Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104415 articles
Browse latest View live

Napenda Kuangalia Maumbo ya Wanawake Ila Sichepuki- Davido

0
0
Napenda Kuangalia Maumbo ya Wanawake Ila Sichepuki- Davido
Msanii wa muziki kutoka nchini Nigeria, Davido amesema kuwa ni moja ya wanaume ambao huwa wanavutiwa kuangalia maumbo na uzuri wa wanawake lakini cha ajabu hajawahi kumsaliti mchumba wake Chioma.

Davido kupitia ukurasa wake wa Snapchat amethibitisha hilo kwa kusema kuwa huwa anapenda sana kuangalia wanawake hususani maumbo yao lakini cha ajabu hajawahi kumsaliti Girlfriend wake.

“Sijawahi kuchepuka ila napenda kuangalia kila sketi (Mwanamke) inayopita mbele yangu, Mimi sio mwanaume msaliti napenda sana kufanya mapenzi na Chioma,“ameandika Davido kwenye ukurasa wake wa SnapChat.

Ijumaa ya wiki iliyopita mchumba wake na Davido, Chioma aliandamwa na skendo mitandaoni nchini Nigeria kuwa anamsaliti Davido.

Hata hivyo Davido siku hiyo hiyo ya Ijumaa baada ya kuzagaa kwa skendo za kusalitiwa na Chioma aliposti picha akiwa naye kitandani kuudhihirishia umma kuwa hajali maneno ya walimwengu.

Dogo Janja- Mke Wangu Kanifanyia Make Up na Kunivesha

0
0
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Dogo janja ambaye sasa hivi ameachia video ya wimbo wake mpya wa 'Wayu wayu' na kuacha gumzo kwa mashabiki kwa kuvaa uhusika wa mwanamke, na kusema kuwa mke wake ndiye alimfanya awe hivyo.


Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Dogo Janja amesema mke wake ambaye ni muigizaji wa filamu za bongo, Irene Uwoya, ndiye alianza kumfanyia make up wakiwa mapumzikoni Zanzibar, na kumvalisha vitu vya kike, ndipo walipopata idea ya kufanya video akiwa kama mwanamke.

“Mke wangu kabla sijaanza kushoot alianza kunifanyia make up na kunivesha vesha tulipokuwa vacation (mapumzikoni) Zanzibar, akawa ananicheka, mpaka siku tunaenda kushoot ile make up ilibidi anifanyie yeye lakini ilitokea dharula hakuwepo, akaniambia niende kwa mtu anifanyie make up ya nude mimi hata siijui, hata lile wigi alinipa mke wangu na mimi nikapita nalo”, amesema Dogo Janja.

Kitendo cha Dogo Janja kuigiza kama mwanamke kimeonekana kuwakwaza watu wengi wakisema sio kitu kizuri mwanaume kuvaa hivyo na kujipodoa kama mwanamke, lakini kwa upande wake amesema ilikuwa ni ubunifu kwa lengo la kuboresha kazi.

Watu Waofiwa Kufa Baada ya Ndege Kuanguka na Kuwaka Moto

0
0
Watu Waofiwa Kufa Baada ya Ndege Kuanguka na Kuwaka Moto
Ndege ya shirika la ndege la US-Bangla iliyokuwa imebeba abiria 67 na wafanyakazi wanne imeanguka na kuwaka moto ilipokuwa inataka kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kathmandu.

Maofisa wamesema wamefanikiwa kutoa miili kadhaa na majeruhi kutoka kwenye mabaki ya ndege hiyo ya Bangladesh. Ndege hiyo ilikuwa inatokea Dhaka, Bangladesh ilipoanguka kwenye uwanja wa mpira ambao upo karibu na uwanja wa ndege.

Msemaji wa serikali hakuweza kutaja idadi lakini alisema waliokufa na majeruhi wameondolewa kwenye mabaki ya ndege hiyo. Ofisa mwingine aliliambia shirika la habari la AFP kwamba watu 20 walijeruhiwa na walipelekwa hospitalini.

Miali ya moshi mzito na moto iliweza kuonekana kutoka kwenye uwanja wa mpira ambako ndege iliangukia mashariki mwa sehemu ya kukimbilia ndege katika uwanja pekee wa kimataifa mjini Kathmandu.

"Polisi na jeshi wanajaribu kukatakata mabaki ya ndege katika juhudi za kuokoa wengine," alisema msemaji wa uwanja wa ndege Prem Nath Thakur.

Picha zilizorushwa kwenye mtandao wa Facebook zinaonyesha miali ya moshi mzito ikipanda juu nyuma ya sehemeu ya ndege kukimbilia, ambako ndege nyingine ilikuwa imesimama.

Huu Hapa Ukweli Mchungu Kwa Wadada Wanaolalamika Hawana Bahati za Kuolewa....

0
0
Wanaume wengi hawajafikia ndoto zao, wanatamani kupata wanawake watakaowatia moyo kuwafikisha kwenye ndoto zao! Ukweli mchungu ni kwamba wanawake hawawataki wanaume ambao bado wako safarini kuelekea ndoto zao! Wanataka waliokwisha fika, na bahati mbaya zaidi waliokwisha fika wako 'occupied !! Linalotokea ni nini? Wanawake wanadhani wana bahati mbaya?

Unaweza kuwa unalalamika kuwa una mkosi WA kuolewa yaani kila mwanaume anakuja na ahadi nzuri, baadae anakuacha! Lakin upande mwingine huenda maamuzi yako ndiyo maumivu yako.

Kweli huenda we ni mtoto WA kike mzuri wa sura umbo na hata kila kitu ila umenyimwa hekima!

Una mpaparikia kijana mtanashati kisa ana gari na kazii nzuri. Unamwona kijana anaeenda kumbi za usiku ndo mjanja..anae vaa suruali chini ya makalio ndo sahihi kwako lakini yule anaeenda ibada kila ijumaa au jumapili unamwona mruga ruga tu!

Una mpuuza Na kumdharau mtu 'A' kisa tu yeye ni kijana aliye soma ila hana ajira. Ama ni kijana ambae kipato chake hakizidi laki 2 kwa mwezi badala yake una mkumbatia mtu 'B' ambae ni baba fulani na ni mume WA Fulani kisa tu anapesa na shida zako zote anakutatulia...!!

SWALI!!
Utaolewa vipi ikiwa mpaka sasa unapenda toka na waume za watu au vijana wenye magari ya mikopo, au kijana yeyote ambaye unajua huna future naye? Au ndo unam'please ili asiache kukupa pesa!? Nani atakae KUOA wakati vijana wanaotafuta mke wewe una wasema vibaya kuwa hawana hadhi ya kutembea na wewe kisa hawana misuli ya uchumi kwa muda huo?

Funguo ya NDOA utaipata wapi wakati hapo ulipo una mnunia mke wa mtu kisa una toka na mume wake?

DADA maisha yanabadilika mwanaume mpiga debe wa Leo kesho unaweza mbadilisha akawa dereva kisha akamiliki gari lake...hakuna MTU aliye zaliwa kuwa masikini ndo maana juhudi zinahitajika...Mwanaume anae tumia pesa kukufanya uwe wake anafanya hivyo kwa wengi ila usijifanye hujui kisa unafaidika jua muda unaenda.

Weka malengo mbele lini unatamani uwe na ndoa na umri gani uzae kuliko anasa. Mwaka WA ngapi huu bado unatoka na wanaume ambao hawana malengo ?

Ombea Mumeo Asifanikiwe na Kuwa Tajiri...Ugumu wa Maisha Ndio Unamfanya Akupende

0
0
Kwa jamii zetu za kiafrika nilikua nikiamini kwamba familia yenye amani,furaha na upendo ni ile yenye mafanikio na uhuru wa kifedha. Ila kadiri ninavyozidi kukua najiona sikua sahihi pale ninapoona mambo yanayotokea kwenye jamii yangu. Wanawake wengi ambao waume zao wana fedha wanalia na kusaga meno.

Binti ikitokea mumeo anakupenda na kukujali basi ombea sana hiyo mbuzi isifanikiwe,kwani tabia halisi ya mwanaume huonekana pindi anapopata fedha. Unaweza ukadhani anakujali kumbe ni ugumu tu wa maisha ndio unaomfanya awe mnyenyekevu kwako ila hela zikimchanganyia my dear utalazwa chini na kimada atalala kwenye kitanda chako.

Nimeshuhudia wanaume waliooa wakiwa na "official michepuko" yani mtu kafunga ndoa kwenye nyumba ya ibada ila ana binti pembeni ambae familia na mkewe wanamjua na anafanya makusudi kwa kua ana fedha na familia inamtegemea yeye.

Kwa tabia hizi blaza usitegemee hata siku moja kusikia mkeo akikuombea ufanikiwe zaidi kwa sababu anajua fika ya kwamba hatua moja zaidi ya mafanikio ni sawa na wewe kuongeza mwanamke mwingine wa nje official hivyo siku zote maombi yake yatakua ni kukuombea ili ufilisike na heshima kwa mkeo na familia irudi.

Ukimheshimu mkeo na familia yako basi waheshimu katika hali zote. Usijione wewe ndio master planner ukadhani mafanikio uliyo nayo ni juhudi zako pekee. Hakuna kisicho na manufaa duniani kwani hata saa mbovu hua sahihi mara mbili kwa siku.

Dada Jifunze Alafu Badilika Namna Unavyojiweka

0
0



  • Jinsi unavyojiweka ndivyo watu watakavyokuchukulia. Mavazi unayovaa, marafiki ulionao na hata tabia yako kwa ujumla.
  • Mabinti wengi wanafeli sana kwenye eneo la mavazi, mavazi ya kuacha maungio ya ndani wazi yanawashushia heshima mabinti wengi sana bila wao kujua, wengi wanaona kama wanaenda na wakati lakini wanajidhalilisha.
  • Hakuna mwanaume anayependa kuoa mwanamke asiyejiheshimu, kama yupo basi hatakuwa muaoji. Mwanaume gani anayependa kutembea na mkewe akiwa maziwa yapo wazi yananing'inia kama yanataka kuanguka? Sketi fupi mapaja yote yapo wazi na tena ina mpasua? Suruali imembana mpaka maumbile ya ndani, michirizi ya nguo ya ndani inaonekana.
  • Sidhani kama kuna mwanaume anayependa mwanamke ambaye mwili wake ni maonyesho ya saba saba, Sidhani kama kuna mwanaume anayependa kuwa na mwanamke ambaye hata nyumbani kwao hana ujasiri wa kumpeleka, Sidhani kama kuna mwanaume anayependa kuwa na mwanamke ambaye starehe yake ya usiku na Mali yake ipo wazi kwa marafiki zake na watu kama Mali ya umma.
  • Niwasaidie dada zangu,ukivaa mavazi ya ajabu ajabu utavutia Wanaume wa kulala na wewe na kukuacha na si waoaji, utakuwa ni kiburudisho cha usiku mmoja na si mwanamke wa maisha.

Yanga yatoa dozi kwa Stand United, yaifikia Simba kileleni

0
0
Mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Dar es Salaam Young Africans imefanikiwa kupata pointi tatu muhimi dhidi ya timu ya Stand United baada ya kuchomoza na ushindi wa mabao 3 – 1 mchezo uliyopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mabao ya mabingwa hao watetezi yamefungwa na Mhilu na Ajibu katika kipindi cha kwanza na Obrey Chirwa akihitimisha mabao matatu kipindi cha pili huku kwa upande wa Stand United likifungwa na Vitalis Mayanga.

Kwa matokeo hayo unaifanya Yanga SC kuwa na jumla ya alama 46 sawa na vinara Simba SC wakiwa na tofauti ya magoli ya kufungwa na kufunga.

Wakili Jebra Kambole Ashindwa Kuonana na Abdul Nondo Mwanafunzi Aliyepotea na Kujikuta Iringa

0
0

Mwanasheria Jebra Kambole na Wakili wa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo amefunguka na kusema kuwa mpaka sasa ameshindwa kuonana wala kuongea na mteja wake huyo ambaye anashikiliwa na jeshi la polisi.

Akiongea na www.eatv.tv Wakili huyo amesema kuwa amejaribu kufika ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) ili kujua hali ya mteja wake pamoja na kuweza kuongea naye lakini ameshindwa.

"Mpaka sasa sijafanikiwa kuzungumza wala kumuona kwa sababu mara ya mwisho wakati tunafanya mazunguzo na DCI ambaye ana mamlaka juu ya hilo kwa sababu Abdul Nondo alikuwa anashikiliwa ofisini kwake mpaka dakika ya mwisho, tulipokwenda ofisini kujaribu kumuona akasema sisi huyu mtu tunamshikilia kama kama mlalamikaji lakini siyo kama mtuhumiwa kwa hiyo nyinyi kama Mawakili hamtakiwi kumhoji ila tukiona kwamba huyu mtu ni mtuhumiwa basi tutawaita muweze kuongea naye na kusikiliza maelezo yake, sisi tulimweleza tunahitaji kumuona ili tuweze kujua afya yake ili tuweze kurejesha mrejesho kwa familia na Watanzia wengine kwa ujumla ambao wanahofia juu ya usalama wake akasema yupo salama" alisema Kombole

Aidha Wakili huyo aliendelea kudai kuwa mpaka sasa Abdul Nondo anashikiliwa kinyume na sheria kwa kuwa sheria ya makosa ya jinai haitoi ruhuusa kwa jeshi la polisi kumshikilia mlalamikaji.

"Anayeshikiliwa ni mtuhumiwa lakini mpaka siku ya leo hajaachiwa kama ni mtuhumiwa kweli kwa sababu mtu ambaye anakwenda kutoa taarifa polisi anaachiwa arudi nyumbani huwezi kushikiliwa huko polisi na kwa kuwa wao wanasema wanamshikilia ana haki ya kupata uwakilishi kwa sababu kwa mujibu wa sheria yetu ya mwenendo wa makosa ya jinai sura namba 20 ya sheria za Tanzania, kifungu cha tano kinasema kwa muda gani mtu atakuwa chini ya dola au polisi, mtu ambaye amewekwa chini tu akiwa hana uhuru wa kwenda anakotaka huyo ina maana yupo chini ya ulinzi kwa hiyo kama upo chini ya ulinzi una haki ya kupata wakili kuweza kuongea naye na kujua nini kinaendelea na hatma yake na kupata fursa ya kuongea na ndugu zake na familia lakini fursa hiyo kwa Nondo haijapatikana kwani saizidi ni zaidi ya masaa 10 yamepita akiwa ameshikiliwa na jeshi la polisi" alisema Kombole

Mbali na hilo Wakili huyo amesema kuwa mpaka sasa wao hawajui Abdul Nondo ameshikiliwa kwa sababu zipi na kusema kuwa kijana huyo ameshikiliwa kinyume na sheria, kinyume cha Katiba, kinyume cha haki za binadam na kinyume na utaratibu wetu kama taifa kiujumla.

Kauli Nne Tata Mwanafunzi Aliyetekwa..Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya March 13

0
0


Kauli Nne Tata Mwanafunzi Aliyetekwa..Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya March 13

Aliyemtaja Mange Kimambi, Zitto Kabwe, Tundu Lissu na wengine kuwa ni watu 10 hatari zaidi Tanzania kuburuzwa mahakamani

0
0
Mjasiriamali/Mwanahabari na Mkurugenzi wa Compass Communications, Maria Sarungi amefungua kesi ya madai katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu dhidi ya Mhariri wa Gazeti la Tanzanite na Mwanasheria Cyprian Musiba kwa kumkashifu na kuchafua jina lake kupitia mkutano wake na Waandishi wa Habari uliyofanyika tarehe 25 Februari, 2018.

Barua hiyo iliyotolewa na Mwanasheria wa Maria Sarungi, Benedict Alex Ishabakaki imeeleza kuwa mteja wake alitajwa na gazeti la Tanzanite toleo Namba 50 lililotoka Februari 26, 2018 kuwa ni moja ya watu hatari kwenye usalama wa taifa.

Kwa upande mwingine, barua hiyo imeitaka  Dar24 kufuta habari hiyo na kuomba radhi hadharani kwa kitendo cha kuandika habari hiyo yenye lengo la kumfedhehesha mteja wao.

Zari: Natafuta Pesa, Sina Muda wa Kutafuta Mpenzi Mpya

0
0
Zari ameibuka na jipya tena huku safari hii akisisitiza kuwa wale wanaume wakware wote waliopanga foleni kusubiri penzi la Zari hawana nafasi kwani hana muda wa kuwa na mpenzi kwa sasa.

Zari alitangaza kumuacha mpenzi wake na Baba watoto wake staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, mwezi uliopita lakini tangu hapo Kumekuwa na tetesi nyingi juu ya Zari kupata mwanaume mwingine wa kuchukua nafasi ya Diamond.

Kupitia kurasa yake ya SnapChat  Zari ameweka wazi kuwa haitaji mpenzi kwa sasa baada ya marafiki zake kumtumia ujumbe uliosema;
“Kama mwanaume wako akienda kutafuta vimada  wenye msambwanda mpya inabidi umkumbushe kuwa na wewe msambwanda wako mpya ni kwa ajili ya mwanaume mpya”.

Zari amedai kuwa marafiki zake wanamtumia meme hizo kama vijembe kwa EX wake lakini amejibu kuwa hataki mwanaume mpya kwa sasa:

"Marafiki zangu siwawezi hivi kwanini wamekazana kunionyesha hizi Mambo lakini hazinifai mimi….. Nahitaji kutafuta pesa mpya na sihitaji mwanaume kwa muda huu samahani!!!!”.

Upande Wa Mashtaka Wafunga Ushaidi Kesi Ya Wema Sepetu

0
0
Upande wa Jamhuri katika kesi inayomkabili msanii wa filamu nchini, Wema Sepetu na wenzake jana ulidai mahakamani kuwa umefunga ushahidi dhidi ya mashtaka kutumia na kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi kwa msanii huyo.

Madai hayo yalitolewa jana na Wakili wa Serikali, Constantine Kakula katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam wakati wa kusikiliza ushahidi wa shahidi wa nne na wa tano mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.

Awali, shahidi wa nne, mjumbe wa nyumba 10, Steven Ndonde alidai mahakamani hapo kuwa siku ya tukio aliitwa kushuhudia upekuzi nyumbani kwa Sepetu.

Alidai kuwa wakati upekuzi unaendelea walikuta kipisi cha msokoto katika chumba cha nguo na viatu cha msanii huyo na chumba cha mfanyakazi wake walikuta kipisi kingine.

Hata hivyo, shahidi huyo alipohojiwa na wakili wa utetezi Albart Msando alikana kuwakuta washtakiwa wote wakiwa na dawa za kulevya aina ya bangi katika upekuzi huo.

Shahidi wa tano, Koplo wa Polisi Robert (31), alidai kuwa Februari 4, 2017 alipokea maagizo kutoka kwa bosi wake ya kupeleka vielelezo kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ikiwamo msokoto mmoja na vipisi viwili vya dawa za kulevya idhaniwayo kuwa bangi.

"Nilipeleka, vilipokelewa ofisi ya mkemia mkuu, baada ya kupokelewa niliandika barua kuhusu vielelezo hivyo," alidai Koplo Robert.

Kakula alidai baada ya kuita mashahidi watato dhidi ya washtakiwa upande wa Jamhuri imefunga kesi yao.

"Mheshimiwa hakimu tunaiachia mahakama iamue sisi upande wa Jamhuri tumefunga kesi yetu..." Alidai Kakula.

Wakili Msando aliomba upande wa utetezi kuwasilisha hoja za kama washtakiwa wana kesi ya kujibu au la ndani ya siku 10.

Upande wa Jamhuri ulidai utawasilisha majibu Aprili 3, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa.

Mbali na Sepetu, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Angelina Msigwa na Matrida Abbas.

Kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya na kutumia dawa za kulevya.

Inadaiwa kuwa Februari 4, mwaka jana katika makazi ya Wema huko Kunduchi Ununio, washtakiwa hao walikutwa na msokoto mmoja na vipisi vya bangi vyenye uzito wa gramu 1.08.

Ilidaiwa kuwa Februari mosi, mwaka jana katika eneo lisilojulikana jijini Dar es Salaam, Sepetu alitumia dawa za kulevya aina ya bangi. Washtakiwa walikana mashitaka.

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Siku ya Leo

Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH simba Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili

0
0
Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH issa simba said Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Maalim Hussein Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU. Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
Atamfanya Atimize 5 zote kwa Muda Mfupi.

Issa simba said Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumal6uiza Tatizo lako..
Anatibu kwa Kutumia Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA. Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI. Nguvu za KIUME, Humaliza Kesi zilishindika ndani ya siku 14 tu..na mengi zaidi

Piga simu +255 622588038au 0679119679 au +255 764318107

NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE...

Tunda na Casto Dickson Wamezungumza ‘Tukiwa Wapenzi Kuna Ubaya Gani?”

0
0
Tunda na Casto Dickson Wamezungumza ‘Tukiwa Wapenzi Kuna Ubaya Gani?”
Baada ya kuonekana kuwa karibu na kuibua headlines mitandaoni kati ya Staa Tunda na Mtangazaji Casto Dickson kudaiwa kuwa wanatoka kimapenzi, sasa mastaa wote wawili tena wakiwa pamoja ambapo wamezungumzia hilo.

Casto Dickson amesema kwamba yeye ni meneja wa Tunda na kuna project mpya inakuja inayowahusu ma-house girl ambapo Tunda atakuwa Balozi wao na kwa upande wa Tunda na yeye alisema ni kweli ni project inakuja ila watawaeleza mashabiki ikishakamilika.

TMA Yawataadharisha Wananchi Kuhusu Mvua Kubwa Zinazotarajiwa Kunyesha

0
0
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Yawataadharisha Wananchi Kuhusu Mvua Kubwa Zinazotarajiwa Kunyesha
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya vipindi vya mvua kubwa vinavyotarajiwa kuendelea katika maeneo ya mikoa 11 nchini.

TMA imetaja mikoa itakayoathirika na mvua hizo ni Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara, Morogoro, Ruvuma, Rukwa, Mbeya, Songwe, Iringa na Njombe.

Taarifa iliyotolewa leo na mamlaka hiyo inabainisha kuwa kuanzia leo Machi 12 hadi 13 ,2018 kunatarajiwa vipindi vya mvua kubwa inayozidi milimita 50 ndani ya saa 24.

“Hali hii inatokana na kuendelea kuimarika kwa ukanda wa mvua, wakazi wa maeneo yaliyotajwa wanatakiwa kuchukua tahadhari stahiki na kuendelea kufuatilia taarifa na tahadhari zinazotolewa, TMA inaendelea kufuatilia hali hii na itatoa mrejesho kila itakapobidi,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Serikali, Airtel Zaanza Mazungumzo

0
0
Serikali, Airtel Zaanza Mazungumzo
MAZUNGUMZO kati ya kamati maalum iliyoundwa na Rais John Magufuli na kampuni ya Bharti Airtel inayomiliki hisa katika kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania yameanza rasmi jana jijini Dar es Salaam, imeelezwa.

Katika mazungumzo hayo, taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais ilisema, kamati iliyoundwa na Magufuli inaongozwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi na timu ya Bharti Airtel inaongozwa na Mwanasheria Mkuu wake, Mukesh Bhavnani.

"Mazungumzo hayo yana lengo la kufikia makubaliano yatakayokuwa na tija kwa pande zote mbili (Serikali ya Tanzania na Bharti Airtel) na kuimarisha sekta ya mawasiliano nchini Tanzania," ilisema taarifa ya Ikulu.

Kampuni ya Bharti Airtel iliomba kufanyika kwa mazungumzo hayo baada ya kamati iliyofanya uchunguzi kuhusu umiliki wa kampuni ya Airtel Tanzania kuwasilisha ripoti yake kwa Rais, taarifa hiyo ilisema zaidi.

Mapema mwaka huu kamati hiyo ya uchunguzi ilitoa taarifa iliyosema ubinafsishaji wa kampuni ya Airtel uligubikwa na ukiukwaji wa sheria, kanuni na taratibu.

Januari 11, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango aliwasilisha taarifa ya kamati kwa Rais Magufuli ambaye aliagiza kufanyika kwa uchunguzi huo Desemba 20, mwaka jana.

Dk. Mpango alisema serikali imejiridhisha kuwa ubinafsishaji wa Shirika la Simu Tanzania (TTCL) kwenda Celtel, baadaye kuhamishiwa Zain na sasa Airtel ulifanyika kwa ukiukwaji mkubwa wa sheria, kanuni na taratibu.


Kufuatia ukiukwaji huo, Dk. Mpango alisema serikali inayomiliki asilimia 40 ya hisa za Airtel imeamua kufanya mazungumzo na kampuni ya Airtel inayomiliki asilimia 60 ya hisa, ili nchi iweze kupata haki yake.

“Lakini niwaambie Watanzania yale ambayo tumeyaona ni machafu sana, ni mambo ya ovyo kabisa, nchi yetu kwa kifupi tuliingizwa mkenge, ni fedha nyingi zimepotea kwa hiyo sisi katika majadiliano haya lengo letu litakuwa ni kuhakikisha Watanzania wanapata haki yao,” Dk. Mpango alisema siku hiyo.

Na sasa mazungumzo hayo yameanza, kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Ikulu.

Sumatra Yafafanua Ujumbe Huu 'Mke Mmoja Analemaza Akili'

0
0
MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra), imetoa ufafanuzi kuhusu tiketi ya basi la daladala yenye ujumbe unaohamasisha wanaume kuwa na wanawake wengi, ambayo imezua gumzo kwenye makundi ya mitandao ya kijamii, ikiwamo WhatsApp.


Tiketi hiyo ambayo inaonekana kudaiwa kuwa ni ya daladala inayofanya safari zake kati ya Mbagala Rangi Tatu na Kivukoni jijini Dar es Salaam, ilizagaa katika mitandao ya kijamii ikiwa na ujumbe usemao 'Mke mmoja analemaza akili.'

Sumatra imewataka abiria watakapopewa tiketi hizo watoe taarifa kwenye mamlaka hiyo kwa kuandika barua ya malalamiko pamoja na kuambatanisha tiketi husika.

Meneja Leseni wa Sumatra, Leo Ngowi alitoa ufafanuzi huo alipoulizwa na Nipashe lililotaka kufahamu kanuni za Sumatra zinasemaje kuhusu maandishi hayo ya kwenye tiketi.

"Hakuna adhabu ya moja kwa moja kwa gari lenye tiketi yenye ujumbe usiokuwa na maadili, lakini gari husika linaweza kuadhibiwa kwa kosa la kushindwa kufuata taratibu, sheria za barabarani, pamoja na sheria zinginezo, ambayo faini yake ni Sh. 250,000," alisema Ngowi.

Ngowi alisema kwa mujibu wa kanuni za Sumatra, kifungu namba 33(2) (a) inayohusu mabasi yaendayo nje ya miji, tiketi zao zinapaswa kuwa na jina la abiria na namba ya kiti.

Alisema tiketi inapaswa kuonyesha muda wa kuwasili na kuondoka kituoni, kituo cha kuondokea, pamoja na njia itakayopita na mwisho wa safari.

Alitaja kingine kuwa ni nauli ya safari, sanduku la posta na namba ya leseni, namba ya usajili ya gari husika, tarehe ya kukata tiketi na siku ya kusafiri, namba ya tiketi, namba ya Sumatra na polisi.

Ngowi alisema kwa magari ya mijini, tiketi zinapashwa kuwa na namba ya usajili ya gari, njia ya gari itakayopitia, nauli halisi, tarehe ya kukata tiketi, pamoja na namba ya leseni. 

Mwakyembe Kuwachongea Maofisa Habari Wazembe Ili Watumbuliwe

0
0
Mwakyembe Kuwachongea Maofisa Habari Wazembe Ili Watumbuliwe.
Waziri  wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, amesema atawasilisha kwa Waziri Mkuu majina ya maofisa habari wazembe, ili watumbuliwe.

Alisema hayo kufuatia uzembe unaofanywa na baadhi yao huku wakibweteka kukaa maofisini bila kufanya kazi.

Alisema maofisa habari wasiojituma ni sawa na kuwa na maofisa habari hewa, ambao wanakula mishahara wasioifanyia kazi, jambo ambalo hakubaliani nalo.

Dk. Mwakyembe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano wa kazi wa siku tano wa maofisa habari, mawasiliano na uhusiano serikalini, unaofanyika jijini Arusha, aliwataka kubadilika na kutekeleza malengo waliojiwekea.

"Kweli naangalia tovuti za halmashauri zipo tisa tu zinazofanya vizuri, zingine wahusika wamelala; na mikoa 18 tu inafanya vizuri kuhabarisha, sasa hawa wengine wajitathmini vinginevyo nitapeleka majina yao kwa Waziri Mkuu, ili watumbuliwe, tutoe ajira kwa wengine," alisema.

Aliwataka wafanye kazi ya kuhabarisha wananchi kazi zinazofanywa na serikali, ili wasitumbuliwe.

Alisema hata wizara husika pia wapo wazembe nao atapeleka taarifa ngazi ya juu ili wachukuliwe hatua, lengo kazi nzuri zinazofanywa na serikali zitambulike kwa wananchi na kuziba mianya kwa wapotoshaji wa taarifa za serikali.

Dk. Mwakyembe aliwataka maofisa habari hao kujituma na kutoa taarifa za kazi zinazofanyika kila siku kwenye mitandao ya kijamii na endapo watazuiwa na mtu yeyote, wawafichue hata kwa siri ili wizara ishughulike na muhusika.

Naye Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN), Alvaro Rodriguez, aliwataka maofisa habari hao kubadilika na kuleta tija kwa taifa baada ya mkutano huo kuisha.

Alisema dunia sasa imeunganishwa kwa teknolojia, hivyo ni vema jamii ikapata taarifa zilizo sahihi kwa wakati.

Aidha, alisema serikali pia inahitaji kusikiliza jamii na sauti za wananchi, ili kupiga hatua katika kufikia Tanzania ya Viwanda.

“Sisi kama wadau tunahitaji kusikia zaidi habari za wananchi wa vijijini, ili tuone jinsi wanavyobadilika katika hali walizonazo,” alisema.

Madee : Sifungi Ndoa kwa Kufuata Mkumbo Kisa Staa Fulani Ameoa

0
0
Madee : Sifungi Ndoa kwa Kufuata Mkumbo Kisa Staa Fulani Ameoa
MEMBA wa Kundi la Tip Top Connection ambaye pia ni Mkurugenzi wa Lebo ya Manzese Music Baby ‘MMB’, Hamad Ally ‘Madee’ amefungukia ndoa yake kuwa hawezi kufunga kwa kufuata mkumbo kisa staa fulani amefunga ila atakachofanya ni kufanya sapraiz siku yoyote kuanzia sasa na kufunga bila kutangaza.

Madee anayebamba na Ngoma ya Sema alisema, kwa sasa bado anaangalia lebo yake hiyo iweze kutanuka zaidi na tayari amefanikiwa kwa msanii Gaza na Dogo Janja ambao ‘wameshasimama’.

“Ujue suala la ndoa si la kukurupuka tu unaenda kufunga. Ndoa ni kitu binafsi kabisa na ni maamuzi ambayo yanachukulia kwa mara moja huwezi kuwa na uamuzi tena kwa hiyo mimi kama mimi kufunga ndoa ni mipango na familia yangu ambayo siwezi kuiweka wazi lakini muda wowote kuanzia sasa naweza kufunga,” alisema Madee.
Viewing all 104415 articles
Browse latest View live




Latest Images