Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104774 articles
Browse latest View live

Inasikitisha Mume Ampasua Mkewe na Shoka Kichwani

$
0
0

Inasikitisha Mume Ampasua Mkewe na Shoka Kichwani
Ukatili dhidi ya wanawake unaendelea! Siku chache baada ya Mtanzania Leyla Mtumwa kudaiwa kuuawa kwa kuchomwa visu na mumewe, Keme Kasambula jijini London, nchini Uingereza, Mtanzania mwingine Elisha Misefa ‘Rasi’, mkazi wa Mtaa wa Yange Yange, Kata ya Msongola, Ukonga jijini Dar amedaiwa kumpasua kichwa kwa shoka mkewe, Habiba Said na kutokomea kusikojulikana.




Shemeji mtu akionyesha eneo la tukio, kitandani.



NI IJUMAA ILIYOPITA

Tukio hilo la kusikitisha lilitokea Ijumaa iliyopita majira ya saa 4 asubuhi ambapo awali, majirani waliwaona wanandoa hao wakiwa pamoja lakini baadaye walikuja kushtuka kuona mwanamke huyo akiwa amezimia ndani ya chumba wanachoishi huku akiwa amepasuliwa kichwani na damu zikimvuja.



SHEMEJI AFUNGUKA

Akizungumza na Gazeti la Amani, shemeji yake Habiba aitwaye Mbaraka Abdallah, alisema siku hiyo ya tukio, alipewa taarifa na kijana aitwaye Abdallah Hamisi ambaye alikwenda kumtazama Habiba ambaye ni mama yake mdogo na kumkuta akiwa uchi wa mnyama kitandani huku mwili mzima ukiwa umetapakaa damu.




“Unajua siku hiyo, shemeji (Habiba) alikuwa anatakiwa akawapokee watoto Stendi ya Mabasi ya Mikoani Ubungo waliokuwa wanatoka Morogoro.

“Sasa alikuwa akiwasiliana na watu wa Morogoro kwenye simu lakini ghafla majira ya saa nne hivi, mawasiliano yalikata wakati wakiwa tayari wameshawapakiza watoto kwenye basi la kuja Dar,” alisema shemeji huyo.



Aliongeza kuwa wale ndugu wa Morogoro walipoona mawasiliano yamekatika ndipo walipolazimika kumtafuta Abdallah ambaye ni mtoto wa dada yake Habiba ili aweze kwenda kumuangalia mama yake mdogo nyumbani kwake kujua kulikoni amekata mawasiliano.


Habiba Said kabla ya kujeruhiwa.



AKUTA MLANGO UMEFUNGWA

Shemeji huyo aliendelea kueleza kuwa, baada ya kijana huyo kufika kwenye chumba cha mama yake mdogo, alikuta mlango umefungwa na alipojaribu kuita, hakuna mtu aliyeitika.



AINGIA NDANI

Shemeji huyo alisema baada ya kuita kwa muda, kijana huyo aliamua kuufungua mlango na ndipo alipomkuta mama yake mdogo akiwa amelala kitandani akiwa amepoteza fahamu na kichwani kuna majeraha makubwa, akamfuata yeye na kumpa taarifa.

“Baada ya kunieleza, nilitoka mimi pamoja na ndugu wengine wa karibu ambapo kweli tulipofika tukamkuta Habiba akiwa ameumia na amezimia, chumba kizima kikitapakaa damu,” alisema shemeji huyo.


Jilani.



WARIPOTI POLISI

Baada ya kuona Habiba amezimia na ana hali mbaya, ndugu hao walikwenda kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi cha Msongola ambapo walipewa fomu maalum ya matibabu (PF 3), wakamchukua mgonjwa wao na kumpeleka Hospitali ya Mbagala lakini nako walishauriwa wampeleke Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

“Tulipomfikisha Muhimbili, Habiba alilazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) ambapo hadi leo (Jumatatu iliyopita) ndio tumepata taarifa kuwa amezinduka na kuanza angalau kunywa uji kwa kutumia mrija,” alisema shemeji huyo.


Eneo alipokuwa akiuza chakula.

MAFUNDI WALIMUONA MTUHUMIWA

Katika mazungumzo mengine, shemeji huyo alisema baadhi ya mafundi waliokuwa wanajenga katika nyumba za jirani, karibu na nyumba aliyokuwa anaishi Habiba, walimuona Rasi akitoweka huku akiwa na damu kwenye mwili wake na hata walipomuuliza, alisema amepata ajali.

“Kuna mafundi walimuona wakati anaondoka na walipomuuliza kwa nini ana damu kwenye mwili wake, aliwajibu kuwa amepata ajali,” alisema shemeji huyo.



JIRANI NAYE ANENA

Shuhuda wa tukio hilo ambaye ni jirani yake Habiba aitwaye Mariamu Kiburura, alilielezea tukio hilo na kusema liliwashtua kwani hawakutegemea kama lingeweza kufanyika muda wa mchana kweupe.

“Nilitoka kwenye mihangaiko yangu, muda wa saa nane hivi nafikiri ndipo tulisikia kuwa kuna tukio limetokea hapa nyumbani kwa Habiba ndipo tukaenda pale tukaingia ndani na kumkuta akiwa amelala kitandani na mwili wake ukiwa umetapakaa damu, ndio ndugu zake wakamchukua wakapitia polisi na baada ya hapo wakampeleka hospitali.

“Inauma maana tukio limetokea mchana kabisa, tunamuombea kwa Mungu ili aweze kupona ili aendelee na shughuli zake,” alisema shuhuda huyo.


Shoka lililotumika.


MWENYEKITI ENEO LA TUKIO

Mwenyekiti wa Mtaa wa Yange Yange, Kata ya Msongola, Ukonga Dar, George Mohele, alipoulizwa na gazeti hili la Amani alikiri kutokea kwa tukio hilo katika eneo lake ambapo aliambata na wanahabari wetu hadi nyumbani hapo na kushuhudia chumba kilichofanyika unyama huo kikiwa kimetapakaa damu.



Mwenyekiti huyo alisema kwa kuwa suala hilo lipo chini ya polisi, wanaliacha jeshi hilo liendelee kufanya uchunguzi wake na kuweza kumweka mtuhumiwa kwenye mikono ya sheria ili ifuate mkondo wake.

Alipotafutwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, ACP Salum Hamduni, simu yake iliita bila kupokelewa kisha alipopigiwa kwa mara nyingine, alituma ujumbe mfupi akieleza kuwa yupo kwenye kikao. Hata hivyo, baadhi ya maofisa wa polisi ambao waliomba majina yao yasiandikwe gazetini kwa kuwa siyo wasemaji walikiri kutokea kwa tukio hilo.



Daimond Harmonize Wapania Kuziondoa Ngoma za Kibongo

$
0
0
Daimond Harmonize Wapania Kuziondoa Ngoma za Kibongo
Msanii wa muziki Bongo kutoka label ya WCB, Harmonize amesema ngoma yake mpya na Diamond inayokwenda kwa jina la Kwa Ngwaru ni mwanzo wa kurudisha ngoma za kuchezeka.

Muimbaji ameiambia Funiko Base, Radio Five kuwa nyimbo za kuchezeka Bongo zimepungua kwani ambazo zinazotoka sasa hivi zimepoa kitu ambacho kinafanya nyimbo za wasanii wa Nigeria kupewa nafasi hasa club.

“Inafikia wakati tunaona ni lazima tucheze, so tukaona this time around tukija na Kwa Ngwaru kama ngoma nyingi zilitoka kama zimelala ndio maana ukienda club unasikia Wanigeria wakati sisi tunaweza tukafanya muziki mzuri watu wakapenda na wakacheza,” amesema.

“Mwisho wa siku tunapenda tu ngoma zao kwa sababu ya beat lakini lugha hatuijui,” ameongeza.

Kwa Ngwaru ni ngoma ya pili kwa Harmonize kumshirikisha Diamond baada ya hapo awali kumshirikisha katika wimbo iitwayo Bado iliyotoka mwaka 2016.

Irene Poul Amwagia Sifa Zari " Hakuna Staa Mkubwa Bongo Kama Zari"

$
0
0
Irene Poul Amwagia Sifa Zari " Hakuna Staa Mkubwa Bongo Kama Zari"
MUIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Irene Paul amewakata vilimi mastaa wa Bongo kwa kuwaambia kuwa hakuna staa mkubwa Bongo kama Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’.

Akizungumza na Amani hivi karibuni, Irene alisema mrembo huyo wa Uganda ni mfano wa kuigwa kwani anajua kutengeneza jina lake na ni mtafutaji wa kweli.

“Ni staa mkubwa, anajua kumaintain jina lake, simuoni staa wa kumshinda yeye Bongo,” alisema Irene.

Kauli hiyo iliungwa mkono na baadhi ya mashabiki waliomsikia muigizaji huyo alipokuwa kwenye utoaji wa tuzo za wasanii wa Kibongo ambazo ziliandaliwa na kituo cha Azam TV.

Waziri Mwigulu Aagiza Kukamatwa kwa Madereva Wanaosababisha Ajali

$
0
0
Waziri Mwigulu Aagiza Kukamatwa kwa Madereva Wanaosababisha Ajali
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Mwigulu Nchemba amelitaka Jeshi la Polisi kuwaweka ndani madereva wanaosababisha ajali kutokana na mwendo kasi na baadaye kupelekwa Mahakamani.



Dkt. Mwigulu ametoa agizo hilo leo Bungeni Mjini Dodoma alipokuwa akijibu muongozo wa Mbunge wa Ulanga Morogoro Mhe. Goodluck Mlinga, juu ya chanzo cha ajali ya basi la City Boy kutoka Karagwe Mkoani Bukoba kuelekea Dar es Salaam ambalo liligongana uso kwa uso na lori aina ya Fuso lililokuwa linatoka Singida kuelekea Igunga usiku wa Aprili 04 mwaka huu na kusababisha vifo vya watu 12.

“Hatuwezi kuacha watu wanapotea kwa ajili ya uzembe wa mtu mmoja na kuleta hasara na vilio vikubwa kwa Watanzania,” alisema Dkt. Mwigulu.

Amesema, ajali nyingi zinazotokea hapa nchini zinasabishwa na mwendokasi na sio tatizo la miundombinu ambapo katika ajali zilizoripotiwa ajali 1500 zilisababishwa na mwendo kasi na ajali 89 zimetokana na miundombinu.
Aidha Dkt. Mwigulu amesema, Tanzania ni moja ya nchi zenye barabara bora hivyo ajali nyingi zinazotokea husababishwa na uzembe wa madereva pamoja na mwendokasi.

Penzi la Uchebe Lazidi Kumvuruga Shilole Aamua Kuchora Tattoo Yenye Jina la Uchebe

$
0
0
Penzi la Uchebe Lazidi Kumvuruga Shilole Aamua Kuchora Tattoo Yenye Jina la Uchebe

Staa wa muziki kutokea kwenye Bongo Fleva Zuwena Mohamed “Shilole” amezua gumzo katika mitandao ya kijamii baada ya kuamua kupost picha kupitia instagram account yake na kuonyesha tattoo mpya aliyoichora kwenye mwili wake kwa kuandika jina la mume wake Uchebe.

Shilole amepost sehemu ya mwili wake alipochora tattoo hiyo yenye jina la Ashrafu ambalo ni jina halisi la mume wake ambaye wengi tunamfahamu kama Uchebe, Shilole amepost picha hiyo na kuandika >>>“Kwa mara ya kwanza na ya mwisho nimechora tatooooo ya jina la mume wangu Nampendaa sana”



Shilole aliwahi pia kuchora tattoo ya aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Nuh Mziwanda na baadae kuifuta na hii itakuwa tattoo yake ya pili kuichora lenye jina la mwanaume ambae ni mpenzi wake na kuionyesha hadharani.

Rais Magufuli Leo Kuzindua Ukuta Mererani

$
0
0
Rais Magufuli Kuzindua Ukuta Mererani

Rais John Magufuli , leo anatarajiwa kuzindua ukuta wa machimbo ya madini ya Tanzanite, uliopo eneo la Mererani mkoani Manyara.


Rais Magufuli aliagiza kujengwa ukuta kuzunguka mgodi wa Tanzanite mwaka jana ikiwa ni katika kutafuta jitihada za kudhibiti na kuzuia utoroshwaji wa madini hayo, ambayo yanapatikana nchini Tanzania pekee.

Rais Magufuli aliagiza kujengwa kwa ukuta kuzunguka mgodi wa Tanzanite Mirerani ambapo ukuta huo una urefu wa kilomita 24.5 na urefu wa mita tatu kwenda juu.

Pamoja na hayo dhamira nyingine iliyosababisha kujengwa kwa ukuta huo ni kuzuia uhalifu na si kuwazuia wachimbaji wakubwa na wadogo kupata riziki zao.

Ukuta huo umejengwa kwa gharama za Kitanzania isiyozidi bilioni 6.

Mbunge Aitaka Serikali Kufuta Mfumo wa Vyama Vingi

$
0
0
Mbunge Aitaka Serikali Kufuta Mfumo wa Vyama Vingi



Mbunge wa Viti Maalum Chadema, Cecilia Pareso amesema kama serikali ina lengo la kuwabana na kuwanyima haki wapinzani, basi ni bora mfumo wa vyama vingi ukafutwa ili ifahamike kwamba nchi ni ya chama kimoja.



Pareso ameyasema hayo jana Aprili 5, Bungeni Mjini Dodoma wakati akichangia katika Mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Ofisi ya Waziri Mkuu mwaka 2018/19 huku akidai kwamba vyama vya upinzani vimekuwa vikionewa ikiwemo viongozi wake kukamatwa mara kwa mara na kufunguliwa mashtaka huku wengine wakifungwa jela. Amesema vyama hivyo vimekuwa ni adui mwingine kwa kuwa kwa sasa vinapigwa vita na Serikali iliyopo madarakani, kuzuiwa kufanya shughuli za siasa majukwaani.



Pia alidai chaguzi ndogo zilizofanyika hivi karibuni, zilikuwa ni kati ya Chadema na Jeshi la Polisi na kudai kwamba wabunge na madiwani walinunuliwa, wakahama vyama vyao, hivyo kukalazimika kufanyika chaguzi nyingine ndogo alizodai zimegharimu zaidi ya Sh bilioni 6.



“Kama mnakataza vyama vya siasa visifanye mikutano ya hadhara, hamuwezi kuja bungeni na kutueleza vyama hivi vimeendelea kufanya vizuri miaka 26 iliyopita. Enzui za Mwalimu Nyerere maadui wa nchi hii walikuwa watatu ambao ni umaskini, ujinga na maradhi, lakini kwa yanayoendelea, leo adui mwingine ni vyama vya siasa,” alisema Pareso.



Hata hivyo, madai ya Pareso yalipingwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Mwigulu Nchemba.



“Nataka kuwashauri wabunge, tunapoongelea taasisi ambazo zipo kikatiba, zinafanya kazi kwa ajili ya wananchi, tuheshimu kazi zinazofanywa. Uhalifu wowote unaofanyika ndani ya nchi, iwe wakati wa uchaguzi au wakati si wa uchaguzi, unahitaji kuwahakikishia raia usalama wao.



“Kuna uchaguzi mmoja chama chako (Chadema) hakikushiriki, hakukuwapo na matukio ya yoyote. Sisi kama Jeshi la Polisi tupo kwa ajili ya kuwahakikishia wananchi usalama, wala hatuwezi kuacha wananchi wakakatana mapanga na kuuwana,” alisema Mwigulu.

Soma Nafasi za Ajira 221 Zilizotangazwa Leo Ijumaa

$
0
0

Weka Vizuri Muonekano Wako Sasa Kwa Kutumia Tiba Asilia

$
0
0

*PENDEZA_KESSY_ PRODUCT* : WEKA MUONEKANO WAKO VIZUR SASA, NIWAUZA TIBA NA UREMBO NA MAFUTA YASIO NA MADHARA YEYOTE WALA KEMIKALI KWA MATUMIZI NA MATOKEO NI MUDA WA KUANZIA WEEK (2) HADI (4)🍌🌾🥑



1) KUTOA MVI SUGU PIA ZA KUZALIWA NAZO _100,000/

2) KUREFUSH NYWELE KUZIJAZA NA KUZUIAKUKATIKA -100,000/

3) TENGENEZA MWILI WAKO KUWA NA UMBO ZURI (@)KUPAK-100,000/(B) KUNYWA (C)VIDONGE-130,000/

4)ONDOA NYAMA UZEMBE MIKONONI, TUMBON KUPAK -100,000/

5)TOA KITAMBI KABISA(@) KUPAK-10O,000/ (B)VIDONGE/SLIMING YAKUNYWA-130,000/

6) PUNGUZA MWILI MZIMA KUANZIA KILO UNAZOITAJI WEWE

@) DAW YA MAJIN NA VIDONGE_130,000/

7)PUNGUZA MAZIWA NA YASIMAME KAMA MWANZO _90,000/

8) KUONGEZA MAZIWA SAIZI UNAYOHITAJI WEWE_90,000/

9)ONGEZA UNENE WA MWILI MZIMA_100,000/

10) ONDOA MICHIRIZI ILIYO SHINDIKANA_90,000/

11) TOA MAKOVU, CHUNUSI, WEUSI KWENY MAPAJA KIKWAPAN_80,000/

13) KUWA MWEUPE NARANGI NZURI VIDOGO(WHITE SOLUTION)_130,000/(B)MAFUTA YAKUPAK 100,000/

14)TOA NDEVU KWA WANAWAKE NA VINYWELEO MWILINI _100,000/

15/ ONGEZA NGUVU KWA WANAUME (@)JELI AINAZOTE -100,000/(B)VIDONGE MAX MAN NA AINA NYINGI_ 100,000/

16) KUREFUSH MAUMBIL YA WANAUME

@) (HANDSOME UP) MASHINE _200,000/

@) JELI NA VIDONG VYA SHARK_130,000/

17) RUDISHA HAMU YA TENDO NA KUCHELEWA KUMALUZA HARAKA_100,000/

18) MAFUT YAKURUDISH USCHANA-100,000/

19) TOA MAFUT USON NA WEUSI WAMACHO _90,000/

20) ONDOA MIKUNJO USON_80,000/(21) ENGEZA MGUU (WABIA)_100,000/ 21) PATA MIKANDA YAKUPUNGUZA TUMBON AINA ZOTE 22) DAW YA NGIRI YAKUVIMBA NA KULEGEA 100,000/🍍🌾🥑


TUNAPATIKAN DAR E SALAAM:PIA NJE YA NCHI TUNATUMA MIZIGO,NA KWA MIKOAN KOTE UTAPATA *KESSY* NI WAAMINIFU WA KUTUM MIZIGO NA KUFIKA KWA WAKATI PIGA CM (+255) 0719955528

0756259180

0785371237

@ *Pendeza_kessy_product*

Delivery POPOTE ULIPO,



Baadhi ya Bidhaa zetu..

Hata Mama Yangu Aniulizi Kuhusu Madawa ya Kulevya- Chid Benz

$
0
0
Hata Mama Yangu Aniulizi Kuhusu Madawa ya Kulevya- Chid Benz
JANGA la matumizi ya madawa ya kulevya hapa nchini limekuwa kubwa siku hadi siku na hata duniani kwa jumla, watu mbalimbali wamekuwa wakiathirika na madawa hayo hususani wasanii ambao baadhi yao wamepotea katika soko la muziki kutokana na kujiingiza katika matumizi hayo.



Miongoni mwa wasanii wa Muziki wa Kizazi Kipya ambao wameathirika kwa kiasi kikubwa kutokana na matumizi hayo ni Rashid Makwiro ‘Chid Benz’.



Msanii huyu ni muhanga mkubwa kutokana na kushindwa kujimudu kwa sasa katika muziki kutokana na athari alizozipata za madawa.

Chid kabla ya kujiingiza kwenye matumizi hayo, alifanikiwa kuwa miongoni mwa wasanii wakubwa hapa nchini na kufanya vyema katika gemu la muziki ambapo alitambuliwa zaidi kupitia wimbo wake wa Dar es Salam Stand Up ambao ulipokelewa vyema na mashabiki wake.


Chid alikuwa akisifika kwa sauti nzuri yenye mvuto katika nyimbo zake kadhaa alizowahi kuimba hali ambayo iliwavutia kwa kiasi kikubwa wasanii wenzake kufanya naye kolabo.

Championi Ijumaa inakuchambulia jinsi msanii huyo alivyoathirika kutokana na matumizi ya madawa ya kulevya na maendeleo yake kwa sasa.



Ikumbukwe kuwa, umaarufu wa Chid Benz ulipotea ghafla baada ya kuanza kujiingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya zaidi ya miaka mitatu nyuma hali iliyoathiri mfumo wake mzima wa maendeleo pamoja na afya kwa jumla.



Chid aliwahi kukiri kujiingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya kupitia kituo kimoja cha redio hapa nchini katika siku za nyuma kwa kuomba msaada kwa ajili ya kujiondoa katika matumizi hayo jambo ambalo lilifanyika baada ya Babu Tale na mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ kujitolea kumsaidia kwa kumpeleka katika Sober House ya Bagamoyo inayoitwa Life and Hope ambapo alikaa kidogo kabla ya kurejea uraiani na kuimba kibao cha Chuma ambacho hakikuweza kutamba vilivyo.


Sikio la kufa halisikii dawa, hivyo ndivyo unavyoweza kusema, kutokana na msanii huyo kurejea tena katika matumizi ya madawa ya kulevya kwa mara nyingine na kusababisha apelekwe katika soba ya Iringa alikokaa kwa siku kadhaa kabla ya kurejea tena uraiani na kuendelea na matumizi yake kama kawaida.



Rais wa zamani wa Korea Kusini Ahukumiwa Miaka 24 Jela

$
0
0
Rais wa zamani wa Korea Kusini Ahukumiwa Miaka 24 Jela
Mahakama ya Korea Kusini imempata na hatia Rais wa zamani wa nchi hiyo, Park Geun-hye.

Geun amekutwa na makosa 18 ikiwemo kutumia vibaya madaraka yake na kupokea rushwa hivyo mahakama hiyo imemuhukumu kifungo cha miaka 24 gerezani.

Akisoma hukumu hiyo Jaji wa Mahakama hiyo alisema, “The President abused the power which was given to her by the citizens.” Hakimu huyo aliongeza kuwa hukumu kali ilihitajika ili kutuma ujumbe wa wazi kwa viongozi wa baadaye wa nchi hiyo.

Hata hivyo waendesha mashitaka walimwomba Hakimu kumhukumu Geun kifungo cha miaka 30 jela. Pia Rais huyo wa zamani wa Korea Kusini atatakiwa kulipa faini ya dola milioni 17 mbazo ni zaidi ya shilingi bilioni 38 za Kitanzania.

Kesi ya Geun a=ilifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanaza January 3 mwaka jana japo kiongozi huyo hakuweza kuhudhuria mahakamani hapo.

Harmonize Akubaliana na Zari Kumbwaga Daimond

$
0
0
Harmonize Akubaliana na Zari Kumbwaga Daimond
Stori za ua jeusi la aliyekuwa Baby Mama wa Diamond Platnumz, Zari The Boss Lady bado zipo kwenye headlines, hatimaye Harmonize amezungumzia hatua ya Zari kuachana na Diamond.

Muimbaji huyo wa WCB ameiambia Funiko, Radio Five kuwa yeye binafsi anaheshimu maamuzi ya Zari kwa kuwa ana sababu zake za msingi.

“Mimi na heshimu sana maamuzi ya mtu, siwezi kuzungumza kama ni vibaya au ni vizuri, kwanza muda wa kumshauri mtu kuhusu mahusiano ndio sina,” amesema.

Alipoulizwa iwapo kipindi wawili hao walikuwa katika mahusiano kuna baadhi ya vitu alinufaika navyo kutoka kwa Zari, Harmonize alijibu;

“Kuzungumza amenisaidia au hajanisaidi sio kitu kizuri halafu kwa njia moja au nyingine unaweza kuonekana ni mnafiki, kwanini usiseme siku zote uje useme leo,” alieleza.

Mnano February 14 mwaka huu katika siku ya wapenda nao Zari The Boss Lady ambaye ni mzazi mwenzie na  Diamond Platnumz, aliposti Ua Jeusi katika mtandao wa Instagram na kutangaza kuachana kimahusiano na msanii huyo rasmi.

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma Afikishwa Mahakamani

$
0
0
 Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma Afikishwa Mahakamani
Aliyekuwa rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amefikishwa mahakamani leo katika mji wa Durban ili kujibu mashtaka ya rushwa, udanganyifu na kujitajirisha kinyume cha sheria. Kesi hii inasikilizwa kwa mara ya kwanza na inahusu biashara ya zamani ya mauzo ya silaha tangu miaka ya 1990.

 Rais wa zamani wa Afrika Kusini anashutumiwa kupokea rushwa kutoka kwa Thomson CSF – jina la zamani la kampuni ya Thales – katika mpango wa mkataba wa mauzo ya silaha wenye thamani ya karibu Euro Bilioni 4 ulioafikiwa mnamo mwaka 1999.
Wakati huo, Jacob Zuma alikua makamu wa rais wa nchi ya Afrika Kusini. Anashutumiwa kuwa alipokea jumla ya euro milioni 50 kutoka kampuni ya Ufaransa ya Thales. Kwa upande mwingine, aliahidi kupatishia zabuni kampuni hiyo ya Thales.

Kwa jumla, Afrika Kusini iliamua kutumia zaidi ya dola bilioni 10 kurejelea upya silaha zake. Silaha ambazo nchi hiyo haikuweza kuzihitaji wakati huo na ambazo hazitumiwi leo. Lakini sababu kuu ni kwamba zaidi ya dola milioni 300 (hongo) zililipwa wakati wa mikataba hii.

Ndugai Afunguka Haya Kuhusu Matibabu ya Lissu

$
0
0
Ndugai Afunguka Haya Kuhusu Matibabu ya Lissu
Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema utaratibu wa Bunge kugharamia matibabu ya Tundu Lissu unaendelea kufanyiwa kazi na ukikamilika utatolewa ufafanuzi.

Spika Ndugai ametoa kauli hiyo jana Alhamisi Aprili 5, 2018 wakati akihojiwa na Kituo cha Televisheni cha Azam ikiwa ni siku moja kupita tangu aliporejea nchini akitokea India kwa matibabu.

Lissu ambaye ni mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya Chadema alishambuliwa kwa risasi zaidi ya 30, Septemba 7, 2017 na kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma na siku hiyohiyo alihamishiwa Hospitali ya Nairobi ambako alilazwa hadi Januari 6 alipohamishiwa Ubelgiji katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Leuven, anakoendelea na matibabu.

Tangu wakati huo, familia yake na viongozi wa Chadema wamekuwa wakililalamikia Bunge kutogharamia matibabu ya mbunge huyo huku Lissu naye mara kadhaa akizungumzia jambo hilo.

Lakini katika mahojiano hayo aliyofanya na mtangazaji wa televisheni hiyo, Charles Hilary, Ndugai amesema, “Lile tukio (la kushambuliwa Lissu) limekuwa ni jipya, linataka watu wengi waweze kuangalia jinsi ya kufanya. Kwa kifupi kila anayekwenda kutibiwa nje anakuwa na barua ya Wizara ya Afya au kibali kutoka Muhimbili, ndivyo sisi Watanzania tunafanya.”

“Hiyo ni kwa mbunge na asiye mbunge, hata mwananchi wa kawaida utaratibu ndio huo. Sasa kwa mheshimiwa Lissu alivyotoka Dodoma kila mtu anafahamu alipewa rufaa Nairobi na ndio maana tunaona kwa wabunge wengine wote wanaotibiwa kwa utaratibu huu huwa hawachangiwi hata na Bunge lenyewe.”

Amefafanua zaidi kuwa, “lakini mheshimiwa Lissu pale pale tulichanga sisi wenyewe wabunge kama wabunge kwa sababu tulikuwa tunajua safari hii ina tatizo ndio maana ikabidi watu wachange kutoka mfukoni.”

Amesema ni sawa na mtu aliyekata rufaa yeye mwenyewe kwenda katika hospitali aliyochagua, “kwa maana ile hakuchagua yeye mheshimiwa Lissu lakini familia yake na chama chake na kadhalika, halijawahi kutokea jambo kama lile katika Bunge letu, lina upya wa aina yake.”

Amesema upya huo unahitaji ushirikiano mkubwa wa familia na Bunge kuweka utaratibu ambao hautakuwa kwa kwa Lissu pekee.

“Hata kesho na keshokutwa huo ndio utakuwa utaratibu utatumika siku zijazo, kwa hiyo bado linafanyiwa kazi siku ya siku litakuja kutolewa maelezo kama linawezekana au haliwezekani.”

Kuhusu wabunge kupewa ulinzi baada ya Lissu kushambuliwa, Spika Ndugai amesema Dodoma hali ya ulinzi ni kubwa.

“Dodoma ni salama na tumemwomba RPC wakati wa Bunge na wakati wote ulinzi uwepo na umeimarishwa na sidhani kama litatokea tena,” amesema.

Kitwanga Awa Mbogo Bungeni " Mtu Ukiwa Msema Ukweli Lazima Wakuondoe Katika Nafasi Yako"

$
0
0
Kitwanga Awa Mbogo Bungeni " Mtu Ukiwa Msema Ukweli Lazima Wakuondoe Katika Nafasi Yako"
Mbunge wa Misungwi, Charles Kitwanga amefunguka na kusema kuwa mtu ukiwa msema ukweli lazima wakuondoe katika nafasi yako kwa kuwa hawataki watu wasema kweli.


Kitwanga amesema hayo bungeni alipokuwa akichangia mjadala wa kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2018/2019, mjini Dodoma na kudai hata ukiwa mtenda haki kwa kila mtu lazima wakuhamishe.

"Kichwa changu na kichwa cha Jenista Mhagama ni vichwa viwili tofauti kabisaa na uwezo wetu wa kufikiri upo tofauti kabisaa, kwa hivyo ni vyema tukapima na kuhakikisha kwamba pale anapofaa Jenista Mhagama aende Jenista Mhagama, pale anapofaa Kitwanga aende Kitwanga lakini hii ya kubebe jumla jumla na wakati mwingine ndugu zetu hii tabia ife na mimi siwezi kukubaliana na hilo na bahati nzuri ukiwa msema ukweli hata ukikaa pazuri watakuondoa tu. Na ukiwa unatenda haki kwa kila mtu hata ukikaa Kolomije watakuondoa wakupeleke Mtwara" alisisitiza Kitwanga

May 21, 2016 Mh Charles Kitwanga, alitenguliwa nafasi yake kama  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kwa sababu ya kuingia bungeni na kujibu swali linalohusu wizara hiyo akiwa amelewa.

Hatimaye Majibu ya Rufaa ya Wambura Kujulikana Leo

$
0
0
Hatimaye Majibu ya Rufaa ya Wambura Kujulikana Leo
Taarifa kutoka TFF zinaeleza kuwa Kamati ya Maadili ya Shirikishi hilo inatarajiwa kutoa majibu ya rufaa ya aliyekuwa Makamu wa Rais, Michael Richard Wambura, dakika kadhaa zijazo kuanzia sasa.

Wambura alikata rufaa kupinga kufungiwa maisha kujihusisha na soka baada ya kudaiwa kufanya ubadhirifu wa fedha za shirikisho pamoja na makosa mengine ndani ya TFF.

Kamati ya Maadili Yamfungulia Kifungo Abajallo na Kumpa Onyo Kali

$
0
0
Kamati ya Maadili Yamfungulia Kifungo Edgar Chibula na Kumpa Onyo Kali
Kamati ya Rufaa ya Maadili imeitupilia mbali rufaa ya Dustan Mkundi Ditopile na kuiagiza Sekretariati kulipeleka suala kake katia vyombo vya ulinzi kwa uchunguzi zaidi.

Dustan alifungiwa kutokana na kuwasilisha fomu ya mapato tofauti na fomu halisi ya Bodi ya Ligi.

Wakati huohuo Mwenyekiti wa Abajalo FC na mjumbe wa Bodi ya Ligi alikiri kutoa maneno makali mbele ya vyombo vya habari akiwa kama kiongozi.

Kutokana na kukiri kwake, Kamati imemfungulia kifungo cha kutojihusisha na soka Edgar Chibula na kumpa onyo kali.

Mgunduzi wa Tanzanite Apata Neema ya JPM Amwagiwa Milioni 100

$
0
0
Mgunduzi wa Tanzanite Amwagiwa Milioni 100 Kutoka kwa Rais Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameahidi kumpatia pesa kiasi cha Tsh. Milioni 100, Mgunduzi wa Madini ya Tanzanite, mzee Jumanne Ngoma imsaidie katika matibabu ya ugonjwa wake unaomsumbua wa kupooza.

magufuli amesema hayo leo, Aprili 6, 2018 katika eneo la Simanjiro ambako anazindua Ukuta uliojengwa kuzungushiwa Migodi ya Tanzanite, Mirerani ili kuzuia utoroshwaji wa madini hayo.

“Madini haya yalivumbuliwa na mzee Jumanne Ngoma mwaka 1967, na kupeleka sampuli kwa Geologist (mtaalam wa miamba) kwenda kuyapima, pamoja na kutambuliwa na Baba wa Taifa, Mwl Julius Kambarage Nyerere kwenye barua aliyoisani Oktoba 8, 1980 akitambua kazi nzuri ya mzee Ngoma.

“Hata alipoyavumbua hakujua yatakuwa na thamani kubwa kiasi hicho, lakini mzee Ngoma hakufaidika chochote, sasa naambiwa amepooza, nitampatia shilingi milioni 100 zikamsaidie katika matibabu,” alisema Magufuli.

Simuonyeshi Kuwa Nimeshtushwa na Kitu Ambacho Anakifanya – Nandy

$
0
0
Simuonyeshi Kuwa Nimeshtushwa na Kitu Ambacho Anakifanya – Nandy
Hitmaker wa ngoma ‘Kivuruge’, Nandy a.k.a African Princess amesema moja ya vitu asivyovipenda katika muziki wake ni kuingia katika beef na msanii mwingine.

Muimbaji huyu ameiambia Clouds TV kuwa yeye sio msanii wa kupenda ugomvi na yeyote anayetaka ugomvi kwake huwa anampuuzia.

“Mimi sio mtu wa ugomvi wa mara kwa mara kwa hiyo sitamani kuingia kwenye ugomvi na mtu. Huwa napuuzia kwa kumuonyesha kuwa anachokifanya ni cha kijinga sifuatili, yaani Simuonyeshi kuwa nimeshtushwa na kitu ambacho anakifanya au labda nakifuatilia,” amesema Nandy.

Utakumbuku kumekuwa na stori zinazodai kuwa Nandy na Ruby wana beef, hata hivyo wote wawili wamekuwa wakikanusha hilo kila wanapoulizwa na vyombo vya habari.

Kesi ya Zuma Yahairishwa Mpaka Juni 8

$
0
0
Kesi ya Zuma Yahairishwa Mpaka Juni 8
Kesi ya rushwa inayomkabili aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma imehairishwa mpaka Juni 8, 2018, itakaposomwa tena.

Jacob Zuma alifika mahakama kuu ya Durban leo asubuhi kusikiliza kesi yake ambayo ina mashtaka 16, yakiwemo ya rushwa, matumizi mabaya ya madaraka na utakatishaji wa fedha.

Wafuasi wa Zuma walijikusanya maeneo ya karibu ya mahakama hiyo huku wakiimba nyimbo za kumsifu, wakisema hawatamuacha mpaka mwisho, na wengine wakikikesha kumuombea.

Kesi hiyo dhidi ya Zuma ilishwahi kufunguliwa na kusikilizwa, kisha kufutwa mwaka 2009, lakini sasa imeanza kusikilizwa tena baada ya kuondolwa madarakani, huku Rais aliyechukua wadhifa huo Cyril Ramaphosa akiahidi kukomesha vitendo vya rushwa nchini humo.
Viewing all 104774 articles
Browse latest View live




Latest Images