Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live

Kufuru:Bunge Lakodi Vipaza Sauti kwa Sh8.9 Milioni Kila Siku

0
0
Wakati kukiwa na malalamiko kwamba Bunge la Maalumu la Katiba linagharimu fedha nyingi za walipakodi, uongozi wa taasisi hiyo umetumia Sh142.56 milioni kukodi vipaza sauti kutoka Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).

Katibu wa Bunge Maalumu, Yahya Khamis Hamad alithibitisha kukodiwa kwa vipaza sauti hivyo kwa ajili kamati zote 12 na kwamba kila gharama ya chumba kimoja kwa siku ni Dola 450 za Marekani (Dola moja ni wastani wa Sh1,650).

Kwa maana hiyo Bunge, hilo linatumia Dola 5,400 sawa na Sh8.91 milioni kwa siku kugharimia vipaza sauti katika vyumba 12 vinavyotumiwa na kamati hizo na kwa siku 16  ambazo kamati zitakutana, gharama hizo zitafikia Sh142.56.

“Vifaa vya sauti tulivyokuwa navyo vinalalamikiwa, vilikuwa siyo standard (viwango) hasa vya mazungumzo, tumekodi kutoka Ukumbi wa Mikutano wa AICC na tumekuwa nao usiku mzima kuvifunga,” alisema.

Alisema tangu wavifunge, hawajawahi kupata malalamiko tena kutoka katika kamati kuhusu ubora na kwamba gharama za kukodisha vifaa hivyo itatoka katika fungu la dharura la Bunge Maalumu.

“Mara ya kwanza walituambia gharama zao ni Dola 500 kwa siku lakini tukajadiliana nao, hivyo tukafikia kiwango hicho cha Dola 450,” alisema.

Hamad alisema vifaa vya awali ambavyo vililalamikiwa na wajumbe kuwa havitoshi, vinatoa sauti nje ya majengo na kwa jinsi vilivyo, vinalazimika kutembezwa ukumbini, hivyo kusababisha usumbufu.

Malalamiko ya gharama

Suala la gharama limekuwa likiibuka mara kwa mara na wakati mwingine kutajwa kama sababu ya kuahirishwa kwa Bunge hilo kwa kuwa hakuna uhakika wa kupatikana kwa akidi inayotakiwa kufikia uamuzi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), Deus Kibamba alilalamikia kile alichokiita “matumizi ya kufuru” ya Bunge Maalumu wakati hakuna uhakika wa kupatikana kwa Katiba Mpya.

Aunt Ezekiel: Nitahakikisha Nampa Penzi Mume wa Mtu Mpaka Achanganyikiwe

0
0
Stori: Musa Mateja

Makubwa! Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson amefungukia madai ya kutoka na dansa wa Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ aitwaye Moze Iyobo ambaye ni mume wa mtu akisema hakuna ukweli wowote zaidi ya kutaka kuchafuliwa.

Akizungumza na Ijumaa Wikienda wikiendi iliyopita, Aunt ambaye gazeti ndugu la hili, Risasi Mchanganyiko liliripoti tukio la kutaka kufanyiziwa na mke wa dansa huyo aitwaye Mwengi Ally, alisema anamshangaa mwanamke huyo lakini ili kumkomoa atahakikisha anafanya kweli ili kama ni kunuka, kinuke kihalali.
Alisema kwamba yeye ni mke wa mtu asiyeweza kujirahisi kwa kutembea na kijana huyo na kwamba kama ni kujuana ni kwa sababu ya Diamond ambaye ni shemeji yake kwa Wema.

Amenichafulia sana, siwezi kutembea na Moze, najiheshimu. Lakini kwa kuwa ameamua kunipakazia, nitahakikisha namtega mumewe na nikimnasa nampa penzi ili kama ni hizo vurugu azifanye kihalali,” alisema Aunt na kusisitiza:

Siwezi kuwa na uhusiano na Moze, yule mwanamke alikuwa na nia ya kuifanya jamii inifikirie vibaya lakini amenoa.” Hivi karibuni kundi la watu likiongozwa na  Mwengi lilifika nyumbani kwa Wema Sepetu likimsaka Aunt ili kumshikisha adabu kutokana na madai ya kutoka na mume wa mtu huyo.
GPL

Undani Mtangazaji Kibonde Alivyotiwa Ndani Selo Baada ya Kugonga Gari na Kutoa Lugha ya Matusi

0
0
WIKIENDI iliyopita haikuwa njema kwa mtangazaji Ephraim Kibonde baada ya kutupwa nyuma ya nondo katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar kwa msala wa kudaiwa kugonga gari na kutoa lugha ya matusi, Ijumaa Wikienda lina full stori.

Kwa mujibu wa chanzo chetu makini cha habari ambacho kimeshuhudia sakata hilo mwanzo mwisho, ishu nzima ilianzia maeneo ya Makumbusho ambapo gari alilokuwa akilitumia Kibonde, liligonga kwa nyuma gari jingine na kisha kukimbia.

“Baada ya kugonga, Kibonde alirudi nyuma kisha kuanza kukimbia ambapo trafiki alitumia gari lililogongwa na Kibonde kumkimbiza,” kilimwaga data chanzo hicho.Chanzo hicho kilifafanua kuwa baada ya polisi kumkimbiza kwa saa kadhaa, walifanikiwa kumkamata maeneo ya Mwenge ambapo trafiki alipanda kwenye gari la Kibonde na kumuamuru arudi eneo la tukio lakini Kibonde hakuwa tayari kurudi ndipo alipoanza kukimbia tena, huku askari aliyemkamata akiwa ndani ya gari.

“Inaonekana kulitokea kutoelewana kati ya askari na Kibonde ndipo askari huyo alipowasiliana na wenzie kwa njia ya radio call ili wambananishe na alipofika Ubungo kwenye mataa wakamtaiti na kumpeleka kituoni, Oysterbay,” kilihitimisha chanzo chetu.

Baada ya kupata maelezo hayo, kachero wa Ijumaa Wikienda alitia timu katika kituo cha Oysterbay ili kutaka kujua mustakabali mzima wa ishu hiyo ambapo alimshuhudia Kibonde akiwa amesimama nyuma ya nondo huku akiwa anaimba ‘nyimbo’ anazozijua mwenyewe.

Mtangazaji huyo amefunguliwa kesi iliyopewa RB namba OB/RB/13806/20014 KUGONGA NA   LUGHA YA MATUSI.
GPL

Mrema Awatambia UKAWA, Amuonya Mbatia, Asema Atishwi Kabisa na Ukawa

0
0
Moshi. Mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema (TLP) amedai kitendo cha yeye kubaki kwenye Bunge Maalumu la Katiba kumetumiwa vibaya na wahasimu wake wa kisiasa jimboni kwake.

“Ukawa na ubunge wa Vunjo vimegeuka propaganda chafu dhidi yangu. Wamediriki kuwaambia wananchi wangu kuwa nimeahidi kuwaachia jimbo langu,” alisema.

Mrema ambaye pia ni mwenyekiti wa taifa wa TLP, alitoa kauli hiyo jana jimboni kwake katika mkutano na waandishi wa habari aliouitisha kuelezea kwa nini hakuwaunga mkono Ukawa.

Mrema alisema malengo ya Ukawa siyo katiba bali Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na ndiyo maana tangu waliposusia Bunge agenda yao imebadilika na kuwa muungano wa kuelekea uchaguzi 2015.

“Mimi nimeamua kubaki bungeni kwa ajili ya masilahi mapana ya wananchi wa jimbo langu la Vunjo na Watanzania kwa jumla. Sitishwi na Ukawa na nitatetea kiti changu 2015,” alisisitiza.

Mrema alitumia mkutano huo kumshambulia mbunge wa kuteuliwa na Rais, ambaye ni James Mbatia kutokana na uamuzi wake wa kutangaza nia ya kuwania ubunge wa Jimbo hilo mwakani. Kwa mujibu wa Mrema, ndiye Mtanzania pekee mwenye sifa na aliweza kugombea ubunge katika majimbo matatu tofauti na kushinda.

“Mimi ni Mtanzania pekee ambaye nimewahi kuwa mbunge wa majimbo matatu tofauti ya Moshi Vijijini, Temeke na Vunjo. Sifa hizo hazipo kwa wengine,” alisema.

Chanzo: Mwananchi

Simba Wamtimua Kocha Loga Sababu Matokeo Mabovu Pia Demu wa Bongo Movies Ahusishwa

0
0
Simba Imeamua Kumtimua Kocha wake  kutokana na Matokeo Mabaya Toka alivyoanza kuifundisha Simba , Pia stori za chini ya Kapeti zinasema Mmoja wa wasanii wa kike maarufu wa Tasnia filamu ambaye jina lake lina fanana na moja ya sofa maharufu Duniani ametajwa akuwa ni chanzo cha kufukuzwa kwa kocha wa simba Zdravko Logarusic mara baada ya kumfungia mpaka saa saba za usiku mara baada ya kumalizika kwa mechi ya simba day.

Msanii huyo ambaye alishatajwa amara kwa mara katika baadhi ay mitandao ya kijamii kuwa namhusiano na loga na ni mmoja kati ya wasanii wajane ambao wapo katika tasnia ya filamu hapa nchini ameweza kumduwaza kocha huyo kiasi cha kusahau majukumu yake.

Clouds FM ni Noma Imeingia Katika Oradha ya Radio Bora Kumi Barani Afrika

0
0
Kituo cha radio cha Tanzania, Clouds FM kimetajwa kuwa miongoni mwa Radio Bora za Afrika kwa kuingia kwenye orodha ya ‘Top 20 Best Radio Stations In Africa,’ iliyotolewa na mtandao wa Network Africa. 
Clouds FM imeshika nafasi ya saba kwenye orodha hiyo na kuwa radio pekee ya Tanzania iliyoingia. Radio Citizen ya Kenya ndio inayoongoza katika nafasi ya kwanza, huku radio nyingine ya Afrika Mashariki iliyoingia ni Radio Simba ya Uganda iliyokamata nafasi ya nane.

Vijana wa CHADEMA Wadaiwa Kumpiga Mjumbe Bunge la Katiba

0
0
Mjumbe wa bunge maalum la katiba kutoka kundi la 201,Thomas Magnus Mgoli amelazwa katika hospital ya mkoa Dodoma baada ya kupigwa na wanaodaiwa kuwa 'vijana ambao mashabiki wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)'.

Akizungumza na Udaku Specially akiwa kitandani kwake, Mgoli amesema alishambuliwa na vijana hao jana usiku majira ya saa moja eneo la area D anakoishi.

Wivu wa Mapenzi: Binti Muuza Duka Huko Singida Amwagiwa Uji wa Moto na Mke wa Bosi Wake!

0
0

MSICHANA mmoja mkazi wa eneo la Minga katika Manispaa ya Singida (muuza duka), amenusurika kifo baada ya kumwagiwa uji wa moto na mke wa tajiri yake na kumsababishia maumivu makali kutokana na kile kinachosadikiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.

Muuguzi wa zamu katika Hospitali ya mkoa wa Singida, wodi namba mbili ya wanawake, Anna Sprian ameifahamisha Udaku Specially kuwa binti huyo amejeruhiwa sehemu za sikio la upande wa kulia na mgongoni, ambapo amesema hali ya mgonjwa huyo inaendelea vizuri kutokana na matibabu anayoyapata hospitalini hapo.

Akizungumza na Udaku Specially leo Agosti 10, 2014 kwa tabu, binti huyo Jackline Lasway (23), maarufu kwa jina la Pendo, amesema majeraha ya moto katika sehemu ya sikio la upande wa kulia na mgongoni.

Pendo amesema kuwa tukio hilo limetokea jana Jumamosi Agosti 9, 2014 saa nane mchana wakati akiwa dukani kwa bosi wake aliyemtaja kwa jina la, Charles Kamnde.

Amesema akiwa anaendelea na kazi zake za kuuza bidhaa mbalimbali dukani hapo, gafla alitokea mke wa bosi wake akiwa na chupa yenye uji wa moto na kuwa alimmwagia usoni ambapo baada ya kumwagiwa uji huo alitaka kujiokoa ili usimmwagikie usoni na ndipo ulimuunguza kwenye sikio la kulia na mgongoni na kuwa baada ya mke wa bosi wake kumkosa uso alitoa kisu kutaka kumchoma kifuani.

“Mimi sikuwa na ugomvi naye wala sijui chanzo cha yeye kufika dukani na kunifanyia vile jana, maana kama ni kazi mimi ninafanya kulingana na maelekezo kutoka kwa bosi wangu Chale lakini sijui kilichomfanya afikirie kunifanyia huu unyama” alisema.

Aidha, amesema katika purukushani za kujiokoa kuwa asichomwe kisu hicho, alifanikiwa kumkamata mkono mwanamke huyo na kupiga kelele za kuomba msaada ambapo watu walifika na kumwokoa baada ya muda mchache ambapo alichukuliwa na bosi wake hadi Kituo cha Polisi mjini Singida na kupewa PF3 kwa ajili ya matibabu na kupelekwa katika hospitali hiyo ambako amelazwa huku akiwa ma majeraha mwilini.

Kwa upande wake, mmiliki wa duka hilo Chale Kamnde alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa hayuko tayari kulizungumzia kwani maelezo aliyotoa binti huyo yanajitosheleza.

Wakiongea kwa nyakati tofauti na Udaku Specially baadhi ya majirani wa familia hiyo, wameonyesha masikitiko yao juu ya tukio hilo na hatua ya mwananmke huyo kummwagia uji msichana huyo huku wakihusisha tukio hilo na wivu wa kimapenzi baina ya mfanyakazi huyo na mume wa mtuhumiwa.

“Kama aliona kama kuna sehemu kamkosea angemuonya au kama ameshindwa kueleweka basi angemshitaki hata polisi kwani kitu alichokifanya hakiendani na haki za binadamu kwakuwa ni kumdhalilisha huyu msichana ambaye alikuwa akifanya kazi kwa ajili ya kujipatia kipato chake na familia yake.

Kamanda wa Polisi Mkoani hapa, Geofrey Kamwela, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwa wanamshikilia mtuhumiwa kwa mahojiano na mara baada ya upelelezi kukamilika atafikishwa Mahakamani kujibu tuhuma hizo.

Maskini:Mtoto wa Mwaka Mmoja Abakwa Jijini Arusha

0
0
Mtoto wa kike mwenye umri wa mwaka mmoja tunayemtaja kwa jina moja la Devota wa Sokoni One jijini Arusha, amelazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru kufuatia kubakwa na njemba moja iitwayo Rajabu Mkoba (30), mkazi wa eneo hilo.

Tukio hilo lilitokea Jumapili ya Agosti 3, mwaka huu ambapo mtuhumiwa huyo anadaiwa kumbaka mtoto huyo kwa saa 9 na alimrejesha nyumbani kwa mama yake usiku wa manane.

Akizungumza na Udaku Specially , mama wa mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la  Mwitango alisema siku ya tukio, asubuhi alimkabidhi mtoto wake kwa jirani yake aliyemtaja kwa jina la Mustafa Kabananga na yeye kwenda kwenye kikundi cha akina mama.

Usiku saa mbili alikwenda kwa jirani yake huyo kumchukua mtoto wake lakini akaambiwa alichukuliwa na Rajabu.

“Nilikwenda nyumbani kwa mtuhumiwa, yeye anaishi na wazazi wake. Hata hivyo, sikumkuta mwanangu wala mtuhumiwa, nikarejea nyumbani.

“Lakini kabla sijarudi, nilimwambia mama wa mtuhumiwa kuwa mwanaye kaondoka na mtoto wangu akaniambia  nirudi nyumbani nikaendelee kumtafuta nikimkosa niende kwake ili akajue cha kufanya, aliamua kwenda polisi’’ alisema mwanamke huyo.
MWAKA

“Ilikuwa saa 9 usiku nikiwa narejea nyumbani kutoka polisi, nilimkuta mama mzazi wa mtuhumiwa akiwa na mtoto wangu akimrejesha kwangu lakini mtuhumiwa hakuwepo.

“Niliamua kumchunguza vizuri mwanangu ndipo nilipogundua kuwa sehemu zake za siri zimevimba kupita kiasi huku damu zikimtoka.

“Nilikwenda kumweleza mama yake jinsi mwanaye alivyomtenda mtoto wangu na kumwachia mtoto ampeleke hospitali, alinisihi nisitoe taarifa za tukio hilo popote na akaniahidi kunipa shilingi laki moja,” alisema mama huyo.

Imeelezwa kuwa mama wa mtuhumiwa baada ya kukabidhiwa mtoto huyo hakumpeleka hospitali badala yake alikuwa akimtibu kwa kutumia miti shamba.

Baadhi ya majirani walikerwa na kitendo cha mwanamke huyo ambapo walimvamia na kumtolea maneno makali ya kumtaka alifikishe suala hilo kwenye vyombo vya sheria.

Kufuatia kelele za majirani ndipo alipokubali kurudi Kituo cha Polisi cha Unga Ltd ambapo polisi walifika nyumbani kwa mama wa mtuhumiwa na kumchukua mtoto huyo kisha kumwandikia hati ya matibabu (PF3) na kumpeleka mtoto huyo katika Hospitali ya Mount Meru ambako anatibiwa.

Polisi hao walifungua jalada la mashtaka la kubaka na kunajisi lenye namba Ung/RB/2473/2014, bado mtuhumiwa hajakamatwa kwani alikimbia baada ya tukio hilo lakini mama yake ameshikiliwa kwa mahojiano .

Wanawake Kaeni Mbali na Wanaume wa Kikongo Otherwise Utajuta

0
0
Kwa kipindi kirefu sana Mdakuzi Wako nimefanya uchunguzi wa kina juu ya mahusiano ya kimapenzi baina ya Watanzania (wanawake) na Wakongo (wanaume).

Kiufupi hapa Africa hakuna wanaume na waongo zaidi ya wakongo, wakongo ni waongo waongo waongo mpaka kero. Hata wanaume wa kitanzania hawawafiki wakongo.

Tabia kuu ya wakongo ni kuchuna wanawake wa kitanzania na wanawake hao wakifulia wakongo wanawakimbia. Mwanaume wa kikongo hawezi kuwa na mwanamke asiye na pesa kwa hapa Tanzania kwani wengi wao wamejazana kinondoni na hawana shughuli maalumu.

Huwa wanawapumbaza wanawake kwanjia kuu mbili:
1. Kumpatia mwanamke kitu kidogo ili wapate kikubwa. Kwa mfano; Mwanamke ana mtoto anasoma shule na ada ni milioni moja, basi mkongo atalipa hiyo ada ya milioni moja then baada ya wiki mbili tu utasikia anajieleza kwa mwanamke anashida ya milioni tatu na dada zetu huwa wanatoa kama wanayo na kama hawana wataenda kukopa. Mwanamke huwa anasema "ngoja nimpe tu jamani, mtu mwenyewe anaupendo sana kwangu na mwanangu yaani alinilipia na ada ya shule" bila ya kufikiri anachotoa ni kikubwa kuliko alichopewa.

2. Kulia; Wakongo wanapenda sana kuigiza wanalia, na si kidogo. Analia kabisa na machozi yanatoka huku akikwambia "sheriiii usiniache, jua nakupenda sana". Dada zetu hawajawahi kuliliwa na mwanaume basi wanachanganyikiwa wanatoa kila walichonacho.

KUMBUKA: Siku ukifulia Mkongo anakuacha na atakutukana matusi yote unayoyajua na hautaamini kama niyeye aliyekuwa analia.

Kwa Hili Wema Sepetu Unaishusha Hadhi yako ya Kuwa Mke wa Diamond Platnumz

0
0
Mara nyingi Wema amekuwa akimsupport mchumba wake kwa kupanda naye jukwaani na hivyo kusababisha shangwe kubwa.

ushabiki wa Wema kwa Diamond kidogo umepitiliza na hata kama umekuwa ukishangiliwa, tunahisi anajishusha kiaina. 

Kuna ile hadhi ya mke lazima ilindwe hasa kama mke ama mpenzi wako si msanii kama wewe. Wema ni muigizaji si dancer ama mwanamuziki na kwa muigizaji wa filamu mwenye mashabiki wengi, kupanda jukwaani na kukata viuno design kama ni kushusha brand ama nini? Si mbaya kama angekuwa akipanda na kutoa salamu fupi kisha kushuka na kuwa mtazamaji kama watu wengine.

Tupe Mtazamo wako

Hatimaye John Shibuda Ajifukuzisha Chadema Mwenye, Atoa Shutuma Kali Dhidi ya Chadema

0
0
WAKATI Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kikijipanga wakuchukulia hatua wabunge wake waliosaliti msimamo wa Kamati Kuu na kuhudhuria vikao vya Bunge la Katiba, Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda ametangaza kutogombea ubunge tena kupita chama hicho.

Shibuda, Said Arfi (Mpanda Mjini) na Leticia Nyerere (Viti Maalum) wamewasili mjini Dodoma na kujisajili kwa lengo la kushiriki vikao hivyo, licha ya kuzuiliwa na chama chao ambacho kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kimesusia Bunge hilo.

Shibuda alitangaza uamuzi huo kwa nyakati tofauti jana, wakati akizungumza na wazee wa mji wa Maswa na Malampaka wilayani humo, walipotaka kujua hatima yake ya kisiasa ndani ya CHADEMA.

Alidai kauli za vitisho na kejeli dhidi yake zinazofanywa na baadhi ya viongozi wa CHADEMA, ndizo zimemfanya achukue hatua hiyo.

“Mimi niliingia CHADEMA kwa hiari yangu baada ya kuona dhuluma zilizokuwa ndani ya CCM, chama ambacho kimenilea kisiasa, nikaona heri niende CHADEMA ambako nilidhani kuna demokrasia na ukombozi wa kweli.

“Lakini nilichokikuta humo ni tofauti, kwani kila siku wazee wangu mnasikia napata misukosuko isiyo na maana,” alisema.

Bob Junior Azungumzia Tetesi Za Kufanyiwa Fujo Na Mume Wa Msichana Aliyekuwa Akifanya Nae Video

0
0
Siku mbili zilizopita kumekuwa na taarifa mitaani kuwa mwimbaji ambaye pia ni producer wa Sharobaro Records, Bob Junior alifanyiwa fujo na mwanaume mmoja anaedaiwa kuwa mume wa msichana aliyekuwa anafanya naye video.

Taarifa hizo zilieleza kuwa tukio hilo lilifanyika maeneo ya Mlimani City wakati Bob Junior alipokuwa akishuti vipande vya wimbo wake wa ‘Bolingo’ huku msichana huyo akijiachia mbele ya lens. 

Ghafla mumewe akatokea na kuzua tafrani, video ya wimbo ikageuka kuwa ya ndondi na mwisho wa siku mwimbaji huyo alilazimika kukimbia kupisha shari.

Tovuti ya Udaku Specially imeongea na Bob Junior kuhusu tetesi hizo ambapo yeye amekiri kutokea kwa fujo hiyo lakini amekanusha kuhusu suala la kufanya video na msichana huyo ingawa alikuwa na directors wake na vifaa.

“Hapana, naona watu wanakuwa kama wambea. Mimi nilikuwa nimekaa pale Mlimani City tunapiga story niko na mwanamke wangu. Rafiki yangu mwingine alikuwa kaka na mwanamke mwingine, sasa sijui kama ni mke wa mtu au nini, ndio ikatokea vurugu lakini huyo mwanamke aliyefanyiwa vurugu mimi simfahamu.” Ameeleza Bob Junior.

“Tulikuwa tumekaa tu tunaenjoy tunapiga story, tunakula…mimi sijui kama ni mwanamke wake au ni mke wake. Amemfanyia vurugu, amemvuta nywele. Wamezinguana kidogo lakini sifahamu kama ni mke wake au ni mchumba wake ila najua ni mtu ambaye ana uhusiano nae.” Ameongeza.

Akizungumzia kuhusu taarifa kuwa alitoka nduki na kumuacha rafiki yake akifanyiwa fujo, Bob ameeleza kuwa aliondoka kupisha shari na sio kukimbia kama ilivyotafsiriwa.

“Hapana siwezi kukimbia siwezi kukimbia. Tanzania ni nchi yenye amani kwa nini nikimbie kuna vita gani jamani hapo. Mimi nilichukua vitu vyangu na vijana wangu na team Sharobaro wangu, nikaondoka taratibu nikachukua gari langu nikaondoka. Unapoona mtafaruku hupaswi kukaa kuendelea kuangalia jambo. Unapaswa kupisha uliache jambo liendelee.”

Tetesi: Ndoa ya Jay Dee na Gardner Habash Yavunjika

0
0
Ndoa ya mwanuziki Jay dee na mtangazaji mashuhuri wa radio Gardner G. Habash inasemekana imevunjika huku Gardner akihama Kimara alikokua akiishi na mkewe na kuhamia kwa moja wa ndugu zake wa karibu sana.

chanzo cha kuvunjika ndoa hiyo bado hakijajulikana moja moja kwa moja ila wawili hao wamekuwa katika migogoro kwa muda.. na si mara ya kwanza kutengana ila this time hali si shwari. yazidi kusemekana kaka Gardner kazidi michepuko amekua haibi tena anafanya bayana mpaka mwenye mali anajua anavyoibiwa.

kudhihirisha hayo katika ukurasa wake wa IG dada jide ameandika "Walking Away From Troubles" ambapo umbepuzi yakinifu waonesha
mambo si sawa hata kidogo.

Gardner kabla ya kumuoa Jide alikua tayari na mke halali wa ndoa na mtoto mmoja.


Ushahidi Mwingine wa Chris Brown na Rihanna Wapo Karibu Kurudiana Ushahidi Mwingine wa Chris Brown na Rihanna Wapo Karibu Kurudiana

0
0
Baada ya siku moja tu Chris Brown ku-post poster la tour ya Rihanna na Eminem kwenye instagram, Chris Brown ameonekana kuendelea kuongeza ukaribu zaidi na Rihanna.
Japokuwa picha haipo clear sana lakini inaonyesha Chris Brown alivyokwenda back stage ambapo alikuwepo Rihanna kwenye moja ya show za tour hiyo.
Picha haionyeshi vizuri lakini kuna mashahidi wengi wanasema kwamba Chris Brown alikuepo backstage akiwa na Tyga na welienda kwa ajili ya Rihanna.


Lil Wayne Ajitangaza Hadharani Kuwa Yeye ni Mwasiriki wa Virusi vya Ukimwa-Shocking

0
0
Lil Wayne Ataingia katika Orodha Ya Mastaa Wanaoishi na virusi vya Ukimwi Akiwemo Gwiji wa Mpira wa Kikapu Magic Johnson.
Katika Ukurasa Wake wa Tweeter Ameandika Hivi:

"Its Time to tell my Fans aka my family. I tested positive for HIV. But i Wont Let it Get the Best of me#Young"

Akiwa na Maana kuwa Ni muda muafaka sasa wa Kuwaambia mashabiki na familia yangu kuwa Nimepima HIV na Kukutwa ninao. lakini Sinta kubali uchukue Mazuri yangu


Njama za Kuuawa Kwa Dk. Slaa: IGP Adai CHADEMA Wanapiga Siasa

0
0
JESHI la Polisi nchini limesema hakuna mtu yeyote anayehojiwa au kushikiliwa na jeshi hilo akihusishwa na madai ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ya kuwepo kwa njama za kutaka kumuawa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Wilbroad Slaa.

Ijumaa iliyopita, madiwani wawili wa chama hicho kutoka mkoani Shinyanga, waliorejea tena na Chadema baada ya mapema mwaka huu kukihama na kuingia Chama Cha Mapinduzi (CCM), waliibua tuhuma nzito dhidi ya baadhi ya viongozi waandamizi wa CCM kwamba walikuwa na mpango wa kuidungua helikopta aliyokuwa akiitumia Dk. Slaa na viongozi wengine wa juu wa chama hicho. Madiwani hao ni Peter Sebastian ‘Obama’ wa Kata ya Ngokolo na Martine Mfuko wa Kata ya Msekelo, Shinyanga.

Akizungumza jana na Raia Tanzania, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Ernest Mangu, alisema mbali na kuzisikia na kuzisoma tuhuma hizo kwenye vyombo vya habari, jeshi hilo halijapokea taarifa au malalamiko kutoka kwa viongozi wa Chadema Mkoa wa Shinyanga wala Makao Makuu Dar es Salaam kuhusu suala hilo zito.

Alisema kama Jeshi la Polisi lingepata taarifa hizo, ni wazi hatua stahiki zingechukuliwa ikiwa ni pamoja na kufanyika kwa upelelezi dhidi ya yeyote anayehusika au kuhusishwa na suala hilo.
“Hatuwezi kuchukua hatua yoyote kwa sasa kwani viongozi hao (madiwani wa Chadema) hawajatoa taarifa. Inawezekana kuwa hizo ni siasa tu,” alisema Mangu.

“Kazi zetu zinafanyika kwa taratibu zake, na katika hili, hatuna kitu chochote cha kukifanyia kazi kwani hakuna taarifa iliyoripotiwa kwetu. Ingekuwa ni busara kwa viongozi hao kutoa taarifa juu ya njama za kudunguliwa helikopta ya Chadema. Sasa kukaa kwao kimya, jeshi litaanzia wapi uchunguzi?” alisema na kuhoji IGP, huku akisistiza kuwa taarifa hizo ni michezo ya kisiasa tu.

Mcheza Show wa Diamond Ampiga Chini Aunt Ezekiel, Ampigia Magoti Mkewe na Kumuomba Msamaha

0
0
Dancer wa Kundi La wasafi linalotumiwa na Diamond Platnumz ameamua kumwacha Aunty Ezekiel na kurudiana na mpenzi wake waliyezaa nae mtoto mmoja, kwa mujibu wa Baby Mama wa Moze  Iyobo bibie Mwengi amefunguka kuwa ni kweli AUnty Ezekiel alikua anatoka na bwana wake lakini baada ya yeye kushtukia mchongo huo akamuuliza na Moze akakiri kuwahi kuhusiana kimahaba na Star Bongo Movie Aunty, Iyobo Ameomba msamaha na sasa wako Sawa na Mkewe

Epuka Vitu Hivi Unapoamua Kuwa na Mchepuko ambao ni Mume wa Mtu ama Mke wa Mtu

0
0
Ku date mke wa mtu siyo jambo zuri, na ukiweza kuepuka ni vyema ukafanya hivyo. Hivi karibuni rafiki yangu wa karibu amekumbwa na balaa kubwa kutokana na kitendo hiki. Pamoja na kwamba si jambo zuri lakini ukweli ni kwamba kwa sababu tofauti totauti watu wataendelea ku date wake za watu. Offcourse hata wanawake wengine kutokana na sababu mbalimbali kwenye ndoa zao wataendelea kuchepuka. hivyo mada hii inalenga kuwasaidia wote wanaochepuka wake kwa waume wasikumbwe na zahama kama iliyomkumba rafiki yangu. Kwa experience yangu zifuatzo ni rules ambazo wachepukaji wanatakiwa ku zi observe.

1. Jua kuwa mwanamke au mwanamme anayechepuka siyo mwaminifu. Hivyo anaweza kuwa na mchepuko zaidi yako. That is you are not alone. Hivyo always jaribuni kutumia kinga. Hata kama hana mchepuko mwingine possibility ni kubwa kuwa mme au mke wake pia ana mchepuko. So kutumia kinga ni jambo jema.

2. Hata kama mkiamua kuplay bare inabidi mjitahidi kuzuia mimba. Kumpa mimba mke wa mtu ni jambo baya ambalo linaweza kutokea na kuharibu kabisa maisha ya mmoja wenu au wote.

3. Avoid texting. Sms za ma lavi davi ni nzuri katika kuhamasishana na ku furahia pale mnapokuwa mbali. Lakini linapokuja swala la mume au mke wa mtu meseji ni njia mbaya kabisa ya mawasiliano. Usipende kabisa na ikiwezekana acha sms kabisa. Pale inapobidi kuwasiliana tumieni voice. Piga simu. Watu wengi wamekamatwa kwa sababu ya sms.

4. Msiweke utamaduni wa kukutana. Namaanisha msikutane sehemu na siku zinazofanana. E.g kila jumatano au jmosi sehemu A. Msiwe na kawaida. Badilisheni hotel, siku na wakati as many times as possible. Msiwe na kawaida.

5. Tafuta muda wa faragha ambao sio questionable for both of you.

6. Msipende kutumia usafiri mmoja na kukaa sehemu moja. Kutaneni eneo la tukio na kila mmoja aende kivyake. Msipende kukaa pamoja eneo la wazi kama bar. Huwezi kujua mtu aweza kuwaona. Hata kama mnakunywa nyweeni chumbani.

7. Hata kama mnapendana na ku enjoy kiasi gani kamwe msitelekezw wenza wenu au kufanya wenza wenu wahisi kuwa kuna kitu kinaendelea. Kama lara1 anavyosemma ni lazima uonyeshe high degree ya unafiki.

8. Mchepuko ni siri ya watu wawili. Never intoduce or let your best friends, shoga etc know about it. Hata rafiki zako wa karibu vipi hawatakiwi kujua kama una chepuka.

Wengine wataongezea. Wish you safe michepuko

Kibonde wa Clouds FM Aachiwa Kwa Dhamana Oysterbay

0
0
Mwandishi wa habari, Ephraim Kibonde jana aliachiwa kutoka Kituo
 cha Polisi Oysterbay, Dar es Salaam alikokuwa akishikiliwa tangu 
mwishoni mwa wiki kwa tuhuma za kusababisha ajali ya gari na kutoa lugha
 ya matusi kwa askari wa usalama barabarani

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Camillius 
Wambura alithibitisha jana kukamatwa kwa Kibonde na kwamba walikuwa 
wakiendelea kufanya uchunguzi wa tukio hilo.

Hata hivyo taarifa zilizopatikana jana jioni zilidai kuwa Kidonde aliachiwa kwa dhamana wakati uchunguzi ukiendelea.
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live




Latest Images