Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104416 articles
Browse latest View live

Mtuhumiwa Adai Gari Lake Mahakamani

0
0
Mtuhumiwa Adai Gari Lake Mahakamani
Mfuasi wa CHADEMA, Ally Rajabu anayekabiliwa na kesi ya kufanya mkusanyiko usio halali ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa anaomba arejeshewe gari lake ambalo lipo mikononi mwa polisi.

Ally Rajabu ni mshtakiwa wa 28 kati ya 31 wakiwemo watatu waliopigwa risasi na Polisi ambao ni wafuasi wa chama hicho wanaokabiliwa na kesi ya kufanya mkusanyiko usio halali maeneo ya Kinondoni Mkwajuni Dar es Salaam.

Awali kabla ya kueleza hayo, Wakili wa Serikali Aldo Mkini, amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.

Naye Wakili wa utetezi, Alex Massaba amedai kuwa wateja wake wawili ni wagonjwa na wameshindwa kufika mahakamani hapo.

Baada ya kueleza hayo, mshtakiwa wa 28, Ally Rajabu ameieleza mahakama kuwa anaomba kurudishiwa gari lake ambalo linashikiriwa na Jeshi la Polisi tangu siku ya maandamano.

Hata hivyo, Hakimu Mashauri amesema kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kuingilia masuala yaliyofanyika Polisi ambapo ameahirisha kesi hiyo hadi April 4, 2018.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Thabitha Mkude, Khaji Lukwambe, Emmanuel Kimio, Mohamed Juma, Husein Mnimbo na wenzao kwa pamoja wanadaiwa kati ya  February 16, 2018 maeneo ya Mkwajuni Kinondoni DSM walifanya mkusanyiko usio wa halali kinyume cha sheria.

Kesi Watuhumiwa Bomba la Mafuta Yashindwa Kuendelea

0
0
Kesi Watuhumiwa Bomba la Mafuta Yashindwa Kuendelea Kesi ya uhujumu uchumi kwa kutoboa bomba la mafuta inayomkabili mfanyakazi mstaafu wa Shirika la Mafuta Tanzania na Zambia (Tazama), Samwel Nyakirang'ani(63) na wenzake sita imeshindwa kuendelea.

Kesi hiyo ya namba 1 ya mwaka 2018, imeshindwa kuendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya hakimu anayesikiliza shauri hilo, Thomas Simba  kutokuwepo mahakamani hapo.

Wakili mkuu wa Serikali, Peter Maugo amedai leo Alhamisi Machi 8, 2018, mbele ya  Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wakati shauri hilo lilipokuja kwa ajili ya uamuzi wa dhamana.

Mbali na Samwel, washtakiwa wengine katika kesi hiyo  ni Nyangi Mataro( 54) mwalimu wa shule ya msingi Ufukoni na mkazi wa Kisiwani Mkajuni Kigamboni.

Wengine ni mfanyabaishara, Farijia Ahmed (39) mkazi wa soko Maziwa Kigamboni, Malaki Mathias (39) mkazi wa Magogoni, Kristomsi Angelus(25) mkazi wa Soko Maziwa,  Fundi Ujenzi Pamfili Nkoronko(40) mkazi wa Tungi Kasirati na Hunry Fredrick (38) mkazi wa Tungi Kigamboni.

Kwa pamoja washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matatu ya uhujumu uchumi kwa kujiunganishia isivyo halali bomba la mafuta ya  dizeli, kinyume cha sheria ya uhujumu uchumi.

"Mheshimiwa Hakimu, washtakiwa wote wapo hapa Mahakamani na kesi imekuja kwa ajili ya uamuzi wa dhamana dhidi ya washtakiwa na upande wa Jamhuri tupo tayari kuendelea, "amedai Maugo.

Baada ya maelezo hayo, Hakimu Shaidi amesema hakimu anayesikiliza shauri hilo hayupo na hivyo aliahirisha kesi hiyo hadi Machi 22, 2018  itakapokuja kwa ajili ya uamuzi, kama washtakiwa hao watapata dhamana au la.

Awali, Februari 15, 2018 upande wa utetezi ukiongozwa na wakili Agustine Kusalika uliwasilisha maombi ya dhamana dhidi ya washtakiwa hao katika mahakama hiyo.

Katika shtaka la kwanza, inadaiwa tarehe tofauti kati ya mwaka 2015 hadi Januari 8, 2018 katika eneo la Tungi Muungano wilayani Kigamboni washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa kujiunganishia bomba la mafuta ya dizeli lenye upana wa inchi moja kutoa katika bomba kubwa lenye upana wa inchi 24, bila kuwa na kibali kutoka Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA)

Maugo amedai katika shtaka la pili ambalo ni kuharibu miundo mbinu, inadaiwa kuwa siku na tarehe isiyofahamika kati ya mwaka 2015 hadi Januari 8, 2018 katika eneo la Tungi Muungano washtakiwa walitoboa na kuharibu bomba la mafuta ya dizel lenye upana wa inchi 24 ambalo lilikuwa likitumika kufirisha mafuta  mali ya TPA.



Katika shtaka la tatu, inadaiwa kuwa siku na tarehe isiyofahamika kati ya mwaka 2015 hadi Januari 8, 2018 katika eneo hilohilo, washtakiwa kwa pamoja walitoboa na kuharibu bomba la mafuta mazito (crude oil) lenye upana wa inchi 28 ambalo lilikuwa likitumika kusafirisha mafuta ghafi mali ya TPA.



Kwa mara ya kwanza washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo Januari 16, 2018 na kusomewa mashtaka yanayowakabili.



Hata hivyo, washtakiwa hao hawakutakiwa kusema chochote mahakamani hapo kutokana na mashtaka yanayowakabili kutokuwa na dhamana.

Serikali ya Kenya Yakubwa na Upungufu Mkubwa ya Kifedha

0
0
Serikali ya Kenya Yakubwa na Changamoto Kubwa ya Kifedha

Wizara ya fedha nchini imekiri kwa serikali inakubwa na changamoto kubwa za kifedha na haiwezi kabisa kutimiza mahitaji yake.



Ufadhili wa miradi muhimu ya serikali umeathiriwa zikiwemo serikali za kaunti amabazo bajeti zao, serikali itazipunguza kwa shilingi bilioni 15 na 17 au dola [147,913,193 na 167,634,953].

Kutoka na ukosefu huo wa fedha mashirika ya serikali yametakiwa kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na kutumia fedha zilizopo kwa njia inayostahili.

"Kila shirika ni lazima lijisatiti. Tumebuni njia ya kupunguza matumizi. Tunapunguza matumizi kwa kila sekta ili kwenda sambamba na fedha zetu," alisema waziri wa fedha Henry Rotich.

Amesema kuwa hali hii imetokana na kushindwa kwa halmashauri ya ukusanyaji ushuru nchini Kenya KRA kushindwa kutimiza malengo yake yote ya kukusanya ushuru na kipindi kirefu cha shughuli za uchaguzi.

"Tumeongea na KRA Jinsi tunaweza kukabiliana na hilo kupitia ukusanyaji wa kodi ya ndani na ya nje," Rotich aliiambia Kamati ya ya seneti.

Kulingana na Rotich serikali inakabiliwa na upungufu wa ukusanyaji ushuru wa bilioni 70 kwenye makadirio ya serikali ya mwaka 2017/2018.

Kutokana hilo, kuna uwezekano kuwa wakenya watakumbwa na nyakati ngumu kwa sababu serikali itaendelea kukopa ndani ikishindana na watu, hali ambayo itachangia biashara ndogo kuwa na ugumu wa kupata mikopo kutoka kwa benki.

Hadi Disemba mwaka 2017 deni la Kenya lilikuwa shilingi trilioni 4.55, deni ambalo limesababisha nchi kutenga asilimia 54 ya pato lake kulipa madeni.

Maseneta walitaka kujua ni kwa nini serikali za kaunti hazijapokea fedha kwa miezi minne licha ya seneti kuidhinisha kutolewa kwa fedha hizo.

Alijibu na kusema kuwa ni shilingi bilioni 134 tu zimetolewa kwa serikali za kaunti kinyume na fedha zilizokuwa zikihitajika dola bilioni 302.

VIDEO: Bashe Aibua Mapya! Asema Haogopi Kufa, Kupoteza Ubunge

0
0
Mbunge wa Jimbo la Nzega, Hussein Bashe amesema hana hofu na kifo kutokana na uamuzi wake wa kupeleka hoja binafsi bungeni ili kuundwa kwa tume maalumu ya kuchunguza mauaji dhidi ya wananchi, viongozi wa kisiasa ambao pia wamekuwa wakitekwa na kujeruhiwa.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI

Maboresho Katika Application ya Udaku Special, Fanya Ku Update Ama Download Hapa Kwenye Simu yako

0
0
Maboresho Katika Application ya Udaku Special, Fanya Ku Update Ama Ku Download HAPA Kwenye Simu yako, Tumebadili Logo pamoja na Kuifanya App iwe nyepesi zaidi bila kuchukua nafasi kubwa katika Simu yako

UPDATE HAPA

DOWNLOAD HAPA

Bashe: Ni kweli nilisema CCM wawapige CHADEMA, sababu ni hii

0
0
Mbunge wa Nzega, Hussein Bashe amekiri kusema kwa wafuasi wa CCM wawashambulia CHADEMA kweny mkutano wa kameni za Udiwani Mbweni mwezi Septemba mwaka jana.

Bashe amesema sababu ya kusema hivyo ni kuwa walikuwa wakielekea kwenye kampeni na kushambuliwa na wafuasi wa CHADEMA lakini polisi hawakuchukua hatua yoyote, na hivyo kuwaasa wana CCM wajilinde wenyewe watakaposhambuliwa na CHADEMA

Bashe amesema pia Freeman Mbowe aliwahi kutamka Siha akiwaambia wafauasi wa CHADEMA kuwajibu wafuasi wa CCM wanaowashambulia kwa kuwa polisi hawafanyi chcochote wanaposhambuliwa, ila hakuna mtu aliyezungumzi kauli yake hiyo

VIDEO:

JIBU: Wanaouliza Uamuzi Gani Ungetolewa Mechi ya Simba vs Al Masry ingevunjika Kwa Giza au Mvua

0
0

Wakati mchezo wa kombe la shirikisho Afrika ukiendelea kati ya Simba dhidi ya Al Masry uwanja wa taifa, ghafla umeme ukakatika na kukawa na giza ambalo haliruhusu mchezo kuendelea na mvua kubwa ikaanza kunyesha. Mwamuzi wa mchezo huo Thando Helpus kutoka Afrika Kusini akasimamisha mchezo na timu zikarudi vyumbani.

Baada ya muda kupita baadhi ya taa za uwanjani zikawashwa ambapo mwanga ulitosha kuruhusu mchezo kuendelea na mvua iliyokuwa ikiendelea ikapungua. Wawakilishi wa timu zote mbili wakakutana na waamuzi na kukubaliana mechi iendelee ili kumalizia dakika zilizosalia.

Sasa maswali na mijadala imekuwa mingi kuhusu uamuzi ambao ungetolewa endapo umeme usingerudi au maji yangejaa uwanjani kiasi kwamba mechi isingeweza kuendea?

Mwenyekiti wa zamani wa Simba Ismail aden Rage amefafanua kanuni za mashindano hayo zinavyoelekeza nini cha kufanya endapo mechi inavunjika katika mazingira kama yaliyotokea wakati wa mchezo wa Simba dhidi ya Al Masry.

“Kwa kawaida katika mechi kama hizi za mashindano ya kombe la shirikisho kanuni zinasema kwamba, mwamuzi atasubiri kwa muda wa dakika 45 kama muda huo utakwisha umeme ukiwa haujarudi basi atavunja mechi na itarudiwa ndani ya saa 24 kama ni mchezo wa raundi ya kwanza ‘first leg match’ lakini ikiwa ni mchezo wa raundi ya pili ‘second leg’ taa zikazimika, atasubiri tena kwa dakika 45 lakini ikitokea umeme haujarudi, timu ngeni itapewa ushindi na timu mwenyeji itakuwa imeondolewa kwenye mashindano.”

“Sasa kuna watu wanajiuliza, wameona maji mengi uwanjani yaliyotokana na mvua kubwa lakini mwamuzi akaamua mchezo uendelee, tunarudi kwenye sheria 17 za mpira wa miguu, hakuna mtu yeyote mwenye mamlaka ya kuvunja mchezo au kuutambua uwanja unafaa au haufai kwa mechi isipokuwa mwamuzi peke yake.”

“Kwa hiyo mwamuzi aliona hali ya uwanja ina ridhisha ndio maana akaacha mechi iendelee.”

Tunamchunguza Nondo Kama Kweli Alitekwa! – Jeshi la Polisi Iringa

0
0

Jeshi la Polisi Mkoani Iringa limefunguka na kuweka wazi kuwa mwanafunzi wa mwaka wa tatu UDSM, Adbul Nondo alifika kituo hicho cha polisi jana Machi 7, 2018 na kusema kuwa alitekwa na watu wasiojulikana.

RPC mkoa wa Iringa, Juma Bwire amesema kuwa jeshi la polisi limefungua jalada la uchunguzi ili kubaini ukweli kama mwanafunzi huo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania kama kweli alitekwa au la.

“Jeshi la polisi mkoa wa Iringa limefungua jalada la uchunguzi kubaini ukweli kama alikuwa ametekwa na kama alitekwa tunaaidi kwamba sisi jeshi la polisi likiwapata watuhumiwa sheria itachukua mkondo wake aidha tunaendelea kuchunguza kama ametoa taarifa za uongo kwa njia ovu kwa lengo la kutaka kuhamasisha wanafunzi wenzake ili kuleta uvunjifu wa amani nchini tutamshughulikia kama waalifu wengine”

Aidha RPC amesema kuwa mwanafunzi huyo kwa sasa anaendelea vizuri na wala hana majeraha yoyote yale kwani hajapigwa na ni mzima wa afya njema na kusema jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kujua nini kilimsibu.

Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania Abdul Nondo alipotea katika mazingira ya kutatanisha Machi 6, 2018 akiwa jijini Dar es Salaam majira ya saa tano usiku na kupatikana Mafinga Iringa Machi 7, 2018.

Kama Haupotezi Marafiki Huwezi Kukua – Shetta

0
0
Kama Haupotezi Marafiki Huwezi Kukua – Shetta
Msanii wa muziki Bongo, Shetta amefunguka kwa kutoa somo kwa wanaodhania kupoteza rafiki au marafiki basi hawezi kusonga mbele katika maisha.

Hitmaker huyo wa ‘Vumba’ ametoa somo hilo kwa katika mtandao wa kijamii wa Instagram “Kama haupotezi marafiki basi haukubali kukuwa.”

“If You’re Not losing friends… You’re Not growing up….. !! 😎”

Baadhi ya watu katika maisha wamekuwa na rundo la marafiki na wengi wao wamekuwa waoga kupoteza marafiki kwa kuamini kuwa ni jambo baya, hivyo Shetta anatukumbusha kuwa endapo unaihitaji kusonga mbele basi huna budi kukubaliakana na mambo yote ikiwemo kupunguza marafiki wasio na faida.

Rosa Ree Atoboa Siri Zitakazowawezesha Wanawake Kupata Mafanikio

0
0
Rosa Ree Atoboa Siri Zitakazowawezesha Wanawake Kupata  MafanikioKatika kuhadhimisha siku ya wanawake duniani msanii wa muziki Bongo, Rosa Ree ameeleza vitu ambavyo vitawawezesha wanawake wenye vipaji kuweza kufanikiwa.

Rapper huyo anayetamba na ngoma ‘Marathon’ ameiambia Dj Show ya Radio One kuwa wanawake wanapaswa kujiamini, kuamini wanachofanya na kuwa na bidii.

“Kwa wanawake wote wenye vipaji ni kujiamini, unatakiwa ujiamini ili uweze kukamilisha ndoto,” amesema.

“Pili ni kuwa na imani kwenye kitu ambacho unakifanya, tatu ni kutia bidii, huwezi kuwa na ndoto halafu hutii bidii ili kuweza kukamilisha malengo yako,” amesisitiza.

Hapo kesho, March 9, 2018 Rosa Ree anatarajia kuachia video ya ngoma yake inayokwenda kwa jina la Marathon ambayo amemshirikisha Bill Nass.

Bashe: Chochote Kitachonifika Amekipanga Kupeleka Hoja Binafsi ni Wajibu Wangu Kikatiba

0
0
Bashe Asimamia Msimamo Wake "Kupeleka hoja binafsi ni wajibu wangu kikatiba"
Mbunge wa Nzega Mjini (CCM),Hussein Bashe amesema amechukua hatua ya kuwasilisha hoja binafsi kwa Katibu wa Bunge kwa kuwa ni wajibu wake kikatiba.

Bashe amesema amechukua hatua hiyo kwa sababu amefanya uchunguzi kwa miezi mitano juu ya matukio ya utekaji, mauaji na watu kupotea yaliyotokea tangu mwaka 2010.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 8, 2018 huku akinukuu vifungu vya Katiba,  Bashe amesema hoja yake hiyo inawakilisha mawazo ya wananchi kuhusu matukio ya uhalifu, utekaji na watu kupokea.

Amesema katika hoja hiyo, ataambatanisha matukio ya tangu mwaka 2010 yakiwamo yaliyotokea katika uchaguzi mbalimbali kwa maelezo kuwa amefanya uchunguzi wa kutosha.

"Watanzania wanalalamika na haya ninayoyafanya yapo katika Katiba ya chama changu. Msingi wangu wa kubeba hii hoja ni katiba ya chama changu na katiba ya nchi.

"Ili CCM iendelee kuimarika lazima isimamie misingi yake. Nakwenda bungeni na hoja hii kama mbunge wa CCM. Nimechukua hatua hii sababu ni kiapo changu kwa Chama Cha Mapinduzi. Siwezi kulalamika mitaani nitatumia nafasi yangu kuwasilisha jambo hili," amesema.

Amesema mpaka sasa viongozi wa CCM waliouawa Kibiti wanafika 14, huku viongozi wengine wa upinzani nao wakipoteza maisha akiwamo aliyekuwa kiongozi wa Chadema, Alphonce Mawazo.

"Nani anafanya haya matukio mbona hakuna haki? Rais amezungumzia mambo haya likiwamo la Akwilina. Ila kauli ya Rais haizuii sisi wengine kufanya haya nifanyayo. Azory Gwanda mpaka leo hajulikani alipo," amesema.

Amesema kuwasilisha hoja hiyo ni kutimiza wajibu wake kama mbunge wa CCM,

"Nitaheshimu mawazo ya wengine kuhusu hoja yangu ili mwisho wa siku tufikie uamuzi kwa maslahi ya nchi na chama change,” amsema.

Amesema amefanya utafiti kwa zaidi ya miezi mitano na kwamba ataukabidhi utafiti huo ili kila Mtanzania ajue mambo hayo aliyoainisha katika hoja yake.

RC Amuweka Rumande Afisa Kazi Kiwanda cha Dangote

0
0
RC Amuweka Rumande  Afisa Kazi Kiwanda cha Dangote

Soma Hizi Habari Zetu Kirahisi Kupitia Application ya Simu, Bonyeza HAPA
-----
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa, amemwagiza kamanda wa polisi Mkoa wa Mtwara, Lucas Mkondya  kumuweka ndani ofisa kazi wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote, Nadhiru Omary  kwa madai ya kushindwa kutatua malalamiko ya wafanyakazi ambayo yanaelekezwa katika ofisi yake.

Byakanwa ametoa maagizo hayo leo Jumatano,  Jana Machi 7, alipofika kiwandani hapo baada ya baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda hicho kugoma kuendelea na kazi kwa muda usiojulikana kwa madai mbalimbali.

Wafanyakazi hao wanadai kunyanyaswa, kutolipwa mishahara yao kwa wakati na kufukuzwa kazi bila kuzingatia sheria.

“Tangu nimefika hapa wewe bwana umelaumiwa na umetuhumiwa kwa mambo mengi,hata vikao vyote tulivyokaa hujabadilika, kwa sababu kama ungebadilika taarifa hizi tungezijua mapema,” alisema na kuongeza kuwa:

“Sisi kama Serikali tungekaa na watumishi hawa kabla hawajaanza kuandamana, RPC huyu akapumzike kwanza, kamata huyu mtu tuondoke naye hatuwezi kuendelea na watu ambao badala ya kusikiliza malalamiko ya watu.”

“Kama unakaa sehemu ya kazi halafu chama cha wafanyakazi hakipo na ofisa kazi hauchukui hatua zozote unapoteza sifa zote, inaonekana ni tatizo la kudumu na ni tatizo sana.”

Mhasibu idara ya usafirishaji kiwandani hapo, Justie Fumbuka ameiomba Serikali kuchunguza utaratibu wa utoaji vibali vya kufanya kazi na kuishi nchini kwa kuwa umegubikwa na rushwa inayotolewa kwa watendaji wa idara ya kazi na Uhamiaji wasiokuwa waadilifu.

“Mchakato uchunguzwe kwani vibali vimekuwa vikitolewa kwa wasio na sifa na ni wanyanyasaji wa wafanyakazi na tunaiomba Serikali iwaondoe nchini mara moja,” ameeleza Fumba mbele ya mkuu wa mkoa.

Machi 3 mwaka huu, waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage alitembelea kiwandani hapo na kuzungumza na uongozi wa kiwanda hicho na baadaye alikutana na baadhi ya wafanyakazi wakiwamo madereva.

Wafanyakazi hao walimpa malalamiko yao ambapo aliahidi yatafanyiwa kazi baada ya kiwanda hicho kuanza uzalishaji Machi 15.

DPP Alalamikiwa Kuchelewesha Kesi ya Malinzi

0
0
DPP Alalamikiwa Kuchelewesha Kesi ya Malinzi
 Soma Hizi Habari Zetu Kirahisi Kupitia Application ya Simu, Bonyeza HAPA
--------
Upande wa utetezi umemlalamikia Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kuchelewesha kesi ya utakatishaji fedha inayomkabili aliyekuwa Rais wa TFF, Jamal Malinzi na wenzake.

Mbali ya Malinzi washtakiwa wengine ni Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Joas Selestine na Mhasibu wa TFF,  Nsiande Mwanga.

Akiwasilisha malalamiko hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, Wakili wa utetezi Dominician Rwegoshora amedai kuwa DPP amekuwa akipitia jalada la kesi hiyo kwa muda mrefu.

Amedai kuwa kesi hiyo imechukua muda mrefu ambapo washtakiwa wapo rumande kwa takribani miezi 8 sasa tangu walipofikishwa kwa mara ya kwanza mwezi January 2017.

Naye Wakili Nehemiah Nkoko amedai kuwa hati ya mashtaka ipo wazi ambapo inaonesha risiti na kiasi cha fedha zinazodaiwa kuibiwa hivyo wanataka kuambiwa ukweli ni kitu gani kinachokwamisha upelelezi katika kesi hiyo kukamilika.

Hakimu Mashauri baada ya kusikiliza hoja hizo ameahirisha kesi hadi March 15, 2018 kwa ajili ya kutoa uamuzi.

Katika kesi hiyo, Malinzi na wenzake wanakabiliwa na mashtaka 28 ya uhujumu uchumi ikiwamo kughushi na utakatishaji wa fedha dola za marekani 375,418.

Wanawake 527 Burundi Wameuzwa Uarabuni Kwa Kiasi Hiki cha Fedha

0
0

Ikiwa leo March 8, 2018 maadhimisho ya Siku wa Wanawake Duniani yakiendekea, kutoka nchini Burundi inaelezwa kuwa wanawake na wasichana zaidi ya 500 wa nchi hiyo wameuzwa katika biashara watu kwenda nchi za Uarabuni.

Kwa mujibu wa ripoti ya mwaka ya shirika la kutetea haki za binadamu la ONLCT nchini Burundi, wanawake na wasichana hao wanapelekwa zaidi kwenye nchi za Oman, Saudi Arabia, Kuwait na Lebanon.

Uchunguzi ambao umefanywa na shirika hilo umebaini ya kuwa wanaojihusisha na biashara hiyo ya watu huwauza kwa hadi Dola za Marekani 1000 sawa na Shilingi za Tanzania Milioni 2.4 kwa kila mwanamke au msichana mmoja.

Enyi Wanaume Ishini na Wake Zenu Kwa AKILI" La Sivyo Mwanamke Atakukoroga Maisha Yako Yote

0
0

Soma Hizi Habari Zetu Kirahisi Kupitia Application ya Simu, Bonyeza HAPA

BIBLIA ILIPOSEMA "Enyi Wanaume Ishini na wake zenu kwa AKILI" Mungu alikuwa anajua anachosema.Kama huna akili Mwanamke atakukoroga maisha yako yote na utaishia kusema "Women are so Complicated"

Wanawake huwa wanaongea vitu 'Kirahisi-rahisi tu' lakini huwa vinamaanisha 'Vitu Vigumu Ajabu'
Wanawake wanaweza kukwambia "Mi nataka Mwanaume anipende tu BHAASSS!!Ukidhani kwamba Upendo wako unatosha kwake UTAKUWA UMEFELI
Wanawake wanahitaji vitu 4 na vyote VIENDE KWA PAMOJA(Perpendicularly),vitu hivyo ni

1.HELA
2.GOOD S3X
3.CARING MAN
4.MUDA

Kuna Wanaume wanajua "Kukaza vizuri" mwanamke anatosheka,na wana hela ila WAKO BUSY...Hii factor ya wewe kuwa Busy tu itamfanya mtu mwingine mwenye Muda "Amkaze kiulaini kabisa" halafu wewe utashangaa..."Mke wangu nampa kila kitu,hela za kila kitu nampa..YES,Amekaa muda mrefu uko bize unasaka hela na adui namba 1 wa Mwanamke ni LONELINESS....

A lonely Woman can easily be trapped by anyone..hata Houseboy akimpa ATTENTION endlessly anakula mzigo

Unataka Mwanamke awe wako peke yako???Fuata kanuni ya KIBIBLIA, ishi nae kwa akili....Mpe MUDA..Mpe HELA...Mpe Kisago kitandani...Mpe CARE na ATTENTION
Sikiliza maneno ya Nabii Seth uyatendee kazi,maana TB JOSHUA hatakwambia haya KAMWE!Nimemaliza!

Source:Nabii Seth

''Rais Wafukuze kazi Makonda, Sirro, Nchemba'' BAVICHA

0
0
Baraza la Vijana Chadema Taifa ( BAVICHA) linamtaka na kumshauri Rais Magufuli kuwafukuza kazi mara moja Mwenyekiti wa baraza la usalama Jijini Dar es salaam, IGP Sirro na Waziri Mwigulu Nchema kutokana na kutochukua hatua kwa matukio yanayoendelea hapa nchini.

VIDEO:

Rafiki wa Mume Wangu Ananitaka Kimapenzi....

0
0
Jaman, hebu nisaidieni ktk hili, mimi nimeolewa na nnampenda sn mume wangu, sijawahi kumsaliti tokea nimekutana naye.

Hivi keribuni amenitambulisha kwa rafiki yake ambaye alionekana mstaarabu kumbe mnafiki. Rafiki yake huyo ameoa ila cha kushangaza ananitaka mimi wakati mi ni mke wa mtu. Amekuwa akinishawishi kwa kw mme wangu ni mtu wa safari na yeye mke wake anafanya kazi mkoani. Mi nimemgomea kabisaa.

Asa nisaidieni, je nimweleze mume wangu, ila naogopa kuharibu mahusiano yao, na vilevile naogopa siku mume wangu akijua kaam jamaa ananitokea alafu sijamwambia... Naombeni ushauri!

Soma Hizi Habari Zetu Kirahisi Kupitia Application ya Simu, Bonyeza HAPA

INASIKITISHA: Wauza Unga Wanavyonyongwa China

0
0
Inasikitisha!  kufuatia matukio mbalimbali yanayoonyesha jinsi watu wanavyonyongwa nchini China  baada ya kukutwa na makosa ya Kuuza dawa za kulevya.

kwa mujibu wa mitandao mbalimbali unapokutwa na makosa ya kujihusisha na dawa za kulevya sheria yao kuu ni kuua.

Mbali na kunyongwa kwa kutumia kitanzi, Mitandao hiyo inaonyesha kuwa kuna staili maarufu zaidi na iliyo kwenye sheria mama ambayo ni ya kunyongwa kwa kutumia sindano ya sumu na kuua kwa kutumia risasi.

VIDEO:


Soma Hizi Habari Zetu Kirahisi Kupitia Application ya Simu, Bonyeza HAPA

DJ Majizzo amkumbuka Lulu kwenye siku ya wanawake Duniani

0
0

Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya EML Francis Anthony Ciza Majey (DJ Majizzo) alhamisi hii ambayo ni siku ya Wanawake Duniani, ameitumia kumkumbuka mpenzi wake, Elizabeth Michael (Lulu) ambaye amehukumiwa miaka miwili jela baada ya kukutwa na hatia ya kumuuwa bila kukusudia, mwigizaji mwenzake, Steven Kanumba.

Majizo toka hukumu hiyo isomwe alikaa kimya bila kuzungumza chochote.

Kupitia instagram, Majey ameandika ujumbe na kupost picha yake hudu akimwambia siku moja atakuja usoma ujumbe huo.

“In life all people may probably be necessary. Very useful if everything goes right or wrong. You are very important because you can be strong in all situations. Happy Women’s Day #utakujaisomaOneday,” aliandika Majey.

Pia bosi huyo ameweka profile picha ya mrembo huyo kupitia mtandao huo.

Ticket Hii ya Daladala yaimeibua Mjadala Mkubwa

0
0

'Ticket' hii imeibua Mjadala: Ni sahihi kwa vyombo vya usafiri kuweka ‘Kauli mbiu’ kwenye risiti za malipo kwa abiria kama lilivyofanywa pichani?

Je, hapa nchini kuna taratibu za kuongoza wanaotaka kufanya hivyo?

Na kama hakuna, Kuna haja ya mamlaka kuweka taratibu?

Je, Hali hii ikiachwa iendelee hivi haiwezi kupelekea wengine kuweka nukuu hatari zaidi?
Viewing all 104416 articles
Browse latest View live




Latest Images