Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104414 articles
Browse latest View live

Upelelezi Kesi ya Mhasibu TAKUKURU Wakamilika

0
0
Upelelezi Kesi ya Mhasibu TAKUKURU Wakamilika
Leo March 20, 2018 moja ya stori ninayokusogezea ni kutoka Mahakamani ambapo Upelelezi wa kesi inayomkabili Mhasibu Mkuu wa (TAKUKURU), Godfrey Gugai anayedaiwa kumiliki mali za Shilingi Bilioni 3 ambazo haziendani na kipato chake umekamilika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Mbali na Gugai, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni George Makaranga, Leonard Aloys na Yasini Katera.

Hayo yameeleza na Wakili wa TAKUKURU, Vitalis Peter mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba wakati shauri hilo lilipoitishwa kwa ajili ya kutajwa.

Wakili Vitalis amedai kuwa upelelezi wa shauri hilo umekamilika, hivyo anaomba tarehe kwa ajili ya kumsomea mshtakiwa maelezo ya awali (Ph).

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi April 10, 2018 kwa ajili ya mshtakiwa kusomewa maelezo ya awali.

Kwa pamoja washtakiwa wanaokabiliwa na mashtaka 43 yakiwemo 20 ya utakatishaji fedha haramu, kumiliki mali zisizoendana na kipato na kughushi mikataba ya mauziano ya viwanja katika maeneo mbalimbali.

Gugai na wenzake wanasota mahabusu kutokana na kukabiliwa na mashtaka ya utakatishaji fedha ambayo hayana dhamana kwa mujibu wa sheria.



Waziri Shonza: Nimesikia Malalamiko ya Daimond Mimi Siwezi Kujibizana Naye

0
0
Nimesikia Malalamiko ya Daimond Mimi Siwezi Kujibizana Naye
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Juliana Shonza, amesema amesikia malalamiko ya mwanamuziki Diamond lakini hawezi kumjibu kwa sababu zipo taratibu za kufuata kama anaona hajatendewa haki.

Shonza analijibu hilo ikiwa ni siku moja tangu mwanamuziki  'Diamond' amtaje waziri huyo katika malalamiko yake, akidai amekuwa akikurupuka  na kutolea mfano wa kufungia nyimbo na wasanii wakati akihojiwa na kituo cha redio cha Times.

Waziri huyo amesema hayupo tayari kumjibu Diamond  ingawa wasanii wanapaswa kuelewa kuwa hakuna aliye juu ya sheria hata kama msanii mkubwa namna gani.

"Aliyewafungia wasanii si Shonza bali ni mamlaka na kama mlivyoona safari hii hadi Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeingilia kati suala hilo, sasa mtu anaporusha tuhuma kumlaumu Shonza atakuwa hanitendei haki. Isitoshe ofisi zetu zipo wazi anayeona ameonewa afuate taratibu katika kudai haki yake na si kulalamikia pembeni," amesema Waziri Shonza.

Kuhusu kutoitwa kwa wasanii kabla ya kufungiwa kwa nyimbo zao Shonza amesema hilo waulizwe Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) maana ndio wenye kujua sababu na kwa baadhi ambao aliwaita ameeleza kuwa ni kutokana na kupewa maagizo ya kubadilisha nyimbo zao na kuwahi kukiri makosa lakini wakashindwa kutekeleza.

Katika mahojiano hayo na redio Times, Diamond alielekeza mashambulizi zaidi kwa Waziri Shonza na kudai kwamba amekuwa akifanya maamuzi yake kwa kukurupuka akisahau kwamba viongozi hawana mchango wowote kwao na pia wamekuwa wakiziumiza familia zao.

"Hivi leo unanifungia nyimbo yangu niliyoitengeneza kwa mamilioni ya pesa unadhani nitazirudishaje, au unadhani watoto wangu Nillan, Dyllan na Tiffah watanunuliwa na nini ‘pampas’? Ifike mahali viongozi wetu wavae viatu vyetu na si kuona raha tu kutufungia wakati tumetaabika katika kuyajenga majina yetu hadi sasa tunajulikana duniani," amesema Diamond.

Februari 28 TCRA iliandika barua kwa vituo vya redio na televisheni ikiviagiza visitishe kuonyesha nyimbo 15 za wasanii kadhaa kutokana na kuwa na maudhui ambayo yanaenda kinyume na maadili na kanuni za Huduma za Utangazaji(Maudhui) 2005.

Nyimbo hizo na jina la msanii aliyeimba  kwenye mabano ni  Hallelujah na Wakawaka (Diamond), Kibamia (Roma Mkatoliki), Pale Kati patamu, Maku (Makuzi) na Mikono Juu (Ney wa Mitego), Hainaga Ushemeji(Manifongo), I am Sorry JK(Nikki Mbishi.

Nyingine ni Chura (Snura) na Nimevurugwa (Snura), Tema mate tumchape(Madee), Uzuri wako(Jux), Nampa papa(Gigy Money), Nampaga(Baranaba) na Bongo Bahati mbaya(Young D).

Rais wa Zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy Ashikiliwa na Polisi

0
0
Rais wa Zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy Auiliwa na Polisi
Aliyekuwa Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy anazuiliwa na polisi akihojiwa kuhusu tuhuma kwamba alipokea pesa za kufadhili kampeni zake kutoka kwa kiongozi wa zamani wa Libya Kanali Muammar Gaddafi.

Polisi wanachunguza tuhuma hizo kuhusiana na ufadhili wa fedha alizotumia kwenye kampeni za uchaguzi wa urais mwaka 2007.

Msaidizi wake wa zamani Alexandre Djouhri pia alikamatwa jijini London karibuni.

Bw Sarkozy alishindwa katika juhudi zake za kutaka kurejea madarakani mwaka 2012.

SHINDA GARI LA BUREEEE !!!

0
0
Jee!! Katika Maisha yako umewahi kuwa na ndoto ya kumiliki Gari lako?  Kama jibu ni Ndio Basi Kampuni ya Kijapan inakupa Fasi ya kushinda Gari Buree yani Buree bila kulipa chochote..

Chakufanya ni kubofiya neno SHINDA GARI  hapo chini na kisha Bonyeza Neno APPLY NOW kwa kujisajili...

Kumbuka huduma hii ni ya Bure kabisaaaaa...


>> SHINDA GARI <<

>> SHINDA GARI <<

>> SHINDA GARI <<

Maskini Mtoto Afariki Baada ya Kuibwa Akiwa Ndani ya Gari

0
0
Maskini Mtoto Afariki Baada ya Kuibwa Akiwa Ndani ya GariKutoka nchini Uingereza polisi wanachunguza kisa cha mtoto wa miaka miwili kufariki baada ya kukutwa akiwa ndani ya gari ambalo limekutwa limedumbukizwa mtoni.

Inaelezwa kuwa mtoto huyo Kiara Moore alifariki akiwa katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Wales katika jimbo la Cardiff baada ya kuokolewa kutoka kwenye gari hilo.

Polisi wameeleza kuwa mama mzazi wa mtoto huyo aliripoti kuwa watu wasiojulikana waliliiba gari lake katika eneo la Emlyn hilo huku likiwa na mtoto huyo ndani na ndipo likakutwa limedumbukizwa kwenye mto Teifi siku ya jana March 19, 2018.

Model wa Video ya ‘Ntampata Wapi’ ya Diamond Ashinda Taji la Top Model SA

0
0
Model wa video ya ‘Ntampata Wapi’ ya Diamond ashinda taji la Top Model SA
Unamfahamu Melissa Magiera ambaye amewahi kuonekana kwenye video ya ‘Ntampata Wapi’ ya Diamond? Nadhani utakuwa umeshamkumbuka kupitia video hiyo niliyokutajia.

Mrembo huyo ambaye kwa sasa yupo chini ya kampuni ya Fan Jam Model Management, wiki iliyopita amefanikiwa kushinda taji la Top Model 2018 nchini Afrika Kusini.

Melissa ameshinda taji hilo kwa kuwabwaga washiriki wengine 38 ambao walifanikiwa kutinga katika hatua ya nusu fainali.

Mrembo huyo ataiwakilisha Afrika Kusini kwenye mashindano ya Top Model ya dunia ambayo yatafanyika Ijumaa ya April 6 na 7 ya mwaka huu mjini London.

Jokate Atangaza Ndoa " Natarajia Kuwa Mke wa Mtu Hivi Karibuni"

0
0
Jokate Atangaza Ndoa " Natarajia Kuwa Mke wa Mtu Hivi Karibuni"
Mwanamitindo na Mjasiliamali Jokate Mwegelo ambaye pia ni Kaimu Katibu Hamasa wa Jumuiya ya Vijana wa CCM, ameibuka na kudai anatarajia kuolewa 'kuwa mke wa mtu siku za hivi karibuni' licha ya kumficha mwanaume ambaye atamuoa.


Jokate ametoa kauli hiyo mchana wa leo (Machi 20, 2018) kupitia ukurasa wake wa kijamii akiwa wahabarisha wadau wake wakae mkao wa kula kusherehekea tukio hilo ambalo amelipanga kulifanya katika siku za usoni.

"March Quen, karibu nitakuwa mke wa mtu fulani na mama watoto wake. 'God is great and faithful, grown but forever a baby girl'. Ni kwa neema tu na rehema zake Mungu. Thank you loves for dragging me out to take these", amesema Jokate.

Jokate Mwegelo ameweza kuweka uwazi wa maisha yake ndani ya siku aliyoweza kuletwa duniani 'kuzaliwa' miaka kadhaa iliyopita tarehe na mwezi kama wa leo

Ugonjwa wa Hatari wa Dengue Waibuka Tena

0
0
Ugonjwa wa Hatari wa Dengue Waibuka Tena
Wizara ya Afya, Jinsia, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto imethibitisha kulipuka tena kwa Ugonjwa wa Hatari wa Dengue Waibuka Tena ambao uliwahi kuibuka nchini na kuua baadhi ya watu.


Akizungumza na mwandishi wa www.eatv.tv , msemaji wa Wizara ya Afya Nsachris Mwamwaja, amesema ni kweli ugonjwa huo umeripotiwa kuibuka tena, na taarifa kamili inatarajiwa kutolewa leo mchana na Waziri Ummy Mwalimu.

“Na kweli Katibu Mkuu aliitoa, lakini rasmi tutaoa wakati wowote leo, kuna shughuli ambayo ataifanya Waziri kwa hiyo kuna uwezekano akatoa taarifa hiyo kwa sababu imeshandaliwa”, amesema Bwana Mwamwaja.

Ugonjwa huo ambao unasababishwa nakirusi ambacho kinaenezwa na mbu wa aina ya Aedes., husababisha homa kali na hatimaye kifo, hivyo wananchi wanatakiwa kuwa makini na kutumia vyandarua wakati wa kulala, na kuepuka kukaa sehemu zenye mbu.

Mchungaji Huyu Kiboko Awalazimisha Waumini Kulamba Viatu Vyake

0
0


Leo March 20, 2018 stori ninayokusogezea ni ya Mchungaji mmoja kutoka Nigeria ambae makao yake yapo Afrika Kusini ambapo amezua gumzo katika mitandao ya kijamii baada ya ku-post picha zake wakati wa kuabudu mitandaoni.

Anafahamika kwa jina ‘Nabii’ Andrew Ejimadu ambae ni msimamizi mkuu wa kanisa la Christ Freedom Ministries alishangaza maelfu ya watu baada ya kupigwa picha zilizoonyesha waumini wa kanisa lake wakibusu na kulamba viatu vyake ili kupata baraka na miujiza.



Nabii huyo ndie aliyeweka picha hizo katika ukurasa wake wa Facebook na kuandika: “Nimebariki miguu yako, nimeosha nyayo zako.”

“Kitu cha kwanza kesho asubuhi, ikiwa utaandika Amen na ushirikishe ujumbe huu, kuna mtu atakupigia simu na miguu yako itakubeba hadi huko kuchukua zawadi maalum. Watu wengi watakosa hilo, jaribu,” – Andre Ejimadu





Maneno ya Irene Uwoya kwa Msami ‘Usi-force, Panic na Yako’

0
0
Maneno ya Irene Uwoya kwa Msami ‘Usi-force, Panic na Yako’
Leo March 20,2018 kwa upande wa burudani story ambayo na yenyewe inachukua headlines ni kutoka kwa mke wa msanii Dogo Janja, Irene Uwoya ambaye leo amechukua dakika zake kuandika Instargram ambapo amem-post staa wa muziki wa Bongo Fleva ambaye pia ni dancer Msami na kuandika caption ambayo imezua gumzo mtandaoni

Irene Uwoya ameandika…. >>> Mchezaji muziki bora Afrika usi-force ndio kuwa hapana na tafadhali panic kwa hatari yako mwenyewe @msamibaby

Lakini kwa upande wa comments muigizaji Steven Nyerere alionekana ku-comment kutokana na kile ambacho Irene Uwoya ameki-post kwenye page yake ya instagram.

Steven Nyerere ameandika…….>>>“Umeanza tena heee we mwanamke doh leo umemkumbuka tena wewe huyo linda ndoa tushachoka vikao vya ndoa”

Man Water Afunguka Kuhusu Alikiba

0
0
Mtayarishaji mkongwe wa muziki wa BongoFleva, Man Water amefunguka na kuwahakikishia mashabiki wa Alikiba kuwa kuna ngoma mpya imeshafanyika mpaka 'video' na muda wowote kutoka sasa inaweza kuachiwa ili kuvunja ukimya uliokuwepo kwa kipindi kirefu.


Man Water amebainisha hayo wakati alipokuwa anapiga stori na 'BIG CHAWA' kutoka katika kipindi cha Planet Bongo 'PB' ya East Africa Radio baada ya kuwepo na malalamiko mengi yanatoka kwa mashabiki wake waliokuwa wanadai wanataka kumsikia mfalme wao aking'uruma katika muziki.

"Kuna ngoma ambayo tumefanya na imeshafanyiwa video tayari kwa jinsi nilivyosikia, kwasababu Alikiba yupo South Afrika 'SA'. Pengine wimbo huo unaweza ukawa ndio unaofuata kwa sasa baada ya 'Seduce me", amesema Man Water.

Familia ya Abdul Nondo Yakata Tamaa Baada ya Kushindwa Kumuona Tangu Ashikiliwe na Polisi

0
0
Familia ya  Abdul Nondo Yakata Tamaa Baada ya Kushindwa Kumuona Tangu Ashikiliwe na Polisi
Imeelezwa kuwa familia ya  Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP) Abdul Nondo imeanza kukata tamaa  juu ya hatma ya mtoto wao baada ya kushindwa kumuona kwa zaidi  ya siku 10 tangu ashikiliwe na Jeshi la Polisi.


Hayo yamesemwa na Wakili wa mwanafunzi huyo, Jebra Kambole  wakati akizungumza na www.eatv.tv ambapoameweka wazi kuwa familia ya Nondo imeanza kurudi nyuma katika kumtafuatilia kijana wao na kwamba aliyebaki na moyo wa kumtafuta kijana huyo ni baba mzazi tu.

Wakili Kambole amesema kuwa Baba yake Nondo ndiye ambaye amekuwa kwa sasa wakihangaika naye kufahamu ni wapi Nondo alipo huku mzazi huyo akisema anamuomba Mungu kijana wake aonekane ili wafahamu shida ni nini.

Kwa upande mwingine Kambole amesema kuwa tukio la Nondo kutoonekana katika vituo vya polisi linamshangaza sana na hii imekuwa mara yake ya kwanza kukutana nalo tangu aanze kufanya kazi hiyo.

Mwenyekiti huyo wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo, ambaye pia ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) aliripotiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha usiku wa Machi 6 na kesho yake machi 7 kujikuta Iringa na baada ya kuripoti kituo cha polisi mkoani huko alisafirishwa mpaka polisi Kanda Maalum Dar es salaam.

Mama Uwoya Amkana Dogo Janja

0
0
Mama Uwoya Amkana Dogo Janja
Mama mzazi wa msanii wa filamu nchini Irene Uwoya amefunguka na kuweka wazi kuwa yeye hatambui kuhusu ndoa ya mtoto wake na msanii mwenzake Dogo Janja na kusema kama wamefunga ndoa wanaijua wao ila yeye na baba mzazi wa Irene hawaitambui.


Mama mzazi wa Irene Uwoya ameweka wazi hilo alipokuwa akifanya mahojiano na moja ya chombo cha habari na kusema kuwa yeye na baba wa Irene hawaitambui hiyo ndoa ya mtoto wao na Dogo Janja.

"Kwanza huyo kijana sijui niongee lugha gani mimi nilishaongea toka mwanzo na nilisema nadhani wote mlishuhudia hata kwenye msiba wa mkwe wangu Irene alikuwa bado kwenye ndoa sasa wao kama wamefunga ndoa yao wanaijua wao mimi na baba yake mpaka leo hatuijui hiyo ndoa, mimi kwanza hata sijawahi kumtia machoni huyo kijana sasa sijui kama anasema alikuja kujitambulisha simjui huyo mzazi wake na sielewi aliowaozesha ni kina nani, labda ana wazazi wengine na ndugu wengine na hao ndugu anaosema walidhuria kwenye harusi yake ni kina nani?

Mzazi huyo wa Irene Uwoya aliendelea kutoa ufafanuzi juu ya jambo hilo

"Anavyosema hajabadili dini mimi sijawahi kuona Muislam akafungisha ndoa ya mmoja Mkristu mwingine Muislam, nachofahamu mimi kwenye dini ya Kislamu huwezi kufunga ndoa ya mseto lazima ubadilishe dini kwa hiyo aeleze vizuri kama amebadili dini kwanini anaficha, ila kama amebadilisha dini yeye ni mtu mzima na sisi wazazi hatuwezi kuhusika hapo. Ila yeye na huyo mume wake hatujawahi kuwaona hapa nyumbani. Ila mimi malumbano na mtoto niliyemzaaa sipendi na sina tatizo lolote na yeye atabaki kuwa mtoto wangu lakini sipendi kuingizwa kwenye vitu vya kipuuzi" alisisitiza Mama Irene

Waziri Majariwa Ataka Suluhisho la Magonjwa Yasioambukiza

0
0
Waziri Majariwa Ataka Suluhisho la Magonjwa Yasioambukiza

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Afya wa Uganda, Sarah Opendi, wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 65 wa Baraza la Mawaziri wa Afya wa Jumuiya ya Nchi  za Mashariki Kati na Kusini mwa Africa (ESCA Health Community) kushoto ni Wazri wa Afya wa Malawi Atupele Muluzi,Waziri Mkuu amefungua mkutano huo jana March 19/2018 Jijini Dar es salaam .


Baadhi ya washiriki kutoka nchi tisa za Afrika wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (katikati).




WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewataka Mawaziri wa Afya kutoka nchi tisa za Afrika kutoa mapendekezo ya namna ya kutokomeza magonjwa yasiyo ambukiza kwa wakuu wa nchi hizo ili yafanyiwe kazi.

Aliyasema hayo jana jioni (Jumatatu, Machi 19, 2018) wakati akifungua Mkutano wa 65 wa Mawaziri wa Afya kutoka nchi tisa wanachama wa Jumuiya ya Afya kwa nchi za Afrika Mashariki, Kati  na Kusini (ECSA-HC).



Alisema magonjwa yasiyo ambukiza ni miongoni mwa magonjwa ambayo yameendelea  kuwatesa wananchi kwa kiasi kikubwa katika nchi nyingi za Bara la Afrika, hivyo vema mawaziri hao wakatoa mapendekezo ya namna ya kuyatokomeza.



Waziri Mkuu alisema magonjwa hayo yanaweza kudhibitiwa kwa kuhamasisha wananchi kuboresha lishe na kusisitiza ulaji wa vyakula bora, kufanya mazoezi na kubadili mitindo ya maisha.



“Magonjwa yasiyoambukiza yanaongoza kwa kusababisha vifo katika baadhi ya nchi wanachama wa ECSA. Magonjwa haya yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya mfumo wetu wa lishe na maisha, hivyo ni muhimu suala hili likatafutiwa ufumbuzi.”



Waziri Mkuu alisema magonjwa yasiyoambukiza pamoja na magonjwa mengine ya milipuko kama ebola, homa ya bonde la ufa, dengue, homa ya manjano yamekuwa kikwazo cha maendeleo kwa katika baadhi ya nchi.



Pia, Waziri Mkuu aliongeza kuwa sekta ya afya ni muhimu kwa ajili ya kuboresha maendeleo ya nchi zote zikiwemo zilizoendelea na zinazoendelea, hivyo changamoto zote zinazoikabili zinapaswa zipewe kipaumbele katika utatuzi.



Kwa upande wake, Waziri wa Afya, Jinsia, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto, Bibi Ummy Mwalimu alisema malengo ya mkutano huo ni kuzungumzia changamoto mbalimbali zinazohusu sekta ya Afya na kuyapatia ufumbuzi.



Mkutano huo ulihudhuriwa na Mawaziri wa Afya kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afya kwa nchi za Afrika Mashariki, Kati  na Kusini ambazo ni Tanzania, Malawi, Lethoto, Uganda, Kenya, Rwanda, Zambia, Zimbabwe na Muwakilishi kutoka nchini Mauritious.



Pia Katibu wa jumuiya hiyo Profesa Yoswa Dambisya, Muwakilishi wa Benki ya Dunia Dkt. Paolo Belli pamoja na wadau wa sekta ya afya kutoka nchi hizo.

Msemaji wa Yanga Awapa Makavu Mashabiki wa Timu Hiyo "Acheni Kulaumu"

0
0
Msemaji wa Yanga Awapa Makavu Mashabiki wa Timu Hiyo "Acheni Kulaumu"
Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa mabingwa wa soka nchini Yanga SC, Dismas Ten amewaambia mashabiki wa timu hiyo kuacha kulaumu na kuwafundisha viongozi chakufanya bali waje uwanjani kuunga mkono timu zao.


Ten ameyasema hayo leo kwenye mkutano na wanahabari muda mchache kabla ya uzinduzi wa masuala ya kidijitali ya klabu hiyo, ambayo yatatoa huduma ya taarifa mbalimbali zinazohusu timu hiyo kwa mashabiki wake.

''Tunao mashabiki wengi kwasasa wamekuwa wakizungumza vitu vingi, kusema watu, kutukana watu ni wakati sasa wakuacha kufanya hivyo badala yake wajitokeze uwanjani kutoa nguvu ya 12 kusapoti wachezaji'', amesema Ten.



Ten pia amefafanua kuwa watu wengi walikuwa wanamuuliza kwanini hajaenda na timu Botswana ambapo amesema Yanga ni taasisi kubwa na ina wafanyakazi wengi ambao wanafanya majukumu wakati yeye yupo kwenye shughuli zingine za taasisi.

Ten amesisitiza kuwa masuala ya benchi la ufundi kupangiwa kikosi yameshapitwa na wakati, kwasababu benchi lina uwanja wake mpana wa kufanya maamuzi kwenye kikosi ili timu ifanye vizuri hivyo kila mtu afanye majukumu yanayomuhusu.

Faru wa Kipekee Aliyekuwa Amesalia Duniani Afariki

0
0
 Faru wa Kipekee Aliyekuwa Amesalia Duniani Afariki
Sudan, faru pekee wa kiume aina ya Northern White Rhino (Faru Weupe wa Kaskazini) aliyekuwa amesalia hai duniani, amekufa akiwa na miaka 45, shirika la Ol Pejeta limetangaza.

Faru huyo alikuwa akitibiwa kwa muda na matabibu katika shamba kubwa la uhifadhi wa wanyama la kituo hicho kwa muda kutokana na matatizo yaliyotokana na kuzeeka kwake.

Alikuwa na vidonda ambavyo vilikuwa vinakosa kupona kutokana na umri wake.

Shirika la Ol Pejeta limesema hali yake ilidhoofika sana katika kipindi cha saa 24 zilizopita.

"Hakuweza hata kusimama na alikuwa anateseka sana," Ol Pejeta wamesema kupitia taarifa.

Ripoti: Faru John alikufa kwa kukosa uangalizi wa karibu
"Matabibu wa wanyama kutoka kituo cha uhifadhi wa wanyama cha Dvur Kralove kutoka Jamhuri ya Czech, Ol Pejeta na Shirika la Wanyamapori kenya waliamua kukatisha uhai wake."

Sudan alikuwa maarufu sana duniani na alikuwa nembo ya kutetea juhudi za kupigana na ujangili na kuwaokoa wanyama walio katika hatari ya kuangamia.


Mwaka 2009, alirejeshwa Afrika na kuanza kutunzwa katika kituo cha Ol Pejeta katika jimbo la Laikipia.

Alichangia kuendeleza faru wa aina yake kwa kutungisha mimba faru wengine na kuchangia kuzaliwa kwa faru wengine wawili wa aina yake ambao sasa ndio pekee waliosalia hai.

Mfanyabiashara Dar Apandishwa Kizimbani kwa Kusafirisha Dawa za Kulevya

0
0
Mfanyabiashara Dar Apandishwa Kizimbani kwa Kusafirisha Dawa za Kulevya
MFANYABIASHARA Hariri Mohammed (45) mkazi wa wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam,  amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na tuhuma  za kusafirisha zaidi ya gramu 214 za madawa ya kulevya.

Akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali, Clara Chalwe,  mbele ya hakimu mkazi mkuu, Huruma Shahidi, alidai kuwa Machi 2 mwaka huu katika eneo la Matitu, katika  wilaya ya Kinondoni, mshtakiwa alisafirisha dawa za kulevya aina ya Heroine Hydrochloride zenye  uzito wa gramu 214.11.

Baada ya  kusomewa hati ya mashtaka mtuhumiwa hakuruhusiwa kujibu chochote mahakamani  hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza  kesi za dawa za kulevya isipokuwa kwa kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).

Hivyo, upande wa mashtaka umeiambia mahakama kwamba upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika, hivyo kesi imeahirishwa hadi Aprili 4 mwaka huu.

Rais wa Ufilipino Atangaza Nia ya Kukifungia Kisiwa Maarufu Nchini Humo

0
0
Rais wa Ufilipino Atangaza Nia ya Kukifungia Kisiwa Maarufu Nchini Humo
Leo March 20, 2018 nakusogezea stori kutoka kwa Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte ambapo ametangaza uwezekano wa kuamua kukifunga kisiwa maarufu nchini humo cha Bocaray siku za usoni.

Ameeleza sababu za kutaka kufunga kisiwa hicho kuwa kinapelekea uharibifu wa mazingira na hivyo lengo ni kuepuka athari za uharibifu huo wa mazingira ambao kwa sasa unaendelea katika kisiwa hicho.

Kisiwa hicho cha Boracay kinatajwa kutembelewa na watalii zaidi ya milioni moja na kuingiza mapato ya Dola za Marekani 772.5 ambayo ni sawa na Shilingi za Kitanzania Trilioni 1.8 kila mwaka.

Utafiti wa mwaka 2015 uliofanywa na Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Japani (JICA) lilionyesha kuwa mwamba wa matumbawe wa kisiwa hicho umeharibiwa sana na shughuli zinazohusiana na utalii.

Utafiti pia umebaini kuwa ubora wa maji katika kisiwa hicho umeharibika sana kutokana takataka zinazotupwa kwenye maji hayo.

Millen Amtole Povu Shabiki Kuhusu Mtoto Wake " Kama Sikumnyonga Tumboni Sitomnyonga Duniani"

0
0
Millen Amtole Povu Shabiki Kuhusu Mtoto Wake " Kama Sikumnyonga Tumboni Sitomnyonga Duniani"
Mwanamitindo Millen Magese amejikuta akiongea kwa hasira na uchungu baada ya moja ya mashabiki zake kumsema na kumwambia kuwa kwa mavazi anayomvalisha mtoto wake ni kama anataka kumuu kwa kumnyonga,.

Mwanamitindo huyo ambae amepata mtoto wake hivi karibuni baada ya kukaa kwa muda mrefu bila kupata mtoto kutokana na ugonjwa aliokuwa nao ambao kwa wanawake wengi unasababisha ugumba aliongea na kusea kuwa kwa muda mrefu sana amekuwa akitafuta mtoto huyo kwaio hawezi kufanya kitu kama icho.

Katika ukurasa wake wa instagram millen aliweka picha a mtoto wake ndipo alipoanza kupokea maneno ya kukera kutoka kwa mashabiki na kuamua kumjibu mmoja wapo.

Picha ya mtoto wa millen iiliyozua utata katika mitandao.



Belle 9 Afunguka " Basata na Waziri Wanatafuta Kiki"

0
0

Msanii wa muziki wa RnB kutoka Tanzania Damian Abelnego a.k.a Belle9, amesema suala la wasanii kufungiwa nyimbo zao na BASATA kwa upande wake haoni kama kuna lingie kubwa zaidi ya kiki tu.

Akizungumza na Dizzim Online Belle9 Amesema mwanzoni alichukulia jambo hilo kuwa kubwa sana lakini kwasasa anaona ni KIKI.

Je unakubaliana na Belle 9 au Unampinga?
Viewing all 104414 articles
Browse latest View live




Latest Images