Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live

Amuua Mkewe Kisha naye Kujinyonga

$
0
0

Mwanaume mmoja anatuhumiwa kumuua mkewe kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali sehemu za mwili wake kisha na yeye mwenyewe kujinyonga hadi kufa kwa kutumia waya wa umeme wilayani Magu ambapo kitendo hicho ni kosa kisheria.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Naibu Kamishna wa Polisi, Ahmed Msangi amesema kuwa mtu huyo ametambulika kwa jina la John Ntemi (23) mkazi wa Kijiji cha Mahaha ambaye anatuhumiwa kumuua mkewe Casta Edward.

Aidha, Kamanda Msangi amesema inadaiwa wawili hao walikuwa wanaishi peke yao na kabla ya tukio hilo kutokea wanandoa hao walikuwa wakiishi kwa amani na upendo bila ya mgogoro wa aina yeyote kati yao, lakini ilipofikia Machi 26, 2018 majira ya saa 6:00 mchana mwenye nyumba waliyopanga alipita karibu na maeneo ya nyumba yao ndipo alipoona damu chini ya mlango, na kuweza kutoa taarifa kwa majirani pamoja na Jeshi la Polisi.

Pamoja na hayo, Kamanda Msangi amesema polisi walipofika katika eneo la tukio waliweza kukuta mwili wa mwanamke ukiwa mlangoni ndani ya nyumba eneo la tukio likionesha miburuzo ya damu toka chumbani hadi mlangoni huku mlango ukiwa umefungwa kwa kufuli.

Uchunguzi wa awali unaonesha mauji hayo yalitekelezwa usiku wa Machi 25, 2018 kutokana na kuwepo kwa mvua kubwa katika kijiji hicho kiasi kwamba majirani wasingeweza kusikia kilichokuwa kikiendelea ndani kwa wawili hao.

BASATA, Wazifungulia Nyimbo za Diamond Walizokuwa Wamezifungia

$
0
0


Baada ya Diamond na Uongozi wake Kukaa na BASATA pamoja na Waziri wa Sanaa, Hatimaye nyimbo Nyimbo zake Zimefunguliwa Kuchezwa kwenye TV na Radio Nchini Tanzania, Nyimbo hizo ni

1. Hallelujah (uliomshirikisha Morgan Heritage )
2. Waka Waka (uliomshirikisha Rick Ross).

Upigaji wa Kutisha Kila Kona Ripoti ya CAG...Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya March 28

Kenya Na Tanzania Wahakiki Mpaka Wa Kimataifa wa Tanzania Na Kenya

$
0
0

Timu za watalaamu wa upimaji ardhi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Tanzania na taasisi za usimamizi wa Ardhi nchini Kenya zimekutana wilayani Tarime mkoani Mara kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa kazi ya kuhakiki na kuimarisha mpaka wa Kimataifa baina ya nchi hizi mbili.

Mapema mwezi Machi, Naibu Waziri wa Adhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula alitangaza azma  ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanza  kuimarisha mipaka yake kwa nchi jirani za Kenya na Uganda baada ya ziara yake ya kukagua mpaka wa Tanzania na Kenya katika Mbuga ya Wanyama ya Taifa ya Serengeti iliyopo mkoani Mara.

Hatua ya  uhakiki na uimarishaji wa alama za mipaka ya mikataifa inatokana na mpaka huu kuwa wa siku nyingi na haukuwa wazi katika maeneo mengi pia baadhi ya alama hizo kuharibiwa, kung’olewa au kuchakaa na hivyo kusababisha Serikali pande zote kushindwa kusimamia kwa ufanisi shughuli za mipakani, rasilimali za nchi pamoja na ulinzi na usalama.

Katika uimarishaji wa alama hizo za mipaka hivi sasa, kutaongezwa alama mpya ndogo zinazoonana kwa umbali wa mita 100  pamoja na kubainisha eneo la ardhi huru kwa kila upande wa nchi (buffer  zone).

Mpaka kati ya Tanzania na Kenya una jumla ya urefu wa Kilommita 760 kuelekea bahari ya Hindi ambapo awamu ya kwanza ya kazi ya uimarishaji mpaka  inayofanyika hivi sasa itahusisha urefu wa Kilomita 238 kutoka kando ya Ziwa Victoria mkoani Mara hadi Ziwa Natron mkoani Arusha.

Baadaye, kazi ya uhakiki na uimarishaji wa mipaka itaendelea katika mikoa ya Kilimanjaro na Tanga na kisha itafanyika katika maeneo yote yanayohusika na  mipaka ya kimataifa nchini.

Uimarishaji wa mipaka ya kimataifa nchini umefanyika mara ya mwisho mwaka 1975 kwa kurudishia alama  ambazo ziliondolewa na kuongeza  nyingine mpya kwa kuzingatia alama zilizopo.

Mbali na Kenya nchi nyingine zinazopakana na Tanzania ni; Msumbiji, Malawi, Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Burundi, Rwanda, Uganda pamoja na visiwa vya Komoro na Shelisheli.

TRA Yazindua Rasmi Vitambulisho vya Wafanyabiashara Wadogo

$
0
0

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)  jana imezindua rasmi utoaji wa vitambulisho vya Wafanyabiashara wadogo walio kwenye sekta isiyo rasmi ikiwa ni pamoja na Wamachinga.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya uzinduzi huo iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo Charles Kichere alisema kuwa, utoaji wa vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo unatokana na marekebisho ya Sheria ya Usimamizi wa Kodi ya Mwaka 2015 yaliyofanywa na Bunge la Bajeti la Mwaka wa Fedha 2017/2018 ambapo moja ya marekebisho hayo ni kuwatambua na kuwapatia vitambulisho maalum wafanyabiashara wadogo walio kwenye sekta isiyo rasmi.

“Baada ya marekebisho ya Bunge la Bajeti la Mwaka wa Fedha 2017/2018, zoezi hili la kuwatambua wafanyabiashara wadogo lilianza kutekelezwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania  kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kama vile Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) pamoja na Idara ya Uhamiaji”, alisema Kichere.

Kichere alieleza kwamba, TRA  kwa kushirikiana na wadau hao, ilianza kutekeleza jukumu hilo kwa kuutambua Umoja wa Wamachinga wa Kariakoo jijini Dar es Salaam na kufanikiwa kuwapatia vitambulisho vya Taifa na Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) ambapo leo hii baadhi yao wamepatiwa vitambulisho maalum vya wafanyabiashara wadogo kama ishara ya uzinduzi wa utoaji wa vitambulisho hivyo.

Aliongeza kuwa,  zoezi la kutambua vikundi mbalimbali vya wafanyabiashara wadogo na kuwapatia Kitambulisho cha Taifa na Namba ya Utambulisho wa Mlipa kodi linaendelea kufanyika nchi nzima na kubainisha kuwa, ili wafanyabiashara wadogo waweze kupata vitambulisho hivyo maalum,  wanatakiwa kujiunga katika vikundi vinavyotambuliwa kisheria na Serikali, kuwa na Kitambulisho cha Taifa, kuwa na Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi ya kikundi alichojiunga nacho pamoja na kuchangia shilingi 10,000.

“Zoezi la kuwatambua wafanyabiashara wadogo linaendelea kufanyika nchi nzima na vitambulisho maalum vinavyotolewa kwa  wafanyabiashara hao vitadumu na kutumika kwa kipindi cha miaka mitatu (3). Maelezo ya mfanyabishara mdogo yaliyopo kwenye kitambulisho hicho maalum ni pamoja na jina na picha ya mfanyabiashara, jina la eneo analofanyia biashara, Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi na Sahihi ya mfanyabiashara husika”, Alifafanua Kichere.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam Mhe. Sophia Mjema aliishukuru Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Rais John Pombe Magufuli kwa kuwatambua wafanyabiashara wadogo ili waweze kupiga hatua kiuchumi kutoka daraja la chini hadi la kati na hatimaye kuweza kuchangia maendeleo ya nchi kupitia ulipaji wa kodi mbalimbali.

“Lakini kwanza naomba nimshukuru Mhe. Rais wetu John Pombe Magufuli kwa hii ndoto yake ya kuwasaidia wanyonge waliokuwa wanafanya biashara ndogo ndogo kutambulika na Serikali na kisha waondoke katika hali ya daraja la chini na kufikia daraja la kati.  Nafurahi kuwaeleza kwamba, ndoto ya Mhe. Rais wetu imetimia”, alisema Mjema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Shirikisho la Wamachinga wa Kariakoo jijini Dar es Salaam Steven Lusinde alisema kuwa, wamefurahishwa na azma ya Serikali ya kuwatambua wafanyabiashara walio kwenye sekta isiyo rasmi kwa kuwa wamekuwa na hamu ya kuchangia maendeleo ya Taifa kwa muda mrefu.

“Sisi wamachinga tumekuwa na hamu kubwa sana ya kuchangia Taifa letu kwa sababu tunaamini chochote tunachokiona katika nchi hii bila sisi kuchangia hakiwezi kwenda”, alieleza Lusinde.

Moja ya majukumu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania ni kukusanya mapato ya Serikali sambamba na kutoa elimu kwa walipakodi na watanzania kwa ujumla ili kuongeza uhiari wa ulipaji kodi na kuongeza mapato ya Serikali ambayo yanahitajika katika kuleta maendeleo ya nchi pamoja na wananchi wake.

Serikali ya Wanafunzi (Daruso), TNSP Yashangazwa na Kusambazwa Barua ya Kumsimamisha Abdul Nondo, Yafunguka Haya..

$
0
0

Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Daruso), imeshangazwa na kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii kwa barua ya kumsimamisha masomo mwanafunzi wake Abdul Nondo, badala ya kumkabidhi mwenyewe.

Hata hivyo, Rais wa Daruso Jeremiah Jilili, ameikosoa barua hiyo kuwa na makosa mengi ikiwamo kukosewa kwa kozi anayosoma Nondo lakini pia haikuwa na muhuri kuonyesha uhalali wake.

Barua ya kusimamishwa kwa Nondo iliyosainiwa na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa William Anangisye, ilianza kusambaa jana Jumatatu saa tatu usiku, ikielezea kumsimamisha kwa sababu ya kuwa na kesi ya kutoa taarifa za uongo katika mitandao na kudanganya kutekwa, ambapo kutokana na sababu hizo Nondo atarudishwa chuoni baada ya kumalizika kwa kesi hiyo.

Jilili amesema hata yeye barua hiyo ameiona kwenye mitandao ambapo aliwasiliana na Ofisi ya Mshauri wa Wanafunzi kwa sababu ndiyo mtu anayehusika na uhusiano wa wanafunzi ambapo amemjibu  ana taarifa za barua hiyo na amepelekewa nakala.

“Nikamuuliza ni kwanini barua hiyo kwanza haina muhuri halafu imeandikwa College of Humanity idara ambayo haihusiani na Nondo ambaye anasoma Social Science, akanijibu hiyo imeshabadilishwa.

“Lakini nikamwambia ni kwanini imewekwa kwenye mitandao wakati lengo la hiyo barua si kuwekwa kwenye mitandao kama hivyo kwa sababu ile inamhusu mhusika na si umma akasema zile barua ziko mbili ya kwanza ni ile inayoonekana kwenye mitandao ya pili imeelekezwa kwa Nondo na Ofisi ya mshauri wa Wanafunzi na watu wengine wanaostahii kupata barua hiyo, lakini barua zote zinazotakiwa kwenda sehemu husika zimeshafika zinakoelekezwa,” amesema.

Aidha, akifafanua hatua watakazochukua baada ya Nondo kusimamishwa masomo, amesema suala hilo ni kwa mujibu wa sheria za chuo ambazo zinasema kwamba mtu ukiwa na kesi ya jinai au ukifunguliwa mashtaka unasimamishwa, ndiyo maana Nondo hajafukuzwa chuo ila amesimamishwa.

“Sasa ukizingatia kesi yenyewe iko mahakamani ni suala ambalo halihitaji kuzungumziwa kwa mujibu wa katiba.

“Sisi kuna namna ambayo tulijaribu kulifuatilia tangu mwanzo kwa maana ya kutumia utawala na mawasiliano na polisi na vitu kama hivyo, lakini sasa kwa hapo tulipofikia hapo kesi ya Nondo ikishaisha kwa mfano Nondo akishinda anarudi chuoni na akishindwa sijajua utaratibu unakuwaje,” amesema.

Kwa upande wake Ofisa Habari wa TSNP, Helen Sisya amesema wanachama wa mtandao huo na yeye binafsi hawajaiona barua hiyo na Nondo bado hajafika chuoni hivyo hajakabidhiwa.

“Hata sisi tunasikia tu kwenye mitandao, tumesikia Profesa amethibitisha na kama amethibitisha sawa, hatuwezi kusema lolote.

“Lakini hizo hatua ni kwa mujibu wa sheria ndogo za chuo zinaruhuzu hivyo kwamba mwananfunzi akiwa na kesi ya jinai mahakamani anasimamishwa chuo, lakini unaweza kuona kuwa ni sheria mojawapo kandamizi kwa hiyo mimi kwa sasa naomba nisiseme lolote hadi niongee na wenzangu tuone tunafanyaje,” amesema Helen.

Mwakyembe, BASATA, Wakutana na Diamond, Wafanya Mazungumzo Masaa Matatu

$
0
0

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe leo Jumanne Machi 27, 2018 amekutana na mwanamuziki Nassib Abdul maarufu Diamond Platnumz,  jijini Dar es Salaam.

Tarifa iliyotolewa leo na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano serikalini, Lorietha Laurence imesema lengo la kukutana kwa wawili hao ni kurejesha maelewano kwenye tasnia ya muziki  kufuatia hatua zinazochukuliwa na wizara hiyo kufungia baadhi ya nyimbo, zikiwemo mbili za mwanamuziki huyo.

Imeeleza kuwa katika kikao hicho kilichofanyika ofisi za wizara hiyo na kuchukua zaidi ya saa tatu,  kilihudhuriwa na naibu waziri wa wizara hiyo, Juliana Shonza, Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Godfrey Mwingereza.

Wengine ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce Fisoo huku Diamond akifuata na mameneja wake watatu, Sallam Sharaff,  Hamis Taletale na Said Fela.

Taarifa hiyo inaeleza mazungumzo hayo, Diamond alimhakikishia Dk Mwakyembe kushirikiana kwa karibu na Shonza na uongozi mzima wa wizara katika kusimamia maadili ya kazi za sanaa na kuwa mfano bora wa wasanii nchini katika kulinda utamaduni wa Tanzania.

Kwa upande wake Dk Mwakyembe amesisitiza kuwa Serikali haina ugomvi wowote na wasanii nchini bali ina tatizo na mmomonyoko wa maadili, kwamba kila msanii ana wajibu kulinda maadili ambayo ni sehemu ya utamaduni wa nchi.

“Mwakyembe alikumbushia kauli ya Mwalimu Julius Nyerere baada ya uhuru kwamba Taifa lisilo na utamaduni wake ni sawa na Taifa mfu na Watanzania kamwe tusigeuke Taifa mfu,” inaeleza taarifa hiyo ikimnukuu  Dk Mwakyembe.

Waziri huyo ameagiza watendaji wa wizara na taasisi zake ikiwemo Basata, Bodi ya filamu na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),  kukutana na makundi ya wasanii wa muziki kwa lengo la kuelimishana kuhusu taratibu za kuwasiliana na mamlaka husika za sanaa.

"Maamuzi ya kuzifungia baadhi ya nyimbo yanayafanywa kwa mujibu wa sheria na si kwa utashi binafsi wa kiongozi wa wizara. Hivyo basi ieleweke kwamba hatua zilizochukuliwa na Shonza hivi karibuni zilikuwa za wizara kwa mujibu wa sheria za nchi,” amesema Dk Mwakyembe.

Kwa upande wake Shonza amesisitiza umuhimu wa wasanii kufuata utaratibu kwa kuwasilisha kazi zao mapema kwenye mamlaka husika iii kuepusha matatizo baadaye.

Lorietha Laurence
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.
27/03/2018.

Waziri Jafo Asimamisha Kazi Wakurugenzi Wawili kwa Maagizo ya Rais Magufuli

$
0
0

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  Selemani Jafo  amewasimamisha kazi wakurugenzi wawili kati ya watatu wa Halmashauri za Pangani na Kigoma baada ya kupata hati chafu katika matokeo ya Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2016/17.

Ripoti hiyo iliyowasilishwa leo Machi 27, 2018 inaonyesha halmashauri 166  kupata hati safi, 16 hati zenye shaka na halmashauri tatu kupata hati chafu.

Umauzi huo unafanyika ikiwa ni dakika chache baada ya Rais John Magufuli kutoa agizo hilo.

Halmashauri zilizopata hati chafu ni Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji na Halmashauri ya Kigoma na Pangani.

Waziri Jafo amesema baada ya kuwasimamisha,  amemwagiza katibu mkuu wa wizara hiyo kuunda timu ya watalaamu kuchunguza hati hizo na kutoa matokeo ndani ya wiki tatu.

Amesema wakurugenzi waliohusika katika hati chafu ni Daud Mlahagwa (Pangani), aliyekuwa Mkurugenzi wa Kigoma Ujiji, Judethadeus Mboya ambaye amestaafu kwa sasa.

“Amestaafu lakini ameacha mambo yakiwa hayako sawa, wakati akiwa ‘account officer’ mambo yalikwenda kombo na halmashauri hiyo ilipata hati chafu kwa miaka mitatu mfululizo,” amesema.

Mwingine ni Mkurugenzi wa halmashauri ya Kigoma, Hanji Godigodi na Damian Chambasi wa Pangani.

“Wakurugenzi hawa waliosababisha hati chafu nawasimamisha kazi kuanzia leo Machi 27, 2018 hadi hapo uchunguzi wa utendaji wao utakapokamilika, hawa wawili nawasimamisha kazi, kutokana na hili namwagiza katibu Mkuu wa Tamisemi kuunda timu ya watalaamu kwenda kuchunguza utendaji kazi wa wakurugenzi hao na kunipatia taarifa ndani ya wiki tatu,”amesema.

Amesema taarifa itakayopatikana itabainisha kiwango cha uchafu huo na Serikali itachukua hatua nyingine za kisheria kadri uchunguzi utakavyoelekeza.

Pia, amewataka wakurugenzi katika halmashauri zilizofanya vizuri katika ukaguzi huo, waendelee kutekeleza na majukumu yao na kutoa majibu ya hoja zote zilizobainishwa na ripoti ya CAG.

Amesema Serikali imeanza kufanya vizuri katika ukaguzi huo baada ya kufikia asilimia 90 na matumaini yaliyopo ni kuondokana na taarifa ya hati chafu ili kuhakikisha fedha za Serikali zinatumika kwa maendeleo ya wananchi.


Kanuni za Mitandao, Radio na Televisheni Tanzania Zatangazwa

$
0
0

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harisson Mwakyembe (Mb) ametangaza rasmi kanuni mbili za Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) ya Sura namba 306 ya mwaka 2010, katika gazeti la Serikali namba 133 (GN.No.133) na 134 (GN.No.134) zilizochapishwa tarehe 16/03/2018.

Kanuni za Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Maudhui ya Habari za Mtandaoni) ya mwaka 2018 ijulikanayo kama The Electronic and Postal Communications (Online Content) Regulations, 2018 zimetangazwa kupitia Tangazo la Serikali Namba 133 (GN.No.133).

Kanuni nyingine ni Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Maudhui ya Utangazaji katika Redio na Runinga) ya mwaka 2018 ijulikanayo kama The Electronic and Postal Communications (Radio and Television Broadcasting Content) Regulations, 2018 ambazo zimetangazwa kupitia tangazo la Serikali namba 134 (GN.No.134).

Kanuni hizi kwa pamoja zimetengenezwa chini ya Kifungu cha 103 cha sheria ya EPOCA na zimetiwa saini na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ambaye ndiye mwenye dhamana na Maudhui ya Habari na Utangazaji.

Kwa ujumla kanuni hizi zinalenga kuongeza ufafanuzi wa mambo muhimu katika Sekta ya Habari, kwa ajili ya kuongoza vyombo vyenye mamlaka ya kusimamia pamoja na kurahisisha utekelezaji kwa watumiaji mbalimbali wa huduma ya Sekta hiyo.

Mchakato wa kuandaa Kanuni hizi ulihusisha wadau mbalimbali wa Habari wakiwamo wamiliki wa vyombo, watoa huduma za mawasiliano ya mtandaoni, watumiaji wa mtandao, waandishi wa habari, pamoja na wanaharakati na watetezi wa haki za walaji wa huduma za sekta hii pamoja na Wizara ikisaidiana na wataalamu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Kanuni za Maudhui ya Utangazaji wa kwenye redio na kwenye runinga pamoja na mambo mengine zimefafanua juu ya dhana kuu mbili ambazo zimekuwa katika mijadala ya watoa huduma na watumiaji wengi, mambo hayo ni kuhusu Chaneli ambazo ni lazima kubebwa na anayemiliki miundombinu ya kurushia matangazo hata kama hazijalipiwa kwenye king’amuzi cha mlaji wa mwisho ( free to air channels).

Aidha, Kanuni zinawaelekeza wamiliki wa mitambo ya kurushia matangazo kulazimika kurusha hewani Chaneli ya umma (must carry public broadcaster channel) pasipo chombo cha umma kinachorusha chaneli hiyo au mwananchi anayemiliki king’amuzi kulipia chochote.

Vilevile Kanuni hizo zimeeleza juu ya taratibu za utoaji wa leseni za maudhui kwa vyombo vya habari, aina za leseni, masharti ya utoaji wa maudhui kwa vyombo vya habari, masharti ya urushaji vipindi, masharti ya jumla kwa leseni za huduma za maudhui.

Pia, Kanuni hizo zimeeleza juu ya viwango vya kitaalamu na kiufundi katika huduma za utangazaji, utoaji wa vibali vya ujenzi wa miundombinu ya utangazaji, aina za huduma na leseni za maudhui, wajibu wa vituo vya umma, wajibu wa vituo vya kibiashara, wajibu wa vituo vya kijamii, wajibu kwa utangazaji wa maudhui yanayolipiwa pamoja na masharti kwa kampuni za miundombinu ya maudhui.

Kanuni hizi pia zimezingatia kuwalinda watoto dhidi ya maudhui yasiyofaa, muda kwa vipindi ambavyo watoto hawaruhusiwi kuona kama vile utangazaji wa maudhui yenye vitendo vya ngono au maudhui yanayoonesha vurugu.

Mambo mengine ni masharti ya kutangaza mwenendo wa Mahakama au Bunge, masuala ya uchaguzi, masharti ya kutangaza maudhui kwa watu wenye mahitaji maalum, masharti kwa utangazaji wa vipindi vya mahojiano, lugha ya kutumia katika utangazaji.


Zimeelezea pia juu ya utangazaji wa maudhui ya ndani ya nchi na vipindi vyenye maslahi ya Kitaifa, vipindi vya taarifa za kiuchunguzi au masuala ya watu binafsi (Faragha), Utangazaji wa vipindi vya moja kwa moja.

Vilevile kumewekwa utaratibu wa kupokea na kusikiliza malalamiko ya walioathiriwa na habari za mtandaoni pamoja na adhabu kwa wanaofanya makosa kupitia mawasiliano ya mtandaoni.

Kanuni hizi zitafanya kazi chini ya Kamati ya Maudhui ambayo nayo imeundwa chini ya Sheria hiyo. Wadau mbalimbali wa vyombo vya habari na utangazaji pamoja na watumiaji wa mawasiliano ya habari kwa njia ya mtandao wanashauriwa kuzipitia kanuni hizo na kuzisoma kwa kina ili kuelewa mambo yaliyofafanuliwa.

Kanuni  hizi  zinapatikana  katika  Tovuti  ya  Wizara  ya  Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo  (www.habari.go.tz) kisha ingia sehemu ya machapisho bofya kipengele cha Sera, sheria na kanuni, pia waweza kutembelea tovuti ya  TCRA (www.tcra.go.tz)


Ripoti ya CAG: Deni la Taifa Linatia Mashaka, Serikali Ichukue Hatua Mapema

$
0
0

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali  (CAG), Profesa Mussa Assad amesema deni la Taifa linatia wasiwasi hivyo Serikali inatakiwa kuchukua hatua kupunguza ukubwa wa deni hilo.

Profesa Assad ametoa kauli hiyo leo Jumanne Machi 27, 2018 na kubainisha kuwa  deni hilo ni Sh46 trilioni kutoka Sh41 trilioni la mwaka uliopita, kwamba ni ongezeko la asilimia 12.

Ametoa kauli hiyo leo Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa uwasilishaji wa ripoti yake ya ukaguzi mwaka 2016/17 iliyobaini madudu Serikali za Mitaa na Mashirika ya Umma.

“Tulichosema hapa kwa kweli ukuaji wa deni tunasema ni himilivu lakini jinsi linavyoongezeka tunakaribia maeneo ya wasiwasi. Asilimia 72 ya GDP (Pato la Taifa) siyo mbaya lakini ikifika asilimia 76 nchi nyingine zimepata shida, inabidi tuangalie sasa namna gani tunaweza  ku-control ukuaji wa deni hilo,” amesema.

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Madawa Afunguka Alivyokataa Rushwa ya Milioni 800

$
0
0

MAMLAKA ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya imemtia mbaroni mfanyabishara wa kemikali bashirifu, mkazi wa Mwanza ambaye alitaka kuwahonga mamilioni ya fedha makamishna wa mamlaka hiyo ili wavuruge kesi inayomkabili.

Mfanyabiashara huyo ambaye jina lake halikutajwa kutokana sababu za usalama, inasemekana baada ya kukamatwa, aliahidi kumhonga Sh milioni 800  Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo, Rogers Siang’a   amsaidie kufuta shitaka lake.

Pia, mtuhumiwa huyo aliahidi kumpa rushwa ya Sh milioni 400  Kamishna wa Sheria wa Mamlaka hiyo, Edwin Kakolaki ili naye amsaidie kuvuruga kesi iliyokuwa ikimkabili.

Siang’a alikuwa akizungumza juzi mjini hapa wakati wa semina ya Kamati ya Kudumu ya Bunge inayoshughulikia Ukimwi na Dawa za Kulevya.

Alisema viwango vikubwa vya kemikali bashirifu ambayo mara nyingine hutumika kutengenezea dawa za kulevya,  imekuwa  ikiingizwa nchini.

“Kuna zaidi ya kampuni 2000 zimekuwa zikiingiza kemikali bashirifu nchini  lakini kasi ya kuzikagua kemikali hizo imekuwa ndogo kutokana na wingi wa kampuni na uchache wa rasilimali watu na fedha.

“Lakini  Desemba mwaka jana, kuna mfanyabiashara mmoja wa kemikali bashirifu alitaka kumpa hongo Kamishna Kakolaki, ya Sh milioni 400  avuruge kesi, ila kwangu alisema akinifikia  atanipa Sh milioni 800,” alisema   Siang’a.

Kamishna wa Kinga na Tiba kwenye mamkala hiyo, Dk. Peter Mfisi, alisema hadi sasa   Watanzania 1050 wamekamatwa katika nchi mbalimbali wakituhumiwa kuhusika na biashara ya dawa za kulevya.

Alisema kitendo hicho kimekuwa kikichafua hadhi ya Tanzania katika sura ya  mataifa.

“Hata hivyo, udhibiti wetu umefanikiwa kudhibiti uingizwaji wa dawa hizo nchini na kusababisha kuongezeka kwa watu wanaohitaji matibabu ya ‘methadone   na kupanda kwa bei ya dawa hizo mtaani.

“Kwa ujumla, hali bado ni mbaya kwa watumiaji wa dawa hizo hasa kutokana na kuambukizana magonjwa ya Ukimwi, TB na homa ya ini kwa sababu watumiaji hao  wana tabia ya kuchangia sindano.

“Lakini mtumiaji akimuona mwenzake anasinzia wakati akiwa amejichoma sindano, basi hunyonya damu ya mwenzake kwa kutumia sindano kisha kujidunga akiamini kuwa damu ya mtu huyo ina dawa za kulevya,” alisema.

Waziri wa Nchi, Sera, Uratibu, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, alisema kutokana na udhibiti wa dawa hizo kuimarika, wafanyabiashara wameanza kuwatumia watoto wa viongozi na matajiri wakiamini wana uwezo wa kununua dawa kwa urahisi.

“Pamoja na hayo, Serikali itawasaka kila kona bila kujali mtu au nafasi aliyonayo   kuhakikisha mtandao huo unatokomea,” alisema.

Naye Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Bunge, Oscar Mukasa, alisema lengo la semina hiyo ni kuwapa mwanga wajumbe wapya wa kamati hiyo  wafahamu utendaji kazi na muundo wa mamlaka hiyo.

Pamoja na hayo, alisema kamati yake itashirikiana na mamlaka husika na Serikali ili vita dhidi ya dawa za kulevya, ifanikiwe.

Pata Huduma za Matibabu ya Asili na Nyota Pamoja na Pete za Bahati

$
0
0

Mtabibu Mongwa husafisha nyota na kutoa Pete za bahati na kwawale walio sumbuka kwaajili ya matibabu na hawakufanikiwa chochote sasa njoo ujionee miujiza hapo kwahapo bila malipo yoyote malipo baada yakazi napia humpa mtu jini la mali kwayule anaye taka kumiliki bila mashariti yoyote
Tunatibu magonjwa mbalimbali yaliyo shindikana mpenzi aliye kukimbia nakumrudisha kwa masaa 24 tu napia natoa dawa za nguvu za kiume kuurefusha uume paka pale unapotaka .

Natoa dawa za biashara na mvuto ==tunatoa dawa zauzazi kwa wale kina mama wenye matatizoya uzazi walio angaika kwa muda mrefu bila kupata mafanikio yoyote njoo umalize tatizo lako sasa
Natoa mazindiko yanyumba na mwili biashara na mvuto kazini

Kupandisha nyota ili kungaa kupandishwa cheo kazini kurudisha mali zilizo pote zilizo ibiwa kuzulumiwa
Kesi zilizo shindikana uzimaliza mara moja namengine mengi ya siri piga simu

+255 764291657

Prof. Jay aandika haya baada ya Mbowe Kukosa Dhamana

$
0
0

Msanii mkongwe na Mbunge wa Mikumi kupitia chama cha CHADEMA Joseph Haule  Prof. Jay ameandika kupitia ukurasa wake wa Instagram muda mfupi baada ya Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe kukosa dhamana katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu.

Sasa msanii Prof. Jay ameandika ikiwa ni baada ya Mbowe kukosa dhamana akiwa na viongozi sita wa Chadema, haya hapa maneno ya Prof. Jay kwenye ukurasa wake wa Instagram….

>>“Yana mwisho Haya… Giza linapozidi kuwa Totoro jua kuwa karibu kunapambazuka..TIME WILL TELL.” – Prof. Jay

Tetesi: Zari Hassan Atoa Bongo Madale Kimya Kimya

$
0
0

Taarifa za Chini Ya Carpet Inasemekana Zarithebosslady Amewasili Bongo Kimya kimya Bila Ya Escort yeyote kutoka WCB Lakini Ametua Madale

Vyanzo Vyetu tayari Vimeingia Chimbo kuhakikisha updates zote kuhusu ujio Wa Zari Nchini zinapatikana

Stay tuned

Nikki wa Pili Amtetea Dogo Janja Baada ya Kuvaaa Uhusika wa Mwanamke Katika Video

$
0
0

Hatua ya Dogo Janja kuvaa uhusika wa mwanamke katika video ya wimbo wake wa ‘wayu Wayu’ inachukuliwa na Nikki wa Pili kuwa ni katika kuitendea haki sanaa kwakuwa hakuna mipaka inayomzuia msanii kufanya kitu kama hiki.

Baadhi ya Wadau wamekuwa wakikikosoa kitendo hicho na kudai amejizalilisha kwa kuvaa uhusika wa kike

Profesa Jay: Wanamuziki wa Zamani Watu Bado Wanawaheshimu Msikate Tamaa

$
0
0
Profesa Jay: Wanamuziki wa Zamani Watu Bado Wanawaheshimu Msikate Tamaa
Msanii Mkongwe Bongo katika muziki wa hip hop, Professor Jay amesema wasanii wa zamani bado mchango na muziki wao vinahitajika kwa sana kinachotakiwa ni wao kujipanga na kurudi upya.

Jay ambaye hivi karibuni ameachia ngoma inayokwenda kwa jina Pagamisa ameiambia Clouds TV yeye amekuwa akifanya muziki toka 1995 akiwa na kundi na hadi sasa anatoa ngoma na watu wanazipokea.

“Lakini niwaambie wasanii wa zamani watu bado wananaheshimu, wamekuwa kama wamechonga barabara ambapo wasanii wa sasa wamepata mifano kwao, hii ni game wasikate tamaa, watu bado wanawamisi, bado wanapenda nyimbo zao, watu wanapenda mashairi yao,” amesema Professor Jay.

“Nimeshakuwa na kundi langu la Hard Blaster mabingwa wa Tanzania mwaka 1995 wasanii wengi wa sasa hivi ndio walikuwa wanazaliwa lakini hadi sasa natoa ngoma kutokana na mazingira yaliyopo na watu wananipokea vizuri,” ameongeza.

Tangu Professor Jay kuchaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la Mikumi amekuwa si msanii wa kutoa ngoma mara kwa mara ukilinganisha na hapo awali, ngoma alizotoa hivi karibuni ni pamoja na Kibabe na mpya ya sasa.

Hashim Rungwe Apotelewa na Ndugu Zake Wawili

$
0
0

Hashim Rungwe Apotelewa na Ndugu Zake Wawili
Mwenyekiti wa chama CHAUMA Hashim Rungwe ambae pia alikuwa miongoni mwa wagombea wa Urais kwa mwaka 2015 ametangaza kutoonekana kwa ndugu yake anaeitwa Saida Hilal na wao hawajui yuko wapi.

“Kuna binti anaitwa Saida Hilal amepotea haonekani tangu alipoaga kuwa anaenda kazini, alichukuliwa na gari ya kazini na baada akaaga anaenda oysterbay polisi, tangu hapo hajaonekana na wala hapatikani kwa simu yake ya mkononi” -Rungwe

Baada ya Kumaliza Beef la Daimond na Waziri Shonza Haya Hapa Maneno ya Mwakyembe "Utake Usiitake, Diamond ni Balozi wa Tanzania"

$
0
0
Baada ya Kumaliza Beef la Daimond na Waziri Shonza Haya Hapa Maneno ya Mwakyembe "Utake Usiitake, Diamond ni Balozi wa Tanzania"
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema msanii Diamond anafaa kuwa balozi wa maadili kutokana na ushawishi alionao kwa sasa.

Waziri Mwakyembe amesema hayo baada ya kikao kilichowakutanisha watu wa Wizara hiyo, kutoka Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) na menejiment ya msanii huyo ambapo walijadili mvutano uliojitokeza mara baada ya nyimbo mbili za Diamond kufungiwa.

“Ndio balozi wetu, balozi wa maadili pia, kwa sababu Diamond utake usitake yeye ni balozi wa Tanzania kwa kila kitu na safari hii tumemuomba hata maadili awe balozi wetu, kwa sababu watu wengi wanamfuta Diamond, yeye ni Super Star na tunajivunia Watanzania,” amesema.

Pia Waziri Dkt. Mwakyembe amesema maamuzi ya kuzifungia baadhi ya nyimbo yanafanywa kwa mujibu wa sheria na si kwa utashi binafsi wa kiongozi wa wizara, hivyo ieleweke kwamba hatua zilizochukuliwa na Naibu Waziri Shonza hivi karibuni zilikuwa za Wizara kwa mujibu wa sheria za nchi.

“Nawaagiza watendaji wa Wizara na Taasisi zake ikiwemo BASATA, Bodi ya Filamu na TCRA, kuweka madaraja ya kazi zetu za sanaa, kuna kazi za sanaa ambazo kuonekana ni kuanzia saa sita hadi saa 12 asubuhi na hii inafanyika nchi nyingi ndio maana nimesema wakae na wenzetu,” ameongeza.

Kwa upande wake Naibu Waziri, Juliana Shonza alisema suala la kulinda maadili ni endelevu na wakati umefika sasa kwa Bodi ya Filamu na TCRA kukamilisha zoezi la kuoanisha kanuni za madaraja ya kazi za sanaa ili kazi zinazofaa kuonekana na watu wazima zianze kuangaliwa saa sita usiku hadi saa 12 asubuhi.

Naye Diamond alisema, “Nitashirikiana kwa karibu na Naibu Waziri Shonza na uongozi mzima wa wizara katika kusimamia maadili ya kazi za sanaa na kuwa mfano bora wa wasanii nchini katika kulinda utamaduni wa mtanzania”.

Mchungaji Akamatwa na Polisi Akijaribu Kumfufua Marehemu

$
0
0
Mchungaji Akamatwa na Polisi Akijaribu Kumfufua Marehemu
Stori ninayokusogezea leo March 28, 2018 ni kumhusu Mchungaji mmoja ambaye amejikuta akiingia mikononi mwa Polisi baada ya kushindwa kumfufua mwanaume mmoja eneo la kati huko Msumbiji.

Mchungaji huyo alidai kuwa roho mtakatifu alimwambia asafiri hadi katika hospitali inayofahamika kwa jina Chimoio iliyopo katika jimbo la Manica, ili akafanye muujiza ambao alidai ana uwezo wa kufanya na alipowashawishi Maafisa wa hospitali walimruhusu aingie ndani ya chumba cha kuhifadhi maiti ili atekeleze muujiza huo.

Hata hivyo baada ya siku mbili za maombi, hakuweza kurejesha uhai wa marehemu na familia hiyo haikushangazwa na kushindwa kwake.

Dada wa marehemu  ambaye hakutaka jina lake litajwe aliwaambia waandishi wa habari kuwa “Kasisi aliomba, akaomba na kuomba hadi akanena kwa lugha. Alizungusha kichwa cha marehemu huku na kule huku akiomba.

“Lakini hakuna hata sehemu ya marehemu kaka yangu iliyoweza kutikisika. Wakati mmoja kasisi alipaza sauti akisema, ‘amka, kijana wa Mungu!, Hatukuamini angefanya mwujiza wowote. Hii ni kwa sababu hakuwahi, hata wakati mmoja, kuthibitisha uwezo wake wa kumrejeshea mfu uhai wake.” -Dada wa Marehemu

“Tangu wakati huo kasisi alikamatwa na yuko mikononi mwa polisi akishtakiwa kwa kosa la kumkosea heshima mfu. -Dada wa Marehemu

Shamsa Ford: Naishi Maisha Yangu Sitamani vya Mtu

$
0
0
Shamsa Ford: Naishi Maisha Yangu Sitamani vya Mtu
Msanii wa filamu nchini Shamsa Ford amefunguka na kudai hata adhauriwe kwa kiasi gani hawezi kuthubutu kutamani au kujilinganisha maisha yake na mtu mwingine kwa kuwa anaimani kila mmoja Mungu amempangia fungu lake.


Shamsa ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake wa kijamii ikiwa kama somo au fundisho kwa baadhi ya watu wenye tabia ya kupenda kutamani na kujilinganisha maisha na watu fulani waliowazidi uwezo na matokeo yake huwa wanaishia kuaibika kutokana na wanachokifanya hakipo katika uwezo wao.

"Huwa naishi maisha ninayoyaweza siku zote, sitamani vya watu wala kulinganisha maisha yangu na mtu yeyote kwasababu huwa naamini Mwenyezi Mungu amempa kila mtu kwa wakati wake na kila mtu ana kalma yake", amesema Shamsa.

Pamoja na hayo, Shamsa Ford ameendelea kwa kusema "hata unidharau mpaka kunitemea mate kwa kuhisi una vikubwa kuliko nilivyo navyo mimi, huwa siumii kwasababu naamini Mungu amenipa maisha mazuri ingawa kwako unaona ni mabovu".

Kwa upande mwingine, Shamsa Ford amewashauri walimwengu 'jamii' wawe na tabia ya kujipenda na kujitathimini wao wenyewe binafsi hata kama ikitokea mtu akamdharau kiasi gani.
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live




Latest Images