Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Mrembo Tunda Amuomba Msamaha Aunty Ezekiel

$
0
0
Miezi kadhaa iliyopita kupitia mtandao wa instagram wa video vixen maarufu Tunda alirushiana  maneno na muigizaji Aunty Ezekiel  pamoja na mzazi mwenzake Mose Iyobo na kusemekana kuwa Tunda alishindwa kulipa deni alilokuwa akidaiwa na Aunty Ezekiel.

Leo March 10,2018 kupitia mtandao wa instagram wa Tunda ameomba radhi kwa kile ambacho alikifanya dhidi ya Aunty na kuamini kuwa hata yeye atakuwa mama wa baadae, hivyo ameamua kuomba radhi.

“Let me take this opportunity kumuomba radhi Aunty kwa kumtukana mtoto wake ilikuwa ni hasira naomba msamaha kama mwanamke ambaye nitaitwa mama pia soon” Ujumbe huo pia umezua maswali kuwa Tunda ni mjamzito? kwa nini asema atakuwa mama soon?.

Ifahamu sheria ya maandamano Kikatiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

$
0
0
Maandamano ya aina yoyote ni haki ya mwananchi na yanaruhusiwa kisheria lakini maandamano hayo lazima yafuate sheria na taratibu zilizobainishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Sheria ya maandamano inamtaka mwananchi au kundi la wananchi wanaohitaji kufanya maandamano kutoa taarifa kwa maandishi kwa Mkuu wa Polisi wa eneo husika kabla ya masaa 48 ya kuanza kwa maandamano hayo ikieleza dhumuni la maandamano hayo.

Pia wahusika wanatakiwa wawe tayari kwa jibu lolote kutoka kwa mkuu huyo kwa kuwa chochote watakachojibiwa lazima kiwe na sababu.

Endapo wahusika watakataliwa kufanya maandamano na hawatoridhishwa na sababu zilizotolewa na Mkuu wa Polisi kuna hatua mbili muhimu zinazotakiwa kufuatwa na sio wahusika kujiamulia kuandamana kilazima kwa kuwa kufanya hivyo ni kosa.

Hatua hizo muhimu zinazotakiwa kufuatwa ni kuandika barua kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na kumueleza kutoridhishwa na sababu zilizotolewa na Mkuu wa Polisi ili Waziri naye kwa upande wake aamue kuruhusu au kukataza.

Endapo wahusika hawatoridhika na majibu ya Waziri, waandamanaji watatakiwa kwenda Mahakamani ambapo ndipo uamuzi wa mwisho utatolewa.

Hakuna sheria inayotambua maandamano ya nchi nzima kufanyika kwa siku moja kwa sababu kila eneo lina Mkuu wa Polisi mwenye haki ya kukubali au kukataa ombi la kufanya maandamano kulingana na hali halisi ya eneo lake.

Kila jambo lina faida na hasara zake lakini kuna mambo ambayo faida huwa chache kuliko hasara, maandamano yana athari kubwa kiuchumi na kijamii kwa sababu maandamano yoyote ni lazima Jeshi la Polisi liwajibike katika kuongoza na kulinda maandamano hayo, hivyo kupelekea wanajeshi wengi kusitisha kazi zingine kwa ajili ya kuzuia vurugu zisitokee.

Athari zingine ni kusitishwa kwa shughuli mbalimbali zikiwemo za usafiri , kufungwa kwa maduka na masoko pamoja na athari zitokanazo na vurugu zinazoweza kutokea kwa sababu ya maandamano hayo.

Hivyo itambulike kisheria hatua hizo zinatakiwa kufuatwa kabla ya kufanya maandamano, aidha maandamano kisheria ni jambo halali endapo tu litakuwa limehalalishwa kisheria.

Eti Boyfriend Wangu Anafikiria Mimi Bado ni Bikira

$
0
0
Admin
Mimi ni Msichana wa Miaka 21 , Nasoma chuo kimoja hapa dar ..nimetokea mkoa niko mwaka wa Pili sasa , huko nilipotokea nina Boyfriend ambae nimekuwa nae kwa muda mrefu toka secondary ila swala mapenzi hatujawahi fanya kwa vile kabla ya kuja chuo nilikuwa Bikira ..Baada ya kuja chuo naweza sema nimekutana na vijana wajanja na nadiriki kusema sina tena Bikira washaitoa ...

Sasa nashindwa ni namna gani nimwambie boy wangu huyo wa mkoa ..Likizo nilienda nikamtega tufanye ili nijidai yeye ndio kaitoa lakini aliniambia tutafanya mapenzi siku ya ndoa ...Naombeni ushauri mie nataka nimwambie kwamba sina tena na tuwe tunafanya mapenzi ..Nitaanzia wapi ?

ETI BOY FRIEND WANGU ANAFIKIRI MIMI BADO NI BIKIRA

Vigogo Wanne wa Madawa ya Kulevya Wakamatwa..Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Lewo Jumapili ya March 11

$
0
0
 


Vigogo Wanne wa Madawa ya Kulevya Wakamatwa..Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Lewo Jumapili ya March 11

Tafsiri sahihi ya kosa la uhaini na adhabu yake Kwa Mujibu wa Katiba ya Tanzania

$
0
0
Uhaini  ni  kosa  la  jinai, kwa tafsiri nyepesi ina maana kwamba ni kosa kubwa ambalo mtu analifanya dhidi ya nchi yake na mtu anyefanya kosa hili anajulikana kama msaliti, mfano wa watu wasaliti wanaojulikana duniani ni Yuda ambaye kidini alimsaliti Yesu, mwingine ni Benedict Anold huyu jamaa aliisaliti nchi yake ya Marekani dhidi ya Mbritishi, wengine ni Vidkun Quisling, na Marshall Pe’tain.

Kisheria ukubwa wa kosa hupimwa kwa adhabu yake, kosa likiwa kubwa mtuhumiwa hutumikia adhabu kubwa vivyo hivyo kosa likiwa dogo mtuhumiwa huadhibiwa kiasi.

Kwa mujibu wa sheria ya Tanzania, mtu akifanya yafuatayo huhesabiwa kama amefanya kosa la jinai la uhaini hivyo huadhibiwa kulingana na ukubwa wa kosa hilo.

Kifungu cha 39 ( 1 ) cha kanuni za adhabu kinasema kuwa mtu yeyote ambaye yumo ndani ya Jamhuri  ya Muungano au popote, kujaribu kumuua Rais, kuanzisha vita dhidi ya Jamhuri ya Muungano,  kusababisha, kuwezesha, kuchochea, kushawishi, kushauri kuhusu  kifo, kumlemaza, kumzuia, kufungwa kwa Rais, kumwondolea Rais heshima na jina la mkuu wa nchi, amiri jeshi mkuu, au kiongozi wa serikali, kupindua serikiali iliyo madarakani, kutishia serikali, bunge au mahakama kwa makosa haya na yale yaliyotajwa hapo juu mtu wa namna hiyo atakuwa  ametenda kosa la jinai ambalo ni kosa la uhaini

Aidha ifahamike kuwa kwa mtu yeyote atakayekutwa na hatia ya kutenda kosa la uhaini adhabu yake ni kifo na sheria hiyo ya kifo imeelezwa katika kifungu cha sheria namba 39 na 40 cha kanuni za adhabu.

Hivyo watanzania kwa umoja wetu tunapaswa kuzijua sheria za nchi yetu ili kuweza kujiepusha kutenda makosa ya uhaini  dhidi ya nchi yetu.

Mapya Yaibuka..Emmanuel Mbasha Amwangukia Flora Mbasha

$
0
0
MWIMBAJI wa injili Emmanuel Mbasha amefunguka na kumshukuru aliyekuwa mkewe, Madam Flora kwa kumzalia mtoto wa kike mzuri huku akilalama kwa kunyimwa fursa ya kuonana na mwanaye huyo kwa muda wa miaka miwili sasa.

Mbasha kupitia Instagram amefikisha kilio chake kwa mzazi mwenzake huyo ambaye sasa ameolewa na Daudi Kusekwa na kumtaka japo kumpa haki ya kuonana na mtoto wake huyo ambaye anadai kuwa amemlea tangu akiwa mdogo.

 “Ulinizalia mtoto mzuri sana kwa hilo nakushukuru mno. Nimemmiss Lizy sana unipe basi mtoto unaninyima kabisa daah karibu mwaka wa pili inaelekea wa tatu sasa sijamwona mtoto. Du, mimi baba yake tu ila nakuomba hata siku moja moja nifurahie maisha na dogo basi nakuomba nimwone mwanangu Lizy.
“Najua hata mtoto amenimiss sana, kwa mana ameondoka kwangu akiwa mkubwa na nimemlea tangu mtoto ila anashindwa kuongea tu, najua ananikumbuka sana.” 
“Mahakama iliamua mtoto akae na Mama ila niwe namwona, sasa unapingana na mahakama. Sitaki povu nimeongea na mzazi mwenzangu X wife, mke wa mtu.. njia za kawaida naona imeshindikana unakaza sana aise sasa inabidi nikuombe Insta tu,” alisema Mbasha

Man United Yaichakaza Liverpool Vibaya..Marcus Rashford Aibuka Shujaa

$
0
0
Jumamosi ya March 10 2018 katika uwanja wa Old Trafford Man United waliikaribisha Liverpool kucheza mchezo wao wa Ligi Kuu England msimu wa 2017/2018, huo ukiwa ni mchezo wa kumaliza ubishi kati ya Jurgen Klopp na Jose Mourinho.

Mchezo huo ambao umechezwa Old Trafford umemalizika kwa Man United kupata ushindi wa magoli 2-1, magoli ya Man United yote yakifungwa na Marcus Rashford dakika ya 14 na 24 wakati goli pekee la Liverpool kilipatikana kwa beki wa Man United Eric Bailly kujifunga dakika ya 66 baada ya kushindwa kuzuia mpira uliopigwa na Sadio Mane.

Huo unakuwa ni ushindi wa 88 wa Man United dhidi ya Liverpool toka wakutane kwa mara ya kwanza April 28 1894 katika mchezo uliyomalizika kwa Liverpool kushinda kwa magoli 2-0, hadi kufikia leo Man United na Lverpool wamecheza jumla ya game 228, wakitoka sare game 65 huku Liverpool akishinda katika game 75 pekee.

Miujiza ya Sharifu Seif Mohamed..JE Umeachwa na Mme/Mke au Mpenzi, Umesongwa na Mitihani ya Maisha

$
0
0
SHARIFU SEIF MOHAMED ANAWASHUKURU WALE WOTE WANAOENDELEA KUPIGA SIMU, WENYE MATATIZO NA WALE WANAOTOA  SHUKRANI NA SHUHUDA JINSI TIBA ZAKE ZINAVYO WASAIDIA,

(Rudisha mahusiano yako ndani ya masaa 72 tu)

SHARIFU MOHAMED Ni  mtaalam na mnajimu maarufu wa nyota na kubashiri mambo yanayo watesa binadamu duniani kote na kupata ufumbuzi, Anatumia kitabu cha QUR'AN na Nyota

Je Umeachwa na UMPENDAE awe Mme/Mke na bado unampenda? Je Umekimbiwa na Mmeo/ Mkeo n anaishi na mtu mwingine? Je Umejaribu sehemu nyingi bila mafanikio? Mpigie simu SHARIFU SEIF sasa hivi ujionee Muujiza wa Papo kwa Papo, Anauwezo wa hali ya juu wa kusambaratisha mahusiano yao na kumrejesha kwako haraka sana na Kumfanya Atimize Ahadi zote Ndani ya Muda Mfupi Endapo Utafwata Atakacho Kuelekeza

 ZINDIKO LA NYUMBA NA BIASHARA, PETE ZA BAHATI, HUMALIZA KABISA TATIZO   HUZUIA CHUMA ULETE KWENYE BIASHARA, HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA, NA KUPONYA MAGONJWA SUGU ANAO UWEZO WA KUMRUDISHA ALIE MBALI AU ALIECHUKULIWA MSUKULE, KUPANDISHA NYOTA NA KUSHINDA BAHATI NA SIBU, KASAFISHA NYOTA NA KUKUPA MVUTO WA AJABU, KUTOA NUKSI NA VIFUNGO MBALIMBALI,  MAFANIKIO YA MAISHA NA UTAJIRI BILA MASHARI, NA MENGINE MENGI YA SIRI,

JE UMAHANGAIKA KUPATA MTOTO BILA MAFANIKIO? WASILIANA NA MTAALAMU HUYU KWANI YEYE HUFAULU PALE WOTE WALIPOSHINDWA, PIA UMALIZA KAZI ZILIZO SHINDIKANA NA WATAALAM WENGINE NDANI YA MASAA 24 TU,

(NA ANATIBU KWA NJIA YA SIMU UKIWA NCHI YOYOTE AU MKOA WOWOTE ENDAPO UTAFWATA MAELEKEZO YAKE)

Kwa ushauri na mawasiliano  zaidi Piga SIMU No:

Mobile +255 654-836970
WhatsApp 0622766715

Mahari ya Sanchi yapanda Kutoka Million 10 Mpaka Million 20

$
0
0
Mrembo Jane Rimoy kwa jina maarufu anajulikana kama Sanchi au Sanchoka anayefanya shughuli za umodel nchini Tanzania , ameweka wazi kwa mwanaume mwenye nia ya kumuoa mahari yake kwa sasa ajiandae kutoa million 20.

Mahari yake imepanda ghafla kutoka million 10 mpaka million 20 baada ya kushinda shindano la Ijumaa Figa Bomba Girl 2017 lililoandaliwa na Global Publishers.

Hizi ni baadhi ya picha akiwa kwenye office ya Global Publisher akisubiri mahojiano baada ya kushinda.

VIDEO Mpya: Rosa Ree Feat. Bilnass -Marathon

$
0
0
Baada ya Wimbo wa DOW Kufanya Vizuri Ndani na Anga za Kimataifa, Mwanamuziki Rosa Ree Ameachia VIDEO ya wimbo Wake Mpya ambao amemshirikisha Bilnass

Tazama Wimbo Huo Hapo alafu toa Maoni yako:

Mdau Amshukia Mtangazaji TBWAY Kwa Tabia ya Kukimbiza Gari Vibaya iliyopelekea Akapata Ajali Mbaya

$
0
0

By King Kong III

Imeniladhimu nimuandikie waraka mfupi ndugu yetu Tonny Aka Tbway360 ili watu walio karibu nae au yeye akipitia humu JF aweze kuusoma.Nimeshawahi kukutana na Huyu jamaa mara kadhaa,mara ya kwanza nilimuona maeneo ya Mlimani city akiwa anatoka NSSF kufatilia nadhani mafao yake,nilimuona mtu wa vurugu sana kwenye gari lakini nikaona bado kijana labda bado ana ushamba wa gari.

Mara ya Pili niliona Clip mtandaoni akikimbiza gari kwa speed ya ajabu kisha akakamata Hand-Brake gari ikarotate ikarudi ilipotoka na ilikuwa eneo la wazi kabisa barabarani maeneo ya ununio,nikaona huyu jamaa kumbe ndi0 hulka yake kukimbiza magari kwa speed za hatari >160km/hr tena maeneo ya mjini.

Mara ya tatu tena nilimuona live akiwa quality plaza katoka kwenye ATM kutoa pesa,alitoka na speed kubwa sana hadi nikashangaa inakuwaje anatoka na speed kubwa namna ile wakati mbele tu kama mita 20 kuna foleni? Nikagundua jamaa bado haijui gari vizuri,yes ni dereva lakini haijui gari vizuri,mtu anayeijua gari lazima ataiheshimu.

Kilichonituma niandike huu waraka ni kwamba Jana Tbway360 alikula mzinga wa hatari na gari kubilingika mara mbili,kwa mujibu wa maelezo yake eti anasema alikuwa speed ndogo tu akapushiwa na Suzuki aliyekuwa anaendesha mfanyakazi wa tigo ikamgusa ubavuni na kupelekea gari kubilingika mara mbili.Tbway anatufanya sisi watoto wadogo,gari kwenye speed ndogo uguswe tena na suzuki swift ubilingike mara mbili?

Dogo Tbway360 hiyo umegewa kama funzo,hiyo ni rasharasha tu,punguza sifa barabarani,kwa mtu anayefahamu gari hawezi kufanya ujinga wa kukimbiza gari kwa mispeed ya hovyo hovyo tu,next time hutopata hata muda wa kwenda TIGO HQ kuwatukana SGA....Haya sasa kama ulikuwa na bima kubwa fuatilia michoro ya ajali uende bima kama ulikuwa na 3rd party ugulia maumivu ya Legacy.

Gari ya TBWAY Kabla ya Ajali

Maboresho Katika Application ya Udaku Special, Fanya Ku Update Ama Download Hapa Kwenye Simu yako

$
0
0
Maboresho Katika Application ya Udaku Special, Fanya Ku Update Ama Ku Download HAPA Kwenye Simu yako, Tumebadili Logo pamoja na Kuifanya App iwe nyepesi zaidi bila kuchukua nafasi kubwa katika Simu yako

UPDATE HAPA

DOWNLOAD HAPA
 

JE, ni Kweli Kuwa Kila Mwanamke Anajiuza na Sio Wale tu Wanaosimama Barabarani?

$
0
0

Huu ni ukweli hata tukipinga hakuna mwanamke asiyejiuza tofauti kuna aina mbili tu za hii biashara.

1. Wale wanaojiuza kwa kutafuta wateja kusimama mabarabarani.
2. Hawasimami barabarani wanaenda kwa special order, kufahamiana kwanza kama urafiki, kupitia mitandao, kukutana kwenye bar na magari n.k

Ukitaka kujua kuwa wote hawa wanajiuza, mlale mwanamke halafu usimpe noti uone zali litakavyokuwa! Fanya uchunguzi hapahapa jijini Dar, nakuhakikishia ni wanawake wachache sana labda 2%-10% ambao hawako kibiashara juu ya mapenzi.

1. Kuna demu mzuri sana anafanyakazi (ofisi kubwa) ya sirikali mshahara wake ni zaidi ya Tshs m2 kwa mwezi anabwana ake tena wameshibana lakini juzi tu akawa anataniwa na rafiki yangu mmoja mwenye nchi ndafuu sana kuwa nataka kukuoa, kama vipi uje home tuonje tunda bana, tena demu aliweka mafuta yake akaja na gari yake akavurugwa kisa uanjua nini hapa?? Pesa huyu anajiuza ila yeye ni kwa investiment huyu ni MUWEKEZAJI!!

2. Kuna demu anasoma chuo kikuu anatamba sana kwenye mitandao na kuweka picha ya bwana ake kila mara juzi kati mchizi wangu kamuanzishia chat kwa fb mpaka muda huu kashatoa uroda biashara ni ileile kila akitaka kutoa nauli, alipewa mara ya kwanza elfu 20 alikasirika sana, huyu ni mjasiriamali.

3. Nenda Bar yoyote Dar, hata mhudumu unayemuona anajiheshimu akikuletea soda au bia yako mnong'oneze mwambie nina lfu 50 tukalale wote, hakikisha una simu maana tayari mzigo umepata hii nayo ni biashara anauza sema tu ni parti time.

4. Usimuone mmama wa makamo mkubwa na mkurugenzi wa kampuni fulani mwambie ninajua kula mzigo lazima utampata tu wewe usiogope sura yake na heshima yake ongea tu, huyu naye anauza sema yeye ni doner.

5. Mademu karibia 80% Dar wanamabwana zaidi ya 5 kila mmoja amepengwa kisawasawa, kweli anao watano aende buguruni kufanya nini?


Hata mkikataa mnajiuza tena mnajiuza vibaya sana dunia imeisha tu

JF

Nataka Kupenda Kama Mjinga, Nizame Nipotee! Kama limbwata ni Kweli Lipo Basi Nilishwe Hata Hilo

$
0
0
It may sound strange but this has been my major wish for a while,

Nataka kupenda kama mjinga, yaani niwe zombiee, nizame mapenzini nipotelee huko. Kila nachoambiwa nione sawa niwe mjinga mjinga no reasoning.

Yale mapenzi usipowasiliana ama kumwona mtu wako for a day unajisikia mgonjwa, mapenzi ambayo unaongea na mtu wako for two or three hrs and you feel like its just 5 minutes na haujui mlikuwa mnaongea nini.

Yaani mapenzi ambapo nikiachwa au nililazimika kuacha basi nichanganyikiwe, nishindwe kula, nikose usingizi, nipungue uzito, nione kama dunia imekwisha shughuli zangu nishindwe kufanya, kichwa kigome kufukiri

Kama limbwata ni kweli lipo basi nilishwe hata hilo, haya mapenzi ya kupenda robo robo with a lot of reasoning sio nayotaka.

Natamani kupenda with all my heart, soul, mind, body and my everything, nataka kupenda kamili kamili, kwa kila kitu, mpenzi wangu awe kila kitu, awe ndio dunia na maisha yangu.

Trust me I want to love like nothing else,

Hivi ni mimi tu?

Tundu Lissu Kufanyiwa Upasuaji Mwingine

$
0
0
 Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu anatarajiwa kufanyiwa upasuaji mwingine wa goti la kulia Machi 14, 2018 katika Hospitali ya Chuo kikuu cha Leuven, Gasthuisberg ili kumnusuru asipatikane na athari za mifupa kutojiunga kwa wakati.

Lissu amebainisha hayo usiku wa kuamkia leo wakati alivyokuwa anawafahamisha umma juu ya maendeleo ya afya yanavyoendelea huko alipo na kusema anaendelea vizuri na matibabu na sasa anaweza kusimama kwa miguu yote miwili bila ya msaada wa magongo ya kutembelea.

"Timu ya madaktari bingwa wa mifupa wanaonitibu, wamenitaarifu kwamba kasi ya mfupa wa juu ya goti kuunga ni ndogo sana na  kwamba wasipoingilia kati na kurekebisha mfupa huo, itachukua muda mrefu sana kuunga na hata ukiunga baada ya huo muda mrefu, hautaunga kwa namna itakayoondoa hatari ya kuvunjika siku za mbeleni. Kwa sababu hizi, madaktari wangu wamependekeza kufanya operesheni nyingine kwenye mfupa wa juu ya goti la kulia", amesema Lissu.

Pamoja na hayo, Lissu ameendelea kwa kusema "Niko kwenye mikono salama ya kitabibu. Madaktari wangu, Prof. Dr. Stefa Nijs na Prof. Dr. Willem-Jan Mertsemakers, ni madaktari bingwa wa mifupa wanaosifika barani Ulaya kwa utaalamu wao katika fani hiyo. Hivyo msiwe na hofu, Mungu wetu aliyeniwezesha kuwa hai sasa, ataendelea kutenda miujiza yake kupitia kwa madaktari bingwa hawa. Nitaendelea kuwataarifu maendeleo ya matibabu yangu kadri itakavyokuwa lazima na muhimu kufanya hivyo".

Mbunge Tundu Lissu alishambuliwa na watu wasiojulikana tangu Septemba 7,2017 akiwa mkoani Dodoma, na kisha kupelekwa nchini Nai

Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH simba Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili

$
0
0
Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH issa simba said Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Maalim Hussein Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU. Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
Atamfanya Atimize 5 zote kwa Muda Mfupi.

Issa simba said Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumal6uiza Tatizo lako..
Anatibu kwa Kutumia Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA. Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI. Nguvu za KIUME, Humaliza Kesi zilishindika ndani ya siku 14 tu..na mengi zaidi

Piga simu +255 622588038au 0679119679 au +255 764318107

NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE...

Kocha wa Yanga; Tukishinda kesho Simba ijiandae

$
0
0
KOCHA Mkuu wa Yanga, Mzambia, George Lwandamina amesema kuwa endapo kikosi chake kitaibuka na ushindi kesho Jumatatu dhidi ya Stand United, basi Simba ijiandae kukaa pembeni.

Habari za ndani ambazo Spoti Xtra imezipata kwa viongozi wa Yanga ni kwamba wamegomea rai ya baadhi ya wadau kutaka mchezo wao dhidi ya Stand uahirishwe kwa madai kwamba wanaucheza kwa mipango maalum.

“Makocha wamekataa kuahirisha mechi ya Stand kwa vile wanasema ni mkakati mzuri wa kukaa kileleni na kwenda sambamba na Simba kama Simba wameahirisha yao ni juu yao, makocha wanautumia huu mchezo kama mzuka wa kwenda Botswana,” alidokeza kiongozi mmoja wa Yanga. Aliongeza kwamba wanataka kufuta tofauti yao na Simba ili wakitoka kwenye michuano ya kimataifa wajue wamebaki na kazi moja tu ya kukomaa kileleni.

Yanga itapambana na Stand United kesho Jumatatu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, katika mchezo wa ligi na endapo itashinda itafikisha pointi 46 sawa na Simba inayoongoza msimamo wa ligi hiyo lakini itakuwa nyuma kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Akizungumza na Spoti Xtra, Lwandamina alisema; “Mpaka tunafika hapa wengi walikuwa hawaamini kutokana na kuwa na majeruhi wengi, hata hivyo endapo tutashinda mchezo wa Jumatatu dhidi ya Stand United naamini kabisa tunaweza kuishusha Simba kutoka nafasi ya kwanza.”

“Ushindi huo, pia utasaidia kurudisha hali ya ushindani kwa wachezaji wangu lakini hamasa kwa wale ambao hapo awali walionekana kukata tamaa kama tunaweza kuwa mabingwa kwa mara nyingine tena, namuomba Mungu iwe hivyo hiyo Jumatatu katika mchezo huo,” alisema Lwandamina ambaye kiongozi mmoja wa Yanga alikiri kwamba angekuwa Kocha mzungu angeshatimka.

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Hussein Nyika alisema; “Tumejipanga vizuri na tunapambana vilivyo kuhakikisha tunaweka mambo sawa ndani ya timu ili kurudisha hali ya ushindani kwa wachezaji wetu ambayo hapo awali ilikuwa imepotea.”

“Lakini pia tunapambana kuhakikisha wachezaji wote waliokuwa majeruhi wanakuwa sawa baada ya kutoka Botswana kucheza mechi yetu ya kimataifa dhidi ya Township Rollers, ili waweze kuongezea nguvu timu yetu katika harakati zetu za kuhakikisha tunaishusha Simba kutoka nafasi ya kwanza,” alisema Nyika. “Thabani Kamusoko tayari amerejea uwanjani, lakini pia Donald Ngoma naye muda si mrefu anarudi kwa hiyo mambo yatakuwa ni moto.”

Breaking News:Tazama Kubenea Akizungumza na Waandishi wa Habari

$
0
0
Mbunge wa Ubungo kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Saed Kubenea anazungumza na waandishi wa habari ambapo mbali na mambo mengine, anazungumzia ishu ya chaguzi zisizo huru.

Bunge la China Lafanya Mabadiliko ya Katiba na Kuondoa Ukomo wa Rais..Sasa Kuongoza Miaka Anayotaka

$
0
0
Bunge la China limefanya mabadiliko ya katiba na kuondoa kifungu cha ukomo wa muda wa Rais kukaa madarakani, na hivyo kumpa Rais Xi Jinping nafasi kuwa kuongozi wa taifa hilo muda wote atakaokuwa hai.

Paul Makonda Atoa Agizo Kwa Jeshi la Polisi Kuwakamata Wanaotukana Viongozi wa Kitaifa

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameliagiza Jeshi la Polisi kuwakamata na kuwafikisha mahakamani watu wote wanaowatukana viongozi wa kitaifa. Pia, RC Makonda ameitaka TCRA kushiriki katika ukamataji wa halifu wa mitandao.
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images