Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live

Ajali Nyingine ya Gari la Polisi na Lori

0
0

ARUSHA: Askari watatu wa Jeshi la Polisi wamejeruhiwa vibaya katika ajali iliyohusisha gari la Polisi na lori usiku wa kuamkia leo, Machi 8 katika barabara ya Tengeru-Arusha

Askari hao wamepata ajali hiyo majira ya saa 9 alfajiri wakati gari la Polisi lilipokuwa likisindikiza gari la Benki Kuu kupeleka fedha mkoni Tanga

Ajali hiyo iliwajeruhi askari waliokuwa katika gari hilo na dereva kuvunjika miguu yote na kuumia vibaya kichwani

Jeshi la Polisi linamsaka dereva wa lori ambaye alikimbia baada ya ajali hiyo

Mambo ya Kufanya uwe na Umbo Dogo la Kuvutia

0
0
Unaweza kujiuliza, hivi inawezekanaje kuwa na umbo dogo la aina hii? Ukweli ni kwamba inawezekana, lakini inahitaji kazi ya ziada kufikia kwenye lengo hilo.


Unalifahamu umbile la sifuri au saizi zero?
Kwa wale wanaojali maumbo ya kupendeza saizi zero linatafsiriwa ni kuwa na kiuno kisichozidi inchi 23, nyonga 32 na kifua 31.  Kikubwa unachotakiwa kuzingatia ni mazoezi na ulaji wako, kwa kuwa mwangalifu katika kiasi cha kalori unachoingiza mwilini kila siku.

Unatakiwa kuwa mwadilifu katika uchaguaji wako wa chakula, haimaanishi ukae na njaa. Inawezekana ikawa ni vigumu kuelewa makala haya.


Kinachosisitizwa katika mpango huu, ni kuwa waangalifu katika upangiliaji wa vyakula. Aina hii ya mpangilio wa ulaji inafahamika zaidi kitaalamu kama ‘crash diet’ Kula kiasi cha kalori 400- 500 kwa siku. Lakini unatakiwa kufanya mazoezi angalau kwa saa mbili kwa siku, ili kupunguza mara mbili ya kiasi cha mafuta uliyokula katika siku hiyo.

Kunywa maji kwa wingi:
Kwa kunywa kiasi kikubwa cha maji itakusaidia kurahisisha umeng’enyaji wa chakula mwilini. Ni vyema mwili wako ukawa na maji ya kutosha ikiwa umeingia kwenye mpango huu wa ulaji Kula mboga za kijani: Zina Vitamini, protini na virutubisho vingine kwa wingi ambavyo ni muhimu kwa afya. Kama ilivyoainisha awali, utaratibu huu hauhamasishi kukaa na njaa, bali kula vyakula vilivyo bora kiafya.


Kula vyakula visivyokobolewa:
Mara nyingi vyakula vya aina hii, huwa na virutubisho muhimu na vinavyohitajika katika ustawi wa mwili.


Punguza wanga katika mlo wako:
Badala yake unaweza kula protini na kuingiza vyakula kama mayai na samaki kwenye mlo wako.

Epuka kula vyakula vya mtaani:
Vyakula kama chips, mihogo ya kukaanga na jamii yake vinachangia kwa kiasi kikubwa kuongeza uzito wa mwili na pia hulifanya zoezi la umeng’enywaji wa chakula tumboni kuwa gumu.

Kula supu za mbogamboga;
Supu kama ya kabichi licha ya kujaza tumbo, husaidia katika kurahisisha mfumo wa umeng’enyaji chakula tumboni.

Kula saladi na matunda kwa wingi:
Hii itasaidia kukuweka sawa kiafya.


Jizuie kula vyakula vyenye sukari nyingi na hata vile vya mtaani unavyohisi vinaweza kukwamisha mpango wako wa kupungua.


Lakini pamoja na yote jipe mazoezi ya kutosha kama kukimbia, kuruka kamba au mazoezi ya kupunguza tumbo na maziwa.

Utata Mwanafunzi Aliyetekwa UDSM, Habari Ziliizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya March 9

‘Mjomba Husein’ Mwanamke wa Kwanza Kuchimba Tanzanite Akijifanya Mwanaume

0
0
Jana March 8, 2018 ilikuwa ni Siku ya Wanawake Duniani AyoTV imempata Pili Husein au jina maarufu “Mjomba Husein”ambae ni mwanamke wa kwanza kuchimba madini ya Tanzanite katika mgodi wa Mirerani uliopo mkoani Manyara nakujifanya mwanaume kwa zaidi ya miaka 15 ili asitolewe kwenye mgodi huo kwa kuwa walikuwa hawaruhusiwi wanawake.

AyoTV na millardayo.com imempata ‘Mjomba Husein’ amesema pamoja na changamoto alizokutana nazo ameweza kuwasomesha watoto wa ndugu zake zaidi ya 32 kwa gharama zake ambapo mmoja wapo ameongoza kwenye masomo nakupata daraja la kwanza mwaka 2016 nchini Tanzania

Pamoja na hayo amempongeza Makamu wa Rais Samia Suluh Hassan kwa kumpa tuzo yakuwa mchimbaji namba moja mwanamke.

UFAFANUZI: Kauli ya Mbunge Elibariki Kingu ”KUTEKWA NI JAMBO LA KAWAIDA”

0
0
Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu amefafanua kuhusu kauli iliyosambaa mtandaoni ikidai kuwa amesema watu kutekwa na kuuawa ni jambo la kawaida na kushauri bunge kutounda tume kuchunguza kwani itazua taharuki na Serikali haijashindwa kusimamia usalama wa nchi.

“Sijasema kutekwa kwa watu ni matukio ya kawaida, mimi nimesema matukio ya kihalifu yapo Duniani kote, tusilipake taifa matope ili lionekane limekuwa katika hali tete, hatuwezi kuanza kwenda kujadili hali ya usalama kwa matukio haya,” -Kingu

VIDEO

Ray Kigosi Amwagia Misifa Kibao Mrembo Chuchu Hans...

0
0
LEJENDARI wa sinema za Kibongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ amemwaga sifa nyingi kwa mzazi mwenziye, Chuchu Hans, kwa kusema kuwa ni mama bora anayejua kumlea vziuri mtoto wao, Jaden.

 Akizungumza na gazeti hili, Ray alisema kuwa, Chuchu amekuwa ni mstari wa mbele katika kuhakikisha mtoto wao anakuwa na afya njema na pia anakuwa kwenye mazingira mazuri siku zote.
“Unajua angekuwa mwanamke mwingine, angeona mtoto anamzibia vitu vingi hasa kwenye upande wa kuendelea kucheza filamu, lakini aliweka pembeni lengo likawa moja tu, kumuangalia mtoto tu,” alisema Ray.

Muigizaji huyo aliongeza kuwa, anamuombea sana kwa Mungu mzazi mwenziye huyo aendelee kuwa na moyo huo wa malezi bora kwa mwanaye kwani mama ndiye hubeba kwa asilimia kubwa jukumu la malezi.

Stori: Imelda Mtema, Amani

Chid Benz Auza Mjengo wao wa Ilala..Sasa Anaishi Vichochoroni

0
0
Bwana wee al-manusula wazichape na Duwe Santana baada ya Enewz kutimba mtaani anapoishi sasa Chid Benz. Kwani tulipofanikiwa kuingia kwenye nyumba anayoishi sasa tulimuuliza mzee mbona huku uchochoroni sana na tunasikia Flet ile ya ilala umeuza??? Unaambiwa palikua hapatoshi hapo...

VIDEO:

Black Pass Binti Kiziwi Afunguka Alipotoka...Adai "EBITOKE Ndio Nani ? Siwezi Fanya Nae"

0
0
Black Pass aka Binti Kiziwi Katika Bifu zito na Ebitoke: 

Black Pass "EBITOKE Ndio Nani ? Siwezi Fanya Nae

VIDEO:

Diamond Platnumz Aweka Wazi Mipango yake ya Ndoa

0
0
Msanii wa muziki mwenye mafanikio makubwa hapa nchini, Naseeb Abdul ‘Diamond Platinumz’ ameweka wazi mipango yake ya ndoa huku akiomba baraka kutoka kwa mama yake mzazi.

Diamond ameandika katika ukurasa wake wa instagram akimtakia mama yake heri ya siku ya wanawake ambpo amemshukuru kwa malezi aliyompa tangu akiwa mtoto mdogo.

“Happy Women’s day Mama na wanawake wote Ulimwenguni… Nashkuru sana kwa kunizaa na kunilea…Wewe ni Mboni na Nguzo ya Maisha yangu mama…Licha ya shida na Mateso uliyoyapata kwenye kunizaa na kunilea, lakini hata sasa ambapo ulitakiwa walau Upumzike nimekuwa nikikukosea kwa kukuingiza hata kwenye Matatizo Yasiyokuhusu…Wanakutukana, wanakukebehi na kukutupia kila neno lililo baya, yote kwa sababu yangu mimi, lakini sikuzote umekuwa mwenye kunisamehe, kunipenda na Kunithamini…..Nakupenda sana Mama, Na nisameh kwa yote nilokukosea… Inshaalah, Mwenyez Mungu anibariki Mwaka huu Mwanao nifanikishe Ndoa yangu na kukupa Furaha ya Milele ambayo siku zote umekuwa Ukiitaka….. @mama_dangote

Njia za Asili za Kuondoa Rangi Kwenye Viwiko vya Mkono na Magotini

0
0
Unaweza kuwa na ngozi laini sana kwenye uso wako au mwilini kwako lakini kuna baadhi ya maeneo ni tofauti hasa viwiko vua mikono na magoti.

Kwingine kote kunaweza kuwa laini lakini sehemu hizi mbili unaweza kuzikuta na weusi, ngozi haiko sawa na hata kuwa na vipele au unakuta pamebabuka, ngozi kutokatoka, kimsingi ngozi ya kiwiko na goti huwa siyo laini.

kutokana na ugumu wa sehemu hizo, baadhi ya watu huona hata aibu kuvaa nguo zinazoonesha kiwiko au magoti, lakini kama na wewe ni muhanga, basi leo tunakupa vidokezo vya tiba ambavyo unavipata jikoni kwako ili kukusaidia kuifanya ngozi ya kiwiko na goti kuwa nzuri.

Angalizo; sehemu hizi zina ukosefu wa tezi za mafuta kitu kinachofanya ziwe kavu haraka na hadi kuwa nyeusi kuliko kawaida. Mara nyingi wengi wetu hizi sehemu huwa hatuzijali, tunaziacha zenyewe unakuta lile tabaka la ngzi linakufa na haliondolewi na kufanya pawe pagumu na pakavu.

Vile vile mkusanyiko wa seli zilizokufa kwenye sehemu hizi husababisha ngozi kutokuwa katika hali nzuri, na hilo tabaka la ngozi inatakiwa kuondoloewa mara kwa mara ili kuihuisha ngozi upya.

Cha kufanya basi ili kutoa huo ugumu na weusi wa magoti na viwiko vya mikono, unaeza kufanya vifuatavyo.

Skrabu ya Sukari; skrabu inasaidia kuondoa na kubandua seli zilizokufa ambazo zinasaidia seli mpya kutengenezwa na kufanya ngozi kuonekana nzuri na laini. Changanya kijiko kimoja cha asali na sukari ya kawaida, pakaa/sugulia kwenye goti lako au viwiko vya mikono kwa mwendo wa duara, sukari itasaidia kutoa ngozi ambayo haitakiwi, kisha osha na majisafi, unatakiwa kufanya hivi kwa wiki mara moja.

Limao na juisi ya viazi ulaya; viazi ulaya na limao vina viambata vya blichi, ambazo inazifanya ziwe chaguo la wengi kwenye mambo ya urembo. kata limao nusu sugulia kwenye kiwiko na magoti au kata pia kipande cha kiazi mviringo na ufanye hivyohivyo  na limao, hii itasaidia kufanya ngozi hii iwe nyepesi zaidi. Kisha tumia asali ambayo itasaidia kufanya ngozi kwa unyevunyevu.

Mafuta ya kukandia; mafuta yanaingia kwenye ngozi na kukusaidia kuifanya ngozi kuwa na unyevunyevu wa asili, sababu hizi sehemu hazina tezi za mafuta kwa kuzikanda na mafuta mara kwa mara na mafuta ya zeituni, lozi au nazi. Mafuta ya nazi husaidia pia kung’arisha, hivyo kanda na aina mojawapo ya mafuta na yaache yaingie kwenye ngozi. Tumia dodoki au jiwe lile laini; ukioga unaweza tumia jiwe lile laini; ukioga waweza tumia jiwe laini au dodoki kusugua sehemu za magoti na viwiko vya mikono, usisugue kwa nguvu, taratibu itasaidia kubandua ngozi iliyokufa, siyo lazima kufanya kila siku unaweza  pata vidonda na ukiwa unasugua fanya kwa mwendo wa mduara.

Kuifanya ngozi nyevunyevu; chukua mafuta yako paka kwenye ngozi ili kusaidia peaendelee kuwa laini, baada ya hizo tiba zote, ukishafanya hivyo hakikisha huachi magoti yako na viwiko bila kupaka mafuta hii itasaidia pasiwe pakavu na mbaya au kakamavu.

Wachina Wagombea Wowowo la Aunty Lulu

0
0
KATIKA hali ya kustajabisha, Wachina ambao hawakuweza kufahamika majina yao, wamenaswa wakipagawa na kugombea kumshika kalio, mtangazaji maarufu Bongo, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ nchini China.

 Mrembo huyo amekwenda nchini humo hivi karibuni ambapo tukio hilo lilitokea alipohudhuria shoo ya mwanamuziki wa Tanzania anayeishi nchini humo aitwaye Zitha, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Shenzhen.
Kwenye video nilyoipata, ilimuonesha Aunty Lulu akigombewa na Wachina hao huku wengine wakionekana kumrekodi video kupitia simu zao ambapo wengi walionekana kuvutiwa zaidi na kalio kubwa la Aunty Lulu.

“Unajua wameshangazwa na kalio langu huku wanawake wao hawana makalio hivi, niliona wanacheza nikainuka kucheza nao hilo lilikuwa ni kosa kwangu walipagawa ile mbaya,” alisema Aunty Lulu.
Wachina hao walikuwa wakimgombea huku wengine wakiomba kupiga naye picha na wakati walipokuwa wakipiga naye picha, kila mmoja alikuwa akimgusa kalio.

Soma Nafasi za Ajira zilizotangazwa Leo Ijumaa

Nicole Franklin Afunguka 'Nilimpenda MC Pili Pili Kwa Ushamba Wake Huo Lakini Alinivunja Moyo sana Najuta"

0
0
Nimejaribu kumsikiliza huyu dada Nicole Franklin Miss Shinyanga 2014 kuhusu mahusiano yake na MC Pilipili au Emmanuely yalivyovunjika lakini hayaeleweki maana inaonekana huyu dada alimpenda sana MC Pilipili na alikuwa na uhakika naye kimaisha lakini MC Pilipili alipotea na kumkatisha tamaa kabisa huyu dada.

Kweli mapenzi huwafanya wanadamu kubadilika kabisa na kubadili hata mitazamo yao kimaisha.

VIDEO:

Dawa Bora za Nguvu za Kiume na Kukosa Hamu ya Tendo la Ndoa

0
0

DAWA BORA ZA NGUVU ZA KIUME NA KUKOSA HAMU YA TENDO LA NDOA
Baada ya utafiti wa muda mrefu juu ya matatinzo ya upungufu wa nguvu za kiume na ukosaji wa hamu ya tendo la ndoa ama kushindwa kurundia tendo kwa haraka Sasa inakuletea suluhisho juu ya matatizo haya kwa kutumia dawa za FULL POWER

Full Power dawa asili yenye vidonge inayotibu tatizo la upungufu au ukosefu wa nguvu za kiume dawa hii inamchanganyiko wa kutosha kuzalisha vichocheo vingi vya hernone za gestro gen zikiwemo vitamin b6 na b1 vitamin e pamoja na madini aina ya zinc

Itakufanya kuwa na nguvu na mzunguko mzuri wa damu na kuongeza hamu na uwezo wakufanya tendo la ndoa zaidi hatua nne au zaidi na kuchelewa kufika kileleni zaidi ya dakika 20/30 ZAT 50

Inarundisha maumbile ya uume yaani kurefusha na kunenepesha nchi 3/7 na upana cm 3/4 standard.kiafya haijalishi umri wako hata kwa wazee ukitumia maumbile yatabaki kuwa hivyo siku zote pia anatibu matatizo mengine kama presha kisukari ngiri chango la tumbo kujaa gesi kutopata choo vizuri minguu kuwaka moto matatizo ya uzazi bawasili na magonjwa ya zinaa kama kisonono na kaswende

Tunapatikana Dar es Salaam  na mikoan wasiliana na DR Oshinda no 0755505099 au 0714126118  Karibuni kwa hunduma bora

Yanga Kama Ishatoka ni Vyema Ikajipanga kwa Msimu Ujao- Mzee Akilimali

0
0
Yanga Kama Ishatoka ni Vyema Ikajipanga kwa Msimu Ujao- Mzee Akilimali
BAADA ya Yanga kufungwa huku Simba ikiambulia sare katika michuano ya kimataifa, Katibu wa Baraza la Wazee la Yanga, Ibrahim Akilimali amefunguka kuwa ni wazi timu hizo zimejiweka katika mazingira magumu ya kusonga mbele.

Yanga ilifungwa 2-1 na Township Rollers ya Botswana katika Ligi ya Mabingwa Afrika huku Simba ikitoka 2-2 dhidi ya Al Masry ya Misri katika Kombe la Shirikisho, michezo yote ikichezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Akilimali alisema timu zetu kimataifa msimu huu hazikuwa na maandalizi, hivyo siyo rahisi kuweza kusonga mbele.

“Ukweli ni kwamba, timu zetu kwenye michuano ya kimataifa msimu huu zimeshindwa, ni vyema wakajipanga kwa ajili ya michuano hii mwakani na siyo kwa sasa.

“Sababu wote wamekutana na timu ambazo zina uwezo na zimejiandaa vyema ndiyo maana zikashindwa kupata matokeo hapa nyumbani na siyo rahisi wao kwenda kupata matokeo huko ugenini ni ngumu sana.
“Wanatakiwa kujipanga upya na kuangalia wapi wamekosea ili kuweza kurudi kwenye mstari lakini kusema watasonga mbele kwenye michuano hii siyo rahisi kabisa,” alisema Akilimali.

RC Makonda Atangaza Vita na Wanaume Wasiotunza Watoto Wao

0
0
RC Makonda Atangaza Vita na Wanaume Wasiotunza Watoto Wao
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ametangaza vita na wanaume wanaowapa ujauzito wanawake na kuwatelekeza kwa kuandaa jopo la Wanasheria watakaoanza kuchukuwa hatua za kisheria kwa wanaume hao kuanzia Aprili 09 mwaka huu kwenye ofisi yake.


Taarifa hiyo imetolea na ofisi ya Mkuu wa Mkoa ambapo imesema kwamba kitendo cha Wanaume kukwepa majukumu ya malezi na matunzo kwa mtoto imepelekea pia baadhi yao kutoa ujauzito, kutupa watoto na wengine kupeleka wajukuu kulelewa na wazee na kusababisha mzigo kwa familia.

Aidha RC Makonda amesema kuwa wataangalia pia utaratibu wa kufanya marekebisho sheria ya gharama za matunzo ya mtoto kwakuwa ni ndogo na haiendani na hali ya sasa.

RC Makonda amesema lengo lake ni kuleta ukombozi kwa kinamama ili kuhakikisha wakihitaji fedha ya matumizi wanapatiwa na sio kupigwa, kusimangwa, kutukanwa na kudhalilishwa.

Hata hivyo Makonda amesema katika zoezi hilo lengo lake ni kuleta ukombozi kwa kinamama ili kuhakikisha wakihitaji fedha ya matumizi wanapatiwa na sio kupigwa, kusimangwa, kutukanwa na kudhalilishwa.

Pamoja na hayo Kiongozi huyo wa Mkoa wa Dar es salaam amesena kwamba  ameamua kutoa muda wa mwezi mmoja ili kama kuna baba kwenye huu Mkoa huo anajijua ametelekeza mtoto na hatoi fedha za matunzo akamtafute na kuanza kutoa matunzo kwakuwa itakapofika Aprili 09  atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Ajari Yaua Wanne Mbeya 20 Wajeruhiwa Vibaya

0
0
Ajari Yaua Wanne Mbeya 20 Wajeruhiwa Vibaya
Watu wanne wamefariki dunia na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya Super Rojas kugongana na lori jana Machi 8, 2018 katika eneo la Igawa wilayani ya Mbarali mkoani Mbeya.

Ajali hiyo imetokea katika barabara inayounganisha mikoa ya Mbeya na Iringa, baada ya basi hilo lenye namba za usajili T 170 DKS lililokuwa likitoka Mbeya kwenda Njombe kugongana na lori lenye namba za usajili T 838 DRE aina ya Scania lililokuwa limebeba kontena.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo,  chanzo cha ajali ni dereva wa basi aliyekuwa akijaribu kulikwepa tawi la mti lililokuwa limeegeshwa barabarani kama ishara ya kuonyesha kuwepo kwa gari bovu mbele yake.

Mnyeti Apingana na Waziri Kigwangalla Atengua Agizo Alilotoa kwa Wananchi

0
0
Mnyeti Apingana na Waziri Kigwangalla Atengua Agizo Alilotoa kwa  Wananchi
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti ametengua agizo la Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla aliyewapa miezi tisa wananchi wa Kijiji cha Kimotorok kuondoka katika maeneo wanayoishi wakidaiwa kuvamia Hifadhi ya Tarangire wilayani Simanjiro.

Akizungumza na wanakijiji hao juzi, Mnyeti alisema hakuna atakayekwenda kuwafukuza na kama hilo lipo, yeye ndiye atawaambia wanafukuzwa au la, hivyo wawe na amani.

Mnyeti alisema ofisi ya mkoa inajiandaa kutuma wataalamu kwenda kupima eneo hilo ili kutatua mgogoro.

Februari 25, Waziri Kigwangalla aliwapa wananchi wa kijiji hicho, vitongoji vya Massas na Loon’benek miezi tisa wawe wamehama kwa kuwa wamevamia eneo la Hifadhi ya Tarangire.

Baadaye alitoa ufafanuzi akisema kabla ya kuondoka, Serikali itawalipa fidia na watatafutiwa maeneo mengine ikiwa ni pamoja na kujengewa zahanati nje ya hifadhi kutokana na iliyokuwapo kuwa ndani.

Dk Kigwangalla alipotafutwa jana kuzungumzia kauli ya Mnyeti alisema, “Sijapata taarifa rasmi kwa maandishi. Siwezi kufanyia kazi taarifa za kwenye mitandao. Nitasubiri barua kama itakuja. Hata hivyo, sina hakika kama mkuu wa mkoa anaweza kusema hivyo.”

Mkuu wa mkoa Mnyeti alitoa kauli baada ya msafara wake kusimamishwa na wananchi wa Kimotorok alipokuwa akienda kwenye mkutano wa kuwapokea wanachama zaidi ya 3,000 wa CCM kutoka vyama vingine.

Wananchi wa Kimotorok

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Saringo ole Meeki alimuomba mkuu wa mkoa kuwasimamia katika kupata haki ya ardhi yao wanayotaka kuporwa na watu wa hifadhi bila hata kuwashirikisha kwa lolote juu ya jambo wanalolifanya ikiwamo kuweka alama (bikoni) ndani ya ardhi ya kijiji hicho ambacho kina hatimiliki tangu miaka ya 1970.

“Bikoni zimewekwa hapa hivi karibuni chini ya ulinzi mkali tukiwa hata hatuelewi na baadhi yetu waliouliza walijibiwa ‘hatuna nafasi ya kuongea na mtu yeyote’ lakini baada ya kufuatilia kwa undani ndipo tukagundua wanasema ni mchoro wa eneo la hifadhi,” alisema Meeki.

Alisema, “Mheshimiwa jambo hili limefanywa kinyume cha utaratibu kwa kuwa mbali na kutoshirikishwa kwenye uwekaji wa bikoni lakini pia hatukuulizwa juu ya upitishwaji michoro ya makubaliano ya mipaka ya kijiji na hifadhi kwa kuwa alama mpya zimesogezwa na zimemega vitongoji viwili.”

Mkazi mwingine, Baby Noah alisema mbali ya alama kuwekwa kwenye maeneo yao, agizo la waziri wa maliasili la kuwapa miezi tisa kuhama limewaathiri.

“Mkuu tusaidie kutatua mgogoro huu maana hapa ni kwetu na hatujui pa kwenda, hivyo hatutakubali kuhama maana tuko hapa kwa miaka mingi na kijiji kilipata hati miaka ya 1970 lakini mwaka huu tunakuja kuwekewa bikoni eti ni maeneo ya hifadhi kitu ambacho hakiingii akilini,” alisema.

Majibu ya Mnyeti

Akijibu hoja za wananchi, Mnyeti aliomba apewe siku 10 awe amefanya utaratibu wa kupeleka wataalamu kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambao wako katikati ya wananchi na hifadhi hivyo hawatapendelea upande wowote.

“Sasa chagueni kamati ndogo au Serikali ya kijiji watakaokwenda na wataalamu kukagua alama za mipaka. Watapitia mipaka yote kujua ramani maana hifadhi nayo ina umuhimu wake, hivyo muwe tayari kukubaliana na majibu yatakayosomwa na mtaalamu baada ya ukaguzi maana hata ofisi ya ardhi mkoa haijui utekelezaji wa uwekaji alama hizo,” alisema Mnyeti.

Alisema, “Lakini pia inawezekana mko sahihi maana tunajua hawa watu wa hifadhi mara nyingi wao wanataka kusogeza tu eneo, kila siku wanataka eneo liongezeke, leo anaweza akaja akaishia hapa kesho akija anaishia hapa, sasa tunaleta mtu ambaye yuko katikati ya hifadhi na wananchi na atapima kuleta ukweli.”

Wanaume Wamekuwa Waoga Wameanza Kurudi Nyuma- Halima Mdee

0
0
Wanaume Wamekuwa Waoga Wameanza Krudi Nyuma- Halima Mdee
Wanaume na vijana ni waoga na wameanza kurudi nyuma katika harakati za kisiasa.Hivyo ndivyo anavyodai Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), Halima Mdee.

Mdee aliyasema hayo jana katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani akidai wanaume wamekuwa waoga na wameanza kurudi nyuma.

Maadhimisho hayo yamefanyika nchi nzima kwa wanawake katika sekta mbalimbali kutoa misaada kwa wenzao waliolazwa katika hospitali mbalimbali nchini, kufanya usafi, kuwatembelea wazee na yatima.

Katika maadhimisho hayo, mawaziri mbalimbali wanawake walishiriki makongamano na kutoa kauli za kuhimiza usawa wa kijinsia na maendeleo kwa wanawake.

Akizungumza jijini Mbeya katika maadhimisho hayo, Mdee ambaye pia ni Mbunge wa Kawe aliwataka wanawake kusimama na kuonyesha uwezo wao katika kupigania demokrasia kwa vitendo.

“Kwa sasa vijana wanarudi nyuma, hivyo wanawake ndio kimbilio la mabadiliko ya kweli katika nchi, tusimame kidete tusife moyo, tupambane kwa vitendo dhidi ya dhuluma ya kidemokrasi inayotoweka katika nchi yetu,” alisema Mdee.

Alisema wengi wanaohama vyama vya upinzani na kujiunga na CCM, wakiwamo wabunge na madiwani ni wanaume na kusema kuwa hizo ni dalili za woga.

Alisema hakuna kitu chochote kinachohitajika kwa sasa katika Taifa kama Katiba mpya hivyo kuwataka Watanzania bila kujali itikadi, ukabila, dini ama rangi zao wapaze sauti zao kuidai akisema ndiyo itakayokuwa suluhisho.

Wanawake MCL wamliza mke wa Azory Gwanda

Katika kuiadhimisha siku hiyo, wafanyakazi wanawake wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), walimtoa machozi Anna Pinoni, mke wa Azory Gwanda walipomtembelea nyumbani kwake Kibiti mkoani Pwani.

Azory, ambaye alitekwa na watu wasiojulikana Novemba 21, 2017 katika mji wa Kibiti alikokuwa anaishi na kufanya kazi hadi jana alikuwa hajapatikana.

Pamoja na mambo mengine, wanawake hao wa MCL walimpa bima za afya kwa ajili ya matibabu ya watoto wake wawili, mmoja akiwa amezaliwa hivi karibuni, wakati Azory akiwa ameshatoweka.

Walimkabidhi pia misaada mbalimbali yenye thamani ya zaidi ya Sh700,000.

Anna alijikuta akibubujikwa machozi na kushindwa kuzungumza alipoona kundi la wafanyakazi wanawake wa MCL, likiwasili nyumbani kwake kuungana naye katika kuadhimisha siku hiyo.

“Sijui niseme nini, mwenzenu nashindwa hata cha kuongea, mmekuwa wema sana kwangu hasa wakati huu ninapopitia kipindi kigumu... sina cha kuwalipa zaidi nawashukuru,” alisema.

Awali, kiongozi wa msafara wa wanawake hao wa MCL, Lilian Timbuka alisema upendo, umoja na mshikamano ndio uliowasukuma kuadhimisha siku hiyo pamoja na Anna.

“Tunajua mwenzetu upo katika kipindi kigumu, lakini tukutie moyo na shime kwamba usichoke kupiga goti na kumuomba Mungu na sisi tupo nyuma yako tunaendelea kukuombea upate nguvu,” alisema Lilian.

Mama Janeth Magufuli

awasifu wanawake wa Dar

Katika maadhimisho hayo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, mke wa Rais, Mama Janeth Magufuli aliupongeza Mkoa wa Dar es Salaam kwa kuanzisha vikundi zaidi ya 400 vya wanawake vinavyojishughulisha na usindikaji mazao, ushonaji na uchoraji.

Pia aliupongeza mkoa huo kwa kuwa na vikundi vya kukopeshana (Vicoba) vipatavyo 2,748 ambavyo kwa pamoja, vina mtaji wa jumla ya Sh10.4 bilioni

“Ni imani yangu kuwa mikoa yote na taasisi nyingine za kiserikali na kiraia zitaiga mfano wa Dar es Salaam katika kuwawezesha wanawake kiuchumi,” alisema.

Mawaziri wanawake

walivyoadhimisha

Akiwa mkoani Rukwa, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu aliwaonya wakurugenzi watendaji wa halmashauri nchini wasiotenga asilimia nne ya mapato ya ndani ya halmashauri kwa ajili ya mikopo ya wanawake.

Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika katika Uwanja wa Nelson Mandela, Waziri Ummy alisema atachukua majina ya wakurugenzi wasiotenga fedha hizo na kuyakabidhi kwa Rais John Magufuli ili awachukulie hatua za kinidhamu ikiwamo kuwaondoa katika nafasi zao.

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako alisema Rais Magufuli ana imani na utendaji wa wanawake ndio maana amewateua kwenye wizara nyeti kama vile elimu, afya na madini akiamini kwamba watafanya kazi kikamilifu kuleta maendeleo ya nchi.

“Tunafanya jitihada kuboresha elimu hapa nchini. Tunaangalia pia elimu ya juu, tunashirikiana na wadau mbalimbali katika kuboresha mfumo wa elimu hapa nchini,” alisema Profesa Ndalichako.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji alisema usawa wa kijinsia unaoonekana katika elimu ya msingi na sekondari utatoa matokeo chanya katika elimu ya juu.

Akizungumza katika kongamano la sita la Wanawake Wenye Mafanikio Tanzania (TWA) lililofanyika jijini Dar es Salaam katika alisema ili wanawake wapige hatua, wanahitaji kuwa na uelewa wa kutosha ambao bila shaka ni elimu.

Katika hatua nyingine, Serikali imewapiga marufuku wanaume wanaotumia mali za familia kama dhamana za mikopo bila kuwashirikisha wake zao.

Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Fabian Daqarro ameyasema hayo jana kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

Daqarro alisema wapo wanaume wanaotumia mali za familia kama nyumba kukopa bila kuwashirikisha wake zao na wakishindwa kulipa mikopo, mali ya familia hupigwa mnada.

Mbasha Amuandikia Waraka Mzito Mzazi Mwenzake Baada ya Kumnyima Mtoto

0
0
Mbasha Amuandikia Waraka Mzito Mzazi Mwenzake Baada ya Kumnyima Mtoto
Msanii wa muziki wa injili nchini Emmanuel Mbasha amefunguka katika ukurasa wake wa instagram kwa kumuandikia barua ndefu aliyekuwa mke wake wa ndoa Florah Mbasha kuhusu kumnyima mtoto wake wa kike waliezaa nae walipokuwa wakikaa wote miaka ya nyuma.

Emanuel Mbasha na Flora Mbasha walifunga ndoa kanisani na kuishi pamoja na hata kufanya kazi zao za muziki wa injili pamoja lakini walikuja kuachana na hata  kupelekana mahakamani kwa makosa ya kubaka ambapo baada ya upelelezi kukamilika ilikuja kuonekana kwamba Florah Mbasha alitunga kesi hiyo na kumsingizia  mume wake hivvyo Emanuel Mbasha alichukua jukumu la kumtaliki mwanamke huyo.

Lakini Emanuel Mbasha anaonekana kuumia kukaaa mbali na mtoto wake wa kike walimpata  na mzazi mwenzie huyo ambae alipewa mamlaka ya kukaa na mtoto huyo na mahakama kutokana na umri wa mtoto, Mbasha anasema kuwa pamoja na kwamba mahakama iliamuru mtoto kukaa na mama yake na yeye kuruhusiwa kumuona kwa muda tu lakini hata muda kidogo amekuwa akinyimwa na mzazi mwenzie huyo.

"Happy women’s day, ila ulinizalia mtoto mzuri mno nakushukuru sana,nimemmiss sana lizy unipage basi hata mtoto , unaninyima hata kumuona , karibia mwaka wa 2 unaelekea wa 3 sasa sijawahi kumuona mtoto daah mie babake tu ila naomba siku moja moja nifurahie maisha , aah nakuomba nimuone mwanangu lizy,najua hata mtoto amenimiss sana maana najua ameonoka kwangu akiwa mkubwa na nimemlea tamgu akiwa mtoto , atakuwa anshindwa tu kusema ila amenikumbuka sana.mahakama iliamua mtoto akae na mama ila niwe namuona mtoto ,sasa unapingana na mahakama…. sitaki povu hapa naongea na mzazi mwenzangu maana naona njia za kawaida zimeshinikana sasa inabidi nikuombe insta."

Mbasha anAsema kuwa ameamua kutuma ujumbe huo kwa Florah Mbasha ambae kwa sasa ameshaolewa na mwanaume mwingine kupitia instagram kwa sababu hakuna njia nyingine wanaweza kuwasiliana zaidi ya hiyo,

Viewing all 104417 articles
Browse latest View live




Latest Images