Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104429 articles
Browse latest View live

Aliyekuwa Rais wa Brazil Ahukumiwa Kifungo cha Miaka 12 Gerezani

0
0
Aliyekuwa Rais wa Brazil Ahukumiwa Kifungo cha Miaka 12 Gerezani
Leo April 5, 2018 Mahakama ya rufaa nchini Brazil imeagiza aliekuwa rais wa nchi hiyo, Luiz Inacio Lula da Silva kuwa ni sharti aanze kutumikia kifungo chake cha miaka kumi na mbili gerezani, baada ya kupatikana na hatia ya kuhusika katika ufisadi.

Majaji sita kati ya kumi na mmoja wa mahakama ya rufaa walipinga rufaa hiyo huku watano kati yao wakimuunga mkono. Kesi hiyo imezua hali ya wasi wasi wa kisiasa nchini humo.

Lula amekutwa na hatia kutokana na uchunguzi wa muda mrefu wa sakata la rushwa linalojulikana kama ”Operation Car Wash’‘

Lula aligundulika kukubali rushwa yenye thamani Euro laki 7

Hatimaye Pretty Kind Amaliza Kifungo Afunguka Watu Walivyomnyanyapaa na Kunidhalilisha" Maisha Yalikua Magumu"

0
0
Hatimaye Pretty Kind Amaliza Kifungo Afunguka Watu Walivyomnyanyapaa na Kunidhalilisha" Maisha Yalikua Magumu"
JINA lake kwenye vyeti ni Suzan Michael ‘Pretty Kind’. Huyu ni msanii wa muvi, moja ya filamu alizoigiza ni Kilio cha Mnyonge, pia ni msanii wa Bongo Fleva.

Pretty ana wimbo mmoja tu uitwao Vidudu Washa, aliomshirikisha mwanamuziki Gigy Money. Amejizolea umaarufu mitandaoni hasa kwenye Mtandao wa Kijamii wa Instagram, kutokana na umbo lake lenye mvuto na kutupia picha akiwa amejiachia kihasarahasara.

Kutokana na picha hizo zinazopishana na maadili ambazo amekuwa akiposti, ilisababisha mpaka Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza kumfungia kujihusisha na sanaa kwa kipindi cha miezi sita.

Baada ya kutumikia miezi mitatu kati ya sita, juzikati alifunguliwa kuendelea na kazi zake, kwa onyo kali na kutakiwa kuwa balozi wa wasanii wenzake ambao wanamomonyoa maadili, kuhakikisha wanarudi kwenye mstari.

Showbiz Xtra, limempata Pretty ambapo amefunguka mambo mengi aliyopitia wakati akiwa amepigwa pini.

Showbiz Xtra: Hongera sana kwa kufunguliwa Pretty.

Pretty Kind: Asante, kwangu ulikuwa ni muujiza na ninamshukuru Mungu kwa kusikia kilio changu.

Showbiz Xtra: Ilikuwaje kwani, wewe na R.O.M.A, ambaye alikuwa amefungiwa pia mliomba msamaha au nini kilitokea?

Pretty Kind: Kwa upande wangu, nilikuwa nimeshaandika barua kadhaa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), za kuomba msamaha lakini sikuwa nimejibiwa. Siku moja kabla ya kufunguliwa nikiwa nimekaa tu nyumbani nilishangaa simu ikiingia na kuambiwa natakiwa na Naibu Waziri Shonza.

Siku ya pili nikaenda na kumkuta R.O.M.A na wasanii wengi, baadaye ndiyo tukazungumza na Waziri Harrison Mwakyembe na naibu waziri ambao waliniambia wamenisamehe na ninaweza kuendelea na kazi zangu.
Showbiz Xtra: Baada ya kuambiwa hivyo hali ilikuwaje?

Pretty Kind: Nilifurahi kiukweli maana maisha niliyokuwa ninaishi ni Mungu tu mwenyewe anajua. Watu walikuwa wananinyanyapaa na kunifanyia vitendo vingine vya kunidhalilisha.

Showbiz Xtra: Kwa nini watu walikuwa wanakudhalilisha na kukunyanyapaa?

Pretty Kind: Eti sina maadili. Ilifikia hatua wengine wakawa wananiita mkaa uchi. Kuna sehemu nilienda kuulizia fremu kwa ajili ya kuanzisha biashara wakanitimua kisa kufungiwa na hizo picha za mtandaoni. Jamani, maisha yalikuwa magumu kiukweli na kuna wakati nilikuwa ninakaa ndani mpaka nalia mwenyewe.

Showbiz Xtra: Maisha ya kawaida ulikuwa unayaendeshaje, maana huna biashara na ulikuwa hufanyi kazi yoyote ya sanaa?

Pretty Kind: Yalikuwa magumu, nilikuwa nakosa hata shilingi mia moja. Nakunywa mpaka maji ya bomba.

Showbiz Xrta: Lakini si una mpenzi, si alikuwa anakupiga tafu kiaina?

Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza (katikati) akiwa na Roma na Pretty.

Pretty Kind: Mh! Baada ya kupata matatizo huyo mpenzi sijui hata alipotelea wapi, sina mpenzi kiukweli nipo mimi kama mimi.

Showbiz Xtra: Unamaanisha Nuh Mziwanda?

Pretty Kind: Huyohuyo.

Showbiz Xtra: Si kuna kipindi ulisema mliachana, nilifikiri una mwingine?

Pretty Kind: Tulikuwa hatujapotezeana kabisa. Baada ya majanga ndiyo mambo yalienda kombo zaidi.

Showbiz Xtra: Kutokana na mnyoosho huo wa waziri kuna kitu umejifunza?

Pretty Kind: Nimejifunza mengi sana kiukweli. Tena sana. Siwezi kukaa tena uchiuchi huko mitandaoni. Kwa maana jamii ikiamua kukuadhibu, inakuadhibu kweli kiasi kwamba utaionja chungu ya maisha.


Suala la Wakina Baba Kubambikiziwa Watoto Latikisa Bungeni

0
0
Suala la Wakina Baba Kubambikiziwa Watoto Latikisa Bungeni
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile amesema kuwa si kweli kwamba watoto sita kati ya watoto waliopo nao wakina baba sio wa baba huyo au wazazi husika.

Dkt. Ndugulile ametoa kauli hiyo leo Bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge Busega, Raphael Chegeni aliyehoji kuwa,

Kwakuwa takwimu zinaonyesha zinaonyesha kwamba kila watoto wanaozaliwa watoto wanne sio wa baba muhusika, Je? Serikali inaonaje juu ya udhalilishaji wa kina baba kwakubambikiziwa watoto ambao sio wa kwao kigenetic.

“Si kweli kwamba watoto sita kati ya watoto wetu tuliokuwa nao sio wababa au wazazi husika naomba niweke vizuri takwimu ile na wale waliopeleka kupeleka vipimo vyao kwaajili ya vina saba kutambua uhalali wa mzazi, ni sawa sawa na unaenda katika wodi ya TB unataka kujua maambukizo ya wagonjwa wa TB katika wodi ya TB wale wote waliopeleka sample kwenye ofisi maabara ya Mkemia Mkuu wa serikali ni wale wote wenye wasiwasi kuhusiana na uzazi wa wale watoto na ndio maana hicho kiwango kilichopatikana kikawa hicho,” amesema

“Sio kwamba kwa ujumla wa Tanzania nzima hususa kwa kina baba watoto si wao sio kweli nilitaka niweke hiyo taarifa wazi ili wabunge especially wanaume tusianze kukimbia majukumu yetu ya msingi,” ameongeza.

Hata hivyo Naibu Spika, Tulia Ackson amesema kuwa “nilidhani wabunge wanawake wanataka kuandamana, Mh. Chegeni hilo swali lako na maelezo yako watu tuna watoto wengi humu ndani. Waheshimiwa wabunge Kiswahili cha kawaida kabisa kinasema kitanda hakizai haramu unaenda kupima wa nini.”

Ndugai Apinga Hoja Binafsi ya Bashe " Alitakiwa Kupeleka Kwenye chama Kabla ya Kuleta Bungeni"

0
0
Ndugai Apinga Hoja Binafsi ya Bashe " Alitakiwa Kupeleka Kwenye chama Kabla ya Kuleta Bungeni"

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Yustino Ndugai amesema suala la Mbunge wa Nzega Mjini (CCM), Hussein Bashe kutoa hoja binafsi bungeni, alitakiwa kuipeleka kwenye chama chake kwa ajili ya kujadiliwa kabla ya kuipeleka bungeni.

Ndugai amesema hayo ikiwa ni siku chache baada ya kurejea kutoka India alikokuwa akipatiwa matibabu. Amesema Kanuni za Bunge zipo na Kanuni za Uendeshaji wa Shughuli za Bunge kwa wabunge wa CCM kama chama tawala na zipo, kama kwa wabunge wa kambi ya upinzani ambazo zote ni sehemu ya uendeshaji wa shughuli za Bunge.

Amesema Bashe kama mbunge wa CCM, kanuni za wabunge wa CCM zinamtaka aipeleke hoja yake kwenye chama chake kwanza, ikajadiliwe huko na ikikubaliwa Bunge liweze kuipokea.

Amesema Bunge bado halijapokea hoja hiyo kutoka kwa Bashe, pia halijapokea taarifa kutoka kwa katibu wa wabunge wa CCM kama wameipokea hoja hiyo na wameshaurianaje.

Mwezi uliopita, Bashe alisema amemuandikia barua Katibu wa Bunge kuhusu ombi la kuwasilisha hoja binafsi bungeni ya kutaka kuundwa tume teule itakayochunguza matukio ya kihalifu yanayofanyika nchini.
Kuhusu afya yake, Ndugai ameeleza kwamba imeimarika kulinganisha miezi michache nyuma.

John Heche Afikishwa Mahakama

0
0
John Heche Afikishwa Mahakama
Mbunge wa Tarime Vijijini kupitia (CHADEMA), John Heche amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kusomewa mashtaka yanayomkabili.

Heche nae anakabiliwa mashtaka kama waliyofunguliwa Viongozi saba wa CHADEMA akiwemo Mwenyekiti Freeman Mbowe ambao wapo nje kwa dhamana.

Ester Bulaya Aitwa Polisi Dar

0
0
Ester Bulaya Aitwa Polisi Dar
Mbunge wa Bunda Mjini kupitia CHADEMA Ester Amos Bulaya, ameitwa kituo cha polisi cha kati jijini Dar es salaam huku akiwa hana taarifa za sababu ya wito huo


Akizungumza na www.eatv.tv, Ester Bulaya amesema amepata taarifa za kuitwa kwake polisi kutoka kwa mwanasheria wake na hivi sasa yuko njiani kuelekea kituoni hapo, ingawa hajui kitakachomkuta huko.

“Ni kweli nimepata taarifa kutoka kwa mwanasheria wangu, naitwa kituo cha Polisi na sasa hivi ndio nalekea huko central, sababu za wito huo sijui lakini huenda ikawa kama ya wenzangu kina Mdee”, amesema Ester Bulaya

Hivi karibuni kumekuwa na matukio ya kuwakamata viongozi na wabunge wa CHADEMA na kuwafungulia mashtaka, ambayo baadhi yao wengine wameshapandishwa mahakamani, kwa mashtaka ya kufanya maandamano bila kibali na kusababisha vurugu.

Roma Mkatoliki Akabidhiwa Cheti cha Usajili BASATA Awapa Ujumbe Huu Wasanii Wenzake

0
0
Roma Mkatoliki Akabidhiwa Cheti cha Usajili BASATA Awapa Ujumbe Huu Wasanii Wenzake
Rapa Roma Mkatoliki leo Alhamisi Aprili 05, 2018 amekabidhiwa cheti cha usajili kutoka BASATA hii ni baada ya kupewa masharti ya kufanya hivyo na Wizara ya Habari ili aweze kufutiwa adhabu yake ya kutojihusisha na muziki kwa miezi sita.

Roma akiongea na waandishi wa habari baada ya kukabidhiwa cheti hicho, amewashukuru watu wote walipaza sauti hadi kufutiwa adhabu hiyo, pia amewaasa wasanii wenzake kuchukua hatua mapema za kujisajili.

Wema Sepetu Ampa Ahadi Nzito RC Makonda " Nakuahidi Sitokuangusha"

0
0
Wema Sepetu Ampa Ahadi Nzito RC Makonda " Nakuahidi Sitokuangusha"
Baada ya kuibuka mshindi wa tuzo mbili za Sinema Zetu International Film Festival Award (SZIFF), Wema Sepetu amemuhaidi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutomuangusha katika suala zima la uigizaji.

Muigizaji huyo amemshukurua RC Makonda kwa kumtia moyo kwani ni kitu ambacho anakihitaji sana kwa kipindi hiki.

“Lakini pia naomba nikuahidi, sitokuangusha maana kumuangusha RC wako nako sio pambe kabisa,” amesema Wema.

Kauli ya Wema inakuja mara baada ya RC Makonda kumtaka muigizaji huyo kuweka picha ya tuzo aliyoshinda katika ukurasa wake wa Instagram baada ya baadhi ya watu kujitokeza na kukosoa tuzo hizo.

“Picha ya hapo juu uliyoomba ni mmiliki halali wa Filamu ya Heaven Sent ambaye kajisajili Cosota na Bodi ya Filamu, anazo haki miliki zake zote na ndio aliyeshinda Best Actress 2018 kwa kuwa amekidhi sababu zote za kuwa Mshindi,” amesema.

Wema ameendelea kwa kusema anataka tasnia ya Filamu iwe na watu wenye kujielewa na wenye upeo mkubwa, sio wenye kukurupuka na kuvamia jambo bila kudadavua na kujua ni kitu gani kinatakiwa kufanyika.

“Yote yanawezekana, wasanii ni watu wenye wadhifa mkubwa sana, najivunia kuwa mmoja kati yao. Ninajua hata wewe unajivunia kuwa kati yetu sisi ukiwa kama Mlezi ukituongoza kila leo kutaka tufike sehemu nzuri na Inshallah tutafika,” ameeleza Wema.

Vikundi Vyajitokeza ‘Kum-Support’ Jacob Zuma Makahamani

0
0
Vikundi vyajitokeza ‘kum-support’ Jacob Zuma Makahamani
Vikundi mbalimbali nchini Afrika Kusini ikiwemo vya kidini vimeandaa mkesha maalumu utakaofanyika usiku wa April 5, 2018 Jijini Durban kama ishara ya kuwa nyuma ya Rais Mstaafu wa nchi hiyo Jacob Zuma anayetarajia kupandishwa kizimbani.

Wafuasi hao wameandaa mkesha huo saa chache kabla ya Zuma kufikishwa Mahakama Kuu ya KwaZulu Natal kujibu mashtaka 16 ya ubadhirifu, rushwa na utakatishaji fedha ambayo yanahusishwa na malipo 783.

Malipo hayo yanadaiwa kufanywa kwa kuhusishwa na biashara ya silaha ambayo yanakadiriwa kuwa na thamani ya mabilioni ya Rand (aina ya pesa) ya nchini humo.

Mwenyekiti wa Chama cha Maveterani wa Jeshi wa chama cha siasa cha ANC Kebby Maphatsoe amesema atahudhuria kesi hiyo kwani amejifunza kusaidia rafiki wakati wa dhiki.

Tatua Matatizo yako Kwa Mtaalam wa Dua na Dawa za Kiarabu Pamoja na Mitishamba...

0
0
YULE MTAHALAM WA DUA NA DAWA ZA KIARABU NA ZA KIASILI YANI MITI SHAMBA SHARIFU LUKUMANI SASA YUPO HEWANI WENYE SHIDA ZITUATAZO CHEO KAZINI,KUONGEZEWA MSHAHARA KAZINI,MWENYE TATIZO LA NGUVU ZA KIUME,ALIEPOTELEWA NA HAMU YA KUFANYA TENDO LA NDOA, MWENYE KIFAFA,KISUKARI,FANGASI SEHEMU ZA SIRI KWA WALE WENYE MIILI MINENE MTOTO WA JICHO PAMOJA NA WALE WAKINA MAMA WANAOSUMBULIA NA CHANGO LA UZAZI PUMU YA MUDA MREFU WANAWAKE KUJAA MAJI SEHEMU ZA SIRI MWANAUME KUWAI KUFIKA KILELENI AU KUTOA MANII MFANO WA MAJIMAJI YAKIWA MEPESI AUTOWEZA KUMPA MKEO UJAUZITO JAMBO HILI LINAWASUMBUA WANAUME WALIO WENGI DUNIANI KWA KAWAIDA WANAUME ASIE NA TATIZO HILI UTOA MANII MAZITO NDIO YENYEUWEZO WA KUMPA MWANAMKE MIMBA.MWANAUME KUPATA MPENZI KWA ULAISI PASIPO NA GHARAMA YOYOTE YANI KWA WALE MADOMO ZEGE KUWA NA UWEZO WA KUSIKILIZWA HATAKAMA RAIA WA INCHI GANI NA UWEZO WA KURUDISHA MPENZI ALIE POTEA NA KUMFANYA AWE WAKO KWA WALE WASIO TAKA MITALA PIA UFANYA KAZI YA KUNG'ALISHA NYOTA SASA MATATIZO YAKO YAMEPATA SULUHISHO

 ANAPATIKA KWA MASAA ISHIRINI NA NNE WASILIANA NAE KWA NAMBA
 0762899488
0656145170
WhatsApp namba +255620665635

UTAFITI: Wasichana Wanaofukuzia ndoa, Hupenda Kupiga Picha Huku Wakionesha Kiganja cha Mkono wa Kushoto

0
0
Nimefanya utafiti kwa kuchunguza picha za wanawake wapatao mia ambao hawana hali ya ndoa.
Nimebaini kuwa 99.999% ya hao, hupenda kupiga picha huku wakiwa wame display kiganja cha mkono wa kushoto wakionesha kuwa 'mambo bado' probably ili kuhamasisha waoaji wajisogeze kunako inbox...

Tazama Baadhi ya Picha Kutoka kwa Wadada Tofauti:










Punguza Unene Unaokusumbua Katika Mwili Kwa Kutumia Bidhaa za Edmark

0
0

Tumia Dawa za Edmark za Kupunguza uzito uliozidi Mwilini Mwako, Edmark ni Vurutubisho na Chakula Mbadala na Zimehakikiwa na TFDA...

Ni uhakika kwa afya yako,👉 kupunguza uzito na sumu mwilini, Mafuta Sehemu Mbaya, Kitambi na nyama uzembe na kutibu MAGONJWA Mbalimbali kwa msaada wako mfuate instagram: @my_health_my_wealth @my_health_my_wealth


Au Mtafute WhatsApp Huyu Dada kwa kutumia Namba +255783 566844

Pia Dawa za Edmark Zinaweza kupa Fursa ya Biashara Uweze pata Kipato Kirahisi kwa Kuwasaidia watu Kuimarisha Afya zao

Serikali yaanda Maandamano ya Michezo April 26

0
0

Halmashauri ya jiji la Arusha imeaanda maandamano makubwa ya michezo ambayo yatafanyika siku ya sherehe ya maadhimisho muungano April 26, 2018 jijini Arusha 

Afisa michezo wa jiji la Arusha, Benson Maneno amethibitisha hilo na kusema kuwa maandamano hayo yatafanyika asubuhi kuelekea katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Karume ambapo ndipo zitafanyika fainali za michuano ya Muungano Cup na kumpata mshindi wa michuano hiyo, ambapo mshindi wa kwanza atapata milioni mbili, mshindi wa pili milioni moja na mshindi wa tatu laki tano. 

"Mashindano hayo ambayo yameanzishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa jiji la Arusha akishilikiana na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Dakalo wameanzisha mashindano haya maalum kwa kata zote 25 ambapo watashirikisha vijana wenye umri chini ya miaka 26, hivyo kila kata itacheza na kata nyingine ili kupata mshindi wa michuano hiyo. Fainali hizo zitafanyika jioni lakini asubuhi ya tarehe 26 kutakuwa na maandamano makubwa ya wana michezo kuelekea uwanja wa Sheikh Amri Abeid Karume kwa ajili ya kufanya fainali hiyo ya Muungano CUP" alisema Benson Maneno 

Lakini kwa upande mwingine, siku hiyo hiyo ya Muungano 26 April, 2018 watu mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii wakiongozwa na mwanaharakati wa mitandao Mange Kimambi pia wamepanga kufanya maandamano ya nchi nzima kupinga baadhi ya vitu ambavyo vinaendelea nchini kwa sasa.

Afande Sele Awapa Wosia Watoto Wake "Nikifa Msikubali Nizikwe Msimamie Nichomwe Moto”

0
0
Afande Sele Awapa Wosia Watoto Wake "Nikifa Msikubali Nizikwe Msimamie Nichomwe Moto”
Msanii wa muziki kutoka mkoani Morogoro, Afande Sele ameacha wosia kwa watoto wake wawili kwamba akifariki wahakikishe anachochwa moto.


Rapa huyo amewata watoto wake wasimamie hilo kwa kuwa hiyo ni zawadi ambayo anaona itamfaa kutokana na malezi kwa watoto wake hao.

“Kila wakati nikipata nafasi ya kuongea na hawa binti zangu wawili huwa nawakumbusha kwamba yote ninayowatendea chini ya jua ni wajibu wangu na ni haki yao lakini kitu pekee kikubwa kwangu wanachoweza kunilipa ni wao kuhakikisha kuwa siku yangu ya mwisho ikifika wasiruhusu kivyovyote mwili wangu kuzikwa/kufukiwa udongoni bali zawadi iliyobora kwangu watakayopaswa kunipa ni kuhakikisha mwili wangu unateketezwa kwa Moto💥 na kubakia majivu ambayo ndio watayazika ardhini na kubakia kama alama ya pale nilipo lala mimi ule usingizi mzito na usiokua na ndoto…’maisha ni kupanga na kupanga ni kuchagua’….usifosi tufanane.,” aliandika Afande Sele.

Rapa huyo awali aliwahi kutoa taarifa ya kutaka asizikwe na achomwe moto huku akidai hana dini hivyo hataki hausishwe na dini yoyote.

Aveva Afika Mahakamani Akiwa na Hali Mbaya Atembea Akishikiliwa

0
0
Aveva Afika Mahakamani Akiwa na Hali Mbaya Atembea Akishikiliwa
Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva ambaye alikuwa akiugua kwa muda mrefu, leo Aprili 5, amefika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuhudhuria kesi yake inayomkabili licha ya hali yake kuonekana imedhoofika huku akishikwa mkono kumsaidia kutembea.



Akiwa mahakamani hapo, muda mwingi alionekana kusaidiwa na makamu wake Godfrey Nyange maarufu kama Kaburu ambaye ni mtuhumiwa mwenzake katika kesi hiyo ambapo wawili hao wanakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi, nyaraka na kutakatisha fedha kiasi cha Dola za Marekani 300,000.



Katika kesi hiyo, upande wa mashtaka umeiomba mahakama kusogezwa mbele kesi ili kubadili hati ya mashtaka na kuongezwa mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo. Aidha, mahakama imeahirisha kesi hadi April 12, mwaka huu.

Mtanzania Aliyemuua Mkewe Apandishwa Kizimbani Uingereza

0
0
Mtanzania Aliyemuua Mkewe  Apandishwa Mahakamani
Stori kutokea Uingereza leo April 5, 2018 ni kumhusu Kema Salum ambae ni Mtanzania amepandishwa kwa mara ya kwanza Mahakamani katika Mahakama ya Crown kwa tuhuma za kumuua mke wake, Leyla Mtumwa.

Salum mwenye miaka 38 anadaiwa kumuua mke wake, Leyla, siku ya Ijumaa kuu kwa kumchoma visu mara shingoni na kifuani. Mauaji hayo yalifanyika nyumbani kwa wanandoa hao, Kirkstall Avenue, Haringey, Uingereza.

Kesi hiyo ya Salum haikuweza kusikilizwa baada ya kuwepo kwa mgomo wa wanasheria wa ngazi za juu nchini humo ulioanza tangu April 1, 2018.

Wakili anayemtetea Seona White amesema amewasiliana na vitengo zaidi ya 20 vya wanasheria, lakini hakuna aliyekubali kumtetea Salum kutokana na mgomo wa Wanasheria unaoendelea,

Jaji wa mahakama hiyo, Anuja Dhir amesema kesi hiyo itasikilizwa tena June 20 na akaamuru mtuhumiwa arudishwe mahabusu.

Muigizaji Maarufu wa Filamu za Kihindi Salman Khan Amehukumiwa Miaka Mitano Jela

0
0
Muigizaji Maarufu wa Filamu za Kihindi Salman Khan Amehukumiwa Miaka Mitano Jela
Muigizaji marufu wa filamu wa India Salman Khan amehukumiwa miaka mitano jela, kwa kosa la ujangili alilolifanya mwaka 1998.


Hukumu hiyo imetolewa leo na mahakama ya India baada ya kumkuta na hatia, huku waigizaji wenzake Saif Ali Khan, Tabu, Sonali Bendre na Neelam Kothari wakiachiwa huru kutokana na kutokutwa na hatia.

Salman Khan alishtakiwa kwa kosa la ujangili la kuua wanyama wawili wanaojulikana kama 'blackbucks' ambao ni jamii ya swala wa kipekee walioko nchini India, na serikali ya nchi hiyo inawatunza kwa uangalizi mkubwa.

Salman Khan alifanya tukio hilo katika kijiji cha Kankani ambako alikuwa akiigiza filamu yake ya Hum Saath Saath Hain , akiwa na waigizaji wenzake.


Aina ya wanyama ambao Salman Khan amewaua na kusababisha afungwe

Mbasha Afunguka Kumpa Ujauzito Agness

0
0
Mbasha Afunguka Kumpa Ujauzito Agness
Msanii wa nyimbo za Injili nchini, Emmanuel Mbasha amesema amesikitishwa na taarifa alizozipata kuwa amempa ujauzito msichana anayevuma kwenye mitandao ya kijamii Agness na kudai hana mahusiano yeyote na mtu huyo zaidi ya kumfahamu kupitia mitandaoni


Mbasha amebainisha hayo kupitia kipindi cha eNewz kinachorushwa na tinga namba moja kwa vijana baada ya kuwepo na tetesi za muda mrefu zinazozidi kuzagaa kwenye mitandao ya kijamii zikiwa zinadai kuwa wawili hao wana mahusiano ya kimapenzi na mpaka kufikia hatua ya kukubalia kupeana ujauzito.

"Agness mimi namfahamu kama shabiki yangu kupitia mitandao ya kijamii. Sasa sielewi mambo yamegeuka vipi mpaka kufikia hatua ya kuambiwa mimi nina mahusiano naye. Sijawahi kuwa na mahusiano na Agness na wala sijawahi kuwa na chochote kile kinachoashiria mapenzi", amesema Mbasha.

Pamoja na hayo, Mbasa ameendelea kwa kusema "sitegemei kupata naye mtoto kama watu wanavyosema kwa kuwa sina mahusiano nae kwa vyovyote vile huyo msichana ni shabiki wangu tu".

Mbunge Ataka Wanaume Wabakaji Wahasiwe

0
0
Mbunge Ataka Wanaume Wabakaji Wahasiwe
Mbunge wa viti Maalum CUF Rukia Kassim Ahmed, ameibua hoja bungeni kutaka serikali iweke sheria ya kuhasi wanaume watakaobainika na makosa ya ubakaji wa watoto wadogo.


Mh. Rukia Ahmed ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akiuliza swali Bungeni kwa wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na watoto, akitaka kujua hatua stahiki wanazochukuliwa watu wanaofanya vitendo vya ubakaji kwa watoto, kwani zilizopo anaona ni ndogo hivyo zinachangia kuongezeka kwa vitendo hivyo.

“Kwa kuwa serikali inachukua hatua za kutosha dhidi ya udhalilishaji huu, lakini bado vitendo hivi vinaendelea kwa kasi kubwa katika jamii zetu, je, serikali haioni kwamba adhabu inayotolewa ni ndogo, hivyo basi, iletwe sheria hapa Bungeni tuipitishe, yeyote atakayepatikana na hatia ya kubaka mtoto mdogo ahasiwe?”, amesema Mbunge huyo.

Licha ya hilo Naibu Waziri wa Afya Faustine Ndugulile alijibu swali hilo akisema kwamba serikali inatambua vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa watoto, na ndio maana ikatunga sheria za watoto ili kuwalinda.

Rais Magufuli Asikitishwa na Ajali Iliyoua Watu 12 Atoa Tamko

0
0
Rais Magufuli Asikitishwa na Ajali Iliyoua Watu 12 Atoa Tamko
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa ajali iliyotokea usiku wa jana Mkoani Tabora na kusababisha vifo vya takribani watu 12.


Dkt. Magufuli ameeleza hayo kwenye salamu zake za rambirambi alizozitoa leo Aprili 05, 2018 baada ya kupita siku moja tokea basi la kampuni ya City Boy lililokuwa limebeba abiria kutoka Karagwe Mkoani Kagera kuelekea Dar es Salaam kugongana uso kwa uso na lori aina ya Fuso lililokuwa linatoka Singida kuelekea Igunga.

“Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa ya vifo vya watu 12 waliopoteza maisha katika ajali ya barabarani iliyotokea jana usiku katika wilaya ya Igunga mkoani Tabora, nawapa pole wafiwa wote, ndugu, jamaa na marafiki walioguswa na msiba huu mkubwa. Nalitaka Jeshi la Polisi, Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa na Wilaya na Mamlaka zote zinazohusika na usalama wa barabarani kujitathmini, na kutafuta majawabu ya kwa nini ajali za barabarani zinaendelea kutokea kwa kusababishwa na uzembe na uvunjaji wa sheria za barabarani?”, amesema Dkt. Magufuli.

Pamoja na kutoa pole kwa wafiwa, Dkt. Magufuli amewataka viongozi wote wanaohusika na usimamizi wa usalama wa barabarani kutafakari kwa nini ajali nyingi zimekuwa zikitokea katika maeneo yaleyale na kutafuta ufumbuzi ili kuepusha madhara ya watu kupoteza maisha, kupata ulemavu wa kudumu na kupoteza mali.

Kwa habari kamili soma hapa chini.
Viewing all 104429 articles
Browse latest View live




Latest Images