Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104702 articles
Browse latest View live

Mwigulu Akagua Ujenzi wa Nyumba za Polisi Arusha

$
0
0
Mwigulu Akagua Ujenzi wa Nyumba za Polisi Arusha
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Dk. Mwigulu Nchemba  ametembelea kukagua ujenzi wa nyumba za polisi Mkoani Arusha ambazo ziliungua kwa ajali ya moto iliyotokea mwaka jana ambapo amekiri kufurahishwa na kuridhishwa na hatua za ujenzi zilipofikia.


Dk Nchemba amesema ameridhika na hatua iliyofikia katika  ujenzi wa nyumba hizo ambazo ni za kisasa ambapo amedai kwamba hata polisi hao watakuwa wanajisikiam vyem kuishi katika nyumba hizo.

Aidha Waziri huyo mwenye dhamana ya mambo ya ndani  ameshukuru hatua iliyochukuliwa na Rais Magufuli kusaidia fedha ili ujenzi huo uanze haraka pamoja Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo na wafanyabiashara wa Arusha kusaidia ujenzi wa nyumba hizo mpaka sasa ulipo fikia kwa kusema kwamba walichukua hatua za mapema pale moto ulipotokea.

"Leo hii mmeona nyumba hizi za kisasa ambazo zitafanya askari wangu kuanza kupigia selfie katika nyumba zao kwamba hapa ndipo ninapokaa, hiili ni jambo kama waziri napaswa kumshukuru sana Rais kwani litaongeza morali ya kuendelea kufanya kazi nzuri wanayoifanya," Dkt. Nchemba.

Naye mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amemshukuru Waziri Nchemba kwa msaada wake wa kufanikisha ujenzi huo ikiwa ni pamoja na kuwa karibu nao kati kipindi chote hicho, ambapo pia amemuomba Waziri Nchemba awasaidie gari la polisi katika kituo cha polisi Murieti na amekubali kuwasaidia kuwaletea gari ili kusaidia kupunguza matukio ya kihalifu maeneo hayo kwani kwasasa mji huo watu wengi wanaishi maeneo hayo na askari wanategemea gari linalotoka Kituo Kikuu cha polisi Arusha.



Taifa Stars Kucheza na Algeria na Dr Congo Mwezi Huu

$
0
0
Taifa Stars Kucheza na Algeria na Dr Congo Mwezi Huu

Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars inatarajia kucheza michezo miwili ya kirafiki mwezi huu wa Machi kwenye tarehe za kalenda ya FIFA.

Taifa Stars itakuwa ugenini nchini Algeria Machi 22,2018 kucheza dhidi ya Algeria kabla ya kucheza na DR Congo Machi 27,2018 Uwanja wa Taifa Dar es Salaam,Tanzania.
Tayari mechi hizo zimethibitishwa na pande zote mbili kuchezwa katika tarehe hizo.

Benki ya Dunia Yampongeza Rais Magufuli Kwa Kusimamia Uchumi Vizuri

$
0
0
Benki ya Dunia Yampongeza Rais Magufuli Kwa  Kusimamia Uchumi Vizuri
Mkurugenzi wa Uchumi Mpana, Biashara na Uwekezaji wa Benki ya Dunia, Dkt. Felipe Jaramilo, ameipongeza Serikali ya awamu ya tano ya Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kazi nzuri inayofanya ya kusimamia uchumi mpana.


Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania, Bi. Bella Bird na Mkurugenzi wa Uchumi, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Felipe Jaramilo, mara baada ya kikao kilichofanyika Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango alikutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Uchumi Mpana, Biashara na Uwekezaji wa Benki ya Dunia, Dkt. Felipe Jaramilo katika ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es Salaam.

Katika kikao hicho, Waziri wa Fedha na Mipango aliishukuru Benki ya Dunia kwa kuendelea kuisaidia Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dk. John Pombe Joseph Magufuli katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maedeleo hapa nchini.

Dkt. Mpango ameeleza kuwa uchumi wa nchi umeendelea kukua kwa kiwango cha kati ya asilimia 6-7 kwa muda na hivyo kuiwezesha Serikali kuendelea na utoaji wa huduma za jamii na kuwekeza katika miradi mbalimbali ya maendeleo.

Dkt. Mpango ameeleza kuwa pomaja na nia ya kuendeleza mafanikio mazuri yaliyopatikana katika awamu za Serikali zilizopita, Serikali ya Awamu ya Tano ya Dkt. John Pombe Joseph Magufuli imedhamiria kwa dhati kujenga uchumi imara kwa kuendeleza viwanda na kuweka mazingira mazuri ya biashara ili kuvutia wawekezaji wa ndani na wale wa nje kuja kuwekeza nchini , kujenga miundombinu ya barabara, reli, umeme , viwanja vya ndege na kuongeza uwekezaji katika utoaji wa huduma za jamii kama vile elimu, afya na maji.

Aidha, ameeleza kuwa katika kufikia malengo hayo , Serikali imefanya juhudi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusimamia vizuri ukusanyaji wa mapato, kusimamia vizuri matumizi ya fedha za Serikali, kuongeza bajeti ya maendeleo hadi kufikia asilimia kati ya 35 na 40 ya bajeti nzimat, kuongeza ufanisi katika utendaji wa umma na kupambana na rushwa pamoja na mambo mengine.

Pamoja na ukuaji mzuri wa uchumi, Dkt. Mpango alisema kuwa Taifa bado linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa ajira kwa vijana, kiwango cha umasikini bado kiko juu, ukuaji mdogo wa Sekta ya kilimo ambayo imeajiri takribani asilimia 70 ya watanzania unaosababishwa na ukosefu wa mbegu bora, miundombinu ya umwagiliaji na soko la uhakika, na kupungua kwa mikopo ya benki za biashara kwa sekta binafsi pamoja na mambo mengine.

Katika kusaidi juhudi za Serikali kupambana na changamoto mbalimbali , Dk. Mpango aliiomba Benki ya Dunia kupitia kwa Dk. Felipe kuisadia Serikali mkopo wa Dola za Kimarekani milioni 150 kwa ajili ya kuchochea ukuaji wa uchumi na utoaji huduma ( Growth and Service Delivery) amabao uko katika hatua ya maandalizi.

Mkurugenzi wa Uchumi Mpana, Biashara na Uwekezaji wa Benki ya Dunia, Dkt. Felipe Jaramilo, kwa upande wake aliipongeza Serikali ya awamu ya tano ya Dk. John Pombe Joseph Magufuli kwa kazi nzuri inayofanya ya kusimamia uchumi mpana, kuongeza makusanyo ya ndani ambayo yanasaidia upatikana fedha kwa ajili ya kugharamia uwekezaji katika miradi mbalimbali ya maendeleo, kupambana na rushwa, kusimamia matumizi ya fedha za umma, na kuongeza ufanisi katika utendaji wa kazi za umma.

Sijaona Tatizo Kwenye Wimbo wa Diamond wa Hallelujah

$
0
0
Wadau nimejaribu kuutazama kwa umakini sana wimbo wa Diamond Uitwao Hallelujah, kimsingi sijaona tatizo lililofanya wimbo huo kufungiwa.

Huku ni kutaka kuuwa vipaji vya wanamuziki wetu ambao wanajaribu kufikia level za kimataifa kwa juhudi zao wenyewe, Kwa mimi binafsi ningeipa hongera Basata na Wizara husika wangekuwa mara kwa mara wakikaa na hawa vijana na kuwapa elimu jinsi ya kuweza kufanya ili wafaidike na kazi zao za sanaa badala ya kujenga uadui ambao unaonekana kama ni kutafuta kiki ili waonekane wanafanya kazi..

By Jorome

Serikali yawajibu Umoja wa Ulaya(EU) na Marekani kuhusu kutokuwepo usalama na haki za binadamu Tanzania

$
0
0

Serikali ya Tanzania imekanusha tuhuma kwamba inaminya demokrasia nchini humo na kusema kuwa imesikitishwa na matamko kadhaa yaliotolewa na Marekani na Umoja wa Ulaya (EU) na kuungwa mkono na baadhi ya balozi za nchi za Magharibi.

Taarifa ya serikalli ya Tanzania imefuatia matamko yaliyotolewa na nchi za magharibi wiki za hivi karibuni yakielezea wasiwasi wao kutokana na matukio ya kiusalama ambayo wameeleza yanatishia utawala wa kisheria na maadili ya kidemokrasia nchini Tanzania.

Katika wiki za hivi karibuni polisi wa Tanzania wameshutumiwa kwa kutumia nguvu za kupita kiasi kushughulikia mivutano ya kisiasa na pia wanasiasa kadha wa upinzani wakiwemo wabunge mara kwa mara wameitwa polisi kwa mahojiano kutokana na madai ya kufanya mikutano isiyo halali.

Mbunge wa upinzani Joseph 'Sugu" Mbilinyi na afisa mwingine wa chama cha Chadema mjini Mbeya walihukumiwa kifungo cha miezi mitano gerezani mwishoni wa Februari baada ya kukutwa na hatia ya kumkashifu Rais John Pombe Magufulu

Taarifa hiyo iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania pia imesema kuwa tayari nchi hiyo imechukua hatua kukubaliana na vikwazo vilivyowekwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa dhidi ya Korea Kaskazini. Nchi za magharibi ziliishutumu Tanzania kwa kukiuka vikwazo hivyo.

Hata hivyo Tanzania imesema tuhuma kwamba imekiuka vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya silaha za nyuklia za Korea Kaskazini na programu yao ya makombora ya balistika hazijaweza kuthibitishwa..

Taarifa hiyo imeeleza kuwa suala la utawala wa sheria na demokrasia katika tamko hilo la mabalozi linaonyesha sintofahamu iliyoko juu ya usalama na changamoto za kisiasa ambazo Tanzania imekuwa ikikabiliwa nazo kwa kipindi cha miezi 18 na kwamba matamko hayo yamekuwa sio tafsiri sahihi ya hali ya kisiasa na usalama iliyopo Tanzania.

“Ni kawaida kwa wanadiplomasia wa kigeni kufuatilia na kuripoti hali ya kisiasa na usalama inayoendelea katika nchi walizotumwa. Lakini tunashangazwa na ukimya uliowazi katika kipindi cha nyuma wa mabalozi hawa juu ya vitisho vya uvunjifu wa amani uliokuwa haujawahi kutokea na changamoto nyingine ambazo Tanzania imekuwa ikikabiliana nazo katika maeneo matatu ya Kibiti-Mkuranga –Rufiji yanayopakana,” limesema tamko hilo.

Wizara hiyo imeeleza kuwa vitisho hivyo vimewauwa watu wasio na hatia na kwa sadfa ya ajabu, wengi wa waliouwawa walikuwa kutoka chama tawala.

Mauaji hayo yalikuwa yametanguliwa na matukio kama hayo ya uvunjifu wa amani katika maeneo mbalimbali ya nchi yakiwa ya aina yake yalihusisha uvunjifu wa amani.

Kwa mujibu wa tamko hilo pamoja na kuwepo taarifa za matukio haya ya uvunjifu wa amani yalitolewa na vyombo vya habari nchini, hakukuwa hata na tamko lililolaani vitendo hivyo kutoka kwa mabalozi hao.

Wizara imehoji kuwa ni hivi sasa tu ndio EU inataja juu juu shambulizi la silaha lililotokea Mkoa wa Pwani katika kipindi cha miaka miwili.” Kuchelewa kutolewa kwa matamko hayo baada ya muda mrefu na wakati mgumu unastaajabisha.

Moja ya matamko yaliyotolewa na mabalozi wizara imesema ni jambo zuri kwa mabalozi wametambua wito wa Rais Magufuli akitaka uchunguzi ufanyike wa matukio mengine ya uvunjifu wa amani katika wimbi la operesheni ya Kibiti, Mkuranga na Rufiji.

Lakini wizara imesema kuwa matamko hayo ya mabalozi hayakutambua uhusiano uliokuwepo kati ya hatua za kishujaa ambazo zimechukuliwa na Rais Magufuli kuondoa ufisadi, madawa ya kulevya, ukwepaji kodi, ujangili wa nyara za serikali na kuhakikisha uwajibikaji katika sekta binafsi na za umma, na matukio ya usalama.

“Hatua za serikali ya awamu ya nne bila shaka zimewakasirisha watu wenye nguvu ndani na nje ya nchi ambao wanamaslahi binafsi katika hali ya uzembe iliokuwa inaendelea hapo awali nchini,” taarifa hiyo imesema.

Jeshi la Polisi Lakamata Kikundi cha Wauaji

$
0
0
 Jeshi la Polisi Lakamata Kikundi cha Wauaji
Kundi la vijana 29 wanaodaiwa kufanya uhalifu mkoani Mbeya maarufu kama wakorea weusi wamekamatwa na Polisi kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya kiuhaulifu, kupiga, kuua na kuibia watu vifaa mbalimbali.


Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya Naibu Kamishina wa Polisi, Mohammed Mpinga amewaambia wanahabari ofisini kwake leo, Jumamosi kuwa watuhumiwa hao bado wanaendelea kuhojiwa na wengine watafikishwa Mahakamani mara tu baada ya upelelezi utakapokamilika.

Aidha mwanzoni mwa mwezi Januari, 2018, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanikiwa kuwakamata watuhumiwa nane kutokana na kujihusisha na vitendo vya uhalifu katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Mbeya ambao walifikishwa Mahakamani na kwa sasa wanatumikia vifungo vya nje.

 Kwa upande mwingine, Kamanda MPINGA ametoa wito kwa vijana na jamii kwa ujumla kuacha kujihusisha na vitendo vya uhalifu kwani ni kinyume cha sheria na badala yake wajishughulishe na kazi halali kwa ajili ya kujipati kipato.

Chamwino Yajipanga Kutokomeza Mimba za Utotoni

$
0
0
Chamwino Yajipanga Kutokomeza Mimba za Utotoni
Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma imejipanga kupambana na kutokomeza mimba za utotoni katika Wilaya hiyo.


Akizungumza katika uzinduzi wa Kapeni ya Kutokomeza Mimba za Utotoni katika Shule za Msingi na Sekondari katika Kata ya Haneti Wilayani Chamwino, Diwani wa Kata ya Haneti Mhe. Peter Elia Chidawali amesema kuwa Kata yake na Wilaya kwa ujumla wamejipanga katika kupambana na vitendo vya ukatilia wa kijinsia yakiwemo matukio ya mimba na ndoa za utotoni .


Mhe. Peter Elia Chidawali ameongeza kuwa hawatakubali kuona watoto wao wanapoteza haki yao ya msingi ya kuendelezwa ya kupata Elimu kwa kupata mimba au kuolewa wakiwa bado shuleni.

“Tutaendeleza Kampeni katika ngazi za familia kwa kuwaelimisha wazazi na walezi kuhusu madhara ya mimba za utotoni ili tuokoe kizazi cha kesho”alisema Mhe. Chidawali.

Naye Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Watoto kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi Rose Minja amesema kuwa suala la mimba za utotoni limezidi kuongeza siku hadi siku hivyo basi Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto alizindua Kampeni ya Kutokomeza Mimba za utotoni kwa lengo la kuwezesha utoaji wa elimu kwa wanafunzi, wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kushiriki mapambano dhidi tatizo hili.

“Wanafunzi, Walimu, Wazazi na walezi tuweke mikakati thabiti ya kupambana na tatizo hili la mimba za utotoni” alisisitiza Bi. Rose.

Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Bi. Shukuru Shanjala ameeleza kuwa Wilaya ya Chamwino imejipanga katika kuzuia mimba za utotoni kwa kuhakikisha wanawafikia wahusika katika ngazi za shule na familia na kutoa elimu kwa watoto wote wa kike wanaowazunguka ili kuondokanana tatizo la mimba za utotoni katika wilaya yao.

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inaendelea na kampeni ya kuzuia mimba za utotoni chini katika shule za Msingi na Sekondari ijulikanayo kama Mimi ni Msichana Najitambua Elimu ndio Mpango Mzima sambamaba utekelezaji wa Mpango Kazi 
wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na watoto katika ngazi mbalimbali nchini ili kupunguza ukatili kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2021/2022.

Mr. Nice Awapa Pongezi BASATA

$
0
0

Mr. Nice Awapa Pongezi BASATA
Msanii ambaye alifanya vizuri katika muziki kipindi cha nyuma kwa staili yake ya Takeu, Mr Nice amefunguka na kuwaasa wasanii wenzake kuimba vitu vyenye msingi ili kusudi wasije kuwapotosha mashabiki zao wanaowatazama.
Mr. Nice ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha 'Bongo Flava Top 20' kinachorushwa na East Africa Radio baada ya kupita siku chache kupita tokea Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kupeleka orodha ya nyimbo 15 zisizokuwa na maadili kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ambazo zina maudhui ambayo ni kinyume na maadili na Kanuni za Huduma ya Utangazaji ya mwaka 2005.

"Mimi ninachoweza kusema bila ya kuficha, vijana na watoto wadogo ndio wanaopenda muziki sasa hivi, hivyo basi msanii atakapoimba kitu ambacho hakina maana, adabu wala mantiki atakuwa anampotosha mtoto. Maana vijana hao hao wanaosikiliza na kutazama muziki wetu wengine husema natamani kuwa kama msanii fulani bila ya kujua mtu huyo anaimba matusi matupu 'so' unategemea nini hapo", amesema Mr. Nice.

Darassa Apotezwa na Dawa za kulevya ?

$
0
0

Darassa Apotezwa na Dawa za kulevya ?
Mtayarishaji wa muziki nchini Tanzania, Abba amefunguka na kudai si kweli ukimya wa Darassa unatokana na matumizi ya dawa za kulevya kama baadhi ya watu wanavyodhani na kuwataka wawe wavumilivu kwani muhusika mwenyewe atakuja kujitokeza.
Abba ametoa kauli alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha eNewz inayorushwa na EATV baada ya kuonea mfululizo wa tetesi zinazomuhusisha Darasa na matumizi ya dawa za kulevya na kupelekea kupotea katika tasnia ya muziki mpaka hii leo.

"Nashindwa kuwaelewa kwa jinsi mnavyosema Darasa haonekani sasa mmemuona vipi akiwa anatumia dawa za kulevya ?. Darasa yupo poa kabisa na labda hayo madude wanaosema wao wanayatumia wenyewe kwenye ndoto zao wanaoziota hao watu", amesema Abba.
Pamoja na hayo, Abba ameendelea kwa kusema "Darasa yupo poa na familia yake na wala hatumi kitu chochote mimi kama mwanae nasema yupo 'fresh' na kila siku nipo na Darasa na muda wote nikimuhitaji huwa nampata".

Jeshi la Polisi Dodoma Lawashikilia Wahamiaji

$
0
0

Jeshi la Polisi Dodoma Lawashikilia Wahamiaji
Jeshi la Polisi mkoani Dodoma linawashikilia wahamiaji haramu wawili raia wa Rwanda pamoja na watoto 20 wa mitaani wenye umri kati ya miaka 7 hadi 15 ambao wamekuwa wakitumiwa na wahalifu kuiba vifaa mbalimbali vya magari.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma Giles Muroto akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma  , amesema katika msako uliofanywa tangu Februari 28 mwaka huu, wamefanikisha kukamatwa kwa wahamiaji wawili na watoto hao ambao wamekuwa wakitumia dawa za kulevya aina ya gundi.

Kamanda huyo amesema wazazi wa watoto hao wanapaswa kufika kituoni kuwachukua watoto hao ili kuepusha kushtakiwa kwa mujibu wa sheria kwa kushindwa kuwalea watoto wao.

Aidha amesema pia katika msako huo jeshi hilo limewakamata wahamiaji haramu wawili februari 28, mwaka huu ambao ni raia wa Rwanda katika 'check point' ya polisi mtera wilayani Mpwapwa barabara ya kuelekea Iringa.

Neymar Awasili Belo Horizonte kwa Ajili ya Upasuaji

$
0
0
Neymar Awasili Belo Horizonte kwa Ajili ya Upasuaji
NYOTA wa Paris Saint-Germain, Neymar amewasili mjini Belo Horizonte akiwa na mama yake, Nadine Goncalves Da Silva and na Daktari wa timu ya taifa ya Brazil, Rodrigo Lasmar jana tayari kwa upasuaji wa mguu.

Nyota huyo wa anatarajiwa kufanyiwaupasuaji wa mguu baada ya kuumia enka Jumamosi iliyopita, timu yake PSG ikishinda 3-0 katika Ligi ya Ufaransa, Ligue 1 dhidi ya Marseille.

Pamoja na klabu yake awali kusema mchezaji huyo hakuhitaji upasuaji, lakini mshambuliaji huyo jana usiku aliwasili katika hospitali ya Mater Dei Hospitalhuyo nchini kwao, Brazil.

Brazil imeamua kumchukua Neymar kumtibu haraka ili isije ikamkosa kwenye Fainali za kombe la Dunia nchini Urusi katikati ya mwaka.

Sasa PSG wanaelekea kwenye mchezo wa marudiano wa 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya wiki ijayo bila Neymar wakitakiwa kuifunga Real Madrid 2-0 mjini Paris ili kwenda Robo Fainali, kufuatia kufungwa 3-1 kwenye mchezo wa kwanza Madrid.

Waandamanaji wakabiliana na Polisi Ukraine

$
0
0
Waandamanaji wakabiliana na Polisi Ukraine
Watu kadhaa wamejeruhiwa mjini Kiev nchini Ukraine, wakati wa makabiliano kati ya waanamanaji wanaoipinga serikali na Polisi.

Vyombo vya habari nchini humo vimesema makabiliano hayo yalianza wakati waandamanaji walipowasha moto matairi ili kuwazuia maafisa wasifanyie ukaguzi Kambi ya waaandamanaji iliyokuwa nje ya Bunge.

Polisi wa Ukraine wamesema watu 50 wamekamatwa.Wamesema walikuwa wanafanyia uchunguzi kambi hiyo ili kupata ushahidi kuhusu makabiliano yaliyofanyika jumatatu iliyopita na kusababisha maafisa polisi kadhaa kujeruhiwa.

Katika kamatakamata hiyo Polisi wamekamata maguruneti ya kurushwa kwa mkono yaliyokuwa kwenye turubai la kambini hapo.

Kutana na Mtabibu Mongwa Mganga wa Waganga Sasa Anapatikana Mikoa Yote

$
0
0
KUTANA NA MTABIBU MONGWA MGANGA WA WAGANGA SASA WAKO MIKOANI KARIBU YOTE NCHINI...
.
HIVYO WATATOA TIBA MAENEO YOTE YA MBEYA ,DODOMA, IRINGA , MOROGORO, MWANZA,ZANZIBAR

==>KWA WALE WENYE KUHITAJI TIBA

Husafisha nyota na kutoa Pete za bahati na kwawale walio sumbuka kwaajili ya matibabu na hawakufanikiwa chochote sasa njoo ujionee miujiza hapo kwahapo bila malipo yoyote malipo baada yakazi napia humpa mtu jini la mali kwayule anaye taka kumiliki bila mashariti yoyote
Tunatibu magonjwa mbalimbali yaliyo shindikana mpenzi aliye kukimbia nakumrudisha kwa masaa 24 tu napia natoa dawa za nguvu za kiume kuurefusha uume paka pale unapotaka .
Natoa dawa za biashara na mvuto ==tunatoa dawa zauzazi kwa wale kina mama wenye matatizoya uzazi walio angaika kwa muda mrefu bila kupata mafanikio yoyote njoo umalize tatizo lako sasa
Natoa mazindiko yanyumba na mwili biashara na mvuto kazini
Kupandisha nyota ili kungaa kupandishwa cheo kazini kurudisha mali zilizo pote zilizo ibiwa kuzulumiwa
Kesi zilizo shindikana uzimaliza mara moja namengine mengi ya siri piga simu

+255 764291657
+255 764291657
+255 764291657

Mkuu wa Chuo Afunguka Kuhusu Mwanafunzi wa CBE Alieanguka Toka Gorofani

$
0
0
Mkuu wa Chuo Afunguka Kuhusu Mwanafunzi wa CBE Uuanguka Toka Gorofani
Siku za hivi karibuni kumekuwa na taarifa kuwa mwanafunzi Shija wa Chuo cha Biashara CBE Dar es salaam amefariki kutokana na ugomvi wa mapenzi na ikadaiwa kuwa alirushwa kutoka gorofani kwenye Hostel baada ya kutokea ugomvi huo.

Mkuu wa Chuo hicho Profesa Emmanuel Mjema ambaye ameeleza kuwa tukio hilo lilitokea katika hosteli binafsi maeneo ya Ilala na sio katika hosteli ya chuo kama ilivyokuwa ikizungumzwa kwenye mitandao ya kijamii.

Profesa Mjema ameeleza kuwa Marehemu anayetambulika kwa jina la Shija alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanafunzi mwenzake na siku ya tukio alikwenda kumtembelea na kumkuta akiwa na Mwanaume mwingine.

Baada ya kuwakuta ugomvi uliibuka na kupelekea Shija kujirusha mwenyewe kutoka ghorofani na kufikwa na mauti.

Baraza la Maaskofu Lakomalia Katiba Mpya

$
0
0
Baraza la Maaskofu Lakomalia Katiba Mpya
Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), limesema ili amani iendelee kuwepo majadiliano ndio nyenzo kuu itakayosaidia kuhuisha mchakato wa Katiba Mpya.

Pia limeitaka Serikali kuweka nia ya dhati na kutii kiu ya Watanzania iwapo wengi wao watahitaji mchakato wa Katiba Mpya uendelezwe.

Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu wa TEC, Padri Daniel Dulle, wakati akifungua kongamano la kujadili Katiba na ujenzi wa amani wakati wa uchaguzi lililoandaliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).

Hii ni mara ya pili katika kipindi kisichopungua mwezi mmoja kwa TEC kutoa kauli kama hiyo, kwani kumbukumbu zinaonyesha kuwa Februari 11 mwaka huu, Baraza hilo katika ujumbe wake wa Kwaresma lilitoa msimamo katika masuala matatu kisiasa, kiuchumi na kijamii ambapo lilionya kutozingatia matakwa ya Katiba katika kuendeleza shughuli za kisiasa.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Baraza hilo, Padri Raymond Saba, Padri Dulle, alisema baada ya mchakato wa Katiba Mpya kukwama sasa ni fursa nzuri ya kuendeleza mchakato huo kwa njia ya majadiliano ili kudumisha amani.

“Majadiliano ni nyenzo ya kupambana na tabia ya ubinafsi, ili kujenga umoja huo lazima kuwepo na upendo, mshikamano na maridhiano ya watu na kila mtu kupewa nafasi ya kutoa maoni hata kama yanapingana na mtu mwingine na ukiwa unapatanisha kwa njia hiyo unaitwa mwana wa Mungu.

“Ndilo lengo la kukaa hapa na kujadiliana ili kujenga Taifa letu kwa lengo la kupata Katiba Mpya ambayo kila mmoja anaitamani. Kunapotokea mtafaruku ndipo kunakuwa na chuki kama kikundi kingine hakishirikishwi.  Haki na amani ni matunda tu, kwani ukosefu wa haki ni chanzo cha vita inayoacha makovu na chuki za kisiasa kwenye chaguzi. Kama tunataka kukwepa haya makovu lazima watu tujenge tabia ya kujadiliana,” alisema.

Alisema tangu miaka ya 1800, Kanisa Katoliki limekuwa likitoa miongozo kuhusu masuala ya utawala ili kudumisha amani.

“Suala la Katiba ni nia ya watu wote si ya mtu mmoja, ni sauti ya watu na kadiri watu wanavyohitaji sheria na miongozo. Pengine kikundi kikubwa kinahitaji kidogo hakihitaji cha msingi ni kuangalia wananchi wanahitaji nini kwani kwa mujibu wa ibara ya nane ya Katiba ya sasa, Katiba ni mali ya wananchi,” alisema.

Aidha, akichangia mjadala katika kongamano hilo, Profesa Mwesiga Baregu ambaye alikuwa akimwakilisha Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia nchini (TCD), James Mbatia, alionya Serikali kuhakikisha kabla ya kuingia kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2020, Katiba Mpya inapatikana.

Baregu ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, alisema ni vema kukamilisha kiporo hicho cha Katiba kwa sababu viashiria vyote vya hatari vimekwishaonekana katika chaguzi ndogo zilizofanyika hivi karibuni hususani Jimbo la Kinondoni.

“Tujitahidi kwa vyovyote vile kuhakikisha uchaguzi unaokuja si tu wa haki lakini matokeo yake yawe ya kuaminika. Kwa sababu inaelekea chaguzi zetu kuwa ‘security election’.

“Uchaguzi uliopita Kinondoni tunaambiwa kuna vituo ambavyo polisi walizidi wapiga kura, huu uwapo wa polisi kwenye chaguzi ni tatizo kwa sababu inatafsirika kuwa lazima kutakuwa na machafuko au kuna kitu polisi wamegundua,” alisema.

Aidha, Profesa Baregu, alipendekeza njia tatu za kuendeleza mchakato wa Katiba Mpya kwa kuwa hali iliyopo lazima kuwepo na njia ya kuishawishi Serikali.

“Kwanza twende kwenye kura ya maoni, tunaweza kutangaza kura ya maoni kuhusu Katiba pendekezwa ila sijui kura ya maoni kama itaendeshwa kwa uhuru au haki. Kwa sababu hata katika Katiba pendekezwa tumeona asilimia 85 ya maoni ya wananchi yamenyofolewa.

“Pili kuundwe Bunge la Katiba lenye wajumbe wasiokuwa wabunge kwani hawa waliopo bungeni watatengeneza Katiba ya kuwalinda na tatu kuundwe tume ya wataalamu wa Katiba kama walivyofanya wenzetu Kenya, kwani mahali tulipofika lazima tutoke kwenye ujumla ujumla tuwe na mashinikizo ya kuitaka Serikali ifanye nini kabla ya uchaguzi mkuu ujao,” alisema.

Pamoja na mambo mengine alieleza kushangazwa na baadhi ya mawaziri wanaodai kuwa rasimu ya pili ya Katiba Mpya iliwalisha wananchi maoni jambo ambalo si kweli.

“Baadhi ya mawaziri wanasema mambo ya kipumbavu eti watu wamelishwa maneno na tume, kusema kweli hiyo ni dharau kwa watu kuwa hawawezi kusema Rais apunguziwe madaraka na mambo mengine,” alisema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha ACT – Wazalendo, Yeremia Maganja, alisema hitaji la Katiba ni tangu vizazi na vizazi hivyo Serikali haitakiwi kupuuza takwa la wananchi.

“Pia tunaona tatizo linaloikabili nchi yetu ni taasisi ya rais kutokuwa na mamlaka inayoisimamia, ndiyo maana rais anaonekana kuwa amegeuka Mungu mtu,” alisema.

Aidha, Rais mstaafu wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), John Seka, alisema ili kuwepo na chaguzi za kidemokrasia lazima kuwepo na mfumo wa kisheria unaozingatia kutibu vidonda vya chaguzi zilizopita.

“Pia kuwe na miundombinu wezeshi kwa vyama vyote ikiwamo kupatiwa gharama za uchaguzi pamoja na mambo mengine,” alisema.

Kwa upande wake mwakilishi kutoka Zanzibar, Musa Kombo Musa, alilaumu baadhi ya Wazanzibari walioshiriki kupitisha Katiba pendekezwa na kudai kuwa hao ndio wamesababisha mchakato huo wa Katiba Mpya usitimie.

“Sijui Wazanzibari waliokuwa kwenye bunge lile waliingiwa na wazimu gani, wamesababisha tuendelee kukandamizwa na Tanzania Bara. Wazanzibari tumechoka na mambo tunayofanyiwa, tunahitaji Katiba ya Jaji Warioba,” alisema.

Naye Mwakilishi wa Asasi za kiraia, Deo Bwire, alitoa wito kwa Rais John Magufuli, kukutana na makundi mbalimbali ikiwamo viongozi wa dini na wa kisiasa kama alivyokuwa akifanya mtangulizi wake Rais Jakaya Kikwete, ili kufufua mchakato wa Katiba Mpya.

Akifunga kongamano hilo, Kaimu Mkurugenzi wa LHRC, Anna Henga, alisema uhitaji wa Katiba Mpya hujitokeza kila mara baada ya chaguzi kufanyika.

Alisema ili kuzuia matukio ya uvunjifu wa amani, ni vema Serikali ikahuisha mchakato wa Katiba Mpya kabla ya kuelekea kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2020.

Why Your Side Chick Looks Hotter Than Your Wife

$
0
0
Dear men, side chicks look hotter than wife because you don't live with them.

You only see them when they’ve perfected their makeup.

Don't leave a wife because of a hot side chick.

Her hotness is a mirage that will disappear once you start living with her.

Don’t let your emotions deceive you that you have fallen in love.

Falling in love is not as deep as standing in love.

A person who falls in love can fall out of love. But when you stand in love, it means you stand up for your partner for better or worse.

Falling in love is emotional.

Standing in love is a choice of commitment.

Uchunguzi wa UN wa mauaji ya Wanajeshi wa Tanzania Congo Umeonesha Kuna Mapungufu Katika Mafunzo ya vikosi vyake

$
0
0
Umoja wa Mataifa umesema uchunguzi wa mashambulizi yaliyowauwa Wanajeshi 15 wa kulinda Amani wa Tanzania waliokuwepo katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, umeonesha mapungufu katika mafunzo yanayotolewa kwa Vikosi vyake.

Shambulio lililosababisha mauaji hayo lilitekelezwa na Waasi katika Kambi iliyopo huko Beni katika eneo la Kivu Kaskazini na lilikuwa shambulio baya zaidi kuwahi kutoka

From the Source:

The United Nations on Friday conceded that an attack that killed 15 peacekeepers in the Democratic Republic of Congo late last year exposed "gaps" in how UN troops are trained.

The December 7 attack in the Beni territory of North Kivu province was one of the worst to target UN peacekeepers in recent history in the country.

Fifteen Tanzanians were killed and 43 other peacekeepers wounded.

It was the bloodiest attack against MONUSCO, the UN force deployed in DR Congo since 1999, and the worst against a UN force since the death of 24 Pakistani peacekeepers in Somalia in June 1993, leading to a special UN investigation.

UN investigators were tasked with evaluating the response of the UN peacekeepers and making recommendations on how to prevent such violence.

"The team found a number of gaps in the training and posture of MONUSCO and its Force Intervention Brigade," the United Nations said in a statement Friday.

"Moreover, the investigation team noted that the mission did not have an actionable contingency plan to reinforce and extract its peacekeepers during the attack. 

"Issues of command-and-control, leadership and lack of essential enablers such as aviation, engineers and intelligence were also major obstacles and need to be addressed urgently," it added.

UN Secretary-General Antonio Guterres had appointed Dmitry Titov, a Russian who has worked in UN peacekeeping, to lead the special investigation.

The United Nations had said the ambush was carried out by suspected ADF rebels, a shadowy group dominated by hardline Ugandan Muslims that is one of several armed groups active in the North Kivu region.

Citing the conclusions of the investigation, the world body said Friday that "all available evidence" pointed to the ADF as the culprits.

A UN report made public last month recommended that UN peacekeeping forces change the way they operate and not shy away from using force to reverse a worrying trend of escalating fatalities.

DR Congo's east has long been wracked by violence, but fighting between government soldiers and militia groups, as well as inter-ethnic clashes, increased in 2017.

Source: New Vision

NEC Yawajibu LHRC Waliodai Wapinzani Walionea Uchaguzi Kinondoni na Siha

$
0
0
NEC Yawajibu LHRC Waliodai Wapinzani Walionea Uchaguzi Kinondoni na Siha
Baada ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kutaja hadharani dosari kumi zilizojitokeza katika uchaguzi mdogo uliofanyika kwenye majimbo ya Kinondoni na Siha, Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Kailima Ramadhani amedai kuwa kituo hicho kimefanya makosa.

Alisema kituo hicho kimetangaza dosari hizo za uchaguzi uliofanyika Februari 17, bila kufuata sheria na kanuni za uchaguzi.

Uchaguzi huo ulifanyika baada ya waliokuwa wabunge wa majimbo hayo, Maulid Mtulia (CUF-Kinondoni) na Dk Godwin Mollel (Chadema-Siha) kujitoa kwenye vyama vyao na kuhamia CCM.

Wabunge hao wawili waliopitishwa tena kwenye uchaguzi huo kupitia CCM walishinda nafasi hizo.

Kutokana na uchaguzi huo, LHRC ilitoa dosari zilizofanana na zile zilizotolewa na vyama vya upinzani hasa Chadema.

Akizungumza wakati wa mahojiano na kituo cha Magic FM, Kailima alisema LHRC imefanya kosa la kisheria na kanuni kwa kutoa taarifa hiyo.

Alisema kifungu namba 4 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi kimeielekeza tume hiyo kutunga kanuni wakati kifungu namba 64(4) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi kinasema Tume itatoa muongozo kwa watazamaji wa uchaguzi.

Alieleza kwamba hata katika uchaguzi wa mwaka 2015, tume hiyo ilitoa muongozo kwa watazamaji wa uchaguzi.

“Kipengele cha 12(d) kinasema mtazamaji hatatakiwa kutoa taarifa kwa umma juu ya mchakato wa uchaguzi hadi taarifa ya awali itakapokuwa imekabidhiwa na tume kukiri kupokewa kwa taarifa hiyo,” alisema Kailima.

Alifafanua kuwa kituo hicho kiliandika barua kwa tume na kuiwasilisha Februari 26 ambayo iliifikia tume Februari 28 jioni wakati ofisini kukiwa hakuna viongozi.

“Kutozingatia sheria ni kama wembe, utakukata tu,” alisema.

Mkurugenzi huyo alisema tume hiyo inatafakari iwapo itawapa kibali kingine cha utazamaji wa uchaguzi.

Kuhusu hoja zilizo kwenye taarifa hiyo ikiwamo ya matumizi ya watoto kwenye kampeni za chama kimojawapo, Kailima alisema wao si Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na Watoto na kwamba hoja hizo ilipaswa zipelekwe huko.

Mgunduzi wa Madini ya Tanzanite Aomba kuonana na Raisi Magufuli

$
0
0
Mgunduzi wa Madini ya Tanzanite Aomba kuonana na Raisi Magufuli
Tanzania imebarikiwa kuwa na madini ya aina mbalimbali ikiwemo Tanzanite ambayo hayapatikani nchi nyingine yoyote duniani.

Hata hivyo, Mgunduzi wa madini hayo ya Tanzanite Mzee Jumanne Ngoma amesema kuwa licha ya kugundua madini hayo miaka 52 iliyopita bado hakuna alichonufaika nacho.

Mzee Ngoma amesema kuwa anatamani kuonana na Rais John Magufuli ili amueleze adha anayokutana nayo kwa sababu anaumia kuona hathaminiwi wala kunufaika na chochote licha ya ugunduzi alioufanya.

“Nina mengi ya kumwambia Rais Magufuli kuhusu madini yaliyopo Tanzania mengine ni siri ya nchi siwezi kuyaweka hadharani,” -Mzee Ngoma

Mwanafunzi aua Wazazi Wake kwa Risasi

$
0
0
Mwanafunzi aua Wazazi Wake kwa Risasi
Polisi nchini Marekani katika Jimbo la Michigan wamemkamata mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Michigan baada ya kuwapiga risasi hadi kufa wazazi wake ambao walikwenda shule anayosoma ili kumchukua kwaajili ya likizo.

Kijana huyo aliyetambulika kwa jina la James Eric Davis Jr anatuhumiwa kuwapiga risasi wazazi wake hao wakiwa katika bweni analoishi, siku moja baada ya kwenda hospitali kutokana na suala linalohusiana na matumizi wa dawa za kulevya.

Wazazi hao ni Diva Davis, 47, na James Erick Davis Sr, 48, ambao inaelezwa kuwa walipigwa risasi na mtoto wao wakiwa ghorofa ya nne ya Ukumbi wa Campbell ulioko ndani ya chuo alichokuwa anasoma ambapo ndipo bweni lake lilikuwepo.

Mwanasheria wa Jimbo la Illinois aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa familia hiyo inaishi eneo la Chicago ambapo baba wa mtoto huyo alikuwa ni Askari Polisi hadi mauti ilipomfika leo.
Viewing all 104702 articles
Browse latest View live




Latest Images