Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live

Breaking News : Ajali Mbaya Yatokea Tabora, Fuso na Basi la City Boy Zagongana Uso kwa Uso

$
0
0

Taarifa zilizotufikia usiku huu zinaeleza kuwa kuna ajali mbaya sana ya basi la City Boy linalofanya safari zake kati ya Dar na Karagwe Kagera limegongana na Fuso huko Igunga mkoani Tabora
-
Taarifa zaidi zinasema ajali hiyo imesababisha vifo kadhaa (idadi kamili bado haijafahamika)
-
Tunaendelea kufuatilia kwa kina ajali hii na tutawajuza zaidi..

Msajili Apewa Rungu la Kufuta Vyama vya Siasa....Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya April 5

$
0
0


Msajili Apewa Rungu la Kufuta Vyama vya Siasa....Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya April 5

Abdul Nondo ahojiwa Uraia Wake na Idara ya Uhamiaji.....Anatakiwa Apeleke Vyeti vya Kuzaliwa vya Baba, Mama, Babu, Bibi

$
0
0
Mwanasheria TSNP, Mkurugenzi wa Idara ya Sheria TSNP, Paul Kisabo amesema kuwa ni takribani wiki sasa Mwenyekiti wao wa Mtandao wa Wanafunzi(TSNP), Abdul Nondo amekuwa akihitajika uhamiaji ili akahojiwe uraia wake na pamoja na wazazi wake.

Kisabo ameeleza kuwa jambo hilo la kuhojiwa uraia wake wamelitimiza jana baada ya kutoka Mahakama Kuu kwenye kesi yake iliyohairishwa mpaka tarehe 11, April mwaka huu.

Aidha ameeleza kwamba Kwa muda wa takribani wiki moja mpaka sasa mwenyekiti wa TSNP Abdul Nondo amekuwa akihitajika uhamiaji ili akahojiwe kuhusu taarifa za uraia wake pamoja na za ndugu zake.

Ameeleza kuwa Nondo hakupata nafasi ya kwenda sababu hakuwa sawa kutokana na changamoto alizokumbana nazo siku za hivi karibuni.

"Mnamo sa sita mchana tuliweza kumfikisha Abdul Nondo makao makuu ya ofisi za uhamiaji mkoa (makao makuu ya wizara ya mambo ya ndani) na wanataka kupata taarifa zake binafsi, za wazazi wake, babu na bibi zake pande zote mbili (upande wa baba na upande wa mama) pamoja na za ndugu zake,kwani Afisa uhamiaji mkoa alitamka kuwa sheria inawaruhusu kumuhoji mtu yeyote wanaotilia mashaka uraia wake.

"Wanamashaka na uraia wa Abdul Nondo, hivyo alitakiwa awathibitishie kuwa yeye ni raia wa Tanzania. Nondo amejaza taarifa zile anazozifahamu tu.

"Baada ya kujaza taarifa hizo, ametakiwa  kupelea cheti chake cha kuzaliwa pamoja na vyeti vya wazazi wake wote wawili, babu na bibi zake mnamo April 20, 2018. "Amesema Kisabo

Pata Habari Masaa 24......Pakua Upya Application Yetu Tukuhabarishe Usiku na Mchana

Zitto Kabwe Afunguka Mazito Baada ya Abdul Nondo Kuhojiwa Uraia Wake..Adai Uhamiaji Inatumika Kisiasa

$
0
0
Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo amefunguka na kuonyesha kuchoshwa na baadhi ya mambo ambayo yanaendelea nchini na kuamua kuwaomba wazee wa Ujiji Kigoma wakae ili kuweza kumaliza mambo hayo anayodai ni ya kipuuzi.

Zitto Kabwe amesema hayo baada ya Idara ya Uhamiaji kumuhoji kuhusu uraia wake Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi nchini Tanzania, Abdul Nondo jambo ambalo Zitto Kabwe anasema idara ya uhamiaji inatumika kisiasa dhidi ya mwanafunzi huyo.

"Sio kosa hata kidogo Abdul kuzaliwa Ujiji Kigoma. Imekuwa tabia ya Serikali kuwapa kesi za uraia watu wanaotoka mikoa ya magharibi hasa Kigoma. Suala la Nondo ni vita dhidi ya Watu wa Kigoma. Tutapambana. Tutampigania Abdul Nondo. Watanzania tusikubali upuuzi huu wa watu wa Uhamiaji kuwafanya raia wa mikoa kama Kigoma kuwa raia wa daraja B" alisema Zitto Kabwe

Aidha Zitto Kabwe alikwenda mbali na kusema kuwa mwanafunzi huyo ni mjukuu wa moja ya muasisi wa TANU ambaye pia alipigania uhuru wa Tanganyika

"Abdul Nondo Abdul Omar Mitumba, mjukuu wa Marehemu Mzee Omar Mitumba, mwasisi wa TANU na mpigania Uhuru wa Tanganyika leo anaitwa na maafisa Uhamiaji eti kuhojiwa uraia. Hao maofisa uhamiaji na aliyewatuma hawana 'credentials' ambazo Babu yake Nondo, Mwenyekiti wa TSNP anazo. Wazee wa Ujiji sasa mkae. Tumalize haya mambo ya kipuuzi" alisisitiza Zitto Kabwe

Mwanafunzi Abdul Nondo aliitwa jana idara ya uhamiaji kuhojiwa juu ya uraia wake na kujaza fomu hivyo anapaswa kufika tena ofisi za uhamiaji tarehe 20 mwezi huu kwa ajili ya kupeleka vyeti vya kuzaliwa yeye, baba na mama yake, na bibi na babu kwa pande zote mbili za wazazi wake

Mwenyekiti UVCCM: Simfahamu Mtu Anayejiita Mange Kimambi

$
0
0
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), (UVCCM), Kheri James amefunguka na kusema yeye hamtambui wala kumjua mwanaharakati wa mitandaoni Mange Kimambi na kusema angekuwa anamtambua angeweza kumzungumzia.

Kheri James amesema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha Kikaangoni kinachorushwa na kituo cha  EATV.

Mbali na hilo Kheri James alidai kuwa yeye hatambui wala kufahamu juu ya maandamano ya nchi nzima ambayo yanahamasishwa kupitia mitandao ya kijamii ambayo yanadaiwa kufanyika April 26 mwaka huu.

Hata hivyo Mwenyekiti huyo wa wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi, Kheri James amewalalamikia baadhi ya watanzania na wapinzani ambao wamekuwa wakiisema na kuitangaza nchi kwa mambo mabaya yaliyopo ndani

Amesema  jambo hilo ni baya sana kwani litaleta athari kubwa kwani wawekezaji, watalii watahofia kufika nchini  kwetu jambo ambalo litafunga milango ya maendeleo ya nchi.

Mbowe Katoa Msimamo Mkali: Hatusomi Hotuba Zetu na Wala Hatutasusia Vikao Vya Bunge

$
0
0
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni (KUB), imesema haitasoma hotuba wala taarifa zake bungeni endapo utaratibu wa kuziwasilisha kwa Katibu wa Bunge hatua ya kuhaririwa kwanza kabla ya kusomwa bungeni itaendelea.

Pamoja na hayo, wamesema hawatatusa bunge kwa ajili hiyo wala sababu nyingine yoyote.

Mwenyekiti wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe amesema hayo jana Mjini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mustakabali wa wabunge hao kuhudhuria vikao vya bunge na kuhusu kukataliwa kusomwa kwa hotuba yao bungeni  jana.

Mbowe alisema anamshangaa Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson kukataa kutosomwa kwa taarifa ya kambi hiyo bungeni jana kwa sababu tu haikuwasilishwa kwa Spika siku moja kabla ya kusomwa bungeni.

“Naibu Spika anasema hotuba ya KUB haipo wakati anajua kambi ilikuwa ina watumishi wanne ambao walikuwa wanafanya utafiti, kuandaa randama ya serikali, kuandaa hotuba zote zikiwamo za serikali sasa watumishi hao tangu Desemba mikataba yao iliisha na niliandika dokezo kuomba wapewe mkataba upya hadi sasa Katibu wa Bunge amekataa kufanya hivyo akidai Spika wa Bunge yuko nje kwa matibabu.

“Sawa walitaka hotuba hiyo niiandikie Segerea, kwa sababu wale vijana ndiyo walikuwa wakifanya hayo na bunge lina watumishi wa mikataba 30 wakiwamo wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, wote wana mikataba ya miaka miwili miwili lakini wengie wako ofisini isipokuwa wa kambi ya upinzani ambao walikufukuzwa kama mbwa katika bunge la Januari,” alisema Mbowe.

Pamoja na mambo mengine, Mbowe amesema hapatakuwa na hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzania Bungeni hadi watumishi  warejeshwe lakini pia hata watakaporejeshwa, hawatakuwa tayari kupeleka hotuba zao kwa katibu wa Bunge akachague ni nini cha kusoma bungeni na nini cha kuacha na kwamba Bunge liking’ang’ania kufanya hivyo, hawatasoma hotuba hizo.

Akizungumzia suala hilo, Katibu wa Bunge Stephen Kagaigai alisema bunge lina watumishi wa kutosha kuhudumia wabunge na ofisi zao.

Alisema hadhani kama aliyozungumza Mbowe yatakuwa na ukweli wowote kwa sababu bunge linahudumiwa na Sekretarieti ya Bunge na watumishi wake walioajiriwa na kuhudumia wabunge.

“Hatujakosa sekretarieti, nina watumishi wa kutosha kuhudumia wabunge.Kulikuwa na watumishi wa mkataba ambao mkataba wao ulimalizika Desemba, sasa alitakiwa kusema kama anawahitaji hao lakini mwenye uwezo wa kusema waendelee au wasiendelee ni Tume ya Utumishi wa Bunge.

“Kwangu alikuja akaniambia lakini sasa mimi ni mtumishi wa Bunge na kama unavyofahamu Spika wa Bunge alikuwa nje kwa matibabu.

“Watumishi walioajiriwa na Bunge wapo, mimi nikiwa mmojawapo kama mbunge anawahitaji anapewa lakini si kwa kazi binafsi. Kama anataka watumishi wa bunge kumhudumia yeye peke yake hiyo ni juu yake, wanaweza kuwa hawataki lakini sisi hatuwezi kuwalazimisha,” amesema Kagaigai.

Zitto Kabwe Ajitolea Kumsindikiza Abdul Nondo Uhamiaji...Adai Kwenda Kuhoji kama Wakigoma sio Watanzaniia

$
0
0
Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amesema Aprili 20 ataongozana na Mwanafunzi Abdul Nondo kupeleka vyeti vya kuzaliwa katika ofisi za Idara ya Uhamiaji kama alivyotakiwa kuthibitisha uraia wake

Zitto amesema yeye kama Mbunge wa Kigoma ambapo ndipo nyumbani kwa mwanafunzi huyo, ataruhusu wapiga kura wake kumsindikiza ili kuhoji kama Wanakigoma sio Watanzania maana kila mara wamekuwa wakihojiwa juu ya uraia wao

Abdul Nondo alifika Idara ya Uhamiaji mapema leo kuitikia wito ambapo baada ya mahojiano akaamriwa awasilishe cheti chake cha kuzaliwa pamoja na vya wazazi wake ifikapo tarehe 20 mwezi huu

Tangaza Biashara Yako Hapa Uweze Kupata Wateja wa Haraka

$
0
0
Mtu wangu wa nguvu unaweza Tangaza Biashara yako hapa nasi uweze kuwafikia watu wengi zaidi kwa mara moja kupitia blog ya Udaku Special..

Piga simu 0714604974

Majizzo Ampongeza Daimond Amtabiria Makubwa Wasafi Tv, Radio

$
0
0
Majizzo Ampongeza Daimond Amtabiria Makubwa Wasafi Tv, Radio
Mkurugenzi Mtendaji na Muanzilishi wa kituo cha Radio EFM na TVE, Francis Ciza maarufu kama DJ Majizzo ametoa pongezi kwa msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz kwa kuingia rasmi kwenye Media Industry hapa Tanzania.

Majizzo amesema kuwa vituo vyake vya EFM na TVE vimejitahidi kuifikisha tasnia ya habari sehemu fulani hivyo anaamini kuwa ujio wa Wasafi TV na Radio vitaifikisha mbali tasnia ya habari.

“Ni mpango mzuri uliochukua na mimi binafsi nakupongeza juu ya kuchagua sekta ya vyombo vya habari, kama vijana ni wajibu wetu kuwahamasisha vijana wengine kufanya kazi kwa bidii ili kujenga taifa letu leo na kizazi cha baadae. Sisi kama “E” tumefanya kidogo na tunaamini kuwa Wasafi (TV na Radio) zitafanya mengi zaidi. Karibu tujenge Tanzania.Karibu kwenye tasnia ya habari @diamondplatnumz,“ameandika Majizzo kwenye taarifa yake aliyochapisha kwenye mtandao wa Instagram.

Kituo cha Wasafi TV kinachomilikiwa na Diamond Platnumz kimeanza kurusha matangazo yake Jumatatu ya Aprili 02, 2018 na tayari wasanii na wadau wa muziki wameanza kutoa pongezi kwa kile wanachodai kuwa kituo hicho kimekuja kubadili ufumo dume wa upendeleo wa upigwaji wa ngoma za wasanii wa muziki.

Mwenyekiti UVCCM Awalipua Jokate, Wema "Simjui Wema Kama Kurudi Amerudi CCM si UVCCM"

$
0
0
Mwenyekiti UVCCM Awalipua Jokate, Wema "Simjui Wema Amerudi CCM si UVCCM"
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Kheri James amefunguka hatima ya Wema Sepetu na Jokate Mwegelo ndani ya umoja huo.

Akizungumza leo Kikaangoni, EATV amesema hawezi kujibu kuhusu Jokate kuondolewa UVCCM kwa sasa.

“Kama ambavyo hatukuwaeleza sababu za kuteuliwa kwake Jokate ndivyo ambavyo hatutawaambia sababu za kutolewa kwake” amesema.

“Wema mimi simjui namsoma tu kwenye magazeti, amerudi CCM lakini si UVCCM,” amesisitiza.

March 25 mwaka huu Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM ilitengua uteuzi wa aliyekuwa Kaimu Katibu wa Hamasa na Chipukizi wa umoja huo, Jokate Mwegelo.

Pia utakumbuka February 24, 2017  Wema alijiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akitokea Chama cha Mapinduzi (CCM) December 01, 2017 alitangaza kurejea CCM.

Liverpool Yaichapa Bila Huruma Manchester City Bao 3-0

$
0
0
Liverpool Yaichapa Bila Huruma Manchester City Bao 3-0
Michuano ya klabu bingwa barani Ulayani, hatua ya robo fainali inaendelea usiku wa kuamkia leo.

Liverpool wamewachapa bila huruma vinara wa ligi kuu ya England Manchester city bao 3-0, Magoli ya Liverpool yamefungwa na Mohamed Salah, Oxlade Chamberlin pamoja na Sadio Mane.


Barcelona wakiwa nyumbani dhidi ya As Roma wamepata ushindi wa mabao 4-1.

Mabao ya Barcelona katika mchezo huo, yamefungwa na wachezaji De Rossi ,Kostas Manolas ambao walijifunga wenyewe.Goli la tatu limefungwa na Gelard Pique huku bao la nne likipachikwa na Luis Suarez, bao la kufutia machozi la As Roma likifungwa na Edin Dzeko.

Haji Manara Amvaa Wema Sepetu “Sio Vizuri Kuingilia Lifestyle ya Mtu”

$
0
0
Haji Manara Amvaa Wema Sepetu “Sio Vizuri Kuingilia Lifestyle ya Mtu”
Jina la Haji Manara ni miongoni mwa majina maarufu kwa Tanzania katika mitandao ya kijamii, inawezekana hii inatokana na kuwa afisa habari wa club ya Simba SC ambayo ni moja kati ya club kongwe na kubwa Tanzania na ina mtaji mkubwa wa mashabiki.

Mara nyingi Haji Manara amezoeleka kwa misimamo yake anayopenda kuitoa sehemu mbalimbali akiwa anatetea hoja yake au anaitetea club yake ya Simba SC, leo kupitia ukurasa wake wa instagram ameamua kumshauri muigizaji na Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu, kupitia ukurasa wake wa instagram Manara ameandika hivi.



“#TBT.…. Juzi kwenye tuzo za Azam TV nilikaa jirani na muigizaji nyota kutoka India, Aaliyah @preetika_pree ..wakati jina la @wemasepetu lilipotajwa kwenda kuchukua tuzo yake alishangaa kusikia kelele za ushangiliaji..akaniuliza huyu ni nani?nikamjibu ni mmoja kati ya wanawake maarufu sana Bongo”

“Pengine ni namba mbili au tatu kama c moja..kisha aliwahi kuwa miss TZ..akashangaa alipomuona coz Wema sasa kanenepa. Ila nilimsisitiza kuwa Wema ni Star halisi bongo msingi wa hayo nilioandika ni kwako bibie..Linda image yako sasa..waangalie fans wako wanavyokupenda na kukutetea”

“Kuna vitu ukichange kidogo Taifa hili litakutumia kwa maslahi ya jamii yetu…ingawa sio vizuri kuingilia lifestyles ya mtu..ila wewe ni icon kwa wanawake..natamani one day nikuone katika level kubwa zaidi wangu 🙏🙏 @wemasepetu @azamtvtz”

Mrisho Mpoto Ampa Makavu Steve Nyerere" Mbona Huna Jema Ndugu? Punguza Gubu Ndugu Yangu"

$
0
0
Mrisho Mpoto Ampa Makavu Steve Nyerere" Mbona Huna Jema Ndugu? Punguza Gubu Ndugu Yangu"
Kupitia mitandao ya kijamii tumeona maneno mbalimbali yakisambaa kuhusiana na tuzo za Sinema Zetu zilizofanyika Jumapili ya April 1,2018 na kusemekana kuwa kuna baadhi ya waigizaji hawakuridhika na ushindi wa baadhi ya waigizaji wenzao.

Kupitia mtandao wa instagram waigizaji mbalimbali wameandika maoni yao kupitia yao na baadhi kuoneshwa kutoridhishwa kuhusiana ugawaji wa tuzo hizo akiwemo Steve Nyerere ambaye alionesha kutoridhishwa pia kwa upande wa Mrisho Mpoto ameonekana kupinga kile ambacho Steve Nyerere amekikosoa na kukiandika katika mitandao ya kijamii.



Mpoto ameandika maneno haya “Steve Nyerere Mbona huna Jema ndugu? Uzalendo ni Hali ya Mtu kujitoa kufa na kupona Kwa maslahi ya wengi yenye Tija Kwa Taifa, nikakusikia kwenye vyombo vya habari unasema Uzalendo ni project yako, tena ukaenda Mbali zaidi ukasema nimedandia project yako kwa mbele”

“Nikahisi tofauti kidogo Kwakuwa kilikua kipindi cha jua kali kidogo….Sasa hivi umeibuka na kuanza kuponda Tuzo za Sinema zetu ambazo ndiyo kwanza zinaanza ili kujaribu kurudisha Heshima ya filamu zetu ambazo wewe umechangia kufa kwake”

“Hauoni unakatisha tamaa watu wenye nia njema na filamu? Ebu punguza gubu ndugu yangu angalau tuwe na kitu kimoja Chenye heshima cha kujivunia kwenye tasnia ya sanaa ya uigizaji zile Tuzo zilitolewa Kwa wenye Umiliki wa filamu na aliyewasilisha kwenye Mashindano na siyo anaeonekana sana kwenye Runinga”

“Sio lazima apewe unaemtaka wewe Steve. Najua kile kilikua kipindi cha jua, hiki cha mvua labda utanielewa kidogo…wadau na Mashabiki wa Bongo Movie msikatishwe tamaa”

“Nimenyang’anywa Gari la Serikali Licha ya Kuwa ni Haki Yangu” -Mbowe

$
0
0

“Nimenyang’anywa Gari la Serikali Licha ya Kuwa ni Haki Yangu” -Mbowe
Mwenyekiti wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni (KUB), Freeman Mbowe amesema amenyang’anywa gari la serikali alilokuwa akitumia na Ofisi ya Bunge ambalo ni haki yake kuwa nalo.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma leo Jumatano Aprili 4, Mbowe amesema amenyang’anywa gari hilo tangu January, 2018.

“Sina gari la serikali wala dereva, nilinyang’anywa tangu Januari natembelea gari binafsi kwa sasa, licha ya kuwa ni haki yangu.” -Mbowe

“Lakini mimi sijililii mwenyewe, ninayo magari mengi nitatumia na hata nikikosa wabunge hapa watanipa gari la kutembelea,” amesema Mbowe bila kuelezea zaidi sababu za kunyang’anywa gari hilo.

Katibu wa Bunge Stephen Kagaigai akijibu tuhuma hizo amesema gari lipo isipokuwa Mbowe mwenyewe ndiyo hataki kulitumia.

“Gari la kiongozi wa upinzani lipo na dereva yupo, ila Mbowe halitaki gari wala dereva,” -Kagaigai.

Uhamiaji Inatumika Kisiasa Dhidi ya Abdul Nondo Sio Kosa Kuzaliwa Kigoma –Zitto Kabwe

$
0
0
Uhamiaji Inatumika Kisiasa Dhidi ya Abdul Nondo Sio Kosa Kuzaliwa Kigoma –Zitto Kabwe
Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amesema kuwa atampeleka Mwenyekiti wa Mtandao wa wanafunzi(TSNP), Abdul Nondo Uhamiaji ambapo jana alipelekwa katika ofisi hizo kwaajili ya kuhojiwa uraia wake.

Zitto kupitia mitandao yake ya kijamii amesema kuwa Idara ya uhamiaji imekuwa ikitumika kisiasa dhidi ya mwanafunzi huyo na sio kosa hata kidogo Abdul Nondo kuzaliwa Kigoma Ujiji.

Nitampeleka Abdul Nondo Uhamiaji tarehe 20/4/2018 kwa mamlaka yangu kama Mbunge wa Kigoma Mjini ( Jimbo analotoka Abdul na wazazi wake na mababu zake).

Idara ya Uhamiaji inatumika kisiasa dhidi ya mwanafunzi Abdul Nondo, Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania. Sio kosa hata kidogo Abdul kuzaliwa Ujiji Kigoma. Imekuwa tabia ya Serikali kuwapa kesi za uraia watu wanaotoka mikoa ya magharibi hasa Kigoma. Suala la Nondo ni vita dhidi ya Watu wa Kigoma. Tutapambana. Tutampigania Abdul Nondo. Watanzania tusikubali upuuzi huu wa watu wa Uhamiaji na Serikali ya Awamu ya awamu ya Tano kuwafanya raia wa mikoa kama Kigoma kuwa raia wa daraja B

Majambazi Wavamia Kanisa Katoliki Mbezi na Kupora Fedha na Vifaa vya Kuendeshea Misa

$
0
0
Majambazi Wavamia Kanisa Katoliki Mbezi na Kupora Fedha na Vifaa vya Kuendeshea Misa
Majambazi wamevamia na kuvunja kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu-Mbezi Mwisho jijini Dar es salaam, na kupora fedha na vifaa vya kuendeshea misa.


Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Kanda Maalum jijini Dar es salaam, Lazaro Mambosasa, amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo, ambapo majambazi hao waliingia kanisani hapo na kuiba vitu hivyo, ikiwemo fedha za sadaka zilizokusanywa tangu sikukuu za pasaka mpaka sasa.

“Ni kweli nimepokea simu kuwa kuna hilo tukio, ni vibaka wameingia hapo kanisani na kuiba pesa na baadhi ya vitu, pesa ambazo zilikuwa za sadaka tangu sikukuu, ila thamani yake bado hatujaijua kwa sababu ndio tukio limeripotiwa sasa, baada ya muda nitakuwa na taarifa kamili”, amesema Kamanda Mambosasa.

Kamanda Mambosasa amesema jeshi la Polisi linafanya uchunguzi kuwabaini waliohusika na tukio hilo, ili kuwafikisha mbele ya sheria.

Zitto Kabwe Alifikisha Sakata la Abduli Nondo kwa Wazee wa Kigoma “Wazee wa Ujiji Sasa Mkae Tumalize Haya Mambo ya Kipuuzi”

$
0
0
Zitto Kabwe Alifikisha Sakata la Abduli Nondo kwa Wazee wa Kigoma “Wazee wa Ujiji Sasa Mkae Tumalize Haya Mambo ya Kipuuzi”
Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo amefunguka na kuonyesha kuchoshwa na baadhi ya mambo ambayo yanaendelea nchini na kuamua kuwaomba wazee wa Ujiji Kigoma wakae ili kuweza kumaliza mambo hayo anayodai ni ya kipuuzi.


Zitto Kabwe amesema hayo baada ya Idara ya Uhamiaji kumuhoji kuhusu uraia wake Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi nchini Tanzania, Abdul Nondo jambo ambalo Zitto Kabwe anasema idara ya uhamiaji inatumika kisiasa dhidi ya mwanafunzi huyo.

"Sio kosa hata kidogo Abdul kuzaliwa Ujiji Kigoma. Imekuwa tabia ya Serikali kuwapa kesi za uraia watu wanaotoka mikoa ya magharibi hasa Kigoma. Suala la Nondo ni vita dhidi ya Watu wa Kigoma. Tutapambana. Tutampigania Abdul Nondo. Watanzania tusikubali upuuzi huu wa watu wa Uhamiaji kuwafanya raia wa mikoa kama Kigoma kuwa raia wa daraja B" alisema Zitto Kabwe

Aidha Zitto Kabwe alikwenda mbali na kusema kuwa mwanafunzi huyo ni mjukuu wa moja ya muasisi wa TANU ambaye pia alipigania uhuru wa Tanganyika

"Abdul Nondo Abdul Omar Mitumba, mjukuu wa Marehemu Mzee Omar Mitumba, mwasisi wa TANU na mpigania Uhuru wa Tanganyika leo anaitwa na maafisa Uhamiaji eti kuhojiwa uraia. Hao maofisa uhamiaji na aliyewatuma hawana 'credentials' ambazo Babu yake Nondo, Mwenyekiti wa TSNP anazo. Wazee wa Ujiji sasa mkae. Tumalize haya mambo ya kipuuzi" alisisitiza Zitto Kabwe

Mwanafunzi Abdul Nondo aliitwa leo idara ya uhamiaji kuhojiwa juu ya uraia wake na kujaza fomu hivyo anapaswa kufika tena ofisi za uhamiaji tarehe 20 mwezi huu kwa ajili ya kupeleka vyeti vya kuzaliwa yeye, baba na mama yake, na bibi na babu kwa pande zote mbili za wazazi wake.

Kamati ya Bunge Yampa Rungu Msajili Kuvifutia Usajili Vyama vya Siasa

$
0
0
Kamati ya Bunge Yampa Rungu Msajili Kuvifutia Usajili  Vyama vya Siasa
Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria imemtaka Msajili wa Vyama vya Siasa asisite kufuta usajili kwa chama chochote cha siasa kitakachokiuka sheria, kanuni na utaratibu wa uendeshaji wa vyama vya siasa nchini.

Pia, imeshauri ofisi ya msajili wa vyama vya siasa ihakikishe kuna usimamizi wa karibu wa kuchunguza mienendo inayoharibu sifa na vigezo ya vyama vya siasa nchini.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria, Mohamed Mchengerwa alisema hayo bungeni jana alipowasilisha maoni ya kamati kuhusu hotuba ya mapitio na mwelekeo wa kazi za Serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za ofisi ya Waziri Mkuu na ofisi ya Bunge kwa mwaka 2018/19.

Akiwasilisha maoni hayo baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kusoma hotuba yake, Mchengerwa alisema ofisi ya msajili ivifutie ruzuku vyama vitakavyobainika kutumia fedha kinyume cha madhumuni yaliyokusudiwa ili kutoa fundisho kwa vyama kuzingatia matumizi stahiki ya fedha za wananchi.

Kamati imeiagiza ofisi ya msajili kufanya ufuatiliaji na ukaguzi wa matumizi ya ruzuku kwa vyama vya siasa, hatua inayolenga kuhakikisha fedha zinatumika kama ilivyokusudiwa.

“Kamati inaishauri Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kuzingatia sheria, kanuni, utaratibu na weledi katika usimamizi na utoaji wa ruzuku kwa vyama vya siasa,” alisema.Akizungumzia maoni ya kamati hiyo kuhusu vyama vya siasa, Naibu Spika, Dk Tulia Ackson alisema ushauri uliotolewa ni mzito, hivyo nakala ya taarifa ya kamati atapewa Msajili wa Vyama vya Siasa.

Mchengerwa pia alizungumzia mgogoro ndani ya CUF na kusema kamati inashauri msajili kufanya jitihada za kutosha kuusuluhisha ili kuepusha athari kubwa zinazoweza kujitokeza katika Muungano.

CUF kwa muda mrefu sasa imekuwa katika mgogoro ulioigawa pande mbili; moja inayomuunga mkono katibu mkuu Maalim Seif Sharif Hamad na nyingine Profesa Ibrahim Lipumba, mwenyekiti anayetambuliwa na ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.

Mbali ya masuala hayo ya vyama vya siasa, Mchengerwa aliitaka Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Ofisi ya Bunge kuiwezesha kamati yake kufanya ukaguzi wa hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa makazi ya Waziri Mkuu ili kujiridhisha na ujenzi wake na kiasi cha fedha kilichotumika.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi

Kamati hiyo pia imeishauri Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ihakikishe inafuatilia wasimamizi wa uchaguzi na kuwawajibisha wanapofanya uzembe unaosababisha madhara ambayo yangeweza kudhibitiwa mapema na msimamizi aliye makini na anayetambua na kutekeleza wajibu wake kwa mujibu wa sheria.

“Kamati inashauri tume kujitahidi kufanya kazi kwa weledi ili kuendelea kuaminika kwa wadau wa uchaguzi. Hii ni pamoja na kuhakikisha inawashirikisha wadau wakati wa uhuishaji wa daftari la wapiga kura ili kuepuka migogoro isiyokuwa na tija kwa Taifa,” alisema.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi, Oscar Mukasa akiwasilisha maoni kwa hotuba ya Waziri Mkuu alisema kamati yake inashauri Serikali kuipa fedha Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya kwa ajili ya miradi ya maendeleo ili iwe karibu na wananchi.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Hawa Ghasia alisema kamati maalumu zimekuwa zikiteuliwa kushughulikia mambo muhimu yenye masilahi ya kitaifa ambazo hazikutengewa bajeti kwa mwaka wa fedha husika hivyo kushauri Serikali ihakikishe inazirejesha mapema fedha zitakazotumika kutoka mfuko wa Bunge.

Soma Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Asubuhi ya Leo

Viewing all 104785 articles
Browse latest View live




Latest Images