Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live

Rayuu Aomba RADHI Familia Yake Kwa Picha zake za Uchi Zilizo Sambaa Mitandaoni

$
0
0
Mwigizaji Maarufu Anayejulikana kwa jina la Rayuu Amejitokeza Baada ya kimya cha muda mrefu na kuiomba familia yake Radhi kwa Picha Chafu zilizosambaa mtandaoni.

Rayuu Kipindi cha nyuma amekuwa akivujisha picha zake mbali mbali za sehemu za mwili za kutatanisha ambazo sio nzuri kimaadili, Picha nyingi zake amekua akionyesha sehemu alizojichora Tattoo ambazo mpenzi wake pekee ndio angepaswa kuona


Watangazaji Kibonde na Gadner Habash Wapandishwa Kizimbani leo

$
0
0
MTANGAZAJI wa Clouds FM, Ephraim Kibonde na mwenzake, Gardner Habash wa Times FM leo wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya Kinondoni jijini Dar es Salaam kwa kusababisha ajali na kudharau amri ya polisi na kutoa lugha ya matusi.

Watangazaji hao wamesomewa mashitaka hayo na Wakili wa Serikali, Salim Mohammed mbele ya Hakimu Aniseta Wambura.

Kibonde na Gadna wanadaiwa kutenda makosa hayo Jumamosi ya Agosti 9, mwaka huu saa 12 asubuhi, katika eneo la Makumbusho, ambapo Kibonde akiwa anaendesha gari walilokuwa wamepanda aliligonga gari la raia mmoja wa kigeni (Mzungu) na kukimbia.

Kesi yao imeahirishwa mpaka Septemba 10 mwaka huu itakaposikilizwa tena.

Mwigizaji JB na Shamsa Ford Kunani, Mbona Kila Movie Zenu Nyie Tuu

$
0
0
Mimi sio mpenzi sana wa kuangalia filamu, ila mara chache tu huwa naangalia hasa kwenye mabasi ninaposafiri.

Kitu kinachonikera kwenye hizi Bongo movie hasa za JB ni kutumia wahusika wale wale na theme ile ile mwisho ana bore sasa.

Mfano ni huyu Shamsa Ford, huwezi kuangalia picha ya JB usimkute, tena kwenye filamu hiyo lazima ataishia kuolewa na JB. 

Ni kweli Shamsa ni mzuri, lakini kwani yuko pee yake kwenye filamu? 

Halafu kwa nini theme iwe mapenzi tu?

Nachoka kabisa

Sababu Zilizomfanya Dogo Janja Aache Shule, Hili Atakuja Kulijutia Baadae

$
0
0
Rapper kutoka Arusha, Dogo Janja ameamua kuacha shule ili kusomea masomo ya muziki. Akiongea na 255 ya kipindi cha XXL cha Clouds FM, Janjaro amedai kuwa usumbufualiokuwa akiupata shuleni ndio sababu kubwa iliyomfanya aache shule.

“Shule ambayo mimi nimesoma nilikuwa napata matatizo kwasababu kitu kidogo ambacho mnaweza mkafanya wote lakini wewe ukaonekana chanzo. ‘Msanii mhuni, huyu hivi,” alisema rapper huyo.

“Sometimes unaweza ukawa unasoma watu wengi wako dirishani wanapita wanakuangalia. Au unaweza ukakosea.. yaani wanakuwa wewe ni mtu ambaye upo sahihi all the time. Kwa mfano labda unajua zile za kushtukizwa ‘fulani jibu swali’ kila saa unaulizwa wewe,” aliongeza.

“Kwahiyo unakuwa hakuna pale Uabdul, unakuwa unaweka Ujanjaro Udogojanja. Kwasababu unajua ile kushtukizwa kila saa unakuwa unahisi kama mwalimu anakuandama sana. Au kwenye mtihani, mnaweza mkawa mnafanya wote mtihani lakini mwalimu anakuja kukusimamia wewe, anakukazia kinoma.”

Nini mtazamo wako kuhusiana na sababu hiyo ya Dogo Janja iliyomfanya aache shule?

Mwanaume Mmoja Ameua Watu Sita Baada ya Mkewe Kuchepuka na Wanaume Hao Kingono

$
0
0
Mwanaume mmoja ameua watu 6 baada ya mkewe kujihusisha na wanaume hao kingono,kutokana na tukio hilo mwanamume huyo amehukumiwa adhabu ya kifo nchini China. 

Shao Zongqi, mwenye umri wa miaka 38 alikutwa na hatia baada ya kutekeleza mauaji hayo mwezi January mwaka huu. 

Kwa muujibu wa mahakama, Shao alipanga kulipiza kisasi baada ya kugundua kua mkewe alikua na mahusiano na wanaume wawili tofauti,shirika la habari la Xinhua limeeleza hayo. 

Wakati wa sherehe za mwaka mpya wa kichina,Shao alijeruhi wanaume tisa, na kumuua mmoja pamoja na familia yake na wanaume wengine wawili wa jirani,wakati mwanamume mmoja akiwa na mkewe na mtoto wao wa kiume walinusurika katika tukio hilo.

Wakati hukumu hiyo ikitolewa siku ya jumatatu, iliamuriwa Shao alipe kiasi cha yuani 604,000/- sawa na dola za kimarekani 98,000/- kwa familia walio hai ambao waliondokewa na jamaa zao kutokana na shambulio hilo.

Pamoja na kulipa faini hiyo Shao ameapa kukata rufaa kutokana na hukumu hiyo ya kifo inayomkabili.

OMG!!! Meninah Shares A Killing Photo….Look At Huo Upaja

$
0
0
Mtangazaji na Mwana Bongo Flava Mrembo Meninah Ameshare nasisi Picha Hiyo hapo 
Hot or Not ?

Pigo Kubwa Kwa Afande Sele Afiwa na Aliyekuwa Mke Wake MamaTunda

$
0
0
Afande Sele akiwa katika picha ya pamoja na familia yake (picha ni ya muda kidogo), kutoka kulia ni mama wa familia hiyo Marehemu Asha Msindi, Seleman Msindi .a.k.a dume la simba, aliyempakata ni mtoto wake mdogo anayeitwa Asante Sana na wa mwishoni Tunda.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook Afande Sele amepost taarifa ifuatayo kuhusiana na kifo cha mzazi mwenzake aneitwa Asha au Mama Tunda.

Martini Kadinda Ashutumiwa Kushindwa Kumsimamia Wema Sepetu Kama Manager

$
0
0
Baadhi ya Mashabiki wa Wema Sepetu Wamekuja Juu Baada ya Kuona Wema Sepetu Anazidi Kupata Umaarufu tu Kwa Kupitia Skendo Badala ya Kutumia Umaarufu alio nao kufanya Vitu vya Maana, Shutuma nyingi zinapelekwa kwa Manager Wake Ambae Wengi Walizani Atafanya Mambo Makubwa Kupitia Jina la Wema Sepetu Lakini Mpaka sasazaidi ya Mwaka hakuna cha maana alichofanya zaidi ya Mapicha picha tu Instagram...

Baadhi ya Waliomnanga Martini Kadinda ni huyu Hapa jisomee mwenyewe:


Martin Kadinda Ajibu Tuhuma za Kushindwa Kumsimamia Wema Sepetu Ipasavyo

$
0
0
Maswali mengi yamekuja baada ya Wema kufanya show Mwanza mpenzi wake alipokuwa akiperform jukwaani, pamoja na hayo mashabiki waliyo wengi wametaka kuona Wema akijishughulisha kuliko hivyo anvyo zunguka na hawajui anafanya nini. Wema ana mashabiki wengi sana wanaompenda na kutaka mafanikio yake. Baada ya swali hilo hapa chini ndo jibu alilitoa kaka Meneja wa Wema amejielezea vizuri sana baada ya Kuambiwa Kashindwa kazi:



Penny Kumchezesha Diamond Ngololo Kwenye Harusi Yake Hivi Karibuni

$
0
0
Mtangazaji  wa 93.7  E-FM  kupitia  kipindi  cha  Genge,  DVJ Penny  ambaye  wiki  kadhaa  zilizopita  picha  zake  zilisambaa  mtandaoni  zikimuonyesha  akiwa  amevishwa  pete   ya  uchumba  huku  mwanaume  aliyefanya  tukio  hilo  akiwa  ni  kitendawili, hatimaye  mwanadada  huyo  ameibuka  na  kumuweka  wazi  mpenzi  wake…..

Akiongea  na  mwandishi  wetu, rafiki  wa  karibu  wa  Penny  amesema  kuwa  jamaa  aliyemvalisha  pete  ni  kigogo  mwenye  pesa  chafu  anayemiliki  migodi  kadhaa  ya  madini  anayefahamika  kwa  Jina  la  Johnson  raia  wa  Angola….

Rafiki  huyo  amesema  kuwa  kutokana  na  jeuri  ya  pesa  ya  kigogo  huyo, Penny  anatarajia  kufanyiwa  bonge  la  harusi  na  watafanya  kila  namna  ili  Diamond  awe  mtumbuizaji  katika  sherehe  hiyo…

Wengi Wanaopinga Uraia Pacha Hawana Sababu za Msingi Kuupinga Kwa Sababu Hizi

$
0
0
Nimechunguza sana na kuona kwamba wengi sana ya wanaopinga suala la Tanzania kuwa na uraia pacha hawana sababu za msingi za kuupinga. Wengi wao wanapinga kwa ajili tu kuwaonea husuda Watanzania wenzetu waliopata nafasi za kutafuta maisha nje kwa kuwa wao hawana uwezo wa kupata nafasi hizo. Wakiwa na hili akilini, wanatumia visingizio vya kila aina kupinga uraia pacha. Sababu kubwa tatu zinazotolewa dhidi ya uraia pacha ni zifuatazo;

Uraia pacha utaendeleza ufisadi
Uraia pacha utafanya watu wa nje matajiri wanunue ardhi yetu yote
Uraia pacha ni kukosa uzalendo


Uraia pacha na ufisadi
Hivi hili ni la kweli? Je, tunataka kusema wale Watanzania wenzetu walioko diaspora wote ni mafisadi na hiyo ndio sababu ya wao kutaka uraia pacha? Na kweli wao ni mafisadi zaidi ya hawa mafisadi tulio nao humu nchini? Na hawa mafisadi tuliojaza nchini ni raia pacha wa nchi gani? Na ni ufisadi gani ambao mtu akiwa raia pacha ataufanya - kuondoka na shilingi ya Tanzania kupeleka nje? Kutorosha nyara za serikali? Au kuleta fedha za kigeni nchini? Hata kama ni kutorosha nyara na fedha, sheria na kudhibidi hayo mambo, kama money laundering laws, zitakuwa wapi?

Uraia pacha utafanya matajiri wa nje wanunue ardhi yetu yote
Kwani nani aliyesema tukiruhusu uraia pacha ina maana kila mtu aliyeko nje anaruhusiwa kuwa raia wa Tanzania na kuwa raia pacha akiomba uraia wetu? Hii inaonekana kuwa watu hawajui kwamba walengwa wa kwanza wa uraia pacha ni Watanzania ambao wako nje, ambao wengi wao wanaogopa kuchukua uraia wa huko nje wakihofia kupoteza uraia wa Tanzania, kulingana na sheria ya sasa ya uraia. Na walengwa wa pili ni raia wa nje ambao labda wameoa au kuolewa na Watanzania, na wangependa kutambulika kama raia wa Tanzania pia. Na mwisho ni raia wa nje waliokaa sana nchini na kupata ukazi wa kudumu akini bado wana uraia wa kwao. Sasa hili la matajiri kuchukua ardhi yetu linatoka wapi? Na hata kama ukioa au kuoelewa, kuna sheria ambazo hazikuruhusu kuwa raia wa Tanzania mara tu ukioa bali hadi miaka kadhaa ipite ukiwa mkazi wa hapa nchini. Sasa tatizo liko wapi?

Uraia pacha ni kukosa uzalendo
Jamani, hebu tachane na hizi kauli za kipropaganda. Kwani uzalendo maana yake nini au unaonyeshwa kwa vitendo gani kiasi kwamba mwenye uraia pacha aone kuwa na uzalendo pungufu ya yule asiye na uraia pacha? Jambo la kukumbuka hapa ni kwamba wanaotaka uraia pacha wana hiyo ari kwa ajili ya uzalendo walio nao na Tanzania. Japo wameishi nje muda mrefu bado wanaona shida kukata mizizi na nchi yao Tanzania. Angalia kwamba nchi kama Norway na Israel zina raia wengi nje ya nchi kuliko wale walio ndani ya nchi; na hawa walioko nje uzalendo wao haujapungua hata kidogo kwa kuwa tu wamekuwa raia wa huko wanakoishi. Juzi hapa nimesikia Mkurdishi wa Iraq, yeye na mwanae, ambao kwa sasa ni raia wa Sweden, wamerudi Iraq kwenda kupigana dhidi ya ISIS. Sasa anayesema uraia pacha ni kukosa uzalendo, ni kwa kigezo kipi?

Uchafu Unaofanywa na Wanafunzi wa Kike Shule za Boarding Jinsia Moja

$
0
0




Ukiangalia Picha hizo zinajieleza vizuri hao ni wanafunzi wa shule za sekondari , Je Vitendo hivyo wanavyofanya ni matokeo ya shule za boarding jinsia Moja ? 

 Nakumbuka mtoto wa jirani yangu alienda shule moja ya Boarding hapa Bongo alivyorudi likizo akaanza kuwatongoza wasichana wenzake wa hapa mtaani kwetu

Mke Wangu Amenishangaza, Kaniambia Nikipata Demu wa Nje Nimlete Tufanye Threesome

$
0
0
Wadau mimi nimeoa hivi karibuni Basi siku moja tulikuwa tunaangalia movie moja ya Chriss Rock inaitwa Down to Earth Basi Kuna Sehemu Mke wa Chriss Rock Amemleta Demu wa Nje ndani ya Nyumba na Kumwambia mmewe Wafanyaje Three Some kwani jamaa alikuwa anapenda, Sasa Hapo mke wangu akaanzisha hako kamjadala na kuniuliza kama naweza kufanya hivyo nikamwambia sijawahi kujaribu, basi kwa macho makavu akaniambia kama nataka kujaribu nitafute demu wa nje alafu nimlete ndani tufanyaje mapenzi watatu yaani Mimi, mke wangu na huyo demu, Nikaamuuliza "Are u serious ?" Akanijibu ndio pia nae anawish kujaribu ...Sasa Hapa nimebaki na Maswali Mengi sana ikiwemo kujiuliza kama ndo ulikuwa mchezo wake kabla sijamuoa ...Wadau Naomba ushauri

Kwa Uzalendo Alionao, Mwigulu Apatiwe Ulinzi wa Kutosha, Mafisadi na Wapinzani Wasimguse

$
0
0
Sote tunajua uzalendo na utendaji wa Mheshimiwa Mwigulu.

Pamoja na kuwa anayofanya ni kwa faida ya taifa, lakini mjue wazi kuwa maadui zake sio wahujumu uchumi na mafisadi tu. Mwigulu atachukiwa sana na wapinzani hasa wale wanaoandamana kwa chopa na pia hata wana ccm wenzake kwani kazi anayofanya itamfanya apendwe na wananchi kitu ambacho kitasababisha wivu wa kisiasa.

Mimi nina uhakika asilimia mia kumi kuwa kadri anavyochapa kazi ndivyo anavyozidi kuongeza maadui, na maadui lazina watajaribu kupunguza spidi yake.

Tumuombee afya njema na ulinzi Sokoine wetu mpya. 

Kiongozi huheshimiwa kwa utendaji wake, sio kwa kususia kazi uliyotumwa na wananchi au kwa kutoa matamko huku ukitokwa povu..

Kimenuka kwa Diamond, Mashabiki wa Wema Wamtaka Aache 'Kumtumia' Wema Kibiashara.

$
0
0
Kundi la watu wanaojiita mashabiki wa Wema Sepetu, limeanzisha kampeni kwenye mtandao mmoja wa maarufu wa kijamii kampeni iliyopewa jina la #BringBackOurWema likimshinikiza mpenzi wake Diamond Platnumz amrudishe kwenye maisha yake ya zamani na kukuza career yake ya filamu.



Mashabiki hao wanaamini kuwa Diamond anampoteza Wema na amekuwa akitumia umaarufu wake (Wema) kujidhatiti zaidi yeye huku Miss Tanzania huyo wa zamani akiendelea kudidimia.

Hivi ndivyo maelezo yanavyosema:

@diamondplatnumz mambo vipi? Sisi mashabiki wa @wemasepetu tunakuomba umsaidie Wema kama yeye anavyokusaidia. Labda niseme kwa uwazi bila woga kwamba mahali ulipo kimziki umefika sababu ya Wema. Wengine hatukuwa mashabiki wako lkn sababu ya mapenzi kwa Wema tukajilazimisha kukupenda tu… so unajua vema bila wema we mziki huna!

Tunakuteteaga tu lkn huwezi kujilinganisha na wanamuziki wengine tunaowajua wanafanya vema kuliko wewe….leo sitawataja majina! nije kwa point yangu sasa wewe si mwanaume? Tuoneshe sasa! “Umetembea tembea nchi mbalimbali” umekutana na watu wa aina mbali, hujamtambulisha wema huko kibiashara, unaishia kusema maneno maneno ya sifa lkn unamwacha Wema anapotea.

Angekuwa Wema she’s always proud of you kukutaja popote hata angepata ile nafasi ya kuongea na Karuache angekutaja, umeonana na kina Davido+Iyayna bila kutaja waigizaji wakubwa Nigeria…Wema ni brand tunamlinganisha na top stars Africa!! We una nafasi kubwa sana kumfanya Wema aonekane..but what your doing unampoteza kwa makusudi. Unamchezesha viduku, Ulipomwacha alikuwa na maendeleo makubwa alikua ameshatengeneza wanamuziki wake, nyumba yake, kipindi chake cha in my shoes kilianza bila mkono wako. Ukaona hapa atakuzidi na unajua jinsi anavokupenda ukamtumi, hujawahi kusema hadharan feelings zako kwake zaidi ya mafumbo mafumbo
Hujawahi kukanusha ile interview ya spora uliyomdiss vibaya Wema….

Je tueleweje sasa? Si lazima kuanika kila kitu mambo yenu binafsi. Wema haoni kwa sasa sababu ya mapenzi yake kwako…tunakuambia leo kama hauna nia nzuri na Wema tunakuomba umuache. Maana unajua tu akimpigia promo mwanamuziki wake Mirror utapotea kwa game. She has all this power tunaomba usimtumie kwa maslahi yako binafsi. #bringbackourwema.

Haya ni maoni ya wengine:

lula_marii

Daaaaaaah kwa ukweliii wema unalegealegea ..yaani how comes you don’t have any respect from da guy who claims to love yuh?anawezaje kushikashika na kusugulia madem haswaaa ukiwa na yy kwa stage…juzi fiesta everyone saw wat diamond did with linah…wit out even thinking of da feelings of our madam…booooo pliz dnt say that is his professionals…coz its only singing that is his profsional…..@wemasepetu.open ur eyes….@diamondplatnumz pliiiiiz wit all due respect ,achaaa tabia za utoto

bintijasho

Siku nyingi nilikua nataka kusema hichi kitu lakini leo @mrekebishatabia umesemakweli kabisa @diamondplatnumz anaakili san amepinga hesabu akaona wema anamsanii wake nawema anamashabiki wengi alijua tu mirror atakuja kua juu sasa akaona heri arudia na wema apate kumvuringia mipango yake wallah na muonea huru huyu mdogowangu maski yana siku hizi hata mirror simsikii akimtaja @mrekebishatabia umefanya jambo zuri sana l hope @wemasepetu ataupata ujumbe wako

gennomaxmillan

@diamondplatnumz ww sio mwanammebora kwa wema bali n kvuli cha mwanamme japo mm n nwananch wa kawaida sio star lkn bby wangu kanpa maisha mazur na tunafamilia yenyefuraha.@mekebishatabia maisha ya wema hayavutii kbsa haelewek na ni kwel kbsa biła wema huyo jamaa alkuwa hajui ata kuomba maji kwa kizungu chek wema kajitoa kampa darasa badała alipe fazla anakaz ya kujtangaza na kutukandamizia mdogowetu@wemasepetu mm nakapenda sana kawema ni kazr lkn huwa hakubali ukwel ebu kataa kuanikwa kwa magazet ish kama wakna monalisa jack happy magese nancy angel damas na wengne weng ambao walpata kujulkana kama ww mbona maisha yataenda tu humuon mama krsh alivyo sasa eti mpnz ebu tazama alipo uwoya ameona bora kuish kawaida na bado yupo vzr sana huwez jua kama n mama wa jembe@uwoya kaa na .mwenzako bby anapotea

dougiemasta14

lawama zang mm zinaenda kwa @diamondplatnumz ni mtu ambae ntamlaumu milele kubadilika kwa wema hiv dai unajiskiaje mwanamke wako akipanda juu ya stage nakuanza kukata viuona chini yake kuna maelf ya watu wanamshangilia hiv unajua kuna wangapi wanao mtamani? Kuna wengine wakimuona tu wema huko chin hatr...dai srry for saying dis but in another point ww ndie unae mrudisha wema nyuma kuna muda huwa najiulize do u real love her ss hapa hamjaona ukishamua sindo tunampoteza kabisa...kwa ninavyo jua mpnz wako ndio mshaur wako wakwanz lakin ss mpnz ww uko busy kumshaur akacheze show for real...ok iko wap ile movie yenu ya china kila siku coming soon yan mnafanya watu wawaoneni waongo na hamna akili me vipo vingi navijua sema kwa heshima ya wema naonaga nijikaliege kimya..mm najua dai huskindwi kumkatia wema ticket uende nae out de country since merudiana tunaona post za wema kukununulia vitu but I had nvr seen ww kumfanyia wema something is dis wat u call love? O kunyonyana kimya kimya we kama mwanaume huwez mruhus mwanamke wako anaenda kweny vigodoro kufanya nn ss...wema if giving u makavu will help u to realise that we want dat am ready to start giving u makavu ...dont make ppo loss interest with u kutupenda sio kusema na kutuchezea show but kuonesha but listen to wat we want...ss tutaanza kukuchapa fimbo na leo hii me natangaza @martinkadinda nakuingilia kazii yakooo ss tutaanza kwenda kitemi maana kimya kimya hatuelewani...baadae ntarud kwa nyie washabikiii

Wema Sepetu Tutaanza Kukuchapa Fimbo na Kwenda Kitemi Maana Kimya Kimya Hatuelewani

$
0
0
Leo ndio leo Mashabiki wa Wema wamecharukajeeee.....
Ona huyu anaejiita Douguemasta14 alivyomshukia:

Lawama zang mm zinaenda kwa @diamondplatnumz ni mtu ambae ntamlaumu milele kubadilika kwa wema hiv dai unajiskiaje mwanamke wako akipanda juu ya stage nakuanza kukata viuona chini yake kuna maelf ya watu wanamshangilia hiv unajua kuna wangapi wanao mtamani? Kuna wengine wakimuona tu wema huko chin hatr...dai srry for saying dis but in another point ww ndie unae mrudisha wema nyuma kuna muda huwa najiulize do u real love her ss hapa hamjaona ukishamua sindo tunampoteza kabisa...kwa ninavyo jua mpnz wako ndio mshaur wako wakwanz lakin ss mpnz ww uko busy kumshaur akacheze show for real...ok iko wap ile movie yenu ya china kila siku coming soon yan mnafanya watu wawaoneni waongo na hamna akili me vipo vingi navijua sema kwa heshima ya wema naonaga nijikaliege kimya..mm najua dai huskindwi kumkatia wema ticket uende nae out de country since merudiana tunaona post za wema kukununulia vitu but I had nvr seen ww kumfanyia wema something is dis wat u call love? O kunyonyana kimya kimya we kama mwanaume huwez mruhus mwanamke wako anaenda kweny vigodoro kufanya nn ss...wema if giving u makavu will help u to realise that we want dat am ready to start giving u makavu ...dont make ppo loss interest with u kutupenda sio kusema na kutuchezea show but kuonesha but listen to wat we want...ss tutaanza kukuchapa fimbo na leo hii me natangaza @martinkadinda nakuingilia kazii yakooo ss tutaanza kwenda kitemi maana kimya kimya hatuelewani...baadae ntarud kwa nyie washabikiii

Baby Madaha Amwaga Radhi Kenya, Awaacha Wanaume Wamchungulie Kunako Nyeti

$
0
0
Baby Madaha Amewaacha hoi mashabiki wa Mziki huko Kenya Hasa wanaume wenye uchu baada ya kupanda jukwaani akiwa amevalia kigauni ambacho kiliwezesha wanaume kumchungulia kirahisi wakati akiimba jukwaani , Nao wanaume Wakenya Pande ya Naivasha hawakufanya ajizi jionee mwenyewe hapo kwenye picha jamaa wanavyomchungulia

Video Kali sana ya Wimbo wa Victoria Kimani Feat. Diamond and Ommy Dimpoz-Prokoto

$
0
0


Siku si nyingi Mlimsikia Mrembo Mkenya aitwaye Victoria Kimani Akiwa Hapa nchini kufanya Video na Kina Diamond na Ommy Dimpoz , Sasa ile Video Imeshakamilika ndio hii hapa ..Embwa ni kali kinoma jionee mwenyewe na Utoe Maoni yako :


Hatimaye Jacklie Cliff Amehukumiwa Kifungo Jela-Huu Ndio Muda Atakao Kaa Jela

$
0
0
Kama wengi Mjuavyo Kuwa Mrembo wa Bongo Jack Cliff alikamatwa China Mji wa Macau kwa Tuhuma za Kubeba Madawa ya Kulevya , Sasa mpya kutoka huko zinasema Kesi ya mrembo huyo imesomwa na Amehukumiwa Kifungo cha Miezi Sita Gerezani.

Chanzo cha habari hiyo hakijatoa maelezo ya kutosha kwanini iwe miezi sita tuu na wakati tunasikiaga kuwa huko adhabu kwa makosa kama hayo ni kali sana na hufikia hata kunyongwa....tutaendelea kufuatilia na kukuletea habari kamili ...

Mtoto wa Miaka Sita Afariki Dunia Baada ya Kugongwa Gari na Mama Yake Kwa Bahati Mbaya

$
0
0
Mtoto mwenye umri wa miaka sita amefariki baada ya kukanyagwa na gari la mamake.
Bolutito Shodipe mwenye umri wa miaka sita aligongwa na mamake aliyekuwa anajaribu kuegesha gari lake nje ya kituo cha treni cha Hounslow West Tube nyakati za asubuhi Jumatano wiki hii.

Juhudi za kuokoa maisha ya Bolitito katika eneo hilo ziliambulia patupu kwani alisemekana kuaga dunia alipofikishwa hospitalini.
Taarifa kutoka kwa familia ya Bolitito ilisema kuwa wanajaribu kuikubali hali iiliyowakuta kutokana na ajali hiyo mbaya.
Familia hiyo inayoishi eneo la Hayes Magharibi mwa London, iliongeza kusema: "Bolutito alikuwa mtoto wetu wa kwanza na alikuwa nuru kwetu. ''
"alikuwa mrembo, mwenye maadili mema, na mpenzi wa Ballet, na tutamkosa sana.''
Polisi walithibitisha kwamba kifo cha mtoto huyo kilikuwa ajali kwani walifika wote katika kituo cha treni na mamake, ila mtoto aligongwa na kufariki wakati mama akijaribu kuegesha gari lake.
Polisi wanachunguza tukio hilo.
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live




Latest Images