Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104747 articles
Browse latest View live

Soma Nafasi za Ajira na Scholarships Zilizotangazwa Leo


Ulichaguliwa na Mungu kututambua Wanyonge – Mgunduzi wa Tanzanite kwa Rais Magufuli

$
0
0
Mtanzania aliyegundua madini ya Tanzanite, Mzee Jumanne Mhero Ngoma amesema kuwa Rais Magufuli alichaguliwa na Mungu kwa ajili ya kutetea wanyonge.

Kauli hiyo anakuja mara baada ya Rais Magufuli kumtambua rasmi kama mgunduzi wa madini hayo leo April 06, 2018.

“Asante kwa kunitambua kuwa ni mimi nilifanya shughuli hii hapa Mirerani, watu wote hawa wanashiba kwa ajili ya jamsho la mkono wangu,” amesema.

“Mhe. Rais inaeleweka wewe ulichaguliwa na Mwenyenzi Mungu ili uje hapa uweze kututambua wanyonge,” ameongeza.

Hapo awali Rais Magufuli alitangaza kutoka Tsh. Milioni 100 kwa ajili ya matibabu ya Mzee Ngoma ambapo aliitaka familia yake kufungua akaunti maalum kwa ajili ya kuingiza fedha hizo haraka.

Baada ya Kifesi Kuacha Kazi WCB Harmonize Atangaza Nafasi ya Kazi

$
0
0
Baada ya Kifesi Kuacha Kazi WCB Harmonize Atangaza Nafasi ya Kazi
Ikiwa ni wiki mbili tu zimepita tangu aliyekuwa mpiga picha wa Diamond Platnumz, Kifesi kutangaza kuacha kazi na kuvunja mkataba wake na WCB, hatimaye Harmonize ametangaza nafasi a kazi.

Harmonize kupitia ukurasa wa Instagram ametangaza nafasi moja ya kazi ya videographer ambapo amesema kuwa anahitaji kijana mwenye ujuzi na kipaji.

Kama unakipaji kwa sasa unaweza kuomba nafasi hiyo kwa kupiga simu namba 0623300333 ili uweze kupata maelezo zaidi ya jinsi ya kuwasilisha CV yako.

Hii Hapa Siri ya Bata Analokula Zari Dubai

$
0
0
Hii Hapa Siri ya Bata Analokula Zari Dubai
Wakati suala la mzazi mwenzake Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kutanua pande za Dubai likidaiwa kuwezeshwa na kigogo mmoja, imebainika tofauti na maneno ya watu mitandaoni.

Kwa takriban wiki moja na zaidi, Zari ameonekana Dubai akiwa na wanaye wakubwa watatu, wakila bata katika viunga mbalimbali vya kuponda raha hali iliyofanya watu wengi kutoa maoni yao mitandaoni.

Kuna baadhi ya watu walimsifia kwa kueleza kuwa anachokifanya ni sahihi kwani anao uwezo wa kifedha hivyo kula bata si tatizo, tofauti na wanawake wenzake waliowahi kutoka na Diamond, Wema Sepetu na Hamisa Mobeto.

Kuna wengine walimponda kwa madai kuwa fedha hizo anazotumia, si zake bali kuna kigogo anayemwezesha hivyo asijishebedue na kuwarusha roho kina Wema na Mobeto.

Risasi Jumamosi lilifanikiwa kuzungumza na mtu wa karibu na Zari ambaye aliomba hifadhi ya jina na kubainisha, licha ya Zari kuwa na fedha zake lakini nyuma ya safari yake hiyo, yupo mdhamini anayemwezesha.Alisema, safari hiyo Zari amedhaminiwa na kampuni moja (jina kapuni) ambaye ndiye anayempa jeuri hiyo.

“Watu hawajui tu. Nimeona wanasema mengi sana mitandaoni, ooh sijui kuna kigogo sijui Zari hana pesa ya kukaa Hoteli ya Dusit Marina pale Dubai, kwanza watambue Zari ana fedha.

“Mtu anamiliki mashule, ana maduka Afrika Kusini atashindwa kulipia hoteli shilingi milioni tano kwa siku? (Chumba cha hoteli hiyo gharama yake kwa siku ni kati ya shilingi laki 5 na milioni moja na ushee),” alisema mtu huyo wa karibu na Zari.

Kama hiyo haitoshi, mtu huyo aliweka bayana kuwa licha ya kujimudu kifedha, safari hiyo Zari alidhaminiwa na ndio maana hata picha alizoposti kwenye mtandao wa Instagram, amewataja wadhamini.

Risasi Jumamosi liliingia kwenye kurasa mbalimbali katika mtandao wa Instagram na kukutana na kampuni hiyo iliyomdhamini Zari.

Hadi tunakwenda mitamboni juzi, imeelezwa kuwa Zari pamoja na wanaye watatu wakubwa pamoja na kijana mwingine, walikuwa bado wapo Dubai wakitumbua maisha.

Inasikitisha Mtoto wa Miezi Sita Afariki Muda Mchache Baada ya Mama Yake Kutoka Mahabusu

$
0
0
Inasikitisha Mtoto wa Miezi Sita Afariki Muda Mchache Baada ya Mama Yake Kutoka Mahabusu
Mtoto wa miezi sita, Halfani Lema, mkazi wa Mtaa wa Ibanda Kata ya Nyegezi amefariki dunia saa chache baada ya mama yake kuachiwa kutoka Kituo cha Polisi Igogo, Nyegezi jambo ambalo limeibua utata.

Mama wa mtoto huyo, Ashura Theonest (26) alikamatwa na polisi Aprili 2, akidaiwa kuiba simu ya jirani yake hivyo kupelekwa mahabusu akiwa na mtoto wake.

Mwenyekiti wa mtaa huo, Vedastus Mushola alisema jana kwamba mama huyo alipofikishwa kituoni hapo aliwaomba askari waliokuwa zamu ajidhamini ili arudi nyumbani kwani hakuwa na maziwa ya kumnyonyesha mwanaye usiku kucha lakini hakuruhusiwa.

“Pamoja na mwanamke huyo kueleza sababu hiyo, hakuna askari aliyemruhusu, lakini baadaye usiku hali ya mtoto ilibadilika na Aprili 3 mchana ndipo walimruhusu kwenda hospitali ya Wilaya Butimba kwa ajili ya matibabu,” alidai Mushola.

Mwenyekiti huyo alisema mtoto huyo alifariki dunia baada ya kufikishwa hospitali wakati akitibiwa jambo lililozua hasira kwa wakazi wa eneo hilo wakisema polisi ndiyo waliosababisha kifo hicho.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema si kweli kwamba polisi ndio waliosababisha kifo cha mtoto huyo akisema mama wa mtoto alijidhamini na kuruhusiwa kwenda nyumbani, “Yule mama alipofika nyumbani mtoto wake, aliumwa akampeleka hospitalini na alifia hospitali. Hizi taarifa za kwamba mtoto alifia kituoni si za kweli, kwanza kituo cha Igogo hakina mahabusu ya wanawake kuna mahabusu ya wanaume tu, kwa hiyo ukweli ndio huo.”

Mushola alilitaka jeshi la polisi kuwashirikisha wenyeviti wa mitaa husika pindi yanapotokea matukio kwenye mitaa yao ili kuepusha adha kama hizo, “Matukio madogomadogo yawe yanasuluhishwa kwenye uongozi wa mtaa, kwanza mimi nilikuwa sijui tukio hilo hatujashirikishwa mpaka linafika polisi.”


Ashura hakutaka kuzungumzia suala hilo kwa sasa akieleza kuwa ana maumivu makali ya kupoteza mtoto wake lakini wananchi wenzake wa Mtaa wa Ibanda walisusia msiba huo wakitaka maelezo ya kina kutoka polisi.

Hali hiyo ililazimu maiti kukaa mochwari kwa siku tatu hadi pale uongozi wa polisi ulipotolea ufafanuzi suala hilo ndipo wananchi walipokubali kumzika mtoto huyo jana katika makaburi ya mtaa huo.

Ofisa utumishi wa Hospitali ya Nyamagana Andrew Chinduo alisema hakuwa na taarifa kuhusu tukio hilo lakini alitaka atafutwe Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba kwani ndiye msemaji mkuu.

Hata hivyo, Kibamba alipotafutwa simu yake iliita bila kupokewa.

Imeandikwa na Ngollo John, Jesse Mikofu na Sada Amir, (Mwanz

Mambo Ni hivi Kajala Aivuruga Ndoa ya P Funk

$
0
0
Mambo Ni hivi Kajala Aivuruga Ndoa ya P Funk
MAMBO ni moto! Staa wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja anadaiwa kuitifua vikali ndoa ya mzazi mwenzake, Paul Matthysse ‘P-Funk’ kwa madai kuwa, amerudisha majeshi kwa prodyuza huyo wa muziki wa Bongo Fleva.

Mtoa taarifa makini ameeleza kuwa, kwa sasa ndoa ya P-Funk imetifuka kwani mkewe aitwaye Samira amemjia juu mumewe kuhusu ishu yake ya kurudiana na Kajala kwani watu mbalimbali wamekuwa wakimpigia simu na kumweleza kwamba wamemuona mumewe huyo akiwa na Kajala.

“Ndoa ya P-Funk kwa sasa inawaka moto kwa kweli maana hakuna maelewano kabisa na mkewe ana mimba kubwa tu ya mtoto wa tatu na vurugu zote hizo zimesababishwa na Kajala ambaye anasemekana amerudiana na mzazi mwenzake huyo ambaye kabla ya kuachana walijaliwa kuzaa mtoto mmoja wa kike ambaye ni Paula,” alivujisha mchapo mtoa taarifa.

Licha ya chanzo kuzungumza hayo, katika mtandao wa kijamii wa Instagram hivi karibuni kulichafuka kutokana na mke wa P-Funk kutoa maneno makali ya jinsi anavyosumbuliwa na watu kuhusu mumewe kurudiana na Kajala ambapo aliandika pia kwamba P-Funk amwache atailea mimba mwenyewe kwa kuwa siyo ugonjwa.

Katika kurasa za umbea habari kubwa ilikuwa ni hiyo huku Kajala akitakiwa kuachana na P-Funk ili ndoa yake iwe na amani kuliko hivi sasa imetibuka huku mkewe akiwa ni mjamzito hivyo amhurumie mwanamke mwenzake huyo.

Ijumaa lilimtafuta Kajala ili kuzungumzia madai hayo ya kutibua ndoa ya P-Funk baada ya kurudiana naye kimapenzi ambapo alikuwa na haya ya kusema;

“Nashangaa kwa nini huyo mke wa P-Funk hajiamini wakati anatarajia kuzaa mtoto wa tatu sasa, mimi sijarudiana naye ila huyo ni mzazi mwenzangu tu, namsihi ajiamini maana huyo ni mume wake tu.”

Kwa upande wa mke wa P-Funk alipoulizwa alieleza; “Huyo Kajala kama yeye anajiamini sana kwa nini asiposti picha za huko anakoendaga na P-Funk kwenye Instagram…kwanza simfahamu muulizeni huyo P-Funk kuhusu hayo mambo yao.”

Ijumaa lilifanya jitihada za kumtafuta P-Funk ili kuzungumzia suala hilo lakini simu yake ya mkononi iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa.

Sipelekeshwi na Mapenzi na Wala Sijawahi Kumlilia Mwanaume- Nisha

$
0
0
Sipelekeshwi na Mapenzi na Wala Sijawahi Kumlilia Mwanaume- Nisha
Baada ya kuanzisha drama la aina yake hivi karibuni na kuingia katika headline na aliyekuwa Boy Friend wa J kwa kile kilichodaiwa walikuwa mapenzini, muigizaji Nisha amesema hajawahi kupelekeshwa na mapenzi.

Mingizaji amesema video zilizotoka katika mitandao zikimuonyesha akilia si kwa sababu ya mapenzi kama ilivyokuwa ikielezwa bali ni promotion ya ngoma yake ‘Bachela’.

“Yes, sijawahi kumlilia mwanaume yeyote, kipindi ambacho naanza kuposti nalia ndio kipindi ambacho tupo production, ukiusikiliza ule wimbo kuna sehemu natakiwa niwe nalia na ndio promotioni yangu ya kwanza kuiposti Instagram,”  Nisha ameiambia Times FM.

“No! no! hakuna binadamu ambaye hajawahi kuumizwa kwenye mapenzi ila sasa hivi nimeshakuwa mkubwa ambapo moyo wangu umeshashonwa vizuri unajielewa zaidi unaweza kuji-control na sipelekeshwi na mapenzi,” amesema.

Muigizaji huyo kutoka industry ya Bongo Movie kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la Bachela.

Balozi Wilbroad Slaa Awasilisha Hati Zake Za Utambulisho Kwa Mfalme Wa Sweden

$
0
0
Balozi Wilbroad Slaa Awasilisha Hati Zake Za Utambulisho Kwa Mfalme Wa Sweden
Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mhe. Wilbroad Slaa jana akiwasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Mfalme Carl XVI Gustaf wa Sweden.


Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mhe. Wilbroad Slaa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maofisa wa ofisi ya Mfalme wa    Carl XVI Gustaf wa Sweden baada ya utambulisho

Yanga : Ushindi Upo Pale Pale

$
0
0
 Yanga : Ushindi upo pale pale
Yanga, wanawakaribisha Welayta Dicha FC kutoka Ethiopia katika mechi ya kwanza ya hatua ya mtoano ya Kombe la Shirikisho Afrika itakayofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ikiwakosa nyota wake muhimu wa kikosi cha kwanza.

 Awali Yanga ilishuka uwanjani kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika bila washambuliaji wake tegemeo Donald Ngoma na Amissi Tambwe ambao ni majeruhi na leo inawakosa Kelvin Yondani, Pappy Tshishimbi, Said Makapu na Obrey Chirwa kutokana na kuwa na kadi za njano.

Akizungumza na gazeti hili jana, Kocha Msaidizi na beki wa zamani wa timu hiyo inayodhaminiwa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo ya Michezo ya SportPesa, Shadrack Nsajigwa, alisema jana kuwa ushindi mnono ndiyo utawaweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele katika michuano hiyo na si jambo lingine.

Nsajigwa alisema benchi la ufundi la timu hiyo limewaandaa wachezaji waliopo kuhakikisha wanapambana na kupata matokeo mazuri katika mchezo huo na kukubaliana na changamoto zinazowakabili.

"Msimu huu kwetu hauko vizuri, kwanza tulikuwa tunakabiliwa na wachezaji wengi majeruhi, na sasa kadi za njano zinatugharimu, ila tulishajiandaa na hali hii, kabla ya kujua kama tungetolewa katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Tunataka kupata ushindi, ni wazi kama tutatumia vyema uwanja wetu wa nyumbani tutakuwa tumejiweka mahali salama, ukitumia vizuri uwanja wa nyumbani unakuwa umejirahisishia safari yako," alisema Nsajigwa.

Yanga ambayo ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara walihamia kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho baada ya Township Rollers ya Botswana kuwaondoka katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa jumla ya mabao 2-1.

Kikosi hicho cha Mzambia, George Lwandamina, leo kitashuka uwanjani kikiwa na kumbukumbu ya kutolewa katika mashindano ya Kombe la FA na Singida United kwa kufungwa penalti 4-2 baada ya kutoka sare ya 1-1.

Rose Ndauka Amkumbuka Kanumba " Kanumba Ndiye Kanifikisha Hapa Nisingekuwa Hapa Bila Yeye"

$
0
0
Msanii wa filamu nchini Tanzania, Rose Ndauka amefunguka na kudai bila ya mafundisho na ushauri aliyopewa hapo awali na marehemu Steven Kanumba, muda huu watanzania na watu wengine wasingeweza kumtambua kama mmoja wa wasanii wazuri.


Ndauka ameeleza hayo kupitia ukurasa wake maalumu wa kijamii asubuhi ya leo na kusema Tanzania na dunia kiujumla itaendelea kumkumbuka marehemu Kanumba kutokana na ubora na uzuri wa kazi zake alizokuwa akifanya.

"Ushauri wako bado naufatisha. Waswahili husema rafiki wa kweli sio yule atakae kupa samaki ukiwa na njaa bali ni yule atakae kufundisha kuvua samaki ili kesho uweze kukidhi mahitaji yako hata ukiwa mwenyewe pia uweze kuambukiza ujuzi huo wengine. Ulinifunza vyema, nisingekua hapa umekua sababu kubwa ya hapa nilipo. Tutakukumbuka Daima na milele... 'Rest In Peace Teacher", amesema Ndauka.

Rose Ndauka ametoa hisia zake hizo kwa jamii ikiwa leo siku ya kumbukumbu ya kifo cha marehemu Steven Kanumba. Aliyekuwa nguli wa bongo 'movies' ndani na nchi na nje ya mipaka ya Tanzania.

Kuwa Mwanaume Halisi na Mwenye Nguvu Kunako Kwa Kutumia Products Hizi

$
0
0
Bidhaa original na zilizothibitishwa kiafya zinapatikana NATURAL BEAUTY PRODUCTS sasa zinapatikana kwa bei ya punguzo la %10. Bidhaa hizi zimetengenezwa kwa mimea na matunda hazina kemiko wala madhara yoyote. Hakikisha unapewa risiti original ya natural beauty production

TUNAZO KAMA HIZI

1.HANDSOME UP ORIGINAL_ Inaongeza uume kwa size uipendayo na kuimarisha misuli (wiki 2) @250,000/=

2.SHARK POWER GELY_ Inaongeza uume inch 6 (wiki 4) @150,000/=

3VigRX CREAM_ Inaongeza uume inch 6.5 hadi 8 (wiki 2-3) @200,000/=

4.Vidonge maalum vya kuongeza nguvu na hamu ya tendo hata kwa wenye kisukari na BP @170,000/=

5. MAXMAN 2-Hii ni vidonge vinavyoongeza nguvu za kiume pamoja na uume @240,000/=

6.VIGA SPRAY OG_ Inaongeza uwezo ktk tendo na kuchelewesha kufika kileleni @150,000/=

7.BODY BOOSTER_ Hii ni yakuongeza mwili pamoja na hamu ya kula vizuri @140,000/

8.DISCREET ORIGINAL_Hii ni dawa ya kuondoa mvi na zisiludi tena milele @150,000/= N.K

NB:Hakikisha unapata risiti yenye muhuri na garantii ili kukuhakikishia ubora na usalama wa bidhaa za NATURAL BEAUTY LTD

Wasiliana nasi Popote
ulipo duniani kwa (+255)
0659618585 au
0759029968

Twitter: Ina Watumiaji Wazungumzaji Sana Lakini Haitengenezi Pesa

$
0
0
Katika mitandao ya kijamii ambayo ni maarufu na inawatumiaji wenye mazungumzo mengi sana ni Twitter, lakini tatizo lake moja kubwa ni kwamba mtandao huu wa kijamii bado hautengenezi pesa za kutosha ukilinganisha na mitandao mingine ya kijamii.

Mtandao wa Twitter ingawa inavutia mazungumzo mbalimbali kuanzia ya kisiasa, kiutani, n.k yanayohusisha hadi watu mashuhuri kama Rais wa Marekani wa sasa, wasanii na watu wengine mashuhuri kwa wadogo bado mtandao huu unapata shida katika kuvutia makampuni kutumia pesa kujitangaza katika mtandao huo.

Mtandao wa Twitter bado upo nyuma katika kuvutia mapato yanayotokana na matangazo ukilinganisha na mitandao mingine kama vile Facebook na ata Instagram na Snapchat.

Katika ripoti ya mapato na ukuaji ya kampuni uya Twitter iliyotoka Alhamisi hii inaonesha bado mtandao wa kijamii wa Twitter unapata shida kukuza idadi ya watumiaji, matangazo na mapato.

Kwa mfano katika miezi mitatu ya mwisho ya mwaka 2016 Twitter ilikuwa na wastani ya watumiaji milioni 319 kwa mwezi, huu ni ukuaji wa asilimia 4 tuu ya watumiaji ukilinganisha na kipindi cha mwaka mmoja nyuma, pia namba hii ni ndogo ukilinganisha na mtandao wa Facebook. Facebook ina takribani wastani wa watumiaji bilioni 1.86 kwa mwezi.

Twitter wanategemea kupata mapato ya dola milioni 91 tuu katika kipindi cha miezi hii mitatu ya mwanzo, hii ni chini sana ukilinganisha na pato la dola milioni 191 ambalo wengi waletegemea wafikie.

Ingawa bado kibiashara mtandao huo upo katika hali ngumu ila ni uhakika bado hautaenda popote kwa sasa. Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Bwana Jack Dorsey anasema itaitaji muda mrefu kidogo na mabadiliko kadhaa ili kuweza kuona ukuaji wa watumiaji pamoja na mapato

Hapa Bungeni Wabunge Kama 100 ni Darasa la Saba – Mbunge Msukuma

$
0
0
Mbunge wa Geita Vijijni, (CCM) Joseph Msukuma ameitaka Serikali kuwarudisha kazini watumishi wa umma waliofukuzwa kwa kuwa wana elimu ya darasa la saba hadi watakapostaafu.


Msukuma ameyasema hayo ijumaa hii alipokuwa akichangia hotuba ya bajeti ya ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2018/19.

“Wabunge wenzangu, tuwatake Serikali wawarudishe kazini hadi hapo watakapostaafu. Hapa bungeni wabunge kama 100 hivi ni darasa la saba, wengine wamefeli, wengine wana vyeti feki,” amesema.

Amesema iwapo hawatawarejesha watumishi hao basi wawafukuze hata wabunge ambao wana elimu hiyo au wabunge hao warejeshwe kuwa wa viti maalum.

Baba mzazi wa Abdul Nondo Aishangaa Serikali Kuhoji Uraia wa Mtoto Wake...Afunguka Mazito

$
0
0

Baba mzazi wa Abdul Nondo amesema kuwa, anashangaa wanaohoji kuhusu uraia wa mwanae kwani Babu yake Nondo ni mzaliwa wa Ujiji, Kigoma na Muasisi wa TANU.

Asema, hana hofu sababu vyeti walivyoviomba vipo, lakini waelewe kuwa wao ndio Wamanyema halisi na ni raia wa nchi hii

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo


Download Upya Application Yetu ya UDAKU SPECIAL .....Ile Ya Zamani Tutaifuta

$
0
0
Mpendwa msomaji wetu, tunakukumbusha Kuidownload Upya Application yetu ya UDAKU SPECIAL Maana ile ya Zamani Tutaifuta.

Kuna Marekebisho Makubwa tumeyafanya ikiwa na tatizo la Notification kutatuliwa

NB: App mpya ina Icon Nyekundu

 Bonyeza Hapa Chini

==>>Unaweza Kuidownload << kwa Kubofya Hapa>>

Rais Magufuli Atoa Agizo kwa IGP Sirro

$
0
0
Rais Magufuli atoa agizo kwa IGP Sirro
Rais Dkt. John Magufuli amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro kuhakikisha inapofika kesho (Aprili 8, 2018) awe ameshawaingiza askari Polisi walionguliwa nyumba zao hapo awali katika nyumba mpya ambazo zimezinduliwa hii leo.


Dkt. Magufuli ametoa agizo hilo leo (Aprili 7, 2018) wakati alipokuwa anazungumza muda mchache alipomaliza kuzindua nyumba za askari zilizojengwa mkoani Arusha na kusema anawapa pole kwa majanga yaliyotokea ya kuunguliwa moto, huku akiwapongeza wadau mbali mbali waliojitolea kwa mioyo yao katika ujenzi wa nyumba hizo.

"Nimepata mawazo ni kitu gani tunaweza kufanya kuhusina na matatizo ya nyumba za Polisi, sasa ninachoomba Mhe. IGP wale walionguliwa nyumba, kesho waingie katika nyumba zao hizi mpya ambazo zimemalizwa kujengwa. Kwasababu najua muda mwingine wanaweza wakachomekwa Polisi wengine halafu waliokuwemo wakaambiwa hapana", amesema Dkt. Magufuli.

Pamoja na hayo, Rais Magufulia ameendelea kwa kusema "sasa nataka wale wale walionguliwa ndio waingie humo kwenye nyumba kwasababu Mungu aliwasaidia, moto ukaungua ungua kwa faida ya wao lakini hii inadhihirisha ni kwa namnagani makazi ya nyumba za polisi yalivyo kuwa mabovu".

Kwa upande mwingine, Rais Magufuli amesema maisha ya polisi anayafahamu vizuri kwa kuwa ndio zilizompa mke pamoja na kumtunzia.

Rwanda Kuwakamata Walemavu Ombaomba

$
0
0
Rwanda Kuwakamata Walemavu Ombaomba
Serikali ya Rwanda imetangaza kuwa kamata na kuwaweka gerezani walemavu wote wanaojihusisha na vitendo vya kuomba omba barabarani kwa madai kuwa ni chanzo cha uchafu mjini.

Uamuzi huo ambao unaweza kutekelezwa wakati wowote kuanzia sasa umewaonya walemavu hao kuwa kama hawatositisha shughuli uombaji, watatiwa ndani.
Kwa upande wa walemavu wamepokea umamuzi huo kwa shingo upande huku baadhi ya raia wakisema kwamba uamuzi huo umekuja kwa lengo la kukandamiza walemavu na watu maskini.

Serikali Yawapa Siku 23 Wamiliki wa Nyumba

$
0
0
Serikali Yawapa Siku 23 Wamiliki wa Nyumba
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema serikali itawafikisha Mahakamani na kuwafutia hati ya umiliki wananchi wote wanaomiliki ardhi ambao wamekuwa hawalipi kodi ya ardhi.


Lukuvi ametoa kauli hiyo mara baada ya kupokea taarifa mbalimbali kutoka kwa watendaji wake ambapo amesema serikali inapoteza mapato mengi kwa kuwa baadhi ya wananchi kukosa uaminifu wa kulipa kodi ya ardhi kwa wakati.

Kutokana na hali hiyo, Waziri Lukuvi amesema ameamua kutoa muda hadi Aprili 30, 2018 ili kila mtu anayemiliki ardhi awe amekwisha lipa kodi hiyo na kwa wale ambao hawatalipa kodi kwa wakati ni wazi serikali itawafikisha mahakamani, kuwafutia hati za viwanja hivyo na kuviuza upya kwa wamiliki wengine ama kuuza nyumba zao.

Aidha Mhe. Lukuvi amewataka wafanyakazi wa wizara hiyo kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika zoezi hilo ili kupunguza ukubwa wa kazi na kukusanya fedha kwa wakati na kuongeza pato la taifa.

Rais Magufuli Atoboa Siri Alipokutana na Mkewe "Nyumba za Kota za Polisi Zimenipa Mke Janeth’'

$
0
0
Rais Magufuli Atoboa Siri Alipokutana na Mkewe "Nyumba za Kota za Polisi Zimenipa Mke Janeth’'
“Nyumba za polisi ndizo zimenipa mke kwa hiyo nyumba za polisi ninazifahamu, huyu mke wangu niliye naye alikuwa mtoto wa polisi, marehemu baba yake hakuwa na cheo kikubwa alifariki akiwa sajenti,” ni maneno ya Rais Magufuli akizindua nyumba za askari Arusha nakukiri kuwa Janeth alimpata kwenye nyumba za kota.

Ameyazungumza hayo leo April 7, 2018 wakati wa uzinduzi wa nyumba 31 za polisi na kusema baba mkwe wake alikuwa sajenti wa polisi.

“Nyumba za polisi ndizo zimenipa mke kwa hiyo nyumba za polisi ninazifahamu, huyu mke wangu niliye naye alikuwa mtoto wa polisi, marehemu baba yake hakuwa na cheo kikubwa alifariki akiwa sajenti,” -Rais Magufuli

 “Ingekuwa nazindua Moshi, angenionyesha nyumba walizokaa lakini za Oysterbay alizoishi alishanionyesha na za Ukonga na za sehemu nyingine. Kwa hiyo maisha ya polisi ninayafahamu.” -Rais Magufuli
Viewing all 104747 articles
Browse latest View live




Latest Images