Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live

TFF Yafunguka Baada ya Kupokea Ombi la CECAFA

0
0
TFF yafunguka baada ya kupokea ya CECAFA
Kufuatia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupokea barua kutoka Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), ikiomba Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano ya KAGAME, TFF wamesema watafikiria ombi hilo.

Kwa mujibu wa Afisa Habari wa TFF, Clifford Mario, amesema kuwa ni kweli wamepokea barua hiyo, ila watakaa wajadili kama taasisi ili baadaye waweze kuja na majibu rasmi ya michuano hiyo kama itafanyika au kutofanyika.

Clifford ameeleza kuwa watahitaji kufikiria ombi hilo kulingana na hivi sasa ina ratiba ya mashindano ya soka la vijana kuelekea kufuzu AFCON chini ya miaka 20, hivyo watakuja na jibu rasmi baadaye.

CECAFA imetuma barua hiyo ikiiomba Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano ya Kombe la Kagame kwa ngazi ya klabu ambayo yanataraji kuanza mwezi Juni 2018.


Mke wa Roma Aingia Hofu "Dah Nawazaa Sijui Baba Ataimba Nini Sasa 'Round' Hii!"

0
0
Mke wa Roma Aingia Hofu "Dah Nawazaa Sijui Baba Ataimba Nini Sasa 'Round' Hii!"
Mke wa Rapa anayefanya vizuri sana Bongo, Roma Mkatoliki ameweka wazi hofu yake juu ya kazi za sanaa anazofanya mume wake huyo ambapo amesema anamuwazia kwa sasa atakuwa anaimba nini.


Mke wa msanii huyo anayefahamika kwa jina la Nancy ambaye pia ni mama wa watoto wawili wa msanii huyo ameonyesha wasiwasi wake huo kutokana na matatizo yaliyomuandama mume wake huyo ikiwa ni pamoja na kufungiwa kufanya kazi za sana kwa miezi sita ingawa siku ya Ijumaa iliyopita Waziri husika alitangaza kumfulia na kumpatia sharti mija la kujisajili kwenye Baraza la Sanaa Taifa.

Nancy amesema kwamba "Dah nawazaa sijui Baba ataimba nini Sasa 'Round' hii!!!! Nways Tutegee sikio Tu.

Hata hivyo kabla ya kuuhariri ujumbe huo Mke wa  Roma alidai kuwa mumewe anakaziwa kila njia anayojaribu kupenya ambapo amemshauri mumewe kukaa kimya kwani bado anamuhitaji huku akionyesha hofu kwenye wimbo aliouandika jina "NIKIFA CHIMBENI MAKABURI MATATU”.

Roma ni msanii ambaye ni muhanga wa kufungiwa katika kazi zake za sanaa ambapo 2015 alifungiwa wimbo wa 'Viva Roma, na mwaka 2017 mwishoni alifungiwa wimbo wa Kibamia ambao ndiyo uliopelekea kupewa kifungo cha miezi sita.

Huenda Ukurasa Wako wa Kijamii Ukachunguzwa Iwapo Utaomba Visa ya Marekani

0
0
Huenda ukurasa wako wa kijamii ukachunguzwa iwapo utaomba Visa ya Marekani
Utawala wa Trump umesema kuwa unataka kuanza kukusanya historia ya mitandao ya kijamii ya karibu kila mtu anayetaka visa ya kuingia Marekani.

Pendekezo hilo , ambalo limetolewa na wizara ya mambo ya nje, litawataka wengi miongoni mwa waombaji wa visa kutoa maelezo yao ya akaunti zaoi za Facebook na Twitter

Watatakiwa kufichua majina ya akaunti zao zote za mitandao ya kijamii waliyotumiwa katika kipindi cha miaka mitano ya nyuma

Taarifa hizo zitatumiwa kutambua na kuwachunguza watu wanaoomba viza za uhamiaji pamoja na zisizo za uhamiaji.

Waombaji wa visa pia wataulizwa kuhusu nambari za simu walizotumia katika kipindi cha miaka mitano, barua pepena historia yao ya kusafiri.

Watatakiwa kusema ikiwa hawajawahi kurejeshwa kwa lazima kutoka nchi waliyotembelea kwa lazima , ama ikiwa kuna ndugu yao yeyote aliyewahi kuhusika katika harakati za ugaidi .

Pendekezo hilo litazidisha masaibu kwa wasafiri ambao nchi zao hazina mkataba na marekani wa kuziondolea visa
Pendekezo hili halitawaathiri raia kutoka nchi ambazo Marekani ilizipa hadhi ya kutokuwa na visa - miongoni mwake Uingereza , Canada, France na Ujerumani . Hata hivyo raia kutoka nchi ambazo hazijapewa hadhi hiyo kama India, China na Mexico wanaweza kujipata katika hali ngumu kama wataitembelea Marekani kikazi ama kwa mapumziko.

Chini ya sheria iliyowekwa mwezi Mei mwaka jana, maafisa waliambiwa wachunguze kurasa za mitandao ya kijamii ya watu ikiwa tu wanahisi kufanya hivyo " kwamba taarifa za aina hiyo zinahitajika kuthibitisha utambulisho ama kufanya uchunguzi wa kina zaidi kwa ajili ya usalama wa taifa ", ilisema wizara ya mambo ya nje wakati mmoja.

Pendekezo hilo linakuja baada ya rais Trump kuahidi kutekeleza''uchunguzi mkali'' kwa raia wa kigeni wanaingia Marekani, jambo ambalo alisema lilikuwa ni moja ya mkakati wa kupambana na ugaidi.

"Kuimarisha viwango vya upelelezi mkali kwa waombaji wa visa ni kazi inayotakiwa kufanywa vizuri ili kukabiliana na vitisho vilivyopo," ilieleza taarifa ya wizara ya mambo ya kigeni, iliyonukuliwa nagazeti la New York Times.

"Tayari tunaomba taarifa chache zamuombaji wa visa kama vile historia ya muombaji, taarifa za wanafamilia, na anuani za awali kutoka kwa waombaji wote wa visa.

Trump ajitetea kuhusu Sweden
Kukusanywa kwa taarifa hizi zote kutoka kwa waombaji wa visa kutaimarisha mchakato wetu wa kuwachunguza wahamiaji hawa na kuthibitisha utambulisho wao ."

Wazo hili litatakiwa kuidhinishwa na ofisi ya Utawala na Tna bajeti ya Marekani.

Umma utakuwa na miezi miwili ya kutoa maoni yake juu ya pendekezo hili kabla ya kuchukuliwa kwa uamuzi rasmi wa utekelezwaji wake.

Hata hivyo makundi yanayochunguza uhuru wa raia yamelaani sera hii wakiitaja kuwa ni uingiliaji wa masuala binafsi jambo linaloweza kuathiri uhuru wa kujieleza.

"Watu sasa wataanza kufikiria juu ya ikiwa kile wanachokisema mtandaoni kitachukuliwa ama kueleweka vibaya na afisa wa serikali ," alisema Hina Shamsi kutoka Muungano unaopigania uhuru wa raia nchini Marekani -( American Civil Liberties Union).

" Pia tuna hofu juu ya namna utawala wa mtizamo wa Trump kuhusu maneno yanayofaa ama yasiyofaa '' kuhusiana an shughuli za ugaidi ' kwasababu neneo ugaidi lilikuwa ni la kisiasa na linaweza kutumiwa kuwabaguwa wahamiaji ambao hawajafanya kosa lolote ," alisema .

Mitandao ya kijamii iliyohusishwa na pendekezo hilo ni pamoja na Instagram, LinkedIn, Reddit na YouTube. Hata hivyo gazeti la New York Times linaripoti kuwa mitandao ya nchi za nje kama vile ule wa Uchina wa Weibo na wa Urusi VK pia itajumuishwa..

Mnyama Mrefu Zaidi Duniani Amegundulika Kuwa Ana Sumu

0
0
Mnyama mrefu zaidi duniani amegundulika kuwa ana sumu
Wanasayansi kila kukicha wanafanya tafiti ili kugundua vitu vipya sasa leo March 31, 2018 imegundulika kuwa Mnyama mrefu zaidi duniani ana sumu.

Watafiti nchini Sweden wamegundua kuwa mnyoo wenye urefu wa Mita 55 ana sumu lakini sumu hiyo haina madhara yoyote  kwa binadamu.

Profesa wa chuo kikuu cha Uppsala nchini Sweden,Prof. Dr. Ulf Göransson wakati alipohojiwa na kituo che television cha taifa amesema kuwa  utafiti kuhusiana na minyoo inayoishi katika hali ya baridi nchini humo umeoyesha kuwa minyoo hiyo ina sumu.

Kwa mujibu wa habari taarifa iliyotolewa Sweden, inawezekaan siku za baadae minyoo hiyo inaweza kuja kutumika kutengeneza dawa.

Minyoo hiyo kwa lugha ya kirumi inaitwa “Lineus longissimus”,na ina urefu wa mita 55-60

Video: Viongozi Chadema Waungana Kula Pasaka Gerezani na Sugu, Mbowe

0
0
Baadhi ya Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) wamejigawa wengine wataenda mkoani Mbeya kumtembela Sugu gerezani na wengine wataenda Segerea kumtembelea Mwenyekiti wao na viongozi wengine wa Chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mwenyekiti wa Baraza la vijana Chadema (BAVICHA)Taifa, Patric Sosopi amesema kuwa ni haki yao kuwatembelea viongozi hao gerezani.

Dogo Janja akubali kuwa ‘Video Queen’ katika video ya Nikki Mbishi

0
0
Dogo Janja akubali kuwa ‘Video Queen’ katika video ya Nikki Mbishi
Takribani wiki mbili zilizopita Dogo Janja aliingia katika headlines hasa katika stori za kidaku mara baada ya kutokea katika video ya ngoma yake ‘Wayu Wayu’ akiwa na muonekana wa kike.

Kitendo hicho kilizua mjadala mpana kiasi katika music industry kwa hapa Bongo. Sasa Rapper Nikki Mbishi hajawa nyuma katika hilo, kupitia ukurasa wa twitter Nikki ameandika; Dogo Janja ni “VIDEO QUEENG” .

Baada ya tweet hiyo Dogo Janja amejibu; Chupa Lako Ukinihitaji Onana Na Management bei yangu SIO GHALI SANA.

Jibu hilo linaweza kutafsiriwa kuwa Dogo Janja yupo tayari kufanya hivyo katika video ya Nikki au msanii yeyote ila kinachotakiwa ni kuonana na menejimenti yake kwa ajili ya malipo kitu ambacho mwishoni amesisitiza sio ghali.

Madee ambaye anafanya kazi na Dogo Janja kupitia Tip Top Connection anatajwa kuwa ndiye alimpatia Janjaro idea ya video hiyo. Madee alikaririwa akisema idea hiyo alitaka kuitumia katika video yake ila hakuwa na wimbo wa kutoa hivi karibuni ndipo akaitoa kwa dogo Janja.

Mbowe Atuma Salamu Toka Gerezani

0
0
Mbowe Atuma Salamu Toka Gerezani
Viongozi sita wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Freeman Mbowe, wamewataka Watanzania na wanachama wao wasiogope kwa sababu katika kupigania haki, demokrasia, amani na ustawi wa nchi lazima wapatikane watakaoumia kwa ajili ya wengine.

Ujumbe huo wameutoa wakiwa ndani ya Gereza la Segerea, Dar es Salaam jana ikiwa ni siku moja imepita baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuamuru viongozi hao wafikishwe mahakamani Aprili 3, mwaka huu ili kutimiza masharti ya dhamana zao baada ya juzi kudaiwa kushindwa kufikishwa kutokana na gari kuwa bovu.

Ujumbe huo wa Mbowe na viongozi wenzake ulitolewa jana na Mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini na kada wa chama hicho, Dk. Makongoro Mahanga, waliopata muda wa nusu saa kuzungumza mambo mbalimbali na viongozi hao.

Selasini na Mahanga waliweka ujumbe huo katika akaunti zao za mtandao wa Facebook, pamoja na mambo mengine walisema wamewaona viongozi na haya ndiyo maneno yao: ‘Tuko imara, tuko vizuri. Wapelekeeni wenzetu ujumbe huu. Msiogope. Taifa linatutegemea. Chadema ndiyo pekee itakayobadilisha uonevu unaofanywa na watawala kwa Watanzania na kuwahakikishia demokrasia, amani ya kweli, haki na maendeleo. Tukiwa waoga tutakuwa wasaliti wa matamanio hayo ya Watanzania.’

“Wamesema pia wamepata muda mzuri wa kupumzika na kufanya retreat (tafakari ya kina. Tumemkuta Mbowe akiwa na Biblia mkononi. Amesema amesoma na karibu anamaliza Injili zote. Pia yeye pamoja na Mchungaji Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini leo (jana) wataadhimisha ibada ya Ijumaa Kuu kwa kuwashirikisha mahabusu na wafungwa wote wao kama watumishi wa neno la Mungu.”

Moi Yatoa Taarifa Wabunge Sita Waliopata Ajali Morogogo

0
0
Moi Yatoa Taarifa Wabunge Sita Waliopata Ajali Morogogo
Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) imeeleza umma kwamba hali ya wabunge sita kutoka Zanzibar waliopata ajali ya Alhamisi mkoani Morogoro wanaendelea vizuri na matibabu katika taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.

Taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa taasisi hiyo Patrick Mvungi leo Machi 31, kwa njia ya simu imeeleza kwamba wabunge hao wanaendelea kupewa huduma na madaktari bingwa wa mifupa katika taasisi hiyo.

“Wanaendelea kupata huduma kutokana majeraha waliyopata kwenye vichwa, mikono, vifua na miguu. Kwa ujumla hali zao zinaendelea vizuri,” amesema.

Wabunge hao wamelazwa katika taasisi hiyo kwa ajili ya matibabu baada ya gari walilokuwa wanasafiria kutoka Dodoma kuja Dar es Salaam kupata ajali eneo la Bwawani katika barabara kuu ya Dar es Salaam-Morogoro siku ya Alhamisi saa mbili usiku.

Kabla ya kupelekwa Muhimbili, wabunge hao walipelekwa katika hospitali ya mkoa wa Morogoro kwa matibabu.

Wabunge walionusurika katika ajali hiyo ni Haji Amir Kimbe (49), kutoka Makunduchi,  Hamis Ally (54), (Mkwajuni) Bagwanji May (Twaka); Makame Mashaka (46), (Kijini); , Juma Athman Hija (Tumbatu) na Masudi Ally Hamis (Makunduchi).


Siri imefichuka Kumbe Kifesi Amefukuzwa Kazi na Diamond Platnumz

0
0
Baada ya  Kifesi kuandika kupitia Instagram kuwa ameamua aache kazi ya upiga picha WCB, Hatimae dada yake Diamond Platnumz anajulikana kwa jina la Esma Platnumz amesema kuwa kifesi amefukuzwa kazi wala hajaacha kazi kwasababu ya kufatilia mambo ya Bosi wake,  Akasema wao wamemshindwa sembuse yeye mtu baki

Esma Platnumz Ameandika hayo pia kupitia ukurasa wake wa Instagram kama inavyoonyesha kwenye picha hapo juu.....Mambo ni Moto!

Hashimu Rungwe: Watu wasiojulikana waliokuwa wamemteka binti yangu wamemwachia tarehe 28/03/18

0
0
Mwenyekiti wa chama CHAUMA Hashim Rungwe ambae pia alikuwa miongoni mwa wagombea wa Urais kwa mwaka 2015, March 27, 2018 alitangaza kutoonekana kwa ndugu yake anaeitwa Saida Hilal.

Leo March 31, 2018 amewaita waandishi wa habari na kusema tayari amempata Binti yake huyo amabe alikuwa ametekwa na watu wasiojulikana.

“Napenda kuwajulisha kwamba siku ya tarehe 28 jioni kuamkia 29, binti huyu Saida Hilal alionekana na waliomteka walimuacha Sinza, walikuwa wamemfunga kitambaa, nilipopata hizi habari nilimfuatilia”

Inasikitisha! Mwanamke wa Kitanzania Auwawa Kikatili Uingereza

0
0
Inasikitisha! Mwanamke wa Kitanzania Auwawa Kikatili Uingereza
MTANZANIA Leyla Mtumwa (36) mkazi wa Arusha aliyekuwa akiishi Uingereza anadaiwa kuuawa kwa kuchomwa visu sehemu mbalimbali za mwili wake na mwanaume mwenye umri wa miaka 38 (jina halijatajwa) ambaye pia ni Mtanzania anayesemekana kuwa ni mpenzi wake waliokuwa wakiishi naye pamoja.

Tukio hilo la kusikitisha lilitokea usiku wa kamkia jana Machi 30, 2018, katika nyumba wanayoishi Watanzania hao iliyopo eneo la Haringey, Kirkstall Avenue, N17  jijini London, baada ya kuzuka ugomvi baina yao ikiwa ni muda mfupi baada Leyla kurejea nyumbani akitokea disco la usiku alikokuwa amekwenda na marafiki zake.

Vyanzo mbalimbali vinaeleza kuwa, alirudi kutoka disco akiwa na rafiki yake wamelewa na kuingia ndani, ambapo alimkuta mpenzi wake  ambaye alianza kufoka na kutukana jambo lililoibua mzozo mkali baina yao.

Baada ya mzozo huo kuwa mkubwa rafiki aliondoka na ndipo jamaa huyo alianza kumshushia kipigo kisha kumchoma visu mbele ya mtoto wake wa miaka 12, ambaye Leyla alizaa na mumewe wa kwanza anayedaiwa kuwa ni raia wa Nigeria.

Ikiwa ni majira ya saa 1:00 asubuhi, hali ya Leyla ilikuwa mbaya, kijana huyo alipiga simu katika kitengo maalum cha polisi cha makosa ya jinai (Met’s Homicide and Major Crime Command), kuwajulisha tukio hilo.

Baada ya polisi kuwasili walimkuta Leyla akiugulia majeraha ya visu huku akilia maumivu makali aliyokuwa akiyapata, walimchukua kwa Ambulance na kumpeleka hospitali.

Licha ya jitihada za polisi kuwahi, lakini Leyla aliaga dunia majira ya saa 2:11 asubuhi kwa saa za London. Polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo huku wakimshikilia mwanaume huyo wa Leyla kama mtuhumiwa namba moja wa tukio hilo.

Arnold Schwarzenegger Amefanyiwa Upasuaji wa Moyo

0
0
 Arnold Schwarzenegger Amefanyiwa Upasuaji wa Moyo
Muigizaji  staa wa Hollywood Arnold Schwarzenegger amefanyiwa upasuaji wa moyo.

Arnold Schwarzenegger ambae amecheza katika filamu takriban 50 na alikuwa Gavana wa zamani wa California amefanyiwa upasuaji wa moyo ambao umemalizika salama.

Meneja wa nyota huyo amesema kuwa mnamo mwaka 1997 Arnold Schwarzenegger aliwekewa “pulmonary valve”,na upasuaji huu umefanywa ili kumuwekea “pulmonary valve” mpya.

Kama kawaida katika filamu zake Schwarzenegger hutumia sana neno la “I’ll be back”na baada ya upasuaji amerekodiwa akisema, “I am back”.

Zaidi ya Shule Ishirini Zachomwa Moto Kwenye Mapigano DR Congo

0
0
Zaidi ya Shule Ishirini Zachomwa Moto Kwenye Mapigano DR Congo
Takriban shule ishirini zimechomwa moto kutokana na mapigano yanayoendelea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Kwa mujibu wa habari,ndani ya wiki mbili zilizopita shule za msingi na sekondari zimekuwa zikiangamizwa kwa moto katika mapigano ya kikabila kaskazini mashariki mwa DRC.

Afisa polisi Ivan Legu amekiambia kituo cha habari cha Anadolu kuwa zaidi ya shule 60 zimefungwa katika vijiji sita eneo la  Djugu,Ituri.

Hii ni kutokana na mapigano na mashambulizi ambayo yamekuwa yakifanywa kati ya jamii za Lendu na Hema.

Zaidi ya watu arobaini wamepoteza maisha katika mapigano hayo,hali iliyoilazimu serikali kutuma majeshi kutuliza ghasia lakini bado haikusaidia.

Eneo la Ituri linaongoz katika mapigano ya kikabila na kusababisha vifo vya wengi.

VIDEO: Hali ya Taharuki Yatanda kwa Familia Nne Dar

0
0
VIDEO: Hali ya taharuki yatanda kwa familia nne Dar
Katika hali isiyokuwa ya kawaida leo Mtaa wa Kibasila, Kata ya Upanga Mashariki, jijini Dar es Salaam, kundi la mabaunsa wamevamia nyumba wanayoishi wanawake na kuwafanyia vitendo vya udhalilishaji.

Kamanda wa Polisi Mkoa Maalumu wa Kipolisi, Salumu Hamduni, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa wanamshikilia mtuhumiwa mmoja aliyeshiriki na wanaendelea na mahojiano huku msako kwa wahusika wengine ukiendelea.

Pata Huduma za Matibabu ya Asili na Nyota Pamoja na Pete za Bahati

0
0
Mtabibu Mongwa husafisha nyota na kutoa Pete za bahati na kwawale walio sumbuka kwaajili ya matibabu na hawakufanikiwa chochote sasa njoo ujionee miujiza hapo kwahapo bila malipo yoyote malipo baada yakazi napia humpa mtu jini la mali kwayule anaye taka kumiliki bila mashariti yoyote
Tunatibu magonjwa mbalimbali yaliyo shindikana mpenzi aliye kukimbia nakumrudisha kwa masaa 24 tu napia natoa dawa za nguvu za kiume kuurefusha uume paka pale unapotaka .

Natoa dawa za biashara na mvuto ==tunatoa dawa zauzazi kwa wale kina mama wenye matatizoya uzazi walio angaika kwa muda mrefu bila kupata mafanikio yoyote njoo umalize tatizo lako sasa
Natoa mazindiko yanyumba na mwili biashara na mvuto kazini

Kupandisha nyota ili kungaa kupandishwa cheo kazini kurudisha mali zilizo pote zilizo ibiwa kuzulumiwa
Kesi zilizo shindikana uzimaliza mara moja namengine mengi ya siri piga simu

+255 764291657

Nyundo za Maaskofu Zaitesa Serikali...Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya April 1

0
0

Nyundo za Maaskofu Zaitesa Serikali...Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya April 1

Profesa Kitila asema maudhui ya waraka wa maaskofu hayaakisi wajibu na msingi wa kanisa

0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Profesa Kitila Mkumbo amemwandikia barua Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), Askofu Frederick Shoo akitoa maoni yake binafsi kwa kanisa hilo kuhusu maudhui ya waraka wa maaskofu wa kanisa hilo uliotolewa hivi karibuni.

Waraka wa maaskofu 27 wa KKKT ulitoka hivi karibuni na ulitarajiwa kusomwa katika makanisa yote ya kilutheri Machi 25, 2018.

Katika waraka huo maaskofu walizungumzia  Katiba mpya, uchumi, siasa na jamii.

“Katika kutoa maoni yangu kuhusu Waraka huo, ninalenga mambo makubwa mawili ambayo ni pongezi kwenu, na pili ni mtazamo wangu juu ya baadhi ya masuala yaliyomo katika Waraka huo,” amesema Kitila katika barua yake aliyoisaini Machi 29 mwaka huu.

Pamoja na kuwapongeza maaskofu hao, Kitila ameandika katika barua yake kuwa maudhui yaliyowekwa katika waraka wa maaskofu hao, hayaakisi hadhi na wajibu wa msingi wa kanisa.

“Kama ambavyo mmekuwa mkitufundisha siku zote, na vile tusomavyo katika Biblia Takatifu, ninafahamu kuwa kazi za msingi za kanisa ni zile ambazo Bwana wetu Yesu Kristo alizifanya alipokuwa duniani,”amesema.

Kitila ambaye ameandika barua hiyo kama muumini wa KKKT, amesema anakubaliana na mengi maaskofu waliyogusia katika Waraka huo akiamini yamefundisha na kuponya roho za waumini kwa kiasi kikubwa.

Hata hivyo, alichambua hoja katika maeneo matano zilizoibuliwa na maaskofu hao na kusema ni sahihi lakini akatahadharisha kuwa ni muhimu kwa kanisa kujiepusha na kuonekana lipo upande fulani katika mijadala ya kitaifa inayogusia jamii.

“Kwa kufanya hivyo, mtaepusha migawanyiko isiyo ya lazima kwa waumini ndani ya kanisa na wananchi kwa ujumla.” Amesema.

Amesisitiza kuwa ni muhimu kwa kanisa kupima kwa umakini mkubwa uzito wa kila neno kabla ya kutoa kauli katika umma.

“Ni hatari kwa Kanisa kutoa kauli inayosababisha maumivu na mifarakano badala ya kuponya.”

TFF Hatimaye Yasikiliza Rufaa Ya Wambura Sasa Yasubiri Maamuzi Ya Kamati Ya Maadili Kutoa Hukumu

0
0
Ile rufaa inayomhusu aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Michael Richard Wambura, imesikilizwa jana kwa pande zote mbili kukutana katika makao makuu ya shirikisho hilo yaliyopo mitaa ya Karume, Ilala.

Kwa mujibu wa Wakili wa Wambura,Emmanuel Muga, amesema pande zote mbili zimemaliza vizuri kikao hicho na mambo yamekwenda sawia, kinachosubiriwa tu sasa ni maamuzi ya Kamati ya Maadili kutoa hukumu.

Muga ambaye anamtetea Wambura, ameeleza TFF wamesikiliza kwa umakini utetezi wa Wambura vilevile TFF nao wakizungumza ya kwao kuhusiana na mustakabali mzima wa kesi hiyo.

Wambura alikata rufaa kupinga kufungiwa kujihusisha na soka baada ya TFF kumfungia kwa madai ya kufanya ubadhirifu wa fedha za shirikisho hilo pamoja na makosa mengine.

Kamati ya Maadili itakaa na kuandaa rasmi na majibu ya hukumu juu ya rufaa hiyo iliyosikilizwa jana Jumamosi.

Mpiga Picha wa Diamond Ajibu Kuhusu Kufukuzwa WCB

0
0
Baada ya Mpiga Picha wa Diamond Platnumz ‘Kifesi’ kutangaza kuacha kazi hiyo, kumeibuka stori kuwa Kifesi amefukuzwa kazi kitu ambacho amekikanusha vikali.

Kifesi amesema taarifa zinazodai kuwa amefukuzwa kazi hazina ukweli wowote na kilichotokea ni maamuzi yake binafsi.

“Hapana sijawahi kuachishwa kazi, kama niliachishwa basi niliachishwa pasipo kupewa taarifa, ninachofahamu nimechukua maamuzi haya na ni kitu ambacho nilikuwa nimepanga kufanya kutoka siku nyingi, so jana nikasema i think it right time to do this,” Amesema Kifesi

Pia amejibu kuhusu kuingilia masuala ya Diamond na Zari ndiko kumepelekea hayo, Kifesi amejibu; “Kumtetea zari sijaanza leo, ukiangalia Instagram kuna posti za zamani nilikuwa nafanya hivyo lakini ni suala gumu kulielezea”.

Dada wa Diamond, Ema Platnumz baada ya kusikia taarifa za Kifesi kuacha kazi, kwenye moja ya post Instagram ali-comment; “Acha uongo Kifesi umefukuzwa kwa kuacha kazi na kufuatilia maisha ya bosi wako yametushinda sie wee mtu baki utaweza”.

Tatua Matatizo yako Kwa Mtaalam wa Dua na Dawa za Kiarabu Pamoja na Mitishamba...

0
0
YULE MTAHALAM WA DUA NA DAWA ZA KIARABU NA ZA KIASILI YANI MITI SHAMBA SHARIFU LUKUMANI SASA YUPO HEWANI WENYE SHIDA ZITUATAZO CHEO KAZINI,KUONGEZEWA MSHAHARA KAZINI,MWENYE TATIZO LA NGUVU ZA KIUME,ALIEPOTELEWA NA HAMU YA KUFANYA TENDO LA NDOA, MWENYE KIFAFA,KISUKARI,FANGASI SEHEMU ZA SIRI KWA WALE WENYE MIILI MINENE MTOTO WA JICHO PAMOJA NA WALE WAKINA MAMA WANAOSUMBULIA NA CHANGO LA UZAZI PUMU YA MUDA MREFU WANAWAKE KUJAA MAJI SEHEMU ZA SIRI MWANAUME KUWAI KUFIKA KILELENI AU KUTOA MANII MFANO WA MAJIMAJI YAKIWA MEPESI AUTOWEZA KUMPA MKEO UJAUZITO JAMBO HILI LINAWASUMBUA WANAUME WALIO WENGI DUNIANI KWA KAWAIDA WANAUME ASIE NA TATIZO HILI UTOA MANII MAZITO NDIO YENYEUWEZO WA KUMPA MWANAMKE MIMBA.MWANAUME KUPATA MPENZI KWA ULAISI PASIPO NA GHARAMA YOYOTE YANI KWA WALE MADOMO ZEGE KUWA NA UWEZO WA KUSIKILIZWA HATAKAMA RAIA WA INCHI GANI NA UWEZO WA KURUDISHA MPENZI ALIE POTEA NA KUMFANYA AWE WAKO KWA WALE WASIO TAKA MITALA PIA UFANYA KAZI YA KUNG'ALISHA NYOTA SASA MATATIZO YAKO YAMEPATA SULUHISHO

 ANAPATIKA KWA MASAA ISHIRINI NA NNE WASILIANA NAE KWA NAMBA
 0762899488
0656145170
WhatsApp namba +255620665635
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live




Latest Images