Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live

Rufaa ya Wambura Yafika Patamu

$
0
0
Rufaa ya Wambura Yafika Patamu
RUFAA ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Richard Wambura, sasa imefikia patamu baada ya juzi Jumamosi kusikilizwa katika makao makuu ya shirikisho hilo, Karume jijini Dar es Salaam na hivi sasa watu wengi wanataka kujua nini kinachofuatia.



Hivi karibuni, Wambura alikata rufaa Kamati ya Rufaa ya Maadili ya TFF kupinga maamuzi ya Kamati ya Maadili ya shirikisho hilo ya kumfungia maisha kujihusisha na soka kwa madai ya kufanya ubadhirifu wa fedha za shirikisho hilo pamoja na makosa mengine.



Wakili wa Wambura, Emmanuel Muga, ameliambia Championi Jumatatu kuwa, kamati hiyo iliziita pande mbili zote zinazochuana katika sakata hilo na kuzisikiliza kwa umakini mkubwa.

Alisema katika kikao hicho, mambo yalienda vizuri, kwa hiyo kinachosubiriwa tu hivi sasa ni maamuzi ya hiyo kamati.



“Kamati imesikiliza kwa umakini utetezi wa Wambura, vilevile TFF nao wakizungumza ya kwao kuhusiana na mustakabali mzima wa kesi hiyo. Kwa hiyo tunachosubiri ni hukumu, “ alisema Muga.

Ofisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo alipoulizwa kuwa ni lini hukumu hiyo itatolewa, alisema: “Itakapokuwa tayari basi itatolewa, kwa hiyo wapenzi wa soka waendelee kuwa wavumilivu.”

Mzungu Aiweka Kiporo Yanga

$
0
0
Mzungu Aiweka Kiporo Yanga
Lechantre, raia wa Ufaransa, ameiweka Yanga kiporo baada ya kusema kuwa, mechi hiyo itakuja kuamua bingwa wa ligi kuu msimu huu kama wote wawili watavuka salama mechi za hapa kati.

Simba na Yanga ambazo zinatarajiwa kupambana Aprili 29, mwaka huu, kwa sasa zote zina pointi 46 ambapo Simba inaongoza ikiwa na mabao mengi ya kufunga.



Kabla ya Aprili 29, Simba itacheza dhidi ya Njombe Mji, Mtibwa Sugar, Mbeya City, Prisons na Lipuli, huku Yanga ikicheza na Singida United, pamoja na mechi mbili za kimataifa za Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Wolaitta Dicha ya Ethiopia.

Lechantre amesema: “Mechi dhidi ya Yanga ipo mbali, hivyo kama wote tukivuka salama hapa kati ni wazi mechi hiyo itaamua nani bingwa msimu huu.”



Simba ambayo ili msimu ujao ishiriki michuano ya kimataifa kama msimu huu, inatakiwa iwe bingwa wa ligi kuu tofauti na wenzao Yanga ambao kwa sasa wana nafasi tatu za kuiwakilisha nchi kimataifa msimu ujao.

Nafasi ya kwanza ni kwenye Kombe la FA ambapo jana Jumapili walitarajiwa kucheza robo fainali dhidi ya Singida United, pia wana nafasi kwenye ligi kuu kama wakiwa mabingwa, lakini pia katika Kombe la Shirikisho ikitokea wamefika fainali na kuwa mabingwa wataiwakilisha tena nchi.

Askofu Cheyo Awaonya Watanzania " Fanyeni Kazi Njema Zinazompendeza Bwana"

$
0
0
Askofu Cheyo Awaonya Watanzania " Fanyeni Kazi Njema Zinazompendeza Bwana"Askofu Kiongozi wa  Moravian Tanzania jimbo la Kusini Magharibi Alinikisa Cheyo, amewaasa Watanzania kuacha kulalamika na badala yuake wajikite katika kufanya kazi njema inayompendeza Mungu.


Askofu Cheyo ametoa kauli hiyo katika ibada ya Pasaka iliyofanyika katika Kanisa Moravian Tanzania jimbo la kusini Magharibi ushirika wa Mbeya Mjini.

Askofu amesema ili  Watanzania waweze  kujiletea maendeleo yenye tija kufikia uchumi wa kati wanapaswa kuachana na mambo ya kisiasaili waweze  kufanya shughuli zao za kujiingizia kipato.

Askofu Cheyo pia ametumia fursa hiyo kuwaasa viongozi wake wengine wa dini nchini kutofautisha dini na siasa ili kujenga upendo miongoni mwa Watanzania ikiwa ni pamoja na kudumisha amani ya nchi.

Miguna Miguna Asafirishwa Kutoka Dubai Kwenda Canada

$
0
0
Miguna Miguna Asafirishwa Kutoka Dubai Kwenda Canada

Mwanasiasa wa upinzani aliyezuiwa kuingia Kenya wiki iliyopita na kusafirishwa kwa lazima hadi Dubai amewasili nchini Canada.



Bw Miguna Miguna, ambaye ni wakili, alisafiri kwa ndege iliyokuwa ikielekea Toronto, Canada, baada ya kukaa katika uwanja wa kimataifa wa Dubai kwa siku nne.

Mmoja wa mawakili wa mwanasiasa huyo Nelson Havi ameandika kwenye Twitter kwamba Bw Miguna amesafiri kwenda Canada kwa hiari kupitia usaidizi wa ubalozi wa Canada katika Umoja wa Milki za Kiarabu (UAE).

Bw Havi amesema Miguna atafanyiwa uchunguzi wa kimatibabu na "atarejea baadaye".

Ruka ujumbe wa Twitter wa @NelsonHavi

Nelson Havi
@NelsonHavi
 Miguna Miguna has, out of his own voalition and with the assistance of the Canadian Consulate in UAE, travelled to and arrived in Toronto, Canada. He will undergo toxicology tests and treatment for the chemicals used to sedate and poison him. He will return thereafter.

1:21 PM - Apr 2, 2018
373
289 people are talking about this
Twitter Ads info and privacy
Mwisho wa ujumbe wa Twitter wa @NelsonHavi
Gazeti la Nation, limesema afisa mmoja wa serikali amewafahamisha kwamba Bw Miguna aliondoka Dubai akitumia ndege ya Air Canada 57 (ACA57) baada ya kuwasilisha pasipoti yake ya Canada.

Bw Miguna alikuwa amesema hakuwa na pasipoti hiyo alipowasili uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta, Nairobi Jumatatu wiki iliyopita.

Miguna asafirishwa tena kutoka Kenya
Wahusika mpango wa kumuapisha Odinga Kenya
Bw Miguna ndiye aliyeidhinisha kiapo cha Bw Raila Odinga alipokuwa anajiapisha kuwa 'Rais wa Wananchi' mwezi Januari.

Bw Miguna Miguna alijaribu kurejea Kenya Jumatatu lakini akazuiwa kuingia baada yake kudaiwa kutowasilisha pasipoti ya Canada ambayo ilitumiwa kumsafirisha kwa nguvu hadi Canada.

Wakili huyo alisisitiza kwamba ni raia wa Kenya na hafai kuzuiwa kurejea.

Taarifa zinasema Bw Miguna, ambaye pasipoti yake ya Kenya ilitwaliwa na polisi kabla ya kuondolewa kwake Kenya mwezi jana, alikuwa ametakiwa kuwasilisha ombi la kupata visa ya kukaa Kenya kwa miezi sita kwa kutumia pasipoti hiyo yake ya Canada.

Alikataa jaribio hilo na badala yake kutoa kitambulisho chake cha taifa kuonesha kwamba yeye ni Mkenya na kutaka aruhusiwe kuingia.

Bw Miguna, aliyekuwa amewasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta mwendo wa saa nane adhuhuri, alikesha kwenye uwanja huo.

Maafisa walijaribu kumsafirisha kutoka uwanja huo mara ya kwanza kwa kutumia ndege ya shirika la Emirates ambayo ilikuwa inaelekea Canada kupitia Dubai usiku huo wa Jumatatu lakini hawakufanikiwa.

Haki miliki ya pichaAFP/GETTY
Image caption
Bw Odinga alijaribu kumsaidia Bw Miguna kuondoka uwanja wa ndege bila mafanikio Jumatatu
Hata hivyo, walifanikiwa usiku wa kuamkia Jumatano.

Bw Miguna asubuhi aliandika kwenye Facebook kwamba aliamka na kujipata yuko Dubai na kwamba anahitaji matibabu.

Mwanasiasa huyo alisema alisindikizwa na afisa wa idara ya ujasusi na kwamba amemuona daktari uwanja wa ndege.

Bw Miguna alisisitiza kwamba hatasafiri kwenda popote ila kurejea Nairobi.

Serikali imechukua hatua hiyo licha ya kuwepo kwa maagizo ya mahakama ya kuzuia kutimuliwa kwake na ya kuitaka serikali kufanikisha kurejea kwake nchini humo.

Jaji wa Mahakama Kuu George Odunga aliwapata na hatia waziri wa usalama nchini humo, mkuu wa polisi na mkuu wa idara ya uhamiaji ya kukaidi maagizo ya mahakama iwapo wangekataa kumwachilia huru.

Aliwatoza faini ya Sh200,000 (Dola 2,000) kila mmoja.

Kukamatwa kwa Miguna mara ya kwanza
Bw Miguna alikamatwa na polisi kwa mchango wake katika kuapishwa kwa Bw Odinga kuwa "rais wa wananchi", hafla iliyofanyika uwanja wa Uhuru Park, Nairobi mnamo 30 Januari.

Bw Miguna, ambaye pia ni wakili, ndiye aliyetia saini hati ya kiapo ya Bw Odinga.

Serikali ilikuwa imeeleza hatua hiyo ya kiongozi huyo wa upinzani kuwa uhaini wa hali ya juu.

Bw Odinga anadai kwamba alimshinda Rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi mkuu wa 8 Agosti ambao matokeo yake yalifutiliwa mbali na Mahakama ya Juu kwa sababu ya kutokea kwa kasoro nyingi.

Mahakama iliamuru uchaguzi mpya ufanyike lakini Bw Odinga akasusia uchaguzi huo mnamo 26 Oktoba.

Haki miliki ya pichaHISANI
Image caption
Bw Miguna alisambaza picha anazosema ni zake akiwa hospitalini kumuona daktari uwanja wa ndege Dubai punde baada ya kufikishwa Dubai
Chini ya Kifungu 17 cha Katiba ya Kenya, mtu aliyezaliwa nchini Kenya anaweza tu kuupoteza uraia wake iwapo itabainika kwamba aliupata uraia huo kwa njia ya ulaghai, au ibainike kwamba mtu huyo au wazazi wake walikuwa raia wa nchi nyingine, au ibainike kwamba mtu huyo alikuwa na umri wa zaidi ya miaka minane alipogunduliwa akiishi Kenya.

Serikali ya Kenya imekuwa ikisisitiza kwamba chini ya katiba ya zamani, Wakenya hawangekuwa na uraia wa nchi mbili.

Serikali inasema hatua ya Bw Miguna ya kupata pasipoti ya Canada mwaka 1988 ina maana kwamba aliupoteza uraia wa Kenya wakati huo.

Raila Odinga: ''Hatutambui uchaguzi wa Uhuru Kenyatta''
Ingawa Bw Miguna aliwasilisha maombi na akapewa pasipoti ya Kenya mwaka 2009, serikali inasema pasipoti hiyo ya Kenya si halali kwa sababu hakufichua kwamba wakati huo alikuwa raia wa Canada pia.

Serikali imesema mwanasiasa huyo hakuwasilisha tena ombi la kuruhusiwa kuwa raia wa Kenya katiba ilipofanyiwa marekebisho mwaka 2010 na Wakenya wakakubaliwa kuwa na uraia wa nchi mbili.

Bw Miguna amekuwa akisisitiza kwamba hakuwahi kuukana uraia wake wa Kenya na kamwe hawezi kufanya hivyo.

"Katiba iko wazi kabisa: hakuna mtu yeytoe anayeweza au anayeweza kudai kuufuta uraia wa Mkenya aliyezaliwa nchini Kenya," alisema awali.

Matukio makuu mzozo kuhusu Miguna
30 Januari: Miguna aidhinisha hati ya kiapo cha Raila Odinga kuwa 'Rais wa Wananchi'

2 Februari: Atangaza kwamba amekamatwa na polisi Nairobi

6 Februari: Afurushwa kutoka Kenya na kupelekwa Canada

16 Machi: Odinga waambia wafuasi wake kwamba baada ya mapato yake na Bw Kenyatta, Miguna anafaa kuruhusiwa kurejea Kenya bila masharti

26 Machi: Arejea Kenya lakini azuiliwa uwanja wa ndege wa JKIA. Baadaye usiku, anusurika jaribio la kumpeleka Dubai.

28 Machi: Miguna apelekwa Dubai kwa nguvu. Asema anafahamu mipango ya kumpeleka hadi London.

Miguna Miguna ni nani?
Miguna alizaliwa katika kijiji cha Magina, katika jimbo la Kisumu, magharibi mwa Kenya.

Bw Miguna amekuwa kiongozi wa kundi linaloitwa National Resistance Movement (NRM, Vuguvugu la Taifa la Kupinga Serikali), ambalo liliundwa na muungano wa upinzani wa National Super Alliance siku moja kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa marudio ambao Bw Odinga alisusia mnamo 26 Oktoba mwaka jana.

"Utakuwa ni muungano wa ukombozi," alisema Bw Odinga akitangaza kuundwa kwa vuguvugu hilo.

"Tumesema hatutaheshimu serikali dhalimu."

Bw Miguna baadaye alijitangaza kuwa Jenerali wa NRM.

Mnamo 30 Januari, siku ya kuapishwa kwa Bw Odinga kuwa 'Rais wa Wananchi', muungano huo uliorodheshwa kuwa kundi haramu na waziri wa usalama Dkt Fred Matiang'i.

Hiyo haikuwa mara ya kwanza kwa Bw Miguna kujipata akikabiliana na serikali na nguvu zake.

Mwaka 1988, alikamatwa na serikali ya wakati huo ya Rais Daniel arap Moi.

Bw Miguna baadaye alitorokea Kenya ambapo alipata hifadhi kama mkimbizi wa kisiasa.

Alirejea nchini Kenya na akashiriki katika kampeni za uchaguzi za Bw Odinga na chama chake cha Orange Democratic Movement (ODM) mwaka 2007.

Uchaguzi wa mwaka huo ulikumbwa na utata na baada ya serikali ya muungano kati ya Bw Odinga na Rais Mwai Kibaki kuundwa, ambapo Bw Odinga aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu, Bw Miguna alihudumu kama mmoja wa washauri wake kati ya 2009 na 2011

Wawili hao walizozana na Bw Miguna akawa mmoja wa wakosoaji wakuu wa Bw Odinga.

Aliandika kitabu kwa jina Peeling Back the Mask ambapo alimkosoa sana Bw Odinga na uongozi wake.

Mwaka 2013, alimuunga mkono Bw Kenyatta katika uchaguzi wa urais mwaka huo.

Lakini alibadilisha tena msimamo wake na kurejea upande wa Bw Odinga mwaka 2017, mwaka ambao aliwania pia wadhifa wa Gavana wa Nairobi katika uchaguzi uliofanyika Agosti ingawa kama mgombea ambaye hakuwa na chama.

Januari 30 mwaka huu, ndiye aliyetia saini hati ya kiapo cha Bw Odinga kuwa 'Rais wa Wananchi'.

Bw Odinga alipokutana na Bw Kenyatta mnamo 9 Machi na wakaahidi kuunganisha Kenya, Bw Miguna ni miongoni mwa waliomkosoa kiongozi huyo wa upinzani kwa hatua hiyo akisema huo ulikuwa sawa na usaliti.

Tumbili Aiba Mtoto na Kutoroka Naye

$
0
0
macau monkeyPolisi nchini India wanamsaka tumbili mmoja ambaye aliiba mtoto na kutoroka naye katika jimbo la Orissa, mashariki mwa nchi hiyo.

Mwili wa mtoto huyo ulipatikana baadaye kwenye kisima.

Mamake mtoto huyo mvulana anasema alishuhudia kisa hicho kikitokea lakini hakuweza kumuokoa.

Jamaa wake aliupata mwili wa mvulana huyo kwenye kisima nyuma ya nyumba yao, siku moja baada ya mvulana huyo kuibwa na tumbili huyo.

Mnyama huyo alikuwa ameingia ndani ya nyumba ya familia hiyo na kumtwaa mtoto huyo.

Polisi wanasema kisa hicho ni cha kipekee sana, ingawa mara kwa mara tumbili hupatikana wakiharibu mali eneo hilo.

"Tunatumai kwamba tutafanikiwa kumkamata tumbili huyu katika kipindi cha wiki moja," afisa mmoja wa polisi kwa jina Pradhan ameambia BBC.
"Ingawa visa vya tumbili kuwashambulia binadamu au kuingia kwenye manyumba ya watu wakitafuta chakula ni vya kawaida, hiki ndicho kisa cha kwanza kwa tumbili kutoroka na mtoto," ameongeza.

Polisi wanashirikiana na watu wa jamii moja eneo hilo, ambao ni stadi wa kuwakamata tumbili.

Maafisa wa idara ya msitu wameambia BBC kwamba tumbili huyo aliingia kwenye nyumba ya familia hiyo Jumamosi asubuhi na kutoroka na mtoto huyo.

Wanyama waliowahi kushinda nyadhifa uchaguzini
Nyani azima umeme kwa karibu masaa 6 nchini Zambia
Daktari aliyeuchunguza mwili wa mvulana huyo anasema haukuwa na alama za majeraha.

"Inaonekana alifariki kutokana na kukosa hewa pengine kutokana na kuzama kwenye maji kisimani," amesema daktari huyo.

Wakazi wameambia wanahabari kwamba huenda tumbili huyo alimwangusha mtoto huyo akitoroka.

Mwigulu: Wanaoanzisha nyumba za ibada wapewe masharti mepesi

$
0
0
Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba amesema watu wanaoanzisha nyumba za ibada wapewe vibali haraka na masharti mepesi, kwani nyumba hizo zinapunguza vitendo vya ukatili na kuleta amani nchini.

Akizungumza kwenye Tamasha la Pasaka jijini hapa Kwa Niaba ya Mgeni Rasmi Makamu wa Rais  Samia Suluhu, mara baada ya uzinduzi wa albamu ya Rose Mhando iitwayo "Usivunjike Moyo" aliwataka wanaotoa vibali vya nyumba za ibaada watoe vibali haraka ili wananchi wapate huduma hiyo ya kiroho.

"Unakuta vibali vya nyumba za starehe vinatolewa ndani ya wiki moja huku vibali vya nyumba za ibada vinatoka kwa miaka kadhaa, sitapenda hali hiyo ijitokeze tena  hapa nchini, ukizingatia watu wanataka amani kupitia nyumba hizo muwapungizie masharti ya uanzishaji," alisema Waziri huyo.
Aidha aliwaomba watoa huduma katika nyumba za ibada wasihubiri kukebei, kubagua, na kutukana  imani za watu wengine kwani italeta chuki na amani haitakuepo tena.

Pia aliwashukuru waimbaji wa nyimbo za injili na kuahidi kupeleka waraka katika  mikoa yote na kuhakikisha wanaanza kuwakamata wanaofanya uhalifu wa nyimbo za injili.

Baadhi ya waimbaji waliohudumu katika tamasha hilo Boniphace Mwaitege, Martha Mwaipaja, Christina Shusho na Martha Baraka.

Wema Sepetu: Sioni Wivu Diamond Kumkumbatia Hamisa Mobeto

$
0
0
Wakati habari zilizopo mjini kwa sasa ni tukio la mwanamitindo Hamisa Mobetto na msanii wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ’Diamond’ kuteka tukio la utoaji tuzo za filamu za Sinema Zetu International Film Festival Award (SZIFF), kwa mrembo Wema Sepetu yeye kaichukulia kawaida.

Diamond na Mobeto katika tuzo hizo zilizofanyika jana ukumbi wa Mlimani City , walikwenda kama wageni waalikwa, walichaguliwa kukabidhi tuzo kwa mshindi wa kipengele cha ‘Best Original Music’ ambayo ilikwenda kwa filamu ya Safari ya Gwalu.

Katika kipengele hicho watu walikuwa wanasubiri kwa hamu kuona namna gani Wema ataweza kukabidhiwa tuzo na wawili hao, kwa kuwa filamu yake ya ‘Heaven Sent’ ilikuwa ni mojawapo iliyokuwa ikishindanishwa lakini bahati ndiyo hivyo haikuwa yake.

Akizungumzia namna alivyochukulia  kitendo cha Mobetto na Diamond kufika eneo hilo na kuweza kukabidhi tuzo, Wema ambaye aliwahi kuwa mpenzi wa Diamond miaka kadhaa iliyopita na hivi karibuni kuelezwa kwamba wamerudiana, amesema kitendo hicho kwake amekichukulia kawaida kwa kuwa Mobetto na Diamond ni mtu na mzazi mwenzake.

“Wee ulitaka nichukuliaje labda, Mobetto na Diamond hawa ni wazazi jamani , ulitaka nikasirike au,halafu isitoshe mimi sina uhusiano wa kimapenzi na Diamond  bali ni washkaji tu na siyo kama watu wanavyosema,”amesema Wema.

Kuhusu hatua yake ya kupata tuzo mbili ya msanii bora wa kike na chaguo la watu (People’s Choice Award) kupitia filamu yake ya ‘Heaven Sent’, Wema amesema amefurahi kuona majaji wameweza kuona kipaji alichonacho.

Pia, aliahidi kuendelea kuwapa mashabiki wake kazi nzuri na kuwaondoa hofu wadau wa filamu waliokuwa wanasema kuwa bongo movie imekufa kuwa siyo kweli bali ilikuwa imelala tu.

Hata hivyo, hakusita kutoa shukurani kwa mashabiki zake ambao amesema ni  kati ya watu ambao waliweza kushiriki kumpigia picha hadi kuhakikisha anapata ushindi huo.

Breaking News: Winnie Mandela Afariki Dunia!!

$
0
0

Winnie Mandela, ambaye ni mke wa zamani wa Rais wa Afrika Kusini, Nelson Mandela amefariki leo akiwa na umri wa miaka 81
Mungu ametoa na Mungu ametwaa, Jina Lake Lihimidiwe...R.I.P Mkombozi wa Africa!

Guardiola Ahofia Safu ya Mbele Inayoongozwa na Salah

$
0
0
Guardiola ahofia safu ya mbele inayoongozwa na Salah
Kocha wa vinara wa ligi kuu soka ya England EPL Manchester City Pep Guardiola, amesema safu ya mbele ya klabu ya Liverpool inayoongozwa na Mohamed Salah haizuiliki kirahisi.



Guardiola ameyasema hayo kuelekea mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo Man City watakuwa wageni wa Liverpool Jumatano April 4 kabla ya kurudiana wiki mbili zijazo.

"Sio Salah tu ni wote watatu Mane na Firmino, wameshindaka kutoka na kiwango chao cha kufunga, kwasasa ni safu kali na yakuogopa sana'', amesema Pep Guardiola ambaye timu yake inaongoza ligi ikiwa na alama 84.

Msimu huu tayari Mohamed Salah ana mabao 37 huku Roberto Firmino na Sadio Mane kwa pamoja wana mabao 38. Nyota hao wote walihusika kwenye ushindi wa mabao 4-3 iliopata Liverpool dhidi ya Man City Januari 14.

Aidha Guardiola ameongeza kuwa mchezo huo utakuwa mgumu kwani Liverpool kwa ujumla ipo kwenye kiwango kizuri msimu huu na michuano ya Ligi ya Mabingwa ikifikia hatua ya robo fainali kila mechi huwa ni ngumu.

Video: Haji Manara Awafananisha Daimond, Alikiba na Ronardo na Messi

$
0
0
Video: Haji Manara Awafananisha Daimond, Alikiba na Ronardo na Messi
OFISA Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara, amewakutanisha mahasimu wawili wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz na Ali Kiba.





Haji Manara amewakutanisha wasanii hao kwa kuweka video mbili tofauti moja ikiwa ni ya Diamond na nyingine ya mchezaji Ronaldo, zote pamoja katika akaunti yake ya Instagram huku akiwaongelea kila mmoja kwa namna yake anayotambua vipaji vyao.



Manara amemuelezea Diamond kuwa anajituma kwa kupambana zaidi huku akimuita kama Mfalme. Wakati huo huo Manara amesema anampenda Ronaldo lakini Messi anajua mno huku akieleza kuwa Ronaldo anajiongeza zaidi kwa kile anachokifanya jambo ambalo ni sawa na Diamond na Kiba.



“Chibu na Kiba wote wana vipaji, ingawa Kiba ana sauti na tone kali zaidi, lakini Chibu amezaliwa kuwa msanii mkubwa na amejiongeza zaidi. Napenda vipaji lakini napenda wanatumia fursa kikamilifu,”

Azam Yafunguka Hali ya Mlinda Mlango Wake Aliyezimia Uwanjani

$
0
0
Azamu Yafunguka Hali ya Mlinda Mlango Wake Aliyezimia Uwanjani
Klabu ya soka ya Azam FC imeeleza kuwa mlinzi wake David Mwantika, anaendelea vizuri baada ya kupata hitilafu ya mwili wakati wa mchezo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho (ASFC) dhidi ya Mtibwa Sugar.


Daktari wa Azam FC, Dr. Mwanandi Mwankema, anayeshughulikia taratibu za matibabu ya Mwantika amesema kuwa beki huyo anaendelea vizuri na matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

“Tunamshukuru Mungu David anaendelea vizuri na matibabu na yupo kwenye hatua za kuruhusiwa kurejea nyumbani baada ya kupata nafuu kutoka kwenye tatizo lililompata juzi,” alisema.



Mwantika alizimia dakika ya 64 na kupatiwa matibabu ya awali kabla ya kukimbizwa Hospitali ya Mbagala Zakhem na kuhamishiwa Hospitali ya Wilaya ya Temeke, na baadaye Muhimbili (MNH) ambako anaendelea kupata matibabu.

Aidha Dkt. Mwanandi amesema taratibu zinazofanyika kabla ya mchezaji huyo kuruhusiwa ni kufanyiwa uchunguzi wa moyo ili kufahamu kama ana tatizo hilo kwaajili ya matibabu zaidi.

Vikao vya Bunge Kuanza Kesho Dodoma

Waziri Mkuu Aitaja Mikoa Minne Inayoongoza kwa Utoro wa Wanafunzi

$
0
0
Waziri Mkuu Aitaja Mikoa Minne Inayoongoza kwa Utoro wa Wanafunzi
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameitaja mikoa ya Tabora, Geita, Mtwara na Shinyanga kuwa inaongoza kwa utoro wa wanafunzi wa sekondari.

Waziri mkuu pia ameitaja mikoa ya Rukwa, Geita, Tabora, Singida na Simiyu kuwa inaongoza kwa utoro wa wanafunzi wa shule za msingi.

Majaliwa ambaye pia ni mbunge wa Ruangwa ameitaja mikoa hiyo leo Jumatatu Aprili 2,2018 akizindua mbio za Mwenge wa Uhuru katika uwanja wa Magogo mkoani Geita.

Mbio za Mwenge zitakazohitimishwa Oktoba 14,2018 mkoani Tanga zinaongozwa na kauli mbiu “Elimu ni ufunguo wa maisha, wekeza sasa kwa maendeleo ya nchi yetu.”

Majaliwa amesema Mkoa wa Tabora unaongoza kwa asilimia 9.7 ya wanafunzi watoro wa sekondari ukifuatiwa na Geita (asilimia 8.1), Mtwara (asilimia 6.1) na Shinyanga (asilimia 6.3).

Kwa shule za msingi, Rukwa inaongoza kwa asilimia 3.2, ukifuata Geita (asilimia 3.1), Tabora (asilimia 2.9), Singida (asilimia 2) na Simiyu (asilimia 2).

“Kwa jumla utoro wa wanafunzi wa sekondari ni mkubwa kuliko shule za msingi. Naikumbusha mikoa yote niliyoitaja kuhamasisha wananchi wakiwamo wazazi na walezi kuhusu umuhimu wa elimu na mahudhurio endelevu shuleni kwa kutumia utaratibu wa sheria zilizowekwa,” amesema Majaliwa.

Hii ni Habari Njema kwa Wanaume na Wanawake Wote Wanaopenda Muonekano Mzuri

$
0
0

*PENDEZA_KESSY_ PRODUCT* : WEKA MUONEKANO WAKO VIZUR SASA, NIWAUZA TIBA NA UREMBO NA MAFUTA YASIO NA MADHARA YEYOTE WALA KEMIKALI KWA MATUMIZI NA MATOKEO NI MUDA WA KUANZIA WEEK (2) HADI (4)🍌🌾🥑

1) KUTOA MVI SUGU PIA ZA KUZALIWA NAZO _100,000/
2) KUREFUSH NYWELE KUZIJAZA NA KUZUIAKUKATIKA -100,000/
3) TENGENEZA MWILI WAKO KUWA NA UMBO ZURI (@)KUPAK-100,000/(B) KUNYWA (C)VIDONGE-130,000/
4)ONDOA NYAMA UZEMBE MIKONONI, TUMBON KUPAK -100,000/
5)TOA KITAMBI KABISA(@) KUPAK-10O,000/ (B)VIDONGE/SLIMING YAKUNYWA-130,000/
6) PUNGUZA MWILI MZIMA KUANZIA KILO UNAZOITAJI WEWE
@) DAW YA MAJIN NA VIDONGE_130,000/
7)PUNGUZA MAZIWA NA YASIMAME KAMA MWANZO _90,000/
8) KUONGEZA MAZIWA SAIZI UNAYOHITAJI WEWE_90,000/
9)ONGEZA UNENE WA MWILI MZIMA_100,000/
10) ONDOA MICHIRIZI ILIYO SHINDIKANA_90,000/
11) TOA MAKOVU, CHUNUSI, WEUSI KWENY MAPAJA KIKWAPAN_80,000/
13) KUWA MWEUPE NARANGI NZURI VIDOGO(WHITE SOLUTION)_130,000/(B)MAFUTA YAKUPAK 100,000/
14)TOA NDEVU KWA WANAWAKE NA VINYWELEO MWILINI _100,000/
15/ ONGEZA NGUVU KWA WANAUME (@)JELI AINAZOTE -100,000/(B)VIDONGE MAX MAN NA AINA NYINGI_ 100,000/
16) KUREFUSH MAUMBIL YA WANAUME
@) (HANDSOME UP) MASHINE _200,000/
@) JELI NA VIDONG VYA SHARK_130,000/
17) RUDISHA HAMU YA TENDO NA KUCHELEWA KUMALUZA HARAKA_100,000/
18) MAFUT YAKURUDISH USCHANA-100,000/
19) TOA MAFUT USON NA WEUSI WAMACHO _90,000/
20) ONDOA MIKUNJO USON_80,000/(21) ENGEZA MGUU (WABIA)_100,000/ 21) PATA MIKANDA YAKUPUNGUZA TUMBON AINA ZOTE 22) DAW YA NGIRI YAKUVIMBA NA KULEGEA 100,000/🍍🌾🥑

TUNAPATIKAN DAR E SALAAM:PIA NJE YA NCHI TUNATUMA MIZIGO,NA KWA MIKOAN KOTE UTAPATA *KESSY* NI WAAMINIFU WA KUTUM MIZIGO NA KUFIKA KWA WAKATI PIGA CM (+255) 0719955528
0756259180
0785371237
@ *Pendeza_kessy_product*
Delivery POPOTE ULIPO,

Baadhi ya Bidhaa zetu..


Al Shabaab Waua Wanajeshi Wanne Kutoka Uganda

$
0
0

Wanajeshi wanne wa jeshi la Uganda katika kikosi cha kulinda amani  nchini Somalia AMISOM wameauwa katika shambulizi lililotkelezwa na wanmagambo wa kundi la kigaidi la al shabaab. Shambulizi hilo limetekelezwa Jumapili.

Msemaji wa jeshi la Uganda  Richard Karemire  aliambia shirika la habari la Anadolu kuwa  wanajeshi wanne wa Uganda katika kikosi hicho cha kulinda amani Somalia wameuawa na wengine 6 wamaejeruhiwa.

Shambulizi hilo limetekelezwa katika kambi inayopatikana Bula Marer.

Kwa mujibu wa msemaji huyo , wanagambo wa kundi la al shabaab  wapatao 30  waliuawa katika operesheni walipokuwa wakijaribu  kushambulia kambi tofauti za jeshi la ushirika la kulinda mani nchini Somalia AMISOM.

Kambi zilizokuwa zikilengwa na magaidi hao ni kambi ya Qoryoley, Buulo Marer na Golwen.

Watu 18 wameuawa na wengine 84 wamejeruhiwa

$
0
0

Takriban watu 18 wameuawa na wengine 84 wamejeruhiwa katika shambulizi lililofanywa na waasi wa Boko Haram waliokuwa wakipambana dhidi ya wanajeshi wa serikali karibu na mji wa kaskazini mashariki wa Maiduguri usiku wa kuamkia leo.

Shirika la kitaifa la kushughulikia maafa na matukio ya dharura nchini Nigeria limesema kufikia sasa wamepata miili 18 kutoka vijiji viwili vya Bale Shuwa na Bale Kura vilivyoko mkoa wa Maiduguri na kuongeza wahanga hao waliuawa walipokuwa wakijaribu kukimbia mapigano yanayojiri kati ya waasi na wanajeshi.

Maiduguri ambao ni mji mkuu wa jimbo la Borno ndiyo chimbuko la kundi hilo la waasi la Boko Haram ambalo lilianza uasi miaka tisa iliyopita kaskazini mashariki mwa Nigeria.Kiasi ya watu 20,000 wameuawa tangu wakati huo na karibu milioni mbili kuachwa bila ya makazi.

Waziri Mkuu Mpya wa Ethiopia Aapishwa Rasmi

$
0
0

Bunge la Ethiopia limemchagua Abiye Ahmed kuwa waziri mkuu wa taifa hilo la pili barani Afrika kuwa na idadi kubwa ya watu kufuatia kuteuliwa kwake na chama tawala wiki iliyopita.

Abiye ameapishwa rasmi leo kuwa Waziri mkuu akimrithi Hailemariam Desalegn ambaye alijiuzulu wadhifa huo kati kati ya mwezi Februari baada ya misururu ya maandamano dhidi ya serikali yaliyosababisha vifo vya mamia ya raia wengi wao kutoka maeneo ya Oromia na Amhara.

Abiye mwenye umri wa miaka 42, ndiye mwanasiasa wa kwanza kutoka jamii ya Oromo kuwa Waziri mkuu na kuna matumaini kuwa atatuliza maandamano dhidi ya serikali yaliyozuka tangu mwaka 2015.

Ameahidi kuleta mageuzi, kuanzisha mazungumzo na Eritrea kudokeza kuwa utawala wake utavipa vyama vya kisiasa uhuru zaidi na kuwataka waethiopia walio nje ya nchi kushiriki kikamilifu katika siasa na maendeleo ya nchi.

Waoromo takriban milioni 100, ambao ndiyo wengi zaidi Ethiopia wamekuwa wakilalamika kuwa wanatengwa kisiasa na kiuchumi na utawala.

JPM Atoa Msimamo Mkali...Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya April 3

$
0
0

JPM Atoa Msimamo Mkali...Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya April 3

Makonda 'Awashitaki' Kwa Rais Magufuli Wanaoingia Dar na Kutoa Matamko ya Kichochezi

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam amewashtaki kwa Rais Magufuli baadhi ya watu (hajawataja kwa majina) kwa kudai kuwa wanaingia ndani ya mkoa wa Dar es salaam na kutangaza uchochezi.

Mh. Makonda amewasilisha mashtaka hayo kwa Rais leo wakati alipokuwa akiweka jiwe la msingi la  ujenzi mradi wa kuongozea ndege katika vituo vinne hapa nchini.

Mh. Makonda amemuambia Rais Magufuli kwamba kuna watu wanaingia ndani ya mkoa wa Dar es salaam na kutangaza uchochezi hivyo yeye kama kiongozi wa mkoa wanajaribu kuangalia utaratibu mzuri wa kisheria watolee matamko katika mikoa yao.

Aidha amesema kwamba "Mh. Rais Tumesikia sikia huko kwingine ila sisi kwetu hakuna waraka. Hakuna waraka popote pale ulipopita. Watu wamemwabudu bwana na mwokozi wao na Tumeungama dhambi zetu kupitia kufa kwake msalabani, tumefufuka naye na tunaendelea kufanya kazi kikamilifu".

Mbali na hayo Mku huyo wa Mkoa ameweka wazi kwamba wakazi wa Mkoa wa Dar es salaam wamesherehekea sikukuu ya Pasaka salama salimini kwani wananchi wametambua thamani ya amani.

Mbunge Joseph Haule ‘Prof J’ Kumtembelea Lulu Michael Gerezani

$
0
0
MKONGWE kwenye gemu la Muziki wa Hip Hop Bongo ambaye pia ni Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule ‘Prof J’, amefunguka kuwa yupo mbioni kumtembelea muigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’, ambaye yupo Gereza la Segerea.

 Akipiga stori na Star Showbiz, Prof J anayebamba na Ngoma ya Pagamisa alisema kama msanii na mdau wa sanaa Bongo, anatafuta nafasi siku moja aweze kwenda kuonana naye.

“Ninatamani kuonana na Lulu na niweze kuzungumza naye. Ninafahamu ana mengi ya kuzungumza, kwa hiyo ninapanga muda na ikiwezekana mtafahamu lini nitakwenda kuonana naye,” alisema Prof Jay
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live




Latest Images