Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104689 articles
Browse latest View live

Haji Manara afunguka kuachana na Klabu yake

$
0
0
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Klabu ya Simba SC, Haji Manara amefunguka na kusema kwa sasa ameamua kuachana na klabu yake ya Manchester United hadi Kocha wa klabu hiyo Jose Mourinho atakapoondoka.

Haji Manara amesema hayo siku moja baada ya klabu yake hiyo kupigwa bao 2 kwa moja na klabu ya Sevilla hivyo Manchester United kuondolewa kwenye mashindano ya klabu bingwa ulaya.

"Guys kuna vitu siwezi kuviasi..1.Dini yangu,,2.wazazi wangu..Mke na watoto wangu na Simba...ila Manchester nimeiacha hadi Mourinho aondoke...Europe nimebaki na Madrid tu.....Kwangu Jose ndio mtu wa hovyo kupita wote duniani kwa sasa" alisema Haji Manara

Siku tatu zilizopita wakati Manchester United ikikipiga na Liverpool aliahidi kama timu yake itafungwa angehama Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuhamia CHAUMA lakini baahati nzuri timu yake ikashinda ila baada ya kupigwa na Sevilla ameamua kukaa pembeni mpaka kocha Jose Mourinho atakapoondoka.


RC Gambo Atoa Onyo Kali Kwa Watu Watakao Andamana

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ametoa onyo kali kwa watu watakaothubutu kuandamana mkoani humo baada ya kuzagaa kwa taarifa mitandaoni kuwa tarehe 26 April kutakuwa na maandamano ya nchi nzima.

RC Gambo amesema Arusha ni mji wa kitalii hivyo asingependa kuona usalama na amani inatoweka mkoani humo na kupoteza watalii ambao wanasaidia kukuza uchumi wa nchi.

“Arusha ni mkoa wa kitalii hatuwezi kuruhusu mambo yatakayoharibu uchumi na usalama wetu, kama kuna kikundi chochote kinampango kutujaribu, tunatoa tahadhari na kuwakumbusha kuwa upanga haujaribiwi shingoni,“ameeleza Mrisho Gambo kwenye taarifa yake.

Onyo la Gambo ni muendelezo wa maonyo mengine yaliyotolewa na viongozi wengine serikalini akiwemo Rais Magufuli juu ya watu watakaoandamana siku hiyo

Laana ya Kutembea na Mume wa Mtu

$
0
0
Kutembea na mume wa mtu sio jambo zuri japo wanawake wengi wanaona ni kawaida bila kujua wanajilimbikizia laana itakayofanya maisha yao kuwa magumu mbeleni.

Machozi ya uchungu ya mwanamke mwenzio juu ya mume wake hayafutiki haraka.. Ni kama zigo la kinyesi mgongoni linavutiwa na inzi pekeake.

Huyo mwanaume unaemuona Leo ana mke, Pesa na mali na kuona ndo fursa kwako kumpata kwasababu anajua kujali na anapesa za kutosha kukugharamia.... Ukirudi nyuma miaka 10-15-20 mwanaume huyo huyo alikuwa kama huyu unae mkataa leo

Unaye muona hajui kuvaa.... Hana pesa za kutosha.. Hana mali kwahiyo hakufai.

Wanaume wengi wanaanzia chini... Jitihada za wake zao zinawafikisha walipo Leo. Heshimu jitihada hizo.

Heshimu siku walizofunga kwa ajili ya waume zao.
Heshimu machozi waliomlilia Mungu awafikishe walipo...
Heshimu muda na jasho walilolitoa kuhakikisha waume zao wanaonekana watu mbele za watu.

Muombe Mungu akupe wa kwako hata kama masikini mpate utajiri pamoja. Na wewe ubige magoti , ulie na kufunga.

Wanawake wengi wanalalamika hawaolewi au Wachumba wanawaacha bila sababu za msingi. Wanasahau zigo LA kinyesi walilobeba mgongoni. Mwanamke piga magoti muombe Mungu akusamehe kwa kumliza mwanamke mwenzio.

Tuwaombee watoto wetu na kuwaonyesha njia iliyo bora. Kuwafundisha dini ili wawe na mahusiano mazuri na Mungu... wasikumbwe na laana hii.

Ewe mama elimisha watoto wako. Ewe dada elimisha wadogo zako.
Tukishirikiana kwa pamoja tutayafuta machozi ya wanawake

Diamond: Media Zinazokataa Kupiga Nyimbo Zangu Zinapotea

$
0
0
Mwanamuziki wa Bongo fleva na CEO wa label ya WCB, Diamond Platnumz amefunguka na kusema kuwa chombo chochote cha habari ambacho kinaibania WCB kwa njia yoyote basi kitapotea kwani yeye ni kama maji usipokunywa utayaoga.

Diamond amekuwa mmoja wa wasanii ambaye amekuwa na migogoro na media mbali mbali ambapo siku za hivi karibuni Kumekuwa na sintofahamu kati yake na mkurugenzi wa Clouds Fm, Ruge Mutahaba.

Hii imekuja baada ya Diamond kutangaza kuanzisha stesheni zake za redio na Tv ambazo ni Wasafi Radio na Tv ambavyo amesisitiza vitacheza nafasi kubwa katika kukuza mziki wake na hata wasanii kutoka WCB kwa ujumla.

Diamond hivi sasa yuko nchini Kenya, Nairobi ambako ameenda kwenye uzinduzi wa albamu yake ya ‘A boy from Tandale’ ambayo inategemewa kuanza kuuzwa hivi karibuni.

Kwenye mahojiano na Dizzim Online, Diamond amefunguka kuhusu albamu yake ambayo ndani yake kuna nyimbo ambazo amewashirikisha wasanii kadhaa ikiwemo Rick Ross, Neyo na Omarion.

Lakini pia Diamond amefunguka kuhusu Wasafi Tv na Redio ambavyo vinategemea kuanza kuruka hewani siku za hivi karibuni lakini Diamond ameshangaa media zinazotaka kubania mziki wake kwani yeye ndio burudani yenyewe kwaiyo wao kumzuia yeye wanapotea:

"Yaani mimi nimejiwekea mazingira ambayo hata nikilala chumbani lazima utaniongelea huwezi kulala bila kunitaja aidha utawataja watoto wangu, au wasanii wa WCB au hata wapenzi wangu yaani Diamond ni kama Azam vile au mimi kama maji aidha utaninywa au utanioga yaani utajua mwenyewe lakini mimi huwezi kulala bila kunitaja kwaiyo media zinazozuia kazi zangu wanapoteza muda maana mimi ndio burudani na mzalisha burudani”.

Wastara Kikaangoni EATV, Aibua Mapya ya Mange Kimambi, Ali Kiba Kumpa Msaada na Hasimu Wake Kumnyima

$
0
0
Wastara amesema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa kupitia ukurasa wa facebook wa EATV kila siku ya Jumatano kuanzia saa nane mchana mpaka saa kumi jioni, Wastara anasema kuwa alimuandikia barua Diamond Platnumz kuomba msaada pamoja na Alikiba lakini kwa Diamond alionekana yeye ni kama tapeli.

"Niliandika barua kuomba msaada hivyo nilimuandikia Diamond lakini watu wake walimfikishia taarifa kuwa mimi tapeli hivyo hakuweza nisaidia ila pia wakati huo huo nilimuandikia Alikiba na Alikiba akaniambia kuwa kuna watu walikuwa na show yao Kenya ila walikuwa hawana fedha yeye anazohitaji hivyo akaniahidi kuwa atakwenda kufanya show hiyo ili aje kunisaidia, kweli alikwenda na aliporudi aliniletea fedha hizo" alisema Wastara.

Mbali na hilo Wastara amesema kuwa moja ya sababu kubwa kuachana na mumewe Sadifa ilikuwa ni pamoja na mumewe huyo kulazimisha apewe risiti zote alizokwenda nazo kwenye matibabu kwa fedha alizochangiwa na Alikiba, Makamu wa Rais Mama Samia ili yeye akalipwe fedha zote na Bunge.

Aibua mapya kuhusu Mange Kimambi

Msanii wa filamu nchini Tanzania Wastara Juma amefunguka na kumchana mwanaharakati wa mitandaoni Mange Kimambi na kusema kuwa dada huyu ana matatizo ya akili ndiyo maana anakurupuka katika baadhi ya mambo.

Wastara amesema hayo kupitia kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa na EATV kupitia ukurasa wa facebook wa EATV kila siku ya Jumatano saa nane mchana mpaka saa kumi jioni na kusema kuwa Mange Kimambi alizusha juu ya Cannula aliyowekwa mkononi na kusema alijiwekea mwenyewe, Wastara amesema kuwa mbali na kuzusha huko lakini dada huyo alikwenda mbali mpaka kuwauliza madaktari wa hospitali aliyokuwepo kama anatibiwa hapo.

"Mange Kimambi, aliwahoji madaktari India, mimi nikashangaa wale madaktari wanakuja wananiuliza kwani wewe ni nani Tanzania nikawaambia kuwa mimi ni msanii tu wa kawaida kule, wakaniuliza unamfahamu huyu mtu anajiita Mange Kimambi kwenye Instgram anasema ni dada yako, pia mwandishi wa habari anakuulizia mimi nikawaambia sina dada ana cheti cha Milembe" alisema Wastara

Mbali na hilo Wastara amesema kuwa kama Mange Kimambi angekuwa na akili timamu basi alipaswa kuangalia vizuri ile Cannula ambayo alikuwa amewekewa kwani ilikuwa imewekwa vizuri tu na wala si huo uzushi ambao yeye alikuwa anazusha.

JPM Aishukia TRA, Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya March 15

$
0
0

JPM Aishukia TRA, Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya March 15

WASTARA Juma Ataka Mume, Ataja Masharti yake !

$
0
0

Msanii wa filamu nchini Wastara Juma amedai anawachukia wanaume wenye rangi nyeupe kwasababu wanakuwa na matatizo mengi pindi anapokuwa nao katika mahusiano ya kimapenzi ndio maana kwa sasa anawapenda weusi kama aliyokuwa nayo marehemu Sajuki.


Wastara amebainisha hayo wakati alipokuwa anajibu miongoni mwa maswali yaliyokuwa yanaulizwa na mashabiki zake waliokuwa wanataka kufahamu ni mwanaume wa aina gani Wastara anamvutia kuwa naye katika mahusiano ya kimapenzi au kwa sasa endapo atatokea.

"Mimi kiukweli namtaka mwanaume ambae anajiamini ambae hata tukitembea mbele za watu hawezi kuona aibu, anaejali, mwenye mapenzi ya dhati, awe mwanaume wa kweli yaani asiwe 'Punga' ila asiwe na rangi nyeupe maana nawachukia sana wenye rangi hiyo, nampenda mwenye rangi nyeusi", amesema Wastara.

Aidha, Wastara amesema kipindi cha awali alipokuwa anaanza kujihusisha katika masuala ya mapenzi alikuwa na vigezo vingi alivyokuwa anavitaka awe navyo mwanaume kama kifua kikubwa, Six Pack na vinginevyo.

"Kwa sasa sitaki vigezo kwasababu nimejifunza mengi kutoka kwa marehemu Sajuki maana mume wangu alikuwa na Six Packs za ukweli lakini alipokuwa anaumwa zote zikaondoka 'so' kutoka hapo nimejifunza kupenda jinsi mwanaume alivyo maana vingine vinakuja na kuondoka wakati wote", amesisitiza Wastara.

Kwa upande mwingine, Wastara amesema yupo tayari hata sasa kuolewa na mwanaume mwingine ambaye wataridhiana wenyewe kwa kuwa dini yake ya kiislamu inampa fursa ya kuolewa mpaka pale kifo chake kitakapomchukua endapo hatakuwa katika ndoa.

HAWA Watu Ndani ya Serikali Hawamuogopi Mungu - Prof Tibaijuka

$
0
0
Mbunge wa Muleba Kusini(CCM), Anna Tibaijuka amefunguka na kusema kuwa wapo watu ndani ya Serikali ya awamu ya tano hawamuogopi Mungu ndiyo maana wanakuwa wanawaonea wananchi na kuichafua serikali pamoja na Rais Magufuli.


Tibaijuka amesema hayo wakati akiongea na wananchi katika mkutano wa hadhara baadaa ya kuona watu wakilipishwa kodi na kupewa risiti za mwaka 2015 fedha ambazo zinaonekana hazifiki serikalini.

"Serikali ya Rais Magufuli haiwezi kukubali haya mambo wanataka tu kuchafua jina la Rais amini usiamini serikali zinahujuma ndani yake sasa watu wanatokaje Mwanza na kumlazimisha huyu mvuvi mkubwa ambaye ana mitumbwi 28, anakuja mtu mla rushwa serikali ya Magufuli haiwezi kumtoa mtu kule aje kula rushwa huku, Rais Magufuli huyu anayelia usiku na mchana mambo yakae vizuri ila leo nitamtumia risiti zile za watu wake wamekusanya kodi hapa kwa risiti za mwaka 2015" alisema Tibaijuka 

Aidha Tibaijuka amesema kuwa yeye anaamini kuwa Rais Magufuli hawezi kutuma watu kwenda kuchoma nyavu za wavuvi

"Yaani wamemkuta mvuvi yupo stoo anaendelea na mafundi wake kurekebisha hawa watu ambao hata hawamuogopi Mwenyezi Mungu wanaingia mle stoo na kuchoma zile nyavu, sasa watu wanasema siku za mwizi arobaini" alisema Tibaijuka 

BIFU Mpya Mjini, Wasanii Wakufokafoka Watifuana na Kupeana Michambo Kuntu

$
0
0

Wasanii Nikki Mbishi na Moni wa Centrozone wametupiana maneno baada ya hivi karibuni Nikki kusema kuwa kundi jipya la Moni linalofahamika kama MOCO ni lakupita tu wala haliwezi kufika mbali.

 Akiongea kupitia eNEWZ  Moni amesema kwamba  anamshangaa sana Nikki amekuwa ni mtu wa kulalamika na lawama huku akiongeza kuwa siku hizi hata kazi za Nikki  hazioni zaidi anasikika akiwa analalamika tu.

Moni amesema yeye na kundi lake hawafanyi Rap ya kilingeni bali anafanya Rap ya biashara hivyo hayo maneno ya Nikki wala hayamsumbui kwasababu tayari wamefanya kazi nyingi na wanashukuru Watanzania wamewapokea.

Kwa upande mwingine Moni ambaye anatamba na ngoma yake mpya ya Nichum amesema kinachomsumbua Nikki ni uzoefu wake wa kuvunjikiwa na kundi kutokana na uzembe wake huku akimshauri kuwa afanye kazi kwa bidii kwa kuwa anamizizi mizuri na nimuandishi mzuri hivyo asimamie sanaa yake kwanza.

WASTARA Sajuki Ajutia ndoa yake na Mbunge wa CCM

$
0
0

Muigizaji na Mfanyabiashara, Wastara Juma amesema kwenye maisha yake mwanaume anayejutia kuwa naye kwenye mahusiano ni Mbunge wa jimbo la Donge, Sadifa Khamis Juma kwani hakumjua vizuri kabla ya kukubali kufunga naye ndoa.


Akizungumza leo kwenye  kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa kupitia ukurasa wa facebook wa EATV kila siku ya Jumatano kuanzia saa nane mchana mpaka saa kumi jioni, ambapo amesema kwamba alikubali kufunga ndoa na mwanaume huyo pasipo kumjua ni mtu wa aina gani.

"Najuta kuwa na mahusiano na Sadifa kwa sababu sikuwa namjua vizuri. Tulifunga ndoa baada ya kujuana kwa kipindi cha wiki moja. Alikuja kwa njia ya kunipa faraja kwa vile mimi ni yatima, pia mjane lakini pia ni mlemavu. Mtu mimi akiniambia kitu kama hicho anaweza kuiteka akili yangu kabisa," Wastara.

Hata hivyo Muogizaji huyo amesema kuwa moja ya sababu kubwa kuachana na mumewe Sadifa ilikuwa ni pamoja na mumewe huyo kulazimisha apewe risiti zote alizokwenda nazo kwenye matibabu kwa fedha alizochangiwa na Alikiba, Makamu wa Rais Mama Samia ili yeye akalipwe fedha zote na Bunge.

Sheria Hairuhusu Wimbo Uliofungiwa Nchini Kutumika Katika Show Nje ya Nchi- Waziri Shonza

$
0
0
Sheria Hairuhusu Wimbo Uliofungiwa Nchini Kutumika Katika Show Nje ya Nchi- Waziri Shonza

Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa, na Michezo, Juliana Shonza amesema sheria hairuhusu wimbo uliofungiwa nchini kutumika katika show nje ya nchi.

Naibu Waziri amesema hayo leo kupitia kipindi cha XXL cha Clouds ambacho kuliwakutanisha wasanii, wizara na Baraza la Sanaa Taifa (BASATA).

“Sheria hairuhusu wimbo wa msanii husika uliofungiwa hapa Tanzania kwenda kuufanyia show nje ya nchi. Endapo atafanya hivyo atakuwa anakiuka kanuni na sheria za nchi.” amesema Juliana Shonza.

February 28 mwaka huu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilipokea list ya nyimbo 15 zisizokuwa na maadili kutoka kwa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) na kuamuru kutopigwa katika vyombo vya habari.

Chelsea Ndio Basi Tena Aondolewa UEFA Champions League kwa Kichapo cha Magoli 3-0

$
0
0
Chelsea Ndio Basi Tena Wakubali Kichapo cha Magoli 3-0
Baada ya kumalizika kwa baadhi ya game za UEFA Champions League hatua ya 16 bora msimu wa 2017/2018, game ya mwisho ya marudiano ya hatua ya 16 bora kati ya FC Barcelona dhidi ya Chelsea iliyochezwa katika uwanja wa Camp Nou ilikuwa inasubiriwa zaidi.

Matokeo ya game hiyo yalikuwa yanasubiriwa zaidi kutokana na game hiyo kuzikutanisha timu ambazo zinarekodi nzuri katika michuano hiyo miongoni mwao lakini game ilikuwa 50 kwa 50 yoyote anaweza kuchukua ushindi kutokana na mchezo wa kwanza uliyochezwa London ulimalizika kwa sare ya 1-1.

Chelsea wakiwa ugenini usiku wa leo wamejikuta wakikubali kipigo cha magoli 3-0, hivyo Barcelona wamefuzu kwa jumla ya magoli 4-1, magoli ya FC Barcelona ya leo yalifungwa na Lionel Messi aliyefunga mawili dakika ya 3 baada assist safi ya Suarez na dakika ya 63 na Osmane Dembele dakika ya 20.



Ushindi huo sasa unaifanya FC Barcelona kuungana na timu za Juventus, AS Roma, Sevilla, Real Madrid, FC Bayern Munich, Liverpool na Man City zilizokuwa tayari zimefuzu robo fainali, hivyo kwa sasa wanasubiri droo ya UEFA kufahamu kila timu itakutana na timu ipi robo fainali.



Ikumbukwe tu kufunga magoli mawili katika mchezo wa leo kwa Lionel Messi kumemfanya kufikisha jumla ya magoli 100 UEFA Champions League lakini likiwa ni goli la 20 kwa kuvifunga vilabu vya England katika michuano hiyo lakini Barcelona wao wamelinda rekodi yao ya kutowahi kuruhusu magoli mawili katika game za mtoano

Kajala Amkana P Funk " Atabaki tu Kuwa Mzazi Mwenzangu"

$
0
0
Kajala Amkana P Funk " Atabaki tu Kuwa Mzazi Mwenzangu"
STAA wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ‘Kay’, amekanusha vikali madai ya kurudiana na baba mtoto wake, prodyuza Paul Matthyasse ‘P Funk’.

Madai hayo yalikuja hivi karibuni baada mwanamama huyo kutupia kipande cha video katika Mtandao wa Snapchat kinachomuonesha akiwa na P Funk.

“Jamani siwezi kurudiana na P, yule atabaki tu kuwa mzazi mwenzangu. Hiyo video tulikuwa tumekwenda shule kumwona mwanetu, Paula, baada ya hapo kila mtu alichukua hamsini zake,” alisema Kajala aliyezaa mtoto huyo mmoja na P Fun

Natamani Kanumba Angekuwa Hai Amuoe Wema - Mama Kanumba

$
0
0
 Natamani Kanumba Angekuwa Hai Amuoe Wema - Mama Kanumba
Mama Mzazi wa marehemu Steve Kanumba amezungumza baada ya uvumi wa story kusambaa kuwa alikwenda kwa Wema Sepetu na hakufunguliwa mlango kitu kilichopelekea yeye kulalamika, Sasa Mama Kanumba kasema hajawahi kumuomba Wema msaada wala kwenda kwa WEMA.

Ameongezea kwa kusema anampenda Wema Sepetu na isitoshe kama Kanumba angekua hai basi angetamani Kanumba amuoe, pia amezungumzia ishu ya Lulu kasema hana shida naye na ameomba msamaha kwa watu aliowakwaza kuhusu Lulu na isitoshe kama atatoka jela akajishusha kwake yeye hana shida atamkaribisha nyumbani kwake.

Maisha Bado Ninayataka Sithubutu Kujiusisha na Unga- Davina

$
0
0
Maisha Bado Ninayataka Sithubutu Kujiusisha na Unga- Davina
MUIGIZAJI mahiri wa Bongo Movies, Halima Yahaya ‘Davina’ amefungukia safari zake zake za Dubai akisema ni kwa ajili ya biashara halali na si biashara haramu ya madawa ya kulevya (unga).

Akizingumza na Amani kwa njia ya simu akiwa Dubai, Davina alisema kuwa, kila anapokuwa huko kibiashara na akaweka picha mtandaoni, watu humhisihisi kuwa anasafirisha unga, jambo ambalo kamwe hawezi kulifanya.

“Yaani mimi safari zangu ni kwa ajili ya biashara zangu tu na kuhusu kujihusisha na biashara haramu za madawa ya kulevya, mimi huwa nasikia kwenye redio na kwenye magazeti, sithubutu, maisha bado ninayataka,” alisema Davina bila kutaja biashara inayompeleka Dubai mara kwa mara.

Zinaweza zikafungiwa nyimbo zetu zikachezwa za kina Nicki Minaj – Diamond

$
0
0
Zinaweza zikafungiwa nyimbo zetu zikachezwa za kina Nicki Minaj – Diamond
Msanii Diamond Platnumz bado anaonekana kutokubaliana na uamuzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) wa kuzifungia nyimbo zake mbili ambazo ni Waka na Hallelujah.

Muimbaji huyo akizungumza na Classic FM nchini Kenya amesema serikali ni lazima iangalie maudhui ya wimbo husika na msanii husika nini hasa alilenga.

“Huwezi kuimba nyimbo za mapenzi usitaje maneno ya kimahaba, ni uongo kwa sababu utakuwa haufikishi ujumbe,” amesema.
“Nyimbo kama Waka na Hallelujah ni nyimbo ambazo nilifikiria kufanya kitu ili soko lingine watusikilize, serikali lazima ielewe. Na kinachouma zaidi zinaweza zikafungiwa nyimbo zetu zikachezwa za kina Nick Minaj, so ni lazima tuangalie,” amesisitiza Diamond.

February 28 mwaka huu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilipokea list ya nyimbo 15 zisizokuwa na maadili kutoka kwa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) na kuamuru kutopigwa katika vyombo vya habari. Katika list hiyo Nay wa Mitego alifungiwa nyimbo tatu na Diamond nyimbo mbili.

Upasuaji wa 19 Aliofanyiwa Lissu Wafanikiwa

$
0
0
Upasuaji wa 19 Aliofanyiwa Lissu Wafanikiwa
Upasuaji mkubwa wa mguu wa Tundu Lissu uliofanyika  Brussels, Ubelgiji, umefanikiwa.

Taarifa kutoka katika hospitali alimofanyika upasuaji huo, zinaeleza kuwa madaktari wamefanikiwa kurekebisha mguu wa Lissu kwa mafanikio makubwa.

Huu ni upasuaji wa 19 kufanyiwa Lissu baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana akiwa mjini Dodoma, Septemba, mwaka jana.

Lissu ambaye ni mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), yuko Brussels kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa akiendelea na matibabu, akitokea Nairobi, Kenya alikokaa kwa zaidi ya miezi minne akitibiwa.

Kutana na Mtatibu Mongwa Anayesafisha Nyota na Kutoa Pete za Bahati

$
0
0


 KWA WALE WENYE KUHITAJI TIBA

Husafisha nyota na kutoa Pete za bahati na kwawale walio sumbuka kwaajili ya matibabu na hawakufanikiwa chochote sasa njoo ujionee miujiza hapo kwahapo bila malipo yoyote malipo baada yakazi napia humpa mtu jini la mali kwayule anaye taka kumiliki bila mashariti yoyote
Tunatibu magonjwa mbalimbali yaliyo shindikana mpenzi aliye kukimbia nakumrudisha kwa masaa 24 tu napia natoa dawa za nguvu za kiume kuurefusha uume paka pale unapotaka .

Natoa dawa za biashara na mvuto ==tunatoa dawa zauzazi kwa wale kina mama wenye matatizoya uzazi walio angaika kwa muda mrefu bila kupata mafanikio yoyote njoo umalize tatizo lako sasa
Natoa mazindiko yanyumba na mwili biashara na mvuto kazini

Kupandisha nyota ili kungaa kupandishwa cheo kazini kurudisha mali zilizo pote zilizo ibiwa kuzulumiwa
Kesi zilizo shindikana uzimaliza mara moja namengine mengi ya siri piga simu

+255 764291657

Miili ya Watu Yaokotwa Katika Mto Arusha

$
0
0
Miili ya Watu Yaokotwa Katika Mto Arusha
Watu wawili ambao ni wanandoa wamefariki dunia katika Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha baada ya kuchukuliwa na mafuriko katika mto Piyaya Kata ya Piyaya wilayani humo.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Yusuph Ilembo amesema miili hiyo imeonekana leo majira ya asubuhi baada ya maji ya mto huo wa msimu kupungua.

Aidha, Kamanda Ilembo amewataja marehemu hao kuwa ni Ormins Sunguyo na mkewe Nembris Sunguyo ambao walikuwa na mtoto wa mdogo aliyefahamika kwa jina la Oloosukuta Sunguyo ambaye alinusurika kifo.

Kamanda Ilembo alitumia fursa hiyo kuwataka wananchi katika mkoa wa Arusha kuchukua tahadhari kipindi hiki cha mvua na kuepuka kuvuka mito wakati maji yanafurika.

Nabii Aliyemuamuru Muumini ‘Piga Kelele’ Aeleza Tukio lilivyokuwa

$
0
0
Nabii Olivia kutoka kanisa la Repohim Ministry Sinza jijini Dar es salaam amefunguka kwa mara ya kwanza kuzungumzia clip ya video ambayo ilisambaa mtandaoni wiki hii ikimuonesha akimuamuru muumini kupiga kelele kwa nguvu wakati anamuombea hali iliyoleta taharuki mtandaoni.

VIDEO:

Viewing all 104689 articles
Browse latest View live




Latest Images