Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104431 articles
Browse latest View live

Yusuph Mhili: Nimetumwa Kuokoa Jahazi la Yanga Lisizame

0
0
Yusuph Mhili: Nimetumwa Kuokoa Jahazi la Yanga Lisizame
MSHAMBULIAJI chipukizi wa Yanga, Yusuph Mhilu amesema, ana kila sababu ya kuipigania klabu yake ifanye vizuri tangu siku 'alipovutwa sikio' na kuambiwa aende akafanye kazi ya kuokoa jahazi lao lisizame.

Mhilu amesema, baada ya wachezaji wakubwa kama Wazimbabwe Donaldo Ngoma, Thaban

Kamusoko na  Amiss Tambwe kuwa majeruhi kwa muda mrefu.

Yeye pamoja na wachezaji wengine chipukizi, walikalishwa chini na kuambiwa, timu inawategemea

wao na hivyo wanatakiwa kupambana na kuokoa jahazi la Yanga lisizame .

"Binafsi nina kila sababu ya kuipigania timu yangu ya Yanga baada ya wao kuniamini. Baada

ya kuona wachezaji wale wakubwa wamekuwa majeruhi wa muda mrefu na wao ndiyo walikuwa wanategemewa, sisi vijana tulikalishwa chini na kuambiwa ndiyo wa kwenda kuikoa Yanga na hivyo tukapambane,"anasema Mhilu.

Hata hivyo tangu kikosi hicho kianze kumtumia Mhilu na vijana wengine, mambo yamekuwa

mazuri ndani ya kikosi hicho ambapo sasa wako nafasi ya pili na pointi 46 sawa na za Simba

wanaoongoza, wakifuatiwa na Aazam FC yenye 44, Tanzania Prisons 26 na Singida iliyo ya tano 36.

Chemical Sababu ya Kufanya Movie na Wema Sepetu

0
0
Chemiko Sababu ya Kufanya Movie na  Wema Sepetu
Msanii wa muziki Bongo, Chemical amefunguka sababu iliyopelekea kufanya movie na muigizaji Wema Sepetu.

Chemical amesema licha ya kutoa ngoma ‘Mary Mary’ aliamua kutumia title hiyo katika movie yake hiyo na kufanya na Wema ni kutokana na sababu za kibiashara.

“Alipenda stori na kuna watu wa karibu waliongea naye na yeye aliona ni biashara sio tu kuangalia ukubwa au jina la msanii, kwa hiyo tumemfuta Wema Sepetu kibiashara,” amesema Chemical.

“Mimi sio msanii wa Bongo Movie, mimi nafanya muziki, kwa hiyo ile nimefanya kama by the way,” amesisitiza.

Ameongeza kuwa hajasita kuachia movie hiyo licha ya kuwepo stori kuwa soko la Bongo Movie limeshuka kwani movie yao ‘Mary Mary’ ina story nzuri pamoja na muziki, hivyo anakutanisha mashabiki wake na wale wa Wema Sepetu.

Kikosi cha Yanga Yawafuata Township Rollers kwa Mechi ya Marudio

0
0
Kikosi cha Yanga Yawafuata Township Rollers kwa Mechi ya Marudio
Kikosi cha Yanga SC kimeondoka alfajiri ya kuamkia leo kuelekea nchini Botswana tayari kwa mchezo wa marudiano wa klabu bingwa barani Afrika dhidi ya Township Rollers FC Machi 17 mwaka huu.

Jumla ya wachezaji 20 na viongozi 11 wakiwemo nane wa benchi la ufundi wamekuwa sehemu ya msafara huo.

 Yanga SC yawaliza Watanzania, Warudi jangwani vichwa chini

Wawakilishi hao wa Tanzania Bara katika  michuano ya klabu bingwa Barani Afrika, Yanga walikubali kipigo cha mabao 2 – 1 kutoka kwa Township Rollers FC katika mchezo wa awali uliyopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.









Serikali Yasema Deni la Taifa Lafikia Sh47.756 Trilioni

0
0
Serikali Yasema Deni la Taifa Lafikia Sh47.756 Trilioni
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amesema hadi Desemba 2017, deni la Taifa lilikuwa limefikia Sh47.756 trilioni na tathmini zinaonyesha bado ni himilivu.

Akiwasilisha mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na ukomo wa bajeti ya Serikali kwa mwaka 2018/19 mjini hapa leo Machi 13, 2018, Dk Mpango amesema deni la nje lilikuwa  Sh34.148 trilioni sawa na asilimia 71.5 na deni la ndani ni Sh13.607 trilioni sawa na asilimia 28.5.

Hata hivyo amesema uwiano wa deni hilo na Pato la Taifa kwa mwaka wa fedha 2017/18 ni asilimia 34.4 ikilinganishwa na ukomo ambao ni asilimia 56.

“Uwiano wa deni la nje na mauzo ya nje ni asilimia 81.1 ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 150. Hii inamaanisha kuwa uwezo wetu wa kulipa deni bado ni imara,” amesema.

Amesema Serikali inaendelea kuchukua tahadhari kwa kukopa kwenye vyanzo vyenye masharti nafuu kuhakikisha mikopo hiyo inaelekezwa kwenye miradi ya maendeleo.

Baraza la Wazee wa Chadema Laomba Kukutana na Rais Magufuli

0
0
Baraza la Wazee wa Chadema Laomba Kukutana na Rais Magufuli
Baraza la Wazee wa Chadema limemuomba Rais John Magufuli kukutana na  wazee ili kubadilishana nao mawazo sambamba na kumpa ushauri wa masuala mbalimbali yanayoendelea nchini.

Akizungumza leo Jumanne Machi 13, 2018 katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, katibu mkuu wa baraza hilo, Roderick Lutembeka amesema kumekuwa na mambo mengi yanayopigiwa kelele, ni vyema rais akakutana na wazee ili wamueleza mambo hayo.

“Ni lazima kama Taifa tuchukue hatua mapema kabla hatujachelewa. Rais Magufuli akubali kuitikia wito wa kukutana na wazee ambao watakuwa na ujasiri wa kumshauri ili kuepusha Taifa kuingia kwenye majanga,” amesema.

Amesema suala la wazee kukutana na rais, kimekuwa ni kilio cha muda mrefu na kwamba nchini Kenya viongozi wameweza kukaa meza moja na kumaliza tofauti zao.

“Lazima tukae tujue mustakabali wa Taifa hatuwezi kusema hakuna tatizo. Tunamtaka akutane na wazee, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa tuzungumze kwa kuwa hii ni nchi yetu wote na si ya chama kimoja,” amesema.

Amesema mambo yanayopaswa kuzungumziwa ni suala la Katiba Mpya, hasa katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Amesema pia matukio ya watu kutekwa na kuuawa yameongezeka, “miezi sita iliyopita tulizungumzia mambo haya lakini naona ndio yanaongezeka.”

“Wazee tumeuziwa mno kuhusu suala la Abdul Nondo hasa pale Waziri wa Mambo ya Ndani (Mwigulu Nchemba) alipotoa kauli kuwa kijana huyu alijiteka. Tulitegemea polisi wafanye uchunguzi, sasa kama waziri mhusika tayari ameshatoa hukumu tutegemee nini kwa hawa polisi. Tunajenga nini ndani ya mioyo ya hawa vijana ambao walijitoa kumtetea kijana mwenzao kama si chuki.”

Mapenzi Yamliza Nisha Atamani Kuwa Bachela Ajifariji na Sikomi ya Diamond

0
0
Mapenzi Yamliza Nisha Atamani Kuwa Bachela Ajifariji na Sikomi ya Diamond
Wimbo wa msanii Diamond Platnumz ‘Sikomi’ wamfariji  na kumtoa machozi muigizaji Nisha   baada ya mpenzi huyo kuonekana kupitia kipindi kigumu katika mapenzi  na kutamani kuwa Bachela.

Hivi karibuni kumekuwa na stori kuwa aliyekuwa mpenzi wa Nisha amekwapuliwa na mwanadada Snura Mushi ambaye ndiye anatoka naye kimapenzi.

Hata hivyo muimbaji huyo amekuwa akikanusha hilo kwa kueleza wapo pamoja kikazi tu na si vinginevyo.

Wimbo huo ambao maudhui yake unazungumzia mapenzi kwa mtu ambaye ametendwa, unasikika katika video ambayo ameiposti Nisha katika ukurasa wake wa Instagram ambapo anaonekana akiliakwa uchungu.



Breaking News: Mkuu wa Wilaya awaweka ndani Diwani na Mtendaji kata

0
0

kuu wa Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe John Palingo amemuweka ndani Diwani wa Kata ya Vwawa kupitia tikeki ya Chama cha NCCR Mageuzi Saul Mwakatundu na Mtendaji wa kata hiyo Rose Vicent kwa kile kinachodaiwa wamefanya ubadhirifu wa Fedha za Mradi wa Zahanati. 
Aidha yameelezwa leo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Vwawa. 

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya hiyo alipoulizwa na Muungwana blog kuthibitisha tukio hilo amesema ni kweli, lakini hawezi kuelezea kwa undani kwakua
yupo kwenye kikao. 

"Ni kweli lakini siwezi kueleza kiundani, nipo kwenye kikao hivyo nitafute kesho asubuhi" Palingo 

Shamsa Ford afichua kinachowashinda mastaa wa kike katika mahusiano

0
0

sanii wa Filamu Bongo, Shamsa Ford amefunguka sababu ya baadhi ya mstaa hasa wa kike kutodumu katika mahusiano. 

Muigizaji huyo amesema mahusiano ya watu maarufu hayadumu kutokana wanaingiza umaarufu wao katika mahusiano yao. Kupitia ukurasa wake Instagram Shamsa ameandika; 

“Nimegundua mahusiano mengi ya watu maarufu hayadumu kwa sababu wengine huwa wanaleta Ustar hadi kwenye mahusiano, hata mtu wa kawaida akiwa na uhusiano na mtu maarufu ni mara chache sana kudumu,” amesema. 

“Hasa kwa upande wa wanawake huwa tunaamini ustar ndo kila kitu kwa mwanaume kumbe sio, sasa sijui hatuna elimu ya ustar au vipi kwa hapa Bongo, maana ingekuwa ustar shida Beyonce na Jay Z wasingedumu mpaka leo na hawa ndo mastar wa dunia,” amesisitiza. 

Soma Pia; Hayawi hayawi, Shamsa Ford aolewa 

September 2016 Shamsa Ford alifunga ndoa na mfanyabiashara wa maduka ya nguo Rashidi Saidi a.k.a Chidi Mapenzi.

Rais wa Ufaransa apongeza utendaji kazi wa serikali ya Tanzania

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan jana amekutana na kuzungumza na Balozi mpya wa Ufaransa nchini Mhe. Frederic Clavier ambaye aliongozana na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) Bw. Emmanuel Baudran.

Katika mazungumzo hayo ambayo yalifanyika Ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Balozi Clavier aliwasilisha salaam za Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na kusema, “Rais wa Ufaransa ana uhakika na Tanzania ijayo na anaunga mkono jitihada za maendeleo zinazofanywa na Rais Magufuli.”

Balozi huyo mpya wa Ufaransa nchini ambaye amekutana na kuzungumza na Mheshimiwa Makamu wa Rais aliipongeza Tanzania kwa kuwa mstari wa mbele katika masuala mbali mbali ya Kimataifa na kusema “Tanzania ni nchi yenye utulivu na Amani kitu ambacho kinaipa taswira nzuri Umoja wa Mataifa”.

Mhe. Balozi alimjulisha Makamu wa Rais kwamba Ufaransa imekusudia kuimarisha uhusiano zaidi na Tanzania wa Uchumi na Siasa na kuanzisha majadiliano mbali mbali katika masuala ya Mazingira,Mabadiliko ya Tabia Nchi.

Balozi Clavier alimjulisha Makamu wa Rais kuwa mwezi ujao kutakuwa na ugeni wa wafanya biashara kati ya 30 au 40 kutoka nchi ya Ufaransa ambao watakuja kujionea fursa mbali mbali za kibiashara na uwekezaji zinazopatikana nchini Tanzania.

Mhe. Balozi alimuelezea Makamu wa Rais azma ya Ufaransa kushirikiana na Vyuo Vikuu vya Tanzania katika kuanzisha na kuendesha kozi mbali mbali kwa manufaa ya pande zote mbili.

Mwisho aliipongeza Serikali kwa mapambano dhidi ya rushwa na urasimu jambo litakalo wavutia wawekezaji wengi nchini.

Aidha, Bw. Emmanuel Baudran Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa alisema Shirika lao linakusudia kuanzisha kiwanda cha vifaa vya umeme wa jua (solar) mkoani Shinyanga pia shirika hilo limeshafanya miradi ya uboreshaji maji taka katika manispaa ya Temeke na wanaendelea na mikakati ya uanzishwaji wa miradi mingine.

Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alimshukuru na kumpongeza Balozi wa Ufaransa kwa kazi nzuri wanazofanya hapa nchini.

Alimhakikishia kwamba Serikali ya Tanzania ipo tayari kutoa ushirikiano kwa mambo yote muhimu yenye maslahi kwa wananchi.

Wakati huohuo Makamu wa Rais alikutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkazi wa WFP nchini Mhe. Michael Danford.

Upungufu wa Nguvu za Kiume Waishtua Serikali...Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya March 14

0
0


Upungufu wa Nguvu za Kiume Waishtua Serikali...Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya March 14

TANZIA: Mwanafizikia Maarufu Stephen Hawking Afariki Dunia

0
0
Prof Stephen Hawking, mwanafizikia maarufu duniani, amefariki dunia akiwa na miaka 76, familia yake imetangaza.

Mwingereza huyo alifahamika sana kwa kazi yake ya kisayansi kuhusu uwepo wa eneo katika anga za juu ambapo nguvu za mvutano huwa za juu sana kiasi kwamba miali nururishi au hata mwanga hauwezi kuponyoka.

Kwa Kiingereza, eneo hilo hufahamika kama 'Black Hole', Alitumia hilo katika kujaribu kufafanua kuhusu asili ya vitu vyote duniani na angani.

Alikuwa mwandishi wa vitabu kadha maarufu vya sayansi kikiwemo A Brief History of Time (Historia Fupi kuhusu Wakati).

Watoto wake, Lucy, Robert na Tim, wamesema: "Tumehuzunishwa sana kwamba baba yetu mpendwa ametuacha."

"Alikuwa mwanasayansi muhimu na mtu wa kipekee ambaye kazi zake na mchango wake vitaendelea kukumbukwa kwa miaka mingi."

Polisi yawashikilia Viongozi na wafuasi 20 Chadema

0
0
Takribani watu 20 wanaodaiwa kuwa wafuasi wa Chadema akiwemo diwani wa Kata ya Mabatini, Deo Mbibo wanashikiliwa na polisi baada ya kukamatwa walipokuwa wameenda kuhani msiba wa mwanachama mwenzao.

Akizungumzia tukio hilo mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Mwanza, Leonard Nundi amesema tukio hilo limetokea leo Machi 13, saa kumi jioni ambapo wafuasi hao wakiwa zaidi ya 500 walienda kuhani msiba huo na ghafla polisi waliwavamia na kumtaka mfiwa kuongea naye.

“Chanzo cha vurugu ni baada ya askari hao kuvamia msibani na kumhitaji mfiwa ambaye ni Laurent Chiro kwa ajili ya mazungumzo, waliposhindwa kuelewana walimchukua diwani na viongozi wengine waliokuwa meza kuu na kuwapandisha kwenye gari la polisi,” amesema Nundi.

Amesema wanachama waliokuwa msibani waliogomea kitendo hicho na kuanza kuwarushia mawe polisi ambao nao walianza kujihami kwa kupiga mabomu ili kuwatawanya.

Akizungumzia tukio hilo, kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi pamoja na kudai yuko wilayani Kwimba, lakini amesema wafuasi hao wamekuwa na kawaida kukusanyika na kufanya vikao vyao vya kisiri.

Mmoja wa wanachama aliyekuwa eneo la tukio, Emmanuel Tumbo amesema wafuasi hao wametoka katika kata zote 18 za Jiji la Mwanza amba

Chemical Afunguka "Sio Rosa Ree tu, Sitaki Ku-Battle na mtu yeyote"

0
0
Rapper Chemical amesema moja ya vitu asivyovipenda ni kushindanishwa katika muziki.

Msanii huyo ambaye anafanya vizuri na ngoma ‘Asali’ ameiambia ITV kuwa suala la kushindanishwa na Rosa Ree lingeanza wakati anatoka na ngoma zake kama Sielewi na VIP ila sio sasa.

“Sio Rosa Ree tu, sitaki ku-battle na mtu yeyote, mimi nafanya muziki wangu mwenyewe, ukitaka kushindana na mimi maana yake unaingia kwenye anga la Chemical, na ukiingia kwenye anga ya mtu huwezi kwa sababu kila mtu ana namna anavyopeleka muziki wake,” amesema.

“Nishatoa Sielewi mkaniona, nishatoa VIP mkaniona kabla hata ya huyo Rosa Ree, nilitoka kipindi kulikuwa hamna female rapper,” ameongeza Chemical.

Chemical kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya iitwayo Struggling wakati Rosa Ree anatamba na ngoma ‘Marathon’ aliyomshiirikisha Bill Nass.

Yanga timu pekee iliyoshinda mechi nyingi mfululizo VPL hadi sasa

0
0
Kwa mujibu wa takwimu za michezo ya ligi kuu Tanzania bara (VPL) Yanga ndiyo timu pekee ambayo imeshinda mechi nyingi mfululizo kati ya timu tatu za juu zinazowania ubingwa wa ligi hadi sasa.

Yanga imeshinda mechi nane zilizopita mfululizo na kujikusanyia alama 24. Tangu Januari 21, 2018 iliposhinda 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting, mabingwa hao mara tatu mfululizo wa VPL wameendelea kushinda mechi zao za ligi hadi Machi 12 walipoishinda Stand United kwa magoli 3-1.

Mara ya mwisho Yanga kushindwa kupata ushindi kwenye mchezo wa ligi ilikuwa Januar 17, 2018 Mwadui ilipowalazimisha suluhu kwenye uwanja wa Uhuru, Dar.


  • 21/01/2018 Ruvu Shooting 0-1 Yanga
  • 27/01/2018 Azam 1-2 Yanga
  • 03/02/2018 Lipuli 0-2 Yanga
  • 06/02/2018 Yanga 4-0 Njombe Mji
  • 14/02/2018 Yanga 4-1 Majimaji
  • 18/02/2018 Ndanda 1-2 Yanga
  • 09/03/2018 Yanga 3-0 Kager Sugar
  • 12/03/2018 Yanga 3-1 Stand United
Simba inafuata nyuma ya yanga, wekundu wa msimbazi wameshinda mechi tano mfululizo kati ya nane lakini imeshinda mechi sita kwa ujumla kati ya hizo nane (kuna mechi ambayo walishinda lakini haikuwa kwenye mfululizo wa mechi za ushindi) walijikuta wakilazimishwa sare mbili na timu za shinyanga (mwadui 2-2 simba, simba 3-3 stand united).

Simba bado inashikilia rekodi ya klabu ambayo bado haijapoteza mchezo hata mmoja wa ligi baada ya kucheza mechi 20.

Vinara hao wa ligi hadi sasa wamefanikiwa kutengeneza alama 20 kati ya 24 ambazo walikuwa wakiziwania katika michezo nane iliyopita.


  • 18/01/2018 Simba 4-0 Singida United
  • 22/01/2018 Kagera Sugar 0-2 Simba
  • 28/01/2018 Simba 4-0 Majimaji
  • 04/02/2018 Ruvu Shooting 0-3 Simba
  • 07/02/2018 Simba 1-0 Azam
  • 15/02/2018 Mwadui 2-2 Simba
  • 26/02/2018 Simba 5-0 Mbao
  • 02/03/2018 Simba 3-3 Stand United

Azam bado ipo kwenye mbio za ubingwa wa ligi licha ya mwendo wake wa kusuasua, katika mechi nane ziliopita imeshinda mechi tatu tu mfululizo, lakini katika hizo mechi nane wameshinda michezo minne wamepoteza mechi mbili na kutoka sare michezo miwili.

Katika michezo nane iliyopita, azam wamepata jumla ya pointi 14.


  • 27/01/2018 Azam 1-2 Yanga
  • 03/02/2018 Azam 3-1 Ndanda
  • 07/02/2018 Simba 1-0 Azam
  • 11/02/2018 Kagera Sugar 1-1 Azam
  • 16/02/2018 Lipuli 0-0 Azam
  • 03/03/2018 Azam 1-0 Singida United
  • 08/03/2018 Azam 1-0 Mwadui
  • 11/03/2018 Azam 2-1 Mbao
Dick Dauda

Mourinho “Ni Kocha Mbovu Katika Historia ya EPL”

0
0
Manchester, England
Kocha mkuu wa Man United amejibu wa vijembe ambavyo vililengwa na aliyekuwa kocha wa Crystals Palace Bwana Frank De Boer. De Boer alisema Rashford ni mchezaji mzuri lakini hapaswi kucheza chini ya Jose Mourinho. Kauli hii imekuja baada ya rashford kufanya vizuri kwenye mchezo wake dhidi ya Liverpool Ugani Old Trafford kwa kudumbukiza kamba mbili.



Jose Mourinho nae hakukaa kimya baada ya kusema kuwa hawezi kujibizana na kocha mbovu kuwahi kutokea katika historia ya Ligi kuu England. De Boer alifukuuzwa Crystals Palace mwezi wa 9 mwaka jana baada ya matokeo mabovu. Alifanikiwa kuiongoza Palace kwenye michezo mitano na siku 77 kama meneja wa Palace. Matokeo mabovu ya kufungwa michezo minne kati ya mitano iliwatia wasiwasi mkubwa sana uongozi wa Palace hali iliyofanya kumtimua.



Kauli ya Mourinho imekuja baada ya kuulizwa kuhusu uwezekano wa Rashford kuanza kwenye mchezo wa klabu bingwa dhidi ya Seville.



akasema “nimeona baadhi ya komenti kutoka kwa kocha mbovu kuwahi kutokea katika ardhi ya waingereza akiongelea wachezaji wangu, anachokisema huyo kocha hata simuelewi, anadai kuwa Rashford hapaswi kufundishwa na kocha kama mimi? Mimi nachoangalia ni ushindi tu sio vingine, kama Rashford angefundishwa na yeye angekuwa amejifunza kufungwa tu maana hakuna kitu De boer anachojivunia zaidi ya kupoteza mechi ovyo”


“wanasema kuwa simpi kijana nafasi, nadhani hao wanaosema hivyo hawajielewi, ukijaribu kuangalia takwimu, Rashdord ni moja kati ya wachezaji watano waliocheza michezo mingi zaidi Man United,. Sasa unasemaje simpi nafasi? Kikubwa alichohitaji Rashford ni nafasi ya kucheza basi, mimi sifundi mtu namna ya kucheza, nachompa ni nafasi ya kupata uzoefu mengine ni jitihada za mchezaji.”

Kauli hizi zimeambatana pia na maneno yaliyotolewa na Garry Neville lakini Mourinho aliona asimwache De Boer hivi hivi. De Boer anasema nafasi ambayo Rashford anayopewa ni finyu, na mara nyingi amebanwa na mbinu za mourinho ambazo zinalenga zaidi kupata matokeo bila kuangalia namna ya kukuza vipaji vya vijana wadogo.

United Inajianda kukutana na Sevila katika mchezo wa marudiano ugani Old Trafford baada ya mchezo wa kwanza kutoka sare ya bila kufungana. Man United haijawahi kupoteza mchezo wowote nyumbani kwenye michuano ya UEFA tokea mwaka 2013 walipofungwa na Real Madrid.

Michael Owen alishagazwa sana na matokeo yale kwa kuai ni aibu kwa Man United kufunga magoli 7 kwenye michezo 15 dhidi ya Vilabu vya Hispania. Ila Michael Owen bado anaamini Ol Trafford ni mlima mkubwa sana maana Man United imeruhusu magoli machache sana kwenye michuano ya uefa hivyo hategemei Sevilla kupata magoli mengi. Matokeo ya awali yalipondwa sana na mchezaji wa zamani wa Man United Roy Keane.

Kauli za Roy keane zimekebehi aina ya uchezaji wa Man United kwa kudai kuwa hakukuwa na haja ya Kikosi cha Man United kuhangaika kumkaba Ever Banega kana kwamba wanamkaba Messi au Ronaldo.

Amesema kwa sasa United inemtegemea De Gea ni aibu kubwa kwa tinmu kubwa kama hii kuishi kwa kudra za Golikipa huku miguu ya washambuliaji ikiwa na kigugumizi. Anaamini kuwa lawama nyingi ziwaendee Sanchez na Lukaku ambao wameshindwa kabisa kupenya lango la wapinzani na anaamini kuwa watakuwa na deni kubwa sana mbele ya mashabiki kwenye mchezo wa hivi leo. Hofu kubwa ipo kwa Anthonio Martial, Paul Pogba, pamoja na Ander Herrera ambao wote haijulikani kama wataanza au lah.

Kutana na Mtatibu Mongwa Mganga wa Waganga Sasa Tupo Mikoa Karibu Yote Nchi Kukusaidia Wewe

0
0
KUTANA NA MTABIBU MONGWA MGANGA WA WAGANGA SASA WAKO MIKOANI KARIBU YOTE NCHINI...
.
HIVYO WATATOA TIBA MAENEO YOTE YA MBEYA ,DODOMA, IRINGA , MOROGORO, MWANZA,ZANZIBAR

==>KWA WALE WENYE KUHITAJI TIBA

Husafisha nyota na kutoa Pete za bahati na kwawale walio sumbuka kwaajili ya matibabu na hawakufanikiwa chochote sasa njoo ujionee miujiza hapo kwahapo bila malipo yoyote malipo baada yakazi napia humpa mtu jini la mali kwayule anaye taka kumiliki bila mashariti yoyote
Tunatibu magonjwa mbalimbali yaliyo shindikana mpenzi aliye kukimbia nakumrudisha kwa masaa 24 tu napia natoa dawa za nguvu za kiume kuurefusha uume paka pale unapotaka .
Natoa dawa za biashara na mvuto ==tunatoa dawa zauzazi kwa wale kina mama wenye matatizoya uzazi walio angaika kwa muda mrefu bila kupata mafanikio yoyote njoo umalize tatizo lako sasa
Natoa mazindiko yanyumba na mwili biashara na mvuto kazini
Kupandisha nyota ili kungaa kupandishwa cheo kazini kurudisha mali zilizo pote zilizo ibiwa kuzulumiwa
Kesi zilizo shindikana uzimaliza mara moja namengine mengi ya siri piga simu

+255 764291657

Trump Amfukuza Kazi Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Rex Tillerson

0
0
Trump Amfukuza Kazi Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Rex Tillerson
RAIS Donald Trump  amemwondoa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Rex Tillerson, na amepanga kumteua Mkurugenzi wa Shirika la Ujasusi la nchi hiyo (CIA), Mike Pompeo, kuchukua nafasi ya waziri huyo.

Maofisa wa Ikulu ya Marekani wamesema hatua hiyo ya rais huyo ni kutaka kuonyesha mabadiliko makubwa katika timu ya maofisa wa masuala ya usalama wa taifa katika juhudi zake anazozifanya, yakiwemo mazungumzo na Korea ya Kaskazini.

Ijumaa wiki iliyopita, Trump alimtaka Tillerson aachie ngazi, ambapo waziri huyo alikatisha safari zake barani Afrika jana na kurejea Washington. Kutoelewana kati ya Trump na Tillerson kumekuwepo kwa miezi mingi ambapo ilimbidi rais huyo kufikia uamuzi huo alioufanya.

Sababu hasa ya kutoelewana huko haifahamiki, lakini imeonekana kwamba wawili hao wamekuwa wakitofautiana katika sera za masuala la zana za nyuklia kuhusisna na Iran. Hata hivyo, msemaji wa Tillerson alisema kwamba waziri huyo alikuwa na dhamira ya kuendelea katika nafasi hiyo na hakuelewa sababu yoyote iliyosababisha ang’olewe.

Rex Tillerson ameondolewa madarakani ikiwa ni siku moja tangu aondoke nchini Kenya alipokuwa kwenye ziara ya kikazi na kuelekea Ghana ambako alikuwa anaendelea na ziara yake Barani Afrika.

Aidha, Trump amemteua Gina Haspel kama mwanamke wa kwanza kuwa Mkurugenzi wa CIA. Tillerson aliapishwa Februari 2017 kushika wadhifa huo

Mtandao wa Wanafunzi: Hatuamini Uchunguzi Uliofanywa na Polisi Kuhusu Abdul Nondo

0
0
Mtandao wa Wanafunzi: Hatuamini Uchunguzi Uliofanywa na Polisi Kuhusu Abdul  Nondo
Mtandao wa wanafunzi nchini Tanzania (TSNP) umesema taarifa walizo nazo za nini hasa kilichomsibu mwanafunzi mwenzao, Abdul Nondo zinakinzana na zile zilizotolewa na Jeshi la Polisi baada ya kufanya uchunguzi.

Taarifa za kupotea kwa Bwana Nondo katika mazingira ya kutatanisha ziliibuka tarehe 6 Machi baada ya Nondo kutuma ujumbe kwa mmoja wa marafiki zake usiku wa manane akisema kuwa usalama wake uko hatarini.

Akizungumza na Shirika la Utangazaji la BBC Jumanne hii muda mchache baada ya kutoa ripoti yao juu ya uchunguzi, msemaji wa TSNP Helllen Sisya amesema bado wanasubiri kauli na Nondo mwenyewe ili kujua nini kilitokea.

“Sisi bado hatuamini Uchunguzi uliofanywa na polisi kwa kuwa hatujamsikia Nondo akiongea na kile tulichoelezwa na polisi mkoani Iringa na hiki tulichokisikia leo kwa polisi Dar es Salaam haviendani”, alisema Sisya.

Mtandao wa Wanafunzi Tanzania ambao ulitoa taarifa kwa Umma kuhusu kupotea kwa Abdul Nondo,hawakubaliani na taarifa hiyo ya polisi kwa kudai kuwa inakanganya,Polisi wanadai kuwa alipatikana akiendelea na shughuli zake za kawaida alipoenda kumtembelea mpenzi wake na wakati wao walipata taarifa kutoka kwa jeshi la polisi wa Iringa kuwa Nondo alifika kituoni hapo akiwa hajitambui.

Mapema leo Jeshi la polisi nchini Tanzania lilizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam,Abdul Nondo aliyedaiwa kupotea katika mazingira ya kutekwa ulikuwa uzushi.

Kamanda wa Polisi,Lazaro Mambosasa amedai kuwa taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamii na kuzua taharuki mnamo tarehe 6,Machi kwa madai kuwa mwanafunzi huyo ametekwa na watu wasiojulikana si za kweli kwa kuwa uchunguzi wa jeshi la polisi umebaini kwamba mwanafunzi huyo alikutwa akiendelea na shughuli zake za kawaida na wala hakutekwa au kutoa taarifa kuwa ametekwa.

Baada ya Kumwagana na Zari, Diamond Kufunga Ndoa na Huyu

0
0
Baada ya Kumwagana na Zari, Diamond Kufunga Ndoa na Huyu
Mara baada ya kumwagana na mama watoto wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kisha kumuahidi mama yake kuwa mwaka huu lazima afunge ndoa, staa wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, ameibua gumzo la aina yake juu ya ni nani atakayemuoa huku warembo kadhaa wakianikwa.

Machi 8, mwaka huu ilikuwa ni Siku ya Wanawake Duniani ambapo Diamond alitumia siku hiyo kuwatakia heri wanawake mbalimbali wakiongozwa na mama yake, Sanura Kassim ‘Sandra’, zilipendwa wake watatu, Zari, Wema Sepetu na Hamisa Mobeto.

Kufuatia kauli yake hiyo, kuliibuka tafrani kwenye mitandao ya kijamii ambapo warembo kadhaa walihusishwa kuwa huenda mmojawapo ‘akaokota dodo chini ya mpera’ kwa kuolewa na Diamond.

Gazeti hili la Risasi Mchanganyiko linakuletea uchunguzi na uchambuzi wa kina juu ya uwezekano wa mwanamke ambaye ataolewa na jamaa huyo;

Pamoja na kwamba Zari hataki kusikia ishu ya msamaha, lakini uchunguzi wetu ulibaini kwamba, endapo wawili hao wataamua kusameheana kwa kusikiliza maombi ya mashabiki wao ambao wanataka warudiane kisha wakaweka ustaa pembeni na kukubali kusameheana, basi wanaweza wakafunga ndoa.

Zari anabebwa na kigezo cha kuwa boss lady. Kwamba hamtegemei Diamond kwa lolote kwani bibiye pesa imemtembelea, jambo ambalo kwa Diamond anaona atapata mteremko wa malezi ya kifamilia hivyo yeye atabaki kujikita kwenye ishu ya kusaka tu mafanikio kupitia muziki wake.

Hata hivyo, ilibainika kwamba, uwezekano wa Diamond kumuoa Zari ni mdogo kwa kuwa alishapata alichokitaka yaani watoto wawili, Tiffah na Nillan na mbaya zaidi bado suala la umri wa Zari wa miaka 36 ni tatizo kwani ndiyo kwanza Diamond ana 26 na damu inachemka.


Mobetto.

Hamisa Mobeto na Diamond hawakuanza mapenzi yao juzi. Kwa mujibu wa Mobeto, wamedumu kwenye uhusiano yapata miaka tisa kabla ya kujaliwa mtoto mmoja wa kiume, Prince Dully baada ya Diamond kuchepuka kutoka kwa Zari.

Inaaminika kuwa, uhusiano wa Mobeto na Diamond ulianza hata kabla hawajawa mastaa hivyo ni vigumu kuwatenganisha kwani wametoka mbali na wanajua kuvumiliana kwa mengi.

Hata hivyo, suala la Diamond kumuoa Mobeto lina uwezekano mdogo mno kwani walichokitaka ni mtoto na tayari wamempata huku mrembo huyo akiwa ameshazaa na bosi maarufu wa redio jijini Dar. Inaaminika alizaa na bosi akiwa bado yumo ndani ya uhusiano na Diamond hivyo kuna ishu ya usaliti ambayo inapunguza asilimia za wawili hao kufunga ndoa.


WEMA

Baada ya Diamond kumwagana na Wema yapata miaka minne iliyopita alitua kwa Zari. Uchunguzi wetu ulibaini kwamba, tangu Wema aachane na Diamond hajawahi kutulia na mwanaume huku kukiwa na shinikizo kubwa kutoka

kwa mashabiki wao wakiomba usiku na mchana warudiane na wafunge ndoa, japokuwa hakuna aliye tayari kwa hilo.

Hata hivyo, uwezekano wa Diamond na Wema kufunga ndoa haupo kwa sababu wameshasema kwamba, hakuna mapenzi tena kati yao badala yake wapo kikazi zaidi.

Wema atakuwa miongoni mwa watangazaji wa Wasafi TV ambapo anamchukulia Diamond kama bosi wake.


TUNDA

Video queen Tunda Sebastian, anapenda kujiita Boss Baby ili aonekane ana pesa. Naye anatajwa kuwa mmoja wa warembo wanaomchanganya Diamond kutokana na uzuri na taarifa kuwa ‘eti hajatumika sana’ ukilinganisha na wengine. Pia Tunda anabebwa na utoto na kutozaa hivyo Diamond anadaiwa kutaka kuzaa naye ili amwachie ‘chata’ kama alivyofanya kwa Mobeto.

Kufuatia hali hiyo, Tunda amekuwa ‘kiguu na njia’ kila anapokatiza Diamond naye anakuwa nyuma kuanzia safari za Rwanda, Kenya na Afrika Kusini.

Hata hivyo, uwezekano wa Tunda kuolewa na Diamond inasemekana ni kiduchu mno kwa kuwa Tunda hana pesa kama Zari pamoja na kwamba wanapendana kama makinda ya njiwa.



Huddah ‘Boss Chick’

Kuna taarifa kuwa, endapo Diamond atataka kutoka nje ya Tanzania, basi anaweza kujituliza nchi jirani ya Kenya. Mrembo Huddah Monroe wa Kenya amekuwa kwenye mkwaruzano wa mara kwa mara na Zari baada ya kugundua kuna kinachoendelea kati ya mrembo huyo na Diamond.

Kama ilivyo kwa Zari, Huddah anayejiita Boss Chick ni mwanamuziki na mjasiriamali ambaye huvuna mkwanja mrefu kwa kulipwa kwa kuonekana kwenye matukio makubwa.

Mbali na Kenya, kuna taarifa kuwa, hivi karibuni Diamond alitangaza kukita mizizi nchini Rwanda ambapo aliahidi kununua nyumba na kujenga kiwanda nchini humo. Wataalam wa mambo wanasema, kutokana na uzuri wa warembo wa Rwanda ambao ni warefu kama twiga, ni vigumu kwa Diamond kuchomoka hivyo kuna uwezekano wa atakayeolewa akatoka nchini humo.


MSHINDI BBA Dillish Mathews

Uchunguzi huo pia ulibaini kwamba, endapo Diamond atataka kutoka nje ya Tanzania na Afrika Mashariki, basi mrembo kutoka Namibia, Dillish Mathews ambaye ni mshindi wa Big Brother Africa mwaka 2013 anaweza kutwaa nafasi ya kuwa mke wa Diamond.

Dillish anatajwa kuwa miongoni mwa wanawake waliokuwa wakimnyima Zari usingizi kutokana na kuwepo kwa tetesi za muda mrefu kwamba wanatoka kimapenzi japokuwa ilikuwa ni kwa siri kubwa.

Mwishoni mwa mwaka jana, Diamond na Dillish waliripotiwa kuonekana wakijiachia kwenye Visiwa vya Zanzibar katika hoteli ya kifahari ya La Gemma.

Dillish anabebwa na vigezo vingi. Moja, ni mwanamuziki kama yeye na ni hosti wa vipindi vya runingani (television personality) kama ilivyo kwa Zari, Wema na mtangazaji Peniel Mungilwa ‘Penny’ ambaye naye aliwahi kuwa mpenzi wa Diamond.

Kigezo kingine kikubwa ni kwamba, Dillish ni boss lady kwani baada ya kuibuka Mshindi wa BBA alilamba Dola za Kimarekani laki tatu (300,000) zaidi ya shilingi milioni 600 za Kibongo ambazo amewekeza kwenye miradi mbalimbali ikiwemo migahawa nchini kwake, Namibia na Afrika Kusini.

Pia ana jina kubwa Afrika na ni kifaa matata kama Wema.

Hata hivyo, hakuna uhakika kwa asilimia mia moja kuwa ndiye wa kuolewa, lakini kwa kuwa ana mkwanja kama Zari, anaweza ‘kuokota dodo’ kwa Diamond kwani kuna madai mazito kwamba ‘eti anapenda kitonga, ganda la ndizi au mteremko’.

DADA ZAKE

Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, dada zake Diamond, Esma Khan ‘Esma Platnumz’ na Mwanahawa Abdul ‘Queen Darleen’ walisema kuwa, hawawezi kumpangia kaka yao huyo juu ya mke atakayetaka kumuoa.

“Mimi yeyote atakayeletwa ni wifi yangu,” alisema Esma.

“Diamond haniingilii kwenye mambo yangu ya uhusiano na mimi siwezi kumpangia, yeyote atakayemuoa kwetu ndiye huyohuyo,” alisema Queen Darleen

DIAMOND ANASEMAJE?

Katika mazungumzo na gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita juu ya atakayemuoa, Diamond alisema kuwa, hakumtaja jina mrembo yeyote, lakini ni lazima mwaka huu afunge ndoa.

“Nipo busy na uzinduzi wa albam yangu ya A Boy From Tandale kwa wiki kama mbili hivi, nikitulia tutazungumza hilo. Lakini sijataja jina lolote,” alisema Diamond.

Baada ya Mambo Kumwendea Kombo Pretty Kind Amwangukia Waziri Shonza

0
0
Baada ya Mambo Kumwendea Kombo Pretty Kind Amwangukia Waziri Shonza
KUTOKANA na hivi karibuni kufungiwa kujihusisha na sanaa kwa miezi sita na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza kutokana na kujiachia nusu utupu mitandaoni, msanii wa filamu na muziki, Suzan Michael ‘Pretty Kind’ amemwangukia waziri huyo kwani mambo yanamwendea kombo.

Akipiga stori na Za Motomoto News, Pretty Kind alisema kuwa, kwa sasa yupo kwenye harakati za kuandika barua kwa Waziri Shonza kwa ajili ya kumuomba msamaha, angalau ampunguzie adhabu kwa kuwa amekuwa hohehahe asiyejielewa afanye nini.

“Nimeshaomba sana msamaha na ninaendelea kuomba ambapo kwa sasa ninaandika barua ya kuomba msamaha kwa naibu waziri maana maisha hayaendi,”  alisema Pretty Kind.
Viewing all 104431 articles
Browse latest View live




Latest Images