku nyimbo hizo kuendelea kurushwa katika vyombo vya habari huku ikisema hatua za kisheria kuchukuliwa kwa watakaokiuka.

Matonya Afunguka Ishu ya Kukamatwa na Dawa za Kulevya China

$
0
0
Matonya Afunguka Ishu ya Kukamatwa na Dawa za Kulevya China
Matonya amefunguka kuhusu tuhuma zilizosambaa kuwa amekamatwa na Madawa ya Kulevya nchini China akisisitiza kuwa sio kweli na wala yeye hajawahi kujihusisha na biashara hiyo kwenye maisha yake.


Mkali huyo wa Bongofleva akiongea na eNEWZ amesema taarifa hizo zilimkwamisha sana kwenye mipango yake mingi pamoja na mama yake kuumizwa nazo kiasi cha kumpigia simu na kumuuliza kama ni kweli.

''Kiukweli nimesikitika sana na sio mimi tu hata mama na familia yangu kwa ujumla, mama alikuwa akinipigia simu kila muda akitaka kujua kama ni kweli lakini tulizushiwa wengi akiwemo Alikiba japo ya kwangu ilivuma sana ila ni fununu tu haina ukweli'', amefunguka.



Msanii huyo pia ametoa ya moyoni kuhusu stori zilizopo kuwa anabifu na msanii Alikiba kitu ambacho amesema anashangaa kimetokea wapi kwasababu wao wako poa ila hajua fununu hizo zimetoka wapi

Rais Shein Apangua Baraza la Mawaziri, Aongeza Wizara

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt Ali Mohamed Shein amefanya mabadiliko katika Baraza la Mapinduzi huku akiongeza wizara moja zaidi.


Kwa mujibu wa taarifa Ikulu ya Zanzibar, shughuli za Vijana zimehamishiwa katika wizara mpya ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo; shughuli za Mazingira zimehamishiwa katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais huku shughuli za Wakala wa Serikali wa Uchapaji zimehamishiwa Wizara mpya ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale.

Mabadiliko hayo yanaifanya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwa na Wizara 14 zenye Mawaziri na Naibu Mawaziri kama ifuatavyo:

1. OFISI YA RAIS NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI

i. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi- Issa Haji Ussi Gavu

2. OFISI YA RAIS, KATIBA SHERIA, UTUMISHI WA UMMA NAUTAWALA BORA

i. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora –Haroun Ali Suleiman

JE Umehangaika na Matatizo ya Kimapenzi Kwa Muda Mrefu? Muone Shehe Chalo Atakutatulia Matatizo yako Kirahisi

$
0
0
JE umehangaika na matatizo haya kwa muda mrefu mtalamu Challo anayo dawa ya kuvuta mpenzi Je unasumbuliwa na mpenzi umeachwa na mpenzi au Mme mke na Bado unampenda na umejaribu sehemu nyingine Bila mafanikio njoo utatuliwe haraka na kundumisha ndoa yenu..

Umekimbiwa na mmeo mkeo au mpenzi na anaishi na mtu mwingine atarundi haraka kusafisha nyota mvuto wa mwili na biashara minguu kufa ngazi kuwaka moto ngiri tumbo kuunguruma na wakina Baba wasiojiweza katika tendo la uyumba kuchelewa kufika kileleni tunatibu Busha Bila oprasheni bali kwa kutumia vitabu vya dini

Tunatoa pete ya utajiri Bila mashariti mkufu wa bahati unauza Mali ya haindi unapoteza pesa kwenye biashara yako Bila kujua unataka kupandishwa cheo

Wasiliana na mtalamu Shehe Challo 0714006521

Kutana na Mtabibu Mongwa Mganga wa Waganga Sasa Anapatikana Mikoa Yote

$
0
0

 

KUTANA NA MTABIBU MONGWA MGANGA WA WAGANGA SASA WAKO MIKOANI KARIBU YOTE NCHINI...
.
HIVYO WATATOA TIBA MAENEO YOTE YA MBEYA ,DODOMA, IRINGA , MOROGORO, MWANZA,ZANZIBAR

==>KWA WALE WENYE KUHITAJI TIBA

Husafisha nyota na kutoa Pete za bahati na kwawale walio sumbuka kwaajili ya matibabu na hawakufanikiwa chochote sasa njoo ujionee miujiza hapo kwahapo bila malipo yoyote malipo baada yakazi napia humpa mtu jini la mali kwayule anaye taka kumiliki bila mashariti yoyote
Tunatibu magonjwa mbalimbali yaliyo shindikana mpenzi aliye kukimbia nakumrudisha kwa masaa 24 tu napia natoa dawa za nguvu za kiume kuurefusha uume paka pale unapotaka .
Natoa dawa za biashara na mvuto ==tunatoa dawa zauzazi kwa wale kina mama wenye matatizoya uzazi walio angaika kwa muda mrefu bila kupata mafanikio yoyote njoo umalize tatizo lako sasa
Natoa mazindiko yanyumba na mwili biashara na mvuto kazini
Kupandisha nyota ili kungaa kupandishwa cheo kazini kurudisha mali zilizo pote zilizo ibiwa kuzulumiwa
Kesi zilizo shindikana uzimaliza mara moja namengine mengi ya siri piga simu

+255 764291657
+255 764291657
+255 764291657

Wolper Achoshwa na Wanaoongeza Makalio Amkumbusha Waziri Kuwachukulia Hatua

$
0
0
Wolper Achoshwa na Wanaoongeza Makalio Amkumbusha Waziri Kuwachukulia HatuaMsanii wa filamu na mjasiriamali Jackline Wolper amefunguka na kumkumbusha Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza kuchukua hatua kwa watu ambao wamekuwa wakionyesha makalio yao kwenye mitandao ya jamii.


Wolper amesema hayo leo Marchi 1, 2018 baada ya kuona watu bado wanaendelea kuweka video na picha zikionyesha makalio yao wakiwa nusu uchi na kusema kuwa hilo jambo linamshangaza mpaka jasho la damu linamtoka.

"Haki ya ukweli yule kiongozi wakukomesha vichupi yuko wapi, mbona bado tunaona makalio Insta au ndio sanaa kila sehemu mimi nashangaaa mpaka jasho la damu linanitoka chaaaaa" alisema Wolper

Januari 7, 2018 Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza alimfungia msanii Suzan Michael maarufu kama Pretty Kind kujihusisha na shughuli za sanaa kwa muda wa miezi sita kwa madai ya kuwa msanii huyo alikuwa akiweka picha zisizo na maadili lakini Naibu Waziri huyo alisema na kuwataja watu wengine kuwa wanafuata akiwepo msanii msanii Gift Stanford maarufu kama Gigy Money pamoja na Jane Rimoy maarufu kama Sanchi ambaye bado anaendelea kujiachia kwa picha hizo kupitia mitandao yake ya kijamii. 

"Namuonea Huruma Mama Anayezaa kwa Mshono- Roma Mkatiliki

$
0
0
Namuonea Huruma Mama Anayezaa kwa Mshono- Roma Mkatiliki Rapa Roma Mkatoliki ambaye mpaka sasa anatamba na wimbo wake 'Zimbabwe' amekuwa miongoni mwa watu walionesha hisia zao za kuguswa na maisha wanayopitia wanawake katika nyanja zote na kudai anawaonea huruma sana japokuwa anawapenda kupita maelezo.


Roma amebainisha hayo kupitia ukurasa wake maalumu wa kijamii ikiwa kama ishara ya kuonesha mapenzi yake aliyokuwa nayo katika kuelekea siku ya wanawake duniani ambayo huwa inaadhimishwa kila ifikapo Marchi 8 ya kila mwaka ulimwenguni kote.

"Namuonea huruma mama anayezaa kwa mshono na hata anayesukuma huku daktari kaweka mgomo, wengi wanaishi kama watumwa au chombo cha starehe ya ngono. Je kipi kinawea kukuuma mwanaume 'buzi' aliyechunwa au kahaba aliyenyimwa mtonyo. Nawapenda sana dada zangu pamoja na wanawake wote", amesema Roma.

Kwa upande mwingine, Roma amewafumbua macho wanaume wenzake kwa namna moja ama nyingine kwa kuwaambia wawe makini na wanawake kutokana na wao kuwa chombe chenye thamani kubwa duniani na kuwataka wavitunze imara.

ACT Wazalendo Watelekeza Ahadi Yake Sasa Kujenga Zahanati Dodoma

$
0
0
ACT Wazalendo Watelekeza Ahadi Yake Sasa Kujenga Zahanati Dodoma
Chama cha ACT Wazalendo kimekabidhi mifuko 40 ya Saruji  kama mwendelezo wa utekelezaji wa ahadi ya kujenga Zahanati kwenye Kijiji cha Chidolu kilichopo Wilaya ya Bahi Mkoa wa Dodoma ambacho kinaongozwa na ACT Wazalendo.


Ahadi ya kujenga zahanati hiyo ilitolewa na Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Ndugu Zitto Kabwe.

Akizungumza wakati wa kukabidhi mifuko hiyo ya Saruji, Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi wa ACT Wazalendo Ado Shaibu amesema kwamba chama cha ACT kinaamini kuwa mbali na kuikosoa serikali pia wanawajibu wa kushirikiana na wananchi katika kufanya maendeleo.

"Sisi ACT Wazalendo tunaamini kwa dhati kuwa mbali na kutekeleza wajibu wa kuikosoa serikali, tunao pia wajibu wa kushirikiana na wananchi katika kujiletea maendeleo. Kazi ya upinzani haiwezi kuwa kupiga mdomo pekee. Itakuwa ni faraja iwapo Kijiji hiki ambacho hakina Zahanati tangu uhuru kitapata Zahanati katika Uongozi wa ACT Wazalendo" Ndg. Shaibu.



Ameongeza "Nipo hapa kumuwakilisha Kiongozi wa Chama Ndugu Zitto Kabwe ambaye aliahidi kushirikiana na nyinyi kuhakikisha Kijiji hiki ambacho kinaongozwa na ACT Wazalendo kinapata Zahanati ya Kijiji. Yeye yupo kwenye ziara ya kuzitembelea Kata zinazoongozwa na ACT Wazalendo".

Mbali na hayo Kiongozi huyo wa ACT Wazalendo amewapongeza wananchi wa Chidolu kwa kujitolea kuchimba msingi wa Zahanati na kufyatua matofali na kuwakumbusha kwamba maendeleo ya kweli hayawezi kushushwa kutoka juu bali lazima wananchi nao washiriki kikamilifu kwenye programu za maendeleo.

Video ya Utupu Yamponza Eric Omondi ...Wakenya Wataka Ashitakiwe

$
0
0
Image result for Eric Omondi
Mchekeshaji maarufu kutoka nchini Kenya, Eric Omondi amejikuta katika wakati mgumu baada ya kuachia video ikimuonesha akiongelea kwenye mto akiwa mtupu na watoto wadogo.

Kwenye video hiyo Omondi anaonekana akioga akiwa mtupu huku watoto wadogo ambao kwa muonekano wao ni makadirio ya chini ya miaka 10.


@VictorMochere
WTF!!! Eric Omondi, naked in front of the camera! Wah!

Baada ya kuposti video hiyo kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii, alianza kushambuliwa na mashabiki wake na wanaharakati nchini Kenya wakitaka aburuzwe mahakamani kwa kujibu mashtaka ya kuwadhalilisha watoto wengine wakimsapoti kwa kusema kuwa anaenzi tamaduni.

Bell 9 Aleta Kali Aifananisha Basata na Baba Asiyejua Jina la Mwanaye

$
0
0
Bell 9 Aleta Kali Aifananisha Basata na Baba Asiyejua Jina la Mwanaye
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Belle 9 amelishangaa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kwa kushindwa hata kuwajua wasanii japo hata kwa majina.


Belle 9 amesema hayo baada ya BASATA kuchanganya majina kwa kumtaja kwenye orodha ya wasanii waliofungiwa nyimbo zao jana Februari 28, 2018 badala ya kuweka jina la Roma Mkatoliki.

“Kwahiyo mimi ni Roma Mkatoliki haya basi tongwe record baby jei mada yo yo yo Roma!  Hii ni sawa na kua na baba ambaye akisikia umekosa ana kuhukumu lakini akiulizwa jina la mwanao anaitwa nani anajiuma uma halafu analitaja jina la mtoto wa jirani ambalo huwa analiskia akiwa anakuja kukuhukumu,“ameandika Belle 9 kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Soma zaidi – TCRA yazifungia nyimbo 15, Diamond na Nay maumivu zaidi

BASATA walikosea kumtaja Belle 9 kwenye kipengele cha wimbo wa Kibamia ambapo waliandika Abemego Damiani a.k.a Roma Mkatoliki.

Mfanyakazi Mwingine wa Ikulu ya Trump Ajiuzulu, Atoa Sababu Hii

$
0
0
Mfanyakazi Mwingine wa Ikulu ya Trump Ajiuzulu, Atoa Sababu HiiIdadi inaendelea kuongezeka ya wafanyakazi wa Ikulu ya nchini Marekani kujiuzulu ambapo mwanzoni mwa Mwezi February, 2018 iliripotiwa kuwa wafanyakazi wawili wa Ikulu ya Marekani walitangaza kujiuzulu kwa sababu zilizohusishwa na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia na kingono.

Wafanyakazi hao ni pamoja na Katibu wa Wafanyakazi wa Rais Donald Trump, Rob Porter na Mwandishi wa hotuba za Ikulu hiyo David Sorensen.

Sasa leo March 1, 2018 taarifa kutoka nchini Marekani zinaeleza kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano na mmoja wa washauri wa karibu wa Rais Trump wa muda mrefu ajulikanaye kama Hope Hicks pia ametangaza kujiuzulu.

Hicks ameeleza sababu yake ya kujiuzulu ni kwamba, tayari ametimiza wajibu wake katika ikulu hiyo ya White House.

Watu 108 Waokolewa Katika Ajali ya Boti DRC

$
0
0
Watu 108 Waokolewa Katika Ajali ya Boti DRCIdadi kubwa ya watu inasadikiwa kupotea baada ya boti kuzama nchini DRC,huku jitihada za kuwaokoa zikiendelea. Mpaka sasa taarifa juu ya idadi kamili ya watu waliokuwemo ndani ya boti hiyo hazijasemwa, huku mbunge wa jimbo lilipotokea ajali hiyo Didas Pembe alitangaza kuwa inawezekana ni zaidi ya watu 500 ndio wamepotea.

Licha ya kutangazwa kutokea kwa ajali ya boti hiyo usiku wa Jumatatu hadi Jumamne nchini DRC jimboni Mayi -ndombe magharibi mwa mji mkuu wa Kinshasa,mbunge wa jimbo hilo ambae alitangaza taarifa hiyo alisema idadi aliyoitangaza awali hazikuwa za uhakika kwa kuwa taarifa alizopata hazikuwa za kweli. Lakini mara baada ya mbunge huyo kufika katika eneo la tukio alisema boti hiyo ilikuwa na abiria 121 na watu 108 wameokolewa huku watu 12 ndio wamepotea mpaka sasa na kifo cha mtoto moja wa miaka tano.

Aidha kuna ripoti kutoka kanisa la jimbo hilo wamesema kwamba watu kumi na tano ndio waliofariki ,Huku wahudumu wa afya wamethibitisha kupokea miili ishirini na tano na wakisema boti hiyo ilikwa na abiria wengi waliokuwa wakisafiri mjini Kinshasa.

Leo bado inasubiriwa ripoti kutoka msalaba mwekundu maana bado idadi kamili haijatajwa na imekuwa inatofautiana sana.

Ajali za boti zimekuwa zikiripotiwa karibu kila mwaka nchini Jamuhuri ya kidemokrasia ya kongo kufuatana na ubovu wa boti na mashua na huku wakisafiri bila mavazi ya kujiokolea katika maji.
Viewing all 104659 articles
Browse latest View live




Latest Images