Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Mwanafunzi Ampa Mimba Mwalimu Wake...

$
0
0
Wakati ikiwa imezoeleka kuwa baadhi ya walimu wa kiume huwarubuni wanafunzi wao wa kike na hata kuwaharibia kabisa ndoto zao za kielimu kutokana na kuwapa ujauzito, hali imekuwa tofauti mkoani Rukwa ambako mwanafunzi wa Kidato cha Pili anadaiwa kumzalisha mwalimu wake.

Mwanafunzi huyo aliyemzalisha mwalimu wake ana umri wa miaka 17, wakati mwalimu huyo anayefundisha katika Shule ya Sekondari ya Umma ya Nkasi, iliyopo mwambao mwa Ziwa Tanganyika wilayani Nkasi, Rukwa, ana umri wa miaka 25.

Tukio hilo linalotajwa kuwa la kwanza kutokea wilayani hapa, limekuwa gumzo kubwa kwa wakazi wa Nkasi na wilaya jirani.

Hata hivyo, kwa wanafunzi, wamekuwa wakimpongeza mwenzao kwa kujaliwa kupata mtoto katika umri wake huo mdogo, huku mzazi mwenzake akiwa na uhakika wa maisha kutokana na kuwa ni mtumishi serikalini.

Imeelezwa kuwa licha ya tukio hilo, mwalimu huyo aliyezaa na mwanafunzi wake bado anaendelea na masomo shuleni hapo, huku `mzazi’ huyo wa kiume akifundishwa na mzazi mwenzake.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mjini Namanyere hivi karibuni, Mkuu wa Shule ya Sekondari Nkasi mjini Namanyere ambayo ni ya mchanganyiko ya umma, Amiamie Nanga alisema mwalimu huyo alianza kazi shuleni hapo ikiwa ni mara yake ya kwanza kufundisha baada ya kuhitimu mafunzo ya ualimu chuoni.

“Yameshatokea, lakini haileti picha nzuri sana, lakini mimi nina uzoefu mkubwa na wakazi wa mwambao wa Ziwa Tanganyika, kwao si ajabu kuwa na uhusiano na watu waliowazidi umri, iwe kwa mtoto wa kike au wa kiume, wote ni sawa tu", alisema Mwalimu mkuu.

“Lakini katika kisa hiki, inaonesha walimu sasa wanapoteza haiba ya ualimu. Hii kazi ina miiko na maadili yake …kwa mwalimu huyu hii ni ajira yake ya kwanza, nikimaanisha ni kituo chake cha kwanza cha kazi tangu ahitimu masomo yake…” alisema. Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda alisema hakuna kosa kwa mwalimu huyo wa kike kwa kuwa tayari ni mtu mzima.

“Isitoshe katika kisa hiki ni nadra kumpata mlalamikaji … Mwalimu mwenyewe huyu wa kike hawezi kuwa tayari kujidhalilisha kuwa amebakwa, yalikuwa maamuzi yake.”

Aliongeza kuwa, kwa mwalimu huyo kupata ujauzito wa mwanafunzi wake hakuwezi kuathiri ajira yake, tofauti na mwalimu wa kiume akimpatia ujauzito mwanafunzi wake wa kike ambaye huathirika kwa kukatisha masomo.

Jitihada za kumpata mwalimu huyo wa kike na mwanafunzi huyo zimegonga mwamba baada ya watu wao wa karibu kulieleza gazeti hili kuwa hawako tayari kuuzungumzia mkasa huo.

Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo waliohojiwa na mwandishi wa habari hizi kwa masharti ya kutoandikwa gazetini kwa hofu ya kuchukuliwa hatua za kinidhamu shuleni hapo, pamoja na kukiri kutambua uhusiano baina ya mwanafunzi mwenzao na mwalimu wao, lakini walisema hivi sasa mwalimu huyo amesitisha uhusiano na mwenzao na kuanzisha uhusiano mpya na mwalimu mwenzao.

Walisema pamoja na mambo mengine ni kama mwanafunzi mwenzao ameathirika kisaikolojia baada ya ‘kupinduliwa’ na mwalimu wake wa kiume ambaye kwa sasa ndiye baba mlezi wa mtoto.

“Huyu mwalimu wa kike sisi sasa tunamwita shemeji yetu alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwenzetu… penzi lao lilikolea hadi sasa ameweza kumzalia mtoto huyo…, lakini kwa sasa inavyoelezwa ni kwamba penzi limehamia kwa mwalimu mwenzake,“ alisema mmoja wao.

Baadhi ya watu wa karibu na mwanafunzi huyo wanakiri kuwa mwanafunzi huyo hana uwezo wa kifedha kumudu kumpatia malezi stahiki mtoto wake huyo, hivyo hata mzazi mwenzake alipoanza uhusiano na mwalimu mwenzake hakuwa na jinsi, bali kukubaliana na matokeo.

“Usiniandike jina gazetini, sisi tunashauri mwalimu huyo wa kike na mpenzi wake huyo wa kiume ambaye ni mwalimu mwenzake wahamishiwe shule nyingine kwa sababu kama kioo katika jamii wameteleza kwa kiasi kikubwa na watashindwa kuwajenga na kuwalea wanafunzi wao kimaadili.

“Isitoshe tunajiuliza sheria hapa inasemaje maana kama angekuwa ni mwalimu wa kiume amempatia mwanafunzi wake wa kike ujauzito angeshitakiwa na kufikishwa mahakamani na pengine kuhukumiwa kifungo kisichopungua miaka 30 jela, sasa kwa hili sheria inasemaje?” Alihoji.

Baadhi ya wazazi mkoani hapa waliohojiwa na mwandishi wa gazeti hili kwa nyakati tofauti wameelezea kushangazwa na tukio hilo, na hasa kwa jinsi mwalimu alivyoshindwa kujizuia `kujiachia’ kimapenzi kwa mwanafunzi wake.

KRC Genk yala Kichapo, Samatta Atokea Benchi

$
0
0
NAHODHA wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta jioni ya leo ametokea benchi timu yake KRC Genk ikifungwa mabao 2-1 nyumbani na KAA Gent katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa Luminus Arena mjin Genk.

Samatta aliingia dakika ya 78 kuchukua nafasi ya kiungo Mspaniola, Alejandro Pozuelo Melero katika jitihada za kocha Mbelgiji Philippe Clement kuiongezea nguvu safu ya ushambuliaji wasawazishe mabao, mara baada ya Gent kufunga la pili.

Mabao ya Gent yalifungwa na Birger Verstraete dakika ya 11 na mshambuliaji Mnigeria Samuel Kalu dakika ya 77 na baada ya Samatta kuingia, Genk ikapata bao moja, lililofungwa na Leandro Trossard dakika ya 87.

Samatta leo amecheza mechi ya 78 tangu alipojiunga na Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Na katika mechi hizo, Samatta, mshambuliaji wa zamani wa Mbagala Market, African Lyon na Simba za Tanzania, amefunga mabao 22 kwenye mashindano yote.

Kikosi cha KRC Genk kilikuwa; Vukovic, Uronen, Colley, Aidoo, Maehle, Seck, Writers/Wouters dk45, Pozuelo/Samatta dk77, Ndongala/Trossard dk70, Buffalo na Karelis.

AA Gent; Kalinic, Gigot, Rosted, Verstraete, Chakvetadze/Kubo dk61, Yaremchuk/Janga dk23, Kalu/Christiansen dk80, Asare, Simon, Foket na Esiti.

Jinsi Ya Kumfanya Mwanamke Apagawe Kwako

$
0
0
Kuna vitu vingi ambavyo unaweza kutumia kwa manufaa yako ili kufanya wanawake wakuone unavutia. Amini usiamini, hivi vitu si lazima uwe tajiri wala uwe na urembo wowote. Mwanzo kati ya vitu hivyo vingi ni rahisi kuvitumia kwa urahisi. Hii hapa ni orodha ya mambo ambayo ukiyazingatia yatakufanya wewe uwe na mnato kwa mwanamke yeyote yule.

1. Uwezo wako wa nishati
Nishati inaweza kuwa na mkusanyiko wa vitu kadhaa, kama vile kuhisi kwa vipepeo ndani ya tumbo, kusuka, wasiwasi ama vitu tofauti kabisa. Kwa mtizamo wa moja kwa moja, nishati inahusiana na yote yale ambayo yanamfanya mwanamke kujiskia raha wakati anapokuona ama kutaka kuutumia muda wake mwingi akiwa na wewe. Nishati inacheza nafasi kubwa katika mapenzi kama wataka kumtongoza mwanamke na ufaulu kwa urahisi. Ili kupeana nishati zaidi kila wakati unapokuwa na mwanamke, hakikisha kile kikuu unachohitaji kufanya ni kumchekesha, kumsapraiz, umguse kwa bahati mbaya mara kwa mara, kuwa mwenye michezo nk. Zote hizo zitamfanya kukufikiria wewe mara 24/7.

2. Mbinu utakayoitumia kumsifu
Kulingana na utafiti kutoka NBC unadai ya kwamba wanawake wengi hawajiskii huru kupewa ama kupokea sifa kutoka kwa wanaume. Lakini usikatwe na tamaa! Vile ambavyo utampongeza mwanamke inaweza kucheza pakubwa kufaulu kumpata mwanamke unayempendae baada ya muda. Afterall ukimsifu kitofauti tofauti anaweza kukubali ama kukuona kama wewe ni mzaha kwake. So kuhepa aibu kama hizi ndogo ndogo, unafaa umsifu mwanamke kwa jambo ambalo ni la kwake pekee, yaani kitu ambacho utamsifu nacho hakipatikani kwa mwingine. Mfano waweza kumakinika kwa kitu ambacho anafanya wakati flani na utumie ujuzi wako wa kiume kumsifia na jambo hilo. Mfano unaweza kumsifu kwa uwezo wake wa kuimba, kuchora, mtindo wake wa kutembea nk. [Soma: Mbinu ya kutongoza kwa wale wanaojifunza]

3. Upambo wako
Si lazima uwe mwanamume wa kuvutia ili umvutie mwanamke. Utafiti umebainisha kuwa wanawake hawavutiwi na urembo wa mwanamume, nywele zake wala ngozi yake. Mwanzo kuwa mrembo kama mwanamume kuna ubaya wake mwingi ikizingatiwa kuwa unaweza kuonekana kama pleya ambaye unapendwa na wanawake wengi.

Kile ambacho unachohitajika hapa ni uhakikishe kuwa uwe nadhifu kimwili na mavazi yako. Kufanya hivi kutakusaidia wewe kuonekana mtu timamu halikadhalika inakufanya wewe kuwa na confidence ya kapproach demu yeyote yule.

4. Ujuzi wako wa kutangamana
Lazima atleast uwe na ujuzi ambao utakusaidia wewe kuweza kutangamana na wengine. Kama mwanamume lazima uwe na ujuzi ambao utakusaidia wewe kutangamana na wengine kwa urahisi. Hii inamaanisha kuwa lazima uwe na ujuzi flani wa kuongea na wanawake ndipo utakapojua jinsi ya kumfanya apagawe na wewe.

5. Kiwango chako cha kujiamini
Kitu cha mwisho ambacho ni muhimu kwako kuwa nacho ni kujiamini. Kujiamini ni njia moja wapo ya lazima uwe nayo ili uweze kuiteka hisia ya mwanamke yeyote yule.[Soma: Njia za kuwa na confidence kama mwanaume]

KUMBUKA: Vitu vyote tulivyoeleza hapo juu havitakuwa na manufaa yeyote yale iwapo kama hutaweza kujiamini kama mwanamume. Hivyo ni lazima kwako kuhakikisha kuwa mwanzo unajijenga kwa kuwa na confidence. Hii ni kuanzia kujitambua wewe mwenyewe bila kujishuku, kuongea bila woga wowote wala kutoingiwa na wasiwasi wakati wowote ukiwa karibu na mwanamke.

Tarehe / Siku Nzuri kwa Mimba Kuweza Kutungwa

$
0
0
Leo napenda nizungumzie jambo moja tu ambalo ni juu ya  jambo moja tu, nalo ni namna wanavyoweza kui-pin point siku ile ya kilele (i.e fruitful/productive/fertile day), hapa nina maana ya siku ile ambayo wao wanaiita siku ya 14.

Ikumbukwe kuwa wanawake wanatofautiana katika suala zima la urefu wa MENSTRAL CYCLE, yaani idadi ya siku kati ya period ya kwanza hadi ile ya pili inayofuatia. Kundi kubwa la wanawake wana fall kwenye range ya siku 22-35. Japo walio-normal wana siku 28. Vile vile kuna wengine huwa na menstral cycle mbili, yaani fupi na ndefu. Hivyo walio na menstral cycle fupi, mathalani wale wenye siku 22, huwa vilevile wana kipindi kifupi sana cha kutokwa na damu (period), yaani damu inaweza kukatika ndani ya siku 2 tu! Na wale wenye siku 35 au zaidi huwa wana kipindi kirefu sana cha kutokwa na damu (period) ambapo wengine huwachukua hata siku kati ya 5 hadi 8.

Hivo basi, kama wewe ni mwanaume inakubidi umwelewe vizuri mwenzi wako juu ya hayo niliyoyasema hapo juu ili ikusaidie kui-pin point ile fertile day (yaani siku ya mimba).

Swali: Je siku ya mimba ni ipi?
Jibu lisilosahihi: Watu wengi na hata baadhi ya wanasayansi wanafikiri siku ya mimba ni ile ya 14 baada  ya dalili za kwanza za damu ya hedhi! Wao huhesabu kuanzia siku ile damu ilipoanza kutoka hadi siku ya 14! Utaratibu huu ume-prove failure! Hii ni kwa sababu wanawake wana menstral cycle
zinazotofautiana kwa urefu. Hivo basi jibu sahihi ni hili hapa chini:

Jibu sahihi: 
1. Kwanza inabidi ujue kama mwenzi wako ana menstral cycle ipi? Fupi au ndefu, ama zote mbili?

2. Baada ya kujua urefu wa menstral cycle ya mwenzi wako then pin point siku ile ya mwisho halafu
uhesabu backwards siku 15 kuanzia siku ile ya mwisho. Siku hii ya 15 kuanzia mwisho ndiyo siku ya  mimba kwa mwanamke yeyote!

Once you know the '15th day' from the last one, then you can manoeuvre whatever you want to get her pregnant or to avoid pregnancy!

With this new approach of pin pointing the fertile day you will find that all women (menstral cycles)
are covered, whereas the old way of counting fits only to women whose menstral cycles are 28 days!


Naomba nitoe mifano hai kwa faida ya dada zetu na wengine:
1. Kama mwanamke ana menstration cycle ya siku 22 inabidi afanye kama ifuatavo: Kwanza
itabidi atengeneze kalenda yake mwenyewe ya siku zake zote za menstration cycle kama hapa
chini:

1st, 2nd, 3rd, 4th, 5th, 6th, 7th, 8th, 9th, 10th, 11th, 12th, 13th, 14th, 15th, 16th, 17th, 18th, 19th,
20th, 21st, 22nd.

Kisha ahesabu kuanzia ile 22nd day kurudi nyuma mpaka afikishe siku 15. Ataona kuwa siku ya
kumi na tano inaangukia kwenye 8th day ya kalenda yake. Hivo 8th day ndiyo siku ya mimba
kwa mwanamke yeyote ambaye ana menstration cycle ya siku 22. Akumbuke kwamba 1st day
ndiyo siku anayoanza ku-bleed!


2. Kama mwanamke ana menstration cycle ya siku 28 inabidi afanye kama ifuatavo: Kwanza
itabidi atengeneze kalenda yake mwenyewe ya siku zake zote za menstration cycle kama hapa
chini:

1st, 2nd, 3rd, 4th, 5th, 6th, 7th, 8th, 9th, 10th, 11th, 12th, 13th, 14th, 15th, 16th, 17th, 18th, 19th,
20th, 21st, 22nd, 23rd, 24th, 25th, 26th, 27th, 28th.

Kisha ahesabu kuanzia ile 28th day kurudi nyuma mpaka afikishe siku 15. Ataona kuwa siku ya
kumi na tano inaangukia kwenye 14th day. Inamaana kwamba 14th day ndiyo siku ya mimba
kwa mwanamke yeyote ambaye ana menstration cycle ya siku 28. Akumbuke kwamba 1st day
ndiyo siku anayoanza ku-bleed!


3. Kama mwanamke ana menstration cycle ya siku 35 inabidi afanye kama ifuatavo: Kwanza
itabidi atengeneze kalenda yake mwenyewe ya siku zake zote za menstration cycle kama hapa
chini:

1st, 2nd, 3rd, 4th, 5th, 6th, 7th, 8th, 9th, 10th, 11th, 12th, 13th, 14th, 15th, 16th, 17th, 18th, 19th,
20th, 21st, 22nd, 23rd, 24th, 25th, 26th, 27th, 28th, 29th, 30th, 31st, 32nd, 33rd, 34th, 35th.

Kisha ahesabu kuanzia ile 28th day kurudi nyuma mpaka afikishe siku 15. Ataona kuwa siku ya
kumi na tano inaangukia kwenye 21st day. Inamaana kwamba 21st day ndiyo siku ya mimba kwa
mwanamke yeyote ambaye ana menstration cycle ya siku 35. Akumbuke kwamba 1st day ndiyo
siku anayoanza ku-bleed!


4. Kama mwanamke ana abnormal menstration cycle ya siku 15 , BASI KUNAUWEZEKANO
WA KUTOPATA MIMBA KABISA KAMA INAVYOONEKANA HAPA CHINI:

Kwanza itabidi atengeneze kalenda yake mwenyewe ya siku zake zote za menstration cycle kama
kawaida:

1st, 2nd, 3rd, 4th, 5th, 6th, 7th, 8th, 9th, 10th, 11th, 12th, 13th, 14th, 15th.

Kisha ahesabu kuanzia ile 15th day kurudi nyuma mpaka afikishe siku 15. Ataona kuwa siku ya
kumi na tano inaangukia kwenye 1st day. Inamaana kwamba, the 1st day of her bleedind ndiyo
siku ya mimba kwa mwanamke yeyote ambaye ana menstration cycle ya siku 15. Akumbuke
kwamba 1st day ndiyo siku anayoanza ku-bleed, na ndiyo hiyo hiyo siku ambayo mwanamke wa
kundi hili anaweza kupata mimba!

Hii inamaana kwamba, siku ambayo linaharibika lile yai la upande mmoja ndiyo siku hiyo hiyo
ambayo yai la upande wa pili linapevuka tayari kwa kurutubishwa. Mwanamke wa aina hii
anaweza kupata mimba tu kama atakutana na mwanaume siku ile anayoanza kubleed, kwani siku
ambayo yai moja linaanza kuharibika ndio siku hiyo hiyo ambayo yai la upande wa pili
linakuwa tayari kurutubishwa!

Na wanawake wa kundi hili la nne ukiwauliza vizuri watakiri kwamba hawajawahi kuona au ku-feel ule ute mweupe ambao wenzao huwa wanaupata siku ile yai linapokuwa tayari kwa
kurutubishwa, kwani ute wa wanawake wa kundi hili la nne huwa unachanganyikana na damu
kwa vile unatoka siku ile ile wanapoanza ku-bleed. Pia wanawake wa kundi hili huwa
wanatokwa na kiasi kidogo sana cha damu; na bleed hukatika ndani ya siku moja au mbili tu!

Jambo la kushangaza ni kwamba, wanawake wengi hawana knowledge ya kutosha juu ya hili
suala la siku ya mimba; hasa wale ambao wana menstration cycle inayobadilikabadilika! Wao
husitukia tu wameanza ku-bleed. Ndo maana hawawezi hata ku-plan kutopata mimba! Hawana
ujanja kabisa ndio sababu wengi wanatumia sindano na njia zingine nyingi za artificial ambazo
mwisho wa siku huwaletea matatizo ya uzazi, kwani nyingi hu-block njia ya uzazi! Nimeona
wengi wenye matatizo ya uzazi unaosababishwa na hizi artificial family planning. Wengine
hulazimika kwenda hospital kuzibuliwa ili wapate mimba jambo ambalo ni hatari kwa afya zao!
Full maelezo ya kujitosheleza, ukikosa kudaka au kudakisha mimba basi kuna walakini...

Magufuli Aanika Siri Kutosafiri Nje ya Nchi, Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya March 12

$
0
0


Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya March 12

Mama Kanumba Afanya Yeke Sendi ya Mabasi

$
0
0
MAMA wa aliyekuwa mwigizaji kinara wa Bongo Movies, marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa, kama kawaida yake ameangua kilio cha nguvu kwenye Stendi ya Mabasi ya Segerea jijini Dar, baada ya kuona bango kubwa la mwanaye huyo kwenye duka moja eneo hilo.

 Akizungumza na gazeti hili kwa uchungu, mama huyo alisema kuwa, siku hiyo alikuwa anakwenda kurekodi filamu maeneo ya Segerea na alipofika kituoni hapo, alishuka kwenye basi ndipo ndipo akakutana uso kwa uso na picha kubwa ya mwanaye huyo.

 “Kila mara naziona picha za Kanumba kwenye mabango, lakini sijui ni kwa nini hii nilipoiona, imenifanya niishiwe nguvu,” alisema mama huyo.

Na Imelda Mtema

JPM: Mimi ni Jiwe Kweli Kweli, Sitishwi Wala Sitishiki

$
0
0
Rais Dkt. John Pombe Magufuli amesema uwepo wake madarakani ni kutaka kuwatoa Watanzania katika shida mbalimbali walizokuwa nazo na kuwapelekea hali amayo wataishi kwa raha ili siku atakapokuja kufa basi hata Mungu ampe nafasi ya kuwaongoza Malaika mbinguni.

 Magufuli ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Mkoa wa Singida wakati wa kuzindua kiwanda cha mafuta ya Alizeti, Mount Meru Millers kilichojengwa mkoani humo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John P. Magufuli akiombewa na viongozi wa Kidini kutoka Singida mara baada ya kufungua kiwanda cha usindikaji wa Alizeti hii leo – Machi 11, 2018,

“Nataka niwahakikishie Watanzania kuwa mna Rais kweli kweli, jiwe kweli kweli. Sitishwi wala sitishiki, mimi jukumu langu ni kuhakikisha nawavusha Watanzania kutoka kwenye shida na kwenda mahali kwenye raha.

 “Ninajua hiyo ndio itakuwa sadaka yangu kwa Watanzania ili kusudi hata siku moja nikienda huko mbinguni, kutokana na mimi kuwa kiongozi mzuri, Mungu atakaponihitaji akanichague niweze kuongoza Malaika polepole kwa sababu ninajua kuna maisha mengine baada ya maisha ya hapa duniani”, amesema Magufuli.

Pamoja na hayo, Rais amewaomba sana viongozi wa dini, masheikh na wale watu mbalimbali katika imani zao tukuitanguliza Tanzania kwanza, huku akiwataka wasitumike. Amewataka wananchi kufanya kazi kwa bidii ili waweze kujikomboa na kujiongezea kipato cha maisha.

Serikali Yaiunda Upya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali

$
0
0

Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi amesema Serikali imefanyia mabadiliko Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kuanzisha Ofisi nyingine mbili mpya kwa lengo la kuongeza Tija na Ufanisi katika utendaji kazi.

Prof Kabudi alikuwa akizungumza na watendaji wa Wizara na Taasisi zinazounda sekta ya Sheria nchini makao makuu ya Wizara mjini Dodoma ambao wanakutana mjini humo kujadili na kuandaa makadirio ya Bajeti ya Wizara na Taasisi zake.

Prof. Kabudi amesema uundwaji wa Ofisi mbili mpya za Ofisi ya Taifa ya Mashitaka na Ofisi ya Wakili Mkuu unafanya sasa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kubaki na jukumu lake la msingi la kuishauri Serikali katika masuala yote ya kisheria, kufanyia uhakiki mikataba ya kitaifa na kimataifa na kuratibu wanasheria wote walioko katika Wizara, Idara za Serikali zinazojitegemea, Wakala, Mamlaka, Mashirika ya Umma na Serikali za Mitaa.

Amesema Ofisi ya Taifa ya Mashitaka sasa itajikita katika uendeshaji wa mashitaka ya jinai mahakamani ikiwa na wanasheria wake wakati Ofisi ya Wakili Mkuu kupitia wanasheria wake itajikita katika uendeshaji wa mashitaka ya madai ya kitaifa na kimataifa, utatuzi wa migogoro kitaifa na kimataifa na ushughulikiaji wa mikataba ya kitaifa na kimataifa ambayo taasisi za umma zinaingia kwa niaba ya nchi.

Amewataka watumishi wa umma ambao ni wanasheria kuwa tayari na kujipanga kutokana na mabadiliko hayo ambayo yatasababisha uhamisho wa kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine ili kuyatekeleza kwa vitendo yale yote yanayotarajiwa kupatikana baada ya mabadiliko hayo.

Amesema serikali imefikia uamuzi huo ili kuweza kufanikisha azma ya kuwaweka pamoja wanasheria wote na kuwaratibu ili kujua nani yuko wapi na anafanya nini n a kuongeza kuwa wanasheria hao sasa watawajibika kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye atakuwa na jukumu la kumpeleka mwanasheria yoyote atakayemuona anafaa kufanikisha jambo jema la Serikali.

“Wakuu wa Idara na Vitengo vya Sherioa katika mashirika makubwa ya umma na ambayo Serikali imetoa mabuiloni ya fedha zake ili kuyaendesha wataangaliwa na mwanasheria mkuu na kama akionekana hakamilishi lengo la kuwepo katika ofisi husika basi mara moja atapelekwa mwingine mwenye uwezo wa kuisadia Serikali,” alisema Prof Kabudi.

Akizungumza katika kikao hicho Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Alderaus Kilangi amewataka watendaji wa ndani ya Sekta ya Sheria kufanya kazi kama timu moja ili kuweza kurejesha imani ya wananchi kwa wataalamu wa sekta hiyo ambayo inapaswa kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya Taifa.

“Niwaombe wanasheria wenzangu tuwe timu moja na tufanye kazi zetu kwa weledi na ufanisi mkubwa ili kuhakikisha maendeleo ya kweli ya nchi yanafikiwa, ni kweli kama sekta tulianza kupoteza mwelekeo, tuyachukulie maboresho haya ya miundo ya Ofisi zetu kama chachu ya kuleta tija na ufanisi katika kazi zetu,” alisisitiza

Mkutano huo ulihudhuriwa na watendaji wa Wizara ya Katiba na Sheria, Mahakama ya Tanzania, ofisi ya Mwendesha Mashtaka, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Tume ya Kurekebisha Sheria,Wakala wa Ufilisi na udhamini (RITA), Tume ya Utumishi wa Mahakama, Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo( Law School) Chuo cha Uongozi wa Mahakama
Lushoto.

Kutana na Mtatibu Mongwa Mganga wa Waganga Sasa Tupo Mikoa Karibu Yote Nchi Kukusaidia Wewe

$
0
0
KUTANA NA MTABIBU MONGWA MGANGA WA WAGANGA SASA WAKO MIKOANI KARIBU YOTE NCHINI...
.
HIVYO WATATOA TIBA MAENEO YOTE YA MBEYA ,DODOMA, IRINGA , MOROGORO, MWANZA,ZANZIBAR

==>KWA WALE WENYE KUHITAJI TIBA

Husafisha nyota na kutoa Pete za bahati na kwawale walio sumbuka kwaajili ya matibabu na hawakufanikiwa chochote sasa njoo ujionee miujiza hapo kwahapo bila malipo yoyote malipo baada yakazi napia humpa mtu jini la mali kwayule anaye taka kumiliki bila mashariti yoyote
Tunatibu magonjwa mbalimbali yaliyo shindikana mpenzi aliye kukimbia nakumrudisha kwa masaa 24 tu napia natoa dawa za nguvu za kiume kuurefusha uume paka pale unapotaka .
Natoa dawa za biashara na mvuto ==tunatoa dawa zauzazi kwa wale kina mama wenye matatizoya uzazi walio angaika kwa muda mrefu bila kupata mafanikio yoyote njoo umalize tatizo lako sasa
Natoa mazindiko yanyumba na mwili biashara na mvuto kazini
Kupandisha nyota ili kungaa kupandishwa cheo kazini kurudisha mali zilizo pote zilizo ibiwa kuzulumiwa
Kesi zilizo shindikana uzimaliza mara moja namengine mengi ya siri piga simu

+255 764291657

Kwa Kipigo Hiki! Wenger Atabaki?

$
0
0
Arsenal imefanikiwa kuiadhibu Watford magoli matatu. Kipigo hiki kinaipa Arsenal nafasi nzuri ya kurudi michuano ya Yuropa hapo mwakani. Shukrani za Pekee zimwendee Petr Cech aliyefikisha rekodi ya kutokufungwa katika michezo 200 ya ligi kuu baada ya kuokoa mkwaju wa Penalti Troy Deeney.

Piere Aubameyang alimpiga chenga golikipa na kuiandikia Arsenal bao la pili. Henrekh Mkhtaryan alifunga goli la tatu na kuipa Arsenal uhakika wa ushindi.
Hii ni Penati ya kwanza kwa Petr Cech kuokoa tokea mwaka 2011. Mara ya mwisho alidaka Penati dhidi ya Fulham. ni penati yake kwa 16 akiwa na Arsenal na ni penati ya kwanza akiwa kama mchezaji wa Arsenal.

Ozil amekuwa mchezaji wa kwanza kufikisha asisti 50 kwa haraka zaidi akiwa amecheza michezo 141 na kuvunja rekodi ya Eric Cantona aliyecheza michezo 143. Huu ni ushindi wa 700 kwa Arsene Wenger katika michezo 1222. Kufikia hapo Arsenal wamebakiza alama 10 ili kwenda Top Four licha ya kucheza mechi nyingi zaidi.

Kituko kikubwa ni mashabiki wa Arsenal kususia mchezo kwa kile wanachodai ni kutofurahishwa na mwenendo wa matokeo mabovu ya klabu hiyo. Mashabiki walio wengi wameonekana kuchoshwa kabisa na Arsene Wenger wakimtaka aachie hatamu kwa ajili ya mwalimu mwingine.

Tatizo kubwa mashabiki wa Arsenal wamekuwa na kusumba ya kukosa msimamo hasa pale timu yao inapopata matokeo chanya husahau vilio vyao. Je awamu hii watakubaliana na Wenger? Hasa baada ya kutoa kichapo kwa Ac milan ugani sansiro?

Dah kumbe Michael Ballack alikuwa ananuka hadi akawa anakimbiwa uwanjani

$
0
0
“Dunia ina mambo” ndivyo unavyoweza kuanza kusema kutokana na madai yaliyotolewa na golikipa wa zamani wa timu ya taifa ya Paraguay kuhusu kiungo wa zamani wa Chelsea na timu ya taifa ya Ujerumani Michael Ballack.

Sijui ni chuki kutokana na kuondolewa na Wajerumani katika kombe la dunia 2002 au ni kweli lakini Jose Luiz Chilavert amedai ya kwamba kati ya sababu kubwa wachezaji walikuwa wakimhofia Ballack ilikuwa harufu.

Chilavert amesema ni kweli Ballack alikuwa na nguvu sana uwanjani lakini hilo silo kubwa lililokuwa likifanga wachezaji wengine wamhofie, lakini ukweli ni kwamba Michael Ballack alikuwa akitoa harufu kali sana mwilini.

Akiongea na kituo cha ESPN Chilavert aka Bulldog amesema kwamba ulikuwa ukimkaribia Ballack unasikoa harufu ya malimao limao na vitu ambavyo vilikuwa na harufu kali sana hadi unakosa raha.

Hii ilikuwa ikiwakera sana haswa viungo wa Paraguay na ndio sababu Ballack alionekana bora dhidi yao kwa kuwa walikuwa hawamsogelei kabisa na Chilavert anadhani labda hii ilikuwa mbinu ya Ballack.

Chilavert ameichezea Paraguay michezo 74 kuanzia mwaka 1989 hadi mwaka 2003 lakini golikipa huyj ndio mlinda lango namba mbili mwenya mabao mengi(67)lakini ndio mlinzi pekee ambaye amewahi kufunga hattrick, ilikuwa 1999 wakati akiichezea Vélez Sarsfield.

Dawa Bora za Nguvu za Kiume na Kukosa Hamu ya Tendo la Ndoa

$
0
0
DAWA BORA ZA NGUVU ZA KIUME NA KUKOSA HAMU YA TENDO LA NDOA
Baada ya utafiti wa muda mrefu juu ya matatinzo ya upungufu wa nguvu za kiume na ukosaji wa hamu ya tendo la ndoa ama kushindwa kurundia tendo kwa haraka Sasa inakuletea suluhisho juu ya matatizo haya kwa kutumia dawa za FULL POWER

Full Power dawa asili yenye vidonge inayotibu tatizo la upungufu au ukosefu wa nguvu za kiume dawa hii inamchanganyiko wa kutosha kuzalisha vichocheo vingi vya hernone za gestro gen zikiwemo vitamin b6 na b1 vitamin e pamoja na madini aina ya zinc

Itakufanya kuwa na nguvu na mzunguko mzuri wa damu na kuongeza hamu na uwezo wakufanya tendo la ndoa zaidi hatua nne au zaidi na kuchelewa kufika kileleni zaidi ya dakika 20/30 ZAT 50

Inarundisha maumbile ya uume yaani kurefusha na kunenepesha nchi 3/7 na upana cm 3/4 standard.kiafya haijalishi umri wako hata kwa wazee ukitumia maumbile yatabaki kuwa hivyo siku zote pia anatibu matatizo mengine kama presha kisukari ngiri chango la tumbo kujaa gesi kutopata choo vizuri minguu kuwaka moto matatizo ya uzazi bawasili na magonjwa ya zinaa kama kisonono na kaswende

Tunapatikana Dar es Salaam  na mikoan wasiliana na DR Oshinda no 0755505099 au 0714126118  Karibuni kwa hunduma bora

Chege Apata Mtoto wa Kike

$
0
0


Chege Apata Mtoto wa Kike MSANII Mkongwe wa Bongo Fleva, Saidi Juma Hassani maarufu kama Chege Chigunda amepata mtoto wa kike baada ya mkewe anayefahamika kwa jina la Zahra kujifungua salama salimin jana.

Mkali huyo wa ngoma ya Runtown amebainisha hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram baada ya kuweka picha na mkewe huyo na kui-tag akaunti mpya ya mwanaye huyo aliyempa jina la Jadah.

Watu 16 Wapoteza Maisha Baada ya Kupigwa na Radi

$
0
0
Watu 16 Wapoteza Maisha Baada ya Kupigwa na Radi
Watu 16 wamepoteza maisha nchini Rwanda baada ya kupigwa na radi wakiwa kanisani katika wilaya ya Nyaruguru iliyo Kusini mwa nchi hiyo.


Watu wote 140 waliokuwa katika kanisa hilo walipelekwa hospitali, lakini wengi waliruhusiwa kurudi nyumbani, isipokuwa watatu ambao bado wako katika hali mahututi.

Meya wa wilaya ya Nyaruguru Habitegeko Francois, amesema kuwa siku moja kabla, Radi nyingine ilikuwa imepiga kundi la wanafunzi 18 katika wilaya hiyo, na kuuwa mmoja wao.

Nkurunzinza Atangazwa Kuwa Kiongozi wa Milele

$
0
0
Nkurunzinza Atangazwa Kuwa Kiongozi wa Milele
Leo March 12, 2018 taarifa kutokea nchini Burundi katika Chama tawala cha CNDD/FDD ni kuwa kimemtangaza Rais wa sasa wa taifa hilo  Pierre Nkurunzinza kama kiongozi mkuu wa kudumu au kiongozi wa milele ndani ya chama hicho.

Uamuzi wa kumtangaza Nkurunzinza umefikiwa baada ya vikao vya siku tatu vilivyofanyika katika eneo la Buye mahali anapozaliwa Rais Kaskazini mwa Burundi

Uamuzi huo pia unachukuliwa wakati Burundi inajiandaa kufanya marekebisho ya katiba ili kumruhusu Rais Nkurunzinza kuendelelea kuongoza taifa hilo hadi mwaka 2034.

Taarifa ya chama cha CNDD/FDD imesema vikao vimekubaliana kuimarisha chama tawala na taasisi zake.

Naibu Katibu Mkuu wa Bavicha Ajiuzulu Wadhifa Wake

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Bavicha Ajiuzulu Wadhifa Wake
Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), Gertrude Ndibalema amejiuzulu wadhifa huo kuanzia jana Machi 11,2018.

Gertrude aliyeshika wadhifa huo tangu mwaka 2014 ametangaza kujiuzulu kupitia taarifa kwa umma akidai anabaki kuwa mwanachama ili kutimiza majukumu yake binafsi.

Akizungumza na Mwananchi leo Machi 12,2018 Gertrude amesema, “Ni kweli nimeamua kuachia nafasi yangu ili kutimiza malengo ya shughuli zangu binafsi.”

“Kwa kuwa nakipenda chama changu na kwa taaluma yangu (mawasiliano kwa umma) ili kuepuka mgongano, nimeamua kukaa pembeni ili kutimiza azma yangu na nitabaki kuwa mwanachama,” amesema.

Gertrude ni kiongozi wa pili wa ngazi ya juu Bavicha kujizulu akitanguliwa na aliyekuwa mwenyekiti wa baraza hilo, Patrobas Katambi aliyejiunga na CCM.

Mavazi ya Wanafunzi wa Shule za Yamtoa Machozi Snuna " Natamani Siku Zirudi Nyuma Nami Nipate Elimu"

$
0
0
Mavazi ya Wanafunzi wa Shule za Msingi Yamtoa Machozi Snuna
STAA wa miondoko ya mduara Bongo, Snura Mushi amefunguka kuwa amejikuta akizitolea macho sare za wanafunzi wa sekondari baada ya kuishia kuvaa za shule ya msingi kutokana na uwezo duni waliokuwa nao wazazi wake.


Snura au Mamaa Majanga aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, huwa anawaasa wasichana kwamba wamepata fursa ya kusoma, watumie nafasi hiyo kwa sababu yeye hakubahatika kabisa kukanyaga sekondari wala kuvaa sare hizo, jambo ambalo linamfanya sasa hivi atumie nguvu ili wanaye wapate elimu.

“Kiukweli nikiona wasichana wamevaa sare za sekondari huwa ninazitolea macho sana. Natamani siku zirudi nyuma ili nami nipate elimu hiyo,” alisema Snura aliyeishia darasa la saba.

Yanga Kumuondoa Simba Kileleni?

$
0
0
Yanga Kumuondoa Simba Kileleni?
Klabu ya Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga imewataka mashabiki zake na wapenzi wa mpira wa miguu kujitokeza kwa wingi leo uwanja wa Taifa ili waweze kushuhudia jinsi wanavyochukua alama zao tatu dhidi ya Stand United.


Hayo yameelezwa na mlinzi wa nyuma upande wa kulia wa wanajangwani Juma Abdul muda mchache alipomaliza kufanya mazoezi kwa ajili ya kuelekea mchezo wao wa Ligi kuu unaotarajiwa kuchezwa katika dimba la Taifa Jijini Dar es Salaam.

"Kwanza tunamshukuru Mwenyezi Mungu tumeweza kumaliza salama mazoezi kwa siku ya leo ila kikubwa tunachoweza kusema tunawaomba mashabiki wa Yanga SC kesho waweze kujitokeza kwa wingi. Wao wanaojitokeza kwa wingi sisi ndio inatupa hamasa na kuweza kufanikisha katika mchezo wetu dhidi ya Stand United", amesema Juma Abdul.

Pamoja na hayo, Abdul ameendelea kusema "ubingwa unawezekana hakuna kukata tamaa, pointi tatu leo kama kawaida".

Timu ya Yanga inashuka dimbani ikiwa imeshika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi kuu kwa alama 43, Azam FC imeshika nafasi ya pili kwa pointi 44 baada ya kufanikiwa kumchapa Mbao FC siku ya jana kwa mabao 2-1 huku Simba SC akiwa ameshikilia usukani mpaka dakika hii kwa alama 46 ambapo leo hii kuna hati hati ya kunyanganywa kijiti hicho na Yanga SC endapo watafanikiwa kuwaburuza Stand United.

Simba Kuondoka Jumatano Kwenda Misri kwa Mchezo wa Marudiano

$
0
0
Kikosi cha Simba kinatarajia kuondoka nchini kuelekea Misri kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Masry SC, Jumatano ya wiki hii.

Simba itaondoka Jumatano hii ya Machi 14 2018 ikiwa na kumbukumbu za kulazimishwa sare ya mabao 2-2 kwa mawili, hivyo itakuwa na kibarua kigumu ugenini.

Matokeo iliyoyapata Simba awali, sasa inapaswa kwenda kupata ushindi wa bao moja bila majibu ama zaidi ya hilo moja ili kujiwekea nafasi ya kusonga mbele kwenye mashindano hayo.

Katika mchezo wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, Bocco na Okwi ndiyo walikuwa wafungaji wa mabao ya Simba yaliyofungwa kwa njia ya adhabu ya penati.

Mechi hii ya marudiano itapigwa Jumamosi ya wiki hii, Machi 17 2018 kwenye Uwanja wa Port Said huko Misri.

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Jumatatu

Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images