Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104415 articles
Browse latest View live

Hiki Hapa Kikosi cha Simba Dhidi ya Stand United Leo

0
0

Vinara wa ligi kuu soka Tanzania Bara klabu ya Simba majina ya wachezaji wake ambao watacheza katika mchezo wao wa leo wa ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya Stand United.

Simba imewataja wachezaji wake akiwemo Aishi Manula, Shomari Kapombe, Asante Kwasi, Yusufu Mlipili, James Kotei, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Mzamiru Yassin, Laudit Mavugo, Shiza Kichuya na Nicholas Gyan.

Wachezaji wa akiba ni Ally Salim, Mohamed Hussen, Rashid Juma, Moses Kitandu, Juma Luizio, Juuko Murshid na Mwinyi Kazimoto.

Mchezo huo utachezwa majira ya saa 10 Alasiri katika uwanja Mkuu wa Taifa

Upande wa Utetezi Wataka Kitilia na Wenzake Wafutiwe Mashtaka ya Utakatishaji Fedha

0
0
Leo March 2, 2018 nakusogezea stori ya Kimahakama ambapo Upande wa utetezi katika kesi inayomkabili Kamishna Mkuu wa TRA, Harry Kitilya, na wenzake umeutaka upande wa mashtaashtaka ya utakatishaji fedha ili washtakiwa wapate dhamana.

Mbali na Kitilya washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni aliyekuwa miss Tanzania (1996), Shose Sinare na Ofisa wa benk ya Stanbic Sioi Solomon.

Wakili wa serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi amemueleza Hakimu Mkazi Mfawidhi, Victoria Nongwa kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, hivyo anaomba kesi iahirishwe hadi tarehe nyingine.

Pia amedai kuwa mashtaka yanayo wakabili washtakiwa hayana kikomo na kwamba bado wanafanya juhudi za kuharakisha huo upelelezi.

Hata hivyo, wakili wa utetezi Majura Magafu amedai kama upande wa mashtaka haujakamilisha upelelezi basi liwe ahirisho la mwisho na pia wayafute mashtaka ya utakatishaji fedha ili washtakiwa wapate dhamana.

“Upelelezi umekuwa ndio wimbo wa kila siku takribani miezi 6 sasa, pendekezo letu kama upelelezi bado basi mashtaka ya utakatishaji fedha dhidi ya wateja wetu yaondolewe kusudi wapate sifa ya kudhaminiwa,” Wakili Magafu.

Baada ya kutolewa kwa hoja hizo, Hakimu Nongwa ameahirisha kesi hiyo hadi March 16,2018 Kwa ajili ya kutajwa.

Washtakiwa wanakabiliwa na makosa ya utakatishaji fedha, kwa kuhamisha, kuchukua na kuweka kiasi cha Dola za Marekani Milion 6 katika akaunti tofauti tofauti  za benki ambapo inadaiwa walitenda makosa hayo kati ya March 2013 na September 2015.

Klabu ya Simba Yapewa Agizo na Rais

0
0
Klabu ya Simba Yapewa Agizo na Rais

Wachezaji wa Klabu ya Simba imeagizwa kufanya vizuri katika mechi zake anazoendelea kucheza ili iwe njia moja ya wapo ya kumuenzi mchezaji wao wa zamani Mzee Arthur Mambeta aliyefariki jana (Marchi mosi, 2018) Jijini Dar es Salaam.


Agizo hilo limetolewa na maarufu kama 'Try again' wakati alipokuwa anazungumzia jinsi walivyoguswa na taarifa za msiba wa nyota wao zamani kama viongozi wa klabu hiyo.

"Marehemu Mambeta ni hazina ambayo Mungu ametupatia lakini sasa Mwenyezi Mungu mwenyewe amepitisha rehema yake kwa hivyo sisi kama Klabu ya Simba kwa masikitiko makubwa tunawaomba wanachama wetu na wapenzi wa wekundu msimbazi tumuenzi mzee huyu", amesema Salim.

Pamoja na hayo, Salim ameendelea kwa kusema "wachezaji wetu wafanye vizuri  katika mechi zinazokuja ili kumuenzi shujaa wetu huyu kwani ni moja ya wazee wachache waliokuwa wamebaki katika tasnii hii kwa wazee ambao walifanya vizuri na kuitendea mema klabu".

Nyota huyo wa zamani wa Simba, Mzee Arthur Mambeta anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumamosi (Machi 3, 2018) katika makaburi ya maeneo ya Buguruni Jijini Dar es Salaam.

Ray Awapa Makavu Wanawake Wasionyonyesha Watoto kwa Kuogopa Maziwa Kulala

0
0
Image result for Ray Kigosi
Msanii wa filamu Bongo, Ray Kigosi ametoa somo zito kwa wadada wanaonyonyesha watoto.

Muigizaji huyo amesema amekuwa akipokea jumbe nyingi kutoka kwa watu mbali mbali zikimtaka kueleza siri ya mtoto wake na Chuchu Hansy, Jaden kukua haraka na kuonekana mchangamfu. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ray amekuwa na haya ya kusema; kuhusiana na hilo;

Unamkuta mdada kajifungua mtoto eti anaogopa kumnyonyesha mtoto wake kwa kipindi kirefu akiogopa  maziwa yake kuanguka bila kujua kama maziwa ya mama ni lishe bora ya mtoto kuliko vyakula vyote unavyovijua wewe.

Kumfanya mtoto kutoumwa mara kwa mara kumfanya mtoto awe mchangamfu muda wote coz maziwa ya mama ni kinga kubwa sana kwa mtoto kitaalamu hata kidini kama sijakosea wanakwambia mtoto lazima anyonye kwa muda wa miaka miwili, sasa je hao madada kwa kipini hiki wapo?.

Maana unamkuta madada kajifungua mtoto leo baada ya wiki utamkuta yupo disco anaruka majoka sasa hapo unategemea mtoto awe na afya gani ndio maana hata kwa madada wanaofanya kazi kipindi wajifunguapo utapata miezi mitatu ya kupumzika angalu basi mtoto apate malezi bora ya mama kitaalam wanaita (maternity leave) kama umeamua kuwa na mtoto jitahidi kumpa malezi yanayostahili kama mzazi.

Kwa kweli nimpongeze sana Chuchu kwani ni mwanamke wa tofauti sana maana mpaka sasa bado mtoto wetu ananyonya maziwa yake bila kuogopa wale kujali kama yataanguka na kizuri zaidi kaniambia mpaka ifike miaka miwili ndio mtoto atamuachisha kumnyonyesha.

January mwaka jana Ray Kigosi na mpenzi wake Chuchu Hansy walijaliwa mtoto wa kiume ambaye wamempatia jina la Jaden.

Soma Zaidi; Picha: Mpenzi wa Ray Kigosi, Chuchu Hans ajifungua mtoto wa kiume

Kwa sasa Jaden ni miongoni mwa watoto maarufu Bongo, ana followers 107k katika mtandao wa Instagram akiwafukuzia kina Tiffah, followers Milioni 1.6 na Nillan, followers 543k (wote wa Diamond, pia kuna Cookie wa Aunt Ezekiel na Mose Iyobo, followers 420k na wengineo.

Diamond Apata Mchongo wa Kushiriki Wimbo wa Kombe la Dunia

0
0
Diamond Apata Mchongo wa Kushiriki Wimbo wa Kombe la Dunia
Msanii wa muziki Bongo, Diamond Platnumz anatarajiwa kushiriki katika wimbo maalumu wa Kombe la Dunia. Wimbo huo utakuwa unawakilisha bara la Afrika.

Wimbo huo ambao umedhaminiwa na kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola, Diamond atashirikiana na wasanii wengine kama Sami Dani kutoka Ethiopia, Ykee Benda kutoka Uganda na Lizha James kutoka Msumbiji.

Hapo awali msanii wa Marekani Jason Derulo alidokeza juu ya wimbo huo ambao unakwenda kwa jina la Colors ambao utatoka March 16 mwaka huu.

Soma Zaidi; Msanii wa Afrika apata dili la kushiriki wimbo rasmi wa Kombe la Dunia 2018

Leo Diamond Platnumz kupitia ukurasa wake wa Instagram ameposti picha inayoashia ushiriki wake katika Fainali za Kombe la Dunia ambazo zinatarajiwa kufanyika nchini Urusi kuanzia June mwaka huu.

Raia ya China Ahukumiwa Miaka 20 Jela kwa Kosa la Kukutwa na Meno ya Simba

0
0
Raia ya China Ahukumiwa Miaka 20 Jela kwa Kosa la Kukutwa na Meno ya Simba
Leo March 2, 2018 nakusogezea hukumu iliyotolewa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo imemuhukumu Raia wa China, Liu Xiu Feng jela miaka 20 ama kulipa faini ya Shilingi Milioni 110 baada ya kukiri kosa la kukutwa na Meno ya Simba mawili.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya Wakili wa serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi kueleza kuwa mshtakiwa huyo amekiri kosa.

Hakimu Shaidi amesema kuwa kutokana na mshtakiwa huyo kukiri kosa mahakama inamuhukumu kwenda jela miaka 20 ama kulipa faini ya Tsh.Mil 110.

“Unahukumiwa kwenda jela miaka 20 ama ulipe faini ya Shilingi Milioni 110,”  Hakimu Shaidi.

Baada ya kutolewa hukumu hiyo, mshtakiwa Feng aliepuka kwenda jela baada ya kulipa faini hiyo ya Shilingi Milioni 110.

Raia huyo wa China alikabiriwa na kosa la kukutwa na Meno mawili ya Simba katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).

Inadaiwa alikutwa na Meno hayo February 7,2018 ambapo yanathamani ya Shilingi Milioni 11, 029,900.

Seth, Rugemalira Mambo Bado Mahakamani

0
0
Seth, Rugemalira Mambo Bado Mahakamani
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo Upande wa mashtaka katika kesi inayowakabili Habinder Seth na James Rugemalira umedai upelelezi wa shauri hilo haujakamilika.

Washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi, utakatishaji fedha na kuisababisha Serikali hasara ya Dola 22.198 Milioni za Marekani (Sh309.5 Bilioni) katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Mwendesha mashtaka kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU),  Leonard Swai amedai hayo mahakamani leo March 2, 2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wakati shauri lilipotajwa.

“Upelelezi wa kesi hii bado haujakamilika, hivyo tunaomba Mahakama ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa,” -Swai.

Hakimu Shaidi aliahirisha kesi hiyo hadi Machi 16, 2018 itakapotajwa. Washtakiwa wamepelekwa rumande.

Hatimaye Ahmed Albaity Kwenda China kwa Matibabu

0
0
Hatimaye Ahmed Albaity Kwenda China kwa Matibabu
NDOTO na shauku ya kijana Ahmed Albaity alieteseka kwa zaidi ya Miaka 10 Kitandani kwa kushindwa kumudu gharama za matibabu leo imebadilika kuwa furaha baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda kumkabidhi Tiketi za Ndege za watu Wanne kwaajili ya safari ya kwenda kupatiwa matibabu Nchini China kwenye Hospital ya Beijing Puhua International huku akijitolea pia kugharamia fedha za Matibabu na Malazi.


RC Makonda alitoa ahadi kumsaidia Ahmed Albaity wakati wa Zoezi la Upimaji Afya Bure kwenye Meli ya Jeshi la China mwishoni mwa Mwaka Jana baada ya kugundulika Ahmed anahitaji Matibabu Maalum ambayo hayapatikani kokote kule duniani isipokuwa China, jambo lililomfanya RC Makonda kutokwa na Machozi na Kuhaidi Kumpeleka kwenye matibabu kwa gharama yoyote ile Maumivu na Mateso anayopitia kijana huyo.

Ahmed Albaity anasumbuliwa na tatizo la uti wa mgongo baada ya kuanguka na kuvunjika Shingo alipokuwa akiogelea ambapo kwa sindano moja pekee inagharimu Dollars 26,000/= sawa na shillingi million 52.

RC Makonda amesema Ahmed atasafiri Nchini China Siku ya Jumapili akiongozana na watu watatu wa kumsaidia kumuhudumia ambapo gharama zake ni zaidi ya Shilingi Million 100.


Aidha RC Makonda amesema Shauku yake ni kugusa maisha ya Mwananchi hata kama ni mmoja atakaekwenda mbele za Mungu na kusema Asante Mungu kwa kutupatia viongozi wetu, ifike mahali tumtumikie Mungu katika nafasi zetu, na katika hilo watu wote watakuwa Sawa na tutawahudumia bila kutarajia chochote kutoka kwao kama sehemu ya utumishi wetu ambapo amewashukuru watu wote waliomchangia na kufanikisha matibabu.

Hata hivyo RC Makonda ametoa wito kwa wananchi wa dini zote kumuombea Ahmed ili aweze kupona na kuendelea na shughuli za ujenzi wa Taifa.
Kwa upande wa Ahmed Albaity amemshukuru RC Makonda kwa moyo wa ukarimu aliouonyesha ambapo ameeleza kuwa ameishi kwa mateso muda mrefu kutokana na kukosa uwezo wa kumudu gharama za matibabu.

 Aidha amesema alipokuwa akiomba watu wamchangie wapo waliokuwa wakimvunja moyo kwa kumwambia hawezi kupona lakini RC Makonda ameonyesha moyo wa kipekee.



Inasikitisha Mtanzania Auwawa Kikatili Afrika Kusini

0
0
RAIA wa Tanzania aliyekuwa mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Chuo Kikuu cha Johannesburg (UJ) nchini Afrika Kusini, Baraka Nafari ameuawa baada ya kugongwa na gari na watu wasiojulikana akitokea katika matembezi ya usiku.


Akizungumzia suala hilo, Waziri  wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dkt. Augustine Mahiga amesema bado ofisi yake haijapata taarifa yoyote rasmi kuhusiana na kifo hicho. Licha ya kuwa nje ya ofisi, amesema hadi asubuhi hakukuwa na taarifa kutoka Ubalozi wa Afrika Kusini kuhusu kijana wa Kitanzania kufariki nchini humo.



“Ngoja niwasiliane na wenzangu waliopo ofisini na ubalozi wetu nchini Afrika Kusini kwa maelezo zaidi, kama limetokea wakusanye taarifa za kina kabla ya kuzituma, hilo linaweza kuchelewesha kutufikishia taarifa mapema,” amesema Balozi Mahiga.

Kisa-100 ya Roma Chadema Wataka Basata Ichukuliwe Hatua

0
0
Kisa Kibamia Chadema Wataka Basata Ichukuliwe Hatua
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana CHADEMA, Patrick Ole- Sosopi amesema Baraza la Sanaa la Taifa linapaswa kuchukuliwa hatua kwa kushindwa kusimamia majukumu ya kazi zao ndiyo maana walishindwa kuzichukulia hatua nyimbo zinazodaiwa kutokuwa na maadili.


Akizungumza na vyombo vya habari, Ole- Sosopi amesema hayo leo ambapo amesema kwamba kama nyimbo zimeweza kusikilizwa kwa muda mrefu basi ni wazi maadili na jamii zilishapotoka kwa muda mrefu kutokana na uzembe wa viongozi waliopaswa kuchukua hatua za haraka pindi  nyimbo hizo zilipoka.

Mwenyekiti huyo anayewakilisha vijana wa CHADEMA Tanzania, ameongeza kuwa hakuna mtu anayependa kusikia au kuona nyimbo zenye maudhui mabaya lakini anashangaza na jinsi baraza hilo linavyofanya kazi kwa mashinikizo huku akiongeza kwmba adhabu zilizotolewa kwa wasanii hazistaili.



Pamoja na hayo Sosopi amemtaka Naibu Waziri, Juliana Shonza kutengua adhabu yake hiyo kwani sheria haimpi yeye mamlaka ya kutoa adhabu alizotoa na badala yake wajibu huo upo chini ya BASATA.

Hapo jana Naibu Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo alitangaza kumfungia Msanii Hip Hop bongo, Roma Mkatoliki kufanya shughuli za muziki kwa muda wa miezi sita kwa kile kilichodaiwa msanii huyo kudharua wito wa BASATA na Naibu Waziri huyo w kurekebisha wimbo wao wa 'KIBAMIA' waliouimba yeye na Stamina (ROSTAM)

Sijutii Kuchora Tattoo ya Jackline Wolper – Brown

0
0
Sijutii Kuchora Tattoo ya Jackline Wolper – Brown

Aliyekuwa mpenzi wa muigizaji wa filamu Bongo Jackline Wolper , Brown amesema hajutii kuchora tattoo yoyote mwilini mwake kwani anazipenda. Brown na Wolpewr walidaiwa kuwa wapenzi lakini mpaka sasa bado haijabainika kama wameachana.

Witness Afunguka Kuhusu Kutoa Rushwa ya Ngono

0
0
Msanii wa muziki Bongo, Witness Kibonge Mwepesi amekiri kuwepo kwa rushwa ya ngono katika muziki.  Rapper huyo anayetamba na ngoma ‘Kwani Shingapi’ amekiambia kipindi cha The Playlist cha Times Fm vitendo hivyo havijaaza leo bali ni kitu ambaho kipo kwa muda mrefu na hadi sasa kinaendelea.  “Nilikutana nazo kipindi hicho, sema inaenda inafika kipindi watu wanaanza kufanya kwa kutilia ugumu ili ujiongeze mwenyewe,” amesema Witness.  “Kwa sasa hivi mtu haniambii direct, anaongea indirect kwa sababu kwangu watu wengi hawataki kupokea pesa na hawatopokea lakini inaonekana kabisa dizani kama kwanini huyo mtoto watu hawamkamui?,” alisisitiza.  Ameongeza kuwa vitendo hivyo haviwezi kuathiri muziki wake ile ufikishwaji wa ngoma zake kwa mashabiki unakuwa mgumu/unakutana na vigingi.  Soma Zaidi; Witness adai ameombwa rushwa ya ngono ili ngoma zake zichezwe  “Hii haiwezi kusaidia industry kwa sababu mimi ni kama dada au mama yako, pata picha dada yako akafanyiwa kitu kwa ajili apewe kitu how did you feel, is not good,” amesema Witness.
Msanii wa muziki Bongo, Witness Kibonge Mwepesi amekiri kuwepo kwa rushwa ya ngono katika muziki.

Rapper huyo anayetamba na ngoma ‘Kwani Shingapi’ amekiambia kipindi cha The Playlist cha Times Fm vitendo hivyo havijaaza leo bali ni kitu ambaho kipo kwa muda mrefu na hadi sasa kinaendelea.

“Nilikutana nazo kipindi hicho, sema inaenda inafika kipindi watu wanaanza kufanya kwa kutilia ugumu ili ujiongeze mwenyewe,” amesema Witness.

“Kwa sasa hivi mtu haniambii direct, anaongea indirect kwa sababu kwangu watu wengi hawataki kupokea pesa na hawatopokea lakini inaonekana kabisa dizani kama kwanini huyo mtoto watu hawamkamui?,” alisisitiza.

Ameongeza kuwa vitendo hivyo haviwezi kuathiri muziki wake ile ufikishwaji wa ngoma zake kwa mashabiki unakuwa mgumu/unakutana na vigingi.

Soma Zaidi; Witness adai ameombwa rushwa ya ngono ili ngoma zake zichezwe

“Hii haiwezi kusaidia industry kwa sababu mimi ni kama dada au mama yako, pata picha dada yako akafanyiwa kitu kwa ajili apewe kitu how did you feel, is not good,” amesema Witness.

Hali Mbaya ya Hewa Yawa Tishio Ulaya

0
0
Hali Mbaya ya Hewa Yawa Tishio Ulaya

Hali mbaya ya hewa imeendelea kuleta taharuki katika eneo kubwa la Bara la Ulaya, ambapo watu kadhaa kufa na mamia ya nyumba kukosa umeme kufuatia hali mbaya ya baridi iliyofikia nyuzi joto ya chini ya sifuri.


Nchini Ireland usafiri wa aina mbalimbali pamoja na ule wa ndege umeahirishwa kufuatia upepo mkali uliosababishwa na dhoruba kali iliyoziacha nyuma takribani 24,000 na maeneo ya biashara kukosa umeme wakati nchini Uingereza maelfu wakikumbwa na giza.


Barafu na theluja inayomiminika katika nchi hizo imesababisha hali ya maisha kuwa ngumu kwa wasafari na wananchi kwa jumla.

Tahadhari imeendelea kutolewa kwa wananchi huku kwa wasio na makazi, wakipatiwa hifadhi.

Mwenyekiti wa BAVICHA Asimamishwa Kazi na Chadema

0
0
Mwenyekiti wa BAVICHA Asimamishwa Kazi na Chadema
HALI si shwari ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mkoa wa Kilimanjaro, baada ya chama hicho kuchukua hatua ya kumsimamishwa uongozi Mwenyekiti wa Baraza la Vijana, Dickson Kibona.
Kibona alisimamishwa kazi Februari 28, mwaka huu, ikiwa zimepita siku 11 tangu kufanyika kwa uchaguzi wa marudio wa kiti cha ubunge Jimbo la Siha, ambalo Chadema iliangushwa na Chama Cha Mapinduzi katika uchaguzi huo.
Taarifa kwa umma iliyotolewa jana na Katibu wa Chadema, Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa, imeeleza kuwa Kibona anasimamishwa kazi kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake.
Waraka huo kwa umma haujaeleza wazi kwamba Kibona anasimamishwa kazi kupisha uchunguzi gani.
Sehemu ya waraka inasema: “Ofisi ya Chadema Kanda ya Kaskazini, ambayo ni mamlaka ya nidhamu na uwajibishaji kwa viongozi wa mikoa, ilimwandikia barua Kibona ambaye ni Mratibu wa Bavicha Kilimanjaro, kwa mujibu wa ibara ya 6.5.2 ya kanuni za chama ya utaratibu wa kuchukua hatua ya kinidhamu sehemu ya kazi kuhusu tuhuma zinazomkabili kama kiongozi na kama mwanachama wa Chadema.”
Kwa mujibu wa maelekezo hayo ya Golugwa ambayo yanasema kwa uzito na unyeti wake, Ofisi ya Kanda imeelekeza Kibona kusimama na kupisha uchunguzi.
Imeeleza kuwa hatua hiyo ni ya kiutawala na itatoa fursa kwa kipindi ambacho Kibona ameelekezwa kwenye barua aliyopewa kujibu tuhuma kuhusu ama aachishwe uongozi au afukuzwe uanachama kwa mujibu wa ibara ya 6.3.4 (b) na (c)

Mwanajeshi Kumburuza Maimatha Mahakamani

0
0
Mwanajeshi Kumburuza Maimatha Mahakamani
MWANAJESHI aliyefahamika kwa jina la Pendo Masatu amepania kumburuza mahakamani mtangazaji Maimartha Jesse ‘Mai’ kwa madai ya kumdai shilingi laki mbili.

Rafiki wa karibu wa Mai aliyeomba asitajwe jina lake alisema kuwa, pesa hizo anazodaiwa Mai zilitokana na mwanajeshi huyo kwenda kukodi gauni la harusi kwake, akawekesha shilingi laki mbili lakini hakwenda kulichukua na baadaye kutaka kurudishiwa pesa zake ambapo Mai aligoma.



“Yule mwanajeshi baada ya kutolichukua lile gauni na kwenda kukodi kwingine, kuna siku akaenda kwa Mai kudai arudishiwe pesa zake, Mai akagoma ndipo taarifa zikafika Kituo cha Polisi Kilwa Road.

“Mai naye alienda kufungua mashtaka kwenye Kituo cha Changombe, wakaitwa na kuambiwa wayamalize lakini mwanajeshi huyo amepania kumpeleka mahakamani Mai,” alisema rafiki huyo.



Baada ya habari hizi kutua kwenye dawati la Risasi Jumamosi, mwandishi wetu alimtafuta mwanajeshi huyo ambaye alikiri kumdai Mai fedha hizo na kueleza dhamira yake ya kumpeleka mahakamani.



Naye Mai alipotafutwa na kuulizwa juu ya msala huo alisema yupo tayari kwa lolote akidai kuwa ‘mjeda’ huyo amekuwa na tabia ya kutisha watu.

“Nimejaribu sana kuwa muungwana, biashara yangu siyo ya kuichezea na kutisha wafanyakazi wangu, sheria itafuata mkondo wake,” alisema Maimartha

RC Makonda ni Kama Malaika Aliletwa Duniani Kuja Kufanya ya Mola Wako- Wema Sepetu

0
0
RC Makonda ni Kama Malaika Aliletwa Duniani Kuja Kufanya ya Mola Wako- Wema Sepetu
Muigizaji wa filamu mwenye nyota yake bongo na Afrika Mashariki Wema Sepetu, amefunguka na kudai Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ameletwa duniani na Mungu kwa lengo la kusaidia watu nasio vinginevyo.


Wema ametoa kauli hiyo mara baada ya Mhe. Makonda kuonesha nia ya kumsaidia kumsafirisha kijana Ahmed Albaity kwenda nchini China kwa lengo la kupatiwa matibabu juu ya ugonjwa aliokuwa nao wa kupooza mwili mzima.

"Nikisema 'RC' wangu ni mtumishi wa Mungu basi namaanisha, mimi 'sometimes' nasema uliletwa duniani kuja kufanya ya Mola wako tu. Mungu azidi kukubariki 'my RC you are just like a guardian angel', ipo siku wataelewa tu. 'I got a Good Feeling about Ahmed and Inshallah God will work a miracle, kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho", amesema Wema Sepetu.

Kijana Ahmed Albaity alipooza mwili wake mnamo 2007 baada ya kucheza vibaya michezo ya kujirusha 'dive' katika bahari na kwa bahati mbaya alikosea na kujipiga kichwa chini ambapo ilipelekea kupata matatizo yote hayo mpaka sasa.

JE Umehangaika na Matatizo ya Kimapenzi Kwa Muda Mrefu? Muone Shehe Chalo Atakutatulia Matatizo yako Kirahisi

0
0
JE umehangaika na matatizo haya kwa muda mrefu mtalamu Challo anayo dawa ya kuvuta mpenzi Je unasumbuliwa na mpenzi umeachwa na mpenzi au Mme mke na Bado unampenda na umejaribu sehemu nyingine Bila mafanikio njoo utatuliwe haraka na kundumisha ndoa yenu..

Umekimbiwa na mmeo mkeo au mpenzi na anaishi na mtu mwingine atarundi haraka kusafisha nyota mvuto wa mwili na biashara minguu kufa ngazi kuwaka moto ngiri tumbo kuunguruma na wakina Baba wasiojiweza katika tendo la uyumba kuchelewa kufika kileleni tunatibu Busha Bila oprasheni bali kwa kutumia vitabu vya dini

Tunatoa pete ya utajiri Bila mashariti mkufu wa bahati unauza Mali ya haindi unapoteza pesa kwenye biashara yako Bila kujua unataka kupandishwa cheo

Wasiliana na mtalamu Shehe Challo 0714006521

Niyonzima Afuguka Kuhusu Hali Yake "Afya Yake Inaimarika Siku Hadi Siku"

0
0
Niyonzima Afuguka Kuhusu Hali Yake "Afya Yake Inaimarika Siku Hadi Siku"KIUNGO wa Simba, Haruna Niyonzima ametoa kauli za matumaini kwa mashabiki wa timu yake akisema anaendelea vizuri na matibabu ya kifundo cha mguu kilichomweka nje ya uwanja kwa miezi mitatu sasa.



Kwa wiki ya pili sasa Niyonzima yupo nchini India katika Hospitali ya Jeevika ya nchini humo, akipatiwa matibabu ya enka bila ya kufanyiwa upasuaji wa aina yoyote kama wengi walivyodhani.



Akizungumza na Championi Jumamosi, Niyonzima alisema afya yake inaimarika siku hadi siku, hivyo anamshukuru Mungu kwa kuendelea kumsimamia katika maendeleo ya afya yake.



Niyonzima raia wa Rwanda aliyejiunga na Simba akitokea Yanga msimu huu, alisema kutokana na maendeleo yake mazuri ya afya anaamini siku zake za kurejea uwanjani zinakaribia.



“Kwanza nina furaha timu yangu inaendelea kufanya vizuri, halafu nina faraja kuona majeraha yangu yanaendelea, natambua Mungu anaendelea kunipa wepesi wa kupona.



“Naamini siku si nyingi nitaungana na wenzangu kwani matibabu ninayopata ni mazuri kiasi kwamba naona Mungu ni mwema sana kwangu, kwani nilijua nitafanyiwa upasuaji kitu ambacho hakijafanyika.



“Sina uhakika zaidi lakini nategemea kurudi Jumamosi (leo) kama mambo yakikaa sawa,” alisema Niyonzima.

Serikali Yaiomba Benk ya Dunia Kukopeshwa Dola Milioni 150

0
0
Serikali Yaiomba Benk ya Dunia Kukopeshwa Dola Milioni 150
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango ameiomba Benki ya Dunia (WB), kuipa Tanzania mkopo wa Dola 150 milioni za Marekani ili kuchochea ukuaji wa uchumi na utoaji wa huduma nchini.

Dk Mpango ametoa ombi hilo alipokutana na Mkurugenzi wa Uchumi Mpana, Biashara na Uwekezaji wa Benki ya Dunia, Felipe Jaramilo katika ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango jijini DSM ambapo Waziri Mpango alifanikiwa kumuelezea Mkurugenzi huyo namna Uchumi wa Tanzania unavokua.
Waziri Mpango ameishukuru Benki ya Dunia kwa kuendelea kuisaidia Serikali ya Tanzania haswa hii iliyopo madarakani katika kutekeleza miradi ya maedeleo nchini.

“Pamoja na ukuaji mzuri wa uchumi, Taifa bado linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwamo ukosefu wa ajira kwa vijana, kiwango cha umasikini bado kiko juu, ukuaji mdogo wa sekta ya kilimo na kupungua kwa mikopo ya benki za biashara kwa sekta binafsi,” Dk Mpango.

Baby Madaha Ashindwa Kulipa Kodi Aamua Kuhamia kwa Shogaake

0
0
Baby Madaha Ashindwa Kulipa Kodi Aamua Kuhamia kwa Shogaake
SKENDO iliyomganda msanii wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph Madaha ni ya kushindwa kulipa kodi kwenye nyumba aliyokuwa akiishi awali na kuhamia kwa ‘shogaake’ Issabela Mpanda ‘Bela Fasta’ maeneo ya Mbezi Beach.

Madai ya awali yalieleza kuwa, mambo sasa hivi yamemuendea kombo staa huyo kiasi cha mkwanja kumpitia pembeni, mazingira yaliyomfanya ashindwe kwenye baadhi ya mahitaji muhimu likiwemo hilo la kodi ya pango.

Kufuatia madai hayo, paparazi wetu alimtafuta Madaha na alipopatikana alishangazwa na madai hayo na kusema:

“Hayo ni maneno ya watu wenye chuki na mimi. Si kweli kwamba nimefulia. Na ifahamike kwamba siku nyingi nakuwa niko Dubai ambako nafanya shughuli zangu, ninapokuja huku Bongo kufikia kwa Bela siyo tatizo.

“Nilirudi hivi karibuni kwa ajili ya harusi ya mdogo wangu na siishi hapa kwa hiyo suala la kushindwa kulipa kodi na kwenda kuishi kwa Bela halina mashiko!

Viewing all 104415 articles
Browse latest View live




Latest Images