Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live

Ajari Nyingine Mbaya Yatokea Kimara

$
0
0
Ajari Nyingine Mbaya Yatokea Kimara
Ajali mbaya imetokea Kimara Mwisho jijini Dar es Salaam ambapo gari aina aya Toyota Noah namba T.871 BTU iliyokuwa ikitokea Mbezi kuelekea Ubungo na gari aina ya Cami namba T.840 DHE liliyokuwa likitokea Ubungo kuelekea Mbezi, nakupelekea gari hiyo aina ya Noah kupinduka.

Aidha katika ajali hiyo hakuna mtu aliyejeruhiwa wala kupoteza maisha.

Msaga Sumu Amuwashia Moto Fid Q " Kausha Kama Wenzako"

$
0
0
Msaga Sumu Amuwashia Moto Fid Q " Kausha Kama Wenzako"

Mfalme wa singeli nchini Tanzania, Msaga Sumu amefunguka na kumtaka rapa Fid Q akae kimya kama alivyofanya mwenzake Afande Sele kuliko kuonesha wivu na roho mbaya yake katika kuzungumzia vitu ambavyo havijui undani wake.




Msaga Sumu ameeleza hayo katika kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya kusikia kauli ya Fid Q ilikuwa inadai utunzi wa nyimbo za singeli umekaa kihuni na usela mwingi jambo ambalo kwa mtazamo wake anahisi anarudishwa nyuma katika ile miaka ya muziki kuonekana hauna maana ni uhuni mtupu kwa jamii.

"Ungekuwa muziki wa kihuni inamaana hata serikali ingeingilia kati suala hilo, chamsingi mtu anatakiwa akaushe tu kuongelea mambo mengine. Haya ni maisha na huu ni muziki kama anavyoona mingine tena muziki huu unaweza kuwa bora kuliko ambao wao wanaofanya. Singeli inapendwa na kila rika", amesema Msaga Sumu.

Pamoja na hayo, Msaga Sumu ameendelea kwa kusema "yeye kama hana mambo ya kufanya akaushe kama mwenzake Afande sele. Fid Q ndio mtu wa kwanza namsikia kusema muziki huu ni wakihuni tokea nazaliwa huu ni wivu na roho mbaya kwa sababu hakuna mtu yeyote aliyewahi kuzungumzia hii roho mbaya lakini labda nimwambie tu amechelewa".

Mbowe Awekwa Chini ya Uangalizi wa Madaktari

$
0
0
Mbowe Awekwa Chini ya Uangalizi wa Madaktari



Mdakatari waliokuwa wakichunguza maendeleo ya afya ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC ya Moshi wamemruhusu kuondoka hospitalini hapo huku wakimtaka awe chini ya uangalizi kutokana na maradhi yake


Mbowe ameruhusiwa kuondoka hospitalini hapo jana saa 1:30 usiku, akiwa ameambatana na mkewe Dk. Lilian Mbowe, baada ya madaktari wa hospitali hiyo kuridhishwa na afya yake kurejea katika hali ya kawaida.

Katibu wa Chadema, mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema amesema Mbowe aliondolewa KCMC na kwenda mapumzikoni nyumbani kwake Nshara, Machame, Wilaya ya Hai.

Kwa mujibu wa Lema, Mbowe ameshaondoka hospitali ya KCMC na sasa  yuko nyumbani kwake, baada ya madaktari kushauri akae mahali ambapo atapata muda mrefu wa kujitenga na kupumzika vya kutosha, mbali na kazi yake ili amalize dozi yake ya dawa alizopewa.

Alipotafutwa Ofisa Uhusiano wa Hospitali hiyo ya KCMC, Gabriel Chisseo kuthibitisha ukweli wa taarifa hizo amekiri Mbowe kuruhusiwa kuondoka hospitalini hapo, baada ya madaktari kuridhishwa na maendeleo ya afya yake.

Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni (KUB) na Mbunge wa Hai, alikuwa amelazwa katika Wodi ya Watu Mashuhuri (VIP), tangu Jumapili ya Machi 4, mwaka huu. Alipofikishwa hospitalini hapo saa 9:20 siku hiyo, aliwekewa mashine ya oxygen kwa azidi ya saa moja, huku ikielezwa pia kwamba alipopelekwa wodini kulazwa, vipimo vilionyesha shinikizo la damu kuwa juu ya wastani.

Hatimaye Wafuasi wa Mugabe Waunda chama cha Upinzani cha Kupambana na Mnangagwa

$
0
0
Hatimaye Wafuasi wa Mugabe Waunda chama cha Upinzani cha Kupambana na Mnangagwa

Jenerali mstaafu na mfuasi wa zamani wa Rais mstaafu Robert Mugabe, Ambrose Mutinhiri ameunda chama cha kisiasa ili kupambana na Rais Emmerson Mnangagwa katika uchaguzi mkuu baadaye mwaka huu.

Mugabe, mwenye umri wa miaka 94 alilazimishwa kustaafu Novemba iliyopita baada ya shinikizo la kijeshi.

Vyanzo karibu na kiongozi huyo wa zamani vinasema kuwa analalamikia namna utawala wake wa miaka 37 ulivyoondoshwa na anaunga mkono chama kipya cha New Patriotic Front (NFP).

Mutinhiri, mkongwe wa Zimbabwe aliyeshiriki vita vya kupigania uhuru miaka 1970 alijitoa kwenye chama cha Zanu-PF na kubwaga ubunge Ijumaa iliyopita, kisha alikutana na Mugabe Jumapili kumfahamisha maendeleo ya hivi karibuni, taarifa ya NPF ilisema.

Taarifa ya NPF imesema chama hicho kiliundwa na wafuasi wa Zanu-PF "waliokasirishwa na hatua isiyo ya kikatiba na udhalilishaji aliofanyiwa Mugabe kwa kuondolewa madarakani kama mhalifu ... na wahalifu wa kweli ambao wameharibu dhamana ya kidemokrasia nchini Zimbabwe".

Sera za Mugabe zimekuwa zikikosolewa na wengi kwa kusababisha Zimbabwe ishuke kutoka nchi yenye neema hadi kuwa isiyo na kitu, ukosefu wa ajira kuzidi asilimia 80, miundombinu ya umma iliyoharibika na uhaba mkubwa wa sarafu hali iliyozidisha mfumuko wa bei.

Chama hicho kipya cha upinzani kimesema kitafungua mashtaka kupinga uhalali wa serikali ya Mnangagwa katika Mahakama ya Katiba.

Hata hivyo, Novemba mwaka jana Mahakama Kuu ilitoa uamuzi kwamba hatua ya jeshi la Zimbabwe kuingilia kati ilikuwa halali kwa kuwa lilidhibiti jitihada za watu katika msafara wake kuchukua majukumu ya Mugabe na tayari nchi za Afrika na za Magharibi zimetambua urais wa Mnangagwa.

Gazeti la Herald linalomilikiwa na serikali ambalo huakisi mawazo ya Serikali lilisema kuwa Mutinhiri alikuwa shina lililokuwa nyuma ya siasa za Mugabe, mke wake Grace na kikundi cha G40 ndani ya Zanu-PF G40 kilichokuwa kinapinga kupanda kisiasa kwa Mnangagwa.

Mbali ya Mugabe na Grace, watu wengine waliopo nyuma ya chama hicho ni mawaziri waliopo uhamishoni Jonathan Moyo, Patrick Zhuwao na Saviour Kasukuwere.

Bunge la China Kuimarisha Zaidi Mamlaka ya Rais Xi

$
0
0
Bunge la China Kuimarisha Zaidi Mamlaka ya Rais Xi



Bunge la China lililoanza vikao vyake Jumatatu linatarajiwa kuidhinisha hatua za kuimarisha zaidi mamlaka ya Rais Xi Jinping ili kwenda sambamba na mabadiliko ya Katiba yaliyopendekezwa hivi karibuni.

Mabadiliko ya katiba yaliyopendekezwa kwenye mkutano wa mwaka wa bunge hilo ni pamoja na kujumuisha itikadi za kisiasa za Rais Xi Jinping kwenye sheria kuu ya China na kuondoa ukomo wa mihula ya Rais kuwa mamlakani.

Mapendekezo ya kuondoa ukomo wa mihula ya urais yanatarajiwa kuidhinishwa Machi 11 mwaka huu. Ikiwa yatapitishwa, Rais Xi ataweza kuendelea kuwa mamlakani bila ukomo baada ya kumalizika kwa mhula wa pili wa utawala wake mwaka 2023.

Mabadiliko makubwa ya nyadhifa katika nafasi za kiserikali pia ni miongoni mwa ajenda kuu za mkutano huo wa Bunge.

Mshirika muhimu wa Rais Xi Jinping, Wang Qishan amehudhuria mkutano huo wa bunge, sambamba na viongozi wengine.

Wang alimsaidia Rais Xi katika kampeni ya kukabiliana na rushwa nchini, lakini alistaafu kutoka kwenye Kamati Kuu ya Siasa ya Chama cha Kikomunisti mwaka jana, kwa mujibu wa umri wa kustaafu kwenye chama hicho.

Upo uwezekano mkubwa kwa Wang kupewa nafasi muhimu, huenda ya kuwa makamu wa rais na kuendelea kuwa na ushawishi katika diplomasia na kampeni ya kukabiliana na rushwa.



Ndoa za Utoto Zapungua Duniani

$
0
0
Ndoa za Utoto Zapungua Duniani

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa leo Machi 06, 2018 Shirika la Umoja wa mataifa linaloshughulikia masuala ya watoto ulimwenguni ( UNICEF) limesema kuwa kuna mafanikio makubwa ya kupungua kwa ndoa za utotoni duniani.

UNICEF wamekadiria kuwa ndoa za utotoni zipatazo milioni 25 zimeweza kuzuiliwa kwa kipindi cha muongo mmoja uliyopita.

Ripoti hiyo imeeleza kuwa msichana mmoja kati ya watano anaolewa chini ya miaka 18 tofauti na miongo iliyopita ambapo ilikuwa msichana mmoja anaolewa kati ya wanne.

UNICEF wamesema bara la Asia hususani Asia ya Kusini limejitahidi zaidi katika kupunguza ndoa za utotoni, ambapo ripoti imesema wamepunguza kwa asilimia 20 kutoka 50 iliyokuepo miaka 10 iliyopita.

Mshauri wa masuala ya jinsia kutoka UNICEF, Anju Malhotra amesema kuwa mabadiliko hayo ni kutokana na sera nzuri za serikali ikiwemo elimu kwa watoto juu ya ndoa za utotoni.

“Kama msichana atalazimishwa kuolewa akiwa mtoto, atkabiliwa na madhara makubwa siku za usoni. Kwani itakuwa ni kikwazo kwa kupata elimu pia ni rahisi kudhalilishwa na mumewe na inahatarisha maisha kipindi cha kujifungua. Mbaya zaidi ndoa za utotoni zina madhara makubwa kwenye jamii ikiwemo umasikini.”amesema Bi. Malhotra.

Ripoti hiyo imeeleza kuwa nguvu kubwa ya kutokomeza tatizo la ndoa za utotoni imehamia barani Afrika,ambapo jitihada za ziada zinahitajika ili kupunguza tatizo hilo.

Soma ripoti hiyo kamili iliyotolewa na UNICEF ->25 million child marriages prevented in last decade due to accelerated progress, according to new UNICEF estimates

Zaidi ya Vibanda 600 vya Wafanyabiashara Vyateketea kwa Moto Mbagala

$
0
0
Zaidi ya Vibanda 600 vya Wafanyabiashara Vyateketea kwa Moto Mbagala
Habari kutoka Mbagala Charambe leo March 6, 2018 ni kwamba zaidi ya vibanda 600 katika soko la Mkochela, vimeungua moto alfajiri ya leo na chanzo cha moto kinasadikiwa kuwa ni hitilafu ya umeme.

Afisa Habari wa Jeshi la Zima Moto Dar es Salaam Peter Mwambene ameeleza kuwa kwa mwaka huu hii ni mara ya pili, mwingine ulitokea mwezi February na sababu ya moto huu imekuwa ile ile kwa awamu zote mbili.

Mwambene pia ameeleza kuwa sababu ya moto huo kufanya uharibifu mkubwa ni kwamba vibanda vilikuwa vingi na ambavyo viko karibu karibu na ndani vilikuwa vina nguo ambazo zinachochea moto.

“Ni vizuri tukazingatia ujenzi wa kisasa wa mabanda ya biashara, mabanda ambayo yatapunguza athari endapo moto utatokea, lakini pia watu wawe na tahadhari ya vizimia moto vya awali, kwasababu havipo athari za moto zinakuwa kubwa zaidi.” – Peter Mwambene

Mtandao wa wanafunzi Tanzania (TSNP) Wailaumu TAHLISO Kuwakataza Kupigania Haki ya Marehemu Akwilina

$
0
0
Mtandao wa wanafunzi Tanzania (TSNP) Wailaumu TAHLISO Kuwakataza Kupigania Haki ya Marehemu Akwilina
Mwenyekiti wa mtandao wa wanafunzi wa Tanzania (TSNP), Abdul Nondo, akiongea na waandishi wa habari leo.

Ndugu waandishi wa habari, leo tunapenda kutoa ufafanuzi kidogo juu ya tuhuma zilizotolewa na TAHLISO dhidi ya TSNP mnamo tarehe 3/3/2028.

Taasisi yetu ni taasisi isiyo ya kiserikali iliyosajiliwa tarehe 23/10 /2001.  Lengo kubwa ikiwa ni kutetea wanafunzi kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu na kuwapa utambuzi watambue na kutimiza wajibu wao kikamilifu.

Ndugu waandishi wa habari, tumekuwa tukishirikiana na wizara ya elimu ambapo Waziri wa Elimu, Mh. Dkt. Ndalichako, Naibu Waziri, Ole Nasha, pamoja na Naibu Katibu wa wizara hiyo, Dkt.  Ave Marie Semakafa wamekuwa wakitusaidia kutatua changamoto za wanafunzi vyuo tofauti-tofauti kama vile MWECAU, CBE, ARDHI na MZUMBE.

Pia, tumekuwa tukishirikiana na taasisi mbalimbali za kiserikali katika utatuzi wa matatizo ya wanafunzi nchini. Kwa mfano, tumekuwa tukipata ushirikiano mzuri kutoka bodi ya mikopo wanafunzi wa elimu ya juu nchini kuhusiana na mchakato wa utoaji mikopo.
Pia tumekuwa tukishirikiana na tume ya vyuo vikuu nchini ( TCU) katika kutatua changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikijitokeza katika suala zima la udahili wa wanafunzi wa elimu ya juu nchini.

Na vilevile tumekuwa pia tukitumia vyombo vya habari kutoa mapendekezo yetu, kuelimisha wanafunzi na hata kuwajulisha watendaji wa serikali kuhusiana na uwepo wa tatizo mbalimbali kuhusu wanafunzi.

Lakini jambo la kushangaza mbali na kutimiza wajibu wetu kisheria, TAHLISO iliamua kwa makusudi kutushambulia bila kuwa na hoja zozote zile za msingi.

Tukumbuke kuwa TSNP haifadhiliwi na mtu yeyote wala taasisi yoyote ile, lakini tumekuwa mstari wa mbele kuwa sauti ya wanafunzi nchini.

TAHLISO ambayo kila chuo kikuu nchini kinatoa ada isiyopungua shillingi laki tano kwa mwaka ili TAHLISO iweze kutetea maslahi ya wanafunzi wa vyuo vikuu nchini, imeacha kutimiza wajibu wake wa msingi na badala yake imegeuka kuwa taasisi yenye kusema kwa niaba ya serikali pamoja na kushambulia taasisi ambazo zinatetea maslahi ya wanafunzi nchini ikiwemo TSNP.

KUHUSU KIFO CHA AQUILINE

Ndugu waandishi wa habari, marehemu Aquiline alikuwa na haki zake za msingi kama binadamu ikiwemo haki za kuishi,na kila taasisi au mtu yeyote ana haki ya kukemea matendo yeyote maovu dhidi ya binadamu.
Tuwaulize TAHLISO, wao wanapata wapi mamlaka ya kukataza, kuonya, kukemea makundi, watu,taasisi zilizoguswa na suala hili kusemea juu ya tukio lile?

Pili, Aquiline alikuwa ni mwanafunzi pia, TSNP ni mtandao wa kutetea wanafunzi, tunayo hayo mamlaka kusemea, kukemea, kushauri na hata kutoa mapendekezo yetu juu ya tukio lolote linaloashiria upotevu wa haki kwa wanafunzi.  TAHLISO wanatoa wapi ujasiri, mamlaka ya kutuzuia TSNP tusitimize wajibu wetu?

Tatu, TSNP tumekuwa mstari wa mbele kusemea shida za wanafunzi mikopo, udahili, wanafunzi kufukuzwa na tumeshirikiana na taasisi za serikali na hata viongozi wa serikali katika utatuzi wa shida za wanafunzi, TAHLISO inayojinasibu kuwa inatetea wanafunzi ije iseme ilifanya nini kati ya haya hadi leo iwe na ujasiri na mamlaka ya kushambulia TSNP.



KUHUSU TSNP KUTUMIWA NA WANASIASA

Ndugu waandishi, TSNP ni taasisi ambayo haifungamani na chama chochote kile cha siasa na haifanyi kazi ya chama chochote.
Na ndiyo maana mara zote mmekuwa mkituona huwa tuna agenda zinazohusu wanafunzi tu kama vile mikopo ya wanafunzi, udahili wanafunzi, mmetuona katika makongamano ya wanafunzi.
Pia tulitoa maoni na mapendekezo yetu kuwa kama hatua stahiki hazitachukuliwa Mh. Mwigulu ajiuzulu (individual ministerial responsibility) kutokana na matendo dhidi ya uvunjifu wa haki za binadamu kushamiri bila kuwepo kwa taarifa juu ya uchunguzi na hatua stahiki kwa wahusika.
Lakini jambo la kushangaza TAHLISO wametoka mbele kutetea serikali na wizara ya mambo ya ndani na kuacha jukumu la kuwatetea wanafunzi.
Inashangaza sana kuona TAHLISO inaishambulia TSNP na kudai kuwa inatumiwa kisiasa ilihali tunashughulika na shida za wanafunzi, na wao wamejisahau wanavyoshughulika na majukumu ya kusemea na kutetea serikali.

Kwa mantiki hii sasa, kama TAHLISO wanatulaumu na kutushambulia, wanatushambulia na kwa lipi?

HITIMISHO

Tunawataka TAHLISO waache kuwa wasemaji wa wizara na serikali na wakumbuke majukumu yao mazito ya kusemea wanafunzi wa vyuo vikuu kwa sababu wanalipishwa ada vyuo vikuu.
Hivyo kulipishwa ada pasipo kutimiza wajibu unaotakiwa kutimiza, hiyo ni silent corruption.

Imetolewa na:
Mtandao wa wanafunzi Tanzania (TSNP)

Mbuzi wa Tambiko Aleta Kizaazaa Moshi

$
0
0
Mbuzi wa Tambiko Aleta Kizaazaa Moshi

Mtu mmoja aliyetajwa kwa jina la James Mallya amejeruhiwa baada ya kukatwa mapanga na kiongozi wa tambiko baada ya kumshika mbuzi wa tambiko katika msiba kwenye Kata ya Kibosho wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro.

Akizungumza leo Machi 6, 2018 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamis Issah amesema Mallya amekatwa mapanga Machi 5, 2018 baada ya kumshika mbuzi huyo aliyeandaliwa kwa ajili ya msiba na amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC, mjini Moshi.

Amesema alikatwa mapanga baada ya kiongozi wa tambiko kuchukizwa na jinsi alivyokuwa akimshika mbuzi wa tambiko, kwa kuwa kitendo hicho kiliharibu utaratibu wa mila.

“Mallya ni mkazi wa Dar es Salaam alifika kwa ajili ya kushiriki msiba, akiwa msibani alikwenda kumshika mbuzi aliyekuwa amefungwa jirani ambaye alikuwa ni kwa ajili ya tambiko kwenye msiba huo,” amesema Issah.

“Alipomshika mbuzi ndipo kiongozi wa tambiko hilo jina tumelihifadhi alipomsogelea na kuanza kumkata kwa panga kichwani.”

Kamanda huyo amesema kiongozi huyo wa tambiko alipoulizwa sababu za kufanya hivyo, amesema amechukua uamuzi huo kwa sababu Mallya aliharibu utaratibu wa tambiko, kwamba kwa mujibu wa mila zao hairuhusiwi kumshika mbuzi wa tambiko.

Katika tukio jingine, mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Rama amekutwa amefariki dunia na mwili wake kutupwa katika shimo la maji machafu jirani na nyumba aliyokuwa akiishi kwenye kijiji cha Oria Kata ya Kahe Magharibi wilayani Moshi.

Sijaona Hasara Kufungiwa Bongo Bahati Mbaya- Young D

$
0
0
Sijaona asara Kufungiwa Bongo Bahati Mbaya- Young D
Msanii Young Dee amezungumza baada ya kufungiwa wimbo wake wa Bongo bahati mbaya ambapo ameeleza kuwa hata yeye hajapewa taarifa yoyote kuhusu kufungiwa wimbo huo zaidi ya kuona kwenye mitandao, isitoshe hajui sababu ya kufungiwa kwa wimbo wake na haelewi nini wanataka na nini hawataki.

Amesema hajafikiria kwenda BASATA kuuliza kuhusu hilo na kwasasa hajaona hasara maybe baadae na hawezi kusema moja kwa moja kama haimuumizi sababu wapo wasanii ambao inawaumiza.

Bocco Awaomba Mashabiki wa Simba

$
0
0
Bocco Awaomba Mashabiki wa Simba
Nahodha wa klabu ya soka ya Simba mshambuliaji John Bocco, amewaomba mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi kwenye mechi ya kesho dhidi ya Al Masry kwani ni nafasi nzuri ya timu yao kuwapatia furaha.


''Kesho tunaimani tutacheza mchezo mzuri na tutawapa raha mashabiki wetu, ukizingatia mechi iliyopita dhidi ya Stand United hatukupata matokeo mazuri hivyo kesho ni nafasi nzuri ya kuwapa raha Wanasimba'', amesema Bocco kwenye mkutano na wanahabari.

Simba kesho itashuka dimbani kucheza mchezo wake wa kwanza wa Kombe la shirikisho Barani Afrika dhidi ya Al Masry kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam kuanzia saa 12:00 jioni.

Kwa upande mwingine Bocco amesema wamejipanga kucheza kitimu zaidi kesho ili kuepuka makosa ya mtu mmoja mmoja ambayo yamekuwa yakiigharimu timu katika mechi za hivi karibuni.

Kikosi cha Al Masry ambayo inashika nafasi ya 4 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 48 kwenye mechi 25 ilizocheza tayari kipo nchini tangu jumamosi iliyopita.

Manowari ya Marekani Iliyozamishwa Maka 1942 Yagunduliwa Baharini

$
0
0
Manowari ya Marekani Iliyozamishwa mMaka 1942 Yagunduliwa Baharini

Mabaki ya manowari ya Marekani ambayo ilizamishwa wakati wa vita vya pili vya dunia yamegunduliwa nje ya pwani ya Australia.

Manowari ya USS Lexington iligunduliwa umbali wa kilomita 3 chini ya bahari karibu kilomita 800 kutoka pwani ya Australia.

Manowari hiyo ilikuwa ilitoweka wakati wa vita vya Coral Sea, kati ya tarehe 4-8 Mei mwaka 1942. Zaidi ya wanajeshi 200 waliuawa wakati wa kuzama kwa meli hiyo.

Mabaki ya meli ya abiria iliyozamishwa 1939 yagunduliwa baharini
Jeshi la wanamaji la Marekani lilithibitisha kuwa meli hiyo ilikuwa imegunduliwa na kundi la kutafuta, linaloongozwa na mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Microsoft Paul Allen.

Meli hiyo ilizamishwa pamoja na ndege 35 ilizokuwa imebeba
Tangazo la kugunduliwa meli hiyo na ndege 11 kati ya 35 ilizokuwa imebeba, lilitolewa na kampuni ya Bw Allen ya Vulcan siku ya Jumapili

Nyambizi ya Ujerumani iliyozama wakati wa vita vya kwanza vya dunia yapatikana
Bomu kubwa la vita vya pili vya dunia kuharibiwa Ujerumani
Vita vya Coral Sea vinatajwa kama hatua kubwa ya kuizuia Japan kuwa na ushawishi huko Pacific wakati wa vita.

Jeshi la Marekani lilisema kuwa wanajeshi 216 waliuawa wakati meli hiyo ilishambuliwa. Zaidi wa wengine 2,000 waliokolewa.

Mwaka uliopita Vulcan ilingundua mabaki ya meli ya USS Indianapolis, ambayo ilizama mwezi Julai mwaka 1945.

Imegundua vyombo vingine vikiwemo meli ya vita ya Japan, Musashi na nyingine ya Italia Artigliere zote kutoka eneo hilo.

Jarada la Kesi ya Mke wa Bilioni Msuya Bado Lipo Mikononi mwa DPP

$
0
0
Jarada la Kesi ya Mke wa Bilioni Msuya Bado Lipo Mikononi mwa DPP
Upande wa mashtaka katika kesi ya mauaji inayomkabili mke wa bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita (41), umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa jalada la kesi hiyo bado lipo mikononi kwa mkurugenzi wa mashtaka (DPP) kwa ajili ya kulifanyia uamuzi.

Wakili wa Serikali,  Mutalemwa Kishenyi amedai leo  Machi 6, 2018  mbele ya hakimu mkazi mkuu, Thomas Simba wakati shauri hilo lilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Mbali na Mrita, mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ya mauaji namba 5 ya mwaka 2017 ni mfanyabiashara Revocatus Muyela (40) na wote wanakabiliwa na shtaka moja la mauaji ya dada yake Erasto Msuya, Aneth Msuya.

Itakumbukwa kuwa, Februari 21, 2018 upande wa mashtaka ulidai mahakamani hapo kuwa jalada la kesi hiyo lipo kwa DPP kwa ajili ya kufanyiwa kazi.

"Shauri lilikuja kwa ajili ya kutajwa na jalada la kesi hii lipo kwa DPP kwa ajili ya kulifanyia maamuzi, hivyo tunaomba tarehe nyingine kwa ajili ya (kesi) kutajwa," amedai Kishenyi.

Baada ya Kishenyi kueleza hayo, wakili wa utetezi, Peter Kibatala amekubaliana na upande wa mashtaka na kuiomba mahakama hiyo kupanga tarehe katika muda mfupi.

Kutokana na maelezo ya pande zote, Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Machi 13, 2018 itakapotajwa.

Washtakiwa kwa pamoja wanakabiliwa na shtaka la mauaji ambapo wanadaiwa kumuua dada wa bilionea Msuya, Aneth Msuya.

Februari 23, 2017 waliachiwa huru na mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa na kisha wakakamatwa tena na baadaye kusomewa shtaka moja la mauaji.

Washtakiwa wanadaiwa kumuua kwa makusudi Aneth tukio linalodaiwa kutokea Mei 25, 2016 maeneo ya Kibada Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Ahukumiwa Miaka 30 kwa Kosa la Kusafirisha Kilo 32.57 za Bangi

$
0
0
Ahukumiwa Miaka 30 kwa Kosa la Kusafirisha Kilo 32.57 za Bangi

Leo March 6, 2018 nakusogezea hukumu iliyotolewa katika Mahakama ya Wilaya Kinondoni ambapo imemhukumu miaka 30 jela mkazi wa Kinondoni Mkwajuni Agnes Mhoja (40), baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kukutwa akisafirisha Kilo 32.57 za dawa za kulevya aina ya Bangi.

Mbali ya Mhoja mshtakiwa mwingine ni Samwel Jangwa (25), ambae aliachiwa huru kutokana na upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha makosa dhidi yake.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Boniface Lihamwike, amesema mshtakiwa Mhoja ametiwa hatiani baada ya mahakama kuridhishwa na ushahidi uliowasilishwa na mashahidi watatu wa upande wa mashtaka.

Amesema ushahidi wa upande wa mashtaka uliotolewa na Ofisa wa ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Mpelelezi na Ofisa wa Polisi aliyemkamata mshtakiwa ulikuwa na vielelezo vya kutosha.

“Kwa mazingira hayo mahakama hii inakutia hatiani kwa kosa hilo kutokana na ushahidi wa kina uliowasilishwa hapa ambao nimeuthibitisha pasi na shaka,” Hakimu Lihamwike.

Hakimu Lihamwike amesema kutokana na mshtakiwa kutiwa hatiani anamuhukumu kwenda jela miaka 30 ambapo hilo litakuwa ni onyo na fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo za kusafirisha Bangi.

Awali Wakili wa serikali, Yussuf Aboud, aliieleza mahakama kuwa hakukuwa na kumbukumbu za makosa ya nyuma dhidi ya mshtakiwa, hivyo mahakama itoe adhabu kali.

Katika utetezi wake, mshtakiwa Mhoja ameiomba mahakama impunguzie adhabu kwa sababu Bangi aliyokamatwa nayo haikuwa mzigo wake halali, pia yeye ni mtu mzima anayetegemewa na familia.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka katika kesi hiyo namba 472/2016 Mhoja anadaiwa akiwa eneo la Kituo cha Mabasi yaendayo mkoani Ubungo, alikutwa akisafirisha Kilo 32.57 za dawa za kulevya (Cannabis Sativa) maarufu kama Bangi.

Inadaiwa ametenda tukio hilo October 30, 2016 eneo hilo la Ubungo ambapo November 15, 2016 alifikishwa mahakamani hapo na kusomewa shtaka lake.

Mzee Akilimali Amuwakia Mkwasa "Acha Kuudanganya Umma"

$
0
0
Mzee Akilimali  Amuwakia Mkwasa "Acha Kuudanganya Umma"
Katibu wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimali, amemuomba Katibu Mkuu wa klabu hiyo kuacha kuudanganya umma.

Kauli ya mzee Akilimali imekuja mara baada ya kikosi cha leo kitakachocheza dhidi ya Township Rollers FC kuwekwa wazi huku baadhi ya wachezaji waliotajwa kuwepo wakikosekana.

Katika mkutano alioitisha jana na waandishi wa habari, Katibu Charles Mkwasa, alisema wachezaji Thaban Kamusoko, Yohana Nkomola pamoja na Ramadhan Shaibu 'Ninja' watakuwa fiti asilimia 100 kucheza leo.

Akilimali amemuomba Mkwasa kuwa mkweli haswa linapotokea suala la mechi za kimataifa, kwani huhitaji kikosi chenye wigo mpana na si kuwadanganya watu kuwa fulani atakuwepo kisha baadaye akosekane.

Na kuelekea mchezo wa leo, Akilimali amewaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kuipa hamasa timu yao, ili iweze kusonga mbele katika Ligi ya Mabingwa Afrika.


Mwigulu Atoa Msaada wa Cement na Mabati Kwaajili ya Ujenzi wa Zahanati na Mabweni

$
0
0
Mwigulu Atoa Msaada wa Cement na Mabati Kwaajili ya Ujenzi wa Zahanati na Mabweni

Mbunge wa Iramba Magharibi Dk. Mwigulu Nchemba ametoa mabati 210 na cement mifuko 100 kwa ajili ya ujenzi wa zahanati na mabweni ya wanafunzi, Kata ya Mtoa ili kusaidia kupunguza adha wanayopata wananchi  kufata huduma umbali wa zaidi ya kilimota 10.




Mh.  Nchemba amesema anakerwa na jengo kukaa mda mrefu bila kumaliziwa hivyo ameamua kutoa bati 210 na kuchangia shilingi milioni moja na nusu kwa ajili ya ununuzi wa mbao ili ujenzi uanze mara moja na kikamilike ndani ya mwaka huu ili kianze kutoa huduma.

"Mimi nakerwa na jengo kukaa mda mrefu hivi, hatulali hata sekunde tunaendelea kutafuta mbao na bati nyingi zikafunike baadhi ya vituo kwahiyo ninapoona jengo lipo hivi wala mtu asidhanie nafurahia jengo libaki vilee" amesema Dk. Nchemba

Nao wananchi wa kata ya mto awamemshukuru mbunge wao kwa kuwaletea mabati na cement kwa ajili ya kumalizia zahanati yao ya mtoa pamoja na mabweni kwani ni jambo ambalo walikuwa wanalilia kupata zahanati hiyo.

Mh. Nchemba yupo jimboni Iramba kwa ziara maalumu ya kutekeleza ahadi alizotoa wakati akitafuta nafasi ya ubunge 2015.

Hili Hapa Swali la Lema Leo "Ni kweli Tunahitaji Kamati Teule Kuhusu Utekaji ?

$
0
0
Hili Hapa Swali la Lema Leo "Ni kweli Tunahitaji Kamati Teule Kuhusu Utekaji ?
Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA), Godbless Lema amesema wanapita katika maumivu makali katika siasa wanazozifanya hivyo hawaitaji kuona sinema tena zikiendelea kutoka kwa miongoni mwa wabunge wenzao.

Hiyo inakuja baada ya Mbunge Hussein Bashe kupelekea barua hiyo kwa Katibu wa Bunge kutaka iundwe kamati Teule ya kuchunguza baadhi ya mambo yanayoendelea nchini.



Lema ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram amehoji kuwa Hivi ni kweli tunahitaji Kamati teule kuhusu utekaji na kufifia kwa demokrasia Nchini ?.

Nina fikiri ninapaswa kusema kidogo juu ya hoja binafsi ya Mh Husein Bashe katika mkutano wa Bunge unaokuja.Hivi ni kweli tunahitaji Kamati teule kuhusu utekaji na kufifia kwa demokrasia Nchini ?

Ni maamuzi ya ccm ktk mikutano yao ya ndani ya Bunge na nje ya Bunge kuhusu hali ya demokrasia na siasa Nchini, ujenzi wa vyama vya siasa na mikutano imepigwa marufuku .

Mikutano ya Bunge live pia imepigwa marufuku , Wabunge na Madiwani wa Upinzani waneendelea kupitia mateso makubwa,vitisho vya mauaji , kuwekwa mahabusu na kufungwa.

Wakati mambo haya yanaendelea kutokea Bunge limekataa hata kulipa matibabu ya Mh Lissu.
Hakuna Mbunge mmoja wa ccm akiwemo Husein Bashe alishawahi kwenda kumjulia hali Mh Lissu Hospital, unajiuliza ni kwa nini ?

Mambo haya yako wazi hayahitaji PHD kujua msimamo wa Wabunge wa ccm kuhusu haki,ukweli na nuru ya mabadiliko .

Wabunge wa ccm wakibadili mtazamo kuhusu Nchi Bunge litakuwa imara na Bunge imara ndio msingi wa Serikali bora na Bunge imara linatokana na Wabunge majasiri, wako wapi ndani ya ccm ?
Msingi wa kwanza wa ukomavu wenu ni kurudisha hadhi ya Bunge kwa umoja na idadi yenu , platform nyingine nje ya kujitathimini kwa masilahi ya Nchi ni unafiki.
Bashe unafikiri Kamati teule inaweza kuwa na maana kwenye Bunge hili ? hotuba za Wapinzani Bungeni zime endelea kuwa sensored ndani ya Bunge na haya ni maoni mbadala ya ushauri kwa Serikali lakini siku zote mmekaa kimya.

Chama chako ni tatizo na Viongozi wake,na wewe unafahamu mambo haya, hivi kweli tunahitaji tena kugundua kanuni ya kutengeneza gari wakati kuna magari yana tembea barabarani ?
Tunahitaji umoja wenu kwa masilahi ya haki ndani ya Bunge kwenye mambo yote yanayo rudisha heshima ya Wabunge , wingi wenu umekuwa hasara kwa Nchi badala ya faraja.

Tunapoona maigizo yanayotaka kupotosha haki yanazingatiwa hapa ndipo tunapatwa hasira na kuondoa nidhamu katika mahusiano yasiyo na tija na Nchi , hata hivyo andiko hili sio ugomvi lakini pia limejengwa hasira na hali zetu kisiasa tunayopitia, sisi Wabunge wa upinzani karibu wote tuna kesi sehemu mbali mbali Nchini, mmoja wetu sasa ni mfungwa (Sugu) .

Tunapitia maumivu makali sana kwa sasa hatuitaji tena sinema.

Msaga Sumu Amshukia Vikali Fid Q, Asema Atafute Kazi ya Kufanya, Aache Roho Mbaya

$
0
0
Mfalme wa singeli nchini Tanzania, Msaga Sumu amefunguka na kumtaka rapa Fid Q akae kimya kama alivyofanya mwenzake Afande Sele kuliko kuonesha wivu na roho mbaya yake katika kuzungumzia vitu ambavyo havijui undani wake.

Msaga Sumu ameeleza hayo katika kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya kusikia kauli ya Fid Q ilikuwa inadai utunzi wa nyimbo za singeli umekaa kihuni na usela mwingi jambo ambalo kwa mtazamo wake anahisi anarudishwa nyuma katika ile miaka ya muziki kuonekana hauna maana ni uhuni mtupu kwa jamii.

"Ungekuwa muziki wa kihuni inamaana hata serikali ingeingilia kati suala hilo, chamsingi mtu anatakiwa akaushe tu kuongelea mambo mengine. Haya ni maisha na huu ni muziki kama anavyoona mingine tena muziki huu unaweza kuwa bora kuliko ambao wao wanaofanya. Singeli inapendwa na kila rika", amesema Msaga Sumu.

Pamoja na hayo, Msaga Sumu ameendelea kwa kusema "yeye kama hana mambo ya kufanya akaushe kama mwenzake Afande sele. Fid Q ndio mtu wa kwanza namsikia kusema muziki huu ni wakihuni tokea nazaliwa huu ni wivu na roho mbaya kwa sababu hakuna mtu yeyote aliyewahi kuzungumzia hii roho mbaya lakini labda nimwambie tu amechelewa".

Mtazame hapa chini Msaga Sumu na Fid Q wakifunguka mengine zaidi.

Video: Nabii Olivia Asikika Akimpanga Muumini Apige Kelele Kuashiria Anatolewa Mapepo

$
0
0
Kweli siku za mwisho zimekaribia, Shuhudia katika Video Nabii Olivia wa Kanisa la Repohim Church amesikika akimpanga muumini apige kelele akiashiria mapepo yanamtoka.

Tazama Video Hapa Chini:



Biashara ya Viungo vya Maiti Dar Yaibua Hofu

$
0
0
Hofu imetanda kufuatia kusambaa kwa taarifa kuwa kuna biashara ya viungo vya maiti inayofanyika kwenye maeneo ya makaburini, Uwazi linaripoti.

Makaburi yanayotajwa kwenye biashara hiyo ni Kinondoni na Sinza jijini Dar.

 Taarifa hizo zilidai kuwa, biashara hiyo inadaiwa kufanywa na baadhi ya wafanyabiashara kwa kushirikiana na vijana wanaotoa huduma za kuchimba makaburi katika maeneo tajwa.

Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika vilivyozungumza na Uwazi, taarifa hizo zilidai kuwa, viungo hivyo vinauzwa kwa bei chee kabisa.


Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob.

“Kutokana na hali ya kimaisha kuwa ngumu, kuna vijana, wale wanaotoa huduma ya kuchimba makaburi ‘gravediggers’ au kuyafanyia usafi, inasemekana pia wanauza viungo vya maiti. Nasikia ishu hiyo ipo hasahasa kwenye Makaburi ya Kinondoni na Sinza-Makaburini,” alidai mmoja wa watoa taarifa wetu, Fresha Mariki, Mkazi wa Sinza- Palestina, Dar.

 “Mimi nadhani ni kwa ajili ya kuvitumia viungo hivyo kwenye biashara maana sasa hivi hali ni mbaya na kila mtu anafanya juu-chini kuhakikisha anapata chochote kwenye biashara.

“Kwa vyovyote jambo hili lina uhusiano mkubwa na mambo ya kishirikina,” alisema mtoa habari mwingine, Vincent Kabesi, mkazi wa Kinondoni-Kwamanyanya, Dar.

 Baada ya kuelezwa juu ya jambo hilo la kutisha, Uwazi halikuzipuuzia badala yake liliamua kuzifungia kazi kwa kwenda kwenye makaburi yaliyotajwa ili kufanya uchunguzi.

KINONDONI-MAKABURINI

Katika Makaburi ya Kinondoni, waandishi wetu walikutana na vijana wengi ambao wanajishughulisha na masuala ya kusaidia mazishi makaburini hapo.

Vijana hao waliwakaribisha waandishi wetu kwa bashasha kwa ajili ya kupatiwa huduma ya kuchimba kaburi, kujengea, kusafisha makaburi na kutengeneza majeneza.



Wakiwa eneo hilo, waandishi wetu walijifanya wanataka huduma, hivyo walimuita mmoja wa vijana hao pembeni na kuzungumza naye.

Waandishi wetu walimweleza jamaa hiyo kuwa wanahitaji kiungo cha binadamu kwa bei yoyote ile kwa sababu walikuwa wamepewa dili.

 Awali, kijana huyo alionekana kushtuka, lakini baada ya kumuondoa wasiwasi, aliwaambia kwamba wanaweza kupata kiungo chochote cha maiti kwa sharti la kulifanya jambo hilo kwa siri kubwa na endapo watatoa kiasi cha shilingi laki mbili.

 Wakati wa majadiliano hayo, Uwazi lilikuwa likirekodi mazungumzo kati yake na kijana huyo ambaye alikuwa akijinasibu kwa vitu vingi huku akiongeza kwamba watu wengi, tena wazito, hufika makaburini hapo kwa sababu mbalimbali ikiwemo ishu hiyo ya kuhitaji viungo vya maiti, kutupa vitu vyao vya kiganga makaburini au kuvunja nazi maeneo hayo.

 Bila kusema kama huwa wanawauzia viungo hivyo, jamaa huyo alijikuta akitoboa siri kuwa viungo vinavyouliziwa zaidi na watu hao ambao wengi ni wafanyabishara wakubwa na wanasiasa ni vidole vyote, viungo vya sehemu za siri, fuvu la kichwa na vinginevyo kama vile kipande cha sanda.

 SINZA-MAKABURINI

Baada ya uchunguzi wa kina kwenye makaburi hayo ya Kinondoni, waandishi wetu waliweka kambi kwenye Makaburi ya Sinza-Makaburini ambako nako walifanikiwa kuzungumza na vijana waliowakuta makaburini hapo ambao pia hali ilikuwa vilevile.

Kwa upande wa makaburi hayo, waandishi wetu walizungumza na vijana wawili ambao walisema kuwa, wenyewe wanaweza kufanya biashara hiyo kwa kiasi cha shilingi hata laki moja na kwamba wana mfuko ambao una viungo vingi waliouchimbia chini. Zaidi waliongeza kwamba, wao hufanya hivyo kwa waganga na watu wanaopenda masuala ya kishirikina.

POLISI WANAUJUA UHALIFU HUU?

Uchunguzi ulipokamilika, Uwazi lilimtafuta Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai, DCI Robert Boaz lakini simu yake iliita bila kupokelewa. Likamgeukia Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Jumanne Muliro na kumuelezea kinagaubaga juu ya uchunguzi huo.

 Katika mazungumzo yake na Uwazi, Kamanda Muliro alisema kuwa, hana taarifa hizo na kwamba kwa kuwa alizipata kutoka kwa mwandishi wetu, basi atazifanyia kazi.

“Kiukweli sijasikia kabisa kuhusu suala hilo, kwa kuwa mmeniambia nitazifanyia kazi,” alisema Kamanda Muliro.

MEYA WA UBONGO

Kwa upande wake, Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob alipoulizwa alisema: “Sina taarifa ya suala hilo, kikubwa mimi nitazifanyia kazi taarifa hizi ambazo mnanipa.”

NENO LA UWAZI

Gazeti hili linalaana vikali vitendo hivi kwa sababu ni kinyume na maadili, haki za binadamu na sheria za nchi. Pia linaviomba vyombo vya dola kufuatilia na kuwatia nguvuni wote wanaoshiriki vitendo hivi hasa pale itakapobainika kwamba taarifa hizo zina ukweli ndani yake.

STORI: WAANDISHI WETU | GAZETI LA UWAZI
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live




Latest Images