Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live

Chirwa kuivaa Simba Aprili 29

$
0
0
Chirwa kuivaa Simba Aprili 29
Straika wa Yanga, Obrey Chirwa alienda kwao Zambia kutokana na matatizo ya kifamilia, sasa uongozi wa klabu hiyo umesema mchezaji huyo anarudi muda wowote kuanzia sasa kujiandaa na mchezo dhidi ya Simba.

Chirwa hatacheza mechi ya leo ya Yanga dhidi ya Wolayta Dicha ya Ethiopia ya kuwania kufuzu kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwani ana kadi mbili za njano, hivyo kwa mujibu wa kanuni hatocheza.

Chirwa alipata kadi hizo katika mechi mbili za Ligi ya Mabingwa dhidi ya Township Rollers ya Boswana.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten alisema kuwa, Chirwa atarejea baada ya wiki moja ili kuwahi maandalizi ya mechi dhidi ya Simba itakayochezwa Aprili 29, mwaka huu.

“Chirwa aliondoka kwa ruhusa ya wiki moja kwenda nyumbani kwao kutokana na kuwa na matatizo ya kifamilia, hatutarajii akae sana huko kwa kuwa anatakiwa awahi kurudi kwa ajili ya maandalizi ya mechi yetu dhidi ya Simba,” alisema Ten. Chirwa ana mabao 12 kwenye Ligi Kuu Bara, na amekuwa msaada mkubwa kwa Yanga kutokana na uhodari wake wa kuzifumania nyavu.

Raiola Asema Guardiola ni Muongo

$
0
0
Raiola asema Guardiola ni muongo
Wakala wa kiungo wa Manchester United Paul Pogba Mino Raiola amesema alichosema kocha wa Manchester City Pep Guardiola kuwa Pogba alitaka kuuzwa kwenye usajili wa Januari si kweli.


''Sijawahi kuzungumza na Guardiola kuhusu mchezaji yeyote aliyechini yangu, si Pogba wala Mkhitaryan, hata Man City kama klabu sijawahi kuongea nayo lakini naiheshimu ni timu bora na ina kocha bora'', amesema.

Jana kwenye mkutano na wanahabari kuelekea mchezo wa 'Derby' ya jiji la Manchester, Guardiola alisema kuwa Pogba alitaka kuuzwa Manchester City kwenye dirisha dogo la janauri kitu ambacho kimepingwa vikali na nyota huyo wa Ufaransa.



Kwa upande wake Pogba kupitia ukurasa wake wa mtandao wa 'Twitter' ameeleza kushangazwa na alichosema Guardiola kwani hajawahi kuongelea suala hilo hata siku moja.

Mchezo wa leo ambao utapigwa kwenye uwanja wa Etihad nyumbani kwa Man City, unaweza kuamua bingwa endapo wenyeji watashinda basi wataibuka mabingwa wapya wa EPL msimu wa 2018/1

Madiwani Dar Walia na Itikadi za Kisiasa Kuwakwamisha Katika Maendeleo

$
0
0
Madiwani Dar Walia na Itikadi za Kisiasa Kuwakwamisha Katika Maendeleo
Vitendo vya kuingiza itikadi za kisiasa vinavyofanywa na baadhi ya madiwani wa vyama mbalimbali jijini Dar es Salaam, vinadaiwa kukwamisha juhudi za maendeleo na huduma za kijamii kwa wananchi.

Wakijadiliana katika semina iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), baadhi ya madiwani wa mkoa huo walisema itikadi hizo zimegeuka kuwa mwiba wa maendeleo.

Diwani wa viti maalumu kutoka Ubungo, Rehema Mayunga alisema linapokuja suala la kuwaletea maendeleo wananchi kila mmoja anapaswa kushirikiana na mwenzake.

Diwani wa Kivule, Wilson Molel alisema suala la kuingiza siasa katika kila jambo la maendeleo linachelewesha na kukwamisha miradi mingi, lakini waathirika ni wananchi.

Ofisa programu na uchechemuzi wa TGNP, Deogratius Temba aliwaomba madiwani kuhakikisha mikutano ya kisheria inafanyika kwa wakati na kuweka kwenye mbao za matangazo maazimio ya Serikali za vijiji na mitaa, mapato na matumizi ya fedha za umma.

Rosa Ree Ajisogeza Kufanya Kolabo na Wanigeria

$
0
0
Rosa Ree Ajisogeza Kufanya Kolabo na  Wanigeria
Baada ya kurekodi na rapper Emtee kutoka nchini Afrika Kusini Emtee, Rosa Ree ameweka wazi mipango yake ya kufanya kolabo na wasanii wa Afrika.

Rapper huyo ambaye kwa sasa yupo Nigeria amesema hata nchini humo kuna uwezekana akafanya kazi na baadhi ya wasanii.

“Hata hapa pia nina mpango wa kukutana na wasanii fulani ni kwa sababu tunajuana kupitia watu wengine” amesema.

Kuhusu idadi ya kolabo za kimataifa amesema, “The so many lakini at least nimeweka moja wazi, mkae mkao wa kula na huku pia tunaomba tutarudi na kitu kikubwa,”.

Kolabo ya Emtee na Rosa Ree ikitoka itamfanya kufikisha kolabo mbili na rapper wa kiume baada ya ile aliyofanya na Khalighraph Jones kutokea nchini Kenya.

Bombadier Yamtoa Povu Mbunge

$
0
0
Bombadier Yamtoa Povu Mbunge
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Rukwa, Aida Joseph Kenan amehoji bungeni mjini Dodoma kuhusu ununuzi wa ndege mpya ya Bombadier Q400 aliyoipokea Mhe. Rais Magufuli hivi karibuni, iwapo ndicho kipaumbele cha taifa la Tanzania

Mhe. Aida amesema kwamba ingekuwa vyema kama serikali ingenunua meli na kuzitawanya sehemu mbalimbali nchini kwani wananchi wengi wa hali ya chini waliopo vijijini wanatumia meli katika kusafirisha mazao na shughuli zao zingine na hawana uwezo wa kupanda ndege.

Aidha, amewataka mawaziri kumshauri Rais na Bunge kuisimamia serikali kwa ajili ya manufaa ya Watanzania wote.

Kwangu Bado Kila Siku ni Msiba Japo Kila Nafsi Itaonya Mauti- Mama Kanumba

$
0
0
Kwangu Bado Kila Siku ni Msiba Japo Kila Nafsi Itaonya Mauti- Mama KanumbaWadau wa tasnia ya filamu na familia ya marehemu Steven Kanumba, leo wanaadhimisha miaka sita tangu kufa kwa msaanii huyo.

Mama yake Flora Mtegoa, amesema yeye kwake msiba huo bado upo kila siku na kudai kila nafsi itaonja mauti.

Mtegoa ameyasema hayo leo Aprili 7 katika makaburi ya Kinondoni ambapo walifanya ibada fupi kwa ajili kumbukumbu hiyo akiwa na baadhi ya wasanii hususani wa kikundi cha Soweto ambao ndio wameisimamia shughuli hiyo kwa mwaka huu.

Amesema pamoja na kujitokeza kwa wasanii wachache ambao waliwahi kufaya kazi na mtoto wake enzi za uhai wake anaamini ni kutokana na wao kuona wameshamaliza msiba, lakini kwake upo kila siku na kamwe hauwezi kufutika mpaka mwisho wa uhai wake.

"Ni kweli idadi ya wasanii maarufu waliokuja hapa ni wachache ukilinganisha na namna Kanumba alivyoishi nao, lakini ndio hivyo huwezi kuwalazimisha na isitoshe wao labda wanaona wamemaliza msiba lakini kwangu bado upo ila ninachowaombea yasije yakawakuta kama haya ndio watajua nini namaanisha,’’ amesema Mama Kanumba.

Wito wake kwa wasanii Mama Kanumba amewashauri kuwa na upendo kauli ambayo Kanumba alikuwa anapenda kuisema enzi za uhai wake.

Kwa upande wake Emmanuel Myamba, mmoja wa wasanii maarufu aliyeshiriki ibada hiyo, amesema kwake Kanumba atabaki kuwa moyoni kwa kuwa ana mchango mkubwa katika sanaa yake na ndiye aliyemfanya ajulikane kwenye filamu.

Kwa ambao hawajahudhuria amesema labda wametingwa na ratiba zao na pia kushiriki jambo kama hilo inatokana na mtu mwenyewe kuguswa.

Keita Nestory, mwalimu wa kikundi cha Soweto, amesema wameamua kuibeba shughuli hiyo mwaka huu kwa kutambua mchango wa Kanumba kama mlezi wao, enzi za uhai wake.

"Kwa kweli tuna-umiss ushauri wa Kanumba, enzi za uhai wake alikuwa ana mchango mkubwa sana kwetu ukizingatia ni kikundi ambacho kilikuwa bado hakina jina," amesema Nestory.

Gambo Amuahidi Rais Magufuli Kupambana na Vita ya Uchumi "Nitakuwa wa Mwisho Kufa"

$
0
0
Gambo Amuahidi Rais Magufuli Kupambana na Vita ya Uchumi "Nitakuwa wa Mwisho Kufa"
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amemwambia Rais John Magufuli kuwa atakuwa naye hadi atakapokufa, akimsaidia katika vita ya kiuchumi.

Gambo ameyasema hayo leo Aprili 7 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha wakati Rais Magufuli alipokuwa akizungumza na wananchi baada ya kuzindua kituo cha polisi na nyumba 31 za polisi.

“Nikuhakikishie kuwa nitakuwa mtu wa mwisho kufa hadi vita uliyoanzisha inafikia mwisho,”amesema.

Gambo amesema kuna watu ambao wanakwamisha kwa makusudi juhudi za Rais na wanataka viongozi wengine wasimpe ushirikiano na hivyo akasema yeye atakuwa pamoja na Rais Magufuli mpaka mwisho.

“Nia yao ni kuona tunakuacha peke yako, lakini hatutafanya hivyo, tutakuwa na wewe katika vita hii mpaka mwisho,” amesema.

Pia, amesema wapinzani wamekuwa wakilalamikia mambo mengi ikiwamo suala la ndege, lakini ndege imekuja na bado wanasema.

“Umeleta ndege sita, sasa wanalalamika mbona umenunua hii na kuacha kile. Hawa ni popo siyo ndege wala wanyama hivyo usihangaike nao,” amesema na kuongeza:

“Wapinzani wangependa wote tukate tamaa ili ubaki peke yako, mimi kama msaidizi wako nakuhakikishia nitakuwa wa mwisho kufa katika vita hii.”

Wambura Apinga Maamuzi Yaliyotolewa na Kamati ya Rufaa TFF

$
0
0
Wambura Apinga Maamuzi Yaliyotolewa na Kamati ya Rufaa TFF
Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)  Michael Richard Wambura amesema hajakubaliana na maamuzi yaliyochukuliwa na kamati ya rufaa ya maadili ambayo imetupilia mbali rufaa yake hapo jana.


Akiongea leo na wanahabari, Wambura amesema kuwa kamati iliyopitia rufaa yake na kutoa maamuzi jana haina uhalali na wala sio huru hivyo maamuzi yake yameegemea kulinda maslahi ya upande wa walalamikiwa ambao ni TFF.

Aidha Wambura amesema kamati hiyo haijatoa haki ya kumsikiliza mlalamikaji badala yake kamati imesimama kama chombo cha kupitia malalamiko kisha kumtetea mlalamikiwa hivyo anaamini majibu yaliyotolewa hayana mtazamo wa kamati huru.

Kamati hiyo jana ilitangaza kutobadili maamuzi ya kamati ya nidhamu ambayo yalitolewa Machi 15 ya kumfungia Wambura kutojihusisha na soka maisha, adhabu ambayo imekuwa ikipingwa na Wambura mara kwa mara.

Makosa matatu ambayo yamesababisha kufungiwa maisha kwa Wambura ni kupokea fedha za shirikisho malipo yasiyo halali, kugushi barua na kushusha hadhi ya Shirikisho.



Nguvu ya Pesa Yamtoa Katika Kifungo cha Miaka Mitano Salman Khan.... Akaa Jela Siku Mbili Apewa Dhamana"

$
0
0
Nguvu ya Pesa Yamtoa Katika Kifungo cha Miaka Mitano Salman Khan.... Akaa Jela Siku Mbili Apewa Dhamana"
Siku mbili baada ya Mahakama nchini India kutoa hukumu ya miaka mitano kwa Staa wa filamu nchini India Salman Khan kwa kosa la ujangili mwaka 1998, staa huyo ameachiwa huru kwa dhamana.

Khan ameachiwa huru kwa dhamana baada ya kukata rufaa, ikiwa ni siku mbili baada ya kulala jela na mahakama kumwamuru alipe faini ya Dola za Marekani 154 sawa na takriban Shilingi za Kitanzania 369, 600.

Khan anadaiwa kuua swala wawili wa aina ya ‘blackbucks‘ ambayo hulindwa sana nchini humo. Alifanya kosa hilo katika mji wa Rajasthan wakati wakitengeneza filamu.

Inasikitisha Mchungaji Aangu kana Kufa Madhabauni

$
0
0
Inasikitisha Mchungaji Aangu kana Kufa   Madhabauni
Waumini wa kanisa la Katoliki katika Dayosisi ya Jimbo la Bungoma nchini Kenya, wako kwenye maombolezo baada ya mchungaji wao kuanguka na kufa papo hapo akiwa madhabahuni.

Kwa mujibu wa Askofu Mkuu wa Jimbo hilo la Bungoma, Norman Kong’oo Wambua, marehemu alianguka majira ya saa 8 mchana katika kanisa la Mabanga ma dakika chache mbele akatangazwa kuwa ameshafariki.

Inaelezwa kuwa kiongozi huyo alikuwa na maradhi ya figo ambayo wanahisi ndio yaliyosababisha kifo chake cha ghafla. Mwili umekwisha hifadhiwa mortuary ukisubiri kufanyiwa uchunguzi.

JPM Apiga Stop Askari Kufyeka Mashamba ya Bangi "Kamata Kijiji Kizima Wafyeke Mpaka Atakapotajwa Muhusika"

$
0
0
JPM Apiga Stop Askari Kufyeka Mashamba ya Bangi "Kamata Kijiji Kizima Wafyeke Mpaka Atakapotajwa Muhusika"
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemuagiza IGP, Simon Sirro kutowaagiza Polisi kufyeka mashamba ya bangi badala yake watumie nji za intelijensia kuwakamata wahusika na ikishindikana wakamate kijiji kizima wafyeke hiyo bangi mapaka atakapo tajwa muhusika.

Rais Magufuli ameyasema hayo wakati wa Uzinduzi wa nyumba za Jeshi la Polisi mkoani Arusha ambapo amesema hilo ndio jambo linalomkera.

“IGP mimi kuna kitu kinaniudhi jinsi polisi wanavyoenda kukata bangi hamkuajiriwa kukata bangi, kama bangi iko kijiji fulani shika kijiji kizima wazee na wakina mama wakafyeke bangi,” amesema Rais Magufuli.

“Askari wasiende kufyeka bangi. Hawakuajiriwa kufyeka bangi, usiwatume Maaskari wako kufyeka bangi, mtaumwa nyoka mle mna uniform nzuri, msidhalilishe jeshi kwa kufyeka bangi.”

Gambo Amtoa Hofu Rais Kuhusu Maandamano"Mh Usitishwe na Mbwebwe za Mitandaoni"

$
0
0
Gambo Amtoa Hofu Rais Kuhusu Maandamano"Mh Usitishwe na Mbwebwe za Mitandaoni"
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho gambo amemtaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kutotishwa na mambo ya mitandaoni, kwani mkoa wa Arusha uko salama.


Mrisho Gambo ameyasema hayo leo alipokuwa akitoa salam zake kwa Rais Magufuli, kwenye sherehe za uzinduzi wa nyumba za polisi mkoani Arusha, kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abedi.

Kwenye salamu hizo Mrisho Gambo amesema mkoa wa Arusha ni salama na wakazi wa Arusha hawana haja ya maandamano, kwani wanachohitaji ni uongozi wake ambao unawaletea maendeleo makubwa.

Mrisho gambo aliendelea kwa kueleza kuwa anatambua kazi ya kubwa aliyonayo Rais ya kupigana vita ya uchumi, na watu wengi wasiopenda nchi hii watachukia kutokana na hilo.

“Mheshimiwa Rais nikuhakikishie tu Arusha ni salama, wala usitishwe na mbwembwe za kwenye mitandao, watanzania halisi ni hawa hapa wenye Arusha yao. Watanzania wa Arusha wamechoka na maandamano, wanataka uongozi wa kwako ambao unawaletea maendeleo. Ninajua vita uliyokuwa nayo ni kubwa sana, Mwl. Nyerere alikuwa na vita ya ukombozi, akaimaliza salama, Mheshimiwa Rais vita yako wewe ni ya kiuchumi, ni vita inayopigana na mabeberu ambao wanawatumia wengine kukwamisha jitihada zako. Watu wengi ambao hawaitakii mema nchi hii hawawezi kuipenda”, amesema Mrisho Gambo.

Sambamba na hilo Mkuu wa mkoa huyo wa Arusha amemshukuru Rais Magufuli na wadau kwa kufanikisha ujenzi wa nyumba hizo za askari polisi, ambazo awali ziliteketea kwa moto.

Mwanafunzi Aamriwa Kubandika Bandeji Kwenye Chuchu Baada ya Kuwachanganya Wanafunzi

$
0
0

FLORIDA, MAREKANI: Uongozi wa shule moja ulimuagiza mwanafunzi mmoja(17) ambaye hakuvaa sidiria kufunika chuchu zake kwani alikuwa akiwachanganya wanafunzi wengine

Mwanafunzi huyo aliyefahamika kwa jina la Lizzy Martinez hakuvaa sidiria ila alivaa blauzi yenye mikono mirefu

Lizzy alisema alihisi kama wanafunzi wenzake walikuwa wakimghasi lakini mshauri wa wanafunzi akamuambia alikuwa akiwachanganya kutokana na alivyovyaa

Lizzy aliagizwa kuvaa shati jingine juu ya blauzi aliyokuwa amevaa na kisha akaagizwa kwenda kwa nesi na kupewa bandeji ambazo aliambiwa abandike kwenye chuchu zake

Kitendo cha Lizzy kupewa nguo nyingine na kisha bandeji apandike kwenye chuchu zake kilimfanya ajihisi anadhalilishwa na kumfanya atokwe machozi

VIDEO:Rihama Amwaga Chozi kwa Uchungu Ataka Waandaaji wa Tuzo za Sinema Zetu Wamuombe Radhi

$
0
0
VIDEO:Rihama Amwaga Chozi kwa  Uchungu Ataka Waandaaji wa Tuzo za Sinema Zetu Wamuombe Radhi
Muigizaji Nguli wa filamu za Kibongo Rihama Ali amejikuta akitokwa na machozi na kulia kwa uchungu live wakati akihojiwa kwenye kipindi cha XXL kinachorushwa na clouds baada ya kupata matusi na kuzarauliwa na mashabiki zake baada ya kukosa tuzo hizo.

 Rihama amesema  kitendo walichomfanyia waandaaji wa Tuzo za  hizo akikumfurahisha na hatokisahau maishani mwake kwakua heshima inashuka wakati hakuhusishwa katika tuzo hizo toka zinaanza matokeo yake wanaamua kuandaa shindano kwa lengo la kumshusha heshima.

"Nimeumia sana sana lengo lao ni kunishushia heshima mimi sikujua lolote linaloendelea chakushangaza naambulia matusi kutoka kwa mashabiki zangu mimi Tamko langu nataka waniombe Radhi sivyo wasinihusishe kwenye tuzo zao na hata wasije kunipa tuzo ya heshima hata nitakapokufa' alisema Rihama

' Hata kama walikua na mambo yao wangefanya bila ya kunihusisha mimi' mimi ni brand ambassader wao wanataka kuniharibia kazi yangu mimi sideal na mtu kwanini wanataka kunizibia riziki yangu  kazi yangu ndo inanisaidia kulea familia yangu nimeumia na hili kovu halitakuja kufutika na linaweza kunivunja moyo nikaona makubwa niliyofanya si kitu na kama hawataniomba radhi wasiniusishe milele

IGP Sirro Awatumia Ujumbe Mzito Wanaotaka Kuandamana

$
0
0
IGP Sirro Awatumia Ujumbe Mzito Wanaotaka Kuandamana
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro amesema Jeshi lake liko imara kweli kweli katika kupambana na watu wanaotaka kuleta uvunjifu wa amani nchini, huku akiwasii wanaotaka kuandamana kuacha mara moja kwani kitakachowapata wasije kulaumiana


IGP Sirro ametoa kauli hiyo leo (Aprili 7, 2018) wakati akitoa salamu zake kwa Rais Dkt. Magufuli katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid uliopo mjini Arusha baada ya uzinduzi wa nyumba za askari na kushuhudia maonesho ya utayari ya jeshi hilo katika kukabiliana na uhalifu.

"Mhe. Rais Magufuli Jeshi lako Polisi liko imara tena imara kweli kweli, kwa kupambana na watu wote wanaotaka kuleta uvunjifu wa amani hapa nchini na kwa bahati nzuri wananchi wapo pamoja na wewe Rais na Jeshi lako. ila naomba nitoe ushauri wa bure kwa wale wote wenye nia ya kuchafua amani ya nchi yetu , ni wasii waache mara moja na kama wataona ushauri huo hauna maana basi baadae tusilaumiane", amesema IGP Sirro.

Pamoja na hayo, IGP Sirro ameendelea kwa kusema "upo uhamasishaji kwenye mitandao, na hili niseme  naamini wameshaandamana kwenye mitandao na wameshamaliza maandamano yao. Kwa hiyo la msingi sana tujenge nchi yetu".

Kwa upande mwingine, IGP Sirro amesema katika kipindi cha mwezi Januari hadi Februari mwaka 2018 kuna jumla ya matukio ya jinai yaliyoripotiwa ni 96,363 ikilinganishwa na matukio 104,073 yaliyoripotiwa kipindi kama hicho mwaka 2017.

Rais Magufuli Ametangaza Ajira Mpya 1,500 kwa Askari Polisi.... Ameahidi Kutoa Bilioni 10

$
0
0
Rais Magufuli Ametangaza Ajira Mpya 1,500 kwa Askari Polisi.... Ameahidi Kutoa Bilioni 10
Leo April 7, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli akiwa katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid ameahidi kutoa BILIONI 10 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za Maaskari wa vyeo vya chini.

“Mimi nimeoa kambini, mke wangu ni mtoto wa Askari Polisi, kwahiyo maisha ya askari wa chini nayatambua, leo nitatoa bilioni 10 ili zikasaidie kujenga nyumba za maaskari na hizi nyumba ziwe za maaskari wa chini”– Rais Magufuli

Dangote Awakosoa Maofisa Kenya

$
0
0
Dangote awakosoa maofisa Kenya
Mfanyabiashara anayeshika nafasi ya kwanza kwa utajiri barani Afrika, Aliko Dangote amekosoa utawala wa Kenya kwa ubinafsi wao na kuendelea kushindwa kuweka mbele masuala yenye maslahi kwa taifa linapokuja suala la maendeleo.

Akizungumza katika mahojiano na mwandishi mashuhuri wa Kenya Jeff Koinange, Dangote alisema alifuta mipango ya kujenga kiwanda kikubwa cha saruji baada ya kukatishwa tamaa na watoa maamuzi ambao aliwaita ni “mafisadi kuliko Wanigeria.”

Akizungumza katika kipindi cha alfajiri cha studio za redio FM, Jeff alielezea mazungumzo binafsi aliyofanya na Dangote alipohudhuria hafla iliyoandaliwa na bilionea huyo kwa ajili ya kumuaga binti yake mwezi uliopita nchini Nigeria.

“Nilimuuliza, ‘Al Hajj lini utakuja tena Kenya?’ na yeye alisema ‘Jeff, kuna watu wako kule (Kenya) ambao wametanguliza ubinafsi wao na maslahi binafsi kuliko ya taifa. Sikuwahi kufikiria Kenya ingekuwa imekubuhu kwa rushwa kuliko Nigeria,’” alielezea Koinange.

Dangote, anayekadiriwa kuwa na utajiri unaofikia Shilingi za Kenya 1.5 trilioni kwa utafiti wa jarida la Forbes, alitembelea Kenya Septemba 2013 katika msafara wa wafanyabiashara matajiri 50 kutoka Nigeria walioongozana na rais wa wakati huo Goodluck Jonathan.

Tajiri huyo wa Nigeria hivi karibuni alisogeza hadi mwaka 2021 kuleta kiwanda chake nchini baadala ya mwaka ujao.

Dangote anafahamika kwa kupanga bei ya chini ili kudhibiti soko jipya na hatua ya kusogeza mbele itawapa nafuu wafanyabiashara wengine katika soko hilo ambalo linashuhudia ushindani mkali.

Watekaji Wamwachia Huru Padri Baada ya Kulipwa Bilioni Moja

$
0
0
Watekaji wamwachia huru Padri baada ya kulipwa Bilioni Moja
Jumapili ya Pasaka April 1, 2018 Padri wa kanisa moja la Katoliki nchini Congo alitekwa na wanaume ambao walikuwa na silaha ambao waliomba kupewa Dola za Marekani 500,000 sawa na Shilingi bilioni 1.2 ili wamwachie huru.

Jana April 6, 2018 watekeaji hao walimwachia huru Pardi huyo Celestin Ngango baada ya kupewa pesa hizo, lakini inaripotiwa kuwa watu wengine watatu waliokuwa pia wametekwa kuwa wameuawa.

Kwa mujibu wa Kituo cha Utafiti cha Kukuza Amani, Demokrasia na Haki za Binadamu CEPADHO Padri Ngango ni mmoja kati ya watu 10 ambao waliotekwa nyara katika wilaya ya Rutshuru.

Rais Magufuli Aukumbuka Wimbo wa 'WAPO wa Ney wa Mitego

$
0
0
Rais Magufuli Aukumbuka Wimbo wa 'WAPO wa Ney wa Mitego
Rais John Magufuli ameukumbuka wimbo wa Ney wa Mitego wa ‘Wapo’ ambao ulifungiwa na baadaye kuagiza ufunguliwe.

Tukio hilo limetokea leo Aprili 7, alipokuwa akimaliza kuhutubia katika uzinduzi wa Kituo cha Polisi cha Utalii na Diplomasia mjini Arusha kitakachosaidia kutoa huduma kwa watalii na maofisa wa kibalozi.

Hafla hiyo imekwenda sambamba na uzinduzi wa nyumba 31 za polisi, ambapo wageni mbalimbali walihudhuria wakiwemo wakuu wa polisi wastaafu.

Hata hivyo, katika kutaka kuwataja mmoja mmoja waliohudhuria, Rais Magufuli alijikuta akitaja baadhi ya majina na kuongeza neno yupo na baadaye kusema kuwa angekuwa msanii angeimba ule wimbo wa ‘Wapo’, maneno yaliyosababisha umati uliohudhuria shughuli hiyo kushangalia.

Machi 26, mwaka jana wimbo huo wa Ney ulifungiwa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), uliodaiwa kuwa ulimkashifu Rais.

Hata hivyo siku inayofuata, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe alitangaza kuufungulia, agizo ambalo alidai limetoka kwa Rais.

Kwa mujibu wa Dk Mwakyembe, Rais alifurahishwa na ‘Wapo’ huku akimshauri mwanamuziki huo kutaja majina ya watu wengine kwenye wimbo huo kama vile wakwepa kodi, wauza unga, wabwia unga na watu wengine wasiokuwa na maadili.

Mbali ya kufungiwa wimbo, pia Ney alijikuta akikamatwa na Jeshi la Polisi akiwa mjini Morogoro ambapo nao waliamuriwa kumwachia huru.

VIDEO:Yanga ilivyoifunga 2-0 Waloitta ya Ethiopia leo

$
0
0
Yanga wakiwa nyumbani watimiza matarajio ya wengi ya kupata ushindi dhidi ya Wolaitta ambao wanaonekana wageni katika michuano hii na ndio mara yao ya kwanza kushiriki hatua hii, kitu ambacho kimeisaidia Yanga kupata ushindi wa magoli 2-0  ambayo yamefungwa na Rafael Daudi dakika ya 1 na Emmanuel Martin dakika ya 54.

VIDEO:

Viewing all 104709 articles
Browse latest View live




Latest Images