Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104414 articles
Browse latest View live

"Asiefanya Kazi Asile, Asipo Kula Afe- Rais Magufuli

0
0
"Asiefanya Kazi Asile, Asipo Kula Afe- Rais Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo March 14, 2018 ameweka  jiwe la msingi katika sehemu ya pili ya ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa yaani “Standard Gauge” inayoanzia Morogoro hadi Makutupora Mkoani Dodoma.

Akiongea na wananchi na viongozi katika hafla hiyo JPM amewata Watanzania kufanya kazi kwa bidii ili kuacha kulalamika vyuma vimekaza.

"Asiefanya kazi asile, asipo kula afe, hiyo ndiyo lugha ya kuwaambia ukweli, mtu kama hafanyi kazi halafu analalamika vyuma vimebana amevibana mwenyewe" -Rais Magufuli

"Asiyefanya kazi na asile na asipokula afe" -Rais Magufuli

Mwanajeshi Aliyemuua Askari Mwenzie Afikishwa Mahakamani

0
0
Mwanajeshi aAiyemuua Askari Mwenzie Afikishwa Mahakamani

Mwanajeshi MT 109795 Private Ramadhan Mlaku mwenye umri wa miaka 28 amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka la mauaji ya askari mwenzie, MT 79512 SGT Saimon Munyama.

Mshtakiwa huyo alifikishwa mahakama hapo akiwa kwenye gari la Jeshi la kubebea wagonjwa huku akiwa na majeraha miguuni.

Akisomewa shtaka lake na Wakili wa Serikali, Mosie Kaima mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba amedai kuwa mshtakiwa anakabiliwa na kosa moja la mauaji.

Inadaiwa mshtakiwa huyo ambaye ni Mwanajeshi wa Kambi ya Jeshi Makongo ametenda kosa hilo October,30, 2017 akiwa Makao Mkuu ya JWTZ Upanga Ilala Dar es Salaam ambapo alimuua askari mwenzie MT 79512 SGT Munyama.

Baada ya kusomewa shtaka hilo, Hakimu Simba amesema mshtakiwa haruhusiwi kukiri wala kukana kosa hilo kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.

Pia Hakimu Simba amesema kosa hilo halina dhamana kwa mujibu wa sheria. Wakili Mosie ameeleza kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, anaomba kesi iahirishwe hadi tarehe nyingine.

Hakimu Simba ameutaka upande wa mashtaka kuhakikisha unakamilisha upelelezi kwa wakati, ambapo ameahirisha kesi hiyo hadi March 28,2018.

Baada ya kusomewa shtaka hilo mshtakiwa alipandishwa tena katika Gari la Jeshi la kubebea Wagonjwa na kupelekwa mahabusu.

Nay wa Mitego: Nimechoshwa na Skendo Huu ni Mwaka wa Roho Mbaya

0
0
Nay wa Mitego: Nimechoshwa na Skendo Huu ni Mwaka wa Roho Mbaya
Msanii wa muziki Bongo, Nay wa Mitego amesema kwa sasa hataki tena kusikia mambo ya skendo zaidi ya kufanya kazi tu.

Nay wa Mitego ambaye anafanya vizuri na ngoma ‘Mikono Juu’ ameiambia Planet Bongo ya EA Radio kwa mwaka huu anahitaji kutoa ngoma kali pekee na si vinginevyo.

“Huu sio mwaka wa kupigishana na watu kelele ni kazi tu ndio zinakuwa zinaongea, hata kwa wewe mtangazaji ukisikia skendo hata usinipigie simu, so huu ni mwaka wa roho mbaya, panapo majaaliwa next week tutaonyesha huu ni mwaka wa roho mbaya,” amesema Nay.

Hata hivyo licha ya kauli hiyo ya Nay kwa sasa kumekuwepo na stori kuwa Nini na Nay wa Mitego wapo katika mahusiano ya kimapenzi tangu kutoa ngoma yao iitwayo Niwe Dawa ingawa wote wawili hukanusha pindi wanapoulizwa.

Makamu wa Rais TFF Michael Wambura Aingia Matatani

0
0
Makamu wa Rais TFF Michael Wambura Aingia Matatani

Makamu wa Rais wa Shirikisho la soka nchini TFF Michael Richard Wambura, ameimgia matatani kwa tuhuma za kupokea pesa kinyume na taratibu za shirikisho hilo pamoja na makosa mengine ya kinidhamu.

Wambura amefikishwa mbele ya Kamati ya maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF ambayo inakutana leo Jumatano Machi 14, 2018 ambapo pamoja na mambo mengine kamati hiyo itajadili suala lake.

Makosa matatu ya Wambura yatakayojadiliwa na kamati leo ni kupokea fedha za shirikisho malipo yasiyo halali, kugushi barua na kushusha hadhi ya Shirikisho.

Wambura ambaye amewahi kushika nyadhifa mbalimbali kwenye soka la Tanzania ikiwemo klabu ya Simba na Chama cha soka mkoa wa Mara, alichaguliwa kuwa makamu wa Rais kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Dodoma mwaka jana.

Mama Kanumba: Natamani Kumtembelea Lulu Gerezani Tatizo Sina Maelewano Mazuri na Ndugu Zake

0
0

Mama Kanumba: Natamani Kumtembelea Lulu Gerezani Tatizo Sina Maelewano Mazuri na Ndugu Zake
Mama wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa amesema anatamani kwenda kumuona mwigizaji Lulu Michael anayetumikia kifungo cha miaka miwili jela lakini kwa bahati mbaya hawana maelewano na ndugu zake.

Akizungumza na MCL Digital leo Machi 14, 2018 Flora amesema yeye kama mzazi anaumizwa na hali anayopitia Lulu na anatamani kwenda kumuona ili kumpa moyo, ila ndugu wa mwigizaji huyo wanamuona kama ndiyo chanzo cha kufungwa.

Amesema wanaomlaumu wanapaswa waelewe kwamba yeye alishasamehe kwani hata angefungwa miaka 100, haiwezi kumfanya Kanumba arudi.

“Tangu Lulu kahukumiwa nimekuwa nikipokea lawama na watu kunitusi kuwa mimi ndiyo sababu, huku wakisahau kwamba mimi nilishasamehe kama binadamu na siyo niliyekuwa mlalamikaji katika kesi hiyo isipokuwa alishatakiwa na Serikali,” amesema Flora na kuongeza:

“Lakini yote namuachia Mungu kwa kuwa naamini kufungwa kwa msichana huyo hakuwezi kunirudishia mtoto wangu.”

Novemba 13, mwaka jana Lulu alihukumiwa kifungo cha miaka miwili baada ya kupatikana na hatia ya kumuua bila kukusudia mwigizaji mwenzake, Kanumba.

Siku ya Kanumba

Wakati mwaka huu, Kanumba akiwa anafikisha miaka sita tangu afariki dunia ghafla, wasanii waliopitia mikononi mwake wanatarajia kuibeba siku ya Kanumba ambayo huadhimishwa Aprili 7 kila mwaka.

Akilizungumzia hilo, Flora amesema mwaka huu shughuli hiyo imebebwa na wasanii hao kupitia kikundi chao kinachoitwa Soweto.

Ameeleza ratiba ya siku hiyo, ni watu kukusanyika nyumbani kwake Kimara Temboni kuanzia asubuhi na baadaye wataelekea katika kaburi lake lililopo Kinondoni kwa ajili ya kufanya ibada, kisha kurejea tena nyumbani kwa ajili ya chakula cha pamoja.

Vilevile, siku hiyo kutazinduliwa jarida linaloelezea maisha ya Kanumba tangu kuzaliwa hadi kifo chake huku ndani yake kukiwa na filamu mbili zilizofanya vizuri ya ‘Uncle JJ’ na ‘This is It’.

Mimi Nasema Tuzaliane Tu- Rais Magufuli

0
0
Mimi Nasema Tuzaliane Tu- Rais Magufuli
Rais John Magufuli amesema idadi kubwa ya watu nchini haina budi kuendana na maendeleo kwani watu wanapokuwa wengi wanakuwa na sauti na hivyo akawataka Watanzania waendelee kuzaliana.

“Juzi tuliambiwa kwa sasa tumefikia watu milioni 55, watu wanasema kwa nini tunazaliana, mimi nasema tuzaliane tu,” amesema.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Machi 14, wakati wa uzinduzi wa reli ya kisasa (Standard Gauge), Makutupora, Dodoma.

“Lakini idadi hiyo ya watu ni lazima wachape kazi, mfano Denmark ina watu milioni tano lakini wana maendeleo mpaka wanazisaidia nchi nyingine zenye watu milioni 55 kama Tanzania,” amesema.

Amesema ujenzi wa reli utatoa ajira za moja kwa moja zaidi ya 30,000 na zisizo za moja kwa moja 600,000.

Nikiandika Wimbo na Kalamu Nyekundu Una hiti Balaa- Chidi Benz

0
0
Nikiandika Wimbo na Kalamu Nyekundu Una hiti Balaa-  Chidi Benz
Msanii wa muziki wa hip hop Bongo, Chid Benz amedai katika maisha yake ya kimuziki ikitokea akaandika wimbo na kalamu nyekundu ni lazima ifanye vizuri (hit).

Rapper huyo ameiambia Clouds Fm kuwa kitu hicho kilitokea katika kolabo kati yake na Mwasiti ‘Hao’ na alimueleza wazi muimbaji huyo kuwa hiyo ngoma ingekuwa kubwa kabla hata ya kutoka.

“Nilimwambia Mwasiti mimi nina tatizo moja nikiandika wimbo na kalamu nyekundu, hiyo ni balaa, hit balaa, lakini sio wewe umeenda kuninunulia dukani unipe,” amesema Chidi Benz.

Katika hatua nyingine Chidi Benz amesema kolabo yake bora kwa muda wote ni hiyo aliyofanya na Mwasiti kwani ilichukua hadi tuzo nchini Kenya.

Wivu wa Mume wa Linah Wamkosesha Mikataba ya Kazi

0
0
Wivu wa Mume wa Linah Wamkosesha Mikataba ya Kazi
Mwanamuziki aliyekuwa anafanya kazi nchini Kenya, Mr. Kesho amefunguka na kudai kila wivu aliokuwa nao mume wa Linah ambaye pia ni meneja wake Shaban Mvhomvu unamkosesha mkataba wa kazi na Linah.

Mume wa Mwanamuziki wa Bongo fleva Linah Sanga ambaye pia ni mzazi mwenzake Shaban Mchovu maarufu kama Director Ghost amedaiwa kuwa na wivu sana kwa mkewe kiasi ya kwamba ameshindwa kupata kazi.

Mr. kesho amefunguka kuwa aliporudi kufanya nchini Tanzania alianza kusimamiwa na Adam Mchomvu ambaye pia alikuwa anamsimamia Linah lakini baada ya kutoa wimbo mmoja aliondoka kwenye label hiyo na inasemekana kabisa kuwa chanzo ni ukaribu wake na Linah.

Ukaribu wake na Linah ulisababisha habari kuenea kuwa anatoka kimapenzi na Linah jambo ambalo linasemekana halikumfurahisha meneja ambaye ni mpenzi wa Linah.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Enews ya East Africa Tv, Mr. Kesho amefungukia tuhuma hizo za kuwa na Linah na ukaribu wao:

Hapana hakuna kilichoendelea kati yangu mimi na Linah ila tu alikuwa ni mshkaji wangu ambaye nina nyimbo naye tumefanya naye wimbo hakuna mapenzi kati yangu na Linah lakini kama meneja alikataa kurenew mkataba kisa wivu basi sio kosa langu”

Rayvanny Afuata Nyayo za Diamond Naye Kufunga Ndoa Hivi Karibuni

0
0
Rayvanny Afuata Nyayo za Diamond Naye Kufunga Ndoa Hivi Karibuni
Baada ya Diamond kuomba baraka kwa mama yake kuhusu kufunga ndoa mwaka huu, naye Rayvanny amedokeza kuhusu suala hilo hilo la ndoa.


Dokezo hilo la ndoa limekuja  wiki chache baada ya msanii huyo na mpenzi wake kurejea kutoka  Mkoani Mbeya, nyumbani kwa akina Rayvanny.

Kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram, Ray aliweka picha yake akiwa katika vazi la suti na kuandika “Bwana Harusi” naye mpenzi wake Fayvanny hakubaki nyuma na akuamua kujibu kuashiria wapo katika michakatao hiyo ya ndoa.

“Ohh bby ❤ I can’t wait for the day 💍………🙈😷 …………….. & you will be mine forever (sooooooon) @rayvanny ❤”

Irene Uwoya Ampa Onyo Kali Dogo Janja " Thubutu Uwone Tena Ndo Utanijua "

0
0
Irene Uwoya Amuwashia Moto Dogo Janja Baada ya Kutaka Kuoa Mke wa Pili " Thubutu Uwone Tena"

Mke wa msanii wa muziki Dogo Janja, Irene Uwoya ametoa majibu juu ya habari zilizopo za mumuwe kutaka kuongeza mke wa pili hadi wanne.

Uwoya ametoa majibu hayo baada ya kukuta habari zimezagaa katika mitandao mbalimbali juu ya mpingo ya mumuwe aliyoweka ya kutaka kufikisha idadi ya wake wanne katika ndoa.

“Ndoutajua mim Kabila gani…thubutu uwone tena wasikudanganye @dogojanjatz,” ameandika mrembo huyo katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram mapema leo baada ya kuona stori za mumuewe za kumuongezea mke zikitawala.


Katika kipindi cha The Playlist ya Times Fm kilichoruka juzi ( 12-03-2018) mkali huyo wa ‘Wayu Wayu’ alidai kuwa anampango wa kuongeza mke wa pili hadi wanne kila baada ya miaka 10.

Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH simba Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili

0
0
Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH issa simba said Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Maalim Hussein Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU. Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
Atamfanya Atimize 5 zote kwa Muda Mfupi.

Issa simba said Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumal6uiza Tatizo lako..
Anatibu kwa Kutumia Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA. Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI. Nguvu za KIUME, Humaliza Kesi zilishindika ndani ya siku 14 tu..na mengi zaidi

Piga simu +255 622588038au 0679119679 au +255 764318107

NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE...

Sakata la Mwanafunzi wa UDSM Kujiteka...Lazidi Kuzua Utata...Taarifa ya Kamanda Mambosasa Yatofautiana na Kamanda wa Polisi Iringa

0
0
Kamanda wa Polisi Dar, Lazaro Mambosasa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Juma Bwire wameonekana kutofautiana kimaelezo katika kuelezea sakata la kutoweka kwa Mwanafunzi wa UDSM na Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi, Abdul Nondo...

Hapo awali, RPC Bwire alieleza kuwa kijana Abdul Nondo alifika katika kituo cha Polisi Wilayani Mafinga na kuelezea kuwa ametekwa na watu wasiojulikana

Naye RPC Mambosasa, hapo jana alieleza kuwa Polisi Kanda Maalumu ya Dar ililetewa taarifa kutoka Polisi Iringa kuwa Abdul Nondo alipatikana Mafinga akiwa mwenye afya njema na akiendelea na shughuli zake za kawaida na hakuripoti mahali popote si kwa Mwenyekiti wa Mtaa, Mtendaji wa Kata, wala Polisi.

Mapokezi ya a Boy From Tandale ya Diamond Platnumz Nchini Kenya

0
0
Kwanza kabisa Diamond kafanya kitu kizuri kwa kuonesha ni kwa namana gani nchi hizi mbili zipo vizuri na kushirikiana vema si kama ambavyo watu wengine huleta ushirikiano wa maneno

Sasa hivi Kenya na Tanzania wamekuwa ndugu kwa kuunganishwa na msanii wetu Diamond planumz.

Kwa haraka haraka nimejaribu kupitia taarifa mbali mbali za kwenye media nikaona kenya wanampo support ya kutosha kijana wetu.

Kwa pamoja tunapaswa kumsapot na kumpongeza kwa hatua hiyo na kwa ukalimu wa watu wa kenya wanao ufanya kwa ndugu yetu huyu.

VIDEO:

Wafuasi CHADEMA waliokamatwa msibani kupandishwa kizimbani

0
0
Mwanza. Wafuasi zaidi ya 10 wa Chadema waliokamatwa wakiwa nyumbani kwa mwanachama mwenzao kuhani msiba wanatarajiwa kupandishwa kizimbani muda mfupi ujao.

Watu hao, leo Machi 14, 2018 tayari wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza na kuwekwa katika mahabusu mahakamani hapo kusubiri kukamilika kwa taratibu za kimahakama ili wasomewe mashtaka dhidi yao.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi watu hao walikamatwa eneo la Mabatini Machi 13, 2018 baada ya kutokea kutoelewana kati yao na askari polisi.

Amesema askari hao walikuwa wakifuatilia nyendo za wafuasi hao tangu walipokuwa wakikusanyika kutoka sehemu mbalimbali za Jiji la Mwanza kwenda nyumbani kwa wanachama mwenzao kwa kile kinachodaiwa ni kuhani msiba.

Katika tukio hilo, polisi walilazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi kutawanya kundi la watu zaidi ya 500 waliokuwa kwenye eneo hilo.

Chanzo: Mwananchi

Viongozi Wawili Mtandao wa Wanafunzi Wahojiwa DCI

0
0
Viongozi Wawili Mtandao wa Wanafunzi Wahojiwa DCI
Mpaka kufikia leo Machi 14, 2018 saa 7:45 mchana viongozi wawili wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP) walikuwa wamekwisha hojiwa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).

Akizungumza na MCL Digital, ofisa habari wa mtandao huo Helleh Sisya ambaye naye pia miongoni mwa watakaohojiwa, amesema hadi muda huo waliohojiwa ni mkaguzi wa haki za binadamu , Alphonce Lusako na katibu wa mtandao huo, Malekela Brigthon.

Viongozi wengine ambao hawajahojiwa hadi muda huu ni Sisya na mkurugenzi wa Idara ya sheria, Paul Kisabo.

TFF Yateua Ammy Ninje Kuwa Kocha wa Muda

0
0
TFF Yateua Ammy Ninje Kuwa Kocha wa Muda
Shirikisho la mpira wa Miguu Tanzania TFF leo limetangaza kumteua Ammy Ninje kuwa kocha wa muda wa timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 20 Ngorongoro Heroes.

Ngorongoro Heroes inatarajia kucheza michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Morocco na Msumbuji, kabla ya kuwavaa DR Congo katika mchezo wa kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Vijana (AFCON U20).

Kocha huyo ambaye amewahi kukaa kwenye benchi la ufundi la klabu ya Hull City ya nchini England, sio mara ya kwanza kufundisha timu ya taifa ambapo mara ya kwanza aliiongoza Kilimanjaro Stars kwenye michuano ya kombe la CECAFA japo haikufanya vizuri

Timu hiyo inaundwa na baadhi ya nyota waliofanya vizuri kwenye kikosi cha vijana wenye umri chini ya miaka 17 Serengeti Boys kilichoshiriki fainali za AFCON U17 mwaka jana nchini Gabon.

Tanzia: Mwalimu wa Sekondari Afariki Ghafla Baada ya Kupewa Uhamisho wa Kufundisha Shule ya Msingi

0
0
Tanzia: Mwalimu wa Sekondari Afariki Ghafla Baada ya Kupewa Uhamisho wa Kufundisha Shule za Msingi
Mwalimu Mathew Clement wa shule ya Sekondari Milongodi iliyopo wilayani Tandahima Mkoani Mtwara, ambaye ni mwenyeji wa Kilosa mkoani Morogoro, amefariki dunia kwa shinikizo la moyo baada ya kupewa uhamisho wa kwenda kufundisha shule ya msingi.


Kwenye taarifa iliyotolewa na Mkiti CWT (W) Kilosa Bwana Mussa Mnyeti, imesema kwamba Mwalimu Clement amefariki ghafla baada ya kupata presha, siku moja baada ya kuitwa na kupewa barua ya uhamisho wa kwenda kufundisha kutoka shule ya sekondari na kwenda kufundisha shule ya Msingi.

Taarifa zaidi zinasema kwamba mwalimu Clement licha ya kupata presha hiyo, pia alikataa kupokea barua ya uhamisho huo.

Mwili wa marehemu tayari umeshasafirishwa kwenda mkoani Morogoro kwa mazishi na taarifa zinasema kwmaba mwalimu huyo ameshazikwa, huku akiwa ameacha mke na watoto wawili.

Hivi karibuni serikali imeanzisha mfumo wa kuhamisha walimu wa sekondari na kwenda kufundisha shule za msingi, ikiwa na lengo la kukidhi uhaba wa walimu na kuboresha elimu ya msingi, jambo ambalo limekuwa likilalamikiwa na baadhi ya walimu waliokumbwa na sakata hilo.

Mbunge Akamatwa na Polisi kwa Kupanga Mauaji

0
0
Mbunge Akamatwa na Polisi kwa Kupanga Mauaji
Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Laikipa Mshariki nchini Kenya Mathew Lempurkel, amekamatwa tena na polisi nchini humo, baada ya kuachiwa siku ya tarehe 12 machi, kwa tuhuma za kupanga mauaji.


Kwa mujibu wa Polisi wa Laikipa Kaunti Kamanda Simon Kipkeu, bwana Lempurkel ambaye alikuwa mbunge kupitia chama cha ODM, atafikishwa mahakamani baada ya wapelelezi kukamilisha taarifa zao.

Lampurkel alikamatwa baada ya kutishia kukichoma moto kituo cha polisi cha Rumuruti, kwa lengo la kumtoa mtuhumiwa ambaye alikuwa mahabusu mwezi Julai, 2016.

Mahakama iliamua kuwa Lampurkel ana kesi ya kujibu juu ya vurugu alizofanya, na kisha kukamatwa tena kwa tuhuma za kupanga njama hizo za mauaji.

ZFDA Yateketeza Kilo 48 za Nyama Kutoka Afrika Kusini

0
0
ZFDA Yateketeza Kilo 48 za Nyama Kutoka Afrika Kusini

Mamlaka ya Chakula na Dawa Zanzibar (ZFDA), imeteketeza  kilo 48 za nyama kutoka Afrika Kusini baada ya Serikali kusitisha uingizaji nyama kutoka nchini humo kutokana na mlipuko wa bakteria wa listeria.

Ilibainika kuwa nyama hizo ziliingizwa nchini kinyume cha sheria.

Nyama hizo ni mali ya kampuni ya Qamar ya Vingunguti jijini Dar es Salaam, ilikamatwa Uwanja wa wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Karume mwishoni mwa wiki iliyopita.

Akizungumza leo Machi 14 wakati wa zoezi hilo, mkuu wa kitengo cha uchambuzi wa hatari zinazotokana na chakula wa ZFDA, Aisha Suleiman amesema kilichosababisha kuteketezwa kwa nyama hiyo ni katazo lililotolewa na ZFDA baada ya kutokea mlipuko wa ugonjwa wa listeriosis.

Amesema ZFDA ndiyo yenye majukumu ya kuhakikisha wananchi wanapata chakula salama.

Aisha amesema uamuzi ya katazo hilo umetokana na uwapo wa maradhi ya Listeriosis nchini Afrika Kusini, hivyo ofisi yao imepiga marufuku uingizwaji nyama, maziwa na samaki kutoka nchi hiyo.

 Bakteria wa listeria, wanaosababisha maradhi ya listeriosis, wamesababisha vifo vya watu zaidi ya 180 Afrika Kusini.

Amesema katazo hilo si kwa Zanzibar pekee bali na Tanzania bara na nchi nyingine kutokana na utaratibu wa biashara kimataifa.

“Hili katazo siyo sisi tu, ni utaratibu wa kimataifa kwamba kutokana na maradhi ya listeriosis bidhaa za nyama, samaki, maziwa ni marufuku kuingizwa nchini sasa hii kampuni ya Qamar LTD ya Dar es Salaam wao waliamua kuingiza nyama hiyo, tumeikamata na kuiangamiza.” amesema Aisha.



Wanawake Wengi Wanafunga na Kumuomba Wapate Mume Bora Lakini Wanashindwa Kumtambua Pale Anapokuja

0
0
Namna mojawapo ya wewe kuwa mwanamke bora na mwenye busara ni kuwa na uwezo wa kujua na kutambua mwanaume sahihi na kisha kum-keep! Wanawake wengi wanafunga na kumuomba Mungu awape mume bora lakini wanashindwa kumtambua pale anapokuja katika maisha yao.

Kwa wanaosoma Biblia, Abigaili mke wa Nabali anatabainishwa kwa namna alivyokua na uwezo kumtambua mwanaume bora. Unaambiwa Abigaili alivyosikia kwamba Daudi anakuja katika mji aliopo kulipiza kisasi kwa mumewe Nabali ambaye alimtukana Daudi, alijiandaa haraka haraka, akaandaa misosi mitamu na kukimbia kwenda kumpokea Daudi.

Na alivyoonana nae tu, alimuinamia na akazungumza maneno matamu ya kumpamba Daudi, ambayo kwayo Daudi hajawahi kuyasikia kwa mtu yeyote yule.. Alimsifia kuhusu ukuu wake (Daudi). Alimwambia kuwa ulimwengu mzima una taarifa ya namna Daudi alivyo mbabe wa vita
..alizungumza maneno matamu sana juu ya Daudi na maneno hayo yaliugandisha kabisa moyo wa Daudi. (1 Samuel 25: 18- 32). Maneno matamu yakamfanya Daudi aghairi mipango ya kumuangamiza Nabali, na akarudi alikotoka.

Wiki moja baadae, Nabali, mume wa Abigaili alivyofariki kwa kupigwa na MUNGU, Daudi akamtumia Abigail WHATSAPP MESSAGE akimwambia.."Nimesikia kuwa mumeo amefariki. Ninapita katika mji wako kesho, je utapenda upate kahawa na mimi ? Kilichotokea kinabaki kuwa historia, Abigaili akawa Malikia wa mfalme Daudi.

Kuolewa na mtu sahihi sio kuomba tu, bali inaendana na uwezo wako wa kujitambua wewe binafsi, vipaumbele vyako visivyoathiri matakwa ya huyo mwanaume, kutambua mwanaume sahihi anapokuja kwako na kufahamu ni jinsi gani utamkamata kwa maneno matamu ya kinywa chako...Yes mkamate kwa busara zitokazo kinywani mwako!
Viewing all 104414 articles
Browse latest View live




Latest Images