Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Okwi,Bocco Waahidi Kupata Ubingwa wa Ligi Kuu

$
0
0
Okwi,Bocco Waahidi Kupata Ubingwa wa Ligi Kuu
BAADA ya Simba kutolewa katika Kombe la Shirikisho Afrika, mastraika wa timu hiyo John Bocco na Emmanuel Okwi kwa pamoja wameapa kufia uwanjani ili Wekundu wa Msimbazi wabebe ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

Simba iliondolewa na Al Masry ya Misri katika Kombe la Shirikisho baada ya awali kutoka sare ya mabao 2-2 jijini Dar es Salaam halafu ugenini wakatoka suluhu.

Kutokana na hali hiyo, Okwi na Bocco wamesema lengo lao sasa ni kuhakikisha wanapambana kufa na kupona kwenye Ligi Kuu Bara ili waweze kuiwezesha Simba kutwaa ubingwa.

Simba inaongoza katika ligi kuu ikiwa na pointi 46 sawa na Yanga, inayoshika nafasi ya pili, lakini wenyewe wana tofauti kubwa ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Okwi alisema, mipango yao ya kuiwezesha Simba kutwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho imekwama, sasa wanaelekeza nguvu zao kwenye ligi kuu.

“Tunarudi kujipanga kwenye ligi kuu, kwani ndiyo sehemu pekee tunapotakiwa tupambane kufa na kupona ili mwakani tuweze kushiriki tena michuano ya kimataifa, tutapambana tuwe mabingwa,” alisema Okwi.

Kwa upande wake, Bocco ambaye pia ni nahodha wa Simba, yeye alisema; “Kiu yangu na wachezaji wenzangu ni kuhakikisha tunatwaa taji la Ligi Kuu Bara, maana ndiyo silaha pekee tuliyonayo kwa sasa, hiyo ndiyo tiketi ya sisi kucheza mechi za CAF mwakani.

“Pia tunajua furaha ya mashabiki wa Simba kwa sasa ni kuona tunatwaa ubingwa na siyo kitu kingine, hivyo tumejipanga kuhakikisha hilo linatokea bila tatizo.”

Simba leo Jumamosi inatarajiwa kuanza mazoezi kujiandaa na mchezo dhidi ya Njombe Mji, Aprili 3, mwaka huu.

Mwanamke Ampa Mimba Mwanaume Ajifungua Mtoto

$
0
0
Mwanamke Ampa Mimba Mwanaume Ajifungua Mtoto
INAFAHAMIKA dunia nzima kwamba wanawake ndiyo wanaobeba ujauzito, lakini je, umewahi kudhani kwamba inawezekana kwa mwanaume kubeba ujauzito kwa miezi tisa na kujifungua?

Vuta picha unakutana na watu wawili barabarani, mmoja amevaa mavazi ya kiume na hata mwonekano wake ni wa kiume na mwingine amevaa mavazi ya kike na hata mwonekano wake ni mwanamke kabisa, lakini mmoja kati yao ni mjamzito, unajua ni yupi kati yao? Ni yule aliyevaa mavazi ya kiume na mwenye mwonekano wa kiume!
Ni jambo lisilowezekana si ndiyo? Basi kwa taarifa yako, tukio kama hilo limetokea nchini Ecuador ambapo Fernando Machado, 22, amepewa ujauzito na ‘demu’ wake, Diane Rodriguez, 33.

Ilikuwaje? Diane Rodriguez alizaliwa akiwa mwanaume lakini mwenyewe akawa hajikubali kabisa, akawa anatamani kuwa mwanamke, jambo ambalo baadaye lilimfanya abadili jinsia na kuwa mwanamke. Hata hivyo, katika zoezi lake la kubadili jinsia, Diane anaeleza kwamba viungo vyake vya uzazi havikufanyiwa mabadiliko yoyote.

Kwa nje akawa na mwonekano wa kike kabisa, akawa na matiti kama wanawake wote walivyo, akajibadilisha kila kitu kuanzia mavazi, mitindo ya nywele, kutembea na kila kitu, maisha yakaendelea. Baadaye, akiwa ‘mwanamke’, Diane alikutana na Fernando Machado ambaye naye alikuwa akifanana naye baadhi ya vitu.

Tofauti yao ikawa ni kwamba Fernando alizaliwa akiwa mwanamke lakini akawa hapendi jinsia yake halisi.
Hali hiyo ilimfanya naye abadili jinsia na kuwa ‘mwanaume’ lakini kama ilivyokuwa kwa Diane, viungo vyake vya uzazi havikubadilishwa chochote zaidi ya mwonekano wa nje.

Wawili hao walikutana kwenye mitandao ya kijamii, wakajenga urafiki na baadaye wakawa wapenzi lakini mapenzi yao yalikuwa ya kustaajabisha sana kwa sababu yule ambaye kila mtu alikuwa akiamini kwamba ndiyo mwanaume, kiuhalisia alikuwa ni mwanamke. Na yule ambaye watu wa nje walikuwa wakimuona kama ndiyo demu, kiuhalisia ndiye aliyekuwa mwanaume.

Maisha yaliendelea na baadaye, Fernando ambaye sasa alikuwa na mwonekano wa kiume, akanasa ujauzito aliopewa na Diane ambaye ana mwonekano wa kike. Kwa hiyo ikawa ‘mwanamke’ amempa mimba ‘mwanaume’.

Septemba, 2016, Fernando alijifungua salama na sasa wanalea mtoto, huku wakieleza malengo yao kuwa ni kupata watoto wengi zaidi.

Rais Buhari Akutana na Wasichana 106 Walioachwa Huru na Boko Haramu Nigeria

$
0
0
Rais Buhari Akutana na Wasichana 106 Walioachwa Huru na Boko Haramu Nigeria
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amewapokea wasichana 106 na mvulana mmoja jijini Abuja.Wasichana waliwasili mapema kwenye makazi ya Rais wakionekana wenye afya njema, isipokuwa wanne ambao wanaelezwa kuwa walivunjika miguu.
Wasichana walisafirishwa kwa ndege mpaka mjini Abuja siku ya Jumatano ambapo walitakiwa kwenda kufanya uchunguzi wa kitabibu na kiusalama baada ya kukabidhiwa kwa mamlaka za kiraia.
Buhari amewataka wasichana waendelee kutimiza ndoto zao bila kuogopa machafuko, amevitaka vyombo vya ulinzi kuhakikisha usalama unakuwepo kwenye shule zote zilizo hatarini kushambuliwa na kuonya kuwa iwapo tukio hilo litatokea tena hatalichukuliwa kirahisi.
Buhari amewataka wazazi ambao bado watoto wao wanashikiliwa kutokata tamaa wakati serikali yake inafanya jitihada kuwanasua.
Wasichana wanatarajiwa kupewa ushauri nasaha kabla ya kukabidhiwa kwa wazazi wao.
Haijulikani kama kurejea kwao kwenye maisha ya kawaida ni suala la uchaguzi wakati huu ambao mustakabali wa elimu yao haujulikani, iliripotiwa kuwa wakati mabinti hao walipokuwa wakirejeshwa, wanamgambo walitoa tahadhari kuwa wasirejee tena shuleni.
Wakati hayo yakijiri Serikali ya Nigeria imesema haitapunguza jitihada zake za kumkomboa msichana mmoja aliyebaki mikononi mwa Boko Haram baada ya kutekwa mjini Daptchi mwezi uliopita.
Msichana huyo ni miongoni mwa wasichana 110 waliochukuliwa wakiwa shuleni, wanamgambo walipovamia mji tarehe 19 mwezi Februari.
Wengi wao waliachiwa siku ya Jumatano isipokuwa msichana mmoja, Mkristo ambaye alikataa kubadili dini kuwa muislamu, anashikiliwa bado .
Rais alisema msichana huyo hatatelekezwa.
''Rais Muhammadu Buhari amejitoa kuhakikisha msichana wa Dapchi aliyebaki anakuwa huru''. Ilieleza taarifa ya serikali.
''Serikali ya Buhari haitaacha jitihada za kumnasua binti na kumrejesha kwa wazazi wake.Msichana huyu hatatelekezwa''.
Kati ya waliotekwa, wasichana 104 waliachiwa siku ya Jumatano na watano wanaripotiwa kupoteza maisha wakiwa mateka.
Watu wengine wawili , mvulana na msichana mwingine kutoka mji wa Dapchi waliachiwa huru wakati huo huo, serikali imesema.
Serikali imekana madai kuwa Boko Haram walilipwa pesa kuwakomboa wasichana, au kubadilishana na mfungwa.
Waziri wa Habari Lai Mohammad ameiambia BBC kuwa kurudi kwa wasichana ni sehemu ya mazungumzo yanayoendelea kuhusu msamaha na kusitisha mapigano.
''hatukulipa pesa yoyote kwa ajili ya wasichana.Tulijadiliana mpango wa kumaliza mapigano tukiahidi kuwasamehe''.Alieleza.
''Kama wao(Boko Haram) wataweka silaha zao chini na kuukana uasi, sisi tutawapa njia huru kabisa kurejea kwenye jamii''.Alisema bwana Mohammad.
Amesema serikali ilikuwa imerudishwa nyuma na kitendo cha utekaji wa wasichana na kuharibu mazungumzo .
Wakati huohuo, Baba wa msichana mmoja kati ya waliotekwa ameeleza uchungu alioupata kutokana na kumpoteza binti yake tena baada ya kwenda kukutana na Rais muda mfupi baada ya kuachiwa.
Ameiambia BBC aliweza kumuona binti yake hospitali tu,tena kwa dakika chache.
''Ingawa nilimhakikishia sitamuacha pale, sote tulitakiwa kuondoka wakawachukua'' alisema.
Utawala wa Buhari umekuwa kwenye shinikizo kukomesha vitendo vya utekaji nyara, uliorudisha kumbukumbu ya mwaka 2014 , wasichana 276 mjini Chibok walipotekwa
Rais wa zamani wa Nigeria , Goodluck Jonathan alikosoa namna ambavyo rais Buhari anavyoshughulikia utekaji nyara wa Chibok, takriban umbali wa kilometa 275 kusini mashariki mwa mji wa Daptchi.
Zaidi ya nusu ya waliotekwa Chibok wamerejea lakini 100 bado hawajulikani walipo.
Shirika la waangalizi wa haki za binaadam, Amnesty International limekosoa namna serikali inavyoshughulikia suala la utekaji nyara uliofanyika Daptchi, likisema serikali ilipuuza maonyo mbalimbali kuhusu nyendo za wapiganaji wa Boko Haram kabla ya kuwateka nyara wasichana.
Jeshi la Nigeria limesema madai ya Amnesty International ni uongo mtupu.Shirika la habari la Ufaransa AFP limeripoti.

Waziri Shonza Amponza Pretty Kind Atimuliwa na Mwenyenyumba Kisa.....

$
0
0
Baada ya Kufungiwa na Waziri Shonza Pretty Kind Amekwaa Balaa Lingine
BAADA ya kufungiwa kujishughulisha na sanaa ya filamu na muziki kwa miezi sita na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza kwa kuvaa nusu utupu, mwanadada Suzan Michael ‘Pretty Kind’ ameponzwa na waziri huyo kwani amekutwa na balaa lingine, Risasi Jumamosi linakupa habari kamili.

Habari za awali zilidai kwamba, Pretty kwa sasa yupo kwenye wakati mgumu kwani amefukuzwa katika nyumba aliyokuwa akiishi kisa mwenye nyumba hataki mpangaji anayevaa nusu utupu.

“Mambo ni magumu sana kwa Pretty kwani amepewa ‘notice’ kwenye nyumba aliyokuwa akiishi maeneo ya Sinza, sasa ndiyo anahaha kutafuta pa kuishi, kiukweli tangu amefungiwa amejikuta akipoteza dira kabisa,” alidai rafiki wa Pretty.
Risasi Jumamosi lilimtafuta Pretty ili kujua ukweli ambapo alipopatikana alifunguka kwa kuthibitisha madai hayo na kueleza kuwa amepewa ‘notice’ ya kuhama kwenye nyumba aliyokuwa akiishi.
“Ukweli ni kwamba tangu nimefungiwa na naibu waziri nimekuwa nikinyanyasika sana, hapa baba mwenye nyumba kanifukuza na kwenye sehemu niliyokuwa nimelipia kwa ajili ya biashara nako amenifukuza, naumia kwa kweli maana nimeshabadilika lakini bado watu wananiona ni mvaa nusu utupu tu,” alisema Pretty na kukiri kuwa kwa sasa anahaha kutafuta nyumba ya kuishi

Wanawake Poland Waandamana Kupinga Sheria ya Utoaji Mimba

$
0
0
Wanawake Poland Waandamana Kupinga Sheria ya Utoaji Mimba
Wanawake nchini Poland wameandamana kupinga serikali ya nchini hiyo kupitisha sheria mpya ambayo itakataza moja kwa moja utoaji mimba wa aina yoyote ile.
Wanawake hao wakiwa wanaandamana pamoja na wanaharakati wa haki za binadamu wameeleza kuwa kutoa mimba kukifanywa haramu kutahatarisha maisha ya wanawake ambao maisha yao yanakuwa hatarini kutokana na kubeba ujauzito.
Takribani mashirika yasiyo ya kiserikali 200 yamejiunga kwenye harakati hizo za kupinga serikali kukataza utoaji wa mimba, kwa kuandika waraka wa rufaa kwa Bunge la nchi hiyo likisema sheria hiyo itahatarisha maishaya wanawake.
Waraka huu pia umeungwa mkono na Ofisi ya Tume Kuu ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa.

Wolper "Sijawahi Kuachwa na Mwanaume Kwenye Mahusiano ya Mapenzi"

$
0
0
Wolper "Sijawahi Kuachwa na Mwanaume Kwenye Mahusiano ya Mapenzi"
Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara maarufu Jacqueline Wolper amefunguka na kuweka wazi kuwa hajawahi hata siku moja kuachwa na wanaume.

Kumekuwa na stori nyingi za kimbea mtandaoni ambazo zinaongelea kufeli kwa mahusiano ya Wolper na wanaume mbali mbali anaokuwa nao kwenye mahusiano.

Kiukweli kabisa Wolper ni moja kati ya watu waliokuwa na bahati mbaya kwenye mahusiano inawezekana ikawa pia ni wanaume ambao anachagua kuwa nao.

Kwa mwaka Jana pekee Wolper alikuwa kwenye mahusiano na wanaume watatu tofauti ambao ni Harmonize, Brown na Engine.

Lakini hivi sasa Wolper anaweka wazi kuwa mahusiano yake kuvunjika sio yeye mwenye makosa na wala hajawahi kuachwa yeye ndio anaacha kwenye mahusiano.

Wolper amefunguka hayo kwenye mahojiano aliyofanya na The playlist ya Times FM ambapo ameongea Mengi zaidi:

"Kiukweli kabisa naamini kuwa hakuna siku ambayo Ex wangu hata mmoja ambaye ameshawahi kuja kuniongelea vibaya kwenye interview yoyote kwaiyo kama ningekuwa na matatizo wangekuwa wanakuja kuniongelea vibaya kwaiyo mimi na wao ndio tunajua ukweli kuwa nani ana matatizo lakini pia sipendi sana kuongelea maex ila kikubwa ambacho kipo kwangu sipendi ujinga na sipendi kuonekana mpumbavu kwa sababu mimi ni mzuri najiamini natafuta hela yangu napenda kazi yangu na napenda kuheshimiwa kwaiyo kama ukinizingua nakufuta na by the way sijawahi kuachwa"

Majaji Watatu Kusikiliza Kesi ya ACT Wazalendo Dhidhi ya Jeshi la Polisi

$
0
0
Majaji Watatu Kusikiliza Kesi ya ACT Wazalendo Dhidhi ya Jeshi la Polisi
Mahakama  kuu ya Dar es salaam Aprili 5, 2018 itaanza kusikiliza kesi ya madai ya chama cha ACT Wazalendo dhidi ya jeshi la polisi

Tarifa iiliyotolewa jana  na Afisa Habari wa ACT Wazalendo, Abdallah Khamisi  ilisema kuwa kesi hiyo itasikilizwa chini ya Majaji watatu, Jaji Ferdinand Wambari, Jaji Sameja na Jaji Rose Teemba.

"Machi 18 tulizungumza na umma juu ya hali mbaya ya nchi Kiuchumi, na tukaeleza hatua ambazo kama chama tutachukua katika kutatua masuala kadhaa ya kinchi. 
"Kwenye eneo la DEMOKRASIA tulieleza kuwa tumefungua Kesi ya Madai Na. 8/2018 Mahakama Kuu hapa Dar Es Salaam, kulishtaki Jeshi la Polisi, kutokana na Jeshi hilo kuingilia, visivyo halali shughuli za ziara yetu ya kuhamasisha maendeleo katika Kata tunazoziongoza.

"Leo Mahakama imeipangia tarehe kesi husika, itasikilizwa kwa mara ya kwanza, Aprili 5, 2018 chini ya Majaji watatu, Jaji Ferdinand Wambari, Jaji Sameja na Jaji Rose Teemba."- Ilisema taarifa hiyo

Rosa Ree Akimbilia South Afrika...Aonekana Studio na Msanii Mkubwa Emtee

$
0
0
Msanii wa mkali wa Hip Hop Bongo Rosa Ree ameonekana akipost picha akiwa nchini South Afrika ambapo haijulikani ameenda kufanya nini mpaka sasa ila baadhi ya picha zimeonyesha akiwa na Msanii Mkubwa wa Hip Hip Mwenye Awards Kibao Anayejulikana kama Emtee
Picha hizo zinaonyesha Wakiwa Studio Kitu ambacho kinaonekana ni Bongo la Collabo linapikwa...

Rosa Ree ni Msanii ambae ameweza kuteka watu mbali mbali nje na ndani ya Tanzania kutokana na style yake yakuchana....

Picha zingine zinazoonyesha akiwa South Afrika hizi Hapa chini:


Rosa Ree Akiwa na Don Bambino Director wa Dimo Production


Rosa Ree Akiwa na Meneja wake John Kiandika

FBI Aliyetambua Shambulio la Osama Bin Laden Afariki Dunia

$
0
0
FBI Aliyetambua Shambulio la Osama Bin Laden Afariki Dunia
SHIRIKA la Uchunguzi la Marekani (FBI) limesema limempoteza mwanamama mmoja ambaye ni miongoni mwa waliotambua shambilizi la kigaidi la Septemba 11, 2001 lililofanywa na Osama BinLaden, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 48.




Melissa S. Morrow alifariki juzi Alhamisi akiwa na miaka 48 kwa kansa ya ubongo huku ikielezwa kuwa, huenda kifo chake kilisababishwa na kuwekewa vitu vyenye sumu (kemikali).

Mtaalam huyo wa uchunguzi, amefanya kazi ndani ya FBI kwa miaka 22, na wakati umauti unamfika alikuwa ana siku chache tangu ahamishiwe katika kituo kipya cha kazi, Kansas City.




Taarifa ya FBI imeeleza kuwa, Morrow alikuwa amejitoa kwa kiasi kikubwa kulitumikia taifa lake kwa kuchunguza na kubaini ukweli wa shambulio la Spetemba 11, katika Makao Makuu ya Jeshi la Marekani, Pentagon,.

Inadaiwa mama huyo baadaye alikutwa kwenye  ghala lenye sumu mwaka 2013 jambo lilliloplekea kuzorota wa kwa fya yake  licha ya kutibiwa kwa zaidi ya wiki 10 huku akikusanya taarifa kuhusu shambuilio hilo lililotikisa dunia.


Morrow alijiunga na FBI mwaka 1995 na mazishi yake yatafanyika Country Club Christian Church eneo la Kansas City, Jumanne mchana.

Msiba huo umetokea ikiwa ni wiki moja tu tangu kifo cha aliyekuwa kapteni kwenye kikosi cha uokoaji, Thomas Phelan aliyewaokoa waathirika wa shambulio la September 11 ambaye naye amefariki kwa Kansa akiwa na miaka 45 huko Lower Manhattan.



Thomas Phelan, March 16  ambapo naye anadaiwa kifo chake kimesababishwa na kuwekewa mvuke wa sumu huko Ground Zero.

Ben Pol Kumuoa Ebitoke ?

$
0
0
Ben Pol kumuoa Ebitoke ?Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye inasemekana yupo kwenye mahusiano ya kimapenzi na muigizaji wa vichekesho Ebitoke, amewataka watu kuwa na subira juu ya kujua ukweli uliyopo baina yao kwa madai hakuna jambo linaloweza kufichika milele.


Ben Pol ametoa kauli hiyo baada ya kila kukicha kusumbuliwa na waandishi pamoja na mashabiki zake kiujumla kutaka kujua ukweli juu ya ukaribu wake na mchekeshaji huyo ambaye yeye binafsi anatangaza kuwa yupo kimapenzi na Ben kimapenzi kila aulizwapo na watu.

"Sijawahi kutoka katika mahusiano na Ebitoke yaani kila kitu kipo vile vile hakuna kilichobadilika baina yetu. Siwezi kusema kama nipo kwenye mahusiano naye ila tupo karibu sana", amesema Ben Pol.

Pamoja na hayo, Ben Pol ameendelea kwa kusema "watu wawe wanasubira maana wanauliza sana juu ya hilo lakini mimi ninachoweza kusema watu wawe na subira kila kitu kitakuja kuwa bayana kwasababu hakuna kitu kinachowez kuwa siri milele au kukwepeka kila siku. Wanachotaka kukiona watu watakiona tu wenyewe kwa macho yao kwa hiyo wasiwe na haraka kiasi hicho".

Kwa upande mwingine, Ben Pol jana kupitia EATV ameweza kutambulisha rasmi video ya wimbo wake mpya inayojulikana kwa jina la 'natuliza boli' ambayo mpaka sasa inaendelea kufanya vizuri katika mtandao wake.

Diamond amtaka Lulu Diva kumzalia mtoto Rich Mavoko

$
0
0



Baada ya kukanusha kwa muda mrefu, hatimaye imebainika kuwa Rich Mavoko na Lulu Diva ni wapenzi.

Aliyeweka wazi hilo ni Diamond Platnumz ambaye anafanya kazi na Rich Mavoko kupitia label yake ya WCB. Katika kumtakia kheri ya siku ya kuzaliwa Lulu Diva, Diamond amemwandika haya mrembo huyo.

We @luludivatz nae Utulete Mtoto sasa, Tushachoka picha zenu za Kuviziwa kwenye ma Parties😏👌🏼#AfricanBeauty

Utakumbuka Fiesta ya Dar es Salaam iliyofanyika November, 2017 kuna picha zilisambaa mtaandaoni zikiwaonyesha Rich Mavoko na Lulu Diva katika mapozi ya kimahaba ingawa wenyewe walikanusha na hilo pia ila kwa kauli hii ya Diamond ni wazi lilokuwa likisema lipo.

Amber Rose Atokwa Povu Kisa Mwanaye

$
0
0
Amber Rose Atokwa Povu Kisa Mwanaye


MWANAMUZIKI Amber Rose, amejikuta akitokwa povu la kutosha baada ya njemba mmoja kumkashifu mwanaye mwenye umri wa miaka mitano, Sebastian kupitia Mtandao wa Kijamii wa Twitter, kwamba anatabia za kishoga.



Kashfa hizo kwa Sebastian ambaye Amber Rose amemzaa pamoja na rapa Wiz Khalifa, zilifuata baada ya Amber Rose kutupia mtandaoni video ikimuonesha Sebastian akifungua zawadi na kumkabidhi mwanamuziki Taylor Swift, ambapo katika zawadi hiyo kulikuwa na tiketi mbili kwa ajili ya ziara za kimuziki anazotarajia kufanya Taylor.



Njemba huyo aliandika hivi;“Ukimuangalia mtoto huyo,anavyoongea, anavyotenda lazima utaelewa tu hawezi kuwa mwanaume sawa!”Baada ya komenti hiyo baadaye Amber naye alijibu mapigo kwa kusema; “Huwezi kusema motto wa miaka mitano anajihusisha na ushoga. Hata hivyo mtoto wangu si wa jamii, atabaki kuwa wangu na lazima maneno mengi yasemwe kwa sababu ni wa kipekee zaidi.”

Wanaume Wananifanya Nibadili Laini Mara 7 kwa Mwezi – Diva

$
0
0
Wanaume Wananifanya Nibadili Laini Mara 7 kwa Mwezi – Diva
Mtangazaji maarufu wa kituo cha Clouds FM, Diva The Bawse amedai kuwa baada ya kumwagana na aliyekuwa Boyfriend wake Heri Muziki amekuwa akipata usumbufu kutoka kwa wanaume hadi inakuwa kero.


Diva

Akifunguka kwenye mahojiano yake na Bongo5, Diva amesema kupitia simu yake ya mkononi amekuwa akipata meseji zaidi ya 2,000 na zote kutoka kwa wanaume wengi wakimtongoza, kitu ambacho kila mwezi kinamfanya abadilishe laini zake mara saba.

“Maisha ya kuwa single ni mazuri ingawaje nimekuwa nikipata usumbufu mkubwa kwenye simu yangu yaani napata meseji zaidi ya 2,000 na zote kutoka kwa wanaume, kitu ambacho kinanipa wakati mgumu kwani wananifanya nibadili laini mara saba kwa mwezi,“amesema Diva.

Mbali na usumbufu huo, Diva amesema kuwa kwenye ukurasa wake wa Instagram pia amekuwa akikumbana na usumbufu kama huo DM.

Kwa sasa mrembo huyo amesema kuwa ameshapata mwanaume ambaye ndiye anaamini kuwa atakuwa baba watoto wake siku za usoni ingawaje amekataa kumuweka wazi kwa sasa.

Kwa upande mwingine Diva ametangaza kuachia albamu yake mwaka huu ya ‘ALA ZA ROHO’ ambayo itakuwa na mastaa kibao kutoka nje ya nchi.

Hivi Ndivyo Daimond, Dogo Janja Wanavyowatesa Mama Wema , Mama Irene Uwoya

$
0
0
Hivi Ndivyo Daimond, Dogo Janja Wanavyowatesa Mama Wema , Mama Irene UwoyaNDOA au uhusiano wa mapenzi bila shaka ni jambo la kheri ambalo kila mmoja wetu hupenda watu wanaomzunguka kufurahia chaguo lake na kumpa Baraka anazostahili.



Hivyo ndivyo ilivyo kwa watu wengi, lakini tofauti kwa mastaa wa fi lamu Irene Uwoya pamoja na Wema Sepetu, ambao uhusiano wao umekuwa ni jambo lisilokubalika kwa wazazi wao kwa msemo rahisi unaweza kusema paka na panya, huku wakiamini kwamba wapenzi walionao hawawastahili.


Kwa upande wa wawili hawa zilianza kama tetesi kwamba wanatoka kimapenzi lakini baadaye wakaibuka na ndoa kabisa na kuhalalisha tetesi za ‘kumegana’ kisela.Hata hivyo toka wadai kufunga ndoa, kwa upande wa mama mzazi wa Uwoya, ameonekana dhahiri hamkubali hata kidogo Dogo Janja.

Mara kwa mara akihojiwa na waandishi wa habari amekuwa akikanusha juu ya kuitambua ndoa hiyo na kusema mwanaye hajafunga ndoa kwani hajahusishwa pamoja na maneno mengine ya kumponda Dogo Janja.Ambapo kutokana na maneno hayo inawezekana


Wema akiwa na Mama yake

kabisa hata akiwa anasali, mama Uwoya pengine huomba Mbongo Fleva huyo amuache mwanaye.Lakini kwa Uwoya inaonekana hasikii wala haambiliki. Kwa upande wa mahaba, kwa Dogo Janja ndiyo amefi ka Kigoma mwishowa reli na kama kuongea, ameamua kumuacha mama yake azungumze tu lakini anasonga mbele.



WEMA SASA NA DIAMOND!

Kama ilivyo kwa mama yake Uwoya,kwa upande wa mama Wema ndiyo hataki kabisa kumsikia Diamond. Si mara moja wala mbili mama Wema kuibuka na kuanza laivu Diamond,kwamba hamfai mwanaye na si mtu sahihi, wakati mwingine amekuwa mpaka akimkashifu kwa kumuita ‘domo’ japokuwa Wema mwenyewe amekuwa akiingia naye kwenye uhusiano na kutoka



Sasa pamoja na hayo jiulize Wema breki zinakaba kwa Diamond? Jibu ni kwamba hapana!Maana ingekuwa hivyo Wema angekuwa mbali na Diamond kimahaba, kwani tetesi mpya mjini kwa sasa ni kwamba wawili hawa wanatoka tena kimapenzi baada ya kumwagana kipindi cha nyuma.



Sasa ili watu hawa wanne wapate furaha na Baraka kutoka kwa wazazi wao ninashauri ni muhimu kutazama pia suala hili kwamaelewano kati ya wapenzi wao na mama zao.Ikiwezekana hata kukaa chini na wazazi wao na kuzungumza juu ya maisha yao ya uhusiano maana katika suala la kupenda kila mtu ana uhuru wa kupenda na kupendwa.



Kama ni machaguo yao sahihi na wakizungumza vyema na wazazi wao bila shaka atawaelewa na kuwapendapia. Zaidi watawapa baraka katika uhusiano huo na kuwatakia kheli kwani raha ya uhusiano ni watu wenu wakaribu kufurahia uhusiano huo na kuishi nanyi vizuri.

Miujiza ya Sharifu Seif Mohamed..JE Umeachwa na Mme/Mke au Mpenzi, Umesongwa na Mitihani ya Maisha

$
0
0

SHARIFU SEIF MOHAMED ANAWASHUKURU WALE WOTE WANAOENDELEA KUPIGA SIMU, WENYE MATATIZO NA WALE WANAOTOA  SHUKRANI NA SHUHUDA JINSI TIBA ZAKE ZINAVYO WASAIDIA,

(Rudisha mahusiano yako ndani ya masaa 72 tu)

SHARIFU MOHAMED Ni  mtaalam na mnajimu maarufu wa nyota na kubashiri mambo yanayo watesa binadamu duniani kote na kupata ufumbuzi, Anatumia kitabu cha QUR'AN na Nyota

Je Umeachwa na UMPENDAE awe Mme/Mke na bado unampenda? Je Umekimbiwa na Mmeo/ Mkeo n anaishi na mtu mwingine? Je Umejaribu sehemu nyingi bila mafanikio? Mpigie simu SHARIFU SEIF sasa hivi ujionee Muujiza wa Papo kwa Papo, Anauwezo wa hali ya juu wa kusambaratisha mahusiano yao na kumrejesha kwako haraka sana na Kumfanya Atimize Ahadi zote Ndani ya Muda Mfupi Endapo Utafwata Atakacho Kuelekeza

 ZINDIKO LA NYUMBA NA BIASHARA, PETE ZA BAHATI, HUMALIZA KABISA TATIZO   HUZUIA CHUMA ULETE KWENYE BIASHARA, HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA, NA KUPONYA MAGONJWA SUGU ANAO UWEZO WA KUMRUDISHA ALIE MBALI AU ALIECHUKULIWA MSUKULE, KUPANDISHA NYOTA NA KUSHINDA BAHATI NA SIBU, KASAFISHA NYOTA NA KUKUPA MVUTO WA AJABU, KUTOA NUKSI NA VIFUNGO MBALIMBALI,  MAFANIKIO YA MAISHA NA UTAJIRI BILA MASHARI, NA MENGINE MENGI YA SIRI,

JE UMAHANGAIKA KUPATA MTOTO BILA MAFANIKIO? WASILIANA NA MTAALAMU HUYU KWANI YEYE HUFAULU PALE WOTE WALIPOSHINDWA, PIA UMALIZA KAZI ZILIZO SHINDIKANA NA WATAALAM WENGINE NDANI YA MASAA 24 TU,

(NA ANATIBU KWA NJIA YA SIMU UKIWA NCHI YOYOTE AU MKOA WOWOTE ENDAPO UTAFWATA MAELEKEZO YAKE)

Kwa ushauri na mawasiliano  zaidi Piga SIMU No:

Mobile +255 654-836970
WhatsApp 0622766715 

Nape Nnauye Afunguka Tukio la Kutolewa Bastola

$
0
0

Mb unge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye amezungumzia kitendo cha yeye kutishiwa bastola wakati akitaka kuongea na waandishi wa habari katika hotel ya Protea baada ya Rais Magufuli  kumtengua katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Nape Nnauye amekikumbuka kitendo hicho kilichotokea mwaka 2017.

“Mwaka mmoja uliopita tarehe kama ya leo Mwemyezi Mungu aliniokoa na mdomo wa bunduki wa wanyama wasiopenda haki! Mungu mkubwa, mbegu ya haki haifi!” -ameandika Nape Nnauye

Mbwana Samatta Amtabiria Makubwa Msuva Ligi ya Mabingwa Ulaya

$
0
0
Image result for Mbwana SamattaNyota

Nyota wa Tanzania Mbwana Samatta anayekipiga kwenye klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji amesema anaimani kubwa kwamba Simon Msuva anayechezea klabu ya Difaa El Jadidi atafanya vizuri katika ligi ya Mabingwa Afrika kutokana na uzoefu aliokuwa nao kwa sasa.




Samatta ametoa kauli hiyo kufuatia hatua ya makundi ya mashindano ya Mabingwa Afrika kupangwa ambapo timu anayochezea Winga Simon Msuva kuangukia kundi B ikiwa pamoja na timu ya TP Mazembe, Mouloudia Club D’alger pamoja na ES Setifienne.

"Nimeangalia makundi yote lakini inaonekana kundi lao ndio lenye uzito na kuna mtu nilimwambia hili kundi ambalo wamepangwa kina Msuva sio jepesi lakini kwa sasa Msuva ana uzoefu wa pande zote mbili kwa sababu anacheza katika nchi ya kiarabu kwa hiyo amezoea hali ya soka la kiarabu. Tayari ameshacheza na  AS Vita ya DRC Congo kabla ya hawajaingia kwenye hatua ya makundi na ameshacheza sana Afrika kwa hiyo anafahamu nini kinachotakiwa katika soka la Afrika", amesema Samatta.

Pamoja na hayo, Mbwana Samatta ameendelea kwa kusema "naimani atafanya vizuri kwa sababu kama aliweza kufanya vizuri kwenye mechi ya AS Vita na TP Mazembe basi hata sasa atafanya zaidi pia na kwa timu yake ninavyoiona na mwenendo wao wanaweza kuvuka kwenye hilo kundi".

Kwa upande mwingine, Samatta amesema anatumaini kubwa juu ya Simon Msuva kufanya vizuri katika michuano hiyo kwasababu kwa sasa ameweza kuimudu hali ya hewa ya ubaridi.

Sitokaa Nigombana na Ex wa Mose Iyobo- Aunt Ezekiel

$
0
0
Sitokaa Nigombana na Ex wa Mose Iyobo- Aunt Ezekiel


Msanii wa Filamu Bongo, Aunt Ezekiel ambaye pia ni mpenzi wa Mose Iyobo amesema alikuja kugundua kugombana na mpenzi wa zamani wa Iyobo ‘Mwengi’ ni kitu ambacho hakina maana yoyote.

Muigizaji huyo amesema hata wangeendelea kugombana kusingebadilisha majina ya watoto wao ambao wamezaa na Iyobo na si kitu kizuri kwa watoto hapo baadae.

“Katika vitu ambavyo vilipita nilishaandika nikasema sitakaa nigombane na Mwengi tena kwa sababu nimekuja kugundua ni ujinga mwisho wa siku hata nigombane naye miaka mia yule mtoto wake hawezi kuja kubadilika jina,” amesema na kuongeza.

“Lazima mwisho wa siku ataitwa fulani fulani Iyobo, hivyo hivyo kwa Cookie, kwa hiyo wale tayari ni ndugu halafu sasa hivi mitandao ni mengi baadae wakija kuone mama yangu na huyu walikuwa wanagombana itakuja kuwaletea shida watoto,” Aunt Ezekiel ameiambia Bongo5.

Kwa sasa Aunt Ezekiel yupo mbioni kuachia filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la Mama, katika filamu hii amecheza na mwanae, Cookie.

Mwigulu Awataka Walimu Kutumia Fimbo Kutoa Maadili kwa Wanafunzi

$
0
0
Mwigulu Awataka Walimu Kutumia Fimbo Kutoa Maadili kwa Wanafunzi

Waziri wa Mambo ya ndani, Dk  Mwigulu Nchemba amewataka walimu kuendelea kutoa elimu bora kwa wanafunzi kwa kuwafundisha maadili mema na inapobidi matumizi ya fimbo yatumike.


Akizungumza katika harambee ya ujenzi wa mabweni ya Shule ya Sekondari  Lulumba Wilaya ya Iramba mkoani Singida,  Dk Nchemba amesema walimu wanatumia fimbo kunyoosha nidhamu za wanafunzi ili kutengeneza hatma ya nchi.

"Kuna wakati walimu wananyoosha nidhamu za wanafunzi lakini kuna watu wengine hawaoni haya ila wao ni kulalamika tu, kinachofanyika ni kwa manufaa yetu. Niwaombe kwenye kutumia mifano tumieni mifano na kwenye kutumia fimbo fanyeni hivyo ili kutengeneza taswira ya nchi yetu," amesema Dk Mwigulu.

Amesisitiza kuwa ni lazima kuendelea kulinda hadhi za walimu kwa kuwapatia miundombinu bora ya ofisi na vyumba vya madarasa.

Mbali na hayo Dk. Nchemba ameongeza kwamba majengo ya taasisi yanapaswa kuwa bora zaidi na sio kutumia ramani za awali pekee kwani zinapaswa kuboreshwa kulingana na maendeleo yaliyopo.

"Naunga mkono ujenzi huu wa mabweni ya wanafunzi, ukarabati wa vyumba vya madarasa na ofisi za walimu hivyo nachangia mifuko 200 ya saruji nawaahidi pia kutoa Sh milioni sita," alieleza.

Mungu Aliniokoa na Mdomo wa Bunduki wa Wanyama Wasiopenda Haki- Nape Nnauye

$
0
0
Mungu Aliniokoa na Mdomo wa Bunduki wa Wanyama Wasiopenda Haki- Nape Nnauye

Leo March 24, 2018 Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye amezungumzia kitendo cha yeye kutishiwa bastola wakati akitaka kuongea na waandishi wa habari katika hotel ya Protea baada ya Rais Magufuli  kumtengua katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Nape Nnauye amekikumbuka kitendo hicho kilichotokea mwaka 2017.

“Mwaka mmoja uliopita tarehe kama ya leo Mwemyezi Mungu aliniokoa na mdomo wa bunduki wa wanyama wasiopenda haki! Mungu mkubwa, mbegu ya haki haifi!” -ameandika Nape Nnauye


Nape Moses Nnauye

@Nnauye_Nape
Mwaka mmoja uliopita tarehe kama ya leo Mwemyezi Mungu aliniokoa na mdomo wa bunduki wa wanyama wasiopenda haki! Mungu mkubwa, mbegu ya haki haifi!

9:51 PM - Mar 23, 2018

Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images