Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live

Baada ya Kifesi Kuacha Kazi Kwa Daimond Afunguka Kufanya kazi na Msanii Huyu

$
0
0
Baada ya Kifesi Kuacha Kazi Kwa Daimond Afunguka Kufanya kazi na Msanii Huyu
Aliyekuwa mpiga picha wa Diamond na WCB kwa ujumla, Kifesi amefunguka iwapo yupo tayari kufanya kazi na wasanii wengine Bongo.

Kifesi amesema yupo tayari kufanya kazi na msanii yeyote ila kazi hiyo isiendane kinyume na matakwa ya imani yake.

“Kama nilivyoelezea sasa hivi nitakuwa ni mfanyakazi huru, kujitegemea mimi kama mimi, nipo huru kufanya kazi na msanii yeyote lakini endapo ufanyaji kazi huo hautanihusisha kwenda kiyume na imani yangu,” Kifesi ameiambia Bongo5.

“Mimi bado ni mpiga picha naendelea na kazi yangu lakini nimeacha kufanya kazi na WCB lakini simaanishi nitaendelea kuwa mwajiriwa wa msanii,” ameongeza.

Mwishoni mwa weekend iliyopita March 30, 2018 Kifesi alitangaza kuacha kazi yake ndani ya WCB kwa kile alichodai kuwa anataka kujiari na kuwa karibu na Mungu wake.

Mbowe na Vigogo Watano Chadema Wafikishwa Mahakamani Kukamilisha Mashariti ya Dhamana

$
0
0
Mbowe na Vigogo Watano Chadema Wafikishwa Mahakamani  Kukamilisha Mashariti ya Dhamana
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na Viongozi wenzake watano tayari wameshafikishwa mahakama ya kisutu ni tangu saa mbili asubuhi hii na sasa wanasubiri shughuli za kimahakama zianze ili wakamilishe masharti ya dhamana.

Mbali ya Mbowe wengine ni Katibu Mkuu Dk Vicent Mashinji, Manaibu Katibu wakuu John Mnyika (Bara), Salum Mwalimu (Zanzibar), Mbunge wa Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa na Mweka Hazina wa Baraza la Wanawake wa chama hicho Ester Matiku wanakabiliwa na kesi ya jinai, wakidaiwa pamoja na mambo mengine ikiwamo kufanya mikusanyiko na maandamano yasiyo halali.

Wamekuwa mahabusu tangu walipopandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka hayo March 27, 2018.

Steve Nyerere Akosoa Tuzo za Sinema Zetu "Wasanii Wazuri Kama Ray, JB, Aunt Ezekiel, Uwoya Batuli Kwanini Hawakupata Tuzo"

$
0
0
Steve Nyerere Akosoa Tuzo za Sinema Zetu "Wasanii Wazuri Kama Ray, JB, Aunt Ezekiel, Uwoya Batuli Kwanini Hawakupata Tuzo"
Baada ya utoaji wa Tuzo za filamu za Sinema Zetu International Film Festival Awards (SZIFF), msanii wa filamu Bongo, Steven Nyerere amesema atazungumza baada ya kuona baadhi ya wasanii ambao anaona walistahili kupata lakini haikuwa hivyo.

Muigizaji huyo amehoji kwanini waigizaji wakubwa kama Ray Kigosi, JB, Aunt Ezekiel, Shamsa Ford, Johari na wengineo kutokuwepo. Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika;

“Nitaongea nilichokiona kwenye tuzo, kwanini Ray, JB, Rich, Roams, Aunt Ezekiel, Shamsa Ford, Duma, Weru, Hemedi, Tausi Mndengela, Mainda, Johari, Uwoya, Marian Ismail, Batuli na wengine wanaofanya vizuri wapo wapi ?,” amehoji.

“Na mbona sijawaona na kuna vijana wasanii chipukizi wanafanya vizuri, nini tatizo,” ameongeza.

Katika Tuzo za filamu za Sinema Zetu International Film Festival Award (SZIFF) zilizotolewa April Mosi mwaka huu, miongoni mwa waigizaji waliofanya vizuri ni pamoja na Gabo Zigamba aliyejinyakulia tuzo tano wakati Wema Sepetu alishinda tuzo mbili.

Lowasa na Mkewe Watinga Mahakamani

$
0
0
Lowasa na Mkewe Watinga Mahakamani
Waziri wa zamani wa Tanzania, Mhe. Edward Lowassa ni moja kati ya watu mashuhuri waliofika katika Mahakama ya Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam kusikiliza dhamana ya viongozi sita wa CHADEMA waliokamatwa wiki iliyopita.

Mwingine aliyefika mahakamani hapo ni mke wa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, Dkt. Lilian Mbowe.

Wanachama na viongozi wa Chadema wamekusanyika  ndani na nje ya viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kusubiri hatima ya dhamana ya viongozi hao

Leo Aprili 03, 2018 viongozi hao wanatarajiwa kutoka rumande kufuatia dhamana waliyopewa na mahakama wiki iliyopita.

Rais Magufuli Atoa Msimamo Mkali

$
0
0

Rais Magufuli Atoa Msimamo Mkali
Rais John Magufuli ametoa msimamo mkali dhidi ya watu wanaobeza jitihada za kuleta maendeleo zinazofanywa na Serikali.

Amesema Serikali ipo na haijalala, akisisitiza kwamba simba aliyelala asisogelewe na kuchezewa mkia.

Pamoja na hayo, Rais amewataka Watanzania kutembelea kifua mbele kwa kuwa nchi iko vizuri na ina uwezo mkubwa kiuchumi.

Alisema hayo jana wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa mfumo wa rada za kuongoza ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).

“Uwezo wetu ni mkubwa mno na wa ajabu, tumeweza kufanya mambo makubwa ndani ya muda mfupi, watu wanashangaa Tanzania tumewezaje kununua ndege bila kukopa,” alisema.

Rais alisema, “Ni sababu hiyo inawafanya watu wenye wivu waumie mno, niliposema nitanunua ndege wakasema nitapata wapi fedha, nikawaambia fedha zangu zipo kwa mafisadi na nilisema watazitoa kwa kutaka au kutotaka hata kwa nguvu nitawabana watazitapika.”

Alisema haumizwi na maneno ya watu kwa kuwa lengo lake ni kuiletea maendeleo Tanzania.

“Wapo watu duniani hata umfanyie vipi haridhiki, niwaambie wazi Watanzania wenzangu tupo pazuri mno, kwa Afrika ni miongoni mwa nchi tano ambazo uchumi wake unakuwa kwa kasi. “Ninafahamu hata makanisani zaka zimepungua kwa kuwa nyingine zilikuwa zinatolewa na mafisadi,” alisema.

Rais Magufuli pia alivipongeza vyombo vya ulinzi kwa kuendelea kuimarisha ulinzi nchini.

Alisema, “Vyombo vya ulinzi vinafanya kazi kubwa sana hata Kibiti unakwenda bila wasiwasi, awali mauaji yalikuwa yakitokea na hatukuona mtu analaani wala kutoa waraka wowote, lakini sijali kwa kuwa nimekabidhiwa Serikali na Watanzania.

“Sitaki kusema sana kwani hakuna lolote lakini niseme Serikali ipo na wala haijalala. Usione simba amelala ukasogea kuchezea mkia wake,” alisema.

Mradi wa mfumo wa rada

Mfumo huo wa rada za kuongozea ndege uliozinduliwa na Rais Magufuli, unajengwa katika vituo vinne vya JNIA, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwanza na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe na unafanywa na Kampuni ya M/S Thales Las France SAS ya Ufaransa ukigharimu Sh67.3 bilioni ambazo zote zinazotolewa na Serikali ya Tanzania.

Akizungumzia ujenzi wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari alisema unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 18 hiyo ikimaanisha kwamba mradi huo ulioanza kujengwa Novemba mwaka jana utakamilika Mei mwakani.

Alisema asilimia 20 ya Sh67.3 bilioni tayari zimelipwa kwa mkandarasi.

Johari alisema anga ni ghali, hivyo linahitaji fedha nyingi na kwamba kukamilika kwa mfumo wa rada Tanzania itakuwa na uwezo mkubwa wa kudhibiti anga, kuongeza ufanisi zaidi na utavutia wageni kuja nchini kutalii.

“Tumesitisha kampeni za nchi jirani kutaka kukasimiwa (kusimamia anga) kutokana na wao kuwa na mifumo mizuri na kuanza kwa mradi huu tumezuia harakati hiyo,” alisema Johari.

Alisema mradi huo unagharimiwa na Serikali Kuu kwa asilimia 55 na asilimia 45 ni fedha kutoka TCAA.

Kuhusu mradi huo, Rais Magufuli aliitaka wizara na TCAA kuhakikisha mkandarasi anasimamiwa ipasavyo ili ujenzi huo ukamilike hata ikiwezekana kabla ya wakati.

“Niviagize vyombo vyote vya ulinzi kuimarisha ulinzi katika viwanja na kuzunguka viwanja vyote,” alisema.

Rais Magufuli alisema kwa sasa kuna rada moja tu. “Uwezo wake ni kuhudumia asilimia 25 ya anga yetu na kwa sasa imechakaa na huo ndiyo ukweli wenyewe.”

Alisema kukamilika kwa ujenzi huo kutarahisisha ulinzi na kuongeza mapato kwa kuwa, “Tozo ya Sh2.2 bilioni ni gharama za kuongoza ndege kwa nchi tulizokasimiwa.

“Haiwezekani unakuwa na ndege zinaongozwa na nchi kutoka nje, ndege inaongozwa kutoka Dar es Salaam kwenda Tabora na nchi ya nje, hatuwezi kuwa na Taifa la aina hii, tunataka tuwe na rada yetu,” alisema.

Aliwapongeza watumishi wa TCAA kwa jitihada wanazozifanya na hasa kuongeza mapato yao na kuvuka lengo.

Pia, Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa aliipongeza TCAA kwa jitihada za kugharamia mradi kama huo na kuagiza mashirika mengine kuige mfano wa mamlaka hiyo.

Alisema wanataka kuifanya JNIA kuwa njia panda ya usafiri wa anga na viwanja mbalimbali vitakarabatiwa kwa fedha za ndani.

Kuhusu ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Mwanza, Rais Magufuli alisema mkandarasi anasuasua na kwamba fedha si tatizo.

Alimwagiza, Profesa Mbarawa kwenda kusimamia ili mkandarasi huyo afanye kazi usiku na mchana.

Waraka wawaibua Ma-RC

Katika hafla hiyo, wakuu wa mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza na Kilimanjaro waligusia waraka wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) na ule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) uliotolewa Machi 24.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alisema, “Tumesikia katika mikoa mingine kuna waraka, hapa kwetu hakuna waraka, watu wamesali bila matatizo.”

Alisema kuna baadhi ya viongozi wa kisiasa wamekuwa wakitoa kauli za kichochezi, “Wanatoka katika mikoa yao kuja kwetu, ifike mahali tuangalie sheria zetu ili wawe wanatoa matamko hayo wakiwa hukohuko kwao.

Alisema, “Mkoa wetu uko shwari, hauna chokochoko.”

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella alisema, “Mwanza iko tayari, hakuna tangazo lolote limetoka, tutaendelea kuwa salama.”

Alisema wataendelea kufanya kazi kwa kutekeleza miradi ikiwamo barabara zinazounganisha nchi jirani.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira alisema rada hizo zitaongeza usimamizi wa anga hasa kwa kuwa ni miongoni mwa mikoa ya mipakani.

Kuhusu matamko ya waraka, Anna alisema, “Naona mkuu wa mkoa wa Mwanza na Dar es Salaam wamenichokoza na matamko, yote yameanzia Kilimanjaro na yataishia hapo... tutapima kila hoja na kukuletea taarifa.”

Waziri Mwigulu Awapa Makali Jeshi la Polisi

$
0
0
Waziri Mwigulu Awapa Makali Jeshi la Polisi
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amelitaka Jeshi la Polisi kuwa wakali kwa watu wanaofanya mzaha pindi wanapokuwa wanaendesha vyombo vya moto ili kuweza kuokoa maisha ya watanzania yanayopotea kila kukicha kwenye ajali.


Waziri Mwigulu ametoa kauli hiyo leo katika Mkutano wa 11 wa kikao cha Bunge cha kwanza kinachoendelea kufanyika katika mkoa wa Dodoma wakati alipokuwa anajibu swali ya nyongeza la Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga aliyetaka kusikia tamko la serikali kuhusiana na faini zinazotozwa na askari wa barabarani pindi wanapowakamata madereva wa magari badala ya kuwapa elimu elekezi.

"Sisi kama Wizara ya Mambo ya Ndani na Jeshi la Polisi kutoza faini au kukusanya faini sio kipaumbele chetu ila kipaumbele chetu ni maisha ya watanzania. Tunapobaini kuwepo uzembe mwingi barabarani ndipo tunapoamua kutoza faini kwa hiyo kama watanzania watazingatia na kuwa waangalifu kwamba wamebeba dhamana kubwa ya maisha ya wenzao katika vyombo vyao moto hili suala la faini litakuwa limeisha", amesema Waziri Mwigulu.

Pamoja na hayo, Waziri Mwigulu ameendelea kwa kusema "nitoe rai kwa Jeshi la Polisi kuendelea kuwa wakali pindi watu wanapofanya mzaha, huku wakiwa wamebeba abiria ili kuokoa maisha yanayotokana na ajali nyingi zinazotokea barabarani, na jambo hili ninalo lisemea ni kwa vyombo vya moto vyote kuanzia magari ya abiria na binafsi pamoja na bodaboda. Nalisisitiza hili kwasababu tumeshuhudia vifo vikiwa vimetokea pindi tunapoenda katika eneo la tukio unakuta gari limekwisha andikiwa faini kutokana na kutembea mwendokasi".

Kwa upande mwingine, Waziri Mwigulu amesema ajali za barabarani zimepungua kwa asilimia 43 hadi kufikia Disemba 2017 ambapo katika kipindi cha mwaka 2016 jumla ya ajali 9,856 zilizosababisha vifo 3,256 na majeruhi 2,128 na mwaka 2017 ajali 5,310 ambazo zilisababisha vifo 2,533 na majeruhi 5,355 wakati kipindi cha Januari hadi Februari mwaka 2018 zimetokea ajali 769 zilizosababisha vifo 334 na majeruhi 698 ambapo katika kipindi hicho wahanga 1583 wakilipwa fidia takribani Bilioni  7 kutoka makampuni mbalimbali ya bima.

Breaking News: Mbowe na Viongozi wa Chadema Waachiwa Kwa Dhamana

$
0
0
Breaking News: Mbowe na Viongozi wa Chadema Waachiwa Kwa Dhamana
Viongozi wa Chadema wakiongozwa na mwenyekiti wao, Freeman Mbowe wametimiza masharti ya dhamana na kuachiwa huru katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Machi 3, 2018. Mahakama hiyo imejiridhisha na nyaraka za udhamini zilizowasilishwa mahakamani hapo.



Masharti ya dhamana yalikuwa ni kila mshtakiwa kuwa wadhamini wawili watakaosaini bondi ya TZS 20m, barua ya utambulisho toka serikali za mtaa.



Aidha, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar ili kusomewa mashtaka yanayomkabiri.



Wakili wa Serikali, Faraja Nchimbi ameomba kufanya marekebisho ya hati ya mashtaka ili kumjumuisha Mdee katika kesi inayowakabili viongozi wenzake sita wa Chadema wanaokabiriwa na mashataka manane yakiwemo ya uchochezi, uasi na kuhamasihsa maandamano, hivyo wote kwa pamoja watasomewa mashtaka upya.



Mdee alikamatwa juzi Jumapili akiwa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar wakati akiwasili kutokea nchini Afrika Kusini. Hata hivyo Mahakama imempa dhamana baada ya kuridhika na sifa za wadhamini.



Mbowe na wenzake ambao ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Vincent Mashinji na manaibu wake wa Bara na Zanzi­bar, John Mnyika na Salum Mwalimu, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko wote wanakabiliwa na mashtaka manane yakiwemo mawili ya uchochezi wa uasi yanayom­kabili Mbowe na wanatarajiwa kuachiwa kwa dhamana leo.

Punguza Unene Unaokusumbua Katika Mwili Kwa Kutumia Bidhaa za Edmark

$
0
0

"Tumia Dawa za Edmark za Kupunguza uzito uliozidi Mwilini Mwako, Edmark ni Vurutubisho na Chakula Mbadala na Zimehakikiwa na TFDA...

Ni uhakika kwa afya yako,👉 kupunguza uzito na sumu mwilini, Mafuta Sehemu Mbaya, Kitambi na nyama uzembe na kutibu MAGONJWA Mbalimbali kwa msaada wako mfuate instagram: @my_health_my_wealth @my_health_my_wealth


Au Mtafute WhatsApp Huyu Dada kwa kutumia Namba +255783 566844

Pia Dawa za Edmark Zinaweza kupa Fursa ya Biashara Uweze pata Kipato Kirahisi kwa Kuwasaidia watu Kuimarisha Afya zao

Nguvu ya Pesa Yaongea...Agness Masogange Aachiwa Huru

$
0
0

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilikuwa imemhukumu kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya Tsh. Milioni 1.5, msanii Agnes Gerald ‘Masogange’ kwa kosa la kutumia madawa ya kulevya aina ya  heroin na Oxazepam..

Msanii Agnes Gerald aka Masogange ameachiwa huru mara baada ya kulipa faini ya Sh milioni 1.5..

Tabia ya wadada/wanawake kubadilisha status kwa hitilafu ndogo za kwenye uhusiano

$
0
0
Leo naomba tujadiliane hili maana nimekua nikiliona sana,
Kwa ushahidi mkubwa nimeliona kwa rafiki zangu wengi sana na hata mimi limewahi kunitokea.

Mdada uliyenae uhusiano mkipishana kauli kidogo na ukawa kimya basi atadhani ndo keshapigwa chenga hapo ataanza kuhangaika na kubadilisha status kwenye social networks kama whatsapp, Facebook etc.

Kwa mfano mlipokua kwenye uhusiano hajawahi kuandika jambo la hivi ila leo mnakwazana jambo dogo utaona Whatsapp au Facebook ameandika: AM SINGLE AND HAPPY, I CAN MANAGE MY LIFE, NAMTEGEMEA MUNGU TU SIO MWANADAMU.

Tatizo linalonikwaza ni kwamba kitendo cha mtu kuandika haya ni kuonyesha watu wengine kua hana siri juu ya mambo yake, yaani likimkuta tu lazima aropoke kwa kuweka status ya ajabu.

Huu naona kama utoto sana watu tujifunze kua na adabu ya kutunza privacy zetu

Pata Habari Masaa 24......Pakua Upya Application Yetu Tukuhabarishe Usiku na Mchana

BREAKING: Halima Mdee Naye Kapata Dhamana kwa Bondi ya Milioni 20

$
0
0
Mbunge wa Kawe Halima Mdee leo April 3, 2018 alifikiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  na kuunganishwa na  akina Freeman Mbowe

Mdee  yeye alisomewa mashtaka mawili ya kufanya mkusanyiko usio halali na kuendelea na mkusanyiko huo, kutotii amri iliyowataka kutawanyika na kusababisha vurugu iliyosababisha kifo cha Akwilina Akwilini na askari kujeruhiwa.

Baada ya kusomewa mashitaka hayo, Mahakama imempa  dhamana kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili watakaosaini kwa maandishi bondi ya Sh milioni 20 na kuripoti mara moja kila wiki.

Mahakama  imesema haiwezi kumnyima mshtakiwa dhamana kwa sababu aliruka dhamana ya polisi maana  polisi ni taasisi nyingine na mahakama ni taasisi nyingine, hivyo ikampatia dhamana mshtakiwa kwa masharti tajwa hapo juu.

Rais Aitaka Tanesco Kupunguza Bei ya Umeme

$
0
0

Rais Aitaka Tanesco Kupunguza Bei ya Umeme
Rais John Magufuli amelitaka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuanza kufikiria kupunguza bei ya umeme kwani nchi inatarajia kuwa na umeme mwingi.

Rais ameyasema hayo leo Aprili 3, wakati wa uzinduzi wa kituo cha kuzalisha umeme cha Kinyerezi awamu ya pili.

Amesema miradi yote ya umeme ukijumlisha na wa Stiegler Gauge itafikia megawati 5000 hivyo wataibana  Wizara ya Nishati ianze kufikiria kupunguza bei ya umeme.

“Muanze kufikiria namna ya kushusha bei ya umeme, mmeanza vizuri muendelee na utaratibu huo.

“Nchi ina vyanzo vingi vya kuzalisha umeme, maji , jua, upepo, makaa ya mawe, hata nyuklia, kwa sababu tunayo madini ya uranium yanayoweza kuzalisha umeme kwa nyuklia, kwa umeme wote huo hakuna haja ya kuwa na bei ya juu, ”amesema Magufuli.

Amefafanua kuwa anayetaka kuwekeza bila kukomoa aje, lakini siyo wawekezaji wababaishaji.

Rais Magufuli atoa maagizo Wizara ya Nishati, Rea

Ameeleza kuwa nchi itakuwa na umeme wa kutosha,  wa uhakika na kwa gharama nafuu.

Magufuli pia alizitaja sababu za bei ya nishati hiyo kuwa ya juu ni kutokana na umeme mwingi kuzalishwa kwa kutumia mafuta (dizeli), huku baadhi ya mikataba kuwa mibovu na ya ovyo.

Ameeleza takwimu zilizofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) mwaka 2015/16 zinaonyesha asilimia 36.6 ya Watanzania ndiyo wameunganishiwa umeme.


Msanii wa Kenya Ajitolea Kumsaidia Wema Sepetu Kupata Ujauzito

$
0
0
Msanii wa Kenya ajitolea kumsaidia Wema Sepetu kupata ujauzito
Ni muda mrefu malkia wa filamu Bongo, Wema Sepetu amekuwa akitamani kupata mtoto – Hilo pia amewahi kuthibitisha wakati alipoongea na EATV.



Katika runinga hiyo Wema alisema, “Kiukweli napenda nimpate mtoto hata sasa hivi kwa sababu nimekuwa nikataka mtoto tokea na miaka 24 sasa hivi na miaka 29.”

Habari njema zinaweza zikawa zinamkaribia mrembo huyo kutokana na msanii kutoka nchini Kenya ambaye alikuwa anaishi Dubai, 2gb Diva amejitolea kumsaidia kupata mtoto ili kutimiza ndoto zake za muda mrefu.

2gb Diva katika video ameonekana akimtaja Sepenga kwa kutaka kumsaidia kwa kusema, ” Wema Sepetu, sweetheart suluhisho tupo nalo. May be soon unaenda kuwa mama.”

Sakata la Nondo Latinga Bungeni Mbunge Ataka Kujua Sababu za Kumuweka Mahabusu

$
0
0
Sakata la Nondo Latinga Bungeni Mbunge Ataka Kujua Sababu za Kumuweka Mahabusu
Mbunge CUF, Dkt. Suleiman Ally Yussuf amefunguka na kuhoji ni sababu zipi zilizopelekea mpaka Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo kuwekwa mahabusu ya Polisi kwa kipindi kirefu bila ya kufikishwa Mahakamani kusomewa mashtka


Dkt. Suleimani amehoji hayo leo (Aprili 3, 2018) katika Mkutano wa 11 wa kikao cha Bunge cha kwanza kinachoendelea kufanyika katika mkoa wa Dodoma wakati alipokuwa anauliza swali ya nyongeza kwenda kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba ambapo alitaka kufahamu uhalali wa Jeshi la Polisi juu ya kuwashikilia watuhumiwa.

"Wako watu wengi wanaowekwa mahabusu ya Polisi kwa zaidi ya siku 15 bila ya kupelekwa Mahakamani akiwemo mwanafunzi Abdul Nondo. Nataka nijue ni sheria gani ambayo inatumika au inatumiwa na Jeshi la Polisi kuwaweka watu mahabusu ya Polisi zaidi ya muda huo mrefu bila ya kupelekwa Mahakamani", amehoji Dkt. Suleiman.

Aidha, katika kujibu hoja hiyo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amesema polisi ni chombo kilichoundwa kwa mujibu wa katiba na sheria na linatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Katiba.

"Polisi wana mamlaka kisheria kutuhumu, kukamata, kuhoji na kuweka watuhumia mahabusu kwa muda ulioruhusiwa kisheria endapo itabainika kuwa kuna viashiria au taarifa ya kuhusika katika kutenda kosa la jinai. Kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za utendaji zinazoongoza Jeshi la polisi inapobainika askari amembambika kesi kwa sababu zozote zile huchukuliwa hatua mbalimbali za kinidhamu ikiwemeo kufukuzwa",amesema Waziri Mwigulu.

Pamoja na hayo, Waziri Mwigulu ameendelea kwa kusema "kwa kuwa jambo la kiusalama ni kipaumbele, kwa mtuhumiwa na rai wengine waliosalia, Jeshi la Polisi hutumia wajibu wake waliopewa wa kulinda usalama wa raia kwa kuweza kuhakikisha kwamba linatimiza majukumu yake na huku likiwaacha watu wakiwa salama kabisa".

Kwa upande mwingine, Waziri Mwigulu hakuweza kujibu suala lolote kuhusu Nondo kama jinsi lilivyo hojiwa na Mbunge Sulleiman juu ya uhalali wa Jeshi la Polisi kumuweka kijana huyo zaidi ya siku 15 mahabusu ya polisi.

Rais Magufuli Atumia Wimbo wa 'Hawawezi Kushindana' ya Goodluck Gozbert Kuwafikishia Ujumbe... Aomba Urudiwe Mara Mbili

$
0
0
Rais Magufuli Atumia Wimbo wa 'Hawawezi Kushindana' ya Goodluck Gozbert Kuwafikishia Ujumbe... Aomba Urudiwe Mara Mbili
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameshindwa kujizuia na kuomba kupigiwa kwa mara ya pili wimbo wa msanii wa injili nchini Goodluck Gozbert, uitwao  'Hauwezi Kushindana'


Rais Magufuli ameweka wazi kuwa amevutiwa sana na wimbo huo wakati akiaanza kuhutubia leo April 3, 2018 katika uzinduzi wa mradi wa kuzalisha umeme Kinyerezi 2, ambao unatarajiwa kuingiza megawatts 240 katika gridi ya Taifa.

Baada ya kumaliza kuhutubia Rais Magufuli aliomba wimbo huo upigwe tena na kukiri kuwa amemkosha sana.

"Naomba niseme tena kale kawimbo kamenigusa sana, naomba kachezwe tena hapa " alisisitiza Rais John Pombe Magufuli

Msanii Goodluck Gozbert ameachia video ya wimbo wake huu Machi 16, 2018  na kuwagusa watui wengi kutokana na utunzi wake na ujumbe ambao upo ndani ya wimbo huo ambao pia umemguda Rais John Pombe Magufuli.

TID Amuweka wazi Mpenzi Wake Ampa Ujumbe Huu

$
0
0
TID Amuweka wazi Mpenzi Wake Ampa Ujumbe Huu
Msanii mkongwe katika game ya muziki wa Bongo fleva Khalid Mohamed “TID” ameamua kuweka wazi mahusiano yake ya kimapenzi kupitia ukurasa wake wa instagram

TID ameandika caption inayosema >>>“Kheri ya Pasaka, usikubali mtu akushushe chini kwenye sikukuu hii, kutoka katika moyo wangu naomba niweke wazi kwa kila mtu kuwa Niko mapenzini”



Inasemekana kuwa TID amefanya hivyo kuwajuza wale wote ambao wamekuwa wakizusha tetesi kuhusiana na mahusiano yake na kuhusishwa kuwa na wanawake tofauti tofauti kwenye mitandao ya kijamii.

Mbowe Afunguka kwa Mara ya Kwanza Baada ya Kuachiwa Huru

$
0
0
Mbowe Afunguka kwa Mara ya Kwanza Baada ya Kuachiwa Huru
Mwenyekiti wa (CHADEMA) Mhe. Freeman Mbowe amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya kuachiwa huru yeye pamoja na viongozi wengine sita wa CHADEMA na kusema kuwa walipokuwa magerezani wameshuhudia mengi na watayaweka wazi karibuni.


Mbowe amesema hayo alipokuwa nje ya Mahakama ya Hakimu mzaki Kisutu baada ya kukamilisha masharti dhamana ambapo kila mmoja alitakiwa kuwa na wadhamini wawili pamoja na kusaini bondi ya shilling Million 20.

"Leo mahakama imetupa ruksa ya dhamana na tunaanza dhamana yetu siku ya leo kwa mashtaka ambayo yananikabili mimi na wenzangu, tumekuwa gerezani Segerea kwa siku saba mimi na wenzangu na tunamshukuru Mungu tuko salama mimi na wenzangu na tumewaona Watanzania wengi zaidi ya elfu mbili ndani ya gereza la Segerea ambao wengi wao haki yao imecheleweshwa kwa hiyo tunasema ni haki iliyominywa, tutazungumza mengi tuliyoyaona Segerea na baadaye tutatoa taarifa rasmi ya chama kuhusiana na kesi hii" alisema Mbowe

Aidha Mbowe aliendelea kusema kuwa "Zamani tuliona nchi hii ina udikteta uchwara ila sasa ina udikteta kamili, tutayazungumza na kutolea ufafanuzi kamili katika muda muafaka" alisisitiza

Waziri Matiang'i: Miguna Lazima Aombe Tena Uraia wa Kenya ili Aruhusiwe Kuingia Kama Raia

$
0
0
Waziri Matiang'i: Miguna Lazima Aombe Tena Uraia wa Kenya ili Aruhusiwe Kuingia Kama Raia
Waziri wa mambo ya ndani nchini Kenya Dkt Fred Matiang'i amesema mwanasiasa wa upinzani aliyetimuliwa nchini humo Miguna Miguna atalazimika kuomba tena uraia.

Waziri huyo amesema Bw Miguna alipoteza uraia wake alipouchukua uraia wa Canada mwaka 1988 na hawezi kuruhusiwa kuingia nchini Kenya kama raia bila kuomba tena uraia.

Dkt Matiang'i, aliyekuwa akihojiwa na kamati ya bunge, amesema mwanasiasa huyo ambaye pia ni wakili alijipatia paspoti yake ya Kenya na kitambulisho cha taifa anachokitumia kwa sasa kwa njia ya ulaghai.

Waziri huyo amesema hakuna shaka kwamba Bw Miguna alizaliwa Kenya.

"Yeyote aliyechukua uraia wa taifa jingine kabla ya katiba ya sasa kuidhinishwa mwaka 2010 ambaye anafikiri kwamba ataweza kurejea bila kufuata utaratibu uliowekwa anajihadaa.

"Hapana shaka kwamba Miguna alizaliwa Kenya. Lakini kwa mujibu wa katiba ya kabla ya 2010, yeyote aliyechukua uraia wa nchi nyingine alipoteza uraia wake wa Kenya. Bunge liliidhinisha sheria inayoeleza jinsi mtu kama huyo anavyoweza kuupata tena uraia wake."

Waziri huyo pia amejitetea dhidi ya shutuma kwamba amekuwa akikaidi maagizo ya mahakama ya kutaka Bw Miguna aachiliwe huru na kuruhusiwa kuingia Kenya.

Jaji wa Mahakama Kuu George Odunga alikuwa ameagiza Dkt Matiang'i, pamoja na mkuu wa polisi Joseph Boinnet, mkuu wa idara ya uhamiaji Gordon Kihalangwa na katibu wa wizara ya mambo ya ndani Karanja Kibicho wafike mbele yake kueleza ni kwa nini walikosa kutekeleza amri ya mahakama ya kumruhusu Bw Miguna aingie Kenya.

Miguna asafirishwa kutoka Dubai kwenda Canada
Dkt Matiang'i amesema: "Jaji alipokuwa anatutaka tufike mbele yake tulikuwa tunahudhuria sherehe za kufuzu kwa maafisa wa polisi wa kukabiliana na fujo (GSU). Tulihukumiwa bila kupewa fursa ya kujieleza, kwa kutumia madai ya uongo."

Jaji Odunga aliwapiga faini maafisa hao Sh200,00 kila mmoja, na akaagiza pesa hizo zikatwe kutoka kwa mishahara yao.

Dkt Matiang'i pia amepuuzilia mbali madai kwamba serikali ilimfurusha Bw Miguna kutoka nchini humo akisema hatua kama hiyo ingehitaji idhini yake.

Bw MigunaHaki miliki ya pichaAFP/GETTY
Image caption
Miguna aliwasili uwanja wa JKIA Jumatatu wiki iliyopita lakini akazuiwa kuingia nchini Kenya
"Hakufurushwa kutoka Kenya. Nilihitaji kutia saini idhini ya kumfurusha. Hatungemfurusha kwani hakuwa ameingia bado ndani ya eneo la utawala wetu," Dkt Matiang'i amesema.

"Tulimuondoa uwanja wa ndege kama mtu ambaye hakuwa na stakabadhi za kumtambua, abiria ambaye hangetambuliwa ambaye kawaida hurejeshwa alikotoka."

Waziri huyo amesema Miguna hataruhusiwa kurejea Kenya bila kuomba kurejeshewa uraia wa Kenya.

Katiba ya kabla ya 2010 haikuruhusu uraia wa nchi mbili kama ilivyo kwa katiba ya sasa.

Vilio Vyatanda Baada ya Kumpata Mtoto Wao Aliyepotea kwa Miaka 24

$
0
0
Vilio Vyatanda Baada ya Kumpata Mtoto Wao Aliyepotea kwa Miaka 24
Familia moja nchini China imeibua hisia nyingi za watu baada ya kumpata mtoto wao wa kike ambaye alikuwa amepotea kwa miaka 24.

Inaelezwa kuwa binti huyo  Qifeng alipotea akiwa na umri mdogo, ambapo siku moja akiwa na wazazi wake Wang Mingqing na Liu Dengying ambao walikuwa wauzaji wa matunda, alipotea na wazazi hao waligundua mtoto wao hayupo pembeni yao.

Walianza kumtafuta, zoezi ambalo lilichukua miaka hiyo yote huku wakitangaza kumtafuta binti yao huyo kwenye vyombo mbalimbali za habari nchini humo huku baadhi ya mabinti wakijitokeza kupiga DNA lakini hawakuwa mtoto wao.

Hatimaye Polisi mchoraji alichukua picha ya utotoni ya binti huyo na kumchora jinsi ambavyo yawezekana ndivyo alivyo baada ya kuwa mtu mzima. Qifeng alipoona picha hiyo alipiga simu kwa namba ambazo ziliwekwa kwenye picha hizo na ndipo wanafamilia hao walipopatana.
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live




Latest Images