Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104705 articles
Browse latest View live

Mama Aliyejifungua Mapacha wa Baba Wawili Tofauti Azua Gumzo

$
0
0
Mama Aliyejifungua Mapacha wa Baba Wawili Tofauti Azua Gumzo
Mama mmoja aliyefahamika kwa jina la Bi, Rashida Nakabugo nchini Uganda, amejikuta akiingia kwenye gumzo kubwa baada ya kutoka kwa vipimo vya vinasaba (DNA) vinavyoonesha kuwa watoto wake mapacha waliyokuwa wakigombaniwa na wanaume wawili kwa zaidi ya miaka mitatu toka kujifungua kwake kila mmoja ana baba tofauti badala ya kuwa wa mtu mmoja kama ilivyozoeleka.

Miaka mitatu ya mgogoro wa wanaume hao ambao waliyokuwa wana wapigania mapacha hao waliyofahamika kwa jina la Babirye na Leticia Nakato umemalizwa kwa kila mmoja kupata mtoto mmoja kufuatia matokeo hayo ya vinasaba yaliyotolewa na kituo cha Health Viber Diagnostics huko Kampala nchini Uganda.

Vipimo hivyo vya DNA vimeonyesha kuwa, Babirye ni mtoto wa Baseka Sengendo mwenye umri wa miaka 25 mkazi wa Mpigi na Leticia Nakato ni wa Patrick Ssegane mwenye umri wa miaka 30 licha ya kuzaliwa siku moja na mama mmoja.

Kwa mujibu wa chombo cha habari cha New Vision kimeeleza kuwa wanaume wote wawili wanaamini kila mmoja ndiye mzazi sahihi wa mapacha hao Babirye na Leticia Nakato.

Duru ya habari inasema kuwa Ssengendo ni mume halali wa mama huyo, Nakabugo ambaye pia kwa wakati huo mwanamke huyo alikuwa na mahusiano na Bw, Ssegane.

Mume wa Rashida Nakabugo, ambaye ni Ssengendo amesema kuwa wakati mkewe anajifungua hakuwepo nyumbani.

Wakati kwa upande wa Ssegane amesema kuwa alimkubali mama huyo baada ya kutengana na mumewe hata hivyo baada ya woto kukua mara kadhaa amekuwa akihitaji kujua ukweli kuhusu mapacha hao.

Chombo cha habari cha Azam tv hapa nchini kimeripoti kuwa Madaktari baada ya kupata matokeo ya vipimo kuwa ni watoto wenye baba wawili tofauti walivipeleka huko Ohio nchini Marekani (USA) na kuhakiki matokeo hayo na kusema inawezekana.

Maamuzi yaliyofikiwa baada ya matokeo ya habari hiyo ya kushtusha na iliyozua gumzo kubwa nikuwa Ssengendo ameridhia kumuachia watoto wote wawili Ssegane ambaye yeye ndiye aliye leta wazo la kufanyika kwa vipimo hivyo vya vinasaba (DNA) kwakuwa amekuwa akiishi na mwana mke huyo na watoto hao kwa muda wote huo.

Soma Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo

Utafiti Unaonyesha Jinsi ‘Smartphone’ Zinavyoua Kumbukumbu za Binadamu

$
0
0
Utafiti Unaonyesha Jinsi ‘Smartphone’ Zinavyoua Kumbukumbu za Binadamu
Utafiti mpya kutoka nchini Uingereza unaonesha kwamba ongezeko la simu aina ya smartphone na mitandao ya kijamii linalosababisha tabia wa watu kupiga picha mara kwa mara linasababisha watu kupoteza kumbukumbu.

Utafiti huo unaeleza kuwa kupiga picha muda wote kunasbabisha watu kupoteza kumbukumbu ya vitu ambavyo wanaviona na hii ni athari kubwa kwa ustawi wa mtu.

Wanasayansi hao ambao wamechapisha utafiti huo kwenye jarida la Journal of Experimental Social Psychology wameeleza kuwa ongezeko la mitandao ya kijamii halijawa tu athari kwa afya za watumiaji bali hata maisha yao ya kawaida.

Urusi Yalipiza Kisasi kwa Marekani Yawafukuza Wanadiplomasia 60

$
0
0
Urusi Yalipiza Kisasi kwa Marekani Yawafukuza Wanadiplomasia 60
Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergey Lavrov  amefahamisha kuwa  ubalozi mdogo wa Marekani mjini Saint-Petersburg umefungwa na kufukuzwa wanadiplomasia 60.

Hatua hiyo imechukuliwa  na Urusi kama jibu kwa Marekani na Magharibi  na washirika wao kuhusu sumu aliopewa jasusi wa zamani wa  Urusi Skripal.

Uingereza imewafukuza  wanadiplomasia 23 wa Urusi na wengine 150 katika mataifa 25 ya mataifa ya Ulaya. Waziri wa mambo ya nje wa Urusi amesema kuwa uamuzi huo umechukuliwa kama jibu kwa huatua zilizochukuliwa  mataifa ya Magharibi dhidi ya Urudi.

Mtibwa Sugar: Tunatafuta Matokeo na Tutaitumia Azam Kama Njia ya Kusonga Mbele

$
0
0
Mtibwa Sugar: Tunatafuta Matokeo na Tutaitumia Azam Kama Njia ya Kusonga Mbele
Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila amesema wamejiandaa vilivyo kuhakikisha wanaitumia Azam FC kama njia na kusonga mbele katika mechi yao ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports.

Mtibwa Sugar inacheza mechi ya robo fainali ya Kombe la FA kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam na Katwila anaamini wamejiandaa hasa.


"Azam wana timu nzuri lakini kweli tumejiandaa sana na tuko Dar es Salaam kutafuta matokeo ya mechi hiyo," alisema.


Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na uwezo wa wachezaji wa timu hizo ambao wamekuwa wakiuonyesha katika mchuano hiyo na Ligi Kuu Bara msimu huu.

Mshindi katika mechi hiyo ataingia nusu fainali ya michuano hiyo ambayo bingwa wake atapata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika mwakani.

Miujiza ya Sharifu Seif Mohamed..JE Umeachwa na Mme/Mke au Mpenzi, Umesongwa na Mitihani ya Maisha

$
0
0
SHARIFU SEIF MOHAMED ANAWASHUKURU WALE WOTE WANAOENDELEA KUPIGA SIMU, WENYE MATATIZO NA WALE WANAOTOA  SHUKRANI NA SHUHUDA JINSI TIBA ZAKE ZINAVYO WASAIDIA,

(Rudisha mahusiano yako ndani ya masaa 72 tu)

SHARIFU MOHAMED Ni  mtaalam na mnajimu maarufu wa nyota na kubashiri mambo yanayo watesa binadamu duniani kote na kupata ufumbuzi, Anatumia kitabu cha QUR'AN na Nyota

Je Umeachwa na UMPENDAE awe Mme/Mke na bado unampenda? Je Umekimbiwa na Mmeo/ Mkeo n anaishi na mtu mwingine? Je Umejaribu sehemu nyingi bila mafanikio? Mpigie simu SHARIFU SEIF sasa hivi ujionee Muujiza wa Papo kwa Papo, Anauwezo wa hali ya juu wa kusambaratisha mahusiano yao na kumrejesha kwako haraka sana na Kumfanya Atimize Ahadi zote Ndani ya Muda Mfupi Endapo Utafwata Atakacho Kuelekeza

 ZINDIKO LA NYUMBA NA BIASHARA, PETE ZA BAHATI, HUMALIZA KABISA TATIZO   HUZUIA CHUMA ULETE KWENYE BIASHARA, HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA, NA KUPONYA MAGONJWA SUGU ANAO UWEZO WA KUMRUDISHA ALIE MBALI AU ALIECHUKULIWA MSUKULE, KUPANDISHA NYOTA NA KUSHINDA BAHATI NA SIBU, KASAFISHA NYOTA NA KUKUPA MVUTO WA AJABU, KUTOA NUKSI NA VIFUNGO MBALIMBALI,  MAFANIKIO YA MAISHA NA UTAJIRI BILA MASHARI, NA MENGINE MENGI YA SIRI,

JE UMAHANGAIKA KUPATA MTOTO BILA MAFANIKIO? WASILIANA NA MTAALAMU HUYU KWANI YEYE HUFAULU PALE WOTE WALIPOSHINDWA, PIA UMALIZA KAZI ZILIZO SHINDIKANA NA WATAALAM WENGINE NDANI YA MASAA 24 TU,

(NA ANATIBU KWA NJIA YA SIMU UKIWA NCHI YOYOTE AU MKOA WOWOTE ENDAPO UTAFWATA MAELEKEZO YAKE)

Kwa ushauri na mawasiliano  zaidi Piga SIMU No:

Mobile +255 654-836970
WhatsApp 0756033670

Dunia Kusimama kwa Muda Leo Kwenye Mpambano wa Anthony Joshua, Joseph Parker

$
0
0
Dunia Kusimama kwa Muda Leo Kwenye Mpambano wa Anthony Joshua, Joseph Parker
Leo Wales na dunia nzima itasimama kwa muda kuangalia pambano la wanamasumbwi wawili mahiri wa uzito wa juu duniani (heavyweight), Anthony Joshua wa Uingereza na Joseph Parker wa New Zealand.


Pambano hilo la kuwania ubingwa wa Dunia wa uzito wa juu katika mikanda minne ya WBA ,IBF, IBO na WBO , litapigwa uwanja wa Principality Cardiff nchini Wales, uwanja mbao Joshua mwaka jana alitetea mikanda yake dhidi ya Carlos Takam,

Wakali hao wa ndonga wameunganisha mikanda yao Joshua akiweka mezani mikanda yake ya ubingwa wa dunia wa WBA,IBF na IBO huku Parker akiweka mezani mkanda wake wa dunia wa WBO.



Mabondia hao wote ni mabingwa wa dunia na wote  hawajapigwa hata pambano moja, Joshua akiwa na rekodi ya 20-0 akishinda yote kwa KO huku Parker akiwa na rekodi ya 24-0 akishinda 18 kwa KO na 6 kwa pointi.

Pambano litaanza majira saa 4:30 usiku kwa saa za Wales (Saa 6 usiku kwa saa za Afrika mashariki) na bingwa ataondoka na mikanda yote minne.

Picha: Zlatan Ibrahimovic Aanza Mazoezi na Timu Yake Mpya LA Galaxy ya Marekani

$
0
0
Hatimaye mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic ameanza kufanya mazoezi na klabu yake mpya ya LA Galaxy ya Marekani.
Zlatan Ibrahimovic aanza mazoezi na timu yake mpya LA Galaxy ya Marekani

Ibrahimovic (36) ambaye amekabiziwa jezi namba tisa, alikubali kujiunga na timu hiyo wiki iliyopita kwa mkataba wa miezi 18.

Mchezaji wakati akiongea kwenye mkutano wake na waandishi wa habari, amesema alitaka kujiunga na LA Galaxy tangu mwaka 2016 wakati alipomaliza mkataba wake na PSG lakini dili hilo lilibadilika na kutimkia Manchester United.




Jamii Inakosa Muelekeo na Kukosa Haki Wanafunguliwa Kesi Wakubaliane na Uovu wa Kimfumo - Padre Shio

$
0
0
Jamii Inakosa Muelekeo na Kukosa Haki Wanafunguliwa Kesi Wakubaliane na Uovu wa Kimfumo - Padre Shio
Padre Riziki Shio wa Kanisa la Minara Miwili Zanzibar amefunguka na kusema kuwa jamii inakosa mwelekeo na kukosa haki huku wengine lukuki wanafunguliwa kesi ili wakubaliane na uovu wa kimfumo.


Padre Riziki Shio wa Kanisa la Minara Miwili Zanzibar aliyasema hayo jana Machi 31, 2018 katika ibada ya Ijumaa Kuu na kusema kuwa wapo watu wachache au wenye uwezo hukandamiza haki za wanyonge jambo ambalo ameliita uovu wa kimfumo.

"Mateso ya kimfumo ni pale wachache au wenye uwezo wanapokandamiza haki za wanyonge na hasa wale wanaoonekana kuwa mwiba katika maslahi yao, ndugu zangu mataifa mengine popote pasipokuwa na amani tunashuhudia watu wanavyouwawa, wanavyovyamiwa. Mwaka jana tulishuhudia askari wetu kule Congo walivyouwawa wakilinda amani, wao walienda kulinda amani lakini waliuwawa na watu wasiopenda amani"

Padre Riziki aliendelea kusema kuwa

"Wapo wengine huwekwa hata maabusu kwa muda mrefu bila kupelekwa mahakamani kwa vile wamesimama katika ukweli kwa hiyo jamii kama wakati wa Yesu inakosa mwelekeo, ina kosa haki, wengine wanafunguliwa kesi lukuki wakubaliane na uovu wa kimfumo"

Video: Mtalii Afunguka Baada ya Duma Kuingia Ndani ya Gari Serengeti Tanzania

$
0
0
Mtalii Afunguka Baada ya Duma Kuingia Ndani ya Gari Serengeti Tanzania
Mtalii Britton Hayes na mjomba wake kutoka Washington, Marekani wakiwa safarini katika mbuga ya Taifa ya Serengeti Tanzania kujionea wanyama, walijikuta katika wakati mgumu baada ya mnyama duma kuingia katika gari yao na kukaa zaidi ya dakika 10. Mnyama huyo ambaye hakutarajiwa alikaa ndani ya gari hilo kwa dakika 10 katika eneo la Gol Kopjes la mbuga hiyo, kabla ya mwishowe kuondoka kwenda kuwinda swara. Britton Hayes anasema wakati duma huyo anaingia alikuwa anamuangalia duma mmoja aliyekuwa ameruka sehemu ya mbele ya gari lao kumbe kuna mwingine aliruka na kuingia kupitia sehemu ya nyuma bila wao kumuona. “Tulianza kugundua duma hao walikuwa wameanza kuvutiwa na gari letu; lakini hatukuwa na muda wa kuondoka au kutoroka kwa sababu hutaki kuwashtua wanyama hao, ukifanya hivyo ndivyo mambo huenda mrama,” Hayes aliambia jarida la Komo News. “Nilikuwa nimejawa na wasiwasi sana. Lakini wakati wote nilikuwa nauhisi uhai wangu,” anasema.
 

Askari Polisi Apandishwa Kizimbani kwa Kumbaka Mtoto wa Jirani Yake

$
0
0
Polisi apandishwa Kizimbani kwa kumbaka Mtoto wa jirani yake
Askari Polisi namba H.3102 konstebo Bariki Michael (28), wa kituo cha Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi, alifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa akikabiliwa na shtaka la kumbaka mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 14 (jina limehifadhiwa).
Michael alifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi, Erasto Phili na kusomewa shtaka linalomkabili na wakili wa serikali, Juma Maige.
Akisoma shtaka hilo, Maige alidai mshitakiwa alitenda kosa hilo March 14, 2018 saa 4:00 asubuhi eneo la Kilimani mjini Ruangwa.
Wakili huyo alidai kuwa mshtakiwa, akiwa anatambua analofanya ni kosa, alipata mwanya wa kutekeleza tendo hilo nyumbani kwa mtoto huyo, ambaye pia ni jirani yake baada ya kubaki peke yake, ndipo akaitumia nafasi hiyo kumfuata na kumwingilia kwa nguvu.
Maige alidai kutokana na kitendo hicho, mlalamikaji alipiga kelele za kuomba msaada kutoka kwa majirani ambao walijitokeza na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo na kumpeleka kituo chao cha Polisi cha Ruangwa mjini.
Mshtakiwa alikana kosa na kupelekwa mahabusu baada ya kukosa dhamana na kesi yake imepangwa kutajwa mahakamani hapo April 12.
Wakili wa serikali Maige alisema upelelezi wa shauri hilo umekamilika.

Singida Unitedi Yabaki Njia Panda Mkataba wa Mudathir

$
0
0
Singida Unitedi Yabaki Njia Panda Mkataba wa Mudathir
Klabu ya soka ya Singida United bado haijaweka wazi endapo itamsajili kwa mkataba wa kudumu kiungo Mudathir Yahya, ambaye ameachwa na klabu yake ya Azam FC baada ya mkataba wake kumalizika.

Mudathir ambaye anaichezea Singida United kwa mkopo wa msimu mmoja kutokea Azam, kwasasa ni mchezaji huru baada ya Azam kuweka wazi kuwa hawataendelea naye hivyo kama kuna timu inamtaka inaweza kumpata akiwa huru.

Kwa upande wa Singida United bado hawajaweka wazi kama watafanya taratibu za kumsajili kwa mkataba wa kudumu kiungo huyo ambaye kwasasa amerejea timu ya taifa ya Taifa Stars baada ya kukosekana kwa muda.

Mkurugenzi wa Singida United Festo Sanga amesema bado wanalishughulikia suala hilo na watalitolea taarifa kwa muda muafaka lakini kwasasa bado wanajua Mudathir ni mchezaji wao kwa mkataba wa mkopo.

''Ni kweli amemalizana na klabu yake ya Azam FC ambayo sisi tulimsajili kwa mkopo kwa mkataba wa mwaka mmoja lakini kwasasa suala lake tunalishughulikia baada ya timu yake kuweka wazi kuwa haitaendelea naye na amemaliza mkataba kwahiyo ni mchezaji huru'', amesema.

Mwakyembe: Nay wa Mitego Acha Kuwadanganya Wenzako

$
0
0
Mwakyembe: Nay wa Mitego Acha Kuwadanganya Wenzako
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amemuonya msanii Emmanuel Elibariki maaruifu Ney wa Mitego, kuacha kuwadanganya wasanii wenzake wasiende kujisajili Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) wakati yeye keshasajiliwa.

Ney ni kati ya wanamuziki waliofungiwa nyimbo zao zisipigwe kwenye vituo vya redio na televisheni kutokana na kukiuka sheria za maadili za utangazaji za mwaka 2005.

Nyimbo za Ney zilizofungiwa ni ‘Hapo kati patamu’ na ‘Mikono juu’ ambazo zilielezwa maudhi yake hayafai kusikilizwa na jamii.

Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari uliolenga kutangaza kuwasamehe wasanii Pretty Kind na Roma Mkatoliki waliokuwa wamefungiwa miezi sita kutojihusisha na sanaa, Dk Mwakyembe amesema tayari baadhi ya wasanii wameanza kujirekebisha akiwemo Ney aliyepeleka kazi zake mbili Baraza la Sanaa kupitiwa kabla hajazitoa.

"Tunashukuru tangu kutolewa kwa adhabu ya kufungia wasanii na nyimbo zilizokiuka maadili baadhi yao wameanza kurudi kwenye mstari akiwemo msanii Ney ambaye kapeleka nyimbo zake Basata zikahaririwe na kuonekana hazina matatizo,” alisema Dk Mwakyembe na kuongeza:

“Japo huko mtaani amekuwa akiwahadaa wenzake kwamba yeye hawezi kufanya hivyo, mwambieni aache hiyo tabia ya kuwapotosha wenzie."

Akizungumza na MCL Digital hivi karibuni, Ney alitishia kuachana na muziki kwa kile alichodai serikali ilipofikia inawapangia vitu vya kuimba.

Ney alikwenda mbali zaidi na kueleza kuwa wao ndio wanajua mashabiki wao wanataka nini na kueleza kuwa kila wimbo anaoachia hupata watazamaji wengi kwenye mtandao jambo linaloashiria ni namna gani wanamkubali.



Mambo ni Hivi! Mpiga Picha Mkuu wa Daimond 'Kifesi' Atangaza Kuacha Kazi WCB "Inatosha Nimeamua Kufuata Moyo Wangu"

$
0
0
Mambo ni Hivi! Mpiga Picha Mkuu wa Daimond 'Kifesi' Atangaza Kuacha Kazi WCB "Inatosha Nimeamua Kufuata Moyo Wangu"
Aliyekuwa nguzo ya Wasafi Classic Baby (WCB) chini ya Diamond Platnumz katika kitengo cha picha akiwa ndiye mpigapicha mkuu, Andrew almaarufu Kifesi ametangaza kuacha kazi ili kupata muda wa kufanya mambo yake.

Kupitia Ukurasa wake wa Instagram kifesi ameandika: “Leo ikiwa ni siku takatifu na siku ya ibada kwangu ni siku niloamua kufanyamaamzi yatagobadili maisha yangu Nimeamua rasmi kuacha kazi kama Mpiga picha wa diamond na mwajiriwa wa WCB.. Well It’s insane to be leaving a stable job u love But that’s reality for me naacha kaz kwa mtu alokua zaid ya Rafiki kwangu naacha kaz ambayo ni ndoto ya Vijana wengi out there but to me..i see miaka yngu 4/5 ya kufanya kaz hapa inatosha nimeamua kufata moyo wangu . . ni uamzi nilokua nao karibu mwaka sasa but kama ilivo kwa waajiriwa wengi is so hard kufnya maamzi ya kuacha kazi but IN ORDER TO GROW WE NEED TO MAKE CHANGE.. Naacha kazi to persue my Dreams life ikiwamo Kujiajiri. Naacha kazi ili nipate muda mwingi wa kuwa flexible nitumie muda wangu mwingi ku-unleash my potential for excellence.  reason ya mwisho na kubwa zaid kwangu.. Naacha hii kaz ili niwe karibu zaid na Mungu wangu kwa iman yngu kama. Mkristo nilkua nafnya kaz Katika lifestyle na mazingira yasompendeza Mungu.. ni swala ambalo limekua likinikosesha aman kwa miaka yote sawa napta pesa umaarufu pia.. But vyote hiv cyo kitu endapo simpendez Mungu at the end we need to choose GOD over everything.. Cfa. Umaarufu na fahari yote ya Dunia vitanifaidia nn endapo nitaukosa ufalme wa Mungu…?? Nimemaua ku drop kila kitu i just want to be happy.. do my works live my life and hav time with God… Ukimchagua Mungu hata hiv vingine atakuongezea najua kutakua na changamoto nyingi.. Up and downs but Mungu ataniongoza He knew me b4 a was born aliahid ukimchagua yeye he will open the door atatufnya kuwa Kichwa na cyo mkia.. Mwisho Ningependa kushukuru familia yote ya wcb  kwa kua nami for all these yrs was great working with u.. but zaid nimshukuru Diamond kwa mda wote nlofnya nae kaz since chini mpka sasa.. Nimefnya kazi kwa mapenz.. bidii na uaminifu mkubwa Kwangu haukua boss bali rafik n nilkua rafik wa kweli kwako a will always appreciate mchango wako kwenye career yangu.. Tusameheane pale tulipowai koseana we are just humans tuna mapungufu tunakosea..hatutakua pamoja kikaz but  Nina iman tutaendelea kua marafiki. God bless u.. Uzid kufika unapopenda kufika.. GOD Bless me.. God bless my next Hustles #happysabbath Day”

Punguza Unene Unaokusumbua Katika Mwili Kwa Kutumia Bidhaa za Edmark

$
0
0

"Tumia Dawa za Edmark za Kupunguza uzito uliozidi Mwilini Mwako, Edmark ni Vurutubisho na Chakula Mbadala na Zimehakikiwa na TFDA...

Ni uhakika kwa afya yako,👉 kupunguza uzito na sumu mwilini, Mafuta Sehemu Mbaya, Kitambi na nyama uzembe na kutibu MAGONJWA Mbalimbali kwa msaada wako mfuate instagram: @my_health_my_wealth @my_health_my_wealth


Au Mtafute WhatsApp Huyu Dada kwa kutumia Namba +255783 566844

Pia Dawa za Edmark Zinaweza kupa Fursa ya Biashara Uweze pata Kipato Kirahisi kwa Kuwasaidia watu Kuimarisha Afya zao

Mpiga Picha wa Diamond Aacha Kazi, Adai Madhingira ya Kazi WCB Hayampendezi Mungu

$
0
0

Hivi Karibu Pamekuwa na Tetesi kuwa Kifesi Mpiga picha wa Diamond Haelewani na Bosi Wake huyo huku Kifesi akionyesha ukaribu zaidi na Zari Hassan aliyekuwa Mpenzi wa Diamond, Leo ameamua kukata mzizi wa Fitina na kutangaza kuacha kazi WCB.......

From Kifesi - Leo ikiwa ni siku takatifu na siku ya ibada kwangu ni siku niloamua kufanya maamzi yatagobadili maisha yangu Nimeamua rasmi kuacha kazi kama. Mpiga picha wa Fiamond na mwajiriwa WCB..

Well It’s insane to be leaving a stable job u love But that’s reality for me naacha kaz kwa mtu alokua zaid ya Rafiki kwangu naacha kaz ambayo ni ndoto ya Vijana wengi out there but to me..i see miaka yngu 4/5 ya kufanya kaz hapa inatosha niachie nafasi kwa vijana wengine nimeamua kufata moyo wangu . . ni uamzi nilokua nao karibu mwaka sasa but kama ilivo kwa waajiriwa wengi is so hard kufnya maamzi ya kuacha kazi but IN ORDER TO GROW WE NEED TO MAKE CHANGE..

Naacha kazi to persue my Dreams life ikiwamo Kujiajiri mwenyewe.

Naacha kazi ili nipate muda mwingi wa kuwa flexible nitumie muda wangu mwingi ku-unleash my potential for excellence.  reason ya mwisho na kubwa zaid kwangu..

Naacha hii kazi ili niwe karibu zaidi na Mungu wangu kwa iman yangu kama. Mkristo nilikua nafanya kazi Katika lifestyle na mazingira ya kazi yasompendeza Mungu . . ni swala ambalo limenikosesha aman kwa miaka yote but at the end we need to choose GOD over everything.. Sifa ,maarufu na fahari yote ya Dunia vitanifaidia nn endapo nitaukosa ufalme wa Mungu...??

Nimeamaua ku drop kila kitu i just want to have peace of mind .. do my works .. live my life and hav time with God... Ukimchagua Mungu hata hiv vingine atakuongezea najua kutakua na changamoto nyingi.. Up and downs but Mungu He knew me b4 a was born aliahid ukimchagua yeye he will open the doors atatufnya kuwa Kichwa na cyo mkia.. Mwisho nashukuru familia yote ya wcb  kwa kua nami for all these yrs was great working with u.. but zaid nimshukuru Diamond kwa mda wote nlofnya nae kaz since chini mpka sasa.. Nimefanya kazi kwa mapenzi.. bidii na uaminifu mkubwa Kwangu haukua boss bali rafiki n nilkua rafik wa kweli kwako a will always appreciate mchango wako kwangu..

Tusameheane pale tulipowai koseana we are just humans ..hatutakua pamoja kikazi but  Nina iman tutaendelea kua marafiki. God bless u.. Uzidi kufika unapopenda kufika.. GOD Bless me.. God bless my next Hustles

Irene Uwoya Awaacha Njiapanda Mashabiki Zake " Nakupenda Sema Unakaujinga"

$
0
0
Irene Uwoya Awaacha Njiapanda Mashabiki Zake " Nakupenda Sema Unakaujinga"
Leo March 31,2018 kwenye upande wa entertainment story inayochukua headlines ni kuhusu wanandoa wawili muigizaji Irene Uwoya na Dogo Janja hii ni kutokana na comment ya Dogo Janja baada ya post ya Irene Uwoya kwenye instagram page yake.

Irene Uwoya ameandika >>>“Nakupenda sema unakaujinga😏😏😏” baada ya caption hiyo ya Irene Uwoya maswali mengi yalijitokeza kwa mashabiki kutokana na Irene Uwoya kutotaja jina la mtu anayempenda na mwenye ujinga na wengi kubaki na maswali


Baada ya muda Dogo Janja alicomment na kuandika….>>>“Au sio?” comment hiyo ilizidi kuleta maswali kwa mashabiki na wengi kujiuliza kama ujumbe ule ni wa Dogo Janja au la.

DC Hapi Awajia Juu ya Watu Waliovunja Nyumba ya Msanii Mandojo

$
0
0
DC Kinondoni Awajia Juu ya Watu Waliovunja Nyumba ya Msanii Mandojo
Tangu Jumatano kumekuwa na picha na video zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii zikimuonesha msanii wa muziki wa Bongo Fleva Mandojo akilalamika kuvunjiwa nyumba yake na watu wasiojulikana wakati yeye akiwa safarini.


Sasa taarifa nzuri ni kwamba Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi amezipata taarifa hizo na tayari ameshawasiliana na Man Dojo na leo Machi 31, 2018 ameahidi kwenda Mbweni kuangalia uharibifu uliofanyika kwenye nyumba hiyo.

Hapi amewataka watu hao waliovunja nyumba hiyo kujisalimisha mara moja kabla ya hatua za kuwatafuta hazijaanza.

“Mchana huu nimeona clip ya msanii Man Dojo ikimuonesha akilalamika kuvunjiwa nyumba yake aliyoijenga kwa jasho lake la muziki na watu asiowajua akiwa safarini. Watu hao (mabaunsa) wanatajwa kufanya tukio hilo kata ya Mbweni wilayani Kinondoni ngawa video haielezi ni mtaa gani.Ofisi yangu haina taarifa yoyote ya kuvunjwa nyumba eneo la Mbweni.
Yeyote mwenye kumfahamu Man Dojo naomba amjulisha kuwa aje anione nyumbani kwangu kesho jumamosi saa 2 asubuhi.Na hao waliofanya tukio hilo popote walipo,wajisalimishe kabla sijawatafuta!,“amesema Ally Hapi kwenye taarifa yake.

Kwa mujibu wa maelezo ya Man Dojo amesema kuwa watu hao hawajulikani kuwa walitoka wapi kwani hata serikali ya mtaa haikuwa na taarifa na watu hao na kwa sasa Man Dojo na familia yake wanalala nje baada ya tukio hilo.

Watekaji Wamwachia Binti wa Hashimu Rungwe .... Binti Asimulia Alichoulizwa na Watekaji

$
0
0
Watekaji Wamwachia Binti wa Hashimu Rungwe .... Binti Asimulia Alichoulizwa na Watekaji
Mwenyekiti wa chama CHAUMA Hashim Rungwe ambae pia alikuwa miongoni mwa wagombea wa Urais kwa mwaka 2015, March 27, 2018  alitangaza kutoonekana kwa ndugu yake anaeitwa Saida Hilal.

Leo March 31, 2018 amewaita waandishi wa habari wa AyoTV na millardayo.com kusema tayari amempata Binti yake huyo amabe alikuwa ametekwa na watu wasiojulikana.

“Napenda kuwajulisha kwamba siku ya tarehe 28 jioni kuamkia 29, binti huyu Saida Hilal alionekana na waliomteka walimuacha Sinza, walikuwa wamemfunga kitambaa, nilipopata hizi habari nilimfuatilia” -Rungwe

Bavicha: Upo Mpango wa Kuifuta Chadema Ila Tupo Tayari Kufa Kukilinda Chama Chetu

$
0
0
Bavicha: Upo Mpango wa Kuifuta Chadema Ila Tupo Tayari Kufa Kukilinda Chama Chetu
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema, (Bavicha) Patric Ole Sosopi, amesema Serikali ya awamu ya tano ina lengo la kuifuta Chadema.

Akizungumza leo, Machi 31, katika mkutano na wanahabari uliofanyika katika ofisi za chama hicho, Sosopi amesema, wapo watu wanaotumwa na Serikali kuichafua Chadema na kupata sababu ya kukifuta chama hicho.

“Tumewapuuza kwa muda mrefu, tukiamini vyombo vitachukua hatua dhidi yake lakini kwa kuwa wanamtuma anaendelea kuwa salama,” amesema.

Amesema Chadema inawahakikishia Watanzania kuwa jitihada za kuifuta Chadema hazitafanikiwa na hakuna yeyote atakayeifuta Chadema.
Viewing all 104705 articles
Browse latest View live




Latest Images