Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live

Tamasha la Mwanamuziki Harmonize Lazua Gumzo Rwanda

$
0
0

Usiku wa kuamkia jana Jumamosi msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Harmonize alikuwa nchini Rwanda ambapo ilikuwa ni mara yake ya kwanza kutumbuiza nchini humo kwenye tamasha la uzinduzi wa lebo ya muziki ya The Mane.

Tamasha hilo ambalo limefanyika mjini Msanze liliibua gumzo nchini Rwanda baada ya kwenda tofauti na muda uliotangazwa awali.

Tamasha hilo ambalo limefanyika wilaya ya Msanze nje kidogo ya mji wa Kigali lilitakiwa kuanza saa 8:00 mchana hadi saa 12:00 lakini cha kushangaza muda huo kwenye viwanja vya tamasha kulikuwa na watu wachache huku waandaji wa tamasha wakikaa kimya bila kutoa taarifa yoyote ile.

Moja ya watu waliyohudhuria kwenye tamasha hilo ambaye pia ni mtangazaji wa kituo cha redio cha Isango FM cha Mjini Kigali, Janvier Popote amesema kuwa hali hiyo ilizua taharuki huku watu wengi nje ya viunga hivyo wakilalamika kuhujumiwa.

“Nilifika majira ya saa 9:00 mchana nilikuta watu wachache ingawaje ndio muda uliyotajwa. Kuna watu walianza kupatwa na hofu na wengine wakilalamika kuwa wamehujumiwa. Lakini cha kushangaza ilipofika saa 1:20 usiku watu wakaanza kufurika kwenye viwanja vya tamasha japokuwa muda uliyokuwa umepangwa kwa ajili ya tamasha ulikuwa umeisha,“amesema Janvier.

Hata hivyo, moja ya waandaaji wa tamasha hilo amekataa katu kuelezea sababu ya tamasha hilo kuchelewa kuanza.

kwa upande mwingine mashabiki na wadau wa muziki nchini humo wamesema kuwa tamasha hilo lilipangwa muda mbaya kwani masaa yaliyotajwa yalikuwa masaa ya kazi.

Hali hiyo pia imejitokeza kwenye show nyingine jana ambapo kama kawaida ilichelewa kuanza kitu ambacho kimezua gumzo kwa wadau wa muziki nchini humo, kwa madai kuwa mapromota wa muziki nchini Rwanda hawapo makini kwenye muda jambo ambalo linakera na linaweza kupelekea vurugu jukwaani.

Kwa upande mwingine, ilipofika saa 2:00 usiku tamasha hilo lilianza rasmi ambapo wasanii lukuki kutoka Rwanda akiwemo Marina, King James, Riderman, Christopher, Jay C, Queen Cha na wengineo.

Harmonize ndiye aliyekuwa msanii wa mwisho kupanda kwenye jukwaa hilo ambapo alitumbuiza nyimbo zake zote.

Serikali Yawataja Wanafunzi wa Vyuo Vikuu kuwa ndio Wanaongoza Kutukana Mitandaoni

$
0
0

Serikali imesema wanafunzi wa vyuo vikuu wanaongoza  kutukana na kutumia lugha zisizo na maadili kwenye mitandao ya kijamii.

Angalizo hilo limetolewa na naibu waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha  Jumamosi Machi 24, 2018 katika hafla fupi ya uzinduzi wa Unilife Compus iliyopo Mkoa wa Kilimanjaro uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Mwenge na kuvikutanisha vyuo vikuu vyote vya mkoa huo.

Alisema  yapo mambo matatu ambayo yanachangia wanafunzi kutofanya vizuri, yakiwamo matumizi mabaya ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), anasa na starehe zilizopitiliza na kujiingiza kwenye siasa ambazo zinawanyima fursa ya kusoma vizuri.

“Serikali imebaini mambo yanayochangia kufifisha na kudidimiza jitihada za elimu tunayoitoa kuonekana bure. Kuna vitu ambavyo siyo vizuri  vinaendelea katika vyuo vyetu, ndizo changamoto tunatakiwa kukabiliana nazo. Chuoni unaweza kutengeneza au kuharibu maisha yako,” alisema.

Naye mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira alisema  wanafunzi wengi hawataki kujifunza  kwa kutumia muda vizuri kwa kusoma vitabu.

"Tunabaki kuwa waigaji wa dhana za wenzetu wa magharibi, hatutaki kujifunza vitu vipya bali vilevile vya wenzetu vinatumika hadi leo. Wasomi wa Tanzania tunajishusha kwa sababu ya kushindwa kuleta mawazo mapya kwenye sekta ya elimu na afya," alisema  Mghwira.

Mkuu wa KKKT: Hatutakubali Kunyamazishwa -Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya March 26

Pwani: Majambazi Yafunga Barabara na Kuteka Magari, Wawili Mbaroni

$
0
0

JESHI la polisi mkoani Pwani, linawashikilia watu wawili wanaodaiwa kuwa ni majambazi kati ya kundi la majambazi zaidi ya sita ambao waliteka magari na kupora mali mbalimbali za watu eneo la Kwang’andu ,Mbwewe barabara ya kuelekea Wami.

Kamanda wa polisi mkoani Pwani,(ACP) Jonathan Shanna alisema tukio hilo limetokea machi 24 saa 8.30 mchana .

Akizungumzia tukio hilo la unyanga’anyi wa kutumia silaha ,alieleza majambazi zaidi ya sita waliteka magari kwa kukata mti kwa msumeno kisha kuziba barabara na kuvamia magari mbalimbali ya wananchi kisha kuwapora mali zao na kuharibu baadhi ya magari yao.

Aidha kamanda Shanna alisema, watuhumiwa wawili wapo mbaroni kupisha uchunguzi.Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Saidi Salim (26) na Nyangwesa Nyangwesa.

Kamanda Shanna aliwataja na wananchi /wasafiri walioharibiwa na kuporwa mali zao akiwemo Peter Kilango, ambae aliporwa simu aina ya techno C9 na gari lake kuharibiwa kioo cha mbele upande wa dereva.

Viatus Bahati aliporwa Lap Top Dell, Usd 900.00 , shilingi 700,000 na pochi yenye document mbalimbali na Imail Meshileki alieporwa simu aina ya Tecno ,na sh .800,000 na gari lake  T.953 BXN Toyota Prado ambayo waliiharibu kioo cha nyuma.

Kamanda Shanna alimtaja mwingine ni Jackson Omary aliyeporwa Tsh.70,000 na begi lenye nguo mbalimbali na Denis Mwavano aliporwa simu Tecno C9.

Jeshi la polisi mkoani humo limekemea vitendo vya kiuhalifu na kuteka magari kwani kwa kufanya hivyo watakula nao sahani moja ,na wale waliofanikiwa kukimbia wataendelea kusakwa

Waraka wa Maaskofu KKKT Wajibiwa.....Soma Hapa Tamko la Watetezi wa Rasiliamli wasio na mipaka (WARAMI) Wakiupinga Waraka Huo

$
0
0

JANA tuliona katika mitandao ya kijamii waraka wa viongozi wetu wa dini,ukizungumzia masuala mbali mbali ya nchi na mwelekeo wake huku sehemu kubwa ya waraka huo ukijikita katika kuikosoa serikali juu ya namna inavyoendeshwa.

Tunafahamu viongozi wa dini wana wajibu wa kiutumishi katika jamii huku wakilinda dhamira yao ya kuhakikisha umoja wa nchi yetu unabaki kuwa salama kwa namna yoyote ile.

Inapotokea mazingira yoyote ya viongozi wetu wa dini kushindwa kusimamia wajibu huo jamii inayoongozwa na viongozi hao inapaswa ijisimamie yenyewe na kuwakumbusha wajibu wao huo

Sisi  Watetezi wa Rasiliamli wasio na mipaka (WARAMI) tunaamini kuwa moja wa wajibu wetu ni kuhakikisha  Jamii inapatiwa haki hiyo pasipo upendeleo wa aina yoyote ule wa kiimani, kisiasa kanda au hata kiukabila

Kwa vyovyote vile tunaona ni sahihi kwa sasa nasi kupaza sauti yetu kwa jamii ili pamoja na viongozi wetu hawa wa dini wakiwemo maaskofu wa KKKT tuone ni namna gani bora ya kuishi katika jamii ambamo watu wake wamechanganyika kwa utofauti tofauti  baina ya dini, kabila, jinsia, ufuasi wa kiitikadi na kadharika

Tunatumia nafasi hii kuwakumbusha viongozi wetu wa dini wajitafakari kwa umakini na kuanza kuchagua aina ya maneno ama kauli sambamba na njia wanazotumia ili kutokuleta taharuki kwa jamii hasa wakizingatia ukweli kwamba mara nyingi sio kila maoni wanayoona wao yanafaa basi kwetu sisi waumini wao pia yanafaa kwa maana tuyafuate kama yalivyo.

Miongoni mwa masuala yaliyoandikwa katika waraka ule wa maaskofu wetu ni malalamiko kuhusu Katiba Mpya, Uhuru wa kutoa maoni, Usawa katika elimu, mauaji ya watu, uchumi Demokrasi, kodi kwa wafanyabiashara na ajira kwa vijana kwa kuyataja kwa uchache.

WARAMI, tunashangaa ni kwanini waraka huu wa salamu za PASAKA haukujikita zaidi katika kuwasisitiza waumini wake kujikita katika kuabudu, kumnyenyekea Mungu, kusoma bibilia na maandiko mengine ya dini na badala yake wakajikita katika maoni yanayong’ata na kupuliza

Watanzania wote ni mashahidi kuwa kwa sasa nchi yetu imejitanabaisha katika kutatua changamoto zilizokuwa zinaimbwa kila siku na wanasiasa hasa wa upinzani na kwa kweli tumeanza kuyaona matunda ya serikali kujikita katika kutatua changamoto hizo

Sote ni mashahidi kuwa Kuilazimisha Serikali kuitisha mchakato upya wa katiba ni jambo ambalo haliingii akilini kwa sasa kutokana na ukweli kwamba ni wanasiasa wenyewe hususan wa vyama vya upinzani ndio waliosusia na kukwamisha mchakato wa katiba kwa kutaka kulazimisha mawazo yao yawe bila kuzingatia msingi mama wa Demokrasia kuwa wachache wanasikilizwa wengi wanashinda.

Maaskofu wetu wamekazana kulalama kuhusu katiba mpya huku waumini wake wanaotuongoza hawana ufahamu kuhusu BIBILIA

Aidha, tumeona hivi karibuni namna Rais wa nchi alivyozungumza na jumuiya ya wafanyabiashara na kuweka wazi changamoto zote zinazowakabili wafanyabiashara ikiwemo suala la kodi na kuweka mkakati wa pamoja kulitatua, sasa kuendelea kulalamika kwenye hili hakuna tofauti na nongwa kwa kuwa hata muda alioutoa Rais kwa watendaji wake haujakwisha.

Maaskofu wetu wamezungumzia kuhusu utekwaji na mauaji ikiwemo utiaji wa hofu lakini hawajajikita kuelezea kwa kina hasa ni yepi?,

Sisi tunafahamu kuwa wapo watu walioathirika moja kwa moja na matukio ya kutekwa na kuteswa kwa vijana kama Mussa tesha wa Igunga, Joseph yona wa Temeke, Halidi Kagenzi wa CHADEMA na wengineo yalipaswa kukemewa tangu siku ya kwanza ya kutokea kwake na si kuyasubiri mpaka leo.

Tunawashangaa maaskofu wetu hawa kusema kuhusu usawa wa elimu huku wakifahamu kuwa wanamiliki chuo kikuu ambacho hivi karibuni kilipandisha ada ya masomo na Askofu mkuu alipoombwa kushusha ada akamwamuru mlinzi afungue geti na anayetaka alipe asome asiyetaka mlango uko wazi atoke, nafikiri Usawa wa elimu ulipaswa kuanza katika chuo kinachomilikiwa na KKKT na si vinginevyo.

Maaskofu wetu wanajaribu kutuaminisha kwamba wao ni wasafi na kila wanachozungumza ni sahihi je wanadhani wapo wasafi kiasi cha kuwa tayari kuchunguzwa na kuwekwa hadharani kuhusu Uhalali wa makanisa yao?.

Je maaskofu wetu hawa ni wasafi kiasi cha kuwa tayari kuchunguzwa matumizi ya mabilioni ya sadaka wanayokusanya kila siku?.

Ama maaskofu hawa wanaweza kuueleza umma kuhusiana matumizi ya misaada, misamaha ya kodi wanayopaswa kulipa na matumizi ya kodi hizo walizosamehewa na serikali.

MAASKOFU WETU WANATUMIKA?

Hatutaki kuamini kwamba viongozi wetu hawa wanatumika na wanasiasa kwa maslahi yao ama ya wanasiasa lakini nafikiri tunapaswa kufikiri sawa kwenye hili kwa kujijibu maswali machache yafuatayo?
Ikiwa waraka huu wa Maaskofu wetu umesainiwa tarehe 15-03-2018, kwanini umetoka leo na si kipindi ulipoandaliwa ama siku ya ibada kama inavyokuwa kawaida ya siku nyingine?
Kwanini waraka huu umetolewa siku moja baada ya waraka wa Mwenyekiti wa CHADEMA Mheshimiwa Freeman Mbowe ambao kimsingi maudhui yanafanana kiasi cha kutia shaka kuwa umeandaliwa na mtu mmoja na maaskofu kushirikishwa kuweka majina yao tu?
 Kwanini waraka huu wa Maaskofu umesambazwa kwa mara ya kwanza na kiongozi wa CHADEMA ambaye pia ni mjumbe wa kamati kuu wa chama hicho mheshimiwa LEMA ambaye ndiye aliusambaza Waraka wa Mbowe katika muda unaofanana na njia zinazofanana?.
Ukijijibu maswali hayo hapo juu unaweza kupata picha halisi

WITO

Tunatoa wito kwa Maaskofu wetu kujikita katika masuala mahsusi yanayohusu Dini, watuelimishe kwenye dini, wamuachie Kaisari yaliyo yake nay a Mungu yaliyo yake
Tunawaomba maaskofu wetu wachague njia sahihi ya kupita kama walivyofanya wenzao waliowatangulia. Wapo viongozi wa dini walipoona wana wito wa kushiriki Siasa waliamua kuachana Upadri na Uaskofu na kujikita kwenye siasa

Mrisho Ngambo Afunguka Alivyoumizwa na Godbless Lema, Ataja Maandamano ya Mange Kimambi

$
0
0

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo amefunguka na kuwaomba viongozi wa CHADEMA jijini humo akiwepo Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema pamoja na Meya wa Jiji la hilo, Calist Lazaro kushirikiana na serikali.

Mrisho Gambo amesema hayo baada ya jana Machi 24, 2018 viongozi hao wa CHADEMA ambao anadai walikuwa wamealikwa kushiriki katika zoezi la utoaji wa mikopo kwa kina mama kutotokea kwa kuwa zoezi hilo lilikuwa likisimamiwa na serikali.

"Nipenda kutumia fursa hii kuwaomba viongozi wenzangu bila kujali itikadi ya vyama vyao maana leo tulimualika hapa mbunge, Meya na madiwani lakini wakasema tu sisi hatuendi sababu lile jambo linasimamiwa na serikali.

"Mimi nataka tu niwaombe viongozi wenzangu kwamba masuala ya maendeleo hayana vyama kwa sababu na sisi pia tungeangalia vyama pengine tungewaambia watu wa CCM wawape tu mikopo hiyo wanachama wao lakini tukasema sisi wenye serikali watu wetu ni wote bila kujali itikadi ya vyama vyao hivyo niwaombe wakubali kwamba Rais wa Tanzania ni Dkt. John Pombe Magufuli"

Aidha Mkuu huyo wa mkoa amezungumzia suala la maandamano ya April 26, 2018 kwa namna na kusema kuwa wapo watu wanafanya kazi ya kushawishi watu kuandamana lakini wao kama viongozi wanatoa njia za watu kupambana na maisha.

"Wakati wao wanahamasisha watu waandamane sisi tunawapa mbinu za kupambana na maisha, wakati wao wanahamasisha waandamane sisi tunawagea mitaji ili waweze kupata ridhiki na familia zao, wakati wao wanahamasisha waandamane Dkt John Pombe Magufuli anatoa elimu bure kwa shule zote nchi nzima" alisema Gambo.

Mwanadada Mange Kimambi ni kati ya watu ambao wapo mstari wa mbele kushawishi Watanzania kote nchini kupitia mitandao ya kijamii kuandamana April 26, 2018 ili kudai haki zao.

Pata Huduma za Matibabu ya Asili na Nyota Pamoja na Pete za Bahati

$
0
0

Mtabibu Mongwa husafisha nyota na kutoa Pete za bahati na kwawale walio sumbuka kwaajili ya matibabu na hawakufanikiwa chochote sasa njoo ujionee miujiza hapo kwahapo bila malipo yoyote malipo baada yakazi napia humpa mtu jini la mali kwayule anaye taka kumiliki bila mashariti yoyote
Tunatibu magonjwa mbalimbali yaliyo shindikana mpenzi aliye kukimbia nakumrudisha kwa masaa 24 tu napia natoa dawa za nguvu za kiume kuurefusha uume paka pale unapotaka .

Natoa dawa za biashara na mvuto ==tunatoa dawa zauzazi kwa wale kina mama wenye matatizoya uzazi walio angaika kwa muda mrefu bila kupata mafanikio yoyote njoo umalize tatizo lako sasa
Natoa mazindiko yanyumba na mwili biashara na mvuto kazini

Kupandisha nyota ili kungaa kupandishwa cheo kazini kurudisha mali zilizo pote zilizo ibiwa kuzulumiwa
Kesi zilizo shindikana uzimaliza mara moja namengine mengi ya siri piga simu

+255 764291657 

Diva Atoa Darasa Huru kwa Watanzania Wanaolalamika ‘Vyuma Vimekaza’ (video)

$
0
0

Mtangazaji wa kituo cha Redio Clouds FM, Diva ametoa darasa huru kwa Watanzania wanaolalamika kuwa vyuma vimekaza ambapo kwa upande wake amesema kuwa yeye maisha yake yapo vizuri kama ilivyokuwa zamani.

Akizungumza na Bongo5 amedai kuwa watu wengi hususani wanawake wanaolalamika vyuma kukaza ni wale ambao zamani walizoea kuhongwa lakini kwa wale wanaofanyakazi halali kama yeye haoni tofauti yoyote maisha ya sasa na ya zamani.

Akitoa ushauri amesema huu ni muda kwa watanzania kujifunza kutumia hela vizuri kwa kuzingatia matumizi muhimu na kuacha matumizi yasiyo na umuhimu

Profesa J aamua Kuwasamehe Waliomsaliti Wakati wa Kampeni

$
0
0

Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Joseph haule maarufu kama Prof. Jay, amesema kwamba ameamua kuwasamehe wasanii ambao walimsaliti wakati wa kampeni za yeye kuingia Bungeni, kwa kujitol.

Prof. Jay amesema kwamba ameamua kufanya hivyo kwani ameona ni jinsi gani wasanii wamekuwa hawana umoja, hivyo sio vema kwa yeye kuwabagua kwa itikadi za vyama japokuwa walimpinga wakati wa kampeni za ubunge, kwa kuwa wanahitaji umoja ulio thabiti kwa ajili ya maslahi yao.

Prof. Jay ameendelea kwa kusema kwamba matatizo mengi wasanii yanawakuta kwa kuwa hawana umoja thabiti, huku wengine wakiwa na ubinafsi, hivyo ni jambo ambalo linatakiwa kukomeshwa kwa manufa yao wenyewe.

Waziri Mkuu Awaasi Wafanyabiashara Kukopa Mitaji Kwenye Taasisi za Kifedha

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wafanyabiashara wilayani Ruangwa kutumia taasisi za kifedha kukopa fedha kwa ajili ya kukuza mitaji yao.

Ameyasema hayo leo (Jumapili, Machi 25, 2018) wakati akizungumza na wafanyabiashara wa wilaya hiyo katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Chama Cha Walimu, wilayani Ruangwa.

Waziri Mkuu ambaye yuko wilayani Ruangwa kwa ziara ya kikazi ya siku mbili amesema ni vema wakatumia taasisi za kifedha zilizopo ili kukuza mitaji yao.

”Naamini sekta ya biashara ni muhimu katika mabadiliko ya maendeleo, hivyo wafanyabiashara ni chachu ya maendeleo kokote na Serikali itaendelea kuwaunga mkono.”

Amesema katika kuhakikisha riba zinapungua, Rais Dkt. John Magufuli anaendelea kuzungumza na wamiliki wa taasisi za kifedha ili waone namna ya kupunguza riba hiyo.

Waziri Mkuu amesema lengo la Serikali la kuchukua hatua hiyo ni katika kutekeleza mkakati wake wa  kuwawezesha wafanyabiashara ili waweze kupata mikopo yenye riba nafuu.

Pia Waziri Mkuu amewahakikishia wananchi wa wilaya hiyo kwamba Serikali ipo pamoja nao na imedhamilia kuboresha huduma mbalimbali za jamii kama maji na afya.

Naye, Mwenyekiti wa Umoja wa Wafanyabiashara wa Wilaya ya Ruangwa, Bw. Said Shea amewaomba wafanyabiashara wenzake watumie fursa za maendeleo zilizoko wilayani humo kwa kupanua wigo wa biashara zao.

Watekaji Boko Haram Wamnga'nga'nia Binti Mmoj, Kisa?.......Soma Zaidi

$
0
0

Kundi la kigaidi la Boko Haram limeendelea kumshikilia msichana mmoja kati ya wasichana 111 waliotekwa katika shule ya bweni eneo la Dapchi nchini Nigeria.

Mkuu wa jeshi la polisi nchini humo amesema kuwa wanaendelea kufanya mazungumzo na kundi hilo na kwamba limeahidi kumuachia msichana huyo hivi karibuni.

Leah Sharibu, msichana mwenye umri wa miaka 15 hakuwa miongoni mwa wasichana 105 walioachiwa na kundi hilo Jumatano.

Imeelezwa kuwa msichana huyo aliendelea kushikiliwa kwa sababu alikataa kubadili dini yake kuwa muislam, kwa mujibu wa mama yake.

Aidha, wasichana wengine watano waliotekwa na kundi hilo wanaaminika kuwa walifariki walipojaribu kutoroka mikononi mwa magaidi hao.

Mkuu wa jeshi la polisi, Jenerali Muhammed Abubakar amesema kuwa ameahirisha ziara yake katika eneo la Dapchi ili asiingilie mpango wa makubaliano ya kuachiwa kwa msichana huyo.

Rais Magufuli Atuma Salamu Kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Kufuatia Vifo Vya Watu 26

Hafla Kubwa Kufanyika, Magufuli Kupokea Magari 181 ya Kusambazia Dawa Nchini

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kesho Machi 26, 2018 anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kupokea magari 181 ambayo yatakuwa yakitumika kusambaza madawa vijijini na mjini.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas imeweka wazi kuwa Rais Magufuli ndiye atakuwa mgeni rasmi na kuzindua magari hayo 181 yaliyopo chini ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD).

"Mageuzi Sekta ya Afya yanaendelea, usikose hafla ya kupokea magari mapya 181 kufikisha dawa na vifaa tiba zaidi mijini na vijijini" alisema Dkt Abass

Maboresho Katika Application ya Udaku Special.... Download Upya Kwenye Simu yako Kupata Habari Zetu Haraka

Hivi Ndivyo Amber Lulu Alivyokula Bata na Prezzo

$
0
0
Image result for prezzo na amber lulu



MWANADA-SHOSTI wa Bongo Fleva, Lulu Eugen ‘Amber Lulu’ amefunguka kuwa aliinjoi kinoma alipokuwa faragha na mpenzi wake ambaye ni mwanamuziki wa Kenya, Jackson Makini ‘Prezzo’.

Akichonga na Over Ze Weekend, Amber alisema kuwa, alishawahi kuwa kwenye uhusiano na wanaume tofauti, lakini kwa upande wa Prezzo ndiye pekee aliyemfurahia alipokuwa naye kwenye sita kwa sita.

“Kwa kweli nilipokuwa na Prezo kunako sita kwa sita niliinjoi sana tofauti kabisa na wanaume wengine,” alisema.

Bethidey Yamtokea Puani Dada wa Alikiba Akwaa Ugonjwa wa Kumlaza

$
0
0
Bethidey Yamtokea Puani Dada wa Alikiba Akwaa Ugonjwa wa Kumlaza
PATI ya bethidei ya dada wa staa wa Afro-Pop, Ali Kiba, Zabibu Kiba aliyofanya juzikati imemtokea puani baada ya kukwaa ugonjwa wa kumlaza kitandani.

Akizungumza na Over Ze Weekend, Zabibu alisema kuwa, wageni waalikwa waliohudhuria kwenye bethidei yake walimmwagia maji mengi bila kupumzika ambayo yalimsababishia ugonjwa wa kifua na kwenda hospitali kuchomwa sindano kutokana na maumivu kuwa makali.

“Unajua baada ya kumwagiwa maji vile, usiku sikuweza kulala kabisa kwa sababu nilibanwa na kifua mno, ilibidi niende hospitalini kuchomwa sindano ili kipoe ndiyo nikapata nafuu kidogo,” alisema Zabibu.

Jacob Zuma Kuburuzwa Mahakamani

$
0
0
Jacob Zuma Kuburuzwa MahakamaniRais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma kuburuzwa mahakamani mwezi Aprili kwa makosa 16 yakiwemo ya kutumia vibaya ofisi wakati akiwa madarakani na ufisadi.

Duru za habari nchini Afrika Kusini kusini likiwemo gazeti la News24 limeeleza kuwa Zuma atafikishwa kizimbani katika Mahakama Kuu mjini Durban tarehe 6 Aprili 2018 kwa makosa 16.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na msemaji wa bodi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini humo, Brigedia Hangwani Mulaudzi amesema kuwa mwishoni mwa wiki hii watawasilisha barua kwa mawakili wa Zuma juu ya wito huo.

Mulaudzi amesema kuwa Zuma atakabiliwa na mashtaka makubwa 16 ambapo rushwa na Matumizi mabaya ya ofisi yanatajwa kuwa ni moja ya mashtaka yaliyopewa kipaumbele.

Imeelezwa kuwa Jacob Zuma alifanya malipo ya risiti 783 kiholela, kwenye ununuzi wa silaha na vifaa vya jeshi nchini Afrika Kusini ambapo inakadiriwa kuwa ametumia mabilioni ya fedha kwenye ununuzi huo.

Mwaka 2012, Zuma aliingia kwenye kashfa nzito baada ya kutengeneza nyumba yake ya kifahari kwa kutumia fedha za serikali, ambapo alitumia zaidi ya dola milioni 25 za kimarekani.

Hata hivyo, kashfa hiyo ilitetewa na baadhi ya wabunge wa chama tawala nchini humo ANC, ambapo walieleza kuwa ukarabati huo ulizingatia vigezo.

Mnamo Februari 14, 2018. Mzee Zuma alitangaza kung’atuka madarakani baada ya shinikizo kubwa kutoka kwa wanachama wa ANC na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa Makamu wake wa Rais, Cyril Ramaphosa.


Hata hivyo, wataalamu wa masuala ya kisiasa barani Afrika wanasema kuwa hatua ya Zuma kufunguliwa mashtaka ni mpango wa chama cha ANC kujisafisha, ili kujiwekea nafasi ya kushinda uchaguzi mkuu ujao wa urais mwakani.

Polisi Yawaonya Watumiaji wa Mitandao ya Kijamii

$
0
0
Polisi Yawaonya Watumiaji wa Mitandao ya Kijamii
Jeshi la Polisi mkoani Mwanza limewaonya watumiaji wa mitandao ya kijamii wanaotumia vibaya mitandao hiyo kwa kufanya uhalifu ikiwemo kuhamasisha maandamano yasiyo halali kuwa kitendo hicho ni kosa kisheria.


Onyo hilo limetolewa jana Machi 24, 2018 na Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Naibu Kamishina, Ahmed Msangi wakati akizungumza na askari waliokuwa kwenye mazoezi mbalimbali yaliyofanyika katika uwanja wa polisi Mabatini mjini humo.

“Nafikiri wote sasa hivi mnafahamu kuna hii mitandao ya kijamii kuna watu wanapeana vihabari vya kwenye mitandao ya kijamii wafanye uhalifu, na uhalifu wenyewe ni wa kufanya maandamano au mkutano usiokuwa na taarifa, na kiukweli umepigwa marufuku,“ameeleza Kamanda Msangi na kufafanua.

“Kuna watu wanafanya fanya hayo kushawishiana, tufanye upelelezi, tuchunguze. Yeyote atayefanya hayo kushawishi tukimng’amua tuweze kumkamata. Tumkamate na tuweze kumhoji wana sababu na nia gani?” amesema Kamanda Msangi.

Hata hivyo, Kamanda Msangi amewaasa wananchi wanaotumia mitandao hiyo vibaya kuacha mara moja kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Kauli hiyo inakuja katika kipindi ambacho kwenye mitandao ya kijamii kuna taarifa za watu kupanga maandamano siku za usoni, kitu ambacho serikali imesema maandamano hayo yapo kinyume na sheria.

Wambura Alia na Serikali Ukiukwaji wa Katiba

$
0
0
Wambura Alia na Serikali Ukiukwaji wa Katiba
Aliyekuwa makamu wa Rais wa shirikisho la soka nchini ambaye amefungiwa kutojihusisha na soka Michael Richard Wambura, ameiomba serikali kuingilia kati kitendo cha uteuzi wa Athumani Nyamlani kuwa makamu wa Rais wa TFF.


Wambura kupitia kwa mwanasheria wake Emmanuel Muga ameeleza kusikitishwa na vitendo vinavyofanywa na shirikisho hilo ambavyo havifuati katiba na ni ukiakwaji wa maadili wa chombo hicho cha Umma. Hivyo ameiomba serikali kuingilia ili kumaliza vitendo hivyo.

''Kamati Tendaji ya TFF imemteua Athumani Nyamlani kuwa Kaimu Makamu wa Rais, kinyume na Ibara ya 34 ya Katiba ya TFF ambayo haitoi mamlaka ya uteuzi kwa kamati Tendaji. Kwa uteuzi wa Bw. Nyamlani, TFF imevunja Ibara (34) a,b,c,d,e,f,g,h,i,j,k,l,m,n,o,p na q ya Katiba ya TFF toleo la 2015'', imeeleza taarifa ya Wambura.

Wakati huo pia Wambura amedai rufaa yake aliyokata kwa hati ya dharura, imecheleweshwa makusudi wakati wajumbe wote wa kamati ya rufaa wapo Dar es salaam huku akieleza kuwa kumekuwepo na ubadilishaji wa wajumbe wa kamati ya rufaa ya TFF bila kufuata kanuni.

Wambura ambaye amewahi kushika nyadhifa mbalimbali kwenye soka nchini ikiwemo ndani ya klabu ya Simba pamoja na chama cha soka mkoa wa Mara, amefungiwa maisha kutojihusisha na masuala ya soka.


Mwigizaji Video za Utupu Adai Alitishiwa Kuhusu Donald Trump

$
0
0
Mwigizaji Video za Utupu Adai Alitishiwa Kuhusu Donald Trump
Mwigizaji wa video za utupu Stormy Daniels, ambaye jina lake halisi ni Stephanie Clifford, amesema alitishiwa na kutakiwa kukaa kimywa kuhusu kufanya tendo la ndoa na Donald Trump mwaka 2006.

Ameambia kituo cha runinga cha CBS News kwamba mwanamume mmoja alifika kwake alipokuwa kwenye maegesho ya magari mjini Las Vegas mwaka 2011.

Mtu huyo ambaye hakumfahamu anadaiwa kumwambia "mwache Trump", kisha akamtazama binti mdogo wa mwigizaji huyo na kuongeza: "Itakuwa aibu sana iwapo jambo litamtendekea mamake."

Bw Trump amekanusha vikali kwamba aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwigizaji huyo.

Mawakili wa Bw Trump wanataka kulipwa fidia ya $20m (£14m) na mwanamke huyo, wakisema alikiuka makubaliano ya kuweka siri ambayo aliyatia saini katika ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2016.

Ameambia kipindi hicho cha Dakika 60, ambacho kilipeperushwa hewani Jumapili jioni, kwamba mwanamume huyo alimjia baada yake kukubali kusimulia kisa chake kwa jarida moja.

"Nilikuwa kwenye maegesho ya magari, nilikuwa naelekea kwenye kikao cha mazoezi niliwa nimembeba binti wangu mchanga," alisema.

"Mwanamume alinijia na kuniambia, 'Mwache Trump. Sahau taarifa hiyo'. Kisha, aliinama na kumtazama binti wangu na kusema, 'Ni msichana mdogo mrembo sana. Itakuwa ni aibu sana iwapo jambo litamtendekea mamake'. Na hivyo tu, akaondoka."

Rais huyo alikuwa kituo chake cha gofu na hoteli cha Mar-a-Lago jimbo la Florida wikendi lakini alirejea White House kabla ya kipindi hicho kurushwa hewani.

Bi Trump hata hivyo alisalia Florida, msemaji mmoja wa White House alisema.

Nini kinadaiwa kutokea 2006?

Bi Clifford aliambia CBS kwamba mara pekee ambapo alifanya ngono na Bw Trump ni wakati alipomwalika kwa chakula cha jioni kwenye chumba chake cha hoteli.

Anasema Bw Trump alimuonesha jarida lililokuwa na picha yake kwenye jalada.

Anasema alilichukua jarida hilo na kumgonga Trump nalo makalioni kama utani.

"Aligeuka na kuteremsha suruali yake chini kidogo, unajua, alikuwa na suruali ya ndani na vitu vingine, na nilimgonga kidogo kidogo kwa utani," anasema.

Bw Clifford anasema ingawa hakuvutiwa kwa vyovyote vile na Bw Trump, alifanya mapenzi naye wakati huo, akisema: "Sikukataa. Mimi si mwathiriwa."

Bw Trump, anaongeza, alikuwa amedokeza kwamba kulikuwa na uwezekano angeshirikishwa kwenye kipindi chake cha runinga cha The Apprentice.

Anasema alichukulia mkutano wao kuwa sawa na "mkutano wa makubaliano ya kibiashara".

Bi Clifford ameambia CBS alipokeza "fedha za kukaa kimya" kutoka kwa wakili wa kibinafsi wa Trump kwa sababu alikuwa na wasiwasi kuhusu usalama wa familia yake.

Amewahi kusema awali kwamba alilipwa $130,000 na wakili huyo Michael Cohen kusalia kimya kuhusu uhusiano wao huo kabla ya uchaguzi mkuu wa 2016.

Bw Cohen alithibitisha Februari kwamba alimlipa mwanamke huyo lakini hakusema alimlipa kwa niaba ya nani.

Wakosoaji wa Bw Trump wamedokeza kwamba kuna uwezekano pesa hizo zilikuwa sehemu ya mchango wa pesa haramu za kampeni.

Bw Cohen alisema mwezi jana kwamba Bw Trump na kampuni yake ya Trump Organization hawakuhusika katika kulipwa kwa pesa hizo.


Bi Clifford ni mmoja kati ya wanawake watatu ambao wameanza kesi dhidi ya Rais Trump kuhusu madai ya uhusiano wa kimapenzi au udhalilishaji.

Wakili wake Michael Avenatti ameambia BBC kwamba kesi ya mteja wake ni tofauti na wengine kwa sababu inahusu "visa vya kutolewa vitisho na mbinu ambazo zilitumiwa kumnyamazisha mteja wangu."

"Nafikiri ni kisa cha kustaajabisha na kinafaa kuwashangaza sio tu Wamarekani bali pia watu katika mataifa yaliyostaarabika ya magharibi," amesema.

Ameongeza: "Hivi sivyo watu walio madarakani wanavyofaa kuendesha shughuli zao."
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live




Latest Images