Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Ufafanuzi Kuhusu Kupungua Kwa Meli Kwenye Bandari ya DSM

$
0
0
Baada ya kusambaa kwa taarifa kwamba kiwango cha meli za mizigo katika Bandari ya DSM zimepungua, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Eng. Deusdedit Kakoko ametoa ufafanuzi leo April 9 2018 katika maadhimisho ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).

VIDEO:


Wekundu wa Msimbazi Simba SC Waendelea Kukusanya Point.....Waitesa Mtibwa Vibaya

$
0
0
Wekundu wa Msimbazi Simba SC Jumatatu ya April 9 2018 walishuka katika uwanja Jamhuri Morogoro kucheza na wenyeji wao Mtibwa Sugar, huo ukiwa ni mchezo wao wa 22 wa Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2017/2o18 kwa Simba ambayo kwa sasa imesalia katika mashindano hayo pekee.

Timu za Dar es Salaam ambazo mara nyingi zimekuwa zikihangaika kupata matokeo katika viwanja vya mikoani kwa madai ya viwanja vibovu, imekuwa tofauti kwa Simba ambayo imefanikiwa kuondoka na point tatu katika uwanja huo kufuatia kupata ushindi wa goli 1-0 lililofungwa na Emmanuel Okwi dakika ya 24.

Ushindi huo sasa unaifanya Simba kufikisha jumla ya point 52 na kuendelea kusalia kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu, wakifuatiwa na wapinzani wao Yanga waliyopo nafasi ya pili kwa kuwa na jumla ya point 46 ila wapo nyuma mchezo mmoja nyuma ya  Simba, wakati Mtibwa Sugar imeendelea kusalia nafasi ya sita kwa kuwa na jumla ya point 30

“Mimi Sielewi Mkisema Nchi Hii ina Amani”-Mbunge Bwege

$
0
0
Mbunge wa Kilwa Kusini Selemani Busagara maarufu Mbunge BWEGE akiongelea matukio ya Askari Polisi kutuhumiwa kuwakamata na kuwaua baadhi ya watu jimboni kwake.

Busagara amesema…
“Jimboni kwangu kuna watu karibu sita  hadi sasa hawajulikani walipo na mara ya mwisho walikamatwa na Polisi lakini kila tunapotaka kujua wamewekwa wapi hatujafanikiwa.  Nchi yetu ina matatizo sana na siamini kama ni nchi yenye amani”

VIDEO:

Mwanamke Akikujibu SMS yako Hivi Acha Haraka Sana Kuchat Nae

$
0
0
Ukiona umemtumia mpenzi wako/mchumba wako/mchepuko wako/mke wako au hata rafiki wa kike wakati mwingine SMS ya kawaida tu kwaajili ya kumsalimia lakini yeye akakujibu moja kati ya majibu yafuatayo, tafadhali sana usiendelee kuchat nae maana kinachofuata hapo ni majanga tu.

KWA MFANO:
1. Ukimtumia sms ''Mambo mpenzi wangu?'' akikujibu ''mambo mabaya'', usimuulize kwanini mambo mabaya, ukimuuliza atakwambia kuwa ''sina hela dear''

2. Ukimtumia sms ''Maisha yanasemaje kipenzi changu'' akikujibu ''maisha magumu hubby wangu we acha tu'' usimuulize kwanini, ukimuuliza kwanini atakwambia ''nimefulia mwenzio kama nini sijui''

3. Ukimtumia sms ''Mbona kimya sana mchumba wangu, umenitupa kiasi hicho'' akikujibu ''sijakutupa wangu yaani mambo hata hayaendi'' usimuulize kwanini mambo hayaendi, ukimuuliza atakwambia kuwa ''yaani sina kitu mpenzi wangu, simu ilikuwa haina hata hela ya kubeep''

4. Au ukiona mwanamke anaanza kwa kukwambia nikwambie kitu? We mkatalie kiutani utani tu, mwambie usiniambie, hata akikomaa vipi akwambie mwambie sitaki uniambie huku unafanya kama utani lakini moyoni unakuwa upo serious.

Ni mara chache sana mwanamke akikwambia kuwa mambo mabaya, maisha magumu au mambo hayaendi huwa na matatizo mengine kama kuumwa, misiba.... n.k lakini THE REST ni wapigaji mizinga tu. Akikwambia maisha magumu mjibu ''pole wangu, mambo mengine vipi?''

Ukipewa majibu kama hayo, chagua moja, either usiendelee kuchat nae mpaka badae kidogo au mbadilishie maada ili kukwepa huo mzinga ambao unakuja mbele yako.

By Dr. MCHUNGUZI HURU

Peter Msechu Asema Hajawahi Kuona Watu ' Wanafiki ' na ' Wabinafsi ' Duniani Kama Watanzania

$
0
0
Akizungumza muda mfupi tu uliopita katika mahojiano na Kituo kimoja cha Television Msanii Peter Msechu amesema kwamba kama kuna kitu ambacho amejifunza kwa Watanzania basi ni tabia zao kubwa mbili ' pacha ' za Unafiki na Ubinafsi.

Alitolea mfano hai kwamba kuna siku moja aliwahi ' Kuposti ' Mtandaoni kuwaomba Watanzania wapakue Nyimbo zake na wampigie Kura lakini cha Kushangaza ndani ya Siku tatu alipata ' mrejesho ' wa Watu wasiozidi 25 tu lakini Kesho yake ' akaposti ' kuwa ameachana na Mkewe Mama Lolo cha kushangaza ndani ya dakika 10 alipokea sms zaidi ya 3200 za Watu huku wengine hata hawajui na wakijifanya kumpa ushauri na kumpoza na akashangaa mno kwamba iweje alipowataka wampe ' sapoti ' katika Kazi yake hawakumpa ' ushirikiano ' ila kwa mambo ya ' Kimbea ' ndipo wengi walijotokeza?

Nami nimuambie tu Peter Msechu kwamba nampa pole kubwa kwa kuchelewa Kwake kujua kwamba hakuna Watu ' Wanafiki ' na ' Wabinafsi ' duniani kama Watanzania na nadhani hicho ' Kipaji / Kipawa / Talanta ' pekee tuliyojaaliwa nayo Watanzania na kwakweli tunatendea haki kabisa.

Nawasilisha.

Kutana na Sheikh Twabibu bingwa wa Magonja Sugu Anatibu kwa Kutumia Dua na Utaalam wa Jadi

$
0
0
Sheikh Twabibu bingwa wa Magonja Sugu Anatibu kwa Kutumia Dua na Utaalam wa Jadi

JE umeangaika kwa mda mref bila mafanikio sasa acha kuteseka mvuto wa mapenzi kumrudisha yule umpendae?

Kuvuta mali iliyo potea au kuchukuliwa na majini wabaya

Mvuto wa biashara na kumiliki mali

Pete za bahati zindiko la mali

Nina tibu uzazi Ulioshindikana na miguu kuwaka moto

JE Una shamba nyumba au kiwanja unauza na Haviuziki Kirahisi ninayo dawa aina ya kafyonkola itakusaidia ndani ya muda mchache tu

Tunasoma Dua maalum kwa wogonjwa wote

Napatikana kwa mawasiliano 0758024610 au Whats App Namba 0656783490

Nedy Musiki Afunguka Kufanya Kazi na Alikiba Pamoja na WCB

$
0
0



Msanii wa muziki Bongo, Nedy Music amefunguka kuhusu mipango yake ya kufanya kazi na Alikiba pamoja na kusaini katika label ya WCB.

Muimbaji huyo wa ngoma ‘One and Only’ ameiambia The Playlist ya Times FM kuwa mipango ya kufanya ngoma na Alikiba ipo ila anahitahitaji watu wamjue kwanza na sio wafanye kwa sababu wanajuana.

“Unajua usifanye kitu kimazoea, usifanye kitu kwakuwa unajuana na mtu nilitamani watu wajue uwezo wangu, nikiwa na maana hata pale ninapoenda na kazi nataka afanye na mimi basi pawe na urahisi na si kinyonge atafanya kwa kuwa tunajuana, kwa hiyo ni wazo bado lipo na panapo majaliwa litatokea,” amesema.

Kuhusu kusaini katika label ya WCB amesema ikitokea nafasi hiyo atasaini kwa sababu ni biashara, pia amekanusha taaarifa za kuachana na label yake ya PKP mara baada ya wimbo wake mpya kutoka bila kuwa na logo ya label hiyo.

PKP ni label ambayo inamilikiwa na msanii Ommy Dimpoz ambaye July 06, 2017 alisaini kufanya kazi na label ya  RockStar4000 inayofanya kazi kwa ukaribu na kampuni kubwa ya muziki duniani, Sony Music Entertainment.

Suala la Walimu Kukosa Udhamini Katika Mabenki Latua Bungeni

$
0
0

Naibu Waziri-TAMISEMI, Joseph Kakunda amesema kuwa hakuna dhamana mtumishi kukopa katika mabenki au taasisi zaidi ya dhamana ya mshahara wake kinachotakiwa mtumishi asiwe anadaiwa mikopo mingine.



Kakunda ameyasema hayo leo Bungeni wakati akijibu swali la Mbunge Grace Victor Tendega aliyehoji kuwa,

Walimu wameukuwa wakikosa udhamini katika mabenki mbalimbali kutoka kutokuwa na mali, na hivyo alivyovisema Naibu Wazii ni vitu visivyohamishika kama viwanja, magari na vitu vingine na tunatambua hali za walimu wetu zilivyo Je serikali haioni haja kuwa ni wakati muafaka mifuko ya hifadhi ya jamii iweze kufanya dhamana kwa walimu wetu wakati wakiwa kazini na sio baada ya kustaafu?

“Karibu mabenki yote na taasisi zote hakuna dhamana zaidi ya mshahara wa Mtumishi kinachotakiwa mtumishi asiwe anadaiwa mikopo mingine hilo ndio jambo la msingi na kama mtumishi hadaiwi mikopo mingine anao uwezo wa kukopa na ataamua mwenye akope kwa kurejesha miaka mitatu u akope kwa kurejesha miaka 10 au akope kwa kurejesha miaka 25 ni yeye mwenyewe katika makubaliano ya sehemu yake kwahiyo napenda kuwasisitiza watumishi wote nchi nzima na Wakurugenzi wa Halmashauri ambao wako chini yangu nataka niwaambie kwamba mikopo hiyo ya watumishi ipo waingie katika makubaliano maalum na hizo taasisi na mabenki ili watumishi waweze kukopeshwa na wajenge nyumba zao binafsi,” amesema Kakunda.

“Kwanza naomba nisisitize kwamba kwenye jibu langu la msingi ile takwimu niliitaja kwa Bunge lako tukufu haikumaanisha walimu hao hawana makazi kabisa nilisema walimu hao katika either nyumba za kupanga au nyumba zao binafsi na sehemu ya kwanza ya swali lake kwamba kwanini jeshi la polisi kujenga nyumba za polisi nchi nzima, hilo naomba Mh. Naibu Spika lina kazi zake maalum waliojenga ukuta wa Mirerani sio Jeshi la polisi,” ameongeza.

Werrason Akubali Uwezo wa Christiani Bella Amuahidi Kufanya Naye Kazi

$
0
0
Werrason Akubali Uwezo wa Christiani Bella Amuahidi Kufanya Naye KaziMsanii Supersatar wa Congo Noël Ngiama Makanda alimaarufu kama Werrason amekubali kufanya kazi na msanii wa muziki wa bongo fleva Christian Bella baada ya kumkubali kutokana na uwezo wake na kazi zake.


Werrason amesema hayo alipokutana na msanii Christian Bella na kuonyesha hisia zake juu ya msanii huyo jambo ambalo Christian Bella ameliona ni jambo kubwa sana katika muziki wake kuona watu ambao alikuwa akiwasikiliza toka wakiwa wadogo saizi wanakubali kazi zake na kukubali kufanya kazi pamoja na yeye.

"Imethibitishwa sasa nitafanya kazi na Werrason  the king of jungle, nadhani kujituma juhudi zangu na kutokata tamaa leo hii ma Star Wakubwa ambao nilikua nawashangaa kwenye TV nikiwa mdogo kutoka DRC wananipa heshima na kunikubali. Nasema Asante Mungu Asante pia sana Kwa watanzania kwa kunipa na fasi na kunikubali na kuni support leo hii miaka 13 kwenye game bado naonekana mpya" alisema Christian Bella

Christian Bella kwa sasa anatamba na wimbo wake 'Niende wapi' ambao amemshirikisha rapa Joh Makini kutoka katika kampuni ya Weusi. Itazame hapa kazi yake mpya.

Ajali Nyingine Mbaya Yatokea Yaua Wanafunzi 12

$
0
0
Ajali Nyingine Mbaya Yatokea Yaua Wanafunzi 12Jinamizi la ajali limeendelea kuangamiza wanafunzi katika nchi nyingine duniani, ambapo takriban wanafunzi 23 wenye umri wa miaka 4 – 12, wamefariki dunia kwa ajali ya gari iliyotokea Jumatatu ya Aprili 9, 2018, baada ya basi lao kuacha njia.


Ajali hiyo imetokea nchini India ambapo basi hilo lililokuwa likisafirisha wanafunzi wa shule binafsi ya Wazir Ram Singh Pathania kuelekea nyumbani, kuacha njia na kuserereka katika eneo la Wilaya ya Kangra huko Himachal Pradesh, kwa mujibu wa polisi nchini India.

Jumla ya miili 27 ya watu wakiwemo dereva wa basi hilo, wafanyakazi wawili wa shule hiyo na mwanamke mmoja imeondolewa sehemu ya tukio, na wanafunzi wengine 11 wamekimbizwa hospitali kutokana na kuwa na hali mbaya waliyonayo baadhi yao, huku ikihofiwa kuwa idadi ya vifo huenda ikaongezaka kutokana na hali walizonazo majeruhi.

Rais wa nchi hiyo Ram Nath Kovind amesema tukio hilo limemuhuzunisha na kutoa pole kwa familia na shule iliyofikwa na misiba hiyo ambayo imeacha baadhi ya familia zikiwa na majonzi makubwa, na kwamba familia hizo zitapatiwa pesa za India rupee lakh 5, ambazo ni zaidi ya milioni 17 za kitanzania kuwapa pole na kuwafariji.

Ikumbukwe kuwa mnamo mwezi Mei, 2016 ilitokea ajali mbaya nchini Tanzania ambayo iliuwa wanafunzi zaidi ya 30 wa shule ya Lucky Vicent ya mkoani Arusha.

Waziri Mwakyembe Awapa Makavu Wabunge Wanaowatetea Wasanii

$
0
0
Waziri Mwakyembe Awapa Makavu Wabunge Wanaowatetea Wasanii
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amefunguka na kuwataka baadhi ya Wabunge Bungeni kuacha kuwatetea wasanii wanaoimba nyimbo zisizokuwa na maadili kwa kuwa kufanya hivyo kuna pelekea kuonekana taifa la Tanzania kuwa mfu lisilokuwa na utamaduni wake.

Waziri Mwakyembe ametoa kauli hiyo leo (Aprili 10, 2018) kwenye mkutano wa 11 kikao cha sita kinachoendelea kufanyika mkoani Dodoma wakati akijibu swali la Nyongeza kutoka kwa Mbunge Catherine Magige ambaye alitaka kufahamu ni kwanini kamati ya maudhui inashindwa kufanya kazi zake kwa wakati mpaka inafikia muda wasanii wanaachia kazi zao za sanaa ndio wao wanaibuka na kuanza kuwafungia kazi hizo, je wameshindwa kazi ?.

"Kila taifa lina utamaduni wake na lazima liulinde kwa udi na uvumba, tunachokifanya sisi sio kwamba tuna vita na wasanii wetu, hapana. Lakini lengo letu ni kulinda maadili ambayo katika kipindi hiki cha utandawazi kumekuwepo na mmong'onyoko mkubwa katika taifa letu na lazima tuchukue hatua. Tunachokifanya sisi hapa sio jambo jipya duniani, kila mtu anafanya hivyo na hawa wasanii wetu tumeshawasamehe wasirudie tena", amesema Dkt. Mwakyembe.

Pamoja na hayo, Waziri Mwakyembe ameendelea kwa kusema kwa kutumia baadhi ya nukuu ya Hayati Baba wa Taifa Julius Kambarage Nyerere kwamba "Taifa lisilokuwa na utamaduni wake ni taifa mfu'. Sisi hatuwezi kukubali kuwa taifa mfu. Yanayotokea Tanzania yanatokea duniani kote".

Kwa upande mwingine, Waziri Mwakyembe amesema Wizara yake kupitia kamati ya maudhui itaendelea kuzifungia nyimbo zisizokuwa na maadili ili waweze kulinda utamaduni wa taifa la Tanzania

Wigi Lamuumbua JDee Lamvuka Ghafla Akiwa Stejini Mwenyewe Anena Haya

$
0
0
Wigi Lamuumbua JDee Lamvuka Ghafla Akiwa Stejini Mwenyewe Anena Haya
Mwanamuziki Lady Jaydee amezungumza ishu ya wigi kumvuka ghafla wakati akicheza.

Kitu hicho kinaonekana katika video ya wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Anaweza ambao amemshirikisha msanii mkongwe kutoka nchini Jamaica, Luciano.

“Lilianguka, (anacheka) ilikuwa kwamba lilianguka chini, ni ajali kazini,” Lady Jaydee ameiambia Bongo5.

Hata hivyo ukitazama video ya wimbo huo kwa makini utagundua ulikuwa ni mpango wa makusudi ili Lady Jadee kuondoka katika scene hiyo na kupisha madansa katika video hiyo kuendelea na shughuli yao.


Katika hatua nyingine Lady Jaydee alizungumza kuhusu project mpya baada ya Anaweza.

“Kwa sababu ndio kwanza project imetoka hautakiwi kuongelea project ya mbele wanatakiwa wafurahie hii baada ya kuwa wamechoka basi tutazungumza kuhusiana na projet mpya,” alisema.

Monalisa Ahaidi Kuwabwaga Wakina Lupita na Kurudi na Tuzo

$
0
0
Baada ya muigizaji wa filamu nchini Yvonne Cherrie 'Monalisa'  kutajwa kuwania tuzo za The African Prestigious Awards kama Muigizaji bora Afrika huku akitarajiwa kushindana na mastaa wakubwa Afrika amesema hata asipopata tuzo tayari anaamini ni hatua


Monalisa Ahaidi Kuwabwaga Wakina Lupita na Kurudi na Tuzo
Monalisa amezungumza hayo wakati akikabidhiwa bendera ya Taifa na Waziri wa Habari, Michezo, Sanaa na Utamaduni, Mh. Harrison Mwakyembe ambapo amesema kuwa ingawa anaamini atarudi nchini na tuzo hizo lakini hata akizikosa ni moja ya ushindi kulingana na kuwania waigizaji anaoshindana nao.

“Tuzo hizi nazichukulia kama ni heshima kubwa sana kwangu kwani kipengele ninachowania kinahusisha wasanii wakubwa katika bara la afrika kwani niko pamoja na Lupita Nyong'o ambaye ni mwigizaji wa Hollywood pamoja na Jackie Apia ambaye naye anafanya vizuri hivyo. Hata nisipopata tuzo hii kwangu kuchaguliwa kwanza katika kipengele hicho tayari ni ushindi kulinga na uwezo wasanii wenzangu tuona shindana,” Monalisa.

Kwa upande wa Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu nchini Bi. Joyce Fissoo amesema anafurahishwa kuona sekta ya filamu ikikua na kuleta taswira mpya katika bara la Afrika ambapo wasanii wa Tanzania nao kazi zao zinavuka mipaka na kuleta changamoto katika ushindani wa tasnia ya filamu Afrika.

Monalisa anatarajiwa kwenda Ghana mapema wiki hii amabapo atawawakilisha wasanii watatu ndani ya tasnia ya filamu ambao ni King Majuto anayewania Tuzo ya Mchekeshaji Bora Afrika, Vicent Kigosi anayewania Tuzo ya msanii Bora wa Kiume Afrika na Monalisa mwenyewe anayewania Tuzo ya Msanii Bora wa Kike Afrika pamoja na Mpiga picha Mahiri Moiz Hussein anayewania Tuzo ya Mpiga Picha Bora Afrika.


Bodigadi wa Mayweather Anusurika Kifo Baada ya Kupigwa Risasi

$
0
0
Bodigadi wa Mayweather Anusurika Kifo Baada ya Kupigwa Risasi
Vyombo mbalimbali vya habari vimeripoti kuwa mtu mmoja anaedaiwa kuwa mmoja wa walinzi wa karibu wa bondia wa Marekani, Floyd Mayweather amepigwa risasi nje ya Hoteli ya Atlanta hapo jana asubuhi siku ya Jumatatu.



Mtandao wa habari za michezo wa TMZ Sports umeripoti kuwa kwamujibu wa taarifa za Polisi, risasi imetoka kwa mtu ambaye alikuwa kati ya moja ya magari matatu yaliyokuwa yamewasili nyuma ya hoteli ya InterContinental Buckhead majira ya saa 3 a.m. asubuhi siku ya Jumatatu.

Kwa mujibu wa chombo cha habari cha CNN kimeripoti kuwa mlinzi huyo ambaye jina lake halija fahamika amefikishwa kwenye Hospitali ya Grady Memorial kwaajili ya kupatiwa matibabu kufuatia risasi hiyo kumjeruhi mguuni na hali yake inaendelea vizuri.

Taarifa kutoka Polisi zinaeleza kuwa wanaamini bondia, Mayweather alikuwa sehemu ya msafara huo uliyoshambuliwa licha ya kutokuwa na uhakika kama yeye ndiye alikuwa mlengwa wa tukio hilo.

Wanaume Waliotelekezewa Watoto na Wake Zao Kutua kwa RC Makonda Leo

$
0
0
Wanaume Waliotelekezewa Watoto na Wake Zao Kutua kwa RC Makonda Leo
WANAWAKE 480 waliotelekezwa na watoto ambao jana waliitikia wito wa kwenda kusaidiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, wamesema walizalishwa na viongozi mbalimbali wa kidini na kisiasa.

Hilo lilibainika baada ya wanawake hao, miongoni mwa mamia waliofika ofisini hapo  ili kupatiwa msaada wa malezi na matunzo ya watoto wao waliotelekezwa na baba zao.

Katika mfululizo wa misaada ya aina hiyo, leo wanaume waliotelekezewa watoto na mama zao, watafika ofisini kwa mkuu wa mkoa huyo kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi wa suala hilo.

Wakati huohuo, Makonda akihutubia wakati wa uzinduzi wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi kwa wasichana wenye umri wa miaka 14 unaofanyika leo katika viwanja vya Zakeem Mbagala, amesema wanawake 47 waliofika ofisini kwake jana wanadai wabunge ndiyo wamewatelekeza na watoto na wengine  wamesema  wamezalishwa na kutelekezwa na viongozi wa dini mbalimbali.

Katika hafla hiyo ya utoaji wa chanjo, mgeni rasmi alikuwa ni Makamu wa Rais Samia Suluhu

Okoa Ndoa yako Sasa...Umepungukiwa na Nguvu za Kiume na Unashindwa Kupanda Mlima Vizuri

$
0
0

KOA NDOA YAKO SASA : JE UMEPUNGUKIWA NA NGUVU ZA KIUME AU UUME WAKO MDOGO AU MPENZI WAKO HAKUTIMIZII UTAKACHO:


Acha kujiona mpweke pale ukutanapo na mpenzi au mke wako kwa sababu ya kutokuwa na nguvu za kiume au Uume wako mdogo

Dawa YA MAPRO POWERA ndio dawa sahihi na tiba tosha kwa sasa Kutibu tatizo na kuponesha kabisa tatizo LA KUWAI KUFIKA KILELENI KABLA MWENZI WAKO BADO AJAKOJOA

KUSHINDWA KURUDIA TENDO LA NDOA NA MWILI KUCHOKA

UUME KUSINYAA NA KUWA LEGELEGE

KUUMWA NA TUMBO WAKATI UNAPOMALIZA KUFANYA TENDO

Dawa hii utumiwa ata na wazee wenye umri mkubwa na haina madhara yoyote

MAKAKANUA HII NI dawa ya maumbili madogo urefusha na kunenepesha saizi upendayo saiz 5-6-7-8 na unene sm 3-4-5 kwa mini huabiki kwa kuwa na UUME mdogo wai sasa upate tiba sahihi kabisa na ni tofauti na ulizowai kutumia :

Tunarudisha mke au mpenzi ndani ya masaa matatu tu zipo dawa za presha kisukali vidonda vya tumbo korodani iliyovimba dawa za uzazi tunapunguza matiti makubwa kitambi na mwili mkubwa dawa zipo FIKA OFISINI KWANGU MBAGALA ZAKHEMU KWA WATEJA AMBAO AMTAKUWA NA NAFASI YA KUJA OFISINI AU MLIO MKOANI MTALETEWA p

Piga simu 0743362017 au 0789234653

DR AGU 

Dodoma Yatajwa Kuongoza Kwa Ugonjwa wa Kipindupindu

$
0
0

Dodoma imetajwa kuongoza kwa idadi kubwa ya wagonjwa wa kipindupindu. Kati ya wagonjwa 1,448 wa nchi nzima, 583 wamepatikana mkoani humo
-
Ruvuma imeshika namba 2 kwa kuwa na kesi 374 sawa na 25%, Rukwa na Iringa ikiwa na kesi 276 sawa na 19%.
-
Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee imeeleza kuwa Mkoa Manyara ndio wenye idadi ndogo ya wagonjwa wa kipindupindu. Kesi zilizoripotiwa ni asilimia 0.6 tu ya wagonjwa wote nchini

Basi la Kampuni ya Maqadir Lapata Ajali Tanga

$
0
0
Basi la Kampuni ya Maqadir Lapata Ajali Tanga

Basi la Kampuni ya Maqadir lililokuwa linatoka jijini Tanga kwenda Kijiji cha Mtae, Wilaya ya Lushoto mkoani humo, limeanguka asubuhi  leo Aprili 10, 2018 katikati ya barabara kuu ya Segera-Tanga katika kijiji cha Mpakani, kata ya Kerenge wilayani Muheza mkoani Tanga.



Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Edward Bukombe, majeruhi wa ajali hiyo ni mmoja na bado hajatambuliwa ambapo  chanzo cha ajali hiyo, pia bado hakijafahamika.

Video: Sarah wa Harmonize Ana Matatizo Anahitaji Msaada- Wolper

$
0
0
Image result for Jacqueline Wolper
Mrembo kutoka kiwanda cha filamu Bongo, Jacqueline Wolper amekanusha tetesi alizozitoa mpenzi wa Harmonize, Sarah kwamba anamsumbua mpenzi wake, Harmonize. Muigizaji huyo ameyasema hayo Jumanne hii wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya kampeni ya yao mpya ya Amka Kijana wa Iringa

Idadi Kubwa ya Wanawake Waliofika kwa RC Makonda Wamezalishwa na Kutelekezwa na Viongozi wa Dini, Wabunge

$
0
0
Idadi Kubwa ya Wanawake Waliofika kwa RC Makonda  Wamezalishwa na Kutelekezwa na Viongozi wa Dini, Wabunge
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda aameweka hadharani kuwa kati ya wanawake 480 waliozungumza na wanasheria siku ya jana Jumatatu katika ofisi za mkoa wamezalishwa na kutelekezwa na wabunge pamoja na viongozi wa dini.


Makonda ametoa kauli hiyo leo mbele ya Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan wakati wa uzinduzi wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi kwa wasichana wenye umri wa miaka 14 unaofanyika leo katika viwanja vya Zakeem Mbagala.

Mh. Makonda amesema  wanawake 47 wanadai wabunge ndio wamewatelekeza na 14 wamesema kuwa wamezalishwa na kutelekezwa na viongozi wa dini.

"Katika Mkoa  wa Dar es Salaam, mwaka 2017 wanawake waliojifungua walikuwa 129,347 na kati ya hao asilimia 60 walitelekezwa na watoto 274 waliokotwa maeneo mbalimbali ndiyo maana tumeona tuje na mkakati huu kuhakikisha tunapambana na wale wanaume wote wanaotelekeza watoto," amesema Makonda.

Mkoa wa Dar es salaam upo kwenye zoezi la kuwapa msaada wa kisheria wanawake wa mkoa huo ambao wametelekezwa na wenzi wao na wale waliokataa kulea watoto wao
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images