Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104431 articles
Browse latest View live

Mwanaume Kulala Usingizi Baada ya Tendo ..Wanasayansi Wagundua Sio Hiari yao

0
0
Jambo hili huwaacha wanawake wakiwa wamechanganyikiwa na kujiuliza maswali chungu mzima kama kuna mahali wamekosea au hawajawavutia wapenzi wao, pale wenzi wao wanapogeukia upande wa pili na kushikwa na usingizi punde tu baada ya kumaliza tendo la kujamiiana.

Lakini utafiti uliofanywa hivi na wanasayansi unawapa wanaume ahuweni katika kuepuka lawama hizo, kwamba, kumbe siyo hiyari yao, bali ni maumbile.

Wanasayansi hao wamebaini kwamba, kwa sababu za kimaumbile ubongo wa wanaume unawalazimisha kulala muda mfupi baada ya kushiriki tendo la kujamiiana. Katika utafiti wao wanasayansi hao walibaini kwamba, kwa jinsi ubongo wa mwanaume ulivyotengenezwa, pale wanapomaliza tendo la kujamiiana na kufika kileleni kuna eneo linalozimika na kuwafanya kupata usingizi.

Wakati hilo likitokea kwa wanawake hali ni tofauti, kwani wao hubaki wakikodolea macho dari wakiwa wamechanganyikiwa na kujiuliza maswali lukuki, wakijihisi kutowaridhisha wapenzi wao.

Utafiti huo ulifanyika kwa kuhusisha kipimo cha kumulika, maarufu kama scan, ambapo kilitumika kuwamulika wanaume katika ubongo wao pale wanapofanya tendo la kujamiiana na baada ya kumaliza kujamiiana na kufika kileleni na kubaini kwamba, eneo linalojulikana kama cerebral cortex, eneo linalohusika na ‘fikra’ huzimika baada ya mwanaume kufika kileleni.

"Utafiti huu unatupa matokeo ya kile kinachotokea ndani ya ubongo pale mwanaume anapofika kileleni.” Gazeti la Mirror lilimnukuu mwanasayansi mmoja wa serikali ya Ufaransa aitwae Serge Stoleru.

“Lakini kwa wanawake inaonekana ni tofauti kabisa……” Aliongeza kusema mwanasayansi huyo.

Mwanasayansi huyo aliendelea kusema kwamba, wanawake hushangazwa sana na jambo hilo na ndio sababu hubaki wakiwashangaa wapenzi wao wanapolala baada ya kumaliza tendo il hali wao wakitaka zaidi….

Kwa hiyo hakuna sababu ya wanawake kuwalaumu tena wanaume baada ya kumaliza tendo na kulala kwa sababu hivi sasa wameshajua sababu, watuwache tupumuwe……

Source: Jamii Forums

Kwa Wema Woote Niliomfanyia Huyu House Girl, Hii Ndio Shukrani yake Aliyonipa

0
0

Ilikuwa miaka kadhaa iliyopita nilipoletewa msichana wa kazi maarufu kama house girl..ukimuangalia kwa sura alionekana mpole na mnyenyekevu.umri wake haukua mdog sana kwani alikuwa na miaka km 20 ivi wkt huo alipofika...alipokuja alionekana wazi kuwa ametoka kwenye familia duni sana kwani hata nguo aliyoivaa ilikuwa imechoka sana..

Nilimpokea vizuri nikamfundisha kazi za nyumbani, na kumuelekeza matumizi ya vitu mbali mbali vya nyumbani kwani hakujua hata jiko la gas linawashwa vipi..Nilimfundisha mapishi mbali mbali ambayo alikuwa hajui kupika..

Alikuja akiwa na begi dogo la marlboro lililokuwa na nguo chache za kuvaa, nilimpa nguo zangu nyingi ambazo zilinibana kwani baada ya mimi kujifungua mwili wangu uliongezeka mara dufu...nikamfundisha usafi wa kuoga asubuhi na jioni ili awe smart na aweze kukaa na watoto akiwa msafi...

alikuwa msikivu na hakuwa mjeuri, niliishi naye kama ndugu yangu na hakika ungenikuta nae tunavyopiga stori usingedhani km ni house girl...kuna watu walijua yule ni ndugu yang kwa jinsi tulivyokuwa tunapatana....nikiwaambia ni house girl hawaamini..

Tuliishi kwa vizuri na hatukuwahi kugombana hata siku moja kwani kwa kiasi kikubwa alitimiza majukumu yake niliyompangia...

Baada ya muda nikaona nimsaidie zaidi kwani pamoja na kuwa ni house girl wang lkn pia alikuwa yatima kwani wazazi wake wote walishafariki dunia..Na pia mtt wangu wa mwisho kwa wakati huo alianza shule kwa hivyo angepata fursa ya kujiendeleza kwani hakukuwa na mtt mdogo aliyebaki nyumbani..

Nikamtafutia shule ya QT ili asome masomo ya sekondari ambayo nilimgharamikia kila kitu..akaanza kusoma hiyo shule kwa makubaliano kwamba atafanya kazi zake zote asubuhi na mchana aende shule..

Nilipokuwa nasafiri na watoto wakati wa likizo au kwenda mapumziko mikoa mbali mbali au nje ya nchi naye pia nilimchukua tukawa pamoja naye..(kumbuka kuwa hapo nyumbani kwangu nilikuwa naishi na watu wengine ambao ni ndugu zangu lkn niliwaacha wao nikawa namchukua yy)

Kila nilipokuwa nasafiri kikazi nilikuwa nawaletea watoto wangu zawadi na yeye pia namletea..

Wakati wa sikukuu nilikuwa nawanunulia watoto wangu nguo mpya na yeye pia namnunulia..na ili kumfanya ainjoi sikukuu yake zaidi nilikuwa nampa pesa ambayo simkati kwenye mshahara wake..

Kila j2 alikuwa free kuanzia saa 4 asb hadi saa 12 jioni, nilimruhusu aende popote lkn ikifika saa 12 awe kesharudi..

Kila mwisho wa mwaka nilimpatia nauli na zawadi za kuwapelekea ndugu zake na wadogo zake na alienda likizo

Nilimkatia bima ya afya na yeye akawa anatibiwa aga khan hospital kama watoto wangu

Nilimnunulia simu ya mkononi na kila simu yake ilipoharibika nilimnunulia nyingine

Kabla sijanunua machine ya kufulia aliniambia yeye hawezi kufua nguo na mikono kwani mikono yake inaharibika na kupata fangas nikamtafuta mtu wa kufua nguo ambaye nilikuwa namlipa..

Kila alipofanya kazi ya ziada kwa mfano kuhudumia wageni au siku za sikukuu ambapo kazi ni nyingi nilikuwa namlipa pesa muda huo huo baada ya kumaliza hizo kazi, na mshahara wake mwisho wa mwezi uko pale pale..

Siku moja moja za wk end nilikuwa namsuka kwani kwa bahati nzuri mie najua kusuka mitindo mingi tu...

Siku kama sijamsuka basi nampa hela ya saluni/msusi

Siku nikienda naye sokoni/supermaket basi hanunui chochote kwa pesa yake, akitaka kitu namnunulia

Kila mwaka unapoisha na mwaka mpya kuingia nilikuwa namuongeza mshahara ili naye ajisikie mwenye thamani.

Kwa muda niliokaa naye aliweza kusave na kununua plot baada ya mimi kumshawishi afanye hivyo ili iweze kumsaidia baadae, japo mimi nilimuongezea pesa kdg iliyopelea.

Nilimuahidi kumsomesha hadi chuo kama yeye angependa na kujitahidi katika masomo ili naye awe na maisha yake baadae..
kichwani mwangu nilipanga kumfundisha gari kwani nilishamchukulia km ndugu yangu...hili nilikuwa sijamwambia, nilitaka amalize kwanza elimu ya sekondari.

NOTE
kwa nature ya kazi yangu huwa nasafiri mara kwa mara lkn nikiwa nyumbani Lakini huwa sina tabia ya kujibweteka na kumuachia house girl afanye kila kitu...
Kila siku jioni napika chakula cha usiku baada ya kurudi kazini, nikichelewa namwambia apike cha watt na watu wengine, changu na cha baba napika mwenyewe nikifika...mara nyingi mimi na mr tunakula ugali wao wanapenda wali, n.k

Nafanya usafi wa chumba changu choote hadi washroom mara 3 au 4 kwa wiki

nafua nguo zangu na za mume wng zote siku ya jumamosi.

siku ya jumamosi na jumapili naingia jikoni kuanzia asb hadi jioni, except kama nimeenda kazn au nimepata dharura..siku za wk end asb huwa natengeneza mchemsho kwa ajili ya familia....na pia napika mwenyewe chakula cha mchana na usiku..(binafsi huwa sipendi kupikiwa hasa nikiwa nyumbani kwani nahisi km chakula kina kasoro nyingi km atapika m2 mwingine,) kwa ivo huwa naingia jikoni mwenyewe.


ALICHONIFANYIA SASA
Baada ya miaka kadhaa nikahisi kama anabdilika na kuwa jeuri lakini sikujali saana, nilijua tu labda yuko days hivi ambayo wkt mwingine yanasababisha mood kuchange..

Nilikuwa na mpaka leo huwa simruhusu house girl kuingia chumbani kwang kwani usafi na kila kitu huwa nafanya mwenyewe hata kama nina mimba ya kujifungua leo..
Sasa kuna kipindi niliposafiri nilikuta kitanda changu kimetandikwa vizuri mpk nikawa na was was, sbb mume wangu huwa hatandiki wala habadilishi shuka mpaka nirudi safari...Siku moja nilimuuliza mume wng nani kamtandikia kitanda? kwani najua kbs hata km ni yeye katandika hawezi kunyoosha shuka vizuri, mara nyingi mume wng yupo rafu, akaniambia amemuomba house girl amsaidie kutandika, nikamuuliza tangu lini house girl anaingia chumbani kwng? akasema samahani mke wng sitarudia tena...nikanyamaza moyoni nikaanza kuwa na shaka lkn sikufatilia saana... huyo house girl siku zooooote hakuwahi kuingia chumbani na mimi sijawahi mruhusu, iweje kipindi hicho tena nikiwa nimesafiri aingie? hapo alikuwa kashakaa muda wa kutosha na keshakuwa mzoefu ila sio chumbani kwang...ila nikapotezea kwani baada ya hapo ikawa hata nikisafiri nakuta vile vile chumba kipo rafu rafu, hakujatandikwa kama zamani, nikajua ni kweli ilikuwa msaada tu kwa mr na nikafutilia mbali was was wng...

Miezi miwili baadae huyo house girl akaniaga gafla akisema bibi yake ni mgonjwa anaumwa, kwa sbb nilikuwa na namba za simu za ndugu zake nikawauliza wakasema kweli bibi yake anaumwa, nikamruhusu aende kumsalimia..akaondoka, lkn kilichonishangaza ni pale alipokusanya mabegi ya nguo zake zote, viatu vyake vyote n.k nikamuuliza mbona umekusanya kila kitu hutegemei kurudi? akasema anaenda kuwagawia ndugu zake yeye ataanza upya akirudi..na vile alikuwa bado anasoma sikumtilia shaka nikajua atarudi tu...

alipofika kwao tu akanitumia ujumbe mfupi wa simu akisema yeye hatarudi tena na ameamua kusomea huko huko kwao.....aaaaaaaaaahhhhhhhhhhh nilikuwa so much dissapointed sababu wakati huo mi nilikuwa mjamzito tena nakaribia kujifungua...kuna ndugu yng alinionea huruma akaniletea msichana wake anisaidie...

Baada ya muda nikasikia yule house girl wangu aliyeondoka ni mjamzito, sikufatilia ila nikajua ndio sababu iliyomfanya aondoke nyumbani kwangu..

Baadae akajifungua nikaambiwa, nami nikampigia simu kumpongeza, na pia nikamnunulia zawadi za mtt nikampa mtu ampelekee...lkn pia mara kwa mara nilikuwa nampigia cm na kumsalimia yy na mwanae..

MIAKA KADHAA BAADAE ndio nikaja kujua kuwa huyo mtoto wa house girl wangu ni wa mume wangu...
Nilipomuuliza mume wng alikubali na kuniomba msamaha saaaana, akasema huyo house girl kila nilipokuwa nasafiri alikuwa akivaa kanga moja na kujilengesha sana mpk akaingia kwny mtego.

SIWEZI SEMA, MAUMIVU niliyopata hayaelezeki.....
NI MIAKA KADHAA imepita toka tukio hili kutokea, lkn mpaka sasa bado nasikia maumivu yake moyoni....in fact ht jana uck nilikosa usingizi baada ya kukumbuka tukio hili, nikajikuta machozi yananitoka bila kuyazuia...

Kwa wema wooooote niliomfanyia huyu house girl kweli hii ndio shukurani yake?,yaaani sina hamu..na mpk leo hii sina hamu...nilibaki nimeshikwa na butwaa..
japo hiyo haijanifanya niwachukie mahouse girl wengine lkn sina hamu nao kabisa hawa watu...

By Sam

Askofu Kakobe Afunguka Tena..Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya March 5

0
0


Askofu Kakobe Afunguka Tena..Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya March 5

Kauli ya Serikali Kuhusu Gazeti la Tanzanite Lililomwandika Mange Kimambi

0
0
Serikali kupitia kwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) ambaye pia ni Msemaji wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas imesema  imewaita wahusika wa gazeti la Tanzanite ambalo limesambaa mitandaoni likiwa limebeba katika ukurasa wa mbele habari inayomhusu Mange Kimambi.

Katika taarifa aliyoitoa kupitia ukurasa wake wa Twitter, Dkt Abbas amesema kuwa, amelazimika kuwaita wahusika hao ambao atakutana nao leo ili aweze kusikiliza upande wao baada ya kupokea malalamiko mengi kuhusu maadili ya kitaaluma ya gazeti hilo.

Ufafanuzi kutoka Ikulu kuhusu Rais kutengua uteuzi wa Waziri Dr. Kigwangalla

0
0
Mkurugenzi wa Mawasilano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa amekanusha taarifa nayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ikieleza kuwa Rais Dkt Magufuli ametengua uteuzi wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dr. Hamis Kigwangalla

Msigwa amewataka wananchi kuipuuza taarifa hiyo kwani ni uzushi.

Picha iliyomsumbua Nape Nnauye muda Mrefu

0
0
Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye amefunguka na kusema kuwa picha za darasa ambalo zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii zilikuwa zikimsumbua kiasi cha kuamua kuchukua jukumu la kufanya mabadiliko katika darasa hilo mpaka sasa kuwa shule.

Nape Nnauye amesema kuwa baada ya yeye kuwa mbunge mwezi mmoja au miwili baadae zilianza kusambazwa picha za wanafunzi wakiwa wanasoma chini ya darasa hilo ambalo hali yake ilikuwa mbaya kwani lilikuwa ni darasa la miti tu huku wanafunzi wakikaa kwenye miti pia.

"Nikiri kwamba msukumo wa ile picha kwenye mtandao wa jamii ulikuwa na mguso wa pekee yake kuliko ningesimuliwa kawaida, baada ya kuona ile picha imesambaa na anayesemwa ni mimi nikaaamua kufunga safari nikaja nikasema jamanii hii ni aibu kwetu tumesemwa kwamba vijana wetu wanasoma kwenye darasa bovu kwa hiyo nikaamua na kukaa pamoja na wenzangu tukaweka mkakati.

"Nikaleta mifuko ya cement na kuanza kazi ya kufyatua tofali tukaanza na madarasa machache hivyo tulipigana kutoka kwenye hili darasa kwenda kwenye hayo madarasa mengine ambayo sasa yamefika manne na tunaendelea kwani tunataka iwe shule yenye madarasa ya kutosha na ikiwezekana na nyumba za walimu" alisema Nape Nnauye

Bunge lazungumzia afya ya Spika Ndugai

0
0
 Spika wa Bunge, Job Ndugai anaendelea na matibabu nje ya nchi ikielezwa hali yake kuendelea vizuri.

Ndugai yupo kwenye matibabu nje ya nchi kwa muda sasa. Katika mkutano wa 11 wa Bunge, hakuonekana na ilielezwa kuwa yupo nje ya nchi kwa uchunguzi wa afya yake.

Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai amesema hali ya spika inaendelea vizuri na kwamba, anatarajia kurejea nchini wakati wowote.

"Ni kweli bado yuko nje ya nchi, lakini ifahamike kuwa afya yake inaendelea vizuri na wakati wowote atarejea nchini kuendelea na majukumu yake wala hakuna hofu kwa jambo hilo," amesema Kagaigai.

Hata hivyo, Kagaigai hakubainisha ni lini hasa kiongozi huyo atarejea na hakuzungumzia ugonjwa unaomsumbua wala nchi anayotibiwa, ingawa mara nyingi amekuwa akitibiwa nchini India.

Hii ni mara ya tatu kwa Ndugai kwenda nje kwa matibabu tangu aliposhika wadhifa wa Spika.

Mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2016 ikiwa ni muda mfupi baada ya kuzinduliwa Bunge la 11.

Mara ya pili alikwenda mapema mwaka jana, lakini kipindi hicho hakukaa muda mrefu.

Afya ya Ndugai imekuwa ikiimarika na hata kuweza kukaa muda mrefu zaidi kwenye vikao anapokuwa Dodoma.

Maboresho Katika Application ya Udaku Special, Fanya Ku Update Ama Download Hapa Kwenye Simu yako

0
0
Maboresho Katika Application ya Udaku Special, Fanya Ku Update Ama Ku Download HAPA Kwenye Simu yako, Tumebadili Logo pamoja na Kuifanya App iwe nyepesi zaidi bila kuchukua nafasi kubwa katika Simu yako

UPDATE HAPA

DOWNLOAD HAPA





Asanteni



Kimenuka..Julius Mtatiro Avuliwa Uanachama CUF Baada ya Kushindwa Kujibu Tuhuma

0
0
KADA wa Chama cha Wananchi (CUF) ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya uongozi ya chama hicho, Julius Mtatiro, amevuliwa uanachama wa chama hicho na Uongozi wa CUF Wilaya ya Ubungo mkoani Dar es Salaam.

Akitangaza uamuzi huo mapema siku ya Jumapili, Machi 4, 2018, mwenyekiti wa CUF wilaya ya Ubungo, ndugu Bashir Ally Muya, amesema kuwa wamefikia uamuzi huo kutokana na Mtatiro kukaidi agizo la chama hicho lililomtaka kujibu tuhuma mbalimbali zinazomkabili, mbele ya Baraza la Utendaji la Wilaya ya Ubungo.

Muya amedai kuwa, mnamo tarehe 20 Desemba 2017, kamati ya utendaji ya chama hicho iliketi ambapo ilimtaka ndugu Mtatiro, na wenzake sita kuja mbele ya kamati hiyo kujibu tuhuma mbalimbali zinazowakabili, agizo ambalo Mtatiro na wenzake walikaidi.

Ametaja makosa mawili makuu yaliyomfukuzisha uanachama Mtatiro kuwa ni: kutolipia kadi yake ya uanachama kwa muda wa miaka mitatu sasa, kitendo ambacho ni kinyume na katiba ya cha hicho, ambapo inasema endapo mwanachama hatalipia kadi yake ya uanachama kwa muda wa mwaka mmoja pekee, basi mwanachama huyo uanachama wake utasitishwa mara moja.

Ametaja kosa la pili kuwa ni kukihujumu (kukisaliti) chama kwa kushirikiana na Chadema katika chaguzi za marudio zilizofanyika ndani ya wilaya ya Ubungo, ambapo amesema licha ya chama hicho kusimamisha wagombea, Mtatiro na wenzake hawakuwaunga mkono, huku wakitumia muda wao mwingi kuzungumzia masuala ya Chadema.

Aidha, Muya amesema kuwa kwakuwa Mtatiro ni mjumbe wa mkutano mkuu wa taifa,  uongozi wa wilaya utamwandikia barua katibu mkuu wa CUF kumtaarifu juu ya uamuzi huo, ili baadaye aandikiwe barua kutaarifiwa juu ya kufutwa kwake uanachama.

Wengine waliofutwa uanachama ni: Twaha Rashidi, Mwinyi Hamis, Khalid Singano, Jumanne Athuman, Kassim Hamis, na Yusuf Lema.

Miongoni mwa sababu zilizotajwa kuwafuta uanachama ni pamoja na; kuwa na kadi za chama cha Chadema, kumnadi mgombea wa udiwani Kata ya Saranga kwa tiketi ya Chadema kwenye uchaguzi mdogo uliopita ilihali chama hicho kilikuwa na mgombea, pamoja na kumkashifu mwenyekiti wa CUF taifa kwenye mitandao ya kijamii.

Soma Nafasi za Kazi zilizotangazwa Siku ya Leo Jumatatu

0
0

Lulu Diva adaiwa kumtelekeza mtoto wake Kijijini

0
0

SIKU zote raha ya ubuyu hauchagui umri wa kuumun’gunya, shida yake usijisahau tu ukameza na mbegu zake! Ubuyu uliotua mezani ni wa msanii anayechipukia na mwigizaji wa Bongo Movies, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ wa kudaiwa kumtelekeza mtoto wake wa kumzaa kijijini kwao huko Handeni jijini Tanga.

MTOA TAARIFA AWEKA WAZI KILA KITU
Msambaza Ubuyu ambaye ni jirani wa msanii huyo alitiririka kuwa, Lulu alimzaamtoto huyo wa kike miaka sita iliyopita huko Handeni, lakini watu wengi hawajui kama ana mtoto mkubwa hivyo.

Ilidaiwa kuwa, hata mchumba wake wa sasa hajui kuhusu hilo na wala hapendi kabisa kuongelea kuhusu mtoto huyo.

“Ninavyokuambia, huyo Lulu alipozaa mtoto huyo alimwacha kwa mama yake muda mrefu sana yeye akaja Dar, lakini kamwe huwezi kumsikia akizungumzia mtoto wake huyo kwa mtu yeyote wala kusema kuwa alishawahi kuzaa,” alidai mtoa ubuyu huyo.

MTOTO ANAMUITA DADA
Mpashaji huyo aliweka wazi kuwa,kutokana na kulelewa na bibi yake kwa muda mrefu, kwa sasa mtoto huyo anamwita Lulu Diva dada nahuwa anamuona mara mojamoja hivyo hata akienda kijijini kwao hajui kama ni mama yake, jambo ambalo Lulu anapenda liwe hivyo.

“Huwezi kuamini, mtoto ameshasahau kabisa kama Lulu Diva ni mama yake badala yake anamuita dada na mtoto wake huyo ameshazoea kumuita hivyo na wala hajali lolote,” kiliendelea kudai chanzo hicho.

MSIKIE LULU MWENYEWE
Baada ya kuunyaka ubuyu huo wa motomoto, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Lulu Diva ambapo alipoulizwa kuhusu hilo la kuzaa na kumuacha mtoto kijijini kwako alifunguka kama ifuatavyo;

Ijumaa Wikienda: Mambo vipi Lulu? Hivi mtoto wako anaitwa nani?

Lulu: Mtoto wangu anaitwa nani? Yupi huyo?

Ijumaa Wikienda: Si yule ambaye umeamuacha kijijini?

Lulu: Hiyo kali jamani… alafu kwa nini nizae nimuache kijijini?

Ijumaa Wikienda: Unaogopa kuonekana mzee?

Lulu: Hakuna kitu kama hicho labda wanamfananisha mdogo wangu kuwa ndiye

mwanangu.

Ijumaa Wikienda:

Watu wanasema ni kweli anakuita dada kwa sababu ulimwacha muda mrefu.

Lulu: Si kweli jamani huyo ni mdogo wangu…

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete atoa mifuko 300 ya sementi Ujenzi wa Zahanati

0
0

Rais Mstaafu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye pia mbunge wa zamani wa Jimbo la Chalinze na Mkewe Mama Salma Kikwete wametoa mchango wa mifuko 300 ya sementi itakayofanikisha ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha Kwakonje na nyumba ya walimu.



Nape Nnauye Alaani Mfumo wa Baadhi ya Viongozi wa Afrika Wanaobadili Mifumo ya Ukomo wa Utawala

0
0
Mbunge wa jimbo la Mtama kupitia tiketi ya CCM, Mhe. Nape Nnauye amelaani mfumo wa baadhi ya viongozi wanaobadili mfumo wa ukomo wao wa utawala na kujiongezea miaka au mihula ya kutawala.

Nape amefananisha kitendo hicho sawa na ushetani na kuwataka vijana wa Kiafrika kupambana  kupinga mfumo huo ambao unakandamiza demokrasia.

“Huu ulevi wa baadhi ya viongozi wa Afrika kutamani na kubadili ukomo wa wao kuwa madarakani ni ushetani na lazima upingwe kwa nguvu zote hasa na vijana kabla utaratibu huu haujaota mizizi na kusambaa! Hii ni zaidi ya kansa“amenena Mhe. Nape Nauye kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Baadhi ya nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Uganda na Rwanda tayari nchi hizo zimebadili mfumo wa ukomo wa urais madarakani ambapo Rais atahudumu kwa miaka 7 na Uganda wamefuta kabisa hadi ukomo wa umri wa Rais kustaafu.

Watu tisa wakamatwa na Jeshi la Polisi Mwanza

0
0

Watu tisa wanaodhaniwa kuwa ni wahamiaji haramu wamekamatwa na Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza kwa tuhuma za kuingia nchini Kinyume cha sheria.

Watuhumiwa hao wamekamatwa katika eneo na Nyashishi Wilayani Msingwi Mkoani humo wakiwa wamejificha katika vichaka kwa ajili ya kwenda kuchukuliwa kwa ajili ya kuendelea na safari yao.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema kuwa kukamatwa kwa raia hao kunafuatia taarifa za raia mwema aliewatilia shaka na kisha kutoa taarifa kwa jeshi la polisi juu ya watu hao waliojificha katika kichaka hicho.

Katika hatua nyingine Kamanda Ahmed Msangi amewataka wananchi kutanguliza uzalendo kwa kuwafichua watu wanaoshi nchini bila ya kuwa na vibali maalumu na kinyume cha sheria.

Mashehe 5 Waliotoweka Zanzibar, Wasimulia Hali Ilivyokuwa Baada ya Kuachiwa Huru Usiku na Wasiojulikana

0
0
Mashehe watano waliotoweka katika mazingira ya kutatanisha kuanzia Febuari 9 mwaka huu huko Zanzibar wameachiwa na kurejea katika familia zao usiku wa kuamkia Machi 4, 2018.

Mashehe hao walitoweka ikiwa hakuna aliyekuwa akifahamu walipokwenda, huku wana familia wakiitaka serikali kufanya uchunguzi ili kuweza kubaini walipo ndugu zao.

Mmoja wa Mashehe hao, Amir Khamis akifanya mahojiano na Azam Tv alisema kuwa hajui eneo walilopelekwa, lakini waliohojiwa na baada ya kuonekana hawana hatia waliachiwa bila kudhuriwa.

“Mimi na wenzangu wanne tulipelekwa kusikojulikana na baada ya kuhojiwa wametuachia tukiwa salama. Wale waliotukamata hawakuwa na nia mbaya…walikuwa wakitekeleza kazi yao ya usalama…na ndio maana baada tu ya kugundua kwamba sihusiki na y ale waliyokuwa wakinihoji waliniachia huru na nimerudi nyumbani…niko na familia yangu,” alisema Khamis.

Mmoja wa wanafamilia wa Shehe Khamis alisema kuwa alikuwa na hofu kwamba huenda ndugu yao hayupo hai, hivyo wamefurahi na kufarijika sana kumuona tena.

“Tulikuwa na hofu kwamba yawezekana ametupwa baharini au vinginevyo, lakini tunamshukuru sana Mungu kwa kumrejesha akiwa salama,” alisema Mke wa Shehe Khamis, Mwanaunguja Hadhar baada ya mumewe kurejea nyumbani.

Ushauri Kwa Wasichana Wenye Wapenzi ama Waume Wafupi

0
0
Ushauri Kwa Wasichana Wenye Wapenzi ama Waume Wafupi

Wasichana waliowengi husema kuwa hawapendi kuwa kwenye uhusiano wa kimpenzi na wanaume wafupi kwa kile wanachosema kuwa hawajisikii amani wanapotembea nao barabarani.

Msichana mmoja kupitia mtandao wa kijamii aliuliza swali akieleza masikitiko yake kuhusu mpenzi wake kuwa mfupi. Katika swali hilo ambalo alikuwa akiomba ushauri kwa watu mbalimbali alisema, amekuwa kwenye uhusiano na mpenzi wake huyo kwa muda wa miezi sita sasa. Mpenzi wake huyo anampenda na wanaishi kwa amani, lakini tatizo ni kwamba ni mfupi.

Msichana huyo alisema mambo mengine yapo sawa, lakini huwa hana amani anapokuwa naye nje kwa sababu watu humuangalia sana, na wakati mwingine huchekwa na wapita njia. Alisema kuwa anavutiwa na mwanaume huyo, lakini ufupi ni tatizo linalomnyima amani kila saa akimfikiria.

Alikuwa akiomba ushauri ni namna gani ataweza kufanya ili ampende mwanaume huyo jinsi alivyo na ajisikie amani anapotembea barabarani.

Watu wengi walitoa maoni yao mengi yakiwa yakumsaidia msichana huyo, lakini pia kuna jambo moja muhimu sana ambalo wengi wa watoa ushauri hawakulizungumzia.

Japokuwa tunatakiwa kuvutiwa na namna mtu anavyoonekana na namna anavyotujali katika mambo mbalimbali, lakini wakati mwingine huwa tunafanya kosa kubwa la kumhukumu mtu kutokana na anavyoonekana.

Lakini pia, mhusika katika uhusiano ndiye anapaswa kufikiria nini chenye manufaa kwake bila ya kujali watu wa nje wanasema au watawaonaje. Huwezi kujilazimisha kumpenda mtu hasa kama huyo ambaye tayari nafsi yako inatilia mashaka kimo cha umbo lake.

Kama unahusiano na mwanamke au mwanaume ambaye kimo chake kinakufanya usiwe na amani hata kutembea nae, ni vyema ukawa mkweli kwa nafsi yako na ukaepusha kupotezeana muda. Kama utandelea na uhusiano huo huku ukiwa na hofu kuhusu watu watasemaje, utakuwa unauweka uhusiano wenu katika hatari ya kutokukua vizuri, na mwisho mwenza wako atajua namna unavyomchukulia kutokana na umbo lake, na hakika jambo hilo litakuwa maumivu kwake.

Kama unaweza kuachana na kuangalia kimo chake, na kuangali namna mnavyoishi, namna anavyokujali na kuhakikishia kuwa unakuwa na furaha wakati wote, basi una nafasi ya kuwa na uhusiano wenye afya. Lakini, kama utaona maoni ya jamii yana uzito zaidi kuhusu uhusiano wenu, basi achana na uhusiano huo kwani hautakuwa na tija.

Sababu zipi Hasa zinazopelekea Kufanya Mapenzi Kwenye Gari?

0
0
Nimepatwa na mshtuko baada ya kusimama barabarani mbele ya gari moja, Mshtuko umekuja baada ya kushangaa hili gari linaunguruma wakati ndani hakuna mtu na kama linatikisika kwa mbali. Ndo kukodoa macho kupitia kioo cha mbele nashangaa kuona jamaa yuko busy anapanda juu na kushuka chini. Mhh nimeshtuka sana aisee maana ni mchana muda wa saa tisa gari limepakiwa tuu chini ya mti.

Nikajiuliza why this? Je wamekosa guest?
Nikapata jibu kuwa wanaofanya huu uchafu ndani ya gari mara nyingi ni wake za watu
Watoto wadogo wa shule Au jinsia moja

Kwa nini nasema hivi kwa sababu haiingii akilini mchana wote huu watu wawe wamejibana kwenye gari wanachoogopa ni nini??? Wamekosa gust bubu hata??

Nyie baadhi ya wanaume wenye mtindo huu muache hayo magari mnapanda na familia zenu, mnaenda nayo makanisani n.k mnayafanya najisi kwa kufanya ngono humo. Ni bora basi mkafanya na wake zenu kwa bahati mbaya.

Kwa upande wangu sijafurahishwa jamani kila mtu ana maono yake au mitizamo yake. Nilichowaza anaweza akawa hata ni mtoto wa jirani yangu au ndugu yangu labda hata anageuzwa humo na libaradhuli aka fataki

By Cajojo/JF

Breaking News: Mbowe Augua Ghafla Akimbizwa KCMC

0
0
Breaking News: Mbowe Augua Ghafla Akimbizwa KCMC
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Elikaeli Mbowe amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC, Moshi kwa kuugua ghafla usiku wa kuamkia leo na kuwekewa mashine ya kumsaidia kupumua.



Katibu wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema amesema, “Ni kweli jana aliugua ghafla na kupelekwa KCMC, madaktari walilazimika kumwekea mashine ya Oksijeni ili kuweka sawa afya yake lakini baadaye waliondoa hiyo Oksijeni baada ya afya yake kuimarika.”

Kutana na Mtabibu Mongwa Mganga wa Waganga Sasa Anapatikana Mikoa Yote

0
0

KUTANA NA MTABIBU MONGWA MGANGA WA WAGANGA SASA WAKO MIKOANI KARIBU YOTE NCHINI...
.
HIVYO WATATOA TIBA MAENEO YOTE YA MBEYA ,DODOMA, IRINGA , MOROGORO, MWANZA,ZANZIBAR

==>KWA WALE WENYE KUHITAJI TIBA

Husafisha nyota na kutoa Pete za bahati na kwawale walio sumbuka kwaajili ya matibabu na hawakufanikiwa chochote sasa njoo ujionee miujiza hapo kwahapo bila malipo yoyote malipo baada yakazi napia humpa mtu jini la mali kwayule anaye taka kumiliki bila mashariti yoyote
Tunatibu magonjwa mbalimbali yaliyo shindikana mpenzi aliye kukimbia nakumrudisha kwa masaa 24 tu napia natoa dawa za nguvu za kiume kuurefusha uume paka pale unapotaka .
Natoa dawa za biashara na mvuto ==tunatoa dawa zauzazi kwa wale kina mama wenye matatizoya uzazi walio angaika kwa muda mrefu bila kupata mafanikio yoyote njoo umalize tatizo lako sasa
Natoa mazindiko yanyumba na mwili biashara na mvuto kazini
Kupandisha nyota ili kungaa kupandishwa cheo kazini kurudisha mali zilizo pote zilizo ibiwa kuzulumiwa
Kesi zilizo shindikana uzimaliza mara moja namengine mengi ya siri piga simu

+255 764291657
+255 764291657
+255 764291657

CHADEMA yazipelekea Barua Balozi za Marekani na Ujerumani Kuhusu Tuhuma za Musiba Kwamba zinaihujumu Tanzania

0
0

CHADEMA wazipeleka Video CD za Musiba Marekani na Ujerumani.

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimekwenda balozi za Marekani na Ujerumani kupeleka video zinazomuonyesha Cyprian Musiba akizituhumu nchi hizo kupanga mikakati ya kuhatarisha Usalama wa Taifa la Tanzania.

Akizungumza na JUPITA, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa chama hicho, Tumaini Makene amekiri chama chake kuandika barua yenye Kumbukumbu Nambari C/HQ/ADM/KS/24/02 iliyofika Ubalozi wa Marekani na yenye Kumbukumbu Nambari C/HQ/ADM/KS/24/01 iliyofikia Ubalozi wa Ujerumani,

Makene alisema barua ya Ujerumani ilielekezwa kwa Mkuu wa Kitengo cha Siasa na Uchumi, John Espinos huku ile ya Marekani ikielekezwa kwa Mkuu wa Kitengo cha Siasa na Uchumi wa nchi hiyo, Joerg Hererra.

“Tumeandika barua hizi tukizitaka nchi hizo zijibu tuhuma zilizoelekezwa kwao na Cyprian Musiba ambaye alisema Marekani kupitia FBI inaendesha mikakati ya kuhatarisha Usalama wa Tanzania.

“Lakini pia, Musiba alikihusisha chama tawala cha Ujerumani CDU kuwa kinashirikiana na Watanzania kula njama za kuhatarisha Usalama wa Taifa,” alisema Makene.

CHADEMA kupitia kwa Makene kimesema kiliguswa sana na tuhuma hizo na kikaona sio za kuzipuuza kwani ni tuhuma nzito na zisipofanyiwa kazi na kuachwa basi mipango hiyo inaweza kuliingiza taifa kwenye hatari kubwa huko mbeleni.

Makene anasema sambamba na barua hizo, pia chama chake kimeambatanisha CD za video zinazomuonyesha Musiba akiongea maneno hayo mbele ya vyombo vya habari Februari 25, 2018.

Chanzo: Media zote.
Viewing all 104431 articles
Browse latest View live




Latest Images