Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104414 articles
Browse latest View live

Video: Nape Nnauye Aitolea Povu Serikali “Hii Sio Sawa Serikali Mmetusaliti”

0
0
“Hii Sio Sawa Serikali Mmetusaliti” –Nape Nnauye
Mbunge wa Mtama Nape Nnauye ameilalamikia Serikali Bungeni kwamba imekuwa ikiwasaliti wananchi wa mikoa ya kusini ikiwemo Lindi na Mtwara kwa kushindwa kuwasaidia katika kuboresha kilimo cha korosho na mbaazi na kusababisha hali mbaya ya kiuchumi kwa wakulima wa mazao hayo ikiwa wakati wa kampeni moja ya ushawishi wao ilikuwa ni kuwasaidia wakulima hao.

Nape amesema…>>>“Ukiacha gesi na mafuta, Lindi na mtwara ni korosho lakini Serikali ilichukua mfuko wa pembejeo. Kulikuw ana mapungufu yalitokea tukaacha kwakuwa ilikuwa ni mara ya kwanza lakini hali ilivyo sasa ni mbaya sana sana ”

“Tumaini pekee lililokuwa limebaki kusini ni korosho, mnajua mbaazi imekwenda kutoka Shilingi 2000 hadi 100 jamani sio sawa kabisa. Mnataka tuende wapi? Tulipotoa kura tuliamini mtatusaidia lakini imekuwa tofauti” –Nape Nnauye



Tanzia: Mke wa Mfalme Mswati Ajiua

0
0
Tanzia: Mke wa Mfalme Mswati Ajiua



Mke wa nane wa Mfalme Mswati wa Swaziland Senteni Masango, amejiua Ijumaa ya wiki iliyopita, wa kunywa dawa za vidonge aina ya amytriptyline, ambazo ndizo zilizoondoa uhai wake.

Malkia huyo amejiua wiki moja baada ya kuhudhuria mazishi ya dada yake Nombuso Masango, ambapo tetesi zinasema kwamba Mfalme alimkataza kuhudhuria mazishi hayo.

Habari zaidi zinasema kwamba mke huyo ambaye aliolewa mwaka 1999 na kuwa mke wa 8 wa Mfalme Mswati, alikuwa akiishi kwenye kasri ya Kifalme peke yake kwa takriban miaka mitatu, bila kutembelewa na mume wake huyo.

Tayari Malkia huyo wa Swaziland ambaye alikuwa miongoni mwa wake vipenzi wa Mfalme Mswati amezikwa kwenye eneo la kifalme la Swaziland, huku Mfalme Mswati akiendelea kupokea salamu za pole kwa viongozi mbali mbali wa serikai.

Habari zinasema kwamba Mfalme Mswati alishawahi kukimbiwa na wake wawili kwa tuhuma za unyanyasaji, huku wengine akiwapa adhabu kali ikiwemo kutengwa na kasri ya Kifalme.

TMA Yatoa Tahadhari kwa Wananchi Kuhusu Mvua Zinazoendelea Kunyesha

0
0
TMA Yatoa Tahadhari kwa Wananchi Kuhusu Mvua Zinazoendelea KunyeshaMamlaka ya hali ya hewa iliyopo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano nchini Tanzania imewatahadharisha wananchi kuwepo kwa vipindi vifupi vya mvua kubwa katika baadhi ya mikoa ya Tanzania kuanzia leo usiku Aprili 09, 2018.


Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa na mamlaka hiyo jioni ya leo (Jumatatu) na kudai kutakuwepo na upepo unaotarajiwa kuvuma kutoka Kusini- Mashariki kwa kasi ya Km 20 kwa saa kwa Pwani yote huku hali ya bahari inatarajiwa kuwa na mawimbi madogo

Kwa taarifa kamili angalia hapa chini.

Uhamiaji Yafafanua Sababu za Kudai Vyeti vya Kuzaliwa Vya Wazazi wa Nondo

0
0
Uhamiaji Yafafanua Sababu za Kudai Vyeti vya Kuzaliwa Vya Wazazi wa Nondo
Idara ya Uhamiaji imesema Watanzania wote waliozaliwa kuanzia mwaka 1978 wanapaswa kuwa na cheti cha kuzaliwa.

Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam, Crispin Ngonyani amesema hayo leo Jumatatu Aprili 9, 2018 alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

Ngonyani amesema hayo alipotoa ufafanuzi kuhusu maagizo yaliyotolewa na Uhamiaji kwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Abdul Nondo ya kuwasilisha vyeti vya kuzaliwa vya wazazi wake, babu na bibi zake linavyoweza kutekelezwa.

"Tulimweleza Nondo na mwanasheria wake kuwa, kama hawana vyeti vya kuzaliwa wanaweza kuleta affidavit (hati ya kiapo) na hilo tulikubaliana," amesema Ngonyani.

Amesema, "Lakini kama mtu umezaliwa kuanzia mwaka 1978 kwa sheria yetu lazima uwe na cheti cha kuzaliwa na tukikuomba utapaswa kutuonyesha kwa hiyo wananchi wanapaswa kulijua hili."

Nondo ambaye ni mwenyekiti wa Umoja wa Wanafunzi Tanzania (TSNP) alihojiwa Aprili 5, 2018 kuhusu uraia wake na ametakiwa kupeleka vielelezo kuthibitisha uraia wake vikiwamo vyeti vya wazazi, bibi na babu wa pande zote

Bwege‘’ Akanusha Bungeni, Asapoti Waraka Wa Maskofu .

0
0
Bwege‘’ Akanusha Bungeni, Asapoti Waraka Wa Maskofu .
MBUNGE wa Kilwa Kusini, Said Bungara (CUF) maarufu kama ‘Bwege’, amesema hakubaliani na kipengele kilichopo kwenye hotuba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, kinachoeleza kuwa nchi yetu ina amani sana.



Bungara amesema hakubaliani na kipengele hicho kutokana na matukio mawili yaliyotokea jimboni kwake; tukio la msikiti kuvamiwa na mtu mmoja kupoteza maisha na mwingine kubaki na ulemavu wa macho, huku tukio lingine ni la vijana kuchukuliwa katika mazingira ya kutatanisha na watu wanaodaiwa kuwa ni polisi ambapo mpaka leo watu wawili hawajajulikana walipo.



“Kuna Noah nyeusi ilikuja Kilwa na kukamata vijana wawili, usiku wake wakakamatwa vijana tisa, hatukujua wamepelekwa wapi, tulifuatilia mpaka Kituo cha Polisi Kilwa Masoko wakasema kweli wapo wameshikiliwa, nikamwandikia barua Waziri wa Mambo ya Ndani (Mwigulu Nchemba), tisa kati yao waliachiwa, lakini wawili hawajarudi mpaka sasa na hatujui wako wapi. Nataka leo, waziri atupatie vijana wetu hao na ushahidi upo.



“Leo mnapotwambia nchi hii ina amani mimi siwaelewi, watu wamepigwa risasi msikitini, mmoja amekufa, mwingine ametobolewa jicho na mwingine kachomwa moto ndevu, hawa watu wapo na serikali haikutoa tamko lolote. Hii nchi imeharibika. Ninaunga mkono waraka wa maaskofu kwa sababu maneno ya maaskofu ni maneno ya Mungu, tunataka amani na utulivu,” amesema Bwege.

Ukiziona Dalili hizi basi ujue Unapendana na Mpenzi Wako

0
0

Wataalamu wa mahusiano wanasema kuwa kuna dalili nne ambazo ukiziona kwenye mahusiano yako basi amini kuwa ninyi mnaendana na pia mapenzi yenu yatadumu

1. Uhusiano wenu uwe na uwiano.

Mahusiano ambayo yamefanikiwa ni yale yenye uwiano sahihi. Katika mahusiano mtakuwa tofauti wakati mwingine, na utofauti huu lazima ulete ulingano.

Mfano, kuna ambao hupenda sana kutoka out na marafiki, huyu anahitaji kupata mtu ambaye si mpenzi sana wa kwenda out ili kuleta mlingano. Unatakiwa kuwa na mtu ambaye unakamilika unapokuwa nae, mtu ambaye mkiwa pamoja mkichanganya tabia zenu mnapata tabia moja ambayo imetokana na kuathiriana kwa matendo yenu.

2. Mnafurahia kusafiri pamoja.

Njia rahisi kabisa ya kujua kama mnaendeana ni kama manafurahia mnapokuwa manasafiri pamoja, Watu wanaoendana hupenda kusafiri pamoja na kwenda sehemu tofauti tofauti.

 Kama wewe unataka kusafiri kwa gari, lakini mwenzako anataka kupanda ndege na ubishani wenu unakuwa mkubwa basi ujue ninyi manatatizo. Wapenzi wanaoendana hukubaliana na njia moja ya kutumia ambayo wote wataifurahia.

3. Uliyenaye anakufanya ujisikie vizuri.

Kuwa katika mahusiano ambayo yanakufa ujisikie kuwa upo katika ubora wako, sio mahusiano ambayo kila ukiyakumbuka unanuna.Kuwa na uhusiano na mtu ambaye mkikaa pamoja huhitaji kupiga miayo na kujinyoosha ili upate cha kuongea. Kuwa na mahusiano ambayo yanakufanya uone fahara hata kuyazungumzia mbele ya rafiki zako.

4. Kuna kitu mnachokipenda ambacho mnafurahia kukifanya pamoja.

Hii ni muhimu kuiona, watu wanaopendana huwa kuna kitu kimoja au zaidi ambavyo wote mnapenda na hufurahia kukifanya pamoja. Hii haimaanishi kuwa basi vitu vyenu kama ni muziki, au vitu vingine vitakuwa sawa, lakini kuna kitu ambacho kitakuwa kinaingiliana kati yenu na ambacho mnafurahia kukifanya.

Kwa ufupi mtakuwa na labda vitu viwili au vitatu mnavyopenda kufanya pamoja mfano kuogelea, kuangalia tamthiliya, muziki, kutembea na vingine. Hii ni ishara kuwa ninyi

Kabla ya Kufunga Ndoa Hakikisha Mmepima haya Magonjwa 4 ya Kuambukizwa

0
0

1. Ugonjwa wa kaswende.

Kitaalamu kama syphilis, huu ni ugonjwa hatari sana ambao umeharibu maisha ya watu wengi bila wao kujifahamu. Ugonjwa huu ambao huambukizwa kwa njia ya kujamiana huanza kidogo na kidonda ambacho hakiumi sehemu ambapo wadudu wamepita mfano mdomoni au sehemu za siri.

Kidonda hicho hupona, upele usiowasha hutokea na baadae vyote hivyo hupotea. Ugonjwa huu baadae huingia ndani ya mwili na kuuanza kuharibu viungo vya ndani. Mwisho kabisa ugonjwa huu huahamia kwenye ubongo na kumfanya mtu kua kichaa.

2. Ugonjwa wa hepatitis B.

Ugonjwa huu ni hatari na unaua haraka kuliko ukimwi, virusi vya ugonjwa huu huambukizwa kwa njia ya kujamiana na kugusana kwa damu au majimaji ya mwili kama ukimwi lakini ni rahisi zaidi kuambukizwa ugonjwa huu kuliko kupata ukimwi.

Ugonjwa huu hushambulia maini na kuacha makovu, Mgonjwa hupata macho ya njano, homa, maumivu ya kichwa na kadhalika. Ugonjwa hii mwishoni hupelekea kansa ya ini ambayo inaua ndani ya miezi sita.

3. Ugonjwa wa ukimwi.

Huu ni ugonjwa unaofahamika kwani unatangazwa sana hasa kwenye vituo vya Radio, Tv, Magazeti na sehemu mbalimbali.

Ugonjwa huu uligundulika karne ya 20 na mpaka sasa umeshaua watu wengi sana na zaidi ya 95% ya wagonjwa waliambukizwa kwa kushiriki ngono bila kinga.

4. Ugonjwa wa gonorea.

Huu ni ugonjwa wa zinaa ambao unashambulia jinsia zote yaani Wanaume na Wanawake, mara nyingi Mwanaume hawezi kujificha na ugonjwa huu kwani dalili za ugonjwa huo kama kutoka na usaa kwenye njia ya kukojolea zitamuumbua lakini kwa wananwake ugonjwa huu huweza kukaa kimya na mwana mke hujikuta akisambaza ugonjwa huo bila kujua. Mwishoni ugonjwa huu hushambulia kizazi na kusababisha ugumba.

Zijue Sababu Zinazopelekea Wapenzi Wengi Kuchokana Mapema

0
0

Hivi uliwahi kujiuliza hivi ni kwanini baadhi ya mahusiano ya kimapenzi hufa mapema, kama si kufa basi kushuka kwa mahusiano hayo? Moja kati ya sababu ambayo husababaisha kufa kwa mahusiano ni ile tabia ya kuchokana mapema katika mahusiano na moja kati ya sababu kubwa ambayo hupelekea kuchokana mapema ni:

1. Mazungumzo

Mazungumzo ni njia muhimu ya kujenga ndoa na kuiimarisha , aidha ni njia ya mkato ya kuchokana na kuchukiana. Mwanamke ambaye hajui wakati gani aseme nini na wakati gani asiseme, hujikuta katika wakati mgumu ndani ya ndoa yake. Kwa mfano: Mwanamke ambaye kila anapoongea na mume wake huanza mazungumzo yake na matatizo na lawama humfanya mumewe awe na woga kila anaposikia sauti yake, na kuiona nyumba chungu, kwa sababu hakuna binadamu anayependa kusikia matatizo tu wakati wote.

Mwanamke wa aina hii huwa anamsubiri mumewe kwa hamu kubwa, na anapofika tu na kabla hata ya kupata rizki, anaanza kumsomea orodha ya matatizo; watoto wamerudishwa shule, karo haijalipwa, shangazi yako amepiga simu mjomba kalazwa Hospitali na kadhalika na kadhalika. Nyumba ya aina hii huzeeka haraka na wanandoa kuchokana.

2. Kuzoeana

kuzoeana baina ya wanandoa ni jambo zuri, kwa maana ya kila mmoja kumfahamu mwenzake, lakini kuzoeana huku kunaweza kuzalisha dharau hususan kwa upande wa mwanamke kwa kutojali usafi wake, mavazi anayovaa, chakula anchopika, nidhamu ya nyumba na mpangilio kwa ujumla.

Matatizo mengi ndani ya nyumba yanaweza kusababishwa na moja au baadhi ya tabia hizo, ambazo huenda ikawa hazitokani na dharau, bali kuzoeana, kwa mfano: siku za utoto wa ndoa mwanamke huwa anajali sana usafi wa mwili wake, umaridadi wa nguo anazovaa, usafi wa nyumba na nidhamu ya hali ya juu, upishi wa chakula unaozingatia vionjo na ubunifu, mapokezi yenye bashasha na wakati mwingine hata kumkumbatia mumewe arudipo kutoka kazini.

Lakini baada ya kuzoeana yote hayo hubadilika, mwanamke huhisi kuwa hana jipya la kumuonyesha mumewe, hujiona wameishakuwa watu wazima sasa, na mara nyingi utakuta mwanamke huyu anashinda na sare (uniform) moja kuanzia asubuhi hadi anapopanda kitandani usiku, mambo ya Hinna, nguo za fashion, salon, manukato, kujipamba na dhahabu huyafanya pale anapotoka kwenda harusini na sio nyumbani. Huku ndio kuzoena, na tafsiri sahihi ni kudharau.



Mambo Yatakayokusaidia Kudumisha Mahusiano ya Mapenzi

0
0

Kuna nukuu inayosema “Uhusiano mzuri hautokei tu peke yake bali huchukua muda, uvumilivu, na watu wawili ambao kikweli wanataka kuwa pamoja.”

Japo inasemwa kuwa mapenzi hayana njia moja ya kufuatwa lakini kuna vitu ambavyo vinajulikana kuchangia katika kuboresha mahusiano baina ya wapenzi.

Mahusiano ya mapenzi yenye kudumu ni sharti yapandwe katika udongo wenye rutuba kama ulivyo mmea, yatahitaji maji ya kumwagilia na mbolea ya kukuzia.  Na zaidi ya yote yanahitaji muda wa kukua kabla matunda kuonekana.

1. Uaminifu
Kumwamini mwenza wako ni jambo la msingi sana katika kudumisha mahusiano. Usimshuku mpenzi wako kuwa si muaminifu bila ushahidi wowote. Kushukiwa kukosa uaminifu pasipo ukweli inasononesha sana na kumkosesha raha mpenzi wako.

Imesemwa na wanafalsafa wa mawazo ya binadamu kuwa “Unachofikiri na kuamini kinatokea” hivyo unashauriwa kutofikiri vibaya juu ya mpenzi wako kwani haileti afya katika mahusiano. Hali kadhalika na wewe uwe mwaminifu na mwenye kusema kweli mara zote. Ongeeni juu ya mipango na mawazo yenu bila kufichana.

Watambulishe kwa mpenzi wako ndugu ,jamaa na marafiki wakaribu ili kumpa mwenza wako amani.

2. Weka muda kwajili ya Mwenza wako
Mahusiano mazuri kati ya wapenzi yanahitaji muda wa wapenzi hao kukaa pamoja. Wapenzi wasio na muda wa kukaa wana hatari ya kupoteza mvuto wa mahusiano yao na hivyo kuhatarisha uhai wa mapenzi kati yao.

Kama wapenzi wapo mbali mbali basi wanahitaji kuweka muda wa kuongea kila inapowezekana. Tafuta muda wa kutoka pamoja, hata kama mtaenda mgahawani kunywa chai au juisi tu inatosha sana na inawaweka karibu zaidi.

3. Mawasiliano
Mawasiliano ni muhimu sana baina ya wapenzi. Hata kama umebanwa na kazi pata dakika chache za kuongea na mpezi wako na kumtaka hali. Andika hata ujumbe wa maneno au barua pepe. Mwambie mpenzi wako ulipo kila mara inapobidi ili kumjengea imani na wewe na kumpa amani moyoni. Tuma ramani ya mahali ulipo kama unatumia simu ya “Smart” (Tuma location kwenye whatsapp)
Mawasiliano ni ufunguo wa kudumisha upendo.

Wakati kuwasiliana na mpendwa wako, kumbuka kwamba upendo ni muhimu. Ongea toka moyoni na si kwa ajili ya kutimiza wajibu tu, kwani mpezi wako atajua tu kama hakuna mahaba katika mawasiliano yenu hivyo kutoleta faida ile inayotegemewa.

Mawasiliano mengine ni yale ya kuelezana yaliyo moyoni. Mweleze mwenza wako linalokusibu ili kupata ufumbuzi wa pamoja. Wapenzi wanaoongea kwa utulivu siku zote watakuwa pamoja.

4. Zawadi
Tafuta kitu cha kumpa mpenzi wako. Si lazima kiwe na thamani kubwa. Inaweza ikawa pipi au matunda tu. Mnunulie zawadi kila inapowezekana hasa unaposafiri au katika siku yake ya kuzaliwa.

5. Onyesha Upendo Wako 
Kila mtu anajinsi yake tofauti ya kuonyesha upendo, lakini vyovyote itavyokuwa ni jambo la muhimu sana kuonyesha hisia zako kwa mpenzi wako. Mara nyingi wapenzi wa muda mrefu wanasahau juu ya hili.

Maneno kama “Nakupenda”au majina ya mahaba kama “Mpenzi” au ”La-azizi” yanachangia sana kuonyesha mapenzi na kumfanya mwenza wako kujisikia vizuri. Maneno haya yanaposemwa kwa hisia halisi na toka moyoni yana mchango mkubwa katika kuboresha mahusiano.

Je, Una Malengo gani Katika Maisha?

0
0

Je, leo unapofikiria maisha yako yaliyopita, unafurahi na kuridhika kuwa uliyaendesha vizuri au hauridhiki? Watu wengi husikitika hadi wakasema kama wengebahatika kupata nafasi kurudia maisha, wasingeishi kama walivyo sasa.

Wanasema wangekuwa makini zaidi katika kupanga maisha yao ili kuyafanya yawe bora zaidi.

Huenda hata wewe unafikiria hivyo. Lakini duniani tunaishi mara moja tu wala hatutarudi tena baada ya kufariki.

Hivyo nafasi tulitonaayo ndiyo hii ya kurekebisha maisha yetu. Na wala hatujachelewa.

Je tunawezaje kufanya maisha yetu yaliyosalia kuwa bora? Hebu tushirikiane kutaafakari kisa hiki tuone kama kitatusaidia kuboresha maisha:

Kijana aliyemaliza chuo kikuu alikwenda kwa mwanafalsafa kumuomba amsaidie kuamua kazi itakayomfaa zaidi. Yule mwanafalsafa akamuuliza “ Kwani wewe unataka kazi gani?” Kijana akajibu, “ Nimekuja kwako kwa sababu sijui cha kufanya”

Mwanafalsafa akamwambia Mimi sitaweza kukusaidia kama wewe mwenyewe hujui nini unachotaka.

Labda fikiri na uniambie baada ya miaka kumi kutoka leo unataka uwe umefikia hali gani ya maisha.

Kutaka ushauri kuhusu maendeleo yako katika maisha ni kama kwenda kukata tikiti ya usafiri. Wale wanao katisha tikiti hawataweza kukupatia tikiti mpaka uwambie lengo lako ni kwenda wapi.

Hivyo ukinipatia maelezo niliyokuomba nitaweza kukusaidia.

Yule kijana akasema “ Nataka baada ya muda huo niwe na maisha mazuri.

Niwe na kazi yenye mshahara mzuri, nyumba nzuri yenye fenicha ya kisasa,gari ndogo inayovutia na familia yenye maisha mazuri”

Kutokana na kisa hiki tumejifunza kuwa ni muhimu binadamu kuwa na malengo katika maisha. Lengo ni shabaha, nia, ama makusudi.

Hivyo kila wakati binadamu anapaswa kuwa na mambo anayofikiria kuyatekeleza ili kupiga hatua fulani anayotarajia katika katika maisha.

Kila siku tunawaona watu wakifanya shughuli mbalimbali.

Wakulima mashambani, wafugaji malishoni, wavuvi baharini na mitoni, warina asali na wapasuaji mbao misituni, wachimba madini migodini, mafundi viwandani, wafanya biashara madukani na masokoni na wajenzi kwenye majengo mapya. Aidha, kuna kundi kubwa la watumishi kama vile madaktari, wahandisi, wahasibu, mameneja, walimu, makarani, askari, walinzi na madereva na wahudumu mbalimbali.

Wote hawa ukiwauliza watakwambia wanashughulika ili kutafuta maisha.

Kwa hakika huwa wanatafuta kipato ili wakidhi mahitaji mbalimbali ya maisha kama vile chakula, malazi, mavazi na huduma kama vile elimu, afya, malezi ya watoto, burudani na huduma nyingine kadha wa kadha.

Pamoja na kushughulika kote huko bado kuna watu wenye maisha duni wakati wengine wana maisha bora.

Ajabu ni kuwa hata wale wanaofanya kazi ya aina moja na kupata mishahara inayofanana na wenye familia zilizo sawa, bado hutofautiana katika hali za maisha yao.

Kinachofanya watofautiane ni nini? Hakuna kingine chochote isipokuwa kuwa na malengo

Wakati mmoja niliwahi kujaribu kuwauliuza watu ninaokutana nao kama wana malengo ya maisha waliyoyaandaa.

Nilistaajabu kugundua watu wengi hawakuwa wameandaa malengo yoyote ya maisha na kulikuwa na wengine ambao hawakuelewa hata maana ya malengo na hawakutambua kama kuna haja ya kuandaa malengo.

Aidha, uchunguzi wangu ulionyesha kuwa watu waliofanikiwa katika maisha kuliko wengine ni wale ambao huhakikisha wakati wote wana malengo. Baada ya kuweka malengo Watu huwa hutumia akili na juhudi zao zote kuyatekeleza.

Baada ya kutambua kuwa kujiwekea malengo ndio ufunguo wa maisha bora sasa inabidi tujifunze namna ya kuweka malengo:

Jinsi ya kuweka malengo

Unapotaka kuweka malengo fuata hatua mbili zifuatazo

1. Kuweka taswira unayoitarajia baadaye

Kwanza fikiria katika akili yako uvute taswira unayoitarajia itokee au uifikie utakapo kamilisha lengo lako. Unapoweka taswira akilini fikiria sehemu tatu zinazo kuhusu yaani kazini, nyumbani na katika jamii

2. Kuchambua vigezo vya matarajio

Katika zoezi hili utataja vigezo vya mafanikio unavyotarajia kwa kujibu maswali kama vile, Ni kitu gani ninachotarajia kukifanikisha katika kipindi cha lengo? Je ninatarajia kuwa katika hali gani nitakapotimiza lengo? Kiwango gani cha mafanikio ninastahili kukifikia ili niridhishe nafsi yangu? Vigezo vichambuliwe kwa kujibu maswali kuhusu kazini, nyumbani na katika jamii. Ifuatayo ni mifano ya maswali.

Kuhusu kazini maswali yanaweza kuwa kama vile: Natarajia kufikia kiwango gani cha mshahara au mapato? Kuwa na madaraka au mamlaka kiasi gani? Kupata kiwango gani cha hadhi na heshima?

Kwa upande wa nyumbani maswali nikama vile: hali ya maisha ya familia yangu ipande juu kiasi gani? Watoto wangu wapate elimu ya kiwango gani? Nyumba ya kuishi iwe ya namna gani?

Kuhusu hali yangu katika jamii maswali yanaweza kuwa kama vile. Niwe na marafiki wa aina gani? Nijiunge na vikundi vya jamii vya aina gani? Nifanikiwe kupata madaraka au uongozi gani katika jamii?

Zoezi la kuweka malengo katika maisha litekelezwe kwa kufanya fikara zako ziwe huru kama vile mtu anayeota ndoto ya mambo yatakavyoweza kuwa baada ya miaka 5 au 10.

Daima hakikisha unaweka malengo na unafanya kila juhudi kuyatekeleza.

Nyumba 12 Zilizopo Kando ya Mto Msimbazi Zasombwa na Mvua Zinazoendelea Kunyesha

0
0
Nyumba 12 Zilizopo Kando ya Mto Msimbazi Zasombwa na Mvua Zinazoendelea Kunyesha



Nyumba 12 zilizopo kando ya Mto Msimbazi,Mtaa Majengo Eneo la Vingunguti jijini Dsm zimesombwa na Maji na huku nyingine zaidi ya 100 ziko hatarini kuanguka kutokana na Mmomonyoko wa Udongo unatokana na kupanuka kwa Mto Msimbazi na kuingia katika makazi ya watu.

Baadhi ya wananchi wanaoishi katika mtaa huo wamesema hali ni mbaya katika eneo hilo, kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha huku mto huo ukiendelea kutanuka baada ya kuacha njia yake ya asili na kuingia katika makazi yao.

Diwani wa Eneo hilo Omar Kumbilamoto amesema walifanya juhudi za kupambana na mto huo kwa kuwashirikisha wananchi ambao kiasi cha Million 2 zilichangwa, lakini alidai baadhi ya watumishi katika manispaa hawakuonyesha ushirikiano na kuomba wizara ya mazingira chini ya ofisi ya makamu wa rais kuingilia kati.

Mchina Aliyemzalisha Mwanamke wa Kitanzania Amtelekeza Mtoto

0
0
Mchina Aliyemzalisha Mwanamke wa Kitanzania Amtelekeza Mtoto

MWANAMME mmoja Raia wa china amemtelekezea mtoto wa miaka miwili binti wa Kitanzania baada ya kumzalisha na kutokomea.


Penzi la Harmonize Lawaingiza Katika Vita Vikali Sarah na Wolper

0
0
Penzi la Harmonize Lawaingiza Katika Vita Vikali  Sarah na Wolper



MKALI wa Bongo Movies, Jacqueline Wolper Massawe na  mzungu ambaye ni mpenzi wa Staa wa Bongo fleva kutoka WCB Harmonize, Sarah wamerudi kwenye ya vita ya mtandaoni.

Wolper na Sarah wamerushiana maneno Kwenye mtandao wa Instagram ambapo Sarah amemtuhumu Wolper kwa kumtumia meseji za Siri Harmonize huku akijua wazi kabisa ni mpenzi wake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Sarah ameandika maneno haya kumtolea povu Wolper na kumchana kuwa anamtongoza Harmonize na kumtumia meseji huku anaona wazi kuwa hamjibu na amemtaka Wolper aishi maisha yake.




Hii  sio mara ya kwanza kwa Wolper na Sarah kugombana kisa penzi la Harmonize, siku za nyuma Sarah ameshawahi kuanika kuwa Wolper bado anamtaka Harmonize jambo ambalo Wolper amekuwa akikataa siku zote.

Inasikitisha Watoto wawili wa Familia Moja Wafariki Dunia Baada ya Kuangukiwa na Ukuta

0
0
Inasikitisha Watoto wawili wa Eamilia Moja Wafariki Dunia Baada ya Kuangukiwa na UkutaWakati mvua zikiwa zinaendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya nchi na kusababisha mafuriko, huko Jijini Mwanza watoto wawili wa familia moja wamefariki baada ya kudondokewa na ukuta kipindi mvua hizo zikinyesha zilizokuwa na upepo mkali.


Akizungumza kutoka kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza, Ahmed Msangi amesema watoto hao wamefariki majira ya usiku wakati wakiwa wamelala katika nyumba waliyokuwa wanaishi katika mtaa wa Buguku kata ya Buhongwa wilayani Nyamagana Jijini Mwanza.

Kamanda Msangi amewataja watoto hao kuwa ni Mariam Saimon (4) pamoja na Musa Baraka (2) hukyu majeruhi wakiwa watatu katika tukio hilo.

Tutawatangaza Hadharani Wake Zao Wajue Wanawatoto wa Nje ya Ndoa- Makonda

0
0
Tutawatangaza Hadharani Wake Zao Wajue Wanawatoto wa Nje ya Ndoa- MakondaPaul Makonda amefunguka na kusema wanaume ambao wamewazalisha wanawake na kuwatelekeza bila kuwapa matunzo pindi watakapoitwa wakikaidi wito huo kwa lengo la kulinda ndoa zao basi watawatangaza hadharani ili wake zao wajue wana watoto nje ya ndoa.


Makonda amesema hayo leo katika ofisi zake wakati akiongea na mamia ya wanawake ambao wametelekezwa na wanaume zao baada ya kuzalishwa, katika mkutano huo Makonda ametangaza kuwa jambo hilo litakwenda kwa siku tano mfululizo ili kutoa nafasi kwa wanawake wote wenye matatizo hayo kuweza kusikilizwa.

"Kama tukikuita hutaki, unajificha unajidai kulinda ndoa yako wakati mama yangu huku anateseka na mtoto huku sisi tutakuanika hadharani mkeo ajue una mtoto wa nje ya ndoa, mimi najua sijaanza leo kupigana hii vita najua wakina baba wasiopenda matokeo yao watanichukia lakini ukinichukia, ukinitukana, kunifedhehesha ni kama unanipaka mafuta yanayoning'arisha zaidi chuma kinaimarishwa na moto na viongozi wanaimarishwa na kebehi" alisisitiza Paul Makonda 

Trump Aapa Kutumia Nguvu Kujibu Shambulio la Kemikali Nchini Syria

0
0
Trump Aapa Kutumia Nguvu Kujibu Shambulio la Kemikali Nchini SyriaRais wa Marekani Donald Trump ameahidi " kutumia nguvu " kujibu madai ya shambulio la kemikali nchini Syria, huku mataifa ya magharibi yakitafakari hatua watakayoichukua.

"Tuna njia nyingi za kijeshi,"aliwambia waandishi wa habari.

Aliongeza kuwa hatua ya kujibu shambulio hilo itaamuliwa katika kipindi cha "muda mfupi".

Bwana Trump alisema kuwa Marekani inapata ''msaada mzuri" juu ya nani aliyehusika na shambulio la Douma Jumamosi.

Duru za kitabibu zinasema makumi kadhaa ya watu waliawa katika shambulio hilo, lakini idadi kamili haijathibitishwa.

Bw Trump pia alijadili tukio hilo la rais wa Ufaransa Emmanuel Macron Jumatatu jioni, na viongozi wote walielezea utashi wao wa "kujibu kikamilifu".

Image caption
Mjumbe wa Marekani Nikki Haley alisema kuwa-wanaounga mkono jeshi la Syrian - wana "damu ya watoto wa Syria " mikononi mwao
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May amesema kuwa "analaani vikali" kitendo cha "ukatili" kinachodaiwa kuwa ni shambulio la kemikali na akatoa wito kwa wanaomuunga mkono rais Bashar al-Assad kuwajibishwa.

Kauli za viongozi wa kimagharibi za kulaani shambulio hilo zimefuatia kikao cha malumbano katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambapo Marekani na Urusi walitupia na maneno makali kuhusiana na tukio la Douma.

Muwakilishi wa Urusi kwenye baraza hilo Vassily Nebenzia alisema shambulio linalodaiwa lilipangwa na akaonya kwamba hatua za kijeshi za Marekani zinazolenga kujibu tukio hilo "litakuwa na athari mbaya".

Mjumbe wa Marekani Nikki Haley alisema kuwa-wanaounga mkono jeshi la Syrian - wana "damu ya watoto wa Syria " mikononi mwao na akambandika jina rais Assad kama "zimwi ".

Image caption
Muwakilishi wa Urusi kwenye baraza hilo Vassily Nebenzia alisema linalodaiwa kuwa la kemikali dhidi ya Douma lilipangwa
Bi Haley alitoa wito wa kupigwa kura juu ya muswada wa maazimio ya kubuniwa kwa tume ya uchunguzi juu ya matumizi ya silaha za kemiikali nchini Syria siku ya Jumanne.

Lakini Urusi inasema haiwezi kuunga mkono pendekezo hilo kwasababu lina "vipengele visivyokubalika''.

Ni kipi kilichotokea Jumamosi?.
Shirika la matibabu la Marekani na Syria linasema kuwa watu zaidi ya 500 waliletwa kwenye kituo cha matibabu katika mji wa Douma, uliopo katika jimbo la mashariki la Ghouta , karibu na mji mkuu Damascus, wakiwa na dalili "zinazoonesha kuwa walishambuliwa na kemikali".

Shirika hilo linasema dalili walizaokuwa nazo ni pamoja na ugumu wa kupumua, ngozi ya samawati , kutokwa na povu mdomoni , kuungua kwa mboni na "walikuwa na harufu kama ya kemikali ya chlorine".

Idadi kamili ya vifo ya na ni nini hasa kilichotokea haviwezi kuthibitishwa kwasababu eneo hilo halina mawasiliano.

Makadirio ya idadi ya watu waliouawa katika shambulio linaloshukiwa kuwa la kemikali ni kuanzia watu 42 hadi zaidi 60, lakini makundi ya kitabibu yanasema idadi hiyo inaweza kuongezeka baada ya wahudumu wa uokoaji kuweza kufika kwenye sehemu za chini za majengo ambako mamia ya familia walikuwa wamekimbilia kuepuka mashambulio ya mabomu.

Muwakilishi wa Ufaransa katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa amesema gesi ya sumu ilitumiwa kwa makusudi kwasababu inaweza kusambaa hadi sehemu za chini za majengo hadi.

Marekani ,ufaransa na Uingereza wameongoza kampeni ya kimataifa ya kulaani shambulio hilo linalodaiwa kuwa la kemikali, huku serikali ya Syria na waungaji mkono wao Urusi wakikana kuwajibika kwao kokote na tukio hilo

Baada ya Kuichapa Ethiopia Yanga Yatuma Salamu kwa Timu za Ligi Kuu Bara

0
0
Baada ya Kuichapa Ethiopia Yanga Yatuma Salamu kwa Timu za Ligi Kuu Bara

BAADA ya Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Wolaita Dicha ya Ethiopia, wachezaji wa timu hiyo wamesema hizo ni salamu kwa timu za Ligi Kuu Bara, ikiwemo Simba ambayo kwa sasa inaongoza msimamo wa ligi hiyo kwani yenyewe inahitaji kutetea ubingwa wake.

Nyota hao wameta­mba kuwa kuanzia sasa hawataacha nyuma pointi yoyote katika mechi zote watakazocheza.



Juzi Jumamosi, Yanga ikiwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Sa­laam, iliibuka na ushindi huo ukiwa ni mchezo wa kwanza wa hatua ya mtoano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Wachezaji wa Yanga ambao keshokutwa Juma­tano watakuwa na kibarua kingine cha kuhakikisha wanapata pointi tatu mbele ya Singida United ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara, wamesema kuwa, kuanzia ushindi dhidi ya Wolaita Dicha, ha­wataacha pointi hata moja kwenye michuano yote wanayoshiriki kwa sasa.



Timu hiyo ambayo kwenye ligi kuu inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi 46 kabla ya mchezo wa Azam jana Jumapili dhidi ya Mbeya City, Aprili 18, mwaka huu inatara­jiwa kurudi­ana na Wolaita Dicha huko nchini Ethiopia.



Akizungumza na Championi Jumatatu, beki wa kati wa Yanga, Andrew Vincent ‘Dante’, alisema: “Unajua baada ya kufungwa na Singida na kuondolewa katika Kombe la FA, wapinzani wetu waliongea sana, sasa tukajipanga na kusema tutawaonyesha kitu.

“Hivi sasa tulivyo ni kama mnyama aliye­jeruhiwa, tukikutana na timu yoyote mbele ni kipigo tu, kuachwa pointi tatu na Simba huku tukiwa michezo sawa si kitu cha ajabu, tutawashangaza wengi mwisho wa msimu.”



Msimu uliopita, Simba iliongoza kwa muda mrefu na kuna wakati kabla ya mechi tatu za mwisho za mzunguko wa kwanza, Simba walikuwa wanaongoza kwa tofauti ya pointi nane lakini walikamatwa na mwisho Yanga wakachukua ubingwa kwa tofauti ya mabao baada ya timu zote kuwa na pointi 68.

Hata hivyo, msimu huu Simba imefunga mabao mengi zaidi ya Yanga na kama wak­ilingana pointi, basi Wekundu wana nafasi kubwa ya kushinda.

Goli la Okwi Lawapa Ushindi Simba Dhidi ya Mtibwa Sugar

0
0
Goli la Okwi Lawapa Ushindi Simba Dhidi ya Mtibwa SugarSimba SC imeendelea kujikusanyia alama katika Ligi Kuu Bara baada ya kuilaza Mtibwa Sugar FC kwa bao 1-0 jioni hii kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Mchezo huo uliokuwa unaambatana na mvua iliyokuwa ikinyesha Uwanjani, ulishuhudiwa nyavu zikitikiswa mnamo dakika ya 24 ya kipindi cha kwanza na Emmanuel Okwi.



Okwi alifunga bao hilo akimalizia kazi mpira wa kichwa kutoka kwa John Bocco na kufanya mchezo huo udumu kwa dakika zote 90 huku matokeo yakisalia kuwa 1-0.

Matokeo hayo yanaifanya Simba izidi kujikita kileleni kwa kufikisha alama 52 dhidi ya watani wao wa jadi Yanga wenye 46 mpaka sasa.



Mechi inayofuatia kwa Simba itakuwa dhidi ya Wajelajela Mbeya City FC, itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Soma Nafasi za Ajira zilizotangazwa Leo

Mwanaume Kuwa Rijali Kunako Sita Kwa Sita Kwa Kutumia Products Hizi

0
0
Bidhaa original na zilizothibitishwa kiafya zinapatikana NATURAL BEAUTY PRODUCTS sasa zinapatikana kwa bei ya punguzo la %10.

Bidhaa hizi zimetengenezwa kwa mimea na matunda hazina kemiko wala madhara yoyote. Hakikisha unapewa risiti original ya natural beauty products

TUNAZO KAMA HIZI

1.HANDSOME UP ORIGINAL_ Inaongeza uume kwa size uipendayo na kuimarisha misuli (wiki 2) @250,000/=

2.SHARK POWER GELY_ Inaongeza uume inch 6 (wiki 4) @150,000/=

3VigRX CREAM_ Inaongeza uume inch 6.5 hadi 8 (wiki 2-3) @200,000/=

4.Vidonge maalum vya kuongeza nguvu na hamu ya tendo hata kwa wenye kisukari na BP @170,000/=

5. MAXMAN 2-Hii ni vidonge vinavyoongeza nguvu za kiume pamoja na uume @240,000/=

6.VIGA SPRAY OG_ Inaongeza uwezo ktk tendo na kuchelewesha kufika kileleni @150,000/=

7.BODY BOOSTER_ Hii ni yakuongeza mwili pamoja na hamu ya kula vizuri @140,000/

8.DISCREET ORIGINAL_Hii ni dawa ya kuondoa mvi na zisiludi tena milele @150,000/= N.K

NB:Hakikisha unapata risiti yenye muhuri na garantii ili kukuhakikishia ubora na usalama wa bidhaa za NATURAL BEAUTY LTD

Wasiliana nasi Popote
ulipo duniani kwa (+255)
0659618585 au
0759029968
Viewing all 104414 articles
Browse latest View live




Latest Images