Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104687 articles
Browse latest View live

Mwanaume ‘Anayeiba Sehemu za Siri’ za Wanawake Ahukumiwa Jela

$
0
0
Mwanaume mmoja Raia wa Denmark ambae alikutwa na viungo vya sehemu za siri za wanawake akiwa ameviweka kwenye freezer amehukumiwa vifungo viwili vya maisha na Mahakama ya Afrika Kusini.

Mwanaume huyu Peter Frederiksen amehukumiwa kwa makosa ya kumbaka mtoto na kuua mke wake, ambapo madai ya kukutwa na viungo vya sehemu za siri za wanawake yalitupiliwa mbali na mahakama baada ya kukosa ushahidi wa kutosha.

Frederiksen amehukumiwa kwa mashtaka 36 ambayo alishtakiwa nayo mwaka jana 2017 ikiwa ni pamoja na kuandaa video za ponografia zinazohusisha watoto

'Nabii Kijana Anaegawa Hela Shillah' Azungumza Kanisa Kufutiwa Usajili, Kuitwa Dodoma

$
0
0
'Nabii anaegawa hela Shillah' azungumza Kanisa kufutiwa usajili, kuitwa Dodoma

Tazama VIDEO:

Breaking News: Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania Theophil Makunga Ajiuzulu Nafasi Yake

$
0
0
Breakin News: Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania Theophil Makunga Ajiuzulu Nafasi Yake
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Theophil Makunga amejiuzulu nafasi hiyo.

Q Chief Ashusha Lawama kwa Papii Kocha

$
0
0
Q Chief Ashusha Lawama kwa Papii Kocha

Msanii wa BongoFleva Q Chief ameibuka na kujitetea kuwa hana tofauti yeyote ile na Papii Kocha pamoja na Nguza Vicking ila kuna baadhi ya watu ndio wanataka kuwatia ubaya kuhusiana na kuzimiwa MIC akiwa kwenye jukwaa akitumbuiza.


Q chief ametoa kauli hiyo akiwa anazungumza kwenye kipindi cha eNewz inayorushwa na tinga namba moja kwa vijana EATV baada ya kupita siku kadhaa tokea msanii huyo kuzimiwa MIC kwenye 'show' ya kuwakaribisha kwa mara nyingine katika tasnia ya muziki Papii na mzee Nguza kutokana na kupotea kwa miaka mingi kwa machoni mwa mashabiki na wapenda burudani wa dansi.

"Wakati mimi nina 'perfom' wimbo wangu wa kwanza katika 'show' wa nikilala naota, nilipata baraka zote kutoka kwa MC wa shughuli, Papii na Baba pia. So kwenye kazi unapoona watu wanamuitikio mzuri inabidi ujiongeze kutokana na wao kuonesha mapenzi yao hivyo mimi nimefanya kazi yangu kama vile ninavyofanya sehemu nyingine kwasababu nina nguvu nyingi katika kazi zangu lakini baadae wakati napanda juu nikashangaa kati kati ya wimbo nimezimiwa kipasa sauti 'MIC'", amesema Q chief.

Pamoja na hayo, Q chief ameendelea kwa kusema "sitaki kuweka kama kulikuwa na tofauti lakini kama zilikuwepo basi nilikuja kujizua baada ya kuangalia zile video tena na watu wa karibu pamoja na mke wangu kuniuliza ni jambo gani lilikuwa linaendelea mpaka kutokea vile. Lengo langu lilikuwa ni kutoa burudani, kumfariji rafiki ambae alipotea machoni mwangu kwa muda mrefu kwa mapenzi yote lakini MIC ikazimwa, sio kosa la Papii wala Mzee wangu Nguza kwasababu wao hawaitahi 'stress' bali ni kosa la ambaye alikuwa fundi mitambo 'technical' aliyekuwepo nyuma anashughulikia masuala ya vyombo vyote"

Mchungaji KKKT Akamatwa na Polisi, Ahojiwa

$
0
0
Mchungaji KKKT Akamatwa na Polisi, Ahojiwa

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro limekiri kumhoji Mkuu wa pili wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi Kilimanjaro Kati, Mchungaji Fred Njama.

Hatua ya polisi kumkamata na kumhoji Mchungaji Njama inakuja ikiwa zimepita siku chache tangu kiongozi huyo wa kiroho kutaja mambo sita aliyodai yanaitafuna nchi.

Akizungumza na Mwananchi leo Machi 17, 2018, Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Hamis Issah amesema; “suala hilo limeshughulikiwa na kamati ya ulinzi ya wilaya na mimi bado halijanifikia ili niwe na nafasi nzuri ya kulizungumzia.”

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba amesema; “suala hilo siwezi kulizungumza katika simu.” Huku akimtaka mwandishi kufika ofisini kwake na atalizungumzia.

 Akiwasilisha taarifa yake ya hali ya usharika katika mkutano mkuu wa  21 wa usharika huo wa Kiranga,  alitaja mambo hayo kuwa ni kuminywa kwa uhuru wa vyombo vya habari, hali ya uchumi kuwa ngumu, miili ya watu kuokotwa, kuminywa kwa vyama vya siasa na ukosefu wa ajira.

Rais Xi Jinpingwa China Achaguliwa Kuwa Rais wa Maisha

$
0
0
Rais Xi Jinpingwa China  Achaguliwa Kuwa Rais wa Maisha

Rais Xi Jinping ateuliwa rasmi kwa rais bila ukomo wa mihula ya kuongoza. Bunge la nchi hiyo pia limemteua Xi ally Wang Qishan kuwa Makamu wa Rais

Rais Xi mwenye umri wa miaka 64 anatajwa kuwa kiongozi mwenye ushawishi mkubwa zaidi baada ya alieyekuwa kiongozi wa kihistoria wa nchi hiyo Mao Zedong

Bunge lilipiga kura kupitisha marekebisho ya Katiba na kuondoa ukomo wa rais kukaa madarakani. Rais wa sasa Xi Jinping aruhusiwa kutawala bila kikomo.

Katika mchakato huo ulihusisha Wabunge takribani 3000 waliopiga kura na wakati wa kutolewa kwa matokeo ni Wabunge wawili tu ndio walipiga kura ya hapana dhidi ya mabadiliko hayo
Katiba ya China ilikuwa ikitoa uhalali kwa Rais kukaa madarakani kwa muda usiozidi vipindi viwili tu huku kila muhula ukiwa hauzidi miaka 5(kama ilivyo kwa Katiba ya Tanzania)
Mwezi uliopita chama cha Kikomunisti cha China kinachoongoza taifa hilo kilitoa pendekezo la kuondolewa kwa ukomo wa mihula ya Rais na Makamu wa Rais na leo wamehitimisha kwa kupiga kura

Video: Nikikosa Kufanya Mapenzi Mda Mrefu Nachanganyikiwa- Qeen Darleen

$
0
0
Msanii wa muziki kutoka label ya WCB, Queen Darleen ameushangaza umma wa Wakenya baada ya kudai kwamba mtu akikosa kufanya mapenzi kwa muda mrefu anachanganyikiwa kabisa. Muimbaji huyo aliyasema hayo mapema wiki hii akiwa nchini Kenya katika uzinduzi wa albumu ya Diamond ‘A Boy From Tandale’

Serikali Yanunua Vichwa vya Treni 11 Vilivyokuwa Katika Bandari ya Dar

$
0
0
Serikali Yanunua Vichwa vya Treni 11 Vilivyokuwa Katika Bandari ya Dar
Mnamo mwezi Julai 2017, Kampuni ya Progress rail Locomotives (PRL) ya Marekani ilileta vichwa vya treni 11 katika Bandari ya Dar es salaa  kwa ajili ya kuviuza vyenye namba 9014, 9015, 9016, 9017, 9018, 9019, 9020, 9021, 9022, 9023 na 9024.

Tarehe 27 septemba, 2017 Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa aliteua kamati ya wataalamu kwa ajili kubaini kama vichwa hivyo ni vipya au la.Wajumbe wa kamati hiyo walitoka chuo kikuu cha Dar es salaam, TEMESA na shirika la Reli Tanzania (TRC).Kamati hiyo ilifanya kazi hadi 15 oktoba, 2017 na kukabidhi ripoti kwa Mheshimiwa Waziri.Kamati ilibaini kuwa vichwa hivyo vya treni ni vipya.

Aidha tarehe 16 Oktoba, 2017 Mheshimiwa Wazirikwa mara nyingine aliteua kamati ya wataalamu wenye taaluma mbalimbali wakiwemo wanasheria wahandisi na wachumi kwa ajili ya kujadiliana bei ya kuvinunua vichwa hivyo.

Awali mwaka 2015,Serikali ilinunua vichwa kama hivyo 13 vyenye namba 9001, 9002, 9003  ,9004,9005,9006,9007,9008, 9009 ,9010, 9011, 9012 na 9013 kwa bei ya dola za kimarekani Milioni 3,200,000 kwa kichwa kimoja.Kamati hivyo ilifanya majadiliano ya bei na kufikia muafaka wa kununua kwa dola za kimarekani milioni 2,400,000 kwa kichwa kimoja ambavyo ni pungufu ya dola 800,000 kwa kila kichwa cha treni kulinganisha na bei ya vichwa tulivyonunua awali,kwa maana hiyo kwa vichwa 11 serikali imeokoa dola 8,800,000.

Majaribio yatakuwa katika awamu  tatu.Kwanza ni ukaguzi kwa kuvitizama(visual inspection),pili ni kuviwasha na kuvipa mizigo  vikiwa havitembei(load box) na tatu ni kufunga na kuvuta mzigo tani 700 toka Dar es salaam hadi Morogoro na tani 1200 toka Morogoro hadi Kigoma na Mwanza.

Ununuzi wa vichwa hivi 11 utaongeza ufanisi wa shirika kwani kwa sasa hivi tunavyo vichwa 29 madhubuti kati ya vichwa 47 tunavyovihitaji ili kutoa huduma nzuri kwa wateja wetu.

Wema Amchanganya Diamond Mahaba Yapambamoto "Kwakuwa Unajua Hizi Picha Ninavyozipenda Wanifanyia Kusudi"

$
0
0
Wema Amchanganya Diamond Mahaba Yapambamoto  "Kwakuwa Unajua Hizi Picha Ninavyozipenda Wanifanyia Kusudi"
STAA wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz ameshindwa kujizuia baada ya mpenzi wake wa zamani na Malkia wa Bongo Movies, Wema Sepetu kutupia picha yake na kumtag akisema “I’m inlove with you there’s nothing dat I wouldn’t do, catch a grenade for you, as long as you want me to…” jambo lililomuibua Diamond na kuanika rasmi mahaba yake kwa Wema.



Hayo yamejiri ikiwa ni saa chache baada ya Wema kuposti kipande cha wimbo mpya wa Diamond aliyomshirikisha staa wa Marekani, Omario, ngoma inaitwa AFRICAN BEAUTY na kumfagilia kwa kazi nzuri aliyoifanya.


Kwa mujibu wa mashabiki wa mastaa hao, inaonekana wamesharudiana na sasa wanaanza kuanika uhusiano wao.

Hivi karibuni ameachana na mama watoto wake, Zari The Bossy Lady kwa kile kilichodaiwa sababu kuwa Diamond amezaa na mwanamitindo Hamisa Mobeto.



Prof. Jay Awasii Watanzania Kuwezesha Soko la Musiki

$
0
0
Prof. Jay Awasii Watanzania Kuwezesha Soko la Musiki
Rapa mkongwe ambaye pia ni Mbunge Joseph Haule 'Prof. Jay' amewasii mashabiki wa muziki nchini kurejesha utamaduni wao wa kununua albumu za wasanii ili kuwezesha soka la muziki kuwa bora zaidi ya zaidi na kutoa ajira kupitia sanaa wanayoifanya.


Prof. Jay ametoa kauli hiyo mchana wa leo (Machi 17, 2018) kupitia ukurasa wake maalumu wa kijamii baada ya kuwepo kwa imani kwa baadhi ya wasanii wakiamini kwamba albamu za muziki haziwezi kuwalipa kutokana na mashabiki zao kuzoea tamaduni ya ku-donwload wimbo bure huku wengine wakiwasubiri wachache wanunue kisha wao waombe watumiwe kwa njia ya simu.

"Ninaamini sana ni haki ya msingi sana ya mashabiki wa muziki kupata albamu kutoka kwa wasanii wanaowapenda na kuwa-support lakini pia albumu ni kipimo kizuri sana kwa msanii kuweza kujua mashabiki wake wanataka nini au wanaipokeaje sanaa yake na anatakiwa aongeze au kupunguza kitu gani ili kufikisha ujumbe wake kwa hadhira aliyoilenga", amesema Prof. Jay.

Aidha, Prof. Jay amesema licha ya yeye kuamini kuwa kuongeza kwa soko la albamu kuna muweka msanii kwenye kumbukumbu isiyoweza kufutika kirahisi lakini wanapaswa wafahamu kwamba albamu ni kama kitabu na nyimbo zinakuwa kama 'chapters' hivyo inaweza kudumu miaka na miaka.

"Kipekee naomba sana nitoe wito kwa mashabiki wote wa muziki Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla kurudisha tena ule utamaduni wa kununua albumu za wasanii wetu ili kuliweka soko la muziki wetu kuwa bora zaidi kuliko ilivyokuwa hapo zamani ili tuweze kupata ajira nyingi zaidi kupitia sanaa yetu, Kwani wakati ni sasa", amesisitiza Prof. Jay.

Mpaka sasa wasanii wachache waliweza kuachia albumu kupeleka kwa mashabiki zao huku wengine wakiwa njiani kufanya hivyo ili kuweza kujiwekea historia ya maisha yao katika kazi ya sanaa ambayo wanafanya kwa kizazi cha baadae.

Napitia Maisha Magumu Katika Muziki Ndomana Nashindwa Kufanya Vizuri- Enock Bella

$
0
0
Napitia Maisha Magumu Katika Muziki Ndomana Nashindwa Kufanya Vizuri- Enock Bella
Msanii wa BongoFleva Enock Bella amedai anapitia wakati mgumu katika muziki kwa sasa ndio maana anashindwa kufanya vizuri katika kazi zake kwa maana kila jambo analisimamia yeye binafsi hakuna wa kumpa ushirikiano kwa jambo lolote lile.


Enock amebainisha hayo kupitia kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya msanii huyo kuonekana kutoa nyimbo tano lakini bado anaonekana kususua sua tofauti na wenzake aliyekuwa nao kwenye kundi la Yamoto Bendi wakiendelea kufanya vizuri ndani na nje ya mipaka ya Tanzania huku baadhi ya watu wakidai kutofanikiwa kwa Enock ni kutokana na sauti yake aliyokuwa nayo tofauti na wenzake.

"Kila kitu kina sababu yake na Mungu pekee ndiye mwenye kujua nafasi ya mtu wapi ilipo kwa hiyo siwezi kulazimisha muda huo huo ninaotoa wimbo na nipate mafanikio hapo hapo, kila mtu ana nafasi yake aliyeba katika maisha yake. Muda wangu utakapofikia mtaoana maendeleo ya kimuziki ambao mimi nafanya kwa maana kuna watu wengine wametajirika wakiwa wazee, muda waliokuwa vijana hawakufanikiwa kupata mafanikio yeyote yale", amesema Enock.

Pamoja na hayo, Enock Bella ameendelea kwa kusema "ridhiki ni mafungu saba lakini sasa hivi imekuwa ni mambo mawili ambayo ni kupata na kukosa kwa hiyo wakati wangu ukifika nami ntakuwa nimeanzia hapo kufanikiwa. Sauti ya yangu hii ya 'base' ndio iliyonitengeneza mimi hii leo kutambulika hivyo sio kweli kwamba sauti yangu ndio sababu ya hayo, kwa hiyo nikisema ghafla niipoteze halafu niambie upande mwingine itakuwa ni tofauti ndio maana nikasema kila mtu ana nafasi yake hivyo nafasi yangu ikifika kwa 'base' yangu hii hii watarudi tu. Kwani mara ya kwanza waliokuwa wananielewa nilivyokuwa kwenye Yamoto ?, si walikuja kunielewa baada ya mashairi yangu kuyatoa".

Wema Sepetu Ashindwa Kuficha Hisia Zake Amuandikia Ujumbe Mzito Diamond

$
0
0
Wema Sepetu Ashindwa Kuficha Hisia Zake Amuandikia Ujumbe Mzito Diamond
STAA wa sinema za Kibongo, Wema Sepetu amevunja ukimya na kuamua kumwandikia ujumbe mzito huku akimwagia misifa mpenzi wake wa zamani na msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’.

Wema amefunguka hayo, kufuatia Diamond kuachia ngoma mpya aliyomshirikisha msanii wa Marekani, Omario inayoitwa AFRICAN BEAUTY huku akimsifia namna wimbo huo ulivyo bora na jinsi alivyommezesha maneno ya Kiswalihi staa huyo wa Marekani.

Baadhi ya mashabiki wamedai huenda Queen huyo wa Bongo Movies anatengeneza mazingira ya kurudi rasmi kwa mpenzi wake huyo ambaye hivi karibuni ameachana na mama watoto wake, Zari The Bossy Lady kwa kile kilichodaiwa sababu kuwa Diamond amezaa na mwanamitindo Hamisa Mobeto.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Wema ameandika ujumbe huu kwa Diamond;

All dat Said… Let’s get back to Reality…. Chibu, Unaweza…!!!Chibu, Unajua….!!! Keep Doin wat you do and Live Your Dream… Bonge moja la Track… Na Hongera kwa kummezesha Omarion Swahili… I can imagine kazi uliokuwa nayo… 😅… Salute kwako… . . . The Video be on Youtube Ladies & Gentlemen… I keep Repeating it wallahy… link on his Bio @diamondplatnumz @diamondplatnumz @diamondplatnumz @diamondplatnumz … . . . Picha twazitwanga Kisela, Post insta wanga kuwakera….😅😅😅 Tatizo wanga wa Insta hawakawii kukukera wewe… 😅😅😅 . . . #AFRICANBEAUTY 😝

Irene Uwoya Atoa Sababu ya Mama Yake Kutoshiriki Kwenye Ndoa Yake

$
0
0
Irene Uwoya Atoa Sababu ya Mama Yake Kutoshiriki Kwenye Ndoa Yake
Muigizaji, Irene Uwoya amefunguka sababu mama yake kutoshiriki kwenye ndoa yake na Dogo Janja.

Irene Uwoya ameiambia Leo Tena ya Clouds Fm, kuwa mama yake amekuwa ni mtu wa kusafiri mara kwa mara hiyo ndiyo sababu iliyopelekea kutompeleka Dogo Janja nyumbani.

“Hakuwepo kwahiyo hakuweza kushiriki kwasababu mama angu ni mtu wa kusafiri sana kwahiyo hakuwepo Tanzania lakini ndoa ameibariki. Mama anaenda anarudi kazi zinakuwa nyingi, kwahiyo hatujapata nafasi ya kusema sasa katulia twende bado, lakini tunaendaga mimi na yeye nyumbani mama anakuwa hayupo sometime baba anakuwepo ,” alisema Irene.

Hata alivyoulizwa kutokuwepo kwa ndugu zake kwenye ndoa yake Irene ameeleza kuwa ndugu zake walikuwepo baadhi japo hawakuwa wengi.

Waziri Mwakyembe Amlilia Mpiga picha wa ITV

$
0
0
Waziri Mwakyembe amlilia mpiga picha wa ITV
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe kilichotokea Machi 16, mwaka huu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar Es Salaam.

Waziri Mwakyembe kupitia taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari ameeleza kupokea kwa masikitiko kifo cha mpiga picha huyo Mkongwe wa ITV.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mpiga Picha mkongwe Bw. Evarist Ottaro kilichotokea jana tarehe 16 Machi, 2018 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar Es Salaam.

Dkt. Mwakyembe ameeleza kuwa kifo cha Bw. Ottaro kimeipokonya tasnia ya Habari mmoja wa Wapiga Picha mahiri waliokuwa tegemeo kubwa la maendeleo ya tasnia hiyo nchini.

Dkt. Mwakyembe ametoa pole kwa familia, uongozi wa Kituo cha Televisheni cha ITV, ndugu, jamaa, marafiki na wanahabari wote nchini na kuwaombea Mungu awape faraja katika kipindi hiki kigumu cha msiba.

Wakati wa uhai wake Bw. Ottaro amewahi kufanya kazi na vituo vya Televisheni vya Channel Ten na DTV kabla ya kuhamia katika kituo cha Televisheni cha ITV ambapo amefanya kazi kwa miaka kumi na saba hadi alipofikwa na umauti.

Imetolewa na:

Lorietha Laurence
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.
17/03/2018.

RC Makonda- Kuanzia Sasa Marufuku Kuwakamata Wasanii

$
0
0
RC Makonda- Kuanzia Sasa Marufuku Kuwakamata Wasanii

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amepiga marufuku kukamatwa wasanii pindi wanapokuwa wanapiga picha au kuigiza katika maeneo ya bandari yanayoonesha taswira ya Jiji inavyoonekana kiujumla kwa madai kitendo hicho wanalitalitangaza kitalii.


Makonda ametoa kauli hiyo leo (Machi 17, 2018) wakati wa ghafla ya uzinduzi wa kazi za kutangaza utalii katika Jiji la Dar es Salaam na kusema amepata malalamiko mengi kuhusiana na wasanii wanaokamatwa na wakiwa wapo katika shughuli za kuutangaza kiutalii mkoa wake.

"Kwenye mkoa huu wa Dar es Salaam nimepewa taarifa kwamba kuna wasanii wakitaka kupiga picha katika baadhi ya kule kwenye meli 'bandarini' kwa kutaka kuonesha tu sura ya Dar es Salam inavyoonekana wakati wakitokea upande wa pili kule wa Kigamboni kuna watu wanajitokeza na kuwakamata wakati wanataka kuutangaza mkoa wao na vitu vizuri vilivyopo ndani yake", amesema Makonda.

Aidha, Makonda amesema wasanii hao hao wakienda kuigiza katika maeneo machafu huwa hakuna mtu anayejitokeza kuwakamata au hata kuwazuia jambo ambalo lina mkera kwa upande wake.

"Sasa kuanzia leo hakuna kuwakamata wasanii wanapofanya matukio yao ya kurekodi ndani ya mkoa wa Dar es Salaam wanakibali kutoka kwangu. Sehemu ambazo utahitaji kupata kibali ni Ikulu, Mahakamani na Jeshi la Polisi lakini hayo maeneo mengine yote unaruhusiwa kurekodi na huko wakitaka kibali njoo ofisini kwangu mimi nitakusaidia upate kufanya kazi yako", amesisitiza Makonda.

Pamoja na hayo, Makonda ameendelea kwa kusema "leo hii Ikulu ya Marekani 'White House' inajulikana kutokana na muvi zao wengine hatujawahi kutembelea baadhi ya nchini lakini ukiangalia 'movie' unaambiwa ndio sehemu fulani unakubali kumbe hata wakati mwingine unadanganywa".

Kwa upande mwingine, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema inapaswa ifike wakati wasanii waliopo nchini Tanzania hasa katika jiji lake wawe wanarekodi kazi za kwa uhuru bila ya kupatiwa shida ya aina yeyote ile.

Waarabu Waigomea Azam Tv Kurusha Mchezo wa Al Masry Dhidi ya Simba

$
0
0
Waarabu Waigomea Azam Tv Kurusha Mchezo wa Al Masry Dhidi ya Simba
Mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Al Masry SC dhidi ya Simba Sc hautorushwa hewani na kituo chochote cha Runinga.

Awali kulikuwa na matarajio ya mechi kuoneshwa na kituo cha Azam TV baada ya kutangaza kurusha mechi ya Township Rollers dhidi ya Yanga.

Kwa mujibu wa Afisa Habari wa Simba, Haji Manara, amesema uongozi wa Al Masry umeigomea Azam TV kurusha mechi hiyo itakayoanza saa 2:30 usiku ambapo sababu hazijajulikana.

Maandamano ya Aprili 26 Bado Yampasua Kichwa Makonda Ampa Salamu Meya wa Jiji Kumpelekea kwa Mbowe

$
0
0
Maandamano ya Aprili 26 Bado Yampasua Kichwa Makonda Ampa Salamu Meya wa Jiji Kumpelekea kwa Mbowe
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amemtuma meya wa jiji kuzungumza na viongozi wake wa chama(Chadema) kufikiria upya kuhusu hali ya usalama katika jiji hilo ili kufanikisha ukuzaji wa sekta ya utalii katika jiji hilo.

“Mstahiki meya wa jiji, leo tunazindua utalii wa ndani na tumemuita waziri wa Tamisemi atuzindulie, kawaulize ndugu zako wale akina Mbowe (Mwenyekiti wa Chadema) na akina nani wale, waulize...wakifanya vurugu, hawana watalii watapita mji gani?”Amehoji Makonda  leo Machi 17, 2018 wakati wa mkutano wa kuzindua utalii wa ndani katika mkoa huo.


Katika hatua nyingine, Makonda ametoa maagizo manne katika kufanikisha utalii wa ndani katika jiji hilo akisema, kwanza ni lazima kuhamasisha utalii huo, kuendeleza usafi katika jiji hilo, kuboresha vituo vya mabasi yaendayo mikoani.

Katika hatua nyingine, Makonda ameahidi kuzindua viwanda 200 katika jiji hilo hapo baadaye badala ya viwanda 100 vilivyoagizwa na Serikali katika kila mkoa

“Ulitupatia maelekezo ya kila mkoa viwanda 100, mie nakuahidi , nitakualika mwenyewe kuzindua ujenzi wa viwanda 200 kwa wakati mmoja, tumeshapata wawekezaji na sasa tuko kwenye mchakato wa kukamilisha suala la ardhi,”amesema Makonda.

Awali, Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Spora Liana ametaja mipango kadhaa iliyoanza kutekelezwa na jiji hilo katika kukuza na kuimarisha sekta ya utalii.

Askari Polisi Afumwa Akifanya Mapenzi na Mwanafunzi Katika Kituo cha Polisi

$
0
0
Askari Afumwa Akifanya Mapenzi na Mwanafunzi Katika Kituo cha Polisi
Askari Polisi wa Kituo Kidogo cha Lukula katika Kata ya Kitunda wilayani Sikonge, Jebasa Charles amekamatwa na jeshi hilo akituhumiwa kukutwa na mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Kiwele akifanya mapenzi kituoni hapo.

Akizungumza na waandishi wa habari  Machi 15, mwaka huu, Diwani wa Kata ya Kitunda wilayani Sikonge mkoani Tabora, Mbwana Seif alisema askari huyo walimfanyia mtego na mzazi wa mwanafunzi Farida Juma kituoni hapo kwa muda wa siku tatu na kufanikiwa kumkamata.

Seif alisema tukio hilo lilitokea saa 11 alfajiri wakati askari huyo alipofungua mlango ili kumtoa mwanafunzi huyo wa kidato cha pili, ndipo akakutana na wananchi na mzazi wakiwa mlangoni kisha kuwakamata wawili hao.

Aidha, diwani huyo alidai taratibu zilifanyika za kumpeleka mwanafunzi huyo hospitalini kupata vipimo, ambako walidai ni mjamzito. Hata hivyo, Seif alisema baada ya kukamatwa kwa askari huyo na kumweka ndani, mzazi hakuridhika na aliomba kituoni hapo aondolewe na kupelekwe Kituo cha Polisi Wilaya ya Sikonge. Diwani huyo alisema wananchi wa Kata ya Kitunda wamekasirishwa Kituo Kidogo cha Polisi Lukula kugeuzwa nyumba ya kufanyia maasi.

Babu wa mwanafunzi huyo, Juma Kaseka ambaye ndiye aliyekuwa anaishi na binti huyo alisema kama hatua hazitachukuliwa ipasavyo na Kamanda wa Polisi mkoani Tabora, Wilbroad Mutafungwa hawatosita kumtafuta Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro ili awasaidie. Kaseka alisema Machi 13, mwaka huu saa 4 usiku, mwanafunzi aliondoka nyumbani baada ya kupata chakula na hakujulikana alipokwenda.

Alisema majirani waliwaambia walimuona Kituo Kidogo cha Lukula na walitoa taarifa kwa uongozi wa kijiji akiwemo mtendaji na mwenyekiti wa kijiji hicho na kuchukua hatua hiyo ya kumvizia na kumkamata. Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Wilbroad Mutafungwa alithibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kueleza kuwa ni mwanafunzi wa shule hiyo wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Kiwele. Kamanda alisema askari huyo amekamatwa jana na kufikishwa Kituo Kikuu cha Wilaya ya Sikonge kwa ajili ya kuhojiwa na wanatarajia kumuhoji mwanafunzi huyo na kumfanyia vipimo ili kuthibitisha madai yake.

Hiki Hapa Kikosi cha Yanga Dhidi ya Township Rillers

$
0
0
Hiki Hapa Kikosi cha Yanga Dhidi ya Township Rillers
Mwakilishi wa michuano ya klabu bingwa barani Afrika klabu ya Yanga imetangaza kikosi chake kitakacho ikabili timu ya Township Rillers FC ya Botswana hii leo.

Yanga SC itashuka uwanjani kuwakabili wenyeji wao Township katika michuano hiyo ya kombe la klabu bingwa barani Afrika huku ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza katika mchezo uliyopita kwa jumla ya mabao 2 – 1.

Kikosi cha Yanga SC kinachoshuka dimbani leo dhidi ya Township Rollers FC ya Botswana 1. Youthe Rostand 2. Juma Abdul 3. Gadiel Michael 4. Vicent Andrew 5. Kelvin Yondani 6. Said Juma 7. Yussuf Mhilu 8. Papy Kabamba 9. Obrey Chirwa 10. Pius Buswita 11. Kamusoko Kamusoko.



Mwanasheria Mkuu wa Serikali Nchini Marekani Amfuta Kazi Kigogo wa FBI Siku Chache Kabla ya Kustaafu

$
0
0
Mwanasheria Mkuu  wa Serikali Nchini Marekani Amfuta Kazi Kigogo wa FBIKutoka nchini Marekani Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jeff Sessions amemfuta kazi aliyewahi kuwa Kaimu Mkurugenzi Mstaafu wa FBI Andrew McCabe ikiwa ni siku chache tu kabla ya kustaafu rasmi na kupata haki zake zote za mafao.

Taarifa ya Sessions imeeleza kuwa McCabe amefukuzwa kazi kutokana na kuvujisha taarifa za uongo na kuwapotosha wapelelezi. Kigogo huyo wa FBI amekataa kuhusika na tuhuma hizo.

Ameeleza kuwa amezushiwa tuhuma hizo kwasababu alihusika katika kufuatilia suala la nchi ya Urusi kuingilia Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo mwaka 2016.

Rais Donald Trump amewahi kumtuhumu McCabe kuwa na upendeleo wa kisiasa kwa kuwa mfuasi wa Chama cha Democrats.
Viewing all 104687 articles
Browse latest View live




Latest Images