Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live

Norah Ashindwa Kuficha Hisia Zake Afunguka Anavyomzimia Gabo

$
0
0
Norah Ashindwa Kuficha Hisia Zake Afunguka Anavyomzimia Gabo
MKONGWE wa sinema za Kibongo, Nuru Nasoro ‘Norah’ amesema kati ya waigizaji wa kiume anaowakubali kutoka Bongo Movies ni muigizaji Gabo Zigamba.

Norah alifunguka hilo hivi karibuni alipokuwa akipiga stori mbili tatu na mwanahabari wetu ambapo alipoulizwa kuhusu listi ya wasanii wa kiume anaowakubali Bongo, moja kwa moja alianza kwa kumtaja Gabo.

“Wapo wengi ninaowakubali na listi yangu inaongozwa na Gabo namzimia kweli. Wengine ninaowakubali ni JB, Frank Mwikongi, Chiki Mchoma na Dude,” alisema Norah.



Alipoulizwa nini kinamvutia zaidi kwa waigizaji hao, alisema ni namna wanavyojua kubadilika kulingana na matakwa ya filamu husika.

Wema Sepetu Ahusishwa Kutumbuliwa kwa Jokate UVCCM Huu Hapa Ukweli Wote

$
0
0
Wema Sepetu Ahusishwa Kutumbuliwa kwa Jokate UVCCM Huu Hapa Ukweli Wote
BAADA ya wikiendi iliyopita aliyekuwa Kaimu Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UV-CCM), Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ kutumbuliwa katika nafasi hiyo, staa wa filamu za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ametajwa, Risasi Mchanganyiko linakupa habari kamili.



Mara tu baada ya sakata hilo kuchukua nafasi kwenye vyombo vya habari na mitandao mbalimbali ya kijamii, habari za ndani zinaeleza kwamba, Wema alianza kutajwa katika kumrithi mwanadada Jokate kwenye kiti hicho.



Chanzo cha ndani ya umoja huo wa vijana kililieleza Risasi Mchanganyiko kuwa, nafasi aliyoondolewa Jokate kuna uwezekano mkubwa wa kushikiliwa na Wema na ndiyo maana siku za hivi karibuni ameonekana kuwa mwenye furaha tofauti na alivyokuwa siku za nyuma.

“Nafasi ya Jokate itachukuliwa na Wema na Jokate atapewa nafasi ya juu zaidi ila kwa sasa ni siri kubwa hata ukiwauliza viongozi hawataweza kukueleza kuhusu hilo,” kilidai chanzo.



MSIKIE KIONGOZI UVCCM

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka alisema kuwa, uamuzi wa kumuondoa Jokate ni wa kawaida na ni wa kamati ya utekelezaji ya UV-CCM na ndicho chombo ambacho kina dhamana ya kuweka na kuondoa na mara zote anapoondoka mtu au anapoletwa mtu, kamati huwa inajiridhisha na ina sababu zake hivyo hayo ni masuala ya kiutawala na kiuendeshaji na yanabakia kwenye uendeshaji wa vikao.


Wema Isaac Sepetu





“Bahati nzuri Jokate alikuwa anakaimu, hakuwa amethibitishwa kwa mujibu wa taratibu zetu ndani ya jumuiya, ndani ya jumuiya ili uweze kuwa kamili ni lazima uthibitishwe na Baraza Kuu la UV-CCM, sasa yeye kwa kipindi chote cha mwaka mmoja hakuwa amethibitishwa kwa sababu alikuwa anakaimu tu.



“Kwa hiyo yapo mambo pengine si mabaya si mema au mema kabisa hayo yote hata kama yapo hatuwezi kuyatoa nje ya kikao chetu, huo ni utaratibu wa kawaida, Jokate hajakosea chochote, bali ni mambo ya kupokezana vijiti tu na hakuna mtu ambaye tumepanga aje achukue nafasi kama wengi wanavyodai kwa sababu yote hayo ni utaratibu wa vikao,” alisema kiongozi huyo.



Aliendelea kueleza kuwa, baada ya vikao vitakapokaa, kama jambo hilo liko kwenye ajenda litajadiliwa na atawekwa mtu, lakini kama halipo halitajadiliwa.

Alipoulizwa kuhusu Wema kudaiwa kuwa ndiye atakayeirithi nafasi hiyo, Shaka alisema kuwa, hayo hayafahamu kwa sasa ndiyo anayasikia na kuhusu Jokate kupewa nafasi ya juu zaidi pia hana taarifa hizo.



Risasi Mchanganyiko lilifanya jitihada za kumtafuta Jokate ili kumsikia ana lipi la kusema juu ya kutumbuliwa katika nafasi hiyo, lakini simu yake ya mkononi iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa meseji kwa njia ya WhatsApp hakujibu chochote.



Jokate ambaye ni Miss Tanzania namba mbili aliteuliwa kushika nafasi hiyo Aprili, mwaka 2017 ambapo ameshikilia kwa mwaka mmoja hadi alipotumbuliwa Jumapili iliyopita baada ya kamati ya utekelezaji ya umoja huo chini ya mwenyekiti wake, Kheri James kukaa kikao cha siku moja kilichofanyika Dodoma na kufikia uamuzi huo.

Diva: Sipo Single Nimeshapata Mwanaume Ambaye Amekubali Kulipa Mahari ya Milioni 500

$
0
0
Diva: Sipo Single Nimeshapata Mwanaume Ambaye Amekubali Kulipa Mahari ya Milioni 500
Mtangazaji wa kituo cha Redio cha Clouds FM, DIVA ameweka wazi kuwa kwa sasa hayupo single tayari ameshapata Boyfriend mpya baada ya kumwagana na mwanamuziki Heri Muziki.

Diva amesema kuwa mwanaume huyo tayari ameshakubali kulipia mahari ya shilingi milioni 500 ingawaje kwa sasa amekataa kumuweka wazi kwenye mitandao ya kijamii.

Kwa upande mwingine Diva amesema kuwa kwa sasa anapata tabu kweli kutoka kwa mwanaume kitu ambacho kinamfanya abadilishe laini mara saba kwa mwezi.

Times FM Waiangukia Serikali Kisa Interview Yake na Daimond

$
0
0
Times FM Waiangukia Serikali Kisa Interview Yake na Daimond
Kitu cha Radio, Times FM kimeomba radhi kufuatia mahojiano waliofanya na msanii Diamond Platnumz March 19 mwaka huu.

Soma taarifa kamili;

Miguna Atimuliwa Tena Kutoka Kenya na Kupelekwa Dubai

$
0
0
Miguna Atimuliwa Tena Kutoka Kenya na Kupelekwa Dubai

Mwanasiasa wa upinzani Kenya aliyeidhinisha kiapo cha kiongozi wa upinzani Raila Odinga kuwa 'Rais wa Wananchi' Januari Miguna Miguna ametimuliwa tena kutoka nchini humo.

Mwanasiasa huyo ametimuliwa huku mzozo kuhusu uraia wake ukiendelea.

Bw Miguna ameandika kwenye Facebook kwamba ameamka na kujipata yuko Dubai na kwamba anahitaji matibabu.

Amesema anafahamu kwamba kuna mpango wa kumpeleka London lakini anataka kupanda ndege ya kurejea Nairobi pekee.

Mwanasiasa huyo amesema amesindikizwa na afisa wa idara ya ujasusi.

Serikali imechukua hatua hiyo licha ya kuwepo kwa maagizo ya mahakama ya kuzuia kutimuliwa kwake na ya kuitaka serikali kufanikisha kurejea kwake nchini humo.

Mawakili wa Bw Miguna wamethibitisha kwamba aliondolewa nchini humo kwa kutumia ndege ya shirika la Emirates iliyokuwa inaelekea Dubai.

Bw Miguna alikuwa amezuiliwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) tangu alipowasili Jumatatu adhuhuri.

Mwanasiasa huyo alikuwa anajaribu kurejea kutoka Canada ambako alikuwa amepelekwa baada ya kufurushwa kutoka Kenya kwa lazima mwezi Februari.

Jaji wa Mahakama Kuu George Odunga Jumatano alisema waziri wa usalama nchini humo, mkuu wa polisi na mkuu wa idara ya uhamiaji watakuwa wamekaidi maagizo ya mahakama iwapo wangekataa kumwachilia huru.

Alikuwa ametoa ilani kwa watatu hao kufika mahakamani baadaye Jumatano lakini baada yao kukosa kufika akawapata na hatia ya kukaidi agizo la mahakama.

Aliahidi kutoa adhabu dhidi yao leo asubuhi.

Maafisa wa Kenya mnamo 6 Febuari walikuwa wamemfukuza kutoka nchini humo kutokana na mchango wake wakati wa kuapishwa kwa Bw Odinga.

Walisema mwanasiasa huyo hana uraia wa Kenya lakini ana uraia wa Canada.

Idara ya uhamiaji ya Kenya imekariri kuwa Miguna alipoteza uraia wa Kenya mwaka 1998 alipopewa uraia wa Canada wakati ilipokuwa ni kinyume cha sheria kuwa na uraia wa nchi mbili nchini Kenya
Kuzuiliwa kwa Bw Miguna kumejadiliwa pakubwa kwenye mitandao ya kijamii Kenya, baadhi wakiunga mkono hatua hiyo lakini wengine wakiwashutumu maafisa wa uwanja wa ndege na serikali.

Mmoja wa mawakili wa Bw Miguna, Nelson Havi, ni miongoni mwa waliokuwa wa kwanza kufichua kwamba Bw Miguna alikuwa ametimuliwa tena nje ya nchi hiyo

"Sitaki Kuolewa na Mpare"- Mimi Mars

$
0
0
"Sitaki kuolewa na Mpare"- Mimi Mars
Msanii ambaye kwa sasa anatamba na kibao chake kipya 'Sitamani' chini ya Mdee Music, Mimi Mars amesema hawezi kujihusisha mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwenye kabila la Mpare kwa madai makabila hayo wanatabia ya ubahili na kujisikia.


Mimi amebainisha hayo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya kuulizwa swali na ripota wa kipindi hicho kuwa anatamani mwanaume wa kabila gani ambaye awe naye katika mahusiano au ndoa.

"Kutokana na mimi mwenye kuwa ni Mpare kwa hiyo tabia za wanaume wa kipare ninazifahamu vizuri halafu wanasema mafahari wawili hawezi kukaa zizi moja hivyo najua tutashindwana tu kwasababu wote tunajisikia, wabahili 'so' tukikaa wawili 'type' hiyo mambo yatakuwa magumu", amesema Mimi Mars.

Pamoja na hayo, Mimi ameendelea kwa kusema "inanibidi nitafute kabila ambalo tofauti na mimi ndio maana sitoweza kuwa kabila hilo ila sio kwa ubaya ila mimi mwenyewe tu nimesema sitoweza.

Msami Baby Kuivunja Ndoa ya Dogo Janja ?

$
0
0
Msami Baby Kuivunja Ndoa ya Dogo Janja ?
Mwanamuziki anayefanya poa na ngoma ya 'Mdundo' Msami baby amesema haoni tatizo lolote la yeye kumsifia mke wa Dogo Janja (Irene Uwoya) kwa madai wana historia ndefu ya maisha yao ya nyuma kabla ya kuolewa hivyo haitokuwa rahisi kuacha kumsifia.


Msami ameeleza hayo kupitia kipindi cha eNewz kinachorushwa na EATV baada ya wawili hao kuzua ngumzo mitandaoni kwa kile kilichoonekana kuwa bado wanatamania kimapenzi japokuwa mmoja wapo amekuwa mke wa mtu kwa sasa.

"Ni kweli Uwoya anapenda ninachokifanya ndio maana ameni-post ni kweli kwani kuna kitu gani cha uongo hapo wakati amezungumza ukweli. Kama kucheza ninacheza kwa hiyo anahaki ya kusema anachotaka. Na mimi kuandika mtu fulani ni mzuri sio dhambi kwasababu kwangu mimi binafsi naona kama upendo wa kumkubali mtu kama yeye alivyoona kuwa mimi ninasifa ya kuwa mchezaji bora", amesema Msami

Pamoja na hayo, Msami ameendelea kwa kusema "mimi namjua Uwoya tokea zamani, kwa hiyo tuna maisha yetu na historia, tunaongea na kutaniana mambo mengi,'so' haviwezi vitu kama hivyo kuanza kupotea tu".

Lema Amzungumzia Nguvu Aliyonayo Mange Kimambi

$
0
0
Lema Amzungumzia Nguvu Aliyonayo Mange Kimambi
Mbunge wa Arusha Mjini CHADEMA Mhe, Godbless Lema amefunguka na kuweka wazi kuwa kama chama cha siasa hakiwezi kufundisha watu wake kufanya siasa za kuleta fujo bali uvunjifu wa amani, uonevu ni vitu ambavyo vinaweza kuwafanya watu wapiganie haki zao


Lema amesema hayo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari Makao Makuu ya CHADEMA na kusema kuwa wapo watu wengi ndani ya CHADEMA na nje ya CHADEMA ambao wamekuwa wakilia na kuumia na mambo yanayoendelea nchini ndiyo maaana hata mwanaharakati Mange Kimambi kupitia mtandao wake wa kijamii amekuwa na nguvu kwa kuwa kuna watu ambao wanasikiliza kutokana na mambo yanayofanywa na serikali.

"Yaani msingi wa kwanza wa Demokrasia ni amani maanake watu washindane kwa hoja sasa inatosha maanake nini kumekuwepo na vilio vya CHADEMA na wanachama wake kwa muda mrefu sana bahati mbaya waandishi wa habari mkafikiri vilio hivi vya CHADEMA, kanisa likafikiri hivyo na msikiti ukafikiri hivyo lakini leo tunalia pamoja wakiwepo wafanyabiashara sasa leo kilio chetu si pekee yetu ndiyo maana kanisa limetoa waraka hivi karibuni Katoliki na Lutherani tunategemea BAKWATA watafanya hivyo hivyo sasa ipo siku na hiyo siku inakuja"

Lema aliendelea kusema kuwa "Kuna uchungu unakusanyika kwa watu na hawa watu wanaandamana moyoni ndiyo maana Mange Kimambo yuko Marekani anatumia Instgram huku anajibiwa na kiongozi, Mwigulu Nchemba, Mambosasa, sasa kama mtu mmoja yupo Marekani anaweza kuhamasisha Tanzania na kukawa na presure tunayoiona hii manake kwamba watu wamechoka, tunasema imetosha lengo la CHADEMA au lengo langu mimi au lengo la kiongozi yoyote wa CHADEMA si kuona nchi hii haina amani lakini lengo la Chama Cha Mapinduzi kwa mwelekeo wao ni kuona watu wanaingia barabarani kwa nguvu kutafuta haki" alisema Lema

Lowasa Atinga Mahakamani Kufuata Dhamana ya Mbowe na Viongozi Wengine wa Chadema

$
0
0
Lowasa Atinga Mahakamani Kufuata Dhamana ya Mbowe na Viongozi Wengine wa Chadema
MWENYEKITI wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na viongozi wenzake watano wa chama hicho wamerejeshwa tena katika Mahakama ya Kisutu, Dar leo Machi 29, 2018 asubuhi ili kuendelea na kesi inayowakabili.

Mbowe na wenzake wamefikishwa mahakamani hapo wakitokea mahabusu ya Segerea ambapo wanakabiliwa na mashtaka manane yakiwemo kufanya maandamano yaliyosababisha kifo cha mwanafunzi wa Chuo cha NIT, Akwilina Akwiline, Feb 16 mwaka huu, uasi na kuhamasisha chuki.

Baada ya viongozi hao kufikishwa mahakamani hapo, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa na viongozi wengine wa chama hicho walifika mahakamni hapo ili kusikiliza kesi hiyo na kufanya jitihada za kuomba dhamana kwa watuhumiwa hao leo.

Viongozi wengine waandamizi wa chama hicho wanaoshtakiwa katika kesi hiyo ni: Katibu Mkuu Dkt Vincent Mashinji, John Mnyika, Salum Mwalimu, Mch. Peter Msigwa na Ester Matiko ambapo wote wamefikia kwenye chemba ya mahakama panaposikilizwa kesi hiyo.

Mjane Aliyemlilia Rais Magufuli Afungwa Jela

$
0
0
Mjane Aliyemlilia Rais Magufuli Afungwa Jela

Mahakama ya Mwanzo Usambara mkoani Tanga imemhukumu kwenda jela miezi mitatu Swabaha Shosi ambae alishawahi kushika headlines kwa kulia mbele ya Rais Magufuli wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria February 2, 2017.

Hakimu wa Mahakama hiyo Khadija Kitogo amemtia hatiani kwa kuingia eneo lisiloruhusiwa kisheria.

Swahaba alifikishwa Mahakamani hapo August 9, 2017 akikabiliwa na shtaka la kuingia Chongoleani ambako hakuruhusiwi Raia kuingia.

Mahakama ilielezwa kuwa aliingia katika eneo lililokuwa limetengwa kwa ajili ya ujio Rais Magufuli na Yoweri Museveni walipokwenda kuzindua mradi wa bomba la mafuta kutoka Uganda mpaka Hoima.

Swahaba alikana mashtaka hayo na kujitetea kuwa alikanyaga eneo wakati akiandaa eneo kwa ajili ya kuwauzia chakula waliodhuria uzinduzi huo na kwamba hakuwa peke yake walikuwa wengi.

Hakimu Kitogo akitoa hukumu hiyo amesema baada ya kusikiliza ushahidi wa pande zote mahakama imemkuta na hatia ya kuvunja sheria ya Makosa ya jinai.

“Ninampa adhabu ya kwenda jela miezi mitatu ili iwe fundisho kwa wengine wanaovunja sheria kwa kuingia maeneo yasiyoruhusiwa” -Hakimu Kitogo

Licha ya Times FM Kuomba Radhi TCRA Yawakalia Kooni Yasema Kibano Kipo Palepale

$
0
0
Licha ya Times FM Kuomba Radhi TCRA Yawakalia Kooni Yasema Kibano Kipo Palepale
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imesema licha ya kituo cha Redio Times kuomba radhi katika kipindi cha mahojiano kati yake na msanii Diamond, hatua ya kufika mbele ya kamati ya maudhui kwa ajili ya kuhojiwa ipo pale pale.

Hayo yamesemwa leo Machi 29 na Ofisa Mkuu Idara ya Utangazaji wa mamlaka hiyo, Andrew Kisaka, alipohojiwa na MCL Digital, na kutakiwa kueleza kama uombaji wa radhi  wa kituo hicho ndio salama yao ya kutoitwa mbele ya kamati hiyo kujieleza kwa nini wasichukuliwe hatua.

Katika maelezo yake, Kisaka amefafanua kwamba suala la kituo cha Redio au Televisheni kinapokosea ni lazima uongozi wake ufike mbele ya kamati hiyo na kuongeza kuwa hiyo ni sheria hivyo huwezi kuikwepa.

Amesema sheria hiyo inabaki palepale hata kama itatokea uongozi huo, ukaomba radhi kwa kupitia njia nyingine kama hiyo waliyoifanya times.

Sakata la Diamond, Times FM waomba radhi

Akielezea kuhusu adhabu inayotolewa kwa kituo ambacho kimekosea, amesema ni pamoja na kupigwa faini au kufungiwa na hii inategemea na uzito wa kosa na kuangaliwa kama makosa ya aina hiyo yamekuwa yakijirudia mara kwa mara.

Jana katika taarifa yao, Kituo hicho cha Redio Times cha jijini Dar es Salaam kilichorusha mahojiano ya  mwanamuziki huyo anayefanya vizuri kwenye muziki wa Bongofleva, kiliomba radhi kwa kauli tata zilizozua mjadala nchini.

Taarifa hiyo iliyowekwa jioni katika mtandao wa kijamii wa Instagram, ilisema Times, imeamua kuomba radhi kutokana na kauli tata alizotumia msanii huyo wakati akihojiwa katika kipindi cha Play List kinachoongozwa na mtangazaji Omary Tambwe.

“Kwa namna ambayo haikutarajiwa , mwanamuziki huyo alitumia kauli  tata dhidi ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo, Juliana Shonza katika mahojiano hayo.

Taarifa ya Times ya kuomba radhi imesema: “Uongozi wa Times unaomba radhi kwa Wizara, Naibu Waziri, TCRA, Basata pamoja na umma kutokana na kauli hiyo ya Diamond kwani Times haikuwa dhamira yetu kwa sintofahamu hiyo na tumekuwa tunafanya jazi kwa kuzingatia sheria na taratibu za utangazaji.”

Hatima ya Dhamana ya Mbowe na Vigogo Watano wa Chadema Kujulikana Leo

$
0
0
Hatima ya Dhamana ya  Mbowe na  Vigogo Watano  wa Chadema Kujulikana Leo
Hatima ya vigogo sita wa Chadema wakiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kupata dhamana au kuendelea kusota gerezani itajulikana leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam ikiwa tayari wamekaa mahabusu saa 48.

Wengine ni katibu mkuu, Dk Vincent Mashinji; mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa; manaibu katibu wakuu, John Mnyika (Bara) na Salum Mwalimu (Zanzibar); na Mweka Hazina wa Baraza la Wanawake la chama hicho (Bawacha), Esther Matiko.

Viongozi hao wa juu wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini wanakabiliwa na mashtaka manane, likiwamo la kuhamasisha uasi, chuki na maandamano yaliyosababisha kifo cha mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini.

Wakati hatima ya viongozi hao ikisubiriwa, jana Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro iliwafutia mashtaka washtakiwa 44 kati ya 57 waliokuwa wakidaiwa kutenda makosa manane, likiwamo la kuchoma moto ofisi ya Serikali ya Kijiji cha Sofi wilayani Malinyi Novemba 26 mwaka jana.

Hakimu Ivan Msack wa mahakama hiyo aliwafutia mashtaka hayo baada ya upande wa mashtaka ukiongozwa na wakili wa Serikali, Sunday Hyera kudai hakuna ushahidi wa kutosha kuwatia hatiani.

Hata hivyo, washtakiwa wengine 13 wakiwamo wabunge Susan Kiwanga (Mlimba) na Peter Lijualikali (Kilombero) wataendelea na kesi hiyo na Aprili 24 itakuwa siku ya kusikilizwa maelezo ya awali.

Wakili wa washtakiwa hao, Fredy Kalonga alisema wanajiandaa kwa ushahidi utakaotolewa na upande wa mashtaka dhidi ya washtakiwa hao waliobaki.

Miongoni mwa waliofutiwa mashtaka ni diwani wa Mkula, Clemence Mjami aliyesema uamuzi wa Mahakama unaonyesha wazi namna upande wa mashtaka ulivyojikosoa kwa ushahidi dhaifu.

Kuhusu Mbowe na wenzake, juzi walisomewa mashtaka katika Mahakamani ya Hakimu Mkazi Kisutu na Wakili wa Serikali, Faraja Nchimbi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri katika kesi ya jinai namba 112 ya 2018. Wakili Nchimbi aliwasilisha pia ombi kwa Mahakama hiyo akitaka iwanyime dhamana washtakiwa akidai ni kwa sababu ya usalama wa umma wa Watanzania.

Hakimu Mashauri baada ya kusikiliza ombi hilo alisema atalitolea uamuzi leo. Katika makosa manane, mawili yanawakabili washtakiwa wote sita ambayo ni kufanya mkusanyiko au maandamano yasiyo halali Februari 16 wakidaiwa kufanya hivyo wakiwa Barabara ya Kawawa, Kinondoni Mkwajuni.

Shtaka la pili, viongozi hao wa Chadema wanadaiwa wakiwa na watu wengine 12 ambao hawajafikishwa mahakamani, waligoma kutii amri ya kusambaratika na kuvunja mkusanyiko huo uliosababisha kifo cha Akwilina huku maofisa wa polisi wakipata majeraha. Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni anadaiwa kuhamasisha chuki kwa wanajamii isivyo halali na ushawishi wa utendekaji wa kosa la jinai. Mchungaji Msigwa anashtakiwa akidaiwa kushawishi raia kutenda kosa la jinai.

Rayvanny aeleza ‘ubabe’ wa Diamond ndani ya WCB

$
0
0

Msanii @Rayvanny kutoka @wcb_wasafi amesema katika utendaji kazi wake na @diamondplatnumz ndani ya label hiyo hawajawahi kufikia hatua ya kupishana kauli katika kazi.

MuimbajMakulusai huyo anayetamba na ngoma ‘#’ ameiambia Funiko Base ya Radio Five mara nyingi mambo yanayotokea ni ya kawaida ingawa kuna mengine huonyesha kutopendezwa nayo.

“Nikikosea lazima anikoromee lakini kunikoromea hajawahi kwa sababu yeye siyo mtu wa kufokafoka lakini kitu akikukataza unajua hiki kitu hajakipenda, kwa hiyo unajua wewe hapo inabidi ujiongeze,” amesema @Rayvanny.

Rayvanny na Diamond wameshafanya ngoma pamoja inayokwenda kwa jina la #Salome, pia wamekutana katika ngoma ‘#Zilipendwa’ ambayo iliwakutanisha wasanii wote walio chini ya WCB.

Shamsa Ford Awatolea Uvivu Wasanii Wenzake Awapa Makavu " Tunakosa Ubalozi Kutokana na Matendo Yenu Machafu Wote Tunaonekana Tupo Hivyo"

$
0
0
Shamsa Ford Awatolea Uvivu Wasanii Wenzake Awapa Makavu " Tunakosa Ubalozi Kutokana na Matendo Yenu Machafu Wote Tunaonekana Tupo Hivyo"
Msanii wa filamu nchini Shamsa Ford amefunguka na kuwataka ma-star wa bongo kuachana na matendo machafu kwa madai jambo hilo linawafanya waonekane wote wapo hivyo na kupelekea kukosa kazi za ubalozi wa makampuni yanayolipa Tanzania na nje ya nchi.


Shamsa ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake kijamii asubuhi ya leo baada ya kupita takribani siku kadhaa tokea kuibuka kwa mjadala mzito mitandaoni kwa kile kilichoonekana kwamba ma-star wa bongo kwa sasa hawana thamani nchini na kupelekea mtu wa kigeni kupewa ubalozi wa jambo fulani ndani ya nchi ambayo yeye haishi.

"Kabla ya kuanza kumtafuta mchawi ni nani ni bora kwanza tukajikague wenyewe kwanza, nina uhakika kila biashara ina 'condition' zake na kila biashara inahitaji faida. Hakuna mfanyabiashara atayekubali kumchukua 'star' wa bongo kisa uzalendo tu halafu apate hasara, tusipinge ukweli sisi wenyewe baadhi ya wasanii tumevunja uaminifu kwa wafanyabiashara wakubwa kutokana na matendo yetu", amesema Shamsa.

Pamoja na hayo, Shamsa ameendelea kwa kusema "unapozungumzia kuwa 'ambassador' unazungumzia kubeba 'brand' ya mtu, sasa ni nani anayetaka kuchafua 'brand' yake ibebwe na mtu asiyeeleweka, suala sio kujulikana tu ila unajulikana vipi? maana kama jamii inakudharau hata hiyo bidhaa unayoibeba itadharaulika. Kikubwa tujifunze, tujipange na kufukiaa mashimo yaliyotoboka ili na sisi tueshimike na kuthaminika".

Kwa upande mwingine, Shamsa Ford amesema kulingana na maisha na karne ya sasa ni muhimu kuambiana ukweli ili kuweza kutengeneza mazingira mazuri ya vizazi vya baadae.

PICHA: Lowassa, Sumaye, Prof. Safari Walivyofika Mahakamani Kushuhudia Kesi ya Akina Mbowe

$
0
0
PICHA: Lowassa, Sumaye, Prof. Safari walivyofika Mahakamani Kushuhudia Kesi ya Akina Mbowe
Viongozi waandamizi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo wanatarajiwa kufikishwa leo asubuhi katika Mahakama ya Kisutu kwa ajili ya kusikiliza uamuzi wa dhamana yao huku wakisindikizwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati kuu CHADEMA.


Kesi hiyo ya Viongozi wa CHADEMA inatarajiwa kutajwa leo chini ya Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri ambaye anatarajiwa kutoa uamuzi kuhusu dhamana ya washtakiwa hao.

Hata hivyo baadhi ya Viongozi wengine wa chama hicho wamefika mahakamani hapo ili kuwasindikiza viongozi wenzao wakiongozwa na Mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA, Edward Lowassa, Makamu Mwenyekiti wa Chadema Profesa Abdallah Safari na  baadhi ya Wabunge.

Miguna Miguna Alazwa Hospitali Dubai

$
0
0

Alieidhinisha Kiapo kwa Odinga, Miguna Miguna Alazwa Hospitali
Mwanasiasa wa Kenya aliyeidhinisha kiapo kwa kiongozi wa upinzani Raila Odinga kuwa ‘Rais wa Wananchi’ Miguna Miguna amelazwa hospitalini Dubai baada ya kulalamika kuwa ana maumivu ya mbavu.

Miguna ambae amefukuzwa nchini Kenya kutokana na mzozo wa Uraia wake amedai alipigwa na askari wakati wanamuondoa Airport.



Nafasi za Ajira Zilizotagazwa Siku ya Leo

Breaking News: Wabunge, Madiwani Chadema Waandamana Kwenda Ofisi za Umoja wa Ulaya Kushinikiza Dhamana kwa Vigogo wa Chama Hicho

$
0
0
Wabunge, Madiwani Chadema Watia Kambi Ubalozi wa Ulaya Kushinikiza Dhamana kwa Vigogo wa Chama Hicho
Wabunge wa Chadema, leo mchana Machi 29, 2018 wameandamana kwenda ofisi za Umoja wa Ulaya (EU).

Wabunge hao wamekwenda katika ofisi hizo kulalamikia kile wanachofanyiwa viongozi sita wa chama hicho akiwamo mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe waliopo mahabusu.

Akizungumza na MCL Digital mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amesema, “Tuko EU (Umoja wa Ulaya). Tupo wabunge wote tumeandamana kuja hapa kuleta kilio chetu.”

Lowassa arejea, Mbowe na vigogo Chadema hawajafikishwa mahakamani

Baadhi ya wabunge hao ni, Peter Liajualikali (Kilombero), David Silinde (Momba), Jesca Kishoa (viti maalumu) na Meya wa Ubungo, Boniface Jacob.

Breaking News: Mbowe na Vigogo Watano wa Chadema Wamepewa Dhamana

$
0
0
Breaking News: Mbowe na Vigogo Watano wa Chadema Wamepewa Masharti ya Dhamana
 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewapa dhamana viongozi sita wa Chadema, akiwemo mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.

Washtakiwa hao wametakiwa kuwa na wadhamini wawili ambao watasaini bondi ya Sh20milioni na kuwa na barua kutoka kwa viongozi wao ama wa vijiji au mtaa ambao watapaswa kuwa na nakala za vitambulisho vyao.

Pia, wametakiwa kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi, Dar es Salaam.

Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Wilbard Mashauri amesema asiyeridhika na uamuzi huo ana haki ya kukata rufaa.

Miujiza ya Sharifu Seif Mohamed..JE Umeachwa na Mme/Mke au Mpenzi, Umesongwa na Mitihani ya Maisha

$
0
0
SHARIFU SEIF MOHAMED ANAWASHUKURU WALE WOTE WANAOENDELEA KUPIGA SIMU, WENYE MATATIZO NA WALE WANAOTOA  SHUKRANI NA SHUHUDA JINSI TIBA ZAKE ZINAVYO WASAIDIA,

(Rudisha mahusiano yako ndani ya masaa 72 tu)

SHARIFU MOHAMED Ni  mtaalam na mnajimu maarufu wa nyota na kubashiri mambo yanayo watesa binadamu duniani kote na kupata ufumbuzi, Anatumia kitabu cha QUR'AN na Nyota

Je Umeachwa na UMPENDAE awe Mme/Mke na bado unampenda? Je Umekimbiwa na Mmeo/ Mkeo n anaishi na mtu mwingine? Je Umejaribu sehemu nyingi bila mafanikio? Mpigie simu SHARIFU SEIF sasa hivi ujionee Muujiza wa Papo kwa Papo, Anauwezo wa hali ya juu wa kusambaratisha mahusiano yao na kumrejesha kwako haraka sana na Kumfanya Atimize Ahadi zote Ndani ya Muda Mfupi Endapo Utafwata Atakacho Kuelekeza

 ZINDIKO LA NYUMBA NA BIASHARA, PETE ZA BAHATI, HUMALIZA KABISA TATIZO   HUZUIA CHUMA ULETE KWENYE BIASHARA, HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA, NA KUPONYA MAGONJWA SUGU ANAO UWEZO WA KUMRUDISHA ALIE MBALI AU ALIECHUKULIWA MSUKULE, KUPANDISHA NYOTA NA KUSHINDA BAHATI NA SIBU, KASAFISHA NYOTA NA KUKUPA MVUTO WA AJABU, KUTOA NUKSI NA VIFUNGO MBALIMBALI,  MAFANIKIO YA MAISHA NA UTAJIRI BILA MASHARI, NA MENGINE MENGI YA SIRI,

JE UMAHANGAIKA KUPATA MTOTO BILA MAFANIKIO? WASILIANA NA MTAALAMU HUYU KWANI YEYE HUFAULU PALE WOTE WALIPOSHINDWA, PIA UMALIZA KAZI ZILIZO SHINDIKANA NA WATAALAM WENGINE NDANI YA MASAA 24 TU,

(NA ANATIBU KWA NJIA YA SIMU UKIWA NCHI YOYOTE AU MKOA WOWOTE ENDAPO UTAFWATA MAELEKEZO YAKE)

Kwa ushauri na mawasiliano  zaidi Piga SIMU No:

Mobile +255 654-836970
WhatsApp 0756033670

Viewing all 104709 articles
Browse latest View live




Latest Images