Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104755 articles
Browse latest View live

KAJALA AFUNGUKA BAADA YA TUHUMA ZA KUTEMBEA NA MUME WA MWASHA (8020 FASHIONS) KUZAGAA MITAANI

$
0
0
Baada ya gazeti moja la udaku linalotoka kila jana kutoa taarifa tata juu ya mwigizaji maarufu wa filamu nchini Kajala Masanja kuwa, kwa  mdada huyu sasa ameamua 'kuiingilia ndoa ya Shamim Mwasha - blogger na mmiliki wa 8020 fashion boutique, leo hii kupitia mtandao wa kijamii maarufu nchini mwanadada huyu amefunguka kuhusu tuhuma hizo na kujibu haya yafuatayo...

Nadhani namjua huyu dada siku nyingi sana kabla ata ya wengine wenu kumjua tunaheshimiana sna na atujawahi kukoseana sasa sijui nani alie anzisha habari ya mimi natembea na mume wake na sijui alifanya ivyo kwa makusudi gani naumia kila siku kwaajiri ya ujinga wa watu na hayo magazeti nikiwaambia nipeni ushahidi wa kuwa natembea na mume wa shamim sijui kama mtafanya daah sijui nisemeni nini @8020fashions mpz enjoy ndoa yako acha na wapumbavu nimevumilia nimeona bora leo niandike unajua sipendagi kuongea lkn gazeti la jana limenikwaza sana,” aliandika Kajala.

JESCA KIKUMBIA AIKANA ACCOUNT YA FACEBOOK INAYOWEKA PICHA ZAKE MBAYA AOMBA MSAADA WA KUIREPORT IFUNGWE

$
0
0
"This thing is getting worse,my friends huyo mtu anayetumia jina langu kwa fb bado unapost picha zangu anajiita same name as me and same profile picture,hiyo acc ukiangalia unajua sio yangu,maana kwa watu wanaonifahamu wanajua mimi sijawahi kusoma UDSM na hata post za zamani za hiyo acc sio zangu nna haters lakini pia naamini nina marafiki zangu wananipenda basi please naomba mnisaidie kureport hiyo acc ifungwe.
Click Hapa Chini ili Uireport to facebook:
https://www.facebook.com/Kikumbi.Jessica?hc_location=timeline" Jessica

SPIKA MAKINDA: MBUNGE ALIYE TAFUNA POSHO KWA MASLAHI YAKE BINAFSI AZIRUDISHE

$
0
0
Dodoma.Spika wa Bunge, Anne Makinda jana alipigilia msumari sakata la wabunge kuchukua posho bila kuzifanyia kazi stahiki kwa kuwaamuru wazirudishe.

Spika alitoa kauli hiyo jana asubuhi wakati akitoa mwongozo ulioombwa na Mbunge wa Mbozi Magharibi (Chadema), David Silinde akitaka ufafanuzi wa hatua ya Mbunge wa Mbozi Mashariki (CCM), Erasto Zambi kutumia Bunge kujitetea kuhusu tuhuma za kuchukua posho za safari bila kusafiri.

Alisema Zambi ni mbunge ,pia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mbeya na Kamishna wa Bunge anayefahamu taratibu za safari zinazoeleza kuwa kuchukua fedha bila kwenda safari ni makosa.

Silinde wakati akiomba mwongozo huo alimtuhumu Zambi kuwa alichukua kiasi cha Sh13 milioni za posho ya safari ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) na nyingine kwa ajili ya safari ya shughuli za michezo lakini hakusafiri.

“Mtu anapozungumza kwa kutumia Bunge lako kujitetea kwa kukiuka taratibu, inaruhusiwa?” alihoji Silinde, ambaye pia ni Waziri kivuli wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge.

Kabla ya Silinde kusimama na kuomba mwongozo, Zambi alikuwa amepewa fursa na Spika ya kuchangia taarifa za Kamati za Bunge za Nishati na Madini na Miundombinu zilizowasilishwa juzi.

“Jana (juzi) kulitokea maneno maneno fulani hapa bungeni. Alisimama ndugu Silinde akasema Zambi kala hela hakusafiri,” alisema lakini kabla hajamalizia kuzungumza Spika alimkatiza... “Naomba hilo uliache unapoteza muda na haliwasaidii wananchi, changia mambo mengine muhimu,” alisema Spika Makinda huku wabunge wengi ndani ya Ukumbi wa Bunge wakipiga makofi.

Hata hivyo, Zambi aliendelea kusisitiza kuwa taswira inayokwenda kwa wananchi ni mbaya na wameanza kumpigia simu kuwa ameiba fedha na kusema hilo ni jambo baya analostahili kulisemea.

Alisema utaratibu uko wazi kama hujasafiri unarudisha fedha na kusema... “Ningekuwa kiongozi wa ajabu sana kama ningekwenda Dubai na Uingereza na kutokwenda ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kutoka chama kinachotawala.”

Baada ya kueleza hayo, Spika alisimama na kusema: “Waheshimiwa wabunge nimesema kama mlichukua pesa bila safari, mnarudisha si basi…. Wote kabisa ninawajua na ninalifanyia kazi. Wote waliochukua pesa warudishe ndiyo utaratibu wa Serikali na ndivyo inavyotakiwa. Wote watarudisha.”

Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Chiku Abwao aliwataka wabunge kutumia kikao cha kupeana taarifa cha wabunge wote kuzungumza kama kuna tatizo lolote badala ya kuumbuana ndani ya Bunge.

Moto wa posho hizo ulikolea juzi pale Mbunge wa Iramba Magharibi (CCM), Mwigulu Nchemba alipoomba mwongozo wa Spika akitaka kujua hatua ya mbunge aliyechukua fedha na kwenda safari binafsi. Nchemba alisoma ujumbe wa simu uliokuwa ukionyesha Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani, Freeman Mbowe alikatisha safari ya Mbunge wa Viti maalumu (Chadema), Joyce Mukya.

AMANDA AANIKA CHANZO CHA USAGAJI KWA MASTAA

$
0
0
Na Mwandishi Wetu
MSANII wa filamu, Tamrina Poshi ‘Amanda’ amefungukia sababu za baadhi ya mastaa kujiingiza kwenye tabia chafu ya usagaji akidai kuwa, kutendwa na wanaume ndiyo chanzo cha yote.

Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Amanda alisema maudhi ambayo baadhi ya mastaa wamekuwa wakiyapata kutoka kwa wapenzi wao waliotokea kuwapenda ndiyo husababisha baadhi yao kuona suluhisho ni kuhamia kwenye usagaji.

“Wasanii wanajiingiza huko sababu wanaumizwa na wanaume, wanadhani usagaji ni raha, wanaona hii ni njia sahii ya kujituliza,” alidai Amanda huku akikwepa kujibu swali la kama naye yumo kwenye kundi la wasagaji ama laa.
GPL

WABUNGE WAZIDI KUMKALIA KOONI WAZIRI MKUU PINDA...FOMU ZA KUMG'OA UWAZIRI ZAINGIZWA BUNGENI

$
0
0
Hali  bado  ni  tete  bungeni.....Wabunge  wanawataka Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamisi Kagasheki, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha kujiuzulu kutokana na maovu yaliyofanywa wakati wa Operesheni Tokomeza wakati wakijadili ripoti iliyotolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli.

Wakati wa bunge la jioni  likianza, Mbunge wa Kasulu Mjini (NCCR-Mageuzi), Moses Machali ameonekana  akiingia na fomu bungeni   kwa ajili ya kukusanya saini za wabunge za kutokuwa na imani na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda..

BREAKING NEWS:WAZIRI WA MALI ASILI NA UTALII HAMISI KAGASHEKI AJIUZULU BUNGENI HIVI PUNDE

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamisi Kagasheki, amejiuzulu bungeni hivi punde baada ya kutakiwa na wabunge awajibike kwa vitendo viovu vilivyofanywa na wanausalama wakati wa Operesheni Tokomeza!

NASSARI AFICHUA MIPANGO YA KUMBAMBIKIZIA GODBLESS LEMA KESI YA MABOMU ARUSHA

$
0
0
Mbunge wa Arumeru Mashariki, Bw. Joshua Nassari (CHADEMA), amesema Mbunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya chama hicho, Bw. Godbless Lema yupo katika hatari ya kubambikiwa kesi.

Alisema ipo mipango inayosukwa ili kumhusisha Bw. Lema na milipuko ya mabomu katika mikutano ya chama hicho, eneo la Soweto na ule wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti, mkoani humo.

Bw. Nassari aliyasema hayo bungeni Mjini Dodoma jana katika kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda na kuongeza kuwa ni wajibu wa Serikali kusimamia haki badala ya kuwabambikia kesi wanasiasa kwa lengo la kudhoofisha vyama vya upinzani.




Alisema kwa mara kadhaa, amewahi kutembelea magereza na kujionea vijana wengi wakiwa ndani bila hatia na kutolea mfano wa kijana ambaye alikamatwa na kuwekwa mahabusu akihusishwa na ulipuaji wa bomu Soweto na Olasiti.

"Huyu kijana yupo tayari kutoa ushahidi...alikamatwa Arusha na kupelekwa Mwanza, baadaye alihamishiwa mkoani Shinyanga ambako aliminywa sehemu zake za siri na kuvunjwa mguu ili amtaje Lema kuwa alihusika na matukio hayo," alisema.

Bw. Nassari alimtaka Bw. Pinda kutoa ufafanuzi juu ya Serikali kuwabambikizia watu kesi ili kuvidhoofisha vyama vya upinzani badala ya kusimamia upatikanaji wa haki kwa raia wake.

Akijibu swali hilo, Bw. Pinda alisema si nia ya Serikali kutaka kuwabambikizia watu kesi ambapo mambo yaliyotokea Soweto na Olasiti si madogo na yeye hana taarifa za suala hilo.

Alisema Serikali inaendelea na uchunguzi ili kuwabaini watu waliohusika na milipuko hiyo na

kama kuna Mbunge anayejua kila kitu ni vyema akatoa taarifa hizo ili ziweze kupelekwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

"Kwa kweli siwezi kujibu swali hilo...Mheshimiwa Nassari anajua kila kitu na mimi sina taarifa lakini si nia ya Serikali kuwabambikizia watu kesi ni vyema uandike maelezo yako kwa maandishi ili niwape wahusika ambao ni Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi wachunguze," alisema.

Kwa upande wake, Bw. Lema alisema amekuwa na wasiwasi juu ya suala hilo kwani yeye hausiki na jambo hilo na mhusika yupo ambaye alilazimishwa ili amtaje yeye.

MGANGA WA DIAMOND ATABIRI DIAMOND KUFULIA KIMUZIKI NA KIFEDHA HIVI KARIBUNI

$
0
0
Mtu mmoja anayedai kuwa mganga aliyemtoa mkali wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz ameibuka tena na kueleza kuwa Diamond Platinumz tayari ameanza kushuka kimuziki kama alivyosema awali.
Mtu huyo anayejitambulisha kwa jina la Dr. Yahya Michael ameuambia mtandao wa mamuafrica kuwa kile alichokisema mwanzo kuwa Diamond Platinumz atashuka kimuziki na kurudi pale alipokuwa kimeanza kutokea ingawa watu wengi hawaoni.
“Diamond alikuwa anapiga show kwa milioni 10 lakini sasa hivi hapewi hata show ya milioni 7. Nilizungumza kushuka sio kupanda na nashukuru kwa sababu rekodi ninayo. Nimeongea kushuka sio kupanda, wale walioko nyuma yake hivi sasa ndio wanaonekana kuongoza. Hata katika mambo yenu ya kumi bora za Tanzania yeye hayumo katika mbili.” Amesema Dr. Yahaya

“Sijawahi kumuona mtu anaepanda anaambiwa ameiba nyimbo, sijawahi kuona mtu anaepanda anashindwa na yule ambaye alikuwa anamshinda mwaka jana. Na wala sijawahi kumuona mtu anaeambiwa anapanda halafu anapigwa mawe na watu waliokuwa wanataka wamuone kwa kiingilio kikubwa.” Ameeleza.

“ Kwa sababu Diamond wa mwaka 2010,2011,2012 ni Diamond aliyekuwa anapiga show Mlimani City sehemu alipozaliwa Dar es Salaam kwa kiingilio cha shilingi 50,000, siku tatu kabla ya tukio tiketi zimekwisha. Kwa hiyo Diamond wa hivi sasa ni yule ambaye anapiga show Tabora sehemu ambayo hajawahi kuonekana, kwa kiingilio cha shilingi 5,000 na watu hawaingii na bado walioingia wanampiga mayai viza na mawe.” Ametoa mchanganuo wake.
Mtu huyo akafika mbali na kuapa, “ amini, sitakufa kabla haki hii haijatendeka, naapa…kwa heshima ya mwenyezi Mungu aliyeniumba. Anasema pigania chako ali hali hata ukifa ili mradi ulikuwa unapigania chako.”
Hata hivyo, Naseeb Abdul aka Diamond aliwahi kumkana Dr. Yahya na kueleza kuwa hamfahamu na hajawahi kumuona.



ACHENI KUVAMIA FANI NA KUFANYA MAMBO YA AJABU KUTUHARIBIA FANI-KING MAJUTO

$
0
0
Kwa mujibu wa tovuti ya mwananchi, mwigizaji nguli Amri Athumani (King Majuto),amewajia juu wanaovamia fani ya vichekesho kwa kufanya vitendo alivyosema vinatia kinyaa kuviangalia.

Alisema kwamba baadhi wa wachekeshaji wanamchukiza kwa kufanya mambo ya aibu na kujidhalilisha wenyewe, badala ya kuchekesha akiwataka wajipange kabla kuvamia fani hiyo.

“Wapo vijana wanafanya kitu ukiangalia unafurahi na kwa sisi wachekeshaji wa siku nyingi unajifunza kitu, lakini hawa wavamizi ukiangalia unaweza kutapika. Sipendi na wananiudhi. Kama vipi wajipange upya,”alisema Majuto bila kuwataja akieleza kuwa anaowakusudia wanajijua.

Aliongeza kuwa kila kazi inahitaji umakini ili iweze kuvutia na kupata soko, akilalamika kwamba wachekeshaji wanaofanya kazi hiyo ili mradi wapate fedha ya siku wanawaharibia wenzao wanaotegemea kazi hiyo kwa maisha yao yote.

Alibainisha kuwa binafsi amefanya kazi ya uchekeshaji kwa zaidi ya miaka 55 na ndiyo inayompa heshima maishani mwake.

PENZI LA DIAMOND NA PENNY LASEMEKANA BASI TENA...WEMA ATAJWA KUWA CHANZO

$
0
0
NDIYO habari ya ‘mujini’ kwa sasa, kwamba staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond Platnumz’ na mwandani wake, mtangazaji wa kituo cha runinga cha DTV, Penniel Mungilwa ‘Penny’ wamemwagana,

KAMA UTANI, WEMA ATAJWA
Kwa sharti la kutotajwa mahali popote, ‘mtonyaji’ wetu ambaye ni mtu wa karibu wa wawili hao aliliambia gazeti hili kuwa chanzo cha Diamond na Penny kuingia kwenye listi ya ‘zilipendwa’ kilianza kama utani.
Awali ilidaiwa kuwa kila mmoja amekuwa akijiona mwenye thamani mbele ya mwenzake huku Wema Sepetu naye akidaiwa kuwa chanzo.

“Hakuna penzi tena kati yao, wameachana na kila mmoja yuko kivyake.
“Walianza kama utani, unajua wale kila mmoja anajiona yuko juu kuliko mwenzake, lakini kitendo cha Diamond kuripotiwa kutoka na wanawake tofauti mara kwa mara hasa Wema, kimemchosha Penny ndiyo maana ameamua kujiweka pembeni kuepuka msongamano.
“Kupangwa kama mafungu ya nyanya inahusu?” alihoji ‘kikulacho’ huyo ambaye ni rafiki wa Diamond. 
RISASI MZIGONI
Baada ya kutojiridhisha moja kwa moja na taarifa za awali kutoka kwa rafiki huyo, timu ya gazeti hili kwa kuwatumia ‘wahangaikaji’ wake maalum, iliingia mzigoni kupeleleza ukweli juu ya tetesi hizo.
Watu kadhaa walio chini ya Wasafi Classic Baby (WCB) ambayo rais wake ni Diamond walihojiwa ambapo majibu yalikuwa yaleyale kwamba, kwa sasa Diamond na Penny imebaki stori! 
 SHAKA ILIPOANZIA
Wakati timu yetu ikiendelea na uchunguzi wake makini juu ya uvumi huo, hivi karibuni Diamond alionekana ‘singo’ kwenye pati ya kusherehekea siku ya kuzaliwa ya ‘dada wa mjini’, Halima Haroun ‘ Halima Kimwana’ ambayo aliiandaa Diamond.
Minong’ono ya kuhoji kutoonekana kwa Penny ilisikika ndani ya Ukumbi wa Business Park, Kijitonyama jijini Dar ilikofanyikia pati hiyo iliyojaa vitendo vya ufuska.
“Haiwezekani leo rais (Diamond) akajiachia peke yake bila Penny. Si kawaida ya Diamond.
“Kwa vyovyote watakuwa wameshamwagana kwa sababu kwenye pati zote huwa wanakuwa pamoja tangu walipoanza uhusiano wa kimapenzi,” alisikika mmoja wa waalikwa katika sherehe hiyo.
Katika tukio hilo, Penny alipigiwa simu na paparazi wetu na kujibu kwa kifupi: “Naumwa. Halafu si lazima nije kwani kila mtu ana ratiba zake.”

PENNY KIZIMBANI TENA
Baada ya kukamilisha udadisi huo kupitia kwa watu wao wa karibu, gazeti hili lilianza na Penny kwa kumuuliza undani juu ya habari hiyo lakini alionekana kuwa ‘mzito’ kwa kutoingia ndani kulizungumzia sakata hilo huku akiahidi kulifungukia muda wowote kuanzia sasa.
“Kwa sasa sina cha kuzungumza juu ya hilo, nitalizungumzia muda wowote tena si siku nyingi zijazo, lakini si leo, tafadhali sana,” alijibu Penny kwa kifupi na sauti ya chini iliyojaa uchovu.
Paparazi: “Hebu nisaidie, mko wote au hamko wote?”
Penny: “Nimesema sitoweza kusema lolote kwa leo, subirini.”


DIAMOND KIMYA
Alipotafutwa Diamond kwa njia ya simu yake ya kiganjani, hakupokea licha ya kupigiwa mara kadhaa kwa namba zake zote. Akatumiwa meseji yenye maelezo yote, hakujibu.

MAMA DIAMOND
Ili kujiridhisha na madai hayo, waandishi wetu walimtafuta mama mzazi wa Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ ambaye alisema hajui na hana taarifa hizo.

NDUGU WA KARIBU SANA
Baada ya mama Diamond, paparazi wetu alimpigia simu ndugu wa karibu sana na Diamond, sikiliza:
Paparazi: “Kumbe Diamond na Penny wamemwagana we huniambii. Sasa wifi yako mpya ni nani?”
Ndugu: “Aka! Sikwambii. Kwanza mi nipo mbali, sipo Dar.

WADAU WANAJUA
Haikuishia hapo, timu yetu ilizungumza na wadau mbalimbali ambao walionesha kusikitika huku baadhi yao wakisema walitabiri tangu awali.
“Duh! Penny ameachia ngazi mwenyewe. Sisi tulijua hawawezi kufika mbali, maana penzi lenyewe lilikuwa na mbwembwe nyingi,” alisema mwanamke mmoja anayejua kila kitu.

TUJIKUMBUSHE
Siku za hivi karibuni Diamond alifanya mahojiano kwa njia ya mtandao mmoja wa kijamii ambapo moja kati ya maswali aliyoulizwa ni pamoja na mpango wa kuoa ambapo alisema kuwa hana mpango huo kwa sasa na hatarajii kumuoa yeyote kati ya wanawake wanaotajwa kwa sana midomoni mwa watu (akiwemo Penny).
Wema alipigiwa simu juzi, lakini simu yake ilikuwa ikiita ‘weee’ mpaka inakatika, inaita ‘weee’ mpaka inakatika.

Source: GPL

RAIS KIKWETE AWAPIGA CHINI MAWAZIRI WANNE YUMO NCHIMBI, VUAI, MATHAYO NA KAGASHEKI

$
0
0
Rais Jakaya Kikwete leo ametengua uteuzi wa mawaziri wanne kufuatia shutuma nzito dhidi yao katika sakata la Operesheni Tokomeza Ujangili. 

Mawaziri waliopoteza ajira zao usiku huu ni pamoja na Khamis Kagasheki (Maliasili na Utalii), David Mathayo (Mifugo na Uvuvi), Emmanuel Nchimbi (Mambo ya Ndani) na Shamsi Vuai Nahodha (Ulinzi na JKT).

Akizungumza Bungeni Dodoma usiku huu, Waziri Mkuu Mizengo Pinda alikiri kulikuwa na matatizo makubwa katika usimamizi wa zoezi hilo.

“Tulifanya operesheni kwa nia nzuri,” alisema Waziri Mkuu Pinda. “Tatizo ni namna operesheni hiyo ilivyotekelezwa.”
Katika mdahalo uliogusa nyoyo za wabunge na wachambuzi mbalimbali wa siasa leo, wabunge waliueleza umma jinsi ambavyo Operesheni hiyo ilitumika kutesa, kunyanyasa na kuua raia wasio na hatia na kuwadhulumu mali zao.

OKWI "NIPANGENI MECHI YA SIMBA NA YANGA NIWAONESHE SIMBA MIMI NI NANI"

$
0
0
 Uwanja wa Bora uliopo Kijitonyama jana ‘ulifurika’ mashabiki wa Yanga waliokuwa na shauku ya kumwona mshambuliaji wao mpya Emmanuel Okwi akifanya mazoezi na timu hiyo.

Okwi alitua nchini juzi Alhamisi tayari kuitumikia klabu hiyo ya Mtaa wa Twiga na Jangwani baada ya kutokea sintofahamu kuhusu uhamisho wake wa kutoka SC Villa kuja Yanga.

Si bajaji, pikipiki achilia mbali magari yaliyofurika kwenye uwanja huo huku Okwi mwenyewe akisema, “Nimefurahi sana na mapokezi niliyopewa na viongozi na mashabiki wa Yanga, nitafurahi kama nitacheza mechi ya kesho,” alisema Okwi ambaye jana alifanya mazoezi kwa mara ya kwanza na Yanga.

Akisisitiza umuhimu wa yeye kucheza alisema, “Mrisho Ngassa nimecheza naye Simba, Hamis Kiiza tunacheza naye timu ya taifa (Uganda), hakuna wasiwasi, mimi nikipangwa nao tutacheza kwa uelewano sana pale mbele  na nitafunga.”

Alisema kwa jumla anaijua Yanga vizuri na anajua uchezaji wa wachezaji wake wengi, hivyo anaweza kucheza vizuri katika mfumo wa timu hiyo.

“Unaweza kuitwa timu ya taifa, siku mbili kabla ya mechi na wakati mwingine unakuta wachezaji wengi hujawahi kucheza nao kabisa, lakini mnafanya mazoezi siku moja mnaelewana na mnacheza vizuri,” alisema Okwi.

Kwa upande wa kocha wa timu hiyo Ernie Brandts alisema Okwi ni mwepesi na anakasi na anajua kutengeneza nafasi za kufunga mabao na atampanga katika mchezo wa leo wa Nani Mtani Jembe dhidi ya mahasimu wao.

Jezi za Yanga zenye jina la Okwi zimetapakaa na zimekuwa zikigombewa kama njugu na mashabiki wa klabu hiyo ambayo mara zote walisikika wakiimba Okwi... Okwi...

Na kabla ya kuanza mazoezi, Brandts alimtambulisha, Okwi kwa wachezaji wenzake na benchi la ufundi.

WABUNGE WA CCM WAMGOMEA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA

$
0
0
Wabunge wa CCM jana mchana walimgomea Mwenyekiti wa Kamati ya Wabunge (Party Cocas) ya chama hicho, Mizengo Pinda na kushinikiza mawaziri watatu ambao wizara zao zimetajwa kushindwa kusimamia vyema Operesheni Tokomeza Ujangili wajiuzulu.

Habari kutoka ndani ya kikao hicho zinaeleza kuwa mawaziri walioshinikizwa kujiuzulu wenyewe ni pamoja na Balozi Khamisi Kagasheki ambaye ni Waziri wa Maliasili na Utalii,  Dk Emmanuel Nchimbi (Waziri wa Mambo ya Ndani)  na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha.

Kikao hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Pius Msekwa bungeni jana kiliitishwa na Pinda ambaye pia ni Waziri Mkuu kwa lengo lililoelezwa ni kuwapoza wabunge.

Chanzo cha habari kutoka katika kikao hicho kilisema kuwa wabunge hao walitaka mawaziri hao kujiuzulu wenyewe ili kukinusuru chama  mbele ya wananchi.

“Tumemtaka Waziri Mkuu akakae na wenzake na kutuambia kama wanajiuzulu au la na kutupa jibu kabla ya kuahirishwa kwa Bunge, mtasikia wenyewe baadaye ndani ya Bunge,”kilisema chanzo hicho.

Hata hivyo, baada ya kukamilika kwa kikao hicho na wabunge kurejea bungeni, Pinda hakurejea bungeni, badala yake ilidaiwa kwamba alikuwa na kikao katika ofisi zake zilizopo bungeni.

Hadi  saa 11.25 alasiri  wakati kikao cha Bunge kikiendelea Waziri Mkuu alikuwa hajarejea bungeni, huku ikielezwa kwamba katika kikao alichokuwepo hakikuwahusisha mawaziri wanne waliokuwa katika shinikizo la kujiuzulu.

MKE AMFUMANIA BWANA AKE GUEST HOUSE..AMPA KICHAPO CHA MBWA KIMADA

$
0
0
DUNIA ina mambo jamani! Mfanyabiashara wa madini aliyefahamika kwa jina moja la Jimmy amejikuta katika wakati mgumu baada ya kufumaniwa na mkewe akiwa na kimada gesti. 
Tukio hilo lililofunga mtaa kwa kujaza wambea kibao, lilitokea hivi karibuni ndani ya gesti hiyo (jina tunalo) Kinondoni jijini Dar es salaam ambapo mke wa mfanyabiashara huyo (jina halikupatikana mara moja), alimnasa mumewe  akijiandaa kuvunja amri ya sita ya Muumba.

Mke wa mfanyaiashara (kulia) baada ya kumfumania kimada akiwa na mumewe gesti maeneo ya Kinondoni, jijini Dar.
Wadakuzi waliokuwa eneo la balaa walitonya kuwa, siku hiyo ya tukio, Jimmy ambaye ni mkazi wa jijini Arusha, alifika Dar kibiashara na baadaye alimsaka kimada huyo wa siku nyingi na kwenda kujirusha naye bila kujua mkewe alishatonywa juu ya usaliti wake.
Awali chanzo makini kinachojua nini maana ya habari kiliwatonya mapaparazi wetu mara baada ya kupata mchongo wa fumanizi kutokea Sinza ya Kumekucha lililoandaliwa na mke wa Jimmy.

“Nyie njooni tu hapa Sinza-Kumekucha ndipo mkewe alipotonywa na dereva wa mumewe kuwa anaibiwa na kimada. Kuna gesti moja ipo ndani kidogo upande wa kushoto kama unaelekea Shekilango,” kilisema chanzo.
Timu ya mapaparazi ilifika katika gesti hiyo lakini bahati mbaya waliambiwa kuwa, Jimmy na kimada huyo walihamisha kiwanja cha starehe na kwenda Kinondoni.

Mapaparazi walipofika katika gesti hiyo ya Kinondoni, walimkuta mke wa Jimmy hivyo wakaambatana naye pamoja na askari polisi wawili kwa ajili ya kwenda kufumania.
Jimmy kabla ya kuingia gesti inadaiwa alijipumzisha katika grosari iliyo karibu na Mango Garden Bar, baadaye akaenda kwenye gesti hiyo ya jirani bila kujua mkewe alikuwa akitua mguu kila pale yeye aliponyanyua, akazama ndani ya gesti hiyo na kuanza kujiandaa kwa zinaa.
Mke wa Jimmy hakuwa mbali, baada ya kujiridhisha mumewe amezama chumbani, dakika kadhaa na yeye alitokea na kugonga mlango wa chumba hicho kufuatia kutonywa na mhudumu mmoja wa gesti hiyo.
Jimmy alikutwa tayari ameshavua nguo zote na kubakiwa na ‘boksa’ huku kimada naye akiwa na ‘kufuli’ pekee.
Kilichofuata hapo ni kipigo, mke wa Jimmy alianza kumtembezea kipigo yule kimada. Mapaparazi walivamia na kutandika picha za timbwili ambapo Jimmy alifanikiwa kupenya mlangoni na kukimbia bila kujali nguo nyingine.
Kutokana na kelele za timbwili hilo, majirani wa eneo hilo walifika kuhoji kulikoni ambapo mfumaniaji huyo alitoboa siri kwamba amekuwa akimfuatilia mumewe kwa siku nyingi baada ya kuambiwa ana kimada Dar.
“Huyo malaya akome kutembea na waume za watu. Nimekuwa nikimfuatilia mume wangu kwa muda mrefu. Nimetoka Arusha mpaka Dar kwa ajili yake. Kweli za mwizi ni arobaini, leo nimewanasa,” alisema mwanamke huyo huku akiondoka eneo la tukio na kutokomea kusikojulikana.
Wakati pakichimbika, kimada huyo alisikika akimlaumu Jimmy kwamba amemuingiza kwenye mkenge akijua mkewe ni mdodosaji wa mambo na anaweza kufika Dar madai ambayo hayakuwa na wa kuyajibu.
Taarifa zaidi zilidai kuwa ndugu mmoja wa mwanamke huyo ndiye aliyekuwa na mchoro mzima wa Jimmy na hivyo ‘kuuza’ kwa mwanamke huyo.

Credit: GPL

DR.SLAA:WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA NAE ANAPASWA KUJIUZULU

$
0
0
Katibu mkuu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA),Dr.Wilbroad Slaa amesema serikali nzima na Baraza la Mawaziri linapaswa kujiuzulu na kwamba kitendo cha kujiuzuru kwa mawaziri wanne tu hakitoshi na badala yake amesema Pinda kama "kiranja" mkuu anapaswa kuwajibika.

Dr.Slaa ametoa kauli hiyo wakati akihutubia mkutano wa hadhara huko mkoani Tabora.

CHANZO:ITV

BABY MADAHA KUZINDUA FILAMU YA "THE GAL BLADDER" LEO NDANI YA UKUMBI WA AKEMI HAPA DAR

$
0
0
Mwanadada anayefanya mambo mengi sana kwenye muziki na filamu Baby Joseph Madaha anatarajiwa kufanya uzinduzi wa filamu yake mpya ya The Gal Bladder hapo kesho kwenye ukumbi wa mgahawa wa Akemi jijini Dar es Salaam.

Akizungumza alipotembelea ofisi za Bongo movies leo mchana, baby Madaha amesema kuwa uzinduzi huu utahusisha waalikwa tu na sio wa viingilio kama ilivyozoeleka kwenye uzinduzi wa vitu mbalimbali hapa nchini.

Katika uzinduzi huu baby Madaha pia anatarajiwa kuzindua nyimbo zake nyingine mbili mpya alizozifanya chini ya label ya Cand and Candy ya jijini Nairobi Kenya ambazo zitajumlisha orodha ya nyimbo nne alizoziachia katika kipindi cha miezi mitatu.

BOB JUNIOR"NDIO NI NGUMU SIKUWA NA FURAHI...SITAOA TENA..UBACHELOR RAHA

$
0
0
Rais wa Masharobaro, Bob Junior amesema hakuwa na furaha kwenye ndoa yake na ndio maana ameachana na mke wake.

Muimbaji na mtayarishaji huyo wa muziki aliiambia tovuti ya Times FM kuwa ugumu wa ndoa umemfanya asifikirie tena kuoa maishani.

“I’m single, sitaoa tena…mimi niko single na sitaoa tena. Kwa sababu nimeona ugumu wa ndoa na wepesi wa kuwa bachelor. Kwa hiyo nimeamua kuwa bachelor na siwezi kuoa tena, sioi tena jamani I’m single. No more kuoa Bob Junior,” aliiambia tovuti huyo.

“Unajua unapokuwa kwenye mahusiano ya boyfriend na girlfriend, hamna ile ‘uko wapi sasa hivi, rudi haraka nyumbani’, umeenda kwenye show ukirudi mara kanuna.”

Bob Junior aliiambia tovuti hiyo kuwa ndoa yake ilikuwa ikirudisha nyuma maendeleo ya kazi yake kwa kuwa katika siku saba za wiki ni siku mbili tu anakuwa na furaha, na kwa kuwa kazi yake inategemea ubunifu na utulivu asingeweza kufanya kazi vizuri.

Alisema mkewe alikuwa na wivu kiasi cha kuiingilia hadi ukurasa wake wa Facebook na kuwatukana watu waliokuwa wanachat naye
Bongo5

ALI KIBA "HAITAWAHI KUTOKA KAMWE MIMI KUFANYA COLLABO NA DIAMOND"

$
0
0
Unategemea kusikia collabo ya Diamond Platnumz, Ali Kiba na Ommy Dimpoz? Kama una ndoto hiyo, basi iondoe kabisa kwasababu kwa mujibu wa Ali Kiba, kuwepo kwa collabo hiyo ni sawa na kudeki bahari, haiwezekani.

Diamond na Ali Kiba ni paka na panya na kamwe mafahari hawa wawili hawawezi kukaa kwenye zizi moja.

RAPPER WITNESS SASA NI MGANGA, ANATIBU WATU KWA TIBA LISHE

$
0
0

Msanii wa zamani wa kundi la Wakilisha, Witness Mwaijaga, amesema pamoja na kufanya hip hop kwa sasa ni mfanyabiashara na mtaalam wa tiba asili zinazotumia vyakula vyenye virutubisho

Akizungumza na kipindi cha The Cruise cha East Africa Radio, Witness alitoa ufafanuzi wa jinsi ulaji mbovu ulivyo na madhara kwa afya.

“Siku hizi watu wengi wamekuwa wanakula vyakula vyenye cholesterol,kwa mfano mtu mwingine anaweza akawa na kansa au inaanza au mwingine anaweza akawa ana high blood pressure,hajui tatizo ni nini. Lakini mimi ninaweza nikakuelezea natural ukaelewa hiyo hali natural. Kwasababu tu kula wengine mazoezi,at the same time. Wakati mwingine kuna tatizo lingine ambalo tunalo hapa obesity, suala la ‘unene’ huku kwetu ndio kabisa kwasababu hata mafuta tunayotumia na vyakula vingi viko namna hiyo, watu wanakula nyama nyama sana na vyakula vingi vyenye cholesterol,” alisema rapper huyo.
Kwa upande wa muziki, rapper huyo amesema amemaliza kurekodi video mbili, moja inaitwa ‘Nadata Nawe’ na nyingine inaitwa ‘Think About’ ambazo zote zitatoka mwakani.

DR.MWAKYEMBE AMCHANA LIVE MBUNGE VITI MAALUM CHADEMA

$
0
0
Juzi tulisikia mipasho ya Mbunge wa Viti Maaluma CHADEMA, Mariamu Msabaha, kuhusiana na matatizo ya Air Tanzania.
Tatizo kubwa la Mama Msabaha ni pengine hakujua anachokiongelea.

Lakini jana ilikuwa zamu ya Dr Harrison Mwakyembe, Waziri wa Uchukuzi, kurudisha mapigo yanayostahili.

Mwakyembe kwanza kaanza na kumtaka Mariamu Msabaha kutosema jambo ambalo halifahamu au hana uhakika nalo.
Mwakyembe alikuwa akijibu hoja ya mama Msabaha kuwa ndege ya Air Tanzania iendayo Burundi, ilikuwa "inavuja".

Mwakyembe alijibu kuwa ili ndege iruhusiwe kuruka angani ni lazima kupata vibali mbali mbali kutoka mashirika mbali mbali likiwemo la kiamataifa la usafiri wa anga (ICAO) na lazima ikidhi viwango.


Mwakyembe alisema....
"Mheshimiwa Naibu Spika inashangaza kuona mbunge anakuja hapa na kudiriki kusema bila woga eti ndege inavuja,tena kimipasho tu 'ndege inavuja', hiyo inashangaza.


Mwakyembe aliendeea kumnanga mbunge huyo kuwa maneno hayo angeyasema Mheshimiwa Nd Omari Nundu, mbunge ambaye ana utaalam wa hali ya juu katika masuala ya ndege, basi asigeshangaa.

Lakini kwa hao wabunge ambao entry point zao bungeni ni kujua kusoma na kuandika tu ( Du F4F????) , anamsgangaa huyu Mariam Msabaha.

Mwakyembe aliendelea , endapo ndege hiyo ingekuwa inavuja isi ngeweza kuruka na kamwe (tatizo hilo lingekuwepo) isingeruhusiwa kuruka.

"Siyo mtu anainuka na kusema ndege hiyo inavuja huku hajui chochote juu ya usafiri wa anga, tena anajaribu kuwakataza hata watu kutumia ndege hiyo hapa Bungenini jambo la kusikitisha"

Du, hapo kuna mtu kaingia mlango si wake!!!
Viewing all 104755 articles
Browse latest View live




Latest Images