Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104694 articles
Browse latest View live

Jacob Zuma Akabiliwa na Mashtaka ya Rushwa

$
0
0
Jacob Zuma Akabiliwa na Mashtaka ya RushwaAliyekuwa rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amepatikana na mashtaka 16 ya rushwa inayohusishwa na mamilioni ya dola yaliotumika katika mpango wa silaha.

Mashtaka hayo ambayo bwana Zuma amekataa kuhusika yanajumuisha udanganyifu aliofanya ili kujipatia fedha na utakatishaji wa fedha.

Bwana Zuma mwenye umri wa miaka 75,chama chake cha ANC kilimlazimishaa kuachia madaraka yake mwezi uliopita.

Zuma alipigiwa kura ya kutoamaniwa mara ya tisa katika bunge kabla hajaachia ngazi.

Mwendesha mashtaka mkuu Shaun Abraham amesema anaamini kuwa kuna sababu ya kuwa na mtazamo chanya juu ya hukumu ya kesi hii.

Msambazaji wa silaha kutoka Ufaransa Thales yeye pia atakabaliwa na mashtaka .Taarifa kutoka AFP zinasema Thales amekataa kuongea chochote kuhusu suala hilo.

Bwana Zuma anatuhumiwa kutaka rushwa kutoka kwa Thales kwa nia ya kuboresha maisha yake ya kifahari.Mshauri wake wa fedha wakati huo alikutwa na hatia ya kuomba rushwa hizo mwaka 2005 na bwana Zuma alimfukuza kazi yake ya usaidizi wa rais.

Mashtaka ya awali dhidi ya bwana Zuma yalikuwa yameondolewa muda mfupi kabla ya kuwa rais mwaka 2009.

Kwa sasa anakabiliana na shitaka moja la kusababisha ghasia,mashtaka mawili ya rushwa,shtaka moja la rushwa na mashtaka 12 ya udanganyifu

Video: Wakili wa Abdul Nondo Afunguka Mazito

$
0
0
Video: Wakili wa Abdul Nondo Afunguka Mazito
Kufuatia sakata la Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Abdul Nonda ambae pia kiongozi wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania TSNP la kudaiwa kutekwa, leo Machi 17 Jebra Kambole ambae ni Wakili wa Mwanafunzi huyo amefunguka na kudai kuwa mpasa sasa hajaonana nae ili kujua kinachoendelea juu yake.


Kikosi cha Simba Dhidi ya Al Masry

$
0
0
 Kikosi cha Simba Dhidi ya Al Masry
Kikosi cha Simba kitachocheza dhidi ya Al Masry katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Africa leo.


Mkurugezi kampuni iliyokuwa inaidai TFF yupo tayari kutoa ushahidi kesi ya Wambura

$
0
0
Mmoja wa wakurugenzi wa Jeksc Systems Limited iliyokuwa inaidai TFF Jost Rwegasira ameibuka na kuzungumzia kuhusu barua au nyaraka za kampuni hiyo zinazodaiwa zilighushiwa.

Rwegasira amesema yupo tayari kutoa ushahidi wake mahali popote endapo utaratibu wa yeye kufanya hivyo utafuatwa lakini kwa sababu tayari hukumu imeshatolewa hawezi kuweka jambo hilo hadharani labda ikitokea ameitwa mamlaka itakayokuwa ikisikiliza rufaa ya kesi hiyo.

“Uamuzi wa mahakama ya maadili umeshatoka, wametoa uamuzi bila kuuliza Jeksc. Nimefuatilia kila kitu tangu kilivyotangazwa lakini sina uwezo wa kuingilia mambo ya TFF lakini kwa kuwa uamuzi umeshatoka, kwa hiyo nilichonacho ni ushahidi kwa atakaekata rufaa au yule atakaekuwa anasikiliza rufaa.

“Naomba umma unielewe, wakati uamuzi umeshatolewa inamaana upande mmoja una uhakika na unachosema na upande wa pili unaopinga una uhakika kwa unachosema kwa hiyo mtu wa tatu atakaepelekewa rufaa kama itakuwepo ndiye mwenye mamlaka ya kumuomba mlalamikaji au mlalamikiwa kupeleka ushahidi.

“Naweza kutoa ushahidi kwa sharti moja, ni ipi barua inayolalamikiwa kwamba ni ya kufoji? Mimi sijaipata, siwezi kukaa pembeni nikatoa ushahidi kwamba hiyo barua sio ya kufoji mpaka wewe mwenye maswali uwe nayo uniulize barua hii unaijua?

“Jambo la pili kwa sababu unapinga hukumu ambayo ilishaotolewa, lazima uwe na ushahidi ambao umeombwa kutoa kwamba hii barua iliyoletwa kwenye kesi sisi tumeiona ni feki lakini kama sijaiona hiyo barua nina kubali nini au nakataa nini?

Shauri likienda mbele kwenye kamati ya maadili ya rufaa upo tayari kutoa ushahidi?

“Hata leo ukienda TFF wakakupa barua kwamba hii barua tuliyoletewa ni feki nipo tayari kuthibisha lakini katika press conference zote zilizotolewa nimeziangalia TFF hawajaonesha barua wanayoilalamikia sasa mimi nakubali au kukataa barua ipi? Ila ninachokubali ni kwamba nilikuwa mkurugenzi katika kampuni aliyoiendesha marehem lakni hiyo barua wanayolalamika imefojiwa naomba wailetwe kwanu mimi nipo tayari kuja kuiona halafu nithibitishe ndiyo au hapana.

Baada ya kufariki mkurugenzi mtendaji tulitangaza kampuni inasimamisha shughuli zake zote mpaka itakapotangazwa vinginevyo.

Rekodi za Simba, Yanga, zinapocheza kimataifa ugenini

$
0
0
Na Baraka Mbolembole

KUELEKEA mchezo wao wa kumi wa Ligi ya Mabingwa Afrika Afrika, rekodi ya Yanga SC katika michezo tisa iliyopita ya michuano hiyo ndani ya miezi 23 iliyopita ‘haishawishi’ walio wengi kuamini mabingwa hao wa Tanzania bara wana uwezo wa kupindua matokeo ya 1-2 wakiwa Gaborone na kufuzu kwa hatua ya makundi kwa mara ya pili.

Tangu walipojaribu kwa kiwango cha juu kuwaondoa ‘wababe wa michuano’ Al Ahly kutoka Misri, April, 2016, Yanga haijapata kukutana na washindani wakubwa katika michuano ya Caf lakini bado wamekuwa wakikwama kufuzu kwa hatua ya makundi.

Mwaka mmoja baada ya kiwango cha juu jijini Cairo ambako waliondolewa katika michuano dakika ya mwisho ya mchezo, mabingwa hao wa  VPL wamemudu kushinda michezo miwili tu ya mabingwa Afrika-tena dhidi ya timu kutoka Shelisheli (Ngaya Club, St. Louis) huku wakichapwa nyumbani kwa mara ya kwanza baada ya miaka nane na Watswana, Township Rollers wiki moja iliyopita.

Yanga ni wagumu na hucheza vizuri ugenini Caf

9 April, 2016 chini ya kocha Hans van der Pluijm, Yanga ililazimishwa sare ya kufungana 1-1 na Al Ahly SC katika uwanja wa  Taifa, Dar es Salaam. Wengi waliamini wangeendeleza ‘mlolongo’ wa matokeo yao mabaya ugenini hasa wanapocheza dhidi ya Al Ahly na timu nyingine za Kiarabu.

Lakini kufikia dakika 90’ jijini Cairo, matokeo yalikuwa 1-1 na wakati wengi wakiamini mshindi ataenda kupatikana kwa njia ya mikwaju ya penati, wababe hao wa Misri walifunga goli la ushindi dakika za mwisho wa mchezo huo wa marejeano.

Kuanzia hapo hadi sasa, Yanga imekutana na wapinzani  watatu tofauti na hawajapoteza mchezo ugenini katika michuano hiyo. Walishinda ugenini 1-5 dhidi ya Ngaya Februari, 2017 na walilazimisha suluhu dhidi ya Wazambia, Zanaco FC, Machi, 2017 licha ya kwamba waliondolewa katika michuano kwa sheria ya goli la ugenini baada ya awali timu hizo kufungana 1-1 Dar es Salaam.

Mpinzani wao wa nne tangu walipochapwa na Al Ahly miaka miwili iliyopita tayari ‘amewaonyesha shoo.’ Ni ukweli ulio wazi kuwa Yanga walichezewa mpira wa kiwango cha juu wiki moja iliyopita walipochapwa 1-2 na Rollers. Bado ninaweka imani kubwa kuwa Yanga watalipa kisasi Gaborene na si ajabu wakaacha simulizi ya ‘shoo’ watakayoionyesha.

Imani yangu inatokana na mwenendo wa timu na uwezo wa mchezaji mmoja mmoja. Kiwango cha Juma Abdul katika mchezo uliopita dhidi ya Stand United siku ya Jumatatu hii, na maendeleo ya vijana kama Makka Edward, Yusuph Mhilu na urejeo wa ‘ufit’ wa Ibrahim Ajib kunatengeneza kundi jingine la wachezaji wasiotarajiwa na wapinzani. Miezi 24 iliyopita Yanga walicheza vizuri sana jijini Kigali vs APR, halafu Cairo.

Kama watakuwa na ‘msukumo wa kulazimisha kupindua matokeo’ naona wakifunga magoli walau matatu dhidi ya Township. Ni kujituma, kuamini, na kuwa tayari kimwili, kiakili, kimbinu na kiufundi. Ni mara moja tu katika washindani wao sita waliokuja Dar kucheza nao CCL, Yanga walicheza vizuri. Dhidi ya APR walicheza vibaya, angalu vs Al Ahly, ila dhidi ya Ngaya, Zanaco, St. Louis na Rollers zote wamecheza vibaya.

Mechi 5 za Yanga ugenini hivi karibuni michuano ya kimataifa, klabu bingwa Afrika (CCL) na kombe la shirikisho Afrika (CCC).

23/08/2016 CCC TP Mazembe 3-1 Yanga
12/02/2017 CCL Ngaya Club 1-5 Yanga
18/03/2017 CCL Zanaco 0-0 Yanga
15/04/2017 CCC MC Alger 4-0 Yanga
21/02/2018 CCL St. Louis 1-1 Yanga
17/03/2018 CCL Township Rollers ?? Yanga
Inasemekana ni presha ndiyo huchangia Yanga kushindwa kucheza vizuri wanapokuwa nyumbani lakini hucheza vizuri ugenini kwa sababu hawasumbuliwi na mashabiki wao wengi wanaopenda kuharakisha ushindi na kutokubali uwepo wa makosa ya kimchezo wanapocheza uwanja wa Taida, Dar.

Watoto wenyewe wa Yanga ndiyo watakaopokelewa kishujaa

Moja kati ya habari zilizovutia sana na kufuatiliwa hadi barani Ulaya-hasa nchini Uturuki mapema mwaka 2003 ni kuangushwa kwa ‘mbabe’ wa soka la vilabu barani Afrika wakati huo, Zamalek. Mahasimu hao wa Al Ahly katika soka la Misri walikuwa na mataji matano ya ligi ya mabingwa Afrika na hadi wanakutana na Simba walikuwa ndiyo mabingwa mara nyingi zaidi wa kihistoria wa ligi ya mabingwa (mabingwa mara tano)

Zamalek walikuwa wanatawala soka la Afrika huku wakiwa klabu tajiri zaidi Afrika wakati huo. Walishinda Confederation Cup mwaka 2001, wakashinda Champions league 2002 lakini mbele ya ardhi yao wenyewe walishuhudia wakiondolewa katika michuano, na kutemeshwa ubingwa ambao wameshindwa kuurudisha tena hadi sasa.

Simba ilikuwa na mchezaji mmoja tu wa kigeni wakati walipopokelewa kishujaa jijini Dar es Salaam. Mrundi, Ramadhani Wasso ambaye alitawala beki ya kushoto pekee ndiye alikuwa katika kikosi kabambe cha kocha Mkenya, marehemu, James Siang’aa (mwenyezi Mungu amrehemu) zaidi ya hao ni vijana wenyewe wa Simba walioweka historia hiyo nzuri isiyofikiwa hadi sasa.

Ilikuwa Simba ya wazawa wenye njaa ya mafanikio na wenye kuhitaji kucheza michuano mikubwa kama ligi ya mabingwa Afrika. Kwa wanasoka wengi barani Ulaya kucheza michuano ya ligi ya mabingwa ni ndoto, hivyo baada ya miaka 20 tangu kizazi cha kina Edibilly Lunyamila, vijana kama kina Kelvin Yondani wanapaswa kukumbuka kuwa hawajawahi kucheza michuano ya makundi ya michuano mikubwa zaidi Afrika hivyo wanapaswa kuwasukumu ‘yosso’ wasio na uzoefu kuhakikisha wanaichapa na kuwaondoa Rollers katika mchezo ujao ili wafike makundi.

Mechi 5 za Simba ugenini hivi karibuni michuano ya kimataifa, klabu bingwa Afrika (CCL) na kombe la shirikisho Afrika (CCC).

18/02/2012 CCC Kiyovu Sports 1-1 Simba
06/04/2012 CCC ES Setif 3-1 Simba
13/05/2012 CCC Al Ahly Shendi 3-0 Simba
03/03/2013 CCL Recreativo do Libolo 4-0 Simba
20/02/2018 CCC Gendarmerie 0-1 Simba
17/03/2018 CCC Al Masry ?? Simba
Yanga ya sasa ni tofauti sana na Simba ya 2003, lakini wana wachezaji nanne hadi tisa wazawa ambao wanaanza kikosi cha kwanza hivyo wanaweza kutumia uzalendo wao kupigana kufa na kupona kuhakikisha klabu inatinga hatua inayofuata ambayo pia itawafanya waingize zaidi ya bilioni 1.2

Kuishinda Rollers na kufuzu kwa hatua ya makundi kutawafanya vijana kama Pius Buswita, Hassan Kessy, Said Juma Makapu, Mwinyi Hajji na wenzao kupokelewa kishujaa watakaporejea nchini huku pia wakitaraji kujiuza zaidi kimpira na kuingiza pesa  katika akaunti zao. Wao ndiyo Yanga, na mashujaa wanaoweza kupewa sifa kemkem baada ya matokeo yao mazuri katika dakika 90’ zijazo Caf Champions League.

Download Application ya Udaku Special kwenye Simu yako Kama Bado Hujadownload

$
0
0
Download Application ya Udaku Special kwenye Simu yako Kama Bado Hujadownload


DOWNLOAD HAPA
 


UPDATE HAPA

Hii ni Surprise Nyingine Kutoka Vodacom Tanzania, Instagram sasa ni Bureeee

$
0
0

Tunajua kuwa Instagram ni moja kati ya mtandao bora sana wa kijamii kwa sasa na
habari kubwa Tanzania leo siku ya Jumamosi ni uzinduzi wa INSTAGRAM YA
BURE kutoka Vodacom Tanzania. Uzinduzi huo umefanywa na Linda Riwa ambaye
ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma na Bidhaa kwa Wateja.

Katika mpango huu Vodacom Tanzania wanakwambia kuwa unapata Instagram
BURE kila unaponunua kifurushi cha Tshs 1,000 au zaidi usambaze na kuangalia
picha BURE ukiwa kwenye mtandao supa pekee Tanzania. Kifurushi hiki
kitakuwezesha kuangalia picha na ukinunua kifurushi chochote cha Pindua Pindua
utapata picha, video na IG stories bure kabisa.
Uzinduzi huo umepambwa na msanii maarufu Vanessa Mdee na mwanahabari
Millard Ayo.


Facebook Yasimamisha Akaunti ya Kampuni Iliyompigia Debe Uhuru

$
0
0
Image result for Mtandao maarufu wa Facebook
Mtandao maarufu wa Facebook umetangaza kusimamishwa kwa akaunti ya Strategic Communication Laboratories kampuni mama ya Cambridge Analytica, kampuni ya uchambuzi wa data inayotuhumiwa kuratibu kampeni za mgawanyiko kuelekea uchaguzi mkuu wa rais mwaka 2017 nchini

Kusimamishwa kwa akaunti hiyo kumetokana na kampuni ya Cambridge Analytica kukiuka sera zake, mtandao huo mkubwa wa mawasiliano ya kijamii ulisema katika taarifa yake Ijumaa.

Facebook imedai kwamba mnamo mwaka 2015 Cambridge Analytica ilipewa maelezo jinsi ya kutumia Facebook bila idhini kutoka mtandao huo kupitia kazi iliyofanywa kwa ushirikiano na Profesa wa Saikolojia ya Chuo Kikuu cha Cambridge aitwaye Dr Aleksandr Kogan.

"Profesa huyo alisema uongo na kukiuka sera zetu za jukwaa kwa kupitisha data kutoka kwenye programu ambayo ilikuwa ikitumia kuingia FB kwenda SCL / Cambridge Analytica, ambayo inafanya kazi za kisiasa, serikali na za kijeshi kote ulimwenguni. Pia alimpatia data Christopher Wyloe wa kampuni ya Teknolojia ya Eunoia," ilisema Facebook.

Ripoti iliyotolewa mwaka jana na kampuni ya kimataifa ya masuala ya faragha yenye makao yake London, Uingereza, inayopigana haki ya faragha duniani, ilisema kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2017, kampuni ya Cambridge Analytica iliongoza kampeni za mtandao ambazo zililenga ama kumshambulia kiongozi wa Nasa Raila Odinga au kumpigia debe Rais Kenyatta.

Facebook ilisema kuwa kampuni hiyo kipekee ilimfanyia kazi Rais Kenyatta wakati wa kampeni yake ya uchaguzi.

Cambridge Analytica ilikanusha madai na ikasema kuwa haikuhusika katika maudhui yoyote hasi ya kisiasa.


RC Makalla Aingilia Kati Tatizo la Kunguni Mbeya “Ni marufuku Kuendelea, Kila Mtu Apambane na Hali Yake"

$
0
0
RC Makala Aingilia Kati Tatizo la Kunguni “Ni marufuku Kuendelea, Kila Mtu Apambane na Hali Yake"Leo March 17, 2018 Wananchi wa Kata ya Igurusi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, wamechangishana fedha kwa ajili ya kumlipa mganga wa kienyeji ambaye walimuita ili awasaidie kuondoa kunguni katika makazi yao.

Mbali na kunguni, wananchi hao wamedai kuathiriwa na viroboto na chawa kwenye makazi yao wakiamini wadudu hao wamepelekwa kishirikina. Zoezi hilo hata hivyo limewagawa wananchi hao katika makundi mawili, baadhi wakiunga mkono na wengine kupinga.

Mgongano huo umesababisha kuwapo kwa viashiria vya uvunjifu wa amani katika kata hiyo, kumfanya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla, kuingilia kati na kupiga marufuku zoezi hilo huku akisema hata kwa bahati mbaya hawezi kuruhusu watu kuamini uchawi katika mkoa wake.

“Mimi sasa hivi naelekea Dodoma kikazi, sasa nikiruhusu zoezi hilo ambalo ni kinyume na sheria za nchi sitafika hata Iringa, nitakuwa nimeshatumbuliwa na rais,” -Makalla.
“Ni marufuku kuendelea… kila mtu apambane na hali yake.”-Makalla

Makonda Amwagia Sifa Meya wa Jiji "Meya Mwita ni Mwanasiasa Mwenye Dhamira ya Dhati"

$
0
0
Makonda Amwagia Sifa Meya wa Jiji "Meya Mwita ni Mwanasiasa Mwenye Dhamira ya Dhati
Meya Mwita ni Mwanasiasa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amemmwagia sifa Meya wa Jiji hilo, Isaya Mwita akisema ni kiongozi atakayeendelea kung’aa katika uongozi wake kutokana na kazi anazofanya kwa ajili ya Watanzania.

Makonda ametoa kauli hiyo leo Machi 17, 2018 wakati wa mkutano wa kuzindua utalii wa ndani katika mkoa huo, akisema meya wa aina hiyo ni lazima kupata ushirikiano wa ofisi yake tofauti na mameya wanaobakia kumtukana rais.

Katika mkutano huo, RC Makonda amesema Mwita ni mwanasiasa mwenye dhamira njema ya kuwatumikia Watanzania, kama ilivyo kwa dhamira ya rais John Magufuli.

“Pia niendelee kukupongeza Meya wa jiji la Dar es Salaam, kaka yangu na ndugu yangu, na timu yako ya madiwani kwa kazi kubwa unayoifanya, katika jiji tunao madiwani wa vyama vyote ila meya wetu wa jiji ni wa tofauti, ni meya anayetazama maendeleo, anayetaka kazi, tangu nifahamiane naye kila anapokuja ofisini kwangu, ni mpango wa namna gani tunafanya kazi, ndiyo maana ataendelea ‘ku-shine’ kuliko mameya wengine wa upinzani,”amesema.

Amesema kundi la mameya wanaoendelea kumtukana rais, litaishia kuhesabu matusi tu na mwisho wake sheria itachukua mkondo wake.

Wazee Kupanda Taxi Bure Afrika Kusini

$
0
0
Wazee Kupanda Taxi Bure Afrika KusiniStori Ninayokusogezea kutoka kwa Madiba yaani Afrika Kusini leo March 17, 2018 ni kwamba raia mmoja wa nchi hiyo ambaye anamiliki taxi kwaajili ya biashara akiwa wa wenzange wamezua hisia kali kwa watu baada ya kutangaza msaada kwa wazee.

Tajiri huyo wa taxi anayejulikana kama Yaseen Abrahams siku za hivi karibuni ametangaza kuwa yeye na wenzake ambao wanahusika kwenye biashara hiyo watakuwa wanawapakia wazee wa miaka zaidi ya 70 bila kuwatoza gharama yoyote.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 25 aliandika tangazo hilo kwenye ukurasa wake wa Facebook akiwa kwenye mji mmoja karibu na Cape Town, jambo lililosababisha watu kumsifu kwa kuchukua hatua hiyo kuwasaidia wazee.

Mwigulu Awapa Makavu Wanafunzi Wanaojiingiza Kwenye Siasa " Usifanye Harakati Ili Uwe Adui wa Serikali

$
0
0
Mwigulu Awapa Makavu Wanafunzi Wanaojiingiza Kwenye Siasa " Usifanye Harakati Ili Uwe Adui wa Serikali
Waziri wa Mambo ya ndani, Dk Mwigulu Nchemba amewataka wanafunzi kuachana na harakati za kutengeneza  taswira mbaya za serikali  badala yake kuwa na mitazamo chanya.

Aliyasema hayo jana katika kongamano la UNILIFE lililofanyika Chuo cha Biashara (CBE), ambalo liliandaliwa na Mbunge wa Viti maalum, Ester Mmasi.

Alisema wanafunzi hawatakiwi kufanya harakati ili wawe adui wa serikali kwani yenyewe haina muda wa kushughulikia mashinikizo ya wanafunzi.

“Nilishawahi kufanya harakati nikiwa chuoni na nilipewa jina la Chifu..majina yangu yamekuja kujulikana nikiwa serikalini lakini nilikuwa napinga baadhi ya ajenda za Taifa ambazo niliona hazina manufaa,” alisema Dk Mwigulu.

Alisisitiza kuwa wanafunzi wengi kwa sasa wamekuwa wakiitafuta taswira mbaya ya serikali bila  kuangalia masuala mengine yanayopaswa kuungwa mkono.

“Kuwa kijana mwema chuoni sio kwa kuwa kimya Bali kuwa na mitazamo chanya nabukiona mwanazuoni anabisha jambo jema ujue kuna kasoro,” alisema

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Jioni ya Leo

Tanzania Kukumbwa na Kimbunga, TMA Yaeleza

$
0
0
Mamlaka ya hali ya hewa iliyopo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano nchini Tanzania imekanusha kutokea kwa hali ya Kimbunga "ELIAKIMU" katika maeneo yanayozunguka nchi na kudai Kimbunga hicho kipo kwenye visiwa vya Madagascar.

Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa hivi punde na kurasa rasmi za mamlaka hiyo Machi 17, 2018 na kusema ni ukweli Kimbunga kinachojulikana "ELIAKIMU" kipo eneo la Kaskazini Mashariki mwa kisiwa cha Madagascar na kinaelekea Kusini mwa kisiwa hicho.

Aidha, Mamlaka ya hali ya hewa imesema imefuatilia mwenendo wa Kimbunga hicho tangu kilipojitokeza mapema mnamo Machi 15, 2018 majira ya saa 11 asubuhi na kutoa utabiri wa hali ya hewa nchini kwa kuzingatia mifumo yote ya hali ya hewa inayojitokeza.

Kwa upande mwingine, mamlaka hiyo imesema itajitahidi kutoa taarifa  na tahadhari za utabiri kadri inapobidi kufanya hivyo.

Makonda Awaagiza Wananchi Kutupa Taka Kwa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amewataka wananchi wa mkoa huo ambao maeneo yao yamekaa na takataka muda mrefu bila kuzolewa kwenda kuzitupa nyumbani kwa wenyeviti wa Serikali za Mitaa.

Ameyasema hayo leo Machi 17, kwenye hafla ya uzinduzi wa mpango wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wa kuendeleza utalii wa jiji hilo.

Makonda amesema haiwezekani tunakuja na mpango wa utalii lakini jiji bado linaonekana chafu na kutaka kila kiongozi kuwajibika katika kulisimamia hilo.

“Nawaambieni wananchi kuanzia leo kama mna uhakika mmelipa tozo ya kuzolea taka na taka hizo hazijazolewa kwa muda mrefu, zipelekeni nyumbani kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mitaa yenu halafu yeye atajua wapi pa kuzipeleka,” amesema Makonda.

Amesema katika mpango huo anategemea kuona mambo manne yakifanyika ikiwamo suala zima la usafi, utalii, stendi za mabasi za kisasa na masoko ya kisasa ambayo yatawawezesha wafanyabiashara kufanya shughuli zao mahali pazuri.

Kwa upande wake Waziri wa Tamisemi, Suleiman Jaffo, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, ameupongeza uongozi wa mkoa wa Dar es Salaam kwa kuja na mpango huo na kuahidi kwamba ofisi yake itatoa ushirikano kuona jambo hilo linafanikiwa

Irene Uwoya: Nimemzidi Dogo Janja Kila Kitu Labda Yeye Kanizidi Dhambi tu

$
0
0
Msanii wa bongo movie  Irene Uwoya amefunguka na kusema kuwa wala hajali watu wanaosema kuwa amemzdi mwanaume aliyemuoa miaka mingapi kwa sababu yeye anachojali zaidi ni mapenzi na wala sio kitu kingine.

Irene Uwoya ameyasema hayo jana alipokuwa katika mahojiano na kipindi cha Leo tena  cha Clouds Radio  alipokwenda yeye na mumewe huyo.

Irene anasema kuwa kwake umri ni namba tu kwa sababu  hata kwa hao wanaume wenye kulingana nao umri hawakuweza kumpa kile alichokuwa anakitaka.

"Ni kweli nimemzidi  umri na sio umri peke yake hata vitu vingine nimemzidi labda yeye kanizidi dhambi(Akiongea kiutani), Kwangu umri ni namba maana nilishawahi kuwa kwenye mahusiano na watu ambao wamenizidi umri au tupo sawa lakini sikupata nilichokuwa nakitaka lakini kwa mume wangu nimekipata.

"Toka nimeolewa watu wengi wamekuwa wakisumbua japo hapo mwanzoni walikuwepo lakini kwasasa kuna aina ya watu ndiyo wamekuwa wakisumbua kwa kuhisi sababu Abdul kanioa basi hata wao wanaweza kupata nafasi hiyo“

Irene anakiri kuwa katika mahusiano yake yote aliyowahi kuwa nayo, dogo janja ndio mwanaume aliyeweza kumpa kitu ambacho hajawahi kupata kwa mwanaume yoyote na wala sio hela bali ni mapenzi ya dhati.

"Sijaolewa na dogo janja kwa sababu ya pesa,kuna vitu vingi ambavyo nimevutiwa kutoka kwake .Kwanza nilipenda mara ya kwanza alivyokuja na kuni-approch.Dogo Janja amenipa kitu ambacho wanaume wote niliokuwa nao walishindwa kunipa."

Mtangazaji Mamy Baby wa Clouds Awachana Basata na Naibu Waziri Kiana Kupitia Ndoto

$
0
0

Ameandika Mamy Baby - NDOTO ZANGU

"Uso Wangu Upo Katika Tabasamu Pana. Ni Ile Nyimbo Inayopendwa Na Wengi Naona Inapigwa Kwenye Kituo Kikubwa Cha Televisheni Duniani, Kwa Furaha Isiyo Kifani Napitiwa Na Usingizi Mororo. Ndoto Zinanijia, Ninaona Tour Za Akina Jay Z Zikiwa Hazikatiki TZ, mara Dar live, mara Mkwakwani Tanga. Taswira Nyingine Inakuja, Naona Tuzo 4 Za BET Kwa Wasanii Wa Bongo na Hall of Fame moja ya Grammy kwa Mkongwe wa Muziki Tanzania. Kuna Picha Za Wasanii 10 Zinapita Mfululizo Wakiwa Kwenye Magari Yao Ya Kifahari Ferrari Mpaka Lamborghini.... Nastuka Usingizini Na Kugundua Nilikuwa Kwenye Ulimwengu Wa Kufikirika, Ulimwengu Ambao Tanzania Haijaamua Kuufuata. Moyo wangu ghafla umefadhaika kwa sababu nilichoota naamini kinawezekana kutokea ila sioni dalli. Mawazo yangu yanapelekea nitume salamu za ndoto zangu kwa Mhe. Naibu Waziri, Juliana Shonza. . .


1. Nakusalimu Mheshimiwa, mimi mwanamke mwenzako ambaye Natamani kuona ukiacha alama kwenye sanaa yetu natamani uache LEGACY ya sisi kujivunia juu yako. Napata shida kufikiria mabadiliko ya BASATA yatakayoendana na kukutana na Teklonojia na mifumo ya kisasa itakayowezesha hata usajili ufanyike online, TUTAFIKA HUKO KWELI? .

2. Pokea Salamu hizi za kipekee, salamu zenye ndoto kubwa. Ndotoni nimeona wasanii wakilipwa vyema na COSOTA kwa nyimbo kupigwa redioni, wakitajirika kwa kupata haki zao miaka 30 toka waanze kupigania hilo jambo.. Naomba nifahamu ndoto hii, itatimia kweli? .

3. Salamu za kheri hizi Mheshimiwa, nimeota Roma Amemfunika Yule Cassper Nyovest Kwenye Show huko Marekani. Hivi Inawezekana kukawepo namna nzuri ya kudumisha urafiki wa wasanii na wizara na kanuni za kisasa ziwasimamie na kwa ukubwa wa wasanii wetu waalikwe Ulaya kuimba kwenye viwanja sio kwenye migahawa? .

4. Usichoke salamu zangu mheshimiwa, wale waliofungiwa kwa maadili ya Video za muziki wao, tunawaambiaje pale ambapo hatuwezi kufungia video za Rihanna zisichezwe nchini au kila mtu atoe nyimbo YOU TUBE tu ambapo watu wenye kipato cha chini wasiweze kuwa na haki ya kuona, tubaki sisi tu wenye kipato kidogo? .


5. Natamani kukusalimu kwa ukaribu zaidi lakini acha nizitume hapa, nakwambia kweli nimeota Wizara imeweza kufanikisha mazingira ya biashara kubwa ya muziki. Utaliwezesha vipi hili mheshimiwa litakusaidia sana kwenye kuondoka na Legacy ya hatari tutakayoikumbuka.... .

6. Kwenye Ndoto zangu nimemtizama Yule Kijana Aliyezoea Kwenda Kwenye Show za wasanii kama Leaders lakini muda umepunguzwa na Leaders yenyewe pamefungiwa. Utamsaidia vipi huyu naye aweze kuhadithia watoto wake kwani naona dalili za matamasha Dar es Salaam kupotea kabisa....bado nakusalimu tu Mheshimiwa. .

7. Ndotoni namwona bibi yangu, najiona mimi na wewe, namwona mdogo wangu na wanangu. Wote tuna hisia tofauti kwa wimbo mmoja, pokea salamu mheshimiwa. Kwani Maadili tunayajudge vipi? Huu wimbo wa maadili nani atamhadithia mwenzake???? .

8. Nisikuchoshe na Salamu Zangu Mheshimiwa, nakaribia mwisho wa simulizi ya ndoto zangu, nimeona Jay Z na Beyonce wapo bongo kwenye ukumbi mmoja wa maana.? .

9. Mwisho kabisa nimekuona Ndotoni ukikabidhi tuzo ambayo ina hadhi kubwa sana na unashangiliwa mno unaposhuka kwani sio tu umempa tuzo msanii mkubwa ila maandalizi yake yamefana sana kwa event hiyo kubwa iliyofanyika Mlimani city. .


Roho inauma ndoto ilikatika sehemu tamu, salamu zangu nawasilisha kwako. Nimeacha kwa Watanzania nao watume salamu zao. Naamini utapata muda uzisome ndoto zetu wote"

Yanga Yaangukia Pua Gaborone Botswana..

$
0
0
Mbingwa wa Tanzania Club ya Dar es Salaam Young Africans jana March 17 2018 wamecheza game yao ya marudiano ya Club Bingwa Afrika ya kuwania kufuzu hatua ya Makundi ya michuano hiyo dhidi ya wenyeji wao Township Rollers.

Yanga walisafiri kwend Gaborone Botswana wakiwa nyuma kwa magoli 2-1 baada ya mchezo wa kwanza nyumbani kupoteza, hivyo waliingia Botswana wakihitaji ushindi wa kuanzia magoli 2-0 na kuendelea ili waweze kufuzu.

Bahati mbaya mambo yamekuwa magumu mjini Gaborone baada ya Township Rollers kuweka ulinzi wa kutosha na kutoruhusu goli, kitu ambacho kimefanya mchezo umalizike kwa sare tasa (0-0), hivyo Township Rollers inakuwa club ya kwanza Botswana kufuzu hatua ya Makundi ya michuano ya club Bingwa Afrika kwa mara ya kwanza katika historia

Simba Out Kimataifa...Haji Manara Hana cha Kuongea

$
0
0
Safari ya Simba kwenye michuano ya kombe la shirikisho Afrika imeishia Misri baada ya kulazimisha suluhu na wenyeji wao Al Masry katika mchezo wa marudiano uliochezwa kwenye mji wa Port Said usiku wa Machi 17, 2018.

Simba ilikuwa ikihitaji ushindi wa aina yoyote ili ijihakikishie kufuzu hatua inayofuata kutokana na sare ya kufungana magoli 2-2 katika mchezo wa awali wa raundi ya pili ya mashindano hayo.

Katika michezo minne ambayo wamecheza katika mashindano ya kombe la shiikisho Afrika, Simba imetolewa huku ikiwa haijapoteza mchezo hata mmoja.

Simba 4-0 Gendarmerie
Gendarmerie 0-1 Simba
Simba 2-2 Al Masry
Al Masry 0-0 Simba
Baada ya kutupwa nje ya mashindano hayo, Wekundu wa Msimbazi wanarejea kupambana kwenye ligi kuu Tanzania bara ambapo hadi sasa wanaongoza licha ya kuwa pointi sawa na Yanga wao wana mchezo mmoja wa kiporo.

Simba inahitaji ubingwa wa ligi ili kujihakikishia nafasi ya kurejea kwenye mashindano ya kimataifa Afrika kwa msimu ujao. Wameshatolewa kwenye kombe la shirikisho Tanzania bara (FA Cup) ambalo walikuwa mabingwa msimu uliopita wakapata fursa ya kucheza kombe la shirikisho Afrika.

Jua Aina 10 ya Wanawake Wanaopendwa na Wanaume Kuwa nao Katika Mapenzi

$
0
0
WENYE MSIMAMO
Wanawake daraja la kwanza wanaopendwa zaidi na wanaume ni wale wenye msimamo, uelewa mkubwa wa mambo na maamuzi sahihi, wako makini kwenye matendo yao na siku zote hufanya vitu kwa ajili ya kupata mafanikio.

WAPENDA USAWA
Aina ya pili inayohitajika katika katika ulimwengu wa kimapenzi ni wanawake wanaoheshimu usawa wa jinsia, walio tayari kubeba majukumu ya kifamilia kwa ulinganifu sawa na wanaume, wenye uwezo wa kuongoza jamii kwa asilimia 50 kwa 50.

WANAOJUA MAPENZI
Wanawake wajuzi wa mambo ya faragha wanapendwa sana. Sifa yao kubwa ni uwezo wa kutosheleza katika tendo la ndoa. Tafiti zinaonyesha kuwa wanaume hupenda sana wanawake watundu katika mchezo wa sita kwa sita. Mara nyingi wanatajwa kuwa na uwezo wa kuteka akili za wanaume bila kujali sifa zao za nje au za ndani.

MARAFIKI
Wanawake wenye sifa sawa na rafiki ni aina ya nne inayowavutia wanaume. Wao hutegemea zaidi nguvu ya kushawishi inayotokana na namna wanavyojali na kujitolea kuhakikisha wanakuwa marafiki wa kweli kwenye shida na raha kwa wapenzi wao. Si wakorofi, waungwana na wapenda amani.

WA WAZI
Aina nyingine ya wanawake inayowavutia wanaume ni wenye msimamo na uwazi. Si wepesi wa kuburuzwa katika maamuzi ya msingi kwa kisingizio cha wao ni wanawake. Utafiti unaonesha wanawake wa aina hii wamekuwa muhimu hasa kwa wanaume wenye tabia za ubabe na udhaifu katika uelewa wa mambo.

WANAOJITEGEMEA
Wanawake wanaojitegemea wana soko kubwa kwa wanaume tofauti na akina naomba vocha kila siku. Uchunguzi unaonyesha kuwa wanaume wa leo hawapendi wanawake tegemezi, wasiokuwa na kazi na wanaoendekeza starehe za upande mmoja.

WASIO NA PRESHA
Nikisema wanawake wasiokuwa na presha namaanisha wasiolazimisha vitu vitokee haraka haraka. Wao siku zote huacha mambo yatokee yenyewe na kazi yao kuwa ni kutenda sehemu ya majukumu yao kama wapenzi.

MARIDADI
Kundi lingine la wanawake wanaopendwa na wanaume ni wanaozingatia usafi na kujiremba. Wanaokwenda na wakati katika mavazi na mvuto wa nje. Lakini pia ni welewa wa mazingira, si wasamba. Wanapendeza kwa muonekano.

WANAORIDHIKA
Wanawake ambao hulidhika na hali walizonazo ni kivutio kikubwa kwa wanaume, hili ni kundi linalohitajika sana katika ulimwengu wa mapenzi kwa upande wa wanaume ambao maisha ya sasa yamekuwa yakiwageuza kutoka juu kwenda chini au chini juu. Kukubali hali zote bila kubadili tabia ni sifa njema ya mwanamke.

WA MMOJA
Wanawake wanaochagua mara moja na kutosheka na kuwa tayari kukwepa kila aina ya vishawishi toka kwa wanaume ambao kimtazamo wana vitu vya ziada zaidi ya waliowachagua mwanzo wanahitajika sana. “Niliye naye ananitosheleza kwa kila kitu sitaki mtu mwingine.” Kundi la wanawake wa aina hii ni adimu na muhimu sana.
Viewing all 104694 articles
Browse latest View live




Latest Images