Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live

Johari Afunguka Kuhusu Kushindwa Kumtembelea Lulu Gerezani

$
0
0
Johari Afunguka Kuhusu Kushindwa Kumtembelea Lulu Gerezani
Msanii nguli wa filamu Tanzania Blandina Chagula alimaarufu kama Johari amefunguka na kuweka wazi sababu kubwa inayomfanya ashindwe kwenda kumtembelea msanii mwenzake wa filamu Lulu Michael gerezani.


Johari akiwa kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV kila siku ya Jumatano kuanzia saa nane mchana amesema kuwa toka Elizabeth Michael amefungwa hajawezi kwenda gerezani kumtembelea na kumjulia hali kwa kuwa anahofia kwenda kwake ni kuzidi kumuongezea uchungu na upekwe.

"Kiukweli toka Lulu amefungwa jela sijawahi kwenda kumsalimia, kwa upande wangu naona unapokwenda kutembelea ni sawa na kumuongezea machungu na upekwe zaidi hivyo mimi naona hivyo ndiyo maana nakuwa mzito" alisema Johari

Aidha Johari amedai kuwa kitendo cha Kanumba kufariki na kuonekana Lulu alihusika kwenye kifo hicho ni jambo ambalo liliwaumiza sana kwa kuwa watu hao wote walikuwa karibu na wao lakini anaamini kuwa yote hayo ni mipango ya Mungu.


Kingu: Serikali Haijashindwa Kusimamia Usalama

$
0
0
Kingu: Serikali Haijashindwa Kusimamia UsalamaMbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu amesema suala la bunge kujadili hali ya usalama wa nchi na kutaka kamati iundwe kuchuguza matukio ya kihalifu kutasababisha taharuki ambayo tafsiri yake ni kama serikali imeshindwa kusimamia usalama.


Mbunge Kingu ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa akifanya mahojiano na www.eatv.tv kuhusu kuunga mkono maamuzi ya Hussein Bashe ya kupeleka hoja binafsi bungeni kuhusu kuteuliwa kwa kamati teule ya kuchunguza matukio ya utekaji, mauaji na kushambuliwa kwa watu mbalimbali nchini.

Mh. Kingu amesema kwamba kwa upande wake anaamini kuwa Serikali haijashindwa kabisa kulinda usalama wa nchi mpaka suala hilo likajadiliwe ndani ya bunge na kusisitiza matukio ya kihalifu yapo nchi nyingi duniani na hata katika tawala zilizopita.

Akiendelea  kutoa ufafanuzi Mh. Kingu amesema kwamba anaamini Usalama wa nchi ya Tanzania upo vizuri kuliko hata mataifa mengine makubwa hivyo ni vyema pia kuangalia Tanzania inafananishwa na nchi gani katika kuangalia hayo matukio ya kihalifu  yanayotajwa.

"We must be smart kwa lengo la kuwa wazalendo kwa nchi yetu na hata serikali ikikosea tunapaswa kuikosoa na siyo kuibebesha mzigo. Lakini kwa vile ni hoja ya Mbunge mwenzangu naheshimu, sina mamlaka ya kuzuia wala serikali haina mamlaka  hivyo nasubiri ikifika bungeni tutaijadili na hata mimi nikipata nafasi nitachangia,"Mh. Kingu.

Pamoja na hayo Mh. Kingu amesema kwamba "Polisi wengine  wanakuwa hawana maadili lakini siyo kwamba serikali imeshindwa mpaka tuanze kuijadili na kuiwajibisha serikali. Jeshi la polisi l;iwe na utayari wa kutoa taarifa za haraka. Hii ni changamoto pia kwa jeshi la polisi na serikali.

P Funk Amefunguka Kuhusu Beef ya Mr. T Touch, S2kizzy na Luffa

$
0
0
P Funk Amefunguka Kuhusu Beef ya Mr. T Touch, S2kizzy na Luffa
Produ
cer mkongwe Bongo, P Funk Majani amefunguka kuhusu kuwepo kwa beef miongoni mwa ma-producer wapya wa sasa.

P Funk ameiambia XXL ya Clouds Fm kuwa wao kama ma-producer wanaheshimiana na suala la malumbano mara nyingi ni kwa wasanii na si kwao kwani kwa upande wa production wapo wachache.

“Labda hao wadogo ambao juzi kati nimeona wanalumbana, sijui S2kizzy, T Touch na Luffa, sijui wanasema muziki wa T Touch wa kizamani, hitu kama hivyo tunacheza taarab sasa,” amesema.

“Kwa sababu kinachoonekana ni kazi, kama muziki umekubali basi ni mzuri uwe wa kizamani au wa kisasa,” amesisitiza.

Mr. T Touch, S2kizzy na Luffa ni ma-producer ambao kwa sasa kila mmoja anafanya vizuri hapa Bongo, wote kwa sasa ngoma walizofanya vinafanya vizuri katika radio station mbali mbali.

Mbinu za Kutunza Ngozi yenye Mafuta

$
0
0
Sababu ya ngozi kuwa na mafuta hutokana na  na tezi za sebaceous na kuzalisha mafuta zaidi ya kiwango ambacho ambacho kinatakiwa. Lakini licha ya tezi hizo aina za sebaceous kuzalisha kiwango cha mafuta kwa wingi, zipo pia sababu nyingine ambazo zinafanya ngozi kuwa na mafuta ambazo kama ifuatavyo.

• Kurithi.
• Lishe.
• Kiwango cha homoni mbalimbali mwilini.
• Ujauzito.
• Baadhi ya vipodozi .
• mabadiliko ya hali ya hewa hasa joto.

Na madhara ambayo yanatokana na ngozi yenye mafuta ni kwamba, ngozi huweza kutengeneza ngozi yenye tabaka lisiloisha vipele pamoja na  chunusi kwa muda mrefu.

Baada ya kuona baadhi ya sababu na athari ya ngozi kuwa mafuta,  sasa tuangalie namna ya kutunza ngozi zenye mafuta:

1. Ngozi yenye mafuta inahitajia kusafishwa vyema kwa maji ya moto na sabuni ili kuzuia vinyweleo visizibwe na mafuta. Lakini Jitahidi kuitunza vyema ngozi yako na kuisafisha vizuri. Jaribu kuosha uso mara mbili au mara tatu kwa siku. Usioshe mara nyingi kwani kufanya hivyo huufanya uso kutoa mafuta zaidi.

3. Epuka kutumia vipodozi ambavyo huifanya ngozi yako ipoteze maji au kukauka. Kwani husababisha sehemu ya juu ya ngozi inyauke, na hivyo kusababisha mafuta kuziba vinyweleo na kupelekea kutokea kwa chunusi ambazo zitaufanya mwili kuwa na mafuta.

4. Chagua kile unachosafishia kwa makini, jiepushe kutumia cream nzito nzito au vifaa vugumu wakati wa kuosha uso wako. Ni bora utumie sabuni za kawaida zisizokuwa na madawa. Unaweza kutumia lotion ya kuua bacteria au sabuni zisizo na dawa nyingi (lightly medicated), au sabuni zenye madini mbalimbali. Ni bora usioshe au kutumia lotion au michanganyiko yenye alkoholi.

5. Lakini pia unashauriwa ya kwamba hakikisha unatumia  mafuta ambayo  yametengenezwa kwa ajili ya ngozi yenye mafuta.

Endapo utayazingatia hayo mwili wako utakwenda kuwa katika hali ya ubora zaidi, na kufurahia ngozi isiyo na kasoro.

Fahamu Madhara Ya Usukaji Wa Nywele Bandia Na Uvaaji Wa Mawigi

$
0
0
Katika karne ya sasa , uvaaji wa wigi umekuwa fasheni katika sekta ya urembo na hutumika hususan na wanawake. Ingawa uvaaji wa wigi huwafanya wanawake hao kuonekana ni walimbwende zaidi.

Wigi huvaliwa zaidi na kinamama wenye asili ya Afrika au Wamarekani wa asili ya Afrika. Lakini tukiangalia moja ya chimbuko hasa la uvaaji wigi ni ubaguzi uliokuwepo wakati wa utumwa ambapo wale wenye ngozi nyeupe na nywele shombeshombe walipewa kazi za ndani na wale wasio na ngozi nyeupe  na nywele zisizo shombeshombe walifanyishwa kazi ngumu za mashambani.

Watumwa waliopelekwa barani Amerika hawakuweza kuzihudumia nywele zao kutokana na hali ngumu, na mabwenyenye waliwashusha hadhi na kuwavunja moyo kwa kuwaambia hawakuwa na nywele bali ni "manyoya".

Lakini sababu nyingine inayodhaniwa kuwaathiri wanawake wa asili ya Afrika ni fikra kuwa mwanamke mwenye nywele ndefu pengine hadi mgongoni ni mrembo zaidi. Pia siku hizi warembo na wanaoshiriki katika mashindano ya urembo hujaribu kurefusha  nywele zao ili kuwa na viwango na aina za mitindo ya ughaibuni.

Pamoja na kuwa wanawake wanajaribu kuwa warembo kwa uvaaji wa wigi, zifuatazo ni baadhi ya hasara au madhara kiafya ya uvaaji wigi na usukaji wa nywele za bandia.

1.    Uvaaji wa wigi au nywele za bandia waweza kukusababishia mzio(allergy), endapo malighafi au kemikali zilizotumika kutengeneza wigi hiyo zitasisimua mfumo wa kinga ya mwili wa mvaaji.

2.    Kupata mba ni tatizo jingine kutokana na uvaaji wigi, hii hutokana na kukosekana kwa hewa ya kutosha ya Oksijeni katika ngozi ya kichwa(scalp hypoxia) na  katika tishu za shina la nywele. Kwa hiyo kama utaamua kuvaa wigi uhakikishe imetengenezwa kwa viwango vya ubora unaotakiwa na inapitisha hewa ya kutosha ya Oksijeni.

3.    Pia waweza kunyonyoka nywele hata kama una nywele nzuri zenye afya, na kama utachagua kuvaa wigi na unataka kuepuka madhara hakikisha kuwa nywele zako ni safi, usilazimishe kuvaa wigi iliyo ndogo na yenye kubana sana, hakikisha unapata muda wa kupata hewa na nywele zako zinapakwa mafuta kuepuka ukavu wa ngozi ya kichwa na nywele kukatika .

4.    Maumivu ya kichwa ni tatizo ambalo laweza kusababishwa na uvaaji wigi au usukaji wa nywele bandia. Wigi iliyo ndogo husababisha mkandamizo kichwani na kusababisha maumivu ya kichwa ya mara kwa mara.

5.    Upotevu wa muda na fedha ni dhahiri kwa kuwa ufumaji wa nywele za bandia waweza kuchukua muda mrefu, itamlazimu mvaaji wigi kubadili kwa kununua mpya kila baada ya muda fulani au kuwa na wigi nyingi kwa ajili kubadili kulingana na fasheni.

6.    Harufu mbaya huweza kujitokeza endapo mba na jasho vitachanganyikana na hupelekea uwepo wa bakteria au fangasi na kusababisha muwasho mkali, hii yaweza kumkosesha raha mvaaji wigi na mwenye kufuma nywele za bandia hasa pale anapokuwa katika majumuiko ya kijamii.Kama utachagua kuvaa wigi hakikisha nywele zako zinasafishwa na shampoo au sabuni, zinakaushwa vizuri na kupakwa mafuta.

Endapo mwanamama atachagua kuvaa wigi,asisahau kuwa nywele zake za asili  zinahitaji matunzo,na azingatie wakati wa kununua  wigi au nywele za bandia, ahakikishe ananunua yenye ubora unaotakiwa ili kuepuka madhara ya kiafya anayoweza pata kutokana na uvaaji wigi au anapofuma nywele za bandia.

Zijue mbinu Za kujitibu chunusi Bila Kutumia Na Gharama Kubwa

$
0
0
Chunusi ni ugonjwa wa ngozi ambao hujitokeza kama viuvimbe au vipele vidogo vidogo hasa sehemu za uso, kifuani na hata mgongoni. Vipele hivi hutokea wakati vishimo vya kupitisha jasho katika ngozi vinapozibwa kwa mafuta au seli za ngozi zilizokufa au wadudu yaani bakteria.

Kwa lugha ya kidaktari chunusi huitwa Acne Vulgaris. Chunusi ndio ugonjwa wa ngozi ambao humwathiri binadamu kwa kiasi kikubwa kwa mfano nchini Marekani pekee huathiri watu zaidi ya milioni 17.

Chunusi huweza kujitokeza katika umri wowote lakini huathiri sana vijana hasa wakati wa balehe (adolescents).

Hivyo zifuatazo ni mbinu za kujitibu chunusi;

1.  Asali:
Matumizi ya asali kutibu chunusi huwezesha ngozi, iwe na afya na nyororo. Kwa sababu kwenye asali kuna virutubisho vingi vyenye kazi ya kuua vimelea (bacteria) na kuzuia uchafu na kusinyaa kwa ngozi.

Weka asali kidogo sehemu ilio athirika na iache kwa muda mrefu kadri uwezavyo. Vilevile unaweza kupaka uso mzima au hata mwili mzima ukitaka. Sababu asali inarutubisha ngozi ya mwili na kuifanya iwe na afya na mwonekano mzuri. Ukisha ridhika na muda wa asali kwenye ngozi yako unaweza kusafisha kwa kutumia maji ya vuguvugu.

2. Limao
Kata limao na kisha kwa kutumia kijiti chenye pamba kiloweke kwenye maji ya limao, sugua sehemu yenye chunusi, kisha acha pakauke, unaweza kurudia rudia kila baada ya masaa kadhaa.
Usitumie maji ya limao ya kwenye chupa (ya dukani), kwa sababu yanaweza kuwa yamewekwa kemikali zingine ili kuyahifadhi kiasi cha kuondoa ubora wa kemikali halisi za kwenye limao. Tumia limao halisi.

3. Dawa Ya Meno:
Unaweza kushangaa, lakini ushangazwi na matokeo mazuri ya meno yako kusafishika kwa dawa ya meno.Kemikali zinazotumika kuuwa Bakteria wa kwenye meno, pia zina uwezo wa kupambana na bakteria wengine. Tumia dawa ya meno isiyo na gel (non-gel) paka kwenye chunusi. Ni vizuri ukatumia usiku wakati wa kwenda kulala, ila si vibaya ukipaka hata muda wa asubuhi au mchana mradi tu uwe na muda wa kutosha wa dawa kukauka ili iweze kufanya kazi vizuri.

Namna nyingine ni kuchanganya dawa ya meno na unga wa mahindi au ngano iliyosagwa na kuwa laini sana. Unaweza kupaka na kuiacha ikauke kwa dakika tano mpaka 10. Lakini pia safisha kwa sabuni. Mchanganyiko huu unasaidia kukausha chunusi.

4. Papai:
Unaweza kushangaa, lakini matumizi ya papai yameonyesha matokeo mazuri sana katika kuondoa chunusi usoni na kusafisha sehemu zingine za mwili.
Ponda ponda kiasi kidogo cha papai na upakae sehemu yenye chunusi, kisha liache kwa muda mrefu kadri uwezavyo. Ukisha ridhika na muda unaweza kujisafisha kwa kutumia maji ya kawaida. Unaweza kurudia mara kadhaa kila siku kama unataka.

5. Mvuke:
Unaweza kutumia mvuke (Steam/vapour) kuondoa mafuta yaliozidi kwenye ngozi ya uso wako. Kwa kujifukisha. Kwa wale ambao hawana mashine wanaweza kujaza sufuria au bakuli kwa maji ya moto na kujifunika kwa taulo huku ukielekeza uso wako kwenye sufuria au bakuli lenye maji yanayotoa mvuke kwa dakika 5 mpaka 10 hivi. Unaweza kufanya hivi pamoja na njia mojawapo nilizo zitaja hapo juu.

6. Poda:
Unaweza kutumia baby powder kwa kupaka nyakati za usiku wakati wa kwenda kulala na kuiacha mpaka asubuhi.

MHIMU: Kunywa maji ya kunywa kila siku glasi 8 mpaka 10, jishughulishe na mazoezi ya viungo na ujiweke msafi kila mara.

Njia hizi za Asili zinaweza kuchukuwa muda kidogo mpaka kuona matokeo ya kuridhisha. Njia zote hizi kama hazijaleta matokeo mazuri, tafadhali muone daktari wa ngozi au nenda hospitali iliyo karibu kwa uchunguzi zaidi wa ngozi yako.

Hivi Ndivyo Vitu Hatari Vinavyoweza Kuharibu Na Kuvunja Ndoa Ya Wapendanao Katika Familia

$
0
0
WAPENZI wanagombana, ndoa zinavunjika na familia nyingi zipo kwenye msoto kwa sababu ya ubinafsi. Tunazungumza mengi lakini ukweli ni kwamba endapo kila mmoja atafanikiwa kuushinda ubinafasi, upendo utashamiri kila kona.

Ubinafsi una matawi mengi. Mtu anaposaliti, maana yake ametekwa na tamaa binafsi. Anashindwa kutambua kwamba yeye ni mpenzi wa mtu, kwa hiyo anatakiwa kulinda penzi la mwenzake. Hajui kama anachokifanya ni dhuluma ya hali ya juu.

Ukweli ni kwamba unapoanzisha uhusiano na mtu, maana yake umeamua kumchagua yeye ndiye amiliki penzi lako. Kwa hiyo ukienda kulitoa kwa mwingine, huo ni ubinafsi. Umeingiwa na umimi kwa kuona kwamba unatoa rasilimali za ndani ya mwili wako mwenyewe.

Kwa nini ukimfumania mwenzi wako panachimbika? Ni kwa sababu alichokitoa kwa mtu mwingine ni chako, kwa maana hiyo amekutendea dhuluma. Ndiyo maana ukawa na jeuri ya kupigana kwa sababu haki yako imetumika ndivyo sivyo.

Hivyo basi, usaliti ni ubinafsi. Umeingiwa na jeuri kwamba unacho ndani ya mwili wako, kwa hiyo unaweza kukitumia bila kumshirikisha mwenzi wako. Hiyo ni tabia mbaya mno. Kabla ya kusaliti, fikiria

Kama inauma, ni kwa nini umtende mwenzako? Je, umemuona yeye hana moyo? Anza leo kukemea ubinafsi. Popote pale utakapoona unachukua nafasi, upinge kwa sababu ni adui mkubwa mno kwenye mapenzi. Siku zote usiseme “nipo”, sema “tupo”.

Unapozunguka, usiwaze “upo”, unatakiwa kuwaza “mpo”. Hii itakusaidia kulinda siti ya mwenzako kila utakapokwenda. Hakikisha nafasi ya mwenzi wako haichafuliwi au kutolewa mkopo. Kama ilivyo kwenye soka, wachezaji huchezea timu nyingine kwa mkopo ndivyo na mapenzi ya sasa yalivyo.

Ni kweli mtu ana mpenzi wake lakini anavyojieleza anatoa
picha kwa muulizaji kuona kwamba aliyepo si muhimu sana. Hii husababisha muulizaji aombe kukaa na baadaye hukaribishwa. Wengi walikaribishwa kwa mkopo, mwisho wakawa wamiliki wa jumla.

Kwa nini umwambie huyo mtu kwamba anaweza kukaa, wakati unajua siti ina mmiliki wake halali? Kwa porojo za kitoto, eti mnaambiana mfanye siri. Kinachosikitisha ni kwamba ukisikia na mwenzako naye kagawa siti yako kwa mwingine, macho yatakutoka kwa hasira.

Si wakati wa kuchukia unapotendwa, bali unatakiwa uache
ubinafsi. Haliitwi penzi bila kuwepo watu wawili. Lazima uhakikishe unalinda la mwenzako ili na lako lilindwe. Somo la mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu, linafundisha kuacha ubinafsi. Mfikirie mwingine.

Kama ambavyo ubinafsi unavyowatesa wananchi pale kiongozi mwenye dhamana kiserikali anaposhindwa kutimiza majukumu yake na kuamua kushughulikia shida zake binafsi, huku akitumia rasilimali za umma, ni kirusi hatari kila upande.

Baba anapoamua kufuja fedha wakati anajifahamu anayo familia inayomtegemea, huo ni ubinafsi. Anafikiria kutumbua yeye binafsi, wakati anatakiwa kujenga msingi wa familia. Anashindwa kujua kwamba fedha anazotafuta si zake peke yake.

Kama anaona anatakiwa kutumia fedha zake peke yake, basi hapaswi kujipa mzigo wa kumiliki familia. Mtu anapokuwa baba au mama, uamuzi wake unatakiwa uwe kwa ajili ya wengi. Kumaliza mshahara kwenye kumbi za starehe ni ukatili kwa familia hususan mtoto ambaye hautakavyoumia pindi utakaposalitiwa. Usijidanganye kwamba unajimiliki mwenyewe. Wewe unamilikiwa na familia yako, kwa hiyo una deni na wajibu mkubwa kwa wale wanaohusika. Kabla ya kwenda nyumba ya kulala wageni na huyo unayemtamani, fikiria kwamba unamilikiwa.

Baba au mama, anapokwenda hoteli na mpenzi wa nje. Akakubali kuvua nguo na kufanya mapenzi. Ajitambue kuwa anachezea maisha ya watu wengine. Kuna maradhi, kwa hiyo unatakiwa uwe na afya njema ili wanaokumiliki waendelee kupata huduma yako.

Unafahamu kwamba mapenzi yanaua. Unaelewa kuwa unaposhindwa kuwa mtulivu nyumbani, unaiba muda wa familia yako. Kumbe sasa, fedha siyo zako ila ni za familia. Unaweza kupata picha kwamba viungo ni vyako lakini penzi si lako. Ukilitoa ni wizi, ni dhuluma iliyopitiliza. ZAIDI
kukuomba umlete duniani.

Sababu Kubwa za watu Kuchepuka Katika Mahusiano ya Kimapenzi ni hii

$
0
0
Niliwahi kusema ya kwamba ya kwamba “mchepuko ni dili feki” wengi wakabishana sana, na leo naomba kurudia kusema ya kwamba mchepuko ni dili feki kwa sababu michepuko ndio chanzo cha mifarakano ya ndoa zilizo nyingi ulimwenguni kote hii ni kwa mujibu wa utafiti usio rasmi lakini ndio ukweli wenyewe. Na miongoni mwa sababu inayopelekea kutokea kwa michepuko ni:

Penzi kupoa au kufa
Penzi linapopoa au hata linapokufa huwa  inaonyesha wazi kabisa dalili zote za awali. Kwenye kupoa mhusika anaweza kuanza kujihisi ndani ya moyo wake kutompenda mwenzake kama alivyokuwa akimpenda awali. Inawezekana mwenzake hajagundua kuanzia mwanzoni kwamba penzi la mpenzi wake limepoa ila kama hali ya kupoa huku itaendelea lazima itagundulika.

Baadhi ya vitu dhahiri vitakavyoweza kukufanya ufahamu kwamba penzi la mwenzako limepoa au kufa nikwamba kuna mambo ambayo uliyazoea kuyaona yakifanywa kawaida hautayaona tena. Kuna vitu vilikuwa vikifanywa pasipo kukumbushana sasa utalazimika kuviomba ili ufanyiwe, utaona kila kitu kinakuwa kigumu kumhusu mwenzako na hata uongeaji au kujibu kwake kunakuwa na walakini.

Kwenye tendo la ndoa nako maranyingi ndiko kwenye kuonyesha taa nyekundu mapema, ule ushiriki, furaha na bashasha zilizokuwapo awali mkiwa kwenye tendo hauzioni tena, tendo la ndoa linafanywa kama jukumu la kawaida na mara nyingine hata hamu ya kushiriki haipo. Hapa ndipo mmoja hukinai hiyo hali ya kulazimishana tendo la ndoa, au kupeana kwa masharti au kunyimwa au hata mmoja kupoteza hamasa ya kulifanya tendo hilo na mtu asiyekuwa na hisia naye.

Huo unakuwa mwanzo wa mmoja au wote kutoka nje ya mahusiano au ndoa. Penzi ni kama moto, ukiwashwa pasipo kuchochewa hupoa au hata kuzima kabisa. Wengi wanapoingia kwenye ndoa wanadhani mkishaoana basi mambo yanajiseti yenyewe tu, mapenzi yanajichanulia yenyewe tu, la hasha! Lazima kuwepo na jitihada za dhati za wanandoa kuhakikisha wanachochea penzi lao, kulilinda na kulipalilia ili liendelee kumea, kunawiri na kuzaaa matunda.

hivyo kupoa kwa penzi husababisha michepuko, hivyo ili uweze kuepuka jambo hili ni vyema ukaepuka visababishi vya ambavyo nimekwusha vieleza hapo awali.

Mwanafunzi wa UDSM Aliyetoweka Dar Apatikana Mkoani Iringa

$
0
0
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania , Abdul Nondo ambaye pia ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) aliyeripotiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha amepatikana akiwa hai eneo la Mafinga mkoani Iringa.

Imeelezwa kuwa, Nondo alijikuta katika eneo hilo baada ya kuzinduka kutoka katika lindi la usingizi na kuwauliza wenyeji wa eneo hilo kuwa hapo ni wapi? Wenyeji hao walimfahamisha kuwa yuko Mafinga mkoani Iringa na kisha akapelekwa katika kituo cha polisi kilichoko karibu.

Polisi walifanya mahojiano na mwanafunzi huyo ili kuweza kujua nini hasa kilitoka na baada ya hapo kupiga simu kwa ndugu zake.

Baada ya Baba mzazi, Mussa Mitumba kupata taarifa za kuonekana kwa mwanae, aliomba namba za askari aliyemfanyia mahojiano ili kujua nini kilimpata mwanae aweze kujua kama jambo jingine alilowaambia kuhusiana na kupotea kwake.

Awali kabla ya tukio hilo mwanafunzi huyo alielezea kwamba alikuwa akifuatiliwa mara kadhaa watu asiowatambua na wenye nguo za kiraia wakijitambulisha kama watu wa usalama ambao wamekuwa wakimpatia vitisho.

Timu ya Simba Yaponea Sare, Mvua Yaharibu

$
0
0
Klabu ya soka ya Simba imalazimishwa sare nyumbani na timu ya Al Masry ya Misri kwenye mchezo uliomalizika muda mfupi uliopita kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

 Mchezo huo ulikuwa na ushindani tangu dakika za mwanzo baada ya Simba kupachika bao la kuongoza dakika ya 9 kupitia kwa John Bocco kwa mkwaju wa Penalti baada ya mlinzi wa Al Masry kuunawa mpira.

Dakika ya 11 Al Masry walisawazisha kupitia kwa Ahmed aliyefunga kwa jitihada binafsi kufuatia walinzi wa Simba kufanya makosa kwenye eneo la hatari. Dakika ya 26 Al Masry waliongeza bao kupitia kwa  Abdalrauf aliyefunga kwa penalti baada ya James Kotei kuunawa mpira.

Kipindi cha pili Simba walijitahidi kushambulia ambapo dakika ya 74 mshambuliaji Okwi alifanikiwa kuipangua ngome ya Al Masry kabla ya mlinzi mmoja kuunawa na Simba kupata penalti ambayo ilipigwa na Okwi na kuisawazishia Simba.



Baada ya Okwi kufunga bao la kusawazisha, Mvua kubwa ikanyesha jijini Dar es salaam hali iliyosababisha umeme kukatika na taa kuzimika kwenye uwanja wa taifa hivyo mechi kusimama kwa muda kabla ya hali kuwa shwari na mechi kuendelea, ambapo mechi imeisha kwa sare ya 2-2.

UTANI MWINGINE HUU: Mkaliwenu Baada ya Sare ya 2-2 ya Simba SC vs Al Masry

$
0
0
Wekundu wa msimbazi Simba Jumatano ya March 7 2018 walicheza mchezo wao wa kwanza wa round ya kwanza wa michuano ya Kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya Al Masry.

Simba walikuwa wenyeji wa Al Masry katika mchezo huo uliyochezwa Taifa, Simba wakiwa nyumbani wamelazimishwa sare ya 2-2, baada ya mchezo huo kumalizika mchekeshaji Mkaliwenu amejirekodi video fupi na kuanza kuleta utani wake kuwa Simba wamesaidiwa na mvua.

Familia Yatoa Neno Kupotea Abdul Nondo

$
0
0

NA GERALD KITALIMA
Familia ya Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo, ambaye pia ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) imefunguka na kuwataka watu ambao wamemteka mwanafunzi huyo kuhakikisha anamrejesha akiwa mzima.


Baba mdogo wa Abdul Nondo amesema hayo leo Machi 7, 2018 wakati akiongea na waandishi wa habari kipindi ambacho viongozi wa mtandao huo wa wanafunzi wakitoa rai yao kwa jeshi la polisi kuhusu kupotea kwa mwenzao.

"Abdul ni kijana mdogo mno na amewahi kutuambia mara kwa mara kuhusu vitisho ambavyo amekuwa akivipata lakini hatuna nguvu kusema kuwa tutamkinga vipi. Sisi kama familia tunaomba kijana arudi akiwa mzima maana ana ndoto zake, mama yake saizi mgonjwa anaumwa pressure baba yake pia. Huyu Nondo ana ndoto zake kama mtoto pia ana ndoto zake kama mwanafunzi atatimiza vipi, sisi kama familia bado tunaendelea kulaani na tunavuta subira katika hili kwamba huenda akapatikana tunachoomba aje salama asije akarudi hana mkono akashindwa kusonga na kumsaidia mama yake" alisema baba mdogo wa Abdul

Baba mdogo wa Abdul aliendelea kusema

"Hatujui alipo lakini kama yupo kwa wale ambao tunawasikia kila siku maanake wanajulikana tunaomba arudi huyu kijana maisha yake na historia yake ni ngumu wamrudishe huyu kijana anatafuta njia hana kingine anachokitafuta pale, kuongea sana vile au kujionyesha sana vile na uwezo wa kufanya ikiwa pamoja na kusoma sana vitabu anafanya vile kutafuta kuing'arisha ndoto yake itimie hivyo wamuache aje akamilishe ndoto yake"

Wito wa Nape Nnauye Kwa Wabunge Wengine Kuhusu Uchunguzi wa Kutoweka Kwa Rais

$
0
0

Mbunge wa Mtama, Nape Nnauy ametoa wito kwa wabunge wote bila kujali itikadi za vyama vyao wamuunge mkono Mbunge wa Nzega Mjini, Hussen Bashe.

Nape ameyasema hayo leo kupitia ukurasa wake wa Twitter ambapo amesema kazi ya mbunge ni kuwakilisha wananchi ambao hawawezi kufika bunge, hivyo ni vyema wabunge wote wakamuunga mkono Bashe kwani hoja binafsi ni moja ya njia ya kupata suluhisho la matatizo ya wananchi.

“Kazi ya mbunge ni pamoja na kuwasemea wananchi ambao kwa namna moja ama nyingine hawana fursa ya kwenda wenyewe Bungeni. Tumuunge mkono Mhe. Bashe bila kujali tofauti zetu za Itikadi, Dini au Rangi! Hoja binafsi Bungeni, ni moja ya njia za kutafuta ukweli na suluhisho!”

Mbunge Hussein Bashe aliwasilisha bungeni taarifa ya kusudio la kuwasilisha hoja binafsi katika mkutano ujao wa Bunge la 11 akitaka kuundwa kwa kamati ya kibunge ili kuchunguza matukio ambayo yamekuwa yakitokea nchini na kutishia usalama wa taifa, umoja wetu na utu wa Mtanzania.

Mbunge wa CCM ataka kuchunguzwa kwa matukio yanayotishia usalama
Bashe katika barua yake alisema miongoni mwa matukio ambayo kamati hiyo maalum itachunguza ni pamoja na, kusinyaa kwa demokrasia nchini na haki za raia, kupotea, kutekwa na kuuawa kwa raia, kupigwa risasi kwa raia ndani ya nchi, matumizi mabaya ya sheria.

Yuko wapi DARASSA? HANSCANA Aeleza Alipo 'Anajua Anachokifanya'

$
0
0
Darassa yuko wapi? Mbona amekuwa kimya sana? Hanscana ana majibu. Sogeza hadi dakika ya 15:15 kumsikia akizungumzia suala hilo VIDEO;

Maboresho Katika Application ya Udaku Special, Fanya Ku Update Ama Download Hapa Kwenye Simu yako

$
0
0
Maboresho Katika Application ya Udaku Special, Fanya Ku Update Ama Ku Download HAPA Kwenye Simu yako, Tumebadili Logo pamoja na Kuifanya App iwe nyepesi zaidi bila kuchukua nafasi kubwa katika Simu yako

UPDATE HAPA

DOWNLOAD HAPA

Mwanafunzi wa UDSM Aliyetaka Mwigulu Ajiuzulu Apotea na Kupatikana..Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisii ya March 8

$
0
0
 Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisii ya March 8



Mwanafunzi wa UDSM Aliyetaka Mwigulu Ajiuzulu Apotea na Kupatikana..Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisii ya March 8

Man City Yafuzu Kinyonge Robo Fainali UEFA

$
0
0
Man City Yafuzu Kinyonge Robo Fainali UEFA
Klabu ya Manchester City Jana usiku imekubali kipigo cha goli 2-1 dhidi ya Fc Basel kwenye mchezo wa Marudiano wa klabu bingwa barani Ulaya.

Magoli ya FC Basel yamefungwa na  Elyounoussi na Lang huku goli la Man City likitupiwa na Gabriel Jesus.

Licha ya kupoteza mchezo huo Man City imefuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo kwa tofauti ya goli 5-2.

Mchezo mwingine uliochezwa Jana ni kati ya Tottenham Hotspurs na wakongwe Juventus ambapo Spurs wamekubali kipigo cha goli 2-1 nyumbani na kutupwa nje ya michuano.

Spurs walikuwa wa kwanza kuona lango la Juventus kupitia kwa Son na baadae goli hilo kusawazishwa na Higuain kabla ya kinda wa Argentina Dybala kupigilia msumari wa ushindi.

Spurs imekuwa timu ya nne kuaga michuano hiyo yenye msisimko zaidi duniani baada ya FC Porto, Basel na PSG ambao nao walitolewa kwa kukubali kipigo nyumbani kwao .


Vazi la 'Baibui' Lamponza Matonya

$
0
0
Vazi la 'Baibui' Lamponza Matonya
Nyota mkongwe katika gemu ya Bongofleva, Matonya amedai hakujua kama amevalishwa vazi la kike 'Baibui' katika video yake mpya ya 'Kiherehere' ila alichokuwa anakihitaji yeye ni kuonekana tofauti na wasanii wengine.


Matonya amefafanua hilo kupitia kipindi cha eNewz kinachorushwa na tinga namba moja kwa vijana EATV baada ya watu wengi kuanza kumfikilia ndivyo sivyo kutokana na kuonekana kuvaa vazi hilo angali yeye ni mtoto wa kiume.

"Napenda video zangu ziwe za tofauti na watu wengine wanavyofanya, navaa vitu fulani vya kipekee. Mimi niliambiwa kwamba hiki kitu ulichopiga siyo nikaona eenh sijui itakuaje, mashabiki zangu wasipate shida na mimi maana zile ni nashki kitu zimetengenezwa kwa ajili ya kazi ndio maana ma-sister zetu wanapiga jeans kali kabisa na inaweza ikawa ya 'boy friend' wake anaamua kuipiga kwaajili ya kunogesha na inamkaa vizuri", amesema Matonya.

Mbaroni kwa Kkunyoa Nywele Mwanafunzi kwa Nguvu

$
0
0
Mbaroni kwa Kkunyoa Nywele Mwanafunzi kwa Nguvu
DAVID Mwaisaka (24), mkazi wa kitongoji cha Bondeni ‘B’ wilayani Kyela mkoani Mbeya, amekamatwa na polisi kwa tuhuma za kumteka mwanafunzi wa darasa la saba Shule ya Msingi kati (12) kisha kumnyoa nywele kwa nguvu.


Jirani wa familia ya mtoto huyo, Mbatumile Kyelu mkazi wa kitongoji cha Ipyana ‘B’, alisema walimuhoji mtoto huyo na kusema Juma pili wakati akiaenda kanisani alipofika kwenye kitongoji hicho alimkuta mtu asiyemfahamu, ambaye alimuomba amchukulie sahani na kigoda amuingizie ndani.

Alisema baada ya mtoto huyo kukubali kumuingizia ndani vitu hivyo, mtuhumiwa aliingia ndani na kufunga mlango kisha kutoa kisu akimtishia kumuua.

Baada ya hapo inadaiwa alitoa wembe na kumnyoa nywele za mbele ya kichwa na nyuma kisha akamueleza aondoke pasipo kuangalia nyuma.

Neema Nakajange, mama mzazi wa mtoto huyo, alisema akiwa na jirani zake walimuona mtoto amenyolewa nywele huku akiwa amechanganyikiwa na baada ya kumhoji, alisema alifanyiwa kitendo hicho na mtuhumiwa, hivyo waliamua kumuita mwenyekiti wa kitongiji ambaye aliitaarifu Polisi.

Mwenyekiti wa kitongoji cha Ipyana ‘B’, Gibson Mwambiji, alisema alipigiwa simu na mzazi wa mtoto huyo akiweleza jinsi alivyofanyiwa, ndipo alipoenda Polisi kutoa taarifa na kupewa RB na kumuamuru ampe mwenyekiti kitongoji cha Bondeni ‘B’ ili wamkamate mtuhumiwa.

Alisema baada ya kufika walimpatia RB mwenyekiti wa kitongoji hicho na kwenda kwenye tukio siku ya Jumanne kisha mtoto kuitaja nyumba hiyo kuwa ndipo alipoonekana mtuhumiwa anayeishi hapo, hivyo kumkamata kisha kumpeleka polisi kwa uchunguzi zaidi.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Mussa Taibu, alithibitisha kuwapo na tukio hilo na kueleza kuwa Jeshi la Polisi linamshikilia mtuhumiwa kwa ajili ya upelelezi na endapo atabainika kuhusika, watamfikisha mahakamani.

Matukio ya aina hiyo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara wilayani hapa, ambapo siku kadhaa zilizopita mtu mmoja alituhumiwa kuwanyoa nywele wanafunzi akidaiwa kuzipeleka kwa waganga wa kienyeji kwa ajili ya kupata utajiri.

Jerry Muro Ampongeza Haji Manara Baada ya Sare na Al ya Misri "Hongera Swahiba si Haba"

$
0
0
Jerry Muro Ampongeza Haji Manara Baada ya Sare na Al ya Misri "Hongera Swahiba si Haba"
Baada ya kuhudhuria katika mtangange wa Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Simba Sc dhidi ya Al Masry SC, Afisa Habari wa zamani wa Young Africans, Jerry Muro, amesema kuwa si vema ushabiki ukasababisha kuondoka kwa uzalendo.

Jerry ameamua kuwa mfano wa wadau wa Yanga waliojitoa kwenda kuipa hamasa Simba katika mchezo ambao timu hizo zimeenda sare ya mabao 2-2.

Na kupitia ukurasa wake wa Instagram, Muro aliandika haya kwa uchache

 
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live




Latest Images