Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live

Hata Nisipoji-Edit Bado Nina Wowowo la Hatari– Chemical

$
0
0

Msanii Chemical amefunguka kuhusu picha yake iliyosambaa mtandaoni ikimuonyesha mwenye umbo kubwa tofauti na muonekano wake wa kawaida.

Chemical ambaye anatamba na ngoma ‘Asali’ ameiambia Bongo Dot Home ya Times Fm kuwa umbo lake siku zote lipo hivyo.

“Hata nisipoji-edit mimi bado nina wowowo kabisa, mimi mtoto wa Kihaya, fresh,” amesema.

Katika hatua nyingine Chemical amezungumzia filamu yake na Wema Sepetu na kueleza anatarajia kuitoa hivi karibuni na itakuwa kazi ya mwisho ndani ya menejimenti ya Kazi Kwanza.

CAF Kuchunguzwa Watanzania kwa Kashfa ya Rushwa

$
0
0
CAF Kuchunguzwa  Watanzania kwa Kashfa ya RushwaShirikisho la soka Barani Afrika CAF linaendelea na uchunguzi juu ya tuhuma za kupanga matokeo (Match fixing) zinazowakabili waamuzi wa Tanzania kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.


Taarifa ya TFF iliyotolewa leo na Kaimu katibu mkuu Kidao Wilfred imeeleza kuwa CAF imewajulisha TFF juu ya tuhuma hizo, zinazowahusu waamuzi wa mchezo wa Ligi ya mabingwa kati ya Rayon Sports ya Rwanda dhidi ya Lydia Ludic Burundi Académic FC ya Burundi.

Waamuzi wa Tanzania waliochezesha mchezo huo uliomalizika kwa Rayon kushinda 1-0  huko Burundi Februari 21, ni Mfalme Ally Nassoro, Frank John Komba, Sudi Idd na Israel Mkongo Mjuni ambaye alikuwa mwamuzi wa akiba.

CAF imeieleza TFF kuwa siku koja kabla ya mchezo viongozi wa timu ya Rayon wanadaiwa kufika hotelini walipokuwa waamuzi na kuingia kwenye vyumba vyao hivyo CAF inahitaji maelezo ya waamuzi kabla ya Machi 6.

Hata hivyo TFF imeweka wazi kuwa haina nia ya kumuonea mtu bali haki itatendeka na kama watabainika kuhusika wachukuliwa hatua kali. Rayon Sports ilisonga mbele baada ya kuwa imetoka sare nyumbani ya 1-1 hivyo kuwa na ushindi wa mabao 2-1.

RC Tanga Ataka Uchunguzi Ufanyike wa Chanzo cha MotoBweni la Wanafunzi

$
0
0
RC Tanga Ataka Uchunguzi Ufanyike wa Chanzo cha MotoBweni la Wanafunzi
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela ametoa siku 14 kwa vyombo vya ulinzi na usalama Wilaya ya Korogwe mkoani humo kufanya uchunguzi na kutoa ripoti ya chanzo cha kuteketea kwa moto  bweni moja la shule ya wasichana Korogwe usiku wa Machi 4, 2018.

Akizungumza mara baada ya kutembelea shule hiyo leo Machi 5, 2018 Shigela amesema ni mapema kuzungumzia chanzo cha moto huo huku akivitaka vyombo hivyo kuanza uchunguzi ili kubaini chanzo pamoja na madhara yaliyojitokeza.

“Kulitokea tatizo la umeme kuwaka na kuzima ambalo hata mkoani lilikuwepo ila hatuna uhakika, hivyo naagiza vyombo vya ulinzi na usalama kwa siku 14 kuchunguza chanzo cha tatizo na athari zake kwa wanafunzi na mali zao ili tujue,” amesema Shigella

Pia, Shigela ameagiza wadau wa elimu kuona umuhimu wa kuchangia shule hiyo kwa maelezo kuwa yanahitajika magodoro na vifaa vingine muhimu shuleni hapo ili wanafunzi waweze kuendelea na masomo yao.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Annisia Mauka amesema hakuna madhara kwa mwanafunzi yeyote kwani wakati moto unatokea wote walikuwa wanajisomea darasani.

Amesema mpaka sasa kuna bajeti ya Sh1.3bilioni kwa ajili ya ukarabati wa shule hiyo yakiwemo mabweni ila hakuna bajeti ya bati kwa ajili ya ujenzi.

Daktari wa Hospitali ya Wilaya ya Korogwe, Frank James amesema walipokea wanafunzi 43 walioonekana wazi kuathiriwa na moshi wakati bweni hilo likiwaka moto lakini walipatiwa matibabu na kuruhusiwa kurudi shuleni.

Mtatiro Afunguka Kuhusu Kuvuliwa Uanachama wa CUF

$
0
0
Mtatiro Afunguka Kuhusu Kuvuliwa Uanachama wa CUF
Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Wananchi CUF, Julius Mtatiro amekanusha habari zinazoenea kwamba amevuliwa uanachama wa chama hicho ambapo kwa upande wake amedai hilo ni tangazo la wahuni na wala haviwezi kumtingisha yeye.


Mtatiro amekanusha taarifa hiyo na kuifafanua kupitia mtandao wake maalum wa kijamii na kusema kuwa anaamini kuwa wanaosambaza taarifa hizo ni vijana wanaotumika ambao yeye kawaita 'wahuni'.

"Ndugu zangu, Nimeona taarifa kwenye mitandao kuwa kuna watu wanajiita viongozi wa CUF wilaya ya Ubungo na kwamba ati wamenivua uanachama wa CUF. Bila shaka hawa ni vijana wa Bwana yule na wanatumika kututoa kwenye ajenda kubwa za kitaifa," Mtatiro.

Aidha Mtatiro amefafanua kwamba taarifa za yeye kuvuliwa uongozi sizo za kwanza  hivyo haziwezi kumshughulisha, "Mwezi Disemba mwaka jana pia wahuni hao walitangaza ati wamenivua uanachama, tangazo lao la jana si jipya! Mimi naendelea na majukumu yangu kama kiongozi wa juu wa chama anayetambuliwa na chama na vikao vya chama, na vitangazo hivyo vya wahuni haviwezi kunishughulisha wala kuwashughulisha wenzangu".

Ameongeza "Nasubiri tangazo lingine la wahuni hao, la kunifukuza uanachama mara ya 3, ya 4, ya 5 na ya 6. Hawatushughulishi kabisa maana dawa ya mgonjwa ni kumpa dawa tu" Mtatiro.

Jana Jumapili Machi 4, 2018, Mwenyekiti wa CUF wilaya ya Ubungo, ndg.  Bashir Ally Muya, alitoa taarifa ya kumvua uanachama , Ndg Mtatiro ambapo alidai kwamba wamefikia uamuzi huo kutokana na Kiongozi huyo kukaidi agizo la chama hicho lililomtaka kujibu tuhuma mbalimbali zinazomkabili, mbele ya baraza la utendaji la wilaya ya Ubungo.

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un Akutana na Ujumbe Kutoka Korea Kusini

$
0
0
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un Akutana na Ujumbe Kutoka Korea Kusini

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un anaandaa mkutano wa chakula cha jioni na wajumbe wawili kutoka Korea Kusini, ikiwa ndiyo mara ya kwanza kiongozi huyo anakutana na ujumbe kutoka Kusini tangu aingie madarakani mwaka 2011.



Shirika la habari la Korea Kusini la Yonhap, liliripoti kuhusu mkutano huo likimnukuu msemaji wa rais nchini Korea Kusini.

Ujumbe huo uko nchini Korea Kaskazini kwa mazungumzo yasiyo ya kawaida yenye lenngo la kuanzisha mchakato kati ya Korea Kaskazini na Marekani.

Uhusiano kati ya nchi hizo mbili umeboreka kufuata mashindano ya olimpiki ya msimu wa baridi.

Ujumbe huo unawajumuisha maafisa wenye vyeo vya mawaziri - mkuu wa ujasusi Suh Hoon na mshauri wa usalama wa taifa Chung Eui-yong.

Awali Bw Chung aliwaambia waandishi wa habari kuwa atawasilisha azimio la Rais Moon Jae-in la kudumisha mazungumzo na kuboresha uhusiano kati ya Korea Kaskazini na Kusini na kuondoa silaha za nyuklia kutoka Rasi wa Korea.

Rais wa Marekani Donald Trump alisema Jumapili kuwa Marekani itakuwa tayari kukutana na Korea Kaskazini lakini akasisitiza kuwa Korea ni lazima iondoe zana zake za nyuklia.

Hata hivyo Korea Kaskazini ambayo imesema inataka kufanya mazungumzo na Marekani, imesema kuwa ni hatua ya "kishenzi" kuwa Marekani inataka kuwepo masharti.

Korea Kaskazini wanataka kufanya mazungumzo na Marekani
Tanzania yajitenga na meli 'zinazoisaidia' Korea Kaskazini
Haijulikani ni nani atawakilisha Marekani ikiwa mkutano kama huo utafanyika.

Mjumbe mkuu wa Marekani kuhusu Korea Kaskazini Joseph Yun alitangaza uamuzi wake wa kustaafu mapema wiki iliyopita.

Wadadisi wanaamini kuwa Bw Yun alikuwa akipendelea sana suluhu ya kidiplomasia na Korea Kaskazini.

Msajili Akataa Maelezo ya Chadema Atoa Siku Tano Kujieleza Tena

$
0
0

Msajili Akataa Maelezo ya Chadema Atoa Siku Tano Kujieleza Tena
Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi ameeleza kutoridhishwa na maelezo yaliyowasilishwa na Chadema kuhusu tuhuma zinazowakabili za kukiuka sheria ya vyama vya siasa na kanuni za maadili ya vyama hivyo.

Mbali na kueleza hayo, msajili ametoa siku tano nyingine kwa Chadema kujieleza kwa nini chama hicho kisichukuliwe hatua kwa kukiuka sheria na kanuni hizo.

Barua ya Jaji Mutungi ya Machi Mosi kwenda kwa katibu mkuu wa Chadema ambayo Mwananchi imeiona imetoa siku tano kuanzia Machi 2 hadi 6, chama hicho kiwe kimewasilisha maelezo mengine.

Jaji Mutungi ameandika barua hiyo baada ya kutoridhishwa na maelezo yaliyowasilishwa na Chadema aliyoiandikia barua ya awali akiipa siku tano kuanzia Februari 21 hadi Februari 25.

Msingi wa barua za Jaji Mutungi unatokana na tuhuma kwa Chadema kufanya maandamano Februari 16 kutoka Mwananyamala kwenda ofisi ya msimamizi wa uchaguzi wa ubunge Jimbo la Kinondoni kudai viapo vya mawakala wa uchaguzi mdogo uliofanyika Februari 17.

Katika maandamano hayo kuliibuka vurugu kati ya polisi na waandamanaji katika eneo la Kinondoni Mkwajuni.

Wakati wa vurugu hizo, mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini (22) aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa ndani ya daladala polisi walipokuwa wakiwatawanya waandamanaji.

Chadema katika majibu ya barua ya awali ya Jaji Mutungi ambayo amesema hajaridhishwa nayo ilitoa hoja kadhaa huku ikihoji hatua alizochukua mpaka sasa kufuatia mfululizo wa matukio ya mauaji ya viongozi wake.

Kaimu katibu mkuu wa Chadema, John Mnyika akizungumza na waandishi wa habari Februari 23 kabla ya kupeleka majibu ofisi ya msajili alisema Jaji Mutungi hakuwaeleza mlalamikaji wa tuhuma zinazowakabili.

“Tunaelewa kwamba msajili anasukumwa na Serikali. Dhamira yao ni kuifuta Chadema. Nawaambia jambo hilo hawaliwezi,” alisema Mnyika ambaye pia ni mbunge wa Kibamba.

Jaji Mutungi katika barua ya Machi Mosi ambayo pia Mwananchi imeiona anasema, “nimesoma vyema barua yako, ila nasikitika kwamba barua yako haikujielekeza kujibu hoja ya msingi ambayo ilihitaji chama chako kitoe maelezo kuhusu uvunjifu wa kanuni za maadili ya vyama vya siasa na sheria ya vyama vya siasa namba 5 ya mwaka 1992, hususan kauli ya mwenyekiti wa chama chenu, Freeman Mbowe ambaye katika mkutano wa kufunga kampeni za chama chenu uliofanyika Mwananyamala kwa Kopa, Februari 16 alisikika akiongea maneno ya uchochezi.”

Ananukuu kauli ya Mbowe akisema, “Nitaongoza mapambano nchi hii, nitaongoza mapambano nchi hii, lazima tukubali kubeba majeneza lazima tukubali kubeba nini? Matokeo ya Watanzania 100 watakaokufa wataleta haki katika nchi hii.”

Jaji Mutungi anasema katika barua hiyo, “Hivyo, narudia wito wangu kukitaka chama chako kuwasilisha maelezo ndani ya siku tano kwa nini kisichukuliwe hatua za kisheria kwa kukiuka sheria ya vyama vya siasa na kanuni za maadili ya vyama vya siasa.”

Alipotafutwa Jaji Mutungi jana kuelezea barua ya majibu ya Chadema na uamuzi wa kuwaandikia barua nyingine hakupatikana, huku msajili msaidizi, Sisty Nyahoza akieleza yupo shule akiendelea na mitihani hivyo asingeweza kulizungumzia suala hilo.

Akizungumzia barua hiyo, mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema alisema, “tutamjibu kesho (leo) Jumatatu. Ila tunamshangaa msajili anajipa mamlaka ya kuwa mdhibiti kinyume kabisa cha sheria ya vyama vya siasa. Huyu ni jaji tulitarajia awe na weledi wa kuitafsiri sheria ambayo anaisimamia na si kama anavyofanya sasa nje ya sheria.”

Ahmed Albaity Awasili Beijing- China Kwenye Matibabu Aliyofadhiliwa na Paul Makonda

$
0
0
Hatimaye yule mtanzania aliyesaidiwa kupata ufadhili wa matibabu na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Mhe Paul Makonda amewasili leo hii majira ya saa 9:20 alasiri katika Uwanja wa kimataifa wa Beijing Capital. Mtanzania huyo aitwaye Ahmed Albaity alipokekewa na Maafisa waandamizi wa ubalozi pamoja na watanzania waishio hapa jijini Beijing na kusindikizwa kwenye hospitali ya kimataifa ya Puhua.

Ndugu Ahmed Albaity  ambaye amekuwa akisumbuliwa na tatizo la uti wa mgongo ambalo limedumu kwa takribani miaka kumi na moja akiwa kitandani,tayari ameanza kupatiwa  Matibabu  katika hatua za  awali  mara tu baada ya kuwasili hospitalini hapo.

Mapema akizungumza kwa niaba ya Wanafunzi wakitanzania Wanaosoma na kuishi nchini humo Bw. Remidius Emmanuel ambaye pia ni Katibu Mkuu Shirikisho hilo amesema wao kama watanzania wanaosoma na kuishi katika Taifa la China  wameshiriki kumpokea Mtanzania mwenzao (Ndugu. Ahmed Albaity )  na kwamba  kwa kipindi chote ambacho atakuwepo hapa Beijing China wataendelea kutoa Ushirikiano na kumjulia hali wakati wote.

 "Tunamshukuru Mwenyezi MUNGU amemuongoza Bw.Ahmed kufika salama hapa Beijing, Tumeshuhudia watanzania wakimsindikiza   uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam na  kuongozwa na  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Paul Makonda, huu ni upendo wa kipekee, na sisi tumeguswa na kuwiwa kumpokea tukiongozwa na Maafisa waandamizi wa Ubalozi wetu hapa China" Alisema Bw. Remidius.

Kwa upande wake ndugu Ahmed Albaity ameushukuru Ubalozi wa Tanzania nchini China pamoja na uwakilishi wa Watanzania wanaosoma na kuishi nchini humo kwa moyo wao wa upendo na namna walivyoweza kumpokea yeye na ujumbe alioambatana nao.

Bw.Michael Semindu moja kati watanzania wanaosoma nchini humo aliyeshiriki mapokezi hayo  alimhakikishia Ndugu Ahmed Ushirikiano kwa kipindi chote atakachokuwa kwenye matibabu jijini Beijing "Nimefurahi kuungana na Maafisa wa Ubalozi pamoja na watanzania wenzangu kumpokea mwenzetu, tunamuahidi ushirikiano kwa kipindi chote atakachoendelea kupata matibabu  nchini China"  Alisema Bw. Michael

Halima Mdee Achukizwa na Kitendo cha Polisi Kuwaita Polisi na Kuwakalisha Muda Mrefu Bila cha Maana

$
0
0
Mbunge wa Kawe, Halima Mdee amesema kitendo cha viongozi kuitwa kituo cha polisi na kukalishwa muda mrefu pasipo kuambiwa vitu vya kueleweka  ni wazi jeshi hilo halijajipanga na endapo wakiendelea na mchezo huo siku zijazo watashindwa kuitikia wito.

Akizungumza baada ya kutoka mahakamani, Mdee amesema kwamba kitendo cha kukalishwa zaidi ya masaa saba kituo cha polisi siyo jambo la kufurahisha hata kidogo huku ikizingatiwa kwamba wao ni viongozi wa wananchi hivyo ni kama usumbufu kwao kuitwa na kukalishwa.

"Tangu asubuhi tumekalishwa tu, aliyechukuliwa maelezo ni Katibu Mkuu peke yake wengine tumekaa tuu pale kwenye korido. Kutuita na kuendelea kusubiri maagizo kutoka juu ina maana hamjajipanga na huu ni usumbufu wetu," Mdee.
Ameongeza "Wametuambia turudi tena Jumanne na ni matumaini yetu siku hiyo watakuwa wamejipanga  na kama itakuwa mambo ni kama haya tena itafika mahali tutachoka na hatutakuja,".

Kwa upande wa Mbunge wa Tarime Mjini Esther Bulaya amesema kitendo cha viongozi wenye kutumikia wananchi kuitwa polisi kisha kupotezewa muda wa nusu siku kitendo hicho kwake anakitafsiri kama dharau.

Freeman Mbowe Aruhusiwa Kutoka Hospital Baada ya Kulazwa

$
0
0
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Rufaa KCMC akisumbuliwa na maumivu makali ya kichwa, ameruhusiwa.

Ofisa Habari wa KCMC, Gabriel Chisseo amesema leo Jumatatu Februari 5, 2018 kuwa Mbowe ameruhusiwa baada ya madaktari kuridhishwa na afya yake iliyorejea katika hali ya kawaida.

Maboresho Katika Application ya Udaku Special, Fanya Ku Update Ama Download Hapa Kwenye Simu yako

$
0
0
Maboresho Katika Application ya Udaku Special, Fanya Ku Update Ama Ku Download HAPA Kwenye Simu yako, Tumebadili Logo pamoja na Kuifanya App iwe nyepesi zaidi bila kuchukua nafasi kubwa katika Simu yako

UPDATE HAPA

DOWNLOAD HAPA

Vitu Kumi Msichana Anavyoangalia Kwa Mvulana Siku ya Kwanza Mnapokutana

$
0
0

Ngoja nikwambie wasichana hukufikiriaje wakikuona siku ya kwanza.

1.Kwanza hutazama tembea yako, kisela au kiheshima ili wajue kama una kazi au la.

2.Kama nguo zako zimefubaa unatembea juani, kama hazijanyooshwa basi hata pasi kwako huna.

3.Kama viatu vina vumbi moja kwa moja gari huna.

4.Kama pesa hutoi kwenye waleti hujazoea kuwa na pesa tena yawezekana hata laki hujawahi kushika.

5.Kama hunukii vizuri basi wanawake huwajui vizuri, na hujui romance, hata hug hujawahi kupewa.

6.Kama hutunzi nywele zako hata zake hutazigharamia.

7.Ukiongea nae muda mrefu na maswali mengi, hata kama hujamtongoza, anajua umempenda.

8. Ukimshika au kumgusa popote kwenye maongezi basi unamtaka kimwili.

9.Kama mkanda wa suruali na viatu havimachi rangi, hujawa na mwanamke kwa muda mrefu.

10. Usipomtazama machoni, yawezekana muongo au hujiamini na unamuogopa.

Shangazi Yangu Ananisaga Kila Mara, Nifanyeje??

$
0
0
Mimi naitwa NASRA na nina mika 24, hilo nalileta kwenu jambo lango wana-Udakuz naomba mnisaidie ushauri ili niwe kutatua tazizo hili linalonikabili hapa chini:

Baada ya mama yangu kufariki 2001 kuna shangazi yangu (ambaye ni mke wa mjomba wangu) alinichukua kwa minajil ya kunilea na kunisomesha ila amekuwa AKINISAGA tokea niko mdogo mpaka sasa! ambapo nikiwa mdogo wakati nimelala nilikuwa nashtuka yupo juu yangu na mimi nipo UCHI huku ananinyonya MATITI na sehemu nyingine za mwili na baadae alikuwa anapanda juu yangu na kunilalia huku akifanya vitu fulani mpaka ananimwagia vitu fulani katika sehemu zangu za siri na kuniambia ninyamaze nisimwambie mjomba "eti atanipa pesa ya kutumia shule na kunipeleka na gari, alipokuwa akimaliza baadae alikuwa akiniogesha na kuninunulia vitu VITAMUTAMU. Nilinyamaza maana sikujua jambo lile ila aliendelea kila mara mchezo wake huo.

Mpaka sasa Nimekuwa Lakini anaendelea mchezo huo na mimi nimeshajua na sometimes nasikia raha ila roho yangu haitaki kabisa mchezo huo , huwa naumia sana ...nataka niwe msichana wa kawaida ni date na wavulana na nisikie raha napokuwa na mvulana.....naombeni ushauri...

Nina Mika 20 Sijawahi Fanya Mapenzi ila Nahisi Bikira yangu Haipo Je ni Kawaida?

$
0
0
Naitwa Nancy Naishi Kijitonyama , mimi ni Msichana na Miaka 20 nimekuwa nikijitunza kwa muda mrefu ili kutunza Bikira yangu kwa mwanaume atakaye nioa mungu akijalia ...so sijawahi fanya mapenzi na mtu yoyote japo napata vishawishi vingi....Saa zingine nikisikia hamu huwa najisugua kwa vidole sehemu zangu ili kutoa hamu....

Sasa hivi karibuni nimehisi huku chini hapako tight kama zamani hata nikiingiza kidole kinaingia bila shida sasa naogopa je Bikira yangu imeshatoka au ni kawaida? na je kujishika kwa vidole sehemu hizo kunaondoa bikira?

Please naomba ushauri.

Amenisomesha, Kaninunulia Gari Lakini Sina Mapenzi Naye! Nifanyeje?

$
0
0
Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 28 Naishi Tabata jijini Dar nimejitokeza kwenu kuomba ushauri, Mimi na mpenzi wangu ambae amenisomesha toka form one hadi sasa nipo chuo kwani wazazi wangu walifariki wakati mimi nikiwa mtoto mdogo sana.

Sasa huyu mpenzi wangu amenigharamia sana yani kuanzia nguo zote hadi chakula nacho kula vyote ni msaada wake yeye na amejitolea kuninunulia gari la kutembelea na kanambia nitafute kiwanja ili tujenge nyumba ya kupangisha.

Ila mimi kwa sasa naona kama huyu mwanaume hatuendani kwani yeye hana elimu ila anafanya kazi kutumia akili ya kuzaliwa, Jamani mimi nataka kuishi na msomi mwenzangu ila huyu kaka mimi naona kama freemasson kwani kanisaidia sana asije akanitoa kafala, Mimi kwa sasa nimepata mpenzi mpya ambae anaelimu ya chuo pia ni sharo sio mshamba kama huyu wa zamani.

Sasa please naombeni ushauri wenu jamani nimwambiaje kama sipo tayari kuishi na yeye huyu mpenzi wa zamani bila kuumiza moyo wake...?

PICHA: Moto Ulivyoteketeza Bweni Korogwe Girls

$
0
0

Moto umeteketeza bweni katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe iliyoko mkoani Tanga na kuwaacha wanafunzi hao katika hali mbaya kufuatia mshtuko wa kupoteza vifaa vyao vyote.

Moto huo ulitokea majira ya saa tatu usiku wa kuamkia leo wakati wanafunzi takribani 40 wanaoishi katika bweni hilo wakiwa darasani wakijisomea.

Hata hivyo licha ya moto huo kutekeza bweni, hakuna madhara ya kimwili kwa upande wa wanafunzi hao isipokuwa kwa wale waliopata mshituko na kuzimia ambao wamelazwa katika Hospitali ya Magunga na Majengo wilayani humo.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, chanzo cha moto kinadaiwa kuwa ni hitilafu ya umeme.




Serikali ya Ufaransa yaipongeza Tanzania kwa kupambana na Rushwa

$
0
0
SERIKALI ya Ufaransa imeipongeza Serikali ya Tanzania kwa mapambano dhidi ya rushwa na inaamini fedha zinazotolewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali zitatumika kama ilivyokusudiwa.

Kauli hiyo imetolewa leo (Jumatatu, Machi 05, 2018) na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Bw. Frederic Clavier alipomtembelea Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye makazi yake Oysterbay jijini Dar es Salaam.alozi Clavier amesema Ufaransa imeridhishwa na mapambano ya rushwa yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli wataendelea kushirikiana nayo katika uboreshaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Pia Balozi huyo amesema Septemba mwaka huu wanatarajia kufungua ofisi ya Shirika la Kimataifa la Misada ya Maendeleo la Ufaransa (AFD) jijini Dar es Salaam ili kurahisisha utoaji wa huduma. Kwa sasa ofisi za AFD zipo Nairobi nchini Kenya.Shirika hilo limekuwa likishirikiana na Serikali, katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo na ya maji safi na maji taka kwenye mikoa ya Simiyu, Mwanza, Musoma na Morogoro.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imeweka kipaumbele katika uwajibikaji na kupambana na rushwa ili kuhakikisha fedha zinazotolewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi zinatumika vizuri pamoja na wananchi kupata haki.

Amesema mapambano dhidi ya rushwa yataiwezesha Serikali kufikia malengo yake ya kukuza uchumi kupitia sekta ya viwanda, uwekezaji, kilimo na utalii, hivyo ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji kutoka nchini Ufaransa ili waje kuwekeza kwenye ujenzi wa viwanda, kilimo, madini na miundombinu mbalimbali.

Pia Waziri Mkuu amesema Serikali itashirikiana na Ufaransa katika kuandaa mikutano mbalimbali itakayowakutanisha wadau wa sekta binafsi kutoka nchi zote mbili ili kuwapa mbinu za namna ya kukuza uchumi.

Mbunge wa CCM Akabidhi Hoja Binafsi ya Kuchunguza Matukio Yanayotishia Usalama

$
0
0

Mbunge wa CCM Akabidhi Hoja Binafsi ya Kuchunguza Matukio Yanayotishia Usalama

Shilingi Trilioni 1 Zatengwa Kulipa Madeni Mbalimbali Mwaka wa Fedha 2017/2018

$
0
0
Na: Lilian Lundo – MAELEZO, Dodoma.
Serikali imetenga jumla ya shilingi Trilioni 1 mwaka wa fedha 2017/2018 kwa ajili ya kulipa madeni mbalimbali ya watoa huduma, wazabuni na watumishi wa Umma.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Dkt. Hassan Abbasi ameeleza hayo leo Mjini Dodoma alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya utekelezaji wa miradi na ahadi mbalimbali za Serikali.

“Kati ya shilingi Trilioni 1 zilizotengwa kulipia madeni kwa mwaka huu wa fedha, shilingi Bilioni 896.3 zimeshalipwa kwa watoa huduma, wazabuni na watumishi wa Serikali,” alisema Dkt. Abbasi.

Amesema hesabu hiyo inajumuisha shilingi Bilioni 43 ambazo zimelipwa Februari, 2018 ikiwa ni malimbikizo ya wafanyakazi  wa sekta ya Umma.

“Madeni mengine uhakiki unaendelea na yataendelea kulipwa siku zijazo na tutawajulisha,” alifafanua Dkt. Abbasi.

Vile vile amesema, Serikali katika kuwaondolea adha ya usafiri kwa wananchi wa maziwa makuu likiwemo Ziwa Nyasa, Tanganyika na Victoria.

Kwa upande wa Ziwa Victoria,  mkandarasi amepatikana na majadiliano ya mwisho na kusaini mkataba na kampuni ya STX ya Jamhuri ya Korea vitafanyika mwezi huu kwa ajili utengenezaji wa meli mpya itakayokuwa na uwezo wa kubeba abiria 1,200 na mizigo tani 400.

Kwa upande wa Ziwa Tanganyika zabuni kwa ajili ya utengenezaji wa meli mpya ya abiria na mizigo itatangazwa mwezi huu. Meli hiyo mpya itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 600 na tani 400 za mizigo na italeta mapinduzi makubwa katika usafiri ziwani hilo.

Aidha Dkt. Abbasi amesema Julai mwaka huu nchi itapokea ndege kadhaa mpya ikiwemo Boeing Dreamliner na ukarabati wa viwanja vya ndege vya Kitaifa, Kimataifa na Kimkoa unaendelea kwa kasi kote nchini.

Rais Magufuli Aagiza Kuendelezwa Kwa Ujenzi wa Msikiti Uliowekewa Pingamizi

$
0
0

Rais John Magufuli ameagiza kuendelea kwa ujenzi wa msikiti wa ISTIQAAMA COMMUNITY katika Manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa uliokuwa umewekewa pingamizi la kujengwa kutokana na kukiukwa taratibu za ujenzi.

Akisoma agizo hilo la Rais Magufuli mbele ya viongozi wa Baraza la Waislamu Tanzania -BAKWATA, waumini na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Jochiam Wangabo amesema uamuzi huo umezingatia kujenga amani na utulivu katika jamii.

Comments

Abiria Adaiwa Kumnyonga Kondakta wa Daladala Hadi Kufa

$
0
0
DAR ES SALAAM: Kondakta wa daladala aina ya Nissan Civilian lenye namba za usajili T 247 DDT lililokuwa likifanya safari zake kati ya Temeke, Dar na Vikindu, Pwani, Abdallah Kikoto (36), anadaiwa kunyongwa na abiria wake hadi kufa, Ijumaa Wikienda linaripoti habari hii mbaya.

Taarifa zilizolifikia Ijumaa Wikienda zilieleza kuwa, katika tukio hilo lililojiri mwishoni mwa wiki iliyopita, abiria huyo alipanda basi hilo wakati likitokea maeneo ya Chamazi ambako linalazwa baada ya kazi. Ilielezwa kuwa, chanzo cha yote hayo ni mgogoro wa kurudisha chenji.

KISA NA MKASA

Akisimulia kisa hicho, dereva aliyekuwa akiendesha daladala hilo, Haji Kitara alisema kuwa, ilikuwa majira ya asubuhi, yeye na kondakta wake walikwenda Chamazi kuchukua daladala hilo na kuanza kazi ambapo wakiwa njiani kuelekea kwenye ‘ruti’ yao walianza kupakia abiria.

Aliendelea kusema: “Tulipofika njiani, nilianza kusikia kondakta wangu na huyo abiria wakilumbana. Huyo abiria alikuwa akisema kuwa ametoa noti ya shilingi elfu moja hivyo anataka arudishiwe chenji yake shilingi mia sita huku kondakta wangu yeye akisema tayari alishamrudishia.

“Waliendelea kulumbana hadi tulipofika Tandika-Msikiti wa Wapemba, Temeke, yule abiria alishuka na kumpora kondakta pesa zote alizokuwa nazo ili kufidia chenji yake.


Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi, (ACP) Emannuel Lukul.

KABARI YA HATARI

“Hapo ndipo mzozo ulikolea maana kondakta naye hakukubali kuporwa pesa zote kwa ajili ya hiyo mia sita. Nilipoona vurugu imekuwa kubwa, nilikimbiza basi hadi Kituo Kidogo cha Polisi cha Tandika, wakati huo yule abiria alikuwa amemkaba kondakta wangu kabari moja ya hatari sana.

“Tulipofika kituo cha polisi yule jamaa alimuachia konda kwa muda, wakati huo alikuwa ameshamchania suti yake ya juu na kumbakiza na ‘singlendi’, lakini wakiwa hapo kituoni waliendelea kubishana ndipo yule abiria akamvaa tena kondakta na kumnyonga kwa singlendi aliyobaki nayo.

“Yule abiria alimng’ang’ania kondakta huku akimnyonga na singlendi aliyovaa ndipo polisi waliokuwa kituoni hapo wakaingilia kati na kumnasua kondakta huyo akiwa amekabwa, lakini abiria huyo aliendelea kufanya hivyo hali iliyosababisha askari watumie rungu kumpiga nalo mikononi ndipo alipomuachia.

“Baada ya kumuachia kondakta huyo alianguka hapohapo na kupoteza fahamu hivyo polisi wa Kituo cha Tandika waliwasiliana na wenzao wa Kituo cha Chang’ombe ambao walipofika walituchukua wote na kutuhamishia Chang’ombe huku kondakta akiwa hajitambui.


AMEKATA ROHO

“Tulipofika Kituo cha Chang’ombe, askari wa pale walipomuona kondakta akiwa hajitambui walipatwa na shaka, wakamdhibiti huyo abiria na kumuwahisha Hospitali ya Temeke.

“Tukiwa pale hospitalini, daktari aliyempokea alituambia tayari kondakta huyo alikuwa ameshakata roho muda mrefu na alipoufanyia uchunguzi mwili wake, alisema kilichomuua ni kukosa pumzi.”

KAKA WA MAREHEMU

Kufuatia tukio hilo, mwandishi wetu alifika nyumbani kwa wazazi wa marehemu huyo, Mtoni-Mtongani Mtaa wa Wandengereko jijini Dar na kuzungumza na kaka wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Musa Kikoto ambaye alisema kuwa, alizipokea taarifa hizo kwa simanzi kubwa kwani kufuatia kifo hicho, mdogo wake huyo alikuwa ameacha mke na watoto wanne.

“Unajua mzazi unapokuwepo ndiyo unakuwa na jukumu la kupambana na malezi ya familia yako na usipokuwepo mambo ni vigumu kwenda inavyotakiwa, sasa mdogo wangu ameondoka mapema na kutuachia majukumu mazito ya kuwalea na kuwasomesha watoto wote hao ambayo bado tunayatafakari,” alisema kaka huyo.

Musa alisema kuwa, mdogo wake alizikwa katika Kijiji cha Mtawanya wilayani Kibiti mkoani Pwani.

KAMANDA TEMEKE

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi, (ACP) Emannuel Lukula alithibitisha kutokea tukio hilo na kusema mtuhumiwa anashikiliwa kwa tuhuma za mauaji.

“Ni kweli kulitokea tukio hilo ila si kwamba kondakta huyo amefia kituo cha polisi kwa kuwa daktari amethibitisha kifo ila hatuwezi kujua kama amefia njiani wakati akipelekwa hospitali au vinginevyo.

“Huyo jamaa (mtuhumiwa) tayari yuko mbaroni akikabiliwa na kesi ya mauaji, hata hivyo ndugu mwandishi sasa hivi sipo ofisini ningekuwepo ningekupa data nyingi zaidi za tukio hilo ikiwemo jina la mtuhumiwa na mengineyo,” alimalizia Kamanda Lukula.



STORI: Richard Bukos, IJUMAA WIKIENDA
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live




Latest Images