Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104689 articles
Browse latest View live

Mahakama Yaishukia Upande wa Mashtaka Kesi ya Malinzi

$
0
0
Mahakama Yaishukia Upande wa Mashtaka Kesi ya Malinzi
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema ni aibu kwa upande wa mashtaka kushindwa kukamilisha upelelezi wa kesi inayowakabili vigogo watatu wa TFF ambao wamekaa rumande kwa miezi tisa sasa.

Vigogo hao ni aliyekuwa Rais TFF, Jamal Malinzi, Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine na Mhasibu wa TFF,  Nsiande Isawayo.

Hayo yameelezwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ambapo amesema ni aibu na ajabu kwa upande wa mashtaka kwenda mahakamani na kusema upelelezi bado haujakamilika.

“Ni miezi tisa sasa imepita bila ya upelelezi kukamilika washtakiwa wapo rumande, kinachotakiwa ni ukamilishwaji wa upelelezi wa kesi,” Amesema Hakimu Mashauri.

Pia ametupilia mbali hoja za upande wa utetezi ya kuwa Mahakama hiyo ina mamlaka ya kuwaachia washtakiwa chini ya kifungu cha 225 ,(5) cha sheria ya Mwenendo wa makosa ya jinai.

Kwa upande wa Wakili wa Malinzi na Mwesigwa, Kashindye Thabiti alilalamika mahakamani hapo kuwa wakienda magereza wanakosa uhuru wa wakuwaona wateja wao wakiwa mahabusu.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Mashauri ameahirishwa kesi hiyo hadi March 28, 2018 kwa ajili ya kutajwa.

Washtakiwa hao walipandishwa  kizimbani kwa mara ya kwanza June 29, 2017, wakikabiliwa na mashtaka 28 ya kughushi na kutakatisha fedha Dola za Marekani 375,418. 7.

Ukichezea Amani Unachezea Maisha Yako- Rais JPM

$
0
0
Ukichezea Amani Unachezea Maisha Yako- Rais JPM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa mtu akichezea amani ya nchi amechezea maisha yake.

Rais Magufuli leo Machi 15, 2018 wakati wa uzinduzi wa kiwanda cha kutengeneza sigara cha Philips Moris International mjini Morogoro.

“Ukichezea amani unachezea maisha yako. Unaweza ukadhani wewe uko mbali ukafikiri haitakupata. Isipokupata wewe, itampata hata ndugu yako,” amesema Rais Magufuli.

Hata hivyo Rais amezungumzia mashamba yanayofutwa ameeleza kuwa “Nilishasema mashamba yote yanayofutwa, wapewe wananchi bure, ni mali yao, walidhulumiwa tangu zamani kwa wakubwa fulani fulani kujimilikisha”.

Wastara Ampa Makavu Mange Kimambi....."Dada Mwenye Cheti Cha Mirembe"

$
0
0
Wastara Ampa Makavu Mange Kimambi....."Dada Mwenye Cheti Cha Mirembe"
Msanii wa maigiizo nchini Wastara Juma amefunguka na kuongelea yaliyokuwa yanajiri alipokuwa hospitali na kusema kuwa kipindi yupo katika matibabu yake nchini india , mwanaharakati Mange kimambi aliwapigia simu madaktari na kuwadanganya kuwa ni dada wa Wastara na kutaka kujua  details zake.

Wastara alisema hayo alipokuwa akifanya mahojiano katika kipindi cha kikaangooni live  kinachorushwa na EATV,  Ambae alizusha uongo mwingi kuhusu matibabu ya msanii huyo baada ya kuonekana kwa cannula ambae ilisemekana kuwa imegeuzwa kwa mujibu wa Mange ingawa Wastara mwenyewe alikataa swala hilo.

"Mange kimambi aliwahoji madaktari nikiwa india,mimi nikashaanga kuona madaktari wanakuja wananiuliza mimi ni nani Tanzania, nikawajibu mimi ni msanii ....wakaniuliza  kama ninamfahamu huyu mtu anaitwa Mange Kimambi anasema kuwa ni dada   yangu, na pa ni mwamndishi wa habari anakuulizia, nikawajibu sina dada mwenye cheti cha milembe."

Wastara anasema kuwa kama mange kimambi angekuwa na akili basi alitakiwa kuangalia ile cannula vizuri kabla ya kuanza kuweka maneno katika mitandao kuhusu kudanganya

Ahukumiwa Jela kwa Kumuua Mpenzi Wake Kisa Youtube

$
0
0
Ahukumiwa Jela kwa Kumuua Mpenzi Wake Kisa Youtube
Habari kutoka nchini Marekani ni kwamba binti mmoja amehukumiwa kifungo jela baada ya kumuua mpenzi wake wakati wakicheza mchezo wa kudanganya watu kwenye mtandao wa Youtube ili wapate followers wengi.

Inaelezwa kuwa ‘prank’ hiyo ambayo ilikuwa imeandaliwa na wapenzi hao Monalisa Perez, 20, na Pedro Ruiz, 22, ililenga kufanya kama kijana huyo Pedro amepigwa risasi na Monalisa ili kwamba video hiyo isambae sana mtandaoni.

Mpango huo haukufanikiwa kwani binti huyo alipofyatua risasi ambayo walipanga ipige kwenye kitabu kikubwa ambacho alikuwa amekishika kijana huyu, risasi hiyo ilipenya moja kwa moja na kwenda kumpiga kijana huyo kifuani na kufa papo hapo.

Binti huyo ambaye ni mama wa watoto wawili amehukumiwa kifungo cha miezi sita kwa kuua bila kukusudia.

Simba Yatua Salama Misri, Yapewa Baraka na Ubalozi wa Tanzania

$
0
0
Simba Yatua Salama  Misri, Yapewa Baraka na Ubalozi wa Tanzania
Klabu ya Simba ambayo iliondoka jana usiku nchini Tanzania kuelekea Misri kwa ajili ya mechi ya marudiano na klabu ya Al-Masry kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho, Klabu hiyo imewasili salama nchini humo.

Simba SC wametua mjini Port Said nchini Misri wakipitia Addis Ababa nchini Ethiopia, ambapo wakiwa huko wamekutana na balozi wa Tanzania nchini humo, Meja General Issa Suleiman Nassor na kupewa baraka zote.

Simba na Al-Masry walitoka sare ya goli 2-2 kwenye mchezo wa kwanza ambao ulipigwa hapa Tanzania na watahitaji ushindi kwa namna yoyote au sare ya kuanzia goli 3 ili waweze kusonga mbele.

Kamati ya Bunge Yasusia Taarifa ya Sido

$
0
0
Kamati ya Bunge yasusia taarifa ya Sido
Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira imesusia kupokea taarifa ya Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (Sido), huku ikitoa onyo kwa wateule wa Rais John Magufuli kutekeleza wajibu wao ipasavyo na kwa kasi inayohitajika.

Agizo hilo limetolewa leo Machi 15, 2018 mkoani Singida ambapo kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake, Suleiman Sadiq walipofika kutembelea viwanda kadhaa mkoani humo na mwenyeji wao alitakiwa kuwa ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage.

Akizungumzia leo, Sadiq amesema kamati ya Bunge inapotembelea anapaswa kuwapo waziri, naibu waziri au katibu mkuu, lakini “tumemkuta naibu katibu mkuu na maofisa wengine wa wizara na wale wa Sido, ambao hawakuwa wamejindaa na tumeikataa taarifa yao.”

Amesema Mwijage alipaswa kuwapo wameelezwa amekwenda Morogoro kuhudhuria ufunguzi wa kiwanda cha Sigara eneo la Kingolwira.

“Kwa sasa tupo tu tunatembea tembea hapa Singida, lakini tuseme hawa watendaji wa Rais Magufuli wanapaswa kujitambua na kutekeleza wajibu wao. Kama wameshindwa kutoa ushirikiano kwetu hata kwa kumtuma naibu waziri (Stella Manyanya) au katibu mkuu, hii Tanzania ya viwanda kweli itakuja kama hakuna ushirikiano,” alihoji Sadiq.

Sadiq ambaye ni mbunge wa Mvomero amesema, “tumsaidie Rais Magufuli na sisi katika taarifa yetu tutajua kipi cha kufanya tutakaporudi Dodoma, kwa hiyo sisi kama wabunge hatujapenda kilichotokea leo.”

Wastara: Napitia Katika Wakati Mgumu kwa Sababu ya Sajuki

$
0
0
Msanii wa filamu za bongo Wastara Juma ambaye alikuwa mke wa marehemu Sajuki, ambaye alikuwa mke wa muigizaji marehemu Sajuki, amesema sasa hivi anapitia katika wakati mgumu sana kwa sababu ya Sajuki.


Akizungumza kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa na ukurasa wa facebook wa East Africa Television, na kusema kwamba Sajuki alikuwa kila kitu kwake, na hivi sasa kwa kuwa hayupo tena, ndio sababu anapata wakati mgumu na kumwaga chozi kila akimkumbuka.

Wastara aliendelea kwa kusema kwamba Sajuki alikuwa akimtetea na kumuangalia kwa macho yote, na kuwajibika kwa kuhakikisha kwamba hakuna jambo ambalo litamkuta mke wake na kumfanya aumie, lakini kwa sasa hana wa kumtetea.

“Sajuki ananipa wakati mgumu sana kwenye maisha yangu, alikuwa na nafasi kubwa kwangu, kwenye utendaji wa kazi, pili alikuwa ana jukumu kubwa la kumuangalia Wastara, nilikuwa kama mtoto wake, mimi nilikuwa fighter sana kwenye familia yangu, hivyo alihakikkisha siumizwi na lolote, hayupo tena mtu wa namna hii sasa hivi kwenye maisha yangu, naweza nikatetea wenzangu lakini nikiumizwa mimi sina wa kunitetea, lakini yeye alikuwa anacover nafasi zote, anahakikisha mke wangu haumizwi na kitu chochote”, amesema Wastara.

Wawili hawa walifunga ndoa ambayo iliwashangaza wengi baada ya kupata ajali na Wastara kukatwa mguu, lakini Sajuki alikubali kumuoa akiwa kwenye kiti cha matairi, bila kujali ulemavu alioupata, na watu kuamini kuwa Sajuki alikuwa na mapenzi ya kipekee kwa Wastara, kwa kutomuacha kwenye kipindi kigumu alichokuwa akipitia.

Mimi Mars Afunguka Mwanaume Ambaye ni Vigumu Kuwa Naye Katika Mahusiano

$
0
0
Mimi Mars Afunguka Mwanaume Ambaye ni Vigumu Kuwa Naye Katika Mahusiano

Mwanamuziki Mimi Mars amefunguka aina ya mwanaume ambaye ni vigumu kuwa naye katika mahusiano.

Hitmaker huyo wa ngoma ‘Sitamani’ ameiambia Bongo5 kuwa ni vigumu kutoka na mtu wa kabila lake, “Kabila, sijawahi waza hilo suala, nahisi Mpare mwenzangu, sitokaa nijaribu hilo,” amesema.

“Tabia zetu kidogo, sasa wote tukikaa wawili kule ndani, kwanza hatutoendani ni ile wanasema mafahali wawili hawakai zizi moja,” amesisitiza.

Mimi Mars kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya uitwao Papara, huu ni wimbo wake nne kuachia official baada ya Sugar, Dedee na Sitamani.

Watu Watatu Waliojifanya Wana Mafunzo ya Kijeshi Wasombwa na Mafuriko na Kufa

$
0
0

DODOMA: Watu watatu wakiwemo wawili ambao walijinadi kuwa wanamafunzo ya kijeshi, wamefariki dunia katika matukio mawili tofauti ya kusombwa na mafuriko

Katika tukio la kwanza lililotokea kata ya Nzunguni, Diwani Aloyce Luhega, alisema kuwa katika eneo hilo watu wawili waliojinadi kuwa wanamafunzo ya jeshi walisombwa na mafuriko wakati wakitoka katika majukumu yao ya kazi majira ya jioni

Alisema watu hao walisomba na mafuriko walipojaribu kuvuka katika eneo lenye kivuko ambapo pamejengwa daraja la chini lililokuwa limejaa maji kutokana na mvua iliyokuwa inaendelea kunyesha juzi jioni.

Alisema miili ya marehemu imechukuliwa na Polisi kwa ajili ya hatua nyingine, ikiwamo walipotolewa na ndugu zao kuitambua. Pia aliwataka wananchi kuchukua tahadhari kipindi hiki cha mvua

Alisema "Sasa hivi Polisi wanashughulikia suala hili, sisi kama Serikali ya Kata tumetoa ushirikiano ikiwa ni pamoja na kuitafuta miili hiyo hadi kuipata"

Mashamba Yanayofutwa Wapewe Wananchi Waliodhulumiwa na Wakubwa

$
0
0

MOROGORO: Rais Magufuli asema mashamba yote yanayofutwa wapewe wananchi bure, ni mali yao. Walidhulumiwa kipindi cha miaka ya nyuma na wakubwa fulani kujimilikisha

Aidha, Rais John Magufuli ameagiza wafanyabiashara ndogondogo wa Stendi ya Morogoro kutobugudhiwa, amchaia Shilingi laki moja mama aliyeibua kero hiyo

Amewataka Watanzania kubadilika kwa kuwekeza katika viwanda, kwamba suala la viwanda linawezekana nchini

Rais amesema “Tusirudie tena kuua viwanda Serikali nitaunga mkono viwanda vyote vinavyoanzishwa. Nafahamu kuna baadhi ya vikodi kodi vinavyoleta kero, tayari nimeshatoa maelekezo kwa waziri wa viwanda kuangalia upya hizo kodi,”

Basata na Wizara Amkeni Mnachofanya sasa ni Kijenga Uadui na Wateja Wenu " Wasanii na Mashabiki"

$
0
0

Thanks @divathebawse BASATA AMKENI WAZIRI WA MICHEZO NA NAIBU AMKENI NYIE NDO MNAUA VIPAJI NA SANAAA YA TANZANIA HAMNA SHERIA ZA KUWAPA WASANII WETU NAFASI YA KUFANYA KAZI KWA UBORA ILA SHERIA ZENU ZINAONEKANA KWENYE KUFUNGIA KAZI ZA WASANII TU...KWA UPANDE WANGU NILITEGEMEA KAMA NAIBU WAZIRI MPYA NA KIJANA UNGEANZA KWANZA NA VIKAO AU SEMINA NA HAO WANAMUZIKI NA KUJUA WANASHIDA GANI AU MATATIZO GANI ILI MUELEWANE NA KUWAELIMISHA LAKINI NAONA HILI LA KUFUNGIA WASANII LINA SABABISHA GAP KUBWA KATI YENU....BASATA NA WAZIRI KIJANA EMBU KAENI NA HAWA VIJANA MZIKI WAMEUPIGANIA SANA MPAKA KUFIKA HAPO KWA NGUVU ZAO WENYEWE....WEKENI MAMBO SAWA..

Kutoka kwa Mdau

Mambosasa: Wakiandamana Mitandaoni Hatuna Shida ila Wakiingia Barabarani Watajuta

$
0
0

Kamanda wa jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam Tanzania, Lazaro Mambosasa amefunguka na kusema kuwa kama April 26 mwaka huu watu wataandamana kwa mitandao ya kijamii wao hawana tatizo kwa hilo ila kama wataingia barabarani basi wasijute.

Mambosasa amesema hayo wakati akiongea na kituo cha habari cha kimataifa na kusema kuwa jeshi la polisi limejipanga kuwadhibiti watu ambao watataka kuvunja sheria za nchi kwa kuandamana barabarani. Mambo sasa amesema kuwa jeshi hilo limejipanga vizuri hivyo wanawakaribisha wale ambao watahamisika kuandamana barabarani.

"Ndani ya kanda mimi nasema hakuna maandamano wanahamasishana wanapotezeana muda na wamezoea kufanya hivyo na walitishia kufanya hivyo wakati uliopita lakini tunachosema tumejipanga vizuri sisi ni wasimamizi wa sheria atakayetaka kuvunja sheria atapambana na sisi lakini asijutie matokeo ya kile atakachokutananacho, wakiandamana kupitia mitandao ya kijamii manake hakuna tutakaokutana nao barabarani hivyo wataandamana kwa kuendelea kupeana habari kwenye mitandao na hilo sisi hatuna shida ndio maana tunaendelea kupuuza yanayopangwa lakini yoyote atakayehamasika kupitia mtandao akaja barabarani kwa maana ya kuleta vurugu kuvunja sheria za nchi tutakutana naye tumejipanga"

Mambosasa aliendelea kusema kuwa

"Ulinzi upo tu unataka kujua kiasi gani tumejipanga kwa namna gani? Sisi tupo vizuri katika hilo na tunakukaribisha barabarani kama unataka kuandamana na wewe" alisisitiza Mambosasa

Mange Kimambi amekuwa akihamasisha sana watu kupitia mitandao ya kijamii kuandamana katika siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo kila mwaka sherehe hizo huwa zinafanyika tarehe 26 mwezi wa nne.

Kenya Hali si Shwari...Mafuriko Yapamba Moto mpaka Magari Yanasombwa

$
0
0

Baadhi ya maeneo nchini Kenya yameathirika vibaya baada ya mafuriko ya ghalfa kukata mawasliano ya barabara.

Ripoti kutoka maeneo mbalimbali nchini humo zinaeleza kuwa nguvu ya maji ilikuwa kubwa hivyo baadhi ya watu na magari kusukumwa.

Shirika la Msalaba Mwekundu imeripoti kuwa watu watano waliokuwa kwenye lori walisukumwa na maji eneo la Kitui kilomita 180 Mashariki mwa Nairobi.

Shirika la Msalaba Mwekundu kwenye ukurasa wake wa Twitter imesema baadhi ya barabara nchini humo zimeharibiwa ikiwemo barabara ya Kajiado-Namanga kusini mwa Kenya, na kufanya eneo hilo kushindwa kupitika.

Maelfu ya wakazi wa Nairobi wamekwama na kushindwa kuendelea na shughuli zao kwa sababu ya mvua hizo.

Mvua kubwa inayoendelea kunyesha hivi sasa kanda yote ya Afrika Mashariki imesababisha mafuriko makubwa ambayo miundo mbinu ya barabara za miji ya Nairobi haziwezi kumudu.

Magari ambayo yalijaribu kutumia mabarabara ya Nairobi yalikwama mengine huku yale yenye kimo cha juu yakifaulu kupita.

Kawaida msimu wa mvua nchini Kenya huwa kati ya mwezi Machi na Mei, lakini wadadisi wanasema kuwa safari hii mvua imenyesha kwa wingi zaidi.

Mwanafizikia aliwasilisha mawazo mapya kuhusu ni namna gani ya kuendelea kuwa mkavu wakati wa kutembea kwenye mvua.

Ukikimbia, unaepuka kuloa kwa muda mfupi, hata hivyo utaendelea kuangukiwa na matone zaidi. Je kasi kiasi gani inahitajika?

Franco Bocci, akiongea na jarida la masuala ya Fizikia la Ulaya,anasema kwa pamoja uelekeo wa upepo na kimo cha mtu vinaweza kuwa na majibu.

Mara nyingi, jibu la ujumla ni kukimbia haraka iwezekanavyo: lakini jibu hili linabadilika kutokana na upepo na wembamba.

Mwaka 1987, mtafiti mwingine mwenye asili ya Italia alitetea kwenye jarida kuwa kubadili mbinu hakuthibitishi utofauti huo.

Mwaka 2011, mtaalam wa kutengeneza nguo alitumia jarida hilohilo akisema kuwa kasi inahitajika, kutegemea na uelekeo wa upepo.

Kitu kinachofanya swali hili kuwa gumu ni pamoja na umbo la mwanadamu.

Profesa Bocci alibaini kuwa jibu la suala hili linategemea urefu, upana, uwiano pia uelekeo wa upepo na ukubwa wa matone ya mvua

Maandamano ya Mange Kimambi Yaumiza Kichwa Serikali...Waziri Masauni Nae Ajitosa

$
0
0

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni amejitosa sakata maandamano linalosambaa katika mitandao ya kijamii, kwa kuwaonya wanaotishia kuandamana kwa kusema kuwa vyombo vya ulinzi na usalama viko imara.


Masauni ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Machi 15, jijini Dar es Salaam wakati akipokea vituo sita vya polisi vinavyohamishika vilivyotolewa na kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni.


“Kuna watu wako ndani ya nchi na wengine nje ya nchi wanaotaka kukwamisha ajenda ya maendeleo watupeleke kwenye ajenda zisizo za msingi.


“Utasikia mwingine anasingizia polisi kuwa katekwa kumbe kajiteka mwenyewe, mwingine anataka watu waandamane, yaani watu waache kutumia fursa zilizopo kwa mfano jana Rais kazindua reli ya umeme ambayo mimi nilikuwa naiona Ulaya leo inajengwa Tanzania, waache  kutumia fursa za viwanda vinavyoibuka kwa wingi kama uyoga eti wakaandamane.


“Ninachoweza kuwahahikikishia ni kwamba vyombo vyetu viko imara,” amesema Masauni.

Miujiza ya Sharifu Seif Mohamed..JE Umeachwa na Mme/Mke au Mpenzi, Umesongwa na Mitihani ya Maisha

$
0
0

 

SHARIFU SEIF MOHAMED ANAWASHUKURU WALE WOTE WANAOENDELEA KUPIGA SIMU, WENYE MATATIZO NA WALE WANAOTOA  SHUKRANI NA SHUHUDA JINSI TIBA ZAKE ZINAVYO WASAIDIA,

(Rudisha mahusiano yako ndani ya masaa 72 tu)

SHARIFU MOHAMED Ni  mtaalam na mnajimu maarufu wa nyota na kubashiri mambo yanayo watesa binadamu duniani kote na kupata ufumbuzi, Anatumia kitabu cha QUR'AN na Nyota

Je Umeachwa na UMPENDAE awe Mme/Mke na bado unampenda? Je Umekimbiwa na Mmeo/ Mkeo n anaishi na mtu mwingine? Je Umejaribu sehemu nyingi bila mafanikio? Mpigie simu SHARIFU SEIF sasa hivi ujionee Muujiza wa Papo kwa Papo, Anauwezo wa hali ya juu wa kusambaratisha mahusiano yao na kumrejesha kwako haraka sana na Kumfanya Atimize Ahadi zote Ndani ya Muda Mfupi Endapo Utafwata Atakacho Kuelekeza

 ZINDIKO LA NYUMBA NA BIASHARA, PETE ZA BAHATI, HUMALIZA KABISA TATIZO   HUZUIA CHUMA ULETE KWENYE BIASHARA, HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA, NA KUPONYA MAGONJWA SUGU ANAO UWEZO WA KUMRUDISHA ALIE MBALI AU ALIECHUKULIWA MSUKULE, KUPANDISHA NYOTA NA KUSHINDA BAHATI NA SIBU, KASAFISHA NYOTA NA KUKUPA MVUTO WA AJABU, KUTOA NUKSI NA VIFUNGO MBALIMBALI,  MAFANIKIO YA MAISHA NA UTAJIRI BILA MASHARI, NA MENGINE MENGI YA SIRI,

JE UMAHANGAIKA KUPATA MTOTO BILA MAFANIKIO? WASILIANA NA MTAALAMU HUYU KWANI YEYE HUFAULU PALE WOTE WALIPOSHINDWA, PIA UMALIZA KAZI ZILIZO SHINDIKANA NA WATAALAM WENGINE NDANI YA MASAA 24 TU,

(NA ANATIBU KWA NJIA YA SIMU UKIWA NCHI YOYOTE AU MKOA WOWOTE ENDAPO UTAFWATA MAELEKEZO YAKE)

Kwa ushauri na mawasiliano  zaidi Piga SIMU No:

Mobile +255 654-836970
WhatsApp 0622766715 

Familia ya Diamond Yacharuka Mbaya Baada ya Zari Kuwapeleka Watoto Kanisani

$
0
0
Familia ya Diamond Yacharuka Mbaya Baada ya Zari Kuwapeleka Watoto Kanisani
Siku chache baada ya Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kuonekana akiwapeleka watoto wake kanisani, imeelezwa kuwa, familia ya mzazi mwenzake, staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ imecharuka vibaya kwani haifurahishwi na kitendo hicho baada ya kuachana kwao.



Taarifa za kuaminika ambazo Amani ilizipata kutoka ndani ya familia ya Diamond zilidai kuwa, awali waliona ni jambo la kawaida lakini kadiri siku zinavyozidi kwenda, wanaona ni tatizo.

“Awali Zari alipotupia picha ya kwanza ikionesha ameenda kanisani na watoto, tuliona labda ni maombi ya mara moja na pengine haiwezi kuwa tatizo lakini kadiri siku zinavyozidi kwenda, tunaona amekomaa na kanisani sasa tunaona kama inaweza kuja kuwa tatizo hapo baadaye na watoto wakawa njia panda.



“Si unajua wale watoto ni waislamu kwa sababu siku zote watoto huwa wanafuata kwa baba, sasa baadaye watakaporudi kwa Diamond na wakawa wameshazoea kwenda kanisani itakuwaje?” alihoji Amani mmoja wa wanafamilia aliyeomba jina lake lisiandikwe gazetini.


Diamond na familia yake.



MAMA, BABA DIAMOND HAWAKUFURAHISHWA

Taarifa hizo za ndani ya familia zilizidi kueleza kuwa, mama na baba Diamond wote hawakufurahishwa na jambo hilo japo Diamond mwenyewe hakuonekana kulimaindi sana.

“Mama na baba Diamond ndiyo wamecharuka sana japo Diamond anaonekana kutomaindi kivile.

“Unajua wazazi bwana wenyewe wanaona kuwaacha watoto wafuate kwa mama si sawa na ndiyo maana wamekuja juu, wanamtaka Diamond asimame kama mwanaume,” taarifa za ndani ya familia zilidai.



TAARIFA ZAIDI

Taarifa zaidi zilieleza kuwa, tayari baadhi ya ndugu wameshaanza kuweka vikao vya siri ili ikiwezekana wamweke kiti moto Diamond ili aweze kumvaa mzazi mwenziye haraka ili awe pia anawapeleka watoto madrasa.

“Unajua bora tungekuwa tunaona hata siku mojamoja anawapeleka madrasa angalau tungeona ni sawa lakini sasa hivi yeye kila siku ni kanisani tu,” alisema mmoja wa wanafamilia.



WATAJA SIRI ZARI KUUPENDA UKRISTO

Aidha, wanafamilia hao wamedaiwa kuwa na hofu zaidi ya Zari kuwabatiza watoto hao kwani historia inaonesha mrembo huyo alikuwa mkristo mzuri baada ya kuolewa na marehemu mumewe, Ivan Ssemwanga hivyo huenda ndiyo sababu ya kufanya maamuzi hayo.

“Unajua Zari alibobea kwenye ukristo na inaonekana anaipenda sana dini hiyo kuliko ya baba watoto wake sasa kama amerejea huko, ni rahisi sana kuwabatiza watoto wa Diamond,” alisema mwanafamilia mwingine.


Tiffah na Nillan.



MAMA DIAMOND ATAFUTWA

Amani lilimvutia waya mama Diamond ili kumsikia anazungumziaje suala hilo lakini simu yake iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi, hakujibu.

Alipotafutwa baba Diamond, Abdul Juma aliweka wazi kuwa kama familia hawajafurahishwa na kitendo cha Zari kuwafundisha kuhusu mafundisho ya Kikristo pekee.

“Hatukatai dini ni dini tu lakini kilichotushtua ni kwa nini tunaona anawapeleka upande mmoja tu.



“Unajua hata kama yeye ameamua kurudi kwenye Ukristo lakini watoto anapaswa kuzungumza na mwenzake ili waamue pamoja,” alisema baba Diamond.

Baba Diamond alimalizia kwa kutoa msimamo mkali kuwa, kama familia watamsisitiza Diamond azungumze na mzazi mwenzake na waangalie uwezekano wa kuwapeleka watoto hao madrasa ili pia waifahamu dini ya baba yao.


Mzee Abdul.



DIAMOND HAPATIKANI

Alipotafutwa Diamond wakati tunakwenda mitamboni juzi, kupitia simu yake ya mkononi, hakuweza kupatikana. Hata hivyo, ilibainika kuwa wakati huo staa huyo alikuwa nje ya nchi kwa shughuli za kimuziki.



TUMEFIKAJE HAPA?

Hivi karibuni, Zari alitangaza kummwaga Diamond kufuatia staa huyo kudaiwa kumsaliti mara kwa mara na habari zake kusambaa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

Baada ya kuachana, watoto wawili waliofanikiwa kuzaa walipokuwa pamoja, wanaishi na Zari nchini Afrika Kusini huku Diamond akiendeleza maisha yake Bongo.

Diva: Nitaolewa kwa Mahari ya Milioni 500 na Mwanaume Anayejua Kingereza

$
0
0
Diva: Nitaolewa kwa  Mahari ya Milioni 500 na Mwanaume Anayejua Kingereza
Mtangazaji Diva ameendela kusisitiza kuwa ataolewa kwa mahari ni milioni 500 na mwanaume anayejua lugha ya kingereza.


Diva ambaye alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na msanii wa muziki Heri Muziki ametoa kauli hiyo kwa kusisitiza kuhusu mahari yake na mwanaume anayemtaka mwaka huu. Kupitia mtandao wa Instagram Diva ametoa ameandika;

Kunioa Ni Milioni 500 …. set that Joke aside 🤦‍♀️deadly serious ….. Na Make sure unaongea English yenyewe hasa … uwe smart uwe very Handsome … uwe Loaded .. No broke niggas in 2018. Tupendane kwa Faida, you can say whateves .. jus heard worse , seen worse SMHFG Nothing mean to me … harshy aint new to me .. ve heard it all , but cha ching Money On da table wagwan 😛
mwenye Povu hana hela so ruksa Na Povu lako Nina OMO na JIKI plus Colgate n toothbrush jus there for u dummy … ps wenye Matangazo ya Biashara 👇🏼 ruksa kwenys comments.. 🤦‍♀️ #JK

January 24 mwaka huu mtangazaji huyo wa kipindi cha Ala za Roho cha Clouds Fm, Diva alidai kwa sasa haangalii tena ukubwa wa mahari bali anachohitaji ni mapenzi ya kweli.

Happiness Magese Aonyesha Sura ya Mwanaye kwa Mara ya Kwanza

$
0
0
Happiness Magese Aonyesha Sura ya Mwanaye kwa Mara ya Kwanza

Kwa mara ya kwanza Miss Tanzania mwaka 2001, Happiness Millen Magese ameonyesha sura ya mtoto wake kwa kutokea kwenye magazine ya nchini Nigeria.

Mrembo huyo ambaye alikuwa anasumbuliwa na tataizo la Endometriosis alijifungua mtoto wake wa kwanza July 13, 2018 lakini hakuonekana hadi leo alipoweka wazi hilo.

Sura ya mtoto huyo aitwaye Prince Kairo ameonekana katika cover la magazine ya Genevieve kutoka Nigeria, Magazine hiyo inatarajiwa kutoka March 16 mwaka huu.

Wambura Agomea Hukumu Alliyopewa na TFF "Kamati ya Maadili Haina Mamlaka Kisheria"

$
0
0
Wambura Afunguka Haya Baada ya Kufungiwa Maisha Kujiusisha na Soka
Muda mfupi baada ya TFF kutoa taarifa hiyo, Wambura naye alikutana na waandi­shi wa habari na kuzungumza.

Alisema kamati hiyo ya maadili haina mamlaka ya kisheria.

“Kisheria makamu wa rais hawezi ku­pelekwa Kamati ya Maadili ambayo in­aundwa na watu wachache na badala yake mkutano mkuu ambao una wa­jumbe wengi walionichagua kuingia ma­darakani ndiyo wanapaswa kunihukumu.



“Kama hiyo kampuni iliyotajwa kwam­ba nimeghushi barua za malipo si inayo meneja wake, basi aje atoe ushahidi wa hicho kinachosemwa kwa sababu wakati kamati inakutana kujadili hakukuwa na shahidi yeyote zaidi ya wakili wangu, Em­manuel Muga.



“Sababu ya yote haya ni nafasi yangu ya makamu wa rais, pili ni ajira zilizopo ndani ya shirikisho, tatu ni kutokana na fedha za shirikisho kwani mimi ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha ya TFF.



“Niliwahi kumuambia rais (Wallace Ka­ria) kwamba nafasi ya katibu mkuu ina­paswa itangazwe wazi ili mwenye vigezo aweze kuajiriwa, hiyo ni kwa mujibu wa Katiba ya TFF, lakini sikujibiwa kitu.



“Katiba inaelekeza kwamba, anayepas­wa kuwa katibu mkuu wa shirikisho hawezi kuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF.



“Anayekaimu kwa sasa (Wilfred Kidao) yeye ni Mwenyekiti wa Chama cha Ma­kocha Tanzania ambaye ni mjumbe wa mkutano mkuu, hivyo hana vigezo.



“Lakini pia kwenye masuala ya fedha ieleweke wazi kwamba kwa kuwa mimi ni mwenyekiti wa kamati ya fedha ndani ya shirikisho huwa naletewa jinsi fedha zina­vyotumika na wanaoidhinisha ni wengine.



“Kwa kipindi ambacho tumeingia ma­darakani mpaka sasa, tumeweza kutumia zaidi ya Sh bilioni tatu ambazo hakuna cha maana sana kimefanyika.



“Utakuta wakati mwingine utaona Kombe la Shirikisho (FA) pamoja na Ligi ya Wanawake mechi zake zinaahirishwa kutokana na matatizo ya fedha.

“Niseme tu huu mkakati umepangwa kwa sababu mpaka Jumanne siku am­bayo nasafiri sikupewa taarifa zozote za kutakiwa kwenye kikao hicho.



“Labda wanataka wanitoe ndiyo wa­pate nafuu ya kuzitumia hizo pesa. Mpa­ka sasa (jana mchana) sijapokea taarifa zozote juu ya kilichoamuliwa na kamati hiyo, nikishapata, nitaongea na vyombo vya habari.”



Awali kabla ya Wambura hajazun­gumza hayo, wakili wake ambaye ndiye aliyekuwa kwenye kikao hicho siku ya kwanza, alisema: “Barua ya wito haiku­pelekwa kwa muhusika kisheria kwani ilitakiwa apelekewe ofisini anapofanyia kazi, badala yake amepelekewa nyumba­ni kwake usiku siku moja kabla ya kikao kufanyika.

Makosa anayoshtakiwa Wambura ni

1.Kupokea/Kuchukuwa fedha za Shirikisho (TFF) za malipo ambayo hayakuwa halali ikiwa ni kinyume na kifungu cha 73(1) cha kanui za Maadili za TFF Toleo la 2013

2.Kughushi barua ya kueleza alipwe malipo ya Kampuni ya JEKC SYSTEM LIMITED huku akijua malipo hayo sio halali ikiwa ni kinyume na kifungu cha 73(7) cha Kanuni za Maadili za TFF Toleo la 2013

3.Kufanya Vitendo vinavyoshusha hadhi ya Shirikisho ikiwa ni kinyume na Ibara ya 50(1) ya Katiba ya TFF (Kama ilivyorekebishwa 2015)

Mafuriko Jangwani: Magari ya Mwendokasi Yashindwa Kufanyakazi Barabara Yafungwa

$
0
0
Mafuriko Jangwani: Magari ya Mwendokasi Yashindwa Kufanyakazi Barabara Yafungwa

Abiria wa mabasi ya mwendokasi wamekosa huduma ya usafiri leo asubuhi, baada ya kampuni ya UDART kusitisha huduma hiyo kutokana na mafuriko eneo la Jangwani.

TAARIFA KWA UMMA

Kampuni inayotoa huduma katika mradi wa mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam, UDA Rapid Transit (UDART), inaujulisha umma kuwa, huduma za mabasi hayo zimesitishwa kuanzia saa 11:00 alfajiri tarehe 16/03/2018 kutokana kufungwa kwa Barabara ya Morogoro eneo la Jangwani kwa sababu ya mafuriko yaliyosababisha maji kupita juu ya daraja la Mto Msimbazi.

Huduma zitarejea mara baada ya barabara kufunguliwa. Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.
Viewing all 104689 articles
Browse latest View live




Latest Images