Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104781 articles
Browse latest View live

Khadija Kopa Afunguka Kuhusu Mahusiano na Kibeniten

$
0
0
Khadija Kopa Afunguka Kuhusu Mahusiano na KibenitenMsanii wa muziki wa taarab nchini, Khadija Kopa amesema moja ya vitu ambavyo havipendi ni kuwa katika mahusiano na mtu mdogo kwake kiumri.

Muimbaji huyo ameiambia Kikaangoni, EATVkuwa licha kutopenda jambo hilo lakini isiwe sababu ya kuwasema vibaya wanawake waliyo katika aina hiyo ya mahusiano.

“Mbona nyinyi wanaume wazee mnaoa wanawake wadogo na sisi hatusemi, sisi kila siku vibenteni vibenteni. Babu wee, mimi sipendi viben ten, mimi nilikuwa na mume wangu, na hata ikiwa dini yetu inaruhusu Mtume wetu alituonyesha njia,” Khadija Kopa.

Katika hatua nyingine Khadija Kopa ameongeza kuwa baada ya mume wake kufariki kipindi kirefu, yeye yupo tayari kuolewa ila na mtu mwenye umri wa kuanzia miaka 40 ila asizidi sana.

Rais Magufuli Amemualika Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu

$
0
0
Rais Magufuli Amemualika Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu
Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemualika Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu kutembelea Tanzania pamoja na kufungua ofisi ya ubalozi wa nchi hiyo hapa nchini. Taarifa ya Ikulu imeeleza.

Mayweather Kuinunua Timu ya Newcastle na Kumsajili Ronaldo

$
0
0
Mwanamasumbwi mwenye sifa, mikogo na majivuno makubwa nchini Marekani, Floyd Mayweather amekuja na jipya wiki hii baada ya kudai anaweza kuinunua klabu ya Newcastle United ambayo ipo sokoni kwa sasa na kumshawishi mchezaji bora wa dunia na mshindi mara tano wa tuzo ya Ballon d’Or, Cristiano Ronaldo kumalizia soka lake lakulipwa ndani ya timu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza.

Mayweather ambaye ni bondia machachari awapo ndani na nje ya ulingo na anayetamba zaidi kuwa na fedha za kutosha amesema kuwa anafikiria kufanya uwekezaji katika soka.

Klabu ya Newcastle imekuwa kwenye harakati za kupata mmiliki mpya baada ya Mike Ashley kusemekana kuvunja mazungumzo kati yake na Amanda Staveley ya kuinunua timu hiyo.

Ni vyema ukaamini kuwa ningeweza kuwekeza, ningekuwa na kwenda mara kwa mara bondia huyo amekieleza chombo cha habari cha the Star siku ya Jumapili.

Nimekutana na baadhi ya wachezaji wa Newcastle mwaka jana, niwatu wema. Siku zote naanzisha nafasi za biashara na napenda michezo yote lakini nawekeza kutokana na kichwa changu kinavyonituma na siyo kutoka moyoni.

Kuwekeza kutoka ndani ya moyo ni rahisi kupata hasara lakini mtu akijitokeza na kushirikiana katika mipango ya kibiashara ni rahisi kutengeneza fedha, hivyo ningependa kuwekeza katika soka hatakama siyo mchezo wangu kwakuwa nina watu kila sehemu.

Ebitoke Afunguka Kuhusu Kutoka Kimapenzi na Mume wa Mamaa Ashura

$
0
0
Ebitoke Afunguka Kuhusu Kutoka Kimapenzi na Mume wa Mamaa Ashura
Mchekeshaji kutoka kundi la Timamu, Ebitoke amejibu tuhuma kuwa amekuwa akitoka kimapenzi na mume wa Mamaa Ashura.

Muigizaji huyo amesema kuwa tuhuma hizo hazina ukweli wowote ni stori tu za kupikwa.

“Kwa wale wanaosema mimi nimempindua si kweli wakati yupo tumemficha sehemu, tutamleta,” Ebitoke ameiambia Bongo5.

“Mama Ashura yupo na anaendelea na mambo mengine, atarudi kama mwanzo na wataendelea kumuona ila sasa hivi hayupo kidogo, kuna mambo ambayo anayafanya,” ameongeza.

Hapo awali kulikuwa na taarifa kuwa baada ya Ebitoke kuanza kutoka kimapenzi na mume wa Mamaa Ashura ndipo kumepelekea muigizaji huyo kutoonekana tena katika kundi hilo.

Mnyika, Heche Wang'ang'aniwa Polisi Wengine Waachiwa kwa Dhamana

$
0
0
Mnyika, Heche Wang'ang'aniwa Polisi Wengine Waachiwa kwa Dhamana
Viongozi watatu waandamizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) walioripoti Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam leo, ambao ni ni Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar), Salum Mwalimu na Dk Mashinji, wameachiwa kwa dhamana huku Naibu Katibu Mkuu (Bara), John Mnyika na Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Serengeti, John Heche wakibaki polisi kwa maelezo kuwa wamekuwa wakikwepa taratibu za dhamana.

Imeelezwa kuwa, Heche na Mnyika hawakuripoti polisi Machi 16, 2018 ambapo Chadema wamesema sababu ya wabunge hao kutoripoti ni kutokana na kuhudhuria vikao vya kamati za Bunge mjini Dodoma.

Aidha, viongozi wengine wa chama hicho waliotakiwa kuripoti polisi leo Machi 22, ni Mbunge wa Kawe, Halima Mdee ambaye yupo nje ya nchi kwa matibabu na Ester Matiko ambaye yuko Dodoma kwa shughuli za kibunge.

Diamond Aiponza Times FM, TCRA Yawawataka Kuwasilisha Kipindi Chote Walichofanya Naye Mahojiano

$
0
0
Diamond Aiponza Times FM, TCRA Yawawataka Kuwasilisha Kipindi Chote Walichofanya Naye Mahojiano
Kituo cha Redio Times cha jijini Dar es Salaam kimetakiwa kuwasilisha kipindi cha mahojiano waliyofanya na mwanamuziki Diamond Platinumz kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Mkurugenzi wa Times FM, Amani Misana ameieleza MCL Digital leo Machi 22, 2018 kuwa amepokea barua ya kuwataka wawasilishe kipindi hicho kilichorushwa Machi, 19, 2018 na kwamba leo wametekeleza agizo hilo.

“Tumepokea barua na tumefanya yale tuliyoagizwa ikiwamo kuwasilisha kipindi chote,” amesema kwa ufupi Misana.

Kaimu Meneja Mawasiliano wa TCRA, Semu Mwakyanjala amesema suala la kituo hicho kupewa barua ni la kiutawala zaidi na mamlaka hiyo haipo kwenye kitengo chake isipokuwa kama tayari barua imefika, wakati wa kutolewa uamuzi vyombo vya habari vitaalikwa.

Mwanamuziki Diamond alizua mjadala baada ya kuzungumzia suala la nyimbo za wasanii kufungiwa akimlalamikia Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza kutowatendea haki wasanii.

Diamond hakuishia katika mahojiano hayo yaliyoongoza na mtangazaji Omary Tambwe, Machi 20 kupitia mtandao wa Twitter alimjibu naibu waziri huyo akisema ametumia njia hizo kumjibu kwa kuwa naye alitumia hizo hizo.

Hata hivyo, jana mamlaka za Serikali ikiwamo Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) na Waziri wa wizara hiyo, Dk Harrison Mwakyembe walimshukia mwanamuziki huyo wakisema amefanya makosa kumshambulia naibu waziri kwa kuwa uamuzi anaotoa siyo wake binafsi.

Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH issa simba said Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili

$
0
0

Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH issa simba said Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Maalim Hussein Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU. Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.
Issa simba said Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
Anatibu kwa Kutumia Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA. Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI. Nguvu za KIUME, Humaliza Kesi zilishindika ndani ya siku 14 tu..na mengi zaidi

+255 622588038au 0679119679 au +255 764318107

TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE...

Mbunge Kenya Ataka Ukomo wa Umri wa Mgombea Rais Uwe Miaka 70....

$
0
0

KENYA: Mbunge apendekeza la kubadili Ibara ya 260 ya Katiba na kuweka ukomo wa umri wa kuwania urais. Wenye miaka zaidi ya 70 kutoruhusiwa

Moja ya sababu ya kuweka ukomo kwa umri wa kugombea urais ni watu walio na umri mkubwa kuwa na uzalishaji mdogo pamoja na kusumbuliwa na maradhi ya mara kwa mara

Endapo mapendekezo hayo yatapitishwa Raila Odinga(78) hatoweza kugombea katika uchaguzi wa mwaka 2022

Hata hivyo mabadiliko hayo hayatomuathiri Makamu wa Rais wa sasa, Willium Ruto anayetajwa kuwa atawania Urasi mwaka 2022

Simba SC Yamwagiwa Mamilioni na MO Dewji

$
0
0

MWANACHAMA na shabiki wa Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’ pamoja na viongozi wa timu hiyo wanapanga mipango madhubuti ya kuhakikisha wanawazidi kete wapinzani wao Yanga kwa kutwaa ub­ingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu, ambapo kwa kulifaniki­sha hilo wametenga pembeni kiasi cha Sh milioni 100.

Iko hivi, Simba na Yanga kwa sasa wote wanalingana pointi kwenye msimamo wa ligi kuu wak­iwa na 46 kila mmoja ambapo vita baina yao inaonekana kuwa kubwa kutokana na kila timu kupanga ka­rata zake vyema wakati huu ambao ligi inaenda mwishoni.

Kwa sasa Simba ambao wenyewe wanaongoza kwa tofauti ya ma­bao, wamebakiza mechi 10 pekee kabla ya kumalizika kwa ligi ambapo uongozi wa timu hiyo umepanga kuwapa milioni 10 wachezaji wake kwenye kila mchezo ambao wa­takuwa wanashinda kwa ajili ya kuongeza hamasa ya kufanikisha jambo hilo.

Katika mechi hizo 10 zilizobakia, wachezaji wa Simba watavuna milioni 100 kama watashinda mechi zote ikiwemo ya watani wao Yanga iliyopangwa kupigwa Aprili 7, mwaka huu ambapo fedha hizo milioni 5 watatoa viongozi wengine huko 5 akitoa Mo, hadi mwisho wa ligi Mo atakuwa ametoa milioni 50.

Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Simba, Haji Manara, alisema: “Huu ni mkakati wa kuongeza hamasa kwa wachezaji wetu kuipambania timu yao kutwaa ub­ingwa wa ligi kwa msimu huu baada ya kuukosa kwa misimu kadhaa nyuma.

“Kiasi hicho cha fedha kitakuwa kinatolewa na makao makuu ambao watatoa milioni 5 kwa kila mechi huku mwekezaji wetu Mo Dewji yeye katika mechi hizo naye atachangia milioni 5, hivyo ukichanganya zote hapo unapata milioni 10 kwa kila mchezo.

“Tena itakuwa mzigo unaingia muda mfupi tu baada ya kumaliza mchezo, kama ikitokea mechi ni Jumapili basi Jumatatu asubuhi hivi kila mmoja atakuwa ameingiziwa fungu lake benki, tunafanya yote haya kwa ajili ya kuonge­za hamasa kwa wache­zaji,” alisema Manara.

Naye kocha Msaidizi wa Simba, Masoud Djuma amefungukia juu ya michezo yao hiyo 10 iliyobakia am­bapo alisema: “Mechi hizi 10 zilizobakia siyo nyingi sana, kikubwa ambacho tunataki­wa kukifanya ni kuende­lea kupigana tupate pointi kwa kila mechi.”

Mo Dewji Amwaga Mamilioni Simba

$
0
0
Mo Dewji Amwaga Mamilioni Simba
MWANACHAMA na shabiki wa Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’ pamoja na viongozi wa timu hiyo wanapanga mipango madhubuti ya kuhakikisha wanawazidi kete wapinzani wao Yanga kwa kutwaa ub­ingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu, ambapo kwa kulifaniki­sha hilo wametenga pembeni kiasi cha Sh milioni 100.

Iko hivi, Simba na Yanga kwa sasa wote wanalingana pointi kwenye msimamo wa ligi kuu wak­iwa na 46 kila mmoja ambapo vita baina yao inaonekana kuwa kubwa kutokana na kila timu kupanga ka­rata zake vyema wakati huu ambao ligi inaenda mwishoni.

Kwa sasa Simba ambao wenyewe wanaongoza kwa tofauti ya ma­bao, wamebakiza mechi 10 pekee kabla ya kumalizika kwa ligi ambapo uongozi wa timu hiyo umepanga kuwapa milioni 10 wachezaji wake kwenye kila mchezo ambao wa­takuwa wanashinda kwa ajili ya kuongeza hamasa ya kufanikisha jambo hilo.

Katika mechi hizo 10 zilizobakia, wachezaji wa Simba watavuna milioni 100 kama watashinda mechi zote ikiwemo ya watani wao Yanga iliyopangwa kupigwa Aprili 7, mwaka huu ambapo fedha hizo milioni 5 watatoa viongozi wengine huko 5 akitoa Mo, hadi mwisho wa ligi Mo atakuwa ametoa milioni 50.

Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Simba, Haji Manara, alisema: “Huu ni mkakati wa kuongeza hamasa kwa wachezaji wetu kuipambania timu yao kutwaa ub­ingwa wa ligi kwa msimu huu baada ya kuukosa kwa misimu kadhaa nyuma.

“Kiasi hicho cha fedha kitakuwa kinatolewa na makao makuu ambao watatoa milioni 5 kwa kila mechi huku mwekezaji wetu Mo Dewji yeye katika mechi hizo naye atachangia milioni 5, hivyo ukichanganya zote hapo unapata milioni 10 kwa kila mchezo.

“Tena itakuwa mzigo unaingia muda mfupi tu baada ya kumaliza mchezo, kama ikitokea mechi ni Jumapili basi Jumatatu asubuhi hivi kila mmoja atakuwa ameingiziwa fungu lake benki, tunafanya yote haya kwa ajili ya kuonge­za hamasa kwa wache­zaji,” alisema Manara.



Naye kocha Msaidizi wa Simba, Masoud Djuma amefungukia juu ya michezo yao hiyo 10 iliyobakia am­bapo alisema: “Mechi hizi 10 zilizobakia siyo nyingi sana, kikubwa ambacho tunataki­wa kukifanya ni kuende­lea kupigana tupate pointi kwa kila mechi.”

Tulia Ackson Afunguka Kuhusu Mange Kimambi "Sina Uhakika Kama Mange ni Binadamu wa Kawaida"

$
0
0
Tulia Ackson Afunguka Kuhusu  Mange Kimambi "Sina Uhakika Kama Mange ni Binadamu wa Kawaida"
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson amefunguka na kusema kuwa yeye hana uhakika kama mwanadada mwanaharakati wa mitandaoni Mange Kimambi kama ni binadamu wa kawaida kama yeye.


Tulia Ackson amesema hayo alipohojiwa na moja ya chombo cha habari na kusema kuwa kwa sasa hawezi kusema kama mwanadada huyo anakosea au laa kwa kuwa hana uhakika kama yupo kama yeye na kusema labda akipata fursa ya kuonana naye na kuona kweli yupo kama yeye ndiye anaweza kuwa na la kusema.

"Sina hakika kama yeye ni binadamu wa kawaida kama mimi kwa hiyo sijui labda nikikutana naye ndiyo nitajua chakuzungumza naye lakini kwa yale nayoyasikia hapa na pale sina hakika kama yeye ni binadamu wa kawaida kama mimi ila kama yupo kama mimi basi nitapata fursa ya kumshauri nikionana naye, siwezi kusema anakosea kama nilivyosema sijajua yeye ni mtu wa namna gani kwa hiyo huenda hakosei labda ni aina yake ya binadamu yaani ni specie tofauti hivyo kama yeye ni specie ya tofauti huwezi kusema anakosea" alisema Tulia Ackson

Binti Mpalestina Aliyemzaba Kofi Mwanajeshi wa Israel Afungwa Jela

$
0
0
Binti Mpalestina Aliyemzaba Kofi Mwanajeshi wa Israel Afungwa Jela
Binti mmoja wa Kipalestina aliyekamatwa baada ya kumchapa kofi mwanajeshi wa Israel amekiri kosa na atatumikia kifungo cha miezi minane gerezani kufuatia maafikiano kati yake na upande wa mashtaka.

Msichana huyo Ahed Tamimi alikiri kuwa na hatia kwa makosa manne aliyokuwa akishtakiwa kati ya 12 yaliyokuwa yakimkabili, ikiwemo shambulio la mwili, wakili wake ameeleza.

Kadhalika, atalipa faini ya shekeli 5,000 sawa na dola 1,440 .

Binti huyo mwenye miaka 17 alikamatwa baada ya kunaswa kwenye picha ya video akiwakabili wanajeshi wawili nje ya nyumba yake mwezi Desemba.

Uamuzi wa mahakama unamaanisha kuwa ataachiwa huru kipindi cha majira ya joto kwa sababu hukumu yake imehesabu siku alizokaa korokoroni, mwanasheria wake Gaby Lasky amenukuliwa na shirika la habari la AFP.

Kwa Wapalestina, Ahed Tamimi, ambaye kwa kipindi hicho alikuwa na miaka 16 wakati tukio lilipotokea Ukingo wa Magharibi, ni ishara ya kutounga mkono makazi ya Israeli.

Lakini waisraeli wanamuona kama mtu mwenye vurugu na kutafuta umaarufu.

Kesi yake ilikuwa ya ndani kwenye mahakama ya kijeshi katika eneo la ukingo wa magharibi tarehe 13 Februari.

Mwanasheria wake alitaka mashtaka hayo yasomwe hadharani lakini Jaji aliamua kesi hiyo iendelee huku ikirekodiwa kwenye kamera.

Ahmed Tamimi alipigwa picha ya video na Mama yake,Nariman, alipokuwa akigombana na wanajeshi wenye silaha, katika kijiji cha Nabi Saleh tarehe 15 mwezi Desemba, baada ya kutokea maandamano yaliyokuwa yakipinga hatua ya Marekani kuutambua mji wa Jerusalemu kuwa mji mkuu wa Israel.

Tukio hilo lililorekodiwa lilikuwa kwenye ukurasa wa Faceook wa Nariman na video ya ugomvi huo ilisambaa sana.Katika video hiyo,Ahed Tamimi alionekana akimpiga teke mwanajeshi mmoja na kumchapa kofi la usoni, na kumtishia kumpiga mwanajeshi mwingine.

Ahed alikamatwa majira ya usiku na kukabiliwa na shutuma 12, kushambulia, kuchochea, kuingilia kazi za wanajeshi na kurusha mawe.

Mama yake pia alishtakiwa kwa makosa ya kufanya uchochezi kwenye mtandao wa kijamii na kushambulia, wakati binamu yake Nour, ambaye alishiriki kwenye tukio hilo alishtakiwa kwa kosa la kushambulia.

Ahed Tamimi alijitetea kuwa alichukua hatua hiyo baada ya kuwaona wanajeshi wakimfyatulia risasi ya mpira kichwani binamu yake Mohammed mwenye miaka 15.

Wanajeshi wa Israel wamesema wamepeleka kikosi kwenye makazi ya Tamimi, ambapo vijana wa kipalestina wamekuwa wakirusha mawe kwa vikosi vinavyotuliza maandamano

Ahed Tamimi amesema alimkaripia mwanajeshi huyo alipompiga binamu yake kwa risasi za mipira
Vijana hao pia waliandamana dhidi ya tukio la kumsababishia Mohammed jeraha kichwani.

Kutokana na tukio hilo, Waziri wa Elimu wa Israel Naftali Bennett amesema Ahed na Nour Tamimi wanapaswa kufungwa maisha gerezani.


Raia wengi wa Israel wanasema kuwa Ahed Tamimi kwa muda mrefu amekuwa akitumiwa na familia yake, ambayo inashutumiwa kumtumia kuwaghadhabisha wanajeshi Israel.


Ahed Tamimi aliwahi kuonekana kwenye video nyingine akitishia kumpiga ngumi mwanajeshi mmoja
Ahed kwa mara ya kwanza alikuwa maarufu alipojitokeza hadharani akiwa na miaka 11, alionekana kwenye video nyingine akitishia kumpiga ngumi mwanajeshi mwingine.

Heche: Viongozi Chadema Wamefungwa Kifungo cha Nje

$
0
0
Heche: Viongozi Chadema Wamefungwa Kifungo cha Nje
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Bara), John Mnyika na Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Serengeti, John Heche wameachiwa kwa dhamana baada ya kuhojiwa kwa zaidi ya saa mbili katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam.

Mara baada ya kuachiwa, Heche ambaye ni mbunge wa Tarime Vijijini amesema kitendo cha viongozi wa Chadema kuripoti polisi na kukaa kwa saa tano bila kuhojiwa chochote na kutakiwa kuripoti siku nyingine ni sawa na kifungo cha nje.

“Hii ni mara ya tano ninaripoti polisi. Polisi Tanzania ni kama wametuhukumu kifungo cha nje, kila baada ya siku mbili wanataka turipoti kituo kikuu cha Polisi Dar es Salaam bila kujali unaishi wapi, gharama unazotumia kuja na kurudi Dar es Salaam na  majukumu yako mengine ya kikazi unayoshindwa kuyatekeleza. Kuna wakati inabidi kukataa uonevu huu,” amesema Heche leo Machi 22, 2018 wakati akizungumza na MCL Digital.

Leo Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe; Katibu Mkuu, Dk Vicent Mashinji; naibu makatibu wakuu, John Mnyika (Bara) na Salum Mwalimu (Zanzibar) pamoja na Heche waliripoti kituoni hapo kwa ajili ya mahojiano.

Hata hivyo, mbunge huyo wa Tarime Vijijini na Mnyika waliendelea kuhojiwa huku wenzao wakiachiwa kwa dhamana, sababu ya wao kubaki kituoni hapo ikielezwa kuwa ni kitendo chao cha kutoripoti  Machi 16, 2018.

Mara baada ya kuachiwa viongozi hao wametakiwa kuripoti tena kituoni hapo Machi 27, 2018.

Akizungumza na MCL Digital, Heche amesema kitendo wanachofanyiwa si sahihi kwa maelezo kuwa baadhi yao ni wabunge na kwa sasa wanapaswa kushiriki vikao vya kamati za chombo hicho.

“Mimi napaswa kuwa katika vikao vya kamati za Bunge Dodoma. Mbali na hilo nikiwa jimboni kwangu, kutoka huko mpaka Dar es Salaam natumia nauli zaidi ya Sh1milioni. Hivi kwa nini hawalioni hili,” amehoji Heche.

Amesema kwa hali ilivyo ni vyema wakaelezwa hatima yao kwa maelezo kuwa mbali na kupoteza fedha, pia wanashindwa kushiriki shughuli za kibunge.

“Mfano wanataka turejee tena Jumanne ijayo (Machi 27, 2018). Hapa ninaondoka nakwenda Dodoma kushiriki vikao vya kamati, nitalazimika kuondoka jumatatu ili kuwahi. Sasa huu ni usumbufu kwa kweli. Katika hili sitakubali nitafanya kitu,” amesema Heche.

Wakili wa viongozi hao, Frederick kihwelo amesema Mnyika na Heche walizuiwa kuondoka na  kutakiwa kuandika maelezo.

"Baada ya kufika,  polisi waliwataka Heche na Mnyika ambao hawakufika Machi 16 . Walitaka wabaki baada ya wenzao kuondoka na kuwaagiza kuandika ahadi ya maandishi kuwa Jumanne ijayo watakuwepo,”amesema.

Hukumu ya Babu Seya, Papii Kocha Kusomwa Kesho

$
0
0
Hukumu ya Babu Seya, Papii Kocha Kusomwa Kesho
Mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu (AfCHPR) kesho Ijumaa Machi 23, 2018 itasoma hukumu ya kesi ya wanamuziki wa dansi, Nguza Viking maarufu Babu Seya na mwanaye, Johnson Nguza ‘Papii Kocha’.

Wanamuziki hao walikata rufaa iliyosajiliwa na kupewa namba 006/2015 katika mahakama hiyo kupinga kifungo cha maisha.

Wakati hukumu hiyo ikitarajiwa kusomwa kesho, Babu Seya ambaye ni mtunzi wa kibao maarufu cha “Seya” na Papii Kocha ambaye wameshirikiana katika wimbo huo ni miongoni mwa wafungwa 8,157 waliosamehewa na Rais John Magufuli siku ya Uhuru wa Tanganyika, Desemba 9, 2017.

Walikuwa kati ya wafungwa 61 waliokuwa na adhabu za vifungo vya maisha na kunyongwa ambazo si rahisi kupata msahama wa kawaida wa mkuu wa nchi unaotolewa siku ya sherehe hizo.

Rais wa mahakama hiyo, Jaji Sylvian Ore alisema itasoma hukumu hiyo baada ya kukamilisha mahitaji yote na kupata taarifa za wakata rufaa.

Hata hivyo, wakati Jaji Ore akiahirisha kusoma hukumu hiyo, wanamuziki hao hawakuwepo mahakamani.

Baadhi ya mawakili waliokuwepo mahakamani hapo wamesema licha ya kuwa wanamuziki hao wamepata msamaha wa rais, hukumu yao itasomwa.

"Mahakama hapa itatoa hukumu ili kuweka rekodi za kimahakama katika kesi za aina hii na hata kama ikieleza walikuwa na hatia haina athari kwao,” amesema wakili Daniel Kalasha.

Katika kesi hiyo, Jamhuri inawakilishwa na mawakili Sara Mwaipopo na Nkasori Sarakikya.

Kutana na Mtatibu Mongwa Anayesafisha Nyota na Kutoa Pete za Bahati

$
0
0

KWA WALE WENYE KUHITAJI TIBA

Husafisha nyota na kutoa Pete za bahati na kwawale walio sumbuka kwaajili ya matibabu na hawakufanikiwa chochote sasa njoo ujionee miujiza hapo kwahapo bila malipo yoyote malipo baada yakazi napia humpa mtu jini la mali kwayule anaye taka kumiliki bila mashariti yoyote
Tunatibu magonjwa mbalimbali yaliyo shindikana mpenzi aliye kukimbia nakumrudisha kwa masaa 24 tu napia natoa dawa za nguvu za kiume kuurefusha uume paka pale unapotaka .

Natoa dawa za biashara na mvuto ==tunatoa dawa zauzazi kwa wale kina mama wenye matatizoya uzazi walio angaika kwa muda mrefu bila kupata mafanikio yoyote njoo umalize tatizo lako sasa
Natoa mazindiko yanyumba na mwili biashara na mvuto kazini

Kupandisha nyota ili kungaa kupandishwa cheo kazini kurudisha mali zilizo pote zilizo ibiwa kuzulumiwa
Kesi zilizo shindikana uzimaliza mara moja namengine mengi ya siri piga simu

+255 764291657 

Mwanamke Aliyedhalilishwa na Kuteswa Wakati Akijifungua Kulipwa Milion 56

$
0
0

KENYA: Mahakama Kuu imeamuru mwanamke(Josephine Majani) aliyedhalilishwa na kuteswa wakati akijifungua katika hospitali ya umma, alipwe fidia ya takribani Tsh. Milioni 56.5.
-
Mahakama ilidai mamlka ya afya ilikiuka haki za kimsingi za Bi. Majani alipotengwa na kukosa kuhudumiwa mwaka 2013
-
Aliyoyapitia Bi. Majani mikononi mwa wauguzi hao yalipata kujulikana baada ya mtu kurekodi video kwenye simu yake na kuiweka kwenye mtandao wa kijamii
-
Akizungumzia uamuzi huo, Bi Majani amesema amefurahia kwa kuwa hatimaye haki imetendeka na kuwa atatumia fedha hizo kumlea mwanaye

Timu ya Taifa Stars Yapigwa Kipigo cha Mwizi

$
0
0

Timu ya Taifa ya mpira wa miguu(Taifa Stars)? - #regrann (Taifa Stars) imeambulia kipigo cha mabao 4 kwa 1 kutoka kwa timu ya Taifa ya Algeria katika mchezo wa kirafiki

Goli pekee la kufutia machozi la Taifa Stars limefungwa na Simon Msuva anayekipiga katika Klabu ya Difaa El Jadid ya nchini Morocco.

Je, una maoni gani kuhusu mwenendo wa Timu ya Taifa ya mpira wa miguu(Taifa Stars)?

Paul Makonda kuwasaidia wanawake waliotelekezwa na wanaume zao

$
0
0

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amewatangazia wawanake wote waliotelekezwa na waume zao na hawapatiwi fedha za matunzo ya mtoto kufika ofisini kwake siku ya Jumatatu ya April 09 kwaajili ya kupatiwa msaada wa kisheria.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi ya RC, inasema Jopo la wataalamu wa Sheria, Maafisa Ustawi wa jamii na Askari Polisi kutoka Dawati la Jinsia wamejipanga ipasavyo kukuhudumia na kuhakikisha mzazi mwenzio anatoa fedha za matunzo ya Mtoto.

“Ewe mwanamke huu sio wakati wa kulia wala kuteseka, serikali yako itasimama na wewe kuhakikisha unapata haki yako uliyoikosa kwa muda mrefu,” Taarifa hiyo inaeleza.

Alisema Huduma hii inatolewa bure chini ya uongozi thabiti wa serikali ya awamu ya tano.

Tunda afunguka hata mume wa mtu naye sumu

$
0
0
Anna Patrick Ki­mario, ‘ Tunda’

Anna Patrick Ki­mario wengi hawali­jui jina hilo na mara nyingi huwa najiuliza sijui kwa nini huwa hapendi uhalisia wa jina lake na kutaka ajulikane kwa jina la Tunda Sebastian.

Kuna wanaomjua zaidi na kusema kuwa amekulia mkoani Morogoro ingawa kuna wakati pia aliishi Moshi na Mtoni-Kijichi hapa Dar es Salaam, hiyo ilikuwa ni kabla hajaanza maisha yake ya kimjinimjini, maisha ya kiu­supastaa ambayo anaishi nayo sasa.

Tunda anajinasibu kwamba kazi inayomuweka mjini ni ‘U-video Queen’. Kwa wasioelewa maana yake, hawa ni wale wa­sichana wanaoonekana kwenye video za wasanii, hasa hawa wa Bongo Fleva.

Ukizungumzia kazi yake, japokuwa wengi wanaweza kuwa hawajui, lakini Tunda amefanya kazi kadhaa, japo siyo kivile lakini huwezi kumuondoa kwenye orodha ya wasichana ambao ukiwaweka kwenye video yako kama wewe ni msanii, basi hawezi kukuangusha.

Kazi yake mpya kabisa, ni kwenye video ya Barnaba aliyo­mshirikisha Aslay, iitwayo Ngo­ma. Zipo nyingine za kitambo kidogo ambazo Tunda amefanya kazi nzuri! Mnyonge mnyon­geni haki yake mpeni! Tazama video kama Why Me ya Amini na Barnaba, video ya wimbo wa Ma­tonya aliyomshirikisha Christian Bella uitwao Agwelina, mtazame kwenye video ya Raha ya TID!

Ninachotaka kukuonesha hapa ni kwamba japokuwa wengi hawamuelewi msichana huyu kama anajishughulisha na nini hasa, anacho kipaji, anayo kazi ambayo inamuingizia kipato na kama akiamua kuwekeza nguvu huko, anaweza kuishi mai­sha ya juu pengine kuliko haya anayofosi sasa.

U-video Queen au wengine wanaita Video Vixen, ni kazi kama zilivyo kazi nyingine na upo ushahidi mkubwa wa watu waliofanikiwa sana kwa kazi hiyo, mfano mzuri ni kama mwa­nadada Tokyo anayeonekana kwenye video ya Kendrick Lamar iitwayo Backstreet Freestyle, au mwanadada mwingine Alisha Je­nay ambaye ameng’ara kwenye video kibao mbele, hasa za Hip Hop na kubwa kuliko ni mwana­dada Esther Baxter, kama humjui itazame video ya The New Work­out Plan ya Kanye West.

Baxter anatajwa kuwa ndiye Video Vixen mwenye mafanikio zaidi kwenye tasnia hiyo, hatua ambayo hata Tunda leo akiamua, anaweza kuifikia.

Unaweza kujiuliza, kwa nini namzungumzia Tunda? Huyu ‘mtoto’, licha ya umri wake mdo­go usiozidi miaka 24, ameshehe­ni matukio, tena mazitomazito!

Fuatilia akaunti yake ya Insta­gram, utagundua kwamba Tunda anapenda sana maisha ya juu, kutwa kucha kuzurura kwenye mahoteli makubwa, kazi yake kubwa ni kula bata! Tena kwenye viwanja vyenye hadhi ya juu!

Unaweza kujiuliza, ni pesa mbuzi anazolipwa na hawa wasanii wanaomtumia kwenye video zao ndizo zinazompa jeuri ya kutamba kiasi hiki? La hasha! Yapo madai mazito kwamba mwa­nadada huyu ameamua kutafuta mafanikio kwa njia ya mkato, anautumia mwili wake kama kitega uchumi!

Orodha ya wanaume wanaotajwa kubanjuka naye ni ndefu! Yupo Dia­mond Platnumz na wengine wengi, wakubwa kwa wadogo, mastaa kwa wasio mastaa!

Ninachotaka kukiweka sawa ni hili suala lililoibuka la kutoka kimapenzi na mtangazaji wa kituo kikubwa cha TV, Casto Dickson huku wakipa picha za kimahaba na kuziachia mitandao­ni.

Nilivyoona kwa mara ya kwanza nilishtuka kido­go nikaona huenda ni sehemu ya kutafuta kiki, mara ya kwanza niliona picha wakiwa katika Ukumbi wa Next Door kama sikosei ilikuwa ni kibao kata, ikaenea mtandaoni hata siku mbili hazikuisha nikaona tena picha wakiwa chumbani kwenye kioo tena wakiwa kwenye mapozi ya kima­haba, nikashtuka zaidi! 

Picha ziliendelea kumiminika hadi hivi ninavyokua­mbia, mbaya zaidi juzikati alifanyiwa mahojiano na moja ya gazeti hili na kukiri kuwa yupo katika uhusiano wa kimapenzi na mtangazaji huyo, akaenda mbali zaidi kwa kusema kuwa yupo tayari kumzalia.

Wakati hayo yakiendelea limeibuka jipya la mzazi mwenziye na mtangazaji huyo aitwaye Don Posh ambaye pia ni Miss Aru­sha 2015 akiomba Tunda amuachie mzazi mwenzake kwa sababu bado yupo naye kwenye uhusiano na ame­shamzalia watoto mapacha.

Ninachotaka kukisema hapa, Tunda akiwa kama staa, kioo cha jamii ni vyema akajitathimini mwenendo wake, sitaki kuingilia sana huko lakini atambue uchungu wa mzazi huwa unauma sana, kutembea na mwanaume ambaye unajua kabisa ana uhusiano na mwanamke mwingine si jambo zuri. Watch out!

Jide na ishu ya kuishi Nigeria

$
0
0

MEI 20, mwaka jana ndani ya Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar, nilibahatika kuwa miongoni mwa waalikwa katika tamasha kubwa la muziki lililotambulika kama Naamka Tena lililoandaliwa na mwanamuziki mkongwe wa kike wa Bongo Fleva nchini, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ ukipenda waweza kumuita Komando.

Hamu kubwa ya kuwepo katika tamasha hilo ni kumshuhudia akiimba wimbo wake ambao ulikuwa gumzo kwa kipindi hicho wa Ndi Ndi Ndi. Nilishangaa ukumbi wote ukilipuka kwa shangwe huku wengi wakiomba wimbo huo urudiwe zaidi ya mara nne.

Jide alikuwa Jide kweli, uwezo wake wa kulitawala jukwaa kwa zaidi ya miaka 15 niliushuhudia ‘live’, na ukija kwenye suala la pumzi yaani kuimba mfululizo bila kuchoka ni komando hasa, ana swagga, anajua ku-baunsi kwa kufuata midundo na jinsi ya kuimba na mashabiki.

Ukiachana na hilo, juzikati nilipata bahati ya kukutana naye na kuzungumza mengi kuhusiana na muziki akiwa kama mkongwe pekee wa kike aliyefanikiwa kuwa na albamu saba hadi sasa ambazo ni Machozi (2000), Binti (2003), Moto (2005), Shukrani (2007), The Best of Lady Jaydee (2012), Nothing But The Truth (2013) pamoja na Woman (2017).

Katika makala haya anafunguka mengi zaidi; Showbiz: Wasanii wengi wamekuwa    wakitoa albamu kwa mwaka huu huku wengine wakiwa kwenye mipango hiyo, vipi kuhusu wewe una mpango wa kuongeza nyingine ya nane?

Jide: Ujue albamu ni kitu ambacho nimekuwa nikitoa miaka yote na hadi sasa tayari nina albamu saba hivyo nitatoa tu.

Showbiz: Ni changamoto zipi unapitia ukiwa kama mkongwe kwenye muziki wa Bongo Fleva?

Jide: Changamoto ni zilezile za kila siku na hazina tofauti sana, kwenye changamoto hakuna ukongwe wala upya. Changamoto ni changamoto tu.

Showbiz: Wasanii wengi wa kike wanakuja kwa kasi kwenye gemu, ukiwa kama mkongwe kwa sasa Bongo?

Jide: Namkubali sana Lady Jaydee kuliko wasanii wengine wa kike wote Tanzania, ila pia namuheshimu sana Khadija Kopa na Patricia Hillary.

Showbiz: Vipi kuhusu Machozi Band ndiyo imekufa kabisa maana hatuisikii tena?

Jide: Siku hizi hakuna Machozi Band kuna The Band na ndio huwa inapiga kwenye shoo zote za Lady JayDee.

Showbiz: Una mpango ya kumiliki bendi tena kwa maana ya kuongeza wigo?

Jide: Bado niko na bendi na watu walewale niliokuwa nao tangu hapo awali sina mpango mwingine kwa sasa.

Showbiz: Hivi ulishawahi kufikiria kumiliki lebo ya muziki?

Jide: Anacheka! (Hapana kwa kweli).

Showbiz: Swali la uzushi. Ulishawahi kufikiria kuishi nchini Nigeria?

Jide: Kwenda na kurudi lakini sio kuishi moja kwa moja kabisa, kwani asilimia kubwa ya maisha yangu nimeyajenga Tanzania. Ila lolote linawezekana pia ikibidi.

Showbiz: Umekuwa mbali na skendo na ndiyo mmoja wa wakongwe wenye sifa hiyo nini siri yake?

Jide: Ni kwa sababu Jaydee huwa sio mtu wa skendo, sio kwamba najiepusha ila sina. Hivyo ndivyo nilivyoumbwa tu!

Showbiz: Ikitokea umepata nafasi ya kuongea na Rais John Magufuli, utamwambia nini?

Jide: Naweza nisijue hata cha kumwambia kusema kweli, huwa najiweka mbali kuzungumzia siasa na wanasiasa kwa ujumla.

Showbiz: Mwisho kabisa, mashabiki watarajie kipi baada ya ujio wako mpya wa Anaweza?

Jide: Waendelee ku-enjoy Anaweza kwa sasa!

Showbiz: Nimeona taarifa kuwa unajipanga kuzindua wimbo wa Anaweza ukiwa na mkongwe wa Reggae kutoka Jamaika, usiku huo utakuwa kama ule wa Naamka Tena wa mwaka jana?

Jide: (Anacheka!) Itakuwa nzuri sana siwezi kusema zaidi ya mashabiki kuja wao kujionea pale Golden Tulip, Machi 31, mwaka huu Golden Tulip.

Showbiz: Asante sana Jide!

Jide: Asante na wewe pia karibu tena.


Viewing all 104781 articles
Browse latest View live




Latest Images