Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104756 articles
Browse latest View live

Tangaza Biashara Yako Hapa Uweze Kupata Wateja wa Haraka

$
0
0
Mtu wangu wa nguvu unaweza Tangaza Biashara yako hapa nasi uweze kuwafikia watu wengi zaidi kwa mara moja kupitia blog ya Udaku Special..

Piga simu 0714604974


Je Unasumbuliwa na Uzito wa Mwili na Unahitaji Kupungua Bila Madhara?

$
0
0

Kama ilivyo katika shughuli nyingine za kibinadamu zenye mpangilio maalum, kupunguza uzito uliozidi lazima uende sambamba na do’s na dont’s zake yaani fanywa na siofanywa. Fanywa/do’s

Jitambue na kubali kwamba unaugua unene na ili kujitibu ni lazima kuwa na adabu katika matibabu hayo. Tambua kwamba vyakula vyoote ni vizuri ILA kula vilivyo rafiki na salama kwa zoezi lako la kupunguza uzito. Tambua kiwango cha chakula unachokihitaji na ule kwa usahihi Tambua muda sahihi unaotakiwa kula na ule kwa wakati

MUHIMU(DONT’S/VISIVYOFANYWA)

Unapopunguza uzito ni kuwa unapunguza mafuta na tindikali ya ziada vilivyorundikana mwilini mwako kwahiyo ni lazima kula milo sahihi inayokuepusha kuongeza mafuta zaidi lakini pia kutouongezea mwili vyakula vyenye kuutengenezea asidi au tindikali nyingi. Hivyo ni vyema kuzingatia kiasi cha chakula kwasababu kuwa mnene unamaanisha unanguvu mwili nyingi usizozihitaji zimejirundika mwilini na mwili umezigeuza mafuta ndio hayo manyama uzembe.

Unatakiwa kupangilia ulaji ili uruhusu mwili kusaga kidogo ulichokula, lakini nguvu nyingine (kalori au calories) uzipate kutoka kwenye mafuta yaleee manyama uzembe. Kana utakula kwa kiwango kikubwa, mwili utakitumia hicho ulichokula tu na kama kitakuwa kingi kuliko kinachohitajika, kitageuzwa mafuta na kuongeza manyama uzembe.

Ni lazima kula kwa muda maalum kwa sababu tunakula ili mwili upate nguvu ya kujiendesha baada ya kukisaga chakula hicho. Ikiwa utakula chakula kingi na kutulia au kulala muda mfupi baadae, unajiumiza kwasababu mwili unapo’relax hauhitaji nguvu nyingi kwahiyo utakigeuza chakula hicho mafuta na hapo tunamaanisha tunapata tena nyongeza ya manyama uzembe. KWAHIYO? Tujitahidi kula milo sahihi, kwa wakati sahihi na kiwango sawia.

KWANINI UNAHITAJI BIDHAA ZETU?

Bidhaa zetu zinavirutubishwa vyoote muhimu vinavyozingatia mlo sahihi, muda muafaka na kiwango sawia. Zaidi huwezi kuzilinganisha bidhaa zetu na hizo nyingine za kichina unazozisikia huko mitaani kwasababu:-

Za kwetu hazina kemikali kwahiyo hizi sio “weka mbali na watoto” maana ni salama kwa watu wote katika familia hata wa kundi dhaifu la watoto, wazee, wajawazito na wanaonyonyesha. Zimethibitishwa na zimeruhusiwa kuwa salama na shirika la viwango duniani ISO, zinatambuliwa kuwa zinafaa kwa dini zote na kupewa ubora wa viwango na HALAL, na hapa kwetu vina kibali cha TFDA.

Sio zile zinazoingizwa kimyakimya kwenye mabegi hatimaye zinawaumiza na kuwatia ubovu na madhara ya kudumu ya miili. Bidhaa zetu huingizwa bila kificho na zinalipiwa kodi zote na zina vibali.

Wa Dar es salaam unaweza kufika ofisini Masaki, au ukituma pesa kabla ya saa 8 mchana utaletewa ulipo. Wateja wa mikoani unatuma pesa kabla ya saa kumi unatumiwa mzigo kwenye basi utakayoelekeza wewe, na wa Zanzibar unatumiwa kwenye boti zenye uhakika, wa nje ya Tanzania tunajadiliana juu courier unayoiamini.



Nipo active muda na saa yoyote kukuhudumia, karibu.

Piga au WhatsApp +255783566844

Instagram
@afyayanguutajiriwangu_ayuw

Facebook: Kwambiwa Nelly Machenje


Youtube : afyayanguutajiriwangu

Kuchukua Mwanamke Malaya ni Uhalifu Dhidi ya Ubinadamu

$
0
0

Papa Francis ameutaja unyanyasaji wa wanawake kwa ajili ya ukahaba kuwa ni uhalifu dhidi ya ubinadamu

Papa aliiomba msamaha jamii kwa niaba ya wanaume waumini wa kanisa Katoliki wanaokwenda kupata huduma kwa makahaba

Papa Francis alitoa kauli yake hiyo ya dhati kabisa katika kikao cha maswali na majibu na vijana kutoka mataifa mbalimbali ya dunia waliokwenda mjini Roma

Papa alisema, "Ni uhalifu dhidi ya ubinadamu. Na unatokana na fikra mbovu kwamba wanawake lazima wadhalilishwe"

Papa Francis alisema nchini Italia kuna uwezekano asilimia takriban 90 ya wateja wanaume wanaokwenda kwa makahaba ni waumini wa kanisa Katoliki waliobatizwa

Abdul Nondo Apandishwa Mahakamani kwa Makosa Haya.... Arudishwa Rumande Baada ya Kunyimwa Dhamana

$
0
0
Abdul Nondo Apandishwa Mahakamani kwa Makosa Haya.... Arudishwa Rumande Baada ya Kunyimwa Dhamana
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo amesomewa mashtaka mawili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Iringa.

Kwa mujibu wa mtandao wa gazeti la Mwananchi umesema, makosa hayo ambayo Nondo ameshtakiwa ni pamoja na kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni March 7 ya mwaka huu kuwa yupo maisha yake yapo hatarini akiwa katika eneo la Ubungo na kuzisambaza kwenye mtandao wa Whatsapp.

Kosa la pili limetajwa kuwa ni kutoa taarifa za uongo kwa mtumishi wa umma Mafinga wakati alipokuwa akitoa taarifa katika kituo cha polisi mjini humo kwa kusema kuwa alitekwa na watu wasiojulikana.

Waziri Mwakyembe: Si Busara kwa Diamond Kushindana na Serikali

$
0
0
Waziri Mwakyembe: Si Busara kwa Diamond Kushindana na Serikali
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo DKt. Harrison Mwakyembe amesema si busara kwa Diamond kushindana na serikali endapo ana ushauri wowote ni vema akauwasilisha kwa njia sahihi na si kumshambulia Naibu Waziri kwa dharua na kejeli.

Mahakama Kuu Iimetoa Amri kwa Serikali Kupeleka Majibu Juu ya Abdul Nondo

$
0
0
Mahakama Kuu Iimetoa Amri kwa Serikali Kupeleka Majibu Juu ya Abdul Nondo
Mahakama Kuu leo imetoa amri kwa serikali kuweza kupeleka majibu ya maombi yaliyofunguliwa na Mawakili wa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi nchini Abdul Nondo kujibu kesi ya kutompeleka Mahakamani kwa zaidi ya siku 10 tangu kukamatwa kwake.


Amri hiyo imetolewa leo Jumatano ya Machi 21 ambapo Mahakama kuu mbele ya Jaji Sameji  iliwataka DCI,IGP na AG kufika mahakamani kwa ajili ya kujibu mashtka juu ya Nondo ambapo leo majibu ya maombi hayo wyametakiwa yapelekwe Machi  26 na walalamikaji  kupeleka majibu yao ya nyongeza yapelekwe Machi 27.

Aidha  mahakama inatarajiwa kusikiliza maombi ya pande zote mbili 04/08/18 kutoa hatma ya Abdu Nondo.

Kwa upande mwengine kesi ya mwanafunzi huyo (Nondo)  iliyosikilizwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa imeahirishwa mpaka Jumatatu ya tarehe 26 March 2018 ambapo Hakimu atatoa uamuzi kwamba mshitakiwa apewe dhamana ama asipewe dhamana, mshitakiwa amerudishwa rumande.


Polisi Wafunguka Kuhusu Tukio la Afisa Ubalozi wa Syria Kushambuliwa

$
0
0
Polisi Wafunguka Kuhusu Tukio la Afisa Ubalozi wa Syria Kushambuliwa
Leo March 21, 2018 Kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa kipolisi wa Kinondoni Jumanne Murilo amezungumza na waandishi wa habari katika ofisi zake kuhusu kushambuliwa kwa Afisa wa ubalozi wa Syria nchini H. Alfaori na kuibiwa Euro 93,000 sawa na Shilingi Milioni 251 za Kita March 20, 2018.

“Tukio la unyanganyi kwa kutumia nondo lililofanyika kwa mhasibu wa ubalozi wa Syria, akiwa anatoka kwenye ubalozi huo akiwa na dereva ambae tunamtafuta, dereva huyo aliacha kupita njia ya kuelekea mjini huku akiendesha gari polepole sana,” -RPC KINONDONI

“Mhasibu alivamiwa na watu watatu ambao wanatuhumiwa kuwa ni majambazi, walimjeruhi kwa kipande cha nondo kichwani, wahalifu wakaondoka na dereva pamoja na gari ya ubalozi,” -RPC KINONDONI

Hukumu ya Papii Kocha na Babu Seya Kusomwa Arusha

$
0
0
Hukumu ya Papii Kocha na Babu Seya Kusomwa Arusha
Mahakama ya Afrika ya watu na haki za binadamu yenye makao yake makuu jijini Arusha, leo inatarajia kutoa hukumu ya kesi ya mwanamuziki nguli nchini, Nguza Viking na mwanawe Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ waliyokuwa wameifungua katika mahakama hiyo dhidi ya serikali.


Nguza na mwanawe walifikisha malalamiko yao mbele ya mahakama hiyo wakidai kunyimwa haki za msingi katika mahakama za Tanzania na kuomba mahakama hiyo ya Afrika kuamuru kuachiliwa. Juni 2004, Nguza na mwanawe Johnson walitiwa hatiani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kuhukumiwa kufungwa jela maisha, baada ya kukutwa na hatia ya kunajisi na kulawiti watoto wadogo 10 .

Wasanii hao kwa sasa wako uraiani baada ya kutoka kwa msamaha wa Rais John Magufuli, Desemba mwaka jana. Katika maombi yao waliyowasilisha katika Mahakama ya Afrika, walalamikaji waliiomba mahakama hiyo kutoa uamuzi kwamba haki zao zilivunjwa na hivyo waachiwe huru na kulipwa fidia.

Walidai katika hati yao ya maombi mbele ya Mahakama ya Afrika kuwa walipokamatwa mara ya kwanza hawakupewa haki ya kuelezwa sababu za kukamatwa kwao, kinyume na mkataba wa haki za binadamu kifungu namba 1,2,3,5,7(1)b),13 na 18 ambapo baada ya kukamatwa waliwekwa kizuizini bila ya kuwasiliana na mwanasheria wao au mtu mwingine yeyote.

Pia walilalamika wakiwa ndani ya mahabusu, Polisi waliwatesa kinyume na haki za binadamu na baada ya kushikiliwa kwa siku nne ndio walielezwa kuwa walikamatwa kwa makosa ya kunajisi na kulawiti, jambo ambalo walilikana.

Aidha walidai kuwa mahakama haikuwatendea haki ikiwemo kutupilia mbali maombi ya kuwasilisha ushahidi wa vipimo vya damu na mkojo katika utetezi wao dhidi ya kesi hiyo iliyokuwa ikiwakabili.

Pia walidai wanaodai kuambukizwa virusi vya Ukimwi (HIV) na kisonono walidanganya mahakama kwa kuwa mdaiwa wa kwanza alikuwa hanithi na aliomba kupimwa hali yake ya uhanithi na kwamba hawezi kufanya vitendo vya ngono lakini maombi yake yalitupiliwa mbali na mahakama.

Walidai pia kuwa mahakama iliyowahukumu haikuzingatia kuwa wazazi wa watoto waliodaiwa kunajisiwa na kulawitiwa walikuwa wakifahamu nyumba waliyokuwa wakiishi na walikuwa wakitembelea eneo hilo mara kwa mara hivyo kujua chumba walichokuwa wakiishi.

Kwa mujibu wa Nguza na mwanawe ushahidi uliokuwa ukitolewa haukuwa wa haki, ikiwemo hata mashtaka yao yaliyowasilishwa mahakamani hapo yalikosea tarehe ya siku tuhuma za makosa yalipodaiwa kufanyw,a jambo ambalo walishindwa kuandaa ushahidi.

Serikali Yawaruhusu Wazazi Kumpa Mtoto Bangi Kama Tiba

$
0
0
 Serikali Yawaruhusu Wazazi Kumpa Mtoto Bangi Kama Tiba
Wazazi wa mtoto mwenye umri wa miaka 6,Alfie Dingley aliye na ugonjwa wa kifafa ambao wamekuwa wakipiga kampeni ili mtoto wao aruhusiwe kutumia mafuta ya Bangi kupunguza matatizo ya kifafa, wamesema sasa serikali ya Uingereza imekubali kuwapa ruhusa ya kutumia bangi hiyo kama tiba.

Wakiongea baada ya mkutano na Waziri Mkuu Theresa May, Drew Dingley na Hannah Deacon walisema wamefahamishwa kuwa kijana wao Alfie anaweza kuruhusiwa kutumia mafuta yatokanayo na mmea Bangi kwa makubaliano maalumu ingawa matumizi ya Bangi ni kinyume cha sheria nchini Uingereza.

Alfie Dingley huanguka kifafa hata mara mia moja na zaidi kila mwezi lakini hali hiyo inaweza kupungua ikiwa atapewa matone matatu ya bangi kwenye ulimi kila siku.

Mama mzazi wa mtoto huyo ameelezea tabu anazozipata, jaziba na hasira ambazo mtoto huyo anamfanyia kutokana na matatizo ya maradhi yake ya kifafa.Ameongeza kuwa watu 380,00 wanaunga ombi hilo na wamewapigia simu familia yao wakidai kuwa wanaridhia wapewe leseni kwaajili ya Alfie Dingley kutumia bangi kwa matibabu.

Hannah Deacon amesema kuwa wamekuwa wakiletewa misokoto mingi ya bangi,watu wakisema wanaelewa tatizo la mtoto.

Hivyo najua wenye mamlaka hawaonji mateso ya maisha ninayo ishi,na wala hawaishi maisha na shida mwanangu,naomba waweke wazi jambo hili.

Muigizaji Sir Patrick Stewart amemwambia mwandishi wa gazeti la Daily Politics Greg Dawson kwamba kwanini anaunga mkono kampeni hiyo.

Muda umefika, Futeni Facebook’ Mmiliki Mwenza Whatsapp

$
0
0

Mwanzilishi na Mkurugenzi wa mtandao wa Facebook Mark Zuckerberg jana March 20, 2018 alipokea barua rasmi ya kuitwa kwenye Kamati ya Bunge la Uingereza ili kutoa ushahidi kuhusiana na kampuni yake kuhusishwa na kuweka ushawishi kwenye Uchaguzi wa Urais Marekani, kinyume na sheria.

Sasa leo March 21, 2018 Mwanzilishi Mwenza wa mtandao wa WhatApp Brian Acton amewaambia watumiaji wa Facebook waifute App hiyo na waache kuitumia, jambo ambalo limesababisha hisia tofauti kwa watu mbalimbali.

Acton ametumia mtandao wake wa Twitter kuandika ujumbe unaosema ‘Muda umefika, futeni Facebook’ jambo ambalo baadhi wa watu wamesema ni ‘usaliti wa kibiashara’ kwani Facebook ndiye aliyeinunua WhatsApp na kumtajirisha Acton na Mwanzilishi mwenzie.

Tweet hiyo ya Acton imesababisha kusambaa kwa hashtag ya ‘Futa Facebook’ jambo ambalo linaelezwa kuharibia kampuni hiyo ambayo hadi sasa ina watumiaji zaidi ya milioni 50 duniani kote.

Facebook inatuhumiwa kuruhusu kampuni ya Cambridge Analytica ya nchini Uingereza kutumia taarifa za wanachama wa Facebook Milioni 50 bila ruhusa yao ili kuweka ushawishi katika Uchaguzi Mkuu wa Urais nchini Marekani uliofanyika mwaka 2016 na ili kumpa ushindi Donald Trump.

Roma Afunguka Mambo Haya Baada ya Kufungiwa na Basata

$
0
0
Roma Afunguka Kuhusu Kufungiwa na Basata
Msanii wa Hip Hop Roma Mkatoliki ni miongoni mwa mastaa waliotajwa na Naibu Waziri wa sanaa, Utamaduni na Michezo Juliana Shonza  kufungiwa kwa nyimbo zao  na kupewa onyo kali ila kwa upande wa Roma alifungiwa miezi sita.

Lakini Leo March 21,2018 nakusogezea mambo matano aliyoyazungumza Roma Mkatoliki katika interview aliyofanya na XXL ya Clouds Fm.

…….>>>“Mwaka jana nilipata ujumbe kutoka BASATA na ulikuja kwa njia ya sms kuhusu wimbo wa Kibamia nikaitikia wito uliyotolewa ila utata ulikuwepo kwenye ujumbe uliyopo kwenye wimbo huo”

….>>>”Nilipokea tamko la kufungiwa katika muziki ila wakati muda haujaisha mke wangu alikuwa anakaribia kujifungua na mambo mengine mengi”

….>>>”Nimeshangazwa kufungiwa kutokana na wimbo wa Kibamia na wimbo huo umejadiliwa kama wimbo wa Roma pekee wakati ni wa kundi la ROSTAM”

…..>>>”Mimi, Madee na Askofu tulienda ofisini kumuona Naibu Waziri wenzangu walimuona lakini mimi sikufanikiwa wenzangu waliitwa pekee yao, mimi nikaambiwa sina ruhusa ya kwenda kuingia ndani, ningefanyaje?”

….>>>”Hapo kati kulikuwa na upepo mzuri wa ROSTAM kwahiyo tulikuwa tushalipwa pesa kwaajili ya show nyingi za miezi ijayo sasa hivi tunapigiwa simu turudishe pesa za watu lakini pia nimefanya jitihada kutafuta viongozi wa BASATA na Wizara ili kupata muafaka wa jambo hili lakini bado sijafanikiwa”

Kimenuka! Bob Juniour Asakea na Polisi Kisa Hiki Hapa

$
0
0
Kimenuka! Bob Juniour Asakea na Polisi Kisa Hiki Hapa
Story kubwa inayosambaa katika mitandao ya kijamii ni kuhusu mmiliki wa Sharobaro records na staa mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva Bob Juniour ambaye kumekuwa na tetesi kuwa anatafutwa na polisi kwa kosa la kumpiga aliyekuwa mpenzi wake na muigizaji wa Bongo movie Sabrina au maarufu kama Sabby Angel.



Sabrina amefanya interview na mtangazaji Soudy Brown wa Clouds Fm katika kipindi  cha U Heard na amesema kuwa Bob Junior amempiga kutokana na yeye kumwambia waachane kwasababu haoni maisha yakiendelea kati yao na amekuwa akilazimisha mapenzi.

Sabrina amesema…...>>>“Kweli kuna matatizo yametokea, unajua mtu huwezi kulazimisha mapenzi nikikwambia it’s over its over lakini yeye anaforce mapenzi, ananipiga mambo ya zamani kwanza siku hizi mwanamke hapigwi unanipiga umenitolea mahari?

“Nimeona hana future nikaamua kumuacha lakini mtu hataki kuelewa anakuja ananipiga mi naona kama naonewa”

Sabrina na Bob Junior inasemekana kuwa wamekuwa katika uhusiano wa kimapenzi kwa zaidi ya miaka nane hata kabla ya Bob Junior kufunga ndoa na aliyekuwa mke wake Halima.

Uporaji wa Pesa za Ubalozi wa Syria Ulipangwa Njama – Kamanda Muliro

$
0
0
Uporaji wa Pesa za Ubalozi wa Syria Ulipangwa Njama – Kamanda Muliro
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni linamshikilia mfanyakazi wa ubalozi wa Syria nchini kwa tuhuma za kumjeruhi usoni mhasibu wa ubalozi huo, Hassan Alfaouri na kumpora Euro 93,000 (Sh237milioni).


Akiongea Jumatano hii, kamanda wa polisi mkoani humo, Jumanne Muliro amesema tukio hilo lilitokea Machi 19, 2018 saa nane mchana eneo la Shule ya Msingi Oysterbay, jijini Dar es Salaam.

Amesema siku hiyo, mhasibu huyo akiwa katika gari na dereva wake wakielekea Benki ya Azania tawi la Mazdu House lililopo mtaa wa Samora wakipeleka fedha hizo, walipofika mtaa wa Zambia dereva huyo alianza kuendesha gari taratibu.

Amesema baada ya kupunguza mwendo, alisimama na kuzima gari ghafla walitokea watu watatu; mmoja kati yao alikuwa na kipande cha nondo mkononi na kuingia katika gari hilo na kumtaka mhasibu huyo awape fedha.

Muliro amebainisha kuwa uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa tukio hilo lilipangwa na baadhi ya wafanyakazi wa ubalozi wasio waaminifu, akiwamo dereva huyo ambaye wakati uporaji ukiendelea, hakutoa msaada wowote.

“Walivyoona anakawia kutoa fedha walimjeruhi usoni kwa kipande cha nondo, walimshusha dereva kwa nguvu na kuondoka na gari hilo,” amesema.

Amesema baada ya tukio hilo, polisi walianza msako na kuikuta gari hiyo ikiwa imetelekezwa Msasani Bonde la Mpunga.

Necta Yafanya Mabadiliko Mtihani Darasa la Saba

$
0
0
Wanafunzi wa darasa la saba ambao watafanya mtihani mwaka huu watakutana na mabadiliko ya mfumo wa utungaji  wa mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi .

Mabadiliko hayo yamefanywa na Baraza la Mitihani la Taifa  (Necta) jana na kutangazwa na Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Dk Charles Msonde.

Ofisa Habari wa Necta, John Nchimbi amesema mabadiliko hayo aliyatangaza Dk Msonde katika mkutano mkuu wa tano wa maofisa elimu mkoa na wilaya unaofanyika Dodoma.

Nchimbi amesema katika muundo huo mpya kila somo litakuwa na maswali 45, kati ya hayo, maswali 40 yatakuwa ya kuchagua jibu sahihi na matano yasiyo ya kuchagua (yatakuwa ya kujieleza/kuonyesha njia na jibu nk).

Amesema maswali 40 kila swali litakuwa na alama moja na maswali matano kila swali litakuwa na alama mbili huku majibu ya maswali 40 yatajibiwa kwenye OMR FORM na maswali matano yatajibiwa kwenye karatasi maalum itakayoandaliwa.

Kutokana na muundo huo mpya, Necta imetoa wito kwa walimu wakuu kuanza kuwapima wanafunzi kwa kutumia mabadiliko hayo ili kuwajengea uzoefu.

Makamu wa Rais Ampa Agizo Hili IGP Sirro

$
0
0
Makamu wa Rais Ampa Agizo Hili IGP Sirro
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro kuwachukulia hatua mara moja askari polisi ambao wamekiuka maadili na taratibu za jeshi hilo katika mkoa wa Kusini Pemba.

Makamu wa Rais ameyasema hayo, wakati wa kuwekwa kwa jiwe la msingi wa ujenzi wa nyumba 36 za askari polisi katika eneo la Mfikiwe, wilaya ya Chake Chake mkoa wa Kusini Pemba.

Makamu wa Rais alitoa pongezi kwa Jeshi la Polisi nchini kwa kuhakikisha nchi inakuwa tulivu na yenye amani pia alitoa pongezi kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Hamad Masauni kwa kusimamia vyema zoezi la ujengaji nyumba za Polisi.

Makamu wa Rais pia alitoa pongezi kwa kampuni ya Twiga Cement kwa kutoa Saruji mifuko zaidi ya elfu sita pamoja na kampuni za Shubash Patel kwa kuchangia vifaavingine vya ujenzi.

Awali Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Nchini, Mhandisi Hamad Masauni alipongeza Jeshi la Polisi kwa kupambana na biashara haramu ya madawa ya kulevya na kusema yeyote atakayevunja sheria achukuliwe hatua bila kujali wadhifa au umaarufu wake.


Sakata la Daimond Kumjibu Waziri Shonza Lazidi Kufika Pabaya TCRA Yamjia Juu" Atambue Serikali Inataratibu Zake"

$
0
0

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kamati yake ya maudhui inafuatilia mahojiano ya mwanamuziki Nasseb Abdul maarufu Diamond aliyoyafanya katika kituo cha Redio cha Times jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na MCL Digital leo Jumatano Machi 21, 2018 Ofisa Mkuu Idara ya Utangazaji ya mamlaka hiyo, Andrew Kisaka amesema wamechukua uamuzi huo kwa kuwa mahojiano hayo yamefanyika katika kituo wanachokisimamia.

Katika mahojiano hayo, Diamond alimjibu Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza kutokana na Serikali kuzifungia nyimbo 15 mwezi uliopita, zikiwemo mbili za mwanamuziki huyo.

Kisaka amefafanua kuwa kiutaratibu wao wanaangalia zaidi chombo ambacho wamekipa leseni na kwamba, masuala mengine yatashughulikiwa na mamlaka nyingine.

Amesema suala hilo kwa sasa linafanyiwa kazi na kamati ya maudhui na kuahidi kulitolea ufafanuzi siku za hivi karibuni akiwataka wananchi kuwa na subira.

Wakati TCRA ikisema hivyo, Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amesema amesikitishwa na matamshi ya Diamond kuhusu kufungiwa kwa nyimbo hizo aliyoyatoa katika kipindi hicho.

“Maamuzi ya kuzifungia baadhi ya nyimbo za wasanii wawili kwa kukiuka maadili yalifanywa kwa mujibu wa sheria na si kwa utashi binafsi wa Shonza ambaye analaumiwa na Diamond,” amesema.

“Diamond atambue kuwa Serikali ina taratibu zake na maamuzi ya naibu waziri ni ya wizara. Kama vikao na wasanii tumefanya vingi sana, lakini Diamond hakuwahi kuhudhuria vikao hivyo, si wajibu wa Serikali kumfanyia kikao cha peke yake.”

Amesisitiza, “Sheria ni ya watu wote bila kujali umaarufu au nafasi ya mtu katika jamii, hivyo msanii Diamond anapaswa kutii sheria na mamlaka zilizowekwa.”

Dk Mwakyembe ameeleza kuwa sio busara kwa Diamond  kushindana na Serikali na endapo ana ushauri wowote ni vyema akawasilisha kwa njia sahihi, lakini si kumshambulia naibu waziri kwa dharau na kejeli kama alivyofanya.

“Diamond kwa mafanikio aliyoyapata katika muziki, anatarajiwa kuwa mfano bora kwa wanamuziki wenzake. Napenda kuwakumbusha wasanii wote kwamba sanaa ni kazi kama zilivyo kazi nyingine,” amesema.

“Pamoja na kuwa na kipaji hicho, wasanii wanatakiwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo inayosimamia tasnia ya sanaa kama ilivyo kwa tasnia nyingine.”

Khadija Khopa Achoka Kuwa Singo Ataka Mwanaume wa Kumuoa "Nataka Mume Sipendi Dhambi"

$
0
0
Khadija Khopa Achoka Kuwa Singo Ataka Mwanaume wa Kumuoa "Nataka Mume Sipendi Dhambi"Malkia wa Mipasho nchini Tanzania asiyekuwa na mshindani, Khadija Kopa ametangaza rasmi kuhitaji mume wa kumuoa ili aweze kuishi naye huku akiweka vigezo vyake kuwa hataki aliyechini ya miaka 40 kwa madai hawezi kufundisha tution.


Khadija Kopa ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa mubashara kupitia kurasa za EATV kila siku ya Jumatano kuanzia saa 8:00 mchana hadi 10:00 alasiri.

"Sijaolewa ila sitaki kusomesha tuition, nataka mwanaume aliyekuwa na umri mkubwa kuanzia 40 kwenda juu, mwenye mapenzi ya dhati na huba, mwenye kujali na kujua ninataka nini, atakayeweza kuijali familia yangu pamoja na watoto wangu, awe mnene kidogo na sio mwembamba, awe na rangi yeyote na kabila lolote lile kwasababu mimi sina ubaguzi katika vitu hivyo", amesema Khadija Kopa.

Pamoja na hayo, Khadija Kopa ameendelea kwa kusema "napenda mwanaume mfanyakazi maana kupata pesa ni majaliwa ila asiwe mwanaume wa kulala nyumbani akanitegemea mimi nikafanye kazi ili yeye aje kula maana maisha ni kusaidia nasio kuegemea upande mmoja tena wa mwanamke".

Aidha, Khadija Kopa amesema sababu kubwa iliyompelekea mpaka sasa kutoolewa ndoa nyingine baada ya aliyekuwa mume wake kufariki ni kutokana na kuwa na wasiwasi na wanaume wa sasa.

"Nina wasiwasi kwa mwanaume atakayekuja kunioa kwa sasa, maana najiuliza mengi je atakuwa na huba kama marehemu mume wangu ndio maana mpaka sasa sijaolewa kwa kuwa nafikiria sana. Mume wangu aliyefariki alikuwa ni mwenye huba, mwenye kunijali, nimekaa naye miaka yote sijawahi kugombana naye, nilikuwa natamani kumuona akinuna ananuna vipi, alikuwa na vigezo vyote", amesisitiza Khadija Kopa.

Maboresho Katika Application ya Udaku Special.... Download Upya Kwenye Simu yako Kupata Habari Zetu Haraka

$
0
0
Kuna Maboresho Mapya Yamefanyika Hatika Application Yetu ya UDAKU SPECIAL. Maboresho hayo yamelenga kukufanya upate habari zetu kwa wepesi zaidi kama vile Magazeti kuliko ilivyo sasa.

Chakufanya, Ingia PlayStore, Download Upya Application yetu

Tumekurahisishia;

==>>Unaweza Kuidownload << kwa Kubofya Hapa>> 

Huyu Ndio Mchumba wa Nikki wa Pili Ambaye Amedai Hapaki Make Up

$
0
0

Msanii kutoka kampuni ya Weusi, Nikki wa Pili amesema uzuri wa msichana au mwanamke unatoka na asili yake aliyozaliwa nayo na wala haitokani na vitu vya kujiremba na kudai haitokuja kutokea mke wake kuonekana amejiremba kwa kuwa anataka awe 'natural'

Nikki wa Pili ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya kupita siku kadhaa tokea msanii mwenzake Dogo Janja ku-comment katika ukurasa wake kwa kumwambia vitu 'natural' aviachie misitu na kumtaka aache ubahili wake amtunze mke wake wa kumrembesha na urembo.

"Sisi binadamu wenye ni wazuri kwasababu ni asili kwahiyo hakuna uzuri wowote duniani unaoweza kuzidi asili. Ninachoamini mimi ni kwamba uzuri wa msichana upo katika asili yangu", amesema Nikki wa Pili

Pamoja na hayo, Nikki wa Pili ameendelea kwa kusema "mimi ni mtu creative kwa hiyo siamini kwenye 'material' ninaamini kwenye nguvu ya ubunifu, kwenye kazi yangu naekeza kwenye ubunifu so labda watu wanatafsiri hivyo lakini ubunifu unanguvu mara elfu. Mimi napenda asili kwa hiyo sitegemei kumuona mpenzi wangu akiwa amejipaka make-up"

Jay-Z na Beyoncé wakiwa kwenye boda boda uswahilini

$
0
0
Kama ni mfuatiliaji wa wasanii wawili wa muziki kutoka nchini Marekani, Beyonce na Jay Z kuanzia jana kwenye mitandao ya kijamii kumekuwa na picha za mastaa hao zikisambaa kwa kasi zikiwaonesha wakiwa kwenye boda boda katika maeneo ya uswahilini.


 Watu wengi mwanzoni walidhani ni picha za kutengenezwa kutokana na hadhi ya wasanii hao, lakini ukweli ni kwamba picha hizo ni zao na ni za kweli.


Kwa mujibu wa mtandao wa Daily Mail umeeleza kuwa picha hizo za wawili hao wamepiga nchini Jamaica kwenye utengenezaji wa scene ya ziara yao ya kimuziki ya OTR II.

Kwa upande mwingine, mbali ya kutangaza tour yao ya pamoja kwa mara ya pili kuna tetesi kuwa wawili hao huenda wakaachia albamu ya pamoja siku za usoni.

Ziara hiyo ya On The Run II (OTR II) itaanzia katika mji wa Cardiff nchini Uingereza ifikapo Juni 6, 2018 na kumalizika Oktoba 2, mwaka huu katika mji wa Vancouver, nchini Canada ambapo itazunguuka zaidi ya miji 35 duniani.
Viewing all 104756 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>